Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 145 | 146 | (Page 147) | 148 | 149 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akikata utepe na familia ya Mshindi wa nyumba wa promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba bwana Silvanus Juma (wa kwanza kushoto) wakati wa makabithiano ya nyumba yalifanyika kigamboni jijini Dar es Saalam.
  Mshindi wa nyumba wa promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba bwana Silvanus Juma pamoja na mke wake wakiingia katika nyumba wakati walipotembelea nyumba kigamboni jijini Dar es saalam.
  Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akimkabithi ufunguo wa nyumba mshindi wa kwanza wa nyumba ya promosheni ya Airtel Yatosha shinda nyumba bwana Silvanus Juma katika halfa makabithiano iliyofanyika kigamboni jijini Dar es Saalam, akishuhudia ni mke wa mshindi wa nyumba.
  Mshindi wa nyumba wa promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba bwana Silvanus Juma akifurahia ushindi na mama yake mzazi mara baada ya kutembelea nyumba kigamboni jijini Dar es salaam.

  0 0

  Taasisi ya Urejesho wa Maadili ya Taifa (Taumata) iliyosajiriwa kwa usajiri namna S.A 18827, imesisistiza kuwa kurejea katika maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa nasio vinginevyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi wa Taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa ndugu Joseph Goliama alisema kutoka katika maadili mabaya na kuingia katika maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo ya Taifa kwasasa

  Alisema kuwa makundi mbalimbali ya wananchi kuacha maadili mema ya Taifa ndio kumekuwa msingi chanzo na kiini cha Taifa kupoteza Sauti moja ya kuisikiliza na mwelekeo mmoja wa kuufuata hali inayosababisha makundi mbalimbali ya wananchi kutokuwa na amani kutopendana na kutokuaminiana

  Goliama alisema kuwa maadili mabaya ambayo yanafanya Taifa kupoteza amani, umoja na mawasiliano ni pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi kuwaziana mabaya, kutazamiana mabaya, kuneneana maneno mabaya, kutendeana mabaya, kuonana kwa jicho baya,kuhusiana kwa uhusiano mbaya, kufanyiana maamuzi yasiyo ya haki na kusimamiana kwa misimamo isiyo ya haki

  Tunawashauri watanzania wa makundi yote kurudi katika maadili mema na kuacha maadili mabaya ambayo yanatishia ustawi na maendeleo ya Taifa letu alisema Goliama

  Alitoa mfano na kusema maadili mabaya ndio yametumbukiza mataifa mengi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe hivyo akawataka wananchi wa makundi yote kulinda na kutetea maadili mema ambayo yameifanya Tanzania kuitwa kisiwa cha amani

  Aliitaka serikali kuangalia uwezekano wakuyakutanisha makundi yote ya wananchi nakuyakalisha pamoja ili yakubaliane ni Taifa gani yanataka kulijenga litakalohakikishia kila kundi ustawi na maendeleo endelevu .

  Akifafanua zaidi alisema wadau wa amani na umoja wa Taifa ni wananchi wa makundi yote yakiwemo makundi ya dini, vyama vya siasa, jinsia, rika, wafanyabiashara, wafugaji, wakulima, wafanya kazi ,Askari nakuyataka makundi hayo kupigania amani na umoja na haki ili Taifa liapate ustawi na maendeleo endelevu.

  Goliama alimalizia kwa kuitaka serikali iishirikishe taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa katika majukum yake ya kutafuta amani ,umoja na mshikamano wa kitaifa.

  0 0


  IMG_3480
  Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyampulukano ya Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wakati alipotembelea shuleni hapo kuhamasisha Wanafunzi kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa.
  IMG_3489
  Mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyampulukano ya mjini Sengerema akiuliza maswali kwa Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
  IMG_3526
  Mwalimu wa Shule Sekondari Nyampulukano ya Wilayani Sengerema akizungumza jambo na Wanafunzi wake.
  IMG_3558
  Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama aliyeambatana na mwenyeji wake Mkuu wa vipindi redio ya jamii Sengerema FM Bw. Andrew Mfungo wakizungumza na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Sengerema Bw. Nelson Rwelengela (kulia) ofisini kwake mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
  IMG_3563
  Mlezi wa UN Club ya Sengerema Sekondari Mwl. John Kimbuli akielezea shughuli za UN Club shuleni hapo na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama alitembelea shule hiyo mwishoni mwa Juma.
  IMG_3575
  Makamu Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Sekondari Sengerema Bw. Nelson Rwelengela (aliyesimama meza kuu) akiutambulisha ugeni kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa Wanfunzi wa shule hiyo.


  IMG_3629
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa Sengerema High School, kuhusiana na umuhimu wa kuanzisha vilabu vya Umoja wa Mataifa mashuleni, na kufafanua kuwa hiyo ni moja ya agenda za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa vijana zake ikiwamo Malengo ya Milenia (MDGs) kwa sababu kupitia wao wataweza kuzifahamu vizuri na mapema agenda mbalimbali za Umoja wa Mataifa wakiwa bado vijana, ili waweze kuzitekeleza hapo baadae.
  Pia amewagusia suala la kujiepusha na marafiki wenye tabia mbaya itakayowapelekea kujihusisha na vitendo visivyo vya kimaadili ikiwemo uvutaji bangi na matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili Tanzania kwa sasa, aidha amewasaa kutojihusisha na ngono pindi wawapo mashuleni ili kujiepusha na gonjwa la Ukimwi.
  Awali akizungumza na vijana wa shule za sekondari Nyampulukano wilayani Sengerema mkoani Mwanza Bi. Usia Nkhoma Ledama amewaeleza vijana upo umuhimu mkubwa sana kwa wao kujitambua, kwani kutawasaidia kupanga maisha yao kwa kuchagua nini unataka kufanya na njia gani ufanye ili uweze kufanikiwa.
  IMG_3633
  Bi.Usia amewaambia kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu vya vijana vya Umoja wa Mataifa (UN Club) mashuleni, basi hawana budi kujiunga kwa wingi zaidi kwani kutawawezesha kujifunza shughuli za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kusaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.
  Aidha amewatolea vijana hao mfano kuwa hata Waheshimiwa January Makamba (Mb) na John Mnyika(Mb) walikuwa wanachama wa vilabu hivyo ya vijana vya Umoja wa Mataifa wakati wakisoma shule za sekondari, kitu kilichowajengea uwezo na kujiamini na mpaka sasa wamekuwa viongozi wenye nafasi za juu hapa nchini, na kuwataka vijana kuiga mfano wao.
  IMG_3679
  Picha juu na chini Wanafunzi wa Sengerema Sekondari wakiuliza maswali kwa Bi. Usia Nkhoma Ledama.
  IMG_3670
  IMG_3689
  Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sengerema wakifura kupigwa picha walipotembelewa shuleni hapo na Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
  IMG_3690
  Bi. Usia Nkhoma Ledama akibadilishana mawazo na Wanachama wa UN CLUB Sengerema Sekondari pamoja na Mlezi wao.
  IMG_3438
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyampulukano ya Wilayani Sengerema Mwl. Vedastus Mlokozi wakati alipofika shuleni hapo kuwahamisha wanafunzi kuanzisha vilabu vya Umoja wa Mataifa.
  IMG_3441
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo.

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi ya Sekretariate ya Baraza la Mawaziri ambako watumishi wake wawili wameteuliwa kuwa manaibu Makatibu wakuu, ambao ni Injinia Angelina Madete (kulia kwa Rais) na Mhe. Consolata Mgimba (kushoto kwa Rais) mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu hao na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Manaibu Katibu wakuu mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu hao Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa tarehe 23 Agosti, 2013, katika viwanja vya Ikulu, amewaapisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.  Ifuatayo ni Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu walioapishwa leo.


  1.    MAKATIBU WAKUU

  Ndugu Sophia Elias Kaduma
  Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

  Ndugu Jumanne Abdallah Sagini
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

  Ndugu Uledi Abbas Mussa
  Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara

  Dr.  Patrick James Makungu
  Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

  Ndugu Alphayo Japani Kidata
  Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  Ndugu Charles Amos Pallangyo
  Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

  Ndugu Sihaba Said Nkinga
  Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  Ndugu Anna Tayari Maembe
  Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

  2.    NAIBU MAKATIBU WAKUU
  Ndugu Dorothy Stanley Mwanyika
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Fedha za Nje na Madeni)

  Ndugu Consolata Philipo Mgimba
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  Eng. Angelina Elias Augustine Madete
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais

  Dr. Deodatus Michael Mtasiwa
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - AFYA

  Ndugu Monica Lyander Mwamunyange
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi

  Ndugu Regina Lucian Kikuli
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu

  Ndugu Kagyabukama Edwin Kiliba
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI)

  Ndugu Zuberi Mhina Samataba
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - ELIMU

  Dr. Yamungu Kayandabila
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

  Prof. Adolf Faustine Mkenda
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (SERA)

  Ndugu Mwitango Rose Shelukindo
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

  Dr. Selassie David Mayunga
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  Prof. Elisante Ole Gabriel Laizer
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  Ndugu Amantius Casmiri Msole
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki


  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu
  Dar es Salaam.


  23 Agosti, 2013

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliofika uwanjani kumlaki.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana .
   Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Adam Kimbisa.

   Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Khamis Sadifa Juma.

  Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM,Kushoto kwake ni Makamu wa CCM Zanzibar Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtumishi wa Chama Cha Mapinduzi  ndugu Octavian Kimario .
   Watumishi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia kwa furaha ujio wa Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais Jakaya Mrisho Kikwete mara tu alipowasili Dodoma tayari kwa Mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama.


   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishina mawazo na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Stephen Wassira kabla ya Kikao cha Kamati kuanza leo Dodoma kwenye Ukumbi wa NEC.
   Wajumbe wa Kamati Kuu wakijadiliana jambo ndani ya ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu,Dodoma 23 Agosti 2013.
   Mjumbe wa NEC, Prof. Anna Tibaijuka akipitia Katiba ya Chama kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ndani ya ukumbi wa NEC.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamau wa Rais - Mazingira,Mh. Dkt Terezya Huvisa akiwa ndani ya boti wakati akitembelea Delta ya Rufiji kujionea uharibu wa mazingira wa ukataji wa mikoko,katika ziara yake mkoani Pwani.
  Mkuu wa Wilya ya Rufiji,Mh. Nurdin Babu, akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Bunwa katika wilaya ya Rufiji.
  uharibifu wa mazingira uliofanywa na wafugaji na wakulima katika bonde la mto rufiji juu ya suala la usafi wa mazingira.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamau wa Rais - Mazingira,Mh. Dkt Terezya Huvisa akitia sahihi katika kitabu cha wageni wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Pwani,Wilani Rufiji.katikati ni Mkuu wa wilaya ya Rufiji Bwana Babu na kulia ni mwenyekiti wa ccm wilaya.

  0 0

  DSC_0240

  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akitoa risala yake kwenye hafla ya kukabidhi Taa 200 za Nishati ya Jua kwa Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande ikiwa ni mwendelezo ya kampeni iliyozinduliwa na Hoteli ya DoubleTree By Hilton jijini Dar kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza hoteli hiyo kwa kubuni kampeni kama hiyo kwani Taa hizo ni rafiki wa mazingira kwa kuwa zinatumia Nishati ya Jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao pia kupata Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme na pia itaongeza ufaulu kwa Wanafunzi kwa sababu watakuwa wanauwezo wa kujisomea nyakati za usiku.

  Aidha amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (wa pili kulia).
  DSC_0234
  Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (katikati) akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia taa ndogo za mezani zinazotumia Nishati ya Jua na umuhimu wake tofauti na kutumia Mafuta ya Taa kwa Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Mji Mpya wakati uongozi wa hoteli hiyo ulipotembelea shule hiyo iliyopo Mabwepande kwa nia ya kuendesha mafunzo na kugawa Taa 200 bure kwa Wanafunzi hao. Kushoto ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
  DSC_0249
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akikabidhi rasmi Taa hizo kwa mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande leo jijini Dar. Katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
  DSC_0229
  Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni akitoa shukrani kwa uongozi wa hoteli ya Double Tree by Hilton kwa kuwa na mkakati madhubuti wa kuwaelimisha vijana umuhimu wa matumizi ya Umeme mbadala wa Nishati ya Jua ambao ni rafiki wa mazingira.
  DSC_0226
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mji Mpya Davis Mkaruka akizungumza baada ya mafunzo yaliyolewa na Double Tree by Hilton kwa wanafunzi wa darasa la saba akisema ilikuwa ni njia nzuri ya kuwaelimisha watoto juu ya nishati ya jua na kuwa wamefurahi kupewa bure taa ndogo za mezani ambazo ni rahisi kutumia na zina faida nyingi kwao na familia zao.
  DSC_0253
  Wanafunzo hao wakifurahia Taa ndogo la ‘Solar Energy’ walizopewa. Nyuma ni Bw. Florenso Kirambata na Meneja Mkuu wa hoteli ya Double Tree by Hilton Hotel Rode Perk.

  Hoteli ya Double Tree by Hilton Dar es Salaam leo imefanya ziara katika Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande kwa lengo la kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wa darasa la saba kuhusu umuhimu wa umeme wa nishati ya jua.

  Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Double Tree by Hilton wa miaka miwili wa kuwakufahamisha na kuwashirikisha wanafunzi juu ya faida za nishati ya jua tofauti na matumizi ya mafuta ya taa, kuni na vyanzo vingine vya mwanga ambavyo vina madhara kwa mazingira, afya na vifaa vya nyumbani.

  Katika ziara hiyo shule hapo Hoteli ya Double Tree by Hiltonimegawa kwa wanafunzi hao taa ndogo za mezani 200 zinazotumia nishati ya jua, ambazo wanafunzi hao wamekwenda nazo majumbani kwao kuzitumia kusomea usiku kwa faida yao na familia yao.

  0 0
   Msanii machachari wa muziki wa bongofleva/filamu Shilole akiimba huku akiwa amebebwa na shabiki wake,huku shangwe na miluzi za mashabiki zikiwa zimetawala kila kona.

   Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kucheza jukwaani,wakionesha umahiri wao wa kukata nyonga mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake,waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi usiku huu.
   Anajiita Raisi wa Manzese,kutoka  kundi la Tip Top Connections,atambulikae kwa jina la Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wake wa NANI KAIBA POMBE YANGU,usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
  Mashabiki wakiitikia kwa pamoja huku mikono yao wakipunga hewani.
  Mmoja wakali wa hip hop,Stamina akikamua jukwaani vilivyo usiku huu mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake waliojitokeza kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

  bdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
   Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah pichani kati akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. 
   Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
   Anaitwa Amin,mmoja wa wasanii mahiri akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye u kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
   Wenyewe mashabiki waki wanamuita Baba Levo na yeye kabaki Levo kwenye gemu ya muziki wa bongofleva,ndiye pichani Baba Levo akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
   Ni shwangwe tu usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
  Wakali wa kudansi kutoka THT,wakijulikana kwa jina la Makomanda wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
   Wanamuita Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake wa muziki wa dansi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,liinalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
   Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 wakiwa wamewasha tochi za simu zao wakiashiria kushoo love ya pamoja
  Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwa kuonesha kukunwa vilivyo na msanii huyo.
   Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.


  0 0


  0 0

  UFAFANUZI KUHUSIANA NA MAKUBALIANO YA RWANDA, KENYA NA UGANDA KUFANYA MOMBASA KUWA KITUO CHA USHURU.


  Utangulizi:


  Marais wa nchi za Rwanda, Uganda na Kenya, walikutana mwanzoni mwa mwezi uliopita, ambapo mojawapo ya maazimio ya mkutano wao, ilikuwa ni kufanya Mombasa kuwa kituo cha kukusanya ushuru, na hivyo Uganda na Rwanda waanze kusafirisha mizigo yao moja kwa moja kutoka Mombasa. (Angalia ambatisho)


  Ufafanuzi:


  Chama cha Umoja wa Wasafirishaji wa Malori nchini (TATOA), kinaamini hatua hiyo itadhoofisha uchumi wa nchi yetu kwa kiasi kikubwa sana.


  Na kama serikali yetu ikipuuzia kujiondoa kwa wateja hawa wawili, Rwanda na Uganda, huenda nchi nyingine zaidi zikazidi kujiondoa kutumia bandari ya Dar es Salaam.


  TATOA inaamini maamuzi kama haya ya nchi za wenzetu ya kurahisisha taratibu za ulipaji ushuru pamoja na kuboresha utaratibu wa bandari ni muhimu kwa bandari yetu pia.


  Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ilidhihirisha namna ambavyo bandari ya Dar es Salaam, ufanisi ukiboreshwa, inaweza ikawa mkombozi mkubwa wa uchumi wetu.


  Faida za bandari hii kwa uchumi ni mtambuka, kwa hiyo TATOA haitapenda kuona mteja yoyote akijitoa kutumia bandari yetu, au kupungua kwa biashara kwa namna yoyote ile, na hivyo itapigania kwa kuishauri serikali katika kuboresha bandari yetu.


  TATOA ni mmoja wa wadau muhimu kwenye sekta hii ya bandari, kwani biashara yake ni kusafirisha mizigo inayofika bandari ya Dar es Salaam kuwafikishia walengwa, hasa nchi zisizo na bandari (land locked countries) kama Congo, Zambia, Rwanda, Malawi,Uganda, Zimbabwe na Burundi.


  Hivyo kuondoka au kupungua kwa namna yoyote ile kwa matumizi ya bandari yetu, ni hofu ya TATOA itaathiri uchumi kwa kiasi kikubwa.


  Ieleweke kwamba, sekta ya usafirishaji wa malori ni muhimu kwa uchumi wetu. Sekta hii inatoa zaidi ya ajira milioni moja (1) za moja kwa moja, na nyingine zaidi ya milioni tatu (3) zisizo za moja kwa moja.


  Sekta ya usafiirishaji wa malori pia, ni yapili kwenye uchangiaji wa pato la taifa (GDP).


  Sekta hii pia, ni mojawapo ya sekta chache nchini ambazo zinagusa nyanja tofauti za kiuchumi kama, huduma za simu za kutuma pesa, matairi, spea pamoja na mafuta, ambazo zote zinafaidika na sekta hii.


  Mabenki pia yamekuwa ni mojawapo ya taasisi zinazofaidika na sekta ya usafirishaji, ukiangalia kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, huduma inayoongoza kwenye mabenki ni Vehicle Asset Financing.


  Zaidi ya hayo, TATOA pia inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye mfuko wa barabara, ambao ndio unatumika kuboresha barabara zetu nchini, kupitia matumizi ya mafuta, ambapo malori pekee yanatumia ziadi ya lita milioni mbili na laki tisa kwa siku kati ya lita milioni tatu na nusu.


  Mwisho TATOA inaamini, uboreshaji wa reli ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya usafirishaji nchini, kwani miundo mbinu hii miwili, reli na barabara, inafanya kazi kwa pamoja.


  Wakati reli inaweza kufikisha mzigo mpaka stesheni, malori yatahitajika kufikisha mzigo sokoni, au mahala pengine mteja atakapohitaji.


  Mifano hai ni nchi ya Uingereza na Afrika Kusini, ambazo zina malori mengi pamoja na kuwa zina mfumo mzuri wa reli.


  Lakini kwa nchi yetu, ambayo sekta ya reli bado inaboreshwa, tunaamini malori yataendelea kuwa na umuhimu mkubwa.


  TATOA inaiomba serikali, kupitia wizara ya uchukuzi kufanyia kazi kero zilizopo katika bandari ya Dar es Salaam lakini pia kufanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wadau wa sekta ya usafirishaji.

  ========  ========  =======

  0 0

  Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mh Ephraimu Mafuru akitoa neno mara baada ya kukaribishwa mbele kwa niaba ya kampuni ya Bia ya Serengeti katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake Cha Tusker Lite
   Meneja wa Kinywaji cha Tusker Sia Shayo akitoa neno mara baada ya kukaribishwa mbele kwa niaba ya kampuni ya Bia ya Serengeti katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake Cha Tusker Lite
   Baadhi ya maafisa masoko kutoka kampuni mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi wakisikiliza kwa makini katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Brewries Limited kupitia kinywaji chake cha Tusker
   Banana Zoro akiwa na wadau waliohudhuria tafrija ya Usiku wa Maafisa Masoko iliyofanyika Katika Hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake cha Tusker Lite, tafrija iliyofanyika usiku wa Kuamkia leo
   Baadhi ya Maafisa masoko waliohudhuria tafrija hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Brewries Limited Mh Steve Gannon akitabasamu mara baada ya Meneja Masoko wa Serengeti Brewries Limited Mh Ephraimu Mafuru (hayupo pichani) kutoa Neno lake kwa niaba ya Kampuni ya Serengeti Brewries Limited ambao Walikuwa wadhamini wa tafrija hiyo ya Usiku wa Maafisa Masoko kupitia Kinywaji Chao cha Tusker Lite.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Http://josephatlukaza.blogspot.com
   Mwanamuziki Banana Zoro akiwa na bendi yake ya B-Band akitumbuiza katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Golden Tulip huku Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake cha Tusker Lite kudhamini tafrija hiyo

  0 0

   Wanenguaji wa bendi ya muziki wa dansi wa Diamond Musica wakionyesha umahiri wao katika ukumbi wa Dar Live, Dar es Salaam kwakati wa tamasha lililoandaliwa na kampuni ya simu ya Vodacom usiku wa kuamkia leo
   Manjonjo ya kila aina.
   Madansa wakali
  Waimbaji wa bendi ya muziki wa dansi wa Diamond Musica wakiimba katika ukumbi wa Dar Live, Dar es Salaam kwakati wa tamasha lililoandaliwa na kampuni ya simu ya Vodacom usiku wa kuamkia leo

  0 0

   Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Hussen Makame akiwaonesha wanafunzi eneo la kupanda miti katika jitihada za kuzuia  mmong’onyoko huko katika skuli ya msingi Mtoni kidatu juu.
   Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Hussen Makame na mwanafunzi Hafsa Juma wakipanda mti katika eneo la Skuli ya Mtoni kidatu juu.
   Mpiga picha wa Maelezo Zanzibar Makame Mshenga, akijumuika na wanajumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar katika zoezi la kupanda miti huko Skuli ya Msingi ya Mtoni kidatu juu.(Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar). Na Miza Othman –Melezo Zanzibar
  =======   ======  =======
  Na Miza Othman –Melezo Zanzibar   
  Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar kwa kushirikiana na wanafunzi wa skuli ya Mtoni kitatu leo imeamua kufanya zoezi la upandaji wa  miti kwa ajili ya kuzuia mmong’onyoko wa ardhi ambao  unaoweza kuleta athari skulini hapo.

  Hayo yaemeelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo baada yakufanya zoezi hilo  huko skuli ya Mtoni kidatu nje kdogo ya mji wa Zanzibar. Amesema lengo la kupanda miti hiyo ni kuyaendeleza  mazingira pamoja na kuyadumisha ili kuwa endelevu katika skuli hiyo.

  Nae Msaidizi wa Mwalimu Mkuu Hamdani Othman Skuli ya Mtoni amesema ikohaja ya kupandwa miti hiyo  kwani  skuli yao ipo juu ya mlima jambo ambalo linaweza kupelekea athari kwa wanafuzi wao. “Skuli inaweza kuathirika na mazingira kwani iko juu ya malima kupanda miti itaondoa mmong’onyoko wa ardhi”,alisema Msaidizi Mwalimu Mkuu Hamdani Othman.

  Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar  Hussein Makame Mohamed amesema zoezi hili la upandaji miti ni muhimu katika maisha ya mwanaadamu  kwani itapelekea kuenzi na kutunza mazingira ya watu wa Zanzibar.

  “Lengo la kupanda miti ni baada ya kuona Zanzibar iko katika uharibifu wa mazingira  ikiwa nchi kavu na baharini”,alisema Katibu Hussein Makame.  Ameongezea kusema pia Jumuiya  ya Uvuvi  na Mazingira Endelevu Zanzibar  inalengo la kuwanyanyuwa vijana ambao waliokosa ajira na kuwawezesha kujiajiri katika Jumuiya  hiyo.

  Wanu Mlekwa Iddi ambaye ni mwana  jumuiya hiyo amesema ameamuwa kujitolea na kujiumga katika Jumuiya  hiyo katika kuyaenzi mazingira kwa ajili ya kulinda afya zao na mazingira yaliyo kwa jumla. Hata hivyo amesema ni bora kupanda miti kwani itasaidia kuzuia  udongo wakati wa mvua nyingi hasa katika skuli hiyo.  Jumuiya hio imeanzishwa 20 /1 /2012  tangu kuanzishwa inawanachama 22 hadi hisasa.

  0 0


  0 0


  Na Edwin Moshi, kilimanjaro
  Imeelezwa kuwa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano mzuri na viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya chini ni moja ya mafanikio yanaolifanya shirika la TUSONGE kuelekweka kwa wananchi wanaofanya nao kazi

  Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la TUSONGE lililopo Moshi mkoani Kilimanjaro Bi. Aginatha Rutazaa (aliyesimama pichani) wakati akizungumza na wafanyakazi wa shirika la SUMASESU lililopo wilayani Makete mkoani Njombe lilipofanya ziara katika shirika hilo yenye lengo la kubadilishana mawazo na kujifunza mbinu mbalimbali wanazozitumia kufikisha ujumbe kwa jamii

  Bi Aginatha amesema wakati wa ufanyajikazi katika shirika lake wamekuwa wakishirikiana kwa pamoja na wananchi pamoja na viongozi wa serikali ikiwemo mitaa na vijiji ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wenye watu na ukiwashirikisha ni rahisi ujumbe kufika kwa jamii

  Shirika hilo ambalo linatoa elimu ya mambo mbalimbali kwa wananchi ikiwemo UKIMWI na ujasiriamali, limefanikiwa kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa kwa wajasiriamali wadogo ( wa hali ya chini) ambapo walipata wasaa wa kutembelea kikundi kimojawapo kilichopo kata ya Karanga na kujionea kinavyofanya kazi

  Pia amesema wanatumia video kuonesha elimu mbalimbali hasa magonjwa ya ngono na UKIMWI ili ujumbe ufike moja kwa moja kwa jamii na kuona hali halisi ya kile kinachozungumziwa

  Kwa upande wake mkurugenzi wa SUMASESU Egnatio Mtawa alishukuru kwa mapokezi mazuri ya shirika la TUSONGE ambapo pamoja na mambo mengine alikiri kujifunza mengi mazuri kutoka kwao na kuahidi kwenda kuyatumia kwenye shirika lake ili jamii iweze kusonga mbele

  0 0

  Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwa mtu yeyote anayejiunga na shirika la NSSF,alifafanua hayo leo kwenye ukumbi wa Luluma,nje kidogo ya mji wa Singida,Salim alibanisha kuwa mtu yeyote atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo ambayo inafanyika ikiwa ni mkoa wa tatu huu,ikianzia Kigoma,Tabora na sasa Singida,iliandaliwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.

   Pichani juu ni sehemu washiriki wa semina ya Fursa kwa vijana,wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa kwenye semina hiyo,ambayo imeonekana kuwavutia vilivyo kwa sehemu ya wakazi wa mji wa Singida waliojitokeza kushiriki. 
     Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washiriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi  wa  Luluma,nje kidogo ya mji wa Singida, kuhusiana na fursa mbalimbali wanazozipata vijana na kuhakikisha wanazitumia ipasavyo,aliongeza kuwa vijana wengi wamekuwa ni watu wa kulalamika lalamika tu na kukata tamaa mapema,aidha Ruge amewataka vijana kuwa na muamko wa kufanya kazi na kujituma kwa bidii pale fursa yoyote inapotokea.
   Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,Millard Ayo akizungumza mbele ya vijana wenzake ,nama alivyobahatika kuzitumia fursa mbalimbali alizokuwa akizipata kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mpaka hapo alipo,anabainisha kuwa kilichompelekea hapo alipo mpaka sasa ni namna alivyojijenga kwa nidhamu,kujituma na bidii kubwa ya kazi kila alipokuwa akiipata fursa,aidha amewataka vijana wenzake kuacha tabia ya kukata tamaa mapema na kutokuwa wavivu wa kufanya kazi,kwani kwa kufanya hivyo maendeleo hayatapatikana kirahisi.
   Pichani juu na chini ni sehemu washiriki wa semina ya Fursa kwa vijana,wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa kwenye semina hiyo,ambayo imeonekana kuwavutia vilivyo kwa sehemu ya wakazi wa mji wa Singida waliojitokeza kushiriki. 
     Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisannii Baba Levo akielezea fursa aliyoipata kupitia muziki ikiwemo na namna alivyohangaika kujijenga na hatimaye kufikia hapo alipo,ingawaje anakiri wazi kuwa mafanikio aliyoyapata bado ni ya kiwango cha chini na kuwa anahitaji zaidi kuzitumia fursa alizonazo kuhakikisha anajikwamua kimaisha

  0 0


  0 0
   

  Msanii Muigizaji wa filamu na muziki wa bongofleva,Shilole pichani shoto akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,ndani ya Singida Motel.
   Sehemu ya umati wa watu wakishangilia burudani iliyokuwa ikiendelea kwenye kiota hicho cha Singida Motel.
   Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature akiwa na wasanii wenzake wa kundi la TMK -Wanaume Halisi,wakilishambulia jukwaa vilivyo.
   Anajiita Raisi wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha mashabiki wake,ndani ya Singida Motel wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea.
   Mashabiki waliokuwa wamejibanza ubavuni mwa jukwaa,nao walikuwa wakipata ile kitu roho inapenda kutoka kwa wasanii mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza jukwaani.
   Pichani kulia ni Niki wa Pili na shoto ni kaka yake Joe Makini,wote ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a hip hop wakiwa sambamba na mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu wakishangilia jambo nyumba ya jukwaa.
   Chumaaaa a.k.a Chid Benz akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.
   Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida.
   Anajiita mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiimba nyimbo zake za mahaba,mbele ya maelfu ya wakazi wa singida na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
   Ommy Dimpo a.k.a pozi kwa pozi akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani
  Kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Themba wakilishambulia jukwaa
   Dj Mahiri kutoka Clouds FM,Dj Zero akifinya finya mashine zake kwa namna ya pekee kabisa,iliyokuwa ikiwafanya mashabiki kibao wazidi kuchenguka na kupiga mayowe kila wakati.
   Wenywewe wanajiita Makomando,wakilishambulia jukwaani kwa pamoja usiku huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea ndani ya Singida Motel.
  Ni full kujiachia usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,wengine wakiwa juu ya miti aaahhh nomaa sanaaa.!
   Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Singida wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linalofanyika kwenye viwanja vya Singida Motel usiku huu.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Petter Msechu akiwaimbisha mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 linaloendelea hivi sasa ndani ya Singida Motel.
   Ni ndani ya Singida Motel tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea hivi sasa 
   Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Lina na Amin wakilishambulia jukwaa kwa pamoja,huku wakazi wa Singida waaliofurika usiku huu ndani ya Singida Motel wakipiga mayowe ya shangwe.
   Amin Jukwaani akiwambisha mashabiki wake,huku mayowe kila kona yakisikika usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Abdul Kiba akiimba jukwaani kwa hisia usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya Singida Motel usiku huu mkoani Singida. 
  Ni burudani Serengeti Fiesta nomaa sanaaa usiku huu,

  0 0

  Ngoooshaaa ukipenda waweza muita Fareed Kubanda kwa jina alilopewa na Wazazi wake na pia waweza muita Fid Q akikamua na msanii mwenzake Izzo Bussines ndani ya Uwanja wa New City Pub, jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Mwanadada nguli katika tasnia ya Muziki hapa nchini, Muite Bint Komando au Lady Jaydee akifanya vitu vyake ndani ya jukwaa moja la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013, lililofanyika kwenye New City Pub, jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Wakazi wa Mbeya wakionyesha furaha yao kwa kupunga mikono juu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0


  Mantra Tanzania Managing Director Asa Mwaipopo (third left) receives a trophy from President Jakaya Kikwete after his company scooped three Presidential Awards to Extractive Industry on Corporate Social Responsibility and Empowerment (CSRE) for 2012.  Looking on are Deputy Minister for Energy and Minerals, Hon. Stephen Masele (second left) and Catherine Liyombe (fourth left) who is the Executive Director of the Extractive Industry Stakeholders Forum.
   =======    ======  ======
  Mantra scoops CSRE Presidential awards.

  Mantra Tanzania, a uranium exploration company, with its Mkuju River Project in Namtumbo Ruvuma Region emerged the best in Corporate Social Responsibility and Empowerment Awards in Education, Health and Employment areas; and overall 2nd best in the Exploration category. 

  Commenting about three awards his company scooped during the first Presidential Award to Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment (CSRE) for 2012, Mantra Tanzania Managing Director Asa Mwaipopo said, “the awards is a cleartestimony of our good community relation programs and engagement.  This recognition will further be a catalyst to upscale performance on our CSRE programs”.

  The award which was presided over by President Jakaya Kikwete, was organized by the Ministry of Energy and Minerals through the Extractive Industry Stakeholders Forum (EISF).  The Extractive industry companies were classified in four categories; Large scale mining, Medium scale mining, Oil and gas companies and Exploration (minerals, oil and gas) companies.

  The ceremony was also attended by Minister for Energy and Minerals Professor Sospeter Muhongo, Ministry’s Permanent Secretary Eliakim Maswi, Acting Commissioner Ally Samaje, Canadian High Commissioner Alexandre Lévêque, some Members of Parliament and various members of the extractive industry sector.

older | 1 | .... | 145 | 146 | (Page 147) | 148 | 149 | .... | 1896 | newer