Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 146 | 147 | (Page 148) | 149 | 150 | .... | 1898 | newer

  0 0

   The Tanzania Portland Cement Company Limited (TPCC) TPCC Managing Director Pascal Lesoinne (second left) briefs members of the Parliamentary Standing Committee on Economic Affairs, Industries and Trade who visited the company’s plant at Wazo Hill in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the right is the Committee’s Chairman Mahmoud Mgimwa
   The Tanzania Portland Cement Company Limited (TPCC) TPCC Managing Director Pascal Lesoinne (second left) briefs members of the Parliamentary Standing Committee on Economic Affairs, Industries and Trade who visited the company’s plant at Wazo Hill in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the right is the Committee’s Chairman Mahmoud Mgimwa
   The Tanzania Portland Cement Company Limited (TPCC) TPCC Managing Director Pascal Lesoinne (second left) briefs members of the Parliamentary Standing Committee on Economic Affairs, Industries and Trade who visited the company’s plant at Wazo Hill in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the right is the Committee’s Chairman Mahmoud Mgimwa
  The Parliamentary Standing Committee on Economic Affairs, Industries and Trade Chairman Mahmoud Mgimwa stresses a point during the visit. 
  =======  =======  =======
  Local cement producers calls for proper payment of taxes and duties on imported cement

  LOCAL cement producers have called upon the Government to put in place measures that will ensure adequate payment of import duties and taxes on imported cement. This will help check influx of sub-standard imported goods entering the country including cement.

  Speaking to members of the Parliamentary Committee on Economic Affairs, Industry and Trade, the TPCC Managing Director Pascal Lesoinne who also doubles as the Chairman East Africa Cement Producers Association (EACPA) said the vice if not checked would lead to a complete collapse of blue-chip companies in Tanzania and associated loss to the local economy.

  “Many Tanzanian cement companies are currently facing stiff competition from imported cement especially from Pakistan. Worse still is that subsidies provided by exporting countries allow dumping of surplus cement into the Tanzanian market.
  “Importers of cement are utilizing loopholes in import and customs systems by under declaring and paying between 5-10 percent of import duty costing the country up to 25 billion shillings. The critical point for us is leveling of the playing field so we can compete favorably,” he said.

  He added that Tanzania does not need imported cement since there are many players to meet the country’s demand. Lesoinne during the occasion also decried fluctuation of electricity that has raised the company’s operation costs as the company has to spend up to $ 2 million per month to ensure steady supply of electricity at the firm.

  “The biggest challenge affecting our production is insufficient power supply. To ensure that our customers don’t suffer from interrupted supply, we have to pay up to $2million every month in running generators. He said the company that currently produces 1.3 million tons of cement per annum will be able to produce up to 2 million tons per annum after commissioning its new plant in October next year.

  He however cleared allegation that cement firms fix prices of the products saying this is baseless as cement companies compete favorably. “The issue of fixing prices does not completely exist. We are direct competitors so each company would like to enjoy the market leader status,” he added. The Kigoma South Constituency Member of Parliament David Kafulila during the occasion expressed concern on the unfair competition into the market urging relevant authorities to investigate deep into the matter.

  “This is a very serious matter. We as a committee cannot allow this to prevail as the vice directly impacts the country’s economic development process,” he said.
  The Director of Industries in the Ministry of Industry and Trade Eliness Sikazwe during the occasion said the Minister for Industry and Trade, Dr Abdallah Kigoda has already formed a seven member to investigate alleged subsidies, tax evasion and the quality of cement imported.

  “The committee has already been formed to investigate the matter and we expect to the committee to handover a detailed report once the process is complete which will be presented to the council of ministers for further discussion,” Sikazwe added.

  0 0


  0 0

  Padri Zenobius Mtewele akiongoza ibada ya kumbukumbu.
  Eric Shigongo akiwa katika maombi.
  Waumini wakifuatilia ibada.
  Mke wa marehemu, Asteria Bukumbi akipewa kumunio.
  Wanakwaya walioipamba ibada hiyo.


  Waumini wa Roman Catholic wakikomunika wakati wa ibada hiyo.
  Mzee Muhidini Gurumo (kulia) akipata chakula. Kushoto ni Juma Mbizo.
  Mtoto wa marehemu, Masha Bukumbi (kushoto) akiteta jambo.
  Waumini wakiendelea na ibada.
  Waalikwa wakijiandaa kwenda kupata chakula.
  Mmoja wa wahariri wa Global Publishers, Elvan Stambuli akiteta na padre aliyeendesha ibada hiyo.
  Padri akifunga ibada kwa sala.
  Shigongo akisalimiana na waalikwa.
  Padri akiagana na Masha Bukumbi mara baada ya ibada kumalizika.
  Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric James Shigongo na familia yake jana waliandaa kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa baba yao mzazi, Mzee James Bukumbi nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar. Marehemu Mzee James Bukumbi alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Agosti 26, 2012 jijini Dar es Salaam. Katika kumbukumbu hiyo, kulikuwa na ibada ambapo watu mbalimbali walijumuika na familia ya Shigongo.
  (PICHA NA HABARI: HARUNI SANCHAWA /GPL)

  0 0

  photo 2
  Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Kijasti’ (mwenye kijibegi mgongoni), akisaidiana na familia, ndugu, jamaa na marafiki kuteremsha zawadi kwa ajili ya watoto wanaoumwa saratani, Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Karibu na ‘Kijasti’ kulia ni ‘Mama Kijasti’. photo 3Baadhi ya watoto wanaotibiwa saratani, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, wakionesha uhodari wa kuchora wakati walipotembelewa na mradi wa Wafanye Watabasamu, unaoratibiwa na Nathan Mpangala, Jumamosi iliyopita. Watoto hao wapatao 80, walizawadiwa sabuni za kuogea/kufulia, dawa za meno, biskuti, toilet papers, mafuta ya kupakaa, matunda na vifaa mbalimbali vya kuchorea toka kwa marafiki wa mradi huo.photo 4Wachora vibonzo, Nathan Mpangala ‘Mtukwao’ wa ITV, (kulia) na Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’ wa Nipashe, wakichora na malaika wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye Watabasamu, hospitalini hapo. 
  photo 1Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano, SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, akiteta jambo na wachoraji nje ya Jengo la Watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, walipokutanishwa na mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, uliobuniwa na Nathan Mpangala. Mradi huo ulikwenda kuwafariji, kuwapa zawadi kisha kuchora na watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani hospitalini hapo, ikiwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia. Kutoka kushoto Gadi Ramadhan (Art director), Nathan Mpangala (ITV, Mratibu Wafanye Watabasamu), Said Michael ‘Wakudata’ (Tanzania Daima) na Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’ (Nipashe).  Mengi kuhusiana na mradi huu, 


  photo 5Rafiki wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni katunisti wa magazeti ya Mwananchi, Masoud Junior, akishuhudia umahiri wa kuchora toka kwa baadhi ya watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, juzi, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye Watabasamu.photo 6Ilikuwa jambo la kutia moyo kuona watoto hawa wanasahau maumivu ya saratani kwa muda na kujikita kwenye uchoraji. Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala, anawashukuru wachoraji wenzake, ndugu na marafiki wote waliochangia muda, sadaka na tabasamu kwa watoto hao.photo 7Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, (kushoto), yeye aliamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuungana na marafiki wa Wafanye Watabasamu, ili kuwafariji watoto waoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, juzi.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, leo Agosti 26, 2013. Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo Agosti 26, 2013 mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kabla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kushoto) kufungua kikao cha NEC, Agosti 26, 2013, mjini Dodoma leo.
   Baadhi ya wajumbe wa NEC, ukumbini. Kulia mstari wa mbele ni Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Viongozi wastaafu wa CCM, John Malecela ambaye ni mwalikwa kwenye kikao hicho.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally Nasoro Rufunga ametoa wito kwa wamiliki wa mashine za kuchambua pamba,kuanza kutengeneza nyuzi ili kuongeza thamani ya zao la Pamba katika kukabiliana na bei ya soko la dunia.

  Mheshimiwa Rufunga ametoa wito huo mwisho wa wiki alipotembelea kiwanda cha Afrisian kilichopo mjini Shinyanga, katika ziara yake ya kawaida ya kuona shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi.


  Amewashauri wamiliki wa mashine za kuchambua pamba kuboresha pamba hiyo ili kuzuia wawekezaji wa Kichina wanaojenga viwanda vya nguo hapa Shinyanga wasichambue pamba, badala yake wabaki na viwanda vya nguo na wanunue malighafi za nyuzi kutoka kwenye viwanda vya ndani ili kutodhoofisha viwanda vya Wazawa.


  Aidha, aliwahimiza wamiliki wa mashine za kuchambua pamba wajitangaze ili wananchi na wadau wafahamu shughuli wanazofanya,kwani wana mchango mkubwa kwenye pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla.


  Awali, Mkurugenzi wa Afrisian alimweleza Mkuu wa Mkoa changamoto zinazowakabili wenye mashine za kuchambua pamba kuwa ni bei ya pamba kushuka, na kutokuwa na mbinu bora za kisasa za kilimo hivyo kuzalisha pamba kidogo sana tofauti na nchi zingine.


  Magdalena Nkulu

  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa


  Shinyanga


  0 0


  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao
  cha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuu
  wa CCM Abdulrahman Kinana.
  BASHIR NKOROMO, Dodoma.

  HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemamliza kikao chake cha siku tatu chini ya  Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar,  Mansor Yusuf Himid.

  Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

  Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM, na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa Umoja wa Vijana wa CCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.

  Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.

  Pia, NEC imeridhia mapendekezo  ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro,  Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.

  Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha  Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).

  Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

  Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na  Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo Agosti 26, 2013 mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kabla ya Mwenyekiti wa CCm Rais Jakaya Kikwete (kushoto) kufungua kikao cha NEC, Agosti 26, 2013
   Baadhi ya wajumbe wa NEC, ukumbini. Kulia mstari wa mbele ni Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Viongozi wastaafu wa CCM, John Malecela ambaye ni mwalikwa kwenye kikao hicho.
   Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakiah Meghji kabla ya kikao cha NEC kuanza, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
   Mjumbe wa NEC, Dk. Fenela Mkangala na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakijadili jambo kabla ya kikao cha NEC kuanza leo Agosti 26, 2013, Makamo Makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Wajumbe wa NEC kutoka Pemba wakiwa nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza. Kutoka Kushoto ni Hamadi Bakari Ali, Mwinyi Fakih Hassan, Ali Issa Ali,  Masoud Mohammed Abdallah, Seif Shaaban Mohammed na Mussa Fumu Mussa.

  0 0

   Mkufunzi wa mafunzo ya kupiga picha yanayofanyika Jengo la ZBC, Karume House Mitsuhiro Hayao Matsuda kutoka Japan akitoa maelezo kwa washiriki   (hawapo pichani) kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
   Mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Habari Maelezo Yussuf Omar Chunda akifungua mafunzi ya miezi sita ya wapiga picha yanayofanyika jingo la ZBC, karume House Mnazimmoja akisisitiza jambo kwa washiriki.
   Mratibu  wa mafunzo ya kupiga picha  Faki Mjaka akitoa neon la shukrani kwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Jengola ZBC, Karume House.
   Washiriki wa mafunzo ya kupiga picha yanayofanyika Jengo la ZBC, Karume House wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi wa mafunzo ya kupiga picha, mkufunzi  na washiriki wa mafunzo hayo. (Picha zote na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar).
  ========  =====  =======
  Na Miza Othman - Maelezo Zanzibar    

  Washiriki wa mafunzo ya  kupigaji picha wametakiwa  kufuatilia kwa karibu mafunzo hayo na kumpa  ushirikiano wa karibu  mkufunzi  ili kutimiza lengo la kufanyika mafunzo hayo. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mstaafu wa Idaraya ya Habari Yussuf Omar Chunda wakati  akifunguwa mafunzo hayo katika  jengo la television, Karume House, Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

  Amesema lengo  la mafunzo hayo   ni kuwapatia taaluma zaidi watendaji wa kada ya habari ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi mkubwa zaidi. Amesema Serikali imeleta mtaalamu kutoka Japan  kutoa mafunzo ya upigaji picha na kuwajengea uwezo wapiga picha wa Taasisi za Serikali na binafsi ili kuwajengea uwezo mkubwa wapiga picha wa Zanzibar. “Iwapo mtafuatilia mafunzo hayo kwa ukaribu mtafaidika nyinyi wenyewe na kutoa picha bora katika magazeti mbali mbali ya hapa nchi na nje ya nchi,” alisema Chunda.

  Amewataka  washiriki wa mafunzo hao kuitumia vizuri nafasi waliyopata na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu mafunzo hayo na baadae kuyafanyikazi kwa faida yao na taifa kwa jumla. Mkufunzi wa  wa mafunzo ya upigaji picha Mitsuhiro Hayao Matsuda  kutoka Japan amewahakikishia washiriki  kwamba atafanya kila analoweza kuwajengea uwezo na utaalamu zaidi wa kupiga picha na kuwa wapiga picha bora.

  Mafunzo hayo ya miezi sita yanafanyika siku mbili kwa  wiki na yanashirikisha  waandishi  na wapiga picha kutoka Idara ya Habari, Shirika la Utangazaji (ZBC) Shirika la Magazeti Zanzibar, Vyombo vya Habari binafsi na wapiga picha wa kujitegemea waliopo Zanzibar.

  0 0

  SwahiliRadio inapatikana Duniani kote kutokea katika mtandao, katika Kompyuta aina zote, katika simu za mkononi za iOS - iphone,ipad,ipod, Android Samsung, LG, Pia katika Blackberry,Tablet aina zote. Ni rahisi kabisa kutupat.coma ingia katika blog yetu www.swahilitv.blogspot.com
  MAELEZO JINSI YA KUTUPATA KWENYE SIMU ZA MIKONONI
  1. Download Tunein (Tunein ni neno moja usiache nafasi) Tunein Radio app kwa simu yako mfano; iphone, ipad,ipod,android au Blackberry
  2. Baada ya ku-download , open app na nenda kwenye browser  na andika neno swahili radio kisha search.
  3. Ukiona logo yetu ya swahili radio bofya na sikiliza.

  TUNAPATIKANA HEWANI MASAA 24 TUKIWATANGAZIA KUTOKA JIJINI WASHINGTON D.C. TUKIWA KATIKA MAJARIBIO  0 0


  Afisa Mwandamizi Chakula na Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Bw. Onesmo Omella akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu matumizi bora ya mtama na jinsi unavyosaidia kuboresha lishe kwa mlaji, katika  mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) Jijini Dar es Salaam leo.  Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.(PICHA NA FATMA SALUM - MAELEZO).
  ======   =====  =======


  SEHEMU YA KWANZA


  1. UMUHIMU WA CHAKULA


  Chakula ni muhimu kwa maisha ya binadamu, kinamuwezesha kupata nguvu na virutubishi ambavyo husaidia kuujenga mwili na vile vile kuupa mwili kinga inayosaidia kujikinga dhidi ya maradhi mbali mbali.


  Kuna aina mbali mbali za vyakula ambavyo pia vina kazi tofauti mwilini na vina virutubishi tofauti tofauti, hivyo, mtu anatakiwa kula vyakula vya aina mbali mbali kwani aina moja ya chakula haiwezi kuwa na virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini. Virutubishi vina kazi maalumu mwilini na hii huwezesha mfumo wa mwili kufanya kazi vizuri.


  Vyakula vimegawanyika katika makundi mbali mbali kulingana na kazi za vyakula hivyo mwilini. Hata hivyo, vyakula vilivyo katika kundi moja huweza kuwa na aina viwango tofauti vya virutubishi na wakati mwingine hata aina ya virutubishi vilivyomo. Kwa hali hiyo basi, mtu anatakiwa kula mchanganyiko wa vyakula mbali mbali ili kuweza kupata virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini.


   Mlo wenye mchanganyiko wa vyakula vyenye virutubishi vya aina zote, huitwa “mlo kamili”. Mlo kamili ni muhimu sana hasa kwa watoto, ambao huwasaidia kukua vizuri na kuwa na afya njema. Mlo kamili humwezesha mtu kujikinga na madhara ya maradhi mbali mbali kama vile malaria, surua, kuharisha, shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo na hata ukimwi.


  Mlo kamili na wa kutosha hutoa virutubishi kama vile protini, vitamini, madini na nishati. Vile vile mlo kamili ni muhimu kwa wazee na wagonjwa katika kujenga mwili, na kusaidia uponaji wa majeraha, na kupata nguvu baada ya kukabiliana na maradhi.
  1.1. Mgawanyo wa vyakula


  ·        Vyakula vyenye wanga

  Hivi ni muhimu katika kuupa nguvu mwili za kufanya kazi mbali mbali. Vyakula vyenye wanga ni pamoja na: nafaka, kama mahindi, mchele, ngano, mtama, ulezi, uwele na kadhalika. Wanga pia hupatikana katika mihogo, viazi vitamu, viazi ulaya, viazi vikuu, magimbi, ndizi, miwa na asali. 


  Protini ni muhimu sana katika kujenga mwili na kuwezesha ukuaji wa mwili hasa kwa watoto na pia husaidia kutengeneza kinga ya mwili. Vyakula vyenye protini ni pamoja na: nyama, (ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata, samaki, mayai, maziwa na kunde, maharage, soya, dengu, choroko, njegere, mbaazi, na  njugu mawe.


  Vyakula vyenye mafuta huleta joto mwilini, na vile vile huleta nguvu mwilini na kulinda  na kulainisha ngozi na pia utando (membrane). Mafuta hutokana na mimea na huwa yanauzwa madukani kama vile, mafuta ya karanga, alizeti, nazi, ufuta, korosho, mawese, mbegu za maboga, mbegu za pamba.


  Matunda na mboga mboga ni muhimu sana katika mwili, kwa vile vyakula hivi vina vitamini na madini mbali mbali ambayo ni muhimu mwilini. Vitamini na madini huhitajika kwa kiwango kidogo sana lakini ni muhimu kwa mwili kuweza kufanya kazi zake vizuri. Upungufu wa vitamini na madini mwilini unaweza kusababisha hitilafu mbali mbali katika mwili na hata kusababisha kasoro zinazoambatana na  maradhi mwilini.


  Kuna vitamini mbali mbali ambazo ni Vitamini A, Vitamini B, Vitamini C, Vitamini, D na nyinginezo.

  ·       Vitamini A.

  Vitamini A ni muhimu katika ukuaji hasa kwa watoto na utengenezaji wa chembe chembe za mwili (cells). Husaidia kuongeza kinga mwilini na kuwezesha macho kufanya kazi vizuri.  Vitamini A ni muhimu katika kutunza ngozi.


  Vitamini A, hupatikana katika matunda Na mboga mboga zenye rangi ya machungwa Na manjano, Kama vile karoti, viazi vitamu vya manjano, maembe, na nyanya. Pia hupatikana katika mboga za majani, maini na maziwa.


  Ni za aina mbali mbali, husaidia kuzuia magonjwa mbali mbali Kama pellagra, inayosababisha ngozi kubabuka hasa katika zile sehemu zinazopigwa Na jua, chakula kushindwa kusagika vizuri na hata kusababisha kuharisha. Ukosefu wa vitamin B unasababisha beriberi, ugonjwa unaofanya mtu anapungua uzito, moyo unaweza kuwa mkubwa, miguu kuvimba na kujaa maji. Ukosefu wa vitamini B pia unaweza kusababisha midomo kupasuka, na dalili nyinginezo mbali mbali.


  Hupatikana katika mboga za majani kama vile spinach, mchicha, matembele na kadhalika.


  Vitamini C ni muhimu mwilini, husaidia ukuaji, kuongeza kinga mwilini na kusaidia mwili kutumia madini ya chuma.


  Hupatikana katika machungwa, limao, machenza, mananasi na mboga za majani ambazo hazikupikwa mpaka kuiva sana.


   Ni muhimu katika kuufanya mwili utumie madini ya chokaa ambayo husaidia katika utengenezaji WA mifupa Na meno, pia husaidia kuimarisha moyo na mishipa ya fahamu.


  Vitamin D hupatikana katika vyakula Kama mafuta ya samaki na maini. Pia hutengenezwa katika ngozi kutumia mionzi ya jua.  ·        Madini

  Haya ni muhimu katika utengenezaji wa chembe chembe za damu ambazo ndizo hubeba hewa ya oksijeni na kuisafirisha mwilini. Mwili huweza kutumia madini ya chuma Kwa ukamilifu Kama kuna vitamini C ya kutosha.


  Madini ya chuma hupatikana katika nyama,( ng’ombe, nguruwe, kondoo), mboga za majani kama mchicha.


  Hutumika katika utengenezaji wa mifupa na meno imara. Husaidia ugandaji wa damu, kama mtu ana jeraha ili kuzuia damu kuendelea kuvuja, na pia ni muhimu katika chembe chembe za mishipa ya fahamu. Madini ya chokaa hupatikana katika maziwa na mboga za majani.


  2.0. ZAO LA MTAMA NA MATUMIZI YAKE

  2.1. Uzalishaji wa mtama

  Mtama ni moja ya mazao ya chakula yanayo tegemewa sana hapa Tanzania.Mazao mengine ni mahindi, mchele, ngano, ulezi nk. Mtama una sifa ya ziada kwamba husitahimili ukame.

  Kwa vile sehemu kubwa ya nchi yetu ni kame na kwa kuwa nchi yetu haitumii kilimo cha umwagiliaji, kama nchi zilizoendelea zao la mtama linabaki kuwa ndilo mkombozi hasa wakati huu ambapo nchi inapo kabiliwa                                                                                                                                                                              na upungufu wa mvua

  Hapa nchini, mtama huzalishwa kwa wingi katika mikoa tisa (9); Dodoma, Singida, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Pwani, Mwanza, na Morogoro.

  Takwimu za uzalishaji wa nafaka nchini

  Takwimu hizi ni kwa nafaka tano (5) muhimu hapa nchini. Takwimu zinaonesha wastani wa uzalishaji wa nafaka hizi kwa nchi nzima (tani kwa mwaka)


  Aina ya nafaka

  Uzalishaji (tani kwa mwaka)

  Idadi ya mikoa

  Asilimia ya uzalishaji

  Mahindi

  2,393,000

  12

  64.8

  Mtama

  553,000

  9

  15.0

  Mpunga

  501,400

  10

  13.6

  Uwele

  172,100

  9

  4.6

  Ngano

  74,700

  4

  2.0

  JUMLA

  3,694,200

  -

  100.0

  2.2. Matumizi ya mtama:


  Kwanza ni budi tufahamu kuwa bidha bora za mtama hutokana na mtama uliotuzwa vizuri shambani, kuvunwa kwa wakati, kukaushwa, kusafishwa vizuri na kuhifadhiwa vema. Maandalizi yanayotakiwa kufanywa kabla ya kupika ni: Kupepeta na kupembua, Kukoboa, Kuosha, Kusaga kama unataka kupata bidhaa ya unga.

  Mtama una matumizi mbalimbali kama:

  ·        Chakula cha binadamu  (ugali,uji,kande,wali,pilau,ubwabwa,mikate,bisi na vyakula vya nyongeza vya watoto),

  ·        Chakula cha mifugo ( kuku, ngombe, au nguruwe)

  ·        Majani yake hutumika kutengeneza saileji.

  ·        Mtama hutumika kutengeneza vinywaji kama (togwa au pombe)

  ·        Unga wa mtama hutumika kuboresha vyakula vyenye upungufu wa protein kama muhogo.

  ·        Pia kimea cha mtama kinatumika kulainisha uji mzito wa mahindi, muhogo nk.unaotumika kuwalishia watoto wadogo

  Sifa za mtama

  Mtama una virutubisho muhimu vinavyotakiwa katika mwili wa binadamu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtama una kiasi cha wanga, nishati, nyuzi nyuzi, na mafuta karibu au sawa na mahindi au nafaka nyingine.


  Mtama una madini aina ya chuma na chokaa kwa wingi kuliko mahindi au nafaka nyingine. Una protini kwa wingi kuliko mahindi, mchele au ngano. Mafuta yake hayana rehamu, Una vitamin B complex, vitamin C  na vitamin E kwa wingi. Mtama una madini ya zinc, phosphorus, potassium, na manganese kwa wingi kuliko nafaka nyingine.


   Mtama una vimelea viitwavyo phenolica mbavyo ni mhimu sana kwa mwili kujikinga na saratani, Mtama hauna  gluten  hivyo ni  salama kutumiwa na watu wenye matatizo au ugonjwa  wa Celiac.


  Muhimu:Sukari yake huyeyuka taratibu sana mwilini hivyo mtama ni chakula kinachofaa kuliwa na watu wenye magonjwa kama kisukari.  3.0. USINDIKAJI

  3.1. Lengo la kusindika mtama

  Namna ya usindikaji wa mtama hutegemea sana aina ya matumizi inayokusudiwa.

  Usindikaji wa mtama (katika mazingira ya hapa nchini) hulenga kuzalisha mojawapo ya bidhaa nne (4) kuu;

  ·        Mtama uliokobolewa,

  ·        Chenga za mtama uliokobolewa,

  ·        Unga wa mtama uliokobolewa,

  ·        Unga wa mtama usiokobolewa.


  Zingatia kuwa kukoboa huondoa ganda la mtama ambalo kwa kawaida huwa na vikemikali-korofi (anti-nutritional factors) ambavyo hupunguza ufanisi wa ufyonzwaji wa viinilishe mwilini, hususan protini.


  3.2. Unga wa lishe wa mtama


  Mtama ni nafaka nzuri sana katika kutengeneza unga wa lishe. Majaribio yameonyesha kuwa unga wa mtama ukitumika kutengeneza vyakula vya kulikiza unatoa chakula laini ambacho pia kitoa ladha nzuri sana. Unaweza kutengeneza fumula nyingi za mtama na nafaka nyingine ukitumia mtama pekee au ukipunguza kidogo kiasi cha mahindi na kuongeza mtama.

  Baadhi ya Fomula za chakula cha lishe ni kama zifuatazo. Tunakukaribisha uzijaribu:

  Mahitaji:

  Mtama                        66%               (660g)

  Soya                                     20%                       (200g)

  Karanga                       5%          (50g)

  Sukari                          9%          (90g) .  4.0. MAPISHI MBALI MBALI YA MTAMA


  4.1. Pilau ya mtama


  Pilau ya mtama inaweza kutumika badala ya pilau ya mchele. Pilau hii inaweza kuliwa na wagonjwa au hata watu wazima, wakubwa na watoto bila shida yeyote. Inaweza kuliwa nyumbani au hata wakati wa sherehe. Mapishi yake yanaweza kuwa kama ilivyoonyeshwa hapo chini au ikapikwa kwa kutumia njia ya kawaida ya kupika pilau ya mchele kwa kutumia viungo vile ulivyovizoea.  Katika upishi huu mpya mahitaji yake ni kama ilivyoonyeshwa hapo chini.


  Mahitaji:

  ·        Kikombe kimoja cha mtama uliokobolewa

  ·        Kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia

  ·        Vikombe vitatu vya mchuzi wa kuku

  ·        Kijiko kimoja cha vitunguu cha vitunguu vilivyokatwakatwa na kukaushwa

  ·        Nusu kijiko cha majani ya viungo

  ·        Moja ya nane ya kijiko cha pilipili manga iliyosagwa

  ·        Robo kikmbe cha matunda yaliyokaushwa

  ·        Vijiko viwili vya giligilani mbichi

  ·        Chumvi kiasi

  ·        Robo kikombe cha korosho

  ·        Majani freshi ya pasle


  Jinsi ya kupika

  1. Safisha mtama katika maji safi na mwaga maji yote uliyosafishia

  2.Bandika sufuria la wastani jikoni na kwa kutumia moto kiasi wa wastani katika   jiko,  weka mafuta ya kupikia ndani ya sufuria na yakisha pata joto  weak mtama uliooshwa na koroga taratibu kwa dakika 2 -3 hadi rangi ya mtama ibadilike na kuwa brauni ya mbali.

  3. Ongeza mchuzi wa kuku, vitunguu, majani ya viungo, na pilipili na ongeza mooto kidogo hadi ianze kuchemka. Punguza moto, funika na acha iive taratibu kwa dakika 30 – 40 au hadi mchuzi umekaukia na mtama umelainka

  4. Ondoa motoni. Na changanya viungo vingine vyote vilivyobaki hapo juu Geuza vizuri hadi vichanganyike na kasha funika na acha katika moto mdogo kwa dakiak 5 ikibidi palia mkaa katika hatua hii.

  5. Gawa katika chombo cha kuipulia na pilau yako iko tayari kuliwa


  Kumbuka: Mtama uliopikwa unaweza kuliwa na vitu vingi kama vile nyama, samaki, maziwa na kadhalika. Ukiongeza korosho au karanga itaongeza ladha yake na kuufanya utafunike vizuri.


  4.2. Kande za mtama

  Kama ilivyo kwa pilau ya mtama, kande za mtama zinaweza kupikwa na kuliwa na mtu yeyote hasa wagonjwa wa kisukari. Kande zinaweza kuliwa na familia au wakati wa sherehe. Mapishi yake ni rahisi kama ilivyoonyeshwa hapo chini.
   Mahitaji:

  ·        Kikombe kimoja cha mtama uliokobolewa na kuoshwa

  ·        Vikombe 3 vya maji

  ·        Kijiko cha chumvi (kutegemeana na kiasi cha kande)

  ·        ¼ kikombe cha juisi ya limau

  ·        Vijiko 2 vya mafuta ya kupikia yaliyochemshwa na kuiva

  ·        Moja ya nane ya kijiko cha pilipili manga iliyosagwa

  ·        Tango moja lililokomaa lililokatwakatwa vipande vidogo

  ·        Vitunguu vitatu vya kijani

  ·        Pilipili hoho nyekundu 1

  ·        pasle iliyokatwakatwa

  ·        Chizi kidogo iliyopondwa pondwa ( kama ipo)

  Jinsi ya kupika

  1.                 Weka mtama maji na nusu kijiko cha chumvi katika sufuria na anza kupika huku ukikoroga

  2.                 Pika hadi ianze kuchemka. Funikia na punguza moto ili iive taratibu kwa dakika 30 – 40 au hadi maji yakaukie na mtama umelainika.

  3.                 Kama maji bado yamebaki, na mtama umeiva yaondoe kwa chujio.

  4.                 Changanya juisi ya limau, mafuta ya kupikia, chumvi iliyobaki na pilipili katika chombo chenye mfuniko. Tikisa sana hadi vichanganyike. Changanya katika mtama wako wa moto uliopika na geuza kwa kurusha rusha hadi vichanganyike. Weka chombo kwenye moto kiasi na juu funikia kwa moto kiasi. Acha iivie kwa dakika 5.

  5.                 Katakata kitunguu, pilipili hoho na itumike kulia kande zako kama kachumbari


  4.3.Maandazi ya mtama

  Maandazi haya hupikwa kwa kutumia unga wa ngano uliochanganywa na unga wa mtama kama ilivyoonyshwa hapo chini:

  Mahitaji:

  ·        Unga wa mtama gramu 200 au kikombe cha  chai

  ·        Unga wa ngano gramu 800 au vikombe 4 vya chai

  ·        Baking poda vijiko vya chakula 2

  ·        Hamira kijiko cha chakula 1

  ·        Mafuta ya kupikia kikombe cha chai 1

  ·        Sukari kikombe cha chai 1

  Njinsi ya kupika

  1.                 Changanya unga wa ngano na wa mtama na sukari na baking powder

  2.                 Weka mafuta yaliyochemka na changanya mpaka mchanganyiko uwe mzuri

  3.                 Weka hamira na changanya vizuri

  4.                 Weka maji na finyanga mpaka mchanganyiko uwe tayari

  5.                 Acha iumuke kwa saa moja

  6.                 Finyanga tena na kata mtindo unaotaka

  7.                 Kaanga kwenye mafuta yaliyochemka hadi yawe ya rangi ya kahawia

  8.             Epua tayari kwa kuliwa.


  4.4.Mkate wa unga mchanganyiko

  Mkate huu hupikwa kwa kutumia unga wa ngano uliochanganywa na unga wa mtama kama ilivyoonyshwa hapo chini:

  Mahitaji:

  ·        Unga wa mtama kikombe 1 cha chai

  ·        Unga wa ngano vikombe 4 vya chai

  ·        hamira vijiko viwili vya chakula

  ·        Chumvi kijiko 1 cha chai

  Njinsi ya kupika:

  1.                 Changanya aina zote mbili za unga

  2.                 Weka chumvi na hamira

  3.                 Finyanga kwa kutumia maji vuguvugu mpaka mchanganyiko uwe laini

  4.                 Acha uumuke kwa saa moja

  5.                 Finyanga tena na tengeneza muundo unaoutaka

  6.                 Acha uumuke kwa dakika 15

  7.                 Oka kwenye moto mdogo hadi uive

  8.                 Epua tayari kwa kuliwa.  4.5. Biskuti za chokleti


  Mahitaji:

  ·        Kikombe:          ¾ unga wa mtama

                                                      ½ unga wa ngano

                                                      ¼ wanga wa viazi

                                                      ¼ siagi (blue band)

                                                      1 sukari

                                                      ¼ karanga zilizovunjwa

                                                      1 vipande vidogo vya chokoleti

  ·        Kijiko kidogo cha chai:

                                                      ½ baking powder

                                                      ¼ chumvi

                                                      2 vanilla

  Yai 1 kubwa.

  Jinsi ya kupika:

  1.     Washa jiko lako na liache liwe na moto mkali. Changaya unga, baking powder, na chumvi kasha weka pembeni. Paka mafuta kwenye chombo chako cha kuokea na weka pembeni.

  2.     Kwenya bakuli kubwa piga piga siagi, sukari, vanilla, na yai mpaka mchanganyiko uwe mzito na uliochanganyika vizuri. Changanya mchanganyiko wa unga na endelea kuchanganya taratibu mpaka umechanganyika kabisa. Korogea vipande vidogo vya chokoleti. Mchanganyiko utakuwa mzito.

  3.     Dondosha katika kiokeo vijiko 12 vya chai vilivyo jaa mchanganyiko katika umbali wa kama nchi mbili kutoka katika kila kimoja.

  4.     Oka kwa kati ya dakika 10 na 12 katikati ya jiko mpaka viwe brauni kiasi. Weka pambeni kwa dakika 2 hadi 3 vipoe kabla ya kutoa kwenye kiokeo.


  Rudia namba 3 na 4 hadi mchanganyiko wote uliobaki uishe. Unatarajia kupata biskuti 24 kwa mchanganyo huu.


  4.6.Keki ya unga mchanganyiko wa mtama


  Mahitaji:


  ·        1/3 ya kikombe cha siagi 

  ·        Kikombe 1 cha sukari

  ·        Mayai 2 makubwa

  ·        Kijiko kikubwa cha maganda ya limau yaliyokunwa

  ·        Kikombe 1 cha unga wa mtama

  ·        1/3 ya kikombe cha wanga wa viazi

  ·        Vijiko 2 vikubwa vya unga wa muhogo

  ·        Robo kijiko cha baking poda

  ·        Robo kijiko ya baking soda

  ·        Robo ya kijiko cha chai ya chumvi

  ·        ¾ kikombe cha maziwa

  ·        kijiko kimoja cha chai cha vanilla
  Jinsi ya kupika

  1       Washa oveni na subiri joto lifikie 160oC. Paka mafuta ya kutosha kwenye kikaango cha kuokea keki. Viache vitulie.

  2       Kwa kutumia miksa ya umeme na bakuli kubwa la kuchanganyia, changanya Blue Band, sukari na mayai kwa kutumia mwendo (speed) wa kati hadi vichanganyike vyema. Ongeza maganda ya limau.

  3       Katika bakuli la ukubwa wa kati, changanya unga wa ngano, “baking powder”,“baking soda”, na chumvi. Changanya maziwa na vanilla katika kikombe cha kupimia. Kwa kutumia miksa katika speed ya chini, changanya viungo vikavu kwenye mchanganyiko wa mayai, ukibadilishana na maziwa (mayai...maziwa...mayai...) ukianzia na kumalizia na viungo vikavu. Changanya hadi vichanganyike sawa sawa. Kwa kutumia kijiko, weka siagi kwenye kikaango (au vikaango, kutegemea kiasi ulichonacho).

  4       Oka keki kwa muda wa dakika 20 hadi 40 kutegemea ukubwa wa kikaango, au hadi sehemu ya juu ya keki iwe rangi ya kahawia iliyoiva (golden brown) au hadi “toothpick” inapochomekwa juu katikati ya keki itoke ikiwa safi. Iache keki ipoe kwa dakika 5 kisha itoe kwenyye kikaango na iache ipoe vizuri. Ikate keki na kuwahudumia watu 12.  


  NINI KIMEFANYIKA

  Taasisi ya chakula na Lishe kwa kushirikiana na chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine, imekuwa ikiendesha mafunzo ya usindikaji wa vyakula ikiwa ni pamoja na zao la mtama katika sehemu mbalimbali za nchi yetu.Mafunzo haya yamekuwa yakiwalenga zaidi akina mama walioko kwenye vikundi.Mpaka sasa tumetoa mafunzo kwa vikundi 17 kama ifuatavyo: Daresalaam (2) Morogoro (1) Dodoma (1) Arusha (1) Pwani (6) Iringa (4) Mwanza (2) na Mtwara (1)

  Lengo la Taasisi ni kuendesha mafunzo haya katika kila mkoa hususani mikoa inayozalisha mtama kwa wingi.  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi Ikulu jijini Dar es salaam leo. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano  ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
   Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
   Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
   Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
   Watalaamu wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka Afrika Kusini wakimueleza Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha mabomba hayo
   Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage, wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akizungumza na baadhi ya vibarua  wa kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage, wilayani Rufiji, Pwani.
   Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
   Mmiliki wa blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda naye akiwa katika ziara hiyo eneo la Nyamwage, Rufiji.
   Kambi ya wafanyakazi wa kamapouni ya kichina eneo la Mkuranga, Dar es Salaam
   Waandishi wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama, zilizokuwa kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani Mkuranga, Pwani
  Baadhi ya mitambo ikiwa imefungwa wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya kuongezea unene wa mabomba maalumu ya gesi yatakayotandazwa baharini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

  0 0


  Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel amkimkabidhi  vitabu mwanafunzi Charles Costantino ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya Shule ya Msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mollel alikabidhi vitabu 30 vyenye thamani ya sh. 300,000. Wanaoshuhudia ni Miss Ilala namba mbili Alice Issack (wa tatu kushoto), mshindi wa tatu Clara Bayo (wa pili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rehema Mketo.


  Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel akiwa na wanafunzi baada ya kukabidhi msaada wa vitabu  30 vyenye thamani ya sh. 300,000 kwa Shule ya msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Wanafunzi wakifurahi pamoja na wanafunzi
   Mshindi namba tatu Clara Bayo akizungumza na mmoja wa wanafunzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Mollel akimkabidhi zawadi shs. 5000 mwanafunzi aliyejibu swali walililoulizwa wanafunzi.
   Mamis wakiwa katika piacha ya pamoja na wanafunzi pamoja na mwalim mkuuu.

   Warembo wakiwa na mwalimu wa shule hiyo, Lugano Mwaikambo ambaye aliwahi shiriki Miss Morogoro mwaka 2000.
   Warembo wakicheza michezo mbalimbali na wanafunzi wa shule hiyo  Warembo wakiondoka shuleni hapo

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi na Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu Mhe John Tendwa baada ya kumuapisha Jaji Mutungi Ikulu jijini Dar es salaam leo.PICHA NA IKULU

  0 0

  Picture: Grace Mbowe
  DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

  Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

  Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.

  Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za 
  kuwadanganya wananchi.

  Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

  “Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.

  Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”

  “Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.
  Picture: Grace Mbowe, Hassan Mtenga
  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
  Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

  Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

  Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

  Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea. Source HabariLeo

  0 0


  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kulia na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakikabidhi Betri za kampuni hiyo kwa  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'EmerGency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kwa ajili ya magari ya kitengo hicho Dar es salaam leo kushoto ni Kaimu Dereva Mkuu Sultan Kitanga na Mkuu wa Idara ya Ufundi ENG,Leonard Elizeus
  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kushoto na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakishusha betri walizopeLeka Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kwaajili ya Msaada katika Kitengo Cha Dharura.
  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kulia na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakishusha betri walizopeleka Muhimbili kwaajili ya msaada katika kitengo cha Dharura
  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kushoto na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya maofisa wa kitengo hicho
  Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru Rashidi akikagua betri hizo baada ya kukabidhiwa
  Baadhi ya Madereva wa kitengo hicho wakikagua
  Baadhi ya wahudumu wakiendelea na shughuli zao katika gari la wagojwa kushoto ni Nikijaeli Ngareni na Josephine Lazaro
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharurua  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kushoto akibadilishana namba za mawasiliano na  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza Na Mwandishi Wetu MRATIBU wa Masoko wa Kampuni ya Chloride Exide Bw, Robert Hiza leo ametoa msaada wa Betri mbili katika kitengo cha Emergency Medicine ya hospitali ya Taifa Muhimbili . 

   Msaada huo wa kwanza kutoa inaendana na miaka 50 ya kampuni hiyo ambapo watatoa viti mbalimbali katika hospital za Serikali vikiwemo Sola kwa ajili ya umeme wa jua . Akipokea msaada huo.Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo amewashukuru kampuni ya Chloride Exide kwa kuliona hilo kwani ni mara ya kwanza katika kitengo chao kupokea msaada kama huo, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali ikiwemo hata magari kama yapo tunaomba msaada maana hapa kitengo chetu ni cha mambo ya dharura na kinategemewa sana kama mnavyojua alisema Prof Victor Mwifongo Nae  Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru Rashidi amendelea kutoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuliona hilo kwani yeye kama Dereva ameona ni jambo bora sana

  0 0

  Afisa mauzo wa kanda ya ziwa Mohamed Kabeke akikabithi vitabu Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba, akishuhudia ni Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi. 
  Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha vitabu vya ada na kiada wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba.

  Airtel Tanzania imeendelea na mradi wake wa kusambaza vitabu katika shule ya Sekondari nchini chini ya mradi wa ‘Shule yetu’ ambapo shule mbalimbali za sekondari nchini zimenufaika na mradi.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema kampuni ya Airtel inaendelea kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu nchini hasa tatizo la vitabu vya kiada kwa shule za sekondari. Kupitia mradi wa ‘Shule yetu’ watoto wengi wa kike watanufaika kwani mradi huu unalenga hasa katika kumkwamua mtoto wa kike kutoka katika ujinga, umaskini na maradhi,”

  Hawa aliongeza kwa kusema Leo tunatoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Bwelanyake hapa Karagwe Bukoba ikiwa ni mwendelezo wa shughuli zetu za kijamii katika kupambana na tatizo la vitabu mashuleni. Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi wa shule ya Bwelanyake kupata nafasi ya kujifunza na kujisomea na kuwawezesha walimu kupata nyenzo muhimu za kufundishia.

  Kwa upande wake Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha alisema “elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kushirikiana na Serikali kupunguza tatizo la vitabu vya kiada vya shule za sekondari hapa nchini.

  Tunaamini msaada huu wa vitabu tulioupata leo utasaidia katika kuinua kiwango cha ufaulu na kuongeza taaluma zaidi kwa wanafunzi wetu na kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi hapa shuleni. /Nachukua fursa hii kuwaomba wanafunzi wavitumie fursa hii kujisomea na wavitunze vitabu hivi ili viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi na kutoa matunda bora na mengi zaidi.

  Mpaka sasa Airtel kupitia mradi huo imewafikia shule takribani 900 za sekondari nchi nzima kwa kuzipatia vitabu vya kiada hasa kwenye masomo ya Fizikia, Hisabati, kemia na Biolojia. mradi huu wa Shule yetu unasambaza vitabu kwa shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na vitabu vya walimu kwa ajili ya kufundishia.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa kamati kuu wa kubatilisha kufukuzwa kwa madiwani wa Bukoba nje ya ukumbi wa NEC.


  TAARIFA KWA UMMA

   Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.   Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao. Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.   Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-  “Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.   Aidha, Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani katika Manispaa na Chama.

  Kamati Kuu pia imeitaka Serikali kumwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali(CAG) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yasilishwe kwenye baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.

  Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM  kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba.

  Imetolewa na:-
  Nape Moses Nnauye,
  KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
  ITIKADI NA UENEZI
  27/08/2013

  0 0

   Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwasili mbele ya jengo la PPF huku akipokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akipewa shada la maua na Afisa Habari Mkuu Idara ya Habari, Bi. Mwanakombo Jumaa kama pongezi kwa kupewa cheo cha Katibu Mkuu.

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akilakiwa kwa shangwe na Mkurugenzi rasilimali watu Bw. Titus Mkapa wakati wa hafla ya kupokelewa na kukabidhiwa kiti cha Unaibu Katibu Mkuu leo jijini Dar es Salaam.

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akipewa mashada ya maua baada ya kupokelewa na wafanayakazi wa Wizara ya Habari kama pongezi ya kupewa cheo cha Unaibu. 
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) aliyesimama katikati Bw.Clement Mshana, kulia kwake ni Kaimu Mhariri Mtendaji Mkuu wa TSN Bw. Gabriel Ndelumaki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ndg. Habari Assah Mwambene.

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akisalimiana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo wakati alipolakiwa na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozana kwa pamoja kuelekea ofisini.

   Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

  Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda akitoa hotuba fupi ya kukabidhi cheo kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani). PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

  0 0

  Na Miza Othumani na Ali Issa - Maelezo Zanzibar

  Msanii chipkizi wa michezo  ya kuigiza hapa Zanzibar  Mussa Salum Maarufu kwa jina la Mr. Mudi amewaambia wapenzi wake wakae tayari mkao wakula kwa kuwaletea igizo kabambe jipya lijulikanalo kwa jina la “SALUTI’’  mchezo ambao ni wakusisimuwa na wenye mvuto kwa watazamaji.

  Amesema igizo hilo linatarajiwa kurushwa hewani  Septemba 15 mwenzi ujao kupitia ZBC TV, Zanziba Cabor TV na Coconurt TV.

  Hayo ameyaleza  leo huko Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wakati alipokutana na muandishi wa habari ofisini hapo akihojiwa muelekeo na hatima ya utzi katika fani ya usanii. Amesema bado yumo katika fani ua utzi na sasa ametunga amachezo mpya utakao kua hewani hivikaribuni kwa kuwapa  burudani safi mashabiki na watamazaji wake  ili wasije kuona MR. Mudi ametoweka. “Nipo mudi na tuna tarajia kutoa kitu kipya chenye  jina la ‘SALUTI” alisema Mr.Mudi.  

  Msanii huyo alisema igizo la filamu ni gharama na itachukuwa muda mwingi kwa wasanii wa Zanzibar kupata maendeleo kwani hadi sasa fani ya usanii Zanzibar thamani yake ni kupendwa mchezo na wasanii wake lakini sio kuwafadhili wasanii kuwapa matumaini ya maslahi katika maisha yao.

  “Zanzibar waliaza mwazo kiusanii lakini sasa wamekuwa wamwisho kulinganisha na wezetu wa bara na hahii inatokana wasani wa Zanzibar kukosa wafadhili hivyo inatutaza kwetu kupata maendeleo ”aliongeza kusema MR.Mudi.

  Msanii huyo alieleza  changamoto zinazo wakabili katika kampuni yake ikiwemo kutokuwa na Ofisi ya kufanyia kazi zake, upungufu wa Vifaa vya kisasa vya kurikodia michezo  na halingumu inayowakabili ya kimaisha.

  Amesema pamoja na yote hayo hawatorudi nyuma kutowa burudani ya maingizo kwa wananchi wa Zanzibar kwani anaamini iko siku moja ukata utaondoka kwao, kwani lengo lao limefahamika kwa jamii na serikali kwa ujumla kwa kutoa elimu inayo faa katika maadili yao.

  “Tume pongezwa sana Jeshi la polisi Wizara za Serikali kutokana na burudani tunayo yenye mafunzo yalio kubalikaa”alisema Msanii huyo.

  Msanii huyo akitowa malalamiko yake amesema wasanii wa Zanzibar hawapewi kipaumbele kama walivyo wasanii wengine kwa kupata wadhamini na kuwatangaza kupitia vyombo vya Habari kwa kuwambatanisha na Matangazo na wao ili kupata kitu kidogo jambo ambalo lina rudisha nyuma juhudizao.

  Aidha alivilalamikia vyombo vya Habari kwa kuwacheleweshea kuwalipa kiyasi cha pesa walicho kubalianapale wanapo onesha michezo yao.

  Hata hivyo  Msanii huyo alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohmed Shein kwa hutuba yake Nzuri  aliyoitowa mwazoni mwa mwaka huu wakati wa ufunguzi  wa jingo jipya  la Utamaduni Rahaleo Studio kwa kusema wasanii waenziwe na wapewe kipaumbele katika kazi zao kwani zinatowa mchango kwa Taifa na burudan.

  “Tungefurahi siku moja Mh. Rais akatwita na sisi wasanii kuwenae karibu na tukazungumza yetu kwani kazi ya usanii Zanibar kunahatari kuporomoka chini, na haitokuwa vyema kuporomoka kazi hii hasa ukuzingatia hutuba yake aliyo itowa wakati wa ufunguzi wa jingo la Utamaduni.older | 1 | .... | 146 | 147 | (Page 148) | 149 | 150 | .... | 1898 | newer