Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 144 | 145 | (Page 146) | 147 | 148 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Akina mama wa Kilombero wakiandaa mlo kwa ajili ya timu za Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakati wa ufungaji pampu katika moja ya visima Wilaya ya Kilombero, Morogoro, uliofanyika hivi karibuni. Zaidi kuhusu mradi huu  bofya; www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA. (Picha zote na Nathan Mpangala wa HUC).
   Mtoto toka Kilombero, akifuatilia ufungaji pampu katika moja ya visima 59 uliofanywa na timu za Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, hivi karibuni.
   Haya twende! Timu ya Help for Underserved Communities (HUC) ikishirikiana na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakichimba moja ya visima 59 Wilaya ya Kilombero, Morogoro, huku wakiangaliwa kwa shauku na watoto hivi karibuni. HUC ni asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayochimba visima kwa kushirikiana na jamii kusaidia upatikanaji wa maji ya kunywa safi na salama mashuleni, vijijini na jamii kwa ujumla. Zaidi, bofya; www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA.
   Timu ya Help for Underserved Communities (HUC), ikishirikiana na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakifunga pampu katika moja ya visima 59 Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Tanzania huku wakifuatiliwa kwa shauku na watoto hivi karibuni.
   Wachimba visima toka Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., kama walivyokutwa na kamera yetu Wilaya ya Kilombero, Morogoro, wakati wa uchimbaji visima vya msaada uliotolewa na taasisi hizo hivi karibuni. Zaidi bofya; www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA
   Wakaazi wa Kilombero wakichota maji toka katika moja ya visima 59 vilivyochimbwa na Help for Underserved Communities (HUC)/Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Tanzania, hivi karibuni.
   Wakazi wa Kilombero wakiangalia kisima kilichochimbwa na Help for Underserved Communities (HUC) kwa ushirikiano na Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, hivi karibuni. Zaidi kuhusu HUC,www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA.
   Uchimbaji ukiendelea. Zaidi kuhusu mradi huu, bofya; www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA. (Picha zote na Nathan Mpangala wa HUC)

  0 0

   Msanii wa Muziki wa kughani Mashairi, Mrisho Mpoto,akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media Group muda mfupi baada ya kumaliza kutoa soma la Kamata Fursa Twenzetu ndani ya ukumbi wa Chuo cha fursa ya chuo cha utumishi wa umma mkoani Tabora mapema leo.
   "Mnanionaaaa.."! Mpoto akiwa amembeba mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho mara baada ya kumuomba apige naye picha ya kumbukumbu.
   Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wakiwa wamejitokeza kwa wingi wakitaka kupiga picha na Mrisho Mpoto mapema leo.
   Wanafunzi hao pia walipata fursa ya kupiga picha na Mpoto.
   Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza mafunzo ya Kamata Fursa Twenzetu katika chuo hicho.
   Mpoto akitoa somo kwa wanafunzi hao mapema leo katika ukumbi wa Chuo hicho.
    Somo la Mpoto liliambatana na mifano hai ambayo ilikuwa ikiwasisimua vilivyo Wanafunzi hao.
  Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Power Break fast Gerald Hando naye alipata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi hao kuhusiana na mpango mzima wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linalotarajiwa kufanyika kesho jioni kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi,aidha pia alibadilishana nao mawazo na  namna ya kutumia fursa mbalimbali wazipatazo katika masoma yao.

  0 0

  Na Amina Abeid-ZJMMC .

  Jumla ya Shilingi Bilion 1.4 za Kitanzania zinatarajiwa kutumika kukamilisha zoezi la Kitaifa la Utambuzi na Usajili wa Ardhi ambalo limeanza rasmi katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

  Zoezi hilo linagharamiwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Finland iliyochangia Shl. Bilion 1 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyochangia Million 400 chini ya Mradi wa Usimamizi endelevu wa Ardhi na Mazingira Awamu ya Pili (SMOLE 11)

  Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Kikwajuni Mkurugenzi wa Ardhi na Usajili Zanzibar  Januari Fusi amesema Usajili wa Ardhi hauhitaji malipo yoyote bali kinachohitajika ni Vielelezo muhimu katika zoezi hilo.

  Amevitaja vielelezo hivyo kuwa ni Kitambusho cha Mzanzibari au Pasi ya kusafiria pamoja na Cheti cha kuzaliwa kwa Mmiliki wa eneo linalohitaji kutambuliwa kisheria.

  Amefahamisha kuwa Mradi wa Smole 2 ulikuwa ni Mradi wa Miaka 4 ulioanza Mwaka 2010 na kutegemewa kumalizika mwaka 2013 lakini kutokana na kutokukamilika Serikali ya Zanzibar na Finland zimekubaliana kuongeza mwaka mmoja hadi Disemba 2014.

  Amesema lengo kuu la kuongeza mwaka ni kuhakikisha Utambuzi na Usajili wa Ardhi katika maeneo yote unafanyika ili kuondoa migogoro ya Ardhi iliyodumu kwa muda mrefu Zanzibar.

  Ameongeza kuwa Zoezi hilo litaongozwa na Ofisi mbili zilizopo chini ya Idara ya Ardhi na Usajili ambazo ni Ofisi za utambuzi wa Ardhi Unguja na Pemba na Ofisi ya Mrajisi wa Ardhi Zanzibar.

  Ameyataja maeneo ambayo zoezi la Utambuzi limeanza kuwa ni pamoja na Nungwi, Jendele, kwa Ali Nathoo na Paje kwa upande wa Unguja ambapo kwa Pemba zoezi hili litaanza kwa Shehia za Selem, Wara na Uweleni.

  Kwa upende wake Afisa Mtambuzi na Msajili wa Ardhi Shawana Sudi Khamis amewataka Wananchi watoe mashirikiano ya kutosha katika maeneo yao ili kulifanya zoezi hilo liweze kufanikiwa kama lilivyopangwa.

  Ametaja baadhi ya faida zinazopatikana kwa kupitia zoezi hilo kuwa ni pamoja na kumuwezesha Mmiliki wa Ardhi kuwa na Ardhi Salama iliyothibitishwa na mamlaka rasmi za Serikali.

  Itakumbukwa kuwa zoezi la Usajili na Utambuzi lilizinduliwa Rasmi Machi 28, 2013 ns Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Dkt ALI Mohamed Shein ambapo alipokea hati ya kwanza ya usajili wa Ikulu ya Zanzibar katika sherehe iliyofanyika Viwanja vya Viktoria Garden.

  Utambuzi na usajili wa Ardhi ni hatua moja wapo ya kutekeleza Mkakati wa kupunguza umasikini Zanzibar  awamu ya pili ambao umeweka lengo la kusajili asilimia 50% ya ardhi ya Zanzibar ifikapo mwaka 2015.

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR .

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu, Balozi Ombeni Sefue, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Agosti 21, 2013, alitangaza orodha ya Makatibu Wakuu wapya.
  Ifuatayo ni orodha ya makatibu hao, kama ilivyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

  UTEUZI WA NAIBU MAKATIBU WAKUU WAPYA NA UHAMISHO WA BAADHI YAO
  1.      Bibi Angelina Madete, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira.
  2.      Bibi Regina L. Kikuli, Ofisi ya Waziri Mkuu.
  3.      Bw. Zuberi M. Samataba, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu).
  4.      Bw. Edwin K. Kiliba, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
  5.      Bw. Deodatua Mtasiwa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya).
  6.      Dkt. Yamungu Kayandabila, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
  7.      Prof. Adolf F. Mkenda, Wizara ya Fedha (Sera).
  8.      Bibi Dorothy S. Mwanyika, Wizara ya Fedha (Fedha za Nje na Madeni)
  9.      Bibi Rose M. Shelukindo, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
  10.  Dkt. Selassie D. Mayunga, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  11.  Bibi Monica L. Mwamunyange, Wizara ya Uchukuzi.
  12.  Bibi Consolata P.M. Mgimba, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
  13.  Prof. Elisante ole Gabriel Laizer, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
  14.  Bw. Armantius C. Msole, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


  UHAMISHO
  1.      Bw. John T. J. Mngodo anatoka Wizara ya Uchukuzi kwenda Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
  2.      Bw. Selestine Gesimba anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii.
  3.      Eng.Ngosi C. X. Mwihava anatoka Ofisi ya Makamu wa Rais na kuhamia Wizara ya Nishati na Madini.
  4.      Bibi Maria H. Bilia anatoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kuhamia Wizara ya Viwanda na Biashara.
  5.      Bibi Nuru H. M. Milao anatoka Wizara ya Maliasili na Utalii na kuhamia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Barclays kitengo cha wateja binafsi Bw.Musa Kitoi akitoa maelekezo kwa  washindi wa droo ya tatu ya maisha bomba na Barclays Golden Briefcase katika halfa ya kuwakabidhi zawadi washindi hao iliyofanyika katika tawi la Kinondoni leo jiji Dar es salaam .
    Dkt.Kunda John akichagua mojawapo ya Golden Briefricase katika droo ya tatu ya Maisha bomba na Barclays ambapo aliibuka na ushindi wa Vocha yenye thamani ya sh 200,000 kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali katika duka la Game.
    Nabil Khan mmojawapo wa wateja wa Benki ya Barclays aliyeshinda Ipad3 katika droo ya tatu ya maisha bomba na Barclays leo jijini Dar es Salaam. 
   Martha  Hewison akionyesha karatasi ya ushindi wa mashine ya kufulia nguo katika droo ya maisha bomba na Barclays.
   Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Barclays kitengo cha wateja binafsi Bw.Musa Kitoi  wa kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa droo ya tatu ya maisha bomba na Barclays  Martha Hewison wa  kwanza kushoto  aliyeshinda mashine ya kufulia nguo ,Nabil Khan  aliyeshinda Ipad3 ,Darvish Bhatt na Kunda John waliojishindia vocha ya manunuzi katika duka la Game,leo jijini Dar es Salaam.
   Eliuteri Mangi akichagua jina la mshindi wa bahati nasibu ya maisha bomba na Barclays iliyofanyika katika Benki hiyo tawi la Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence)

  0 0

   Mkurugenzi wa Ardhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE 2.
   Afisa Mtambuzi na Msajili wa Ardhi Shawana Sudi Khamis kulia akitoa ufafanuzi kwa Waandihi wa habari hawapo pichani, katikati ni Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi na kushoto ni Mshauri wa Kiufundi wa zoezi hilo Andrew Smith. Mkutano huo ulifanyika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE. 
  Baadhi ya Waandishi wa habari waliokuwepo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar Wakimsikiliza Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi(hayupo pichani) kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE 2. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo ZANZIBAR. 

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.

                              KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA KESHO

  Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kinatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Agosti 24 na 25, 2013 mjini Dodoma Chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.     Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika Agosti 23,2013 mjini Dodoma.  Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye, maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambacho kimeketi kwa Siku tatu kuanzia Agosti 20, 21 na leo 22, 2013 mjini Dodoma.   Kwa mujibu wa Ndugu Nape, Ajenda Kuu ya kikao cha NEC ni kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mchakato wa chama Kama Baraza la Katiba la kitaasisi  kukamilisha mjumuisho wa mchango na maoni yake Tayari kuwasilisha kwa Tume ya Katiba.           Ndugu Nape alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kujadili na kutoa maoni yao kuanzia ngazi ya Chini ya mashina na Matawi.
  Mwisho

  0 0


  NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki ametoa msaada wa
  basikeli maalum kwa watoto wenye ulemavu kupitia shirikisho la Vyama
  vya Watu Wenye Ulemavu nchini (SHIVYAWATA).

  Angellah amekabidhi viti hivyo mapema leo, vyenye thamani ya zaidi ya sh.
  milioni 12, kwa baadhi ya watoto hao, na baadaye kuwafikia watoto wote
  wenye mahitaji.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi, alisema viti hivyo ni maalum kwa
  watoto wenye miaka kuanzia sifuri hadi tisa, na ametoa kutokana na
  kuguswa na matatizo ya wenye ulemavu na pale anapopata nafasi
  anawakumbuka.

  "Nimekuwa nikifanya kazi zaidi na watoto wenye ulemavu wa kusikia
  (Viziwi), lakini pia nikaona kuna kundi lina mahitaji zaidi, hivyo kwa
  kidogo nilichopata  nikawambuka, nafanya kazi kwa kushirikisha familia
  yangu,  sitaishia hapa nitawasaidia zaidi kwa kadri
  nitakavyojaaliwa,"aliongeza kiongozi huyo aliyekuwa ameambatana na
  wanaye wawili.

  Akishukuru kwa msaada huo, Katibu wa SHIVYAWATA, Felician Mkudem
  alisema kuwa  wanafarijika sana kuona watu muhimu kama Angellah,
  wanakumbuka na kuwajali.

  "Kiongozi wa serikali ndiye jicho na sauti za watu wenye ulemavu,
  hivyo kwa kutusaidia vifaa saidizi kwa wtaoto wenye ulemavu ni faraja
  kubwa sana, kwani mambo hayo ni miongoni mwa tunayoyapigania,"alisema.

  Mkude alitumia fursa hiyi kukamabidhi nyaraka mbalimbali, ikiwemo
  mpango mkakati wa ukondaishaji wa watu wenye ulemavu na sheria
  mbalimbali zinazowahusu.  Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulemavu wa Viungo, (CHAWATA), Shida Salum aliishukuru serikali ya Rais Kikwete kuwakumbuka watu wenye  ulemavu na kuwafanyia mengi kwa ajili ya ustawi wao.  Wazazi wa watoto hao walishukuru kwa msaada huo na kwamba utawasaidia     
  watoto wanaosoma waliokuwa wanabebwa kwenda na kurudi shule, na 
  wengine waliokuwa hawajaanza masomo kutokana na hali ngumu ya 
  kuwafikisha shuleni.

  Viti hivyo vipatavyo 29, viligawiwa kwa watoto watano, wengine wawili
  wakiwa wanapata huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na
  vingine vilivyobaki watatafutwa wenye mahitaji na kukabidhiwa.

  0 0

   Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi.

   Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni yake ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi.

   Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”.


  Jengo jipya la kisasa la Kampuni ya Proin Promotions ambalo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni likionekana kwa nje. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

  =========   =======   =====

  FILAMU YA “FOOLISH AGE” YAIKUTANISHA LULU NA BODI YA FILAMU.


  Na Benedict Liwenga-MAELEZO.


  KAMPUNI ya Proin Promotions imewasilisha filamu yake iliyopewa jina la “Foolish Age” Bodi ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukaguzi ambapo baada ya kufanyiwa marekebisho filamu hiyo inaweza kuruhusiwa katika uzinduzi wa Kampuni hiyo hivi karibuni.


  Bodi ilifikia hatua ya kuwaita wahusika yaani Proin Promotions na Elizabeth Michael (Lulu) kwa ajili ya kufanya majadiliano kuhusu maudhui na maadili katika filamu hiyo kabla ya kufanyia maamuzi.


  Katika majadiliano hayo Bodi ya Filamu iliwakumbusha wahusika hao kufanya baadhi ya marekebisho katika filamu hiyo ili iweze kuwa kivutio kwa umma, pia Bodi ya Filamu iliwakumbusha juu ya umuhimu wa kuzingatia kifungu cha 14 cha Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ambacho kinaipa Bodi mamlaka ya kukagua filamu, matangazo na maelezo yote na kile cha 24 (1) (d, n na t) cha Kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kinachofafanua mambo yanayotakiwa na yale yasiyotakiwa katika filamu ambayo filamu hiyo imekwenda kinyume.


  Kwa upande wake Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Bi. Gift Msuya alikubaliana na ushauri uliotolewa na Bodi ya Filamu na aliiomba Bodi itoe muda kwao kwa ajili ya kufanyia marekebisho katika filamu hiyo. Naye msanii Elizabeth Michael (Lulu) aliieleza Bodi ya Filamu kuwa Filamu hiyo aliitengeneza muda mrefu na kwa sasa atazingatia maelekezo ya sheria, Kanuni na taratibu hususani katika eneo la maadili. Aidha alikiri kuwa ni kweli maeneo yaliyobainishwa kweli yanahitaji marekebisho.

  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Fissoo alimalizia kwa kuishauri Kampuni hiyo kutotumia filamu hiyo katika uzinduzi wa kampuni yao hadi hapo watakapofanyia marekebisho katika baadhi ya maeneo muhimu ndani ya filamu hiyo.


  Proin Promotions ni Kampuni inayojikita katika kuandaa na kutengeneza filamu za kitanzania na kuzisambaza nchini, pia ni kampuni inayotarajiwa kutoa ushindani mkubwa katika tasnia ya filamu. Kampuni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya maandalizi rasmi kukamilika.


  0 0

   Meneja wa tasisi ya Wazanzibari wanaoshi Canada (ZANCANA) Bishara Al-masroor wakati alievaa mtandio mweupe akiwa na wakilishi wenziwe wakimkabidhi msaada wa sare za wauguzi,(wamwanzo kulia) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa Mamboya, huko Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. 


  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa Mamboya, akiwa na Wazanzibar wanaoshi Canada katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi sare za wauguzi, huko Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0
 • 08/23/13--00:14: RAIS ROBERT MUGABE ALA KIAPO
 •  Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akila kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013
    Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akivishwa shada na medali baada ya kula kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013


    Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akishukuru wananchi baada ya kula kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013.
    Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akisalimia wanannchi baada ya kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013

   JK akimpongeza Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe katika sherehe za kula kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013


  0 0


                      WERUWERU GOLDEN JUBILEE – ALUMNI MEETING

  Weruweru Golden Girls,

  Please be advised that due to unforeseen circumstances, the Alumni Meeting earlier scheduled to be held on Sunday, August 25th 2013 at Cine Club, Mikocheni B, is postponed and will now be held on Sunday, September 1st, 2013 at 3:00pm at the same venue.

   For registration and pledges please visit www.weruweru.mediart.co.tz

  Let us all join together as we prepare for our Golden Jubilee

  “Kumanya, Kupenda, Huduma”

  xoxo
  Missie Popular

  0 0

  Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa  Student's Center,uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
   Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo,kutoka kulia ni Msanii Godzilla,Baba Levo,Amin,Stamina na wengineo.
   Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya mafuta-Lake Oil,Bwa.Ben Temu akizungumza kwenye semina ya Fursa,ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa kujituma na kutokata tamaa,alieleza kwa kuwataka vijana wawe wavumilivu na kutoka tamaa kwa kila fursa wanayokumbana nayo,badala yake waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

   Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

   Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa alizozipata mara baada ya kujiunga na shirika la NSSF,mbele ya Washiriki wa Semina ya Fursa (hawapo pichani),kulia kwake ni Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akimsikiliza kwa makini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
   Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatika mara mtu yeyote anayejiunga ama amejiunga na NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyeote atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

   Baadhi ya Wakazi wa Tabora wakifuatilia kwa makini semina ya ujasiliamali iliyokuwa ikiendelea ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo
  Picha ya pamoja,kiukumbusho zaidi,Msanii Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Diamond
   Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Diamond,akiwaimbisha washiriki wa semina ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye  ukumbi wa Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora,kushoto kwake ni Bwa.Marco Vingila kutoka shirika la TPSF. .
   Mmoja wa akina Mama wajasiliamali kutoka mkoa wa Tabora,Flora Zakaria akiwa na bidhaa zake alizozitengeneza yeye mwenyewe kama mjasiliamali,akiuza ndani ya semina ya Fursa.semina hiyo ambayo imewahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakazi mbalimbali wa mji wa Tabora,Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
   Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Mkuu wa Wilaya ya Igunga ( Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora),Mh. Elibariki Kingu wakitazama paketi ya sabuti iliyotengenezwa na mjasiliamali aliyehudhuria semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
   Wadau wajasiliamali wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo.
    Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi  kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
   Sehemu ya Meza kuu.Kutoka kushoto ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa (Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani Singida,Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group, pamoja na Ben Temu kutoka kampuni ya Lake Oil
   Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa,mapema leo mkoani Tabora.
   Baadhi ya wakazi wa Tabora wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi  Student's Center mkoani  Tabora mapema leo,ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa,ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana,mikopo,akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.

  0 0

  Swahili Radio baada ya kupokea maombi mengi ya wasikilizaji wetu kutoka sehemu mbalimbali duniani, tunapenda kuwatangazia kuwa Radio yetu kwa sasa inapatikana bila mkwaruzo katika simu za viganjani za iPhone, Blackberry, Android phones na katika kila kifaa chenye internet duniani. Endelea Kuangalia Swahili TV na kusikiliza Swahili Radio. Jinsi ya kutupata 
  1. Download Tunein (Tunein ni neno moja usiache nafasi) Tunein Radio app kwa simu yako mfano; iphone, ipad,ipod,android au Blackberry
  2. Baada ya ku-download , open app na nenda kwenye browser  na andika neno swahili radio kisha search.
  3. Ukiona logo yetu ya swahili radio bofya na sikiliza.

  TUNAPATIKANA HEWANI MASAA 24 TUKIWATANGAZIA KUTOKA JIJINI WASHINGTON D.C. TUKIWA KATIKA MAJARIBIO
  0 0


  0 0


  0 0

  OMMY DIMPOZ LIVE -WASHINGTON DMV AKISINDIKIZWA NA AJ UBAO
  TICKET ZIKO DISCOUNTED KUANZIA SASA HADI  TAREHE 13 SEPT
  NUNUA YAKO MAPEMA USISUBIRI MLANGONI ZITAKUWA ZAIDI
  INGIA / BOFYA HAPO CHINI


  0 0


  0 0
 • 08/23/13--08:31: CONFERENCE REGISTRATION


 • 0 0

  Miss Tz 2012 Brigette Alfred aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa bweni la wavulana shule ya msingi Buhangija akiwa pamoja na afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika.
  Miss Tanzania Brigitte Alfred akiwa na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo.
  Miss Tz 2012 Brigette Alfred pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo.

  MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija. Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50.

  Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter Ajali. 

  Briggite alisema kuwa ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu alipotembelea Shinyanga kwa kazi za jamii na kuona changamoto za watoto wanaosoma katika shule hiyo.

  Alisema kuwa mpango huo upo katika mpango wa Miss Tanzania ujulikano kwa jina la Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) nay eye kuamua kufanya kwa vitendo.

  “Ni faraja kwangu kuona kuwa ninatimiza ahadi yangu, nawashukuru wote walionisaidia ikiwa pamoja na familia yangu, na ninaomba wengine wanisaidie kwani badi kuna changamoto nyingi katika ujenzi na kazi za jamii kwa ujumla,” alisema Brigitte.

  Alisema kuwa amepania kuweka historia katika fani hiyo kwani anaamini ujenzi au jingo hilo litakuwa kumbukumbu kubwa kwake tena kwa vizazi na vizazi.

  Brigitte pia aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa hata kwa wale wasiokuwa karibu na familia zao na kwamba wamtegemee zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuwa yeye ndiye mfariji kwa wanyonge huku akiwahimiza kuzingatia zaidi elimu kwani ndiyo msingi wa maisha yao.

   “Nilipata msukumo wa kuisaidia shule hii hususani katika ujenzi wa bweni hilo kutokana na ujio wake wa mwezi Aprili mwaka huu shuleni hapo na kujionea adha wanayopata watoto hao kutokana na msongamano mkubwa mabwenini,” alisema.

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi alimpongeza Brigitte kwa moyo huo wa kujitolea na kuwataka warembo wengine kuiga mfano wake. Nyamubi alisema kuwa alichokifanya Brigitte ni jambo la kukumbukwa nan i msaada mkubwa kwa jamii hasa kwa watu wenye ulemabu wa ngozi.

  Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wazazi wa watoto hao kuwa na tabia ya kuwatembelea watoto wao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwachuku wakati wa likizo. Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Peter Ajali alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo la msongamano mabwenini kwani kuna jumla ya watoto 247 huku mabweni yaliyopo yana uwezo wa kukaa watoto 148 tu.

older | 1 | .... | 144 | 145 | (Page 146) | 147 | 148 | .... | 1898 | newer