Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1464 | 1465 | (Page 1466) | 1467 | 1468 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wananchi Wilayani Igunga mkoani Tabora Wametakiwa Kujenga Tabia na mazoea ya Kutunza miundombinu ya Umeme, kwani kwa Kufanya hivyo kutaifanya Tanzania kuwa nchi yenye Uchumi wa Kati Kupitia Sekta ya Viwanda kutokana na Umeme wa Uhakika.

  Kauli hiyo imetolewa mkoani Tabora na Meneja wa Njia kuu za Umeme, Mhandisi Amos Kaihula, ambapo amesema ni Jukumu la Wananchi Kwenye maeneo yao Kuhakikisha kwamba Miundo mbinu ya Umeme inakuwa Salama wakati wote.

  Sambamba na wito huo, Mhandisi Kaihula amewaasa wananchi kukemea kwa nguvu viashiria na Matukio yenye mrengo wa Kuhujumu Miundombinu ya Umeme." Mtu mmoja mwenye dhamira mbaya anaweza kuleta hasara kubwa kwa jamii yote na nchi nzima pale hujuma na wizi wa vyuma unapofanyika katika njia kuu ya umeme na kupelekea nguzo kubwa ya grid ya taifa kuanguka" alisema Mhandisi Kaihula.

  “Ndugu zangu, miundombinu hii ya Umeme mnayoiona, imetengenezwa kwa gharama na jitihada kubwa mno za serikali, lakini inapotokea mtu amejaribu kuisogelea miundombinu hiyo, madhara yake ni makubwa ikitokea lile tower (muundo mbinu) limeanguka, umeme wake ni mkubwa mno, na inaweza kuleta maafa makubwa na athari kubwa kwa nchi kiuchumi na kiusalama” aliongezea mhandisi Kaihula.

  Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Igunga Robert Mwagala amekemea vitendo hivyo vya Uhujumu wa miundombinu ya umeme, na kusema Serikali ikishirikiana na TANESCO itafanya zoezi la kubaini wahujumu hao, na watachukuliwa hatua za kisheria.
  Afisa Mtendaji wa Kata ya Igunga Robert Mwagala akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo wakati wa Kampeni ya Utoaji Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Kulinda Miundombinu ya Umeme ya Tanesco, katika Kijiji cha Mgongolwa Wilayani Igunga mkoani Tabora.

    Wakazi wa Kijiji cha Mgongolwa wakisikiliza kwa umakini elimu iliyokuwa ikitolewa na Maofisa wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, kuhusiana na umuhimu wa Kulinda miundombinu ya Shirika hilo.


  Baadhi ya miundombinu ya njia kuu ya umeme za Msongo wa Kilovolti 220 na Kilovolti 400 zinazopita katika mikoa ya Singida na Tabora.

  0 0


  Mheshimiwa Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Hamidu Awesso akitoa ngao ya ushindi kwa mjumbe wa kamati ya kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi ya kijiji cha Msaraza wakati wa tamasha hilo

  Mheshimiwa Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Hamidu Awesso akitoa zawadi kwa kijana bora wa mfano wa kuigwa kwa mwaka 2017 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na kijana Selemani Hamisi kutokea kijiji cha Kimang'a(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  Mheshimiwa Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Hamidu Awesso akitoa zawadi kwa mama bora wa mfano kwa mwaka 2017 ambapo nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Mama Hadija Mrisho wa kijiji cha Kwa-Kibuyu pichani


  Hatimae shindano la kutafuta kamati bora za kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi vijijini lililokuwa linaratibiwa na shirika la UZIKWASA wilayani Pangani limemaliza kwa kishindo huku kamati ya kijiji cha Msaraza kikiibuka na ushindi.


  Shindano hilo ambalo lililokuwa linashirikisha vijiji 33 kutokea wiayani humo, limehudhuriwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi.

  Awali akitangaza kamati tatu bora zilizofanya vizuri kwa mwaka huu mbele ya mgeni rasmi, mkurugenzi msaidizi kutokea shirika la UZIKWASA Bwana Novatus Urassa alisema, mchakato wa kupata washindi hao ulikuwa mgumu kwa kuwa mwaka huu kamati zote zilionesha ushindani wa hali ya juu katika kutekeleza mipango kazi yao waliyojiwekea.

  "Mheshimiwa mgeni rasmi, takribani vijiji vyote 33 vilivyoshiriki shindano hili kwa mwaka huu vilikuwa moto, kwa maana kila kijiji kilikuwa na mpango kazi wake, na kwa asilimia kubwa wote wamefanikiwa kutekeleza mipango kazi hiyo, lakini wapo waliotekeleza vizuri zaidi na tukaona hao ndio watakuwa mfano mzuri kwa wenzao, hivyo mpaka kupata kumia (10) bora haikuwa kazi rahisi, hivyo hivyo mpaka kupata hizi tatu (3) bora pia haikuwa rahisi" alisema Bwana Urassa.

  Bwana Urassa alizitaja kamati hizo zilizofanya vizuri kuwa ni kamati ya kijiji cha Msaraza ambacho ndicho kiliibuka na ushindi na kukabidhiwa zawadi ya hundi ya shilingi laki saba, mshindi wa pili ni kijiji cha Mwera ambacho kilipewa hundi ya shilingi laki sita na mshindi wa tatu ni kijiji cha Mkwajuni ambapo walikabidhiwa hundi ya shilingi laki tano.

  Kamati nyengine ambazo ziliingia katika hatua ya kumi bora ni pamoja na kamati ya kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi ya kijiji cha Tungamaa ambacho kilishika nafasi ya nne, Kijiji cha Mwembeni nafasi ya tano, Kijiji cha Mbulizaga nafasi ya sita, Kijiji cha Kimang'a nafasi ya saba, Kijiji cha Mikocheni nafasi ya nane, Kijiji cha Mikinguni nafasi ya tisa, na Kijiji cha Kwa-Kibuyu kilishika nafasi ya kumi.

  Mbali na ushindani wa kamati hizo, pia tamasha hilo liliwatambua na kuwazawadia washindi wa shindano la Kijana Bora wa mfano wa kuigwa pamoja na Mama Bora wa mfano wa kuigwa kwa mwaka 2017 kutokana na kujikita katika shughuli za kimaendeleo na kupambana na ukatili wa kijinsia.

  Upande wa kijana bora wa mfano wa kuigwa kwa mwaka 2017 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na kijana Hamisi Salemani kutokea kijiji cha Kimang'a, nafasi ya pili kijana Geofrey Kalala kutokea kijiji cha Boza, nafasi ya tatu kijana Mohammed Zuberi kutokea kijiji cha Mkwaja, na kwa upande wa mama bora wa mfano kwa mwaka 2017 nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Mama Hadija Mrisho wa kijiji cha Kwa-Kibuyu, nafasi ya pili Mama Pili Yusufu wa kijiji cha Mwembeni na nafasi ya tatu ni ilienda kwa Mama Halima Hamisi wa kijiji cha Mivumoni

  Kwa upande wake mgeni rasmi Mheheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso mbali na kulipongeza shirika la UZIKWASA kwa kuandaa shughuli hiyo, pia aliwapongeza washindi wote wa mashindano hayo na kuwataka waendelee kuwa chachu ya maendeleo wilayani Pangani hasa wakati huu ambao jamii imekuwa ikikumbwa na matukio ya ukatili wa kijinsia.

  "Shirika la UZIKWASA linafanya mambo makubwa sana hapa wilayani Pangani, wananchi walikuwa wanaogopa kupaza sauti zao, lakini leo wananchi wanabanja, wanaeleza matatizo ya ukatili, wanajadili masuala ya maendeleo, wanawahoji viongozi wao wa vijiji kama kuna ubadhilifu, leo wananchi wanafatilia masuala ya elimu kwa watoto wao, kamati za shule zinafanya kazi, na pia tunaona hapa mpaka kamati za kudhibiti Ukimwi zimeanzishiwa mashindano ili kuleta ufanisi wa kazi zao, yote hii ni juhudi za UZIKWASA, na naomba washindi wote mkawe chachu ya maendeleo katika maeneo yenu" alisema Mheshimiwa Awesso.

  Tamasha hilo lilihudhuriwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Pangani Bwana Sabas Damian Chambasi, mkuu wa TAKUKURU wilayani Pangani Bwana Joseph Paul, Ofisi ya manedeleo ya jamii Pangani ikiwakilishwa na Bi Vicky Mfinanga na Bi Rose Kaskazi pamoja na mkurugenzi mtendaji wa shirika la UZIKWASA Mama Vera Pieroth.

  Pia Tamasha lilipambwa na burudani mbali mbali za sanii, ambapo kundi la maigizo na ngoma za asili kutokea Pangani linalofahamika kwa jina la Banja Basi lilikuwa kivutio kikubwa kwa wageni waalikwa, kadhalika wasanii wa Bongo Flava kutokea Pangani G-Man, Ram Bize pamoja Mavokali waliacha historia katika tamasha hilo.

  Tamasha la kukabidhi zawadi kwa kamati bora za kudhibiti Ukwimwi, Jinsia na Uongozi kwa mwaka 2017 limeandaliwa na shirika la UZIKWASA lenye maskani yake wilayani Pangani huku likibeba kauli mbiu isemayo "Lisilowezekana, Linawezekana". Mwaka jana mshindi wa kamati bora kilikuwa kijiji cha Mseko.

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Salim Ahmed Salim leo amewaaga wajumbe Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano.

  Katika salamu zake mwishoni mwa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma Mhe. Dk. Salim amewashukuru Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wakuu wa chama kwa kushirikiana nao katika kipindi chote cha ujumbe wake na pia amempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kwa uongozi uliokiwezesha chama kuimarika.

  Mhe. Dk. Salim amesema kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Dk. Magufuli imeonesha dhahiri kuyaenzi mambo muhimu aliyoyasimamia Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

  Mhe. Dk. Salim ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mh Mrisho Gambo kwa Ushirikiano na Naibu Waziri wa Mifugo (Mhe Ulega) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,mapema leowa wamezindua zoezi la Upigaji Chapa Mifugo Kata ya Nainokanoka Wilayani Ngorongoro. 
   
  Mh Mrisho Gambo aliesma kuwa kampeni hiyo itasaidia Ku-Control movement ya mifugo kutoka ndani na nje ya nchi, kuipa serikali uwezo wa kuwatambua na kuwahudumia wafugaji wetu. Mtu yoyote atakaye hujumu zoezi hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake! Deadline ya kuhitimisha zoezi hili ni tarehe 30 Januari 2018 kwa mkoa wa Arusha!

  Uongozi unao acha alama!

   
    Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mh Mrisho Gambo kwa Ushirikiano na Naibu Waziri wa Mifugo (Mhe Ulega) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,mapema leo akishiriki kuzindua kampeni ya Upigaji Chapa Mifugo Kata ya Nainokanoka Wilayani Ngorongoro.


  0 0

  Benki ya TPB tumeendelea kusogeza huduma zetu karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya maeneo ya Kwa Mrombo, Mkoani Arusha.


  Lengo la kufungua tawi hili ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na pia kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa wa Arusha, hususan waishio maeneo ya Kwa Mrombo, waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.

  Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki hiyo.

  Alisema pia wakazi wa Kwa Mrombo, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.

  ‘Ni furaha kubwa sana kwetu sisi TPB kuweza kufikisha huduma zetu hapa Kwa Mrombo. Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’ alisema Profesa Rutashobya.

  Alisema kwa sasa lengo lao kubwa ni kuendelea kutoa huduma bora zaidi ili kuwanufaisha wananchi wa kipato cha chini. ‘TPB inaendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi kwani mbali na kufungua tawi hili, katika kipindi cha mwaka huu tumeweza kufungua matawi yetu huko Mwanjelwa Mkoani Mbeya, Mto wa Mbu wilayani Monduli na Temeke,’ alisema.

  Kwa upande wake, Meneja wa tawi la Kwa Mrombo Hussein Jalala alisema mwitikio wa wakazi wa maeneo ya Kwa Mrombo umekuwa mzuri, tangu walipoanza kutoa huduma zake maeneo hayo. Alisema tawi lake limejipanga vizuri kuhakikisha kuwa huduma zitakazotolewa kwa wateja wao ziwe za kuridhisha na zenye kukidhi mahitaji yao. Jalala alizitaka taasisi mbalimbali vikiwemo vyuo, mashirika na hata shule kufungua akaunti za taasisi na TPB ili kupata huduma za kisasa na zenye gharama nafuu. 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobya akifurahia  baada ya kufungua rasmi tawi jipya la benki hiyo maeneo ya  kwa Mrombo ,huko Mkoani Arusha. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi .
  Mwenyekiti wa Bodi ya Waurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa, akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw. Tate Looboye Koole, wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya  Kwa Mrombo, Mkoani Arusha. Katikati ni Meneja wa tawi hilo Hussein Jalala.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (wa pili kushoto), akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw. Elias John Malisa, wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya  Kwa Mrombo, Mkoani Arusha. Kushoto  ni Meneja wa tawi hilo Hussein Jalala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobya akifurahia  baada ya kufungua rasmi tawi jipya la benki hiyo maeneo ya  kwa Mrombo ,huko Mkoani Arusha. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi .

   Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa benki ya TPB Noves Moses (kulia) akiteta jambo na mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw. Elias Malisa, aliyehudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya kwa Mrombo, Mkoani Arusha.


   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo pamoja na baadhi ya wakurugenzi, kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo lililopo maeneo ya kwa Mrombo, Mkoani Arusha.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya kwa Mrombo, Mkoani Arusha.

  0 0  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizindua zowezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, (wa kwanza kulia) akizungumza na wananchi wanoishi katika hifadhi ya Ngorongoro jana baada ya kushuhudia zowezi la upigaji chapa mifugo mkoa wa Arusha.katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na kushoto, Naibu Muhifadhi Dkt.Maurus Msuha
  Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Dkt Maurus Msuha akishiriki zowezi la upigaji chapa mifugo mapema jana mkoani Arusha.
  Zowezi la upigaji chapa mifugo likiendelea mkoani Arusha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG Arusha)

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega amefanya ziara mkoani Arusha katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa lengo la kuhamasisha upigaji chapa mifugo.

  Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika halmashauri ya Ngorongoro, Ulega amempongeza mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, kwa utendaji mzuri wa kazi hususani katika kuhamasisha upigaji chapa mifugo mkoani humo.

  Aidha Mhe Ulega amezijata baadhi ya halmashauri zilizofanya vizuri katika zoezi la upigaji chapa kuwa ni pamoja na Chemba,Kondoa,Maswa,Mafinga na Misungwi.

  Mh.Ulega amewahimiza wafugaji kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji chapa mifugo linaloendelea nchi zima.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiwa katika pozi na Msanii aliyeigiza kama mhusika mkuu katika Filamu ya From Nigeria Stick Motela alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo mapema wikiendi hii.Filamu hiyo imeandalliwa na Kampuni ya Jumo Entertainment.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo alipokuwa alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Filamu ya From Nigeria iliyoandalliwa na Kampuni ya Jumo Entertainment mapema wikiendi hii. Katikati ni Msanii aliyeigiza kama mhusika mkuu katika filamu hiyo Stick Motela.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisalimiana na Mkuu wa Promosheni na Matangazo wa Kampuni ya Duma Promosheni Daud Maichel (Duma) alipokutana naye katika uzinduzi wa Filamu ya From Nigeria mapema wikiendi hii. Kampuni ya Duma Promosheni ndiyo iliyoratibu shughuli nzima ya uzinduzi wa filamu hiyo.Picha na Frank Shija – MAELZO

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akinywa maji ya dafu mara baada ya kutembelea kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa kijijini hapo pamoja na kuzungumza na Watumishi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agness Robert (wa tatu kushoto).
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax na Mabula ( wa tatu kulia) wakinywa maji ya dafu mara baada ya kutembelea kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa kijijini hapo pamoja na kuzungumza na Watumishi. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agness Robert, Wengine ni watumishi wa Makumbusho ya Taifa makao Makuu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia) akipewa maji ya dafu na mmoja wa Watumishi wa Kijiji cha Makumbusho mara baada ya kutembelea hapo wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa k pamoja na kuzungumza na Watumishi. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agness Robert (wa pili kulia)
  Baadhi ya Wasanii wakitumbuiza ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa kijijini hapo pamoja na kuzungumza na Watumishi.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Watumishi wa Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki kujionea shughuli zinazofanywa kijijini hapo.
   
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula (kushoto) wakimsiliza kwa makini Mhifadhi Mila Mwandamizi, Wilbard Hema (mbele) wakati akiwapa maelezo kabla ya kutembelea baadhi ya nyumba za makabila 33 zilizopo kwenye Kijiji cha Makumbusho ambapo Naibu Waziri Hasunga alipofanya ziara mwishoni mwa wiki. Nyuma ya Naibu Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Agnes Robert.

  Picha na Lusungu Helela-MNRT

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifafanua jambo mbele ya wanakijiji wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto mbele) akiendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifafanua jambo kwa wakazi wa kijiji cha Magumbani kilichopo wilayani Mkinga mkoani Tanga.
  Mkazi wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga, Mohamed Mengwena akitoa pongezi kwa Serikali kwa kufikisha miundombinu ya umeme kijijini hapo mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo tarehe 16 Desemba, 2017.
  Msimamizi wa Miradi ya Umeme Vijijini (REA) katika mkoa wa Tanga, Mhandisi Kasim Rajabu akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, na wakazi wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na serikali wakisikiliza kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wanakijiji wa kijiji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.

  Na Greyson Mwase, Tanga

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amezitaka kampuni za Derm Electric, Njarita, Agwilla na Radi Services kutoa maelezo kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ya kutokuendelea na kazi katika maeneo yao ya miradi wakati walikwishalipwa malipo ya awali na Serikali.

  Mgalu alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki tarehe 16 Desemba, 2017 alipofanya kikao na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)- Ofisi ya Tanga baada ya kubaini wakandarasi hao hawapo katika maeneo hayo ya kazi na kutohudhuria kikao hicho kama alivyoagiza.

  Kikao hicho kilishirikisha pia watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)

  Alisema kitendo cha wakandarasi kutokuwepo katika maeneo yao ya kazi na kutohudhuria kikao kama ilivyoagizwa kinakwamisha utekelezaji wa miradi na hivyo kuutaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujulisha kampuni husika kuandika maelezo ya kutokuwepo kwenye maeneo ya kazi na kukwamisha juhudi za Serikali katika usambazaji wa umeme vijijini.

  “ Kama Serikali tumeweka mikakati ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2019- 2021 vijiji vyote nchini vinafikiwa na huduma ya umeme, sasa inapotokea baadhi ya wakandarasi wanakwamisha juhudi hizi wakati wamekwishalipwa na Serikali ni lazima Serikali iwawajibishe kulingana na sheria na kanuni za nchi,” alisema Mgalu.

  Mgalu aliendelea kuwataka wakandarasi wote nchini kuwepo katika maeneo yao ya kazi na kukamilisha miradi yao kwa wakati, na kusisitiza kuwa serikali haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayefanya kazi katika kiwango cha chini.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mgalu aliitaka TANESCO kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa madeni na kukamilisha zoezi la uhakiki wa wateja mara moja ili kukabiliana na changamoto ya upotevu wa mapato ya shirika hilo.

  Alisema ni jukumu la TANESCO kujiendesha kwa faida kupitia mapato yake na kazi ya Serikali ni kulipa nguvu shirika hilo kwa miradi mikubwa inayohitaji fedha nyingi.

  Wakati huo huo, akizungumza katika mikutano tofauti katika kijiji cha Zangibari kilichopo wilayani Mkinga na katika vijiji vya Mlingano, Mtindiro, Mpapayu vilivyopo katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Naibu Waziri Mgalu alielekeza wakati wa utekelezaji wa miradi, Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kuhakikisha taasisi, shule, nyumba za ibada, hospitali zinapata umeme.

  Aidha alipongeza wananchi wengi katika vijiji vya Zangibari wilayani Mkinga na Mpapayu wilayani Muheza mkoani Tanga walioonyesha mwitikio mkubwa wa kuunganisha mfumo wa umeme ( wiring) kwenye nyumba zao na kuwataka ambao hawajaunganisha mfumo wa umeme kufanya mara moja kwa ajili ya neema kubwa ya umeme.

  Alisema kwa wale ambao wana nyumba ndogo wanaweza kuwekewa kifaa maalum cha Umeme Tayari (UMETA) na kuanza kufaidi huduma ya umeme.

  Akielezea mikakati ya serikali katika uboreshaji wa upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu, Mgalu alisema kuwa serikali kupitia REA Awamu ya Tatu inasambaza umeme katika vijiji vyote nchini ambapo ifikapo mwaka 2019 karibia vijiji vyote vitakuwa na umeme wa uhakika.

  Aliendelea kuelezea mikakati mingine kuwa ni pamoja na matumizi ya nishati jadidifu kama vile jua hususan katika maeneo yasiyofikiwa na umeme kutoka Gridi ya Taifa, ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji wa Stieglers Gorge na mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I na Kinyerezi II.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewaagiza wahandisi wa ujenzi katika Halmashauri zote hapa nchini kuona uwezekano wa kutumia Tiles badala ya kuweka sakafu ya kawaida ili kuongeza uimara na mandhari majengo hayo.

  Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa na mabweni ya shule ya sekondari Hamza na miundombinu mbalimbali ya kituo cha afya cha zogolo yakiwepo majengo ya upasuaji, maabara, na wodi ambapo majengo yote ameyakuta yamejengwa vizuri sana kwa kuwekwa Tiles. 

  Ameeleza kwamba majengo mengi yanayojengwa na kuwekwa floor(sakafu) ya kawaida yanabomoka kwa muda mfupi na hivyo kuhitajika kufanyiwa ukarabati mara kwa mara.Waziri Jafo amesisitiza kwamba ujenzi wa kutumia Tiles kusaidia hata katika usafi wa majengo hayo. 
  Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya ya Nzega wakiwemo wabunge wao Hussein Bashe, Selemani Zedi, na Hamisi Kigwangwala kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi wao.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
  Viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakipata maelekezo ya matumizi ya Tiles kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakielekea kwenye kukagua jengo jipya la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Zogolo.

  0 0


  Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta akizungumza na baadhi ya washindi wa  promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' ambapo wateja 11 wamejishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 44 wakijishindia zawadi za kila siku za shilingi 500,000  kila mmoja. Pamoja na zawadi hizo za kila siku, zawadi kubwa katika promosheni hiyo inayoendelea ni shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5. 

  Baadhi ya washindi wa  promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' wakimsikiliza Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi zao. Jumla ya wateja 55 wa Tigo wamejishindia zawadi za kila siku za kati ya shilingi laki tano na shilingi milioni moja katika promosheni hiyo inayoendelea ambapo pamoja na zawadi za kila sikiu, zawadi kubwa zinazoshindaniwa ni shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5. 

  Mmoja wa washindi wa promosheni inayoendelea ya  'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' akizungumza na waandishi wa habari. Wateja wa Tigo wanaofanya miamala  kupitia Tigo Pesa wana fursa ya kujishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano. Pia kuna zawadi kubwa ya shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5 zinazoshindaniwa. 

  Mmoja wa washindi wa promosheni inayoendelea ya  'Tumia Tigo Pesa na Ushinde', Rehema Juma Ramadhani, mkaazi wa Pugu Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja. Jumla ya wateja 55 wa Tigo wamejishindia donge nono katika promosehni hiyo inayoendelea ambapo wateja wa Tigo wanaofanya miamala  kupitia Tigo Pesa wana fursa ya kujishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano. Pia kuna zawadi kubwa ya shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5 zinazoshindaniwa. 

  • Wateja 20 wapokea zawadi kemkem za pesa kwa kufanya miamala kupitia Tigo Pesa

  Dar es Salaam, 8 Novemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa leo imewatangaza na kuwazawadia washindi 20 wa promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’ inayoendelea katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka mpya ambapo wateja wanajishindia mamilioni ya pesa.

  Washindi wanne (4) wamepata bahatiya kushinda zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 16 wakijaza mifuko yao na donge nono la shilingi laki tano (TZS 500,000) kila mmoja.  each. Jumla ya shilingi milioni 12 zimetolewa kama zawadi kwa wiki  hii.

  Washindi wa zawadi za TZS 1 milioni ni wafanyabiashara Neema Fredrick Mosha, Fredrick Joseli Mponzi , Sefu Athumani Sefu na Hadija Mohamed Lukulumbale ambaye ni mama nitilie.

  Washindi  wa zawadi za TZS 500,000 ni Michael Joseph Moshi, Moses Muhonga Amuli, Saidi Khatib Kiko, Sylvester Michael Madaga, Aziza Ramadhani Ngozi, Evelyne Gwamaka Mwakyembe, Tumsifu Harold Temu na Sikudhani Constantine Mwenda. Wengine walioshinda TZS 500,000 ni Queentina Msafiri Mbwambo, Hilary Andrew Massawe, Ashura Ally Salim, Halima Saidi Shaabani, Fatuma Ally Makumbo, Halima Saidi Sangiwa, Jenifer Samuel Apolinale na James John Mkanula.

  ‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii. Bado tuna zawadi za thamani ya TZS 108 milioni kutoa kwa washindi 133,’ Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta alisema wakati akikabidi zawadi kwa washindi Dar es Salaam leo.

  Alibainisha kuwa pamoja na zawadi za kila siku, promosheni hiyo ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’  itakuwa na zawadi kubwa za mwezi  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni.

  ‘Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa ambao wanahitaji kutumia huduma ya Tigo Pesa kwenye simu zao ili kupata nafasi ya kushinda. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda,’ alisema.

  Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote.  

  0 0

  Watanzania wameshauriwa kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ili waweze kukuza soko la ndani na uchumi kwa ujumla.

  Hayo yamesemwa na Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, wakati alipokua akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Alisema ili uchumi wa nchi wanchi ukue haraka, watanzania wanapaswa kubadili mitazamo ya kudhani kuwa bidhaa za nje ni bora kuliko bidhaa za ndani, jambo ambalo si sahihi.

  Alisema katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, Watanzania wengi wamepiga hatua katika uboreshaji wa shughuli zao, jambo ambalo limechangia kuwepo kwa bidhaa bora zinakubalika katika soko la ndani nan je ya nchi.

  “ ifike wakati Watanzania tunapaswa kubadili mitazamo yetu na kuamini kuwa, bidhaa zinazozalishwa nchini zina ubora unaokubalika, jambo ambalo linachangia kupata masoko ya ndani na njke ya nchi”, alisema Bisheko.

    Alisema Benki hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo wamiliki wa vyuo na viwanda vidogo ili kuhakikisha wanaboresha shughuli zao na kujiongezea kipato.

  Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Oystebay, Sister Getrude Amandus, alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ya ufundi ili kuwawezesha vijana kujiajiri.

  Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichnopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwa kugonga mkono pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wakijiandaa kupiga kura za kumchagua Mwenyekiti wa CCM katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetional Centre Mjini Dodoma
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wakipiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa CCM katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetional Centre Mjini Dodoma

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wa tatu kutoka (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wa nne kutoka (kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete wa kwanza (kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wa pili kutoka (kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wa pili kutoka kulia wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kufungua mkutano wa Tisa wa Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika mjini Dodoma.


  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM pamoja na wageni mbalimbali katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetional Centre Mjini Dodoma


  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kufungua mkutano wa Tisa wa CCM uliofanyika mjini Dodoma.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula mara baada ya kufungua mkutano wa Tisa wa CCM uliofanyika mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano huo wa tisa uliofanyika mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao katika mkutano huo wa tisa.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipiga kura kwa moja ya wagombea katika mkutano huo wa tisa.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula mara baada ya kupiga kura zao kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi hao.
  Wanachama wa CCM wakiburidika kwa kucheza nyimbo mbalimbali katika mkutano huo wa tisa.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mke wa Hayati Baba wa taifa, Mama Maria Nyerere katika mkutano huo wa Tisa wa CCM uliofanyika mjini Dodoma.

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Mhandisi Mahenda S. Mahenda, Meneja wa Vituo vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro Systems, vinavyohusisha inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Korogwe

  VITUO vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro Systems, ambayo inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97, viko katika hali nzuri, Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S. Mahenda, amesema Leo Desemba 18, 2017.

  Hata hivyo amesema, mashine moja kati ya mbili kwenye kituo cha Hale, haifanyi kazi na iko katika matengenezo. “Niwahakikishie tu kwamba matengenezo hayo ambayo bado hayajaanza hayataathiri upatikanaji umeme kwa sababu vyanzo vya umeme vimeongezeka.” Alisema.Akifafanua zaidi Mhandisi Mahenda alisema, New Pangani Falls inazalisha umeme Megawati 68, Hale Megawati 21, na Nyumba ya Mungu Megawati 8 na uwezo wa vituo kutoa umeme wa kutosha.

  Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea vituo vya Hale na New Pangani Falls Mhandisi Mahenda, alisema, kituo cha Hale kilijengwa mnamo mwaka 1961 na kuanza kufanya kazi mwaka 1964 na kuwa kituo cha kwanza kabisa cha kuzalisha umeme wa maji katika historia ya nchio yetu. 

  “ Utaona umri wa mitambo hiyo ni miaka 53, na moja ya mashine hizo imeharibika na kufanya uwezo wa kituo wa kutoa Megawati 21, kupungua hadi Megawati 8, lakini niwahakikishie wananc hi licha ya upungufu huo, bado TANESCO inao uwezo wa kuzalisha umeme unaohitajika, kwani vyano vya umeme vimeongezeka.” Alisema. 
  Valvu ya kupitisha maji yanayopelekwa kwenye mashine za kufua umeme, kwenye kituo cha nguvu za umeme cha Hale ikivuja. Mhandsi Mahedna alielezea hali hiyo kuwa haina taathira kubwa na inatokana na mashine hizo kuwa na umri mrefu Zaidi.
  Bwawa la maji Pangani Pangani Falls.
  Mhandisi Mahenda akifafanua mambo mbalimbali ya kiufundi kwenye chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme cha New Pangani Falls.
  Exciter, moja kati ya mashine mbili ya kufua umeme kwenye kituo cha Hale, ambayo inafanya kazi. 
  Wahariri na wataalamu wa TANESCO, wakitembelea New Pangani Falls.
  Mhandisi Mkuu wa Pangani Hydro Systems, Lewis Loiloi, akitoa maeelzo kuhusu masuala ya kiusalama kwa wahariri wakiwa kwenye handaki, la New Pangani Falls.
  Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha New Pangani Falls cha 132 kV.

  0 0

  Pangani District Council and other Government organs have been advised against putting hurdles on the work of a non-government organization, UZIKWASA that is spearheading efforts to change traditional mindsets that hinder people, especially women and children form speaking out freely against gender-based violence and other social abuses.

  The advice was given by the Deputy Minister for Water and Irrigation, Jumaa  Awesso when he spoke at a ceremony to award best performing Village Multisectoral Aids, Gender and Leadership Committees (VMACs) held at Msaraza village in Bushiri Ward of Pangani District.

  He said that UZIKWASA is responsible for changing mindsets of the people as regards gender-based violence, early marriages, early pregnancies and other social abuses in the society. “It is very difficult to separate the development of a freedom to speak out on various issues on the people and the work of UZIKWASA,” Awesso, who is also the Member of Parliament for Pangani, pointed out.

  He said that he know that the organization has some challenges that hinder its work and called oin the Council and other Government organs to work closely with UZIKWASA which is spearheading the transformation of a society that was previously regarded as having fear of speaking out.

  Awesso said that the Pangani society would suffer a heavy loss if it cuts down the work of the organization which has trained village leaderships on responsible and transformative leadership and enabled people to speak out on abuses that have been going for years in the society.

  He said the work of the organization has had an impact on increase in reported cases of rape and oithe abuses in the district. He said the number of cases that have been reported this was 58 but 38 out of them have been stalling because culprits have been reported to escape.

  Speaking at the occasion, a young person, identified as a Child Ambassador, Athumani Juma commended UZIKWASA for initiating the formation of a ‘Safe System’ in schools which enables school children to report incidences of abuse to authorities.

  He told the audience, including members of VMACs from 12 villages that 51 cases of abuse against children have been reported from January this year. Thoruhg the safe system initiated by expanded School Committees trained by the organization.

  Reading the children’s message, Juma said that action has been taken against people who perpetrated the incidents against children he mentioned as including harsh penalties, denying food to children by parents and caretakers, missing meals at school, beatings, burning, sexual abuse, rape, sodomy, touching of sensitive body spots and name calling against children.

  He mentioned other such incidents to bewildered audience who included members of 12 VMACs as being denied money for various expenses at school, being given hard work and being burned in sensitive spots using being pricked using sharp tools.

  Juma said that it was a sad that in some incidences were being perpetrated by those who were supposed to protect children and make sure they get better education sometimes turned against those children by abusing them.

   “Headteachers, patron and matron teachers and big age school children, out of schoo youth, including bodaboda drivers and adults in the streets and homes are all culprits in abusing school children. School girls were the main victims, leading to psychological effects that lead to these children absconding and engage in risky jobs,’ he said

  The Child Ambassador called on the Government, private institutions and activists to continue to give awareness education and create an official system that would give school children a chance to be heard as regards to their challenges they face

  Msaraza VMAC scooped the first prize of Sh. 700,000 for best performing VMAC for the year 2017, follwed by Mwera which scooped Sh. 600,000 and Mkwajuni Sh. 500,000.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Watanzania wameshauriwa kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ili waweze kukuza soko la ndani na uchumi kwa ujumla.

  Hayo yamesemwa na Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, wakati alipokua akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Alisema ili uchumi wa nchi wanchi ukue haraka, watanzania wanapaswa kubadili mitazamo ya kudhani kuwa bidhaa za nje ni bora kuliko bidhaa za ndani, jambo ambalo si sahihi.Alisema katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, Watanzania wengi wamepiga hatua katika uboreshaji wa shughuli zao, jambo ambalo limechangia kuwepo kwa bidhaa bora zinakubalika katika soko la ndani nan je ya nchi.

  “ ifike wakati Watanzania tunapaswa kubadili mitazamo yetu na kuamini kuwa, bidhaa zinazozalishwa nchini zina ubora unaokubalika, jambo ambalo linachangia kupata masoko ya ndani na njke ya nchi”, alisema Bisheko.

  Alisema Benki hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo wamiliki wa vyuo na viwanda vidogo ili kuhakikisha wanaboresha shughuli zao na kujiongezea kipato.Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Oystebay, Sister Getrude Amandus, alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ya ufundi ili kuwawezesha vijana kujiajiri.Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichnopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiongea na wakazi wa Mbeya Vijijini waliohudhuria ufungaji wa Mashindano ya Jimbo Cup (Njeza Cup) jana Vijijini hapo.
  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza akiongea wakati wa ufungaji wa mashindano ya Jimbo Cup (Njeza Cup) mashindano ambayo ameyaratibu yeye na kushirikisha vijiji takribani 200 na kata 30.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Kulia) akimpa mkono wa pongezi kiongozi wa Garant Queens Naomy Mbwili wakati wa ufungaji wa Mashindano ya Jimbo Cup (Njeza Cup) jana Mbeya Vijijini.
  Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Kulia) akimpa zawadi ya fedha kiasi cha laki Tano kiongozi wa timu ya Ilunga David Costa (Kushoto walioibuka washindi wa pili wa Jimbo Cup (Njeza Cup) jana Mbeya Vijijini.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Katikati) akiwakabidhi washindi wa kwanza wa timu ya Iyanya Kombe la Jimbo Cup (Njeza Cup) ambapo Inyala iliibuka mshindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Ilunga hapo jana Mbeya Vijijini.Picha na Lorietha Laurence-WHUSM


  *Na Lorietha Laurence-WHUSM, Mbeya Vijijini*

  Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi kudhamini mashindano ya michezo kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kutengeneza wachezaji bora watakaowakilisha Taifa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

  Mhe. Shonza ameyasema hayo alipokuwa akifunga mashindano ya Jimbo yaliyoandaliwa na Mbunge wa Wilaya hiyo Mhe.Oran Njeza katika Wilaya ya Mbeya Vijijini.“Napenda kuelekeza shukrani zangu za dhati kwa Mbunge wa Mbeya Vijijini Mhe.Njeza kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali katika kuibua vipaji vya mpira wa Miguu” amesema Mhe. Shonza

  Aidha, Mhe. Shonza alisema kuwa amefurahishwa zaidi kwa kuona mashindano hayo yameshirikisha watoto wa kike wanaocheza mpira wa miguu.Mhe. Shonza alisema wanambeya wanahaja ya kujivunia vipaji walivyobarikiwa kwa kuwa na wachezaji hodari wa mpira wa miguu, wanariadha, waigizaji na waimbaji wa muziki.

  “Kwa hakika Mbeya mmebarikiwa kuwa na vipaji vingi nami naahidi kuwa Wizara yangu itashirikiana kwa karibu na wadau wa michezo kuhakikisha tunafika mbali ” amesema Mhe. Shonza.Pia Naibu Waziri Shonza amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)kufanya ziara katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ili kuibua vipaji vya wachezaji watakaosaidia kuunda timu nzuri ya vijana chini ya miaka 17.

  Vilevile Mhe. Shonza aliwataka viongozi wa Wilaya ya Mbeya Vijijini , Maafisa Utamaduni na Michezo kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya viwanja vitakavyokuwa vikutumika kwa ajili ya michezo na sanaa.Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njezi amesema kuwa michezo ni chanzo cha ajira na ujenzi wa afya bora hivyo ni budi kuzingatiwa .

  Hata hivyo Mhe. Njezi alieleza kuwa japokuwa mashindano hayo yamefanikisha kukusanya vijiji 200 katika michuano ya awali ukosefu wa wadhamini ndiyo changamoto kubwa walikabiliana nayo pamoja na ukosefu wa viwanja vya mpira.

  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto akizungumza na Wakazi wa Vingunguti juu ya namna alivytokeleza ahadi zake kwa kata hiyo alizoahidi wakati wa uchaguzi kabla ya kuchaguliwa katika kipindi cha Miaka miwili iliyopita
    Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto akikabidhi pikipiki kwa kikundi cha Vijana wajasiliamali kinachojulikana kwa jina la Watoto Pori hili iweze kuwasaidia katika kutunisha mfuko
   Kundi la Vijana wajasilimali wa Kata ya Vingunguti lijulikanalo kama Watoto pori wakifurahi mara baad aya kupokea pikipiki yao aina ya Boxer kutoka kwa  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto
  Wananchi waliofika katika mkutano wa  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto alipokuwa akitoa maelezo ya nini amefanya ndani ya Miaka miwili na kukabidhi pikipiki kwa watoto pori

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni mjini Zanzibar wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Zantel na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ikiwa ni ushirikiano wa kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa kutoka Zantel. Kushoto ni Mkuu Zantel kisiwani Zanzibar, Mohamed Mussa Baucha.

  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (kulia) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (Aliyekaa katikati) wakitia saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa hivi karibuni mjini Zanzibar. Anayeshuhudia kulia ni Makamu wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bi. Khadija Shamte Mzee.
  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (kulia) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (Aliyekaa katikati) wakitia saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa hivi karibuni mjini Zanzibar.
  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (wa pili kushoto) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (wa pili kulia) wakipeana mkono huku wakishuhudiwa na Makamu wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bi. Khadija Shamte Mzee (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Utendaji wa biashara Zantel, Shinuna Kassim baada ya kutiliana saini ya makubaliano na ushirikiano katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Zanzibar. 


  Zantel kwa kushirikiana na Bodi ya Mamlaka ya Mapato ya Zanzibar wameingia katika makubaliano ambayo yatawawezesha wakazi wa kisiwani hapa kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa inayotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel.

  Ushirikiano huo unawezesha wateja wote wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuweza kufanya miamala ya malipo ya kodi bila usumbufu wowote kupitia EzyPesa.

  Hii inamaanisha kwamba walipa kodi wa ndani wataweza kulipa kodi zao husika ikiwamo ushuru wa forodha na kodi zingine kama PAYE na VAT kwenye uingizaji wa biadhaa kupitia mfumo wa EzyPESA.

  Akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano hayo Alhamisi ya tarehe 14 Desemba 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Sherif El Barbary akiwa ameambatana na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Amour Hamil Bakari na Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa (Baucha) alisema lengo kuu la huduma hiyo ni kuwawezesha wakazi wa Zanzibar kulipa kodi kwa urahisi zaidi kupitia huduma ya EzyPesa ya Zantel.

  Alisema kuwa hatua hiyo ya makubaliano inaendana sawa na dira ya Bodi ya Mapato Zanzibar, yenye lengo la kuwa kitovu cha ukusanyaji mapato chenye ufanisi, jambo ambalo litaiwezesha nchi kuongeza pato la taifa la ndani kwa mwaka (GDP).

  “Kama tunaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kupitia huduma ya EzyPesa na pato la Taifa GDP litaongezeka zaidi. Hii itasaidia kuimarisha uchimi wa Taifa zima, na kwa namna nyingine kipato cha mwananchi wa kawaida kitaongezeka.

  Alisema Zantel ni miongoni mwa kampuni inayoongoza katika kuchangia malipo makubwa ya kodi kwa Serikali ya Zanzibar na mtandao huo utaendelea kuhakikisha unaendelea na utaratibu wa kusaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Bodi ya Mapato ya Zanzibar ili kuhakikisha kwamba wanakusanya kodi kwa kadri wanavyoweza kupitia huduma ya EzyPesa.

  Takwimu zinaonyesha kwamba Zantel inalipa Shilingi blioni 2 kama kodi kwa serikali ya Zanzibar kila mwezi ambapo ni takribani shilingi 24 bilioni kwa mwaka.

  “Lengo la ushirikiano huu ni kuhakikisha tunawasogezea wananchi huduma za ulipaji kodi karibu na maeneo yao, nikimaanisha kuwa sasa hawatohitaji kupoteza muda mwingi kuzifuata huduma za kodi ofisini kwetu bali zitakuwepo viganjani mwao,” alisema Kamishna wa Kodi wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Amour Hamil Bakari. Alisema lengo kuu la Bodi ya Mapato Zanzibar ni kusogeza huduma karibu kwa wateja wake, kuimarisha shughuli za utendaji wa kila siku za taasisi hyo ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mbadala za kuongeza ukusanyaji wa mapato Zanzibar

  0 0

  TADB Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (left) chats with Head of Delegation from GCAM Mr. Jalal Bouchama (right) at the farewell ceremony in Dar es Salaam.
  TADB’s Director of Treasury and Funding, Mr. Albert Ngusaru (right) talks to GCAM’s Director of Credit Information System, Mrs. Sanae Benmali (left) and IT Developer, Ms. Sara Nachid (centre) during the farewell ceremony in Dar es Salaam.
  Head of delegation from Group Credit Agricole of Morocco, Mr. Jalal Bouchama (left) who is a Director of Engineering and Agro business receives a souvenir from TADB Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (right) during the farewell ceremony in Dar es Salaam.
  GCAM’s Director of Credit Information System, Mrs. Sanae Benmali (left) smiles after given a Tinga Tinga souvenir by TADB Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (right).
  GCAM’s IT Developer, Ms. Sara Nachid (left) poses for a photo after given a Tinga Tinga souvenir by TADB Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (right).
  TADB Management with a group photo with GCAM Delegation after a farewell ceremony in Dar es Salaam.  Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) has paid a farewell to the delegation from Group Credit Agricole of Morocco (GCAM) which was in country for 11 days mission.

  The delegation was in Tanzania to develop and facilitate TADB’s Credit Scoring System which is to be used in scoring small holder’s farmer’s projects as well as implementing the operationalization of the signed MoU.

  TADB and GCAM signed a memorandum of Understanding (MoU) in October 2016.The signed MoU intends to promote productive investments in the agriculture sector and development of agro-industrial value chain in Tanzania and Morocco.

  According to the TADB Management, these objectives will be achieved through promotion of financing and support systems, especially for smallholder’s farmers.

  The delegation from GCAM was led by Director of Engineering and Agro business, Mr. Jalal Bouchama, other members include Chief of Agroindustry Department, Mrs. Sanae Benmali, Director of Credit Information System, Mr. Abdessamad Danguir and Ms. Sara Nachid, IT Developer.

  TADB is first financial institution in Tanzania to get assistance from GCAM, which aim to enhance agricultural activities and to stabilize rural populations by improving their living standards.

older | 1 | .... | 1464 | 1465 | (Page 1466) | 1467 | 1468 | .... | 1897 | newer