Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

AIRTEL YATANGAZA KUONGEZA GB BANDO ZA YATOSHA INTANETI

$
0
0
Meneja Masoko Airtel Tanzania Aneth Muga akitoa Maelezo wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali nchini kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ .
Baadhi ya watangazaji wa radio mbalimbali nchini wakifuatilia mada kwa umakini wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali nchini na Airtel kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekutana na watangazi wa radio mbalimbali nchini na kuongelea ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia kuzinduliwa kwa bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zilizozinduliwa mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo lengo la kuwapatia wateja na watumiaji wote wa intaneti bando nafuu zaidi.

Meneja Masoko Airtel Tanzania Anethy Muga alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bado za gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kupata MB 40. Vilevile ofa kabambe ya ‘SMATIKA Yatosha bando’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”

kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Yatosha mpya inakupa bado za siku, wik, mwezi gharama nafuu kuliko zote nchini, kwa mfano bado ya 5,000 zamani ilikuwa na GB 1, kwa sasa Yatosha Intaneti Mpya unapata GB 2 kwa siku 7, vile vile kwa shilingi 10,000 zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7 lakini sasa tumeliongeza zaidi unapata GB 6 zakutumia wiki nzima. Alieleza Muga

“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni ishara ya Airtel kuanza vyema shamrashamra kusherehekea sikukuu kwa kuwapatia uhakika wateja na watumiaji wa huduma ya intaneti wa kutoishiwa bando kwa muda mfupi,

Ukiwa na Airtel Yatosha Intaneti hainaga kuzima data tena!” Alisisitiza Mmbando.

SAFARI YA WAZALENDO 47 ILIVYOINGIA SIKU YA PILI WAKATI WAKIELEKEA KILELE CHA UHURU,KATIKA MLIMA KILIMANJARO.

$
0
0

Baada ya kupumzika katika kituo cha Mandara katika siku ya kwanza ,Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara aliongoza Wazalendo 47 kutoka jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),Wanahabari,Marafiki wa China na Tanzania pamoja na watumishi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika siku ya pili ya kuelekea kilele cha Uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania.
Miongoni mwao alikuwepo ,Balozi Mstaafu na Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii ,Tanzania ,Charles Sanga.




Safari ya kuelekea kituo cha pili cha mapumziko cha Horombo ili chagizwa na nyimbo mbalimbali ambazo ziliongeza morali kwa wapandaji.


Makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliwakilishwa vyema na Meneja wake wa Mawasiliano ,Pascal Shelutete .

Mwanahabri Vicky Kimaro aliwakilisha pia Magazeti ya serikali ya HABARI LEO.
Mwanahabari George Mbara alikiwalisha vyema kituo cha luniknga cha ITV.
Mwanahabari Jamila Omar yeye alifanya uwakilishi wa kituo cha Luninga cha Channel ten.
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) liliwakilishwa na Bertha Mwambela
Na Safari iliendelea ikiongozwa na Slogan ya "Mdogo Mdogo"
Mapumziko yalikuwepo mara baada ya kutembea sehemu yenye umbali mrefu.
Wengine walitumia mapumziko hayo kwa ajili ya kupata picha za kumbukumbu ya pamoja.
Na baadae Safari iliendelea.
Hali ya hewa katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro haitabiliki ghafla linaweza onekana jua na muda mchache tu mvua ikanyesha ,hivyo wapandaji hua wamejiandaa na aina yoyote ile ya hali kama inavyoonekana hapa wakiwa katika mavazi rasmi ya kuzuia mvua pindi walipowasili eneo la Nusu njia kwa ajili ya kupata chakula.

Wazalendo wakatumia mapumziko ya Nusu njia kupata chakula cha mchana.
Safari ikaendelea kwa kupita katika mito mbalimbali ambayo imekuwa ikitiririsha maji kwa wingi.
Wazalendo walipita katika madaraja mbalimbali wakati wa upandaji wa mlima huo.
Wenye kuhitaji msaada walipata kwa wakati.



Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook alihakikisha anaongozana na Wazalendo hao katika safari ya kuelekea kilele cha Uhuru akiwa ndiye mwenyeji wa ugeni huo.
Hatimaye safari iliyoanza saa 2:30 za asubuhi katika kituo cha mapumziko cha Mandara ikahitimishwa majira ya saa 11:00 za jioni katika kituo cha mapumziko cha Horombo kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kuelekea kituo cha Kibo kabla ya kuelekea kilele cha Uhuru.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa katika msafara wa Wazalendo hao.

KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD YAZINDUA BIDHAA ZA SUGAR FREE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu (kulia), Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga  na Dk. Mohamed Mohamed wa ugonjwa wa Kisukari katika hospitali hiyo wakikata keki maalumu iliyotengenezwa kwa bidhaa hiyo kuashiria uzinduzi wa bidhaa za Sugar Free uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Muonekano wa keki hiyo
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga akikabidhiwa zawadi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akipatiwa zawadi.

 Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
 Uzinduzi huo.
 Makofi yakipigwa katika uzinduzi huo.
 Hii ndiyo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo.
 Meza kuu ikifuatilia mada katika uzinduzi huo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga, akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mada zikitolewa kuhusu bidhaa hizo.
 Maelezo kuhusu bidhaa hizo yakitolewa.
 Majadiliano yakifanyika.
 Taswira ya ukumbi wakati wa uzinduzi huo.
Ukumbi ulivyokuwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Abacus Pharma (A) LTD imezindua bidhaa za Sugar Free ambazo zitatumika kukabiliana na ongezeko la wagonjwa wa kisukari nchini kutokana na bidhaa hizo kutokuwa na sukari wakati wa matumizi yake.

Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Best Western, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 

Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.

"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.

Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza katika uzinduzi huo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.

Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika.

Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.

Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.

MASHIRIKA 40 YAUNGANA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality fo Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), akizungumza na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia katika mkutano wa pamoja uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Pugu Poverty Alleviation and Development Agency (PPADA), Abraham Silumbu, akitoa taarifa ya utafiti walioufanya katika Soko la Tandale na Magomeni.
 Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
 Ofisa Ufutiliaji na Tathmini wa Shirika la Eguality for Growth (EfG), Shabani Lulimbeye, akitoa mada kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wadau wakisikiliza mada 
 Mkurugenzi wa Shirika la Esscreative and Legal Foundation, Erick Mukiza akimuelekeza jambo Mwanasheria mwenzake, Mchala Hamisi kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Shirika la Wodevota, Catherine Mhagama kutoka mkoani Ruvuma akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Shirika la Nurget Development in Tanzania (NDT), Hemed Ngochele akichangia jambo. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania (Tamwa), Neema Bishubo.
 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi wa EfG, Susan Sita, akiwa katika mkutano huo.
Mratibu wa Programu wa Shirika la Tanzania Network of Women, Kennedy Godwin akichangia jambo.

Na Dotto Mwaibale

Mashirika 40 yasiyo ya kiserikali yameungana na Shirika la Equality for Growth (EfG) katika kukabiliana na ukatiti wa kijinsia masokoni dhidi ya wanawake.

Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa wadau kutoka katika mashirika hayo, Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi wa EfG, Susan Sita alisema shirika hilo liliona ni vizuri kupanua wigo wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia masokoni kwa kuyashirikisha mashirika mengine.

"Tuliona ni vizuri kuyashirikisha mashirika mengine katika mapambano haya ambapo mashirika 40 kutoka Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni yalikubali kati ya hayo manne yameanza kufanya kazi hiyo rasmi kwenye masoko ya Magomeni na Tandale wilayani Kinondoni," alisema Sita.

Aliongeza kuwa, mkutano huo malengo yake ni kuelezea mradi wa mfano kwa wadau na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuaya la utoaji haki ili kupanua wigo wa utoaji wa taarifa juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanyika kwenye masoko.

Alitaja malengo mengine ni kuona mashirika mengine yanavyoweza kutumia mradi wa mfano wa sokoni na kuusambaza katika masoko mengine Tanzania ikiwa ni pamoja na kuandaa mikakati ya pamoja na namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Jane Magigita alisema ushirikishaji wa mashirika hayo ulianza mwaka 2015 na kazi kubwa ya mashirika hayo ni kuwakomboa wanawake masokoni kwa kupinga ukatili wa kijinsia.

Alitaja kazi nyingine ni kuboresha uhusiano kati ya wanawake wafanyabiashara na maofisa wa masoko katika kujenga uwajibikaji pamoja na kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni wanafanya shughuli zao kwenye mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kiuchumi, kimwili, matusi na  kisiasa huku wakipewa heshima kama binadamu wengine na kujipatia kipato chao bila ya vikwazo.

"Tunahitaji kuona tunafanikisha ushirikiano kati ya watekeleza sheria, kamati za masoko, viongozi na maofisa wa Manispaa,  Polisi na wafanyabiashara wote katika kudhibiti ukatili wa wanawake katika masoko," alisema Magigita.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Pugu Poverty Alleviation and Development Agency (PPADA), Abraham Silumbu alisema ushirikiano huo umewapa mori wa kazi kwani utasaidia kupunguza vitendo hivyo vya kikatili masokoni nchini.

"Kwa kweli tumeanza kuona matunda ya ushirikiano huu tumepanga mapambano haya kuyapeleka katika masoko yote hapa nchini," alisema Silumbu.

VIONGOZI WA KIJIJI CHA MSOSA WILAYANI KILOLO WAVULIWA MADARAKA KWA NGUVU

$
0
0
mtendaji wa kata ya Ruaha Mbuyuni Maiko Chabili akiwafafanulia jambo wananchi wa kijiji wakati wa mkutano wa hadhara ulikuwa na lengo la kuwafukuza kamati ya mipango na fedha ya kijiji kwa matumizi mabaya ya pesa zao
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya ruaha mbuyuni walihudhuria mkutano wa hadhara wa kijiji



Na Fredy Mgunda,Iringa.


Wananchi wa kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya ruaha mbuyuni wameifukuza kamati ya mipango na fedha kwa tuhuma za kufanya ubadhilifu wa mali za kijiji na kuunda kamati mpya itakayoleta maendeleo katika kijiji hicho.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho wanachi waliutaka uongozi wa kamati hiyo kuachia ngazi kutokana na tuhuma zinazowakabili. Kwa upande wake mtendaji wa kata MAIKO CHABILI ameafiki kuvuliwa madaraka kwa viongozi wa kamati ya mipangano na fedha kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Hata hivyo kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha msosa walikubali kujiudhuru na kulipa pesa ambazo ilibaini kuwa walizitumia vibaya bila ruhusa ya wananchi.

TABIA ZA KUEPUKA ILI UWE MWENYE AFYA BORA

$
0
0
Na Jumia Food Tanzania

Chakula huupatia mwili virutubisho ili uweze kufanya kazi kwa ufasaha. Chakula pia ni sehemu ya mila na utamaduni wa watu. Hii inamaanisha kwamba kwa baadhi ya watu chakula kina muunganiko mkubwa na hisia zao. Kwa watu wengi, kubadili tabia na mienendo ya kula vyakula vya aina fulani ni jambo gumu kutekelezeka.
Kuna uwezekano umekuwa na aina fulani ya tabia za vyakula unavyokula kwa muda mrefu ambazo haujagundua kama si nzuri kiafya. Au, tabia hizo zimekuwa ni sehemu ya maisha yako ya kila siku, kwa hiyo hauzifikirii sana.
Katika maisha ya sasa imekuwa ni changamoto sana kuthibiti aina ya vyakula tunavyokula ambavyo kwa mujibu wa wataalamu wa afya ni hatari. Jumia Food ingependa kukushauri juu ya hatua za kufuata ili kuachana na tabia au mienendo ya vyakula unavyokula na kukudhuru kiafya kwa namna moja ama nyingine.
Fuatilia mwenendo wa tabia zako. Ni jambo zuri kufuatilia tabia za vyakula unavyopendelea kula. Unaweza kufanya hivi kwa kurekodi kwenye kijitabu kidogo ndani ya kipindi cha muda fulani kama vile kwa wiki. Andika chakula unachokula, kwa kiwango gani, na ni muda gani huwa unakula. Pia weka maelezo kuwa ulikuwa kwenye mazingira na hali gani, kama vile njaa, msongo wa mawazo, uchovu, au kuboreka. Kwa mfano, inawezekana ulikuwa upo kazini umechoka na ukaamua kununua soda au chokoleti kujiburudisha. Mwisho wa wiki, pitia kijitabu chako ili kujua mwenendo wa tabia za ulaji wako. Amua ni tabia zipi ungependa kuzibadili.   
Tafakari. Baada ya kufuatilia na kujua mwenendo wa tabia zako, ni vema kutafakari juu ya mambo yanayokupelekea kuwa na tabia hizo. Je, kuna mazingira ambayo ukiwa karibu nayo yanakufanya ule au uchague aina fulani ya chakula huku ukiwa hauna njaa? Je, ni namna unavyojisikia ndiko hukufanya ule aina fulani ya chakula? Pitia kwa makini kumbukumbu zako na kujua ni mara ngapi tabia hizo huwa zinajirudia. 

Kwa mfano, kula pale unapokiona kile chakula unachokipenda unapopita dukani au kukiona kwenye tangazo luningani au kuboreka na mazingira fulani au kutokuwa na mpango wa kupika usiku. Anza kwa kujikita zaidi kwenye tabia ambazo hujirudia zaidi ndani ya wiki, kisha fikiria namna ya kuziepuka hizo tabia kama vile kutopita karibu na sehemu ambapo wanauza vyakula unavyovipenda au kuamua mapema mpango wa kula usiku.    
Badili tabia zako za zamani. Ukishatafakari mwenendo mbaya wa tabia za ulaji wako kinachofuatia ni kufanya mabadiliko. Kwa mfano, kama huwa unapendelea kunywa soda pale unapochoshwa na kazi badili na kunywa maji au hata badili shughuli unayoifanya ndani ya muda mfupi. Mbali na kubadili tabia, kama ni vigumu kubadili moja kwa moja, angalau punguza kiwango cha tabia hiyo. Kama ulikuwa unatumia chakula hiko kwa kiwango kikubwa, punguza kidogo.  
Zifanyie mazoezi tabia mpya. Inaweza kuchukua muda mrefu kubadili tabia za zamani, na zile za kiafya zaidi. Kumbuka, ilikuchukua muda mrefu kuwa na tabia ulizonazo. Hivyo hivyo, itakuchukua muda kuzibadili pia. KWA HIYO USIKATE TAMAA.
Kwa kumalizia, Jumia Food inakusisitiza kwamba endapo utajikuta unaanza kuzifikiria tabia za zamani, tafakari kwa makini ni kwanini unataka kuzirudia. Jaribu tena kuzibadili. Kuteleza kwenye kufanya jambo fulani hutokea, na hakumaanishi kwamba umeshindwa. Endelea kujaribu tena na tena! 

OFISI YA MWASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

$
0
0
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe. George Masaju  na  Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu akimkaribisha Mhe Waziri wa Katiba na Sheria  kuzindua Baraza  la Wafanyakazi na katika salamu zake alisema ni muhumu kwa Serikali  kuendelea kuiimarisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kutokana na   umuhimu wake  katika maendeleo ya nchi, kiuchumi, kiusalama, katika utawala wa sheria na katiba
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Profesa Paramagamba Kabudi akitabasamu mara baada ya kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  siku ya jumatatu. Baraza hilo linakutana kwa siku mbili katika ukumbi wa LAPF mkoani Dodoma.
 Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo, wajumbe wa   Baraza ni pamoja na  Mawakili  Wafawidhi wa Serikali, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Wajumbe wa TUGHE na mada mbalimbali zilitolewa wakati wa uzinduzi hao.




Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe. George Masaju amesema,  kutokana na mchango mkubwa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika maendeleo ya  kiuchumi, usalama, utawala wa sheria na utawala bora, Kuna   umuhimu wa Serikali kuendelea kuiimarisha Ofisi  hiyo.

Ameyasema hayo  wakati akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe Profesa Palamagamba Kabudi kuzindua Baraza la  Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uzinduzi wa  baraza hilo  umefanyika siku ya jumatatu katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la LAPF  Mkoani Dodoma.

Uzinduzi wa Baraza hilo,  ulitanguliwa  na  uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi.  Zoezi la uchaguzi lilisimamiwa na  Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. John Mchenya,  Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa Bi. Jane Mbura na  Afisa Kazi Bi. Razina Tuusa.  Waliochaguliwa kwa kura  za  Siri ni  Wakili wa Serikali Mkuu Monica Mbono ambaye anakuwa  Katibu na  Bw. Michael Masanja anakuwa  Katibu msaidizi.

Mhe. Masaju  akiwa ni  Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi, ameyataja maeneo ambayo  Serikali  inatakiwa kuendelea kuyaimarisha katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ni pamoja na,  Raslimali fedha, mafunzo, makazi salama kwaajli ya  mawakili wa serikali na  miundombinu ya ofisi.

“Mhe. Waziri, yapo masuala ya kisera ambayo tunaomba  Serikali  inayashughulikie  ipasavyo ili kuiwezesha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Maeneo hayo ni  kuajiri Mawakili wa Serikali na Watumishi wa Kada zingine, kujenga majengo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  katika Ofisi  za Wilaya na Mikoa ili  kuokoa fedha inayotumika kulipia pango”. Ameleza Mwanasheria Mkuu.

Kwa upande wa mafunzo,  Mwanasheria Mkuu, ameishauri Serikali  katika  kuwajengea uwezo wa kitaalam Mawakili wa Serikali na  watumishi wenzao katika maeneo ya kipaumbele na kuimarisha maslahi ya mawakili wa serikali na watumishi wote katika Ofisi ya  Mwanasheria  Mkuu wa Serikali.

Pamoja na kutaja changamoto mbalimbali ambazo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekuwa ikikabiliana nazo katika utekelezaji wa Majukumu yake. Mwanasheria Mkuu  ametaja mafanikio ambayo Ofisi imeyapata katika utekelezaji wa  majukumu yake.

            Baadhi ya mafanikio hayo ni  pamoja na kuokoa fedha nyingi na kuingiza serikalini mapato kupitia uendeshaji wa mashtaka na mashauri mbalimbali mahakamani na katika  mabaraza ya usuluhishi, ushiriki katika majadiliano ya Mikataba na uhakiki wake na kudumisha utawala wa sheria na  utengamano nchini.

Mafanikio mengine ni  pamoja na  kuingiza serikalini kiazi cha shilingi  1.039 Bilioni iliyotokana na faini  baada ya  serikali kushinda kesi 110 zinazohusiana na makosa chini ya sheria ya  uhifadhi wa wanyamapori ya mwaka 2009.

            Mafanikio mengine ni urejeshwaji wa mali zilizopatikana  kwa njia ya uhalifu  ambapo kesi 10 zilitolewa uamuzi na mali zenye thamani  ya zaidi ya   Bilioni  2  zilitaifishwa.  Vile vile    Serikali ilishinda kesi 3 zinazohusiana na utakatishaji wa fedha haramu ambapo mbali na watuhumiwa kutiwa hatiani  kiasi cha fedha kipatacho shilingi milioni 29,439,452 kilitaifishwa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali akifafanua zaidi mafanikio yanayotokana na  majukumu ya Ofisi yake kuwa ni  yale  yanayotokana na mashauri mawili yanayohusu  kuingiza nchini magari mawili ya kifahari yaliyotolewa uamuzi kwa watuhumiwa kupatikana na hatia na magari  hayo ambayo  thamani yake ni shilingi bilioni 1.7 yalitaifishwa kuwa mali ya serikali na fidia ya shilingi milioni 200 kulipwa serikalini.

Akizindua  Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi alipongeza uamuzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  kuzindua Baraza lake na kukutana kwa siku mbili kujadili masuala mbalimbali.

Kwa mujibu wa  Waziri Kabudi, Baraza la Wafanyakazi ni chombo cha kupanga   mipango muhimu na kuhakikisha kuwa kinafanyika pia katika kutathmini  ambacho Ofisi imepanga kukifanya na  kimefanyika  kwa kiwango gani.

Akasema “sote tu mashahidi kuwa tangu  Serikali ya Awamu ya  Tano iingie madarakani  msisitizo umekuwa kwa kila taasisi kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yake. Awamu hii inasisitiza watumishi na taasisi kuondokana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha utendaji wao  unaleta tija katika serikali” ameeleza Waziri

Na akalitaka Baraza hilo la wafanyakazi kutathimini ni jinsi gani  linaishauri serikali na taasisi zake katika masuala yote kwa kuhakikisha kwamba ushauri unaotolewa unabeba maslahi mapaba ya taifa na kuzingatia vipaumbele vya serikali ya awamu ya tano

Akasisitiza pia kwamba tathmini hiyo inatakiwa kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza kama m Miswada inayoadaliwa inakidhi vigezo vya kitaalam, je inabeba maslahi mapana ya nchi, au je jukumu la kuiwakilisha Serikali mahakamani liinatekelezwa kwa kiwango gani cha ufanini, je kesi na mashauri yote yanasimamiwa na kuendeshwa kwa weledi na uzalendo na ni kwa kiasi gani uratibu wa upelepezi na uendeshaji wa mashauri unafanyika kwa weledi na umakini.

Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  linahudhuriwa na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  ambaye ni  Mwenyekiti wa Baraza,  naibu Mwanasheria Mkuu, Bw. Gerson Mdemu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti , Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Biswalo Maganga, Mawakili  Wafadhiwi kutoka Mikoa yote na  Wilaya ambako kuna Ofisi  za Mwanasheria Mkuu wa Serikali,   Wakuu wa Divisheni na  Vitengo na  Na wajumbe wa TUGHE.

Aidha mada mbalimbali zinatolewa zikiwamo zinazohusu maadili katika utumishi wa umma na utunzaji wa siri za serikali. 

Bharti Airtel signs agreement to acquire Millicom’s operations in Rwanda

$
0
0
·         Acquisition to consolidate the Rwandan telecom market and position Airtel as a strong number 2 operator in Rwanda with revenues of over USD 80 million and a revenue market share of over 40%

·         Existing Millicom Rwanda customers will join over 370 million customers on Airtel’s global network across 17 countries and enjoy the benefits of a superior network, international roaming, and high quality 3G, 4G speed as well as Airtel Money services

 Bharti Airtel Limited (“Airtel”), a leading global telecommunications services provider with operations in 17 countries across Asia and Africa, today said that, through its subsidiaries, it has entered into a definitive agreement with Millicom International Cellular S.A. ("Millicom") under which Airtel Rwanda Limited (“Airtel Rwanda”) will acquire 100% equity interest in Tigo Rwanda Limited (“Tigo Rwanda”). The acquisition will consolidate the Rwandan telecom market and position Airtel as a strong number 2 operator in Rwanda. The consideration for the transaction is based on approximately 6x EBITDA multiple, payable over two years. The agreement is subject to regulatory and statutory approvals.

Sunil Bharti Mittal, Chairman, Bharti Airtel, said, “Airtel has taken proactive steps in Africa to consolidate and realign the market structure in the last few remaining countries where its operations are lagging on account of lower market share and presence of too many operators. Airtel and Tigo have already merged their operations to create a strong viable entity in Ghana. Today, it has taken yet another important step to acquire Tigo Rwanda to become a profitable and a strong challenger in a two-player market.

We are also committed to the long term viability of our operations in two other countries i.e. Kenya and Tanzania, to ensure that in 2018 all our 15 operations in Africa start contributing positive margins and cash flows towards a healthy and profitable Airtel Africa.”

The agreement aims to bring together the strengths of Airtel and Millicom in Rwanda and offer benefits to customers in the form of a wider network, affordable voice and data services, and superior customer care. The existing customers of Tigo Rwanda will join Airtel’s global network, which currently serves over 370 million customers across 17 countries. They will enjoy, amongst other things, benefits of the ‘One Airtel’ network with lower roaming rates across Africa and South Asia, an exciting bouquet of innovative services including Airtel Money.

Raghunath Mandava, MD and CEO, Airtel Africa, said, “The acquisition reinforces our commitment to the Rwanda market and is a significant step towards creating a stronger presence in the country. It will create synergies with our existing business and help boost operational efficiencies in the market. The Rwandan telecom market will significantly benefit from this acquisition, further reiterating our stand that in-market consolidations do not just help achieve better market positions but benefit customers and the industry as a whole.”

On completion, the proposed acquisition will undergo seamless integration, both on the customer as well as the network side, and further strengthen our market position.

Over the years Airtel has been solidifying its market position to become a key player in the continent with in-country acquisitions. In the past, Airtel acquired assets in Uganda (Warid) and Congo B (Warid), Kenya (yu Mobile) and consolidated operations in Ghana (Millicom). The customers in these markets today enjoy a superior and wider network, affordable voice & data services, Airtel Money and better customer care.

With presence across 15 African countries, Airtel is one of the largest telecom service providers across the continent in terms of geographical reach and had close to 83 million customers at the end of quarter ended September 30, 2017. Globally, Airtel is ranked as the third largest mobile services provider in terms of customer base.

HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM ... 9 WA CCM DODOMA, 18 DEC 2017

RAIS MAGUFUL ATOA MILIONI 210 KWA AJILI YA UJENZI WA MRADI WA UMEME SONGEA HADI MAKAMBAKO.

$
0
0
Serikali Kupitia Wizara Ya Nishati Imetoa Kiasi Cha Shilingi Milioni 210 Kwa Ajili Ya Mradi Wa Umeme Kupitia Makambako Hadi Mkoani Ruvuma ambao utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 22,000 sawa na vijiji 120 kwa mikoa yote miwili RUVUMA na NJOMBE.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TASAF AWATAKA WATUMISHI WA TAASISI HIYO KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMM KWA VITENDO.

$
0
0
Estom Sanga- TASAF

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF- bwana Ladislaus Mwamanga amefungua kikao kazi cha Watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam na kuwaagiza wazingatie misingi ya Utumishi wa Umma ili kufanikisha jukumu la kuwahudumia wananchi na hivyo kusaidia jitihada za serikali za kupambana na umaskini kwa vitendo.

Bwana Mwamanga amesema Watumishi wa taasisi hiyo wanalo jukumu kubwa mbele yao katika kutekeleza mkakati wa kuwaondolea wananchi kero ya umaskini kazi ambayo amesema mafanikio yake yatapimwa kulingana na mabadiliko ya maisha ya wananchi wanaohudumiwa na Mfuko huo kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Masikini-PSSN.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amewakumbusha wajibu wa watumishi wa taasisi hiyo kuzingatia maadili bora ya utumishi wa umma na kutumia waledi walionao katika kutoa huduma bora kwa walengwa na wananchi wanaotegemea huduma zake kote nchini.

Akizungumzia mafanikio ya PSSN, Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema tangu kuanza kwa Mpango huo, Walengwa wake wameonyesha nia ya dhati ya kuondokana na umaskini kwa kuanzisha miradi midogo midogo huku wengine waboresha makazi yao na kuzingatia masharti ya Mpango katika sekta za elimu, afya na lishe.

Amesema kinachosisitizwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa walengwa hao wanaweka misingi imara ya kujitegemea kwa kufanya kazi za kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao, kama ambavyo maelekezo ya serikali yanavyosisitiza.

Bwana Mwamanga pia amezungumzia namna taasisi yake ilivyoweka mkazo katika ushirikishwaji wa sekta nyingine zikiwemo za maendeleo ya jamii,mifugo na kilimo katika kiuboresha shughuli za walengwa za kujiongezea kipato na kukuza uchumi wao.TASAF hivi sasa inahudumia kaya za walengwa zipatazo MILIONI MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

Kikao kazi hicho kinachowajumusha watumishi wa taasisi hiyo kutoka mikoa yote nchini pamoja na mambo mengine kitapitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Maandalizi sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya maskini na kupata taarifa ya Maafisa Ufuatiliaji juu ya kazi wanazozifanya kwenye maeneo yao ya kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga (aliyeshika kipaza sauti) akifungua kikao kazi cha watumishi wa taasisi hiyo(hawapo pichani ) kinachofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyi mjini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa fedha Bi. Chiku Thabiti, na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Miradi bw. Amadeus Kamagenge. 

Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka baadhi ya watumishi waliopoteza maisha au kupoteza ndugu na jamii zao katika kipindi cha mwaka huu kabla ya ufunguzi rasmi wa kikao kazi chao kinachofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya Watumishi wa TASAF wakiwa katika kikao kazi chao cha kufunga Mwaka katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo,bwana Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) alipofungua kikao hicho.
Watumishi wa TASAF wakifuatialia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi chao kilichoanza leo ,kilichofunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Bwana Ladislau Mwamanga (hayupo pichani.

WAZIRI MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA USHAURI WA MAZINGIRA(NEAC) MKOANI DODOMA

DOKTA MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA NORWAY

$
0
0
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) akizungumza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) mjini Dodoma. Kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza kuhusu umuhimu wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya nchi alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiangalia zawadi ya kitabu kinachohusu masuala ya uchumi na fedha aliyopewa na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad (kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yao Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodoma.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) akiwakabidhi zawadi za vitabu kuhusu uchumi, Kamishna wa Bajeti-Bi Mary Maganga (kushoto) na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga (wa pili kushoto) wakishuhudiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akimsindikiza mgeni wake Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) baada ya kumaliza mazungumzo yao Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodoma.
Balozi wa Noray hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyojikita katika namna ya kuimarisha zaidi uhusiano katika ya Norway na Tanzania, mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango



Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad na kutoa wito kwa wawekezaji kutoka Norway kuja kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo Nishati, misitu, kilimo, gesi na mafuta.

Dkt. Mpango amemweleza Balozi huyo kwamba Tanzania iko katika hatua mbalimbali za kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda na kwamba wawekezaji kutoka Norway watakuwa na mchango mkubwa wa kuiwezesha Tanzania kufikia lengo hilo.

Aliyataja maeneo ya kuongeza thamani ya mazao ya misitu, mifugo, uvuvi, nishati, kilimo na mengine mengi kwamba yataongeza tija katika sekta hiyo na kwamba malighafi za kilimo zitatochea uzalishaji katika viwanda na kuinua kipato cha wananchi.

“Tumeamua kujenga Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa-SGR ambayo inahitaji umeme wa kutosha kwa hiyo bado tunahitaji mchango wa wadau mbalimbali ikiwemo Norway ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na nishati ya umeme ya kutosha na ya uhakika ili kufanikisha mradi huo mkubwa” aliongeza Dkt. Mpango

Kuhusu Sekta Binafsi, Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali imeendelea na majadiliano na Sekta hiyo ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo masuala ya kodi pamoja na kujenga kuaminiana kati ya pande hizo mbili.Amefafanua kuwa Sekta Binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa na kwamba vikao hivyo vya mara kwa mara vimeanza kuzaa matunda.

Ameishukuru nchi ya Norway kwa mchango mkubwa wa maendeleo kwa kusaidia kuboresha masuala ya nishati, kilimo, uboreshaji wa mifumo ya kodi kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kuchangia fedha katika program ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma na kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali kila mwaka.

Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad alisema nchi yake imeridhika na namna Serikali ya Awamu ya Tano inavyopiga hatua kubwa katika maendeleo ya watu wake kupitia kuhamasisha uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa nchi yake imesaini mikataba mikubwa miwili hivi karibuni ukiwemo mkataba wa msaada wa krona milioni 600 (fedha za Norway) kwa ajili ya mradi wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini-REA, hatua anayoamini kuwa itaharakisha maendeleo na uchumi wa kati wa wa nchi ifikapo mwaka 2025 na kuongeza kuwa nchi yake itaendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Amesisitiza umuhimu wa Serikali kuishirikisha kikamilifu Sekta Binafsi katika hatua yoyote inayopiga kuelekea maendeleo ya haraka kwa kuwa sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kufikia mafanikio tarajiwa.

Aliahidi kuendelea kuhamasisha wawekezaji kutoka nchini mwake kuja kuwekeza Tanzania na kushauri kuwa wakati mambo hayo yakiendelea, Tanzania ihakikishe kuwa sera zake za uchumi zinakuwa imara na hazibadilikibadiliki ili wawekezaji waweze kuamini wako salama.

Alishauri kuwa kila aina ya mabadiliko katika sera za nchi yakiwemo masuala ya kodi yanapaswa kuwa shirikishi ili sekta hiyo iweze kutoa mchango wake kikamilifu baada ya kushirikishwa katika maamuzi mbalimbali na kupongeza hatua ya Serikali ya kukutana na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kujadiliana kuhusu masuala mtambuka.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AKUTANA NA UONGOZI WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akizungumza jambo kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere walipomtembelea ofisini kwake Desemba 19, 2017 Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akizungumza jambo kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere walipomtembelea ofisini kwake Desemba 19, 2017 Dodoma.


Katibu Muyeka Msitaafu wa Hayati Mwalimu J. Kambarage Nyerere akieleza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora walipomtembelea Ofisi kwake Dodoma.
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora walipomtembelea ofisini kwake Dodoma na kufanya mazungumzo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere walipomtembelea Dodoma Leo.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Joseph Butiku na kushoto ni Bw.Samwel Hussein Kasori.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA

Balozi, Dkt. Ramadhani Dau Awasilisha Hati Za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Wa Cambodia

$
0
0
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia anayewakilisha pia nchini Cambodia, Mhe. Dkt. Ramadhani Kitwana Dau (kushoto) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Cambodia, Mtukufu Preah Bat Samdech Preah Boromneath NORDOM SIHAMON. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 28 Novemba 2017 Jijini Phnom Pen, Cambodia. 
Mhe. Balozi Dkt. Dau (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mtukufu Mfalme mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Wanaoshuhudia kulia ni maafisa wa Serikali ya Cambodia na kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 1995. Pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji. Vilevile Mtukufu Mfalme aliahidi kumpa ushirikiano Mhe. Balozi Dkt. Dau katika utekelezaji wa majukumu yake. 
Mhe. Balozi Dkt. Dau akimtambulisha Afisa wa Ubalozi wa Tanzania, Bw. Khatib Makenga aliyeambatana naye katika hafla ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho 
Mhe. Balozi Dkt. Dau akipokelewa mara baada ya kuwasili jijini Phnom Penh, Cambodia.

SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA

$
0
0
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga wameendesha zoezi la kuteketeza vifaa vinavyotumika kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning’wa.

Miongoni mwa vifaa vilivyoteketezwa kwa moto ni nyavu za kuvulia samaki,mitumbwi na vibanda vinavyotumiwa na wavuvi kujihifadhi karibu na bwawa hilo.Zoezi hilo limefanyika leo Jumanne Desemba 19,2017 katika bwawa hilo lenye mita za ujazo milioni 10.9 linalopatikana katika kata za Old Shinyanga,Chibe na Pandagichiza zilizopo katika wilaya ya Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mkurugenzi wa SHUWASA,Injinia Sylivester Mahole alisema lengo la oparesheni hiyo aliyodai ni endelevu, ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwani bwawa hilo ni moja vya vyanzo muhimu vya maji vya mamlaka hiyo ukiachilia mbali Ziwa Victoria. 

“Tumeteketeza kwa moto vifaa vilivyokuwa vinatumika kwa shughuli za uvuvi katika bwawa hili ikiwemo mitumbwi,nyavu na vibanda vilivyokuwa vinatumiwa na wavuvi,tunataka waache mara moja kufanya uvuvi hapa kwani wanaharibu vyanzo vya maji”,alieleza Injinia Mahole. 

Aidha alisema shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo,uvuvi na ufugaji zinaharibu vyanzo vya maji katika bwawa hilo ambapo kina chake kimekuwa kikipungua mara kwa mara. 

“Umeibuka utamaduni wa wananchi kulima bustani pembezoni mwa bwawa kisha kuweka pampu majini wakati huo watumia dawa za mazao ambazo siyo nzuri kwa afya ya binadamu,wananywesha mifugo hapa na kuvua samaki kwa kutumia nyavu na vyandarua”,alifafanua Injinia Mahole. 

Alisema pamoja na kuendelea kufanya vikao na mikutano na wananchi kuwapa elimu ya hifadhi ya vyanzo vya maji bado wananchi wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu katika bwawa hilo hivyo wataendelea oparesheni ya kuharibu vifaa na kukamata watu wote wanaokiuka sheria na kanuni za utunzaji mazingira na vyanzo vya maji. "Tulifanya vikao na mikutano na viongozi pamoja na wananchi wao ndiyo wakatoa azimio la kuondoa watu wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika bwawa hili huku wakiipa SHUWASA jukumu la kusimamia zoezi zima,na sisi tangu mwezi Septemba mwaka huu tumekuwa tukiendesha oparesheni ya kuondoa watu wanaoharibu vyanzo vya maji",aliongeza. 

Aidha aliwataka wananchi kuzingatia kanuni na sheria za hifadhi ya vyanzo vya maji na kwamba hawatasita kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuendelea kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa hilo. Vyanzo vikuu vya maji vya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) ni Ziwa Victoria na bwawa la Ning’wa. 

Mpaka mwezi Novemba 2017 idadi ya maunganisho ya maji yaliyofanywa na SHUWASA mjini Shinyanga ni 18,900 ambapo zaidi ya watu 200,000 wanapata huduma ya maji kutoka SHUWASA. 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akielezea lengo la kuendesha oparesheni ya kuteketeza kwa moto vifaa vinavyotumiwa na wananchi kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning'wa.Kulia ni mwandishi wa habari wa Radio Faraja na DW,Veronica Natalis - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akionesha mifugo katika bwawa la Ning'wa 
Kushoto ni ng'ombe wakiingia katika bwawa la Ning'wa, katikati ni askari polisi akitoa maelekezo kwa wananchi waliokutwa katika bwawa hilo na kuambiwa waondoe mitego ya samaki iliyowekwa katika bwawa hilo. 
Askari polisi akishirikiana na mwananchi kuondoa mtego wa samaki katika bwawa la Ning'wa 
Zoezi la kuondoa mtego wa samaki likiendelea 
Askari polisi aliyevaa kiraia akiondoa nyavu ya chandarua katika bwawa la Ning'wa 
Zoezi la kubomoa mtumbwi likiendelea
Askari polisi wakiendelea kubomoa mtumbwi kwa kutumia nyundo 
Askari polisi akimwaga mafuta kwa ajili ya kuchoma moto nyavu zinazotumika kuvua samaki katika bwawa la Ning'wa 
Moto ukiteketeza nyavu 
Nyavu zikiteketea kwa moto 
Zoezi la kuchoma moto nyavu likiendelea 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akizungumza na mmoja wa wananchi aliyekutwa akifanya shughuli za kibinadamu katika bwawa hilo Jackson Kabanda 
Askari polisi wakiangalia vibanda vinavyotumiwa na wavuvi kujihifadhi karibu na bwawa la Ning'wa. 
Vibanda vinavyotumiwa na wavuvi katika bwawa la Ning'wa vikiteketezwa kwa moto 
Moto ukiteketeza vibanda vya wavuvi katika bwawa la Ning'wa. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

AIRTEL YAENDELEA KUTAMBA NA SMATIKA, YATOSHA INTANETI MPYA...

ZANTEL YAKABIDHI MSAADA WA MAJENERETA KWA TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA, ZANZIBAR

$
0
0


Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar Abdulhamid Idrissa Haji (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini Zanzibar mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya kupokea majenerata matatu kutoka Zantel yatakayowasaidia wanafunzi wa chuo hicho katika masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi ambacho Umeme umekatika.
Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha, akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya kukabidhi majenerata matatu kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar ambayo yatawasaidia wanafunzi wa chuo hicho kwenye masomo yao kama mbadala wa nishati katika kipindi ambacho Umeme umekatika.
Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi majenerata matatu kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, mwishoni mwa juma mjini, Zanzibar. Majenereta hayo yana lengo la kuwasaidia wanafunzi wa chuo hicho kwenye masomo yao kama mbadala wa nishati katika kipindi ambacho Umeme umekatika. Pamoja nae tokea kushoto ni Afisa Mkuu wa Biashara Zantel, George Lliakopoulos, Afisa Mkuu wa Masuala ya Fedha Zantel, Jean-Paul Happart na Kulia ni Afisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur.
Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi majenerata matatu kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, mwishoni mwa juma mjini, Zanzibar. Majenereta hayo yana lengo la kuwasaidia wanafunzi wa chuo hicho kwenye masomo yao kama mbadala wa nishati katika kipindi ambacho Umeme umekatika. Pamoja nae tokea kushoto ni Afisa Mkuu wa Biashara Zantel, George Lliakopoulos, Afisa Mkuu wa Masuala ya Fedha Zantel, Jean-Paul Happart na Kulia ni Afisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar Abdulhamid Idrissa Haji (katikati) akimpongeza Afisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur hivi karibuni mjini Zanzibar na kumshukuru kwa msaada mkubwa ambao Chuo hicho wameupata kutoka Zantel. Zantel walikabidhi msaada wa majenerata matatu yatakayowasaidia wanafunzi wa chuo hicho katika masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi ambacho Umeme umekatika.


ZANTEL imetoa msaada wa majenereta tatu zilizotumika kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar mwishoni mwa juma mjini Unguja.

Majenereta hayo yenye ambayo yamekwishatumika yenye thamani ya dola 250,000 yamekabidhiwa kwa Taasisi hiyo ili kusaidia jitihada za Chuo hicho katika kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao kipindi ambacho Umeme umekatika.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano mwishoni mwa juma mjini Unguja, Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Ndugu Mohamed Mussa Baucha alisema mchango huo una lengo la kuwasaidia wanafunzi wa chuo na masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi Umeme unapokua umekatika huku akitumai kwamba wanafunzi wa chuo hicho, watahimizwa kufanya vizuri kutokana na msaada huo.

"Ni jambo la furaha na faraja kwetu kutoa msaada wa majenereta kwa Taasisi hii, na tumaini letu kubwa ni kuwa yatakuwa msaada muhimu kwa wanafunzi katika masomo yao," alisema Baucha.

Aliongeza kuwa ZANTEL imekuwa msatari wa mbela katika kujitolea na itaendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali endelevu na kuunga mkono mipango inayozingatia kuboresha elimu nchini.

Abdulhamid Idrissa Haji, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwa sababu chuo chake hakikuwa na vyanzo mbadala vya nishati, mara umeme unapokuwa umekatika, kitu ambacho kiliwasababishia wanafuzi wengi usumbufu.

"Ukosefu wa umeme vyuoni, hukatisha morali ya wanafunzi hasa hasa kwa masomo ya sayansi na uwezo wa kuyaelewa masomo hayo kwa usahihi." Aliishukuru Zantel kwa msaada wao muhimu katika kuboresha ubora wa elimu nchini na kuhimiza makampuni mengine kufuata mfano huo.

“Msaada huu sio chachu tu katika ufaulu wetu kitaaluma bali pia utaongeza morali kwa wanafunzi,” alihitimisha Haji. wanafunzi wa chuo hicho aliyefahamika kwa jina Abdulkadir Mkubwa Khamis ambaye anachukua masomo ya sayansi, alisema mchango wa Zantel utawawezesha kuboresha utendaji wao na pia kutatua baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili hapo awali.

"Matatizo ya umeme huathiri sana masomo yetu, lakini kwa msaada huu, natumai matatizo hayo yatapungua," alihitimisha.

Mwaka jana, Kampuni ya Zantel ilitoa vitabu vyenye thamani ya 10M/- kwa Taasisi hiyo katika jitihada za kupunguza uhaba wa vifaa vya kufundisha na kujifunzia chuoni hapo.

DIWANI WA CHADEMA ATIMKIA CCM

$
0
0


Diwani wa Chadema wa Kata Donyomurwak, Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro, Ndg. Lwite Ndossi almaarufu “Nsonuu”, leo tarehe 19 Disemba 2017 amejivua uanachama wa Chadema, na amejiuzuru Udiwani wa Kata hiyo na ametangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Ndugu Ndossi ameeleza sababu za kujiunga kwake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ni kujiunga na watu wanaofanya siasa za kufanya kazi za maendeleo na si kulumbana na maneno matupu.


Imetolewa na,


IDARA YA ITIKADI NA UENEZI


CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

BARAZA LA WATOTO TAIFA LA CHAGUA WAWILI KUIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUZUIA UKATILI FEBRUALI MWAKANI NCHINI SWEDEN

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wa Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Yusra Mohamed kulia pamoja na Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Arusha Raphael Denis kushoto mara baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa kimataifa wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto utakaofanyika Nchini Swedeni Februari 2018.


Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wa Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Yusra Mohamed pamoja na Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Arusha Raphael Denis wamechaguliwa na wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa kimataifa wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto utakaofanyika Nchini Swedeni Februari 2018.

Watotao hao wamechaguliwa baada ya kupita katika Mchujo mkali uliowakutanisha wagombea kutoka Mikoa ya Bara na Visiwani na wataiwakilisha Tanzania katika Mkutano huo ambao Tanzania ni moja ya Nchi chache Barani Afrika kupewa kipaumbele cha ushiriki kufuatia hatua kubwa iliyofikia katika juhudi zake za kupambana na ukatili dhidi ya watoto.

Kwasasa Tanzania inatekeleza mkakati wake wa miaka mitano wa kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya wanawaka na watoto unaotekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau mbalimbali wa wanaopambanakuhakikisha Tanzania inakomesha kabisa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images