Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1463 | 1464 | (Page 1465) | 1466 | 1467 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii

  BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)limesema kwa sasa limeimarika kimfumo na kikatiba huku likiweka wazi hakuna chama zozote za kumuondoa Mufti madarakani.

  Akizungumza LEO makao makuu ya muda ya BAKWATA Kinondoni Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu taifa na Msemaji wa baraza hilo, Sheikh Khamis Mataka amesema kinachoendelea sasa ni kuimarisha mifumo kulingana na mahitaji.

  Amesema kutokana na mabadiliko yanayoendelea chini ya usimamizi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania ,Abubakari Zubeir,kuna watu wanaumizwa na mabadiliko ya mfumo na matokeo yake baadhi yao wanalichafua baraza kwenye mitandao ya kijamii.

  Sheikh Mataka amesema wakati baraza likijiimarisha na kufanya mambo makubwa, kuna watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za kuzusha.Ametumia nafasi hiyo kuwaomba Waislamu nchini kuunga mkono jitihada za Mufti katika kuweka mifumo ambayo italifanya baraza kuwa imara zaidi tofauti na huko nyuma ambako lilingia kwenye matatizo makubwa.

  "Kuna mambo mengi yasiyostahili yamefanyika huko nyuma,yakiwamo ya fedha za BAKWATA na mali zake kutumika vibaya.Wapo waliohusika kufanya ubadhirifu huo, wametangulia mbele za haki na hatuna cha kusema zaidi ya kumuachia Mwenyezi Mungu." Tunachoendelea nacho kwa sasa ni kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali na tunaomba Waislamu kutuunga mkono,tunajua wapo wasiofurahia mabadiliko ya Mufti lakini tutaendelea nayo,"amesema.

  Pia amesema kuna taarifa ambazo zinaendelea kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zikiihusisha BAKWATA.Taarifa hizo ni tishio la kumuondoa Mufti,wafanyakazi walia njaa na mgogoro wa walimu wa shule ya sekondari Bondeni mkoani Arusha inayomilikiwa na baraza hilo.Kuhusu tishio la kumuondoa Mufti ,amesema hazina ukweli wowote na wanafuatilia aliyetoa taarifa.Kuhusu wafanyakazi kudai mishahara ni kweli na hiyo imetokana na malimbikizo ya muda lakini chini Mufti Zubeir wameendelea kulipa.

  Amesema malimbikizo yanayodaiwa ni sh Milioni 176 na wanaendelea kulipa.Kuhusu mgogoro haupo kwani ulishaghulikiwa na umepata nafasi kwasababu kuna watu wameondolewa kwa hiyo wanaeneza taarifa mbaya.

  Sheikh Mataka amesema BAKWATA ya sasa chini ya uongozi wa Mufti Zubeir ipo imara na kauli mbiu yake yake ya "Jitambue,mabadilika, acha mazoea" imesaidia kuwabadilisha wajumbe mbalimbali wa baraza hilo.Amesema kwa mara ya kwanza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya baraza hilo wameshiriki kwenye vikao bila kulipana posho yoyote na miongoni mwa wajumbe walisafiri kutoka mikoani.

  Ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua ya BAKWATA kuamua shule 10 za baraza hilo kupewa watu binafsi kuzisimamia na zilizobaki zinasimamiwa kwa utaratibu wa zamani.Amesema lengo ni kuangalia mfumo upi unafaa katika kusimamia sekondari za BAKWATA ingawa kuna baadhi ya watu wamezusha sekondari hizo kapewa Mufti jambo ambalo si kweli.
   Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu BAKWATA Taifa na Msemaji rasmi wa baraza hilo,Sheikh Khamis Mataka(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar Salaam leo wakati akitolea ufafanuzi wa tuhuma tatu zinazoelekezwa kwa Mufti wa Tanzania ,Sheikh Abubakari Zubeir ambazo ameeleza si za kweli.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sawa na Tabligh na Msemaji wa Mufti Sheikh Hassan Chizenga na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu BAKWATA Sheikh Salim Abed.
  Mkurugenzi wa Dawa na Tabligh na Msemaji wa Mufti wa Tanzania sheikh Abubakari Zubeir, Sheikh Hassan Chizenga akizungumzia nia njema ya Mufti katika kuwaongoza Waislamu kupitia baraza hilo.Pia ameonya tabia ya Watanzania kusema uongo kwani athari zake ni kubwa katika nchi.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiteta jambo na Maafisa wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji toka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Desemba 15, 2017 katika Ukumbi wa Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam. Maafisa hao walikuwa hapa nchini kushiriki mazoezi ya Kijeshi ya pamoja kuhusu ulinzi wa amani yaliyohusisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yaliyoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Charles Novart ambaye pia alikuwa mshiriki kutoka Jeshi la Magereza Tanzania katika mazoezi ya Kijeshi ya pamoja kuhusu ulinzi wa amani akitoa utambulisho kwa Maafisa wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji toka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Desemba 15, 2017 katika Ukumbi wa Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam.
  Kamishna Msaidizi wa Magereza toka nchini Uganda ambaye pia ni Msemaji wa Jeshi hilo Baine Frank akijitambulisha mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) kwenye hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika katika Ukumbi wa Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam.
  Naibu Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Magereza toka nchini Kenya James Kodieny(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kulia) kama inavyoonekana katika picha katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Desemba 15, 2017 katika Bwalo la Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam.
  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini walioshiriki hafla hiyo ya kuwaaga Maafisa wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji toka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwa hapa nchini kushiriki mazoezi ya Kijeshi ya pamoja kuhusu ulinzi wa amani.
  Bendi ya Magereza maarufu kwa jina la “MKOTE NGOMA” ikitumbuiza katika hafla hiyo ya kuwaaga Maafisa hao.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

  0 0

  Wanaharakati wa kupinga ukeketaji wakisikiliza kwa makini mafunzo kabla ya kuanza kampeni ya mwezi mmoja ya kupinga ukeketaji wilayani Ngorongoro. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Shrika la UNESCO. Kampeni hiyo inafanywa kwa ushirikiano wa UNESCO, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Baraza la Wazee wa Mila wa Kimaasai (Laigwanan). Kampeni hiyo imeanza Tarehe 5/12/2017 na itaendelea kwa mwezi mzima. Afisa wa UNESCO anayewakilisha miradi ya Ololoswakan Wilayani Ngorongoro Bwana Hamidun Kweka akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Oloirien wilayani Ngorongoro madhara ya ukeketaji katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukeketaji wilayani humo. Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi Tarehe 5 na zitadumu kwa mwezi mmoja. Ngariba mstaafu akiimba na watoto nyimbo za kupinga ukeketaji baada ya mafunzo ya kuwaelimisha madhara ya ukeketaji katika shule ya msingi Oloirine wilayani Ngorongoro mnamo Tarehe 7, 2017. Wafanyakazi wa UNESCO na Walimu wa Shule ya Msingi Oloirien wakiwa pamoja baada ya uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Ukeketaji wilayani Ngorongoro.

  0 0

  1. Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Taasisi ya Mwanamke na Uongozi akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
  1. Baadhi ya Vijana kutoka sehemu mbalimbali za Jijini wakifuatilia mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
  1. Bw. Oscar Munga akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
  1. Bi. Anna Winstone akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
  1. Mmoja wa washiriki wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.  VIJANA nchini wametakiwa kutambua wajibu wao katika Taifa kwa kutumia fursa zinazojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi katika jamii ili kutetea maslahi na agenda mbalimbali zinazogusa maendeleo yao.

  Hayo yamesemwa leo Jumamosi (Desemba 17, 2017) Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Ushawisihi na Utetezi wa Taasisi ya Vijana ya TYVA, Yusuf Bwango wakati wa mdhahalo wa vijana uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.

  Kwa mujibu wa Bwango alisema tafii mbalimbali zimebaini kuwa Vijana wengi wamekuwa na mtazamo hasi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi hususani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kubaki nyuma katika nafasi hizo huwaniwa na kushindaniwa na Wazee pekee.

  “Tumefanya mdahalo huu kwa malengo ya kuwajengea uwezo vijana kutambua kuwa wao ndio Viongozi wa baadae na hili litaanzia katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika katika ngazi za kijamii ikiwemo chaguzi za Serikali za Mitaa” alisema Bwango.

  Bwango alisema umefika wakati kwa Vijana wa Kitanzania kuweza kutumia majukwaa mbalimbali ili kuweza kubadili fikra na mitazamo yao kuhusu mifumo ya kiutawala na kutumia majukwaa hayo kuunda vyombo imara vitakavyoweza kuwasilisha na kupaza sauti zao.

  Aliongeza kuwa mdahalo huo pia umekusudia kuwawezesha vijana kupata taarifa mbalimbali kuhusu nafasi ya vijana kitaifa na kimataifa pamoja na juhudi mbalimbali zilizochuliwa na Serikali kuwasaidia vijana kuweka kupaza sauti zao ikiwemo uanzishaji wa vyombo maalum vya utetezi wa Vijana ikiwemo Mabaraza ya Vijana.

  Akifafanua zaidi Bwango alisema kupitia mitandao hiyo Vijana wataweza pia kuwasiliana na kuunganisha nguvu ya pamoja itakayowezesha kujadili changamoto na mikakati mbalimbali itakayowawezesha kuwaletea maendeleo yao kupitia Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

  Alisema tangu Mwezi Julai hadi Novemba, mwaka huu TYVA imeweza kutoa elimu ya uraia kwa vijana wa Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dodoma, Dar es Salaam,, Morogoro, Tanga, Pwani, Zanzibar na kuwawezesha vijana kutambua wajibu, nafasi na haki za kikatiba waliyonayo katika Taifa.

  Bwango alisema katika midahalo hiyo iliyoendeshwa na TYVA kwa kushirikana na Mamlaka mbalimbali za Serikali, vijana wengi waliweza kupatiwa elimu ya uraia pamoja na fursa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua kiuchumi ikiwemo elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

  Kwa upande wake, Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Taasisi ya Mwanamke na Uongozi alisema mapambano ya harakati za ukombozi katika jamii hususani kwa wanawake zitafanikiwa kwa kujenga mkakati wa pamoja wa ushawishi utakaoweza kuondoa vikwazo mbalimbali vilivvyopo kaika mfumo ya kiutawala.

  “Ili kujikwamua na kufikia na juu katika ngazi za maamuzi ni wajibu wa wanawake wote kuunda mkakati wa pamoja na kuacha kusubiri na tufute dhana ya mwanamke ni kiumbe dhaifu” alisema Sumaiya.

  0 0

  NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.

  MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka amewataka wanawake wa umoja huo kuvunja makundi ya ngazi zote yaliyojengeka wakati wa uchaguzi na badala yake wafanye kazi za kuwatumikia kwa ufanisi wapiga kura waliowapa ridhaa ya kuongoza.

  Pia, amesema UWT kupitia uongozi wake mpya ulioingia kwa sasa ni lazima irejeshe heshima yake ya kuwa chombo cha kuwaunganisha wanawake wote wa mijini na vijijini Tanzania ili wapate maendeleo.Wito huo ameutoa katika hafla ya mapokezi ya uongozi huo yalioandaliwa na UWT Mkoa wa Dodoma katika viwanja vya White house Makao Makuu ya CCM Dodoma.

  Amesema bila kuvunja makundi Umoja huo hautopata maendeleo na watatumia muda mwingi kulaumiana, kuangaishana na hamaye kukosa muelekeo wa kutekeleza ahadi walizotoa kwa mamilioni ya wanawake wa Tanzania.Kabaka ameeleza kwamba Umoja wa Wanawake Tanzania ni chombo cha CCM kinachotakiwa kuwa nguzo na muhimili mkuu katika kusimamia na kulinda maslahi ya Chama kisiasa, kiuchumi na kijamii.

  "Furaha yangu ni kwamba mlituchagua kihalali bila ya kutumia rushwa, hivyo nasi tuna deni la kuwalipa ambalo ni lazima tutimize utumishi bora na uliotukuka kwa miaka mitano ya uongozi wetu.Na nakuombeni tushirikiane kwa pamoja kupinga rushwa na ufisadi ndani ya UWT na Chama kwa ujumla kama tunavyopinga makundi ya kuhatarisha uhai wa Chama cha Mapinduzi", amesema Mama Kabaka.

  Amesema jopo la viongozi wa ngazi mbali mbali wa UWT waliochaguliwa hivi karibuni ndio jeshi la kisiasa la Akina Mama wanaotakiwa kuongoza mapambano ili CCM ishinde na kubaki madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.Kupitia hotuba yake Mwenyekiti huyo, ameagiza miradi yote ya UWT Tanzania iorodheshwe ndani ya miezi miwili kwa lengo la kuijua ipo mingapi na kuweka utaratibu rasmi ili iwanufaishe akina mama wote.

  "Mbali na miradi ya kiuchumi iliyopo Makatibu wa ngazi mbali mbali tafuteni takwimu sahihi zinazohusu masuala ya huduma za kijamii hasa zinazowahusu wanawake." ameagiza Mwenyekiti huyo.

  Pamoja na hayo ametoa shukrani zake kwa wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja huo kwa kuwaamini kisha kuwachagua kwa kura nyingi viongozi wote wa ngazi ya Taifa.“Natoa ahadi yangu tena kwenu kwamba mmeniamini nami nitatenda mema kwenu kwa kurejesha matumaini ya kutenda na kusimamia mambo yote yenye manufaa kwa wanawake wa Tanzania.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa, Thwaiba Kisasi amesema dhamira ya UWT ni kuzitatua changamoto mbali mbali zinazowakabili Akina mama ili wanufaike na matunda ya kuwa mwanachama wa Umoja huo.Ameeleza kwamba viongozi hao hawatowaangusha kiutendaji bali watatumia uzoefu na taaluma zao kuleta maendeleo endelevu ndani UWT.

  Akizungumza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule amesema Umoja huo umevuna wanachama wapya 5000 kupitia Chaguzi za ngazi mbali mbali zilizofanyika katika Mkoa huo.

  Amesema UWT imejipanga kuanzisha miradi mikubwa ya kiuchumi kuanzia ngazi za Wilaya za Mkoa huo na mwanamke mmoja mmoja kwa lengo la kujikomboa kiuchumi.Mapema katika hafla hiyo jumla ya wanachama wapya 1700 wamekabidhiwa kadi za CCM kwa lengo la kuitumikia jumuiya na Chama kwa ujumla.

  Viongozi mbali mbali walioudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Hakson, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Tabia Maulid Mwita na Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Amina Makilagi.
  VIONGOZI Mbali mbali wa UWT walioudhuria katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya UWT ngazi ya Taifa.
  MWENYEKITI wa UWT Taifa, Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya ngazi ya Taifa wa Umoja huo yaliyofanyika katika viwanja vya White House Makao Makuu ya CCM Dodoma.

  0 0
 • 12/16/17--08:56: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

  Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini.
  Rais wa Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) Dkt. Donald Kisanga akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini.Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare, Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mungereza, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
  Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea risala ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) kutoka kwa Rais wa mfuko huu Dkt. Donald Kisanga wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini. Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare na Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mungereza.
  Mwanamuziki mkongwe Mzee Kitenzogi Makassi akitoa ushuhuda wa namna Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) ulivyomnufaisha tangu alipojiunga na uanachama wa mfuko huo leo Jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Kadi ya uanachama wa NSSF mmoja ya wanachama wa Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa NSSF Omary Mzia,Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mungereza na Rais wa Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) Dkt. Donald Kisanga.
  Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Frank Shija – MAELEZO)


  Na; Shamimu Nyaki-WHUSM.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Wasanii wote hapa Nchini kuwa wabunifu na kutumia weledi katika kutengeneza kazi zenye ubora wa hali ya juu kwakua ndio utakaowasaidia kupata soko la uhakika.

  Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kanzi Data ya wasanii iliyoandaliwa na Taasisi ya Muziki hapa nchini (TAMUF) iliyodhaminiwa na Kampuni ya CogsNet Technologies lengo ikiwa ni kusajili wasanii pamoja na kazi zao ili watambulike na wafaidike kupitia kazi hizo, lakini pia kuendelea na harakati za kupambana na wizi wa kazi za wasanii.

  “Nawashukuru sana CogsNet pamoja na TAMUF kwa kuja na wazo hili lenye lengo la kulinda kazi za wasanii,naamini Kanzi Data hii italeta mafanikio kwa wasanii endapo watajisajili na kutengeneza kanzi bora zitakazowapatia soko la uhakika ndani na nje ya nchi”Alisema Dkt.Mwakyembe.

  Aidha ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuwatafutia wasanii Huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo Bima ya Afya inayotolea na mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF lengo ikiwa ni kuwasaidia wasanii kupata huduma ya afya kwa bei nafuu pamoja na mafao mengine yanayotolewa na Mfuko huo lakini pia akiwataka wasanii kuacha tabia ya kuuza Haki Miliki zao.

  Kwa upande wake Rais wa Taasisi hiyo Dkt.Dornald Kisanga amesema kuwa Taasisi hiyo ina lengo la kuondoa unyanyasaji wa kazi za wasanii uliofanywa kwa muda mrefu ikiwemo wizi wa kazi hizo pamoja na kipato kidogo walichokuwa wanapata wasanii kwa kuuza Haki Miliki zao.

  “Kumekuwa na changamoto ya muda mrefu ya wizi wa kazi za wasanii ndio maana CogsNet Technologies imeamua kushirikiana nasi katika kutafuta suluhu ya kazi ya kunufaika na kazi zetu,hivyo wasanii tunapaswa kutumia nafasi hii kwa manufaa yetu”Alisema Bw.Kisanga.

  Naye mwakilishi wa NSSF Bw. Omary Mzia amesema mpaka sasa wasanii 500 wameandikiswa katika mfuko huo ili kupata huduma mbalimbali za hifadhi ya jamii ambapo amewakaribisha wasanii wengine kujiunga na mfuko huu ili wapate huduma zinazotolewa na mfuko huo ikiwa ni pamoja na huduma ya matibabu.

  Hata hivyo muwakilish wa wasanii kutoka Taasisi hiyo ya TAMUF Bibi Leonia Leornad ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono hatua zinazofanywa na Taasisi yao katika kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi zao kwa kupiga vita wizi wa kazi hizo pamoja na kuishukuru NSSF kwa kuwapatia huduma ya matibabu.

  Taasisi ya TAMUF imeahidi kutoa elimu kwa wasanii kutengeneza nyimbo pamoja na video zinazozingatia maadili na Utamaduni wa Watanzania ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kukomesha kazi za sanaa zisizozingatia maadili.

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza  maelezo ya namna ya ufanyaji kazi mara baada ya kutembelea Kitengo cha Unyunyuziaji wa Viuatilifu alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Kushoto) akitembelea baadhi ya maeneo ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akitumia mashine ya Kunyunyizia viuatilifu wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini maelezo ya namna maabara ya kupima masalia ya Viuatilifu inavyofanya kazi wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.

  Na Mathias Canal, Arusha


  Watumishi wa serikali wanaofanya kazi katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) wametakiwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa Weledi, Bidii na Nidhamu.


  Kauli hiyo imetolewa Leo 16 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Taasisi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha.


  Mhe Mwanjelwa aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, Juhudi, Maarifa na Ubunifu kwani kufanya hivyo kutathibitisha matokeo chanya katika utendaji wao huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa moyo na uvumilivu mkubwa pamoja na kuwepo kwa kadhia ya upungufu wa watumishi.


  Sambamba na Taasisi hiyo kuwa na jukumu la kufanya utafiti, kutoa huduma za usajili na udhibiti wa viuatilifu, Mafunzo kuhusu visumbufu na kufanya hifadhi ya Bioanwai husika ili kuchangia uhakika wa chakula lakini pia ina jukumu la kuendelea na kudumisha mashamba darasa kwa ajili ya Utafiti na mafunzo kwa wadau hususani katika matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu.


  Aidha, Alimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kusimamia Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na umakini wa Taasisi katika kufanya kazi zake katika kipindi cha miaka 10 ya utekelezaji wa muundo mkakati wa TPRI (2005-2015).


  Alimsihi Mkurugenzi huyo anayesimamia Taasisi hiyo ya (TPRI) iliyotungiwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The TPRI Act No 18 of 1979) ikisimamiwa na Wizara ya Kilimo, kuongeza ufanisi zaidi katika usimamizi wa kazi kwa mujibu wa sheria na Taratibu za nchi.


  0 0

  Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

  Wafanyakazi kutoka Bodi ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar wameangamiza Tani tisa za Dawa ya meno aina ya Aloe zilizoharibika katika jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja

  Dawa hizo ziliingizwa nchini na Kampuni ya Bacelona Interprises Limited zikiwa zimeharibika baada ya kontena lilikuwa na dawa hizo kuinga maji wakati wa kusafirishwa kuja Zanzibar .

  Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Chakula Dawa Zanzibar Mwadini Ahmadi Mwadini alisema walibaini kuwa dawa hizo zimeharibika wakati wa kuzitoa bandarini na kumshauri mmiliki wa dawa hizo kuzirejesha zilikotoka au kuziangamiza na alikubali ziangamizwe ili kujiepusha na gharama nyengine.

  Mwadini alisema Bodi inaendelea kufanya ukaguzi kwa bidhaa zinazoingizwa bandarini na  maduka mbali mbali ili kuhakikisha zinakuwa salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

  Aliwataka wafanyabiashara kuwa waangalifu wanapoagiza Bidhaa na kujenga ushirikiano wa karibu na Bodi yake kwa kutowa taarifa wanapoona bidhaa zao zinamashaka kuuzwa kutokana na kuharibika au kupitwa na muda wake wa matumizi.Aidha aliwaomba wananchi wanaponunua bidhaa madukani  na kuzigundua kuwa hitilafu watowe taarifa katika Bodi ili hatua zinazofaa ziweze kuchukuliwa kwa usala wao.       

  “Kama mukigundua kunafanyika udanganyifu kwa bidhaa mnazonunua kama kuharibika au kupitwa na wakati musisite kutoa taarifa kwetu, tupo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi.” alisema Mkaguzi Mkuu.  

  Nae mtoa mzigo Bandarini aliesimamia kontena hilo Omar Kombo Sharif alisema mzigo huo uliingia Zanzibar mnamo mwezi wa nane na baada ya kubainika umeharibika walitoa taarifa kwa mmiliki na walikubaliana uzuiliwe kwa ajili ya kuuangamiza.

  Wakati huo huo Mkuu wa Uchunguzi wa Chakula na Dawa Zanzibar Mohamed Shadhil alisema wamekamata Nyama ya ngombe kilo 180 iliyokuwa inasafirishwa kinyume na taratibu zilizowekwa na Bodi hiyo.

  Alisema bidhaa hiyo imekamatwa wakati inasafirishwa kutoka machinjioni kwa kutumia Baskeli pamoja na vespa bila ya kuwa na kibali cha daktari na nikinyume cha utaratibu. Bidhaa za nyama zinatakiwa kusafirishwa kwa kutumia gari kwa ajili ya usalama wa watumiaji.

  Nyama hiyo wameamua kuifukia baada ya kufanyika uchunguzi na kuwaita wamiliki ambao walikubali kuwa wamefanya kosa licha ya kulalamika kuwa utaratibu wa kusafiri bidhaa hiyo kwa kutumia baskeli na vespa umekuwapo kwa muda mrefu.

  Mkuu huyo wa uchunguzi aliwataka wananchi wanaochinja nyama kufuata taratibu zilizowekwa ikiwemo kutumia vyombo vinavyotakiwa vyakuchukulia bidhaa hiyo ili kuepuka usumbufu na hasara katika biashara zao.
   Wafanyakazi wa Bodi ya Wakala na Dawa Zanzibar  wakiteremsha dawa za msuaki tani tisa zilizoharibika katika jaa la kibele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kuangamizwa.
   Maboksi yaliyokuwa na dawa za msuaki zilizoharibika yakichomwa moto na wafanyakazi wa Bodi  ya Wakala na Dawa Zanzibar katika jaa la Kibele, Wilaya ya Kati Unguja.
   Gari aina ya kijiko likisaga dawa zilizoharibika ili kuziangamiza baada ya kuingia maji wakati wakusafirishwa katika jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.

  Picha na Ramadhani Ali – Maelezo.

  0 0

  Member of the House of Representative in Zanzibar, Hon Simai Mohammed Said in discussion with the Ambassador of Kuwait to Tanzania HE Jassim Al -Najim when ambassador visited Zanzibar for work.
  HE Jassim Al Najim, the Ambassador of Kuwait to Tanzania greeting the Deputy Minister of Education and Vocational Training of Zanzibar, during the handing over ceremony of Computers and printers for the 15 schools of Tunguu located in central district of Zanzibar.
  Member of the House of Reps, Hon Simai Mohammed Said addressing the teachers and students of Tunguu.
  Various invited guests, teachers and students, listening attentively during the function of the handing over of computers and printers by the Embassy of Kuwait in Tanzania.
  The computers and printers which were donated by the people of Kuwait through the Embassy of Kuwait in Tanzania
  The Ambassador of Kuwait to Tanzania HE Jassim Al-Najim handing over the computers and printers to the guest of honour, Deputy Minister of Education in Zanzibar Hon Mmanga Mjengo Mjawire at the center. Seen on the right, is the member of the House of Representative of Tunguu Hon Simai Mohammed Said
  Happy faces, The Ambassador of Kuwait with various leaders from Tunguu Constituency and government officials as he officially hands over the 20 Computers and 10 printers worth 23,287,000/- SHS
  As a token of appreciation, the teachers and students of Tunguu rewarded MADAFU (Coconut Juice) as a present on behalf of the people of Tunguu to the Ambassador. 
  Member of the Union Parliament and House of Reps for Tunguu Constituency Khalifa Salim Suleiman ( MIMINA ) and Simai Mohammed Mohammed Said ( MPAKABAS) bidding farewell to the guest of honour from the Revolutionary Government of Zanzibar Hon Mmanga Mjengo Mjawire

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride. 
  Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya. 
  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akiteta jambo na Mshauri Jeshi la Akiba Gairo, Major Balitoga (kushoto kwake) pembeni ni Diwani wa Kata ya Rubeho, Mhe. Mhe. Digwagwala (wa kwanza kulia). 
  Wananchi waliohudhuria hafla hiyo. 
  Mshauri Jeshi la Akiba Gairo, Major Balitoga akitoa machache mbele ya mgeni rasmi. 
  Diwani wa Kata ya Rubeho Mhe. Digwagwala akitoa shukrani zake za pekee kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwa kuweza kuendesha mafunzo katika Kata yake. 
  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride.  Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakiwa katika gwaride la ukakamavu mbele ya mgeni rasmi. 
  Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akitoa hotuba yake. 
  Brass Bendi wakitumbuiza katika hafla hiyo ya kuhitimisha mafunzo ya mgambo yaliyofanyika katika kata ya Rubeho. 
  Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakipita mbele ya mgeni rasmi kwa gwaride la kutoa heshima. Na Kajunason/MMG. 

  Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amewataka wahitimu wa mafunzo ya mgambo kukiishi kiapo cha utii kwa matendo na si maneno. 

  Hayo ameyazungumza leo Disemba 16, 2017 wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya mgambo ambayo yalifanyika katika Kata ya Rubeho halmashauri ya wilaya ya Gairo ambapo mgeni rasmi aliwaasa wahitimu kutii yale yote waliyofundishwa ili kujenga uchumi wa Taifa. 

  Katika hotuba yake Mhe. Mchembe aliongeza kuwa mgambo wanapaswa kutumia elimu waliyoipata ili kuinua uchumi wao na jamii inayowazunguka bila kuwaonea au kuwatesa wananchi. "Nawaombeni sana ndugu zangu mafunzo mliyoyapata ni muhimu sana katika taifa letu ni vyema sasa na nyie mkayaishi yale yote mliyofundishwa kwa kipindi cha miezi mitatu mliyoshiriki," alisema Mhe. Mchembe. 

  Aliongeza kuwa ni vyema mgambo wakawa mabalozi wema wa amani na si wao wawe mstari wa mbele katika vitendo vya rushwa, unyanyasaji wa wananchi na kuepuka kujihusisha kwenye uharifu kwa kukodisha magwanda yao. Mhe. Mchembe aliwataka viongozi wa wilaya kufanya usaili tena kwa wale mgambo wote ambao wameshapitisha miaka 10 ili waweze kurudi kupata mafunzo zaidi.

  "Kazi hii ya mgambo inahitaji kuendelea kujifunza mara kwa mara hivyo nawaomba viongozi wote fanyeni upya usaili wale wote ambao muda wa miaka 10 umepita warudie katika mafunzo waweze kuongeza ujuzi zaidi," alisema Mhe. Mchembe. 

  Alimalizia kwa kuwataka viongozi wa wilaya kuwahamasisha akinamama kujitokeza zaidi katika mafunzo ya mgambo maana idadi yao imeonekana kuwa ni ndogo sana ukilinganisha na wanaume ambao wao wamekuwa mstari wa mbele katika kujitokeza. 

  Mafunzo hayo ya miezi mitatu yalihitimishwa Disemba 13, 2017 yalisimamiwa na Mshauri Jeshi la Akiba Gairo, Major Balitoga kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ambapo jumla ya wahitimu 101 ambapo asilimia 11 tu walikuwa ni wanawake. Wahudhuriaji hafla hiyo walikuwa ni Diwani wa Kata ya Rubeho Mhe. Digwagwala, Mtendaji wa Kata, Wenyeviti wa vijiji, viongozi wa dini, wazee maarufu na wananchi zaidi ya 200 walishiriki maadhimisho hayo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na Mapadri baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
   Kwaya ikitumbuza wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
   Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017


  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha kikao KAmati Kuu ya chama hicho ukumbi wa mikutano wa White House mjini Dodoma leo Desemba 17, 2017.
  Mwenyekiti wa CCM,Rais Dkt John Pombe Magufulia akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho  (Zanzibar),Dkt Shein
  Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akizungumza jambo kabla ya kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi kuanza ndani ya ukumbi wa mikutano wa white House mjini Dodoma leo Desemba 17,2017.
  Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Kamani Kuu ya CCM wakipiga makopi ya kumkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho,Rais Dkt John Pombe Magufuli kabla ya  kuanza kwa kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi ndani ya ukumbi wa mikutano wa white House mjini Dodoma leo Desemba 17,2017.

  0 0

  Wakaguzi wa Migodi Nchini wameagizwa kutembelea mara kwa mara kwenye migodi hususan ya wachimbaji wadogo kwa ajili ya kukagua hali ya usalama na kuwasaidia Wachimbaji kuepusha ajali wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.

  Agizo hilo limetolewa Desemba 14, 2017 Mkoani Tabora na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alipotembelea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua ili kujionea shughuli zinazofanywa mgodini hapo na kuzungumza na wachimbaji.

  Baadhi ya Wachimbaji walimueleza Naibu Waziri Nyongo kuwa wamekuwa wakifanya shughuli zao katika mazingira magumu bila kuwa na elimu ya namna bora ya uchimbaji wa madini.

  Nyongo alisema ni jukumu la Maafisa Madini wakiwemo Wakaguzi wa Migodi (Mining Inspectors) kuhakikisha wachimbaji hususan wadogo wanapatiwa elimu ya mara kwa mara kuhusu afya, uchimbaji salama na uhifadhi wa mazingira ili kuepusha magonjwa na ajali zinazosababishwa na uelewa finyu wa uchimbaji bora.

  “Wachimbaji wadogo wanapaswa kutembelewa na kuelimishwa mara kwa mara na hili ni jukumu lenu, msisubiri hadi kutokee madhara ndio mfike kutoa elimu,” alisema.Aidha, Nyongo aliagiza wamiliki wa machimbo kuhakikisha wanawapatia vitendea kazi wachimbaji kwenye maeneo yao ili kuwalinda na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.

  Alisema suala la kuwapatia vitendea kazi wachimbaji litasaidia kuepukana na ajali na wakati huohuo kuchangia kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli hiyo ya uchimbaji madini.“Inabidi muelewe, mnapowapatia vifaa hawa wachimbaji wenu mtaepukana na ajali kwahiyo muda mwingi mtatumia kwenye kuzalisha na hivyo uzalishaji utaongezeka sambamba na mapato yenu,” alifafanua Naibu Waziri Nyongo.

  Vilevile Nyongo alisisitiza umuhimu wa wachimbaji hao kujiunga katika vikundi ili kuwa na urahisi wa kusaidiwa kuwa na uchimbaji wenye tija kwao na taifa kwa ujumla."Mkijiunga kwenye vikundi itakua ni rahisi kuwafikia kwa pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali yenye tija kwenye shughuli zenu," alisema.

  Aliongeza kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha  Wachimbaji Wadogo wa Madini wanafanikiwa kufikia kwenye uchimbaji wa Kati na baadaye kuwa Wachimbaji Wakubwa.
   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza kwenye mkutano na Wananchi na Wachimbaji Wadogo kutoka Kata ya Silambo Wilayani Kaliua (hawapo pichani).
   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa sita kushoto waliosimama mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kaliua, Maafisa kutoka Ofisi ya Madini, Tabora na viongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua.
   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akielekea kwenye machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kulia) akitazama moja ya shimo la dhahabu lililoko katika Mgodi wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) akielekea kwenye machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) akiongoza ujumbe wake kukagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.

  0 0

  Ukoo wa Patel umekabidhi kiasi cha shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika  kwaajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
  Akikabidhi fedha hizo leo Mwenyekiti wa Ukoo huo Harish Patel alisema watoto wengi wanazaliwa na ugonjwa wa moyo na wengi wao hawana fedha za kulipia matibabu wameona kwa kidogo walichokipata kisaidie kulipa gharama za matibabu ya wagonjwa hao.

  “Kila wakati, kila mwaka kutokana  na kipato tunachokipata tumekuwa tukisaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo  elimu na afya na leo hii tumeona furaha zaidi kusaidia watoto”,  alisema.

  Akipokea fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI  Prof. Mohamed Janabi aliushukuru Ukoo wa Patel kwa kuona umuhimu wa afya ya mtoto na kusaidia kulipia gharama za matibabu na kuziomba Taasisi, Mashirika na watu binafsi wenye uwezo wajitokeza  kulipia matibabu ya watoto.

  Prof. Janabi alimalizia kwa kusema kuwa  watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni wengi   kati ya watoto milioni mbili wanaozaliwa asilimia moja (1%) wanazaliwa na matatizo ya Moyo hivyo bado fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya matibabu.
   Mwenyekiti wa Ukoo wa Patel,  Harish Patel akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na ukoo wa Patel pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo mara baada ya kukabidhiwa  mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
    Ukoo wa Patel ukiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kukabidhi  mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
  Mkurugezi Mtendaji wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi akongea na waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= na Ukoo wa Patel , fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Picha na JKCI.

  0 0

   KAIMU Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya kadi uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mazoezi wilayani humo kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Tafa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe,Rehema Kwasi
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni anaye fuatia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe,Rehema Kwasi

  Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe,Rehema Kwasi akizungumza wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe,John Nyarongo.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Mji,Jumanne Shauri akizungumza wakati wa uzinduzi huo
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe,John Nyarongo akizungumza katika uzinduzi huo
  Afisa Uanachama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF),Sophia akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga,Ally Mwakababu 
   Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe kulia akiteta jambo na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati wa uzinduzi huo


   Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe katikati akipata maelekezo ya namna huduma za upimaji wa afya na uzito zilizokuwa zikitolewa mfuko huo wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya kadi wilayani Korogwe katikati ni Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
    Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akiangalia huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya Kadi kulia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Ally Mwakababu

   Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kushoto akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya kadi wilayani humo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mazoezi wilayani Korogwe
   Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kushoto akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya kadi wilayani humo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mazoezi wilayani Korogwe

    Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kushoto akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya kadi wilayani humo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mazoezi wilayani Korogwe
   Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe mji,Jumanne Shauri mara baada ya kuzinduzi mpango wa toto afya kadi kwenye viwanja vya shule ya msingi Mazoezi wilayani Korogwe kulia ni Meneja wa NHIF mkoani Tanga,Ally Mwakababu
   Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe katika kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe,Rehema Bwasi kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Mji,Jumanne Shauri na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga,Ally Mwakababu
  Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya uzinduzi huo
   Sehemu ya wananchi wa wilaya ya Korogwe wakisubiri kupata huduma mbalimbali za upimaji wakati wa uzinduzi huo wa mpango wa toto afya kadi
   Sehemu ya wananchi wakisubiri huduma ya upimaji wakati wa uzinduzi huo
   Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza kushoto akitoa huduma ya upimaji kwa wakazi wa mji wa Korogwe wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya kadi wilayani humo uliofanyika viwanja vya Mazoezi
   Zoezi la Upimaji likiendelea kwenye uzinduzi huo
  Wananchi wakisubiri kupatiwa huduma ya upimaji kwenye banda la mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wilayani Korogwe wakati wa uzinduzi wa mpango wa Toto Afya Kadi CHabari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Wasamaria wema wakimsaidia mwendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda yenye nambari MC307 BPG (jina halikupatikana) amabaye alidondoka chini baada ya kuganga kwa nyuma gari dogo aina ya Toyota RAV 4 nambari T924 BPG kwenye eneo la Kanisa Kuu Katoliki la Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Dodoma, Desemba 17, 2017. Wasamalilia Wema hao walimpeleka kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa matibabu. (Picha na Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaongoza Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kupiga gwaride la ukakamavu muda mfupi baada ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi. 

  Na Hamza Temba-  Mlele, Katavi
  ...........................................................................

  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wahifadhi wote nchini kushirikiana na wadau wengine hasa mamlaka za Mikoa na Wilaya katika maeneo yenye uvamizi wa mifugo na migogoro ya mipaka ya hifadhi ili kutatua changamoto hizo kwa namna shirikishi ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.


  Ametoa agizo hilo jana Disemba, 16, 2017 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.


  “Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tutaiendeleza, Falsafa yetu ni kuwashirikisha wadau wote, kama kuna taasisi za kiraia kwenye eneo lako la kazi, taasisi za kijamii, mamlaka za mikoa na wilaya, wananchi, halmashauri husika mshirikiane nao ili kupunguza madhara ya operesheni zetu, na zoezi hili la uhifadhi liwe endelevu,” alisema Dk. Kigwangalla.


  Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.


  Awali akizungumzia mafunzo hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu, uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.


  Alisema katika kuelekea mfumo huo, Jeshi hilo litakuwa moja bila kubagua taasisi yeyote ambayo ipo chini ya Wizara yake. “Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 inampa Waziri mamlaka ya kuunda Jeshi Usu, haikusema jeshi la TAWA, TFS, TANAPA au NGORONGORO na kwa vile hili jeshi ni langu nataka liwe moja, na tunakimbiza mchakato huu kwa haraka ukamilike kwa mujibu wa Sheria.


  “Tunafarajika Mhe. Rais ameshaunga mkono na ameshatupa maelekezo, Mwenyekiti wa Kamati ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Ulinzi naye ameshasaini, ni sisi sasa tuendelee kujipanga vizuri ndani ya wizara, tuanze kuishi kwenye mfumo huo, kuanzia kwenye sare, uratibu wa mafunzo, uongozi na mfumo wa utawala,” alisema Dk. Kigwangalla.


  Alisema mfumo huo wa Jeshi Usu utakuwa na mnyororo mmoja wa mamlaka (chain of comand) na kwamba utahusisha taasisi zote za uhifadhi zilizopo chini ya wizara yake kwenye sekta ya wanyamapori, misitu na mali kale. “Sijawaona watu wa misitu hapa au mambo ya kale, wote hawa ni ni muhimu, rasilimali za mali kale nazo ni muhimu sana kulindwa kwani zikiharibika hazitengenezeki tena” alisema.


  Katika hatua nyingine amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa mafunzo yote ya Jeshi Usu ambayo yanaendelea katika kituo cha Mlele, Mkoani Katavi yanaratibiwa moja kwa moja na Wizara tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo uratibu unafanywa na taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.


  Akizungumzia mafanikio ya vita dhidi ya ujangili na matunda ya mafunzo hayo alisema, “Katika siku za hivi karibuni tumepiga hatua kubwa ya kupambana na ujangili hasa wa tembo, Kwa dhati napongeza jitihada zinazofanywa na zinazoendelea kufanywa na wahifadhi, maaskari watumishi wengine na wadau wetu wote kwa ujumla ambazo zimeimarisha hali ya uhifadhi wa maliasili zetu”. 


  Alisema kwa kiasi kikubwa matukio ya ujangili yamepungua na kwamba nyara nyingi zinazokamatwa katika kipindi hiki ni za zamani ambazo zilikuwa zimefichwa na majangili kwa ajili ya kuzitafutia masoko au kukimbia mikono ya sheria.


  Alisema Wizara yake itaendelea kutumia mbinu za kisasa za kiitelijensia za kukabiliana na ujangili ikiwemo kutumia ndege zisizo na rubani kwa ajili ya doria na kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano ambayo haitaweza kuingiliwa na majangili au watu wengine wenye nia ovu na uhifadhi.


  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Dk. Nebo Mwina akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa mafunzo hayo ya Jeshi Usu, aliwataka kuishi kwenye viapo vyao kwa kudumu katika ukakamavu, uhifadhi, maadili mema na nidhamu.


  Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Dk. James Wakibara aliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyopewa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwa kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali, kujiepusha na rushwa na kudhibiti vitendo vya ujangili.


  Mhifadhi Gloria Bidebeli kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA akisoma risala ya wahitimu hao alisema mafunzo hayo yatawawezesha kuboresha ufanisi wa shughuli za uhifadhi kwa kutii amri na kutekeleza maagizo kwa wakati.


  Mafunzo hayo ya wiki nne ambayo yalianza Novemba, 20 mwaka huu yalihusisha Mameneja wa Mapori ya Akiba na Tengefu 20, Wakuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili wanane, Maafisa Wanyamapori 29 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Wahifadhi Wanyamapori watano kutoka TANAPA na Wahifadhi Wanyamapori 26 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.


  Mafunzo hayo yalihusisha matumizi sahihi ya silaha, mbinu mbalimbali za kupambana na uhalifu, huduma ya kwanza, ukakamavu, sheria mbalimbali zinazosimamia maliasili, ukamataji na upekuzi wa wahalifu na jinsi ya kuwafungulia hati za mashtaka.  0 0

  IMG-20171217-WA0060 IMG-20171217-WA0061

  0 0


  Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuzalisha Dawa ya Viuadudu vya Mbu waenezao Malaria Tanzania (TBPL), Mhandisi Aggrey Ndunguru (katikati) akitoa taarifa ya utekelezaji mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu baadhi ya Halmashauri zilizopatiwa dawa ya viuadudu vya mbu waenezao malaria, Wilayani Kibaha Mkoani Pwani 17 Desemba, 2017.
  Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko wa Kiwanda cha Kuzalisha Dawa ya Viuadudu vya Mbu waenezao Malaria Tanzania (TBPL), Bi. Upendo Ndunguru (kushoto) akifafanua masuala mbalimbali mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati wa kiwanda hicho katika kutafuta masoko ndani na nje ya nchi, Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, 17 Desemba, 2017.(PICHA ZOTE NA MAELEZO)


  Na Mwandishi Wetu, Kibaha-Pwani.

  Kiwanda cha kuzalisha Dawa ya Viuadudu vya Mbu waenezao Malari Tanzania (TBPL) kimefanikiwa kusambaza dawa katika Halmashauri zaidi ya 174 nchini zenye viwango vikubwa vya malaria ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali katika kupambana na ugonjwa wa malaria.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Mhandisi Aggrey Ndunguru, usambazaji wa dawa hizo umefuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 22 mwaka huu.

  Akifafanua kuhusu agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mhandisi Ndunguru alisema kwamba, Rais alizitaka halmashauri zote nchini kununua dawa hizo kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwasababu kiwanda hicho kimejengwa na Serikali kwa lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria.

  “Moja ya mambo ambayo Mhe. Rais alituagiza ni kuhakikisha kwamba kiwanda hiki kinatumika kutengeneza dawa za kuua mbu waenezao malaria na pia alituagiza kwamba halmashauri zote nchini zihakikishe zinanunua dawa hizi, na kwamba Serikali ilitenga shilingi bilioni 250 kwa ajili ya kununulia madawa mbalimbali nchini kwa mwaka huu wa fedha”, alisema Ndunguru.

  Aliongeza kuwa, wakati wa ziara ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kiwanda hicho kilikuwa na akiba ya takribani lita 100,000 za viuadudu zenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 ambazo zilikuwa hazijapata wateja, ndipo Rais akatoa agizo kuwa halmashauri zote nchini kufika kiwandani hapo na kuchukua viuadudu hivyo.

  Alifafanua kuwa, kufuatia agizo hilo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilikishauri kiwanda hicho kuanza kusambaza viuadudu hivyo kwa kuanzia Mikoa 14 yenye halmashauri 96 kwa awamu ya kwanza ambayo ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria kisha mikoa 12 iliyobaki ifuatie baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.

  “Hadi kufikia sasa, kiwanda kimefanikiwa kusambaza viuadudu kwa halmashauri 174, halmashauri 96 kutoka katika mikoa 14 zilichukua viuadudu katika awamu ya kwanza na halmashauri 78 kutoka mikoa 12 zilichukua katika awamu ya pili, lakini hadi sasa zimebaki halmashauri nne tu ambazo bado hazijachukua”, alisema Ndunguru.

  Aidha, aliongeza kuwa, hadi sasa kiwanda kina jumla ya lita 64,280 ambazo zipo katika ghala huku akifafanua kwamba, katika soko la Kimataifa kiwanda kimeuza dawa hizo kwa nchi ya Niger lita 90,371 na nchi nyingine kadhaa zimeonyesha nia ya kutaka kununua dawa hizo zikiwemo nchi za Angola ambayo imeonyesha nia ya kuhitaji lita 106,060 na nyingine yenye mahitaji ya dawa hizo ni Msumbiji.

  Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa kiwanda hicho, Bi. Upendo Ndunguru ameeleza kwamba, moja mikakati wanayofanya katika matumizi ya dawa hizo ni uelimishaji kwa jamii ili kuhakikisha kwamba jamii inapata uelewa wa matumizi ya dawa hizo na kuzitumia kwa kuweka katika maeneo yenye mazalia ya mbu ili kuikinga jamii hususani akina mama wajawazito na watoto wadogo.

  Kuhusu suala la upatikanaji wa masoko ndani na nje ya nchi, alifafanua kwamba, wanaangalia sana soko la ndani ambalo kwa ukubwa wake limeongezeka baada ya agizo la Rais kutolewa mwezi Juni mwaka huu, huku akisisitiza kwamba jamii hainabudi kuzingatia suala la kutokomeza mbu kwa kutumia viuadudu hivyo.


older | 1 | .... | 1463 | 1464 | (Page 1465) | 1466 | 1467 | .... | 1898 | newer