Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

ETIHAD AIRWAYS INCREASES MALDIVES FREQUENCY FROM DAILY TO 11 FLIGHTS A WEEK IN SUMMER 2018

$
0
0

Abu Dhabi, UNITED ARAB EMIRATES – Etihad Airways today announced four additional weekly flights on the popular Abu Dhabi – Malé route, taking frequency to the idyllic Maldives to 11 services a week from June next year.
The extra flights, effective 15 June 2018, will operate year-round and provide more travel options with an early morning arrival enabling guests to maximise their stay in the Maldives.

In addition to providing greater choice and flexibility for UAE and GCC residents, overall connectivity and timing options between the Maldives and key countries on Etihad Airways’ European network will be enhanced. These include the major markets of the UK, Germany, France, Italy and Russia.

The expansion from the current daily operation will continue to see a two-class A320 aircraft on the route, offering 16 seats in Business Class and 120 in Economy.

Peter Baumgartner, Etihad Airways Chief Executive Officer, said: “We are increasing frequency to 11 flights a week in order to cater to growing demand on the route, and to provide our guests with more choice of flights so that they can make the most of their stay in the Maldives.”

Since launching the route in November 2011, Etihad Airways has flown more than 550,000 passengers to and from the Maldives. Visitors from the UAE increased 35 per cent over the past 12 months, while Europe continues to be the main source market for the Maldives, one of the world’s premium honeymoon and leisure destinations.

The additional flights (*) will operate every Monday, Friday, Saturday and Sunday from 15 June 2018.

Flight No.
Origin
Departs
Destination
Arrives
Frequency
Aircraft
EY 278
Abu Dhabi
08.40
Malé
14.05
Daily
Airbus A320
EY 279
Malé
20:35
Abu Dhabi
23:50
Daily
Airbus A320
EY 260 *
Abu Dhabi
00:55
Malé
06:20
Mon, Fri, Sat and Sun
Airbus A320
EY 261 *
Malé
18:50
Abu Dhabi
22:05
Mon, Fri, Sat and Sun
Airbus A320
-ends-

Ecobank Tanzania yasaidia kupatikana kwa maji safi kwa Shule ya Hananasif

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee – kulia, akimkabidhi vitabu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hananasifu Idda Uisso iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee akijaribu moja ya mifereji ya maji salama katika wa Shule ya Msingi Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee akikata utepe kuashiria upatikanaji wa maji Shule ya Msingi Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso..
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Hananasifu Idda Uisso akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank baadhi ya mifereji ambayo kwa sasa inatoa maji salama baadhi ya kufanyiwa ukarabati na benki hiyo.
Mmoja wa mfanyakazi wa Ecobank akinawa kuashiria kuanza kupatikana kwa maji salama baada benki hiyo kutengeneza miundombinu na kusafisha mifereji iliyokuwa imeziba katika shule ya Msingi ya Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule ya Msingi Hananasifu, Kinondoni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso.
Diwani wa Kata ya Hananasifu akitoa neon la shukrani kwa uongozi wa Ecobank Tanzania. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule ya Msingi Hananasifu, Kinondoni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso. 
Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo na maeneo yenye uhitaji wa maji kwa wanafunzi na waalimu wote wa shule ya Msingi ya Hananasif iliyopo katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo hufanyika kila mwaka katika nchi 33 barani Afrika ambapo Ecobank inafanya biashara.

Msaada huo wa Ecobank Tanzania kusaidia shule hiyo kupata maji safi umetolewa leo ikiwa njia moja wapo ya kuadhimisha kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya Ecobank inayosema ‘Maji Salama, Ishi na Afya njema’ Safe Water, Healthy Living’

Mbali na Ecobaank kutoa msaada huo, wafanyakazi wa Ecobank Tanzania pia wamejumuika kwenye kufanya usafi wa mazingira shuleni hapo kwa kuzibua mitaro ya maji taka yote pamoja na kuweka dawa kwenye kisima cha maji shuleni hapo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama.

Kwa upande wa elimu, Ecobank pia imetoa vitabu kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao kuanzia darasa la kwanza hadi la sita.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi Mwanahiba Mzee alisema benki hiyo imekuwa ikiadhimisha siku ya Ecobank kwa kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa Jamii inayowazunguka.

“Tuliguswa sana baada ya kupewa taarifa kuwa shule ya Hananasif ina jumla ya wanafunzi 728 lakini miundombinu ya maji imeziba na kubakia na sehemu moja tu ambayo inatumiwa na shule nzima. Vyoo havina maji na hivyo imekuwa ni changamoto ya kiafya kwa wanafunzi, walimu na watu wengine kwenye shule hii, tukaona ni vyema kuja kusaidia ” alieleza Mwanahiba Mzee 

Bi Mzee, alisema kutokana na Benki yake kutoa msaada huo, pamoja na vitabu vya kiada, motisha yaa zawadi kwa wanafunzi itasaidia kutoa hamasa kwa wanafunzi kuendelea kuongeza bidii kwenye masomo yao zaidi

“Ecobank Tanzania inatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora pamoja na kuboresha elimu ikiwa ni dhamira yetu katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu hapa nchini, aliongeza Bi Mwanahiba Mzee .

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Hananasif Mwalimu Idda Uisso Alitoa shukrani kwa juhudi za Ecobank Tanzania kwa kuhakikisha shule hiyo inapata maji salama. “Nachukua hii fursa kuwapongeza uongozi wa Ecobank Tanzania kuchagua kuja shule ya Hananasif kwani hapa kuna shule zingine nyingi.

Alisema changamoto kubwa ilikuwa ni maji kwani kwa Idadi kubwa ya wanafunzi walionao maji safi na salama ni muhimu. “Kwa msaada wa mamboresho ya miundombinu yote mliyofanya, kwa sasa tuna uhakika wa maji safi na salama kwa waalimu pamoja na wanafunzi” alisema.

Vile vile alitoa shukrani za dhati kwa msaada wa vitabu pamoja na zawadi kwa wanafunzi bora kwani kutaongeza hamasa kwa wanafunzi. “Sisi kama shule tumekuwa tukifanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa lakini kwa msaada wa vitabu na kuhamasisha wanafunzi, nina uhakika na ninawaahidi Ecobank tutaendelea kufanya vizuri zaidi”.

Ecobank sasa inafakisha miaka 8 hapa nchini Tanzania huku ikiwa na matawi ya kutoa huduma bora za kibenki katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha

SHEREHE ZA UVISHWAJI PETE WAKINA MAMA WALEZI WA SOS YAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Rais wa SOS Duniani Father Siddhartha Kaul mara baada ya kuwasili katika Kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguja katika Sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar.katikati ni Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Shadya Mohammed Suleiman.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuwasalimia wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Wakina mama walezi 18 wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar waliovishwa Pete katika sherehe zilizofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Duniani Father Siddhartha Kaul akitoa hotuba yake kuhusianana lengo la kuwekwa vituo vya kulelea watoto SOS Duniani katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kushoto akimvisha Pete ya SOS Mama mlezi wa SOS Fatma Suleiman Haji anaelea Watoto Nyumba Namba Nne katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wanne kutoka kulia akiwa na Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Shadya Mohammed Suleiman katika Picha ya pamoja na Wakina mama walezi waliovishwa Pete katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

RAIS DKT MAGUFULI AWASILI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Binilith Satano Mahenge alipowasili Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Novemba 7, 2017 tayari kwa shuguli mbalimbali za kikazi. PICHA NA IKULU

MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA AMALIZA HOFU YA WAFANYABIASHARA 2,500

$
0
0

NA RAMADHANI JUMA,
OFISI YA MKURUGENZI

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amemaliza hofu ya kuhamishwa iliyokuwa imetanda kwa wafanyabiasha takribani 2,500 wa Soko la Sabasaba Mjini Dodoma baada ya kuwahakikishia kuwa wataendelea kufanya shughuli zao katika Soko hilo linalomilikiwa na Manispaa ya Dodoma na kwamba hakuna wa kuwahamisha.

Aliyasema hayo jana alipofanya ziara Sokoni hapo na kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ambao walimueleza Mkurungenzi huyo kuwa wamekuwa wakipata taarifa zisizo rasmi kuwa upo mpango wa wao kuhamishwa katika soko hilo hali inayowakosesha usingizi na kutojua hatma yao.

“Hakuna kuhama hapa ng’oo…Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ndiyo mmiliki wa Soko hili ambalo asili yake hapo awali lilikuwa eneo la Maonesho ya Sabasaba ambapo wadau mbalimbali walikuwa na vibanda vyao vya maenesho” alifafanua Kunambi huku akishangiliwa na wafayabiashara hao.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Kunambi alifuatana na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede.Wafanyabiashara hao waliishukuru Manispaa ya Dodoma baada ya viongozi hao kufika na kuzungumza nao katika wakati muafaka baada ya kufanya biashara zao kwa wasiwasi mkubwa kwa siku kadhaa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba (hawapo pichani) Mjini Dodoma jana ambapo aliwahakikishia kuwa hawatahamishwa katika soko hilo. 
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya DodomaJumanne Ngede akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Mjini Dodoma jana ambapo alifuatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi. 
Sehemu ya Wafanyabiashara ya Manispaa ya Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Mkurugenzi huyo na wafayabiashara wa soko hilo jana.

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA BAADHI YA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU, MKUU WA MKOA WA ARUSHA NA KAMATI SHIRIKISHI YA JAMII KUHUSU UTATUZI WA MGOGOIRIO WA PORI TENGEFU LA LOLIONDO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) na Mkurugenzi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Pastoralist Women Council, Manda Ngoitika baada ya kikao kilichowahusisha baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Kamati Shirikishi ya Jamii kuhusu utatuzi wa Mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo kilichofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, mjini Dodoma Desemba 6, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kilichowahusisha baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Kamati Shirikishi ya Jamii kuhusu utatuzi wa Mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo kilichofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, mjini Dodoma Desemba 6, 2017.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WANANCHI MBALIMBALI NA WASHIRIKI WA SEMINA JIJINI MOROGORO

$
0
0



Maafisa wa UTT AMIS wakitoa elimu ya jinsi mifuko ya Uwekezaji wa pamoja inayosimamiwa na kampuni hiyo na kwamba ni suluhisho kubwa la maisha baada ya kustafu katika semina iliyoandaliwa na National Institute of Productivity (NIP) jijini Morogoro.

PROFESA MBARAWA: MRADI WA UJENZI UBUNGO- KIBAHA KUIPAISHA NCHI KIUCHUMI

$
0
0
Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Rasilimali Watu katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bi. Visensia Kagombora (katikati) kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ubomoaji wa majengo ya Wizara hiyo yaliyopo katika eneo la Ubungo maji Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale. Ziara hiyo ilifanyika jana Desemba 6, 2017.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa kuhusu utekelezaji wa zoezi la ubomoaji wa majengo ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ili kupisha ujenzi wa barabara za njia sita zinazoanzia eneo hilo hadi Kibaha Mkoani Pwani. Wengine pichani ni Watendaji wa TANESCO. Ziara hiyo ilifanyika jana Desemba 6, 2017.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza jambo na Watendaji wa Wakala wa Barabara (TANROADS) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya zoezi la upanuzi wa barabara katika Jiji la Dar es Salaam kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani. Wengine ni Watendaji Wakuu wa TANROAD Mkoa na MakaoMakuu. Ziara hiyo ilifanyika jana Desemba 6, 2017.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale wakati wa ziara ya kukagua zoezi la upanuzi wa barabara kutoka Ubungo Jijini la Dar es Salaam hadi Kibaha Mkoani Pwani. Ziara hiyo ilifanyika jana Desemba 6, 2017.PICHA NA MAELEZO


Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

SERIKALI imesema mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani yenye urefu wa kilometa 16 unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa katika nchi jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo jana Desemba 6, 2017, Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha inamaliza changamoto ya msongamano na kuziwezesha barabara zote za Jiji la Dar es Salaam kupitika katika majira yote yam waka.

Prof. Mbarawa alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mradi huo utakelezwa kwa ufanisi, viwango na ubora wa hali ya juu na kuwahakikisha wananchi waliopitiwa na mradi huo kuwa barabara hizo zitamaliza kero ya muda mrefu ya msongamano wa magari na hivyo hawana budi kuunga mkono juhudi hizo.

Kwa mujibu wa Prof. Mbarawa alisema tangu mwaka 1932 wakati wa utawala wa Gavana wa Kiingereza, Serikali iliweka sheria ya upanuzi wa barabara katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na kutambua ongezeko la idadi ya watu na msongamano wa magari ambayo ingekuwepo katika miaka ya sasa, hivyo zoezi la ubomoaji wa nyumba hizo ulikuwa haukwepeki.

“Katika kutekeleza mradi huu wa barabara za njia sita, majengo ya Serikali ikiwemo Ofisi za Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Wizara ya Maji pia yameondolewa katika maeneo ya hifadhi ya barabara ambapo mradi huu utapita, hivyo nasi wananchi hatuna budi kuunga mkono juhudi hizi” alisema Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa alisema wakati wa utekelezaji wa mradi wa barabara hizo unaotarajiwa kujengwa katika kiwango cha lami, na hakutokuwa na usumbufu kwa wananchi wanaotumia barabara hizo kwani Serikali imejenga njia mbadala za pembezoni mwa Jiji ili kurahisisha usafiri wa abiria na mizigo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale alisema Ofisi yake imejipanga kikamilifu kutekeleza mradi huo ili kuhakikisha kuwa Jiji la Dar es Salaam linaendelea kuwa kitovu cha uchumi na kiungo cha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi jirani.

Mhandisi Mfugale alisema katika kuondoa changamoto ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam, Ofisi yake imeiweka barabara ya Ubungo-Kimara katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo yao.

Naye Mwananchi wa Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam, Said Kilindo alisema wananchi wa maeneo hayo wamepokea kwa moyo mkunjufu utekelezaji wa mradi huo na kuiomba Serikali kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo ukosefu wa miundombinu ya vyoo katika maeneo mengi ya wafanyabiashara waliokuwepo katika maeneo hayo.

UNGANA NA MCHUNGAJI DKT. HURUMA NKONE NA MWINJILISTI JOHANNES KATIKA SEMINA YA SIKU 3 ZA MATUMAINI

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHANDISI KAMWELWE, AMUAGIGA KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA KIUTENDAJI KWENYE BOHARI KUU YA MAJI

$
0
0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe, amesitisha manunuzi yote ya vifaa vya maji yanayofanywa na Bohari Kuu ya Maji jijini Dar es Salaam hadi hapo Serikali itakavyoelekeza vinginevyo.
Lakini pia ameagiza mamlaka zote zinazotekeleza miradi ya maji au zinazoendesha utoaji wa huduma ya maji waende bohari kuu kuangalia vifaa vinavyoweza kutumika kwao ili wavinunue viishe kabla ya kuelekea kwenye hatua nyingine.
Kumekuwepo na ununuzi holela wa vifaa Halmashauri na Mamlaka za maji zimekuwa zikijinunulia vifaa jinsi wanavyotaka nah ii ni hatari sana ndio maana miradi mingi haiendani na thamani halisi ya vifaa, na vinapatikana kwa gharama kubwa mnno, Aalisema Mhandisi Kamwelwe.
“Mamlaka zote za maji zilizo chini ya wizara yangu, mtu asije akaenda kununua vifaa nje ya bohari kuu kama kifaa hicho kinapatikana kwenye bohari hiyo.” Alisema Mhandisi Kamwelwe.
Na kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwenye bohari hiyo kwani kwa hali ilivyo imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake.
Mheshimiwa Waziri alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea bohari hiyo iliyoko Boko jijini Dar es Salaam, mwanzoni mwa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kupitia DAWASA Desemba 5, 2017.
Alilaumu utendaji duni wa watendaji wa Bohari hiyo unaoonyesha kuishiwa ubunifu. Na hivyo kufanya shughuli kulegalega.
“Serikali imenunua vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.83 vingine vinaonekana vimepitwa na wakati, lakini vingine vinaonekana vinaweza kutumika, na boharia inahitaji watu ambaom ni wabunifu, na kwa vile vilivyopitwa na wakati viko viwanda vinatengeneza vifaa kama hivyo uongozi ni bora ukawasiliana na viwanda hivyo ili waone tatizo ni nini na inawezekana kuboresha eneo ambalo linavifanya visitumike ili vikaweza kutumika na kuokoa fedha za serikali.
“Nakuagiza ufanye kazi hiyo kwa haraka na umpatie taarifa Katibu Mkuu, sitaki kuona kitu hata kimoja kinapotea kwani vifaa hivi vimenunuliwa na kode za wananchi na fedha za serikali.” Aliagiza Waziri Kamwelwe.
Katika hatua nyingine, Waziri amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwenye bohari hiyo ili pawepo na wataalamu husika kuloingana na shughuli za bohari.
Aidha Waziri ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wadeni wote wa Bohari Kuu ya Maji, kulipa madeni yao vinbginevyo atachukua hatua baada ya muda huo kupita.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe, akiangalia dira za kupimia maji, alipotembelea bohari kuu ya maji Boko jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.

Meneja wa Bohari Kuu ya Maji Bw. Clepline Bulamo, akizungumza wakatyi akitoa taarifa kwa Mhe. Waziri Kamwelwe.
 Mhe. Kamwelwe, (kushoto), akionyeshwa moja ya vifaa vya maji vinavyotunzwa kwenye bohari kuu ya maji na Meneja wa Bohari Kuu ya Maji Bw. Clepline Bulamo
 Mhandisi Kamwelwe, (Kushoto), akizungumza jambo mbele ya Meneja wa Bohari Kuu ya Maji, Bw. Clepline Bulamo, na watendaji wakuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo, (wapili kushoto) na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, mhandisi Mhandisi Cyprian Luhemeja, wakati wazirin akikagua vifaa vya maji vinavyotunzwa kwenye bohari hiyo, Boko jijini Dar es Salaam.
 Mhandisi Kamwelwe, (Kushoto), akiongozana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mwang'ingo, wakati akikagua vifaa hivyo vya maji kwenye bohari kuu ya maji.
 Mabomba ya maji yakiwa kwenye eneo la wazi kwenye bohari hiyo
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo,  (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja, wakijadili jambo wakati wa ziara ya Mheshimiwa Waziri.
Waziri Kamwelwe, na ujumbe wake akiendelea na ukaguzi wa vifaa vya maji
Waziri Kamwelwe, na akiendelea na ukaguzi wa vifaa vya maji kwenye bohari kuu ya maji, Boko jijini Dar es Salaam
Waziri Kamwelwe, (Kulia), akiuliza jambo mbele ya Meneja wa Bohari Kuu ya Maji Bw. Clepline Bulamo Dar es Salaam.

IN LOVING MEMORY OF MAMA ROSE SHOMARI

$
0
0
It has been 12 years since you departed from us, in this day a memory of a life so beautifully lived and a heart so deeply loved. We will always remember you and the lessons of life you gave us. May the Lord God hold you in Peace. In our hearts, you will always be remembered every day with the whole entire Shomari family your sons, daughters, grandsons, and granddaughters.
We thank God for your life, great advice, as a loving mother and a counselor. May the almighty Lord rest your soul in eternal Peace until we meet again.
Our hope comes from the Lord as he says he will wipe every tear from their eyes there will be no more death or mourning or crying or pain…Rev 21:4.

WAZIRI WA UJENZI PROF. MAKAME MBARAWA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA UBUNGO- KIBAHA

AGPAHI YAMWAGIWA SIFA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BORESHA UNAOHUSU WATU WANAOISHI NA VVU MKOANI SIMIYU

$
0
0


Meneja wa Shirika la AGPAHI kanda ya ziwa, Dk. Nkingwa Mabelele akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za shirika hilo katika kikao cha ushauri cha mkoa wa Simiyu (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT Mjini Bariadi Desemba 5,2017. Picha zote na Derick Milton - Simiyu News blog
Dk. Nkingwa Mabelele, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za shirika la AGPAHI ikiwa pamoja na Mradi wa Boresha, ambao unawahudumia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU mkoa wa Simiyu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoa wa Simiyu Robert Rweyo akichangia taarifa ya shirika la AGPAHI katika kikao cha ushauri cha mkoa (RCC) ambapo alipongeza mradi wa Boresha huku akiomba halmashauri yake kupatiwa gari kama halmashauri zingine zilivyopatiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, akiongea na wajumbe wa kikao cha ushauri cha Mkoa (RCC).
Wajumbe wa kikao cha Ushauri mkoa wa Simiyu (RCC) wakiendelea na kikao.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga akichangia taarifa iliyowasilishwa na Dk Nkingwa Mabelele, wakati wa kikao cha ushauri cha mkoa (RCC) ,ambapo alisema kuwa shirika hilo limefanikisha kufikika kwa haraka huduma za afya kwa wahusika baada ya kutolewa gari katika idara ya afya, na watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wamekuwa wakipata huduma kwa wakati na kutatuliwa changamoto zao.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Wilaya ya Busega Mikness Mahela, akichangia taarifa iliyowasilishwa na Dk. Nkingwa Mabelele.
Dk. Nkingwa Mabelele, alieleza kuwa kwa sasa shirika la agphai linatekeleza miradi wa Boresha katika mikoa sita ambayo ni Geita, Mara, Shinyanga, Mwanza, Tanga na Simiyu.
Wajumbe wa Kikao cha Ushauri Mkoa, wakifuatilia taarifa ya Shirika la AGPAHI kwa ukaribu.
 ****
Uongozi wa mkoa wa Simiyu, Madiwani, pamoja na wabunge wamelipongeza Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI katika kutekeleza mradi wake wa Boresha mkoani Simiyu.
Pongezi hilo zimetolewa na viongozi hao katika kikao cha ushauri cha mkoa kilichofanyika Desemba 5,2017 katika ukumbi wa KKKT Mjini Bariadi, ambapo walisema utekelezaji wa mradi huo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU imesaidia mkoa wa Simiyu kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
Akiongea kwa niaba ya wabunge, mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga mara baada ya Meneja wa Shirika la AGPAHI kanda ya Ziwa, Dk. Nkingwa Mabelele kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za shirika.
Alisema shirika hilo limerahisisha usafiri kwa wasimamizi wa shughuli za UKIMWI wilayani hivyo kufanikisha utoaji wa huduma bora za afya kwa watu wanaoishi na VVU , baada ya kutolewa gari katika idara ya Afya, ambapo wagonjwa wamekuwa wakipata huduma kwa wakati na kutatuliwa changamoto zao.
Kwa upande wake ,mwenyekiti wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Robert Rweyo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Wilaya ya Busega, Mikness Mahela walipongeza kazi za shirika la AGPAHI hasa katika kuwahudumia watu wanaoishi na VVU.
“Tumekuwa tukiona kazi nzuri za AGPAHI, tunalipongeza sana shirika hili kwani ni moja kati ya taasisi zisizo za kiserikali ambazo zinafanya vizuri kwenye mkoa wetu hasa kuwahudumia wananchi ambao wanaishi na VVU ” ,alisema Mahela.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alisema amekuwa akifuatilia kazi za shirika la AGPAHI kwa ukaribu na alilipongeza shirika kwa kutekeleza mradi wa Boresha vizuri huku akiliomba kusaidia mkoa katika kutoa elimu zaidi ya uzazi wa mpango.
“Mkoani kwetu tuna tatizo kubwa la wananchi wake kutopenda kutumia njia ya uzazi wa mpango, tunawaomba kama mnaona inafaa kusaidia katika kutoa elimu kwa wananchi wetu juu ya umuhimu wa elimu ya uzazi wa mpango” ,alisema Mtaka.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Shirika hilo ndani ya mkoa wa Simiyu, Meneja wa Shirika hilo kanda ya Ziwa, Dk. Nkingwa Mabelele alisema katika mradi huo wamewapima jumla ya wananchi 197,649 sawa na asilimia 151% ya lengo la mradi kwa kipindi cha Oktoba 2016 hadi Septemba 2017, na kati ya waliopimwa 6,783 walibainika kuwa na VVU. 
Alisema waliwapima wananchi hao kwa mkoa mzima ambapo waliobainika kuwa na VVU walianzishiwa huduma za matibabu (dawa za ARVs) mara moja.
Aidha Dk. Mabelele alieleza kuwa katika mikoa wanayoendesha mradi wa BORESHA ni Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, na Tanga wamefanikiwa kuwapima watu 1,472,286 ikiwa ni asilimia 146% ambapo walilenga kuwafikia wananchi 1, 018, 591. 
Alisema kati ya wananchi hao waliopimwa afya zao, 63416 walibainika kuishi na VVU, zoezi ambalo lilifanyika katika kipindi cha Mwezi Oktoba 2016 hadi June 2017.
AGPAHI ni shirika la kitanzania lisilo la kiserikali linajishughulisha na programu za kutokomeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi, kuzuia maambukizi mapya ya VVU kwa watoto, matunzo na huduma za matibabu kwa watu wanaoishi na VVU nchini Tanzania.
Kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wahisani, shirika limekuwa likiunga mkono utoaji wa huduma za VVU katika mifumo iliyopo.
AGPAHI imejikita katika kutoa msaada wa huduma zenye ubora wa hali ya juu na kuhakikisha jitihada za kufikia lengo la pamoja la kutokomeza Maambukizi ya VVU kwa watoto linafikiwa.Shirika linafanyakazi katika mikoa ya Tanga, Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu na mkoa wa Manyara wilayani Simanjiro kwenye machimbo ya Mererani.
Na Derick Milton - Simiyu News blog

RC RUVUMA ATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA NCHINI.

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME amewataka wafanya biashara wote nchini kuja mkoani ruvuma kununua mahindi,tamko la kutaka wafanya biashara kuja mkoani Ruvuma linakuja baada ya serikali ya awamu ya tano kufungua mipaka kwa ajili ya wafanyabiashara waweze kupeleka mahindi nje ya nchi

WANANCHI WA KIGAMBONI GEZAULOLE WAIOMBA SERIKALI KUWALIPA FIDIA YAO KUPISHA UJENZI SHIRIKI WA MPANGO MJI.

$
0
0
Na David John

BAADHI ya wananchi wa Kigamboni Gezaulole Kata ya Somangila mtaa wa Mwela jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali kulipa fidia kwa wananchi hao ambao walitakiwa kupisha ujenzi shiriki wa mpango Mji.

Wamesema kuwa ni muda mrefu sasa umepita hawajuwi mstakabali wa fidia hiyo nakudai ni vema serikali ikafanya haraka kuwafidia ili waondokane na hali ngumu wanazokutana nazo.

Akizungumza kwaniaba ya wezake mmoja wa waathirika na mchakato huo Marando Nyanda alisema wakati wanaambiwa wapishe tayari wao walikuwa na mazao mbalimbali ambapo Serikali walisema watafidia.

"Sisi kwa kutambua umuhimu wa mradi huu tulikubaliana na Serikali kwamba wangetufidia lakini cha ajabu hadi kufikia leo sisi baadhi ya wakazi wa maeneo haya hatujalipwa. "amesema Marando

Ameongeza kuwa mchakato huo ulikuwa shirikishi lakini hadi kufikia leo watu zaidi ya 160 hawajuwi mstakabali wa malipo yap na kudai nimiaka mitano imepita sasa.

Wananchi hao amesema hakuna asijuwa juu ya jambo hilo kuazia mkuu wa mkoa hadi mawaziri wenye dhamana wanajuwa huku wakimtaka Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo ili wao wapate haki zao.

Akizungumzia jambo hilo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula alisema kuhusu jambo hilo wananchi hao wanatakiwa waende katika ofisi za halmashauri ya kigamboni.

Alisema kuwa kuhusu uboreshaji wa mpango mji katika halmashauri hiyo upo chini ya halmashauri hiyo ya kigamboni hivyo nivema wakafika huko au kuonana na Mkuu wa wilaya hiyo ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo.
 
Marando nyanda mmoja wa wakazi wa Kigamboni Gazaulole ambaye anasotea fidia ya kupisha ujenzi shirikishi wa mpango mji katika eneo hilo picha na David John. 

CTI WAZINDUA TUZO ZA VIWANDA KWA MWAKA 2017 LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Loedigar Tenga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 kwa wanachama na wasio wanachama wa CTI na kuvitaka washiriki kujitokeza kuchukua fomu za ushiriki.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) limezindua tuzo za President's Manufacturer of the year awards 2017 (PMAYA) ikiwa ni mara ya 12 toka kuanzisha kwake mwaka 2005.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo za PMAYA kwa mwaka 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Leodigar Tenga amesema kuwa tuzo hizi zinaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika kuelekea uchumi wa viwanda.

Tenga amesema kuwa tuzo hizi kwa mwaka huu zimezinduliwa mapema zaidi ili kuwapa fursa wenye viwanda kushiriki kwa wingi, kwani kuanzia mwaka 2016 tuzo za PMAYA zinajumuisha kwa wanachama na wasio wanachama wa CTI.

Akielezea tuzo zilizopita ambapo ziliweza kuleta hamasa kwa wamiliki mbalimbali wa Viwanda, Mkurugenzi Mtendaji Tenga amesema kwa mwaka 2017 anatarajia kuona namba ya washiriki ikizidi kuwa kubwa kutokana na kuruhusu pia wasio wanachama kuja kushiriki na kwa mara nyingine tena kutakuwa na tuzo ya ufanisi wa nishati.

"Kuanzia mwaka jana tumeamua kushirikisha wasio wanachama wa CTI ili kuweza kushiriki nasi katika tuzo hizi za PMAYA na hili ni jambo kubwa sana kwani tunaamini washiriki watakuwa wengi na kwa mwaka huu kutakuwa tena na tuzo ya ufanisi wa nishati, "amesema Tenga.

Kwa upande wa mdhamini mkuu wa tuzo hizo, Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa wateja kutoka benki ya CRDB Tully Mwambapa amesema mwaka huu watadhamini tuzo hizo kwa kiasi cha fedha dola za kimarekani 35,000 sawa na milioni 70 za kitanzania.

Tully amesema kuwa, benki yao imeweza kushirikiana na viwanda mbalimbali kwani benki yao inatoa mikopo kwa viwanda vidogo na vikubwa na ukiangalia kwa mwaka jana walitumia takribani bilioni 160.

Mkurugenzi Mkuu wa ISHARA Consultant Olive Mosha amesema kuwa viwanda vyote vikubwa na vidogo vinaruhusiwa kuja kushiriki katika tuzo hizo ambapo kampuni yao itasimamia kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mashindano hayo.

Tuzo hizo zinazoratibiwa na CTI zimekuwa zinatoa mchango mkubwa sana kwa wamiliki wa viwanda kuweza kujitathmini kila mwaka kwa kuangalia wanapotakiwa kuboresha kuanzia kwenye uendeshaji wa kiwanda.

Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa wateja kutoka benki ya CRDB Tully Mwambapa akizungumza na waaandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 wakiwa kama wadhamini wakuu wa tuzo hizo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania Leodigar Tenga.

Mkurugenzi Mkuu wa ISHARA Consultant Olive Mosha akielezea namna watakavyoweza kupata mshindi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 na wakisisitiza washiriki kuchukua fomu mapema leo Jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wakisikiliza kwa makini.

WAZIRI MKUU AFUNGUA JENGO LA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP. nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga.
Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga.
Baadhi ya washiriki wa Ufunguzi wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kabla ya kufungua Ofisi hiyo eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi yake uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Dr. Augustine Mahiga kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba  7, 2017. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii maarufu wa mjini Dodoma Mwinamila baada ya onyesho la ngoma la kikunid cha msanii huyo kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto kwake), eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mahariki, Dr. Augustine Mahiga akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi w UNDP Nchini uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustinew Mahiga na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashaiki, Augustine Mahiga (kushoto kwake) wakitoka ndani ya Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwkilishi Mkazi wa UNDP, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya msanii maarufu wa Dodoma, Mwinamila baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Dr. Augustine Mahiga na wapili kushoto kwake ni Mratibu Mkazi wa Mshirika ya Umoja wa mataifa ma Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Watatu kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mshariki, Dr. Augustine Mahiga na watatu kulia waliokaa ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini , eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Watatu kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mshariki, Balozi Dr. Augustine Mahiga na watatu kulia waliokaa ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Matifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata keki ikiwa ni moja ya shughuli za ufunguzi wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mahariki, Dr. Augustine Mahiga. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

KUELEKEA 9 DISEMBA

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MAMBO YA NJE KUTOKA BUNGE LA CHINA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China ulioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa kamati hiyo, Mheshimiwa CAO Weizhou (wa pili kulia) wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, pale ugeni huo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimsikiliza Naibu Mkurugenzi wa kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mheshimiwa CAO Weizhou (kulia) pale ugeni kutoka kamati hiyo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimpatia zawadi Naibu Mkurugenzi wa kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mheshimiwa CAO Weizhou (kushoto) pale ugeni kutoka kamati hiyo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Mambo ya Nje kutoka Bunge la China wakiongozwa na Mheshimiwa CAO Weizhou (kushoto waliokaa) pale ugeni kutoka kamati hiyo ulipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA TAIFA YA USAFI WA MAZINGIRA AWAMU YA PILI MKOANI DODOMA

$
0
0


​Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameagiza utekelezaji wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira uwe ni ajenda ya kudumu ya kila ngazi ya Uongozi.

Makamu wa Rais ameyasema hay oleo wakati wa Uzinduzi wa Kamapeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira awamu ya Pili ukiofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe,mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais alisema Serikali imejiwekea mikakati mbali mbali ya kupambana na maradhi ya kuambukiza ambapo usafi wa mazingira ni njia mojawapo ambapo katika awamu ya kwanza ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira ambapo jumla ya kaya 1,662,550 zilijengwa vyoo na shule 2,133 vilijengwa vyoo bora.

Katika awamu ya Pili iliyozinduliwa leo kaya 5,600,000 zinatarajiwa kuongeza idadi ya vyoo bora na shule za msingi 3,500 na sekondari 700 zitapata huduma ya vyoo bora na sehemu maalum ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni.

“Wahenga walisema Samaki mkunje angali mbichi, methali hii inatukumbusha jukumu la kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa usafi wa mazingira tangia wadogo wakiwa mashuleni”alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alitoa Wito kwa Wanawake wote nchini kujifunga Kibwebwe na kujenga vyoo, alisema Wanawake wamekuwa na vikundi mbali mbali vya kusaidiana na kuwezeshana hivyo kwa kupitia vikundi hivyo wanaweza kufanikisha ujenzi wa vyoo bora majumbani.

Makamu wa Rais aliwapongeza Washindi wote wa Afya na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2016/17. Pia aliwashukuru wadau mbali mbali ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine kufanikisha uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mbele ya mfano wa Choo bora mara baada ya kuzindua kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipokea mfano wa funguo kwa ajili ya kumkabidhi Mgeni rasmi Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuzinduliwa mfano wa Choo bora ndani ya uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma. 

Mgeni Rasmi,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwenye moja ya banda lililokuwa likionesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika suala zima la usafi wa mazingira,alipopita kukagua mabanda mbalimbali yaliyokuwepo uwanjani hapo kabla ya uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma.

Sehemu ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi huo mapema leo mkoani Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang'ombe mkoani Dodoma.
Sehemu ya zawadi mbalimbali walizokabidhiwa watu,taasisi na vikundi mbalimbali vilivyofanya vizuri katika suala zima usafi wa mazingira sambamba na vyoo bora,zawaidi hizo kama vile vyeti,piki piki pamoja na matrekta

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images