Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1454 | 1455 | (Page 1456) | 1457 | 1458 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu ya Chamwino kuhusu ujenzi wa Mahakama Kuu mjini Dodoma leo Desemba 7, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo katika Ikulu ya Chamwino kuhusu ujenzi wa Mahakama Kuu mjini Dodoma leo Desemba 7, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu ya Chamwino kuhusu ujenzi wa Mahakama Kuu mjini Dodoma leo Desemba 7, 2017.

  0 0


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Utamaduni na Utaifa yenye kaulimbiu ya "NCHI YANGU KWANZA" uzinduzi huo utafanywa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ijumaa Desemba 08, 2017 katika ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuanzia saa 9 mchana. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Utamaduni na Utaifa yenye kaulimbiu ya "NCHI YANGU KWANZA" ambapo alisema dhumuni ya kampeni hii ni kuendelea kutengeneza Taifa ambalo linajali utamaduni, mila na desturi zake.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Utamaduni na Utaifa yenye kaulimbiu ya "NCHI YANGU KWANZA" ambapo alisema kampeni hiyo itakuwa inafanyika kila mwaka na itakuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya maadhimisho ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholous William

  PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.
  Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo kwenye mkutano i kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akifafanua jambo wakati akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.

  …………….

  Angela Msimbira – OR-TAMISEMI

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wanafunzi 650,862 sawa na asilimia 98.31 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018

  Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 Tanzania Bara kwenye kikao na waandishi wa habari leo katika ofisi za Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Jafo amesema kuwa idadi wa wanafunzi mwaka huu imeongezeka kwa wanafunzi 124,209 ambapo ni sawa na asilimia 23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2016.

  Amesema kuwa wanafunzi 1912 wenye uhitaji maalum (pupils with special needs) waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018 kwenye shule za sekondari za Serikali.

  Mhe. Jafo amefafanua kuwa wanafunzi 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu hususani vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya Halmashauri ya Mikoa ya Lindi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091), Manyara (1,268), Katavi (976) na Simiyu (1,576).

  Amesema kuwa Halmashauri ambazo zimeshindwa kuwapangia wanafunzi wote waliofaulu nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza ni Halmashauri za Lindi wanafunzi (80) Mbeya (207),Halmashauri ya Jiji la Mbeya ( 1,227), Mbarali (1,578), Kalambo (166), Nkasi (1,318), Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (1,054), Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga (1,553), Babati (581). Hanang (687), Mpanda (262), Nsimbo (714), Halmashauri ya Mji wa Bariadi (369) na Halmashauri ya Wilaya ya Busega (1,207).

  Mhe. Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa ambayo haijakamilisha ujenzi wa miundombinu hasa ya vyumba vya madarasa kuhakikisha wanakamilisha hadi kufikia mwezi februari, 2018 ili wanafunzi watakaochaguliwa kwenye awamu ya pili wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018.

  “Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza nimeshatoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018” Amesema Jafo

  Mhe. Jafo amesisitiza kuwa walezi na wanafunzi ambao watakosa nafasi katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kuwa wavumilivu wakati mikoa inajiandaa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wote kuanza na masomo ya kidato cha kwanza.

  Amewaagiza waalimu na watendaji wa elimu katika ngazi zote nchini kuongeza bidii katika usimamiaji na ufuatiliaji wa utoaji wa elimu nchini na kushirikiana na wadau wa elimu kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2018 bila vikwanzao vikiwemo michango na ada ili kutekeleza sera ya utoaji wa elimu msingi bila malipo.

  Aidha amewaomba Wazazi, Walezi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Wilaya, Halmashauri na shule, kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa , wanahudhuria na kubaki shuleni hadi watakapohitimu elimu ya Sekondari.

  0 0

  Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati mbele) akiwa katika chumba cha mikutano cha Kampuni ya ujenzi ya Kimataifa ya Uholanzi (BAM) linalojenga Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) alipofanya ziara. (Wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na (wa kulia) ni Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul.
  Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Wolfgang Marschick (katikati kushoto) akitoa maelezo ya ujenzi huo leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanza nia (TAA), Bw. Richard Mayongela.
  Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela wakati walipokuwa wakitembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII). Nyuma ni Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka.
  Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Wolfgang Marschick (Kulia) akimuonesha waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) leo alipotembelea jengo hilo. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati).
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani mbele) akimsikiliza Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Wolfgang Marschick (aliyenyoosha mkono) na wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.
  Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof.Makame Mbarawa (wa tatu kulia) alipofanya ziara ya kutembelea jengo hilo leo. Wengine katika picha ni Bw. Wolfgang Marschick (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (pili kulia).
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (aliyesimama mbele), leo akiongea na wadau wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), kwenye ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP). Mbele kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.


  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wadau wanaofanya shughuli mbalimbali zinazohusisha na kodi ya pango kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), kuhakikisha ifikapo Februari 1, 2018 wawe wameshalipa madeni yao.

  Prof. Mbarawa alisema leo wakati alipoongea na wadau hao kwenye ukumbi wa watu Mashuhuri wa JNIA-TBII, wakati walipozungumza nao kujadili masuala mbalimbali.

  Alisema baadhi ya wadau wameshalipa madeni yao kati ya bil 10 zilizokuwa zinadaiwa na sasa zimesalia bil. 3.7 ambapo amewataka baada ya kumalizika kwa sherehe za Krismas na Mwaka Mpya wahakikishe wanakamilisja madeni yao.

  “Hatutasita kumuondoa mtu yeyote atakayekuwa akiendelea kudaiwa kwani atakuwa hana sifa za kupangisha katika majengo haya ya viwanja vya ndege kwa kuanzia TBI na hapa TBII,” alisema Prof. Mbarawa.

  Hatahivyo, aliyapongeza mashirika na ofisi ambazo zimekuwa zikilipa kwa wakati fedha za pango, ambapo uaminifu huo utawasaidia kupata nafasi katika jengo jipya la la tatu la abiria, ambalo litakuwa linauwezo wa kuhudumia abiria milioni sita (6) kwa mwaka.

  Pia amewataka wale wasiowaaminifu wachague kulipa madeni ya pango au wanaodaiwa na serikali au kuondoka, ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengine ambao wanania ya dhati ya kufanya biashara na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wasimamizi wakuu wa viwanja vya serikali.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela alisema tayari zabuni mbalimbali zimeshatangazwa na kuwataka wadau waliowaaminifu kujitokeza kuwania na kupata nafasi ya kufanya shughuli zao kwenye eneo la JNIA.

  “Tumeshatangaza zabuni hizo na kama mhe. Waziri alivyosema zitakuwa za uwazi zikishirikisha wataalamu na tunauhakika watapatikana watu wenye mapenzi mema ya kufanya biashara na serikali” alisema Bw. Mayongela.

  Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa alitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi, ambapo amewapongeza TAA, Tanroads na Kampuni ya ujenzi ya Kimataifa ya Uholanzi (BAM).

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Bw. Mayongela, alisema kukamilika kwa jengo hilo kutatoa fursa nyingi za biashara zikiwemo uwekezaji katika hoteli, kumbi za mikutano, ofisi, migahawa, maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali, huduma za kifedha (benki) na karakana za ndege.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mheshimiwa Balozi Maiga akizungumza kwenye sherehe ya Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestine, kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Towers,5 Desemba 2017.
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina. Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na
  Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour wakiwa katika hafla hiyo.
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kushoto) akitembelea picha za maonesho kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
  Hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyoandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ikiendelea.
  Wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina wakipata picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.

  0 0


  0 0


  Maharamia wa kazi za wasanii zaidi ya 200 waliokamatwa katika zoezi laukamataji kazi feki za sanaa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa kwa sasa anaishukuru serikali kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonyesha kwa kuwa bega kwa bega kwa vile wamekuwa wakinyonya wasanii.

  "Ndugu zangu waandishi nimewaita hapa kuwaeleza juu ya zoezi la kumkamata maharamia wa kazi za sanaa bado linaendelea vizuri na sasa wanatarajia kufikishwa mahakamani wiki ijayo ili waweze kusomewa mashtaka yao," Alisema Msama.

  Msama alisema kuwa mpaka sasa msako huo umefanikisha kukamata vifaa vya zaidi ya bilioni 1 ambavyo ikiwemo kopyuta, laptop na cd feki.Aliongeza kuwa watanzania lazima walipe kodi na wauze kazi zilizo na stika za mapato (TRA) ili wasanii wapate mapato na serikali ipate mapato.

  "Wamachinga acheni kulalamika, mnaopoenda kununua Filamu za nje na ndani hakikisheni Filamu hiyo ina Stika ya TRA, ukiuza yenye Stika mtu hatokukamata", amesema Msama.Msama aliwaomba Watanzania watambue awamu hii ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli haitaki ujanja ujanja, lazima kufanya kazi kwa bidii ili upate kipato halali.

  Hata hivyo, zoezi laukamataji Kazi feki za sanaa litaendelea katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam.
  Mzigo ambao mpaka sasa umeshakamatwa ukiwa umeifadhiwa.Picha/Habari na Kajunason/MMG-Dar es Salaam.  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina akizungumuza na Meneja wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) Audax Kalulama katika simu alipotembelea Ranchi ya Uvinza leo na kuamuru mwekezaji huyo kuondoka kabla ya Januari Mosi mwakani kutokana na Mwekezaji huyo kukaa katika eneo hilo kinyume cha Sheria.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (katikati) kitoa maamuzi ya kuitaka Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) kuondoka katika eneo la hekta 20000 kwenye vitalu tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya Uvinza ifikapo tarehe 1/1/2018.
  Sehemu ya Ranchi ya Uvinza.
  .
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (katikati) akiwasikiliza walinzi wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) hawapo pichani wakitoa maelezo alipotembelea Ranchi ya Uvinza .

  …………………………………………………………………….

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameutaka uongozi wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) kuangalia na kupitia nyaraka walizonazo ili kuona uhalali wa umiliki wa eneo la hekta 20000 kwenye vitalu tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya Uvinza inayomilikiwa na Kampuni ya Ranchi za za Mifugo za Taifa (NARCO)kabla ya Selikali kuwatoa kwa nguvu ifikapo tarehe 1/1/2018.

  Waziri Mpina ametoa maelekezo hayo leo alipotembelea Ranchi ya Uvinza kuangalia shughuli mbalimbali katika Ranchi hiyo ambapo ametoa muda wa hadi Januari mosi mwakani kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo endapo atabaini kuwa amekuwa akikaa kimakosa kuanzia katika vitalu namba 41 hadi 49.

  Aidha Waziri Mpina amesema endapo Mwekezaji huyo ataendelea kubaki baada ya tarehe Mosi Januari, Serikali itamuondoa kwa nguvu na atatakiwa kulipa gharama zote za fidia na usumbufu.“Ninakuagiza angalia taarifa mbalimbali ulizonazo kuhusu umiliki wa eneo hili kama utaona umeendelea kukaa hapa bila kufuata taratibu tafadhali uondoke mara mmoja ili kupisha Serikali kuendelea na shughuli zake” alisisitiza Mpina

  Waziri Mpina amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa Philemoni Wambura kuwaandikia barua ya kuwaondoa wawekezaji wote katika Ranchi hiyo ambao hawajaendeleza kwa zaidi ya asilimia 40 na kwamba wawekezaji ambao wamewekeza kwa zaidi ya asilimia arobaini wanatakiwa kukamilisha malipo yote kabla ya Januari mosi mwakani.

  Alionya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa. Aliongeza kwamba Serikali imegundua baadhi ya wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani na kujipatia faida wakati Serikali haipati chochote.

  Awali, Meneja wa (TGTS) Audax Kalulama akizungumza kwa simu na Waziri Mpina kutoka Arusha amesema kwamba eneo hilo wanamiliki kihalali na kuomba muda ili wawasiliane na Wizara ya Mifugo kuonyesha taarifa za umiliki wa eneo hilo.

  0 0

   Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida,Dk.Denisi Nyiraha(wa kwanza kutoka kulia) akipokea kitabu cha ilani ya uchaguzi wa chama cha mapinduzi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida aliyemaliza muda wake,Marther Moses Mlata.
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida aliyemaliza muda wake,Marther Moses Mlata akisisitiza jambo kwenye kikao chake na viongozi wa UVCCM Mkoa mara alipompokea mwenyekiti wa jumuiya hiyon kwenye ofisi za chama hicho zilizopo mjini Singida.
   baadhi ya wajumbe wa UVCCM Mkoa wa Singida waliohudhuria sherehe za mapokezi ya mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida kwenye makao makuu ya chama hicho mkoa wa Singida.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
  Mwenyekiyi wa UVCCM Mkoa wa Singida,Dk.Denisi Nyiraha akiongea na baadhi ya viongozi wa jumuiya hiyo pamoja na wanachama wa ccm waliohudhuria mapokezi yake kwenye ofisiza CCM Mkoa wa Singida.


  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Marther Moses Mlata ameuagiza umoja wa vijana wa Chama hicho kutumia muda wanapokuwa kwenye makambi ya vijana kuwasaidia wazee  wanaosihi katika nyumba zinazotishia maisha yao kwa kuwajengea na kuwakabidhi wazee hao ili waweze kujihakikishia usalama wa maisha yao.
  Mlata ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida alitoa agizo hilo wakati alipokuwa akimpokea mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida,Dk.Denisi Nyiraha alipokwenda kujitambulisha kwenye ofisi za chama hicho Mkoa wa Singida.
  Aidha Mwenyekiti huyo aliyemaliza muda wake aliweka bayana kwamba kumekuwa kukifanyika makambi mengi sana na kambi hizo zimekuwa zikiwasaidia vijana kujifunza mambo mengi sana,lakini wakati vijana hao wanapokuwa makambini na kugundua kuna nyumba ya mkongwe mmoja inayokaribia kudondoka,watumie makambi hayo kuwasaidia wazee kama hao kunusuru maisha yao.
  “Ukiwa kule unamuona ndani anavyozunguka,ninaomba makambi yale kama vijana tusaidieni wazee wale wasiangukiwe na nyumba zao na fanyeni taratibu yeyote mmeweka kambi mkifanya mafunzo yenu,lakini hakikisheni mnafyetua matofali na kuweka harambee kumjengea nyumba mpya na kumwambia bibi au babu ingia hapa”alisisitiza Mlata.  
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida,Dk.Denisi Nyiraha aliahidi kuunda kamati ndogondogo kuanzia ngazi ya wilaya hadi Mkoa ili kurahisisha majukumu ya mwenyekiti wa wilaya na Mkoa ikiwa ni pamoja na kuibua mipango mipya na endelevu ya kukuza na kujenga jumuiya.
  Mwenyekiti huyo alisema ili kufanikisha azma hiyo ni wajibu wa kila wilaya ianze kujiandaa kuunda kamati ya sera na mipango kwenye ngazi ya Mkoa hadi katika ngazi za wilaya na kuitaja kamati nyingine atakayounda ni kamati ya uchumi itakayokuwa na wajibu wa kwenda kubaini vyanzo vya jumuiya katika ngazi hizo.
  “Kwa hiyo kamati hii itakuwa na wigo mpana na kwa mfano nitolee majukumu ya kamati hii ya uchumi ngazi ya mkoa,tutaunda chombo kitakachokwenda kufanya auditing,kitakachoenda kufanya upembuzi yakinifu kwenye miradi yote kwenye ngazi ya Mkoa”alisisitiza Dk.Nyiraha.
  Hata hivyo Dk.Nyiraha alitumia fursa ya kikao hicho kutoa angalizo kwa kiongozi yeyote yule iwapo alishiriki kwa njia yeyote ile katika matumizi mabovu ya miradi na iwapo kuna fedha ambazo bado anazo aliagiza azirudishe bado mapema.
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wale wote waliohusika kuhujumu mali za chama,mali za umoja wa vijana wajiandae kuzirejesha maana hawatafumbiwa macho na kwamba miradi yote ya chama kuanzia ngazi ya wilaya ambayo imetaifishwa na vyombo tofauti tofauti waliombwa kuvirejesha haraka iwezekanavyo,
  Hata hivyo katika risala wa chipukizi iliyosomwa kwa Mwenyekiti huyo wa UVCCM,imeeleza changamoto zinazowakabili vijana hao kuwa ni pamoja na kutokuwa na sare za kijani na suruwali nyeusi na wanatarajia kuwa ombi lao watatekelezewa.


  0 0


  0 0

  Mkazi wa Arusha, Sagi Thomas (37) amejishindia kitita cha sh milioni 86 kwa kubashiri kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet.

  Thomas alikabidhiwa kitita chake jana na Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley. Malley alisema kuwa Thomas alifanikiwa kubashiri sahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 na kuwa mshindi wao wa droo ya 17 tokea kuanzishwa kwa mchezo wa Perfect 12. Alisema kuwa serikali imejipatia jumla ya Sh milioni 15.5 kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria.

  “Kama tulivyosema hapo awali, M-Bet ni nyumba ya washindi na leo tumedhihirisha usemi wetu ambapo Thomas anajisindia mamilion ya fedha kwa kutumia kiasi cha She elfu moja tu, hii imedhihirisha kuwa tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kucheza mchezo wetu ili kujishindia fedha,” alisema Malley.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Thomas alisema kuwa atazitumia fedha hizo kwa kuanzisha vitega uchumi na vilevile kuwaendeleza kielimu ndugu zake.

  “Nina furaha sana, mimi ni mwajiriwa wa serikali, leo hii nina faraja kubwa kuona kiasi cha Sh 1,000 tu kimeniwezesha kushinda mamilioni ya fedha, M-Bet imebadilisha maisha yangu” alisema Thomas. Meneja wa Tehama wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Kabora Mboya aliwashukuru M-Bet kwa kuendelea vyema na shughuli zake mbali ya kuwazawadia washindi mara kwa mara.
   Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (kushoto) akimkabidhi hundi mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Sagi Thomas (kulia) ambaye amejishindia kitita cha sh milioni 86. Katikati ni Meneja wa Tehama wa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Kabora Mboya.
   Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Sagi Thomas 'akipozi' na mfano wa hundi mara baada ya kukabiziwa jana. Kalinga alijishindia kitita cha sh milioni 86.

  0 0  LEO ni siku ya Uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa. Uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa Chimwaga Dodoma,  kwa ratiba itakayoanza saa 9 mchana na kuisha saa 3 usiku.. Kati ya matukio yatakayokuweko ni maandamano yatakayoshirikisha wasanii mbalimbali na pia kazi za sanaa, baada ya watu wote kufika na kutulia Chimwaga kutakuweko na wimbo maalumu wa Uzalendo, filamu ya kihistoria, hotuba za viongozi wastaafu, uzinduzi wa kitabu, na kisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania atatoa vyeti vya udhamini hatimae chakula. Wimbo hapo juu ni kazi ya wanamuziki Anania Ngoliga na John Kitime wakipiga gitaa na rimba kuisifia nchi yao,

  0 0

  Makamu wa pili wa Rais katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Iddi akipokea mfano wa hundi ya malipo yake ya bima ya maisha iliyoiva kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga. Sherehe hizo zilifanyika jana jumatano mjini Zanzibar mbele ya Baraza la Wawakilishi wakati wa mafunzo ya bima yaliyotolewa na timu ya wataalam kutoka Makao Makuu wakishirikiana na tawi la Zanzibar.Kwa kawaida bima ya maisha huiva baada ya miaka kumi. Wawakilishi Zanzibar Zuberi Ali Maulid.
  Makamu wa pili wa Rais katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Iddi kushoto akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga. kbla ya kupokea hundi ya Shilingi milioni 20 kutoka kwa Mkurugenzi huyo baada ya bima ya Maisha ya Makamo huyo wa Rais kuiva.Sherehe hizo zilifanyika jumatano wiki hii mjini Zanzibar mbele ya Baraza la Wawakilishi katikati ni Spika wa Bunge la Wawakilishi la Zanzibar Zuberi Ali Maulid 
  Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga akizungumza katika hafla hiyo

  0 0


  Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza akiongea na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la kisasa la Tigo wilayani humo.
  Baadhi ya wakazi na Biharamulo wakifuatilia uzinduzi wa Duka jipya la kisasa la Tigo
  Meneja Mauzo wa Tigo Biharamulo, Abraham Mchau akiongea na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la kisasa la Tigo wilayani humo.
  Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, ambaye ni Afisa Habari na Mawasiliano Biharamulo, Jonathan Rwekaza(kushoto), akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa la kampuni ya Tigo wilayani humo leo. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Tigo mkoani Kagera, Sadok Phares (katikati) na Meneja Mauzo wa Tigo Biharamulo, Abraham Mchau


  Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu  bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo. 
  Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu  bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo.

  Picha ya pamoja

  Biharamulo, 7 Desemba, 2017- Katika mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata huduma bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera.

  Duka hilo jipya linapatikana katika Jengo la Yusuph Katri lililopo Stendi ya Mabasi ya Biharamulo, mkabala na Kituo cha Polisi na lina uwezo wa kuwahudumia wateja zaidi ya 700,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo na viunga vyake.

  Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo jipya la Tigo, Meneja Mauzo wa Tigo - Biharamulo, Abraham Mchau alisema kuwa ufunguzi wa duka hilo jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni hiyo ya simu unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na wateja wake nchi nzima.

  ‘Tigo imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata suluhisho muafaka kwa mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Biharamulo kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa Ziwa, huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’ alisema.

  ‘Uzinduzi huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za kibunifu, zinazoendana na mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’ Mchau alifafanua.

  Kwa upande wao, wakaazi wa Biharamulo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio wa duka hilo jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa mwendo mrefu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za simu katika wilaya hiyo.

  0 0


  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira baada ya kutangaza rasmi kuhamia Chama cha Mapinduzi, katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete, mjini Dodoma Desemba 8, 2017.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Na,Joel Maduka,Geita

  Serikali Wilayani Geita imesema haitamuhurumia yeyote atakayehujumu zoezi la uandikishaji kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa.

  Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa zoezi la kuwasajili wananchi kwenye halmashauri ya mji wa Geita, Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi alisema kituo chochote ambacho zoezi hilo halitaenda vizuri, hatua zitachukuliwa dhidi ya Mwenyekiti na mtendaji wa mtaa husika.

  “Hatutakuwa na huruma na mtu yoyote ambaye hatahusika na kuhujumu zoezi hilo na kama tukisikia mwenyekiti wa mtaa na mtendaji kunatatizo ambalo limetokea tutakushughulikia hapo hapo na kama ni mwenyekiti wa mtaa sio kukushughulikia tu nitafuta nafasi yako tutachagua kiongozi mweningine hatutaki watu wasio na maadili kwenye Wilaya yetu.”Alisisitiza Kapufi.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Apolinary amewasisitiza wananchi kutumia nafasi hiyo kwa kuwa haitajirudia tena.“Ni waombe tu wananchi kwamba hii nafasi ambayo mmepewa ni nafasi ya kipekee sana haitajirudia tena kwa hiyo ni zamu ya wananchi wote kuhakikisha kwamba mnajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili muweze kupata vitambulisho vyenu”Alisema Modest.

  Mratibu wa NIDA Mkoani Geita Bw Emmanuel Ernest amesema wameanza usajili tarehe 23 August mwaka huu na kwamba wamesajili awamu 6 zenye jumla ya kata 12 na wananchi waliojiandikisha ni Laki moja, elfu 36 na 643 sawa na asilimia 75.33 na kwamba matarajio ni kuandikisha watu Laki moja elfu 81 na 374 hivyo waliobaki ni watu elfu 44 na 731.

  Akielezea faida na umuhimu wa kitambulisho cha Taifa Mratibu alisema kuwa kitasaidia serikali kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato(kodi)pamoja na kuongeza idadi ya wanaotakiwa kulipa kodi,pia vitasaidia kupunguzia serikali gharama za kusafirisha daftari la wapiga kura,na kuwa daftari lenye taarifa sahihi za watu na mahali walipo.

  Bi,Rosemary Yusuf ambaye ni mwananchi wa msalala road alisema vitambulisho vya Taifa vitawasaidia kwani watatambulika kuwa wao ni watanzania harari.
  Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,akizindua zoezi la usajili wananchi kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa , kwenye halmashauri ya Mji wa Geita ,Mratibu wa NIDA Mkoani Geita,Emmanuel Ernest akitoa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa cha usajili. 
  Mratibu wa NIDA Mkoani Geita,Emmanuel Ernest akizungumzia madhumuni ya uandikishaji wananchi kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa kwenye halmashauri ya mji wa Geita. 
  Watoto wa kituo cha Brith light wakiimba wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya wadau wakiwatunza. 
  Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi kulia ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Constatine Molandi akifuatiwa na diwani wa kata ya kalangalala,Sospeter Mahushi wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa vitambulisho. 
  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinaly akizungumza na wananchi juu ya umuhimu wa zoezi la uandikishwaji vitambulisho vya Taifa. 
  Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisisitiza viongozi wa mitaa ambao wataonekana kuhujumu zoezi la usajili wananchi kwenye vitambulisho vya Taifa watachukuliwa hatua kali. 
  Wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha wakiwa kwenye mstaari wakisubilia shughuli za kujisajili kwaajili ya kupata vitambulisho vya Taifa.


  0 0

  Afisa Vigezo wa Tigo, Abdallah Nguba (kushoto) pamoja na Meneja wa Wateja wa Tigo Mary Rutta (kati) wakifanya droo ya kuwapata washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Bahati na Sibu Tanzania, Jehud Ngolo.
  Meneja wa Wateja wa Tigo Mary Rutta (kulia) akiwatangaza washindi wa  wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael

  Mojawapo ya washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,', Saidi Khatib Kiko, mkaazi wa Kimara akionesha sura ya furaha ya ushindi wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es salaam leo. Saidi alikuwa mojawapo ya washindi 20 waliojinyakulia kati ya shilingi laki tano na shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ambapo wateja wa Tigo Pesa wana nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni 15.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akiwatangaza washindi wa  wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kulia ni Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta.
  • Wateja 20 wapokea zawadi kemkem za pesa kwa kufanya miamala kupitia Tigo Pesa

  Dar es Salaam, 8 Novemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa leo imewatangaza na kuwazawadia washindi 20 wa promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’ inayoendelea katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka mpya ambapo wateja wanajishindia mamilioni ya pesa.

  Washindi wanne (4) wamepata bahatiya kushinda zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 16 wakijaza mifuko yao na donge nono la shilingi laki tano (TZS 500,000) kila mmoja.  each. Jumla ya shilingi milioni 12 zimetolewa kama zawadi kwa wiki  hii.

  Washindi wa zawadi za TZS 1 milioni ni wafanyabiashara Neema Fredrick Mosha, Fredrick Joseli Mponzi , Sefu Athumani Sefu na Hadija Mohamed Lukulumbale ambaye ni mama nitilie.

  Washindi  wa zawadi za TZS 500,000 ni Michael Joseph Moshi, Moses Muhonga Amuli, Saidi Khatib Kiko, Sylvester Michael Madaga, Aziza Ramadhani Ngozi, Evelyne Gwamaka Mwakyembe, Tumsifu Harold Temu na Sikudhani Constantine Mwenda. Wengine walioshinda TZS 500,000 ni Queentina Msafiri Mbwambo, Hilary Andrew Massawe, Ashura Ally Salim, Halima Saidi Shaabani, Fatuma Ally Makumbo, Halima Saidi Sangiwa, Jenifer Samuel Apolinale na James John Mkanula.

  ‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii. Bado tuna zawadi za thamani ya TZS 108 milioni kutoa kwa washindi 133,’ Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta alisema wakati akikabidi zawadi kwa washindi Dar es Salaam leo.

  Alibainisha kuwa pamoja na zawadi za kila siku, promosheni hiyo ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’  itakuwa na zawadi kubwa za mwezi  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni.

  ‘Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa ambao wanahitaji kutumia huduma ya Tigo Pesa kwenye simu zao ili kupata nafasi ya kushinda. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda,’ alisema.

  Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote.  

                                                                                   

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa mkutano Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kabla ya kufungua mkutano wao wa Tisa uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
  Wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakishangilia kabla ya ufunguzi wa mkutano huo wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akivalishwa Kitambaa kichwani mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkutano wa tisa wa (UWT) uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

  Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiimba nyimbo za CCM pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wa pili kutoka (kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa pili kutoka (kulia), Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakwanza kulia mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

  Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akishangilia katika mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.


  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo mara baada ya kufungua mkutano huo wa tisa wa (UWT) mjini Dodoma.


  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wajumbe wa Mkutano wa Tisa wa UWT mjini Dodoma.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mama Maria Nyerere ambaye pia alihudhuria katika mkutano huo wa wa Tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza katika mkutano huo wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na bendi ya Tanzania One Theater TOT wakati ikitumbuiza katika mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akicheza pamoja na wajumbe wengine wa UWT mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.


  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT uliofanyika mjini Dodoma.

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano na Wafanyabiashara wa eneo la Jamatini Manispaa ya Dodoma baada ya Vibanda vyao kubomolewa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) kupisha mradi wa ujenzi wa Reli kisasa. Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Godwin Kunambi. Kushoto ni Katibu wa Wafanyabiashara hao John Banda. 
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (wa pili kushoto) akiteta jambo na wafanyabiashara wakati akitoka katika eneo la Stendi ya Jamatini Mjini Dodoma baada ya kuzungumza na wafanyabiashara waliovunjiwa vibanda vyao kupisha mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa.
  Baadhi ya wafanyabiashara wa eneo la Jamatini Manispaa ya Dodoma wakifuatilia mkutano wao na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde, Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Godwin Kunambi. PICHA NA RAMADHANI JUMA-OFISI YA MKURUGENZI

  ………..

  NA RAMADHANI JUMA.OFISI YA MKURUGENZI
  MANISPAA YA DODOMA


  HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma inatarajia kuwapatia eneo wafanyabiashara zaidi ya 550 waliovunjiwa vibanda vyao na kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) katika stendi ya mabasi madogo ya Jamatini ili kupisha utekelezaji wa mradi wa Reli ya kisasa, ili waendelee kufanya biashara zao kama kawaida.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa, Manispaa iko katika hatua za mwisho kuandaa eneo la Makole D-Center kwa kuweka miundombinu muhimu ikiwemo mfumo wa maji safi na maji taka ili wafanyabiashara hao waanze kufanya shughuli zao mara moja na katika mazingira rafiki na salama katika eneo hilo.

  Aliyasema hayo alipotembelea eneo la Jamatini na Stendi Kuu Novemba 6 mwaka huu, akiambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma, pamoja na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Jumanne Ngede kwa lengo la kuwapa pole wafanyabiashara hao na kuwajulisha hatua zilizochukuliwa na Viongozi mbalimbali katika kuhakikisha tatizo linalowakabili linapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

  Aliwatoa hofu ya kuwa eneo hilo halitakuwa na wateja wengi kama ilivyokuwa eneo la stendi ya Jamatini, ambapo aliwaambia tayari Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Daktari Binilith Mahenge ametoa maelekezo kwa Manispaa na Sumatra kuhakikisha daladala zinakuwa na ruti inayopita katika eneo hilo jipya la biashara ambapo abiria watakuwa na kituo cha kupanda na kushuka na hivyo kuongeza mzunguko wa wateja katika eneo hilo, na kwamba utekelezaji wa maelekezo hayo umeshaanza kufanyiwa kazi na Sumatra.

  Akizungumza na wafanyabiashara ya usafiri wa mabasi katika Stendi Kuu ya mabasi ya mikoani, Mkurugenzi Kunambi aliwaambia kuwa, Manispaa kwa kushauriana na uongozi wa Mkoa na wadau kama Sumatra imepanga kuhamishia Stendi hiyo katika eneo la Chaduru au kwenye eneo la viwanja vya Nanenane vilivyopo Kata ya Nzuguni barabara kuu ya Dodoma-Dar es Salaam.

  Alisema Manispaa itazungumza na uongozi wa wasafirishaji ili kupata mapendekezo yao juu ya eneo rafiki zaidi miongoni mwa maeneo hayo mawili.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri Mavunde aliwataka wote walioathiriwa na zoezi hilo la bomoabomoa wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Mamlaka na Viongozi wakifanya juhudi za makusudi kuwatafutia maeneo rafiki kwa shughuli zao huku Naibu Meya Ngede akiwahakikishia kuwa Baraza la Madiwani litasimamia kikamilifu suala la upatikaaji wa maeneo hayo.

  0 0

  Sehemu ya wahudhuriaji wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria kilichofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Dodoma tarehe 8/12/2017.IMG_1048
  Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria katika viwanja vya shule ya sekondari ya Dodoma leo .
  IMG_1084Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Mhe. Prof. Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Tanzania akiongea na wananchi kabla ya kufunga maadhimisho hayo katika viwanja vya shule ya sekondari ya Dodoma.IMG_1140Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akimshukuru Mgeni rasmi baada ya hotuba yake ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria.

older | 1 | .... | 1454 | 1455 | (Page 1456) | 1457 | 1458 | .... | 1897 | newer