Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1452 | 1453 | (Page 1454) | 1455 | 1456 | .... | 1898 | newer

  0 0  0 0

  Shirika la Kimataifa la Save the Children kwa kushirikiana na shirika la Rafiki SDO la mjini Shinyanga wamefanya mkutano wa ‘Klabu za Tuseme’ kutoka shule 8 za msingi na sekondari katika manispaa ya Shinyanga na halmashauri ya Shinyanga (Vijijini) kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya klabu hizo katika kupiga vita ukatili dhidi ya watoto.

  Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Disemba 6,2017 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha wanafunzi kutoka za shule za Ushirika, Mwasele,Solwa,Bugoyi A, Lyabusalu,Masekelo, Iselamagazi na Mwantini.
  Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children Alex Enock alisema klabu za Tuseme zimeundwa kupitia mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawala unaotekelezwa na shirika la Save the Children kwa kushirikiana na Shirika la Rafiki Social Development Organization (Rafiki SDO) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la nchini Sweeden (SIDA).
  Enock alisema lengo la klabu hizo ni kumsaidia mtoto wa kike kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kupewa ujauzito na kuepuka vishawishi mbalimbali ili aweze kumaliza masomo yake salama.
  Naye afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement alisema katika kutekeleza mradi huo wameshirikiana na idara ya elimu msingi na sekondari kuanzisha klabu za Tuseme kwa ajili ya kuhamasisha ufaulu hasa kwa watoto wa kike.
  “Wanafunzi katika klabu hizi tunawajengea uelewa juu ya masuala ya haki,wajibu na ulinzi wa mtoto pamoja kutoa mafunzo elekezi kwa viongozi na walimu walezi wa klabu hizi ili kupaza sauti kukataa ukatili dhidi ya watoto”,alisema Clement.
  Wakizungumza katika mkutano huo,wanafunzi hao walisema klabu hizo zimewasaidia kwa kiasi kikubwa kujiamini,kuepuka vishawishi mbalimbali lakini pia wamekuwa mabalozi wazuri katika kuielemisha jamii juu ya haki za watoto.
  Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika mkutano huo
  Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akizungumza wakati wa mkutano wa klabu za tuseme katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga leo- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akizungumza ukumbini
  Afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement akizungumza katika mkutano huo wa klabu za tuseme
  Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ushirika akielezea namna klabu za tuseme zinavyosaidia katika kupigania haki za watoto.
  Mmoja wa wanafunzi hao akielezea kazi za klabu za tuseme.
  Wanafunzi wakielezea kuhusu klabu ya tuseme katika shule ya sekondari Mwantini.
  Mwanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A akielezea shughuli wanazofanya katika klabu yao ya tuseme
  Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiwasilisha mada kuhusu ukatili dhidi ya watoto
  Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiendelea kuwasilisha mada ukumbini
  Walimu walezi wa wanafunzi klabu za tuseme wakiwa ukumbini
  Wanafunzi wakifanya kazi ya vikundi wakati wa mkutano huo
  Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiangalia wanafunzi wakifanya kazi ya kikundi chao
  Afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement akiangalia wanafunzi wakifanya kazi ya kikundi
  Walimu walezi nao walikuwa na kazi kwenye kundi lao. Kulia ni Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiwa katika kundi la walimu walezi wa wanafunzi
  Washiriki katika mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja
  Picha ya pamoja washiriki wa mkutano huo.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  --
  Mwanaharakati wa Haki za Watoto nchini na Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative , Rebeca Gyumi  akizungumza na Wahariri na Waandishi waandamizi wa Vyombo mbalimbali vya Habari haki za Mtoto na   vita dhidi ya Ndoa za Utotoni zinazoendelea nchini
   Mtaalamu wa kupigania Haki za Watoto kutoka Taasisi ya Save The Children, Neema Bwaira akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo Mbalimbali vya Habari hapa nchini wakati wa Semina juu ya haki za Mtoto Jijini Dar es Salaam
   Mtaalamu wa Masuala ya Haki za Watoto kutoka nchini Thailand anayefanya kazi na Taasisi ya Save The Children nchini, Yui Mutomol  akitoa Elimu kwa Waandishi wa Habari waandamizi na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari Jijini Dar es Salaam
   Sehemu ya Waandishi Waandamizi na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa Makini wakati wa semina ju ya haki za Mtoto iliyoandaliwa na Taisisi ya Save The Children Jijini Dar es Salaam

  Sehemu ya Waandishi Waandamizi  na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya habari waliohudhuria  Semina juu ya haki za mtoto iliyoandaliwa na Tasisi ya Save The Children nchini

  0 0  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Edward Lyimo (wa tatu kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya tiba ya uzazi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa ajili ya Zahanati ya Msongola nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo. Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 7 vitasaidia kupunguza mahitaji ya vifaa tiba kwa wodi ya wazazi ya zahanati hiyo inayohudumia wanawake wazazi Zaidi ya 50 kwa mwezi. Pamoja nao (kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Huduma za matawi na Masoko, Theresia Soka, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Chacha Mwita, Mkurugenzi wa hazina Bahati Minja, Mkurugenzi wa mikopo, Adolphina William na maafisa  wengine wa benki na hospitali hiyo. (Picha na Robert Okanda Blogs)  


   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Edward Lyimo (wa pili kushoto) akimpatia maelezo mafupi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhusu sehemu ya vifaa vya tiba ya uzazi benki hiyo ilivyotoa kwa ajili ya Zahanati ya Msongola nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo kabla ya makabidhiano. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Dkt Mwanahawa Malika. 

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiongea na wana habari wakati wa hafla hiyo ya kupokea msaada wa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 7 vitakavyosaidia kupunguza mahitaji ya vifaa tiba kwa wodi ya wazazi ya zahanati hiyo inayohudumia wanawake wazazi Zaidi ya 50 kwa mwezi. 

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Edward Lyimo (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla hiyo.

  0 0  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mhe. CAO Weizhou alipofika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Tanzania hususan katika sekta ya ujenzi wa miundombinu.
  Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou wakifuatilia mazungumzo. Wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke.
  Sehemu nyingine ya Ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou.
  Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Bi. Justa Nyange, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia,  Bw. Charles Faini, Katibu wa Naibu Waziri,  na Bw. Halmesh Lunyumbu, Afisa  Mambo ya Nje 
  Mhe. Dkt. Kolimba akiagana na Mhe. CAO mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
  Picha ya pamoja


  0 0

  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Victor Kategere (Kushoto) akimtambulisha rasmi  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Doroth Mwanyika kwenye kikao cha watumishi  wa wizara hiyo kilichofanyika Dar es Salaam. Bibi Mwanyika aliteuliwa kuongoza wizara hiyo mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.02
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Doroth Mwanyika akizungumza na watumishi wa wizara anayoiongoza (hawaonekani pichani) katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Bibi Mwanyika aliwakumbusha  watumishi hao kuzingatia uadilifu na kushirikiana miongoni mwao wakati wanapotekeleza wajibu wao wa kutoa huduma za sekta ya ardhi kwa wananchi.
  04
  Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Doroth Mwanyika (hayupo pichani) wakati alipokutana nao ili kujitambulisha rasmi na kusikiliza maoni yao  yaliyolenga kuimarisha  huduma za sekta ya ardhi nchini.
  05
  Bw. Ramadhani Mtawa mmoja wa watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  (aliyesimama) akichangia hoja ya uboreshaji wa utoaji huduma za sekta ya ardhi wakati wa kikao na Katibu Mkuu Bibi Doroth Mwanyika.Picha na Rehema Isango & Simon Kyando,  Wizara  ya Ardhi

  0 0
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb), kulia, akijadiliana masuala ya kiutumishi na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Mhe. Wang Ke (katikati) mapema leo.

  0 0

  Mgeni rasmi, Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mheshimiwa kemboi Cheboi (kushoto) akisalimiana na wachezaji wa mpira wa wavu wa timu ya Tanzania, kabla ya kuanza kwa mashindano ya mchezo huo kati ya Timu ya Tanzania na Uganda uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo ni ya Nane ya Mabunge ya nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki yalioanza tarehe 1 Desemba na kumalizika tarehe 11 Desemba, 2017IMGL7524
  Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu wa Tanzania akiifungia timu yake goli katika mpambano kati ya Tanzania na Uganda, mchezo uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Tanzania iliibuka na ushindi wa seti 3 – 0 dhidi ya Uganda
  IMGL7563
  Mashabiki wa timu ya Tanzania wakishangilia ushindi dhidi ya timu ya Uganda baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa mpira wa wavu uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  IMGL7478
  Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijiandaa kwa mchezo wa mpira wa wavu dhidi ya timu ya Uganda uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  IMGL7430
  Wachezaji wa timu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wa mpira wa wavu uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke, wakati balozi huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania. Katikati ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin.
  PIX 2
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke, wakati balozi huyo alipokua anafafanua jambo katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika ofisi ya Naibu Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walikubaliana kuendeleza ushirikiano zaidi kati ya China na Tanzania. Katikati ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin.
  PIX 3
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke (katikati), wakati balozi huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania. Kushoto ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin.
  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Chamwino wakati alipotembelea kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo.2
  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino  Mh. Vumilia Nyamonga akiongea na wananchi wake (hawapo kwenye picha) juu ya Usafi wa mazingira na matumizi ya choo, katika ziara ya Waziri wa Afya katika Wilaya hiyo mjini Dodoma.
  3
  Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino Athumani Masasi akijibu hoja ya mwananchi wa Kijiji cha Humekwa mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu  kuhusu upatikanaji wa kadi za matibabu ya wazee wilayani hapo.
  4
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Elizabeth Arthur wakati alipotembelea kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo.
  5
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino Athumani Masasi wakati wa ziara ya kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo, wa katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino  Mh. Vumilia Nyamonga.
  6
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongea na mkazi wa Kijiji cha Humekwa Wilaya ya Chamwino Bi Cesilliah Isaya aliyefanikiwa kujenga choo chenye ubora kwa gharama ndogo ya shiringi 55,000 tu.
  7
  Kikundi cha ngoma kutoka Kijiji cha Humekwa kikitoa Burudani mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
  8
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Wakazi wa Kijiji cha Humekwa waliojumuika katika kuunga mkono ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) ili kujionea Usafi wa mazingira na matumizi ya Choo katika Wilaya hiyo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
  ……………
  NA WAMJW-DODOMA
  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kuhakikisha kuwa kila Kituo cha Afya au Zahanati yoyote inaongozwa na kusimamiwa na mganga na sio mhudumu wa afya au nesi kama inavyofanyika kwenye baadhi ya vituo vya afya .
  Hayo yamesemwa na Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira  leo Mkoani Dodoma Wilaya ya Chamwino kata ya aneti Kijiji cha humekwa  kuelekea uzinduzi  wa awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iliyobeba ujumbe wa nipo tayari  ambapo Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi.
  “Hatua ya kuimarisha  upatikanaji wa dawa, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba hususani vya dharura na upasuaji sanjari na kuweka mazingira safi ya upatikanaji wa maji na vyoo safi na salama ili kupunguza magonjwa na vifo vitokanavyo na kutokuwepo kwa huduma bora za  maji na afya kwa wakati ndiyo lengo letu” alisema Waziri Ummy.
   Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kabla ya Serikali ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli haijaingia madarakani bajeti ya dawa ya wilaya ya chamwino ilikuwa milioni 113 lakini mwaka jana bajeti ya dawa  ilikuwa milioni 436 ambapo katika mwaka wa pili wametengewa milioni 505 hali inayoonesha jitihada za dhati za serikali ya awamu ya tano kuboresha hali ya  afya ya wananchi hususani waliokuwa Vijijini.
  Mbali na hayo Waziri Ummy amewataka wananchi wa kijiji cha Humekwa kukata kadi ya matibabu za CHF kwani zinarahisha upatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi na kupunguza gharama .
  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wananchi ambao wana ugonjwa kifua kikuu hawana  budi kuwahi hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kupata dawa ili kuokoa maisha yao kwani dawa hizo hazilipiwi gharama yoyote.
  Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Aneti  Peter Chidawali ameiomba Serikali kuwasaidia Wananchi wa Humekwa katika hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa jengo la upasuaji ambalo wananchi wanajitolea michango yao kujenga ili likamilike kwa matumizi yaliyokusudiwa.
  Kwa upande wake Msomarisala wa Kijiji cha Homekwe Evaline Gidore amebainisha kuwa kampeni ya usafi wa mazingira na ujenzi  wa vyoo bora imeasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa walioathiriwa na magonjwa  yatokanayo na uchafuzi wa mazingira .
  “Kampeni hii imechangia kuepuka magonjwa hatari kama vile kuhara damu, typhoid na minyoo kutoka wagonjwa138 mwezi  disemba 2015 hadi kufikia wagonjwa 26 Novemba Mwaka huu kwa vile tumejitahidi kuzingatia usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora”Alisema Bi Eveline.


  0 0


  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiangalia maboksi ya samaki aina ya Migebuka yenye kilo 240 yaliyokamatwa katika kituo kikuu cha basi cha mjini Kagera hapo jana.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akitoa tamko la kumsimamisha kazi mara moja Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Ayoub Ngoma kwa tuhuma za kushiriki katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= hapo jana.
  . Moja ya boti inayotumika kwenye doria katika ziwa Viktoria na Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera.

  ……………………………………………………………………………………..

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yohana Budeba kumsimamisha kazi mara moja Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Ayoub Ngoma kwa tuhuma za kushiriki katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= hapo jana.

  Akizungumza katika ofisi ya Kitengo hicho iliyopo mjini Kagera, Mpina alisema mnamo tarehe 03/12/2017 majira ya Saa 03:00 asubuhi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ilikamata gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter likiwa limepakia samaki zenye uzito wa kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato kwenye mpaka wa Murusagamba wilayani Ngara.

  “Katika kipindi cha uongozi wangu, tayari nimesha waagiza Makatibu Wakuu waliopo katika Wizara yangu kutembea na barua zilizozosainiwa za kusimamisha kazi watumishi wote wanaohujumu jitihada za Serikali ibaki kujaza jina tu. Kwa sasa hatuna hata nusu dakika ya uvumilivu kwa watu kama hawa, tutawaondoa mara moja.” Alisisitiza Mpina

  Aidha, Waziri alisema Afisa huyo na Dereva wa gari hilo bwana Ayuob Sanga wanashikiliwa na polisi kwa hatua za kisheria kwa kuhusika na tukio hilo, na kuongeza kwamba samaki hawa walikuwa wakitoroshwa kwenda nje ya nchi bila ya kufuata Sheria ya Uvuvi Na 22 ya 2003 na taratibu mbalimbali za usafirishaji wa samaki na mazao yake nje ya nchi.

  Afisa Mfawidhi wa Kanda wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Gabrieli Mageni alimweleza Waziri Mpina baadhi ya taratibu zilizokiukwa kuwa ni pamoja na samaki hao kutopaswa kuvuliwa kwa kuwa walikuwa wakubwa zaidi ya sentimeta 85 na wadogo chini ya sentimeta 50, msafirishaji kutokuwa na kibali cha kusafirisha mazao ya uvuvi, kutolipia ushuru na mrabaha wa Serikali, kutokuwa na cheti cha afya pamoja na leseni ya kuuza mazao ya uvuvi nje ya nchi.

  Waziri Mpina alisema samaki hao walitaifishwa na kugawanywa kwa wananchi wa Murusagamba, Kiteule cha Jeshi la Wananchi la Tanzania Murusagamba, Kituo cha Polisi Murusagamba pamoja na Shule ya Sekondari Murusagamba baada ya kupata kibali cha Mahakama.

  Alisema kazi hiyo ilifanyika chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngara. Luteni kanali,Michael Mtenjele. Aliongeza kuwa, uchunguzi wa awali ilibaini kuwa samaki hao walitokea kwenye kijiji cha Izigo wilayani Muleba.

  Ametaja baadhi ya matukio yaliyotokea hivi karibuni kuwa ni pamoja na kukamatwa kwa furu kilo 9100 zilizokuwa zinatoroshwa kwenda nchini Uganda ambapo zilitaifishwa na kuuzwa kwa amri ya mahakama na watuhumiwa wawili kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo.

  Kukamatwa kwa uduvi kilo 5000 ambazo zililipiwa mrabaha na mtuhumiwa kulipa faini ya shilingi 100,000/=,kukamatwa kwa mafurushi 6 ya Samaki aina ya Migebuka yenye kilo 240 katika kituo cha Basi cha Bukoba zilizokuwa zikitoka mkoani Kigoma kwenda Uganda ambapo mtuhumiwa alikimbia na samaki hao kutaifishwa.

  Katika tukio jingine jumla ya kilo 100 za mabondo mabichi ya samaki yamekamatwa kwenye doria mpakani Mtukula na mtuhumiwa amefikishwa polisi kwa hatua za kisheria.

  Waziri Mpina amewaomba wavuvi kuzingatia Sheria na taratibu mbalimbali za uvuvi nchini ili sekta hiyo iwe na tija na kuchangia katika uchumi wa kati wa viwanda ifikapo 2025.

  Wakichangia kwa nyakati tofauti watumishi wa kituo hicho waliiomba Serikali kupitia kwa Waziri Mpina kuangalia namna ya kuongeza nguvu kazi na vitendea kazi mbalimbali vitakavyosaidia kudhibiti uvuvi haramu.

  Nahodha Mkuu wa kituo hicho, bwana Ernest Maguzu alisema kazi ya doria katika ziwa Viktoria imekuwa ngumu kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia ya mawasiliano kwa kuwa wavuvi wamekuwa wakiwasiliana mara moja kutumia simu za mikononi pindi wanapoziona boti za doria zinaingia ziwani na kufanikiwa kukimbia.

  Naye Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kitengo cha Udhibiti wa Ubora na Masoko bi, Theresia Temu aliiomba kuongeza udhibiti wa usafirishaji wa bidaa zitokanazo na mazao ya uvuvi nje ya nchi kwa kuwa hivi sasa Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kutokana na wafanyabiashara kutorosha mazao hayo mipakani bila kulipa ushuru.

  Bi Temu alisema kuwa inakadiriwa kuwa zaidi ya tani mia moja ya mazao ya uvuvi yanatoroshwa kila mwezi katika mipaka ya nchi jirani hivyo jitihada za pamoja baina ya wadau mbalimbali zinahitajika ili kupambana na tatizo hili

  “Mheshimiwa Waziri hili ni tatizo kubwa tunaomba Serikali kuliangalia kwa jicho la tatu namna nyingine tutaendelea kuibiwa” alisisitiza bi Temu

  Waziri Mpina alisema Halimashauri zote nchini zinatakiwa kushiriki kikamilifu katika kulinza raslimali za majini na baharini kwa kuwa licha ya raslimali hizo kutoa mchango mkubwa wa uchumi kwa taifa pia manufaa yake ni kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

  “Nataka suala la uvuvi wa mabomu na nyavu za kukokota liwe historia katika nchi yetu. Tutaendelea kuchukua hatua kali kwa yeyote atakaje tuhujumu” alisisitiza Mpina

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akikabidhiwa kitabu cha picha na historia ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli alipotembelewa na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisalimiana na Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (wa pili kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika mazungumzo na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akipitia kitabu cha picha na historia ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea mara baada ya kukabidhiwa.Wanafunzi wa chuo wakiwa kwenye mdahalo na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.

  KAMATI maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina imekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa mazungumzo maalum walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Waziri Dk. Mwakyembe, Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck alisema michezo inaumuhimu mkubwa kwa jamii kwani ni kiungo kinachotumika kujenga mshikamano na kudumisha amani kwa mataifa mbalimbali na jamii kwa ujumla.

  Aliwahimiza wanahabari nchini kuendelea kuandika habari za Palestina kiusahihi ili kuielimisha jamii juu ya suala hilo na pia kupaza sauti na hatimaye suluhu kupatikana eneo hilo, aliwataka vijana kupenda kusoma historia za maeneo anuai ikiwemo mvutano kati ya Palestina na Israeli kwa ajili ya kujijengea uelewa wa mambo duniani.

  Kwa upande wake Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour akizungumza na waziri alitoa ombi la mechi ya kirafiki kimataifa kati ya Tanzania na Palestina kudumisha zaidi uhusiano uliopo pande mbili. Kamati hiyo ilipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu katika mdahalo, asasi za kiraia na Jukwaa la Wahariri.

  Hata hivyo baada ya ziara hiyo na kumtembelea Waziri Dk. Mwakyembe kamati hiyo ilihudhuria maadhimisho ya Siku ya kutetea haki za watu wa Parestina yalioandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).  KAMATI maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina imekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa mazungumzo maalum walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Waziri Dk. Mwakyembe, Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck alisema michezo inaumuhimu mkubwa kwa jamii kwani ni kiungo kinachotumika kujenga mshikamano na kudumisha amani kwa mataifa mbalimbali na jamii kwa ujumla.

  Aliwahimiza wanahabari nchini kuendelea kuandika habari za Palestina kiusahihi ili kuielimisha jamii juu ya suala hilo na pia kupaza sauti na hatimaye suluhu kupatikana eneo hilo, aliwataka vijana kupenda kusoma historia za maeneo anuai ikiwemo mvutano kati ya Palestina na Israeli kwa ajili ya kujijengea uelewa wa mambo duniani.

  Kwa upande wake

  Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour akizungumza na waziri alitoa ombi la mechi ya kirafiki kimataifa kati ya Tanzania na Palestina kudumisha zaidi uhusiano uliopo pande mbili. Kamati hiyo ilipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu katika mdahalo, asasi za kiraia na Jukwaa la Wahariri.

  Hata hivyo baada ya ziara hiyo na kumtembelea Waziri Dk. Mwakyembe kamati hiyo ilihudhuria maadhimisho ya Siku ya kutetea haki za watu wa Parestina yalioandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo amesema hatawavumilia wakurugenzi na wenyeviti wa kamati za fedha ambao hawatatoa fedha za maendeleo zinazotokana na mapato ya ndani ya halmashauri kulingana na bajeti zao.

  Alitoa onyo hilo wakati akifungua kongamano la siku mbili la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

  Jafo alisema wakurugenzi na wenyeviti hao wataondolewa katika nafasi zao endapo watashindwa kutoa fedha hizo ikiwa ni pamoja na asilimia tano za mapato ya ndani kwa vikundi vya vijana na wanawake.

  “Wakarugenzi watakaoshindwa kutoa fedha katika mapato yao ya ndani hawatatosha katika kipindi cha utawala huu, umeipanga katika bajeti , umekusanya halafu vijana na akina mama hujawapelekea asilimia tano za mapato ya ndani, basi mkurugenzi utakuwa hutoshi”

  Jafo pia alitaka Bodi za mikopo katika kila halmashauri kuhakikisha wanatoa mikopo kwa kulenga viwanda ili kusukuma agenda ya uchumi wa kati.Aidha, Jafo aliiomba taasisi ya WAJIBU kuja na kongamano la mafunzo kwa madiwani na kamati za fedha kote nchini kupewa mafunzo kama hayo ili isaidie kusukuma agenda ya viwanda.

  “Madiwani wengi bado wanachangamoto kubwa, mkiwaelemisha madiwani na kamati za fedha itasaidia agenda hii ya viwanda, tutapata watu ambao wanawajibika na wanafanya kile wanachokielewa, ninyi WAJIBU ni wabobezi kwenye usimamizi wa fedha.”

  Alisema agenda ya serikali ya Tanzania ya viwanda imetokana na mtazamo wa wananchi wa kutaka mabadiliko na kuwa rais John Magufuli ametafsiri ili kufikia agenda hiyo ni kwa viongozi kufanya uthubutu wa kuamuani na kuongeza kuwa tayari serikali inaendesha miradi mikubwa mitatu ya kuboresha miundombinu ili kuwafikia hata walioko vijijini.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh alisema Mamlaka za serikali za mitaa ni muhimu katika kaendeleo na na pia zina nafasikubwa kusukuma mebele agenda ya uchumi wa kati kupitia viwanda.

  “ Naamini kama viongozi wataacha kufanya kazi kwa mazoea na kufuata kasi ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli basi viongozi wataweza kusaidia maendeleo na kuacha alama,”Aidha, Utouh alisema taasisi yake iko mbioni kuandaa mfumo ambao utasaidia kufanya tathimini ya kisayansi ya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa serikali za mitaa.
   .WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo akizungumza katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda lililofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mtenda wa Wajibu, Lodovick Utouh akizungumza juu madhumuni ya mkutano huo kwa wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi juu ya upangaji mikakati ya kuhudumia wananchi katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
   Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Wajibu, Yona Kilaghane akizungumza juu maazimizio na utekelezaji wa wajibu maombi ya WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu, Hadson Kamoga akizungumza na waandishi wa habari juu utekelezaji wa maazimio yatakayotokana na kongamano hilo katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
   Sehemu wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi
  picha ya pamoja ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo pamoja Wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi  0 0

  Kaimu Mkurugenzi usalama wa chakula makao makuu ya TFDA Bw Lazaro Mwambole akiendelea kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa kusindika chakula Mkoani Geita. 
  Baadhi ya wafanyabiashara wadogo ambao wanashughulika na usindikaji wa vyakula wakifuatilia mafunzo kwa umakini. 
  Baadhi ya wafanyabiashara wadogo ambao wanashughulika na usindikaji wa vyakula wakifuatilia mafunzo kwa umakini. 
  Kaimu Mkurugenzi usalama wa chakula makao makuu ya TFDA Bw Lazaro Mwambole akielezea dhumuni na malengo ya mafunzo hayo wakati alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi. 
  Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa idara ya uchumi na uzalishaji,Bw Emily Kasaga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wafanyabiashara wa kusindika vyakula kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya mji wa Geita. 
  Baadhi ya washiriki mkoani Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasimi na watumishi wa SIDO na TFDA.

  Na,Joel Maduka,Geita.

  Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA imewakutanisha wajasiriamali wanaosindika chakula mkoani Geita na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kutengeneza vyakula vinavyokidhi viwango vya usalama na vitakavyoweza kukuza soko la ndani na nje.

  Akizungumza kwenye mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa usalama wa chakula makao makuu ya TFDA Bw Lazaro Mwambole alisema tafiti walizofanya zimebaini kuwa wengi wenye viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazotengeneza na hawajui kanuni za usindikizaji.

  “Mgeni Rasmi taifiti ambazo zilifanyika mwaka 2016 zilionekana kuwa wamiliki wengi wa viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazozitengeneza hali ambayo imesababisha kutokufanya kwa ubora zaidi usindikaji wao”Alisema Mwambole.

  Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita Bw Emily Kasaga amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha wanarutubisha vyakula ili view salama na vyenye ubora kwa kuwa afya ya watumiaji iko mikononi mwao.Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Bi Fatma Hassan na Bw Edward Geni wamesema mafunzo hayo yamewafungulia mwanga zaidi kwa kuwa wengi walikuwa wakifanya kazi hizo bila kujua kamawanakosea.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mhe. CAO Weizhou alipofika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Tanzania hususan katika sekta ya ujenzi wa miundombinu. 
  Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou wakifuatilia mazungumzo. Wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke. 
  Sehemu nyingine ya Ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou. 
  Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Bi. Justa Nyange, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Charles Faini, Katibu wa Naibu Waziri, na Bw. Halmesh Lunyumbu, Afisa Mambo ya Nje 
  Mhe. Dkt. Kolimba akiagana na Mhe. CAO mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 
  Picha ya pamoja

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  WAKULIMA wa Sikimu ya Umwagiliaji ya Mpunga Katika vijiji vya Katengera na Ruhiti Wilayani Kakonko, wametakiwa kuongeza ufanisi kwa zao la Mpunga ilikuzalisha mazao ya kutosha kutokana na zao hilo kuwa zao la biashara kwa Wilaya hiyo na serikali kwa kushirikiana na wawekezaji wamewekeza fedha nyingi ilikuinua uchumi wa Wananchi hao.

  Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, wakati akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.

  Mkuu huyo aliwaagiza wakulima hao kuongeza uzalishaji kutokana na serikali kwa kushirikiana na Wafadhiri wametatua changamoto ya vifaa vya kupalilia vilivyo kuwa vikisababisha kupata mazao machache na kuwataka kulima misimu miwili na kila hekali moja kuzalisha gunia 40 hadi 45 tofauti na kipindi ambacho walikuwa hawana nyenzo hizo.

  " niwaombe wakulima wote kulima marambili katika sikimu hii sikimu hii ni ya umwagiliaji kwahiyo maana ya kumwagilia lazima mlime na kiangazi, serikali imeweka fedha nyingi sana katika sikimu hii lazima mjitahidi kuzalisha ilituweze kupata viwanda vya kukoboa mpunga na kuinua uchumi wa wanakakonko kwa yeyote atakae shindwa kulima marambili tutachukua shamba lake na tuwagawie wawekezaji iliwaweze kuwekeza zaidi na kupata mazao ya kutosha", alisema Ndagala.

  Hata hivyo Ndagala aliwaagiza Wakulima hao kuzingatia maelekezo ya mabwana shamba katika uwekaji wa mbolea, pamoja na kuzingatia Muda wa kupalilia ilimuweza kuongeza uzalishaji na kupata mazao yenye ubora.

  Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Wafadhiri Mkurugenzi wa Shirika la RERAI shirika linalo shughulika na ongezeko la uzalishaji katika kilimo cha mazao mbali mbali Dr Brigton Gwamagobe, alisema Waliona Wakulima hao wanaahangaika katika upaliliaji na kuomba wafadhiri kuwasaidia kuwapa vifaa na kutoa vifaa 50 vyenye thamani ya milioni kumi na mbili vitakavyo gawiwa katika sikimu ya Katengera na Ruhiti.

  Alisema kabla ya vifaa hivyo kutolewa katika vikundi vya upaliliaji hekali moja ilikuwa ikipaliliwa kwa siku moja bei ya kupaliliwa ilikuwa 13,5000 kwa hekali na sasa itakuwa ni hekali 50000 uzalishaji utaongezeka kutokana na wakulima wengi walikuwa wanashindwa kupata mavuno ya kutosha kutokana na kutopalilia kwa wakati na kutumia kemikali kuuwa wadudu lakini kifaa hicho kitumika kuuuwa wadudu pamoja na gharama nafuu za upaliliaji.

  Kwa upande wake Katibu wa Kikundi cha upaliliaji Yasinta Mathiasi aliishukuru serikali pamoja na Wawekezaji kwa kuja kuwekeza katika sikimu hiyo na vifaa hivyo vitawasaidia kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuepukana na adha ya kuumwa na wadudu waliokuwa wakikaa kwenye maji ya mpunga pamoja na kukatwa na majani.

  Alisema kwasasa uzalishaji utaongezeka kutokana na zao hilo likipaliliwa mapema linaongeza uzalishaji kutokana na kupata nafasi ya kukua vizuri na kuepukana na majani yanayozuaia zao hilo kukua kwa Wakati.
   Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akishiriki kupalilia zao la Mpunga katika shamba la WAKULIMA wa Sikimu ya Umwagiliaji ya Mpunga Katika vijiji vya Katengera na Ruhiti Wilayani Kakonko
    Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, ambae pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma,Abdallah Burembo amewaagiza Viongozi wapya wa Chama hicho Mkoani Kigoma kuhakikisha Wanayarudisha majimbo ya Kigoma mjini na Kakonko na kata zote zilizochukuliwa na upinzani .

  Aidha amewataka kufanya kazi ya chama ya kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwatuma kazi Viongozi wa serikali, na kuwakagua kama Wanatekeleza pamoja na kuwaacha Wabunge kufanya wajibu wao na kuacha Makundi makundi katika siasa kwa kuwaweka Wana CCM pamoja ilikuhakikisha ushindi wa majimbo yote kigoma .

  Wito huo ameutoa  jana, baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Mkoa katika Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Kumchagua Mwenyekiti wa Mkoa , Mjumbe wa baraza kuu taifa NEC na wajumbe wa halmashauri kuu ya Mkoa, ambapo Burembo aliwapa pole viongozi hao waliochaguliwa kwakuwa Wanakazi kubwa ya kuhakikisha Majimbo yanayotawaliwa na chama tawala yaendelea kuwepo na kuyarudisha yale yote yaliyo chini ya upinzani pamoja na kata zote.

  Hata hivyo katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa ilichukuliwa na Amandusi Nzamba aliewashinda wenzake watano kwa kura 371 akifatiwa na Hamis Betese kura 249 akifuata aliekuwa mwenyekiti wa zamani Amani Kabour 97, Philipo Tabhiliho kura mbili na Antony Mpozemenya tisa,pamoja na nafasi ya Mjumbe wa baraza kuu taifa ilichukuliwa na Kilumbe Ngenda alie shinda kwa kura 426 kati ya Wagombea wenzake Asha Baraka na Atanasi dyoya.

  "Tutawapima viongozi mliochaguliwa pamoja na viongozi wa serikali kutokana na ushindi tutakao upata hatuwezi kishindwa katika uchaguzi wakati Dc upo Mkurugenzi Upo na Mkuu wa Mkoa upo, serikali ni ya chama cha mapinduzi waliopo chini ya serikali wanaitumikoa serikali na kutekeleza ilani yetu kama kuna mtendaji au mkurugenzi hafuati utekelezaji wa ilani tutawatoa tuambieni wanao sababisha sisi tushindwe kuaminika hatuwezi kukubari tuyakose majimbo haya tunayataka kwa gharama yoyote ile", alisema Mwenyekiti wa jumuia ya Wazazi.

  Alisema WanaCCM jimbo la kigoma mjini wanaiua CCM kutokana na undugu wao, kwenye kushika dora hakuna undugu hawezi kuhama mtu jimbo lilikuwa la CCM alafu wanagawa jimbo kwa upinzani, hili ndio kioo cha Kigoma kuna miradi mingi inatekelezwa ni kwa ilani ya chama cha mapinduzi miradi ya maji,viwanja vya ndege kigoma mjini mnatakiwa kuomba toba maana ni aibu vitu haiwezekani serikali iwaamini alafu Wanachama wawasaliti .

  Nae Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Kigoma Amani Kabour alisema Ccm inamafanikio Makubwa kwa Mkoa wa Kigoma wanazungumza wakati akiachia madaraka wakiwa na mawaziri watatu na naibu waziri wa kigoma CCM ni chama cha mfano tofauti na kipindi cha nyuma na kigoma imekuwa ni Mkoa waliochagua wabunge wawili na wengi ni wapya pamoja na wabunge sita wa kuchaguliwa na Wawili viti maalumu hivyo viongozi waliochaguliwa kihakikisha majimbo yaliyo chini ya upinzani wanayarudisha.

  Aidha aliwaomba viongozi waliochaguliwa kuhakikisha Wanapambana na ufisadi ,uzembe pamoja na kukemea rushwa ilikuhakikisha mkoa wa kigoma unasonga mbele na kuondokana na dhana ya kwamba mkoa huo ni mkoa wa mwisho kwa umasikini ilikuhakikisha Wananchi wanakiamini chama na kuendelea kutoa ushirikiano.

  wako tayari kufanya uchaguzi waweze kupata viongozi watakao saidia kuipelwka CCm mbele kuhakikisha CCM ni chamaa kinachotawala Mkoa wa Kigoma na kuo mkoa wa maendelea ubadhilifu na ufisadi na ujambazi kuwaomba kama viongozi wakui kusimamia na kuhakikisha Mkoa unaondokana na rushwa na ufisadi katika

  0 0

  Wito umetolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na kwa wapenzi wa Golf nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano maalumu ya Golf yatakayo fanyika katika viwanja vya Lugalo Jijini Dar es salaam Wito huo umetolewa na Bwana William Msheli Mkurugenzi wa kampuni ya WIHAB GROUP kwa kushirikiana na EAG GROUP ambao ndio waandaaji wakuu wa Tamasha hilo la Uhuru Cup Open linalotarajiwa kufanyika tarehem 10/12/2017 siku ya jumapili katika viwanja vya Lugalo Jijini Dar es salaam

  Msheli akizungumza na waandishi wa habari mapema katika uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika katika viwanja hivyo ambapo amewataka wachezaji wa Golf Nchini kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya siku moja yenye lengo la kuenzi Uhuru wetu wa watanzania kutoka kwa wakoloniNia ya kuita mashindano haya Uhuru Cup ni kutaka kuenzi uhuru wetu kama watanzania ambao tulipa kutoka kwa wakoloni na ndio maana pia tukaamua kuyaweka siku moja baada ya sikukuu za Uhuru yaani tarehe tisa Desemba ili watanzania tukutane kwa pamoja kusheherekea sikukuu hiyo ya Uhuru wetu kwa kucheza na kutazama mashindano haya” Msheli
  Kwa upande wa Nahodha wa Mchezo huo Japhet Masai alisema mashindano hayo yamejumuisha wachezaji wa kila rika na yamegawanyika katika vipengele vitano ambavyo yaani, Seniors, Ladies, Juniors,Cadies na Division Competition,
  Masai aliongeza kuwa mchezo huu haulengi wakazi wa Dar es salaam pekee bali ni kwa mtanzania yeyote anayetaka kushiriki anaweza kujiandikisha na kupewa nafasi hiyo

  Katika kuongeza chachu na hamasa kwa washindi, waandaaji wa mchezo huo wameandaa zawadi kwa washindi ikiwemo Baiskel, Simu za mkononi, Tv nk, ambazo zitatolewa kwa wachezaji watakaoibuka washindi kitika kila kipengeleMsheli aliongeza kuwa mashindano hayo hayataishia hapo tu bali yatakuwa endelevu kwa kila mwaka ili kuweza kuongeza hamasa kwa wachezaji wa mchezo huo .

  Wito umetolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na kwa wapenzi wa Golf nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano maalumu ya Golf yatakayo fanyika katika viwanja vya Lugalo Jijini Dar es salaam Wito huo umetolewa na Bwana William Msheli Mkurugenzi wa kampuni ya WIHAB GROUP kwa kushirikiana na EAG GROUP ambao ndio waandaaji wakuu wa Tamasha hilo la Uhuru Cup Open linalotarajiwa kufanyika tarehem 10/12/2017 siku ya jumapili katika viwanja vya Lugalo Jijini Dar es salaam Msheli alizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika katika viwanja hivyo ambapo amewataka wachezaji wa Golf Nchini kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya siku moja yenye lengo la kuenzi Uhuru wetu wa watanzania kutoka kwa wakolon.
   
  Nia ya kuita mashindano haya Uhuru Cup ni kutaka kuenzi uhuru wetu kama watanzania ambao tulipa kutoka kwa wakoloni na ndio maana pia tukaamua kuyaweka siku moja baada ya sikukuu za Uhuru yaani tarehe tisa Desemba ili watanzania tukutane kwa pamoja kusheherekea sikukuu hiyo ya Uhuru wetu kwa kucheza na kutazama mashindano haya” MsheliKwa upande wa Nahodha wa Mchezo huo Japhet Masai alisema mashindano hayo yamejumuisha wachezaji wa kila rika na yamegawanyika katika vipengele vitano ambavyo yaani, Seniors, Ladies, Juniors,Cadies na Division Competition,
   
  Masai aliongeza kuwa mchezo huu haulengi wakazi wa Dar es salaam pekee bali ni kwa mtanzania yeyote anayetaka kushiriki anaweza kujiandikisha na kupewa nafasi hiyoKatika kuongeza chachu na hamasa kwa washindi, waandaaji wa mchezo huo wameandaa zawadi kwa washindi ikiwemo Baiskel, Simu za mkononi, Tv nk, ambazo zitatolewa kwa wachezaji watakaoibuka washindi kitika kila kipengele
  Msheli aliongeza kuwa mashindano hayo hayataishia hapo tu bali yatakuwa endelevu kwa kila mwaka ili kuweza kuongeza hamasa kwa wachezaji wa mchezo huo

older | 1 | .... | 1452 | 1453 | (Page 1454) | 1455 | 1456 | .... | 1898 | newer