Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA

$
0
0
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika  bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mshindi wa fainali alijishindia shilingi milioni moja taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata shilingi laki tano na mshindi wa tatu akiondoka na  shilingi laki tatu.

Akizungumza baada ya fainali Mheshimiwa Bonnah Kaluwa amesema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi wa mwaka huu atapata nafasi ya kwenda Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla ya mchezo wa fainali
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani wa Taifa Stars
Mshambuliaji wa timu ya Sigara FC akijaribu kuwatoka mabeki wa Bodaboda
Mamia ya mashabiki wakifuatilia mchezo


Wachezaji wa Bodaboda Kimanga wakifurahia kombe lao
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akiungana na mashabiki kucheza singeli
Mkali wa muziki wa Singeli Msaga Sumu akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi

MAMIA WAJITOKEZA KUSINDIKIZA MWILI WA MWANAFUNZI WA SCOLASTICA ALIYEUAWA

$
0
0
Msafara wa Magari ya waombolezaji na lililobeba mwili wa marehemu Humphrey Makundi ukipita eneo la Marangu mtoni wakati ukitoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuelekea kanisa la KKKT Usharika wa Mamba Kwa Makundi wilaya ya Moshi.
Ibada ya kumuombea marehemu Humphrey Makundi imefanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi .
Ndugu ,Jamaa na Marafiki wakipita mbele ya jeneza kutoa Heshima zao za mwisho katka kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa heshima za mwisho katika ibada ya marehemu Humphrey Makundi.
Ndugu wakitoa heshima za mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira (wa pili toka kulia) akiwa na viongozi wengine wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Kilimanjaro akiwemo kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hami Issah (wa pili toka kushoto) wakishiriki ibada hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Humphrey Makundi.
Mkuu wa  Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Humphrey Makundi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimfariji Baba mzazi wa Humphrey,Bw Jackson Makundi
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimfariji ,Mama mzazi wa Humphrey ,Bi Joyce Makundi.
Msaidizi wa Askofu ,Mchungaji Elingaya Saria akizungumza wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya Ndugu wa Marehemu wakifuatilia ibada hiyo.
Ndugu wa Marehemu wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Humphrey Makundi wakati ukipelekwa nyumbani kwao kwa ajili ya kuupumzisha katika nyumba yake ya milele.
Baba mzazi wa Humphrey akilia kwa uchungu wakati jeneza lenye mwili wa mwanae likiingizwa nyumbani kwao kijiji cha Mamba kwa Makundi wilaya ya Moshi .
Mama mzazi wa marehemu Humphrey Makundi ,Bi Joyce Makundi akilia kwa uchungu wakati jeneza lenye mwili wa mwanae lilipofikishwa nyumbani kwao kijiji cha Mamba kwa Makundi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu ,Humphrey Makundi likiingizwa kaburini .
Wadogo wa marehemu Humphrey wkiweka shada la maua katika kaburi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiweka shada la maua katika kaburi la Humphrey Makundi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,akijiandaa kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Humphrey.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia kaiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Humphrey Makundi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA 8 LA MWAKA LA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya Wahudhuriaji wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya awali ya Heaven  Moshono Arusha pamoja na walimu wao ambao walikuwa uwanja wa ndege wa Arusha wakati Makamu wa Rais anaondoka Arusha mara baada ya kufungua wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA, AENDESHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akizungumza na  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird leo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akimsindikiza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017.
w4, w5 na w6:  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawari  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017.

PICHA NA IKULU

Tigo yafungua duka jipya la kisasa mjini Sengerema

$
0
0

Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema(shati jeupe) Alan Augustine na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo, Beatrice Kinabo wakikata utepe kuzindua duka la Sengerema mkoani Mwanza jana, Meneja Mauzo mkoa wa Geita Lugutu Lugutu akishuhudia.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema(kushoto) Alan Augustine akibadilishana mawazo na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo Beatrice Kinabo, baada ya kuzindua duka la Tigo mjini Sengerema.
Wananchi wa Sengerema wakishuhudia uzinduzi wa duka.
Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo, Beatrice Kinabo, akizungumza na wakazi wa Sengerma wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo jana.
Meneja Mauzo Tigo mkoa wa Geita ambaye anasimamia hadi Sengerema Lugutu Lugutu, akizungumza na wakazi na wafanyakazi wa Tigo mjini Sengerema wakati wa uzinduzi wa duka hilo.

Duka hilo kurahisisha na kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa simuYazindua promosheni ya ‘Back to school’ mahsusi kwa wateja wa Kanda ya Ziwa
Sengerema, 2 Desemba 2017- Katika mwendelezo wa juhudi zake za kuboresha huduma kwa wateja wa simu nchini, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo leo imezindua duka jipya la kisasa mjini Sengerema, Wilaya ya Geita.     

Duka jipya ya Tigo mjini Sengerema lipo kwenye barabara ya Geita, mkabala na kituo cha mafuta cha Tabasamu. Duka hilo lina uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 660,000 wa Tigo katika mji wa Sengerema na viunga vyake.

Akifungua duka hilo la kipekee, Meneja Huduma kwa Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Beatrice Kinabo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya alisema kuwa duka hilo jipya linaleta huduma zote za Tigo chini ya mwavuli mmoja na karibu zaidi na wakaazi wa Wilaya ya Sengerema.

‘Hiki ni kipindi ambacho TIGO kanda ya ziwa tunafungua maduka yetu mapya 6 (sita), hivyo kufanya idadi kamili ya maduka ya Tigo katika ukanda huu kufikia 15.  Maduka yetu yote ni ya kisasa na yana kaunta nyingi zaidi za kuhudumia wateja pamoja na sehemu ambayo itawawezesha wateja wapya kujaribu bidhaa na huduma bora za Tigo,’ alisema Kinabo.

Alibainisha kuwa Tigo pia inazindua  kampeni ya ‘Back to School’ mahsusi kwa wakaazi wa Kanda ya Ziwa, ambapo  wateja  watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za shule kila watakapotumia huduma mbali mbali muhimu zinazopatikana katika maduka ya Tigo. Huduma hizi ni pamoja na kununua laini mpya, kurudisha laini iliyopotea, kununua smartphone aina ya tecno S1 na R6 pamoja na kujiunga na huduma za Tigo za malipo ya baada.
‘Tumewasilikiza wateja wetu na tunazidi kuleta huduma bora karibu zaidi nao. Pia tunapanua na kuboresha huduma zetu kwa kufungua vituo vipya vya minara, kuongezea uwezo vituo vilivyokuwepo kwa sasa kwa viwango vya 3G na kasi ya juu ya 4G na pamoja na kusambaza huduma za mtandao wa simu katika maeneo ambayo zamani hayakuwa yamefikiwa na huduma za simu za mkononi. Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anafurahia faida kubwa zinazotokana na kuwa sehemu ya ulimwengu wa kidigitali,’ Kinabo  aliongeza. 
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Alan Augustine alisema hii fursa kwa wakazi wa Sengerema kuweza kupata huduma za mtandao uliobora wa Tigo kwa kuweza kujipatia huduma mbalimbali zitolewazo na Tigo kwa ukaribu, hii inaonesha jinsi gani Tigo inawajali, “mimi mwenyewe ni mtumiaji mkubwa wa Mtandao wa Tigo hii inaweza kuturahisishia sisi wakazi wa Sengerema kutokwenda umbali mrefu kufuata huduma za mtandao,” alisema Augustine

Wateja wa Tigo katika Kanda ya Ziwa na hasa wale wanaoishi katika wilaya ya Sengerema wameelezea furaha yao kwa kufunguliwa kwa duka hilo kwani wanaamini litaboresha upatikanaji wa huduma kwa wateja.
‘Zamani tulikuwa tunalazimika kusafiri mwendo mrefu ili kupata suluhisho la huduma mbalimbali za simu. Tunafurahi na kuwashukuru Tigo kwa kusikiliza na kujibu kilio chetu cha muda mrefu kwa kufungua duka karibu zaidi na nyumbani,’ Juma Mabula, mkaazi wa Sengerema alisema.
Tigo ndio mtandao uliojizolea sifa kuu ya  kuelewa mahitaji ya wateja wake na kuhakikisha kuwa wateja wote wanapokea huduma bora, za haraka na uhakika kwa viwango vya kimataifa katika maduka yake 75 yaliyoenea nchi nzima.


BOHARI YA DAWA (MSD) YAPONGEZWA KWA USAMBAZAJI WA DAWA NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI) katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja katika ziara iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI), Respicious Lwezimula (kulia), akizungumza katika kikao hicho.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (wa tatu kushoto), akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika ziara hiyo.

Kikao kikiendelea.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (wa nne kulia), akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI)
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amani Malima, akizungumza na viongozi kutoka MSD. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule. 
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke baada ya kufanya nao mazungumzo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD), imepongezwa kwa kushinda tenda ya kununua dawa Jumuhiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

Pongezi hizo zimetolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Profesa Lawrence Mseru wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na timu yake wakati wakiwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.

"Kwanza tunawapongezeni MSD kwa kufikia hatua ya kununua dawa katika Jumuhiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) hii ni hatua ya kujivunia kama nchi" alisema Profesa Mseru.

Mseru aliongeza kuwa licha ya kuwepo changamoto ndogo ndogo MSD imejitahidi katika huduma ya usambazaji wa dawa hapa nchini hivyo akaomba ushirikiano baina yao uendelee kudumishwa ili kutoa huduma nzuri zaidi ya kuwahudumia wananchi ukizingatia kuwa taasisi hizo zote zinafanya kazi ya Serikali.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI),Respicious Lwezimula alisema kazi kubwa inayofanywa na MSD inapaswa kuungwa mkono kwa kununua dawa na vifaa tiba.

"Tuna kila sababu ya kuwaunga mkono hawa wenzetu kwa kununua vifaa tiba na dawa kutoka kwao badala ya kununua kwenye maduka ya watu binafsi kikubwa tunawaomba bei yao iwe tofauti kidogo" alisema Lwezimula.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amani Malima alisema suala la manunuzi ya dawa na vifaa tiba linachangamoto kubwa lakini MSD wamesaidia sana kuzipunguza kutokana na ushirikiano wanaofanya baina yao na wateja wao hawana budi kupongezwa.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amewaomba wateja wao hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha MSD kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa manunuzi maalumu.

Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.

Akizungumza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Temeke na Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI), Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na kuwa MSD katika kukabiliana na changamoto hizo imepata msaada wa magari 220 kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.

Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.

"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu hivyo tukipata oda mapema itatusaidia kupunguza changamoto hiyo " alisema Bwanakunu.

SERIKALI KUBORESHA KIVUTIO CHA UTALII CHA ENEO LA BARABARA YA LAMI INAYOPITA JUU ZAIDI KUTOKA USAWA WA BAHARI

$
0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akiongozwa na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo kukagua moja ya eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.
Bofya kitufe cha PLAY kuangalia VIDEO

Na Hamza Temba, Mbeya
........................................................
Serikali imesema itaboresha mazingira ya kivutio cha utalii cha barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi kutoka usawa wa bahari kuliko barabara zote nchini ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii na kuongeza idadi ya watalii na mapato.


Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya kutembelea shamba la miti la Kawetire wilayani Mbeya na kujionea sehemu ya barabara ya lami inayopita katikati ya shamba hilo katika mlima Kawetire kwenye safu za milima ya Mbeya.


Eneo hilo la barabara hiyo ambayo hupitisha magari kutoka Jijini Mbeya kwenda katika Wilaya ya Chunya na Mikoa ya Singida na Tabora lina urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari katika Latitude 08’ 35 S na Longitude 33’ 25 E.


“Hatutaki ule utalii wa kutegemea wanyamapori pekee, hii sasa ni sehemu ya aina nyingine ya utalii ambayo ni lazima tuiboreshe tuweke kibao kizuri tuweke mazingira mazuri pamoja na kukitangaza ili watanzania na watalii kutoka nje waweze kutembelea hapa,” alisema Hasunga.


Alisema ili kufikia lengo liliwekwa na Serikali la kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni mbili mwaka 2020 na milioni 8 mwaka 2025 vivutio vyote vya utalii vilivyopo nchini vitatambuliwa, kuimarishwa na kuviwekea miundombinu itakayowavutia watalii kuvitembelea.


Aidha aliuagiza uongozi wa shamba hilo kushirikiana na wakala wa huduma za barabara –Tanroads katika kuboresha mazingira yanayozunguka eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka bango la kisasa la kutambulisha eneo hilo, kujenga bustani na maeneo rafiki ya kupumzikia kwa ajili ya kuwavutia watalii kutembelea eneo hilo na kupiga picha.


Mbali na kivutio hicho aliuagiza uongozi wa shamba hilo kutobomoa majengo ya kale yaliyotumiwa na wakoloni katika shamba hilo na badala yake yatumike kwenye utalii wa mambo ya kale sambamba na utalii wa misitu ya kupandwa inayopatikana pia katika shamba hilo.


Hata hivyo alisema kupitia mradi wa REGROW wa kuendeleza utalii kanda ya kusini Serikali imepokea mkopo wa masharti nafuu wa dola za Kimarekani milioni 150 sawa za zaidi ya bilioni 340 za kitanzania kutoka benki ya dunia kwa ajili ya kusaidia kuboresha miundombinu ya vivutio vya ukanda huo.


Kwa upande wake Meneja wa shamba hilo, Arnorld Shoo alisema eneo hilo la barabara limekuwa ni kivutio cha kipekee cha utalii katika shamba hilo ambapo pia hupata mapato kupitia watu na vikundi mbalimbali ikiwemo wanakwaya na wanafunzi ambao hufika eneo hilo kwa ajili ya kupiga picha za kumbukumbu.  

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo wakiangalia bango linaloonesha eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA, AFUNGUA KONGAMANO LA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI JIJINI ARUSHA

$
0
0
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan  akiongea wakati wa ufunguzi wa   

kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) uliofanyika jijini Arusha leo(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)

Waziri wa Fedha na mipango(Mb)Dkt Philip Mpango akizungumza katika 

kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.


Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dkt.Hellen Bandiho akizungumza katika 

kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.   

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira akiwa  katika 

kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.

Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo akiteta jambo na Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan katika 

kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.



 Wadau wa mkutano huo wakifatilia kwa ukaribu


Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.

Na Pamela Mollel,Arusha

Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya fedha na mipango kuhakikisha wanakamilisha mapema sera yaTaifa ya Ununuzi wa Umma kwa kufanya marekebisho ya sheria ,kanunina taratibu zingine zikakazo ongoza shughuli za ununuzi wa umma hapa nchini


Akizungumza leo jijini Arusha  katika kongamano la nane la wanataaluma ya ununuzi na ugavi(PSPTB)iliyowashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau kutoka nchi jirani ya Kenya


Bi.Samia alisema kuwa kwa kufanyika kwa marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma utasaidia kuongeza kiwango cha uwajibikaji wa wadau wote wanaohusika katika shughuli za umma


Aidha aliongeza kuwa ripoti mbalimbali za ukaguzi zinaonyesha kuwa Serikali imeendelea kupata hasara katika eneo la ununuzi wa umma kutokana na wataaluma wachache kutokuwa tayari kutimiza wajibu wao au shughuli hizo kufanywa na watu wasio na taaluma hiyo


“Napenda kuwaasa ambao bado wanaendeleza vitendo viovu kama rushwa ,upendeleo,wizi,uzembe waache mara moja na watambue kuwa sheria zipo na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao”alisema Bi.Samia


Pia alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano haitamvumilia mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na maadili ya taaluma yake


Kwa upande wake Waziri wa Fedha na mipango(Mb)Dkt Philip Mpango alibainisha mapungufu yaliyoonekana katika taasisi zilizokaguliwa ikiwemo kupungua kwa kiwango cha uzingatiaji wa sheria ya ununuzi wa umma katika Halmashauri kutoka wastani wa asilimia 71 mwaka 2015-16 hadi asilimia 69


Pia Mh.Mpangoalisema kuwa miradi 7iliyokaguliwa yenyethamani ya shilingi bilioni 2.37 imebainika kufanywa chini ya viwangovisivyoridhisha

Aidha aliongeza kuwa kwa upande wa maadili ya ukaguzi umebaini kuwepo kwa viashiria vingi vya rushwa katika usimamiziwa miradi 33 katika taasisi 17 za Umma zilizokaguliwa hivi karibuni


Naye Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dkt.Hellen Bandiho alisema kuwa changamoto inayoikabili bodi hiyo kwa sasa ni pamoja na waajiri kuajiri watumishi wa ununuzi na ugavi ambao hawajasajiliwa na bodi.


MKURUGENZI NAMAINGO AHIMIZA WANACHAMA KUNUNUA HISA VIBIDAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Ubwa Ibrahim akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa Ushirika Vibidar Namaingo Co-operative  Society Ltd) katika Makao Makuu ya kampuni hiyo, Ukonga Dar es Salaam, ambapo aliwahimiza wanachama wa Namaingo kujiunga haraka kwenye Ushirika wa Vibidar ili kurahihisisha upatikanaji wa mikopo kwa lengo  la kuendeleza miradi ya maendeleo inayosimamiwa na kampuni hiyo. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog.
Ubwa Ibrahim akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
 Sehemu ya wanachama wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi huo akiwahutubia






Bi. Ubwa akionesha kitabu chenye mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni ya Namaingo

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA DODOMA

$
0
0
 Usiku wa Kitendawili kufufua upya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dr John Pombe Magufuli anataraji kuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ utakaofanyika Ijumaa hii Disemba 8 2017 kupitia ‘Usiku Wa Kitendawili’ mjini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa habari Msanii  wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ndio wataouratibu usiku huo wa Kitendawili kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Sanaa utamaduni na Michezo.

Usiku wa Kitendawili ulianzishwa baada ya msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kuachia wimbo ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo.

Akiongea na wadau wa sanaa katika Maandalizi ya Kampeni hiyo ya Kitaifa itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, Mrisho Mpoto amesema kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza ndani ya Taifa letu.

Alisema mambo ambayo yatayozingatiwa katika kampeni hiyo ni pamoja na kudhubiti na hatimaye kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma, kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka ufisadi, ubadhilifu wa mali za Umma pamoja kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.

“Usiku wa Kitendawili utatumika kama jukwaa la kuwaleta pamoja watanzania pamoja na viongozi wao ili kukumbushana kuhusu wajibu na kujadili mustakabali wa Taifa. Kutakuwa na vivutio mbalimbali pamoja na wimbo maalumu kutoka kwa wasanii maalumu Mwaka Huu,” alisema Mpoto.

Aliongeza,”Tumekuja kuunadi Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ kwasababu tunaamini Uzalendo na Utaifa lazima uwepo ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kuunga mkono juhudi za Raisi Dkt. John Pombe Magufuli za kujenga Taifa lenye Uzalendo, Utu, Weledi na Uadilifu uliotukuka. Mimi ni mzalendo ndio maana hata kwenye hizi harakati nipo toka nimetoa wimbo wangu wa kwanza, ukiangalia nyimbo zangu zote ni za kuonganisha jamiii 120 za watanzani,”

 “Naamini kwenye kufanya kazi ambayo itawafanya watanzania pamoja na kizazi kijacho kitambue kuna watu ambao walifanya kazi kubwa kwenye hili taifa, kuacha alama ambazo haziwezi kufutika katika maisha ya historia ya nchi hii, kwa sababu hivi vyote ambavyo vinaenda kufanywa ni kufufua upya na kuiweka pamoja mitazamo ya watanzania ili kujenga Taifa la Wazalendo na Wachapakazi kuiga nyayo zilizoachwa na hayati Baba wa Taifa,” alifafanua zaidi.

Mpoto amesema lengo kuu la maadhimisho hayo kuambatana na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa kuanzia mwaka 2018 ni kutumia jukwaa hilo kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kujenga na kuendeleza Utaifa.

Alisema baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo wiki hii huko Dodoma, itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni chini ya Uwenyekiti wa Mkuu wa Mkoa na  Wilaya.

--

UMOJA SWITCH YAHAMASISHA KUBADILI KADI

$
0
0
Umoja Switch inianzishwa miaka zaidi ya kumi iliyopita ili kuwezesha benki ndogo na za kati kuweza kupata huduma za ATM. Kupitia Umoja Switch benki zaidi ya 27 zinawezesha wateja wao kupata huduma kwenye ATM zaidi ya 250 bara na visiwani.Ili kuongeza usalama na pia kutua fursa ya kuongeza bidhaa zaidi, Umoja Switch ilianza mkakati wa kuhamisha wateja kutoka kwenye kadi za zamani zenye ufito (magnetic stripe) kwenda kwenye kadi mpya za kisasa na zenye usalama wa juu (Chip). 
 Zoezi hili ambalo linaishia mwezi huu wa Disemba mwishoni.Ili kuwazawadia wateja wake hususani wale wenye kadi zenye Chip, Umoja switch imeanzisha droo kubwa inayowezesha wateja kushinda fedha wanazotoa kwenye ATM maradufu,shilingi milioni moja,simu za mikononi au T-shirts za Umoja. Droo hii ni kwa wateja wenye kadi mpya ambao wanatumia ATM za Umoja popote Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Danfold Mbilinyi alisema “ Lengo kuu la umoja ni kusogeza huduma za kibenki kwa Watanzania wengi zaidi popote Tanzania. Tunafurahi kuwa tumeweza kufika maeneo mengi Nchini na bado tunalenga kuongeza kasi ya ubunifu na usogezaji wa huduma zetu.
 
Kuboresha ubora wa kadi zetu ili kuongeza usalama na pia kutoa fursa zaidi ya ubunifu ni ishara tosha kuwa Umoja Switch inalenga kuwa msharika madhubuti wa Maendeleo ya Tanzania hususani sekta ya kifedha. Tunawakaribisha wateja wetu na hata ambao si wateja wetu kubadilish kadi au kufungua akaunti kwenye benki yeyote mshirika ili nao washinde kwenye droo hii kubwa“.

RC RUVUMA AWAONYA WATUMISHI WA HALIMASHAURI YA MBINGA

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma CHRISTINE MNDEME amewataka watumishi kuvaa uzalendo wa nchi ilimkuweza kujenga uchumi wa kati wa viwanda , ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halimashauri ya wilaya ya MBINGA wakati wa ziara yake.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMANNE LEO DECEMBER 5,2017

Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya wazinduliwa leo mjini Dodoma

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,akizungumza mapema leo mjini Dodoma mbele ya Wadau mbalimbali wa mambo ya Afya,ikiwa ni sehemu ya kuelekea kilele cha uzinduzi wa kampeni ya Unawaji Mikono kwa vituo vya Afya itakayojulikana kwa jina la NIPO TAYARI awamu ya pili,Ambapo katika uzinduzi wa kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi Desemba 7,2017 mkoani Dodoma,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Makamu wa Rais Mama samia Suluh Hassan
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba ambaye pia ni mgeni rasmi akikata utepe kuzindua  Jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma,uzinduzi wa jarida hilo ni sehemu ya kuelekea kilele cha uzinduzi wa kampeni ya Unawaji Mikono kwa vituo vya Afya itakayojulikana kwa jina la NIPO TAYARI awamu ya pili,Ambapo katika uzinduzi wa kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi Desemba 7,2017 mkoani Dodoma,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Makamu wa Rais Mama samia Suluh Hassan

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akiwaonesha Wanahabari jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma

Mratibu wa Kampeni ya Usafi wa mazingira-wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Anyitike Mwakitalima akizungumza jambo mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo,mapema leo mjini Dodoma,kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa jarida  lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe,Dkt Buru Mwamasage jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akimkabidhi Afisa Afya mkoa wa Dodoma,Edward Ganja jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akimkabidhi Mkurugenzi wa Mipango kutoka shirika la WaterAid -Tanzania Bwa.Abel Dugange  jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akipewa maelezo mafupi kuhusiana na matumizi ya dawa mbalimbali zinazotumika katika usafi wa maeneo mbalimbali ikiwemo ya kunawia mikono na kusafishia vyoo,zilizotengenezwa na wajasiliamali waliokuwepo ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa  jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Mratibu wa Kampeni ya Usafi wa mazingira-wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt Anyitike Mwakitalima akipewa maelezo mafupi kuhusiana na matumizi ya dawa mbalimbali zinazotumika katika usafi wa maeneo mbalimbali ikiwemo ya kunawia mikono na kusafishia vyoo,zilizotengenezwa na wajasiliamali waliokuwepo ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa  jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Baadhi ya wadau wakiangalia vipeperushi mbalimbali nyenye taarifa za mambo ya Afya na usafi kwa jamii.
Baadhi ya Wawakilishi kutoka shirika la UNICEF wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo ambao pia uliwajumuisha wadau mbalimbali wa mambo ya Afya


Tigo na WorldRemit washuhudia ukuaji mkubwa katika huduma ya kuhamisha fedha katika akaunti za simu za mkononi Tanzania

$
0
0
Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni yake na Tigo Tanzania unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda kwa huduma ya Tigo Pesa. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed.

Meneja Uhusiano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni ya Tigo na ile ya World Remit unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda  Tigo Pesa. Kulia ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed na Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit .




Watanzania walioko nje ya nchi wametuma zaidi ya dola milioni 25 katika akaunti za Tigo nchini Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja, kwa kutumia huduma ya WorldRemit au tovuti.

Desemba 2017, Dar es Salaam na London: Huduma ya kuhamisha fedha kidigitali inayoongoza WorldRemit na Kampuni ya kidigitali Tigo Tanzania wameshuhudia ukuaji wa kasi wa huduma za kuhamisha fedha kwenda katika akaunti za fedha za simu za mkononi nchini Tanzania, taarifa zimebainisha.

Katika kipindi cha miaka miwili cha ushirikiano baina ya kampuni hizi, huduma ya Tigo imebainika kuwa ndiyo huduma ya kutuma fedha inayokuwa kwa kasi zaidi miongoni mwa washirika wa WorldRemit.

Huduma hii inawawezesha Watanzania katika zaidi ya nchi 50 kutuma fedha kwenda katika akaunti za fedha za simu za mikononi kwa haraka. Wamiliki wa akaunti za fedha za simu za mkononi pia wanakuwa na uwezo wa kutuma fedha ndani ya nchi, kununua muda wa maongezi, kulipia ankara au kutoa fedha taslimu kupitia mtandao mkubwa wa mawakala wa Tigo.

Licha ya Tanzania kutajwa kuwa ni moja ya nchi ambayo ina gharama kubwa sana kutuma fedha miongoni mwa nchi za Afrika, huduma hii maarufu inapunguza gharama za utumaji wa fedha wakati huohuo ikifanya mchakato wa kutuma fedha kuwa wa haraka na salama zaidi.

Upokeaji wa fedha unachukua nafasi muhimu katika uchumi wa Tanzania. Mwaka 2015 nchi ilipokea zaidi ya dola milioni 400 fedha kutoka nje ya nchi, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

WorldRemit ni mfumo wa kidigitali wa kwanza unaotumia simu za mikononi kutuma fedha unaowaruhusu wahamiaji wanaofanya kazi nje ya nchi kutuma fedha kwa kufuata hatua chache moja kwa moja katika simu zao za mkononi bila kutembelea au kusimama katika foleni kwa mawakala. Kampuni inawajibika kwa 74% ya fedha zote zinazotumwa kupitia mfumo wa kutuma fedha kimataifa kwenda katika huduma za fedha za simu za mikononi.

Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika kutoka WorldRemit, alitoa maoni yake na kusema: Ushirikiano wetu na Tigo unatoa nafasi zaidi kwa mamlilioni ya watanzania wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi kuwa na mbinu mbadala ambayo ni rahisi na salama ya kuwasaidia marafiki na familia zao pasipo kupanga foleni kwa mawakala wa kutuma fedha.”

Mtanzania aliyehamia London, Stockholm au Sydney sasa anaweza kutuma fedha kuja nyumbani kwa haraka na kwa urahisi – ikiwa inasaidia kuhamisha fedha kwa haraka, usalama na uhakika zaidi kushinda mifumo ya kutuma fedha isiotumia mtandao wa simu inayotegemea mawakala wa kutuma fedha.”

Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha za Simu za Mkononi wa Kampuni ya Tigo Tanzania, aliongezea: “Tigo tumejizatiti katika kutoa huduma kamili ya kifedha kwa wateja wetu. Kama sehemu ya malengo yetu ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kifedha, tunatazamia kuhudumia sio tu soko la ndani ya mipaka ya Tanzania bali pia kwa watanzania wote walioko nje ya nchi. Pamoja na hayo tunachukua hatua zote kuwapatia wateja wetu mfumo wa uhakika na salama kwa ajili ya kutuma fedha kimataifa.

Kwa sasa wateja wa WorldRemit duniani kote wanafanya miamala 750,000 ya kuhamisha fedha kila mwezi kutoka katika zaidi ya nchi 50 kwenda kwa zaidi ya nchi wapokeaji 148.

Tembelea tovuti ya WorldRemit kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kutuma fedha Tanzania.



CCM IRINGA WAPIGA KURA KUCHAGUA UONGOZI MPYA LEO

$
0
0
Mjumbe wa NEC Mh. Januari Makamba akizungumza na kutoa utaratibu wa wagombea na wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa unaofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa leo Chama cha mapinduzi kimekuwa na chaguzi za ngazi mbalimbali kuchagua viongozi watakaokwenda kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano tutawaletea taarifa zaidi kuhusu matokeo ya uchaguzi huo.
2
45
Wagombea wa nafasi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika uchaguzi hu.
6
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo.
78
Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni mjumbe wa wa NEC na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza wakiimba wimbo kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa Uchaguzi.
9
Mjumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Iringa na Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Bw. Richard Kasesela akicheza na mmoja wa wajumbe katika mkutano huo.
10
Baadhi ya wajumbe wakiimba nyimbo kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa uchaguzi mjini Iringa.
11
Mjumbe wa NEC na Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Iringa akicheza na mmoja wa wajumbe wenzake katika mkutano huo.
12
Wajumbe wa mkutano huo wakicheza na kuimba.
13
Mmoja wa wagombea wa UNEC Bw. Salim Abri Asas akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa jimbo la Mufindi Mh. Mahmoud Mgimwa.
wag1
Wagombea nafasi ya Uenyekiti wa mkoa wa Iringa kutoka kushoto ni Albert Chalamila, Evance Balama na Daniel Kidava wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kujieleza kwa wajumbe.
wag2
Mgombea nafasi ya Uenyekiti wa mkoa wa Iringa Albert Chalamila akijieleza kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi huo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Abdullah Ibrahim Al-Suwaidi wa pili kutoka (kushoto) aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Balozi Zuhura Bundala wa kwanza (kulia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Abdullah Ibrahim Al-Suwaidi aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Total Momar Nguer mara baada ya kuwasili Ikulu pamoja na ujumbe wake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kampuni ya Total Momar Nguer mara baada ya kamaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya Total Momar Nguer wa tatu kutoka (kushoto ) aliyeambatana na ujumbe wake mara baada ya kamaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage pamoja na Balozi Zuhura Bundala wa kwanza (kulia). PICHA NA IKULU.

Business Council of International Understanding Honours Tony O. Elumelu with the Dwight D. Eisenhower Global Entrepreneurship Award

$
0
0
Business Council of International Understanding Honours Tony O. Elumelu with the Dwight D. Eisenhower Global Entrepreneurship Award

…The Group Chairman, United Bank for Africa Plc (UBA) and Founder, Tony Elumelu Foundation becomes first African to receive the prestigious award.
Chief International Correspondent, CNBC, Ms Michelle Caruso – Cabrera; Vice Chairman of the Forbes Publishing company, Mr. Kip Forbes,; Chairman, Business Council for International Understanding(BCIU), Mr. Bill Mills, BCIU; Award Recipient, Group Chairman, United Bank for Africa Plc and Founder, Tony Elumelu Foundation, Mr. Tony Elumelu; Interior Designer and Granddaughter of General Dwight D. Eisenhower(34th President of the U.S.A), Ms. Anne Eisenhower; CEO, BCIU, Mr. Peter Tichansky, at the conferment of the prestigious Dwight Eisenhower Global Award for Entrepreneurship on Elumelu by Business Council for International Understanding(BCIU), at the Cipriani in New York City on Monday

Picture 1: l-r: Vice Chairman of the Forbes Publishing company, Mr. Kip Forbes; Award Recipient, Group Chairman, United Bank for Africa Plc and Founder, Tony Elumelu Foundation, Mr. Tony Elumelu; and Interior Designer and Granddaughter of General Dwight D. Eisenhower(34th President of the U.S.A), Ms. Anne Eisenhower during the conferment of the prestigious Dwight Eisenhower Global Award for Entrepreneurship on Elumelu by Business Council for International Understanding(BCIU), at the Cipriani in New York City on Monday


Business Council of International Understanding Honours Tony O. Elumelu with the Dwight D. Eisenhower Global Entrepreneurship Award

New York City, U.S.A, December 5th, 2017; The Business council for International Understanding (BCIU), a non-profit U.S Business association dedicated to forging relationships and promoting dialogue between business and government communities across the globe, tonight presented the prestigious Dwight D. Eisenhower Global Entrepreneurship Award to both Tony O. Elumelu and Bill Marriott, Chairman, Marriott International Inc.

The award was conferred on Elumelu in recognition of his outstanding work in promoting Entrepreneurship on the continent of Africa and across the globe. Elumelu, himself a serial entrepreneur, through his Tony Elumelu Foundation, has funded over 3,000 African entrepreneurs to date with his U$D100 million ccommitment to 10,000 entrepreneurs over a period of 10 years. These entrepreneurs are expected to create a million new jobs and over U$D10 billion in revenue as a result of the initiative of Elumelu’s Foundation.

At the award’s gala, former American President George W. Bush, acknowledged the efforts of the African entrepreneur saying ‘I am impressed with Tony’s philanthropic initiatives which are powering job creation and entrepreneurship in a region(Africa), that is very dear to Laura and me. To receive an award founded by President Eisenhower, has added meaning. Eisenhower provided example in leadership, which we can all learn from. Additionally, his belief in promoting international understanding is a vitally important responsibility.

Speaking on the reason why Elumelu was selected as the recipient of this prestigious award, Peter Tichansky, the CEO of BCIU said ‘Mr Elumelu’s bold approach and can-do mindset are exemplary characteristics of a visionary entrepreneur. He embodies the idea that companies must take the lead in bringing business and society together. His advocacy is proving that businesses, acting as businesses and not charitable donors, are the most powerful force for addressing social challenges and economic development’

Indeed this is the philosophy of Elumelu, founder of the concept of Africapitalism, which essentially states that Africa’s private sector must play a leading role in the development and growth of the continent as both governments and the private sector come together to make this happen.

Elumelu who was presented his award by Kip Forbes and Anne Eisenhower(the granddaughter of President Eisenhower,) in his acceptance speech stated: ‘President Eisenhower was a man of many dimensions and most important is his leadership. Being recognized today as a recipient of the inaugural global entrepreneurship award is an honour that resonates with so many people in Africa. What our entrepreneurs in Africa need is powerful leadership to further energise, encourage and motivate them to transform the continent.’ He went on to say ‘ I hope this will further spur on other Africans and friends of Africa, to make sure we work together for an inclusive prosperity'.

Elumelu dedicated his award to his wife and children as well as the staff of UBA, Transcorp, Heirs Holdings, the Tony Elumelu Foundation and all the other companies within his group of companies. He thanked BCIU on behalf of entrepreneurs in Africa: ‘On behalf of the over 3000 entrepreneurs who have benefitted from the Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship programme, I say thank you very much.


The award ceremony and gala took place at the historic venue, the Cipriani on Wall street in New York

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHANDISI ISACK KAMWELE ATEMBELEA MIRADI YA DAWASA YA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI

$
0
0
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, akiteremka kutoka juu ya tenki la maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo Desemba 5, 2017, wakati wa ziara yake ya siku mbili kukagua miradi ya maji inayoendeshwa na DAWASA


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, ameanza ziara ya siku mbili ya kukagua baadhi ya miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji  Safi na Maji Taka, (DAWASA), jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.
Katika siku yake ya kwanza ya ziara hiyo, Waziri alitembelea Mradi wa Uboreshaji Mfumo wa Usambazaji maji ambapo kazi zinazofanyika chini ya mradi huo ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji  yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi milioni 6.0, lakini pia ujenzi wa vituo vine(4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa 16 za kusukuma maji, ununuzi wa transfoma  na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji yatakayokuwa na urefu wa kilomita 477.
Mradi huu utanufaisha maeneo ya Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni , Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo,Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa maji wa Ruvu Chini.
Aidha maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba,Mbezi, Makuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo yote haya hupata huduma kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambao ulizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhurim ya Muungani wa Tanzania Juni 21, 2017.
 Mhandisi Kamwele, mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi, wapili kulia), na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakitembelea eneo la ujenzi wa trenki la kuhifandia maji, Mabwepande nje kidogo ya jijji
 Mhandisi Kamwele akizungumza katika moja ya maeneo aliyotembelea
 Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi, akimsikiliza Mkandarasi anayejenga matenki ya kuhifadhia maji kwenye mradi mjuybwa wa kuimarisha miundombinu unaosimamiwa na DAWASA
 Mhe. Waziri Mhandisi Kamwele, (wapili kushoto), Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya india


 Mhe. Waziri Kamwele, (kushoto), akiwa na Mhandisi Romanus Mwang'ingo, wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi ya ujenzi wa tenki la maji eneo la Salasala kutoka kwa mkandarasi, Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya india
 Mhe. Waziri Kamwele, (kushoto), akifafanua jambo, wakati akipatiwa maelezo na Mkandarasi kutoka kampunin ya India ya WAPCOS, Mhandisi P.G. Rajani
Waziri Mhandisi Isack Kamwele, (kushoto), akiwa na Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus (katikati) na Mtdnaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja.

KIVULINI YAFANYA KIKAO CHA WANA MABADILIKO MRADI WA USAWA WA KIJINSIA SHINYANGA

$
0
0
Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto,Shirika la Kivulini limefanya kikao cha wana mabadiliko kwa ajili ya kufanya tathmini na mrejesho wa shughuli za mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana unaotekelezwa halmashauri wilaya mbili za Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga.
Kikao hicho kilichokutanisha wana mabadiliko 65 kutoka vijiji vitano vya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Shinyanga Vijijini) ambavyo ni Nyida,Nsalala,Butini,Nduguti na Welezo kimefanyika leo Disemba 5,2017 katika Ukumbi wa mikutano wa Empire Hotel mjini Shinyanga.
Akizungumza katika kikao hicho, Afisa mwandamizi wa mradi huo, Bi. Eunice Mayengela alisema lengo la kikao hicho ni kujadili mafanikio na changamoto ambazo wana mabadiliko wanakutana nazo kwenye maeneo yao katika kutekeleza mradi.
Mayengela alisema suala ya ukatili dhidi ya wanawake ni la jamii nzima hivyo panahitajika ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatoweka katika jamii.
“Lazima tushirikiane kwa pamoja kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,wana mabadiliko,serikali na wadau wengine tunapaswa kuungana ili tuwe na nguvu ya pamoja”,aliongeza Mayengela.
Mayengela alitumia fursa hiyo kuwataka wanawake kuacha uoga wanapofanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kubakwa na badala yake watoe taarifa kwenye vyombo vya sheria ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.
Naye afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja aliwataka wanawake kupaza sauti wanapofanyiwa ukatili.
“Akina mama pazeni sauti,fuateni sheria,msiwahurumie sana hawa wanaume,nanyi wanaume acheni mila na desturi zilizopitwa na wakati,wapeni urithi wa mali ikiwemo ardhi wake zenu,hata kupigana katika ndoa nako kumeshapitwa na wakati”,alieleza Mhoja.
Mhoja pia alikemea tabia ya akina baba kuwapa ujauzito watoto badala ya kuwaacha wasome kwa ajili ya kuwasaidia katika maisha yao.
Mhoja aliwataka wana mabadiliko kutumia vyema fursa waliyopewa na shirika la Kivulini ambalo limekuwa likiwapatia ujuzi na mbinu mbalimbali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wao washiriki wa kikao hicho walisema wamekuwa wakitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia kwa jamii,kutatua migogoro ya ndoa na ardhi.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KIKAO HICHO
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana, Eunice Mayengela akizungumza katika kikao cha wana mabadiliko kwa ajili ya kufanya kutathmini na mrejesho wa shughuli za mradi- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana, Eunice Mayengela akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka wana mabadiliko kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii. 
Mayengela akisisitiza umuhimu wa wadau wote kushirikiana ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wana mabadiliko wakimsikiliza afisa mradi wa usawa wa Kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja akizungumza katika kikao hicho ambapo aliitaka jamii kubadilika na kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati zinazogandamiza wanawake na watoto.
Wana mabadiliko wakiwa ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja akisisitiza umuhimu wa wanandoa kupendana kama njia mojawapo ya kukabiliana na ukatili katika familia.
Kikao kinaendelea...
Wana mabadiliko wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa miradi shirika la Kivulini,Glory Mlaki  akizungumza wakati wa kikao hicho
Wana mabadiliko wakiwa ukumbini
Kulia ni Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana, Eunice Mayengela na Afisa Mwandamizi msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa wakiwa ukumbini
Kulia ni Afisa miradi shirika la Kivulini,Glory Mlaki  akitoa mwongozo namna ya kufanya kazi ya vikundi wakati wa kikao hicho cha tathmini na mrejesho wa shughuli za mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana 
Kulia ni Afisa mwandamizi msaidizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijanaVaileth Elisa kutoka shirika la Kivulini akimsikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa washiriki wa kikao hicho wakati wa kazi za makundi.
Kazi za makundi zikiendelea...
Wana mabadiliko wakifanya kazi ya kundi lao
Mwana mabadiliko Mwendwa Yasin kutoka kijiji cha Welezo akiwasilisha kazi ya kundi lake kuhusu shughuli mbalimbali wanazofanya katika kutekeleza mradi wa 
Mwana mabadiliko Monica Simon akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images