Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1449 | 1450 | (Page 1451) | 1452 | 1453 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametembelea vituo sita vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga yenye vituo tisa.

  Mkuu huyo wa wilaya amefanya ziara hiyo leo Jumamosi Disemba 2,2017 kwa ajili ya kujionea stadi za maisha na miradi mbalimbali inayofanywa na watoto wanaopata huduma katika vituo hivyo.Vituo vilivyotembelewa ni vituo vya Kanisa la ACT Shinyanga Mjini,AICT Kolandoto,TAG Shinyanga Mjini,PAG Shinyanga Mjini,KKKT Shinyanga Mjini. 

  Akiwa katika ziara hiyo,Matiro amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na watoto kama vile utengenezaji skonzi,biskuti,keki,nguo,mafuta,sabuni pamoja na ususi,ufumaji,saluni,ufyatuaji wa matofali,uchomeleaji wa vyuma,useremala,masomo ya kompyuta na mambo mengine kadha wa kadha. 

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo,mkuu huyo wa wilaya alilipongeza shirika la Compassion kupitia makanisa yanayosimamia vituo hivyo ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwa watoto ambao wanajengewa uwezo wa kujiajiri. 

  “Nimegundua tuna jeshi kubwa la vijana wenye ujuzi wa aina mbalimbali,vijana tumieni fursa hii ya Compassion kujinufaisha kwa ajili ya maisha yenu,sisi kama serikali tunafarijika sana kuona vijana wakijengewa uwezo wa kujiajiri ili kuleta maendeleo katika jamii”,alieleza. Matiro alieleza kufurahishwa kuona jinsi vijana hao wanavyojengewa uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwashauri kuongeza jitihada ili kutengeneza viwanda kamili vya kutengeneza bidhaa. 

  “Sera ya serikali ni kuwa na viwanda,nimeona vijana wanatengeneza skonzi,biskuti kwa kutumia mashine za kisasa kabisa katika kituo cha AICT Ngokolo,hiki ni kiwanda,naomba kanisa na Compassion kwa kushirikiana na serikali tuangalie namna ya kupanua kiwanda hiki ili kuleta mabadiliko katika jamii na kitasaidia vijana kujikwamua kiuchumi”,alisema Matiro. 

  Katika hatua nyingine aliwataka wahusika katika vituo hivyo kuhakikisha msaada unaotolewa na shirika hilo kuwafikia watoto wanaolengwa huku akiwataka kushirikiana kwa ukaribu na viongozi wa serikaliza mitaa ili kubaini watoto wanaohitaji msaada kutokana na ugumu wa maisha. 

  Awali akisoma taarifa kuhusu vituo vya huduma ya mtoto katika klasta ya Shinyanga,Katibu wa wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Thomas Faida alisema shirika la Compassion linahudumia watoto 2,110 wanaoishi kwenye mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga. Alisema watoto hao hupatiwa misaada mbalimbali kama vile kufundishwa stadi za maisha,kupewa elimu ya ujasiriamali,kupewa sare za shule,madaftari,nguo,ada ya shule,gharama za matibabu na mambo mengine kadhaa. 

  Kwa upande wake Msimamizi wa vituo vya huduma ya mtoto klasta ya Kanda ya ziwa,Emmanuel Pando alisema shirika la Compassion linafanya shughuli zake kwa ushirika wenza na makanisa katika kuwahudumia watoto walioko katika mazingira magumu. 

  Pando alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ili kufanikisha mambo mbalimbali ambayo serikali inataka yafanikiwe. 
  Mwenyekiti wa Wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la TAG Shinyanga akimpokea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini kwa ajili ya kutembelea stadi za maisha na miradi inayofanywa na watoto katika kituo hicho. 
  Mkurugenzi wa kituo cha huduma ya watoto kanisa la ACT Shinyanga Mjini,Hagai Daniel akimwongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwenda kuangalia stadi za maisha na miradi inayofanywa na watoto wanaohudumiwa katika kituo hicho. 
  Vijana wakimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro keki walizotengeneza.Vijana hao walisema wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza keki katika kituo hicho. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi wanavyochomelea vyuma katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba cha ufumaji katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba kwa ajili ya mambo ya ususi.Vijana wanaendelea kusukana. 

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipokelewa katika kituo cha Kanisa la AICT Kolandoto. Wa kwanza kulia ni diwani wa kata ya Kolandoto,Agnes Machiya,ambaye ni pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga.Katikati ni Mchungaji Kiongozi kanisa la AICT Kolandoto,Jacob Osora 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba cha Kompyuta katika kituo cha AICT Kolandoto.Kulia ni mwalimu wa Kompyuta katika kituo hicho, Lucas Masaba. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha AICT Kolandoto. 
  Watoto katika kituo cha AICT Kolandoto wakiimba wimbo 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi watoto wanavyotumia kompyuta katika chumba cha kujifunzia Kompyuta katika kituo cha AICT Ngokolo. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimwangilia kijana akishona nguo kwa kutumia cherehani katika kituo cha AICT Ngokolo 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia mashine zinazotumika kutengeneza skonzi na biskuti katika kituo cha AICT Ngokolo. Mkuu huyo wa wilaya alisema hicho ni kiwanda hivyo kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kukipanua ili kilete maendeleo. 
  Mmoja wa vijana wanaotekeleza mradi wa kutengeneza skonzi na biskuti katika kituo cha AICT Ngokolo akionesha moja ya mitambo waliyonayo katika kituo hicho. 
  Kijana James Emmanuel akionesha mtambo wa kupasulia mbao katika kituo cha AICT Ngokolo.Alisema huwa wanatengeneza samani mbalimbali kama vile stuli,viti na vitanda. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimia watoto katika kanisa la AICT Ngokolo 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa amevaa mkoba uliotengenezwa kwa vitambaa laini katika kituo cha kanisa la TAG Shinyanga Mjini. 
  Kijana Rebeca Jeremiah akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro,moja ya vitambaa laini kwa ajili ya wanawake kujistiri wakiwa katika hedhi 'Pad' ambazo amekuwa akizitengeneza na kuziuza.Rebeca alisema pedi hizo unaweza kuzifua 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia pedi ambayo unaweza kuifua na kuitumia mara nyingi.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpongeza Rebeca kwa ubunifu wa kutengeneza pedi.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiwa katika kanisa la PAG Kambarage wakisalimiana na watoto
  Kulia ni watoto wakiwa katika kanisa la PAG Kambarage 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengezwa na watoto katika kituo cha kanisa la KKKT Shinyanga mjini. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kutoka kwa watoto kuhusu namna wanavyotengeneza sabuni kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani na ofisini. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati akiangalia mitambo ya umeme iliyotengenezwa na watoto katika kituo cha KKKT Shinyanga mjini 
  Hapa ni katika ukumbi wa kanisa la KKKT usharika wa Ebenezer kanisa kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria: Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wa kikao cha majumuisho ya ziara yake kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga. 
  .
  Katibu wa wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Thomas Faida akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga. 
  Msimamizi wa vituo vya huduma ya mtoto klasta ya Kanda ya ziwa,Emmanuel Pando akizungumza katika kikao hicho. 
  Katibu Mkuu wa kanisa la KKKT usharika wa Ebenezer kanisa kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Happiness Gefi akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga. 
  Mwenyekiti wa Wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la TAG Shinyanga akizungumza wakati wa kikao cha kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini.

  Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani na ambapo Kitaifa siku hii inaadhimishwa Mkoa wa Kusini Unguja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni mgeni rasmi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwa kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini.

  Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani na ambapo Kitaifa siku hii inaadhimishwa Mkoa wa Kusini Unguja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni mgeni rasmi.


  0 0


  Maelfu ya Wanafunzi waliojitokeza katika hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa Vyuo vikuu Mwaka wa Kwanza DAR FRESHERS PARTY 2017,iliyofanyika jana nje ya Mlimani City katika viunga vya kupaki Magari huku usiku huo ukipambwa na Wasanii mbalimbali.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametangaza Punguzo la Bei (Discount) la 70% kwa Bidhaa zote zinazopatikana Ndani ya Maduka Mlimani City kwa muda wa Wiki moja kuanzia Leo.

  Punguzo hilo la bei ni kwa Wananchi Wote ikiwa ni zawadi ya RC MAKONDA Kuelekea Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya ili kuwapunguzia Wananchi makali ya gharama.

  RC MAKONDA amesema hayo kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa Vyuo vikuu Mwaka wa Kwanza DAR FRESHERS PARTY 2017,iliyofanyika jana nje ya Mlimani City katika viunga vya kupaki Magari ambapo amesema tamasha hilo litakuwa likifanyika kila Mwaka kwa kushirikisha Wasanii wakubwa kutoka Ndani na Nje ya Nchi.

  Ameshukuru Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo TBC, E. FM na E TV pamoja na Channel Ten kwa kufanikisha Tamasha hilo.

  Aidha amewashukuru wasanii mbalimbali wakiwemo WCB, AY, FID Q,  RUBY, KASSIM MGANGA, MWANA FA,  RAY C, LADY JAYDEE, MSAMI, CHRISTIAN BELLA, DULY SYKES na MRISHO MPOTO kwa kujitolea kutoa Burudani bila Malipo.

  Amesema Lengo la Tamasha hilo ni kujenga umoja kwa kuwakutanisha wanafunzi wa Vyuo mbalimbali kubadilishana mawazo  na kupatiwa maarifa.
  Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Mrisho Mpoto akitumbuiza jukwaani kwa madaha,huku pichani kulia Mkali wa kughani Mashari Mrisho Mpoti akichagiza na umahiri wake wa Mashairi.
  Baadhi ya Askari wakiwa katikati ya kundi kubwa la Wanafunsi wa Vyuo,wakihakikishiwa ulinzi wao huku wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri jukwani kwa usiku ule
  Mmoja wa Wasanii kutoka kundi la WCB akitumbuiza jukwaani.
  Ilikuwa ni shangwe,vifijo na nderemo tuu
  Mwanadada machachari katika anga ya muziki wa bongofleva kutoka kundi la WCB,Queen Darleen akiimbo wimbo wake aliouachia hivi karibuni ujulikanao kwa jina la 'ntakufilisi'.
  Msanii mwingine mahiri kabisa kutoka kundi la WCB,Ray Vann aka Vanny Boy akiwakuna vilivyo maelfu ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali,kwenye pati yao ya ukaribisho iliyofanyika usiku wa kuamkia leo nje ya Mlimani City,jijini Dar Es Salam
  Mkali mwingine wa kucheza na sauti Cassim Mganga akitumbuiza
  Mzee wa Masauti Christian Bella akiwaimbisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali kwenye siku yao maalum ya kukaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda
  Msanii mkongwe katika anga ya bongofleva Rehema Chalamila a.k.a Ray C akitumbuiza jukwaani
  Burudani murua kabisa kutoka kwa wasanii mbalimbali ilitolewa

  0 0

   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifanya usajili wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
   Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiteta jambo wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. Wakiongozwa na Mhe. Ritta kabati (kulia)
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Ndg. Rwigema Celestin (katikati) wakielekea kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson na wa pili kushoto ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Ndg. Edwin Rutageruka
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (aliesimama) akiwatambulisha  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
   Mgeni Rasmi Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ndg. Benard Konga (kulia) wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. NHIF ni watoaji huduma ya afya kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   Wageni Mbali mbali kutoka nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
   Wageni Mbali mbali kutoka nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam.
  Spika waBunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Mbali mbali kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Saba saba hall uliopo Saba saba Mjini Dar es Salaam. watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai

  0 0

    NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
  WAKATI Mwaka 2017 ukifikia ukingoni taasisi mbaliombali nchini zimeanza kuwakusanya watumishi wake na kufanya tathmini ya utendaji na kujadili namna ya kuzikabili changamoto walizokutana nazo ili hatimaye kuongeza ufanisi mwaka ujao 2018.
  Miongoni mwa taasisi hizo ni Mwalimu Commercial Bank, (MCB), ambao wamekutana jijini Dar es Salaam, ili kufanya tathmini ya kiutendaji na kuweka mikakati mipya waingiapo mwaka 2018.
  Wafanyakazi hao kutoka idara mbalimbali wakiongozwa na Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi pia walipatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali ya kiuwajibikaji katika maeneo tofauti kutoka kwa mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka.
  Ili kuonyesha ushirikiano wafanyakazi hao walibadilishana zawadi mbalimbali ambapo kila mfanyakazi alimuandalia zawadi mfanyakazi anayemvutia zaidi kiutendaji.

   Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
  Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
  Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
   Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.
    Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.
    Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.

   Meneja Msoko, Bi. Rahma Ngassa

  Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.

   Msaidizi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Furaha Johnson, akisaini kwenye makubaliano ya kimkakati ambayo kila mfanyakazi atawajibika
   Mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka. akitoa mada.
   Wafanyakazi wakiwa kwenye kikundi wakijadiliana.
  Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, (mwenye t-shirt ya mistari, akiungana na wafanyakazi wenzake katika majadiliano ya vikundi.
   Mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka. akitoa mada.
   Picha ya pamoja.  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini.

  Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani na ambapo Kitaifa siku hii inaadhimishwa Mkoa wa Kusini Unguja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni mgeni rasmi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwa kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini.

  Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani na ambapo Kitaifa siku hii inaadhimishwa Mkoa wa Kusini Unguja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni mgeni rasmi.
   Baadhi ya Walemavu wakielekea  kusherehekea siku yao Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani,ambapo leo kitaifa inafanyika Mkoa wa Kusini Unguja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni mgeni rasmi.

  0 0

  Mwenyekiti anayemaliza muda wake wachama cha mapinduzi mkoa wa ruvuma ODDO KILLINI MWISHO amesema chama hicho katika mkoa wa ruvuma kimekubwa na ukabila kwa baadhi ya ujumbe wa chama hicho,baada ya kuonekana baadhi ya wilaya zimekuwa na ukabila.hayo ameyasema kabla ya uchaguzi mkuu wa chama hicho mkoa wa RUVUMA kufanyika leo ukisimamiwa na waziri husseni mwishi ambaye pia mlezi katika mkoa huo, huku naye akiomba ridhaa ya kurudi tena madarakani kuweza kukitumikia kwa miaka mitano tena ijayo.

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu yaTaifa ya  CCM,  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano Mkuu wa CCM wa Mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea, Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea, Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea, Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Lindi aliyen'gatuka, Ali  Mtopa baada ya kufungua mkutano mkuu wa CCM wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mini Ruangwa, Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati alipotembelea bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2, 2017. 
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati alipotembelea Bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2, 2017.Kulia kwake ni binti yake, Zuleikha Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Watoto wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakiimba wimbo wa Shule yao katika Mahafali ya Kwanza ya Shule hiyo iliyopo Ruangwa Mjini Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Wahitimu wa wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakicheza ngoma ya asili katika Mahafali ya Kwanza ya Shulel hiyo iliyopo Ruangwa Mjini Desemba 2, 2017. 
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa , Bw. Craig Ferla ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Children in Crossfire akimkabidhi cheti kwa mhitimu wa Mafunzo ya Awali katika shule hiyo, Jasmine Madamba, Desemba 2, 2017.Wapili kuil ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
  Baadhi ya wazazi na waalikwa wa Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mjini Ruangwa wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza katika Mahafali hayo Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewaomba wazazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wahakikishe wanatumia sehemu ya kipato chao katika kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao.

  Amesema elimu ndiyo jambo pekee linaoweza kumsaidia mtoto katika kutimiza ndoto zake za maisha pamoja na kumtoa katika kundi la wategemezi.Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumamosi, Desemba 2, 2017), katika maafali ya shule ya awali na msingi ya Wonder Kids, iliyopo wilayani Ruangwa, Lindi.Mke wa Waziri Mkuu alialikwa katika maafali hayo kama mdau wa elimu. Maafali hayo yaliyohusisha watoto wa awali ambao wanaingia darasa la kwanza.

  “Walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri, hivyo wazazi watumie kipato chao kuwekeza katika elimu kwani faida watakuja kuiona baadaye.”Alisema kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo anatambua kuwa walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri na wanakuwa na tabia nzuri, hivyo wazazi hawana budi kushirikiana nao.

  Pia Mama Mary alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawatie moyo walimu kwa sababu kazi wanayoifanya ni kubwa. “Wote ni mashahidi watoto wetu tulivyowaleta na sasa ni tofauti.”Alisema ni vizuri wazazi wakashiriki kikamilifu katika suala la elimu kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya masomo yao badala ya kuwaachia walimu peke yao.

  Kwa upande wake ,mgeni rasmi katika maafali hayo ambaye ni Muwakilishi Mkazi wa Children in Crossifire Bw Craig Ferla aliwapongeza wanafunzi hao kwa kutimiza moja ya hatua katika safari yao ya elimu na aliwasihi waendele kupenda kwenda shule na kusoma kwa bidii.

  Pia aliwapongeza wazazi kwa kutambua umuhimu wa elimu ya awali na kuwapeleka watoto wao kwenye shule hiyo ya Wonder Kids. “Wonder Kids ni mahali sahihi ambapo mtoto anapata elimu na malezi bora.Alisema elimu ya awali ninzuri kwa mtoto kwa kuwa inawawezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, hivyo aliwaeleza Wanaruangwa kutumia vizuri fursa ya uwepo wa shule hiyo katika wilaya yao.

  Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bibi Nancy Tausi alisema Wonder Kid ilianzishwa Januari, 2017 ikiwa na wanafunzi 117 ambao ni wa kuanzia darasa la awali hadi darasa la tatu.Alisema lengo la kuanzisha shule hiyo ni kuhakikisha watoto wanapata kujua kusoma vizuri na kwamba wanatarajia kuanzisha darasa la kompyuta kwa ajili ya watoto kujifunza TEHAMA pamoja na kuanza kufundisha lugha ya Kifaransa.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza wakati Mahafali ya Shule Mikocheni Islamic ambapo aliwaasa wazazi kuwekeza katika kuwapatia watoto elimu ya Duniani na dini hili waweze kuja kuwa watumishi waadilifu baadae pindi wanapokuja kuwa viongozi wa Umma.
  Katibu wa Shule ya Mikocheni Islamic akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo katika mahafali ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic Jijini Dar es Salaam

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akikagua Maonesho ya kisayansi ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakati wa mahafali ya Darasa la Saba ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
  Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakionesha Umahiri wao wa kuimba Kaswida mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi  ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kitengo cha Sayansi na walimu wao wa shule ya Msingi Mikocheni Islamic.

  0 0

  Na Mathias Canal, Mbeya.

  Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Leo Disemba 3, 2017 amewasihi Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kuchagua viongozi makini, weledi, wenye nidhamu na kipawa cha uongozi.

  Mhe Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akitoa salamu za wabunge Wa Mkoa Wa Mbeya kwenye Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya.

  Alisema kuwa wajumbe hao hawapaswi kuchagua viongozi kwa sababu ya kufahamiana, Urafiki, Ujamaa au Undugu badala yake wanapaswa kuchagua viongozi wenye maono na mtazamo chanya ili wawe mfano bora katika kukiimarisha na kukijenga Chama Cha Mapinduzi.

  Mbele ya wajumbe hao Mhe Mwanjelwa kwa ushirikiano na wabunge wote Wa Mkoa Wa Mbeya wamempatia zawadi ya Pawatila Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kwa ajili ya Kilimo cha kisasa ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na ufanisi Wa uongozi wake kama Mwenyekiti katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2012-2017.

  Alisema kuwa Zawadi hiyo inayogharimu fedha za kitanzania takribani Shilingi Milioni Tano ni michango ya wabunge hao kwa Mwenyekiti huyo kutokana na uhodari wake katika kuimarisha Chama katika Mkoa Wa Mbeya sambamba na kuyavunja makundi yote yaliyokuwepo wakati Wa uchaguzi Mkuu Wa mwaka 2015.

  Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu Wa Mkoa Wa Lindi Mhe Godfrey Zambi alimpongeza Naibu Waziri Wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kusafiri usiku wa manane kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano huo pamoja na kuwa na majukumu mengi ya kiserikali Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.

  Zambi alisema Kuwa kitendo cha Mhe Mwanjelwa kushiriki katika Mkutano huo kimeonyesha mfano bora na umakini katika kuheshimu Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

  Kwa upande wake Msimamizi Mkuu katika Mkutano huo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Antony Peter Mavunde aliwataka wajumbe hao kuchagua viongozi wenye uwezo Wa kuwasaidia wanachama na wananchi katika kuchagiza shughuli za maendeleo.

  Aidha, alisema uchaguzi huo unapaswa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi.Mkutano huo utamalizika kwa kuchagua Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mbeya na Mjumbe Wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.
   Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza  na wajumbe wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
   Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
   Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana  na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
   Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
   Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa salamu za wabunge wa Mkoa wa Mbeya wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata na Kaimu Meneja wa pori hilo, Stanslaus Odhiambo.

  Na Hamza Temba, Mbarali - Mbeya.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kukamilisha malipo ya fidia ya shilingi milioni 771.6 kwa kaya 308 za Kitongoji cha Machimbo ili ziweze kupisha eneo la hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.

  Naibu Waziri Hasunga ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara baada kutembelea kitongoji hicho katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi mkoani humo.

  “Kaimu Mkurugenzi (TAWA) kama unavyoona wananchi hawa wapo tayari kupisha eneo hili la hifadhi, wanachosubiri ni malipo yao ya fidia, naagiza mpaka ifikapo mwezi Februari mwakani (2018) wawe wameshalipwa fidia zao, na ikiwezekana hata ndani ya mwezi Januari wawe wameshalipwa,”alisema Hasunga.

  Awali akiwasilisha taarifa ya pori hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, David Kenyata alisema wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 2002 kwa Tangazo la Serikali Na. 483 wananchi wa kitongoji hicho na vitongoji vingine walikuwa ndani ya eneo hilo la hifadhi.

  Alisema mazungumzo yalishafanywa kupitia vikao halali vya uongozi wa viijiji na halmashauri ambapo wananchi hao waliridhia kulipwa fidia ili kuachia maeneo hayo ya hifadhi.

  Alisema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa pori hilo ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji yanayotiririka kwenda mto Ruaha na kwenye mabwawa ya kidatu na mtera yanayotumika kuzalisha umeme nchini.

  Akizungumzia malipo ya fidia kwa vijiji na vitongoji vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo alisema kijiji kimoja kilishalipwa mwaka 2015 jumla ya shlingi milioni 500 na vijiji vilivyosalia vitalipwa kwa awamu ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 fedha zimetengwa kwa ajilia ya kulipa wananchi wa kitongaoji cha Machimbo ambao tayari walishafanyiwa uthamini mwaka 2015.

  Awali akizungumza na watumishi wa Pori hilo katika ofisi zao zilizopo Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, Naibu Waziri Hasunga aliwataka watumishi hao kuongeza nguvu na ubunifu kwenye kuzuia mifugo isiiingie hifadhini badala ya kusubiri iingie ndipo waikamate na kuitoza faini au kuitaifisha.

  “Nyie ni watalaamu, tumieni mbinu na ubunifu wenu wote muhakikishe mnazuia mifugo isiingie hifadhini, sitaki kusikia mmekamata au mmetaifisha mifugo hifadhini, hiyo siyo sifa, sifa ni kuzuia isiingie kabisa, na nitawapima kwa hilo,” alisema Hasunga.

  Aidha aliwataka watumishi hao kuimarisha uhifadhi shirikishi, kujiepusha na vitendo vya rushwa, kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kuongeza ubunifu utakaowezesha ongezeko la mapato ya Serikali.

  Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo aliwatembelea wananchi wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Igomelo ambao awali waligomea zoezi la uwekwaji wa vigingi vya mpaka kwenye eneo lao na Pori la Akiba la Mpanga Kipengele kwa hofu ya kupoteza maeneo hayo.

  Hata hivyo baada ya kuwaelimisha kuwa lengo la zoezi hilo ni kuiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa mwisho wa kumaliza migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu baina ya vijiji na maeneo ya hifadhi nchini wananchi hao walielewa na kuahidi kushirikiana na mamlaka husika kukamilisha zoezi hilo kwa muda uliopangwa.  

  Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Pori hilo, Stanslaus Odhiambo alisema pori hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uwepo wa vijiji na vitongoji 13 ndani ya pori hilo, uchomaji moto maeneo ya hifadhi, ukataji miti hovyo, ujangili na uhaba wa vitendea kazi.

  Pori la Akiba la Mpanga Kipengele lina ukubwa wa Kilometa za mraba 1574.25 katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na Wilaya za Wanging’ombe na Makete Mkoani Njombe.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (waliokaa mbele katikati) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe.
  Baadhi ya watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (hayuko pichani).
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akisalimiana na Kaimu Meneja wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengele, Stanslaus Odhiambo muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya jana ambapo aliiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania kuwalipa fidia ya shilingi milioni 771.6  kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.
  Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye aliwatembelea jana na kuagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania iwalipe fidia ya shilingi milioni 771.6 kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele alipowatembelea.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na wananchi wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Igomelo, wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ambao waligomea zoezi la uwekwaji wa vigingi vya mpaka kwenye eneo lao na Pori la Akiba la Mpanga Kipengele kwa hofu ya kupoteza maeneo hayo. Baada ya kuwaelimisha wananchi hao walikubali kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika ili kukamilisha zoezi hilo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao. Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (hayupo pichani).
  Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao.

  wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma wakinyoosha mikono juu baada ya kuulizwa wangapi wanataka kurudi nchini kwao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara ikiwa ni ziara ya kikazi ya naibu waziri kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika uwanja ulipofanyika mkutano wa hadhara uliowahusisha wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma. Ziara hiyo lengo lake ni kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakiagana baada ya kumaliza kuzungumza na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma. Ziara hiyo lengo lake ni kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

  Mwekezaji mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO amesema amejipanga kushirikiana na wanahisa wenzake wa klabu hiyo kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia kampuni ya Simba Sports Club Limited.Dewji aliyasema hayo wakati akitoa salamu kwa wanachama na mashabiki wa Simba kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo, baada ya kutangazwa na kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba, kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo.Alisema klabu ya Simba inampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongoza serikali ya awamu ya tano, na wao wamedhamiria kuhakikisha wanakwenda sambamba na kasi yake kupitia mchezo wa mpira kwa kutoa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mpya itakayosimamia timu hiyo katika mfumo wa hisa.Mwekezaji mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere."Tamati yangu nielekeze kwa sisi sote kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya ya kuongoza taifa hili. Wote tumtakie kila la kheri, baraka na fanaka tele katika utumishi wake uliotukuka,"Pamoja na kupongeza sera yake ya ujenzi wa viwanda nchini, ambapo sisi kwa upande wetu, klabu ya Simba inamuunga mkono kwa ujenzi wa kiwanda kikubwa kabisa cha soka yaani Simba Sports Club Limited, ambacho licha ya kuongeza ajira lakini pia tutaendelea kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi," alisema Dewji.Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises, alitumia mkutano huo kuelezea mipango ambayo wameipanga ili kuiwezesha Simba kuwa klabu kubwa zaidi barani Afrika kuliko ilivyo sasa, huku malengo ikiwa ni kuwania mataji makubwa barani Afrika.
  Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah akimkabidhi cheti cha ushindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu ya Simba mfanyabiashara na mwanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo, Mohammed Dewji MO kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

  "Katika mwaka wa kwanza, nawaahidi kwa kushirikiana na ninyi tutakuwa na kiwanja cha nyasi asilia, na kiwanja cha nyasi za bandia ambapo viwanja hivi tutavitumia kwa mazoezi kwa kadri ya mahitaji ya mechi tunayokwenda kucheza,"Pia tutajenga hosteli ambayo itakuwa na vyumba 35 ambavyo wataishi wachezaji 30 na support staff, kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 35 square- meter... ili kufanya eneo hilo kuwa bora kwa wachezaji wetu," alisema Dewji na kuongeza."Wote tunaopenda mpira, tunajua kama ukitaka kuwa na wachezaji bora lazima utumie pesa. Nia yetu kwa mwaka wa kwanza, tunatarajia kiwango cha chini cha pesa ya usajili iwe bilioni moja. 

  Pia tumetenga milioni 500 kuboresha benchi la ufundi, kwa kushirikiana na benchi liliopo sasa."Hata hivyo Dewji, alisema klabu ya Simba itajenga kituo cha kukuzia vipaji ambacho kitakuwa na wachezaji vijana. Jambo ambalo litaisaidia Simba kuwa na wachezaji bora vijana ambao wamefundishwa kucheza soka katika kituo cha timu hiyo."Ili kuwa na wachezaji bora kwa miaka ijayo tunahitaji kuwa na kituo cha kukuzia vipaji kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 14, 16, 18. Na mipango yetu ya baadae ni kushirikiana na timu kubwa za ulaya kutuongoza na kutuelemsha jinsi gani ya kujenga kituo chenye hadhi ya kimataifa na mungu akipenda tutakuwa na kituo bora barani Afrika." alisema Dewji.
  Baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba wakishangilia baada ya kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba kumtangaza Mohammed Dewji MO kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaju ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza juzi katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha ambapo pamoja na mambo mengine amewaonya wahitimu nchini kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani hawatabaki salama katika utawala huu. (Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
   Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha uhasibu Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo ya chuo cha Uhasibu Arusha katika mahafali chuoni hapo juzi

  Mkuu wa kitivo cha uhandisi,mazingira na Computer Paul David Greening kutoka Uingereza akizungumza katika mahafali yao juzi katika Chuo cha Uhasibu NjiroArusha
  Kushoto ni mgeni rasmi ambaye ni NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaju akisoma maelezo mafupi ya chuo cha Uhasibu Njiro Arusha katika mahafli juzi chuoni hapo   Wahitimu wakifatilia mahafali hayo kwa ukaribu zaidi

   Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja,wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro,Dk.Faraji Kasidi akiteta jambo Naibu  Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaju katika mahafali chuoni hapo juzi.
  Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi

  Baadhi ya watumishi wa chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi juzi katika mahafali chuni hapo

  Na Pamela Mollel,ARUSHA 
  NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaju ametoa onyo kali kwa  wahitimu wa Uhasibu nchini kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani hawatabaki salama katika utawala huu. 


  Akizungumza juzi  katika mahafali ya 19 katika Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha, wakati akitunuku vyeti vya ngazi mbalimbali viiwemo vya Uhasibu kwa wahitimu 1324, Dk.Ashatu alisema baadhi ya wataalamu wa Uhasibu wanachangia kurudisha nyuma Maendeleo kwa tamaa zao.


  Alisema ni vema watumie elimu waliopata kubuni ajira na pale watakaotoa ajira wafanye kwa weledi na uadilifu.Alisema endapo wataalamu hao watabadilika na kuwa na uadilifu itawezesha Taifa kufanikisha ndoto yake ya kufikisha uchumi wa Viwanda kabla ya mwaka 2025.


  Aidha alipongeza Chuo kuwa wabunifu wa kuongeza kozi kulingana na huhitaji wa jamii hadi kufikia 33 ikiwemo ya Shahada mpya ya Kijeshi ilioanza kutolewa mwaka huu.Kuhusu ombi la ujenzi wa Hosteli na kumbi za Mihadhara, alisema serikali itazitatua kulingana na jinsi wanapopata fedha,japo alishauri uongozi wa Chuo kuhakikisha sekta  binafsi wanaona watawasaidiaje.


  Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro,Dk.Faraji Kasidi alisema mwaka huu wameadhimisha  Mahafali  ya 19 ya Chuo hicho na ya nane ya Chuo hicho Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Coventry ya Uingereza.


  Alishukuru serikali kwa kutoa mikopo kwa nusu ya wanachuo wa mwaka wa kwanza 2017 na kufanikisha ndoto kwa watoto maskini.


  0 0

   Kamati ya Maandalizi ya Bonanza la Familia za Wafanyakazi wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), ikiwa katika picha ya pamoja wanati wa sherehe hiyo, iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es salaam.

  Katika Bonanza hilo, wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na familia zao walishindana katika michezo mbali mbali, ikiwemo ya mpira wa miguu, kivuta kamba, kuogelea, kukimbia na magunia na mingineyo huku watoto walitoana jasho katika kulisakata dansi na kuogelea huku wengine wakiondoka na zawadi kemkem.

  Akizunguma katika Bonanza hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Jared Zerbe alisema lengo kubwa la Siku hiyo ilikuwa ni kuwakutanisha wafanyakazi na familia zao ziweze kufurahi kwa pamoja na pia kusherehekea kuuaga mwaka na kujiandaa kuukaribisha mwaka mpya katika kazi zao.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Jared Zebre (wa nne kulia) akikabidhi kikombe kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo waliounda timu ya Mameneja baada ya kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya wakanyakazi wa ngazi y chini, katika mchezo wa Bonanza la Familia za Wafanyakazi hao, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam. wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa na kushoto ni, Meneja Utekelezaji wa Kampuni hiyo, Patrick Kusiga.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Jared Zebre (pili kushoto) akipikea tuzo maalum kutoka kwa viongozi wa Kamati ya Maandalizi ya Bonanza la Familia za Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Erik Sazs akijaribu kuuzuia mpira bila mafanikio katika mchezo wa Bonanza la Familia za Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkali wao akiondoka na mpira .
  Mkuu wa Kitengo cha Uhandishi wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Cornelis Kwadjik akijaribu kumkoka mmoja wa wachezaji wa timu ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, katika bonanza la familia za wafanyakazi hao, lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
  Mpira wa Wavu
  Kuvuta kamba.


  0 0


  0 0

  Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2017 Mama wa mitindo maarufu hapa Tanzania kama Asya Idarous Khamsin, ambaye kwa sasa makazi yake ni nchini Marekani.  Ifikapo December 9th 2017  ataiwakilisha Tanzania kwa kuonyesha mitindo yake kwenye sherehe za uhuru Oakland Carlifonia.

  Hivyo tukiwa kama Watanzania ni jambo la kujivunia maana Tasnia ya mitindo imekuwa ni moja kati ya vyanzo vizuri vya kuitangaza nchi yetu. Tunapaswa kuonyesha ushirikiano kwa wabunifu (Designers)  wetu wanao jituma kama Mama yetu Asya Idarous Khamsin na wengineo.

  Ukiguswa unaombwa kusambaza ujumbe huu kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wanao penda Fashion  Asante.


  0 0


  Katibu wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa RUVUMA AMINA IMBO amehapa kuwashukulia hatua kali wanachama wa chama hicho wanaojihusisha na utoaji rushwa wakati wa uchaguzi  ,amesehayo wakati wa kuwachagua viongozi wa chama hicho katika ukumbi wa shule ya WASICHANA SONGEA habari kamili hii hapa video yake.

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Kakunda akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara yake. Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akitoa neno wakati wa kikao hicho.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba akifungua kikao kwa ajili ya Mhheshimiwa Naibu Waziri kuzungumza na watumishi. 
  Watumishi wa Halmashauri ya Kishapu na viongozi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.
  Naibu Waziri TAMISEMI, Mh. George Kakunda akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kishapu.


  Na Robert Hokororo, Kishapu DC

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Kakunda amewakumbusha watumishi wa umma uwajibika wenye tija katika maeneo yao ya kazi huku akisisitiza kila idara ina umuhimu wake.

  Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mh. Kakunda alisistiza kwa kusema mtumishi anapaswa kuyajua vyema majukumu yake anayopangiwa na mkuu wake wa kazi.

  Alisema lazima uthibitishe kuwa unatimiza majukumu yako kwa kutekeleza maagizo yote yanayotolewa pamoja na miongozo yote inayokuwepo, sera, programu za nchi pamoja na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali. 

  “Mtumishi lazima ujue kila kitu ‘at a finger tip’ kilichopo katika dawati lake, Mkurugenzi nae anapaswa kujua kila kitu kinachohusu Halmashauri yake. Kama mtu hujui makujumu yako ina maana hata ukienda likizo pengo lako halionekani,” alisema.

  Aliwakumbusha wahasibu hasa katika utunzaji nyaraka za mahesabu na wagavi kutimiza wajibu wao kwa umakini kuepuka hoja huku akionya atakayezalisha hoja atajibu yeye mwenyewe kama ambavyo sheria ilivyopitshwa mwaka jana na si Halmashauri kama ilivyozoeleka 

  Naibu Waziri pia aliwatasisitiza wahandisi waache mazpea ya kukaa ofisini na kusubiri ripo bali watoke wakague miradi wenyewe na kutembea na nyaraka zinazohusu miradi hiyo badala ya kumuachia Afisa Mipango mwenyewe.

  Awali akizungumza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela aliwataka watumishi kujenga utaratibu wa kutembelea wananchi kujua kero zao badala ya kukaa ofisini kusubiri wawafuate.

  Alisema kuwa lengo la viongozi wa mkoa ni kumkumbusha kila mtumishi kwenye halmashauri yake anafanya kazi kwa weledi na kutekeleza taratibu na sheria za utumishi wa umma.

older | 1 | .... | 1449 | 1450 | (Page 1451) | 1452 | 1453 | .... | 1897 | newer