Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

BALOZI SEIF IDDI MGENI RASMI BARAZA LA MAULIDI RUANGWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Wanawake Waislaam Tanzania, Shamim Khan baada ya kushiriki Katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likanglal wilayani Ruangwa Desemba 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia washiriki wa Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya kushiriki Baraza hilo kwenye uwanja wa Shukle ya Msingi Likangala wilayani Ruangwa Desemba 1, 2017.
Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati alipohutubia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Ruangwa Desemba 1, 2017
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya (wapili kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Wanawake Waislaam, Shamim Khan wakati alipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala kushiriki katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S. A.W). Mgeni Rasmi kaaika Baraza hilo alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mgeni Rasmi katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W), Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kuingia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Rungwa Desemba 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mgeni Rasmi katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W),Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani RUangwa Desemba 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Rungwa Desemba 1, 2017. Mgeni Rasmi katika Maulidi hayo alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wapili kushoto) na baadhi ya Viongozi walioshiriki katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) wakimsikiliza Mgeni Rasmi Balozi Seif Ali Iddi wakati alipiwahutubia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Ruangwa Desemba 1, 2017. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Wanawake Waislaam Tanzania, Shamim Khan, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Ikupa Stella Alex , Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na Mbunge wa Viti Maalum,Hamida Muhammad Abdallah
Askofu Mkuu, Bruno Ngonyani wa Jimbo Katoliki la Lindi akizungumza katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Ruangwa, Desemba 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mgeni Rasmi katika Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W),Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani RUangwa Desemba 1, 2017. Kushoto ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubacary Zubeiry Ally.


Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa

$
0
0
Bibi Prisca Mwingira ambaye alifanyiwa upasuaji wa kupandikizwa figo Novemba 21, mwaka huu akiishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), madaktari bingwa wa hospitali hiyo pamoja na Rais John Pombe Magufuli baada ya afya yake kuendelea vizuri. Bibi Prisca ameruhusiwa kurejea nyumbani leo saa 6:00 mchana baada madaktari bingwa wa magonjwa figo kufanikisha upasuaji huo wa kihistoria. Kulia ni Bathelomayo Mwingira ambaye amempatia dada yake figo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Jacqueline Shoo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo Dkt. Kisanga (katikati), wote wa Muhimbili.
Bibi Prisca Mwingira akimshukuru kaka yake, Bathelomayo Mwingira kwa kumpatia figo kutokana na tatizo hilo kumsumbua katika kipindi cha mwaka mmoja.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakishudia tukio hilo lakihistoria ambalo limefanywa na madaktari bingwa wa Muhimbili.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Jacqueline Shoo akizungumza na waandishi wa habari baada ya Bibi Prisca kuruhusiwa kurejea nyumbani kutokana na afya yake kuendelea vizuri.
Baadhi ya wananchi wakishudia tukio hilo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mzazi wa Bibi Prisca, Mzee Mwingira akiwashukuru madaktari wa hospitali hiyo kwa kufanikisha upasuaji huo na sasa mtoto wake anaendelea vizuri kiafya.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

………….

Dar es salaam, Tanzania. Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kihistoria wa kupandikizwa figo leo ameruhusiwa kutoka katika hospitalini akiwa na afya njema.

Bibi Prisca Mwingira ambaye amefanyiwa upasuaji mkubwa na wa kwanza kufanyika hapa nchini alipandikizwa figo Novemba 21, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) chini ya timu ya wataalam wa MNH kwa kushirikiana na watalaam wa Hospitali ya BLK ya nchini India.

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Bibi Prisca amewashukuru watalaamu wote walioshiriki katika kumuhudumia na pia ametumia fursa huyo kumuomba Rais John Magufulu kuendelea kuisaidia MNH ili kuhakikisha huduma za kibingwa wa juu zinaendelea kutolewa katika hospitali hiyo.

“Kipekee namshukuru mwenyezi Mungu, madaktari , wauguzi, uongozi wa Hospitali ya Muhimbili pamoja na serikali kwa kufanisha matibabu yangu, nilisumbuliwa na ugonjwa wa figo takribani mwaka mzima na kuingia katika matibabu ya kuchuja damu, lakini hatimaye leo kaka yangu amejitolea figo yake moja na nimewekewa mimi kwa kweli namshukuru sana.

“Napenda kuwashauri wagonjwa wenye matatizo ya figo na wanaoendelea na huduma ya kuchuja damu wasikake tamaa kwani sasa matibabu yamepatikana na mimi ni shuhuda katika hili,’’ amesema Bibi Prisca.

Kwa upande wake, Bwan Bathelomayo Mwingira ambaye amemtolea figo dada yake, amesema anafuraha kwani amesaidia kufanikisha matibabu ya dada yake na anamuomba Mungu afya ya dada yake izidi kuimarika.

Pia, Baba mdogo wa Prisca , Ainhard Mwingira ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kufanikisha huduma za kibingwa kutolewa Muhimbili.

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya figo, Dkt. Jackline Shoo wa Muhimbili amesema upasuaji wa kupandikiza figo ulitumia takribani saa nne na zoezi hilo limekamilika vizuri na mgonjwa anarejea nyumbani huku afya yake ikiwa salama.

“Mgonjwa anaondoka Hospitalini akiwa mzima salama kabisa , anaenda kujumuika na familia yake ataishi kama binadamu wengine ingawa kuna masharti atatakiwa kuyafuata kama alivyoshauriwa na wataalam,” amesema Dkt. Shoo.

Pia, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hudma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha amesema upasuaji huo umegharimu Shilingi Milioni 21 na endapo mgonjwa angepelekwa nchini India matibabu yake yangegharimu Shilingi Milioni 80 hadi Shilingi milioni 100.

“Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili nawapongeza watalaam wote walioshiriki katika upasuaji huu mkubwa na wa kihistoria na pia naishukuru serikali kwa kufanikisha zoezi hili,’’ amesema.

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AHUDHURIA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD SAW ZANZIBAR

$
0
0
MAKAMU wa Rais Mstaaf Dkt Mohammed Gharibi Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati akiwasili katika viwanja vya maisara kuhuhudhuria sherehe za Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW, yaliofanyika Kitaifa katika viwanja vya maisara Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maulid ya Mfungo Sita Zanzibar Sheikh Shirali Champsi alipowasili katika viwanja vya maisara Zanzibar kuhudhuria katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaaf Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipowasili katika viwanja vya maisara kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Al Hajj Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali wakiwa wamesimama wakati wakutoa Salamu za kumkaribisha qaswida iliokuwa ikisomwa na Madrasatul E Itiswam ya Chukwani Zanzibar
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Wananchi na Viongozi wakisimama wakati wa kutoa salamu ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Alhajj Ali Mohamed Shein alipowasili katika viwanja hivyo kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)


WANAFUNZI wa Madrasatul E’itiswam ya Chukwani Zanzibar wakisoma Qwasid ya Salamu ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Al Hajj, Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya maisra Zanzibar.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alhajj Ali Mohamed Shein, alkisoma ratiba ya hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
KADHI Mkuu wa Zanibar Sheikh Khamis Haji akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar
BAADHI ya waalikwa katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) wakifuatilia hafla hiyo katika viwanja vya maisara Zanzibar.Picha na Ikulu

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland katika hafla iliyofanyika jana mkoani humo.


Na Hamza Temba-WMU-Iringa

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amefungua Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo ambacho kimeanzishwa katika Mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia mradi wa Panda Miti Kibiashara.

Akizungumza kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa kituo hicho jana mjini hapa, Naibu Waziri Hasunga ameishukuru Serikali ya Finland kwa msaada huo na misaada mingine ambayo imekuwa ikiitoa katika kuimarisha sekta ya Misitu nchini toka miaka ya 1970s. 

Alisema lengo la kituo hicho ni kusaidia kutoa elimu kwa vitendo na ujuzi kwa makundi mbalimbali ambayo yapo katika mnyororo wa kuongeza thamani ya mazao ya misitu ikiwemo watu binafsi, viwanda vya misitu na taasisi za Serikali kuanzia hatua za mwanzo za upandaji wa miche ya miti hadi kwenye hatua za mwisho za uchakataji wa magogo.

Aidha, kutokana na kituo hicho kuwa chini ya mradi huo, Naibu Waziri Hasunga amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuangalia uwezekano wa kukiweka kituo hicho chini ya Wizara yake ili mafunzo yanayotolewa yawe endelevu hata kama mradi husika utafikia ukiongoni.Pia, ameagiza mitaala ya kituo hicho ipitiwe na isajiliwe kupitia Mfumo wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi– VETA ili yaweze kutambulika na wahitimu wapewe vyeti kulingana na mahitaji ya soko katika sekta ya viwanda vya misitu nchini.

Katika hatua nyingine amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa kukagua viwanda vyote vya misitu nchini kwa ajili ya kujiridhisha kama vinakidhi vigezo vilivyowekwa na wizara ikiwemo kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi unaostahili.

Alisema uwepo wa kituo hicho cha mafunzo utawezesha viwanda hivyo kuwapatia mafunzo kwa vitendo wafanyakazi wake ambao hawana vigezo ili waweze kukidhi vigezo na ujuzi stahiki ikiwemo kuwa na Fundi Misumeno, Fundi Mwendesha Mashine ya Kuchakata Magogo na Fundi Mitambo.

Alitoa wito kwa wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na maeneo mengine nchini kujiunga na kituo hicho waweze kupata mafunzo ya kitaalamu na ujuzi wa kuotesha miti kwa njia za kisasa iweze kuzalisha mbao na samani zenye ubora zaidi.Kwa upande wa Balozi wa Finland, Mhe. Peka Huka amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha sekta ya misitu nchini iweze kutoa mchango chanya kwa jamii na taifa ujumla.

Naye Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema kituo hicho kitatoa fursa pana ya mafunzo kwa makundi mbalimbali katika sekta ya misitu nchini tofauti na vituo vingine ambavyo huitaji vigezo mbalimbali vya kitaaluma kujiunga. Alisema maelekezo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri Hasunga yatafanyiwa kazi ili kuimarisha sekta hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema Serikali ya Mkoa wake imefurahishwa kwa kuanzishwa kwa kituo hicho cha mafunzo katika mkoa wake na kuahidi kushirikiana na mamlaka zingine kukilinda na kukiendeleza. Alisema katika maeneo aliyopanga kumpeleka Mhe. Rais kwenye ziara zake mkoani humo ya kwanza itakuwa katika kituo hicho.

Toka kuanzishwa kwake mwezi Desemba mwaka jana, 2016 mpaka sasa kituo hicho cha mafunzo kimeshaandaa na kuendesha zaidi ya kozi 20 kwa ajili ya usimamizi wa misitu, afya na usalama kazini, huduma ya kwanza, ujasiriamali na ufundishaji. Wastani wa muda wa mafunzo yanayotolewa kituoni hapo ni siku nne ambapo jumla ya washiriki 400 wameshapatiwa mafunzo hayo huku wanawake ikiwa ni asilimia 35.

Aidha kwa sasa jumla ya wanafunzi 40 kutoka Chuo cha Misitu Olmotonyi na Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi wanapatiwa mafunzo kwa vitendo katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Kutoka kushoto wa tatu ni Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza. 
Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Peka Huka akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Kutoka kulia wa tatu ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi jana muda mfupi baada ya kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Wengine pichani ni Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla hiyo.


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akitoa salamu za shukurani muda mfupi jana baada ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Wengine kushoto kwake ni Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Peka Huka, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Mshauri wa Masuala ya Misitu kutoka sekta binafsi, Sangito Sumari wakati akitoa maelezo juu ya miche ya kisasa ya miti iliyoboreshwa muda mfupi baada ya kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka. 
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akiongoza hafla hiyo ya ufunguzi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akiangalia mbao zinavyoandaliwa katika moja ya karakana ya kituo hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme (wa tatu kulia).
Baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo cha Misitu Olmotonyi na Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi (wanaopunga mikono) ambao wanapatiwa mafunzo kwa vitendo katika kituo hicho.

KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA UKIMWI CHA SHUKA KWA ASILIMIA 3.5 MKOANI GEITA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwahutubia wananchi wa Kijiji na Kata ya Nyawilimilwa Wilaya ya Geita wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipanda Mti kwenye moja kati ya maeneo ambapo kuna zahanati ya kijiji cha Nyawilimilwa. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akipanda mti kwenye zahanati ya Kijiji. 
Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoa wa Geita,Dkt Joseph Odero akimuelezea Mkuu wa Mkoa ,Mhandisi Robert Luhumbi namna zoezi la upimaji linavyoendelea Kijijini hapo. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipewa maelezo na moja kati ya wahudumu wakati alipotembelea banda la huduma za afya kijijini hapo. 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita,Dkt Japhet Simeo akitoa taarifa ya Mkoa juu ya shughuli ya upimaji na watu ambao wameathirika na virusi vya Ukimwi. 
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akihutubia. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa,Mhandisi Robert Luhumbi. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akitoa msaada kwa watoto ambao ni yatima waliondokewa na wazazi kutokana na ugonjwa wa UKIMWI. 







Na Faudhia Sharifu,Geita


Jumla ya watu 1,412 sawa na asilimia 3.5 wameathirika na virusi vya ukimwi Mkoani Geita uku wanawake wakiwa ni 828 na wanaume wakiwa Ni 584.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani ambayo kimkoa yemefanyika kwenye kijiji na kata ya Nyawilimilwa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa huo Dkt Japhet Simeo amesema Takwimu za upimaji wa virusi vya UKIMWI ngazi ya jamii Jumla ya watu waliopimwa maambukizi ya VVU katika kipindi cha Aprili hadi Septemba 2017 ni 40,910 wanaume wakiwa ni 22,569 na wanawake 18,341 na ambao wamekutwa na maambukizi ni 1,412.

Na kwamba kutokana na hali hiyo Kiwango kimeendelea kupungua kutokana na mbinu na mikakati mbalimbali za Mkoa dhidi ya maambukizi ya UKIMWI.

Aidha Dkt Simeo ameongeza kuwa Jumla ya wagonjwa 65,825 ambapo wanaume ni 24,812 na Wanawake 41013 Wamekwishaandikishwa kwenye vituo vya Tiba na matunzo ,ambapo ni kuanzia 2012 – Septemba, 2017kati ya hao walioanzishwa dawa ni 52,550 wakiwemo wanaume 19296 na wanawake  33,254 na wanaoendelea na dawa (matibabu ni 32,709 wanaume 11188, na wanawake 19914) ambayo ni sawa na 62.2.

Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema kuwa kundi kubwa ambalo linaongoza kwa maambukizi ni vijana ambao wanakuwa kwenye umri wa miaka 15 hadi 25 huku wanawake na mabinti wakiongoza kwa kiasi kikubwa Mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi kwenye kijiji hicho,Devid Maduka,ameshukuru zoezi la upimaji kuwepo kijijini hapo huku akiomba serikali kutoa walau siku nyingi za upimaji.Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa yamefanyika Jijini Dar es salaam huku kauli mbiu ikisema i “Changia mfuko wa udhamini wa ukimwi okoa maisha tanzaniabila ukimwi inawezekana”

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
Mhe. Jaji Mkuu akifurahia zawadi ya picha aliyopatiwa na Mgeni wake.
Picha ya pamoja baada ya Majadiliano: wa nne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, katikati ni Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga pamoja na Wajumbe waliombatana na Naibu Waziri.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akimkaribisha Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng pindi alipowasili katika Ofisi ya Jaji Mkuu-Mahakama Kuu Zanzibar.
Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng (katikati) akiongea jambo na Mhe. Jaji Mkuu pindi alipomtembelea Desemba 01, 2017.
Majadiliano yakiendelea; pichani ni baadhi ya Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri huyo, mbali na Wajumbe hao pia kuna Wajumbe kutoka Mahakama ya Tanzania na Wizara ya Katiba na Sheria, wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria-Tanzania.
Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng akipitia nakala ya Kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) alichozawadiwa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akichangia jambo katika majadiliano baina yake na Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria wa China.


Na Mary Gwera, Zanzibar

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim H. Juma ashauri juu ya uwezekano wa kuwa na Kanuni za pamoja za Sheria ya Biashara na Uwekezaji ‘Trade Investment Regulations’ kati ya Tanzania na China zitakazowezesha ukuaji wa uchumi ambao utasaidia kuleta maendeleo baina ya nchi hizi mbili.

Aliyasema hayo, Desemba 1, katika maongezi maalum na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng, pindi alipotembelewa na Naibu Waziri huyo Mahakama Kuu-Zanzibar ambapo Mhe Jaji Mkuu anaendelea na Vikao maalum vya Mahakama ya Rufani ‘court session’

Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa; China ni nchi ambayo tayari imeshapiga hatua kubwa kiuchumi na kimaendeleo, hivyo kuwepo kwa Kanuni wezeshi za Biashara Uwekezaji baina ya nchi hizi mbili (2) utasaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania pia.

“Ni vyema kuangalia juu ya uwezekano wa nchi zetu; Tanzania na China kuwa na kanuni zinazofanana zitakazotoa muelekeo wa jinsi ya kuwekeza kwa manufaa ya pande zote mbili,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng aliafiki ushauri huo uliotolewa na Mhe. Jaji Mkuu na kumtaka kuendelea na hatua za awali za uwasilishaji wa pendekezo hilo kwa taratibu zinazotakiwa kufanyika ili kufanikisha utekelezaji wa ushauri uliotolewa.

Aidha; Mhe. Jaji Mkuu pia alimueleza Naibu Waziri huyo juu ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati unaoendelea kufanyika ndani ya Mahakama kwa kutaja baadhi ya vipaumbele ambavyo Mahakama imejiwekea ikiwa ni pamoja na utoaji wa Mafunzo kwa Watumishi wa Mahakama, Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kadhalika.

Aliongeza kuwa Mahakama ya Tanzania inakusudia pia kuwafikishia huduma ya Mahakama Watanzania wote kwa ngazi ya Kata.“Kwa sasa changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni jinsi ya kuwafikishia huduma ya Mahakama wananchi wote, tuna zaidi ya Kata 3000, lakini Mahakama ya Tanzania ina majengo ya Mahakama za Mwanzo yasiyozidi 900, hivyo Mpango uliopo ni kufikisha huduma za Mahakama kwa wananchi wote ili kuwaondolea aza za umbali pindi wanapotafuta haki zao,” alifafanua Mhe. Jaji Mkuu.

Naye, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mahakama katika uendeshaji wa shughuli zake.“China ni nchi inayoendelea kukua kiuchumi hivyo tunapaswa kutoa mchango kwa Tanzania pia ili kuendelea kukua kimaendeleo,” alisema Mhe. Zhao Dacheng.

Naibu Waziri huyo aliyeambatana na Ujumbe wa Wakurugenzi na Maafia sita (6) kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ya Watu wa China walionana na Mhe. Jaji Mkuu lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili; Tanzania na China.

WAJASIRIAMALI JIJI LA ARUSHA WAPATIWA MKOPO WA MILIONI 605

$
0
0

Na Mahmoud Ahmad,Arusha.

Jumla ya Shilingi milioni 605 zimetolewa kama mkopo wa kuwanufaisha wajasiriamali walioko kwenye vikundi vya kinamama na vijana pamoja na walemavu waliopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Akizungumzia mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Arusha, Hanifa Ramadhani amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kuwawezesha kinamama na vijana kuondokana na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili ili kuinua uchumi .

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amewataka Vijana ambao ni wasomi kujiunga katika vikundi hivyo na kupata mikopo ili kujiendeleza kiuchumi badala ya kusubiri ajira serikalini ile hali nafasi ni chache na wahitimu wa vyuo ni wengi.

Kwa upande wao Wanufaika wa Mikopo hiyo kwa niaba ya Walemavu Mwajuma Juma na Patrick Petro wameishukuru serikali kwa kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.
 Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbi wa Arusha School kupewa mafunzo kabla ya kupatiwa mikopo ya halmashauri. Picha na Ferdinand Shayo
 Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbi wa Arusha School kupewa mafunzo kabla ya kupatiwa mikopo ya halmashauri. Picha na Ferdinand Shayo 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha  Gabriel Daqqaro akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 ya mkopo wa kinamama iliyotolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha .Picha na Ferdinand Shayo

WAZIRI MHAGAMA AKABIDHIWA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU CHUO CHA UFUNDI CHA YOMBO IKIWA NI MSAADA KUTOKA SERIKALI YA KUWEIT

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya watu wenye ulemavu katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana , kulia ni Balozi wa Kuweit nchini Tanzania,  Jasem Al-Najem.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo mara alipowasili katika chuo hicho

  Balozi wa Kuwait nchini,  Jasem Al-Najem akizungumza jambo na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kushoto), wakati mmoja wa mwanafunzi wa Chuo hicho, Lenah Sauli alipokua akishona nguo

 Mkufunzi Mkuu Msaidizi  Regina Makotha (kulia) akizungumza kwa kuwapa ishara yale aliyokuwa akizungumza Waziri Mhagama
 Wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu wakiashiria kupiga makofi wakati walipokuwa wakipewa ishara na Mwalimu wao, Mkufunzi Mkuu Msaidizi  Regina Makotha (pichani hayupo) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza nao
 Balozi wa Kuweit nchini Tanzania,  Jasem Al-Najem akizungumza jambo katika hafla fupi ya kumkabidhi,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto) vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ikiea ni msaada kutoka serikali ya Kuweit, hafla iliyofanyika jana  katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana, wakwanza kushoto ni Katibu Muhutasi wa Balozi na wakwanza kulia ni Mkalimani wa Balozi, Abdallah Yahaya


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cherehani, Lenah Sauli (kushoto)

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimvisha miwani mwanafunzi wa Chuo hicho, Mandela Lamwai ambaye anasomea ufundi umeme
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi mafuta maalumu ya kujipaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi mwanafunzi wa Chuo hicho, Mandela Lamwai ambaye anasomea ufundi umeme, wa tatu kushoto ni  Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem 








HER INITIATIVE 'PANDA' WATOASEMINA SHAWISHI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU JIJINI MWANZA LEO.

$
0
0
Msanii wa Bongo Muvi na Majasiliamali na mshawishinkatika upande wa sanaa, Rose Ndauka akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza katika semina iliyofanyika leo katika chuo kikuu cha Makatifu Agustino jijini humo.
Msemaji na innovator katika fursa za kimataifa, Banji Fernandes akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya jijini Mwanza kwaajili ya kuwavutia kwa njia mbalimbali kutokana na aliyoyapitia katika maisha ya shule pamoja na maisha ya Kawaida.Pia amewashauri wanafunzi hao wa vyuo vikuu vya jijini Mwanzakusoma kwa bidii pamoja na kuwa wavumilivu kwenye vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo. Hayo yamesemwa katika semina fupi ya kuwashawishi iliyoandaliwa na Taasisi ya her initiative Present PANDA iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza leo.


 Msanii wa Bongo Muvi na Majasiliamali na mshawishinkatika upande wa sanaa, Rose Ndauka akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza katika semina iliyofanyika leo katika chuo kikuu cha Makatifu Agustino jijini humo.

 Mchekeshaji na Mshindi wa Big Brother Afrika 2014,Idrisa Sultan akizungumza leo katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
Mwanzlishi wa Taasisi ya Her Initiative Presents PANDA, Moureen akizungumza na katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza Leo.
Baadhi ya wananfunzi wa vyuo vikuu vya jijini Mwanza wakiwasikiliza watoa maada katika semina iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Augustino jijini Dar es Salaam leo.






 Selfii time
 zawadi.

AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema kuwa anakerwa na wakandarasi wasio na uwezo, ambao wamekuwa wakitekeleza miradi bila kuzingatia mikataba, ama kutoikamilisha kwa wakati au kutekeleza chini ya kiwango kwa kukosa thamani halisi ya fedha iliyotumika.

Aweso alisema hayo wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya ya Songea Vijjini, katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma na kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa baadhi ya miradi.

Naibu Waziri alisema kuwa ipo haja ya kufutiwa usajili na kutokupewa kazi yoyote nchini wakandarasi wote wababaishaji, baada ya kutoridhishwa tendaji wao katika baadhi ya miradi wilayani humo.

‘‘Hatutawavumilia wakandarasi wasio na uwezo ambao wanatuangusha, tutawafuatilia na ikiwezekana wafutiwe usajili kabisa nchini ili wasiendelee kufanya kazi mahali popote nchini, tubaki na wakandarasi wenye uwezo’’, alisema Aweso.

Akiwa mkoani Ruvuma, Aweso ametembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa katika wilaya za Tunduru, Namtumbo, Songea Mjini, Songea Vijijini na Madaba lengo likiwa ni kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wa mkoa huo wanapata huduma ya maji ya uhakika.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia kilula cha maji cha mradi wa Liula, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoa maagizo kwa watendaji mara baada ya kukagua Tenki la maji la mradi wa Parangu katika Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoka kukagua chanzo cha maji cha Masimeli, kinachotumika kuzalisha maji kwa ajili ya mradi wa Lipaya katika Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye tenki la mradi wa Matimila, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA NDANI YA SIKU 30 KUJITOKEZA WAMILIKI WA MAGOGO YALIKAMATWA BANDARINI DAR

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ametoa muda wa siku 30 kwa wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika bandari ya Dar e s Salaam (TPA) ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya Nchi, kujitokeza haraka kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani baada ya kuyatelekeza bandarini hapo kwa muda wa miaka 10 sasa huku mengine yakitelekezwa pasipo kuwa na vibali maalum.

Dk.Kigwangalla ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini hapo kukagua mali na bidhaa zinazoshughulikiwa na Wizara yake hiyo ambapo katika zkukagua kwake huko alibaini uwepo wa makontena hayo 55 ambayo yapo kwa miaka 10 sasa yakihifadhiwa huku wahusika wakishindwa kujitokeza.

“Naagiza mamlaka zilizo chini ya wizara yangu kuhakikisha wanahakiki magogo yote yalipo hapa bandarini. Mwenye huu mzigo lazima ajulikane hasa haya magogo 938, Ndani ya siku 30 mwenye haya magogo atangaziwe na ajitokeze vinginevyo itabaki kuwa mali ya Serikali” alisema Dk. Kigwangalla.

Hata hivyo aliagiza pia kontena 55 zilizokutwa bandarini hapo zenye magogo pia nazo wahusika wajitokeze na nyaraka zao kamili ili waeleze kama kweli wameyatoa Zambia magogo hayo ama sehemu gani hivyo wajitokeze na wasipofanya hivyo ndani ya siku hizo 30, magogo hayo yatataifishwa na kuwa mali ya Serikali.

Katika ziara hiyo, Waziri Dk.Kigwangalla aliweza kutembelea bandari ya Dar es Salaam pamoja na maeneo yanayohifadhiwa magogo hayo zikiwemo bandatri ya nchi kavu ya NASACO, Malawi (Malawi Cargo) na baadae eneo hilo la bandari ya Dar es Salaam.

Akiwa katika eneo la Malawi Cargo, Waziri Dk. Kigwangalla aliweza kushuhudia makontena mbalimbali yakiwemo yale ya mbao aina ya mitiki ambayo inatarajiwa kusafirishwa nje ya nchi huku akibaini uwepo mkubwa wa udanganyifu kwa wasimamizi wa upakuaji na usafirishaji katika eneo hilo la bandari ambao awali walitaja idadi ndogo ya makontena ya mbao mbele ya Waziri hali iliyopelekea kuanza kuyakagua makontena yote ndani ya eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangallaakitoa maagizo kwa uongozi wa bandari ya TPA.
Baadhi ya magogo hayo yaliyokutwa katika makontena bandarini hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakiwa katika eneo la bandari ya nchi kavu ya Malawi Cargo. wakati wa kukagua magogo hayo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa nyaraka ya idadi ya makontena katika eneo la Malawi Cargo
Zoezi la ukaguaji likiendelea
Baadhi ya magogo yaliyokutwa bandarini hapo

MAHAFALI YA 11 YA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) YAFANA DAR ES SALAAM

$
0
0

Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishangilia katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017. (Imendaliwa na Robert Okanda Blogs)

Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017

Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017








Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishangilia katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2

Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya (mwenye fimbo) akiwaongoza viongozi wa chuo hicho katika mahafali ya 11 ya ARU katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa naye jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017


Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017

Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017

Bendi ya polisi ikiongoza maandamano ya viongozi wakati wa hafla hiyo.

Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya (mwenye fimbo) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa chuo hicho katika mahafali ya 11 ya ARU katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa naye jijini Dar es Salaam leo Disemba 2 2017

Serikali haitawafumbia macho Wezi wa kazi za Sanaa:Dkt Mwakyembe.

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) na viongozi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment wakionyesha Filamu ya “Queen of Masai”itakayoanza kusambazwa na Kampuni hiyo kuanzia kesho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Tyeeo Entartainment Bw.John Kalaghe wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi.Joyce Fissoo akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.

Na Shamimu Nyaki-WHUSM


Serikali imesema itaendelea kuwachukulia hatua wote watakaobainika kusambaza kazi za sanaa kinyume na utaratibu ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wizi wa kazi za Sanaa uliolalamikiwa na wasanii wote hapa nchini.


Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akizindua Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment itakayohusika na usambazaji wa kazi za Sanaa kuanzia kesho.


“Serikali haitaendelea kuwafumbia macho wezi wa kazi za Sanaa,tutawashughulikia kama ambavyo tumeanza na mafanikio yameanza kuonekana yeyote anaetaka kusambaza kazi hizi aende Barazani Entartainment watamsaidia.”Alisema Dkt Mwakyembe.


Aidha amewataka wasanii wote hapa nchini kutumia Kampuni hiyo kwa manufaa ili waweze kupiga hatua ambapo pia amewahakikishia kuwa ndani ya kipindi kifupi kijacho sekta ya Sanaa itakuwa na mageuzi makubwa.


Kwa upande wake Katibu wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amewahakikishia wasanii hao kuwa Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Wilaya wapo tayari kushirikiana na Kampuni ya Barazani Entartainment katika kuleta mafanikio ya kazi zao.


Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw.John Kalaghe ameishukuru Serikali kwa ushirikiano ilioupatia kampuni hiyo tangu ilipoanzisha wazo hilo ambalo leo limefanikiwa na wasanii wataanza kunufaika na kazi zao kwani Kapuni hiyo itasambaza kazi zao kwa urahisi na salama zaidi.


Kampuni ya Tyeeo Barazani Entartainment itakuwa ndio wakala wa kusambaza kazi za sanaa ikiwemo Filamu za nje na ndani,Muziki,masomo ya watoto,na makala za kielimu kupitia simu ya mkononi kwa mitandao yote kwa malipo nafuu.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI LEO DECEMBER 3,2017

MBUNGE WA KINONDONI CUF AJIUZULU UBUNGE NA KUJITOA UANACHAMA WA CUF,AOMBA KUJIUNGA NA CCM


MEYA MWITA ASHANGAA WATU WA KISIWA CHA MAYOTTE WAKIZUNGUMZA KISWAHILI

$
0
0
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto, akimsikiliza Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda Hamidani Magoma mwenyemiwani walipokutana katika ofisi za Mastahiki Meya jiji.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Saalam Isaya Mwita akimkabidhi Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda wa Mayotte Hamidani Magoma Kamusi ya Kiswahili baada ya kuzungumza Kiswahili.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita watatu kulia mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Kisiwa Cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa walipomtembelea ofisini kwake.
Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda wa Mayotte Nchini Ufaransa Hamidani Magoma akimuelekeza jambo kwenye kwenye dokomenti Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita walipomtembelea ofisini kwake na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya biashara jijini hapa.
………………….
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watu 10 kutoka Kisiwa cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa.
 
Ujumbe huo ulikuwa umeambatana na wabunge watatu kutoka Nchini humo, Rais wa Shirikisho la wafanyabiashara wa Mayotte pamoja na wajumbe wengine ambao ni wawakilishi kutoka kampuni mbalimbali kisiwani humo.
Katika mazungumzo hayo, Mstahiki Meya Mwita na wageni wake wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa hususani masuala ya kibiashara ambapo amewakaribisha na kuahidi ushirikiano kwao.
Aidha Meya Mwita pia ameshangaa kuona ugeni huo kutoka Kisiwa cha Mayotte wakizungumza Kiswahili jambo ambalo alidai kuwa ni la kihistoria kutokana na historia ya Nchi hiyo.
 
Kutokana mshangao huo, ambao uliambatana na furaha ndani yake, aliwakabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili kwa lengo la kuendelea kujifunza zaidi Lugha ya Kiswahili pindi watakaporejea nchini kwao.
“ Nimefarijika na kushangaa baada ya kusikia asilimia 40 ya wananchi wakisiwa cha Mayote wanazungumza lugha ya Kiswahili, hii ni ajabu, lakini inaonyesha ninamna gani ambavyo watu wanaipenda Lugha yetu” amesema Meya Mwita.
 
Awali jumbe huo ulikutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania.
Imetolewa leo Desemba 1 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.

DK MWANJELWA AELEKEZA UONGOZI WA MKOA WA RUVUMA KUHAMASISHA WAKULIMA KUJIUNGA NA VYAMA VYA MSINGI VYA USHIRIKA

$
0
0
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akikagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Wengine Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Pololet Kamando Mgema (Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Katikati) na Meneja NFRA Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya, Jana Novemba 2, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na kina mama waliojipatia kibara kwenye ujenzi wa Kituo cha mafunzo ya kilimo OTC Lilambo kitakachojihusisha na uchakataji wa mahindi kilichopo Mtaa wa Namanditi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017. 
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa tatu Kushoto) akitembelea na kukagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma, Wengine Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe (Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Wa Pili kulia) na Meneja NFRA Kanda ya Songea, Jana Novemba 2, 2017. 
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipotembelea Kijiini Likuyu Fusi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea Mjane Bi Ester Gama ambaye ni mke wa Marehemu Leonidas Gama akimvisha kitenge ikiwa ni ishara ya upendo na faraja. Gama alifariki Dunia Novemba 23, 2017 katika Hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho.
Jana Novemba 2, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi ili kubaini alipotembelea Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akikagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.

Na Mathias Canal, Ruvuma

Uongozi Wa Mkoa Wa Ruvuma leo Disemba 1, 2017 umeelekezwa kuwahamasisha wakulima kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika kwani kupitia vikundi ndio njia muhimu na mkombozi kwa manufaa ya mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amebainisha hayo Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na baadhi ya wakulima sambamba na viongozi Wa wakulima katika Mkutano Wa hadhara ulifanyika katika eneo la Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea.

Pamoja na kuwasisitiza wakulima hao kujiunga katika vikundi vya vyama vya msingi vya ushirika, Mhe Naibu Waziri ameelekeza uongozi Wa Mkoa Wa Ruvuma kutilia msisitizo umuhimu Wa Vyama hivyo kwani ni maelekezo ya ilani ya Ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020 inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ikiongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Alisema kuwa vikundi hivyo vikianzishwa na kuwa na Uongozi vitarahisisha kuuza mazao mazuri kwani kutakuwa na nguvu ya pamoja inayowakutanisha kwa kuongozwa na sheria na taratibu walizojiwekea kama kikundi pasina kuwa kinyume na taratibu za serikali.

"Upo umuhimu mkubwa Wa kujiunga na AMCOS kwani ni jambo lisilokuwa la hiari ambapo itarahisisha kupata mikopo huku kwa serikali ikiwa ni njia rahisi kuwahudumia, Aidha Elimu inapaswa kutolewa juu ya umuhimu Wa Vyama vya msingi vya ushirika" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

Aliongeza kuwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula nchini inapaswa pia kutoa Elimu kwa umma juu ya majukumu yake kwamba ni kununua mahindi na kuyahifadhi ili kuwa na akiba pindi panapotokea Ukame serikali iweze kuwahudumia.

Awali Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembekea na kukagua Ghala La kuhifadhi mahindi Kanda ya Songea ambapo ameshuhudia akiba ya kutosha ya mahindi ambapo mpaka kufikia Leo Disemba 2, 2017 Kanda ya Songea ina mahindi yanayofikia Tani 21,892.924 huku kati yake Tani 10,335.395 ni ununuzi Wa msimu Wa mwaka 2016/2017 na Tani 11,557.529 ni ununuzi Wa mwaka huu 2017/2018.

Aidha, Mhe Mwanjelwa amezuru Kijiini Likuyu Fusi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea na kutoa pole kwa Ndugu na Jamaa akiwemo Bi Ester Gama ambaye ni mke Wa aliyekuwa Mbunge na Diwani wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma, Marehemu Leonidas Gama aliyefariki Dunia Novemba 23, 2017 Majira ya saa 4:25 Usiku katika Hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho iliyopo Songea baada ya kukimbizwa huko kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

MAKAMU WA RAIS APIGA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA CCM MKOA WA KUSINI UNGUJA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akipiga kura kuchagua viongozi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye Hoteli ya Coconut Tree, Marumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdallah Juma Abdalla Sadalla(Mabodi)kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye Hoteli ya Coconut Tree, Marumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akiwasalimu wajumbe kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye hoteli ya Coconut Tree, Marumbi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein wakati alipowasili kwenye kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye hoteli ya Coconut Tree, Marumbi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA

$
0
0
Kushoto ni Muuguzi wa kituo cha Afya Ngamiani Lea Kakunya akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alijitokeza kupima VVU wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani.
Wakazi wa Jiji la Tanga wakiingia kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Ngamiani kwa ajili ya kupima VVU katika zoezi ambalo liliendeshwa na Shirika la AGPAHI katika vituo vya Afya vya Makorora,Ngamiani ,Pongwe na Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo ambapo zaidi ya wananchi 1900 walijtokeza kupima.
Kushoto ni Ochieng Makaranga ambaye ni Mratibu wa Huduma na Tiba kwa watu wenye VVU Kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji hilo wakati wa zoezi la Upimaji wa VVU jana Desemba Mosi 
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wakiwa kwenye kituo cha Afya Makorora wakisubiri huduma ya kupima VVU. 
Afisa Tabibu kutoka kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga,Silvesta Leonard kulia akichukua maelezo kwa mmoja kati ya wananchi wa Jiji hilo ambaye alijitokeza kupima VVU Jana Desemba 1,2017
Muuguzi wa Afya katika Kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga,Salima Athumani akimpima virusi vya Ukimwi VVU mkazi wa Jiji hilo wakati wa upimaji huo uliokuwa ukiendeshwa na Shirika la AGPHA
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga waliojitokeza kupima VVU katika kituo cha Afya cha Makorora Jijini Tanga.Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga waliojitokeza kupima VVU katika kituo cha Afya cha Makorora Jijini Tanga.


Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Care Initiative (AGPAHI) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga wameendesha zoezi la upimaji vya virusi vya Ukimwi kwa wakazi wa Jiji hilo huku zaidi ya wakazi 1900 wakijitokeza kupima na kupatiwa ushauri wa namna ya kuweza kujikinga na maambukizi ya VVU .

Upimaji huo ulifanyika kwenye vituo vya Afya Makorora, Ngamiani, Pongwe na Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani inayoadhimishwa kila mwaka hapa nchini. Zoezi hili la upimaji lililenga wanafamilia wa watu wanaoishi na VVU katika jiji la Tanga. Upimaji huo ulianza siku ya Jumatano hadi Ijumaa (29 Novemba – 01 Disemba) ambayo ndiyo siku ya Ukimwi duniani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupima afya zao mkazi mmoja wa Donge Jijini Tanga, Zilipa Elangwe alisema zoezi hilo limekuwa ni zuri kwa sababu linasaidia watu kuweza kujua afya zao na namna ya kujikinga.

Alisema wanapokuwa wakijua afya zao inawasaidia kuweza kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kupelekea kuingia kwenye maambukizi ikiwemo kujiepusha na ngono zembe.

Aidha alisema huduma hiyo ya upimaji wa VVU ambayo imetolewa na Shirika la AGPAHI likishirikiana na halmashauri ya jiji la Tanga imewasaidia kujua afya zao kutokana na baadhi ya familia kutokuwa na uwezo wa kifedha kwenda kupima mara kwa mara hivyo ni jambo nzuri.

“Kwa kweli tunalishukuru sana Shirika la AGPAHI kwa kutuletea huduma hii ya upimaji wa VVU maana imetusaidia kujua afya zetu lakini pia kuchukua tahadhari ya kuhakikisha tunaepukana na maambukizi mapya “Alisema.

Naye Saidi Sharifu mwenye miaka 72 aliliomba Shirika hilo kuendelea kutoa huduma za upimaji huo kila wakati ili kuweza kuwasaidia wananchi wanaokumbana na maambukizi waweze kujitambua na kuanza kutumia dawa.

Alisema ni ukweli usiopingika wapo watu wanaweza kukumbana na maambukizi kutokana na kushiriki tendo la ndoa bila kujijua hali zao hivyo kunapokuwa na huduma hiyo ya uhamasishaji upimaji wa VVU inasaidia kubaini hali yao ya kiafya na kuanza kuchukua hatua.

Naye Tabu Khamisi ambaye ni mkazi wa Makorora Jijini Tanga, alisisitiza kuwepo na uhamasishaji wa upimaji wa VVU wa mara kwa mara ili jamii iweze kupata fursa ya upimaji VVU na familia zao. Pia alisema upimaji huo umekuwa chachu ya wananchi kuweza kujitokeza kwa wingi kujua hali zao na namna nzuri ya kujikinga na maambukizi hususani wazazi waliojitokeza kwa wingi na watoto wao.
Naye Mratibu wa Ukimwi wa jiji la Tanga, Dr. Hamisi Mvugalo alisema juhudi ambazo zinafanywa na shirika la AGPAHI zinapaswa kuungwa mkono na kuwa endelevu kwani zina manufaa kwa jamii inayotuzunguka.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6

$
0
0
Hussein Makame-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika tarehe 13 Januari mwaka 2018.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Mhe. Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid, alisema Tume imetangaza uchaguzi huo kufuatia kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo nafasi wazi ya jimbo la Singida Kaskazini kufuatia kuvuliwa uanachama wa CCM mbunge wa jimbo hilo Lazaro Nyalandu na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge.

Kwa upande wa Jimbo la Songea Mjini, Jaji Mst. Hamid alisema kuwa Spika aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi ya jimbo hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Leonidas Gama huku Tume ikipokea Hati ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ikithibitisha kuwa Jimbo la Longido kuwa wazi baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo.

Aliongeza kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata sita Tanzania Bara.

Mhe. Jaji Mst. Hamid alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu (Halmashauri ya Jiji la Arusha), Kihesa (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa), Bukumbi (Halmashauri ya Wilaya ya Uyui), Kurui (Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe), Keza (Halmashauri ya Wilaya ya Ngara) na Kwagunda (Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe).

Alisema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya tarehe 12 hadi 18 Desemba, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya tarehe 14 hadi 20 Desemba, 2017.

“Uteuzi wa wagombea katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata za Keza, Kimandolu, Kwagunda, Bukumbi, Kurui na Kihesa utafanyika tarehe 18 Desemba, 2017 na uteuzi wa wagombea katika jimbo la Songea Mjini utafanyika tarehe 20 Desemba, 2017” alisema Jaji Mst. Hamid.

Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza tarehe 19 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018.

Katika jimbo la Songea Mjini, alisema kuwa kampeni za zitaanza tarehe 21 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 Januari, 2017.

Mhe. Jaji Mst. Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi wazingatie Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata Sita.

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images