Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

Wateja wa Tigo Kushinda Mamilioni ya Fedha Katika Promosheni ya Msimu wa Sikukuu

$
0
0
Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa promosheni ya 'Fanya Muamala na Ushinde na Tigo Pesa' jijini Dar es salaam leo, ambapo wateja wa Tigo pesa wana nafasi ya kujishindia hadi shilingi 15 milioni kwa kufanya miamala na Tigo Pesa. Kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum, Mary Rutta na kulia ni Mkuu wa Huduma ya Tigo Pesa, James Sumari. 


Donge nono kushindaniwa kwa miamala yote ya Tigo Pesa
Dar es Salaam, 30 Novemba, 2017- Huduma ya fedha ya simu za mkononi inayoongoza nchini, Tigo Pesa leo imetangaza zawadi kemkem kwa wateja wake ambao watajishindia mamilioni ya pesa kupitia promosheni ya ‘Fanya muamala na ushinde na Tigo Pesa’ inayoendeshwa katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya .

Promosheni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja itashuhudia washindi watatu wa jumla wakijinyakulia vitita vya TZS 15 millioni, TZS 10 millioni na TZS 5 millioni kila mmoja. Pamoja na hayo, kutakuwa na washindi wa kila siku ambapo mmoja atalamba donge nono la TZS 1millioni, huku wengine wanne wakijinyakulia TZS 500,000 kila mmoja, kila siku.

‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii,’ Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema akizindua promosheni hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Wateja watapata nafasi ya kushinda kwa kufanya miamala yoyote kutoka kwa simu zao kupitia Tigo Pesa. ‘Kadri ya unavyofanya miamala mingi zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda ,’ Sayed alifafanua. Hakuna masharti.

“Tunajivunia mchango wetu katika kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha nchini kupitia Tigo Pesa. Tigo Pesa ni zaidi ya huduma ya kutuma na kupokea pesa. Ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo tuna furaha kubwa kuwapa fursa ya kujishindia zawadi hizi nono ambazo zitawawezesha kufurahia msimu hu wa sikukuu huku wakiendelea kufaidika na huduma zetu bora za kidigitali,’ aliongeza.

Zawadi hizi murwa zinakuja kwa nguvu ya mtandao mpana na ulioboreshwa wa Tigo, huku lengo kuu la Tigo likiwa ni kuwasikiliza wateja wake na kuwapa huduma za kisasa zinazoendana na mahitaji yao.

Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini yenye mtandao mpana wa mawakala zaidi ya 70,000 waliosambaa kote nchini. Miamala ya takriban TZS 1.7bn inafanyika kupitia Tigo Pesa kila mwezi.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) UTAENDELEA KUTOA FIDIA BORA – ERIC SHITINDI KATIBU MKUU – OWM

$
0
0
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba ya kufunga Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo alasiri kwenye Kituo cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha Novemba 30, 2017.

NA K-VIS BLOG
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Eric Shitindi amewahakikishia wadau wote wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuwa Mfuko utaendelea kutoa mafao bora kwa wafanyakazi wote sekta binafsi na umma ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Hayo ameyasema leo Novemba 30, 2017 wakati alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Aidha, Bw. Shitindi amesisitiza ya kuwa suala la elimu ni la msingi sana na limejitokeza ambalo mfuko ni lazima uhakikishe umewafikia wadau wote ili wafanyakazi wote nchini waweze kujua kwa ufasaha haki zao ikiwemo kupata fidia pale watakapokuwa wanastahili, pia waajiri wao waweze kufuata matakwa ya kisheria ikiwemo kujisajili na kuwasilisha michango kama kwa wakati. Pamoja na mambo mengine Bw. Shitindi ameahidi kusimamia zoezi la utoaji elimu kwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambavyo ilielekezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama  wakati akifungua Mkutano huo tarehe 29 novemba 2017.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira wakati akitoa salamu aliishukuru Bodi ya Wadhamini pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko kwa kumualika kushiriki katika Mkutano huo, pia amesema Mkoa wake unavyo viwanda vingi na mashamba mengi ambavyo vinapelekea kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyakazi ambao watahitaji huduma ya Mfuko.
“Nitawapeni ushirikiano wa kutosha kuhakikisha waajiri wote wa Mkoa wa Kilimanjaro wanajisajili katika Mfuko ili  wafanyakazi wasijekukosa Mafao endapo wataumia, kuugua au kufariki” alisema Bi. Nghwira
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Emmanuel Humba, amewashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa kutoa michango mingi ambayo imelenga kuboresha huduma za Mfuko.
Katika Mkutano huo uliobeba kauli mbiu ya "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, umeshuhudia Mfuko ukitoa tuzo kwa waajiri waliofanya vizuri katika utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba ya kufunga Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo alasiri kwenye Kituo cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha Novemba 30, 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Laure Kunenge, akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
  
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Bw. Bernard Konga, (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu waMfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) Bwana Daud Msangi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) kwenye Kituo Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel Humba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Radhmina Mbilinyi, wakiongoza kikao.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi. Anna Mghwira, akihutubia Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo Novemba 30, 2017 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha.

 Viongozi wa vyama vya wafanyaakzi wakiteta jambo.


KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.

$
0
0
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kikao kilichofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. James Kibamba(kulia) akiwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya Muundo wa Utumishi wa Idara ya Ustawi wa Jamii uliopitiwa na kujadiliwa na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Deodatha Makani (kushoto) akifafanua masuala ya Kiutawala kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Mendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (kulia) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akisisitiza wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto kuhusu umuhimu wa uzingatiaji wa Kada zote za Ustawi wa Jamii katika rasimu ya muundo unaopendekezwa kwenye Baraza lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Bw. Atupile Mwambene akitoa ufafanuzi kuboresha rasimu ya marekebisho ya Muundo wa Utumishi wa Idara ya Ustawi wa Jamii kwa wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika  mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mwanasheria kutoka  Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Vicness Mayao akifafanua masuala ya kisheria  kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii waliokutana mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bibi. Magreth Mussai akitoa maoni yake kuhusu maboresho ya Muundo wa Utumishi kwa Kada ya Ustawi wa Jamii kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkuu wa chuo cha Buhare Bw. Paschal Mahinyira akitoa hoja kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.


Baadhi ya wajumbe wawakilishi wa Watumishi wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyojiri katika Baraza la Wafanyakazi wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.

Picha na Kitengocha Mawasiliano WAMJW

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DECEMBER MOSI,2017

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akiwa amemkabidhi cheti cha shukrani mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho aliyefanya vizuri kwenye masomo yake, wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi wahitimu waliofanya vizuri iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam Novemba 30 2017. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

Sehemu ya wanafunzi wa chuo Ardhi University wakifuatilia matukio katika hafla ya kukabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali baada ya kufanya vizuri katika masomo kwa mwaka 2017 hafla iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam Novemba 30 2017.
Sehemu ya wanafunzi wa chuo Ardhi University wakifuatilia matukio katika hafla ya kukabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali baada ya kufanya vizuri katika masomo kwa mwaka 2017 hafla iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam Novemba 30 2017.
Sehemu ya wanafunzi wa chuo Ardhi University wakifuatilia matukio katika hafla ya kukabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali baada ya kufanya vizuri katika masomo kwa mwaka 2017 hafla iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam Novemba 30 2017.

UBA Group Emerges African Bank of the Year

$
0
0

Former British Broadcasting Corporation(BBC) correspondent, Mr. Michael Buerk; Chief Executive, UBA Capital(Europe) Limited, representing UBA Group, Mr. Andrew Martin; and Editor, Middle East and Africa, The Banker. Mr. James King, during The Banker Awards 2017, organised by The Banker Magazine, a publication of Financial Times(FT), where UBA Group coveted five awards, including the prestigious ‘African Bank of the Year 2017’, at a ceremony in London on Wednesday

Lagos; Nigeria; 30 -11– 2017; Pan-African financial institution, United Bank for Africa (UBA) Plc has once again proven its leadership on the continent, as the Banker Magazine crowned UBA the “African Bank of the Year 2017”. This Banker Award is premier for Nigeria, as it marks the first time a Nigerian-headquartered bank will be wining the prestigious and highly coveted regional award.

To further demonstrate the group’s strength and dominance in the financial sector on the continent, four of UBA Group’s operations in Africa also led contenders in their respective countries to emerge the Best Bank of the Year 2017 in their respective markets. UBA Congo, UBA Tchad, UBA Gabon and UBA Senegal emerged the Best Bank of the Year in Congo, Tchad, Gabon and Senegal, reinforcing the strong franchise of the Group across its chosen markets in Africa. Notably, UBA Gabon and UBA Senegal won the same awards in 2016, as both subsidiaries of UBA Group remain the Banks to beat in Gabon and Senegal.

A publication of the Financial Times Newspaper, The Banker Magazine is a global financial intelligence magazine that provides global bank ratings/analysis and it is the definitive reference in international banking for high level decision makers globally. According to the magazine, the aim of the award “is to highlight industry wide excellence within the global banking community. The winner is selected from participating banks in each of the 120 countries from which entries are received for the competition.”

Explaining the rationale behind UBA carting multiple categories in its December issue, the Banker’s Magazine noted that Africa’s economic landscape has been unpredictable in recent times which resulted in recession in some of Africa’s best performing economies, while the region as a whole only expanded by about 1.3% in 2016. “In these conditions only the most diversified and innovative of regional banks can prosper. And this is precisely why the United Bank for Africa (UBA) has scooped the 2017 regional winner award. For one, the lender registered impressive top- and bottom-line growth over the review period,” it noted.

The magazine went further to enumerate the various achievements recorded by UBA group during the period, noting that earnings for the year reached N384bn ($1.07bn) signalling 22% growth from its 2015 performance while profit before tax also grew, by 32%, to reach N91bn. According to the organisers, “Equally impressive is UBA’s capital adequacy ratio which, at the end of 2016, stood at 20%, while its nonperforming loan ratio was a healthy 3.9%. Operating across 19 markets in Africa, the bank serves more than 14 million customers.”

It added that the Pan-African bank’s foray into various ventures in Africa also helped to clinch its activities in the year under consideration, stating, “Beyond the numbers, the bank has won and acted on a number of headline deals. These include the financing a new stadium in Douala, Cameroon, for the 2019 Africa Cup of Nations for $285m. In Senegal, more than $250m of trade finance was provided to the state oil company, while the lender acted as arranger and bank agent in the raising of $160m to finance road infrastructure. The bank’s digital tax collection solutions are also helping regional governments in Senegal and Burkina Faso.”

The organisers noted that UBA is making impressive strides in the digital space, adding that in terms of internet banking, the organisation processed 7 million transactions valued at more than N600bn in 2016. Mobile banking processed transactions valued at N70bn over the same period. UBA has also launched eMailMoni, a service that lets customers transfer funds via e-mail, while Chat Banking allows clients to perform basic transactions through social media platforms. “For these reasons, and others, UBA is the winner of our 2017 African Bank of the Year award,” the Magazine stated.

The Group Managing Director/Chief Executive Officer, UBA Plc, Mr. Kennedy Uzoka, who was delighted by the recognition from The Bankers said; “These awards mark another milestone for UBA Group and is a testament of the diligent execution of the bank’s strategic initiatives on customer service. Being recognized as Africa’s best bank complements positive feedback from customers and is a recognition of our improving efficiencies, service quality and innovation. I therefore dedicate it to our growing loyal corporate and retail customers, who are our essence. Given our heritage commitment to Africa’s development, we continue to impact lives through our service as well as funding to individuals, businesses and government.”

Uzoka added; “The bank remains focused on its goal of democratizing banking in Africa, leveraging on new technologies and our rich pool of talent. It is satisfying that our efforts towards leadership are yielding great results. We continue to gain market share across our chosen markets, as we deepen financial inclusion, meeting basic and complex financial service needs of the growing African population. We are Africans and determined to change the narrative of financial services in Africa and this is just the beginning,” he noted.

On his part, Mr. Emeke Iweriebor, Regional CEO, UBA Francophone Africa, described the awards as exciting, stating that the bank’s great work in Africa is increasingly being recognized.

Iweriebor who dedicated the awards to the bank’s esteemed customers, said “Our pioneering innovations in the African banking sector are undoubtedly critical to the growth and development of the continent. Africa’s banking sector has come a long way but we still have a lot to do. We at UBA Group are dedicated to being a critical part of this transformation.”

He added that the bank will continue to leverage its local knowledge, global exposure as well as presence to drive positive change in Africa, working actively with the government, local businesses, regulators and other stakeholders in deepening financial services.

The Banker award’s “Bank of the Year Awards” are widely regarded as the Oscars of the Banking Industry. For 90 years, The Banker has been the world’s leading monthly journal of record for the banking industry. The organisers note that the aim of the awards programme is to highlight industry wide excellence within the global banking community.

The Banker selects one winning bank for each of the 120 countries that are covered. Over 1,000 applications are entered and judges select winning banks based on the ones that have made most progress over the past 12 months.

UBA was incorporated in Nigeria as a limited liability company after taking over the assets of the British and French Bank Limited who had been operating in Nigeria since 1949. The United Bank for Africa (UBA) Plc merged with Standard Trust Bank in 2005 and from a single country operation founded in 1949 in Nigeria - Africa's largest economy - UBA has become one of the leading providers of banking and other financial services on the African continent. The Bank provides services to over 14 million customers globally, through one of the most diverse service channels in sub-Saharan Africa, with over 1,000 branches and customer touch points and robust online and mobile banking platforms.

UBA was the first Nigerian bank to make an Initial Public Offering, following its listing on the NSE in1970. It was also the first Nigerian bank to issue Global Depository Receipts. The shares of UBA are publicly traded on the Nigerian Stock Exchange and the Bank has a well-diversified shareholder base, which includes foreign and local institutional investors, as well as individual shareholders.

SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA

$
0
0
SERIKALI haijatoa ruhusa kwa Chuo Kikuu Huria (OUT) kiendelee kutoa kozi ya ‘Foundation’ kama ambavyo imedaiwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii.

Baadhi ya mitandao ilitoa taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho: Waziri Mkuu aruhusu kozi za 'Foundation' Chuo Kikuu Huria kwa madai kuwa alitoa ruhusa hiyo jana (Alhamisi, Novemba 30, 2017) wakati akiwa mkoani Singida ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu hicho.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Singida waliohudhuria mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki mjini Singida, Waziri Mkuu alisema Serikali bado inafanyia maboresho Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014.

“Kwa sasa Serikali inafanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo kwani sera tuliyonayo haifafanui vizuri jinsi ya kuwasaidia vijana wetu wajiendeleze kwa njia ya mfumo wa elimu huria na masafa,” alisema.

“Programu kama zilizoelezwa na Makamu Mkuu wa Chuo za Foundation, zinahitaji pia kufafanuliwa kwenye sera yetu, ambayo kwa sasa wataalamu wetu wanaendelea kuiboresha. Pindi itakapokamilika, tutaitolea taarifa kwa Chuo Kikuu Huria na wataalamu wataweza kushirikiana na sekta zote ili kuhakikisha jambo hili linakwenda vizuri,” alisema.

Mapema, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Tozo Bisanda alisema wamepokea barua kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwaarifu juu ya nia ya Serikali kutaka kurejeshwa kwa kozi za Foundation katika chuo hicho.

“Tayari tumekwisha wasilisha mtaala wa Foundation ulioboreshwa ili kukidhi matakwa ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na tunasubiri mrejesho kutoka Kamisheni baada ya kikao chao, mapema mwezi ujao,” alisema Prof. Bisanda.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, DESEMBA MOSI, 2017   

RC MAKONDA AJITOLEA KUFANIKISHA MATIBABU YA AHMED ALBAITY


Waziri Mpina Aagiza Mikataba Ya Wawekezaji Wa Vitalu Vya Ranchi Ya Taifa Vyenye Jumla Ya Hekta 68238 Kuvunjwa Mara Moja

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akiwa kwenye picha pamoja na Viongozi wa Wilaya ya Mvomero na Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania alipotembelea ranchi ya Dakawa jana.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Muhamed Utaly kulia akitoa maelezo ya kuhusu eneo la hekta 20000 zilizoshindwa kuendelezwa na mwekezaji Mtibwa Sugar kwa lengo la ufugaji. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo bwana Stan Rau hapo jana.
Meneja wa ranchi ya Mifugo ya Mkata, Iddi Sadalah akimuonyesha Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) banda la Mbuzi linalokadiriwa kuchukua mbuzi 800 kwa wakati mmoja katika ranchi ya Mkata jana.


……………….

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za Mifugo za Taifa, Profesa Philemoni Wambura kuvunja mikataba ya wawekezaji wa vitalu vyenye jumla ya hekta 68,238 kwenye ranchi ya Mkata na Dakawa ndani ya mwezi mmoja baada kushindwa kuviendeleza vitalu vya ranchi na kushindwa kulipia kwa muda mrefu.Mpina ameyasema hayo jana wakati alipotembelea katika ranchi ya Mkata na Dakawa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika ranchi hizo.

Amezitaja kampuni za wawekezaji ambazo zilizomilikishwa vitalu zinatakiwa kuvunja mkataba kwa kushindwa kuendeleza upande wa ranchi ya Mkata katika Wilaya ya Kilosa kuwa ni pamoja na Kadolo Farm Company Ltd kitalu namba 418 yenye hekta 4005,Bagamoyo Farm kitalu namba 419 yenye hekta 3672.96, A to Z Animal Feeds Company Ltd kitalu namba 420 yenye hekta 3692.97 na Ereto Livestock Keepers kitalu namba 422 yenye hekta 4020.54.

Katika Wilaya ya Mvomero kampuni zilizoshindwa kuendeleza vitalu ni pamoja na kampuni ya Overland kitalu namba 415 yenye hekta19446.28, Katenda yenye hekta 2500, Mollel yenye hekta 2500 na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa (Mtibwa Sugar) chenye hekta 20000 walizomilikishwa toka mwaka 1999 na kushindwa kukiendeleza na kukilipia kwa miaka 18.

Mpina amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kumaliza mara moja migogoro inayoendelea baina ya wakulima na wafugaji. Aidha Waziri Mpina amemtaka Diwani wa kata yaTwatwatwa, Katibu Tawala wa Halimashauri ya Wilaya ya Kilosa pamoja na jamii ya wafugaji kumaliza migogoro inayowasumbua kwa muda mrefu kwa njia ya mazungumzo kabla ya kukimbilia muhimili wa mahakama bila sababu yoyote.

Mpina amesema kama vyombo vya Serikali vingetumika vizuri kuanzia ngazi ya kijiji kungepunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika wilaya hiyo. Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Wilaya zinaongoza kwa kuwa na migogoro mingi baina ya wakulima na wafugaji hapa nchini.

Kwa upande mwingine, Waziri Mpina amezitaka Halimashauri zote nchini kutotunga sheria kandamizi dhidi ya wafugaji. Akitolea mfano, wa sheria ndogo ya Halimashauri ya Mvomero ya kutoza faini ya shilingi 25, 000/=kwa kila mfugo kuingia katika Wilaya hiyo bila kufuata taratibu badala ya shilingi elfu kumi iliyoelekezwa katika Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya Mwaka 2003.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Magembe Makoye amesema upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wafugaji kutasaidia kuondoa migogoro baina ya pande hizo na kuendelezwa kwa ranchi hizo za taifa kutawasaidia wafugaji kupata shamba darasa litakalo wasaidia kufuga kwa kisasa na kupata mbegu bora za mifugo.

INDIA KUIKOPESHA TANZANIA DOLA MILIONI 500 KUJENGA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 17 NCHINI

$
0
0
Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya, akieleza nia ya nchi yake kuwekeza katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Ujenzi wa Mji wa Dodoma na miundombinu mingine kama Reli na Barabara wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Kamishna Msaidizi wa Sera, Bi Sauda Msemo wakimsikiliza kwa makini Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya akielezea jitihada za nchi yake katika kuwekeza kwenye masuala ya Afya wakati wa mkutano kati ya pande hizo mbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto) na Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa makini maelezo ya Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya (hayupo pichani) kuhusu utayari wa kuwekeza katika Sekta ya Umeme hasa umeme wa Jua, wakati wa Mkutano kati ya pande hizo mbili Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya (kulia) akielezea kuhusu ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili hasa katika masuala ya kibiashara wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia akielezea kuhusu uwekezaji wenye kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ambao ni fursa kwa nchi hiyo, wakati wa Mkutano na Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya (wa pili kulia), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiagana na Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya, baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kulia), Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya, Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa India wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kumalizika kwa mkutano ulioangazia Uwekezaji na biashara, Jijini Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango



Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Serikali ya India imeahidi kutoa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika miji 17 nchini kupitia Benki ya Exim ya nchini humo.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya.Dkt. Mpango alieleza kuwa mradi huo umelenga kumtua ndoo mama kichwani na kwamba mkopo huo utakapo patikana utasaidia kutatua kero kubwa ya maji inayoikabili jamii hivyo kuchochea kwa kasi ukuaji wa uchumi.

“Tuko katika mazungumzo ya kukamilisha upatikanaji wa mkopo huo ikiwemo kuangalia namna ya kushughulikia madai ya Benki ya Exim ambayo inataka hata kampuni itakayotekeleza mradi huo isamehewe kodi zote zikiwemo zinazopaswa kulipwa na wafanyakazi wake” alieleza Dkt. Mpango

Alibainisha kuwa licha ya kwamba jambo hilo ni gumu kisheria lakini kutokana na umuhimu wa suala hilo la maji, Serikali italipatia ufumbuzi hivi karibuni ili mradi huo uweze kuanza mara moja.Dkt. Mpango alitambua mchango mkubwa wa Serikali ya India katika kutatua changamoto ya maji kwa watanzania ambapo amesema kuwa inchi hiyo inatatekeleza mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga hadi Tabora.

Dkt. Mpango aliiomba Serikali ya India iendelee kuisaidia Tanzania katika Nyanja za utaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano-TEHAMA ili kupata watu wenye ujuzi utakao saidia kuchochea kasi ya maendeleo ya Sekta ya Viwanda nchini.Dkt. Mpango alisema kuwa nchi ya India imepiga hatua kubwa katika masuala ya TEHEMA hivyo ni vema ikawekeza kwenye eneo hilo katika Taasisi za Elimu hapa nchini ili kuweza kuwapatia ujuzi idadi kubwa ya watu watakao kwenda kusukuma gurudumu la maendeleo hasa ya ukuaji wa viwanda.

“Bila kuwa na watu wenye ujuzi katika kada mbalimbali hasa TEHAMA hatuwezi kuwa na nchi yenye uchumi wa viwanda”, aliongeza Dkt. Mpango.Aliyataja maeneo yenye fursa kubwa za uwekezaji kuwa ni pamoja na Sekta ya Kilimo ambapo Tanzania inahitaji kuwa na viwanda vitakavyoongeza thamani ya mazao na pia kuwa na zana bora za kilimo kama utumiaji wa Trekta badala ya kutumia jembe la mkono.

Maeneo mengine ni sekta ya utalii, afya, uendelezaji wa ujuzi kupitia fani nyeti za udaktari ama utaalamu nyeti ya tiba ikiwemo magonjwa ya moyo na figo, ambayo India imepiga hatua kubwa.“Pia ujuzi wa Wahandisi katika Sekta ya Maji unahitajika ili kutoa huduma ya maji kwa weledi kwa jamii kwa kuwa ni moja ya hitaji muhimu kwa maendeleo, hata hivyo zipo sekta nyingine za uwekezaji kama Utalii na Uvuvi hasa katika kina kirefu ambao unahitaji zana bora” aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Sandeep Arya, amesema nchi yake inania ya kuwekeza katika Kilimo, Nishati ya Umeme hasa wa Jua na kusaidia katika mpango wa ujenzi wa Mji wa Dodoma pamoja na ujenzi wa Reli na Barabara.Amesema Tanzania na India zinauhusiano wa muda mrefu hivyo nchi yake itaendelea kuwekeza Tanzania katika Nyanja mbalimbali ili kuendeleza ushirikiano wenye tija kwa wananchi wa pande hizo mbili.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amemshukuru Balozi wa India na Nchi yake kwa nia ya kuendelea kuwekeza Tanzania na kusifu juhudi za uwekezaji mkubwa ambao unafanywa hasa katika Sekta ya Afya na kuahidi kuendelea kudumisha ushirikiano huo.

RC RUVUMA AMSIMAMISHA KAZI MKANDARASI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINE MNDEME amemsimamisha kazi Mkandaras RUKOLO kwa kushindwa kutimiza majukumu yake kwa wake hali inayopelekea wakazi wa wilaya ya songea kupata shida wakati wa kusafirii,mkandarasi amefutiwa makatba wake na kuagiza kutopata tena tenda ya kutengeneza barabara za mkoa wa RUVUMA.

MFUMO WA RAIS WA KUKUSANYA MAPATO KIELEKTRONIKI UMEPEISHA MAPATO YA KODI YA MAKAMPUNI YA SIMU KWA 102%

$
0
0
Na Mwandishi wetu. Mfumo wa Kukusanya Mapato Kielekroniki (eRCS) umeonyesha mafanikio makubwa kwa miezi mitatu ya mwanzo ya Julai, Agosti na Septemba 2017, baada ya Makusanyo ya Kodi kwa Upande wa Zanzibar (ZRB) kupitia eRCS kufikia Shilingi Bilioni.7.2, ukilinganisha na Shilingi Bilioni 3.5, ZRB walizokusanya kipindi Kama hicho mwaka 2016 kabla ya mfumo wa eRCS. Makusanyo hayo yakiwa ni Ongezeko la Shilingi Bilioni 3.6 sawasawa na asilimia102%. Ni zaidi ya Mara mbili ya makusanyo ya mwaka Jana kabla ya mfumo wa eRCS, yanayofikia shilingi Bilioni 7.2 ni majumuisho wa Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty) na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Baada ya kukata Marejesho.
Wakati huo huo Taarifa tulizonazo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni kwamba makusanyo ya kodi yanayotokana na kampuni za simu, kwa kutumia eRCS TRA wamefanikiwa kuongeza makusanyo kwa asilimia 21% kwa kukusanya Jumla ya shilingi Bilioni 128.9 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba 2017, ukilinganisha na makusanyo ya miezi ya Aprili, Mei na Juni 2017 kabla ya kuanza kutumia mfumo wa eRCS. Aprili, Mei na Juni 2017 kabla ya eRCS, makampuni ya simu saba yalilipa jumla ya kodi ya Shilingi Bilioni 101.7. Julai, Augusti na Septemba 2017, baada ya kuanza kutumika eRCS, Makampuni ya simu yale yale yameweza kulipa Shilingi Bilioni 128.9. Kukiwa na ongezeko la Shilingi Bilioni 27.2 sawa na 21% ambazo ni majumuisho yaliyotokana na kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) na Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty).
Ukijumuisha makusanyo yanayotokana na Kodi kutoka kampuni za simu saba kuanzia mwezi Aprili 2017 mapaka mwezi Septemba 2017 TRA imekusanya Jumla ya Shilingi Bilioni 230.7. kwa kipindi cha miezi sita tu, ambazo ni wastani wa shilingi Bilioni 38.5 kwa mwezi. Taarifa tulizopata kutoka chanzo chetu ambao hawakutaka majina yao yatajwe wametueleza kwamba Serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu unaofanywa na kampuni za simu katika Taarifa zao walizozipeleka TRA za input kwa ajili ya “return” ambazo zinakosa uhalisia kwani zinajumuisha taarifa za miezi iliyopita kwa lengo la kuongeza kiwango cha input tax.
Mfumo eRCS ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamad Shein walipozindua Dirisha la kukusanya kodi Kielekroniki Elecrtronic Revenue Collection System (eRCS) tarehe 1 Juni 2017, ukiwa na lengo la kusaidia Mamlaka zote mbili za Mapato yaani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB) kuongeza mapato yanafanyika kupitia njia za kielektroniki. Mpaka Mwezi Novemba 2017, ni kampuni saba za simu ndizo zilizounganishwa katika mfumo wa eRCS, Kampuni hizo ni Vodacom, TTCL, Airtel, tiGO, Halotel, Zantel na Smart. Taarifa hii imeandikwa kutokana na taarifa zinazopatikana IDC, TRA na ZRB Novemba 2017.

TTCL INAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA MAULID

EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika Dar es Salaam jana Soko la Tabata Muslim.
 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita akimpatia fulana Mwakilishi wa Mbunge wa Segerea, Bonah Kaluwa aliyefika kwaniaba yake kama mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed wakati wa uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi.
 Mwenyekiti wa Soko la Tabata Muslim, Haji Mohamed akihutubia.
 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita, akihutubia.
 Wawezeshaji wa kisheria wa EfG wakiwa na furaha katika uzinduzi huo.
 Burudani ikitolewa.
 Burudani ikiendelea.


 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia
 mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed, akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
 uzinduzi ukiendelea.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo
 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akiteta jambo na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akijumuika na wadau mbalimbali na wawezeshaji sheria wa shirika hilo.

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Equality for Growth (EfG) lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, jana limezindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kama taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho hayo.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Soko la Tabata Muslim Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa shirika hilo, Jane Magigita amesema kwa sasa EfG inaendesha mradi unaoitwa "MPE RIZIKI SI MATUSI" ambao umeongeza wigo wa mapambano ya ukatili wa kijinsia  katika Wilaya ya Ilala na Temeke katika masoko sita.

Ameyataja masoko hayo kuwa ni Mchikichini, Kisutu,Tabata Muslim, Feri, Gezaulole na Temeke Stereo.

Magigita aliongeza kuwa, lengo la mradi huo ni kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara katika mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na kisiasa, vilevile kuona wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine ili waweze kujipatia kipato chao bila vikwazo.

"Mbali na kuwepo mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya ukatili wa kijinsia, EfG pekee ndiyo ambayo inajihusisha na kuwasaidia wafanyabiashara katika masoko na kuwapa elimu ya haki za binadamu, sheria na ukatili wa kijinsia," alisema mkurugenzi huyo na kuongeza;

"Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani tulivyoweza kutambua kuwa sekta isiyo rasmi inasahaulika ukilinganisha na sekta zingine."

Aidha, Magigita alitumia fursa hiyo kulishukuru Shirika la UN Trust Fund kwa kuwawezesha ili kufikia azma mahususi.

Mkurugenzi huyo wa EfG amesema madhumuni ya kuwepo kwetu hapa leo ni kutokana na azma yetu sote kama taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na pia kuweka msisitizo kwenye utawala wa sheria na upatikanaji wa haki.

"Kama wote tunavyofahamu, chanzo cha maadhimisho haya ni mauaji ya kikatili ya wasichana wa Mirabelle huko nchini Dominika yaliyofanyika mnamo miaka  ya 1960. 
Kutokana na hali hiyo, mwaka 1991, Umoja wa Mataifa ulitenga siku 16 kuanzia Novemba 25 kila mwaka kama siku ya kimataifa ya kuopinga unyanyasaji dhidi ya wanawake. Vilevile, siku ya kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambayo ni Desemba 10," alisema.

Ameongeza kuwa, utafiti unaonyesha wanawake wa Dar es Salaam walio katika sekta isiyo rasmi ndiyo kundi ambalo linakumbwa kwa kiasi kikubwa na ukatili wa kijinsia wawapo nyumbani hata wanapokuwa maeneo yao ya kazi.

Pia utafiti unaonyesha wanawake hao, wanakosa ulinzi toka kwa serikali na mamlaka husika.

"Wanawake wafanyabiashara sokoni ni kundi mojawapo la wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi walioamua kukataa umaskini na kuingia katika harakati za kuinua uchumi wao na familia zao. 

Utafiti uliofanywa na shirika letu la EfG mwaka 2015 ulionyesha kuwa wanawake katika masoko yetu wanafanyakazi kwenye mazingira magumu na wengi wao wakiendesha biashara duni na zenye ufanisi mdogo.

Akisoma risala hiyo kwa mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Segerea aliyemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mheshimiwa Bona Kilua ambaye hakufika kutokana na tatizo la kiafya, Magigita alisema;

" Katika masoko kumi yaliyotembelewa  wakati wa utafiti huu uliofanywa kwenye Manispaa ya Ilala na Temeke ulionyesha kuwa asilimia 95.97% ya wanawake wanapitia ukatili wa kijinsia wanapokuwa mahala pa kazi yaani sokoni, wanawake hawa hukosa mitaji ya kutosha wakati wa kuanzisha baishara, wengi hawana elimu ya usimamizi wa biashara na wala hawashiriki katika kufanya maamuzi na kugombea nafasi za uongozi katika masoko pia ilionekana kwamba hawana dhamana kwa ajili ya kuchukua mikopo, hivyo kubaki na zana na vitendea kazi duni vya kuendesha biashara zao," alisema na kuongeza;

"Ukatili ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara katika masoko ni pamoja na kushikwa maongo ya mwili, lugha chafu na matusi, vitisho, jaribio la kubakwa na kejeli, rushwa ya ngono. Pia utafiti ulionyesha madhara wanayoyapata wanawake hawa katika masoko ambayo ni kushindwa kuzalisha ipasavyo, kuharibika kisaikolojia, kutojiamini, kuwa na hofu, uwoga, kutoheshimika pia kudhalilika," alisema.

Magigita alisema kuwa kupitia mradi wa "MPE RIZIKI SI MATUSI" unaofadhiliwa na Un Trust Fund, shirika limefanikisha kuwafikia wafanyabiashara wapatao 10,250 kwa kuwapa elimu ya ukatili wa kijinsia, sheria na haki za binadamu, kutoa msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia wapatao 1800 ambao mashauri yao yametatuliwa, kutoa rufaa zipatazo 75, masoko 10 yameridhia kuanza kutumia mwongozo wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko, kugawa machapisho yapatayo 5,500 kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali katika kuongeza uelewa wao.

Ameongeza kuwa, wafanyabiashara wameweza kujitambua na wanajua wapi waende kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa ukatili, pia kumekuwepo na ongezeko la utoaji wa taarifa za ukatili wa kijinsia kwa viongozi wa masoko na polisi, maofisa 120 wa vyombo vya ulinzi na usalama wameongeza uelewa juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia, sheria na haki za wanawake jambo lililofanya ukatili masokoni kupungua kwa asilimia 81 kwa mujibu wa utafiti wa Machi 2017 hasa lugha ya matusi na bughudha kwa wanawake.

Mkurugenzi huyo amesema, kupitia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema; "FUNGUKA! UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO HAUMUACHI MTU SALAMA. CHUKUA HATUA" tunakusudia kutoa elimu kwa wafanyabiashara katika masoko yote ili wasikae kimya wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia kwani madhara yake ni makubwa sana na yanarudisha nyuma maendeleo ya taifa letu.

"Ombi letu kwa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya zinazohusika katika kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ni kuwepo mikakati ya wazi kuhakikisha wanawake katika sekta hii wanapewa kipaumbele ili kuwaweka huru na bughudha zote za ukatili dhidi yao. 

Pia ni muhimu kwa vyombo vya utoaji haki vihakikishe kuwa wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia wanapata haki na wale wanaohusika katika kutenda vitendo hivyo wanakumbana na mkono wa sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

"Kwa hili tunaomba jeshi la polisi lishirikiane kwa ukaribu na watoa huduma wetu ambao hutoa huduma ya rufaa kwa wahanga na wapate fursa za kuongeza kipato na kunia uchumi wa taifa," alisema Magigita.

Naye Ahmed aliyemwakilisha Mbunge wa Segerea akizungumza baada ya kusikia risala hiyo alisema amefarijika sana kuona kuwa ili kuinua uchumi na kutokomeza ukatili wa kijinsia si tu kwa wananchi bali kila mtaalam anachukua nafasi yake ili kutoa mchango wake.

"Hili limenipa faraja kubwa mimi binafsi na serikali kwa ujumla hasa hasa katika kuimalishaaa sekta binafsi, mmeweza kuonyesha kwamba kila Mtanzania anafanya bidii kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu katika ukuaji wa sekta isiyo rasmi Tanzania ambayo ipo katika sekta binafsi. Nawashukuru sana EfG kwa kuwa mfano mzuri kwa hili," alisema Ahmed.


Katibu huyo wa Mbunge wa Segerea aliongeza kuwa, Dira ya Taifa inaeleza kuwa Tanzania itakuwa na jamii yenye usawa wa kijinsia ifikapo mwaka 2020. Hatuwezi kufikia dira hiyo tutaruhusu aina ya ukatili wa kijinsia kujitokeza tena au aina mpya kabisa kujitokeza na kukua miongoni mwetu. Tunahitaji kuwa na jamii yenye usawa kijinsia nyakati zote.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kwa hatua hiyo kubwa ya kupeleka huduma hizo kwa wafanyabiashara kwani mara nyingi baadhi ya wafanyabiashara hawafikiwi katika maeneo yao ya biashara na hivyo kukosa fursa ya kukosa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia," alisema Ahmed.


MWILI WA MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA SCOLASTICA ALIYEUAWA KUZIKWA KWA MARA YA PILI JUMAMOSI HII.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MWILI uliofukuliwa hivi karibuni kwa kibali cha mahakama kuondoa utata wa taarifa za kupotea kwa Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica, Humphrey Makundi(16) utazikwa kwa mara ya pili leo (Jumamosi ) . 

Hatua ya kuzikwa kwa mwili huo uliokaa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa zaidi ya siku 14 sasa inatokana na kutoka kwa majibu ya sampuli ya vina saba (DNA) ikionyesha kuwa mwili ni wa Humphrey Makundi.

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu Humphrey,Bw Jackson Makundi alisema mazishi yatafanyika katika kijiji cha Mamba kwa Makundi ,Marangu wilaya ya Moshi baada ya kupata kibali cha mahakama cha kuruhusu kuzikwa kwa mwili huo.

Makundi alisema shughuli za mazishi ya mwanae yataoongozwa na maaskofu wasaidizi kutoka Dayosisi ya Dodoma akiwemo mchungaji Samwel Mshana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) wakisaidiana na Askofu Msaidizi wa (KKKT) dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Elingaya Saria.


Novemba  6,mwaka huu taarifa za kutoweka kwa mwanafunzi huyo katika shule aliyokuwa akisoma ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo zilianza kuzagaa katika mitandao ya kijamii na baadae Novemba 7 mwaka huu mwili ulikutwa ukiwa umetelekezwa mto Ghona unaokadiliwa kuwa mita 300 kutoka katika shule hiyo.

Mwili huo ambao awali ulifikishwa katika Hosptali ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ulipokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti na baadae kuzikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi katika makaburi ya Karanga  kama mwili usiokuwa na ndugu.

Hata hivyo,baada ya kuwepo kwa taarifa ya kuzikwa kwa mwili huo ,familia ya Makundi iliomba kibali cha mahakama kuruhusu  kufukuliwa mwili huo kwa lengo la kujiridhisha ,mtu aliyezikwa kama kweli ni mzee kama taarifa za awali zilivyotolewa au ni ndugu yao. 

Tayari watuhumiwa  watatu kati ya 11 wanao shikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi huyo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa shtaka la mauaji .

Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Scolastica ,Edward Shayo , aliyekuwa mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha na Labani Nabiswa raia wa Kenya anayetajwa kuwa Mwalimu katika shule hiyo.

Mbele ya mahakama ya Hakimu mkazi ,Moshi ,upande wa Jamhuri katika shtaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi ,Julieti Mawore uliwakilishwa na Mwanasheria wa serikali Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea ,Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko anyemtetea Mshatakiwa wa pili katika shtaka hilo Edward Shayo.

Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo ,Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshtakiwa wa kwanza ,Hamis Chacha(28),wa pili Edward Shayo (63)  na wa tatu Laban Nabiswa (37) walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.

Kutokana na maelezo hayo Hakimu ,Mawore alieleza kuwa washtakuwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shtaka la mauaji huku akiwataka kungojea kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.

Kuhusu upelelezi wa Shtaka hilo Mwanasheria wa serikali Nassiri aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku akiwasilisha ombi la kupangwa tarehe nyingine kwa ajili kutajwa kwa shauri hilo wakati upelelezi ukikamilishwa.

Hakimu Mkazi ,Mawore aliahairisha shtaka hilo na kupanga kutajwa kwa shtaka hilo Desemba 8 mwaka huu  na  kwamba washtakiwa wote watarudishwa Rumande kutokana na  kesi hiyo kutokuwa na dhamana .


DKT MWANJELWA AIPONGEZA NFRA KUANZISHA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI MAZAO KUPITIA UJENZI WA VIHENGE NA MAGHALA NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo desemba 1, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Desemba 1, 2017.

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo desemba  1, 2017.

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ya namna ya ununuzi na uhifadhi wa mahindi kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Desemba 1, 2017.


Na Mathias Canal, Njombe


Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amesifu juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.


Mradi huo utahusisha ujenzi Wa Vihenge vya kisasa, Mghala ya kisasa pamoja na ukarabati Wa Ofisi ambapo baada ya mradi huo kukamilika wakala utakuwa umeongeza uwezo Wa kuhifadhi Shehena ya mahindi ya uzito Wa zaidi ya Tani 250,000 ambapo Vihenge vya kisasa ni 190,000 MT na Maghala 60,000 MT.


Mradi huo unataraji kutekelezwa na kampuni mbili za kandarasi kutoka serikali ya Poland (Feerum na Unia Arab) kwa usimamizi Wa Wakala Wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo unataraji kugharimu zaidi ya Bilioni 150 za Kitanzania.


Tayari maandalizi ya awali yameshakamilika ikiwemo Utiwaji saini mikataba, Uchunguzi Wa udongo, Tathmini ya athari ya Mazingira, Pamoja na kutembelea eneo la mpango kazi.


Akizungumza wakati akikagua Ghala la Kuhifadhia mahindi Kanda ya Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alisema kuwa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umefanya kazi kubwa ya ubunifu na kujiongeza kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima katika Kanda zote saba ikiwemo ya Makambako-Njombe, Kipawa-Dar es salaam, Dodoma, Shinyanga, Arusha, Songea na Sumbawanga.


Alisema kuwa pamoja na Kanda ya Makambako kupangiwa kununua jumla ya Tani 6500 katika msimu Wa mwaka 2017/2018 ambapo baada ya lengo kukamilika ziliongezwa fedha za ununuzi hivyo kununua jumla ya Tani 8,961.530


Akisoma taarifa ya Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba alisema kuwa Kanda ya Makambako ni miongoni kwa Kanda itakayoongezewa uwezo Wa kuhifadhi ambapo tayari kuna kiwanja chenye ukubwa Wa Hekari 2,9965 kilichopo Makambako na Mbozi chenye ukubwa Wa Hekari 53.691.


Alisema Wakala umefanikiwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kununua baadhi ya Mazao ya Chakula cha ziada kutoka kwa wakulima, Kutoa Chakula cha ziada kwa waathirika, Kutekeleza mkakati Wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA) kwa kutoa bei nzuri kwa wakulima wanaouza Mazao yao kwa NFRA sambamba na utekelezaji Wa malengo ya milenia 2025.


Katika ziara hiyo ya kikazi ya Siku Moja katika Mji Wa Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Kilimo pia amekutana na kufanya kikao cha kazi na wafanyakazi Wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya chakula Kanda ya Makambako ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kufanya kazi kwa Nidhamu, Weledi, Kujituma, Uvumilivu, Bidii na mshikamano.


Wakati huo huo amefanya mazungumzo na wakulima kutoka Kanda ya Makambako ambapo wakulima hao wamesifu Juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali ikiwa ni pamoja na kupunguza Tozo na Ushuru.


Wakulima hao kwa nyakati tofauti wameupongeza Uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Makambako kwa kuwashirikisha na kuwajali wakulima katika kila hatua ya ununuzi Wa mazao.

NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA NA NAIBU WAZIRI MIFUGO NA UVUVI ULEGA WAZINDUA UMEME WA NISHATI YA JUA KISIWA CHA KWALE

$
0
0

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Mkuranga Abdallah Ulega wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa mradi wa umeme wa nishati yajua uliojengwa na kampuni ya TANDEM kwa ufadhili wa Wakala wa umeme wa Vijijini REA, uzinduzi ulifanyika jana katika Kisiwa cha Kwale kata ya Kisiju Mkoa wa Pwani.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAIBU waziri wa Nishati Subira Mgalu na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wamezindua umeme wa nguvu za jua (Solar Power) katika Kisiwa cha Kwale uliojengwa na kampuni ya TANDEM na kufadhiliwa na wakala wa umeme Vijijini (REA).

Umeme huo uliogharimu takribani Milion 230 za kitanzania uliweza kuzinduliwa jana na Waziri wa Nishati sambamba na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo wa umeme wa nguvu za jua (solar power) kwa kisiwa cha Kwale kilichopo Kata ya Kisiju, Naibu Waziri wa Nishati Subira alisema kuwa hiyo ni moja ya hatua kubwa sana katika Kisiwa hicho ukizingatia umeme wa Tanesco unaoutumia nguzo hautaweza kufika kwa urahisi.

"Hii ni moja ya hatua kubwa sana kwa kijiji cha Kwale kwani walikaa kwa muda mrefu sana bila ya kuwa na nishati ya umeme na hasa ukiangalia changamoto iliyopo ni kuwa umeme wa Tanesco unaotumia nguzo usingeweza kufika huku, na sio huku tu hata visiwa vingin vya karibu na hapa ikiwemo Koma,"amesema Subira.
Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu akiwasha kitufe cha umeme kuashiria kuanzia sasa umeme unawaka katika Kijiji cha Kwale kata ya Kisiju jana Mkoani Pwani.

Naibu Waziri wa Nishati alisema, anafahamu umeme huo unaopatikana kwa Megawat 5.4 bado hautoshi kwa wanakijiji wote wa Kwale kwahiyo ombi lao la kutaka waongezewe bajeti ya kununua Panel za umeme ili kuweza kupatikana umeme kwa watu wote ambapo amelipokea na kwakuwa ni waziri mwenye dhamana ya kutaka kuhakikisha wananchi wote wananufaika kwa kuwa na umeme atalifanyia kazi.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwa mbele ya wananchi wake wa Kijiji cha Kwale alisema kuwa kupatikana kwa umeme katika Kisiwa cha Kwale kutaleta maendeleo kwa wananchi hususani kwa wavuvi kwani samaki walikuwa wanaharibika kwa kukosa sehemu ya kuweka na kuishia kuharibika.

Alisema umeme huo utawasaidia wanakijiji wa Kisiwa cha Kwale na zaidi amewataka kuutumia kwa manufaa yatakayoleta tija maendeleo kwa kijiji kizima na cha zaidi ni kwenye kuinuka kiuchumi. Msafara wa viongozi hao uliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mkuranga Eng Mshamu Munde.

Wananchi wa Kisiwa cha Kwale wamefurahishwa sana na ujio wa umeme huo wa REA uliojengwa na TANDEM ambapo kwa miaka mingi sana wameshindwa kuwa na nishati ya umeme na kwa saaa hivi hata samaki wao wanauza kwa bei wanayotaka kutokana na kuwa na sehemu za kuhifadhia pamoja na mabarafu yanayouzwa kwa bei nafuu kabsa.

Mbali na hilo, mkandarasi wa wakala wa umeme wa Vijijini REA amefanikisha agizo la Naibu Waziri wa Nishati alilopewa siku ya Jumatatu kuhakikisha umeme unawaka kabla ya Ijumaa katika kata ya Kisiju na Mkamba ambapo Naibu Waziri alifika na kuthibitisha kama agizo lake limefanya kazi na kusema kuwa REA awamu ya tatu wananchi wote watapata umeme kwa haraka zaidi .
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Kwale wakati wa uzinduzi wa umeme wa nishati ya jua uliojengwa na kampuni ya TANDEM kwa ufadhili wa Wakala wa umeme Vijijini REA.
Panel zinazotumika kwa ajili ya umeme wa nishati ya jua kisiwa cha Kwale.
Naibu Waziri Wa Nishati Subira Mgalu na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Mkuranga sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Eng. mshamu Munde wakiwasili katika Kisiwa cha Kwale jana.


TAMKO KUTOKA WIZARA YA AFYA

$
0
0
Kumekuwa na taarifa mbalimbali, hamaki na kejeli zinazoenea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na taarifa iliyotolewa tarehe 27 Novemba 2017, Mnazi Mmoja kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Kondom kuhusu mpango wa Serikali kununua na kusambaza kondom 500,000,000 katika kipindi cha miaka mitatu 2018 hadi 2020.



Tunapenda kuukumbusha umma wa Watanzania kwamba maambukizi ya VVU na UKIMWI bado ni tatizo katika nchi yetu. Takriban watu 1,400,000 wanakadiriwa kuwa na VVU. Hivyo katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI Serikali inaendeleza afua mbalimbali ili kuzuia maambukizi mapya. 

Asilimia 40% ya maambukizi mapya yanatokea miongoni mwa vijana wenye umiri wa miaka 15-24. Aidha makundi maalum kama vile wanaojidunga madawa ya kulevya, wanaofanya biashara ya ngono na wale wanaoamiiana wa jinsia moja wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi.  Makundi mengine ya walio katika hatari ni waendesha magari ya masafa marefu, wavuvi na wananchi wa kwenye migodi.



Wizara inatekeleza afua mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha na kupima uwepo wa VVU, na kisha kuanza tiba na matunzo, pamoja na kutoa dawa za kufubaza kwa watakao kuwa na maambuzi ya VVU. Kuna afua pia za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto, kutoa elimu ya VVU/UKIMWI na afya uzazi kwa vijana, elimu kuhusu VVU/UKIMWI kwa jamii na tohara kwa wanaume. 

Matumizi ya kondom ni moja wapo ya afua katika kuzuia maambukizi mapya. Hata hivyo utafiti wa viashiria vya Malaria na UKIMWI wa mwaka 2011/12 umebaini kuwa kuna matumizi duni ya kondom, kwani ni asilimia 27 tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja waliokiri kutumia kondom mara ya mwisho walipofanya ngono. Hivyo Serikali itaendelea kununua na kusambaza kondom kwa lengo la kuzuia maambukizi ya VVU, magonjwa ya ngono na mimba zisizo tarajiwa ikiwa ni mojawapo ya afua hizo za kudhibiti maambukizi ya VVU.

Tunasisitiza kuwa Wizara na wadau wake inaendelea kutoa elimu ya kondom sambamba na elimu ya kusubiri kufanya ngono kwa wale ambao hawajaanza na wale ambao wameanza lakini wanapaswa kusubiri (Abstinence) na elimu ya kuwa waaminifu kwa mwenza mmoja aliye mwaminifu na anaejua hali yake ya maambukizi ya VVU (Be faithfull). 

Hivi sasa nchini kuna vyanzo vya upatikanaji wa kondom vya aina tatu. Kwanza ni kondom zinazopatikana kupitia sekta ya umma  ambazo husambazwa na Serikali kwa wananchi bila malipo. Pili, kuna kondom zinazosambazwa na wadau ambazo zinauzwa kwa bei ya chini kwa kuwa wadau wamechangia. Mfano kondom za Salama na Dume, na chanzo cha tatu ni kondom za kibiashara ambazo zinauzwa kwa bei ya kati na ya juu.



Kondom za sekta ya umma husambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na huduma za mkoba ngazi ya jamii, Kondom za wadau na zile za biashara husambazwa katika maduka ya dawa, maduka ya bidhaa mbambali, baa na nyumba za wageni.



Kwa mwaka 2016/17 Serikali iliboresha kondom zinazopatikana kupitia ya sekta ya umma kwa kuipa kifungashio kipya na jina la ZANA, ambapo kondom 36,916,911 zilisambazwa. Kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2018 hadi 2020 Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Dunia wa kudhibiti malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu inatarajia kununua kondom za kiume takribani 500,000,000. 

Kondom hizi zitasambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na katika maeneo hatarishi yanayoaminika kuwa na watumiaji wengi. Aidha, kwa vile imebainika kuwa watu ambao hawaumwi hawaendi vituo vya afya kwa  ajili  ya kuchukua kondom tu na hivyo kupelekea kutofikia walengwa, usambazaji na ugawaji huu utalenga maeneo ambayo

Kunamatukio ambayo yanaendana na ngono na yana walengwa wa afua za kondom. Maeneo haya ni kama baa, nyumba za kulala wageni, maeneo yenye mikusanyiko ya magari ya masafa marefu, maeneo ya uvuvi na migodini.



Aidha ikumbukwe kwamba nchi yetu ina sera sheria, mila, desturi na maadili yetu kama watanzania,  Hivyo kondom zote haziruhusiwi kusambazwa bila kufuata miongozo ya Wizara, ili kulinda zisifike kwa wasiolengwa.



Hivyo basi, iwapo tunataka kuzuia na kumaliza maambukizi ya VVU na UKIMWI ifikapo 2030 tunapaswa kama nchi kuwekeza katika kuzuia maambukizi mapya. Matumizi ya kondom, ununuzi wa vifaa tiba, vitendanishi, dawa za ARV na za magonjwa nyemelezi ni afua muhimu. Tunaomba wanahabari na wananchi waunge mkono juhudi hizi kwa kuwa tunahitaji watanzania wenye afya bora na uwezo wa kuzalisha ili kuijenga Tanzania ya Viwanda.


Imetolewa  na:

KATIBU MKUU  - AFYA


30 Novemba, 2017

Mhe. Samia Suluhu Hassan azitaka asasi za kiraia na madhehebu ya dini kuongeza juhudi katika kuchangia masuala yanayohusiana na ukimwi

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka asasi za kiraia na madhehebu ya dini kuendelea kuongeza juhudi katika kuchangia masuala yanayohusiana na ukimwi katika maeneo yao ikiwemo kuhimiza maadaili na tabia njema katika jiamii.

Makamu wa Rais aliyasema haya wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais alisema kuwa kila mtu anapaswa kukumbuka kuwa jukumu kuu la kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi linaanza na mtu binafsi, jamii na hatimaye sote kama nchi.

“Ndugu Wananchi Ukimwi umeendelea kuathiri nguvu kazi ya Taifa, wafanyakazi wa taasisi za serikali na zisizo za serikali wanapata maambukizi kama wana jamii wengine hii inapelekea kupungua kwa ufanisi makazini na kuathiri uchumi kwa ujumla”Makamu wa Rais amezipongeza Taasisi zote ambazo zina mikakati ya kupambana na ukimwi mahala pakazi kwa kuwakinga wafanyakazi wao na pia kuwahudumia bila kuwabagua wala kuwanyanyapaa wale wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Makamu wa Rais alisema Serikali ina nia thabiti ya kutafuta mikakati endelevu ya kufikia TISINI TATU ifikapo mwaka 2020 na kumaliza kabisa ukimwi ifikapo 3030.Makamu wa Rais alisisitiza kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha miundo mbinu ya afya na kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya ikiwa ni pamoja na kuongeza watoa huduma kote nchini.

Makamu wa Rais amesema Serikali imeanzisha mfuko wa ukimwi (AIDS TRUST FUND) ukiwa na lengo la kuboresha rasilimali kwa ajili ya kuboresha huduma za ukimwi yakiwemo matibabu, upimaji wa virusi vya ukimwi na kutokomeza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa motto pamoja, kuhudumia watoto yatima na ujenzi wa vituo vya kutolea elimu ya ukimwi hivyo uwepo wa mfuko huu utapunguza utegemezi na kuongeza kasi na ufanisi katika mapambano dhidi ya ukimwi.

Makamu wa Rais alihimiza elimu ya ukimwi itolewe mashuleni ili vijana wawe na ufahamu wa kutosha .Makamu wa Rais alimaliza kwa kuwapongeza UNAIDS na wadau wote wanaoshiriki katika mapambano dhidi ya ukimwi na kuwahakikishia serikali ipo pamoja nao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Da es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wafanya upasuaji kwa mtoto ambaye moyo wake umekaa upande wa kulia

$
0
0
adaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakifanya upasuaji kwa mtoto ambaye vyumba vyake vya moyo havijakamilika na hivyo damu kwenda kwa wingi kwenye mapafu katika kambi ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo.Picha na JKCI
Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 16 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima saba.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia Russel Lee akiongea na waandishi wa Habari kuhusu upasuaji wa moyo wa mtoto ambao umekaa upande wa kulia na mishipa yake ya damu chafu na safi imeingiliana katika upasuaji huo wameweza kulinda mapafu yalikuwa yanapokea damu kwa wingi kutoka kwenye mishipa ya moyo na mtoto kawekewa kifaa ambacho kitamsaidia moyo wake kufanya kazi vizuri (Pace Maker). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images