Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1445 | 1446 | (Page 1447) | 1448 | 1449 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza katika Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA), Dodoma

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akizungumza jambo na Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem mara walipokutana katika Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA), Dodoma
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem mara walipokutana katika Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA), Dodoma
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (katikati walio kaa) katika pich ya pamoja na maafisa mbalimbali wa serikali, kuanzia kushoto waliokaa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem.


  Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem ameshiriki katika Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki CHAKAMA ambalo limefanyika siku mbili katika mji mkuu Dodoma, kongamano hilo lilihudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Dkt Suzan Kolimba ambao walitoa shukrani zao kwa Ubalozi wa Kuwait kutokana na mchango wake katika kufadhili baadhi ya gharama za kongamano hilo baada ya kupokea ombi kutoka wizara ya Nje.

  Balozi Al-Najem alitoa hotuba katika kongamano hilo ambapo alieleza kuwa swala la kubadilisha biashara na utamaduni baina ya nchi za Ghuba na mataifa ya Afrika Mashariki lilikuwepo tangu mwanzoni mwa karne ya ishirini, bandari za Dar es salaam, Zanzibar, na Mombasa zilikuwa kimbilio la wafanyabiashara, na kwa sifa ya kipekee meli za Kuwait zilikuwa zikitia nanga katika bandari hizo na tunaweza kusema kuwa hakuna nyumba ya Kikuwait ilikuwa inakosa nguzo za ujenzi ambazo zilikuwa zinaletwa kutoka Afrika Mashariki.

  Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki CHAKAMA kilichoanzishwa mwaka 2002 kiliandaa kongamano hilo ambalo pia lilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Zanzibar, Kenya, Uganda, Ghana na Zimbabwe.


  0 0

  Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (katikati) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) picha inayoonyesha muonekano wa ukumbi wa BASATA utakavyokua baada ya kumalizika alipofanya ziara katika taasisi hiyo kujua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa maonyesho wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia ya blue) eneo la jukwaa lilivyozingatia ubora wa maonyesho alipofanya ziara katika taasisi hiyo kujua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa maonyesho wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam.
  Mkandarasi wa ujenzi wa ukumbi wa BASATA Bw. Novart Ludovick (wapili kushoto) akimweleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia ya blue) maendeleo ya ujenzi ulipofikia alipofanya ziara katika taasisi hiyo kujua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa maonyesho wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na watumishi wa BASATA (hawapo pichani) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu BASATA Bw. Godfrey Mngereza.
  Mtendaji Mkuu BASATA Bw. Godfrey Mngereza (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha ya tingatinga Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa BASATA pamoja na kuzungumza na watumishi wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akisikiliza wimbo uliotungwa na kuimbwa na mwanamuziki kutoka Kongo unaosifia Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa BASATA pamoja na kuzungumza na watumishi wa BASATA jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu BASATA Bw. Godfrey Mngereza. Picha na Genofeva Matemu -WHUSM

  0 0

  Zaidi ya milioni 20 zimetolewa na wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali hapa  nchini ikiwa ni mchango wa kusaidia matibabu na kununua vifaa tiba kwa ajili ya  watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.

  Ikiwa Jana ni Jumanne ya kutoa (GIVING TUESDAY) kote duniani na Taasisi ya Foundation for Civil Society iliadhimisha kwa kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapatia vitu hivyo,huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni changia, okoa maisha.


  Akikabidhi misaada hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Bw. Francis Kiwanga alisema kuwa wafanya kazi wa Taasisi hiyo huwa wanatenga asilimia moja kwa kila mtumishi katika mshahara wake kwa ajili ya kurudisha fadhila na asante kwa jamii.

  Aliendelea kwa kusema kuwa wao kama waanzilishi wa kampeni hiyo walichanga na kufikisha million sita, ila michango mingi ilitoka kwa wananchi na taasisi zilizoguswa na tatizo hilo hivyo kuona haja ya kuwasaidia watoto hao.


  Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa msaada huo utalenga watoto 100 waliopo katika camp hizo kwa kufanyiwa upasuaji na mambo mengine madogo madogo yatakayohitajika katika zoezi hilo.


  Lakini pia taasisi ya Foundation For Civil Society ikishirikiana na wadau wake wameweza kutoa kadi za bima ya afya za NHIF 100 ambazo zimegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 5 kuwasaidia watoto hao kwa matibabu hayo na mengineyo.


  Aidha Mkurugenzi huyo aliwasihi  watanzania kujitolea kuwasaidia wenzetu ambao hawajiwezi na wanaohitaji michango yetu kwani kutoa ni moyo na kadiri unavyotoa ndivyo unavyobadirikiwa.


  Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha mifupa MOI Dr. Respicious Boniface alisema kuwa watoto hao wakipatiwa matibabu mapema wanaweza kuwa sawa kama watoto wengine, lakini kinachofanya wazazi washindwe ni gharama za matibabu.


  Daktari huyo alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili wao kama wauguzi ni uchache wa vyumba vya upasuaji kwani vyumba vilivyopo havitoshi kwa kufanyia zoezi hilo ambapo amesema kuwa kwa siku wanawafanyia upasuaji zaidi ya wagonjwa 30.


  Aidha Daktari huyo aliwapongeza shirika la  Foundation for Civil Society kwa kuamua kuwasaidia watoto hao ambao wanapata tabu kwa matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi na asilimia kubwa wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akizungumza katika maadhimisho ya Jumanne ya kutoa maarufu kama GIVING TUESDAY yaliyofanyika kitengo cha MOI Muhimbili Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akitoa neno la shukrani kwa wadau waliotoa msaada katika taasisi hiyo kwa kusaidia watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi Katika Taasisi ya mifupa MOI Jijini Dar es salaam

  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akimkabidhi zawadi ya cheti Mwenyekiti wa UN chapter UDSM Bi. Faith Lawrance Katika shughuuli hiyo.  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akimkabidhi zawadi ya cheti Bi. Adella January Msofe katika maadhimisho ya siku ya kutoa duniani maarufu kama GIVING TUESDAY Muhimbili Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akimkabidhi hundi ya shilingi milioni nane Mkurugenzi  Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.


  Baadhi ya wazazi na wageni walioudhuria hafla hiyo ya kutolewa kwa msaada wa kusaidia matibabu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi jijini Dar es salaam.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema atahakikishia mgogoro wa wafugaji na wakulima katika Wilaya ya Mkuranga unamalizika kwa kufikia makubaliano yenye kuleta tija.

  Alizungumza hayo wakati wa ziara yake katika vijiji vya Kiramba, Mkiu, Bigwa na Kilimahewa Kusini, Naibu Waziri ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Mkuranga amesema kuwa mgogoro baina ya wafugaji na wakulima upo siku nyingi ila kwa sasa anataka kuhakikisha analitatua kabla kufikia kuleta madhara kwa wananchi wa maeneo hayo.

  Ulega amesema kuwa, tatizo la mgogoro wa Wafugaji na wakulima lipo siku nyingi hata kabla ya yeye kuteuliwa na amepita kwenye vijiji hivyo na ameendelea kuliona ila kwa ushirikiano baina yake na Halmashauri ya Manispaa ya Mkuranga watafanikiwa kutatua mgogoro huo ambao bado haujawa mkubwa sana.

  "Tatizo hili lipo siku nyingi, na tunalifahamu na tumeshaliona ila wanakijiji leo wamenikumbusha tena, mimi pamoja na jopo langu la watu kutoka Halmashauri tumejipanga kuona tunalitatua kwani bado halijafikia kuwa donda ndugu," amesema Ulega.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiramba kata ya Nyamato wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga na kuwaahidi kushugulikia mgogoro wa wafugaji na wakulima.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Bigwa wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.

  Katika Kijiji cha Kiramba na Mkiu, baadhi ya wananchi walitoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kuwa wafugaji waliokubaliwa na kijiji kwa ajili ya kuleta mifugo yao kwa sasa imekuwa kero wakiingia mpaka mashambani na kuharibu mazao yao.

  Wanakijiji hao wamelalamika kuwa wafugaji walioidhinishwa katika mkutano wa kijiji wamekaribisha na ndugu zao ambapo kinasababisha mifugo kuwa mingi sana na mingine kuletwa mpaka kwenye mashamba yao kwa ajili ya malisho.

  Mbali na hilo Naibu Waziri aliweza kukutana na changamoto ya barabara ya kimanzichana kulekea Kiramba, Tipo na Mkonoge na kumuagiza Mkandarasi kutoka Manispaa ya Mkuranga na Meneja wa TARURA kuhakikisha tatizo hilo linamalizika kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika mwakani.

  Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega ametoa mifuko ya saruji kwa Kijiji cha Kiramba, Mkiu, Bigwa na Kilimahewa Kusini kwa ajili ya muendelezo wa maendeleo ya kijiji humo.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wanakijiji wa Mkiu wakati wa ziara yake ya Jimbo la Mkuranga na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisalimiana na wanakijiji baada ya kuwasili kwenye ziara yake katika Jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0

  Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa (mwenye Tai nyekundu) amefanya ziara ya kushitukiza katika Bandari ya Dar es salaam leo November 29, 2017 na kubaini Kampuni ya NAS ikitaka kutoa Semi Trela 44 bila ya kufuata utaratibu.


  0 0

  Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Weruweru Swalehe Msenges.kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
  Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Mnadani  Nassib Mdeme ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
  Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi .kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
  Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni .kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mnadani ,Nasib Mdeme,Diwani wa kata ya Weruweru ,Swaleh Msenges na Diwani wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi ,Wengine katika picha ni kulia mwa msimamizi wa uchaguzi ni Msimaizi Msaidizi na Mkuu wa Idara ya Fedha Juma Massatu na kushoto ni Afisa Uchaguzi wilaya ya Hai,Edward Ntakiliho.
  Madiwani waliochaguliwa hivi karibuni wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Hai wakiwa na ndugu zao.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

  MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro , Ndugu Yohana Sintoo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika kata tatu zilizokuwa hazina uwakilishi limekamilika salama na kuwapata viongozi watakaowawakilisha wananchi kwenye kata husika.

  Ndg Sintoo ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani wateule watatu walioshinda  kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu.

  “Ndugu zangu mtakumbuka kuwa mwishoni mwa wiki kulikuwa na uchaguzi kwenye jimbo letu ambapo wananchi wa kata tatu walikuwa katika zoezi la upigaji kura kwa lengo la kuwapata viongozi wa ngazi ya udiwani baada ya madiwani wa kata husika kujiuzulu”

  “Wananchi wa kata za Mnadani , Weruweru na Machame Magharibi walipiga kura ili kuwapata wawakilishi wao  ambapo zoezi hilo limekamilika bila uvunjifu wa amani kuanzia kipindi cha mikutano ya  kampeni hadi siku ya zoezi la upigaji kura na leo tunawapatia washindi vyeti vyao”

  Amesema, katika uchaguzi huo jumla ya vyama vitano vilishiriki kwa kusimamisha wagombea wao kuomba ridhaa kwa wananchi ambavyo vilikuwa ni CCM, CHADEMA, ACT- Wazalendo, CUF na NCCR Mageuzi.

  Vyeti hivyo vilikabidhiwa kwa Salehe Msengesi (CCM) ambaye alishinda nafasi ya udiwani katika kata ya Weruweru, Martini Munis (CCM) wa kata ya Machame Magharibi na Nasibu Mndeme (CCM) kata ya Mnadani.

  Naye diwani mteule wa kata ya Weruweru, Salehe Msingesi  alisema  ahadi alizozitoa kwenye mikutano yake ya kampeni atahakikisha kuwa zinatekelezwa kwa uhakika ikiwemo kutatuankero ya barabara ambazo kwenye hiyo kata hazipitiki msimu mzima wa mwaka kutokana na uharibifu wake.

  Kwa upande wake diwani mteule wa kata ya Mnadani Nasibu Mndeme
  Akizungumzia utekelezaji wa ahadi alizotoa  diwani mteule wa kata ya Machame Magharibi , Martini Munisi alisema ahadi alizotoa atasimamia ili ziweze kufanikiwa kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri pamoja na Chama chake ili kuweza kusogeza huduma kwa jamii kwa wakati.

  “Natambua kuwa katika kata niliyochaguliwa kuna changamoto nyingi sana ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara  , shule zote za msingi  zilizoko kwenye kata zinahitaji ukarabati wa majengo haswa shule ya Msingi Kyeri ambayo jiko lake limeanguka na linahitaji ukarabati wa haraka  ”alisema.


  0 0
  Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili
  ..........................................................................
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesisitiza agizo la Serikali lililotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu kuhusu kukamilisha zoezi la uwekagi wa vigingi vya mpaka kwenye maeneo ya hifadhi nchini ifikapo Desemba 31 mwaka huu.

  Amesema lengo la kukamilisha zoezi hilo ni kuiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa mwisho wa kumaliza migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu baina ya vijiji na maeneo ya hifadhi nchini.


  Mhe. Hasunga ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi ya msitu wa Isalalo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambapo aliziagiza taasisi zilizo chini ya Wizara yake kukamilisha zoezi hilo kabla ya tarehe hiyo ili kuiwezesha Serikali kubaini maeneo yenye mapungufu na kuyatolea uamuzi.


  “Ifikapo tarehe 31 tuwe tumemaliza kuweka hizo beacon (vigingi) za mipaka, baada ya hapo hatua itakayofuata, Serikali tutakaa na kuangaliza ni vijiji vingapi au maeneo gani yameingia ndani ya hifadhi, tuangalie je tuwaachie hayo maeneo wananchi au tuwahamishe tuwapeleke maeneo mengine, maamuzi hayo yatakuja baada ya kufanya tathmini na kubaini penye mapungufu.


  “Sasa ikitokea kwamba imefika tarehe 31 hatujatekeleza hili mimi kama Naibu Waziri nitakuwa sina kazi, maana sijatekeleza agizo la Serikali, kwahiyo lazima tulisimamie, na mimi sasa kabla halijanipasukia nitakupasukia bwana Meneja (Meneja TFS Wilaya ya Mbozi), nitakuja kukagua mipaka, na kabla ya tarehe 31 nitakuja kukagua tena,”alisema Naibu Waziri Hasunga.


  Wakati huo huo amekemea vitendo vya baadhi ya wananchi wanaoingiza mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini na kuwataka kufugia majumbani kwao au maeneo yaliyotengwa kwa ajili hiyo, amewatahadharisha pia juu ya ukali wa sheria za uhifadhi na kwamba endapo mifugo itakamatwa hifadhini sheria zilizopo zinaruhusu utaifishaji.


  Aidha aliwataka wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo ya msitu wa Isalalo kuacha vitendo vya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya mkaa na uanzishaji wa maeneo ya kilimo. Pia alitoa wito kwa wananchi kulinda vyanzo vya maji na kuacha vitendo vya uchomaji moto misitu.


  Katika hatua nyingine ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Nyanda za Juu Kusini kuwashirikisha wananchi wanaoishi jirani na hifadhi hiyo ya msitu kwenye ulinzi wa hifadhi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha miche ya miti ya kutosha kwa ajili ya kupanda  kwenye maeneo yao yanayozunguka hifadhi hiyo.


  Aidha ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi kupima maeneo yao na kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi kwa kuanisha maeneo kwa ajili ya kilimo, ufugaji na maeneo ya hifadhi ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima ya wananchi


  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Mbozi, Fred Mgeni alisema katika kuimarisha mpaka wa hifadhi ya msitu huo wa Isalalo ambao una ukubwa wa hekta 11,552, jumla ya vigingi 30 vimewekwa kuzunguka hifadhi hiyo.


  Alizitaja baadhi ya  changamoto katika hifadhi hiyo kuwa ni uvamizi wa wakulima na wafugaji, uvunaji haramu wa miti, uchomaji mkaa na moto, na ung'oaji wa vigingi vya mpaka na mabango.


  Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo alisema ili kuimarisha uhifadhi wa msitu wa Isalalo ni vema wananchi wakashirikishwa ikiwemo kuanzishwa kwa vikundi vya vijana ambao watawezeshwa bodaboda zitakazowanufaisha kiuchumi na wakati huo huo zikatumika kwenye ulinzi wa hifadhi.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Msitu wa Isalalo na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Mbozi, Fred Mgeni (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua hifadhi hiyo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi mkoani Songwe jana.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo wakati wa kukagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo Mkoani Songwe kwenye ziara yake ya kikazi ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo jana.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na Mkuu wa Wilaya Mbozi, John Palingo (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo uliopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Mbozi, Fred Mgeni (kulia) wakati akikagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo uliopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, John Palingo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malolo wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo jana, alikagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo na kuagiza zoezi la uwekaji vigingi vya mpaka likamilike ifikapo Desemba 3l.

  0 0


  Catherine Triphone wiki iliyopita alitimiza ndoto yake ya kusoma baada ya kushinda milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine ambaye anaishi na wazazi wake, siku ya jumapili alikuwa nyumbani peke yake huku akisinzia alipopigiwa simu iliyobadilisha maisha yake.

  Dada huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akicheza Tatumzuka mara kwa mara kwa kutumia namba zinazoendana matukio mbalimbali yanayohusu maisha yake na ndugu zake ambapo ameshinda mara kadhaa katika droo za kila saa.

  "Namba zangu daima zimekuwa 842. Hizi namba zinawakilisha siku , mwezi na mwaka wangu wa kuzaliwa. Ninaishukuru Tatu Mzuka kwa kutoa fursa hii ambapo mtu yoyote anaweza kucheza na kushinda, " aliongeza Bi Catherine

  Dhamira ya Tatu Mzuka kwa sasa ni zaidi ya kubadilisha maisha ya washindi wetu; tumejizatiti pia kuunga mkono mipango mbalimbali ya serikali katika jamii ili kuboresha maisha ya Watanzania wote. Mpango huu ni sehemu ya kauli mbiu yetu ya ‘Ukishinda, Tanzania inashinda’.

  "Kwa ushirikiano na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori tumeamua kununua vitabu kwa baadhi ya shule Wilayani humo. Tunatarajia kukamilisha taratibu zote na kutoa vitabu hivyo hivi karibuni. “ Alisema Sebastian Maganga, Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka.

  Kwa kuupendezesha msimu huu wa sikukuu, Tatu Mzuka imeahidi kufungua msimu huu wa furaha kwa kutoa shilingi milioni 500 kuanzia sasa mpaka Desemba 31, 2017. Utajisikiaje kama utamaliza mwaka kwa kupata ushindi mkubwa? Endelea kucheza, uendelee kushinda. Natumai Bi Catherine atafurahia sana sikukuu ambapo ni baada ya kucheza Tatumzuka kwa shilingi 500 tu.” Bwana Maganga alihitimisha

  Bi Catherine anapanga kurudi shule kusoma kusoma shahada na kuwanunulia wazazi wake usafiri ili kuwaondolea adha ya usafiri wanayokumbana nayo.

   Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,alipokuwa akimtangaza Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).
   Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).akitoa ufafanuzi namna alivyoshinda hizo milioni 60 na namna atakavyozitumia,ambapo Catherine amesema kuwa fedha hizo atazitumia kujielimisha .
   Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi,Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).

  0 0

   Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge (kulia) akiwatambulisha viongozi wa mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) walipomtemtembelea kumkabidhi hati ya kutambuliwa na Shirikisho la dunia la mchezo huo jana Jijini Dar es Salaam
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akipokea hati ya utambulisho wa mchezo wa Base Ball na Soft Ball kutambuliwa na Shirikisho la dunia la mchezo huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania Dkt. Ahmed Makata (kushoto) jana Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisoma hati ya utambulisho ya mchezo wa Base Ball na Soft Ball baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania Dkt. Ahmed Makata (kushoto) jana Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Base Ball na Soft Ball Tanzania Dkt. Ahmed Makata (kushoto) baada ya kumkabidhi taarifa na hati ya utambulisho wa mchezo huo kutambuliwa na Shirikisho la dunia la mchezo huo jana Jijini Dar es Salaam.
  Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM


  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Umlemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akifungua mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ukumnbi wa Simba, Kituo cga Mikutano cha Kimataifa, AICC Arusha leo Novemba 29, 2017
    
   NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA
  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa mafanikio ambayo Mfuko umepayata katika kipindi cha muda mfupi tangu uanzishwe.
  Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) jijini Arusha leo Novemba 29, 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema, katika kipindi kifupi cha miaka miwili tangu WCF ianizshwe Mfuko umeweza kutekeleza wajibu wake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama na kulipa Mafao ya Fidia.
  “Mfuko umeanza kufikia wanyonge kwani umeonyesha jinsi ambavyo wafanyakazi wanyonge waliokuwa hawalipwa fidia wanapopata madhara kazini, sasa kutokana na kuwepo kwa Mfuko huu wanyonge wameanza kufaidi matunda kama ambavyo serikali ilidhamiria.
  “Nitoe wito kwa viongozi wa Mfuko, endeleeni kutoa elimu kwa wananchi hususan waajiri ili waweze kujisajili na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuwalipa fidia wafanyakazi wao pindi wanapopata madhara wawapo kazini.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba amesema hali ya Mfuko ni njema tangu uanzishwe, “Tunapokutana leo hii kwa mara ya kwanza kabisa, napenda kuwajulisha kuwa Mfuko umekuwa ukifanya vizuri katika kuimarika kifedha ambapo kwa mwaka wa kwanza tu, Mfuko ulifikia kiasi cha shilingi Bilioni 65.68 na katika mwaka wake wa pili ambapo ndio huu tulio nao napenda kuwafahamisha kuwa Mfuko umekuwa hadi kufikia Shilingi Bilioni 135 fedha ambazo bado hazijakaguliwa lakini sitarajii tofauti kubwa sana hata zoezi la ukaguzi litakapofanyika”. Amesema Bw. Mshomba.

  Aidha Bw. Mshomba alisema, madhumuni ya Mkutano huu wa siku mbili ambao umebeba kauli mbiu ya "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”.  ni kutoa taarifa ya mwaka ya Mfuko, kutathmini maendeleo na changamoto zinazoukabili Mfuko na kupokea maoni ya kuboresha huduma za Mfuko.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba amesema, tangu Mfuko uanzishwe, umetoa mafunzo mbalimbali  kwa wadau wa Mfuko ikiwa ni pamoja na Madaktari.
  “Hadi sasa Mfuko umetoa mafunzo kwa Madaktari 504 nchi nzima kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini za ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi”. Amesema Bw. Humba.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofiosi ya Waziri Mkuu, Mhe. Anthony Mavunde, akitoa hotuba yake
  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mashomba, akitoa hotuba yake
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, wakati alipowasili kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha leo Novemba 29, 2017
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati akiwasili kqwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC jijini Arusha leo Novemba 29, 2017
   Mhe. Mhagama na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na 
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar,
   Mbunge wa Chalinze, Mhe., Ridhiwani Kikwete, (kulia), akizungumza na Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Bw. Anslem Peter.
   Afisa wa WCF, Bw. Edward Kirenga, (kushoto), akiwasajili wajumbe wa mkutano
   Kutoka kushoto, Mhe. Waziri Mhagama, Dkt. Irine Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akitoa hotuba yake.

  Dkt. Isaka, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Stella Ikupa, (kushoto), wakati wa mkutano huo.
  Kikundi cha bendi ya Mjomba, (Mrisho Mpoto), kikitumbuiza
  Viongozi wakishuhudia burudani ya kikundi cha bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto.
  Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Bw.Anselim Peter, (wapili kulia), akijadiliana jambo na maafisa wa Mfuko huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Dkt. Irine Isaka, (kulia), akisalimiana na Meneja Mafao wa WCF, Bi. Rehema Kabongo
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), Meshac Bandawe , (kushoto), akisalim iana na Meneje Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele
  Wajumbe wamkien delea kusajiliwa kabla ya kuingia ukumbini.
  Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Emmnuel Humba, (kulia), akibadilishana mawazo na wajumbe wenzake wa bodi, Dkt. Francis Michael, (wapili kulia), na Bw.Richard Wambali
  Baadhi ya wakurugenzi nna mameneja wa WCF

  0 0

    Catherine Amri from UNESCO Dar es Salaam conducting a training in Korogwe 

   282 men and women from selected villages in Tanga region have participated in a three days training organized by UNESCODar es Salaam Office to build their capacities in supporting the implementation of the of Global Learning XPRIZE Project for the Promotion of Early Learning through Innovative Technologies in Tanzania. 

  The group of participants comprised one selected community memberand a member of the village council from each participating village. The selected community members, also known as ‘Kitongoji (hamlet) mama and baba’ will perform the tasks related to the overall monitoring of the project at the community level and conduct the survey in terms of the Social Emotional Impact Study. 

  Each kitongojimama/baba will be supporting a group of about 5 to 21 children, from the selected 141 remote and underprivileged hamlets in Mkinga, Muheza, Handeni, Korogwe, Lushoto, and Pangani districts in Tanga region. The Global Learning XPRIZE Project for the Promotion of Early Learning through Innovative Technologies in Tanzania aims to reach about 2,060 out of school children in Tanga region to promote the improvement of cognitive outcomes in terms of the 3R’s (reading, writing and arithmetic).Catherine Amri from UNESCO Dar es Salaam conducting a training in Korogwe 

   The training equipped vitongojimama and baba with the knowledge on the goals and objectives of the project, reporting procedures of technical issues, overall monitoring activities and basic skills to identify behavioural and social emotional changes occurring in the participating children and their families in the course of fifteen months of the field test, corresponding to the period which children will interact with the software.

  The vitongoji mama and baba are key players for the success of the implementation of the project, and building their capacity in terms of the project knowledge, was one of the most relevant milestones regarding the preparation of the field testing and will contribute to empower members of rural, remote and underprivileged communities. 
   A training session in Pangani

  0 0

  US entertainer, Dj Supreme from Seattle, Washington, is set to rock Dar es Salaam this week. The 3 day event will be held in the company of Tanzania’s own DJ Vasley, DJ Sma and DJ FU. The 3 day events will be held at exclusive but divergent locations and hotels in Dar es Salaam.

  Dj Supreme currently has over 50,000 records in his collection. While in Tanzania he will be looking sinto growing his number of records.

  “I stopped counting (the records’ numbers) at 50,000 but there’s still so many (records) I don’t have that I need. In fact one of my main mission’s while in mama Africa is to acquire original African records on vinyl," says Dj Supreme.

  He adds: "I'm looking for funk, soul, disco, boogie, high life, rock groups like Asiko, Geraldo Pino, Kelenkye, Marijata, Rob, Witch, and William Onyebor vinyl records.They are probably sitting somewhere in someone's house collecting dust. If anyone can help me out with getting records please do so.”

  The events are organised by the new event company in Dar es Salaam, Xfinity Entertainment. Dj Supreme’s official 3 day events will be on 30th November (Thursday), 1st December (Friday) and 2nd December (Saturday). The 3 events are sponsored by Jameson and Red Bull and will have Clouds Media Group as the official media partner.

  Xfinity is a fuse of jazz, funk, soul and lingala wrapped in bongo flava. The events and lifestyle company was founded this year, 2017, to meet the needs of the ever-changing social and entertainment industry in Tanzania and the rest of East Africa.

  Currently Xfinity holds 3 events on a weekly basis on the affluent Masaki area in Dar and within the Central Business District (CBD.) It is headed by DJ Vasley, DJ Sma and DJ FU.The Xfinity DJs (DJ Vasley, DJ Sma, DJ FU) have worked alongside the likes of Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Jux, MiCasa, Black Motion, Tinie Tempah, Furture plus many more artists and a host of local/international world renowned Djs.

  On Dj Supreme's itinerary includes a visit to the historic island of Zanzibar where there’s a spice tour already booked out for him. The Los-Angeles born Dj will also do a media tour courtesy of Clouds Media Group.

  Dj Supeme also known as Supreme la Rock will also get to hang out with local celebrities including Dj D-Ommy where there’s a planned culture exchange where he (Dj Supreme) will be inducted into the Swahili culture.

  He will get a chance to compare techniques with Dj D-Ommy during their sessions together. A major social media calendar has already been planned to keep fans on the loop of his visits around Dar and showcasing of his Dj skills.

  “I’m excited to be coming to East Africa and Tanzania for the very first time after hearing so much about it. Hopefully I will get to learn more on the Swahili culture and music, collect Bongo music along the way and trade a few skills with the Djs in Tanzania,” concludes Dj Supreme ahead of his visit.


  0 0

  Tangu kuzinduliwa Dirisha la Ukusanyaji Kodi kidigitali June mosi 2017 (Electronic Revenue Collection System - eRCS) ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mohamad Shein,  mawaziri kadhaa wa serikali za Muungano na serikali ya Mapinduzi; Kwa mara ya kwanza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipatia bila bugudha Ushuru mkubwa wa bidhaa na kodi ya Ongezeko la Thamani zitokanazo na makampuni ya simu. 

  Mfumo huu uliosukwa na vijana wa Kitanzania wazalendo, umefanikisha kuongeza mapato litokanalo na mtandao (Ciber Space) kwa Zanzibar kwa 51% kwa robo ya tatu ya mwaka 2017 ukilinganisha na miezi kama hiyo 2016. Uchunguzi uliofanyika katika robo hiyo (tatu) ya mwaka 2017 (Julai,August na Septemba 2017), umebaini Zanzibar imelipwa kupitia mfumo wa eRCS Tsh Bil 7.2 ambayo imeongezeka kwa 51% ukilinganisha na miezi kama hiyo mwaka 2016 ambapo makusanyo ya jumla ya kodi yalikuwa  Tsh Bil 3.5 pekee.
  Kwa mujibu wa vielelezo vya makusanyo wa TRA, miezi mitatu kabla ya mfumo huu kuzinduliwa rasmi (April,May na June); Makampuni ya simu yalilipa jumla ya kodi ya  Tsh Bil 101.7 lakini baada ya kuzinduliwa rasimi kwa mfumo huu wa eRCS na makampuni ya simu (TTCL, HALOTEL, AIRTEL, VODACOM, ZANTEL, SMART na TIGO) kuugwa ndani ya mfumo; Kwa kipindi cha miezi mitatu pekee ( Julai,Agost na Septemba 2017), yameweza kulipa kwa njia ya kielektroniki Tsh Bil 128.9 kukiwa na ongezeko la Sh Bil 27.2 sawa na 21% huku ongezeko la kodi ya thamani ikipanda kwa 9% yaani Tsh. Bil 4.7 sambamba na ongezeko la Ushuru wa Bidhaa 29% yaani Tsh. Bil 22.
  Taarifa za kiuchunguzi zimebaini serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu wowote utakao ama uliojitokeza kabla na baada ya mfumo hasa taarifa za makampuni ya simu katika matumizi yaoya kila mwezi.Mpaka sasa, benk kadhaa nchini zimekamilisha taratibu za kuungwa katika mfumo huu na kuanza kulipa kodi kielectroniki.  Huu ni ushindi mkubwa kwa mkakati wa Rais Magufuli katika kupata njia bora za kukusanya mapato nchini. Ikumbukwe wajenzi wa mfumo huu ni vijana wazalendo walioaminiwa na serikali ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika katika ujenzi wa mfumo huo kutumia wataalamu na makampuni ya kigeni.Hivi ndivyo mapato yanavyoonekana katika Dashibodi ambazo viongozi wakuu wa nchi wanaona mapato yanavyokusanywa kielectroniki kwa kutumia mfumo  wa eRCS kila sekunde.
  Jedwali hili linaonyesha  Mabenk yaanza kulipa baada ya yale yaliyokamisha kujiunga na ERCS ambyo ni BANK M na AMANA BANK Tanzania ina Mabenk zaidi  ya 20

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe aliongoza kikao cha wadau kujadili mradi wa maji katika halmashauri za Mkoa wa Simiyu. Tayari tahmini ya mazingira imekamilika na kazi ya upembuzi yakinifu ipo katika hatua za mwisho na zabuni imepangwa kutangazwa mwezi Januari 2018 baada ya kukamilika kwa zabuni, Ujenzi wa Mradi unakadiriwa kuchukua miezi 24.

  Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira iliwasilisha ombi la fedha kwa Mfuko wa Global Climate Fund (GCF) ili kutekeleza Mradi wa maji katika halmashauri zilizopo Mkoa wa Simiyu unaojulikana kama Simiyu Climate Resilience Water Supply Project. Kuibuliwa kwa Mradi huu kulitokana na uhitaji mkubwa wa maji katika Mkoa wa Simiyu kulikosababishwa na ukame wa muda mrefu.
  Mradi huu, umepangwa kutekelezwa kwa awamu mbili katika Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu. Wilaya hizo ni Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu. Katika Awamu ya kwanza, Mradi utatekelezwa katika Wilaya za Busega, Itilima na Bariadi. Kiasi cha Euro milioni 140.7 sawa na takriban shilingi bilioni 375.4 zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa mradi huo.

  Fedha za kutekeleza Awamu ya Kwanza ya Mradi zitachangiwa na Serikali ya Tanzania na Washirika wa Maendeleo ambao ni GCF na Serikali ya Ujerumani. GCF watachangia Euro Milioni 102, Serikali ya Ujerumani watachangia Euro Millioni 25.6 na Serikali itachangia Euro Millioni 13.1 na wananchi nao kupitia nguvu zao watachangia Euro Millioni 1.5. Matumizi ya Fedha za GCF na Serikali ya Ujerumani yatasimamiwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).

  Lengo kuu la Mradi ni kuboresha afya na kuongeza uzalishaji mali ili kuinua hali ya maisha ya wananchi walioathirika na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo husika ya Mradi.
  Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika kwa kujenga mfumo wa uzalishaji na usafirishaji maji na kuboresha mfumo wa usambazaji wa maji katika miji na vijiji husika.

  Mradi pia utahusisha kujenga kwa mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji endelevu (Smart Agriculture) ambayo pia yatatumika kunyweshea mifugo pamoja na kuimarisha huduma za usafi wa mazingira kwa kujenga mabwawa ya kukusanyia na kuchuja majitaka na vyoo vya mfano mashule na vituo vya afya.

  0 0

   Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam, mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu
   Mwenyekiti anayemaliza muda wake   wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha,   akizungumza wakati wa   Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto  aliyevaa kofia ni Mgeni Rasmi na Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni. Mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. 
   Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha Uongozi , Kiongozi anayemaliza muda wake katika Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Ibrahim Mpwapwa (kulia), wakati wa mkutano uliofanyika leo,ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. 
   atibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akipiga makofi baada ya kuwasili  katika Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho,mkoa wa Dar es Salaam, Mkutano huo umefanyika leo Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi,mkoa wa Dar es Salaam, wakishangilia wakati Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo, ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia tarehe 24/11/2017 hadi 25/11/2017 limeendesha zaoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Songo Songo ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri zaidi ya masaa mawili kufuata huduma ya vipimo hivyo katika Hospitali ya Kilwa kivinje.

  Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya TPDC inayosimamia uendesheshaji na utunzaji wa Miundombinu ya Uchakataji na Usafirishaji wa Gesi Asilia inayoitwa GAS COMPANY (GASCO) Mhandisi Baltazari Mrosso wakati wa ufungaji wa zoezi hilo ameeleza kuwa ni wajibu wao kama Shirika kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuboresha maisha ya Wananchi wa Songo Songo ambao pia ni tegemeo kubwa katika shughuli zinazofanywa na Shirika kuanzia kwenye uzalishaji wa gesi visimani, uchakataji kiwandani na usafirishaji.
  Diwani wa Kata ya Songo Songo Mh. Said Mwinyi akifungua rasmi zoezi la upimaji kwa kukipatiwa huduma ya upimaji wa Shinikizo la Damu kutoka kwa Daktari Octavian Modest.

  “Sisi kama Shirika la Umma ambalo limewekeza katika Kisiwa hiki katika shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia tunao wajibu wa kushirikiana na wananchi pamoja na uongozi wa Songo Songo ili kuboresha maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi, kuboresha uhusiano na kuendelea vyema na shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia na hivyo leo hii tunahitimisha zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi wa Songo Songo pamoja na kukabidhi vifaa tiba vya upimaji wa ugonjwa wa Kisukari ambavyo hapo awali havikuwepo.” Alieleza Kaimu Meneja Mkuu GASCO.
  Daktari wa TPDC, Octavian Modest akimtibu moja ya Wazee wa Kijiji cha Songo Songo waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa Afya liloratibiwa na kufadhiliwa na TPDC.

  Mhandisi Mrosso aliongezea kuwa utaratibu huu wa upimaji wa Afya ni endelevu na utakuwa unafanyika mara kwa mara pamoja na kuchangia kwenye ununuzi wa vifaa tiba mbavyo vinasabisha usufumbufu kwa wananchi wa Songo Songo kusafiri baharini kwa mwendo wa zaidi wa masaa mawili kufuata huduma za vipimo na tiba mbalimbali katika Hospitali ya Kilwa Kivinje pamoja na hayo alimuomba Mh. Diwani wa Kata ya Songo Songo kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhamasisha Wananchi kuondoa woga wa kupima afya zao.
  Wahudumu wa Afya wakimsaidia Mmoja wa Wazee waliojitokeza kupima afya zao katika Zahanati ya Songo Songo.

  Aidha Mh. Diwani ndugu Mh. Said Mwinyi wa Kata ya Songo Songo ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha TPDC kutekeleza zoezi hilo kwa wananchi wa Songo Songo ambalo limeonyesha utayari wa TPDC katika kuhakikisha Kijiji cha Songo Songo kinaimarika katika Sekta ya Afya.

  “Kwakweli TPDC mmetupenda wana Songo Songo kwa kutupatia huduma hii muhimu kwa ajili ya kujua afya zetu kitendo ambacho kinamuwezesha kila mmoja kujitambua hali yake, kujikinga na kujitunza na maradhi mbalimbali pamoja na kupata tiba sahihi kulingana na tatizo lililogundulika kama hali halisi ilivyo bado tuna upungufu wa vifaa tiba na leo tunshukuru TPDC kutupatia vifaa vya kupima ugonjwa wa Kisukari ambavyo hatujawahi kuwa navyo na tunaamini vingine hapo mbeleni mtatuletea ili kuhakikisha nasi ndugu zenu tunapata huduma bora ya afya” alieleza Mh. Diwani.
  Baadhi ya Wananchi wa Songo Songo wakiwa kwenye foleni ya kusubiri kufanyiwa vipimo vya magonjwa mbalimbali katika Zahanati ya Kijiji cha Songo Songo Mkoani Lindi.

  Aidha wakati wa ufunguzi wa huduma hiyo, akieleza nia ya zoezi hilo muhimu kwa wananchi, Meneja Mawaasiliano wa TPDC, Marie Msellemu amesema upo umihimu mkubwa wa kila Mtanzania kujua afya yake ili aweze kujikinga na maradhi mbalimbali, kudhibiti madhara ya maradhi aliyonayo, kuimairisha afya zetu na kuweza kulitumikia taifa kikamilifu.

  “Sisi kama TPDC tunaona ni wajibu wetu kuhakikisha ndugu zetu wa Songo Songo ambao eneo lao ndilo gesi iligundulika kwa mara ya kwanza wanapata fursa ya kupima na kutambua afya zao ili waweze kuwa na nguvu na afya bora na hivyo kuwawezesha kutekeleza shughuli zao za kila siku na ndio maana TPDC tumeamua kuendesha zoezi hili muhimu kwa wananchi wa Songo Songo” Alieleza Bi. Msellemu.

  Zoezi la upimaji wa Afya liliambatana na mashindano ya mpira wa miguu, mpira wa pete na utoaji wa hundi ya Shilingi 4,613,100 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mwalimu wa Shule ya sekondari ya Songo Songo.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa kiuchumi nchini(NEEC),Bengi  Issa akizungumza wakati alipokuwa akifungua Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu iliyofanyika katika ukumbi wa Tasisi ya utafiti nchini REPOA Jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na IDRC na TASAF.
  Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya utafiti ya REPOA ,DK .Donald Mmari akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kufungua Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu
  Muwakilishi wa tasisi ya IDRC Kutoka nchini Canada ,Dr Arjan De Haan akizungumza na na wadau waliofika katika warsha hiyo namna taasisi yake ilivyohusika katika tafiti za kumuwezesha mwanamke kiuchumi kupitia mtandao wa simu.
  Mtafiti kutoka Tasisi ya Utafiti ya REPOA , Dr.Abel Kinyondo akizungumza na wadau walioshiriki Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu ambapo alipata fursa ya kuwaeleza wadau faida na changamoto ya huduma hiyo katika mradi wa TASAF.
  Mtafititi kutoka Tasisi ya Utafiti ya REPOA, Dr. Blandina Kilama akitoa neno la ukaribisho kwa wadau waliofika katika Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu iliyoandaliwa na REPOA kwa kushirikiana na IDRC na TASAF
  Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa Warsha Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu
  Washiriki wa warsha hiyo wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa Warsha Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu.

  0 0

  Wasanii wa kizazi kipya wanaochipukia, Ibrahim Jakob na Happy Best wakishambulia jukwaa kwenye Tamasha la wanachuo lijulikanalo kama ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ lililofanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  Msanii wa Muziki wa Bongo Flava, Juma Kassim Nature akiwapagawisha Wanafunzi kutoka Vyuo vikuu  vya  jiji la Dar es Salaam katika Tamasha lililoratibiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel lilopewa jina la ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ ambalo lilifanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

   Msanii wa Muziki wa Bongo Flaver, Young Killer akiimba pamoja na Wanafunzi wa Vyuo vikuu  vya  jiji la Dar es Salaam kwenye Tamasha lililoratibiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel lililopewa jina la ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ ambalo lilifanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Maonyesho ya Utalii wa Tanzania yalivyofanyika mjini Riyadh nchini Saudi Arabia kwa watu mbalimbali kutembelea kwenye maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Aidha Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
  Maonyesho yakiendelea kwa wageni mbalimbali kuelezewa namna ya vivutio vya utalii wa Tanzania.Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza kushoto akiwa na mke wake, Maimuna Mgaza, wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Utalii.
  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza mwenye suti nyeusi mkono wa kushoto akijadiliana jambo na wageni wake waliotembelea katika maonyesho ya utalii yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini hapa. Hapa maonyesho ya chakula yakiendelea mjini Riyadh, nchini Saudi Arabia.

  0 0

  Taasisi ya the voice of the voiceless Jumapili hii ili pata balozi wao mpaya ambaye atakuwa anaiwakilisha taasisi na kuwa balozi wa mradi wao wa TUNZA FUNGUO YAKO.

  Balozi huyo anafamika kwa Jina la SELEMBE ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Awali wakati wa tukio la ukabizishaji wa jezi ya taasisi hiyo Bwana Selembe alishukuru taasisi hiyo na  kuonyesha furaha yake ya kuchaguliwa na kupewa cheo icho kwakuwa yeye pia ni mzanzibar amefarijika kuona kuwa balozi ambaye atasimania kuongoza mradi wa 

  TUNZA FUNGUO YAKO.
  Taasisi ya VOV foundation katika kuboresha mradi wao na kuweza kufika mbali nakupata wadau ambao watachangia kwa mwaka 2018.Kwa upande wake Omary A. Mdogwa ambaye ni mwanzilishi wa taasisi hiyo alikuwa alibainisha kuwa waliamua kumchagua Selembe kutokana na ushawishi wake kwa mchezaji huyo visiwani humo pamoja na kuangalia mambo mengine mbalimbali kama vigezo tosha kwa kuwa balozi wao.

  "Tume mchagua bwana Selembe kwa nia moja tu ya kufanya utofauti na kuangalia upenzi wa mpira kwa upande wa Zanzibar. Pia tutatumia mchezo wa mpira kuweza kufanya 'donation' mbali mbali ili kuweza kusaidia vijana walio mashuleni "Alieleza Mdogwa.
  Balozi mpya wa Taasisi ya the voice of the voiceless ambaye atakuwa anahiwakilisha taasisi na kuwa balozi wa mradi wao wa 'TUNZA FUNGUO YAKO' Selembe ambaye pia ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar
  Balozi mpya wa Taasisi ya the voice of the voiceless ambaye atakuwa anahiwakilisha taasisi na kuwa balozi wa mradi wao wa 'TUNZA FUNGUO YAKO' Selembe ambaye pia ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar
  Viongozi wa Taasisi ya the voice of the voiceless wakimkabidhi jezi maalum Selembe  ambaye atakuwa anahiwakilisha taasisi hiyo kama Balozi wa mradi wao wa 'TUNZA FUNGUO YAKO'. Viongozi hao kulia ni Mwanzilishi wa Taasisi hiyo Omary Mdogwa na kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa vov foundation, Bi Anatolia Kasira

older | 1 | .... | 1445 | 1446 | (Page 1447) | 1448 | 1449 | .... | 1897 | newer