Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1444 | 1445 | (Page 1446) | 1447 | 1448 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na Ujumbe wa Mawaziri kutoka Uganda. Katikati ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter na Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania. 
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na Ujumbe wa Mawaziri kutoka Uganda (hawapo pichani). Katikati ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim Mruma.
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (mbele katikati) akizungumza wakati wa mkutano na Ujumbe wa Mawaziri kutoka Uganda (kushoto) na baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Madini (kulia).
   Mawaziri kutoka Uganda wakimsikiliza Waziri wa Madini nchini, Angellah Kairuki (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter, Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala,  Namugwanya Bugembe na Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki.
   Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka akiwasilisha mada ya masuala mbalimbali ya Sekta ya Madini, nchini Tanzania.
  Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani wa Uganda, Obiga Kania (kushoto). Katikati ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter. 

  Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amekutana na Mawaziri Wanne kutoka nchini Uganda ambao wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa Sekta ya Madini.
  Mawaziri hao ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter, Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala,  Namugwanya Bugembe na Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki.
  Waziri Kairuki amekutana na ujumbe huo Novemba 28, 2017 katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za Madini nchini ikiwemo suala la Sera, Sheria na Kanuni za Madini pamoja na masuala yanayohusu Wachimbaji Wadogo wa madini.
  Majadiliano baina ya Wizara na Ujumbe huo vilevile yalihusisha uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa Kamishna wa Madini, Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
  Ujumbe huo utatembelea migodi mbalimbali ya Dhahabu inayomilikiwa na wazawa iliyoko mkoani Geita ili kujionea uendeshaji wa migodi hiyo na hivyo kupata uzoefu wa namna ya uendeshaji wake.
  Aidha, ujumbe huo wa Mawaziri kutoka nchini Uganda, utatembelea nchi mbalimbali Barani Afrika ili kupata uzoefu wa usimamizi wa Sekta ya Madini hususan suala la Wachimbaji Wadogo.

  0 0

  Mahakamani ya Hakimu mkazi ,Moshi.
  Anayetajwa kuwa mmilikiwa wa shule ya sekondari ya Scolastica,Edward Shayo akifikishwa katika mahakamani ya Hakimu mkazi ,Moshi.
  Anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica,Edward Shayo akijiandaa kuingia chumba cha mahakama Jana.
  Anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji ndogo wa Himo ,Edward Shayo na wenzake wawili ,Hamid Chacha ,Laban Nabiswa wakisindikizwa kuingia chumba cha mahakamani.
  Anayetajwa kuwa mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ,Edward Shayo na wenzake wawili wakitoka nje ya chumba cha mahakamani Mara baada yabkusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia .
  Mmoja wa ndugu wa kijana Humphrey Shayo akilia kwa uchungu wakati akitoka katika chumba cha mahakama
  Ndugu wa anayetajwa kuwa mmilikiwa wa shule ya Sekondari ya Scolastica,Edward Shayo wakionekana kwenye huzuni Mara baada kusomewa kwa mashtaka ya mauaji kwa ndugu yao hiyo
  Anaandika Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,kanda ya Kaskazini.

  WATUHUMIWA watatu kati ya 11 wanao shikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica ,Humphrey Makundi wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa shtaka la mauaji .

  Washitakiwa wawili ,Hamis Chacha aliyekuwa mlinzi wa shule ya Skolastica na Labani Nabiswa walifikishwa mahakamani hapo wakitokea kituo kikuu cha kati cha Polisi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi wenye silaha .
  Baada ya Nusu saa Mmiliki wa shule ya Scolastica ,Edward Shayo alifikishwa mahakamani hapo na askari Kanzu akitokea Hostali ya Rufaa ya KCMC alipokuwa akipatiwa matibabu ya baada ya kupata tatizo la kiafya tangu kushikiliwa kwake.

  Upande wa Jamhuri katika shtaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi ,Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea ,Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko anyemtetea Mshatakiwa wa pili katika shtaka hilo Edward Shayo.

  Akisoma maelezo ya hati ya mashtaka mbele ya mahakama hiyo ,Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshtakiwa wa kwanza ,Hamis Chacha(28),wa pili Edward Shayo (63)  na wa tatu Laban Nabiswa (37) walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.

  Kutokana na maelezo hayo Hakimu ,Mawore alieleza kuwa washtakuwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shtaka la mauaji huku akiwataka kungojea kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.

  Kuhusu upelelezi wa Shtaka hilo Mwanasheria wa serikali Nassiri aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku akiwasilisha ombi la kupangwa tarehe nyingine kwa ajili kutajwa kwa shauri hilo wakati upelelezi ukikamilishwa.

  Hakimu Mkazi ,Mawore aliahairisha shtaka hilo na kupanga kutajwa kwa shtaka hilo Desemba 8 mwaka huu  na  kwamba washtakiwa wote watarudishwa Rumande kutokana na  kesi hiyo kutokuwa na dhamana .

  Washatakiwa hao wamefikishwa mahakamani zikiwa  zimepita siku 11 tangu kufukuliwa kwa mwili wa mtu aliyezikwa na Halmashauri ya Manspaa ya Moshi kuondoa utata wa kupotea kwa Mwanafunzi Humphrey Makundi (16) aliyekuwa anasoma shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro

  0 0


  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge amewataka watumishi na viongozi wa Halmashauri Mkoani humo kuhakikisha wanayapa kipaumbele  mambo matano ikiwemo kudumisha hali ya Ulinzi na Usalama ambayo  ndiyo nguzo muhimu  inayopelekea shughuli nyingine za maendeleo kufanyika kwa ufanisi ili kuifanya  Makao Makuu ya Nchi Dodoma ikue kwa kasi.

  Mambo mengine aliyoyayaorodhesha Mkuu huyo wa Mkoa kama dira ya kuharakisha maendeleo ni pamoja na utayari wa kubadilika kwa watumishi na kutofanya kazi kwa mazoea, utoaji wa huduma bora na zenye viwango kwa wananchi, kudumisha dhana ya Ushirikishwaji baina ya Taasisi na miongoni mwa watumishi, na kuepuka migogoro baina ya watumishi ndani ya Taasisi hali inayoweza kudumaza malengo ya Serikali katika kuwadumia wananchi.

  Mkuu wa Mkoa Mahenge aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma alipofanya ziara ya kujitambulisha katika Wilaya ya Dodoma Novemba 24 mwaka huu.

  Awali alipokea taarifa ya maendeleo ya Wilaya iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakati alipokuwa katika ziara ya kujitambulisha katika Wilaya ya Dodoma Novemba 24 mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge na wa pili ni Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMA-OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA
   Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya kujitambulisha ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge (wa tatu kulia) Wilayani humo. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge na wa pili ni Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi.
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge  akizungumza wakati wa ziara ya kujitambulisha ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge katika Wilaya ya Dodoma ambapo alizungumza na watumishi wa Manispaa katika ukumbi wa Manispaa Novemba 24 mwaka huu.
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Wilaya ya Dodoma kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge (aliyevaa miwani katikati) wakati wa ziara ya kujitambulisha ya Mkuu huyo wa Mkoa katika Wilaya ya Dodoma. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge na wa pili ni Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe.

  0 0

  Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari   (hawapo pichani) mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
  Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akifafanua jambo kwa   waandishi wa habari  mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael. 


  Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo.Kulia ni Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh.

  Pata Simu za Smartphone BURE kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuuu!


  Dar es Salaam, Novemba 28, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo imetangaza dili za kipekee zinazohusu simu za Smartphone ambazo zitahakikisha kila mtu anakuwa sehemu ya maisha ya kidigitali katika msimu huu wa Krismasi na mwaka mpya.


  Akitangaza ofa hizo za msimu wa sikukuu Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema dili hizo kemkem zinapatikana kwa kupiga namba ya menu mpya *147*00#  na kubonyeza kitufe cha ‘Duka la Simu’ ili kuchagua simu unayoipenda, na kisha kutembelea Duka lolote la Tigo nchi nzima ili kuchukua simu uliyoichagua.


  ‘Katika ofa ya kwanza, wateja wa Tigo wanaweza kupata simu ya Smartphone BURE kirahisi kwa kununua bando kuanzia TZS 25 000 ambayo - pamoja na Smartphone ya bure – inawapa 1GB data, SMS 50 na dakika 50 za kupiga Tigo – Tigo,’ alisema.


  Katika dili ya pili, wateja wa Tigo pia wanaweza kupata Smartphone kwa kuchagua mpango wa kulipia kwa miezi sita. Ofa hii inawahusu wateja wa sasa wa Tigo ambao wanakidhi vigezo vilivyowekwa.


  Katika msimu huu wa sikukuu, Tigo pia inatoa ofa ya ‘Lipia sasa, Chukua Baadaye’ ambapo wateja wanaruhusiwa kuchagua simu yoyote ile wanayoipenda na kisha kufanya malipo ya awamu kila mwezi, ambapo wataruhusiwa kuchukua simu waliyoichagua baada ya kumaliza mpango wa malipo ya kila mwezi.


  ‘Kupitia ofa hizi kabambe, Tigo inaendelea kushika hatamu za ubunifu unaoendana na mahitaji ya wateja kwa kuwezesha kila mtu kumiliki mojawapo ya hizi simu bomba za Smartphone, ambazo zimeunganisha na mitandao ya jamii. Hii ndio njia yetu ya kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa sehemu ya maisha na mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ David alisema.


  ‘Tunawakaribisha wateja wetu wachangamkie ofa hizi za kipekee katika msimu huu wa sikukuu kwa kujigiftisha au kuwagiftisha ndugu, jamaa na marafiki kwa simu hizi bora za smartphone. Simu zote zinakuja na mpango rahisi wa malipo, bando murwa na ofa za kipekee ambazo zitahakikisha kila mtu ataweza kufurahia na kutunza kumbukumbu za shamrashamra za sikukuu katika simu yake mpya ya smartphone kutoka Tigo.’


  0 0


  Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart imewaonya Wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam wanaotoa fedha kwa Wafanyabiashara Wadogo wadogo ili kupinga zoezi lakuondoa kazi feki za sanaa.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama amesema Wafanyabiashara hao waache kuwatumia Wamachinga kupinga kuondoa kazi hizo ambazo zinaikosesha Serikali mapato na Wasanii kwa ujumla.

  Msama amewaasa Wafanyabiashara hao kuacha kabisa kuwatumia Wamachinga, amesema Wafanyabiashara hao watakamatwa kutokana na kuhamasisha maandamano.

  Pia amewaasa Wafanyabiashara Wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga kuacha kulalamika kwani Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wananchi hao, Wafanyabiashara wanaolipa Kodi kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.

  "Wamachinga acheni kulalamika, mnaopoenda kununua Filamu za nje na ndani hakikisheni Filamu hiyo ina Stika ya TRA, ukiuza yenye Stika mtu hatokukamata", amesema Msama.

  Hata hivyo, zoezi laukamataji Kazi feki za sanaa litaendelea katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima.
   Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart,Alex Msama alipokuwa akizungumza nao mapema leo ofisini kwake,kinondoni jijini Dar,kuhusiana na mkakati wake wa kupambana na uharamia wa kazi za sanaa
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart,Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.

  0 0


  Na.Vero Ignatus ,Arusha

  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF )umeandaa mkutano wa siku mbili utakaoanza kesho Jijini Arusha katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni Mafaofidia:Haki ya Mfanyakazi na chachu katika uchumi wa Viwanda mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Kassim Majaliwa 

  Akizungumza na waandishi wahabari Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF) Dr.Abdulssalaam Omary amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kutoa taarifa ya mwaka ya mfuko ,kutathimini maendeleo na changamoto zinazoukabili mfuko ,kupokea maoni ya kuboresha huduma za mfuko pia mada mbalimbali za uelimishaji zitatolewa na wataalamu mbalimbali wenye uzoefu kutoka baadhi ya nchi barani Afrika na kutoka Shirika la kazi Duniani (ILO) 

  Hadi sasa Mfuko umekusanya zaidi ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya matibabu kwa wanachama,hadi sasa taasisi 11,705 zimekwisha kujiunga na mfuko huo,2,105 bado hawajajiunga na mfuko huo wa fidia,ambapo Mkurugenzi Omary amesema kwa sasa wanajikita kutoa elimu kwa wafanyakazi waelewe kuhusiana na mfuko,wanatakiwa wafahamu kuwa kujiunga ni lazima  ili hapo baadae sheria itachukua mkondo wake.

  Kwa upande wake Meneja matekelezo (WCF) Victor Luvena amesema kuwa Sekta za Umma pamoja na sekta binafsi zote zinatakiwa kujiunga katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,waajiri wanatakiwa watume mchango wa wafanyakazi wao katika mfuko huo ambao ulianzishwa rasmi julai mosi 2015.

  Ameeleza katika mkutano huo pamoja na mambo mengine ,mgeni rasmi atatunuku tuzo kwa waajiri waliofanya vizuri katika utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi.
   Aliyepo katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF) Abdulssalaam Omary ,kushoto kwake ni Meneja Matekelezo (WCF )Victor Luvena na wakwanza kulia ni Mkuu wa kitengo cha Uhusiano Laura Kunenge.picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog


  0 0

   Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia  Lisa Heywood akibadilishana mawazo na Emma Thomas  na Faustina Mwapinga ambao wote ni Maafisa Uuguzi  wakati wa kambi ya upasuaji wa moyo ya siku tano inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Katika kambi hiyo wagonjwa 23 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua  kati ya hao watoto 13 na watu wazima 10. 
    Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia  wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto wa miezi sita ambaye mishipa yake ya  moyo ilikuwa na tatizo la kupeleka damu kwa wingi kwenye mapafu wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea JKCI. Hadi sasa jumla ya watoto watano na watu wazima wawili wameshafanyiwa upasuaji.
  Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) wakati wa kambi maalum ya upasuaji ya siku tano inayoendelea katika Taasisi hiyo. Hadi sasa jumla ya wagonjwa saba wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto watano na watu wazima wawili.
  Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia  wakiendelea na kazi ya kumfanyia  mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).

  Picha na JKCI

  0 0

    Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa nchi mbalimbali waliohudhulia katika Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Rais Uhuru Kenyatta iliyofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhuria sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. PICHA NA IKULU.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimpongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa awamu ya pili, katika Sherehe zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhuria sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya  ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo na  Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo, ili kubaini changamoto zilizopo za  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola.
   Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)
   Mkutano ukiendelea.
    Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.
   Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
   Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Sinza baada ya kufanya nao mazungumzo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.

  Na Dotto Mwaibale

  MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amewatembelea wateja wa MSD wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Dar e's Salaam ukiwa ni pamoja na Hospitali ya Mwananyamala na Sinza kubaini changamoto zilizopo katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuzipatia ufumbuzi.

  Katika ziara hiyo iliyofanyika jumanne jijini Dar es Salaam Bwanakunu amewataka wateja hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha Msd kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa Manunuzi maalumu.

  Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.

  Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na wamedata msaada wa magari kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.

  Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.

  "Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu na changamoto kubwa " alisema Bwanakunu.

  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola alisema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo kwa sasa ni asilimia  80 .

  "Changamoto iliyopo ni uhaba wa vitendanishi vya maabara na vifaa vya macho na meno ambavyo tunapata chini ya kiwango hivyo havikidhi mahitaji tuliyonayo," alisema.

  Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Daniel Mkungu alisisitiza haja ya ushirikiano baina ya Hospitali hizo na MSD ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.

  Ziara hiyo ya mkurugenzi huyo itaendelea tena kesho katika baadhi ya hospitali zilizopo jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke alisema kukamilika kwa utanuzi wa ujenzi wa Eneo la Maegesho ya Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar utatoa fursa ya kuongezeka kwa huduma za usafiri wa anga baina ya Zanzibar na Mataifa mengine Duniani.

  Alisema matayarisho ya ujenzi huo katika hatua za awali za Awamu ya Pili aliyoyashuhudia baada ya kushuka kwenye Uwanja huo wa Ndege wa Zanzibar yamempa faraja yeye pamoja na Uongozi mzima wa Benki ya Kimataifa ya Exim ya Nchini China iliyoridhia kugharamia Mkopo wa ujenzi huo.

  Balozi Wang Ke alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo wa Kidiplomasia.

  Alisema Zanzibar inaweza kurejesha Heshima yake ya kuwa Kituo cha Kibiashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki chenye uwezo wa kutoa huduma za Kibiashara kupitia mfumo wa kisasa wa Mawasiliano kupitia usafiri wa anga badala ya ule uliozoeleka wa Baharini.

  Alieleza kwamba zaidi ya Watalii 70,000 kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China wanaweza kuitembelea Zanzibar kila Mwaka kupitia usafiri wa anga na hata ule wa Baharini iwapo yataandaliwa mazingira mazuri katika Sekta ya Utalii baada ya kuongezeka kwa huduma za Mawasiliano ya usafiri.

  Bibi Wang Ke aliyeanza majukumu yake Nchini Tanzania Mwezi Mmoja sasa aliahidi kwamba Nchi yake iliyopiga hatua kubwa Kiuchumi ndani ya kipindi cha Miaka 30 itaendelea kuiunga mkiono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika kuona maendeleo ya Kiuchumi yanakua na kushirikisha wananchi wote siku hadi siku.

  Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza faraja yake katika kuona Viongozi wote waliiopo hivi sasa kati ya China na Tanzania bado wanaheshimu ushirikiano wa Mataifa hayo mawili ulioasisiwa na waanzilishi wake Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere na Hayati Mao Tse Tung.

  Balozi Seif alisema mchango mkubwa unaoendelea kutolewa na China kupitia Makampuni na Mashirikia yake mbali mbali umeiwezesha Tanzania kukuwa Kiuchumi na kustawisha Jamii mambo yanayokwenda sambamba na kupungua kwa kasi ya ukali wa Maisha.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza na kumuomba Balozi huyo wa China Nchini Tanzania kwamba Zanzibar bado inaendelea kuhitaji Wawekezaji pamoja na Watalii kutoka Nchini China katika azma yake ya kuimarisha uchumi hasa kwenye Sekta ya Utalii.

  Balozi Seif ameishukuru Serikali ya China kwa misaada yake mikubwa inayotowa na kumuhakikishia kwamba uhusiano wa Kihitoria uliopo wa Mataifa hayo rafiki utaendelea kudumu kila Mwaka.

  Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Mabalozi Wapya Wawili wa Tanzania Nchini Misri na Zambia walioteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

  Mabalozi hao ni Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor anayeiwakilisha Tanzania Nchini Misri na Balozi Abdulrahman Kaniki anayekwenda Nchi jirani ya Kusini mwa Tanzania ya Zambia.

  Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliwakumbusha Mabalozi hao kuzingatia zaidi suala ya Doplomasia ya Kiuchumi ambalo kwa sasa limechukuwa nafasi ya pekee tofauti na lile ya Kisiasa lililozoeleka katika mabadiliko ya Kiuchumi yaliyopo Ulimwenguni.

  Alisema matunda makubwa ya uwakilishi wa Mabalozi hao yataonekana katika kasi ya ongezeko la Miradi ya Uwekezaji kutoka katika Mataifa wanayokwenda kufanya kazi.

  Mapema Balozi wa Tanzania Nchini Misri Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor kwa niaba ya Mwenzake Balozi Abdulrahman Kaniki anayekwenda Nchini Zambia alisema wanaahidi kuitanga Tanzania katika Mataifa hayo rafiki yenye Uhusiano wa muda mrefu.

  Meja Jenerali Nassor aliziomba Taasisi zinazozimamia Sekta ya Utalii Nchini kuwa wazi kwa masuala yanayohitajika katika kuimarisha Sekta hiyo kupitia Wawekezaji na Mikataba ya uanzishwaji wa Miradi ya Hoteli.

  Baadae Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioongozwa na Naibu Waziri wake Dr. Suzan Kolimba.

  Katika mazungumzo hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Suzan alisema wako Zanzibar kufuatilia Rasimu ya Matayarisho ya Ripoti ya Utawala Bora Barani Afrika kwa upande wa Zanzibar inayotakiwa kutayarishwa na Wizara zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Dr. Suzan alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Ripoti ya Utawala Bora Barani Afrika itakuwa ndio Mpango Kazi kwa Maraisi wa Mataifa ya Bara la Afrika watakayoiwakilisha katika Kikao cha Umoja wa Afrika {AU} kinachotarajiwa kufanyika Mwezi Febuari mwaka 2018.

  Alisema hatua ya awali ya matayarisho ya Ripoti hiyo imeonyesha mafanikio kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa mfano bora wa Rasimu yake ya Utawala Bora kiasi cha Wataalamu wa masuala ya Kisiasa wa Bara la Afrika kushauri iwe kigezo cha kuigwa na Mataifa mengine Barani Afrika.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  28/11/2017.
  Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha Rasmi.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mabalozi wa China Nchini Tanzania na yule aliyepo Zanzibar.

  Wa kwanza kutoka Kushoto ni Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ken na wa kwanza kutoka Kulia ni Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bwana Xie Xiaolon.
    Balozi Seif akiagana na Ujumbe wa Kidiplomasia wa Ubalozi wa China Nchini Tanzania na Ule wa Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Balozi wa Tanzania Nchini Misri Meja Jegerali Issa Suleiman Nassor aliyekaa upande wa Kulia yake na Balozi Abdulrahman Kaniki aliyekaa upande wa Kushoto walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika nyadhifa hizo.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Suzan Kolimba Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa Zanzibar na Ujumbe wake kufuatilia rasimu ya Utawala Bora Afrika kwa Wizara za SMZ.
    Balozi Seif akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Muombwa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kati kati yao ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Suzan Kolimba.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria, katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, Mkoani Mara.Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala ikiwa na lengo la udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala , akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria  katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni   kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
   Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria katika kijiji cha Nyangombe, kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni  kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Mwananchi wa  kijiji cha Nyang’ombe akiuliza maswali kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ambapo naibu waziri aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, lengo la ziara hiyo ni kukagua  udhibiti uhalifu na  uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Wananchi wakishangilia jambo wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza  katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyang’ombe ,wilayani Rorya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  udhibiti uhalifu na  uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0  0 0

  Na Agness Francis, Blogu ya jamii.

  Mtandao wa Policy Forum( PF) ambao umetimiza miaka 9 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 ambapo ilianza kutumia  dhana ya  ufuatiliaji wa uwajibikaji  jamii ( Social Accountability Monitoring) wameungana na wadau katika mkutano wa kujadiliana mafanikio, changamoto  pamoja na mafunzo kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotumi dhana hiyo hapa nchini.

  Akizungumza hayo leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Kaimu mwenyekiti  Mtandao wa Policy Forum  ( PF), Herbon Mwakagenda amesema kuwa lengo hasa la mkutano huo ni  kuboresha mbinu zinazotumika na wadau  pamoja na kuangalia mafunzo ambayo yanaweza kutumika kwa ujumla ikiwemo pia kutoa pongezi kwa wananchi  kwa kuwa na muamko mkubwa wa kufatilia  haki zao katika mashirika mbalimbali ya Umma. 

  Nae pia  Mratibu wa mtandao wa Policy Forum  (PF), Semkae Kilonzo amezungumzia lengo kuwa  ni kutaka  kubadiilishana uzoefu na taasisi mbalimbali ili kuweza kuboresha zaidi   uchechemuzi  wa kutekeleza miradi  yao hapa nchini.

  Vile vile Mwenyekiti  Mwakagenda aliongezea hasa kwa kuzungumzi a changamoto zinazo wakabili wakati wa kufikisha ujumbe kwenye Halmashauri  mbalimbali  kutokana na ubadilishwaji wa viongozi wa halmashauri hizo na kusababisha taarifa kuchelewe kufika kama inavyotakiwa.

  Diwani Kiteto Manyara,Paulo Tunyon ametoa pongezi za dhati kwa wadau wa  mtandao wa Policy Forum( PF) kwa kuweza kupeleka mabadiliko  Vijijini kwa kukabiliana na changamoto hizo kutokana na uwelewa mdogo wa wananchi hao..
   Kaimu mwenyekiti  Mtandao wa Policy Forum( PF), Herbon Mwakagenda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mtandao huo jinsi unavyofanya kazi na wadau wa Taasisi mbalimbali hapa nchini leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere .
    Mratibu wa mtandao wa Policy Forum ( PF), Semkae Kilonzo  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna watakavyoweza kukabiliana na changamoto  ili kufikia malengo ya juu zaidi wanayokusudia leo Jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere 
  Wadau wa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini waliojitokeza kuhudhuria mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesisitiza kuwa wizara yake haitakuwa kikwazo cha utekelezaji wa ahadi ya Rais, Dkt. John Magufuli ya kuwapatia wananchi majisafi na salama, bali itasimimamia utekelezaji wa miradi hiyo ipasavyo ili ikamilike kwa wakati na kuleta tija.

  Aweso alizungumza hayo katika ziara yake ya kikazi aliyoianza katika mkoa wa Ruvuma, ambapo anakagua utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya zote mkoani humo.

  ‘‘Niwahakikishieni wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, zaidi ya kuhakikisha miradi yote tunayoitekeleza inaleta tija na kumaliza kero ya maji kwa wananchi kulingana na maagizo ya Rais. Hivyo, lazima fedha zifike kwa wakati na zitumike kwa usahihi ili miradi yote ikamilike kwa wakati kulingana na mikataba,’’ alisema Naibu Waziri.

  ‘‘Ni jukumu langu kusimamia hilo na ninawaagiza watendaji wote wasimamie miradi yote hatua kwa hatua na watoe taarifa sahihi za maendeleo yake, ili sisi viongozi tujue changamoto na kutoa msukumo katika kufanikisha miradi hiyo itakayokuwa na tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika,’’alisisitiza Aweso.

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ametoa pongezi kwa SOUWASA kwa usimamizi mzuri wa miradi na hatua inazozichukua kwa nia ya kumaliza kero ya maji katika maeneo ya mji huo kama Midizini na Misufini ambayo yalikuwa na kero kubwa, lakini kwa sasa wananchi kukiri kupata huduma hiyo.

  Katika ziara hiyo ameanza kwa kutembelea Wilaya ya Songea, ambapo ametembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA) na kuweza kuzungumza na menejimenti yake, pamoja na watumishi.

  Aidha, alitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hiyo ikiwemo eneo la mradi wa Bwawa la Luhira, mtambo wa kutibu na kusafishia maji wa Matogoro, mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi Songea.
  Huduma ya maji kwa mji wa Songea kwa sasa ni asilimia 79, ambapo lita milioni 10.6 zinazalishwa kwa siku na mahitaji yakiwa ni lita milioni 14 kwa siku kwa wakazi wa mji huo. Upanuzi wa mradi wa maji wa Songea mjini unaondelea hivi sasa unategemea kuongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 90 kwa mji wa Songea.                                                                                               
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (wa kwanza kulia) akikagua sehemu ya mtambo wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, pamoja na Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA), Mhandisi John Kapinga.
   Mtambo wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, Songea Mjini, mkoani Ruvuma
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (SOUWASA), Mhandisi Patrick Kibasa katika eneo la Misufini.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishuka baada ya kukagua tanki la mradi wa Mtendewawa, wilayani Songea Mjini, mkoa wa Ruvuma.

  0 0


   UNESCO is planning to carry out a five-day training for 26 practitioners from 24 community radios from both Tanzania Mainland and Zanzibar to promote self-monitoring and evaluation of activities and establish effectiveness of reporting and programming on issues of local concern as part of its implementation of Swedish International Development Agency/Swiss Development Corporation (SIDA/SDC) funded project. 

   The training, which will be attended by participants from community radios, scattered in 21 regions of the United Republic of Tanzania, aims to strengthen capacities of community radio practitioners for effective self-monitoring and evaluation of programmes on issues of local concern, understanding and awareness of SIDA/SDC project results framework and Sustainable Development Goals. Monitoring and Evaluation are key components of the UNESCO’s projects. 

  On an on-going basis, UNESCO closely monitors and evaluates the progress of beneficiaries, which not only allows assessing of the impact of capacity-building exercises but also allows to adapt interventions and support to each station’s particular need.Trainees will be empowered with the necessary skills and knowledge on monitoring the quantity and quality of radio programmes on issues of local concern and self-monitoring skills using SIDA/SDC project monitoring tools to enhance their reporting capacity of project results. 

  The involvement of beneficiaries in monitoring and evaluation will allow local radio practitioners to use the gained knowledge and skills to improve programming performance especially in ensuring there is an increased number of programmes reflecting local development issues of concern and gender balance in voices interviewed. 

   In addition, the training will also enable participants to increase SDG focus reporting and mainstreaming, therefore increase community radios contribution to SDGs, and consequently enhance their skills and knowledge on reporting on those.The training, expected to take place in Iringa from 27 November to 01 December 2017, will be hosted by Nuru FM radio station located in Iringa Municipality in the United Republic of Tanzania.

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumanne, Novemba 28, 2017)  amefungua kongamano la Kitaifa la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Juliasi Nyerere jijini Dar es Salaam.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawavumilia watu wote wanaotumia vibaya fedha za umma ambazo zinapaswa kuleta maendeleo kwa wananchi, zikiwemo na za Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi

  Amesema mfuko huo unalenga kufanikisha ukusanyaji wa fedha za kutosha amabazo ni muhimu kwa Taifa wakati huu tunapoazimia kumaliza ukimwi ifikapo mwaka 2030..

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo leo (Jumanne, Novemba 28, 2017) wakati akifungua kongamano la Kitaifa la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lililofanyika jijini Dar es Salaam.

  Nitoe wito kwa Bodi ya Mfuko huu na watendaji wake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu fedha hizi ili ziweze kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko huu. “

  Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kutenga fedha za mfuko huo na kuhamasisha wananchi, wadau na sekta binafsi kuchangia mfuko huo muhimu.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kujenga nchi ya viwanda ili waweze kufikia uchumi wa kati, jambo ambalo haliwezi kufikiwa iwapo wananchi wake watakuwa hawana afya bora.

  “Hatutaweza kufikia malengo haya kama Taifa iwapo watu wetu hawatakuwa na afya bora kwani nguvu kazi kwa ajili ya Tanzania ya Viwanda itatokana na wananchi wenye nguvu na afya bora.”

  “ Hivyo kama Serikali tutahakikisha tunaendelea kutoa huduma bora za afya ili wananchi wetu waweze kuwa na afya bora. Tutaendelea kuwakinga wananchi wetu hususan ni vijana ili Taifa letu liwe na nguvu kazi ya kutosha hasa wakati huu tunapoanza mageuzi makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.”

  Pia Waziri Mkuu amesema kwamba kwa sasa Watanzania wengi wana uelewa mkubwa wa ukimwi lakini changamoto iliyopo ni kubadili tabia na kuachana na tabia hatarishi zinazosababisha kupata maambukizo mapya.

  Amesema jambo hilo ni hatari kubwa kwa nchi yetu kwa sababu bado wananchi wengi wanaendekeza tabia ya kuwa na wapenzi wengi tena kwa wakati mmoja na hakuna uaminifu katika ndoa.

  Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu “changia mfuko wa udhamini wa udhibiti ukimwi, okoa maisha”.

  Kongamano hilo lilihudhuliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Walemavu Bibi Stella Ikupa Alex, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile, Makamishna wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS).
  Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt Leonard maboko, Mwenyekiti wa Baraza la Wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA), wawakilishi wa wadau wa maendeleo na wadau  wa ukimwi nchini.


  0 0


  Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limetoa warsha kwa Waviu Washauri kutoka mkoa wa Mwanza ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).

  Warsha hiyo ya siku tatu iliyoanza siku ya Jumanne Novemba 28,2017 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza imekutanisha WAVIU washauri kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba,Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana.

  Waviu washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha Waviu kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.

  Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo,Mgeni rasmi ambaye ni Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza Bi Esperance Makuza,(aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza, alisema Waviu Washauri wanayo nafasi kubwa ya kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya tiba na matunzo.

  “Nyinyi ni viungo muhimu sana katika kuwaunganisha wateja na vituo vya kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU,hivyo mafunzo haya yatawafanya mpate ujuzi na uzoefu mzuri katika kuwahudumia wateja”,alieleza. Naye Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona alisema shirika hilo linafanya kazi zaidi kwenye vituo vya huduma na limekuwa likijuhusisha zaidi na watoto.

  Alisema shirika hilo sasa linatekeleza majukumu yake katika mikoa sita nchini ambayo ni Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Geita,Tanga na Mara. Mafunzo hayo yameandaliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC).
  Mgeni rasmi, Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza, Bi. Esperance Makuza,aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza akifungua warsha ya siku tatu ya watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza Jumanne Novemba 28,2017.

  Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akielezea historia ya shirika la AGPAHI na shughuli zinazofanywa na shirika hilo nchini Tanzania.

  Bi. Cecilia Yona alisema shirika hilo limekuwa likishirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi lakini pia kuhakikisha kuwa huduma za afya zinatolewa kama inavyotakiwa.

  Mwezeshaji katika warsha hiyo Gladness Olotu ambaye ni muuguzi msaafu aliyebobea katika fani ya Ushauri nasaha akitoa mada kuhusu namna ya kutoa ushauri nasaha.

  Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa.

  Mwezeshaji Gladness Olotu akiendelea kutoa mada ukumbini.

  Washiriki wa warsha hiyo wakiigiza namna ya kutoa ushauri nasaha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
  Mshiriki wa warsha hiyo Herman Ngika kutoka wilaya ya Magu, akichangia hoja ukumbini.

  Washiriki wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa semina hiyo.

  Mratibu wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA),kanda ya Mwanza,Bi. Veronica Joseph akitoa mada kuhusu hali ya maambukizi ya VVU nchini Tanzania na haki za watu wanaoishi na VVU.
  Bi. Cecilia Yona akitoa mada ukumbini.
  Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii wilaya ya Magu, Bi Ngehu Bussu akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
  Washiriki wakiwa ukumbini.

  Mwezeshaji Bi. Sherida Madanka akitoa mada wakati wa warsha hiyo.

  Washiriki wa warsha hiyo wakicheza mchezo wa igizo namna ya kuhudumia wateja katika vituo vya kutolea huduma za afya. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega (katikati) akikata  utepe kushiria  uzinduzi wa mkakati wa taifa wa kondomu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 27, 2017 kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1,2017. kulia kwake ni, Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko.
  (PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega (katikati) akionesha  mkakati wa taifa wa kondomu mara baada ya kuzindua kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba 1,2017. 
    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua mkakati wa taifa kondomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba 1,2017.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko akieleza jinsi maambukizi ya VVU yalivyo kwa sasa.ambapo amesema takribani watu elfu 55 kwa mwaka wanamaambukizi mapya na kundi kubwa likiwa ni vijana.  kati ya hao asilimia 40 ya vijana wanamaambukizi mapya wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.
   Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
   Mkurugenzi wa wa Habari na Uraghibishi Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania (TACAIDS),    Jumanne Isango akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega huhusiana na maswala ya Ukimwi alipotembelea banda hilo.
   Naibu Waziri, Abdalla Ulega akipata maelezo namna ya kuvaa kondomu ya kiume na muelimishaji kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kutoka T- Marc Tza Benjamin Salema alipotembelea mabanda yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi leo Jijini Dar es Salaam.
   Seemu ya wananchi wakishuhudia uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kandomu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega mara baada ya kusaini kitabu cha wageni.
    Naibu Waziri, Abdalla Ulega akisalimiana na Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira mara baada kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam wakati wa  kuzindua mkakati wa kitaifa wa kandomu.
   Naibu Waziri, Abdalla Ulega akisalimiana  na Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko.

  Naibu Waziri, Abdalla Ulega akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Elizabeth Kaganda.

older | 1 | .... | 1444 | 1445 | (Page 1446) | 1447 | 1448 | .... | 1898 | newer