Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

VIJANA WASOMI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KULILETEA TAIFA MAENDELEO

$
0
0
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Amina Sanga akitoa mada kwenye kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam jana lenye lengo wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.
Vijana wasomi wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakiwa kwenye kongamano hilo.
Muonekano wa ukumbi katika kongamano hilo.
Meza kuu katika kongamano hilo. Kutoka kulia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Philip Sanga, Mgeni rasmi wa Kongamano hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila , Mchungaji John Kanafunzi na Mratibu wa kongamano hilo, Ephraim Mwambapa. 
Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu.
Burudani ikiendelea.
Maombi yakifanyika.
Waratibu wa kongamano hilo wakijitambulisha. Kutoka kushoto ni Sarafina Kabwe, Irene Sadock, Michael Mhagama na Yona Kilindu.
Katibu Mkuu wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli, akitoa mada.
Mratibu wa Kongamano hilo, Ephraim Mwambapa akitoa mada katika kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Maombi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Philip Sanga akihutubia kwenye kongamano hilo.
Mgeni rasmi wa kongamano hilo,Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na waratibu wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja


Na Dotto Mwaibale

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila amewataka Vijana wasomi na wanataalumu nchini kumsaidia Rais Dk.John Magufuli kuliletea Taifa maendeleo.

Ndabila ametoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana wakati akiwahutubia wasomi wanataaluma katika kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark lenye lengo kwa wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.

"Ninyi wasomi mmesomeshwa kwa ajili ya kuwatumia wananchi na taifa msaidieni Rais wetu John Magufuli kuliletea taifa la Tanzania na kanisa maendeleo kwani hakuna mtu mwingine tunaye mtegemea zaidi yenu" alisema Askofu Ndabila.

Askofu Ndabila aliwataka wasomi hao waende kwa wananchi wakawanoe na kuweza kuwiva kisawasawa ili waendenane na kasi ya maendeleo anayoihitaji Rais Magufuli.

Alisema wasomi ndio kundi pekee linaloweza kuitoa nchi katika hatua moja na kuipeleka katika hatua nyingine ya mbali kimaendeleo na kuwa mambo yao makubwa watakayo yafanya yataweza kuwabadilisha wananchi na nchi ikasonga mbele.

"Wananchi hawahitaji kusikia umahiri wenu wa kuongea kiingereza bali wanataka kuona ni jinsi gani mtafanya kwa vitendo kuwasaidia ili kulipeleka taifa mbele kimaenndeleo" alisema Ndabila.

Askofu Ndabila aliongeza kuwa hivi karibuni hapa nchini ilifika meli kubwa ya kitabibu ambayo ilikuwa na madakatari ambapo walikuwa wakitoa matibabu kwa wagonjwa kazi ambayo hata madaktari wasomi wa hapa nchini wakijipanga wanaweza kuifanya kwa kushirikiana na wadau wengine.

Mtoa mada katika kongamano hilo, Amina Sanga mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema vijana wanapaswa kuwa wabunifu badala ya kusubiri kuajiriwa.Aliwataka vijana kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa kujibizana mambo ambayo hayana tija kwa wao na taifa kwa ujuma badala yake waitumie kutafuta fursa za maendeleo.

"Siku hizi vile vijiwe vya kupiga domo mitaani havipo tena vimehamia kwenye makundi ya mitandaoni huko utakuta vijana tena wasomi wakishindani kujibizana vitu ambavyo havina manufaa kwao na taifa" alisema Sanga.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Philip Sanga alisema mabadiliko ya maendeleo yanaanzia kwa mtu mmoja, jamii na hadi taifa na ili kupata mabadiliko hayo yanawategemea wasomi na si mtu mwingine.

Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

Mwambapa alisema lengo la kongamano hilo ni kuona jinsi gani wasomi na wanataaluma wataweza kutumia taaluma na usomi wao kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kufanyiwa kazi wakati jamii inachangamoto nyingi.Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizuri kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA MELI YA HOSPITALI YA CHINA, AAGANA NA KUSHUKURU WANAMAJI NA MADATARI WALIOKUJA NAYO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji na wanaanga wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali na Kiongozi Mkuu wa Meli ya Hospitali ya China Kamanda Guan Bailin   alipoitembele aleo Jumapili Novemba 26, 2017  kuwashukuru na kuwaaga wanamaji na madaktari waliokuja nayo baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali na Kiongozi Mkuu wa Meli ya Hospitali ya China Kamanda Guan Bailin   alipoitembele aleo Jumapili Novemba 26, 2017  kuwashukuru na kuwaaga wanamaji na madaktari waliokuja nayo baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.

Kilele cha Tigo Fiesta 2017 kilivyohitimishwa jijini Dar Es Salaam

$
0
0

Msanii Madee kushoto akiwa na Janjaroo na TundaMan kwa pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia jana.


Msanii Q chief na Jux
Qchila akionesha ukongwe wake jukwaani

Msanii Ritchie Mavoko
Msanii Chege akikamua jukwaani na skwadi lake.


Msanii Ben Pol
Msanii Vanessa Mdee
Wasanii Kassim Mganga na Jux wakishirikiana kuimba pamoja kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam juzi.
Msanii Alli Kiba
Msanii Afande Sele akitumbuiza kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta 2017,katika viwanja vya Lida Club,Kinondoni jijini Dar.
Msanii Ommy Dimpozi akiwa kwenye jukwa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana
Msanii Maua Sama

TBL YAJITOSA KATIKA KAMPENI ZA KUPINGA UKATILI WA JINSIA

$
0
0
 Waziri wa Madini, Mh. Angela Kairuki akibadilishana na mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa WiLDAF,Anna Kulaya wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwa na bango lenye ujumbe wa No Excuse wakati wa maandamano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa kampeni ya No Excuse.

 Kampuni ya Tanzania Breweries Limited na kampuni zake tatu (TBL Group) chini ya kampuni mama ya AB INBEV mwaka huu imeungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hasa watoto wa kike.

 Maadhimisho haya ambayo yalizinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Waziri wa Madini,Mh,Angela Kairuki, huandaliwa kila mwaka na Shirika lisilo la kiserikali la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika- (Women in Law and Development in Africa -WiLDAF) kwa kushirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia nchini (MKUKI),wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi. Kauli mbiu ya maadhimisho haya mwaka huu ni ‘Funguka!ukatili dhidi ya wanawake na watoto haumuachi mtu salama.Chukua hatua ‘ ambayo inalenga kuhimiza kuelimisha jamii ya watanzania kubadilika na kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikitokea kwenye jamii. 

 Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter, amesema katika mahojiano maalumu kuwa TBL itatumia njia mbalimbali kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ikiwemo jumbe kupitia redio,magazeti na mitandao ya kijamii. Vile vile wafanyakazi wa kampuni ya TBL wameungana na jamii katika kushiriki katika maandamano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki .

 “TBL imeamua kutumia maadhimisho hayo kupeleka ujumbe kwa jamii kuacha kujihusisha na matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia kupitia kampeni inayojulikana kama “Acha Sababu,badilika” -(#NoExcuse)”Alisema Walter. 

Alisema TBL imeshiriki kampeni hii ya kuhamasisha mabadiliko dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sababu, , TBL ni kampuni inayoongoza nchini hivyo basi kati ya majukumu lake katika jamii moja yapo ni swala zima la unywaji pombe kiistarabu na pia kwamba pombe isewe na isitumike kama sababu ya ukatili wa kijinsia,TBL ina sera ya uhamasishaji utumiaji wa vinywaji vyenye ulevi kistaarabu kwenye jamii ili kuepusha madhara mbalimbali yatokanayo na matumizi yenye vinywaji vyenye kilevi kupita kiasi .

 Walter aliongeza kusema kuwa kampeni hii ya -#NoExcuse itaenda sambamba na kutoa jumbe mbalimbali za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii sambamba na matukio mengine yanayotokea na kuhusisha na ulevi kama vile kufanya uzembe wakati wa uendeshaji wa vyombo vya moto na kusababisha ajali.

 “Jumbe za kampeni hii yetu ya #NoExcuse zitahamasisha jamii kubadilika na kuacha vitendo mbalimbali vinavyoleta athari kwenye jamii kama vile vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake,vitendo vya ukatili dhidi ya wanaume,vitendo vya kupigana,vitendo vya ubakaji,utumiaji wa lugha za matusi zenye kudhalilisha watu wengine,uasherati n.k”.Alisema. 

TBL inaamini kuwa ukatili wa kijinsia unaweza kutokomezwa nchini endapo jamii nzima itashirikiana na kukemea vitendo hivyo kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha vyombo vya maamuzi vinavalia njuga suala hili na itaendelea kuunga mkono kampeni hizi siku zote. Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa WiLDAF,Anna Kulaya kwa niaba ya asasi za kiraia zinazoshriki katika kampeni hii aliiomba serikali kutunga sheria za ukatili wa majumbani (Domestic Violence Act),Kuanzisha mahakama za familia ili kuharakisha kesi na hivyo kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati,kuharakisha mapitio ya sheria kandamizi zote zinazowabagua wanawake na watoto na kuboresha miundo mbinu rafiki hasa kuwa na maeneo ya kuhifadhi wahanga wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia.

RAIS DKT MAGUFULI AMEFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI JIJINI DAR ES SALAAM NA KUBAINI MAGARI ZAIDI YA 50 YAKIWA YAMETELEKEZWA KUTOKANA NA MMILIKI WAKE KUTOFAHAMIKA

PICHA ZA MATUKIO KATIKA KAMBI YA MATIBABU NA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO KWENYE TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA KUSHIRIKIANA NA SAVE CHILD’S HEART-SACH YA NCHINI ISRAEL

$
0
0
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel Katharina Schmitt akiangali jinsi moyo wa mtoto unavyofanya kazi (Echocardiogram) kwenye kambi ya matibabu na upimaji wa moyo kwa watoto inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Afisa Muuguzi wa JKCI Pal Bhadreshwara na kushoto ni mama wa mtoto.
Mama Judy Shore kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel akielezea jinsi Taasisi hiyo inavyotoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto na mafunzo kwa wafanyakazi wa kada ya afya hapa nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia kambi ya matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization) inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo hadi sasa jumla ya watoto 20 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na hali zao zinaendelea vizuri.Kulia ni Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kutoka JKCI Peter Kisenge.
Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uhusiano wa Taasisi hiyo na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart- SACH) ya nchini Israel ambapo hadi sasa jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji wa moyo bure nchini Israel. Kulia ni Simon Fisher na kushoto ni Mama Judy Shore wote kutoka SACH.
Watoto wakicheza wakati wakisubiri kwenda kufanyiwa kipimo kinachoangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram) katika kambi ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel. Jumla ya watoto 100 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi kati ya hao 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu na 40 watatibiwa hapa nchini.


Picha na JKCI

Naibu Waziri Mhe Anthony Mavunde aongoza mbio za AIDS TRUST FUND MARATHON Jijini Dar

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde (mwenye miwani)  akiongoza matembezi ya  kilometa tano wakati wa mbio za Aids Trust Fund Marathon' za Kilometa 5, 9 na 21  zilizofanyika katika viwanja vya  viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam  Novemba 25, 2017 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, (mwenye kofia nyeupe), Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa OysterbayZefrin Lubuva.
 Matembezi ya kilometa tano yakiendelea....
 Mafoto akiwa kazini.
Matembezi yakiendelea.....
 Mshiriki wa mbio za Kilometa 21,  kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Carlson Konga .
 Mbio za kilometa 21 zikiendelea
 Mama na mwanae wakishiriki mbio za kilometa tano...
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde (mwenye miwani)  akishiriki mazoezi ya viungo baada ya kumalizika mbio hizo (wakwanza kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko.
 Mwalimu wa mazoezi, Bw. Yassin Lupola akiongoza mazoezi.
Wananchi wakiendelea na mazoezi ya viungo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde (mwenye miwani)  akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na viongozi wengine.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Elizabeth Kaganda (wakwanza kulia) akishiriki mazoezi ya viungo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akizungumza mara baada ya kumalizika mbio hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko akizungumza.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira akizungumza.
Seemu ya wananchi walioshiki mbio hizo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimvisha medali   mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 21, Mwasibu kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Carlson Konga .
 Mwenyekiti wa Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, Godfrey Simbeye akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mbio za kilomita 21.
Washiriki wakijisajili wakati wa mbio za Aids Trust Fund Marathon' za Kilometa 5, 9 na 21  zilizofanyika katika viwanja vya  viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam  Novemba 25, 2017 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-MTAZAMO NEWS)

SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU

$
0
0

PIX1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa kupewa Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshinda (kushoto) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshinda (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa mara baada ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wakifutilia hafla ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale mapema wikiendi hii. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akionyesha Tuzo ya Rais wa JICA katika hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshinda, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Toshio Nagase.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake Bi. Beatrice Kosongwa wakati wa hafla ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshinda, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Toshio Nagase.Picha na: Frank Shija – MAELEZO


Na Ismail Ngayonga- MAELEZO


SERIKALI ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la nchi hiyo (JICA) imesema itaendelea kuisadia miradi mikubwa ya maendeleo nchini ikiwemo barabara ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Hayo yamesemwa mwishoni wa wiki Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati wa utoaji tuzo ya heshima ya Rais wa JICA kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale.

Balozi Yoshida alisema tangu mwaka 1980, JICA imekuwa mshirika wa karibu wa maendeleo na Serikali ya Tanzania ikiwemo kuunga mkono juhudi za kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi kupitia ufadhili wa miradi ya kipaumbele kwa ikiwemo barabara.

Aliongeza kuwa utoaji wa Tuzo ya Rais wa JICA kwa Mhandisi Mfugale imedhirisha imani ya Serikali ya Japan kwa Tanzania katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa JICA, na kuahidi kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi wa Mataifa hayo.

“Misaada ya JICA nchini unajumuisha misaada bila masharti, misaada ya kiufundi, kufadhili miradi kwenye maeneo ya vipaumbele kwa serikali hususan katika sekta za kilimo, miundombinu ya barabara, maji, nishati, utawala na afya” alisema Balozi Yoshida.

Akizungumzia kuhusu tuzo ya Rais wa JICA kwa Mhandisi Mfugale, Balozi Yoshida alisema tuzo hiyo hutolewa kama alama ya utambuzi wa heshima kwa wataalamu, wataalamu washauri na wafanyakazi wa kujitolea walifanikisha maendeleo katika nyanja za raslimali watu na maendeleo ya miundombinu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Balozi Yoshida alisema tuzo hiyo imetolewa kwa Mhandisi Mfugale kutokana na mchango wake katika maendeleo ya miundombinu inayounganisha mikoa mbalimbali nchini pamoja na nchi jirani na kueneza ujuzi wake kwa wasaidizi waliomzunguka.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema tuzo ya Mhandisi Mfugale imetoa somo kwa Wahandisi vijana wanaopaswa kuzingatia miiko inayoongoza taaluma ya uhandisi nchini.

Aidha Prof. Mbarawa aliishukuru JICA kwa utekelezaji wa miradi ya barabara nchini hususani katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia uimarishaji wa miundombinu imara ya barabara.

“Uadilifu na uaminifu ni jambo la msingi sana katika taaluma ya uhandisi, ni misingi mikuu iliyoonyeshwa katika utendaji kazi Mhandisi Mfugale hadi anatunukiwa tuzo hii, niwahimize wahandisi vijana muige mfano huu” alisema Waziri Mbarawa.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale alisema tuzo aliyopewa ni zawadi kwa Serikali hususani wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambao amekuwa akifanya nao kazi kwa katika kutekeleza majukumu yake.

CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA KUANZA KUTOA MAFUNZO MAALUM KWA WATOA HUDUMA ZA UTALII NCHINI KUANZIA KESHO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka, Brightone Mbilinyi kuhusu mafunzo ya silaha yanavyotolewa chuoni hapo katika mahafali ya 53 ya chuo hicho yaliyofanyika jana katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya asilimia 60 ya mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo. Wengine Pichani ni Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada (wa pili kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho (wa nne kulia).

 Na Hamza Temba-WMU
..................................................

Katika kutimiza azma ya Serikali kuboresha huduma za ukarimu kwenye sekta ya utalii nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imekichagua Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro kwa ajili kutoa mafunzo maalum kwa waongoza watalii nchini. 

Mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kesho (Jumatatu) chuoni hapo yatakuwa kwenye mfumo wa kujiendeleza na yamelenga kuwawezesha watoa huduma katika sekta hiyo kupata sifa za kusajiliwa na kupewa leseni ya kuendelea kutoa huduma hiyo kwa mujibu ya sheria ya utalii Na. 11 ya mwaka 2008 kifungu cha 48.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga katika mahafali ya 53 ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa chuo hicho katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii.

"Katika kutambua utaalamu na uzoefu wa chuo chenu, Wizara yangu imeichagua Mweka kutoa mafunzo yatakayowawezesha waongoza watalii nchini kupata sifa ya kusajiliwa (cheti) na kupewa leseni," alisema Naibu Waziri Hasunga.

"Nimefurahi kusikia kuwa  mmeshajipanga tayari kuanza kutoa mafunzo hayo baada ya kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo na kuainisha mapungufu kwenye taaluma, ujuzi na mitazamo pamoja na kuandaa mtaala wa mafunzo hayo.

"Nitoe wito kwa waongoza watalii  nchini wajisaji ili wapate mafunzo haya muhimu kwakua katika miaka michache ijayo hawataruhusiwa kutoa huduma hiyo bila kutimiza masharti haya ya kisheria,” alisema Hasunga.

Alisema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa watalii wengi wanaokuja nchini hupata taarifa kutoka kwa wenzao waliotembelea Tanzania ambao muda wao mwingi wanakuwa na waongoza watalii kwenye maeneo ya vivutio.

"Hivyo ni muhimu wapewe mafunzo  maalum waweze kutoa huduma bora zaidi zitakazowafanya watalii wafurahie ukarimu wao waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuutangaza utalii wetu watakaporudi nchini kwao" alisema  Hasunga. 

Alisema licha ya Sekta ya utalii nchini kuchangia asilimia 17 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha za kigeni (watalii milioni 1.28 na bilioni 2 mwaka 2016), mchango wake unaweza kukua zaidi kupitia mikakati mbalimbali inayowekwa  na wizara yake ikiwemo hiyo ya mafunzo ambayo imelenga kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni mbili mwaka 2020 na watalii milioni 8 mwaka 2025 pamoja na mapato ya dola za kimarekani bilioni 20 mwaka 2025.

Akizungumzia kuhusu mafunzo ya jeshi usu chuoni hapo, Naibu Waziri Hasunga aliuagiza uongozi wa chuo hicho kuendesha mafunzo hayo muda wote wa masomo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hutolewa kwa wiki mbili katika kila 'semister'.

"Mafunzo haya yasiishie tu kwa muda wa wiki mbili, ni matarajio yangu kuona yanaendeshwa katika kipindi chote cha mafunzo ikiwemo wanafunzi kuvaa sare za heshima za jeshi usu, kuwa na nidhamu ya kijeshi na muhimu zaidi kuonyesha utayari na uwezo wa kukabiliana na wahalifu ikiwemo majangili," alisema Hasunga.

Aidha, alizitaka taasisi zilizopo chini ya Wizara yake kuajiri wananfunzi wanaomaliza chuoni hapo ikiwa ni pamoja na kutumia fursa ya chuo hicho mahiri kuwaongezea ujuzi wafanyakazi waliopo makazini.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho alimueleza Naibu Waziri Hasunga kuwa Chuo chake kimeshafanya maandalizi yote ya kuanza kutoa mafunzo kwa waongoza watalii nchini kama ilivyoagizwa na wizara yake ambapo tathmini ya mahitaji ya mafunzo hayo imeshafanywa kwa kuainishwa mapungu katika taaluma, ujuzi na mitazamo. 

"Tumeshaandaa pia mitaala ya mafunzo ambayo imezingatia kuondoa mapungufu tuliyoyabaini, na tunatarajia kuanza mafunzo yetu ya kwanza kwa wapagazi 100 kwa muda wiki tatu kuanzia jumatatu ijayo (leo)," alisema Prof. Kideghesho.

Alisema ili kufanikisha mafunzo hayo chuo chake kimepokea msaada wa Shilingi milioni 110 kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wapagazi wanaotoa huduma katika mlima Kilimanjaro, fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya mafunzo na tafiti mbalimbali.

Mahafali hayo ya 53 yalihudhuriwa pia na Balozi wa Nigeria nchini,  Balozi Sahabi Dada, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo hicho, Prof. Faustin Bee, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mkuu wa Wilaya ya Same, Harun Mbogo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Nebo Mwina, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo na baadhi ya wawakilishi wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda.

Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilianzishwa mwaka 1963 baada ya azimio la Arusha mwaka 1961 ambalo lilitaka uwepo wa watu waliopewa mafunzo kwa ajili ya kulinda na kusimamia urithi wa rasilimali za Afrika. 

Chuo hicho ambacho huendesha mafunzo yake kwa vitendo kwa zaidi ya asilimia 60 kimepata ongezeko la wanafunzi kutoka 25 mwaka 1963/1964 hadi zaidi ya wanafunzi 550 mwaka 2016/2017 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi na Cameroon.

Aidha, katika kipindi cha miaka 54 iliyopita chuo hicho kimeweza kufundisha zaidi ya mameneja wa wanyamapori 8,000 kutoka nchi zaidi ya 50 duniani.

Chuo hicho pia kimepewa tuzo na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama Kituo cha Ubora wa Taaluma ya Usimamizi wa Wanyamapori (Centre of Excellence).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Leonard Mgamba kuhusu mafunzo ya taaluma ya wanyamapori yanavyofanywa kwa vitendo chuoni hapo. Wengine pichani ni Balozi wa Nigeria nchini, Sahabi Dada (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Harun Mbogo (kushoto) na Mtenaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiwa ndani ya handaki linalotumika kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa kozi mbalimbali chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akikagua gwaride la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Astashahada na Stashada katika taaluma za usimamizi wa wanyamapori na utalii katika mahafali ya 53 yaliyofanyika chuoni hapo jana katika Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya asilimia 60 ya mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo na wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda ambao walishiriki kwenye mahafali ya 53 ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Faustin Bee (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Harun Mbogo (kushoto) wakiteta jambo wakati wa mahafali ya 53 ya chuo hichao ambayo yalifanyika jana mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Jafari Kideghesho (kulia) akiwasilisha taarifa fupi kuhusu chuo hicho kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) wakati wa mahafali ya 53 ya chuo hicho ambayo yamefanyika jana mkoani Kiliamanjaro. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chuo hicho, Prof. Faustin Bee (wa pili kushoto) na Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka, Prof. Faustin Bee (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Harun Mgogo wakati wa mahafali ya 53 ya chuo hicho ambayo yamefanyika jana mkoani Kilimanjaro. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada.
Mkuu wa Chuo chaUsimamizi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Jafari Kideghesho (kulia) akiteta jambo na Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Ebenezer Mollel kuhusu mafunzo ya taaluma ya wanyamapori yanavyofanywa kwa vitendo chuoni hapo. Wengine pichani ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba.
Sehemu ya taswira ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipanda mti wa kumbukumbu chuoni hao.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi ya Wanyamapori Mweka, pembeni yao ni mifupa ya miguu ya tembo katika chumba maalum cha mafunzo ya wanyamapori.
Sehemu ya wananfunzi 224 waliopewa vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka wakiwasili katika viwanja kwa ajili ya mahafali ya 53 yachuo hicho yaliyofanyika jana katika viwanja vya chuo hicho wilayani Moshi Mkoa wa Kiliamanjaro. Vyeti hivyo vilitpolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
Gwaride la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka wakitoa heshma mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (hayuko pichani)
Naibu Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akimtunuku cheti Mhitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori, katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka, Valentina Fiasco ambaye ni raia wa Italia katika mahafali ya 53 yaliyofanyika jana chuoni hapo katika wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho. Jumla ya wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti.
Naibu Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akimtunuku cheti mmoja ya wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori, katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka wakati wa mahafali ya 53 yaliyofanyika jana chuoni hapo katika Wilaya ya Moshi Mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho. Jumla ya wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti. 
 Naibu Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akitoa tamko la kuwatunuku kozi mbalimbali wananfunzi 224 wa chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka katika mahafali ya 53 ya chuo hicho ambacho yamefanyika jana mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Prof. Faustin Bee (wa tatu kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (mwenye tai) na washiriki wengine katika mahafali hayo.

Kilele cha Tigo Fiesta 2017 chahitimishwa kwa burudani ya kukata na shoka jijini Dar Es Salaam

$
0
0

Msanii Madee kushoto akiwa na Janjaroo na TundaMan kwa pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia jana.


Ommy Dimpozi akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

 Ommy Dimpozi akiendelea kuburudisha katika  jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

Alikiba akiwa na kundi lake wakitumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta liliofanya hitimisho lake usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Vanessa Mdee akiwa na dansa wake wakitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika usiku wa jana  viwanja vya leaders.

Fid q akitoa burudani katika jukwaa la Tigo  fiesta jijini Dar es salaam katika kilele chake kilichofanyika katika viwanja vya Leaders.

Mashabiki wa muziki wakifurahia  burudani mbalimbali zilizotolewa katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.

Fid Q akiendelea kuburudisha katika Jukwaaa la Tigo Fiesta .


Mwanamziki Mkongwa wa BongoFleva Afande sele akiwa  katika jukwaaa la Tigo fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaaam.

Maua Sama akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders .

Benpol akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana 


Wasanii Kassim Mganga na Jux wakishirikiana kuimba pamoja kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam juzi.

Richie Mavoko akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha tigo fiesta usiku wa kuamkia jana.

Chege Chigunda akipagawisha maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliojitokeza katika viwanja vya Leaders katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 27,2017

BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akikabidhi moja ya kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania.

Baadhi wa watoto wanufaika na kadi za bima wakiwa na walezi wao wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu


Baadhi ya wafanyakazi wa Kitengo cha magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao ni mayatima
Baadhi ya wafanyakazi BancABC Tanzania wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao ni mayatima.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kitego cha wateja wakubwa na wadogo wa BancABC Joyce Malai wakati wa kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania.

Picha ya Pamoja
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu aikisisita jambo kwa Mkurugenzi wa Kitego cha wateja wakubwa na wadogo wa BancABC Joyce Malai wakati wa kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania. 
 
BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imeshirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kutoa huduma ya bima ya afya itakayofaidisha watoto 100 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia mradi mpya wa afya wa Muhimbili uliozinduliwa leo.

Akizindua mpango huo wa Afya wa Muhimbili Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliishukuru BancABC kwa kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili katika suala hilo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa watoto.

Alisema mradi huo wa Muhimbili kushirikiana na BancABC unaendea sambamba kabisa na malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma ya Afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani watoto ndio moja ya makundi ambayo huathirika sana wasipopatiwa huduma za Afya za uhakika.

“Natoa wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa na BancABC kwa ushirikiano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafungulia watoto wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha tasilimu pale mtoto anapougua,” alisema.

Alitoa wito pia kwa watoa huduma za kifedha nchini pamoja na mashirika mengine kuhakikisha yanaiga mfano huo wa BancABC kwani wizara yake iko tayarikushirikiana na taasisi ambazo ziko tayari kuimaisha huduma katika sekta ya afya hasa upande wa utoaji huduma.

Naye Mkuu wa Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati, Bi Joyce Malai alisema BancABC inatambua umuhimu wa kuwa kampuni inayowajibika katika masuala ya kijamii kwa kurudisha kwa jamii sehemu ya faida na hasa katika sekta muhimu sana ya afya, dhamira hii ya BancABC kusaidia kwenye kuwezesha Afya ya watoto ni yamsingi sana kwa kuwa pia inasaidia serikali kufikia malengo yake.

Alisema baada ya kufungua akaunti hizo, wazazi wa watoto wenye akaunti hizo watakuwa wanahimizwa wakewe hela mara kwa mara kwa ajili ya bima ya watoto wao ili wapate huduma kupitia akaunti hizo za Mwangaza Junio Kids Accountambayo haina tozo ya kila mwezi.

Bi Joyce Malai aliongeza kuwa huduma hiyo ya bima haitakuwa na masharti kuhusu umri. “Wazazi wanaweza kufungua akaunti kwa mtoto zaidi ya moja na kuweka fedha kiasi chochote wanachotaka kwani itasaidia kuhakikisha watoto wao wana bima,”. 

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa, Prof. Lawrence Museru, aliishukuru BancABC kwa ushirikiano huo na kusema hatua hii haitasaidia watoto kupata tu huduma za afya kwa kupitia bima, bali itawajengea pia utamaduni wa kuweka akiba katika benki kuanzia utotoni hadi wanapokuwa watu wazima ili wapange mambo yao vizuri .

“Kwa sasa akaunti hizi zitafunguliwa na wazazi wao ila watakuwa wakitambua umuhimu wa huduma hii na wataendelea nayo hadi ukubwani,"alisema na kutoa rai kwa wazazi watumie fursa hiyo vizuri.

NBC NA SANLAM WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) akisaini mkataba wa ushirikiano katika ya NBC na Kampuni ya Bima ya Sanlam, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka na kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman.  Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake ndani ya matawi ya NBC nchini kote Waliosisima kutoka kushoto ni, Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. 

 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), wakifurahi baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati), akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano katika ya benki hiyo na Kampuni ya Bima ya Sanlam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General, Manasseh Kawoloka na kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life, Khamis Suleiman. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam General, Manasseh Kawoloka (kushoto), akisaini mkataba wa ushirikiano katika ya NBC na Sanlam. Katikati ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi na kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman.  Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), wakifurahi baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote

 Ni furaha tu baada ya Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), kusaini  mkataba wa ushirikiano. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote.
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) akisaini mkataba wa ushirikiano katika ya benki hiyo na Kampuni ya Bima ya Sanlam, jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawokol na kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman.  Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake ndani ya matawi ya NBC nchini kote Waliosisima kutoka kushoto ni, Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. 
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), wakipiga picha baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano. Wa pili kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote.

TANGAZO MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU WA TANZANIA BARA

RC Wangabo Ameitaka Manispaa Ya Sumbawanga kuboresha Masoko

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Matola katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa samaki wa soko la Sabasaba katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la OTC Kizwite katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akinunua bidhaa alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.


………..

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitaka Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wanaboresha mazingira ya masoko yaliyopo kwenye Manispaa hiyo ili wananchi waweze kupata huduma kwenye maeneo hayo bila ya kulazimika kufika katikati ya mji kupata huduma hiyo.

Amesema kuwa wakuu wa idara katika Manispaa hawanabudi kuhakikisha wanashuka kuwafuata wananchi na wafanyabiashara wa masoko hayo na kusikiliza kero zao na kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya masoko hayo ikiwemo majengo, usafi wa mazingira na vyoo.

“Nimeambiwa changamoto nyingi sana na wafanyabiashara wa soko la sabasaba na wamekuwa wakifanya biashara zao kwenye mazingira machafu hali ambayo haizoeleki na haifai kuendelea kuwepo, hivyo manispaa lazima iweke kambi kusikiliza kero zao na kuzitatua, kwani lipo kwenye uwezo wao,” Mh. Wangabo alisisitiza.

Aidha, ameitaka manispaa hiyo kuhakikisha usalama wa biashara za wafanyabiashara hao unaimarika ili kupunguza malalamiko yao na kuongeza kuwa atahakikisha malalamiko hayo yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Akielezea changamoto za soko la sabasaba, Mwenyekiti wa soko hilo Feston Mwilema amesema kuwa changamoto kubwa ya soko hilo ni usalama na kuwa hakuna kituo cha polisi na wala hawana mgambo wa kulinda soko hilo, na kuomba kusafisihiwa mazingira kutokana na uchache wa vifaa vya kuzolea uchafu unaozalishwa katika soko hilo.

“Tumelazimika kuchimba shimo la muda la kutupia uchafu unaozalishwa na wauza samaki kutoka na kutokuwepo kwa shimo la kisasa, na tuna kontena moja badala ya matatu ambalo huzidiwa na soko kukosa uzio ni jambo linalotoa mwanya kwa vibaka kuendelea na wizi,” Alisema Mwilema.

Mh. Wangabo alitembelea masoko nane yaliyopo kwenye manispaa ya Sumbawanga na kubaini kuwa masoko mengi hayatumiki kwa kukosa miundombinu bora na usimamizi na hatimae wananchi kuanzisha masoko yasiyorasmi na kuhatarisha usalama wa bidhaa zao na usalama wa vyakula kutokana na kuvidandaza chini na kuhatarisha usalama wa wanunuzi.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu na ajali za barabarani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya kifo kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 26.11.2017 majira ya saa 10:00 Asubuhi huko Maeneo ya Kadege, Kata ya Forest, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Gari yenye namba za usajili T.913 BEW aina ya Toyota Ipsum iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye MUGANIZI RAPHAEL [34] Mkazi wa Simike iligongana na gari yenye namba za usajili T.204 CSZ/T.670 BEZ aina ya Scania Lory ikiendeshwa na HOSEA S/O MWASHAMBWA [28] Mkazi wa Uyole na kusababisha kifo kwa dereva wa Gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum.

Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum hasa ukizingatia eneo hilo ni lenye mteremko mkali. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Dereva wa lori alikimbia mara baada ya ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea. Upelelezi unaendelea.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Hata hivyo Kumekuwa na matukio 02 ya mauaji kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 25.11.2017 majira ya saa 22:06 usiku huko katika Kijiji cha Ipwizi, Kata ya Mjele, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MINZA PAUL [25] Mkazi wa Ipwizi alifariki dunia baada ya kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aliyefahamika kwa jina SHILONDI MAKWENGE ambaye alitoroka baada ya tukio.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya mume wa marehemu kurudi nyumbani akiwa amelewa kwa usafiri wa Pikipiki na kumwambia mke wake amlipe pesa dereva bodaboda aliyemlita nyumbani lakini mke wake alimjibu kuwa hana fedha na ndipo SHILONDI MAKWENGE alianza kumpiga mke wake na kusababisha kifo chake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi kwa uchunguzi wa kitabibu. Jitihada za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.

Mnamo tarehe 26.11.2017 majira ya saa 15:00 Alasiri huko Mtaa wa Itumbi uliopo Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja mkazi wa Itumbi aliyetambulika kwa jina la FLORIAN KAGOMBE [46] aliuawa baada ya kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu butu na walinzi wa kampuni ya “Itumbi Reaching Plant” ambao ni 1. IMANI KAYUNI [36] Mlinzi – Panic Security Group na 2. KELVIN NGONYANI [32] Mlinzi – Panic Security Group.

Inadaiwa kuwa, kabla ya kifo chake marehemu alikutwa na walinzi hao eneo la Kampuni ya “Itumbi Reaching Plant” inayojishughulisha na uchenjuaji dhahabu majira ya saa 02.00 usiku na kutiliwa shaka kuwa ni mhalifu/mwizi na hivyo kuanza kumpiga na kumwachia akiwa tabani.

Watuhumiwa wote wawili wamekamatwa na uplelelezi unaendelea. Aidha mwili wa marehemu umehifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.


TAARIFA YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA YA IBIGHI, WILAYA YA RUNGWE.

Mnamo tarehe 26.11.2017 kumefanyika zoezi la uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya udiwani. Kwa hapa Mkoa wa Mbeya, zoezi hili limefanyika katika Kata ya Ibighi Wilaya ya Rungwe ambapo nafasi hiyo ilikuwa ikigombaniwa na wagombea watano.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi kata ya ibighi ndugu STEVEN STANFORD MWAKINGWE ambaye pia ni Afisa Mtendaji Kata ya Ibighi alisema, Jumla ya watu waliotarajia kupiga kura katika kata hiyo ni 4,737 jumla ya vituo vya kupigia kura vilikuwa 13. Idadi halisi ya watu waliopiga kura ni 2,691, kura halali 2,672 na kura zilizoharibika ni 19.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:- 
CCM: SUMA IKENDA FYANDOMO – Kura 1,205 
CHADEMA: SIMBA LUSUBILO EMANUEL – Kura 1,449 
CUF: GRACE NGALABA – Kura 12 
UDP: GEOFREY MWAKAJINGA – Kura 02 
DP: EMANUEL ANDONGOLILE MWAFILAMBO – Kura 0. 

Kutokana na matukio hayo, Msimamizi wa Uchaguzi ndugu STEVEN STANFORD MWAKINGWE alimtangaza rasmi SIMBA LUSUBILO EMANUEL kuwa mshindi na Diwani wa Kata ya Ibighi.
Katika zoezi hilo, hali ya ulinzi na usalama iliimarishwa na zoezi la uchaguzi lilifanyika kwa hali ya amani na utulivu.

WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio la ajali azitoe ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. 

Pia Kamanda MPINGA anatoa wito kwa madereva kuwa makini ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika. Aidha Kamanda MPINGA anaendelea kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za mtu/watu wanaowatilia mashaka katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na wahamiaji haramu kwa hatua zaidi za kisheria.


[MOHAMMED R. MPINGA – DCP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA KITUO CHA UTOTOLESHAJI VIFARANGA VYA SAMAKI WILAYA YA MKURANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akimsikiliza kwa makini mmiliki wa Jan's Aqua Centre Johnson Noni anayejishughulisha na ufugaji wa samaki aina ya sato katika kijiji cha Kisayanu kata ya Mbezi Wilaya ya Mkuranga, ikiwa ni katika ziara ya Naibu waziri.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega amefanya ziara katika vijiji vinne vya kata ya Mbezi na kufurahishwa na hatua kubwa waliyofikia kwenye ujenzi wa zahanati za kijiji sambamba na bwawa la Samaki lenye uwezo wa kutengeneza vifaranga milioni 2 kwa mwezi mmoja.

Akiwa katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega aliweza kufahamu namna utotoshaji wa mayau ya samaki unavyofanyika ikiwemo changamoto wanazokutana nazo wafugaji wa samaki hao.

Ulega amesema, mpaka sasa kuna maeneo makubwa matatu nchini yanayofanya utotoshaji wa vifaranga ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ni Mkuranga pekee ila kuna Kibirizi Kigoma, Naliendele Mtwara na Kigurunyembe Morogoro na amechukua changamoto ya kodi ya Viet kama suala la kwanza kabisa na atalipeleka bungeni.
Mmiliki wa eneo hilo linalopatikana katika katavya Kisayani lijulikanalo kama Jan'S Aqua Centre , Johnson Noni amesema za ufugaji huo wa samaki aina ya sati kuwa ni kubwa sana hasa katika upatikanaji wa chakula cha samaki kwa sababu ya kodi kuwa juu.

Noni amedai kuwa, samaki wanatumia sana Vyakula vya Protein ambapo ni dagaa, soya ila ukiangalia vyakula hvyo viko juu sana ingawa serikali wametoa kodi katika mbegu za soya ila virutubisho vinavyotengenezea chakula cha mifugo bado kipo juu.

Ameeleza kuwa uwezo wa bwawa lake linawezq kutoa vifaranga milioni mbili kwa mwezi kwa ajili ya kuviuza kwa watu wengine wanaotaka kufuga samaki na zaidi pia wana uwezo wa kuacha samaki wakue na kuwauza kwa wateja kwa ajili ya kitoweo.

Kwenye Ziara hiyo, Naibu Waziri alitembelea kijiji cha Ngalambe, Mwazenga na Miyekela na kujionea namba ujenzi wa Zahanati za vijiji hivyo zimefikia katika hatua gani ya ujenzi pamoja na kuwapatia fedha na mifuko ya saruji
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akikagua baadhi ya maeneo ya ufugaji wa samaki aina ya sato yanayomilikiwa na Johnsona Noni.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akikabidhi mifuko ya Saruji kwa wanakijiji wa Miyekela kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Ujenzi Abdalla Ulega akisalimiana na wakina mama wa kijiji cha Mwanzenga wakati wa ziara yake katika kata ya Mbezi wilaya ya Mkuranga.
Picha zote na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii.



WAANDISHI WA KIGOMA KIGOMA WAFUNDWA JINSI YA KURIPOTI KUHUSU WAKIMBIZI NA UMAKINI DHIDI YA CHANGAMOTO YA UWEPO WA SHERIA MPYA YA HABARI.

$
0
0


Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya siku mbili kuhusu kuripoti habari za wakimbizi na umakini dhidi ya changamoto ya uwepo wa sheria mpya ya habari mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa(UN)na kuratibiwa na MISATAN Tanzania.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka kushoto ni Mhariri mtendaji wa Guardian Jesse Kwayu (kushoto)James Marenga Wakili kutoka mahakama kuu.
Afisa uhusiano na mawasiliano,Ofisi ya mratibu mkazi mashirika ya umoja wa mataifa(UN)Didi Nafisa akitoa mada kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)juu mradi wa pamoja wa Kigoma unaofanywa na mashirika 16 ya umoja wa mataifa katika kambi za wakimbizi zilizopo Mkoani humo.
Baadhi washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa makini toka kwa mwezeshaji Jesse Kwayu(hayupo pichani). 
Kaimu Mkurugenzi MISATAN Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo

WANAUME WATAKIWA KUWA CHACHU YA MABADILIKO KATIKA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NCHINI

$
0
0
 Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia, Theodosia Mhulo kutoka WLAC Akifungua maadhimisho hayo katika ofisi za REDESO zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo alitoa wito kwa wana harakati na Wadau kwa ujumla kuanza kuwatumia Wanaume kama chachu ya mabadiliko katika vita ya ukatili wa Kijinsia nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya REDESO, Abeid Kasazi akizungumza kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi kufungua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani kote, yaliyofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo zilizopo kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri kutoka  REDESO, Brigitha  Sedekia akitoa somo juu ya ukatili wa kijinsia  kwa watu waliofika katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliokuwa wamekaa Meza kuu wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani wakishiriki kuimba kwa pamoja
 Kundi la Muziki la Wakimbizi linalojulikana kwa jina la Bana ba Zambe wakitoa Burudani wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani
 Sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani

WAZIRI MKUU AKABIDHI KOMBE KWA TIMU YA AFISI KUU ZANZIBAR

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Afisi Kuu Zanzibar.Bwana Vuai Jecha baada ya timu yake kuibuka mshindi kwakuifunga timu ya Kwahani mabao 3 kwa 1. katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Aman Zanzibar. Novemba 25/2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mwenye nguo nyeupe akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Afisi Kuu Zanzibar. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images