Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

HOW 4G INTERNET EXPAND IN TANZANIA

$
0
0
For years development has brought us better lives through easing the way we live and work. Little over 20 years ago, Tanzanians could not have imagined that travelling from one corner of Tanzania to another could take less than 24 hours, or sending money from one region to another could be a process of one minute, but this all has been made easy with technological inventions that have rapidly shifted our country to where we are today. Such inventions are so useful to a point they seem to be too god to be true, for example the introduction of Internet service.

Internet services have been available since 1995, according to Wikipedia’s internet history there was no international fiber connectivity available until 2009. Before then, connectivity to the rest of the world, including to neighboring countries, was obtained using satellite networks. The SEACOM and the Eastern Africa Submarine Cable System submarine fiber cable projects were implemented in July 2009 and July 2010, respectively, bringing higher speed Internet connectivity to Tanzania with lower costs.

In those years many people could not believe that internet of such speed could exist in this side of Africa, until Smile introduced Africa’s first 4G LTE mobile broadband services in Tanzania in May 2013, thereby revolutionizing the way Tanzanians and people in East Africa access the internet. From then Tanzanians experience the country’s fastest internet services with coverage in Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mwanza, Moshi, Mbeya and Morogoro.

As now Tanzania aims to migrate to the Second World economy, with the focus of being “an Industrial nation” it is vital that it runs with the rapid changes in today’s technological world, biggest of which being to turn to the best internet.

Many Telecom companies in Tanzania have identified themselves as companies that offer good internet technologies through their services, although most times the questions rise in their advertised speeds and value that brings a customer to the decision of who is the most reliable for users’ internet needs.

In the case of Reliability, companies have worked hard to market their internet services, through billboards, sales activities, media advertisements and in many other areas, but when it comes to speed it is somehow hard for the customer to determine the speed he/she is provided, unless it starts to slow down or stops working, which in most cases users get to be very frustrated.

If one goes through marketing ads and writings, one will notice that only Smile Communications is the company that has openly committed its speed lengths to its customer from the time a customer wants to purchase. This has made it easier for their customers to make the right decisions as to which bundles to purchase, depending on their speed need and usage, something which many customers have come to love and which continues to pull more people to the brand.

SPIKA JOB NDUGAI AONGOZA MAWAZIRI, WABUNGE NA VIONGOZI MBALI MBALI KATIKA MAZISHI YA ALIEKUWA MBUNGE WA SONGEA MJINI MAREHEMU MHE. LEONIDAS GAMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza Mawaziri, Wabunge pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.



Viongozi mbali mbali waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.



Wanafamilia waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Viongozi mbali mbali waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Wapambe wa Bunge wakibabe mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama kabla ya kuzikwa leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Mke wa marehemu, Ndg. Esther Gama akiweka shada ya maua katika kaburi la mume wake, aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama, tukio lililofanyika leo makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiweka shada ya maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama aliezikwa leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Christina Mndeme (kulia) baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha Ruvuma tayari kuelekea katika mazishi ya aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama yanayofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.



Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Songea, Mhe. Abdul Mshaweji (kulia) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songea mapema leo, tayari kuelekea katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama yanayofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Christina Mndeme



Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimfariji Ndg. Esther Gama mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama wakati wa mazishi yaliyofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

PICHA NA OFISI YA BUNGE

SERIKALI YAZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA KONDOMU

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega  akikata  utepe kushiria  uzinduzi wa mkakati wa kandomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba Mosi. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, serikali imezindua mkakati wa Taifa wa Kondomu na wiki ya maonyesho na Huduma ili kuhakikisha maambukizi dhidi ya ugonjwa huu yanapungua kwa kiasi kikubwa ama kumalizika kabisa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Adallah Ulega, amesema mkakati huu umetayarishwa kueleza vipaumbele vya kimkakati vinavyohitajika kupungiza maambukizi ya VVU, Magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa
 "Takwimu za matumizi ya kondomu kwa Tanzania ni asilimia 50, matumizi haya yako chini wakati kondomu zikitumiwa kwa usahihi na mara kwa mara zinauwezo wa kupunguza maambukizi ya VVU" amesema Ulega
 Amesema mkakati huo,  unakusudia kuongeza matumizi ya Kondomu kwa wanawake na wanaume kutoka 34% kwa wanawake na 40.5% kwa wanaume ya mwaka 2012 had I 55% kwa wote ifikapo mwaka 2018.  

Aidha amesema vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 watoe taarifa ya kutumia kondomu wakati wa ngono.
"kiwango kidogo cha matumizi ya kondomu kama njia ya kuzuia magonjwa ya ngono kinatishia kufikiwa kwa malengo ya muda mrefu ya nchi tuliyojiwekea hii ikiwa ni pamoja na malengo ya dunia ya sifuri Tatu ifikapo 2030 hasa ikizingatiwa kwamba kondomu zina uwezo wa kings kwa zaidi ya 80%.
Aidha amesema, pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali, Jamii bado inamchango mkubwa katika kupambana na magonjwa ya ngono na ukimwi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko akieleza jinsi maambukizi ya VVU yalivyo kwa sasa amesema, takribani watu elfu 55 kwa mwaka wanamaambukizi mapya na kundi kubwa likiwa ni vijana.  kati ya hao asilimia 40 ya vijana wanamaambukizi mapya wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.
Amesema kati ya hao asilimia 40,  asilimia 80 ni watoto wa kike.
Amesema matumizi ya kondomu yatasaidia sana maambukizi mapya ya VVU na kuwawezesha watu kuishi maisha mazuri huku wakiendesha shughuli zao.

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yanatarajia kufanyika desemba Mosi mwaka huu, n kitaifa yatafanyikia jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa Rais, Samoa Suluhu Hassan.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akitembelea katika mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja leo Jijink Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kandomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba Mosi.
 Naibu Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na taasisi mbalimbali katika uzinduzi wa mkakati wa kondomu uliofanyika leo kwenye Viwanja vyw Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Abdalla Ulega akielezewa namna ya kuvaa kondomu ya kiume na muelimishaji kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kutoka T- Marc Tza Benjamin Salema alipotembelea mabanda yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi leo Jijini Dar es Salaam.

MTENDAJI MPYA WA ETIHAD ATHIBITISHA KUJITOLEA KWA AJILI YA TANZANIA

$
0
0
Meneja Mkaazi wa Shirika la Ndege la Etihad nchini Tanzania, Bw. Ailende 'Allen' Okoromu

27 Novemba 2017- Dar es Salaam. Shirika la Ndege la Etihad Airways limemteua Ailende 'Allen' Okoromu kama Meneja Mkaazi ambaye anasimamia Shughuli zote za Shirika hilo nchini Tanzania.

Akiripoti kwa John Friel, Meneja Mkuu wa Shirika la Etihad Airways, anayesimamia kanda ya Afrika Mashariki na kusini, Bw. Okoromu ataongoza Shirika la Etihad hapa Tanzania likiwa na mikakati mbali mbali ya kujitangaza kibiashara nchini Tanzania, pia kuwajibika kwa kuimarisha zaidi ushirikiano na washirika wa biashara ya usafiri wa anga pamoja na wateja wakubwa wa Shirika hilo.

Okoromu anaanza jukumu hilo jipya jijini Dar es Salaam akitokea kwenye nafasi yake ya awali kama Meneja wa Mauzo wa Shirika la ndege la Etihad nchini Nigeria, ambako alikuwa na jukumu la kuendeleza shughuli za kibiashara za ndege hiyo katika bara la Afrika Kusini mwa Sahara na kanda ya Bahari ya Hindi. 
 
Kabla ya kujiunga na Etihad Airways mwaka 2012, alifanya kazi za mauzo katika vitengo mbalimbali vya juu akiwa katika mashirika ya Aviareps Nigeria Limited na Virgin Nigeria Airways ambako alijenga uelewa wa kina wa masoko biashara na burudani kwa Afrika ya Kati.

John Friel alisema: "Tumejikita kuhakikisha soko letu muhimu sana la Tanzania linakua na ninafurahi kuwa Ailende atakuwa akiongoza timu yetu katika kukuza biashara yetu huko.

Uzoefu wake mkubwa wa biashara na rekodi za mafanikio katika sekta ya anga itakuwa ya thamani sana katika kukuza ufahamu wa Shirika la anga la Etihad, na kumfanya awe mfanyakazi bora wa nafasi hii muhimu mpya nchini Tanzania, ambapo kuna soko lenye nguvu litakalotupa uwezo mkubwa wa kukua zaidi.

Akizungumzia uteuzi wake, Ailende alisema: "Ninafurahi kuchukua nafasi hii mpya nchini Tanzania, ambapo kuna soko lenye nguvu lenye uwezo mkubwa wa kutufanya Etihad kukua zaidi.

"Ninatarajia kufanya kazi na timu hapa kutafuta njia mpya za kupanua ushirika wetu wa kimkakati na ushirikiano wa kibiashara, kuimarisha uhusiano wetu wa kuwapa wateja wetu huduma bora zaidi kwa furaha, na ukarimu.

Shirika la ndege la Etihad lilianza shughuli zake nchini Tanzania Desemba 2015, wakitoa huduma ya kila siku inayoendeshwa na ndege aina ya Airbus A320 zenye viti 16 katika daraja la pili/biashara na viti 120 kwa ndege darja la Uchumi. Dar es Salaam ni njia ya tatu ya ndege kwa nchi za Afrika Mashariki, ikijumuisha Nairobi nchini Kenya, na Entebbe, Uganda.

Waziri Mahiga akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni alipomtembea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba 2017.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Italia. Pia wamejadili mikakati ya kuboresha ushirikiano katika sekta ya elimu hususan elimu ya ufundi, miundombinu, utalii, biashara na uwekezaji. 
Mazungumzo ya Kiendelea.

WANAWAKE TANGA WAVUTIWA NA AMANA BANKI

$
0
0

Wanawake wanaojishughulisha na shughuli za ujasiliamali Mkoani Tanga wamesema wamevutiwa na programu ya ukopeshaji  wa vitendea kazi badala ya fedha taslimu unaoendeshwa na benki ya Amana na kudai unaweza kusaidia kuendesha miradi endelevu.

Walitoa maelezo hayo  wakati wa kongamano la jukwaa la wanawake wa Mkoa wa Tanga lililofanyika jijini hapa kwa lengo la kujadili mikakati ya kujiendeleza kiuchumi.

Wakizungumza baada ya mkuu wa idara ya miradi ya bidhaa na usimamizi wa mambo ya sheria wa benki ya Amana,Muhsin Mohamed (Pichani Juu) kuelezea kuwa benki hiyo inatoa mikopo ya vitendea kazi na uwezeshaji wa kuendesha miradi badala yafedha,wanawake hao walisema programu hiyo itaweza
kuwaendeleza kiuchumi.

“Sisi wanawake tunajijua wenyewe,ukinikopesha fedha taslimu nitaingia tama ya kwenda kupeleka kwenye vikoba badala ya kufanyia mradi niliokopea,ndiyo maana wengi wetu tunaishi kwa madeni na kunyang’anywa samani za nyumbani”alisema  Sophia Juma mkazi wa Chuda Jijini hapa.

Walisema kama benki hiyo itaweka mikakati mahsusi kwa ajili ya
wajasiliamali wanawake,wanaamini kuwa itawasaidia kuendesha miradi ya maendeleo bila vikwazo.

Akizungumza katika jukwa hilo,Muhsin alisema benki hiyo inayofuata misingi isiyokubali utoaji wa riba na kwamba inakopesha wafanyabiashara wakubwa wa ngazi ya kati,wadogo na hata vikundi.

“Ukiomba mkopo kwetu tutahitaji mpango wa mradi unaotaka
kuendesha,ukishakidhi vigezo  kama wewe ni uanataka kufuga kuku tunakununulia vifaranga,vyakula na kuliweka banda lako katika mazingira rafiki ya kiufugaji”alisema Muhsin.

Mwenyekiti wa jukwaa hilo,Mariam Shamte aliitaka benki hiyo
itakapofungua tawi lake jijini Tanga kutenga dirisha maalumu la
kuwahudumia wajasiliamali wanawake ambalo litakuwa na jukumu pia la kuwapa elimu ya namna ya kuendesha miradi mbalimbali.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi ya Mbeya Desemba 8 na Chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam Desemba 22. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya mahafali hayo, Dk. Mrisho Malipula na katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Mrisho Malipula, akitoa ufafanuzi juu ya mahafali hayo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, akitoa ufafanuzi juu ya mkutano wa Baraza la Masajili 'Convocation' utakaofanyika Novemba 29, 2017 Kampasi Kuu Morogoro.

Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.

 

Morogoro, Tanzania-Novemba 27

MAHAFALI ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe yanatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 30, 2017, jumla ya wahitimu 3,461 katika mwaka wa masomo 2016/2017 wanatarajiwa kutunukiwa shahada, stashahada na astashahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas samatta, kati ya wahitimu hao ni

*Shahada ya Uzamivu (PhD) ni 4 (0.12%)

*Shahada za Umahiri (Masters) ni 1,005 (29.04%)

*Shahada za Kwanza (Bachelors) ni 2,063 (59.61%)

*Stashahada (Diploma) ni 191 (5.52%)

*Astashahada (Certificate) ni 198 (5.72%).


Kati ya wahitimu wote waliohitimu Kampasi Kuu ni 2,119 (61.23%).

Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Mbeya ni 734 (21.21) na Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Dae es Salaam ni 608 (17.57%).

Mahafali hayo yanatarajiwa kufanyika Kampasi Kuu Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi Mbeya Desemba 8 2017 na Chuo cha Kampasi Dar es Salaam Desemba 22 2017.

Mahafali hayo yatatanguliwa na mkutano wa 17 wa baraza la Masajili Çonvocation' utakaofanyika Novemba 29 2017 katika ukumbi wa mihadhara wa Fanon, uliopo kampasi Kuu. Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe kuanzia mwaka 2002 na wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Maendeleo (IDM) wanakaribishwa kuhudhuria mkutano huo.

Mjadala mahususi na nafasi ya wahitimu na wanachuo katika kuchangia maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe utafanyika.

Aidha Baraza la Masajili linaendelea kuwahamasisha wahitimu wote wa Chuo Kikuu Mzumbe na wadau wengine kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa hosteli ya wanachuo wa kike kupitia 'Çonvocation Fundraising Account'namba 01o150209448900 iliyopo Benki ya CRDB, Tawi la Mzumbe.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AAGIZA MKANDARASI WA REA KUHAKIKISHA UMEME UNAWAKA KISIJU NA MKAMBA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega katika kata ya Kisiju  wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa umeme wa vijijini REA kwenye Kata ya Kisiju na Mkamba na kuagiza Mkandarasi anayesimamia mradi huo kuhakikisha Ijumaa umeme unawaka kwenye vijiji hivyo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameagiza mkandarasi anayesimamia Mradi wa  umeme wa vijijini REA mkoa wa Pwani kufikia Ijumaa aweze kuhakikisha nyumba 14 za Kijiji cha Kisiju ziwe tayari zimeshaingia umeme pamoja mkandarasi kuweka transfoma zilizoharibika haraka sana kwenye Kijiji cha Kizapara Mkamba.

Akiwa ameambatana na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega, Naibu Waziri Wa Nishati ameyasema hayo mbele ya wananchi wa kata ya Kisiju na Mkamba na kuahidi kuwa ifikapo siku ya Ijumaa ataenda  kuhakikisha kama kweli nyumba hizo zitakuwa zimeshaingia umeme na kuwaka.

Naibu Waziri wa Nishati amemtaka mkandarasi ahakikishe transfoma hizo mpaka siku ya Ijumaa ziwe zimeshafungwa kuanzia kesho huku akiwaagiza Shirika La Umeme Nchini Tanesco pamoja na REA kuhakikisha matatizo hayo yanamalizika.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wanakijiji wa Kisiju wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi wa umeme wa vijijini REA na kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi na kumuagiza mkandarasi kuhakikisha umeme unawaka kufikia siku ya ijumaa kwa kata ya Kisiju na Mkamba.

Subira amesema kuwa, umeme huo wa REA hatua ya tatu  takribani vijini 25 vya wilaya ya Mkuranga vimeingia kwenye mradi huo na kiujumla vitakuwa vijiji 43, na serikali imedhamiria kuanzia 2017 hadi 2021 vijiji vyote 7873 vyote viwe vimepelekewa umeme.

Mbunge wa Mkuranga Ulega, amesema wananchi wa baadhi ya vijiji vya Mkuranga walikwamisha mchakato wa kupatikana kwa umeme wa REA kwa kudai fidia ya maeneo yao yaliyotakiwa kupita mradi huo.

"Umeme wa REA ambao ni wenye gharama nafuu zaidi umekwamishwa kwa kipindi kirefu na wananchi wenyewe kwani wengi wao walikuwa wanadai fidia ya maeneo yaliyotakiwa kupita mradi huo," amesema Ulega.

Ulega amesema kuwa, mradi huo wenye manufaa makubwa kwa wananchi wavijijini ulikwamishwa na wao wenyewe kwa takribani miaka miwili na kufikia wengine kuamua kulipa fidia kwa wanakijiji waliokataa mradi huo kupita kwenye maeneo yao.

Naibu waziri wa Nishati aliweza kutembelea kijiji cha Kisiju na Mkamba na kujionea namna mradi wa REA ulipofikia pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi katika kupata umeme huo.

Takribani Bilioni 469 kwa fedha za ndani na bilioni 30 kwa fedha za nje zimetengewa kwa ajili ya Wizara ya Nishati kuhakikisha umeme unafika katika Vijiji vyote na ifikapo June 2019 kwa awamu ya kwanza vijiji takribani 3559 vitakuwa vimeshapata umeme wa uhakika
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na wananchi wa kata ya Kisiju wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkranga Abdallah Ulega akizungumza na wanakijiji wa Kiparaza kata ya Mkamba wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ya ukaguzi wa mradi wa umeme vijijini REA kwenye kata za Kisiju na Mkamba.
Naibu waziri wa Nishati Subira Mgula akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdalaah Ulega wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi wa umeme wa vijijini REA  katika kata za Kisiju na Mkamba. Picha zote na Emmanuel Masaka.


KUZINGATIA MAADILI NA KUPIGA VITA RUSHWA NDIO MSINGI MKUU WA MAENDELEO YA TAIFA LETU

$
0
0


Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akimkabidhi nyaraka kuhusu maadili mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI Bi. Janeth Mishinga wakati wa uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa nchini.
Sehemu ya washiriki waliohudhuria ufunguzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) 
Baadhi ya wanafunzi waliowawakilisha wenzao wakati wa Klabu za Maadili wakati wa wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo.

Rais wa Zanzibar Dk Shein Azungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Alipofika Kujitambulisha leo Ikulu

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Kijarida cha Mahakama Kuu Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Profesa Ibrahim Hamis Juma alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo 27-11-2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Profesa Ibrahim Hamis Juma alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo 27-11-2017.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa amefuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Profesa Ibrahim Hamis Juma, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha leo. 27-11-2017.9

Picha na Ikulu

Zabuni Mradi wa Umeme wa Stiegler’s yafunguliwa

$
0
0
 Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia kwa waliokaa) akishuhudia ufunguaji wa Zabuni ya Ujenzi wa mradi wa Umeme wa  Stiegler’s Gorge (MW 2100) uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Katikati  ni  Mkurugenzi wa Idara  ya Manunuzi, Wizara ya Nishati, Armon Macachayo na wengine ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na watendaji  kutoka Kampuni mbalimbali. 
Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na watendaji kutoka kampuni mbalimbali zilizonunua zabuni ya Mradi wa Umeme wa Stiegler’s  Gorge wakiwa katika kikao cha ufunguaji wa Zabuni hizo jijini Dar es Salaam.



Zabuni ya Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha Umeme kiasi cha MW 2100 kwa kutumia maporomoko ya maji katika Mto Rufiji (Stiegler's Gorge) imefunguliwa leo tarehe 27/11/2017 ambapo Kampuni 81 zilijitokeza kununua nyaraka za Zabuni hizo na kampuni Nne ndizo zilizorudisha nyaraka za zabuni husika. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ugavi ya Wizara ya Nishati, Armon Macachayo wakati wa kikao cha Zabuni hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.

Macachayo alisema kuwa baada ya ufunguaji wa Zabuni husika, Zoezi linalofuta ni kufanyika kwa tathmini ili kupata Kampuni moja itakayokidhi vigezo vya kukabidhiwa mradi.

Zabuni hiyo ilitangazwa tarehe 30 Agosti, 2017 ambapo Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, ilialika Taasisi Binafsi na Kampuni zenye uwezo kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kuomba zabuni husika.

Akitoa taarifa za kutangazwa kwa Zabuni husika mwezi Agosti, 2017, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alisema kuwa Mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga mradi huo ni yule atakayeridhia kujenga mradi husika kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi na kusema kuwa kukamilika kwa mradi husika kutasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme nchini.

Inatarajiwa kuwa, baada ya zoezi la tathmini na majadiliano ya mkataba wa ujenzi kukamilika, mwanzoni mwa mwezi Januari mshindi wa zabuni hiyo atakabidhiwa Mradi ili kuweza kuanza kazi ya ujenzi wa mradi mara moja.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alishukuru kampuni zote zilizojitokeza kununua zabuni husika na kuwakaribisha kuwekeza katika miradi mingine ya uzalishaji Umeme.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA PESA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU

$
0
0


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katika picha akiongea na wataalam wanahabari na viongozi wa Wizara hiyo kutoka katika sekta ya Uvuvi, baada ya kuonyeshwa zana zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu, katika kanda ya Dar es Salaam.
Katika picha baadhi ya zana zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu katika kanda ya Dar es Salaam.

Kushoto Bw. Obadia Mbogo, Afisa katika sekta ya uvuvi aliyeshiriki katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu, akimuonyesha Waziri Mpina na ujumbe wake aina ya baadhi ya vilipuzi vilivyokamatwa katika zoezi hilo katika kanda ya Dar Es Salaam.


Akiwa katika zoezi la kupongeza kikosi maalum kilichoanza oparesheni ya kupambana na uvuvi haramau katika bahari ya hindi leo, zoezi lililokwenda sambamba na kuonyeshwa vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu vilivyokamatwa katika zoezi hilo lilioanza mwezi Julai mwaka huu, Waziri wa mifugo na Uvuvi Mhe. Luahaga Mpana amezitaka halmashauri ambazo shughuli za uvuvi zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.

Mpina ambaye ameshangazwa na kitendo cha Halmashauri hizo kukusanya fedha za ushuru zitokanazo na shughuli na uvuvi na kujisahau kabisa kuingia katika zoezia la kupambana na uvuvi haramu kwa kutenga fedha hususan za kufanya doria.

Aidha, Mpina Amewataka viongozi wakuu wa Wizara yake, Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba na Kaimu Mkurugenzi wa maeneleo ya Uvuvi Bw. Magese Bulayi kutembea na barua rasmi katika ziara zao za kikazi kwenye halmashauri husika zilizokuwa tayari kuwawajibisha watumishi wazembe katika zoezi zima la kupambana na uvuvi haramu.

“Mkurugenzi wa maendeleo ya uvuvi na katibu Mkuu,nawaagiza mtembee na barua zilizotayari kusimamisha au kufukuza kazi watumishi wazembe katika halmashauri, barua hizo zibaki wazi katika sehemu ya kujaza majina yao tuu, na ndani ya mwaka mmoja nataka tukomeshe kabisa uvuvi haramu. “ Alisisitiza Mpina.

Awali akieleza madhara ya matumizi ya kitoweo cha samaki waliyovuliwa kwa njia ya vilipuzi na mabomu, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yohana Budeba alisema kuwa samaki wanaovuliwa kwa njia hiyo huleta madhara makubwa kwa walaji ikiwa ni mapoja na magonjwa ya tumbo na Saratani

SHAMBA LINAUZWA LIPO MKURANGA MKOANI PWANI PIGA NAMBA 0759239338 NA 0717389688 KWA MAWASILIANO

$
0
0

Mmiliki wa shamba hilo, akiwa amekanyaga bicon za mipaka ya shamba hilo.

Mmiliki wa shamba hilo akionesha bicon zilizopo katika shamba hilo.

SHAMBA LINAUZWA LIPO WILAYANI MKURANGA MKOANI PWANI KIJIJI CHA KIBUYUNI LIPO JIRANI KABISA NA SHULE YA SEKONDARY YA PANZUO. NAULI YA KWENDA KATIKA SHAMBA HILO KWA DALADALA NI SHILINGI, 3,000.

UMBALI KUTOKA KARIAKOO KWENDA KATIKA SHAMBA HILO NI KILOMITA 60 NA BEI KWA KILA HEKARI NI SH.2,999,999 KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA HIZO HAPO ZA ZAIN NAMBA 0687347676

MASAUNI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI NYUMBA MPYA ZA ASKARI POLISI MKOANI MARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima (watatu kulia) na viongozi wengine, baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara, kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari hao
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata ya Mukonde, Mkoani Mara, Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, baada ya kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata ya Mukonde, Mkoani Mara,wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano.Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara kwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
Familia za askari wanaotarajiwa kuhamia katika nyumba mpya zilizopo katika eneo la Mukonde, wakimsikiliza Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati alipotembelea kuona maendeleo ya mradi huo ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani Mara. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMANNE LEO NOVEMBA 28,2017


WADAU WA NGUVU WATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA UONGOZI WA BIASHARA CHUO KIKUU CHA ESAMI ARUSHA

$
0
0
Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) ,Florian Mutabazi akipokea Cheti chake kutoka kwa Waziri wa Elimu wa Malawi,Bright Msaka baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA) Chuo Kikuu cha Eastern and Southern African Management Institute(ESAMI) kilichopo jijini Arusha katika mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,wahitimu wametoka nchi 32 barani Afrika.Picha na Filbert Rweyemamu 
Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Florian Mutabazi akiwa mwenye furaha baada ya baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA) 
Mdau wa blog za kijamii ,Yotham Ndembeka ambaye ni mtumishi katika Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha akipongezwa na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Eastern and Southern African Management Institute(ESAMI)kilichopo jijini Arusha,Profesa Bonard Mwape baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA). 
Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Florian Mutabazi(kushoto) akifurahia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Utawala na Fedha,Jesca Eriyo. 
Picha ya pamoja ya uongozi wa taasisi ya ESAMI. 
Mtumishi Mwandamizi katika Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Grace Mbaruku(kulia) akifurahia baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA). 

MAKAMU WA RAIS AWASILI NAIROBI KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS UHURU KENYATTA LEO

$
0
0


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae na Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Hazara Chana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni katika chumba cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya.
1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya asubuhi hii ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika leo katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. 
Picha na Ikulu

HALMASHAURI ZAAGIZWA KUHAKIKISHA WANAHAMASISHA WANACHI KUWA NA VYOO BORA PAMOJA NA KUVITUMIA

$
0
0
Na,Jumbe Ismailly SINGIDA Nov,28,2017 Magonjwa 

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Joseph Kakundi amewaagiza Maafisa afya wa ngazi zote katika Halmashauri,Hospitalini,Kata na vijiji kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kuwa na vyoo bora kwenye kaya zao pamoja na kuvitumia ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza miongoni mwa jamii.

Naibu Wazziri huyo alitoa agizo hilo alipokuwa akifungua mkutano wa siku tano wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania unaofanyika katika Hoteli ya Katala Beach mjini Singida.

Kwa mujibu wa Kakundi akizungumzia kwa upande wa shule za msingi na sekondari alibainisha kuwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa kila wanafunzi 20 wa kike kutumia tundu moja na kwa wanafunzi 25 wa kiume watumie pia tundu moja,kiwango ambacho hakitoshelezi kutokana na idadi ya matundu yaliyopo katika shule hizo.

“Kwa hiyo lazima walimu wasimamie ili matundu yaliyopo yatumike kikamilifu japokuwa kuna upungufu na tunahitaji hela nyingi sana ili tuweze kufikia viwango vya kitaifa,lakini pale penye upungufu ni lazima tusimamie wanafunzi watumie vile vyoo vizuri”alisisitiza Naibu waziri huyo.

Hata hivyo Naibu Waziri Kakundi alisisitiza kwamba shule yeyote ile isiyokuwa na matundu ya vyoo,shule hiyo haitaruhusiwa kuendelea kutoa huduma kwa wananzi na badala yake serikali haitasita kuifunga mara moja na kuelekezaa kwamba ni lazima pawe na njia zingine za dharura za kuwasaidia wanafunzi hao kwenda kujisaidia.

Akitoa taarifa fupi kwa Naibu Waziri huyo,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Selemani Manyata alisema kwamba takribani asilimia 4 ya wananchi wa Mkoa wa Singida ambao ni sawa na wananchi 11,000 hawana kabisa vyoo bora na asilimia 48 ya wananchi wana vyoo vya muda hali ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji yanayoleta magonjwa ambayo matibabu yake ni gharama kubwa.

“Sisi kama Chama cha Afya ya Jamii Tanzania kuanzia haya magonjwa yanayoweza kuzuilika na kama malengo ya Mileniamu yanavyosema kwamba tupunguze kiwango hicho”alifafanua.Aidha Mganga Mkuu huyo aliweka bayana apia kwamba kutokana na idadi kubwa ya kaya ambazo hazina vyoo wanaendelea kuhamasisha Halmashauri ili wananchi waweze kutumia vyoo.

Hata hivyo Dk.Manyata alitoa mfano kwamba inakadiriwa kuwa mtu mmoja hujisaidia kinyesi kisichopungua uzito wa gramu 250 na kwa mwaka mtu mmoja hujisaidia kinyesi chenye uzito wa kilo 90 kwa siku kinachoenda kwenye vyanzo vya maji.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Afya ya Jamii Tanzania,Dk Mashombo Mkamba alizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliananazzo kuwa ni pamoja na kuelewa na watu kukubali na wawe tayari kupima afya zao kwani mpaka sasa bado watu ni wagumu sana kupima afya zao,labda akishauriwa kupima malaria na siyo ugonjwa mwingine.
 baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tano wa wanachama wa Afya ya jamii Tanzania wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wa Katala Beach mjini Singida wakiendelea na mkutano wao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

KAMPUNI YA BIMA YA RESOLUTION YAWAKUTANISHA MADALALI WA BIMA, WARUDISHA SHUKURANI KATIKA JAMII

$
0
0
Mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma ambaye ni Meneja Mkazi wa Africa Practice mshauri  akitoa shukurani zake za dhati kwa Kampuni ya Bima ya Resolution kwa kuwakutanisha Madalali wa Bima 'Insurance Brokers' toka sehemu tofauti nchini ambapo kwa kufanya hivyo itaongeza zaidi ufanisi na ushirikiano baina yao na Kampuni ya Bima ya Resolution.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mambo mbalimbali kuhusiana na kampuni hiyo na kuwashukuru madalali wa Bima kwa kwa kuungana nao katika chakula cha usiku, pamoja na hayo alisema kuwa wapo Kenya, Uganda na Tanzania, kwa Tanzania wapo Dar es salaam na Arusha lakini hivi karibuni watafika Zanzibar na Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo akieleza kwa ufupi kuhusiana na tukio hilo la kurudisha shukurani, ambapo pia alizitaja baadhi ya huduma wanazozitoa ikiwa nipamoja na; Travel Plan, Medical plan, Liability plan,Home Insurance,Marine insurance na Motor Private Insurance 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo (aliye simama nyuma) akiwatambulisha viongozi wa Idara mbalimbali katika kampuni ya Bima ya Resolution wa nchini Tanzania.
Bwana Melkizedech Nyau ambaye ni mtakwimu wa Bima kutoka kampuni ya Bima ya Resolution akielezea bima ya Afya Bora kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini kuanzia mwaka 0 hadi 64 ambao ni kama Bodaboda, Mama ntilie,wauza maandazi pamoja na makundi mbalimbali yanayofanana na hayo. Alieleza kuwa ili kujiunga na Bima hiyo itakuwa vizuri watu wawe katika kundi au Vikoba waweze kupata kwa pamoja huduma hiyo bora kutoka kampuni ya Resolution.
Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku ambaye pia ni Mchekeshaji maarufu hapa Nchini Tanzania akiendelea kutoa taratibu mbalimbali wakati wa  chakula cha usiku kilicho andaliwa na Shirika la Bima la Resulution katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku akiwauliza maswali mbalimbali kuhusiana na bima.
Bi. Mailda William(Kushoto) kutoka Aste Insurance Brokers ambao walishinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Msichana ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution

Bi. Jenifa Projest (Kulia) kutoka Aste Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma baada ya  kushinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Salvation Army  ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution
 Bi. Fauzia Bairu (Kulia) kutoka Pioneer Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati baada ya  kushinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Sustainable Education ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution.
 Bw. Emmanuel Mkindi, Meneja wa Maendeleo ya Biashara- Biashara kwa ujumla kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution akitoa neno la shukurani kwa madalali wote wa bima waliofika katika tukio lao la 'Appreciation Dinner' ambapo kaulimbiu yao inasema 'Protecting what you value' yani tunalinda unachokithamini.
Madalali wa Bima wakiwa katika hafra ya chakula cha usiku iliyo andaliwa na Kampuni ya Bima ya Resolution kwa ajili ya kurudisha shukurani kwa jamii.

KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA

$
0
0
Katibu mkuu wa  Wizara ya Viwanda ya Biashara na Uwekezaji,  Prof  Elisante   Ole Gabriel  akiwa katika ziara ya kikazi nchini China  (Beijing) ametembelea kiwanda cha  Huanri Medical Group kinachojishughilisha na utengenezaji wa vifaa tiba, Mitungi ya Gesi na Matairi.
Akiwa kiwandani hapo alishuhudia baadhi ya  Vifaa vya tiba vinavyongenezwa kiwandani  hapo Fingertip/Handheld Oximeter ambacho hutumika kupima kiwango cha hewa ya Oxygen katika damu  (vinawafaa zaidi  wakina mama waja wazito na wazee), Anesthesia Machine inayotumika katika upasuaji mkubwa  pale ambapo mtu amewekewa dawa ya usingizi, Ventilator inayotumika ICU kwa ajili ya kusaidia upumuaji kwa mgonjwa aliyezidiwa pamoja na Kifaa kinachofahamika kama Health Machine (Mfano wa Briefcase) kilichotengenezwa mahususi kwa ajili ya soko la  bara la Afrika na kinaweza kutibu takribani magonjwa  16  na kinabeba vifaa vingi ndani yake. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwezeshaji Prof. Elisante Ole Gabriel akishiriki katika kuunganisha Mashine inayofahamika kama  "Anesthesia Machine" inayotumika katika usaidizi wa shughuli za  Upasuaji Mkubwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Prof. Elisante Ole Gabriel (Katikati) pamoja na ujumbe alioambatana nao, alipotembelea kiwanda cha Huanri Medical Group jijini Beijing nchini China.

 Akieleza lengo la kutembelea kiwanda hicho  Prof. Elisante alisema ni  kuzibaini  fursa za uwekezaji zilizopo na jukumu la wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni kuhakikisha kwamba wanajenga mazingira ya  ya wawekezaji  kuwekeza vizuri bila kupoteza muelekeo  na lengo kubwa la kuinua Uchumi wetu. “tungependa tuwe na mikataba ambayo kwa vyovyote vile  hata kizazi kijacho kikija kuangalia hayo makubaliano  kifurahi na kuthamini kwamba  waliongia katika makubaliano waliona mbele na walijali maslahi mapana ya  taifa. 

Tunachoamini  ni kwamba wenzetu hawa wachina  katika tasnia mbalimbali watakuja Tanzania watawekeza,  jukumu letu kubwa sisi  na tunachokifanya ni kuendelea kuwavutia kuwaweka katika mlengo ambao watafanya kazi zao vizuri  katika mazingira wezeshi na rafiki ili mwisho wa siku  ajira ziongezeke  katika nchi yetu ya Tanzania  lakini pia tuweze kuuza vifaa  vingi sana kutoka Tanzania kwenda kwenye masoko ya nje  kwa ajili ya kupata fedha za kigeni  lakini lingine ambalo ni siri kubwa ya mafanikio  ni kupata pia utaalam  ili vijana wa kitanzania waweze kupata taaluma hii  ambayo ni ya kiwango cha  juu”  Alisema Prof. Elisante.
  akifanya mahojiano na vyombo vya habari baada ya kuhitimisha ziara yake kiwandani hapo 
 Akitazama moja ya hatua za kutengenezaji wa Vifaa vya Tiba kiwandani hapo
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Huanri Medical Group Bw. Wang qianjun Mara baada ya kuwasili kiwandani hapo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na Viongozi kutoka China - Asia Economic  Development Association Overseas Cooperation Committee, alioambatana nao Kiwandani hapo.
  Akionyesha furaha yake  Katibu Mkuu  alisema tayari Huanri Medical Group wamekubali walau kwenye masuala ya  taaluma ya vifaa tiba  wataweza kuwaalika vijana wetu wa kitanzania waje wakae China kwa takribani miezi mitatu ili wapate utaalam wa kuunganisha vifaa hivi vya tiba  lakini lengo la serikali yetu ni kuona  kiwanda hiki kikijengwe Tanzania  na hatua hii itapanua wigo wa ajira na pato la taifa litazidi kuongezeka. 

“ Huanri Medical Group  ni miongoni  mwa kundi kubwa la wawekezaji  wanaotarajia kuja  Tanzania Mwezi Machi 2018 kwa ajili  ya mikutano mbalimbali ya uwekezaji  na sisi tunawahakikishia kwamba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais  Dr. John Pombe Magufuli  inawakaribisha sana, na imani yetu ni kwamba Changamoto ya ajira itaweza kupungua pale tutakapoendelea kuleta wawekezaji nchini.” Alisema  Prof Elisante.
Akihitimisha ziara hiyo katika kiwanda hicho  Prof. Elisante amewataka watanzania kuendelea kupenda vitu vinavyozalishwa katika Taifa letu  na kununua vitu vyetu vya ndani. Amesema  jambo la muhimu na kubwa ni  upatikanaji wa uhamisho wa technolojia kutoka China  na kwamba tayari  Tanzania imeahidi kufanya kazi na wawekezaji  hao  kwa  ushirikiano  kwa lengo la  kuhakikisha ndoto na falsafa hii ya serikali ya awamu ya tano  inakamilika na kufikiwa kwa  kwa kasi nzuri.”

Kwa upande wake Rais wa kampuni hiyo ya Huanri Medical Group Bw. Wang qianjun amefurahishwa na juhudi ambazo zinafanywa na Serikali ya Tanzania kwenye sekta ya viwanda  na ameahidi ushirikiano mkubwa na  kuonyesha utayari wake wa kuwekeza Tanzania . 
Katika ziara hiyo Katiba Mkuu  wa Wizara ya  Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel aliambatana na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China Said Massoro, Viongozi kutoka  China - Asia Economic Development  Association Overseas Cooperation  Committee (Naibu Katibu Mkuu Bi.  Rui LU na Makamu wa Rais Bi. Tian Wenhui) Bw.Remidius Emmanuel  Katibu Mkuu wa  Shirikisho la Wanafunzi Watanzania nchini China pamoja  Bi. Muka Kamuzora  Mtanzania anayesoma  Masuala ya Uchumi hapa China.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images