Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1441 | 1442 | (Page 1443) | 1444 | 1445 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mombo mashuka kwa niaba ya Vituo vya Afya vyengine kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Korogwe Vijijini kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini


  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mombo mashuka kwa niaba ya Vituo vya Afya vyengine kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Korogwe Vijijini kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu kulia akiteta jambo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo kuhusu umuhimu wa vifaa hivyo kutunza ili kuweza kuwahudumia wananchi.
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiingia kwenye hospitali ya wilaya ya Korogwe Magunga kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Serikali kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,John Nyarongo
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,John Nyarongo

  Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea vifaa hivyo
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,John Nyarongo naye akizungumza katika halfa hiyo Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini akizungumza na waandishi wa habariMBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Nyong’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu alisifu juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto za afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili wananchi kupata huduma bora


  Proffesa Maji Marefu aliyasema hayo wakati akikabidhi vifaa tiba kwa Halmashauri ya Korogwe Vijijini vilivyotolewa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupitia Bohari ya Madawa MSD wamewapatia vitanda vya kulalia wagonjwa,magodoro na mashuka vikiwa na thamani zaidi ya sh.milioni 17.

  Vifaa tiba hiyo kwa upande wa vitanda vya wagonjwa vitasambazwa kwa baadhi ya vituo vya Afya na Zahanati zilizopo wilayani humo ambavyo ni Magoma, Mombo, Bungu,Mazinde,Manka,Hale,Mashewa,Vugiri na MakumbaKwa upande wa vitanda vya kuzalishia vitapelekwa kwenye zahanati za Mandera,Kwemazandu,Lwengera,Mkomazi na Makumba ambavyo vitasaidia kuondoa changamoto zilizokuwepo hapo awali.

  “Niwaambieni tu serikali yenu chini ya Rais Dkt John Magufuli imejipanga vema kuhakikisha inatatua kwa vitendo changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ya huduma za afya na ndio maana leo hii tunakabidhi vifaa hivi kwa lengo la kuboresha huduma hizo “Alisema.

  Alisema vifaa hivyo vimefika wakati muafaka ambapo vitasaidia kuondoa changamoto mbalimbali ambazo zilikuwepo ikiwemo mashuka,magodoro na vitanda vitakavyosaidia kuhakikisha huduma zinazotolewa vinakuwa bora.

  “Ndugu zangu wananchi serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imefanya mambo mengi makubwa likiwemo la kuhakikisha wanaboresha huduma za Afya katika maeneo mbalimbali nchini hivyo tuendelea kumuombea mungu na kumuunga mkono katika juhudi hizo “Alisema.

  Awali akizungumza katika makabidhiano hayo,Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe (DMO) Dkt Frank Chiduo aliishukuru serikali kwa kuwapatia msaada huo ambao umekuwa chachu ya ya kupunguza changamoto za upungufu wa vifaa tiba kwenye wilaya hiyo kwa kuwapatia vifaa hivyo

  Alisema halmashauri ya wilaya ina jumla ya hospitali moja ,Vituo vya Afya vitatu na Zahanati arobaini na mbili zote zikiwa zinamiliki wa na serikali .

  “Lakini pia Halmashauri ina jumla ya vitanda 330 vya kulala wagonjwa pamoja na magodoro,shuka 624 kati ya shuka hizo 1320 zinahitajika ,vitanda 61 vya kujifungulia katika vituo vyote hivyo kukidhi mahitaji yaliyopo kwa sasa “Alisema.

  “Pia kati ya magodoro yaliyopo 80 yemachakaa na yanahitaji kubadilishwa hivyo kuwa na upungufu wa shuka 690 na godoro 80 “Alisema.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe, (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakiwaonyesha waandishi wa habari, tuzo ambayo PSPF ilinyakua katika mashindano ya kimataifa wakati wa mkutano wa taasisi ya hifadhi ya jamii Duniani, International social security association, taasisi tanzu ya ILO, tuzo ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017 mjini Adis Ababa Ethiopia mwezi uliopita. Tukio hili limefanyika pembezoni mwa mkutano wa kampeni ya uzalendo na utaifa iliyoongozwa na waziri Mwakyembe kwenye ukumbi wa mikutano wa PSPF jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2017.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umenyakua tuzo ya kimataifa ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017, baada ya kuwa Mfuko unaotoa huduma bora kupitia ubunifu wa mafao ya muda mfupi, yaani service quality in short-term products.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuonyesha tuzo hiyo iliyokwenda sambamba na kampeni ya uzalendo na utaifa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu alisema, Mfuko huo unajivunia kwa kuwa Mfuko wa kwanza miongoni mwa Mifuko mitano ya Hifadhi ya Jamii nchini, kuanzisha bidhaa na huduma za muda mfupi ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na hivyo kuvutia mifuko mingine ambayo kwa sasa nayo imeanza kutoa huduma hizo.

  “Mwaka huu katika mkutano wake wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani yaani International Social Security Association, taasisi tanzu ya Shirika la Kazi Duniani,(ILO) imeipatia PSPF tuzo baada ya kuwa Mfuko bora barani Afrika katika utoaji huduma bora kupitia ubunifu wa Mafao ya muda mfupi yaani service quality kwenye short-term products.” Alifafanua Bw. Mayingu.
  Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliipongeza PSPF kwa kujinyakulia tuzo hiyo na kuliletea taifa heshima kubwa kimataifa.
  “Kupambanishwa katika bara la Afrika na kushinda vigezo kadhaa ndipo unaambiwa bwana wewe unapata hii tuzo na tuzo hii imetolewa na taasisi yenye ushirikiano wa karibu sana na ILO hongereni sana.” Alipongeza Dkt. Mwakyembe.
  Alisema ushirikiano wa karibu miongoni mwa wafanyakazi wa PSPF ndio umepelekea mafanikio hayo.
  “Niwapongeze viongozi wote wa PSPF, Wafanyakazi wote wa PSPF, kwa kazi nzuri mnayoifanya mpaka mnatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa.” Alisema.
  Aidha kabla ya tukio hilo, Waziri aliwahamasisha watanzania kujenga moyo wa uzalendo na kujivunia utaifa wao kwani mambo hayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa.
  “Sisi tuliokuwepo kabla ya uhuru, niwaombe sana, tuwasaidie vijana wetu wa sasa kutambua tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi, kwa kujenga uzalendo wa kuipenda nchi yetu kama ambavyo ilikuwa hapo awali.” Alisema.
  Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muunganmo wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao mjini Dodoma, na Waziri aliwahamasisha wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia fedha ili kufanikisha swala hilo muhimu kwa taifa.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyemba, akizungumza kuhusu umuhimu wa jamii kiujenga uzalendo wa taifa lao la Tanzania.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Leah Kilimbi, akizungumzia maudhui ya hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. ASdam Mayingu, akizunhgumza kwenye hafla hiyo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakayti wa hafla hiyo.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw.Sami Khalfan, wakifuatilia hafla hiyo.
  Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Nelly Msuya akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Mkurugenzi wa vipindi wa Azam TV, Bw. Charles Hillary, (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Bw. Mayingu akizungumza huku akipongezwa kwa makofi na waziri Mwakyembe na Bi.Joyce Fisso, Katibu Mtendaji bodi ya Filamu Tanzania.
  Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bi. Grace Michael Kisinga.


  Baadhi ya wageni waalikwa
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fisso, akizungumza.
  Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo

  0 0


  0 0

  Na Mathias Canal, Singida

  Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS) umeendelea kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo ambapo pamoja na mambo mengine umeendelea kusaidia jamii ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali.

  Mapema Leo asubuhi Novemba 25, 2017 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekabidhiwa mabati 100 na Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Penseni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo.

  Mabati hayo yametolewa na PSPF Kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Uongozi wa Wilaya ya Ikungi inayoongozwa na Mhe Mtaturu katika kuimarisha mfuko wa elimu kwa muktadha wa kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuhimiza utatuzi wa Changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi ikiwemo Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.

  Akizungumza katika dhifa ya makabidhiano ya mabati hayo iliyofanyika katika eneo la shule ya sekondari Ikungi Mhe Mtaturu ambaye pia ni mlezi wa mfuko wa Elimu amewasihi wananchi na wadau kuchangia fedha au thamani zozote kadri wawezavyo ili kufanikisha kuboresha miundombinu ya elimu katika wilaya hiyo. 

  Sambamba na hayo pia ameushukuru Uongozi wa Mfuko wa Penseni PSPF kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kuboresha elimu kwa manufaa ya watanzania wote.

  Aidha, ameupongeza mfuko huo wa PSPF kwa mpango wao wa uchangiaji wa  hiari ambapo  mwanachama hutakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 , ili kuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake ambapo kiwango cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally Ameeleza kuwa PSPF ipo karibu na watumishi lakini pia ipo karibu na jamii hivyo wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwashirikisha kwenye jambo hilo muhimu la kuboresha elimu katika wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla wake.


  0 0

   WAKANDARASI wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) na wale wa kigeni, wakiendelea kuchapa kazi leo Novemba 25, 2017 ili kukamilisha hatua ya kwanza ya ujenzi wa mitambo Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambapo kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, kasi ya ujenzi inaridhisha na kwamba katika hatua hiyo ya kwanza TANESCO inatarajia kuingiza kiasi cha umeme Megawati 30 kwenye Gridi ya Taifa ifikapo Desemba 7, 2017 na hivyo kuongeza kiasi cha umeme katika safari ya kupata umeme wa uhakika na wakutosha kwenye ujezni wa uchumi wa Viwanda.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwashudia wahitimu wakiwa wanavaa kofia (hawapo pichani) baada ya kuwatunuku tuzo za fani mbalimbali kwenye mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akihutubia wahitimu na wageni waalikwa katika mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma
   
  Wahitimu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa tuzo mbalimbali katika mahafali ya 31 ya Chuo hicho mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akimtunuku mhitimu Felista Mayunga Shahada ya Uzamili katika Uchumi wa Maendeleo katika mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akiwa na viongozi wa Chuo na wageni waalikwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Stashahada za Uzamili na Shahada za Uzamili katika mahafali ya 31 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewataka  Wahitimu 3108 wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) waliotunukiwa tuzo zao katika Fani mbalimbali kwa mwaka 2016/2017 kuwa sehemu ya suluhisho katika changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi nchini pindi watakapoanza kuwatumikia wananchi hao na siyo kuwa sehemu ya matatizo katika jamii.

  Akizungumza katika mahafali hayo ya 31 ya Chuo hicho yaliyojumuisha Kampasi ya Dodoma na Mwanza yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.Chuoni hapo Maeneo ya Miyuji mjini Dodoma Dkt. Kijaji amesema kuwa elimu waliyoipata wakaifanyie kazi kwa uhalisia wa maisha ya Wananchi waliopo maeneo mbalimbali ili kuliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kati hata kabla ya 2025 kama Dira ya Taifa linavyotuelekeza.

  ‘Wahitimu wetu wana deni, deni hilo ni utumishi uliotukuka. Nendeni mkawatumikie Watanzania nendeni mkairejeshe imani ya Watanzania iliyoanza kupotea kwa Wataalam wa fani ya Mipango ya Maendeleo Vijijini’. alisema Dkt. Kijaji.Dkt. Kijaji aliongeza kwa kuwataka Wahitimu hao kwenda kuwafundisha Watanzania kwa vitendo mipango na mbinu thabiti ili waweze kuzalisha kwa tija kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu na ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja.

  Aidha Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitokuwa tayari kuwavumilia Wataalamu wazembe makazini na kuwataka wakafanye kazi kwa weledi mkubwa kwa manufaa ya Taifa.Dkt. Kijaji amefafanua kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora itakayowaongezea maarifa ili kuwa chachu katika Maendeleo ya Taifa.

  ‘Serikali inatekeleza majukumu yake kwa vitendo, ndiyo maana mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu inapewa kipaumbele cha kwanza (first charge). Alisema Dkt. Kijaji.Dkt. Kijaji ametoa wito kwa Taasisi za Elimu ya Juu zote Nchini kutoa mafunzo yatakayowawezesha Wahitimu mbalimbali kuweza kujiajiri pindi wamalizapo masomo yao ili kuongeza kasi ya uchumi nchini.

  Katika hatua nyingine Dkt. Kijaji amekipongeza Chuo hicho kwa utoaji wa elimu bora katika fani mbalimbali kwa kuwa idadi ya wanachuo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka na kwamba huo ni mfano tosha kuwa taaluma inayopatikana katika Chuo hicho ni nzuri na kutoa rai kwa wananchi wengine kuleta watoto wao kupata taaluma mbalimbali.Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Prof. Hozen Mayaya amesema kuwa wameendeleza, kuboresha na kudumisha mahusiano bora kati ya Chuo na wadau mbalimbali.

  Prof. Mayaya aliongeza kuwa ushirikiano mzuri wa wadau wao umekuwa kichocheo kikubwa katika kutekeleza majukumu yao makuu ya kufundisha, kufanya utafiti na kutoa huduma za ushauri na uelekezi kwa wadau mbalimbali.‘Chuo kinajivunia kuongeza udahili wa Wanafunzi 6,129 kwa mwaka 2016/17 kutoka wanafunzi 4,916 kwa mwaka 2015/16 ikiwa ni ongezeko la asilimia 24’. aliongeza Prof. Mayaya.

  Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Prof. Razack Lokina katika hotuba yake ya kumkaribisha Mgeni Rasmi amesema kuwa Uongozi wa Chuo umeendelea kutekeleza wajibu wake wa kuandaa wataalamu wa mipango ya maendeleo hasa vijijini ambako watanzania wengi wanaishi.‘Utekelezaji wa wajibu huu umeendana sambamba na kuongeza uwezo wa Chuo katika kutoa mafunzo yanayozingatia umahiri, kufanya tafiti na kutoa huduma za uelekezi katika Nyanja zote za mipango ya maendeleo’. aliongeza Prof. Lokina.

  Katika mahafali hayo ya 31 ya Chuo hicho jumla ya wahitimu 3,108, wanawake 1,631 wanaume 1,477 wamehitimu ngazi ya Astashahada, Stashahada, na Shahada za Uzamili.

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Songea  Marehemu Leonidas Gama. Waziri Mkuu aliungana na wanafamilia pamoja na wananchi wa Songea katika kijiji cha Lukuyi Wilayani Songea leo Novemba 25/2017 katika kuomboleza msiba huo.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea machache  nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Songea  Marehemu Leonidas Gamaambako aliungana na wanafamilia pamoja na wananchi wa Songea katika kijiji cha Lukuyi Wilayani Songea leo Novemba 25, 2017  kuomboleza msiba huo.
  Picha na habari na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, wananchi wa Songea katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Songea, Bw. Leonidas Gama, nyumbani kwa marehemu Likuyu wilayani Songea. 
  Marehemu Gama amefariki dunia jana Ijumaa, Novemba 24, 2017 katika Hospitali ya Peramiho mkoani Ruvuma alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, Novemba 27, 2017 katika kijiji cha Likuyu wilayani Songea.

  Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri tangu akiwa mtumishi wa umma na hata baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Songea. 

   Waziri Mkuu amesema msiba huo umeleta mtikisiko mkubwa kwa sababu baada ya kurudi nchini kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu aliwaeleza kuwa hali yake kwa sasa ni nzuri. ”Ametuachia pengo kubwa ambalo hatuna namna ya kuliziba.” 

   Ameongeza kuwa alipokea taarifa za msiba huo kwa huzuni na mshtuko mkubwa kwa sababu siku mbili kabla ya Waziri Mkuu kuanza ziara yake mkoani Ruvuma, Bw. Gama alimpigia simu na kumjulisha kwamba yeye anatangulia Songea kumpokea. 

   “Kifo ni mipango ya Mwenyezi Mungu na kwamba Bw. Gama ametangulia nasi tutafuata, hivyo wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Gama alikuwa kiongozi na mwanga wa maendeleo.” 

   Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaomba wanafamilia, mke wa marehemu na watoto na wananchi wa jimbo la Songea waendelee kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.” 

   Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bibi Christine Mndeme alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kuwafariji wafiwa licha ya majukumu mengi na makubwa aliyonayo. 

   Awali msemaji wa familia Bw. Issa Fusi alimshukuru Waziri Mkuu pamoja na viomgozi mbalimbali waliojitokeza na kuwafariji baada ya kutokea kwa msiba huo.”Kaka yetu tulimpenda sana kazi ya Mungu haina makosa.”


  0 0


  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akielezea ujenzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila wakati wa ufunguzi wa hospitali hiyo leo Novemba 25, 2017
   Muonekano wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila wakati wa  sherehe za ufunguzi leo Novemba 25, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole OCS wa Kibamba Mrakibu wa Polisi (SSP)  Pius  Lutumo akipata matibabu wakati akitembelea  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameongozana na Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong wakifuatiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, makamu wa Rais Mstaafu Mstaafu Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba wakielekea sehemu ya ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya
  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila
  leo Novemba 25, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akifunua kitambaa kuashiria kufungua rasmi Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akisaidiwa na viongozi wengine na wadau wa afya akikata  utepe kuashiria kufungua rasmi  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017.  0 0


  Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akinyajua bango juu lenye ujumbe unaosema “Ukatili wa Kijinsia Unachelewesha Tanzania ya Viwanda” wakati akipokea Maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
  Baadhi ya wananchi na wadau wa maendeleo wakiwa katika maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
  Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akiwaasa wadau na watanzania kujikita katika kupambana na ukatili wa kijinsia wakati akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
  Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akieleza namna Wizara inavyoshikiana na wadau na wananchi kupambana kuondoa ukatili wa kijinsia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
  Mkurugenzi wa Shirika la WILDAF Tanzania Dkt Judith Odunga akitoa salamu kwa niaba ya wadau katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leade’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017.
  Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki(kulia) akiteta jambo na Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(kushoto) wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika Viwanja vya Leader’s club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
  Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akisaliamiana na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017. 
  Waziri wa Madini  Mhe. Angellah Kairuki akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Balozi wa Marekani nchini Bi Inmi Patterson wakti wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017. 
  Baadhi ya wadau na wananchi wakifuatlia hotuba ya Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki(hayupo pichani) aliyemwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017. 
  Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki (watatu kushoto waliokaa )na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(katikati waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja wadau na waharakati wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leade’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017. 


  Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


  ………………………………………………………………………………

  Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

  Watanzania wametakiwa kutumia nguvu zao katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

  Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kimsingi kiwango cha ukatili wa kijinsia nchini na dunia bado ni kubwa na kwa mujibu wa Taarifa ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

  Ameongeza kuwa takwimu zinonesha kuwa asilimia 42 ya wanawake waliowahi kuolewa wamekumbana na ukatili wa wenza wao ama wa kimwili,au ukatili unaohusisha ngono.“Nawaomba watanzania wenzangu katika maeneo yenu pazeni sauti na kufanya kwa vitendo kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia unaowakumba sana wanawake na watoto” alisema Mhe. Angellah.

  Aidha kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa athari za ukatili wa kijinsia ni kubwa sana katika Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

  Ameongeza kuwa kampeni hii ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hasa ilenge kuinua uelewa wa jamii na wadau mbalimbali kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.“Kampeni hii imekuja wakati muafaka na kwakuwa tatizo la ukatili wa kijinsia hapa nchini bado ni kubwa basi itasaidia kulitatua kwa jitihada za pamoja za Wadau na Serikali” alisema Mhe. Dkt. Ndugulile.

  Naye Mkurugenzi wa WILDAF Tanzania Dkt. Judith Odunga ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wao katika kupambana na ukatili wa kijinsia na kuomba kufanyiwa kwa marekebisho ya baadhi ya Sheria ili ziende sambamba na kupinga ukatili wa kijinsia nchini.

  Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 10 na kwa mwaka 2017 Kauli mbiu inasema FUNGUKA! Ukatili Dhidi ya wanawake na Watoto haumwachi Mtu Salama: CHUKUA HATUA!

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea tuzo ya kimataifa waliyotunukiwa PSPF kama taasisi mahiri barani Afrika kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu PSPF Bw. Adam Maingu (kushoto) wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi Maendeleo ya sanaa Bibi. Leah Kihimbi akifafanua jambo wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akihamasisha wadau kuchangia ili kufanikisha usiku wa kitendawili utakaohimiza uzalendo kwa watanzania leo wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku huo Jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaonyesha wajumbe (hawapo pichani) kitabu kilichoandaliwa kuhimiza kampeni ya uzalendo na utaifa wakati wa kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam

  ya wajumbe walioshiriki katika kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha maandalizi ya usiku wa kitendawili unaolenga kuhimaza uzalendo kwa watanzania leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wapili kulia ni Mtendaji Mkuu PSPF Bw. Adam Maingu.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
  Na: Genofeva Matemu – WHUSM


  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Taasisi zake imetangaza kampeni ya kitaifa ya uzalendo ambayo wizara kwa kushirikiana na vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni imeamua kuzindua kampeni hiyo kwa ajili ya kuhimiza uzalendo na utaifa katika taifa letu.

  Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi cha uzinduzi wa kampeni ya uzalendo leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wizara inaona ni muda muafaka sasa kuonyesha njia sahihi ya kujenga nchi kwa kuhimarisha uzalendo na utaifa.

  “Mhe. Rais amesikika mara nyingi sana akitoa wito kwa watanzania kuimarisha uzalendo na utaifa, tunahitaji kutoa elimu kwa vijana ili wajue tulikotoka na tunakwenda maana vijana wengi waliozaliwa baada ya uhuru wamekua wakiuliza mara nyingi uzalendo ni nini, na vijana hawa ndio ambao tunatarajia waongoze nchi katika karne hii” amesema Mhe. Mwakyembe

  Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa watanzania kama taifa moja wanawajibu wa kurithisha kizazi cha sasa yale wanayoyajua ya nyuma ili kulihimarisha taifa kuwa moja, na lenye msimamo mmoja na ambalo litaleta faida kwa watanzania wote kwa misingi iliyojengwa na waasisi wetu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa watanzania hawana budi kuthamini nchi yetu kwa kuendeleza kauli mbiu ya kampeni ya kitaifa ya uzalendo inayosema nchi yangu kwanza.

  Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Kila mtanzania anapaswa kujiona yeye ni wakwanza katika kuhakikisha
  dhana sahihi ya uzalendo inawafikia watanzania wote na kujiweka katika nafasi ya kutambua yakuwa anakwenda kuokoa kizazi cha sasa na kizazi kijacho kwa kuhakikisha kuwa wanakuwa wazalendo, wanakua katika maadili na wanaepukana na mmomonyoko wa maadili unaoletwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

  Kampeni ya uzalendo itatanguliwa na vipindi mbalimbali kwenye redio na televisheni, makala mbalimbali, kuelezea tulikotoka, kuhamasisha utamaduni wa mtanzania, kuonyesha taifa limeegemea katika misingi ipi na kuonyesha umuhimu na ulazima wetu katika kufuata misingi hiyo.

  0 0

  Aliyekuwa Kada wa Chadema akiwa ameshika kadi na bendera za chama hicho baada ya wanachama 91 kurejea CCM katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo. 
  Wafuasi wa CCM wakifurahia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo 
  Wakili msomi Albert Msando akiunguruma kwenye mkutano huo katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo,Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana
  Katibu wa Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za CHADEMA baada ya kupokea wanachama wapya 91 waliojiunga na CCM leo katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Muriet jijini Arusha leo

  0 0


  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank,Bakari Kisuda akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa Afrika ya Mashariki (MJEA) kwa kushirikiana na kampuni ya KO Innovates zimeendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari vya Kiislamu hapa nchini.

  Mwenyekiti wa MJEA, ABUOBAKARI FAMAU,amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari wanaotoka kwenye vyombo hivyo vya habari ili waweze kuendana na mazingira ya sasa ya tasnia ya habari.

  FAMAU ameongeza kuwa vyombo vya Kiislamu vina wajibu kubwa sana kwa jamii na hivyo kuna haja ya kukumbushana juu ya wajibu huo.nae Khadijah Omar amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwakutanisha waandishi wa habari wa vyombo vya Kiislamu na kubadilishana uzoefu.

  Zaidi ya washiriki 25 wamepatiwa mafunzo hayo ambayo yatafanyika Novemba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Tangaza House jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank,Bakari Kisuda akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa Afrika ya Mashariki (MJEA)
  Waandishi wa Habari wa Mashirika ya Kislamu nchini wakifatilia hotuba ya mgeni Rasmi kwa makini

  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi Cheti mwakilishi wa Mkapa Foundation, Deogratius Rimoy, kutambua mchango wa kufanikisha mbio za 'Aids Trust Fund Marathon' za Kilometa 5, 9 na 21  zilizofanyika leo asubuhi kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, kuelekea wiki ya Siku ya Ukimwi Duniani. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi Cheti Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Teddy Mapunda, kutambua mchango wa kufanikisha mbio za 'Aids Trust Fund Marathon' za Kilometa 5, 9 na 21  zilizofanyika leo asubuhi kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, kuelekea wiki ya Siku ya Ukimwi Duniani.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akiongoza matembezi ya Kilometa tano......
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde (wa pili kuli)  akiongoza mazoezi ya viungo baada ya kumalizika mbio hizo.
   Mazoezi yakiendelea....
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  (katikati) akiongoza mazoezi.
   Mbio za Kilometa 21 zikianza...KWA PICJA ZAID BOFYA HAPA

   Washiriki wa mbio hizo wakijiandaa kuanza.....
   Mbio zikiendelea....
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi cheti mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 9, Anold Kahwa.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi cheti mshindi wa pili wa mbio za Kilometa 9, Edgar Mapunda.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi cheti mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 9, kwa upande wa wanawake, Irene Joseph.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akimkabidhi cheti mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 21, Carlson Konga.
  Washiriki wakitimua mbio


   Mafoto akishiriki matembezi ya Kilometa tano.
   Mama na mwana wakishiriki mbio za kilometa 9
   Mazoezi ya viungo
   Mazoezi ya viungo
   Picha ya pamoja .....
   Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Mabok, akiongea baada ya kumalizika mbio hizo.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde,  akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
   Picha ya pamoja
  Picha ya pamoja....

  0 0  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi katika pambano la ngumi la kimataifa lenye mizunguko kumi na mbili dhidi ya Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.
  Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliojitokeza katika pambano la ngumi la kimataifa kati ya mtanzania Ibrahim Class pamoja na Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
  Bondia Mtanzania Ibrahim Class (kushoto) akipambana na na Mwenzie kutoka Afrika Kusini Koos Sibiya katika pambano la kimataifa la ngumi lenye mizunguko kumi na mbil lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambalo mtanzania huyo alishinda.
  Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo (katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja wakifurahia pambano la ngumi kati ya mtanzania Ibrahim Class dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

  Mabondia wanawake Felicha Mashauri (mwenye kaptula nyekundu) dhidi ya Happy Daudi wakizipiga jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.


  Bondia Haidari Mchanjo akifurahia ushindi wa mizunguko sita alioupata dhidi ya Bondia Bakari Magona lililochezwa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.

  ………………………………………………………………………..

  Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

  Mwanamasumbwi Ibrahim Class amewapa raha watanzania jana Jijini Dar es Salaam baada ya kumpiga Bondia Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini katika mtanange wa kimataifa baina yao uliokuwa na mizunguko kumi na mbili.

  Katika pambano hilo lililohuzuriwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Ibrahim Class alishinda katika mzunguko wa kumi na mbili ambapo ameandika historia ya muda mrefu hapa nchini kwa mabondia kutofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

  Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema amefurahiswa sana na ushindi aliopata Ibrahim Class na kuahidi kumpa ushirirkiano zaidi ili aendelee kufanya vizuri katika mashindano mengine

  “Siri ya mafanikio katika Michezo ni kufanya mazoezi,kujiamini kusikiiza mafundisho ya mwalimu pamoja na nidhamu,Ibrahim Class ni mwanamasumbwi anaepaswa kuigwa na mabondia na wanamichezo wengine wote kutokana na uwezo wake wa kujituma hivyo wanamichezo wanapaswa kuiga kutoka kwake ili wafanikiwe na kuitangaza nchi yetu kimichezo.” Alisema Dkt. Mwakyembe.

  Naye bondia Ibrahim Class ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa wakati wa mazoezi mpaka leo amefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania na ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi kila atakapokuwa ulingoni na kushinda mataji na mikanda mingi zaidi.

  0 0

   Tabasamu Mubashara toka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania dada yetu Beatrice Singano Mallya baada ya kuhitimu na kutunukiwa nondoz yake ya Masters in Business Administration (MBA) kutoka chuo cha kimataifa cha ESAMI (The Eastern and Southern African Management Institute) ambao makao makuu yake yapo jijini Arusha Tanzania


  0 0


  Na. MWANDISHI WETU – DODOMA

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

  Ameyasema hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.

  “Ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya soko hili”.

  Kwa upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.

  “Soko hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe wote.”Alisisistiza Badwel

  Kwa upande wake mkazi wa Kigwe Bi.Anastazia Mkatato alieleza kuwa kujengwa kwa soko hilo litatatua changamoto iliyopo ya kukosa soko la kudumu kwani yaliyopo ni madogo yanayomilikiwa na watu binafsi.

  “Ninaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini iliyoamua kutujengea soko hapa Kigwe na hii itatupa nafasi ya kuuza mazao na bidhaa kwa wingi kupelekea kukuza uchumi wetu.”Alieleza Anastazia.

  Naye Mratibu wa Mradi Taifa Bw.Walter Swai alieleza kuwa soko hili ni muhimu kwa wana Kigwe na maeneo jirani , hivyo tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha vifaa vinawekwa ikiwemo Meza za kuuzia mbidhaa sokoni.

  “Tayari Ofisi yangu itachukua changamoto hii ya kukosekana kwa meza za kuuzia na kuitatua ndani ya mwezi mmoja hivyo niwaahidi kutekeleza haya.”Alisisitiza Bw.Swai

  Ujenzi wa soko la Kigwe umegharimu jumla ya zaidi ya shilingi milioni 68 ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ilitoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 50 pamoja na Mfuko wa jimbo kuchangia jumla ya shilingi Milioni 15. Dhumuni la mradi ni kuwa na eneo rasmi la kufanyia biashara na kuwezesha wajasiliamali wa Kigwe na kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleao yao.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kigwe alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la Kidwe Wilayani Bahi Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alipowalisi kukagua ujenzi wa Soko la mazao la Kigwe Lililopo Bahi Dodoma.
  Afisa Mtendaji Kata Bw. John Mchiwa akikabidhi taarifa ya Ujenzi wa Soko Kigwe kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Bahi kuona maendeleo ya ujenzi huo.
  Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa soko la Kigwe lililofadhiliwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) kwa kushirikiana na Halmashauri wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama Wilayani Bahi Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi Bi. Rachel Chuwa wakati wa ziara yake Kigwe.
  Mratibu Taifa wa Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) Bw. Walter Swai akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Kigwe walipotembelea Kijiji hicho kuona ujenzi wa soko la Kigwe unavyoendelea.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)

  0 0

  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akimkabidhi vitabu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM, Profesa Frowin Nyoni (kulia) na kukutana na baadhi ya viongozi na wahadhiri wa Chuo hicho. kushoto ni Mkuu wa Chuo Cha Sayansi ya Kijamii na Masomo ya Kibinadamu Profesa, Albino Tenge.
  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem katika picha y pamoja akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM, Profesa Frowin Nyoni (wa nne kushoto).
  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akimkabidhi kitabu Mkuu wa Chuo Cha Sayansi ya Kijamii na Masomo ya Kibinadamu Profesa, Albino Tenge kushoto na kulia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM, Profesa Frowin Nyoni.
  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akielekeza jambo mara baada ya kukabidhi vitabu kwa uongozi wa Chuo hicho.
  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika Chuo Kikuu cha UDOM

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua sehemu ya magari zaidi ya 6000 yaliyopo bandari ya Dar es salaam mengine yakiwa hapo kwa miaka zaidi ya kumi bila kuchukuliwa na wenye nayo alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo kuhusu magari zaidi ya 50 ya Jeshi la Polisi yaliyopo bandarini toka mwaka 2015 kwa sababu ya kutolipiwa  ushuru alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017

  PICHA NA IKULU


  0 0

  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) ya nchini Israel wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa watoto 20 wenye matatizo ya Moyo.

  Upasuaji huo ambao unatumia mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza tarehe 23/11/2017 na kumalizika kesho tarehe 27/11/2017. Matibabu yaliyofanyika ni ya kuziba matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo.

  Katika kambi hii tunatarajia kufanya uchunguzi wa moyo kwa watoto 100 kati ya hao watoto 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua mwakani na watoto 40 watatibiwa hapa nchini.

  Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 25 tunaamini hadi kambi itakapomalizika watoto wote hawa watakuwa wamepata matibabu. Watoto 20 waliopata matibabu wengine wameruhusiwa na waliobaki hali zao zinaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika.

  Tangu mwaka 2015 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ilianza kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart- SACH) ya nchini Israel ambapo hadi sasa jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na Taasisi hii.

  Tunawashukuru sana wenzetu hawa wa SACH kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma ya matibabu bure kwa watoto wenye matatizo ya moyo. Watoto waliotibiwa wamepona na wale ambao walikuwa wanafunzi wanaendelea na masomo yao.

  Wakati kambi hii inaendelea baadhi ya wafanyakazi wa SACH na JKCI walienda mkoani Kagera kufuatilia maendeleo ya mtoto Julius Kaijage (12) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Green Acres iliyoko Bunazi ambaye alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel mwaka 2013. Tumekuwa na tabia ya kufuatilia maendeleo ya watoto tunaowafanyia upasuaji hii inatusaidia sana kufahamu maendeleo yao.

  Aidha tunatarajia kuwa na kambi nyingine ya matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima itakayoanza kesho tarehe 27/11/2017 hadi tarehe 01/12/2017. Katika kambi hii ambayo tutashirikiana na wenzetu kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia tunatarajia kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto 13 na watu wazima 10.

  Tunawaomba wananchi waendeleee kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanahitaji kuongezewa damu wakati wanapatiwa matibabu. Kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu wanaopenda kuchangia damu tunawaomba wafike Taasisi ya Moyo iliyopo Muhimbili mkabala na Maabara kuu. Kwa maelezo zaidi wawasiliane kwa simu namba 022-2151379au 0713304149.

  Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.

  Kwa namna ya kipekee Bodi ya Udhamini, Uongozi na Wafanyakazi wote wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete tunamshukuru sana Mhe. Rais John Pombe Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa tarehe 25/11/2017 wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila kwa kutupatia jengo ambalo tutalifanya kuwa jengo la watoto.

  Kama mnavyofahamu asilimia 70 ya wagonjwa tunaowafanyia upasuaji wa kufungua kifua ni watoto, tuna jumla ya vitanda 123 kati ya hivi vitanda vya watoto ni 24 tu.

  Kuwa na jengo la watoto kutasaidia watoto kupata sehemu nzuri ya matibabu pamoja na sehemu ya kujifunza mambo mbalimbali kwani watoto wanahitaji kucheza na kujifunza. Watoto wengine wanakaa wodini muda mrefu wakisubiri matibabu, watoto hawa wakiwa na mahali pa kujifunzia wataweza hata kujifunza kusoma na kuandika.

older | 1 | .... | 1441 | 1442 | (Page 1443) | 1444 | 1445 | .... | 1897 | newer