Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1440 | 1441 | (Page 1442) | 1443 | 1444 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Jasem Al Najem leo tarehe 24 Novemba, 2017.
  Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumza masula mbalimbali kuhusu uendelezaji wa Sekta ya Madini nchini.

  Waziri Kairuki amesema kuwa mazungumzo yake na Balozi wa Kuwait yamelenga katika suala la uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ambapo ameikaribisha nchi hiyo kuja kuwekeza nchini ili kuendeleza Sekta husika.
  Aidha, ameongeza kuwa, katika kikao hicho wamezungumzia suala la kuwajengea uwezo Wataalam wa Madini nchini ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

  Vilevile wamejadiliana suala la kubadilisha uzoefu kati ya Kuwait na Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inachangia ipasavyo katika uchumi wa nchi husika.
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akiwa na Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kushoto),  katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akipokea zawadi ya Ngao kutoka kwa Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kulia),  katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam. 
  Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kulia) akimweleza Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) kuhusu alama mbalimbali zilizo katika Ngao kutoka nchini Kuwait, mara alipomtembelea katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza la wafanyakazi mjini Tanga kilichofanyika leo Ijumaa Novemba 24,2017.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, ameuagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuweka mikakati mahususi ya kiutendaji itakayosaidia kuboresha mazingira ya biashara na kukuza ajira nchini. 

  Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara ametoa agizo hilo alipokuwa akiwahutubia watumishi wa OSHA katika kikao chao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

  Shitindi alifafanua kwamba mikakati hiyo inapaswa kujikita katika kuimarisha mifumo ya kiutendaji itakayolenga katika kuboresha huduma zitolewazo kwa wateja na taasisi hiyo ya umma ili kuwaondolea usumbufu watu mbali mbali wanaofanya shughuli mbali mbali za kiuchumi hapa nchini.

  “Wakati mwingine tunashindwa kujipanga vizuri katika utekelezaji wa kazi zetu na hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa wateja. Kwa mfano unakuta mkaguzi mmoja wa Usalama na Afya mahali pa kazi anapita katika eneo fulani la kazi asubuhi na mwingine anakuja katika eneo hilo hilo mchana wakati watu hawa wangeweza kufika katika eneo la kazi kwa pamoja na kukamilisha kazi zao za kaguzi kwa wakati mmoja,” alisema Shitindi.

  Aidha Katibu Mkuu huyo aliwaasa watumishi hao kufanya kazi zao za kila siku kwa kuzingatia kanuni za maadili ya utumishi wa umma ikiwemo kujiepusha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa.

  “Maadili ya utumishi wa umma yanajumuisha mambo mengi ikiwemo mavazi stahiki, matumizi ya lugha nzuri wakati wa kuwasiliana na wateja na pia heshima baina ya watumishi na viongozi wao na miongoni mwa watumishi wenyewe,” alisema Shitindi.

  Vikao vya baraza la wafanyakazi wa OSHA ambavyo hufanyika kwa mwaka mara mbili vina lengo la kutoa fursa kwa wafanyakazi kujadiliana mambo mbali mbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuleta ufanisi zaidi.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza la wafanyakazi mjini Tanga.
  Watumishi wa OSHA wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Eric Shitindi, wakati wa kikao chao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  Watumishi wa OSHA wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Eric Shitindi, wakati wa kikao chao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya OSHA nje ya ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara alikuwa Mgeni Rasmi katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa Wakala huo.
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa OSHA nje ya ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani katika hafla ya kukabidhi mashine mbalimbali kwa vikundi vya wajasiriamali.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa wajasiriamali.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Dodoma wakati akikabidhi mashine kwa wajasiriamali Dodoma
  Wananchi waliohudhuria katika makabidhiano ya mashine
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa wajasiriamali.
  Mashine zilizokabidhiwa kwa vikundi vya wajasiriamali  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde leo amekabidhi mashine mbalimbali kwa wajasiriamali wa vikundi 31 na kuwataka kuhakikisha wanazitumia kwa kujiongezea kipato na kuenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa Viwanda.

  Akizungumza na wanavikundi hao na wakazi wa Dodoma, Mavunde amesema mashine hizo zimenunuliwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo na kwamba dhamira yake ni kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi kwa kubadili maisha yao.

  “Leo Tumegawa mashine hizi mkazitumie zibadilishe maisha yenu msizifungie stoo zikajaa vumbi na msipozitumia kwa malengo yaliyokusudiwa hamuwezi kufikia malengo yenu,Mashine hizi zikaunge mkono falsafa ya Rais ya uanzishaji wa viwanda ili kufikia uchumi wa viwanda,”amesema Mavunde

  Hata hivyo amewahakikisha kuwa amejipanga kuhakikisha anawakwamua wananchi wake kiuchumi kupitia fursa mbalimbali na kwamba anakuja na mradi wa kuchimba mabwawa ya kufugia samaki.

  “Kuna teknolojia imekuja ya kufuga samaki ambayo unaweza kufuga nyumbani, hiyo ndo mipango ya ofisi ya Mbunge ya kuwawezesha wananchi kiuchumi na pia kwa upande wa kilimo nimetafuta wataalamu kutoka India tunaangalia eneo la Nzasa kulitumia kwa majaribio ya kilimo cha mboga mboga na ufugaji samaki,”amesema

  Mavunde amesema dhamira yake ni kuwafanya wananchi wa Dodoma wanufaike na ujio wa serikali mkoani humo kupitia fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

  Akizungumzia kuhusu kilimo cha Zabibu, Mavunde amewataka kuchangamkia fursa ya kilimo cha zabibu kwa kuwa ni fursa pekee ya kuikwamua kiuchumi Dodoma ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa viwanda vidogo vya kukamua mchuzi wa zabibu.

  “Maana kwasasa utambulisho wa Dodoma ni ombaomba na wavivu badala ya kutambulika kwa kilimo cha zabibu, ndugu zangu duniani kote Dodoma ni miongoni mwa maeneo yanayovuna zabibu kwa mwaka mara mbili ni vyema tukatilia mkazo kilimo hichi ili kuwa utambulisho wetu,”amesema

  Mbunge huyo amesema kupitia mshahara wake anatarajia kununua mashine za kukamua mchuzi wa zabibu kutoka nchini Canada kwa kila kata kwa kuwa mchuzi huo una soko kubwa.Amewahamasisha wananchi kupitia vikundi walivyo navyo kuendelea kuwasilisha maombi yao na Ofisi ya Mbunge itaendelea kununua mashine kwa awamu.

  Naye, Mwakilishi wa Umoja wa wajasiriamali Silvesta Wambura amemshukuru Mbunge huyo kwa dhamira yake ya kuwainua kiuchumi na kudai kuwa amekuwa mkombozi wa wanadodoma.Amesema Mbunge huyo ni chombo sahihi na mwenye ubinadamu na wananchi wana matarajio makubwa kupitia yeye.

  Kwa upande wao, madiwani wa kata za jimbo hilo wamempongeza na kumshukuru Mavunde kwa dhamira yake ya kuwakwamua wananchi kiuchumi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba leo akiongea na Wanachama wa Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) amesema Wizara inaendelea na jitihada za kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo hadi sasa tayari baadhi ya nchi wanachama zimeshaweka lugha ya Kiswahili katika mitaala ya Elimu katika shule za Msingi na Sekondari hatua ambayo itawezesha kuongeza wigo wa matumizi ya lugha hii katika Jumuiya yetu.

  Mhe. Dkt Kolimba akizungumza katika kongamano hilo amewapongeza Viongozi na Wanachama wa Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki kwa kuwahusisha baadhi ya Ofisi za Balozi zilipo nchini katika hatua za kufanikisha Kongamono hilo. Kwa namna ya pekee alitumia fursa hiyo kumpongeza Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jaseem Al Najem na Watumishi wa Ubalozi huo kwa kukubamwaliko wa kushiriki Kongamano na kwa mchango waliotoa kufanikisha Kongamano hilo.

  Tokea mwaka 2004 hadi sasa Kiswahili kimekuwa lugha ya kwanza ya Afrika kutumika katika vikao vya Ngazi ya Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, hii ni kufuatia jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Jitihada hizo ilikuwa ni pamoja na kugharamia wakalimani kwa fedha za ndani, na mwaka 2008 Wizara iliishawishi Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuchukua jukumu hilo.

  Aidha Mhe. Dkt. Kolimba amewahakikishia Viongozi na Wanachama wa CHAKAMA kuwa nia ya Serikali ya kufungua vituo vya kufundishia lugha ya kiswahili sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya Tanzania bado iko palepale, "tayari tulishafungua kituo kimoja mwaka 2012 katika Ofisi za Kamisheni ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia" amesema Mhe. Dkt. Kolimba.

  CHAKAMA imehitimisha Kongamano lake leo lililofanyika kwa muda wa siku mbili mjini Dodoma ,likiwa na kauli mbiu ya "Kiswahili na Maendeleo ya Afrika Mashariki" chama hiki kinaundwa na nchi Wanchama za Jumuiya ya Afrika pia kinahusisha wanachama kutoka nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Ghana na Zimbabwe.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akihutubia washiriki wa kongamano la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki lililofanyika katika Hoteli ya African Dream mjini Dodoma 
  Naibu Waziri Mhe.Dkt. Susan Kolimba akimkabithi cheti cha ushiriki mmoja wa wajumbe wa Kongamo la CHAKAMA 
  Naibu Waziri Mhe.Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kongamano

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu akimkabidhi kadi ya bima ya afya, Irene Paul kwa niaba ya watoto wenzanke 139 ambao wanaishi katika mazingira magumu. Kadi hizo zimetolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na mfuko wa Abbott na benki ya ABC. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa benki ya ABC, Joyce Malai, Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Kurasini, Rabikira Mushi na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Miradi Endelevu wa Mfuko wa Abbott, Dkt. Festo Kayandabila na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa hospitali hiyo, Dkt. Juma Mfinanga.
  Baadhi ya walezi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakishuhudia jinsi watoto hao wanavyokabidhiwa kadi za bima ya afya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
  Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza kabla ya kukabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
  Baadhi ya watoto waliokabidhiwa kadi za bima ya afya na Waziri wa Afya wakionyesha kadi hizo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Muhimbili leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza faida za watoto hao kupatiwa kadi hizo.
  Baadhi ya wataalamu wa afya wa Muhimbili wakiwa kwenye mkutano huo leo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya ABC wakishuhudia shughuli ya kukabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto hao leo

  ……………

  Serikali ameipa siku 60 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuandaa mpango utakaowawezesha wateja wa hiari kulipia fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kupata kadi ya bima ya afya.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu kabla ya kukabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto 139 wanaoishi katika mazingira magumu. Kazi hizo zimetolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Mfuko wa Abbott na Benki ABC.

  Waziri Ummy Mwalimu ameuagiza mfuko wa NHIF kuhakikisha ndani ya siku 60 inaweka utaratibu ambao utasaidia wateja wa hiari wanapata kadi za bima ya afya ndani ya muda mfupi kwa kuwa wengi wao hawana fedha taslimu Sh 50,400 za kulipia kwa wakati mmoja.

  “Natoa siku 60 kwa NHIF kuhakikisha inaweka utaratibu wa kuwawezesha watu kupata kadi ya bima ya afya kwa kulipa fedha kidogo, kidogo kwa mfano mteja wa hiari anaweza kulipia Sh 5,000 au Sh 10,000 hadi atakapokuwa amefikisha Sh50,400 ambayo inatakiwa na NHIF,” alisema waziri huyo.

  Katika hatua nyingine, serikali imeipongeza Muhimbili kutokana na juhudi za kuwawezesha wananchi kupata huduma bora ikiwamo kuwapatia kadi za bima ya afya watoto 139 wanaoishi katika mazingira magumu.Waziri huyo amesema uamuzi wa Muhimbili kutoa kadi kwa watoto hao ni mfano wa kuigwa na kwamba unapaswa kuigwa na taasisi nyingine nchini.

  “Naamini mpango huu, utawaamsha wazazi, walezi na wadau wengine wa afya ili kuhakikisha kwamba watoto wa Taifa hili wanakuwa na bima za Afya mara tu baada ya kuzaliwa,” amesema.

  Naye Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema Muhimbili kwa kushirikiana mfuko wa Abbot na Benki ABC imewezesha watoto hao kupata kadi ya bima ya afya ili waweze kupata matibabu popote pale watakapokwenda nchini.“Muhimbili imekuwa ikitekeleza jukumu lake kikamilifu la kutoa huduma bure kwa wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kuchangia huduma kwa kiasi Sh milioni 500 hadi 600 kwa mwezi sawa na Sh. bilioni 6 hadi 7.2 kwa mwaka,” amesema Profesa Museru.

  Profesa Museru amesema kadi hizo zitapunguza mzigo mzito kwa vituo vya kutunzia watoto ambavyo vimekuwa vikigharamia huduma za Afya kwa kutumia fedha taslimu pale watoto hao wanapougua.

  “Mheshimiwa Waziri, nitoe rai kwa wenzetu NHIF kuangalia namna ambavyo huduma kwa kundi hili la watoto itaendelea kuwafikiaw ahitaji wengi ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa na uhakika wa kuzifikia huduma za afya popote pale,” amesema mkurugenzi huyo.

  Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dkt. Juma Mfinanga amesema kutokana na uboreshaji uliofanywa na idara hiyo hivi sasa wanapokea wastani wa wagonjwa mahututi wapatao 200 hadi 250 kwa siku na kuwapatia huduma ya afya.

  “Utafiti uliofanyika Muhimbili na kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya kimataifa unaonyesha kuwa idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali imepunguza vifo MNH kwa zaidi ya asilimia 5 kutoka asilimia 13 kabla ya kuanzishwa kwa idara hiyo hadi asilimia 8 baada kunzishwa,” amesema Dkt Juma.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji wa kihistoria wa kupandikiza figo ambao umefanyika Novemba 21, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni mara ya kwanza upasuaji huo kufanyika nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Lawrence Museru, Dkt. Rajesh Pande, Dkt Sunil na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya figo Muhimbili, Dkt. Jacqueline Shoo wakiwa kwenye mkutano huo leo.
  Wataalamu wa figo wa Muhimbili ambao wameshiriki katika upasuaji huo wa kihistoria wakiwa kwenye mkutano huo leo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Dkt. Rajesh Pande na Dkt Sunil wakifuatilia mkutano huo.

  Baadhi ya wataalamu wa magonjwa ya figo kutoka India wakiwa kwenye mkutano huo leo
  Baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili na wataalamu wakifuatilia mkutano huo.
  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya na wafanyakazi wa hospitali hiyo. PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Hospitali ya BLK ya New Delhi, India imefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria wa kupandikiza figo (Renal Transplant) ikiwa ni mara ya kwanza nchini.

  Upandikizaji wa figo umefanywa na madaktari bingwa wa Mhimbili na Hospitali ya BLK Novemba 21, mwaka huu na taarifa za wataalamu hao zimeeleza upasuaji huo umekuwa wa mafanikio makubwa na kwamba utakuwa endelevu.

  Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kufanyika kwa upasuaji huo ni moja ya mkakati wa Serikali wa kuendelea kuboresha na kuanzisha huduma bora za kibingwa nchini.

  “Serikali inaendelea na juhudi za kuboresha huduma za afya nchini chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli zikiwamo za kibingwa nchini na kupunguza rufaa za wagonjwa wanaohitaji huduma hizo nje ya nchi,” amesema Ummy Mwalimu.

  Amesema upasuaji figo katika Hospitali ya Muhimbili utasaidia kupunguza gharama kubwa ambazo serikali imekuwa ikitumia kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

  Waziri huyo amesema hivi sasa kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo na kwamba takwimu zinaonesha Muhimbili kuna wagonjwa 200 wanaofanyiwa huduma ya utakasishaji damu.

  Amesema kutokana na ongezeko hilo, Serikali imeanzisha vituo vya utakasishaji damu katika hospitali za Mbeya Rufaa, Benjamin Mkapa, KCMC, Bugando na hospitali binafsi zikiwamo Kairuki, TMJ, Regency na Hindu Mandal.

  “Kwa namna ya pekee nawashukuru wataalamu 11 ambao tupo nao hapa wakiongozwa na Profesa. H.S. Batyal, Dkt. Sunil Prakash, Dkt. Rajesh Kumar Pande na Dkt. Anil Handoo ambao kwa kushirikiana na wataalamu wetu wamefanikisha upasuaji huu. Pia, napenda kuwashukuru wakurugenzi, wataalamu pamoja na Wafanyakazi wote wa Muhimbili wakiongozwa na Prof. Lawrence Museru,” amesema.

  Naye Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema kuwa mpango wa kupandikiza figo umewezeshwa na hospitali hiyo ikiwa ni utekelezaji wa mikakati ya kuboresha huduma za afya nchini.

  Profesa Museru amesema awali ilipeleka India wataalamu kwa ajili ya kupata mafunzo ya kutekeleza mradi huo na kwamba umekuwa wa mafanikio makubwa nchini Tanzania.

  Mkurugenzi huyo amesema mpango huo utasaidia kupunguza gharama kwa wagonjwa waliokuwa wanapelekewa nje kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya figo.

  Profesa Museru amesema upandikizaji wa figo ambao unajumuisha kumuandaa mgonjwa, vipimo mbalimbali vinavyohitajika kwa mpokeaji na mtoaji figo unagharimu wastani wa Sh. 21 milioni za kitanzania katika hospitali hiyo ya Muhimbili.

  “Hii ni nafuu sana ukilinganisha na gharama ya Sh.80 hadi 100 milioni iliyokuwa ikitumiwa na Serikali kupeleka mgonjwa mmoja nje kwa huduma hii ikiwamo matibabu, usafiri na malazi. Hivyo basi, licha ya huduma hii kusaidia kuleta huduma za kisasa nchini pia, itakuwa ni nafuu sana na kuwezesha wagonjwa wengi zaidi kupatiwa huduma hiyo,”amesema Profesa Museru.

  Mkurugenzi huyo amesema kuwa mafanikio ya upasuaji huo utasaidia kuweka msingi wa kuanzisha programu nyingine za upandikizaji viungo (organ transplant) hapa nchini kama vile upandikizaji wa ini (liver transplant).

  “Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wataalamu kutoka Hospitali ya BLK New Delhi, India ambao wameshirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa zaidi ya mwaka mmoja katika mipango na maandalizi ya utoaji wa huduma ya upandikizaji figo. Kwa namna ya pekee nawashukuru hawa wataalamu 11 ambao tupo nao hapa wakiongozwa na Profesa H.S. Batyal, Dkt. Sunil Prakash, Dkt. Rajesh Kumar Pande na Dkt. Anil Handoo ambao kwa kushirikiana na wataalamu wetu wamefanikisha upasuaji huu,” amesema Profesa Museru.

  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kulia) akizungumza wakati wa kuwapima uzita mabodia Ibrahimu Class wa Tanzania na Koo’s Sebiya wa Afrika ya Kusini wanaotarajia kupambana kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
  Bondia Ibrahimu Class wa Tanzania akipima uzito kabla ya pambano la kimataifa la ngumi linalotarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam dhidi ya bodia Koo’s Sebiya wa Afrika ya Kusini leo Jijini Dar es Salaam
  Bondia Koo’s Sebiya wa Afrika ya Kusini akipima uzito kabla ya pambano la kimataifa la ngumi linalotarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam dhidi ya bodia Ibrahimu Class wa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam
  Bondia Ibrahimu Class wa Tanzania (kulia) akionyeshana uwezo na bondia Koo’s Sebiya wa Afrika ya Kusini (kushoto) baada ya kupima uzito tayari kwa kushiriki katika pambano la kimataifa la ngumi litakalofanyika kesho katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
  Bondia Ibrahimu Class wa Tanzania (kulia) akimkabidhi kitabu kinachoonyesha vivutio tulivyonavyo Tanzania bondia Koo’s Sebiya wa Afrika ya Kusini (kushoto) baada ya kupima uzito tayari kwa kushiriki katika pambano la kimataifa la ngumi litakalofanyika kesho katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
  Mabondia Ibrahim Maukola (kushoto) na Ibrahim Tamba (kulia) wakionyesha uwezo wao baada ya kupima uzito kwa ajili ya kuonyesha pambano la ngumi kati yao kabla ya pambano la kimataifa kati ya Bondia Ibrahimu Class wa Tanzania na Bondia Koo’s Sebiya wa Afrika ya Kusini litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya mabondia watakaopambana kabla ya pambano la ngumi la kimataifa kati ya Bondia Ibrahimu Class wa Tanzania na Bondia Koo’s Sebiya wa Afrika ya Kusini litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

  0 0

  Na David John

  BAADHI ya wanachama wa Shirikisho la waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) wamewajia juu viongozi wa Shirikisho huku wakihoji uhalali wao wa kuendelea kufanya kazi.

  Wamesema kuwa viongozi hao muda wao wa kuongoza ulishapita na wanachama walishatoa msimamo wa kuwataka kujiudhuru ili kupisha kufanyika kwa uchaguzi mwaka kesho.

  Akizungumza kwa niaba ya wezake mmoja wa wanachama hao Rajabu Hassan amesema wamepata taarifa kwamba kuna baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo wamekwenda mjini Dodoma kusimamia uchaguzi wa shirikisho vyama kwa ngazi ya mkoa kinyume cha taratibu.

  Amesema maamuzi ya Halmashauri kuu ya shirikisho hilo ilikuwa kuwa chaguzi zote ambazo zitafanyika ngazi za wilaya na mikoa zisimamiwe na wajumbe wa halmashauri kuu na si viongozi wakuu na hiyo nikutokana wao walipewa kuendesha shirikisho kwa muda ambapo muda wao umekwisha kimsingi.

  “unajuwa ndugu mwandishi kimsingi viongoza hawa hawana Sifa na kinachosubiliwa na mkutano mkuu na Hata hivyo mwenyekiti anakwenda yeye pekee yake kinyume na katiba kwani kila kitu anakwenda kufanya yeye. “Amesema Hassan

  Nakuongeza kuwa pia mwenyekiti huyo amekuwa mbabe kwani ikitokea mwanachama anahoji jambo basi anatishia kumfutia uwanachama pamoja na kumuondoa kwenye makundi yao ya mawasiliano.

  Naye mwanachama mwingine kwa sharti la kutotaja jina lake amesema wanajuwa mchezo unaofanyika na viongozi hao nikutaka kujitengenezea mazingira ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu ujao uliopangwa kufanyika ndani ya shirikisho hilo mwakani.

  Mmoja wa wataalamu wa Tiba hiyo ya dawa asili nchini akizungumzia hatua ya viongozi hao kuendelea kufanya kazi amesema kimsingi hadi sasa hakuna shirikisho na linasemewa mtaani tu.

  ” Kisheria hakuna chombo kinachoitwa shirikisho kwani uhalali wake ulishapita na hata kinachofanyika ndani ya shirikisho kwa sasa ni batili. “amesema.

  Kwaupande wake Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili nchini Richrd Kayombo amesema mambo yanayoendelea ndani ya shirikisho hilo ni ya kwao wao kama Baraza wanafanya kazi na mganga mmoja mmoja.

  Awali waliwataka watengeneze chombo kitakachowazungumzia mambo yao lakini mambo yanayofanyika wanajuwa wenyewe.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho hilo Abdallahman Lutenga amewataka wanachama wake kutambua kuwa shirikisho ni mahala patakatifu hakuna mchwa wala nani atakayeingia hapo.

  Amesem yeye anamamlaka ya kusimamia chaguzi kwani ndio rais wa shirikisho lakini ndio anaye teua na kuitisha mikutano ya shirikisho hilo.

  ” Nataka nikuambie kwanza wakati mwingine muwe mnauliza kwanza huko chini kabla ya kuja kwangu kwani mimi ni kiongozi mkubwa na nina kazi nyingi na anatambulika na Serikali. “amesema
  Hassan Rajabu mmoja mwanachama wa shirikisho la vyama vya waganga wa tiba asili Tanzani.

  0 0

  Meza Kuu wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) wakiimba Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika Nyanja za Fedha, Uhasibu, Bima, TEHAMA na Hifadhi ya Jamii. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Lettice Rutashobya na wa Pili kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tadeo Satta.
  Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof. Tadeo Satta, akihutubia wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
  Mwenyekii wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof. Lettice Rutashobya, akihutubia wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
  Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa mahafali hayo ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, Dkt. Philip Isdor Mpango Mb), akihutubia Jumuiya ya wanachuo hicho ambapo aliwatunuku vyeti wanafunzi 2692 waliohitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
  Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakipokea zawadi ya hundi kifani yenye thamani ya shilingi 1,200,000 ambayo ni sehemu ya zawadi lukuki walizopewa wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam.
  Mhitimu Bi. Elizabeth Mnzava akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) baada ya kufanya vizuri katika masomo yake.
  Sehemu ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, wakinyanyua juu kofia zao kwa furaha kuashiria kumaliza sehemu ya safari yao ya kimasomo, baada ya kutunukiwa vyeti na shahada nyingine mbalimbali, katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa wahitimu ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akionesha furaha isiyo kifani baada ya kutunukiwa Shahada yake baada ya kuhitimu masomo katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
  Sehemu ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, wakinyanyua kofia zao juu kwa furaha baada ya kutunukiwa shahada zao wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


  Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewaonya wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kuacha tamaa ya kutaka kupata mali za haraka haraka na kutojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi wawapo kazini ili waweze kuisadia nchi kufikia maendeleo ya haraka.

  Dokta Mpango aliyasema hayo wakati akiwatunuku vyeti vya kozi mbalimbali wahitimu 2692 wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, wakati wa mahafali ya 43 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa moja ya changamoto zinazoikabili jamii hivi sasa ni mmomonyoko wa maadili katika utumishi wa Umma hali iliyosababishwa na suala la rushwa na ufisadi kuota mizizi na kuwa tatizo kubwa katika jamii.

  “Katika miaka ya karibuni kumekuwa na matatizo mengi ya matumizi mabaya ya fedha za umma ikiwemo watumishi hewa, wanafunzi hewa na pembejeo hewa, nawataka wahitimu mkafanyekazi zenu kwa kuzingatia maadili na kuepuka tabia ya kutaka utajiri wa harakaharaka” Alisisitiza Dkt. Mpango.

  Dkt. Mpango alitumia fursa hiyo pia kuelezea mafanikio makubwa yaliofikiwa nchini katika sekta ya fedha katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma, mikopo ya mitaji ya kuwekeza katika Sekta mbalimbali na kuhakikisha kuwa sekta hiyo inabaki imara.

  Alisema kuwa kutokana na hatua hizo, idadi ya taasisi za fedha imeongezeka kutoka 31 zilizokuwepo mwaka 1999 hadi kufikia 67 Novemba mwaka 2017 huku taasisi hizo zikiwafikia watu wengi zaidi hadi pembezoni mwa miji hata vijijini.

  “Sekta ya Bima nayo imepiga hatua ambapo kampuni zilizosajiliwa zimefika 31, wakala wa bima 124 kutoka wakala 1 iliyokuwepo miaka ya 70 huku ukwasi katika kampuni hizo ukiongezeka kutoka asilimia 47.1 mwezo Juni 2016 hadi kufikia asilimia 49.8 mwezi Juni, 2017.

  Alisema kuwa licha ya mafanikio hayo, taasisi za fedha zimekuwa zikiathiriwa na uwepo wa mikopo chechefu iliyoongezeka hadi kufikia asilimia 10.74 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 9.07 mwaka 2016 na kutoa wito kwa wahitimu hao kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto kama hizo na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kwa kuzingatia mahitaji ya Taifa ili kuondokana na umasikini.

  Aidha, Dokta Mpango alisema kuwa Serikali itaendelea kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wenye uhitaji ambapo katika Bajeti ya Mwaka huu, imepanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni 427.54 kwa kazi hiyo kwa kuwalipia ada na gharama nyingine za masomo wanafunzi 122,623.

  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM Prof. Lettice Rutashobya ameiomba Serikali kukisaidia Chuo hicho kwa kukipatia fedha ili kiweze kujiimarisha na kuendelea kutoa taaluma bora ya masuala ya fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na Hifadhi ya jamii huku Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tadeo Satta akisema kuwa chuo hicho kimejipanga kujenga kampasi mkoani Pwani na mkoani Dodoma ikiwa ni mikakati ya kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi.

  Aidha viongozi hao wa Chuo cha IFM waliiomba Serikali kutenga shilingi bilioni 2 kila mwaka katika Bajeti ya Serikali ili waweze kuzitumia kujenga kampasi hizo mbili, moja katika eneo la Msata mkoani Pwani na nyingine inayotarajiwa kujengwa mkoani Dodoma.

  “Katika hatua za awali wakati tunataka kutumia eneo la ekari 50 tulilolipata mkoani Dodoma, Chuo kimepanga kuanza kutoa mafunzo ya shahada ya uzamili katika fani ya fedha na uwekezaji kwa kutumia miundobinu ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini mkoani Dodoma.

  Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kilianzishwa mwaka 1972 kikianza na kozi mbili na kutoa wanafunzi 75 lakini hivi sasa chuo hicho kinatoa kozi 23 ambapo mwaka huu wahitimu 2692 wamemaliza masomo yao.

  0 0

   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wanaotoa huduma za maji nchini leo kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini Tanga
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Proffessa Kitila Mkumbo akizungumza katika mkutano huo
   Mwenyekiti wa ATAWAS,Mhandisi Mkama Manyama Bwire akizungumza katika mkutano huo
   Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kulia katikati Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Proffessa Kitila Mkumbo kushoto ni Mwenyekiti wa ATAWAS Mhandisi Mkama Manyama Bwire wakifuatilia mkutano huo
   Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kulia katikati Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Proffessa Kitila Mkumbo kushoto ni Mwenyekiti wa ATAWAS Mhandisi Mkama Manyama Bwire wakifuatilia mkutano huo
   Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa anayehamia Mkoani Shinyanga akifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Isack Kamwelwe.
  Afisa Mtendaji Mkuu DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja kulia akiwa kwenye mkutano huo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Jijini Tanga
   Sehemu wa wajumbe  wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Isack Kamwelwe leo wakati akiufungua uliofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga
   Mmmoja kati ya washiriki wa kikao hicho akijitambulisha kabla ya kuanza mkutano huo
   Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akijitambulisha kabla ya kuanza
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Proffessa Kitila Mkumbo kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga.
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kulia akiteta jambo na mmoja wa wadau wa mkutano huo mara baada ya kupiga picha ya pamoja
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe katikati akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa mara baada ya kufungua mkutano huo kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Athumani Shariff
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo unaofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (wapili kushoto waliokaa) pamoja na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (katikati waliokaa) wakisaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Waliosimama katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
  Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (kulia) akikabidhiana mkataba na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

  Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi wa Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga akielezea namna kampuni hiyo itakavyohifadhi data za wanatasnia ya filamu wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akifafanua jambo wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam

  Na: Genofeva Matemu – WHUSM

  Wadau wa tasnia ya filamu nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiunga katika vyama vilivyopo chini ya Shirikisho la filamu ili waweze kuingia katika mpango wa Kanzi Data inayolenga kuhifadhi taarifa za wasanii na kuinua maslahi ya tasnia kupitia tuzo na mashindano mbalimbali yatakayoandaliwa.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe wakati wa kusaini mkataba wa kanzi data itakayohifadhi taarifa za wasanii wa filamu kati ya Kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.

  “Ni wajibu wetu kuhamasisha wadau wa tasnia ya filamu kuingia katika mfumo wa kanzi data kwani mpango huu umedhamiria kuboresha na kuendeleza maslahi ya tasnia ya filamu na kuleta maendeleo ya msanii mmoja mmoja” amesema Mhe. Mwakyembe

  Awali Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa tasnia ya filamu imekua ikikosa fursa nyingi kutokana na wadau kutokua katika kanzi data inayowatambua vizuri hivyo ujio wa kanzi data hii utakua mkombozi kwa tasnia.

  Bibi. Fissoo amesema kuwa suala la kanzi data limilikiwe na wadau wote kwa kupata uelewa na kila litakalofanyika katika kanzi data hiyo lifanywe kwa maslahi ya sekta ya filamu kwani filamu ni uchumi, filamu ni ajira na filamu ni kwa maendeleo endelevu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga amesema kuwa kampuni yake inaingia mkataba wa kuunda kanzi data ya wanatasnia ya filamu na shirikisho la filamu kwa ajili ya kuongeza msukumo wa kuifanya tasnia ya filamu kukua na kuendelea kwa kasi zaidi.Aidha Bw. Mwasaga amesema kuwa kanzi data hiyo itasaidia kujua mapato yanayopatikana kupitia kazi za filamu lakini pia namna tasnia ya filamu inavyochangia katika pato la taifa.

  Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amesema kuwa mchakato wa kufanikisha kanzi data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu unahitaji wanachama wasiopungua laki tano kwa kuanzia, na wanachama hao ni lazima wawe ndani ya vyama vilivyopo chini ya shirikisho la filamu huku kila mwanachama atakayekuwepo katika kanzi data hiyo atatakiwa kuchangia shilingi elfu moja kwa kila mwezi.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambao walifika katika mkoa huo kwa ajili ya kumjulia hali na kufuatilia maendeleo ya elimu ya mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa Moyo nchini humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwa katika kikao na wafanyakazi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambao walifika katika mkoa huo kwa ajili ya kumjulia hali na kufuatilia maendeleo ya elimu ya mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa Moyo nchini humo.
  Mama Judy Shore kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambaye anaishi nchini Marekani wakizungumza jambo na mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Mama Shore aliamua kuja nchini kumjulia hali mtoto Julius baada ya kupata taarifa za kupona kwake ugonjwa wa moyo.
  Mama Judy Shore na Tamar Shapira kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel wakizungumza jambo na mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini humo. Wafanyakazi wa SACH walitembelea mkoa wa Kagera kwa ajili ya kumjulia hali mtoto huyo.
  Tamar Shapira kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel akipokea zawadi ya kitenge kutoka kwa mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini humo. Wafanyakazi wa SACH walitembelea mkoa wa Kagera kwa ajili ya kumjulia hali mtoto huyo.Picha na JKCI

  0 0  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho. Kushoto ni Ofisa Habari wa TAMWA, Happines Bagambi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho. Kulia ni Afisa Mipango wa TAMWA, Strategic Manager.
  Baadhi ya wanahabari na wasaidizi wa sheria ngazi za jamii wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga katika mkutano huo.
  aadhi ya wanahabari na wasaidizi wa sheria ngazi za jamii wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga katika mkutano huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho.
  Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo (kulia) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari katika mkutano huo.


  CHAMA cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kimebaini kuwa matukio ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho, kwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ubakaji kuwa bado ni changamoto, kwa kile kuendelea kushamiri ndani ya jamii.

  Kwa mujibu wa taarifa ya TAMWA iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga amesema Kitengo cha Usuluhishi, CRC cha TAMWA kuanzia mwezi Januari hadi Agosti 2017 kimepokea kesi za ukatili wa kijinsia hasa ubakaji 57 tofauti na ilivyokuwa mwaka jana kwa kipindi hicho kupokewa kesi 9 tu.

  Bi. Sanga alisema hali hiyo ya ongezeko inashamiriana na taarifa ya utendaji kazi ya Kituo cha One Stop Centre cha Hospitali ya Amana, Dar es Salaam ambapo imeonyesha kiwango cha matukio ya ubakaji kwa mwaka huu kiko juu kwa idadi ya watoto 141 waliochini ya miaka 18, huku watu wazima matukio kama hayo yakiwa ni 27 tu.

  Alifafanua kuwa kuanzia Julai 2016 hadi Juni 2017 kituo hicho kilipokea jumla ya 420 huku matukio ya watoto yakifikia 316 sawa na asilimia 75 na watu wazima wakiwa 104 sawa na asilimia 25 ya ukatili wa kijinsia.

  "...Taarifa hiyo imeonesha idadi ya waliolawitiwa na kuripoti katika kituo hicho ni 44 sawa na asilimia 10.47 kati ya hao watoto ni 39 ukilinganisha na watu wazima ambao ni 5 kwa mwaka. Hali hii ya ukatili iko juu sana kwani watoto waliofanyiwa vitendo hivi wana uwezekano mkubwa wa kufanyia wengine katika kipindi cha makuzi yao.

  Hata hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA, Bi. Sanga aliongeza kuwa jukumu la ulinzi na malezi bora kwa watoto ni la jamii nzima wakiwemo marafiki, wazazi, ndugu, walezi, majirani na viongozi wakishirikiana na Serikali kuboresha na kusimamia utekelezaji wa sera na kubadilisha sheria kandamizi ili wahusika wa ukatili huu hasa kwa watoto wa kike wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

  Siku 16 ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayoongozwa na kituo cha Kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991 kutokana na mauaji ya kinyama ya akinadada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica 1960, Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Funguka! Ukatili dhidi ya wanawake na watoto haumuachi mtu salama. Chukua Hatua'

  0 0


  Mkuu wa chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Abu Mvungi(wa
  pili toka kulia) akizindua Jarida la kitaaluma liloandaliwa na idara ya
  taaluma ya chuo cha Ustawi wa jamii,wa tatu kulia ni Makamu Mkuu wa chuo utawala Dkt.Zena Mabeyo akifuatiwa na mtoa Mada mkuu kwenye kongamano hilo Bw. Kabeho Solo.
  Toka kushoto Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt.Abu Mvungi,Mtoa mada mkuu Mr. Kabeho solo na Makamu Mkuu wa chuo Utawala Dkt.Zena Mabeyo wakimkabidhi cheti Agneta Ishengoma mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwenye masomo kati ya wahitimu wa mwaka huu 2017 kwenye
  kongamano la kitaaluma chuoni hapo.
  Mtoa mada Mkuu Bw Kabeho solo akiongoza mjadala kwenye kongamano hilo lililo hudhuriwa na wahadhiri na alumni wa chuo cha Ustawi
  wa Jamii.

  0 0

  Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile(katikati)akiongea na Viongozi na Watendaji wa Afya Afya Mkoa na Wilaya ya Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao na vyeti kwa vituo vya afya vilivyo na ubora wa huduma za afya.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Evod Mmanda na kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Wedson Sichalwe
  Mkuu wa Wilaya MHE.Evod Mmanda akiongea wakati wa mkutano huo
  Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed akielezea tathimini ilivyofanyika katika Mkoa huo mwaka 2016 na Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Kuibuka mshindi kwa kupata ngao na cheti
  Dkt.Ndugulile akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dkt.Furaha Mwakafyila Ngao baada ya kuibuka mshindi wa Huduma za afya katika vituo vya afya
  Afisa Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Salumu Palango akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wake baada ya kupokea ngao


  Naibu Waziri akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuibuka mshindi.Dkt.Ndugulile aliipongeza Wilaya hiyo kwa mpangilio mzuri wa utoaji huduma pamoja na utunzaji wa kumbukumbu kwenye stoo ya dawa katika kituo cha afya cha Mtambaswala ambacho kimeanza miezi miwili iliyopita lakini kimeonyesha ufanisi wa hali ya juu.
  Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri kutoa ngao na vyeti kwa washindi kwa Mkoa wa Mtwara
  Dkt.Ndugulile akisoma taarifa ya dawa katika Zahanati ya Ziwani iliyopo Manispaa ya Mtwara,ambapo Naibu Waziri huyo alichukizwa hali ya miundombinu na uwajibikaji wa Zahanati hiyo na kuwapa miezi miwili wawe wamefanya marekebisho kama walivyoelekezwa.
  Mkuu wa Zahanati ya Shangani akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya  Na.WAMJW,Mtwara

  Serikali inatarajia kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora wa kutoa huduma za afya ili mwananchi wajue kituo atakachoenda kina ubora gani wa huduma hivyo nchini

  Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiongea na Viongozi na Watendaji wa afya wa Mkoa na Wilaya zake kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao kwa wilaya iliyofanya vizuri na vituo vya afya vilivyofanya vizuri wakati wa zoezi la tathimini ya kutoa nyota kwa vituo vya kutolea huduma za afya.

  Dkt.Ndugulile alisema hivi sasa serikali inasisitiza kuweka ubora wa huduma za afya katika vituo vyote vya afya vya umma ili kukidhi ubora unaotakiwa wa kutoa huduma kwa wananchi”tunakwenda mbali zaidi usipokuwa na vigezo hospitali yako na kituo chako hutopewa leseni”

  Hata hivyo amewataka wale wote waliopewa maelekezo ya nini wafanye basi viongozi wawajibike kwa kurekebisha changamoto zilizopo na wasingoje idara ya uhakiki ubora kutoka wizarani waje kukagua kwani Lengo liliowekwa na wizara ni kila kituo cha afya kupata nyota tatu hadi kufikia mwezi juni mwakani.

  “Nyinyi wengine wote hamkustahili kupata cheti hata kimoja hapa,Mkoa wa Mtwara asilimia 3 za vituo vyenu vina nyota mbili na asilimia 51 vina nyota moja na zaidi ya nusu mna nyota 1 na asilimia 46 mna nyota sifuri hali ya utoa huduma bado”Nimetoka hapo zahanati ya Ziwani,kwakweli hapana,ubora wa kutoa huduma pale hapana wakati mpo mjini.

  Kwa upande mwingine amewataka kamati za afya ngazi ya Mkoa na Wilaya kufanya kazi na kusimamia katika kuyafanyia kazi maelekezo yote waliyopatiwa kwani maboresho mengine hayahitaji fedha hivyo kamati hizo zitimize wajibu wao”Niwaombe mbadilike kwani mambo madogo madogo yatakuja kuwagharimu hivyo msimamie hali ya utoaji wa ubora na huduma za afya kwa mkoa wa mtwara ni mbaya,nikirudi wakati mwingine sitoongea kirafiki hivi”alisisitiza

  Aidha,aliwataka watendaji hao kubadilika katika utendaji wao na hivyo kusimamia upatikanaji wa dawa katika vituo vyao vya afya ili kusiwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wamekosa dawa

  “Dhama imebadilika,hivyo kila mmoja awajibike,awamu hii ni nyingine,hatutaki kusikia dawa hakuna na mwananchi analalamika amekosa dawa kwenye kituo cha afya,Mhe.Rais anaipenda sekta ya afya na ameongeza bajeti ya dawa na anatoa pesa zote,sitaki kusikia dawa hakuna na Wilaya itakayoshindwa basi viongozi wake nao hawatoshi”aliongeza Naibu Waziri

  Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora toka Wizara ya afya Dkt. Mohamed Mohamed alisema wizara ilingia kwenye mpango wa kuboresha huduma kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya ya Msingi mwaka 2014 kwa kuhusisha kufanya tathimini vituo vyote vya afya nchini na kuvipa kategoria ya nyota moja hadi tano ikiwemo wa kuandaa mipango ya kuimarisha ubora katika vituo hivyo.

  “Tathimini ya awali ilifanyika katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini mwaka Aprili,2015 na Desemba 2016”

  Alitaja maeneo yaliyoangaliwa na kufanyiwa tathimini ni uendeshaji wa vituo ,utendaji wa wafanyakazi,uwajibikaji,miundombinu ya kituo,mkataba kwa mteja pamoja na mazingira salama ya kutolea huduma na ubora wa huduma wenyewe.

  Jumla ya vituo 6997 vilifanyiwa tathimini nchini na katika Mkoa wa Mtwara tathimini ya awali ilifanyika mwezi mei 2016 na vituo 221 vilifanyiwa tathimini na matokeo ya awali yalikua vituo 6 vilipata nyota 2(3%),vituo 112 vilipata nyota 1(51%) na vituo 103 vilipata nyota 0(47%).

  Katika zoezi hilo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu iliibuka mshindi kwa kupata ngao,na kituo cha afya Nanyumbu kilipata cheti.Kituo kingine cha afya kilichopaya cheti ni kituo cha Nagaga cha Masasi pamoja na za zahanati ya Nanjota na Nambaya zote za Halmashauri ya Masasi zilifanya vizuri.Pia zahanati ya Shangani ya halmashauri ya Manispaa ya Mtwara ilipata cheti

  0 0  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akisaini kitabu cha wageni alipowasili Chuo Kikuu Mzumbe mkoani Morogoro Novemba 24, 2017.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (katikati), akiongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (kushoto) pamoja na Mratibu wa Mradi wa POLICOFA, Prof. Joseph Kuzilwa (kulia).

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017. Kulia ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundu.

  Baadhi ya washiriki.


  Baadhi ya wanachuo.
  Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa POLICOFA, Prof. Joseph Kuzilwa akitoa mada wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017.
  Washiriki.

  Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa POLICOFA, Prof. Joseph Kuzilwa akitoa mada wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017.

  Mnufaika wa Mradi wa POLICOFA,  Edward Makoye, akitoa mada juu ya utafiti anaofanya kuhusu zao la Tumbaku.

  Mmoja wa wanufaika na Mradi wa POLICOFA anayesomea PHD Chuo Kikuu Mzumbe, Anne Mwakibete, akitoa mada juu ya utafiti anaofanya katika kilimo cha Miwa Kilombero.
  Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba.

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka.
  aibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akionyesha nakala ya kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya fursa na changamoto za kilimo cha mkataba. Kulia ni Mratibu wa Mradi Prof. Joseph Kuzilwa na Katikati ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundui.

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (kushoto), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, nakala ya kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya fursa na changamoto za kilimo cha mkataba wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripo hiyo.

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (wa pili kulia), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (wa pili kushoto), Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundui (kulia) na kushoto ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Dk. Nsubiri Isaga.

  Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo pamoja na watafiti.

  Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo pamoja na wahadhiri wa chuo hicho.


  0 0

  Na John Nditi, Kilimbero

  WAZIRI wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema kuwa suala ya kupanua viwanda vya sukari nchini halina mbadala ni jambo la lazima ili kukidhi uchakataji mkubwa wa miwa inayolimwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa sukari na ya bei nafuu.

  Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Menejimenti ya Kiwanda cha Sukari Kilombero kiwandani hapo pamoja na kwa baadhi ya wakulima na viongozi wa vyama vya zao la miwa wa pande mbili za wilaya ya Kilosa na Kilombero kwenye ukumbi wa Chuo cha Sukari Kilombero.

  Alisema ,Serikali ilipoamua kuuza sehemu ya hisa zake kwa kampuni binafsi , lengo lake lilikuwa ni moja kwamba wanauowezo wa kifedha unaoendana na ufanisi na upanuzi wa viwanda kuweza kukidhi mahitaji ya zao la miwa na utengeenzaji wa sukari.

  Dk Tizeba alisema , kutokana na dhana hiyo, maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona viwanda vya sukari vinapanuliwa kwa ajili ya kukidhi usagaji wa miwa nayolimwa na mashamba ya viwanda nay a wakulima wan je na kutengeneza sukari nyingi za kujitoshereza.

  Alisema ,uamuzi hyo unatokana na kubaini kuwa viwanda uwezo vya sukari ni mdogo kuchakata tani nyingi za miwa kwa msimu wa kilimo ikiwemo miwa ya wakulima wa n je na badala yake kusalia shambani na kuharibika.

  “ Kinachohitajika ni utosherezaji wa sukari nchini na ya bei nafuu ,kama uwezo wa viwanda ni mdogo kuchakata miwa na kuzalisha sukari kinachohitajika ni upanuzi wa kiwanda ” alisema Dk Tizeba.Dk Tizeba alisema, kinachofanyika kwa sasa ni kuweka programu ya wizara na wenye viwanda kutakiwa kuwasilisha mpango kazi wao unaoinesha hatua za utekelezaji wa upanuzi wa viwanda vyao kikiwemo cha Kilombero .

  Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, alimwomba Waziri kuuangalia kwa karibu zaidi mkoa huo kwani utafiti wake umeonesha ni kitovu cha kuzalisha sukari nchini na maziwa makuu kwa kufikisha zaidi ya tani milioni moja za sukari .

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, Guy Willium akitoa maelezo ya uendeshaji na uzalishaji wa sukari katika kikao na Waziri , licha ya kueleza faida na changamoto zinazokikabili alisema ,zinahitajika zaidi ya Sh bilioni 500 kwa ajili ya mpango endelevu wa  upanuzi kiwanda .Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema , mpango huo utatekelezwa kwa awamu nay a kwanza ya miaka minne kulingana na upatikanaji wa fedha ikamilika kufikia June 2021 na kukamilishwa hadi ifikapo mwaka 2025.

  Alisema ,kutokana na mpango wa upanuzi wa kiwanda na mashamba ya miwa , uzalishaji wa sukari utaongezeka kutoka wastani wa tani 125,000 kwa mwaka zinazozalishwa hadi kufikia wastani tani za sukari 260,000 kwa mwaka.
  Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba ( kati kati) akijadiliana na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ( kushoto) alipofanya ziara ya kikazi katika Kiwanda kilichopo sehemu ya wilaya mbili ya Kilombero na Kilosa, mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wa nje
  Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, Guy Willium , wakati alipofanya ziara katika Kiwanda kilichopo sehemu ya wilaya mbili ya Kilombero na Kilosa, mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wa nje.

  Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba akiteremka kutoka katika ndege ndogo baada ya yeye na viongozi wengine wa mkoa , wilaya za Kilombero na Kilosa , Bodi ya Sukari na wataalamu wa Kilimo kukagua eneo la mashamba makubwa ya miwa waliyolimwa na kupanuliwa na Kiwanda cha Sukari Kilombero waiiwa angani mara baada ya kupatiwa taarifa ya Kiwanda hicho na Mkurugenzi Mtendaji Guy Willium , wakati alipofanya ziara kwa ajili ya kuona shughuli za uzalishaji wa sukari na kilimo cha zao la miwa kwa kiwanda na wakulima wan je. ( Picha na John Nditi).

  0 0

  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakicheza ngoma wakati wa shamrashamra za kampeni hizo
  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimnadi Mgombea nafasi ya Udiwani Bwana Mabonde (Hayupo pichani)
  Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde akiwa katika viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,Ndugu Hassani Wakasubi akimadi Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde kwenye viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.
  Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde akiwa amebebwa juu wakati wa kampeni hizo kwenye viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.
  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde wakifanya matembezi wakati wa kuelekea kwenye viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara), Rodrick Mpogolo, Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla leo Novemba 25,2017, wanatarajia kumnadi mgombea nafasi ya Udiwani katika uchaguzi mdogo wa marudio Bwana John Cheyo Mabonde anayewania kiti cha Udiwani Kata ya Nata iliyopo Nzega Vijijini.

  Kampeni hizo za kishindo zinatarajia kufikia tamati leo hii katika Kata hiyo ya Nata ambapo tayari Mgombea huyo ameweza kuninadi katika maeneo mbalimbali ya Kata hiyo.

  Awali Dk.Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo, aliwataka wananchi kuhakikisha wanaendelea kulinda Kata yao ambayo walishashinda tokea 2015.

  “Ushindi tulishamaliza. Tulishinda Kata hii 2015. Kura za kesho ni kuhitimisha tu ushindi wetu hivyo tujitokeze kwa wingi kupiga kura za ndio kwa CCM kwa kumchagua Mabonde.” Alieleza Dk.Kigwangalla wakati wa kumandi mgombea huyo katika kampeni zilizofanyika jana Novemba 24 kwenye tawi la Mwamalulu.

  Kwa upande wake, Mgombea udiwani huyo Bwana Mabonde aliendelea kuwashukuru wananchi wa Kata hiyo kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni zake huku akiwataka kuhakikisha wanaendelea kujitokeza katika kupiga kura siku ya Novemba 26 katika kupiga kura za ndio.

  “Kura zenu ni mtaji wetu. Nawaombeni sana ndugu zangu, wana Nata kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Ushindi huu ni wetu ili kuendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika vita yake ya kiuchumi na kupambanana mafisadi.

  Aidha, katika mkutano huo wa jana jioni, ambao pia ulikuwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho waliweza kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi (CCM).

older | 1 | .... | 1440 | 1441 | (Page 1442) | 1443 | 1444 | .... | 1898 | newer