Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1439 | 1440 | (Page 1441) | 1442 | 1443 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewahamasisha wazee kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la upigwaji picha ili waweze kupatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupatiwa matibabu bure kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hayo ameyazungumza mara baada kuwasili katika Ofisi za Mtendaji Kata ya Kabuku Nov 23, 2017 kuhamasisha huduma za afya. Hatua hiyo ni muendelezo wa agizo la serikali ya awamu ya tano ya rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wazee kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea wanapatiwa matibabu bure. PICHA/HABARI NA KAJUNASON/MMG -KABUKU, HANDENI. Wazee wakisikiliza kwa makini.Diwani wa Kata ya Kabuku, Amina Mnegelo akizungumza machache mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe huku wazee wakimfuatilia kwa makini.
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akisalimiana na wazee wa kata ya Kabuku baada ya kuwasili katika ofisi ya mtendaji kuzungumza na wazee juu ya mpango wa kuwapatia kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupatiwa huduma ya afya bure katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali. Mkutano ulifanyika katika Ofisi za Mtendaji Kata ya Kabuku Nov 23, 2017. Wazee wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiwasikiliza wazee wa Kata ya Kabuku.

  0 0

  Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DKTJOSEPH MAGUFULI itaboresha mfumo wa elimu ili kuweza kumwandalia mwanafunzi maznigira bora ya kielimu, amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa wa sekondari NASULI wilayani NAMTUMBO mkoani RUVUMA ,waziri mkuu yupo ziarani mkoani ruvuma kwa siku tatu,habri kamili hii hapa video yake.

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote baadhi ya vitabu kwaajili ya wanafunzi kujisomea na kuongeza maarifa kupitia vitabu hivyo ambavyo vimetolewa kwa msaada na benki ya UBA Tanzania
   Mkurugenzi Mkuu wa benki ya UBA Tanzania akiongea na mkuu wa shule ya sekondari ya Barbro Johanson pamoja na wafanyakazi wa benki ya UBA na shule hio mara baada ya kukaribishwa ofisini kwa mkuu wa shule hiyo Bi Halima Kamote mapema jana
   Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote akiangalia moja ya vitabu mia nane vilivyotolewa na benki ya Uba katika kuendeleza juhudi zao za kurudisha faida kwa jamii. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA Tanzania Bw Peter Makau.
   Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote akiongea na wafanyakazi wa benki pamoja na shule hio katika ofisi yake mara baada ya kupokea ugeni kutoka benki ya UBA Tanzania ambao walifika shule hapo kwaajili ya kukabidhi msaada wa vitabu takribani mia nane vya kujisomea msaada ambao umekabidhiwa kwa mkuu wa shule hio.
  Imeandikwa na Josephat Lukaza
  Katika kuendeleza kwake kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kusoma na kupata vifaa mbalimbali vya kukuza taaluma zao, Mapema jana benki ya Uba Tanzania walitoa msaada wa Vitabu takribani 800 za kiada ambazo vitasaidia kuongeza hali ya usomaji kwa wanafunzi wa shule hio.
  Msaada huo wa vitabu zaidi ya mia nane ulitolewa mapema jana shule hapo na kukabidhiwa mkuu wa shule hiyo Bi, Halima Kamote huku Mkuu wa shule hio akiishukuru benki hio kwa kujitoa kwake katika kusaidia kuongeza vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wa shule huku akisema amefurahishwa na benki hio kwa msaada huo na kuwakaribisha tena pale ambapo wataguswa kuchangia zaidi na zaidi.
  Naye mmoja wa wanafunzi aliyepokea kitabu kwa niaba ya wanafunzi wenzake ameishukuru pia benki ya UBA kwa msaada huo wa vitabu kwa maana itaongeza hali ya kujisomea na kuongeza ujuzi katika mawasiliano ambapo somo la Ujuzi wa Mawasiliano limekuwa moja ya somo katika Shule hiyo huku likiwa halipo kwenye mitaala ya kufundishwa katika shule za sekondari hapa Nchini.
  Benki ya Uba imekuwa moja ya benki ya kibiashara hapa nchini katika Kuchangia maswala mbalimbali ya kijamii huku ikirudisha faida yake kwa jamii iliyowazunguka.
  Mkurugenzi mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa shule ya Barbro Johanson moja ya vitabu vilivyotolewa na benki hio kama mchango wake kwa jamii. Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu leo amezidua rasmi chuo cha Sayansi ya afya kilichopo Mjini Kahama mkoani Shinyanga ambapo uzinduzi huo umeambatana na mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo hayo katika chuo hicho.Uzinduzi huo umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya wilaya ya Kahama akiwemo Mtanzania aliyejizolea umaarufu hivi karibuni Dr. Louis Shika ambaye ameahidi kutoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kusomesha wanachuo ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia ada na wale ambao ni yatima wazazi wao wamefariki dunia.
  Akizungumza katika hahafali hayo yaliyofanyika leo Alhamis Novemba 23,2017 Nkurlu aliwataka wahitimu wa fani mbalimbali wilayani Kahama kuwa waadilifu pale wanapopata nafasi ya kuihudumia jamii ili kukidhi matakwa ya kusomea fani hizo.
  Nkurulu alisema baadhi ya wahitimu wa mafunzo mbali mbali wamekuwa wakishindwa kukidhi vigezo kutokana na kutokuwa na nia ya dhati ya kutekeleza wajibu wao kwa weledi na uadilifu.
  Katika hatua nyingine Nkurlu alimwelezea Dr. Shika kuwa ni mtu wa pekee mwenye utulivu na usikivu na kuongeza kuwa wadau wengine waige kama alichofanya Dr. Shika katika kuinua elimu nchini.
  Kivutio kikuu katika sherehe hizo akawa Dr. Louis Shika ambaye hivi karibuni amejingea umaarufu, alipojitokeza katika mnada wa nyumba za kifahari za Bilionea Saidi Lugumi zilizoko jijini Dar es salaam, kupitia msemo wake wa “(900 INAPENDEZA)” ambapo katika mahafali hayo ameahidi kutoa bilioni mbili kila mwaka kusomesha watoto yatima katika wilaya ya Kahama.
  Dr. Shika alisema kuwa yeye ni mpenzi wa elimu na anapenda watu wote wapate elimu hivyo kupitia kampuni yake ya Lancefort atasaidia kusomesha wanachuo ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia ada na wale ambao ni yatima wazazi wao wamefariki.
  Ahadi hiyo imekuja kufuatia risala ya chuo hicho iliyosomwa na Mkuu wa Chuo hicho na kuelezea changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na wazazi kushindwa kulipa ada pamoja na waanachuo wengine kushindwa kuhitimu mafunzo yao baada ya wazazi wao kufariki.
  Dr. Shika alitoa wito kwa ofisi ya mkuu wa wilaya imuombe kusaidia kusomesha wanafunzi wasio na uwezo kwani kampuni yake inauwezo wa kusaidia watoto yatima katika wilaya ya Kahama hivyo milango iko wazi na yeye yuko tayari kusaidia watu wenye njaa ya elimu.
  Akielezea kiwango atakachokitoa kusomesha wanachuo hao, Dr Shika amesema kuwa itakuwa ni dola milioni moja za Kimarekani sawa na Bilioni mbili ambazo atakuwa anazitoa kila mwaka kwa chuo hicho kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wanaopenda kusoma lakini wanashindwa kutokana na ukosefu wa ada.
  Katika hatua nyingine Dr Shika aliwataka waandishi wa habari na mwenye chuo wasimuulize kuhusu msaada huo ndani ya wiki mbili kwani kwasasa hana pesa bali wasubiri mpaka mchakato wake wa kuhamisha fedha zake kutoka Urusi ukamilike.
  Naye mkurugenzi wa chuo hicho Yonah Bakungile amesema kuwa kumekuwa na shida ya wanafunzi wanaomaliza vyuo vya uuguzi kutokuwa na maadili na kufikilia masirahi jambo ambalo limechangia kupoteza maana halisi ya masomo hayo.
  Aliwataka kuitumikia jamii bila kuangalia maslahi na kuwahudumia watu walio nacho na wasiokuwa nacho ikiwa ni kutimiza malengo na nia ya kuanzisha vyuo vya uuguzi katika kuihudumia jamii katika maeneo mbali hapa nchini.
  Aidha alisema baadhi ya Wahitimu wa vyuo vya uuguzi wanakosa uadilifu na kuweka mbele maslahi binafsi hulka inayopoteza maana halisi ya fani hiyo.
  Amewataka kuitumikia jamii bila ubaguzi na kuangalia maslahi binafsi ili kwenda sanjari na matakwa na viapo vya kada ya uuguzi duniani.
  Katika Mahafali hayo ya kwanza, Jumla ya Wahitimu 33 wametunukiwa cheti cha Msingi katika Kozi ya Mwaka mmoja ya Ufamasia.
  Chuo cha Sayansi ya Afya Kahama kilianzishwa mwaka 2016 kikitoa mafunzo katika fani za Ufamasia na Utabibu na kwamba jumla ya wanachuo 33 wamehitimu.
  ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
  Wahitimu wakiingia ukumbini katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho.Picha zote kwa hisani ya Kijukuu blog
  Wahitimu wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiingia ukumbini kwa furaha wakiwa na furaha tele.
  Wahitimu wakiwa ukumbini
  Mkuu wa wilaya akiwa na mkurugenzi wa Chuo hicho pamoja na mke wa mkurugenzi Mrs Bakungile.
  Mwanachuo wa Chuo cha Sayansi ya Afya akionyesha burudani ya kucheza nyimbo za utamaduni wa Kisukuma katika mahafali hayo.
  Mwanachuo akiendelea kutoa burudani katika uzinduzi wa chuo hicho.
  Meza kuu ikifuatilia kwa makini burudani ya nyimbo za asili katika mahafali hayo.
  Meza kuu ikifuatilia kwa makini burudani ya nyimbo za asili.
  Familia na ndugu wa Mkurugenzi wa Chuo hicho wakiwa katika sherehe hizo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
  Mkurugenzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya Ndugu Yonah Bakungile akitoa neno kwa wahitimu katika mahafali hayo
  Wageni waalikwa pamoja na wazazi wakiwa katika sherehe za mahafali na uzinduzi wa chuo cha sayansi ya afya
  Mwenyekiti wa bodi ya shule akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Kahama kutoa hotuba yake.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akitoa hutuba kwa wazazi na wahitimu katika mahafali hayo.
  Dr. Shika akitoa neno kwenye mahafali hayo
  Dr. Shika akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu
  Dr. Shika akishikana mkono na mkurugenzi wa chuo hicho
  Mgeni muhimu wa katika mahafali hayo Dr. Louis Shika akipeana mkono na wageni wa meza kuu baada ya kutoa neno lake
  Kikundi cha sanaa kutoka hospitali ya wilaya ya Kahama wakitoa burudani katika uzinduzi huo wa chuo
  Burudani inaendelea
  Wahitimu wakiwa wameketi katika nafasi zao 
  Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasubi Leonard Mayala kulia akiwa na Dr Louis Shika katika sherehe hizo
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akikakugua maabara ya kufundishia kwa vitendo katika Chuo hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama akiendelea kupata maelekezo kuhusu elimu ya vitendo wanayoipata wanachuo katika chuo hicho.
  Msafara wa mkuu wa wilaya ukikagua chumba cha Computer katika chuo hicho.
  Elimu bora ni pamoja na mazingira bora ya kusomea na kufundishia,Hili ni moja ya darasa katika chuo cha Sayansi ya afya Kahama.
  Masomo kwa vitendo,Hili ni moja ya darasa la kufundishia likiwa na vifaa vya kisasa vya kufundishia katika chuo hicho.
  Masomo kwa Vitendo hiki ni chumba maalumu cha kufundishia kikiwa na mfano wa wodi ambapo wanafunzi wanafundishwa kwa vitendo namna ya kuhudumia wagonjwa wakiwa chuoni hapo.
  Moja ya darasa la kufundishia katika chuo cha Sayansi ya afya kilichozinduliwa leo mjini Kahama.
  Baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Kahama wakiwa katika sherehe hizo.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama akiendelea kutembelea vyumba katika chuo hicho
  Wanachuo wa mwaka wa kwanza na wa pili wakiwa katika mahafali hayo
  Wazazi wakiwa katika mahafali hayo
  Picha zote kwa hisani ya Kijukuu blog

  0 0  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha.John Kijazi akionyeshwa ramani ya mpango wa matumizi ya ardhi ya eneo ambalo unajengwa mji  wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw.Nehemia Mchechu  katika eneo la Ihumwa  mjini Dodoma.
  7
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha.John Kijazi akiuliza swali wakati akionyeshwa ramani ya mpango wa matumizi ya ardhi ya eneo ambalo unajengwa mji  wa Serikali katika eneo la Ihumwa  Mjini Dodoma.Wanaompa maelekezo ni Mkurugenzi wa mipango miji nchini Profesa John Lupala na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw.Nehemia Mchechu  

  1
  Baadhi ya Makatibu wakuu kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw.Nehemia Mchechu(hayupo pichani)  kuhusu ujenzi wa Mji mpya wa Serikali unaotarajiwa kujengwa mjini Dodoma.
  2
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha.John Kijazi akipata maelezo kuhusu ujenzi wa Mji mpya wa Serikali unaotarajiwa kujengwa mjini Dodoma katika eneo la Ihumwa kutoka kwa Mkurugenzi wa mipango Miji nchini Profesa John Lupala leo Mjini Dodoma.
  3
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha.John Kijazi  akitembelea eneo ambalo utajengwa mji  wa Serikali katika eneo la  Ihumwa leo  Mjini Dodoma.
  4
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha.John Kijazi akionyeshwa ramani ya   mpangilio wa mji  wa Serikali utakavyokuwa  na Mkurugenzi wa mipango miji nchini Profesa John Lupala wakati katibu kiongozi alipotembelea eneo hilo na makatibu wakuu leo Mjini Dodoma.
  5
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha.John Kijazi akipata maelezo mbalimbali katika eneo ambalo Serikali inajenga mji  katika eneo la ihumwa Mjini Dodoma.Katibu Mkuu Kiongozi aliambatana na Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali katika ziara hiyo.

  Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
  ……………
  Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi na Makatibu Wakuu leo wametembelea na Kukagua eneo utakapojengwa Mji wa Kisasa wa Serikali katika eneo la Ihumwa Mjini Dodoma ili kujionea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
  Akizungumza katika eneo la mradi unaotarajiwa kutekelezwa katika eneo lenye ukubwa ekari 1500 Balozi Kijazi amesema kuwa Mji huo utakuwa wa kipekee na hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa Makao Makuu ya nchi yanakuwa katika mpangilio wa kisasa ili kuleta tofauti kati ya mji huo na miji  mingine.
  “ Niwatoe wananchi shaka kuhusu Serikali kuhamia Dodoma kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeshaanza kutekelezwa kwa vitendo na sehemu kubwa ya Watumishi wa Serikali wameshahamia hapa Dodoma Wakiwemo Mawaziri na  Makatibu Wakuu” .  Alisisitiza Balozi Kijazi
  Akifafanua amesema  kuwa mji huo utakuwa na maeneo kwa ajili ya majengo ya  Wizara, Taasisi, Balozi, na huduma mbalimbali za kijamii  ikiwemo Viwanja vya michezo, Hosipitali, maeneo ya kupumzikia, Maeneo ya Biashara  .
  Aliongeza kuwa upatikanaji wa huduma katika  Mji wa Serikali utakuwa wa uhakika  na utakuwa umerahisishwa kutokana na kuwepo kwa Taasisi za Serikali na Wizara zote katika eneo moja.
  Kwa upande  wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Nehemia Mchechu amesema kuwa ni muhimu kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza mkoani Dodoma kutokana na mipango ya Serikali kujenga mji huo wa Kisasa wa Serikali.
  Aliongeza kuwa mawazo ya awali ya namna ya kujenga mji huo wa Kisasa wa Serikali yapo na kinachosubiriwa ni hatua mbalimbali za kiutendaji  zitakazowezesha kutekelezwa kwa mradi huo.
  Uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma umepata msukumo katika kipindi cha  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na tayari utekelezaji wake unaendelea ambapo Mawaziri wote wameshahamia Dodoma, Makatibu Wakuu na Watumishi Wengine wa Serikali pia wameshahamia.

  0 0


  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na vikundi mbali mbali vya wajasiriamali  havipo pichani  kutoka halmashauri ya Chalinze katika halfa fupi ya  makabidhiano ya hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120 ambayo itaweza kuwasaidia katika kufanya biashara zao.
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu akizungumza jambo na vikundi vya wajasiriamali ambao walifika katika sherehe hiyo ya makabidhiano ambayo ilifanyika katika viwanja vya sokoni Lugoba.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga kulia akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120  mmoja wa wanakikundi wajasiriamali katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya soko la Lugoba(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
  NA VICTOR MASANGU, LUGOBA BAGAMOYO

  KATIKA kukabiliana na wimbi la umasikini na ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na wanawake hatimaye halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani imeamua kuvipatia mikopo wa kiasi cha shilingi milioni 120 Vikundi 40 vya wajasiriamali kutoka kata 15 kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.

  Akizungumza katika halfa ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya fedha hizo iliyofanyika katika kata ya Lugoba Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufui ni kuhakikisha inawawezesha kiuchumi wananchi wake pamoja na kuwapatia mikopo ya fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

  Aidha Mwanga aliwaagiza watendaji na viongozi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu vikundi vyote ambavyo vimeshakopeshwa kufanya ukaguzi wa kina kujua fedha amabzo zimetolewa zinatumika katika matumizi sahihi kwani amebaini kuna baadhi yao wanakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa hivyo kurudisha nyuma kasi ya maendeleo.

  Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Mohamed Sume akisoma taarifa yake amebainisha kuwa fedha hizo zote zimetokana na makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani kwa lengo la kuweza kuviwezesha vikundi hivyo ikiwa ni kutekeleza Agizo la ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kutenga asilimia kumi kwa ajili ya kuwawezesha vijana pamoja na wanawake.

  Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu amesema kuwa fedha ambazo zimetolewa katika vikundi vya wajasiriamali hao ni katika kota ya kwanza ambapo pia wametenga milioni 300 kwa lengo la kuweza kuvipatia vikundi vingine ili kuweza kuongeza pato la Taifa kupitia biashara wanazozifanya.

  Alisema kwamba mipango ya halmashauri hiyo ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 vikundi vyote vya ujasiriamali vinawezeshwa kwa kupatiwa mikopo ya kufanyia biashara zao mbali mbali sambamba na kuwapatiua wataalamu ambao watakuwa wakiwafundisha namna na kuweza kujifunza masuala mbali mbali yanayohusina na namna na kuweza kutafuta masoko katika bidhaa wanazozizalisha.

  Baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na fedha hizo akiwemo Zawadi Rashid pamoja na Mwajuma Shaban walieleza malengo na matarajio yao ni kuhakikisha wanakuza mitaji yao kwa kuendeleza biashara walizonazo, ikiwemo ufugaji, kilimo, ufyatuaji wa matofali pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo ili kuweza kujikwamua kimaisha na kukuza uchumi.
  0 0


  0 0

  Aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Likuyufusi mkoani Ruvuma.

  Gama aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 24,2017 atazikwa Jumatatu Novemba 27,2017 katika makaburi hayo yaliyopo umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini.

  Issa Fussi ambaye ni msemaji wa familia na mdogo wa Gama amesema amefariki usiku wa kuamkia leo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho.

  Amesema Gama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipelekwa hospitalini hapo Jumatano Novemba 22,2017 usiku na kulazwa hospitalini hapo .

  Fussi amesema msiba huo ni pigo kwa familia kwa kuwa Gama alikuwa nguzo akitegemewa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kifamilia.

  Amesema mwili wa marehemu Gama umehifadhiwa katika Hospitali ya Peramiho na utaratibu wa mazishi unaendelea.

  0 0

  kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiendelea nayo muda mrefu ya kukamata wezi wa kazi za muziki na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kupunguza uharamia na kuhamasisha uchangiaji wa pato la Taifa kupitia kazi za sanaa. 

  Katika pongezi hizo Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime amesema, 'Kwa niaba ya wanachama wa chama chetu Tanzania Musicians Network, naomba nitoe shukrani kwa mchango wako mkubwa ambao kampuni yako inaufanya katika jitihada za kupunguza uharamia wa kazi za sanaa Dar es Salaam.

   Tuko tayari kushirikiana nawe kila wakati kwa lengo la kuboresha mazingira yanayohusu uboreshwaji wa stahiki za wanamuziki wakati wowote.Tunarudia tena kushukuru kwa hili'

  Msama amekuwa akifanya kazi hii ya kukamata kazi zisizo halali kwa miaka mingi, na Kitime amekuwa mwanaharakati wa swala la Hakimiliki kwa miaka mingi pia.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali,Msama Auction Mart Alex Msama akizungumza na Waandishi wa Habari mapema jana jijini Dar,kuhusiana na hatua aliyofikia ya kuwakamata maharamia wa kazi zaWasanii na Wakwepa kodi kupitia tasnia hiyo,ampao pia amewashukuru wadau wa Muziki mbalimbali wakiwemo Mtandao wa Muziki Tanzania kumpongeza na kumuunga mkono katika mapambano hayo ya kazi za Wasanii hapa nchini
  Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime

  0 0   Mh.Gama enzi za Uhai wake.

  0 0  0 0
 • 11/24/17--01:06: Article 7


 • 0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akiwa ameshikilia kivutio cha utalii cha Kimondo leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

  Kimondo hicho kinachokadiriwa kuwa na tani 12 kiligunduliwa wilayani Mbozi mwaka 1930 na kimeundwa kwa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.

  Aidha, kimondo hiki ni cha pili kwa ukubwa kati ya 35 vilivyopo barani Afrika na cha nane kati ya 578 vilivyopo duniani kote ambavyo vimeundwa kwa chuma. Sifa kuu ya kimondo hiki ni kuwa na ubaridi wakati wote hata mchana wa jua kali.

  Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo, amekagua ujenzi unaoendelea wa jengo la kituo cha taarifa (Information Centre) katika kivutio hicho ambalo linagharimu Shilingi milioni 400. 

  Alisema Serikali kupitia wizara yake ina mpango thabiti wa kuendeleza kivutio hicho pamoja na vivutio vya ukanda wa kusini ambapo kupitia Benki ya Dunia imepata mkopo nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 150 sawa na shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kuendeleza vivutio vya ukanda wa kusini ikiwemo kuimarisha miundombinu.

  Vivutio vingine vya utalii vinavyopatikana Mkoani Songwe ni pamoja na chemchem ya maji moto, vitalu vya uwindaji vyenye wanyamapori mbalimbali, mifupa ya shingopana songwensis, unyayo wa mtu wa kale, mapango ya popo, maporomoko ya maji, mbega weupe, kituo cha kwanza cha polisi Tanzania, mabaki ya nyumba za kufua chuma,  na ziwa Rukwa
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Muhifadhi wa Mambo ya Kale, Winnie Msacky kuhusu kivutio cha utalii cha Kimondo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi Mkoani wa Songwe jana. 
  Jengo la kituo cha taarifa katika eneo la kivutio hicho (Information Center) ambacho ujenzi wake unaendelea. Ujenzi wa kituo hiki unagharimu Shilingi Milioni 400.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na baadhi ya watumishi wa kituo hicho na wananchi wa vijiji jirani.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na watumishi pamoja na wananchi hao. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akipata maelezo kutoka Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale, Bi. Digna Tilya kuhusu jengo la kituo hicho cha taarifa katika kivutio hicho. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  WANAFUNZI waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kesho wanatarajia kufanya kongamono kubwa la kihistoria kujadili namna watakavyoweza kutumia taaluma zao kusaidia jamii, kanisa na taifa kwa ujumla.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

  Alisema licha ya muungano huo kuundwa na vijana wa kikristo lakini vijana wote wasomi kutoka katika vyuo na shule za sekondari na madhehebu mbalimbali wanaalikwa ili kuchangia mada zitakazo jadiliwa na mgeni rasmi atakuwa ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

  Mwambapa alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali na kuona ni jinsi gani kila mmoja na taaluma yake ataweza kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kuifanyia kazi.

  "Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizurio kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

  Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Mwambapa alisema kongamano hilo litahudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali,sekondari baadhi wa viongozi.
  Mratibu wa Kongamamo la Wasomi Wanataaluma wa Kikristo liitwalo Tanzania for Jesus Prayer Movement ambalo mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus, Ephrahim Mwambapa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Kanisa la Abundant Bressing Center (ABC), Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Hoteli ya Landmark siku ya Jumamosi. Kulia ni Katibu Mkuu  wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli.
  Mratibu wa Kongamano hilo, Ephrahim Mwambapa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

  0 0


  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafikisha huduma ya maji kwenye maeneo yao kwa wastani wa asilimia 75 hadi kufikia mwakani.

  Akihutubia wadau wa Sekta ya Maji jijini hapa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Usambazaji Maji nchini, Mhandisi Kamwelwe alisema Halmashauri zinatakiwa kufikia asilimia hizo, ili kutekeleza Ilani ya chama tawala ya kuwapatia wakazi wa mijini wastani wa asilimia 95 na vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.

  “Nitumie fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafikisha asilimia 75 mwakani, na zile Halmashauri ambazo wanahisi hawatafika waje tuzungumze tuone namna gani ya kuweza kufika hapo” aliagiza Waziri Kamwelwe.

  Mkutano wa wadau wa usambazaji maji hufanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau wa sekta hiyo, ambapo mada mbali mbali hutolewa na wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi, na kwa mwaka huu jumla ya mada 20 zitatolewa kwa washiriki wa mkutano huo.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewashukuru Jumuiya ya Wasambazaji Maji (ATAWAS) kwa jitihada zao za dhati za kuhakikisha Sekta ya Maji inapiga hatua kimaendeleo.

  Pia, amewahakikishia kuwa wizara itatoa ushirikiano wa kutosha, kuhakikisha lengo la kuwapatia wananchi wa Tanzania huduma bora na endelevu ya majisafi na usafi wa mazingira linafikiwa. “Wizara yote leo ipo hapa, Waziri na Katibu Mkuu wote tupo, sasa ni nguvu gani mnayoitaka tena? Tuwahakikishie kuwa tupo pamoja na nyie ili kutimiza lengo la Serikali yetu,’’ alisema Prof. Mkumbo.

  Mkutano wa mwaka wa ATAWAS umeanza tarehe 23 na kukamilika tarehe 25 mwezi Novemba na hufanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana uzoefu na utaalamu katika Sekta ya Maji.
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi. Isack Kamwelwe akihutubia washiriki wa mkutano katika Ukumbi wa Tanga Beach Resort.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati alipokuwa akitoa neno.
  Mwenyekiti wa ATAWAS, Mhandisi Mkama Bwire wakati alipokuwa akitoa maelezo.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe.

  0 0

  Na.WAMJW,Ruangwa.

  Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto inatarajia kutoa mwongozo wa utoaji tiba kwenye hospitali zote nchini ili kuwe na mfumo mzuri wa dawa muhimu ili kuepusha madaktari kuagiza dawa ambazo zipo nje ya mfumo wa dawa muhimu.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali .

  “Kabla ya mwisho wa mwaka tunataka kutoa muongozo huo(Standard Treatment Guidline) kwa sababu imekua changamoto kwani wale wauzaji wakubwa wa dawa wamekua wakizitembelea hospitali kubwa na kuwarubuni wanunue dawa zao ambazo zipo nje ya dawa zetu muhimu”

  Kwahiyo muongozo huo itakua kila ugonjwa dawa ya kwanza itakua ipi na kama itashindika dawa itakayofuata dawa ipo na hizo dawa zitaagizwa na kutunzwa na Bohari ya Dawa(MSD).

  Hata hivyo Dkt.Ndugulile amewataka watendaji wa hospitali hiyo kuweka utaratibu na mpangilio mzuri na unaohitajikwa wa utunzaji wa dawa kwenye stoo ya madawa iliyopo hospitalini hapo,baada ya kukuta hakuna upangaji mzuri wa dawa na vifaa tiba “mmenithibitishia kwamba dawa zote mnazipata kwa asilimia 90 hivyo ni vyema Mfamasia wa Wilaya kuzipanga dawa hizo vizuri na kuweka kiyoyozi ambacho kitasaidia kutunza dawa kwa muda bila kuharibika”

  Alisema hivi sasa nchi haina tatizo la upatikanaji wa dawa kwani bajeti ya dawa hivi sasa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 30 mpaka zaidi ya bilioni 260 kwa mwaka huu wa fedha “bajeti hii imekua ikitolewa na Mhe.Rais amekua akizitoa fedha zote,hivyo hatuna shida ya fedha hivyo nasi hatutarajii kuwa na shida ya dawa na dawa tunazokuwa tunazipata zitunzwe vizuri”.

  Aidha,amezitaka kamati za afya katika ngazi za zahanati,vituo vya afya na hospitali zinafanya kazi ipasavyo kwa kusimamia matumizi mazuri ya dawa.

  Kwa upande wa ubora wa huduma za afya kwa vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali hivyo kumekua na mkakati wa kuwa na ubora wa vituo vya serikali kwa kuwapatia nyota kulingana na ubora uliopo kwenye vituo kwa kuangalia utoaji wa huduma,maabara na sehemu zingine za kutolea huduma.

  Kwa upande wa Mfuko wa afya wa jamii(CHF) Dkt.Ndugulile amewapongeza wilaya hiyo kwa kusajili kaya 13,788 kutoka 978 mwaka 2016/2017,ambapo wamewapatia vitambulishovya matibabu wazee 4,000.“hivi sasa Serikali inataka kuwa na bima kwa wote kwani gharama ya matibabu kwa sasa ni kubwa sana hasa na kumekua na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukizwa,hivyo tunataka kuwasaidia wananchi ambao hawawezi kumudu gharama hizo ili anavyokwenda kwenye vituo vyetu asiwaze masuala ya kutoa fedha”alisema Dkt.Ndugulile.

  Akisoma ripoti ya Wilaya hiyo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Ernest Ntahuka Alisema Halmashauri hiyo imeweza kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa asilimia 85 kutoka asilimia 60 ya mwaka 2015/2016.Hata hivyo alisema Halmshauri ya Ruangwa kwa mwaka 2017/2017 imetenga shilingi milioni 650 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya na tayari imeshatenga eneo la ujenzi lenye ukubwa wa hekari 60 ambapo ramani ya ujenzi huo tayari imeandaliwa

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akifungua Mkutano wa kuvutia wawekezaji uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini China na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza Barani Afrika. Prof. Mkenda yupo nchini China kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC unaofanyika kwa ngazi ya Watendaji. 
  Prof. Mkenda akizungumza na Kiongozi wa Benki ya AIIB iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa mikopo kwa miradi ya miundombinu kwa nchi wanachama wa Belt and Road. Benki hiyo imeikaribisha Tanzania kujiunga nayo ili iweze kufaidika na fursa za mikopo nafuu. Vilevile, Prof. Mkendaamekutana na uongozi wa Kampuni ya Hainan Group inayomiliki mashirika mbalimbali ya ndege na Hoteli zaidi ya 1000 ulimwenguni. Katika mazungumzo hayo Prof. Mkenda amewashawishi wawekeze kwenye ujenzi wa Hoteli katika maeneo ya Utalii Zanzibar na Tanzania Bara. 
  Ujumbe ukifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Kiongozi wa Benki ya AIIB (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Lu Yongqing, aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania na Mhe. Mbelwa Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini China. 
  Ujumbe kutoka Benki ya AIIB 
  Prof. Mkenda akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuvutia Wawekezaji uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini China. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Chen Xiaodong akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika unaofanyika tarehe 24 Novemba, 2017 Beijing, China. Baada ya ufunguzi kiongozi huyo amefanya mazungumzo ya kukuza ushirikiano na nchi nne Tanzania ikiwa ya kwanza kukutana nayo. Katika mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Mhe. Xiaodong, China imeahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja za uchumi hususan kwenye ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. CHEN Xiaodong mara baada ya kukamilisha mazungumzo ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Tabitha Siwale wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho Dar es Salaam jana. Kutoka (kwa waziri Mkuu) ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Prof Joyce Nadlichako, Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, Makamu Mkuu wa ARU, Prof Evaristo Riwa na Rais wa Jumuiya ya ARU, Haruna Masebu. (Picha na Robert Okanda Blogs)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Prof Joyce Nadlichako (wa nne kushoto), Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya (kushoto) na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi wakionesha kitabu kilichozunduliwa wakati ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho Dar es Salaam jana. Pamoja nao (wa tatu kushoto) ni Mwenyekiti wa ARU, Tabitha Siwale,  Makamu Mkuu wa ARU, Prof Evaristo Riwa (kulia) na Rais wa Jumuiya ya ARU, Haruna Masebu.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho Dar es Salaam jana. Pamoja naye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Prof Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto), Mkuu wa ARU, Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya (wa nne kushoto), mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa ARU, Tabitha Siwale (kushoto), Makamu Mkuu wa ARU, Prof Evaristo Riwa (kulia) na Rais wa Jumuiya ya ARU, Haruna Masebu.
  Waziri wa Elimu, Sayansi naTeknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako
  Mawaziri na Manaibu wa Wizara mbalimbali mliohudhuria ufunguzi huu,
  Mkuu wa Chuo Mhe. Cleopa David Msuya,
  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Mama Tabitha Siwale
  Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Evaristo Liwa,
  Manaibu Makamu wakuu wa Chuo,
  Viongozi mbalimbali wa Serikali,
  Vyama vya kitaaluma,
  Wafanyakazi , Wanafunzi  na Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi,
  Wadau mbalimbali wa Elimu,
  Waandishi wa Habari,
  Mabibi na Mabwana;
  Habari za asubuhi!
  Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha sote kufika siku hii Muhimu ambapo tunashuhudia sherehe za kutimiza miaka kumi ya Chuo hiki toka kilipoanzishwa rasmi kuwa Chuo Kikuu kinachojitegemea hapo mwaka 2007. Hakika hii ni safari ndefu ambapo sasa ni muhimu kwa wadau wa Chuo hiki kuketi kwa pamoja na kujadili mustakabali wake katika kipindi kijacho.  
  Aidha napenda kutoa pongezi kwa uongozi wa Chuo kwa kuona umuhimu wa kuandaa siku hii ambapo wadau mbalimbali wa Chuo wanakutana na kujadili maswala muhimu ya Chuo na yanayohusu ustawi wa jamii kwa ujumla. Hii ni fursa nzuri kwa wadau kuweza kutafakari kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazo kabili chuo chetu na Taifa kwa ujumla na hatimae kuweza kupata ufumbuzi wa Changamoto hizo.  Hii ni miongoni mwa faida kubwa sana kwa mihadhara ya Wasomi kwani taifa letu kwa sasa linahitaji majibu zaidi ya changamoto zinazolikabili kuliko maswali.
  Ndugu wanajumuia wa Chuo Kikuu Ardhi, huu sio wakati wa kujiuliza maswali tena bali ni wakati wa kutafuta suluhisho na ufumbuzi wa masuala mbalimbali yanayotuzunguka katika jamii yetu hasa katika sekta ya ardhi na maendeleo yake kama chachu ya kuleta tija katika uzalishaji.
  Ndugu wanajumuiya ya Chuo Kikuu Ardhi
  Mustakabali wa nchi yetu unaongozwa na Dira ya maendeleo ya Taifa, inayoweka mkazo katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya watu wenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Pamoja na mikakati mingine, taifa halina budi kuwa na wataalamu wa kutosha watakaohakikisha majukumu yote yanafanyika kwa umahiri na weledi. Hivyo Chuo Kikuu Ardhi kama taasisi ya Serikali yenye wajibu na mchango mkubwa katika kutayarisha wataalamu mbalimbali wa sekta za ujenzi, ukadiriaji majenzi na uhandisi wa mazingira, hakinabudi kutumia wataalam wake katika kutatua changamoto zinazo ikabili nchi kwa weledi na gharama nafuu.
  Ninafahamu kuwa Chuo Kikuu Ardhi kimefanya tafiti mbalimbali katika jitihada za kubadili mfumo wa utendaji pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu. Hili linafanyika wakati sahihi, kwa sababu kama mnavyofahamu mwelekeo wa Serikali yetu unalenga zaidi kupunguza gharama katika matumizi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu yake. Hivi karibuni Chuo kiliweza kuishawishi Serikali kutumia teknolojia mbadala ya ujenzi wa gharama nafuu, kwa ubora zaidi na kwa muda mfupi kupitia tafiti ya ujenzi iliyofanywa kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania na Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC). Hii inatupa imani kubwa sisi upande wa Serikali na hivyo kuendelea kutambua mchango wa wataalamu wanaozalishwa na Chuo Kikuu Ardhi. Hivyo kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Chuo kilikabidhiwa shughuli ya ukarabati wa shule kongwe ishirini (20) za sekondari na vyuo vya mafunzo ya ualimu.
  Ndugu Viongozi na wanazuoni wa Chuo Kikuu Ardhi
  Tarehe 21 Septemba, 2016 nilipata nafasi ya kuhudhuria katika ufunguzi wa mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha - Pwani, na nilikipongeza Chuo kwa kukamilisha ujenzi nadhifu wa Mahakama hiyo kwa Shilingi za Kitanzania million 520 ukilinganisha na wazabuni wengine walioomba kulipwa zaidi ya billion 1.7.  Binafsi mimi napata faraja nikiona hivi leo Chuo kinapoadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwa sababu nauona mwanga mwisho wa Taneli. Ni matumaini yangu kuwa juhudi nzuri zilizoanzishwa na Chuo, ambazo sasa zinaipa fursa Serikali ketembea kifua mbele katika masuala yote ya matumizi bora ya rasilimali ikiwemo rasilimali fedha zitaendelezwa na kupata maboresho ili kufikia lengo la Serikali.
  Ndugu wadau wa Chuo Kikuu Ardhi
  Aidha, napenda niutaarifu Umma huu kuwa hivi sasa Chuo Kikuu Ardhi ni miongoni mwa wataalamu washauri niliowateua kuishauri Serikali katika marejeo ya mpango kabambe kuendeleza mji wa Dodoma na kuhakikisha Serikali inahamia Dodoma kwa ufanisi. Ndugu zangu nafahamu pia hivi karibuni Chuo kiliongoza uandaaji wa mpango wa ujenzi wa shule mpya za sekondari na ukadiriaji wa gharama za majenzi kufuatia maafa ya tetemeko la ardhi yaliyoukumba mkoa wa Kagera. Shule hizo ni Kahoro na Nyakato. Hii ni baadhi tu kati ya michango mingi inayotolewa na Chuo Kikuu Ardhi.
  Ndugu wadau wa Chuo Kikuu Ardhi
  Mafanikio yote hayo niliyotaja hapo juu, bila shaka ni kutokana na kutoa mafunzo bora kwa fani mnazofundisha, hivyo ni wito wangu kwenu kuendelea kusimamia ubora wa elimu ili kuzalisha wataalamu watakaoenda kukidhi mahitaji mbalimbali ya soko kwenye jamii yetu. Nchi yetu bado inahitaji wataalamu wengi zaidi ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbali hasa za miundombinu. Hivyo ni jukumu lenu kama taasisi ya Elimu ya juu kuzalisha wataalamu wengi zaidi bila kuathiri ubora wa Elimu.
  Japokuwa ni kweli nimesikia kwenye hotuba ya Makamu Mkuu wa Chuo kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazochangia ongezeko dogo la udahili kila mwaka na hivyo kukikosesha Chuo mapato ya ndani ya kutosha, bado Chuo kinapaswa kuongeza kasi ya tafiti zenye tija ili kutoathiri ubora wa elimu itolewayo Chuoni na kuhakikisha huduma nyingine zinapatikana. Kwa upande wa Serikali tunaamini kuwa matokeo ya tafiti mbalimbali ni chachu ya maendeleo ya taasisi za elimu ya juu kama tafiti hizo zitakuwa zimefikiriwa kwa mapana katika kuchangia kwa maendeleo ya Taasisi husika.
  Ndugu Wadau wa Chuo Kikuu Ardhi
  Napenda kusisitiza tena juu ya matumaini yangu kwa kusanyiko hili la leo kuwa tumieni fursa hii kujitafakari kuona mnaweza kuwekeza zaidi katika maeneo gani ili kuongeza tija ya uwepo wa Taasisi hii kwa jamii na Taifa. Wekeni mikakati madhubuti itakayowezesha Chuo kupiga hatua kubwa zaidi katika kipindi cha miaka Kumi ijayo. Siku zote mjikite kuwa bora zaidi ya wakati uliopita.  Fanyeni tafiti zenye kuleta majibu ya maswali na changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa letu na Dunia kwa jumla. Kwa sasa, Tanzania inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, makazi, uharibifu wa mazingira, ujenzi holela, majanga ya asili kama vile mafuriko, matetemeko ya ardhi na mengineyo. Ninyi mkawe majibu ya changamoto zote hizo kwa kuwa na mchango wa kitaalamu wa kutatua changamoto hizo.
  Kwa hotuba yangu hii fupi, natangaza rasmi kufungua sherehe hizi za ufunguzi wa Miaka Kumi ya Chuo KikuuArdhi.
  Asanteni kwa kunisikiliza na nawatakia kila la heri!

older | 1 | .... | 1439 | 1440 | (Page 1441) | 1442 | 1443 | .... | 1897 | newer