Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1438 | 1439 | (Page 1440) | 1441 | 1442 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati mbele) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto mbele) wakiendelea na ziara katika kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, iliyopo jijini Arusha. Kulia mbele ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Zahir Saleh
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC zilizopo jijini Arusha.
  Mmoja wa mafundi wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC akipiga rangi transfoma mojawapo
  Meneja Mkuu wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kulia) akimwonesha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani moja ya mifuniko ya transfoma za umeme inayotengenezwa na kampuni hiyo.
  Msimamizi wa Idara ya Vyuma, Zakayo Mmbaga (kulia) akionesha jinsi mashine ya kukunja vyuma inavyofanya kazi kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto)
  Meneja Mkuu wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kulia) akielezea mafanikio ya kampuni hiyo kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia mbele). Kushoto mbele ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

  Mafundi wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, wakiendelea na kazi
  Meneja Mkuu wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kushoto mbele) akielezea matumizi ya mashine ya kukata bati kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia)
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji na wafanyakazi wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC.
  Meneja Mkuu wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kulia) akielezea usukaji wa nyaya za transfoma za umeme unavyofanyika katika kiwanda hicho.
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akipanda mti kama kumbukumbu ya ziara yake katika kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, iliyopo jijini Arusha.
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( wa nne kutoka kulia waliokaa mbele) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ( wa tatu kutoka kulia waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo.  Na Greyson Mwase, Arusha

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani tarehe 22 Novemba, 2017 alifanya ziara katika kampuni ya kuzalisha transfoma za umeme ya TANELEC iliyopo jijini Arusha lengo likiwa ni kukagua shughuli za kampuni hiyo pamoja na kuangalia namna ya kutatua changamoto katika uzalishaji wa vifaa vya umeme nchini.

  Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Kalemani alisema mara baada ya kukagua shughuli za kampuni hiyo na kujiridhisha uwezo wa kampuni hiyo katika uzalishaji wa transfoma, ni wakati wa TANESCO na REA kujipanga upya katika mahitaji ya transfoma za kutosha na kuwasilisha mahitaji hayo kwa kampuni husika na kuongeza kasi ya miradi ya umeme nchini.

  Alifafanua kuwa mapema Juni mwaka huu Serikali kupitia Wizara ya Nishati ilipiga marufuku uingizwaji wa nguzo za zege na transfoma ili kuepuka gharama kubwa na tatizo la kuchelewa kwa miradi.

  Aliendelea kusema kuwa baada ya kutoa agizo hilo, ameamua kufanya ziara ili kubaini uwezo na mahitaji halisi ya transfoma za umeme ambapo amebaini kuwa kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha transfoma za umeme 10,000 wakati mahitaji halisi ya transfoma za umeme nchini yakiwa ni 6,500

  Alisema kutokana na uwezo mkubwa wa uzalishaji wa transfoma katika kampuni hiyo, ni wakati wa TANESCO na REA kukaa pamoja na kuainisha upya mahitaji ya transfoma za umeme nyingi zaidi ili kuendana na kasi ya utekelezaji wa miradi ya umeme nchini.

  Dkt. Kalemani mbali na TANESCO na REA, aliwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA Awamu ya Tatu kuanza kuainisha mahitaji yao mapema kwa kampuni hiyo ili pasiwepo na kikwazo cha utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

  “ Nimeambiwa kuwa wakandarasi wachache wameagiza transfoma za umeme katika kampuni ya TANELEC, nitoe fursa hii kuwataka wakandarasi wote nchini kuagiza transfoma za umeme mara moja na kuanza utekelezaji wa miradi yao kwa kasi kubwa, pasiwepo na kisingizio cha kukosekana kwa transfoma za umeme,”alifafanua Dkt. Kalemani

  Katika hatua nyingine Waziri Kalemani aliitaka kampuni ya TANELEC kuanza kulipa gawio lake kwa serikali kupitia Msajili wa Hazina kuanzia mwaka huu.

  Alisema Serikali inamiliki asilimia 30 ambapo asilimia 20 zinamilikiwa na TANESCO na asilimia 10 kupitia Shirika la Maendeleo Nchini (NDC)

  Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya TANELEC, Zahir Saleh akielezea biashara ya transfoma za umeme katika kampuni hiyo alisema kampuni hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kusambaza transfoma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile Tanzania, Kenya na Uganda na nchi nyingine kama vile, Nigeria, Zimbabwe na Ethiopia.

  Alifafanua kuwa, wateja wakubwa wa transfoma hizo ni pamoja na wazalishaji wa umeme, wakandarasi wa miradi ya umeme na wateja binafsi na kuongeza kuwa kampuni hiyo imejipanga zaidi kuhakikisha inaongeza kasi ya uzalishaji ili kukabiliana na mahitaji ya transfoma za umeme mara baada ya serikali kupiga marufuku uingizwaji wa transfoma za umeme kutoka nje ya nchi.

  Alisema kuwa kampuni imepanga kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 120 hadi 150 ili kuongeza kasi ya uzalishaji na usambazaji wa transfoma ndani na nje ya nchi.

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samwel Malecela (mwenye kofia ya njano) akimuonesha Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge mizabibu iliyopandwa kwenye shamba la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakipata maelezo juu ya mashine ya kusukumia maji kwa ajili ya umwagiliaji wa matone kwenye shamba la zabibu la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo.
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua bwawa la kutunzia maji kwa ajili ya umwagiliaji wa matone kwenye shamba la zabibu la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo.
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua nyaraka na kusikiliza kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Manzase Wilayani Chamwino wakati wa ziara yake
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Manzase Wilayani Chamwino wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Mahenge (hayupo pichani) wakati alipofanya mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi Kijiji hapo.
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Ghorofa moja la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakati wa ziara yake wilayani humo.
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao akikagua chanzo cha chemichemi ya maji moto Mjini Kondoa, Chanzo hiko kwa sasa ndio kinategemewa kwa huduma ya maji Mjini Kondoa.

  0 0

   Meneja Amana za wateja binafsi NBC Dorothea Mabonye na Meneja Mikopo ya wateja binafsi Mtenya Cheya wakimpigi mteja aliyeshinda katika droo ya kwanza ya kampeni ya Akaunti ya Malengo ijulikanayo kama Malengo na Kirikuu, aliyejishindia zawadi ya shillingi milioni moja. Wanao shuhudia tukio hilo Kutoka kushoto. Meneja masoko wa NBC Alina Maria Kimaryo, na Msimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa Bakari Maggid. NBC iliendesha droo ya kwanza ambayo ilitoa jumla ya washindi 12 walijishindia shillingi milioni moja kila mmoja.
   Meneja masoko wa NBC Alina Maria Kimaryo (katikati) akionyesha vipeperushi vya kampeni ya akaunti ya malengo ijulikanayo kama Malengo na Kirikuu kwenye droo ya kwanza. Kushoto ni Meneja mwandamizi wa mahusiano ya Umma William Kallaghe na kulia ni Meneja Amana za wateja binafsi NBC Dorothea Mabonye. NBC iliendesha droo ya kwanza ambayo ilitoa jumla ya washindi 12 walijishindia shillingi milioni moja kila mmoja.
  Meneja masoko wa NBC Alina Maria Kimaryo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya Malengo ijulikanayo kama Malengo na Kirikuu. Katika droo hiyo jumla ya washindi 12 walijishindia shillingi milioni moja kila mmoja. Wanao shuhudia ni Meneja Amana za wateja binafsi NBC Dorothea Mabonye (kati kati) na Meneja Mikopo ya wateja binafsi NBC Mtenya Cheya.

  0 0

  Ndugu waandishi wa habari: Nimeshikwa na mshtuko, simanzi baada ya kusambaa kwa  taarifa ambazo naweza kusema kuwa ni za uzushi kwamba  ninampango wa kujiondoa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. naomba taarifa hizo zipuuzwe manahazina ukweli wowote na kwamba zinampango wa kunichafua mimi pamoja na Chama Changu.

  Ndugu wandishi wa habari : Napenda ieleweke kuwa  sijawahi kudhani wala kufikiria kuhama Chadema na kwenda kwenye chama chochote kile cha siasa. Chadema ni chama ambacho nimetoka nacho mbali tangu mwaka 2004 hadi leo, nimejenga chama kwa gaharama zangu mwenyewe.

  Ndugu waandishi wa habari: Leo nimekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam kupitia Chama Changu cha Chadema,natambua kuwa  chama kimeniheshimu sana kwa kunipa nafasi hii hivyo sina sababu ya kuondoka kwani  ninania ya kuwatumikia Wananchi ambao wameniamini na wamenichagua kwa mapenzi yao wakiamini kuwa nitawaletea Maendeleo nikiwa ndani ya Chama Cha Chadema.

  .Nafahamu  tuhuma hizi zinatokana na aina ya utendaji wangu katika Jiji la Dar es Salaam kwani nimekuwa nikifanya kazi badala ya kupambana na serikali pale ambapo watu wanaamini kuwa mambo hayajaenda sawa.

  Ndugu waandishi wa habari:  Kukaa kwangu kimya huku ,kutokufanya siasa za kiharakati ndani ya jiji la Dar es Salaam  haimanishi kwamba nipo upande wowote ama kukihujumu chama changu. Ila huu ni mfumo ambao nimeuchagua na kujijengea kwa ajili ya kuwatumikia wananchi nasio kufanya harakati za kisiasa kwakuwa nina  nia  ya kufanya maendeleo ndani ya jiji la Dar  es Salaam.

  Ndugu waandishi wahabari: Naomba ifahamike kuwa hakuna Mkurya ambaye aliwahi kuwa msaliti,katika nafasi yoyote ambayo aliwahi kuwa nayo. Kutokana historia hiyo, naomba niaminike na wanachama na wananchi wote kuwa haitakuja kutokea Mkurya mimi nikakisaliti chama changu.

  Nakama  itakuja kutokea nikafanya hivyo ninaweza kuhatarisha maisha yangu, Familia yangu, na hivyo kujikuta nikaingia kwenye matatizo makubwa ambayo kimsingi sio mazuri. Mama yangu ni mjane, kama itafanya hivyo Chadema wote Mkoa wa Mara hawawezi kuwaacha ndugu zangu salama .

  Ndugu waandishi wa habari : Tangu nimeona watu wote waliohama ,kusaliti vyama vyao, maisha yao yamekuwa mabaya, nahata imani kwa Wananchi wao imepungua. Hivyo na Mimi  sitaki kuwa kama wao, ninania ya dhati ya kukitumikia chama changu kwa uaminifu mkubwa kama ambavyo wao wameniamini.

  Kuliko kuhama Chadema ni heri mkanitafutie Mahala pengine pakuishi ambapo itakuwa ni mbinguni lakini sio hapa duniani ama kwenda kwenye Chama kingine chochote  cha kisisasa.  Kikubwa napenda kuwaeleza wana chama wote wa Chadema kuwa hivi sasa kila mmoja  tujielekeze kwa nguvu zetu zote kwenye kampeni hivi za uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.msikubali kutolewa kwenye maandalizi ya uchaguzi.

  Imetolewa leo Novemba 23/2017
  Christina Mwagala, Ofisa Habari na Msemaji Mkuu wa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam.

  0 0

  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amemnadi mgombea nafasi ya Udiwani Ndugu John Cheyo Mabonde katika uchaguzi mdogo kwenye Kata ya Nata iliyopo katika jimbo hilo la Nzega Vijijini huku akiwaahidi wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi kuwa wataibuka na ushindi wa kimbunga.

  Akiwa katika Kitongoji cha Udutu, Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Dk. Kigwangalla aliweza kumnadi Mgombe huyo wa Udiwani ambapo aliwataka wananchi wa Kata hiyo kujitokeza kwa wingi kumpigia kura za NDIYO ili aweze kushinda nafasi hiyo ili kumuongezea Rais Magufuli watendaji wa kumsaidia kumletea maendeleo ikiwemo Uchumi.

  “Nawaombeni sana, siku ya Jumapili wananchi kujitokeza kwa wingi sana na kuichagua CCM kupitia mgombea wake Bwana John Cheyo Mabonde ili awe Diwani wa Kata hii ya Nata. Kura zenu zitasaidia chachu ya maendeleo kwa Kata hii pamoja na jimbo kwa ujumla na kufanya itimie ile namba tatu! Yaani Rais wa CCM Mh.Magufuli, Mbunge wa CCM, Mimi Kigwangalla na Diwani wenu Mabonde.” Alisema Dk.Kigwangalla wakati akimnadi Mgombea huyo wa Udiwani Bwana Mabonde. Aidha, Dk.Kigwnagalla aliongeza kuwa, CCM itapata ushindi wa kishindo kwani kwa sasa wapinzani wamekosa mwelekeo na wameamua kurudi CCM kwa kuunga juhudi za Rais Magufuli.

  “Kwa sasa historia imeandikwa. Hii ni kwa kura zenu wana Nzega. Muliichagua mimi kuwa Mbunge wenu kwa tiketi ya CCM na Rais akanipa nafasi ya Unaibu Uwaziri ndani ya miaka miwili akanipa tena nafasi ya Uwaziri ili ni jambo la kubwa sana kwani ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wanaNzega na sasa yametimia. Kwa kulipa shukrani hizi ni kwa kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi CCM” Alimalizia Dk. Kigwangalla. Kwa upande wake Mgombea wa Udiwani huyo Bwana Mabonde wakati wa kutoa sera zake, aliweka wazi kuwa, amejipanga kumsaidia Rais Magufuli katika vita mpya ya Uchumi aliyoianzisha.

  “Naombeni kura ilikuwasaidia Wananchi wenzangu wa Nata. Kura zenu zitaongeza chachu ya kumsaidia Rais Magufuli katika uchumi ambao unaanzia chini ngazi ya mwananchi mmoja mmoja hadi juu. Vita hii ya kiuchumi ni yetu sote. Tuwapuuze wapinzani wanaopita huku kwani tunaanza kuwashuhudia wakihama vyama vyao na kuungana na CCM.” Alieleza Mgombea huyo wa Udiwani Bwana Mabonde.

  Pia alimshukuru Mh Mbunge kwa kuendeleza utekelezaji wa ahadi yake ya kusaidia wananchi ikiwemo Kata hiyo na Kata zingine ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini ambapo alisema atashirikiana nae bega kwa bega katika kufanikisha jimbo hilo linaendelea kubaki mikononi mwa CCM vipindi vyote.

  Kampeni hizo zitaendelea mpaka Novemba 25 jioni ambapo siku ya Jumapili ya Novemba 26 ndipo kutafanyika uchaguzi rasmi. Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo wa awali kufariki dunia hivyo nafasi kuwa wazi kwa muda mrefu.
  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimnadi Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde katika Kitongoji cha Udutu, Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 22,2017

  0 0

  Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas  amesema Maafisa Habari na Mawasiliano hapa nchini wanatakiwa kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali ikiwemo Uchumi, siasa na jamii katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

  Dkt. Abbas ameyasema hayo leo, Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya Itifaki na Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi yaliyoandaliwa na Idara ya Habari MAELEZO kwa kushirikiana na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na  Washauri wa Kidiplomasia wa Kiuchumi (Economic Diplomacy Consultants).

   "Itifaki ni moja ya eneo ambalo Afisa Habari yoyote anatakiwa kulijua kwa undani kutokana na jukumu alilonalo la kusimamia matukio mbalimbali yanayotokea katika Taasisi yake," alisema Dkt. Abbas.

  Ameendelea kwa kusema, kuna kipindi Afisa Habari anapata wageni ambao ni wakuu wa nchi na kushindwa kujua namna ya viongozi hao wanavyotakiwa kukaa kutokana na vyeo vyao.Aidha, amesema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo mengine mengi ambayo Maafisa hao watakuwa wakiyapata kila wakati ili kuwapa uelewa katika maeneo mbalimbali ya masuala ya uchumi, siasa, jamii na katika sekta yenyewe ya mawasiliano.     

  "Itafika kipindi tutajifunza hata vyeo vya jeshi namna vinavyokuwa pamoja na majina ya vyeo vyao ambapo itarahisisha katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Maafisa Habari," alisema Dkt. Abbas.
  Mafunzo hayo ya Maafisa Habari na Mawasiliano  ni ya siku mbili ambayo yameanza leo Novemba 23 na yanatarajia kumalizika kesho Novemba 24, 2017.
   Mkurugenzi  Idara ya Habari Maelezo na Msemaji  Mkuu  wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akifungua mafunzo kuhusu Mawasiliano ya Kimkakati na Itifaki  kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali na Sekta Binafsi  (hawapo pichani) yanayofanyika kwa siku mbili  mjini Dodoma.
  Mkurugenzi  Idara ya Habari Maelezo na Msemaji  Mkuu  wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali na Sekta Binafsi wakati ufunguzi wa mafunzo yanayofanyika kwa siku mbili  mjini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)

  0 0

   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga,  Juma Abed akizungumza na waandishi habari mara baada ya kuahirisha kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika mapema wiki hii kikiwa na lengo la kujadili mikakati ya kimaendeleo ya Mkuranga.

  Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Mkuranga limeitaka wakala wa Barabara mijini na vijijini (Tarura) kushirikiana na halmashauri na viongozi wa ngazi za chini katika kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo husika.

  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya baraza la  Madiwani la halmashauri ya  mkuranga mwenyekiti wa baraza hilo, Juma Abed amesema tarura imekua ikifanya kazi zake bila kuwashirikisha madiwani hali ambayo inasababisha utendaji na utekelezaji wa miradi ya barabara kutotekelezeka kwa wakati.

  Aidha Abed amesema kuwa miradi ya ujenzi wa miundombinu  ya barabara ijengwe imara na kuachana na biashara ya ujenzi wa kila mwaka.
   Mkurugenzi wa halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza juu ya mikakati ya Halmashauri hiyo ikiwemo kuboresha miundo mbinu.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abed akiwa katika picha ya pamoja madiwani, watendaji wa Halmashauri.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekipiga marufuku Chuo Kikuu Ardhi kukodi makampuni ya kufanya kazi mbalimbali kwa niaba yake.

  Amesema kitendo hicho kinaharibu kazi na sifa ya chuo hicho kwa kuwa baadhi ya makampuni wanayoyapa kazi hayakidhi vigezo.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 23, 2017) kwenye ufunguzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu Ardhi.

  “Kama kuna umuhimu wa kufanya kazi na kampuni ni bora muanzishe kampuni ya kwenu itakayofanya kazi vizuri ili kujiepusha na matatizo.”Pia Waziri Mkuu amekiagiza chuo hicho kufanya tafiti zenye kuleta majibu ya maswali na changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa na Dunia.

  Ametaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi, ujenzi holela, uharibifu wa mazingira na majanga ya asili kama mafuriko.Amesema Serikali inaamini kuwa matokeo ya kazi zinazofanywa na chuo hicho zikiwemo tafiti ni chachu ya maendeleo ya taasisi za elimu ya juu.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa imeweka mkazo wa kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kupato cha kati ifikapo 2025, hivyo wanahitajika wataalamu wa kutosha na wenye weledi.“Hivyo Chuo Kikuu cha Ardhi kama taasisi ya Serikali inawajibu mkubwa wa kutayarisha wataalamu mbalimbali wa sekta za ujenzi, ukadiriaji majenzi na uhandisi wa mazingira.

  Pia Waziri Mkuu amewataka watumie fursa hiyo ya kuadhimisha miaka 10 ya chuo hicho kujitafakari na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuwekeza zaidi ili kuongeza tija ya uwepo wa taasisi hiyo kwa jamii na Taifa kwa ujumla.“Wekeni mikakati madhibuti itakayowezesha chuo kupiga hatua kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 10 ijayo. Siku zote mjikite katika kutafuta kuwa na ubora zaidi ya wakati uliopita.”

  Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema Serikali inakkitegemea chuo hicho katika kufanikisha ajenda yake ya uchumi wa viwanda kwa kuwa kinatoa wataalamu wengi.

  Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya, Mwenyekiti wa Baraza la chuo Bibi Tabitha Siwale, Makamu Mkuu wa chuo Profesa Evaristo Liwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  ALHAMISI, NOVEMBA 23, 2017.

  0 0

  Naibu waziri  wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi wa mkoa wa Lindi kuacha dhana potofu kuwa kingatiba za matende na mabusha zina madhara.Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji wa mabusha na ngirikokoto(henia) kwa wananchi 200 ambapo zoezi hili limedhafadhiliwa na kampuni ya utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi ya Statoil mjini hapa.

  Naibu waziri afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt.Faustine Ndugulile amewataka wananchi wa mkoa wa Lindi kuacha dhana potofu kuwa kingatiba za matende na mabusha zina madhara Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji wa mabusha na girikokoto(henia) kwa wananchi 200 ambapo zoezi hili limedhafadhiliwa na kampuni ya utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi ya Statoil mjini hapa.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dkt. Faustine Ndugulile(wa pili kulia) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 264 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Statoil, Bw. Oyotein Michelsen. Fedha hizo ni kwa ajili ya kambi za upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa watu wapatao 400 kwa mwaka 2017 na 2018.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dkt. Faustine Ndugulile akihutubia wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa wagonjwa wapatao 200 wa Manispaa ya Lindi.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akipokea mashine ambayo ina kisu cha moto ambacho kinazuia damu wakati wa upasuaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Statoil.
   Mkurugenzi wa Statoil, Bw.Oyotein Michelsen akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa kambi ya upasuaji inayofanyila kwenye hospitali ya rufaa ya Sokoine mkoani Lindi.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amezitaka Halmashauri za Wilaya, Mji na Manispaa Mkoani Dodoma kuhakikisha zinatenga asilimia kumi (10%) ya makusanyo yao ya ndani kwa ajili ya vijana, wanawake na Walemavu kuanzisha miradi ya viwanda vidogo na vya kati.

  Lengo ni kuitikia kampeni ya Serikali inayoitaka Mikoa kuanzisha viwanda kama ilivyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Seleman Jafo.

  Akizungumzia hilo, ameonya tabia ya baadhi ya Halmashauri kutotoa asilimia kumi (10%) ya makusanyo yake ya ndani au kutoa kiasi kidogo kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu na kuwa utaratibu unaotumika sasa wa Halmashauri kukopesha fedha hizo wakati mwingine sio muafaka sana badala yake Halmashauri zitumie fedha hizo kuwafungulia vijana, wanawake na walemavu viwanda vidogovidogo na kuwakabidhi waendeleze uzalishaji na kuviendesha.

  Dkt. Mahenge amebainisha hayo wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Wilaya za Mkoa wa Dodoma kujitambulisha na kukagua miradi ya maendeleo ambapo amesema kuwa viwanda vinavyoweza kuanzishwa ni vya uchakataji wa nafaka, usindikaji mazao na utengenezaji vyakula vya Mifugo.

  Amesema kuwa asilimia kumi hiyo ikitumika na kusimamiwa vizuri inaweza kutekeleza kampeni ya kuanzisha viwanda ambapo vijana na wanawake wanaweza kufaidika kuanzia ngazi za chini kama vijijini kwa kupata ajira kipato na halmashauri kupata ushuru. 

  Aidha, ameongeza kuwa mbali na uanzishaji viwanda miradi mingine Halmashauri inayoweza kuwaanzishia vijana, wanawake na walemavu ni pamoja na ufugaji samaki kwa kuwachimbia mabwawa.

  Ametaja miradi mingine mbali na viwanda kuwa Halmashauri zinaweza kuchimba visima na kujenga miundombinu ya umwagiliaji ili vijana, wanawake na walemavu waendeshe kilimo cha umwagiliaji kuzalisha mazao mbalimbali ambayo yanaweza kuwa malighafi kwenye viwanda vinavyoanzishwa.

  “Sisi ni Viongozi, maana ya kuwa viongozi ni pamoja na kuwasaidia wananchi kuweza kufanya maamuzi yenye manufaa kwao na uanzishwaji wa viwanda utawanufaisha wananchi wengi na Mkoa kwa ujumla” alimalizia Dkt. Mahenge.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selamani Jafo akifungua kongamano ya Chama cha Wahasibu Tanzania  linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa linalofanyika Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa Kongamano linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
  Washiriki na wajumbe wa chama cha Wahasibu Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Ufunguzi wa Kongamano lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe.Selemani Jafo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo(kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa wakati wa Ufunguzi wa Kongamano linalofanyika Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo(Katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wahasaibu Tanzania pamoja na wawwezeshaji wa Kongamano hilo.

  Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo  amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwenye Halmashauri ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa kongamano la siku mbili la Chama cha Wahasibu Tanzania(TAA) lililojumuisha wataalam wa Hesabu na wafanya maamuzi kutoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

  Katika Kongamano hilo ambalo Linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Chama hicho mwaka 1983 limelenga kujenga uwezo kuhusu Uwazi na Uwajibikaji kwa Viongozi waandamizi wa Mamlaka ta Serikali za Mitaa katika Matumizi ya Fedha za Umma.

  Waziri Jafo amesema kuwa Bajeti kubwa ya Serikali inapelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa takribani asilimia 20.7 ya Bajeti ya Serikali huelekezwa katoka Halmashauri hivyo ni eneo ambalo linapata  Fedha nyingi na zinahitajo uangalizi mkubwa.

  Tunafahamu kuwa Viongozi wa Halmashauri mna Mamlaka kamili ya kupanga matumizi ya Fedha hizo lakini angalieni maeneo ambayo yataleta Tija kwa Wananchi na yatatatua changamoto zinazowaathiri wananchi wetu katika maisha yao ya kila siku, huko ndio sehemu ya kutumia  Fedha nyingi na si vinginevyo.

  Katika maeneo ambayo hayanipi amani na bado nayaona kuwa na matumizi mabaya ya Fedha ni eneo la Manunuzi ya Umma nawasihi muwaelimisha vya Kutosha viongozi hawa namna ya kudhibiti mianya yote ya Upotevu wa Fedha uliopo katika eneo la Manunuzi"
  Alisema Jafo.

  Aliongeza kuwa kuna tabia ya kubadilisha matumizi ya vifungu"Realocation" bila sababu za Msingi na bila kufuata taratibu zinazohitajika suala hili limekua likisababisha hoja nyingi wakati wa Ukaguzi wa Hesabu nawasili viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa mkaliangalie hilo kwa jicho la tati na mkalidhibiti.

  Akitoa neno la Ufunguzi Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzani  Fred Msemwa amesema Chama hiki kina umri wa Miaka 34 na kina lengo la kuendeleza Taaluma za Uhasibu Tanzania na kutoa elimu ya Fedha na Biashara kwa wananchi ili waweze kujisimamia katika mapato na matumizi yao.

  Msema alisema kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ya Kodi, Ongezeko la Thamani,sheria za Fedha na mabadiliko yake pamoja na kuanzisha Dawati la Mhasibu ambalo hutoa uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya Fedha, biashara na Rasilimali.

  Kongamano hili ni endelevu na litakua likifanyika kila mwaka  na litakuwa likiwajengewa uwezo viongozi wa Serikali ambao wengine hawana utaalam wa Uhasibu namna ya kuipitia kwa umakini taarifa ya Mkaguzi wa Ndani, viashiria vya Rushwa katika matumizi ya Fedha za Umma, kuzuia vihatarishi, namna ya kuongeza vyanzo vya mapato na namna ya kupata Fedha za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

  0 0


  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili – MUHAS Kampasi ya Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma za Hospitali Prof. Said Abood. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 25 Novemba 2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili – MUHAS Kampasi ya Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma za Hospitali Prof. Said Abood na Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jonas Kamaleki. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 25 Novemba 2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) anayeshughulikia Huduma za Hospitali Prof. Said Abood akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili – MUHAS Kampasi ya Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura Dk. Hendry Sawe. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 25 Novemba 2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili – MUHAS Kampasi ya Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jonas Kamaleki, Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) anayeshughulikia Huduma za Hospitali Prof. Said Abood. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 25 Novemba 2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.Picha na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0

   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika boti kuelekea katika kisiwa cha Mafia ikiwa ni ziara ya kuangalia shughuli za maendeleo ya Uvuvi katika kisiwa hicho ambacho kinategemea kipato chake kwa ajili ya mazao ya baharini .
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Mafia juu ya usimamizi wa shughuli za uvuvi ambazo zinafanyika katika kisiwa cha Mafia
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akikagua kiwanda cha uchakataji samaki kilichopo Mafia ambacho ni kiwanda cha uchakataji samaki kwa ajili ya usafirishaji .
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akipokea ripoti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaib Ahmed Nnunduma (kulia) jinsi shughuli za Uvuvi zinazofanyika katika Kisiwa hicho .
   Watalii wakimuangalia samaki aina ya Papa Potwe ambaye anapatikana Tanzania kwa miezi mitano wakati sehemu nyingine anakaa miezi miwili.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Mafia.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amefanya ziara katika Kisiwa cha Mafia kwa ajili kukagua shughuli za uvuvi pamoja na kumuona Samaki aina Papa Potwe.

  Akizungumza na Wavuvi , Watendaji wa Kisiwa hicho, Ulega amesema kuwa sekta ya Uvuvi inatakiwa ilete maendeleo ikiwa rasilimali hizo zitatumika ipasavyo.Ulega ameiagiza  Halmashauri ya Mafia ndani ya siku saba kuhakikisha wavuvi wapate barafu kwa kuuziwa bei ya chini ili kuweza kupata mapato.

  Amesema kuwa wananchi wa Mafia hawaelewi maana ya Hifadhi ambapo wanatakiwa kupewa elimu ili kuondokana na mgogoro wa hifadhi.
  Ulega amesema Halmashauri  inashindwa kupata mapato ya kujiendesha kutokana  na kutokuwa wabunifu juu ya kutengeneza mapato ikiwa pamoja  kuwasumbua wananchi kwa vitu visivyo na mapato.

  Aidha amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli amefuta ushuru kwa wafanyabiashara wanaochukua biashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Amesema kuwa hakuna sheria ndogo inayozidi sheria Mama juu ya Halmashauri Mafia kutunga sheria ndogo ya kuchukua ushuru wa mazao ya bahari yanayotoka wilaya moja kwenda nyingine wakati sheria hiyo ilishafutwa.


  0 0

   Injinia Mratibu wa maswala ya Mazingira Baharini kutoka ZMA Halfani Hamad Hassan kulia akitoa maelezo kuhusiana na zoezi la vitendo la Udhibiti wa Usambaaji wa mafuta yaliomwagika Baharini katika Mkutano wa kufunga mafunzo hayo uliofanyika Hoteli ya Marumaru Forodhani mjini Unguja.
   Mkuu wa Kituo cha Huduma za Dharura Norwey Helge Munkas Andersen kushoto akionesha namna ya zoezi zima la mafunzo ya  Udhibiti  Usambaaji wa mafuta yaliomwagika Baharini katika Mkutano wa kufunga mafunzo hayo uliofanyika Hoteli ya Marumaru Forodhani mjini Unguja.
   Mkuu wa Kituo cha Huduma za Dharura Norwey Helge Munkas Andersen akijibu baadhi ya maswala yalioulizwa katika Mkutano wa  Ufungaji  mafunzo ya  Udhibiti  Usambaaji wa mafuta yaliomwagika Baharini  uliofanyika Hoteli ya Marumaru Forodhi mjini Unguja.
   Naibu Katibu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji,  Shomari O,Shomari akitoa hotuba ya ufunguaji wa  mafunzo ya  Udhibiti  Usambaaji wa mafuta yaliomwagika Baharini yaliochukua muda wa siku Tatu hafla iliofanyika  Hoteli ya Marumaru Forodhani mjini Unguja.
  Naibu Katibu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Shomari O,Shomari (kulia) akimkabidhi cheti cha Ushiriki wa mafunzo ya Udhibiti  Usambaaji wa mafuta yaliomwagika Baharini Injinia Mratibu wa maswala ya Mazingira Baharini kutoka ZMA Halfani Hamad Hassan katika ufungaji wa mafunzo hayo katika Hoteli ya Marumaru Forodhani mjini Unguja.

  PICHA NA YUSSUF SIAMI/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Mkurugenzi wa Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga(katikati) akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa kutambulisha wasanii watakaopanda katika jukwaa la Tigo Fiesta siku ya jumamosi viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam leo mchana. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na wengine ni wasanii.
  Msanii Ben Pol akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya wasanii wa kiume
   Msanii Vanessa Mdee akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya wasanii wa kike
   Msanii Barnaba akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo
  Mdau akipata picha na msanii Vanessa
  Wasanii Aslay na Rich Mavoko wakisalimiana jna wafanyakazi wa duka la Tigo Mlimani city walipotembelea duka hilo leo mchana
  Msanii Barnaba akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo
  Mkurugenzi mkuu wa Tigo Tanzania Simon Karikari akisalimiana na msanii Vanessa Mdee

  0 0

   Bondia Mtanzania Ibrahim Class Mgendera, anatarajia kutetea ubingwa anaoushikilia wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight dhidi ya bondia kutoka nchini Afrika Kusini

  Pambano hilo la kimataifa la ngumi za kulipwa ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Vodacom PLC pamoja na kampuni ya Azam, litafanyika jijini Dar es Salaam Novemba 25 2017 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

  Mgendera anashikilia ubingwa wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight”ambao alioutwaa nchini Ujerumani tarehe 1 Julai, 2017 kwa kumpiga Jose Forero wa Panama. Bondia huyo atakuwa ni kibarua kigumu cha kutetea taji hilo mbelea ya KOOS SIPHO SIBIYA kutoka AFRIKA YA KUSINI

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi,Yusuph Singo alisema maandalizi ya pambano hili yalianza siku tarehe 5 August siku ya hafla ya kumpongeza bingwa huyo ambapo mgeni  alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Harrison Mwakyembe ambapo Uongozi wa  bondia hiyo ilimwelezea Waziri mwenye dhamana na michezo kwamba, mkanda huo unapaswa kutetewa katika kipindi cha miezi mitatu tangu alipoupata na tayari kulikuwa na ofa mezani za kuutetea mkanda huo kutoka katika nchi za Marekani, Ujerumani na Ufilipino.

  “Mheshimiwa alisikiliza hoja hizo na kuweza kuzifanyia kazi kwa kuwatafuta wadhamini na wadau wa michezo nchini ili kuwezesha pambano la kutetea mkanda huo lifanyike hapa nyumbani kwa kuhamasisha mchezo wa ngumi za kulipwa pamoja na kuwapa burudani mashabiki wa mchezo huo hapa nchini,alisema Singo

  Nikiwa kama mwenyekiti wa maandalizi ninapenda kutoa shukurani zetu za dhati kabisa kwaniaba ya mheshimiwa waziri kwa Wadhamini wakuu wa masumbwi haya AZAM pamoja na Vodacom Tanzania PLC,kamati ya pamoja ya kufanikisha pambano hilo ikijumuisha Baraza la Michezo la Taifa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Menejimenti ya Joe’s Gym na Kamishei ya Ngumi za Kulipwa Tanzania.

  Akizungumzia kuhusu udhamini wao, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC,Matina Nkurlu alisema kampuni yao imeamua kutoa udhamini ikiwa kama ni sehemu yake katika kuendeleza na kukuza mchezo wa ngumi

  “Vodacom imekuwa ikiendeleza na kudhamini  michezo mbali mbali hapa nchini ikiwamo soka ambapo sisi ndiyo wadhamini wakuu wa Ligi ya Tanzania bara(VPL). Udhamini wetu hauishi tu kwenye soka bali kwenye michezo mingine mingi tunapenda kutoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na vilevile tutawawekea na bidhaa mbalimbali ukumbini hapo na watazipata kwa bei nafuu kabisa na pia tutatoa elimu kwao kuhusiana na kifurushi chetu kilichopo sokoni kwa sasa cha Pinduapindua,” alisema Nkurlu

  Bondia atakayepambana na Mgendera anatarajia kuwasili nchini tarehe 22 Novemba, 2017. Pambano hilo  litanogeshwa na mapambano ya utangulizi ya kimataifa likiwakutanisha mabondia kutoka Tanzania na Malawi, mabondia wanawake pamoja na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii nguli wa muziki wa kizazi kipya.

   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu (kushoto)akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,  wakati  wa kuwatambulisha  Bondia Mtanzania Ibrahim  Mgendera(Katikati) anayetarajia kutetea ubingwa wake wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight dhidi ya bondia kutoka Afrika ya Kusini KOOS SIPHO SIBIYA(hayupo pichani)  Pambano hilo la kimataifa la ngumi za kulipwa  limedhaminiwa na Vodacom Tanzania na Azam TV na  litafanyika  jumamosi  kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam,Kulia ni Mkuzaji wa Vipaji  vya ngumi Tanzania, Joe Anea.
   ondia Mtanzania,Ibrahim Mgendera(Kushoto)atakaye utetea ubingwa wake wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight” (kushoto) na bondia kutoka nchini Afrika Kusini,KOOS SIPHO SIBIYA wakitambulishwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC,Matina Nkurlu kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa mkutano na vyombo vya habari  uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, pambano hilo  la kimataifa la ngumi za kulipwa limedhaminiwa na Vodacom Tanzania,Azam TV litafanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akishuhudia mabondia Ibrahim Mgendera kutoka Tanzania na kocha wake (wapili kushoto)na bondia kutoka nchini Afrika Kusini,KOOS SIPHO SIBIYA na kocha wake(wapili kulia)wakitambulishwa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa mkutano na waandishi hao uliofanyika Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,  pambano hilo  la kimataifa la ngumi za kulipwa limedhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC, AzamTV litafanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,Katikati ni mwamuzi wa mpambano huo wa Kimataifa  kutoka nchini Ujerumani, Arno Pokrandt.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za ujenzi wa Zahanati na Shule kata za Ludete na Kakubilo Halmashauri ya Geita kwa kuchangia matofali yenye thamani ya shilingi 2,400,000/= na kufanikisha harambee ya mifuko ya Saruji zaidi ya 420.

  Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za wananchi  baada ya kutembelea kata hizo na kuridhishwa na kazi za ujenzi wa Zahanati za vijiji na Shule zinazofanywa na wananchi kwa kujitolea kufanya kazi bila malipo, kuchangia vifaa mbalimbali vya ujenzi na kuchimba misingi.

  Akiwa Kata ya Ludete Mkuu wa Mkoa amesema " Nimefurahi sana kuona namna mnavyoshiriki katika utekelezaji wa miradi hii niwaombe mshiriki kuanzia mwanzo hadi mwisho na msikubali mtu yeyote kuwavunja moyo kwa kuwa maendeleo ya Ludete yataletwa na wananchi wenyewe hivyo mimi ninawachangia matofali 1000 kwa ajili ya Zahanati na mengine 1000 ya kujenga vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Ludete".

  Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Benedicto Mranda amesema kuwa wananchi wameamua kujitolea kushiriki  ujenzi wa Shule mpya ya msingi baada ya shule ya Msingi Ludete kuwa na Idadi ya wanafunzi 6,616  huku kukiwa na madarasa 20 yenye mikondo 108 ambao unasababisha msongamano wa wanafunzi darasani. 

  Marando ameongeza kusema kuwa Kata ya Ludete haina Zahanati kwa muda mrefu hivyo wananchi wamejihamasisha kujenga ili wapate huduma katika maeneo yaliyo jirani pia kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na shule ya msingi na Sekondari kwa Kata, Kata ya ludete ina wanafunzi 900 wanaotarajia kujiunga na elimu ya Sekondari ikiwa na uhaba wa zaidi ya vyumba vya madarasa 20.

  Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa amefanya harambee ambayo imefanikisha upatikanaji wa mifuko ya Saruji zaidi ya 420 na kuziagiza Halmashauri kutumia vikundi vya mafundi waliokatika maeneo ya miradi ili kupunguza gharama na kusimamia matumizi ya fedha za miradi hiyo.

  Kutokana na Mkoa wa Geita kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Serikali imeamua kushirikiana na wananchi kufanya kampeni ya mkoa mzima kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki na kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo ili wananchi wapate huduma katika majengo bora na mazingira salama.
  Mheshimiwa Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita akitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Geita na kata ya kakubilo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Halmashauri hiyo kuhamasisha ujenzi wa Zahanati na vyumba vya madarasa.
   Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishirikiana na wananchi wa Kata ya Ludete Wilayani Geita kumwaga zege kwa ajili ya lenta kwenye ujenzi wa madarasa 10 ya shule ya msingi Ludete yenye wanafunzi 6,616  alipokwenda kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

   Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na mafundi kupandisha ndoo yenye zege kwa ajili ya uwagaji wa leta katika majengo 10 ya vyumba vya madarasa shule ya Msingi Ludete Wilayani Geita.
   Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akikabidhi fedha shilingi 2,400,000/= kwa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Mranda kwa ajili ya ujenzi wa boma la Zahanati ya Kijiji na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika hiyo.
   Wananchi wa kijiji cha Ludete Kata ya Ludete Wilayani Geita wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Geita za kila kijiji kuwa na Zahanati.
   Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akifuatilia kwa karibu maendeleo ya wanafunzi wa kidato cha Tatu shule ya Sekondari Kakubilo Halmashauri ya Geita baada ya kutembelea shule hiyo na kutoa swali la Hisabati kwa wanafunzi hao.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu), akikagua gwaride la heshima wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu) na Meja Jenerali Simon Mumwi (Mstaafu) (kulia aliyesimama kwenye gari), wakisukumwa kwenye gari inayotembea mwendo wa taratibu kuashiria kumalizika kwa utumishi wao katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakati wa hafla ya kuwaaga, iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu) akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Venance Mabeyo, baada ya kumaliza utumishi katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa jeshi hilo, iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
  Gwaride la Heshima likipita mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu), wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu) na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dk. Florens Turuka(kulia), wakizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Ambapo Meja Jenerali Rwegasira (Mstaafu), aliagwa baada ya kumaliza utumishi wake katika jeshi hilo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu), akizungumza na Meja Jenerali James Mwakibolwa wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Ambapo Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu),aliagwa baada ya kumaliza utumishi wake katika jeshi hilo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, Jenerali Venance Mabeyo,
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu), akiagana na Meja Jenerali, James Mwakibolwa baada ya hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Ambapo Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu), aliagwa baada ya kumaliza utumishi wake katika jeshi hilo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

  The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment giving out the speech at the Bank’s 10 years’ anniversary event, yesterday at Serena Hotel.
  CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah giving out his very exciting and energetic speech during the 10 years’ corporate anniversary event, which took place yesterday at Serena Hotel.
  Deputy Managing Director of BANK OF AFRICA –TANZANIA, Mr. Wasia Mushi giving out his opening remarks and introducing the entire BANK OF AFRICA team present at the 10 years’ corporate anniversary event, which took place yesterday at Serena Hotel.
  CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah hands over a copy of his speech to the guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment.
  The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment in jovial moment while listening to the speech from CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah. To his left hand side is the Board Chairperson of BANK OF AFRICA-TANZANIA, Ambassador Mwanaidi S. Maajar.
  The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment, accompanied by the Board Chairperson of BANK OF AFRICA-TANZANIA, Ambassador Mwanaidi S. Maajar and CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah to take part in a great spread of amazing foods available at the event yesterday.
  The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment together with Board Chairperson of BANK OF AFRICA-TANZANIA, Ambassador Mwanaidi S. Maajar and CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah; in group photo with a section of esteemed clients of the Bank who attended the corporate 10 years anniversary dinner gala.older | 1 | .... | 1438 | 1439 | (Page 1440) | 1441 | 1442 | .... | 1898 | newer