Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

STANDARD CHARTERED BANK MWENYEJI WA ‘ONE BELT- ONE ROAD’ (OBOR) AFRICA-CHINA ROADSHOW

$
0
0
   Mgeni Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akihutubia waalikwa mbalimbali kuhusu fursa zinazopatikana katika uwekezaji. (OBOR Initiative) katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Stanchart bank jana,
    Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa katika hafla fupi ya chakula cha jioni ambayo Standard Chartered Bank iliwaandalia wateja wake ambao ni wenyeji kutoka China.
   Bw. Sun Chengfeng, Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania akizungumza na waalikwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam
   Mgeni rasmi Mh. Charles Mwijage Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji akibadilishana mawazo na Bw, Chengfeng , Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na standard charterd bank
 Wawakilishi kutoka standard chartered bank china, pamoja na afisa mtendaji mkuu wa standard chartered bank Tanzania wakimsikiliza kwa makini Mh. Waziri Mwijage.
     Wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi,Bw Sanjay Rughani, Bw.Sun Chengfeng na wawakilishi mbalimbali katika kitengo cha uchumi na biashara wanaoiwakilisha China nchini Tanzania

 Waalikwa mbalimbali wakimsikiliza bi. Maggie Li alipokuwa akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni ambayo standard chartered iliwaandalia wateja wake wenyeji kutoka nchini China
 Afisa mtendaji mkuu wa benki ya Standard Chartered Tanzania Bw. Sanjay Rughani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu OBOR initiative katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency
 Afisa mtendaji mkuu wa Standard Chartered Bank Tanzania Bw. Sanjay Rughani (kushoto), Bi. Maggie Li Mkuu wa kitengo cha biashara na mauzo katika benki ya Standard chartered China(katikati), pamoja na Bw. Cleophas Ruhumbika ambae ni mwakilishi wa katibu mkuu wa viwanda na uwekezaji (kulia). Wakizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika jana.


 Vijana kutoka kundi la Tanzania House of Talent (THT) wakitoa burudani kwa wageni na waalikwa wa standard chartered bank katika hafla iliyoandaliwa katika hoteli ya Hyatt Regency.
  Burudani kutoka kundi la THT ikiendelea

BALOZI WA JAPAN ATEMBELEA WIZARA YA MADINI

$
0
0
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida,  Novemba 21, 2017 alitembelea Ofisi za Wizara ya Madini za jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki na Naibu wake, Stanslaus Nyongo ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini nchini.

 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akijadiliana jambo na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto). Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto). Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).

 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (Kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (hayupo pichani). Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akijadiliana jambo na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto) alipotembelea Ofisi za Wizara. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo. Masuala mbalimbali ya Sekta ya Madini nchini yalijadiliwa ikiwemo uwepo wa fursa za uwekezaji.

RC MAKONDA ATINGA OFISI ZA CLOUDS MEDIA GROUP KUWAPA POLE.

$
0
0

 Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar,ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda wamefika mjengoni Clouds Media Group kutoa pole  na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar.Pichani wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwa.Joseph Kusaga.
  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar,ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda wakipata maelezo mafupi mara baada ya kufika katika jengo la Clouds Media Group kutoa pole  na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni  ya Clouds Media Group Bwa.Joseph Kusaga mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo kutoa pole  na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar.Pichani kati ni Mmoja wa Maafisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Simon  Simalenga

VIONGOZI WILAYANI HANDENI WASHIRIKI UJENZI KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI NGUVU KAZI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wakikagua moja ya darasa Shule ya Sekondari Kiva.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na viongozi wengine wakishiriki kujaza zege kwenye ndoo kwaajili ya kumwaga kwenye jamvi la matundu ya vyoo.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akishiriki kujaza zege kwa ajili ya kumwaga kwenye jamvi la matundu ya vyoo na viongozi wengine.
 fundi mkuu wa ujenzi wa madarasa na vyoo akitoa maelezo kwa viongozi juu ya ujenzi wa matundu ya vyoo​
baadhi ya wafanayakazi wakiendelea na kazini
 ​Mkuu wa Wilaya ya Hnadeni Mh.Godwin Gondwe akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zavuza kwenye mkutano wa hadhara​
 ​moja ya jengo la darasa linaoendelea kujengwa​
 ​baadhi ya wananchi walioshiriki Mkutano wa Hadhara.
  ​Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.Wiliam Makufwe akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwechigwe wakati wa uhamamsishaji wananchi kushiriki nguvu kazi.

KAMATI YA USALAMA BARABARANI YAADHIMISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA KWA KUCHORA ALAMA ZA VIVUKO VYA WAENDA KWA MIGUU (zebra)

$
0
0

 Mafundi wa kampuni ya Minica Ltd, kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama Barabarani na Benki ya Stan Bic, wakichora alama za kivuko cha waenda kwa miguu 'Zebra' katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi katika makutano ya Taa za kuongozea magari za Ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam, leo mchana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama inayoendelea. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Mafundi wakiweka alama kabla ya kuanza kuchora
Mafundi wakiendelea kuchora alama
Mdau akishiriki kuchora alama

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. JAPHET HASUNGA AAGIZA KUUNDWA KWA CHOMBO CHA KUDHIBITI UBORA WA MAZAO YA MISITU NCHINI

$
0
0


Na Hamza Temba – WMU

..........................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kubuni utaratibu mpya ikiwemo kuanzishwa kwa chombo kitakachosimamia upangaji wa madaraja ya ubora wa mbao zinazozalishwa hapa nchini ziweze kukidhi viwango vya mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo jana kwenye kikao cha majumuisho na watumishi wa Shamba la Miti la Serikali la Kiwira ambalo linasimamiwa na wakala huyo wakati anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

“Kuna changamoto kubwa kwenye soko la mbao, kwa kiwango kikubwa mbao zetu nyingi tunaziuza hapa nchini, Lazima tufike mahali hizi mbao tuwe tunaziexport (uza nje) kwa kiwango kikubwa. Lakini ili tufikie malengo hayo mbao zetu lazima ziwe kwenye kiwango kinachokubaliwa.

“Mbao zinazokuwepo kwenye soko letu la ndani huwezi kuzitenganisha kwamba hizi ni za TFS au za mwananchi wa kawaida, nyingine zina ubora nyingine hazina, agizo langu kwenu kaeni chini kama watendaji tuje na utaratibu utakaotuwezesha kuzipanga kwenye madaraja, daraja la kwanza, la pili, la tatu au la nne ili mnunuzi ajue ananunua mbao ya ubora wa aina gani,” alisema Hasunga.

Alisema amepata taarifa kuwa baadhi ya wananchi wanavuna miti ambayo haijakomaa jambo ambalo linaathiri ubora wa mbao kwenye soko kwa kutokidhi mahitaji ya wateja, hivyo akaagiza Wakala huyo kubuni mbinu mpya za kuwalinda wateja ikiwemo kuanzishwa kwa chombo maalum cha udhibiti wa ubora wake.

"Kwa maeneo mengine tuna TBS, kwenye chakuka tuna TFDA, kwenye mbao je? Nani anaregulate?(dhibiti), ni lazima tufike mahali tuwe na mdhibiti atakayetusaidia kuhakikisha kwamba ubora unakuwepo,” alisema Hasunga.

Aidha alitoa wito kwa taasisi hiyo kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuvuna miti ikiwa imeshakomaa ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa miche ya miti na kuhamasisha wananchi wapande miti zaidi kwa faida yao na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia nidhamu kwenye Utumishi wa Umma, Naibu Waziri Hasunga alisema Serikali ya awamu ya tano haitomvumilia mtumishi yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa, uzembe au uvivu kwenye kutekeleza majukumu ya Serikali kwa kua sifa hizo ni chanzo kimojawapo kikubwa cha umasikini nchini.

Kwa upande wa kampeni ya upandaji miti kitaifa, alisema Serikali itafuatilia nchi nzima kuona utekelezaji wa agizo hilo ambalo linaitaka kila Wilaya kupanda miti milioni moja na laki tano kwa mwaka ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha miti mingi zaidi inapandwa kwa kuwashirikisha zaidi wananchi.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Zawadi Mbwambo alisema taasisi hiyo imewahi kupokea malalamiko juu ya ubora hafifu wa baadhi ya mbao zinazopatikana kwenye soko ambazo baadhi ya wananchi hutumia jina la Shamba la Miti Sao Hill kuziuza na hivyo kuharibu sifa ya shamba hilo.

Alisema maagizo yote aliyoyatoa Naibu Waziri Hasunga yatafanyiwa kazi kupitia vikao halali vya kiutendaji vya taasisi hiyo ikiwemo vile vya kuandaa mikakati ya utekelezaji wa majukumu yake ya uhifadhi.


Awali Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa akiwasilisha taarifa yake kwa Naibu Waziri Hasunga, alisema shamba hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1964 likiwa na hekta 2,713 limekuwa na maendeleo mazuri ambapo mwaka 2016/2017 lilivuka malengo ya makusanyo ya mapato ya Serikali kutoka bilioni 1.3 hadi bilioni 1.7.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja (wa pili kushoto) alipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo akiongozana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (wa pili kulia) kwa ajili ya kujitambulisha wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika shamba hilo jana katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika shamba hilo jana katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Zawadi Mbwambo (kushoto) wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi kwenye Shamba la Miti Kiwira lililopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya jana.

Mti huu wa kumbukumbu ulipandwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1965 katika shamba la miti la Serikali  la Kiwira katika Wilaya ya Rugwe Mkoani Mbeya.
 Mti alipanda Mwalimu Nyerere mwaka 1965 katika shamba la miti Kiwira.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na watumishi wa Shamba la Miti Kiwira  wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi kwenye Shamba hilo katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya jana.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Zawadi Mbwambo akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya watumishi wa shamba la miti Kiwira.

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATOA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 102 KWA VIKUNDI 49 VYA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya mikopo ambayo iatawasaidia katika kuendeshea shughuli zao za biashara pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe Happiness Seneda aliyesimama akizungumza na vikundi vya wajasiriamali kutoka kata mbali mbali katika halfa fupi ya kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili mkopo wa kuwawezesha kiuchimi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda akizungumza jambo katika halfa fupi ya vikundi vya wajasiriamali.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza na vikundi vya wajasiriamari hao hawapo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuwawezesha mikopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.


PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU


……………..


NA VICTOR MASANGU, KISARAWE

HALMASHAURI YA wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kuwa na uchumi wa viwanda imetoa kiasi cha shilingi milioni 102 kwa vikundi vya wajasiriamali vipatavyo 49 vya wakinamama,vijana pamoja na walemavu kwa lengo la kuweza kuwasaidia kuendesha shughuli zao mbali mbali za biashara mbali mbali ikiwemo na kuwawezeha ili waweze kujikita zaidi katika kujenga viwanda vidogo vidogo.

Akizungumza katika halfa fupi ya kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyohuduriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa vikundi hivyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama alisema kwamba fedha hizo za mikopo zimetolewa kwa vikundi hivyo kutokea kata zote 17 ambapo zimetokana na makusanyo ya mapato ya ndani.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuweza kukuza uchumi wa nchi kutokana na kuweza kuwapa fursa wajarisiamali hao kupania wigo wa kibiashara pamoja na kuanzissha viwanda vingine vidogo vidogo ambayo vitaweza kuongeza upatikanaji wa ajira mpya na kupunguza wimbi la umasikini.

“Kwa kweli sisi kama halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejipanga kuweka mipango madhubuti katika kuviwezesha vikundi vyetu vya ujasiriamali kwa kutumia fedha zetu ambazo zinatokana na makusanyo ya mapato ya nadani, hivyo vikundi hiivi ni moja ya mipango yetu katika kuhakikisha ile asilimia 10 iliyotengwa inawafikia walengwa na kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo,”alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ameviasa vikundi vyote vilivyopata mkopo huo hususan kwa wakinamama kuachana kabisa na vitendo vya kutumia fedha hizo vibaya kwa shughuli ambazo hazina manufaa yoyote kwa jamii, kama vile kuwachezesha watoto wao ngoma wakati wa kufunga shule pamoja na kununulia madela kitu ambacho amekilaani vikali.

Aidha Seneda alisema kuwa malengo ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha wananchi wake wanawezeshwa kwa namna mbali mbali ikiwemo kuwapatia mikopo ambayo itaweza kuwapa fursa ya kukuza biashara zao pamoja na wengine kufanya biashara zao ndondogo amabzo zitaweza kuwapatia kipato na kujikwamua kiuchumi.

“Jamani mimi kama kiongozi wenu napenda kuwaasa wale wote mlionufaika na mkopo huu, kuhakikisha mnazitumia vizuri fedha hizi hasa kwa upande wa wakinamama ambao wamekuwa na tabia pindi wanapotata pesa wanazitumia katika matumizi mengine ya kununulia madela kwa ajili ya sare pamoja shughuli nyingine kama vile kuwacheza ngoma watoto wao hii tabia kwa kweli sipendi kuiona katika Wilaya yangu,”alisema Seneda.

Nao baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na mkopo wa fedha hizo akiwemo Monica Muhoza ambaye ni mlemavu wa miguu, Faudhia Kasikasi, pamoja na Gudluck Akyoo wameshukuru uongozi mzima wa halmashauri ya Kisarawe na kusema kuwa fedha hizo walizopatiwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao kwani zitaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi pamoja na kujikimu kimaisha na kuendesha familia zao.

VIKUNDI hivyo vya wajasiriamali 49 kutoka kata 17 za Wilayani Kisarawe zimewahusiha wakinamama, vijana, pamoja na makundi vya walemavu ambapo vimepata mkopo wa fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 102 ikiwa ni makusanyo ya mapato ya fedha za ndani.

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO NA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUFANIKISHA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI.

$
0
0
Na Clarence Nanyaro – NEC

Mwenyekeiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi nchini Kuwashirikisha Viongozi wa Vyama vya siasa katika maamuzi mbalimbali wanayofanya yenye maslahi kwa pande zote ili kuendeleza amani na utulivu ulipo nchini.

Akizungumza na Wasimamizi wa uchaguzi katika Manispaa ya Moshi, Jaji Kaijage alisema kuwa katika kipindi hiki ambapo vyama vinashiriki katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakafanyika Novemba 26,2017 ni muhimu kwa Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Maadili ya Uchaguzi wakati wa kampeni yanazingatiwa ili kuepusha uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.

Jaji Kaijage ambaye yuko katika ziara ya kutembelea Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha kushuhudia utekelezaji wa maadili ya Uchaguzi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani, amewataka Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Vifaa vyote ambavyo vinahitajika ili uchaguzi uweze kufanyika vimepatikana na vile ambavyo havijapatika wawasiliane na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kasoro zinazobainika ziweze kupatiwa ufumbuzi mapema kabla ya siku ya Uchaguzi.

Wakati katika mkoa wa Tanga Uchaguzi utafanyika Katika Kata ya Majengo iliyoko katika Halmshauri ya Mji Korogwe,Mkoani Kilimanjaro,Uchaguzi mdogo wa Udiwani utafanyika katika Kata ya Bomambuzi katika Manispaa ya Moshi na Katika Kata za Machame Magharibi ,WeruWeru na Mnadani katika Halmashauri ya Hai.

Aidha,Jaji Kaijage alitoa wito kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha Kuwa siku ya Upigaji Kura ulinzi unaimarishwa katika Vituo vya Kupigia kura lakini usiwe ulinzi wa kuwatia wananchi hofu wakashindwa kufika katika vituo vya kupigia kura viongozi wanaowataka ili washirikiane nao katika kujiletea Maendeleo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidi wa Uchaguzi Katika Manispaa ya Moshi 20.11.2017. Kushoto ni Mwanasheria Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mtibora Selemani.

WAZIRI MWAKYEMBE ATUMA SALAMU ZA POLE KWA KITUO CHA RADIO NA TELEVISHENI CHA CLOUDS MEDIA

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI MHE. MASAHARU YOSHIDA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida alipokutana na na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2017. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2017

TPB Bank Plc, Multichoice kuwapatia Watanzania DStv kwa Mkopo

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kusaini makubaliano rasmi na Benki ya TPB ambapo sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Multichoice Tanzania, Salum Salum.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakisaini makubaliano ya ushirikiano, ambapo kwa sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Nyuma yao ni mashahidi kutoka pambe zote mbili.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakisaini makubaliano ya ushirikiano, ambapo kwa sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Nyuma yao ni mashahidi kutoka pambe zote mbili.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kusaini makubaliano rasmi na kampuni ya Multichoice Tanzania inayotoa huduma za DStv, sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja sasa wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande.

 BENKI ya TPB imeingia kwenye makubaliano rasmi na kampuni ya Multichoice Tanzania inayotoa huduma za DStv ambapo wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja sasa wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo.

Hafla hiyo ya kusaini makubaliano imefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande wamesaini hazi za makubaliano. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi alisema kwa sasa Watanzania wanaotaka kumiliki ving’amuzi vya DStv, wataweza kupata mkopo maalum kutoka TPB utakaowawezesha kufungiwa huduma za DStv na kisha kulipa kwa awamu kwa kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja.

Alisema kuwa benki yake siku zote imekuwa ikijitahidi kubuni huduma mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kupata huduma muhimu na pia katika kuboresha hali zao kiuchumi na kijamii. 

Amesema kuwa wameamua kuingia kwenye makubaliano na kampuni ya Multichoice ili kuwapa fursa wafanyakazi na wateja wa benki hiyo waweze kupata huduma muhimu za DStv kwa mkopo, hii ikimaanisha hawatalazimika kulipa fedha yote kwa mkupuo mmoja badala yake watakuwa wanalipa kwa awamu kadhaa.

 “Benki yetu ni benki ya Watanzania wa kada zote, na wenzetu wa Multichoice nao hali kadhalika, sasa tumeamua tuungane ili tuwawezeshe ndugu zetu Watanzania kupata fursa ya kuwa na huduma ya DStv kwa njia ambayo ni rahisi kwao” alisema Moshingi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande aliishukuru TPB kwa kukubali kuwawezesha watanzania kupata huduma za DStv kihimiza wananchi kuitumia vema fursa hiyo. Alisema huduma za ving’amuzi vya DStv ni bora nchini Tanzania hivyo urahisishaji wa wananchi kuipata unaongeza wingo wa wananchi kufurahia huduma hizo. 
 Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.

IGP SIRRO AFUNGA MKUTANO WA URRA SACCOS MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro pamoja na Viongozi wengine wa Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) wakiimba wimbo wa maadili ya ofisa wa Polisi wakati wa hafla fupi ya kufunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama hicho uliokuwa ukifanyika mkoani Morogoro ambapo aliwataka Viongozi hao kuhakikisha kuwa Mikopo inawafikia walengwa kwa wakati ili waweze kuboresha maisha yao.(Picha na Jeshi la Polisi)
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro( hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mkutano huo uliokuwa ukifanyika mkoani Morogoro ambapo aliwataka Viongozi hao kuhakikisha kuwa Mikopo inawafikia walengwa kwa wakati ili waweze kuboresha maisha yao.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro pamoja na Viongozi wengine wa Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SACCOS hiyo wakati wa hafla fupi ya kufunga mkutano huo uliokuwa ukifanyika mkoani Morogoro.(Picha na Jeshi la Polisi)

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KUU WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Joseph K. Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo K. Philip ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Joseph K. Malongo(kulia) na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo K. Philip  (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa amefanya ziara katika kivuko cha Kigamboni na kujionea namna mashine mpya za kieletroniki zilivyoweza kufungwa na kumtaka  mhandisi aanze kuzifanyia majaribio kabla ya mwaka huu kuisha ili Januari 2018 zianze kutumika.

Akizungumza baada ya kumaliza ziara yake na kujionea namna wafanyakazi wanavyotoa huduma kwa abiria wanaofika kwa ajili ya usafiri kwa kivuko kutoka Kigamboni na Kivukoni, Naibu Waziri Kwandikwa amesema kuwa amefurahishwa na huduma zinazotolewa na zaidi amezungumza na baadhi ya wananchi na wote wameonekana kufurahishwa. 

" Nimezungumza sehemu mbalimbali na kujionea namna watoa huduma wanavyotoa huduma zao kwa abiria na pia nimezungumza na takribani wananchi kumi wanaotumia usafiri wa kivuko na wote wameonekena kufurahishwa na huduma zenu ,"alisema Naibu Waziri Kwandikwa.

Katika ziara yake ameweza kuzungumza na wahudumu wanaokatisha tiketi na kuwauliza changamoto wanazokutana wakati wa ukatishaji tiketi, ametembelea na kupanda kivuko cha MV KAZI ambacho ni kipya pamoja na kuona namna Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) wanavyofanya shughuli zao za kila siku.

Amesema, kama serikali wanahakikisha watumiaji wa kivuko hicho wanapata huduma bora na zinazostahili ikiwemo usalama wa safari zao za kila siku.
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na mhudumu wa kukata tiketi katika kituo  cha Kivukoni wakati alipofanya ziara kuangalia namna abiria wanavyopata huduma zao, juu akikata tiketi ya kuingia ndani.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake katika kivuko cha Kivukoni na Kigamboni na kujionea uendeshaji wa huduma bora kwa abiria kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na Mhandisi wa kivuko Ally Daudi na akipewa maelezo ya maendeleo ya vivuko vyote vilivyopo chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akikagua mashine za kieletroniki za tiketi zilizofungwa katika Kivuko cha Kigamboni na Kivukoni wakati wa ziara yake iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wananchi wakizungumzia baadhi ya kero ndogo ndogo wanazokutana nazo pia huduma bora wanazozipata.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akiwa ziarani katika kivuko cha Kivukoni na Kigamboni iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Zainab Nyamka.

MICHUZI TV: DC GONDWE AAMURU KUKAMATWA WALIOKULA MILIONI 12 ZA MRADI WA TREKTA


VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO NOVEMBA 23,2017

DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiongea na wananchi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitokea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua kimaendeleo. PICHA NA KAJUNASON/MMG - HANDENI, TANGA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akimsaidia Diwani wa Kata ya Kwamgwe, Sharifa Abebe alipokuwa akitoa machozi ya shukrani kwa shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kuweza kushirikiana na wananchi kuwajengea jengo la zahanati lililoweza kugharimu shilingi milioni 190 ambapo wao World Vision Tanzania waliweza kutoa Milioni 100 na wao wananchi waliweza kujitoa kwa nguvu zao kwa thamani ya milioni 90. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya Kwamgwe ambapo ndipo jengo hilo lilipojegwa.
Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania,  Humphrey Bernard akisoma risala ya mradi wa ujenzi wa zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwamgwe ambapo aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akikabidhiwa mikataba wa zahanati na mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard (kushoto) ambao ndiyo waliojenga kwa kushirikiana na wananchi waliojitoa kwa hali na mali.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni, William Makufwe akitoa ufafanuzi jinsi wananchi walivyoweza kujitoa ujenzi wa zahanati.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Dokta Credianus akitoa nasaha zake kwa wananchi wa Handeni waweze kujua umuhimu wa kuwekeza katika afya. Jengo la zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwangwe, Wilayani Handeni.
Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea zawadi ya kuku kutoka wa mwenyekiti wa kitongoji cha Migombani, Michungwani-Segera Bi. Amina Njama ambaye amekuwa msitari wa mbele katika uhamasishaji wa kukusanya matofali ili yaweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa na zahanati.
 Mkuu wa Wilaya akifurahi na viongozi.
 Mkuu wilaya akipata maelezo machache kutoka kwa wananchi waliitikia wito wa kuchangia maendeleo kwa kuchimba msingi wa zahanati ya  Migombani, Michungwani - Segera.
Mkuu wa Wilaya akiwashukuru wananchi kwa moyo wao wa kujitolea katika maendeleo. Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewataka wananchi wa Kata ya Kwamgwe kuendelea kujitoa kikamilifu katika kuchangia shughuli za kijamii ili kuendana na kasi ya rais Dkt. John Magufuli katika kuleta maendeleo endelevu. 

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitolea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua. "Nawaomba ndugu zangu, sisi wote ni wanaKwamngwe, lazima tuamue kuchangua mambo muhimu matatu, kutambaa, kutembea au kukimbia. Jambo la msingi ni lazima tuwe katika mwendo, tuendelee kujitoa tuzidi kuleta maendeleo kijijini kwetu," alisema Gondwe. 

 Awali akikabidhi mradi huo wa zahanati hiyo, Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP, Humphrey Bernard aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati. Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya Handeni aliweza kutembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Michungwani, Segera ambapo ujenzi wake unaanza hivi karibuni kwa nguvu za wananchi kupitia kampeni ya mkuu huyo ya kuongeza zahanati na madarasa.

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA GARI KWA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

$
0
0


Gari lililotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akikata utepe wakati wa hafla ya kupokea msaada wa gari lililotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akikata utepe wakati wa hafla ya kupokea msaada wa gari lililotolewa na Benki ya CRDB kwa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akimkabidhi Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, msaada wa gari kwa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Kamanda Mambosasa akijaribu gari lililotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utendaji wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.

DKT MWIGULU AMEWAAKIKISHIA WANACHAMA WA CCM MKOA WA RUVUMA KUIBUKA NA USHINDI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI

$
0
0
Mbunge wa IRAMBA MAGHARIBI DKT MWIGULU NCHEMBA amewahaakikishia wanachama wa ccm mkoani RUVUMA kuwa chama hicho kitachukua kata zote zinazoshiriki uchaguzi mdogo wa madiwani katika wilaya ya TUNDURU na MBINGA hayo amesema wakati wa kumnadi mgombea wa wa udiwani katika kata ya MHONGOZI wilayani MBINGA HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE

KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR, AFANYA ZIARA OFISI YA UHAMIAJI MKOA WA KUSINI UNGUJA:

$
0
0
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu akielezea jinsi Idara ya Uhamiaji inavyopiga hatua katika kutatua changamoto ya Makaazi ya Askari wake katika Wilaya zote Unguja na Pemba. Aliayasema hayo wakati akikagua nyumba za Watumishi wa Uhamiaji iliyopo Makunduchi, Wilaya ya Kusini wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Akijibu hoja mbali mbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.  Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdullah Mbarouk Ramsa.
 Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Khamis Ali Juma akitoa maoni juu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika eneo la uendeshaji wa mashtaka ya Kiuhamiaji, wakati wa kikao cha pamoja cha Wafanyakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kati kati), akifatilia kwa makini majadiliano katika kikao cha pamoja na watumishi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017. Kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Mkemimi Mohamed Mhina na Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdullah Mbarouk Ramsa.


Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images