Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Airtel Money kugawa gawio la bilioni 2 kwa wateja

$
0
0
Wakati msimu wa sikukuu ya krismasi umewadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeupokea msimu huo kwa kuendelea kuwanufaisha wateja pamoja na mawakala wa huduma ya Airtel Money nchi nzima kwa kuwagawia gawio la shilingi bilioni 2 kutokana na utumia wao wa huduma ya Airtel Money 

Taarifa ilitolewa na kampuni hiyo leo ikiwa na kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso imethibitisha kuwa,

Gawio la faida kutokana na huduma ya Airtel Money hutolewa katika kila robo ya mwaka ambapo gawio la awali lilianza kutolewa Mwaka 2015, hadi kufikia leo hii jumla ya shilingi bilioni 11.8 zimeshagawiwa kwa wateja wa Airtel Money. Kila mteja wa Airtel Money hupata sehemu ya gawio hilo kulingana na salio linalosalia katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku.

“Tunapoingia katika shamrashamra za msimu wa sikukuu, Airtel tunatambua umuhimu wa kuwazawadia wateja wetu. katika msimu au wakati kama huu watu wengi hupanga ratiba za jinsi watakavyosherehekea kwa kupeana zawadi wakiwa na familia zao, tunafurahia kuona tuko katika wakati sahihi kwa kutoa gawio hili ili kutoa fursa kwa wateja wetu kuweza kutumia wakiwa na familia au wawapendao kwa kujipatia mahitaji yao muhimu ndani ya msimu wa sikukuu”.

Gawio hili la Airtel Money linaloaanza kutolewa leo linalotokana na faida iliyopatiikana kuanzia ya robo mwaka kuanzia mwezi Juni hadi Septemba 2017, ambapo watakaofaidika ni wateja wote wanaotumia huduma ya Airtel Money pamoja na mawakala wake nchini nzima. Tunajisikia furaha sana kugawa gawio hili ambapo kila mteja wa Airtel Money tapata na kisha mteja mweyewe ataamua kuitumia pesa yake atakavyo iwe kununua bando, muda wa maonge, kulipia LUKU au kufanya malipo ya bili za huduma mbalimbali” ilieleza taarifa hiyo

Airtel Tanzania itaenendelea na utekelezaji wa dhamira yake ya kutoa huduma za kifedha bora kwa njia ya mtandao ili kuongeza tija kwa watumiaji , unafuu na usalama wakati wowote. Huduma ya Airtel Money imekuwa na kuongeza watumiaji kutokana kuwa na umuhimu zaidi kwa wateja. Tunapenda kuwashauri wateja wa Airtel wot kutumia huduma hii ya Airtel Money kwa kukamilisha au kutimiza baadhi ya mahitaji yao ya huduma za kifedha ili kuwa sehemu ya gawio kama hili linayotolewa sasa” ilieleza taarifa hiyo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu mgao wa gawio  la faida la bilioni 2 kwa wateja na watumiaji wa huduma ya Airtel Money. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Isack Nchunda.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu gawio la bilioni 2 kwa wateja na watumiaji wa huduma ya Airtel Money. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano.

NAIBU WAZIRI,KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI WAZUNGUMZA NA WANANCHI

$
0
0
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi aliombatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala(watatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo.Lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli mbalimbali zilizopo chini ya idara za wizara na kukagua mipaka iliyopo katika mkoa huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, akizungumza na wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akijibu baadhi ya hoja zilizoulizwa na wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiambata na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kulia) 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala(wapili kulia),Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima() na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga(kulia), wakisikiliza maswali ya mmoja wa wananchi wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo. 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala( kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima(watatu kulia) wakisikiliza maswali ya mmoja wa wananchi wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka Tanzanua na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo

Na Abubakari Akida-WMNN

NAIBU Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewataka wananchi na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao karibu na Kituo cha Mpaka wa Sirari unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya kuhakikisha wanashirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Mara kudhibiti matukio ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu hao kwa jeshi hilo.

Hayo ameyasema akiongea na wananchi wakati wa ziara ya kikazi katika mkoa wa Mara, ikiwa na lengo la kutembelea mipaka iliyopo katika mkoa huo inayotenganisha nchi ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda ambapo katika ziara hiyo aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce Malibiche na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

“Tumekuwa tukipata taarifa wananchi wa hapa kushirikiana na wahalifu katika kupitisha mali za magendo hapa hasa wakitumia vijana wanaoendesha bodaboda kupitisha mizigo yao na kuripotiwa matukio mbalimbali yanayohatarisha usalama wa raia wetu, natoa wito kwa wananchi wa hapa kushirkiana na jeshi la polisi kudhibiti matendo hayo ya kihalifu,” alisema Masauni

Aidha,Naibu Waziri Masauni amewataka wananchi hao kuacha mara moja tabia inayokua kwa kasi katika eneo hilo ya kulizuia Jeshi la Polisi kufanya shughuli zake na endapo atabainika mtu yoyote atakumbana na mkono wa sheria huku akitoa ushauri kwa jeshi kuzifanyia utafiti taarifa zitakazoletwa ili kuepuka kumuonea mtu.

Akizungumza na wananchi hao Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, amewataka wananchi hao kupeleka taarifa za wahamiaji haramu pindi watakapowagundua ili kuweza kudhibiti tatizo la wahamiaji hao kuingia nchini huku akiweka wazi viwango vya udhibiti vilivyoweka na idara yake kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini.

“Idara ya Uhamiaji kupitia wawakilishi wetu mkoani hapa tupo tayari na tunaomba mtu yoyote mwenye taarifa za wahamiaji haramu azifikishe kwenye ofisi ya uhamiaji nasi tutazifanyia kazi kwani tushapunguza tatizo hilo na tuko katika jitihada za kulimaliza kabisa,” alisema Dk. Makakala

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taida (NIDA), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce Malibiche, alisema NIDA imezindua zoezi la usajili wa vitambulisho kwa wakazi wa Mkoa wa Mara na wanatarajia kumaliza zoezi hilo mapema ili wananchi wa Mkoa huo na wilaya zake wawe na vitambulisho vya Taifa vitakavyozuia baadhi ya changamoto lakini lengo kubwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anakua na Kitambulisho cha Taifa.

MKUU WA WILAYA YA MBOGWE AMEZINDUA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA SHENDA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi amezindua Ujenzi wa Zahanati ya Shenda ambayo inatarajiwa kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na serikali katika uzinduzi huo mkuu Wilaya ameshirikiana na wananchi kukamilisha zoezi la kumwaga Zege na kuendesha harambee ya kupata vifaa vya ujenzi.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wote kutoa ushirikiano wa nguvu kazi kwenye ujenzi wa zahanati hiyo kwani zahanati hiyo itahudumia wananchi wote wa Shenda bila ubaguzi. Mkuu wa wilaya amewasisitiza wananchi wote kuungana bila kuangalia itikadi za chama wala dini .

Pamoja na uzindinduzi huo Mkuu wa Wilaya amemwagiza Mtendaji wa Kata ya masumbwe kugawa zamu za kufanya kazi kwenye zahanati hiyo kwa vitongoji vyote vya Shenda kwani Serikali itagharamia gharama za Fundi tu kazi nyingine zote zitafanywa na wananchi wa kijiji husika ili kupunguza gharama na kwenda na kasi ya mkuu wa mkoa wa Geita inayotaka kila kijiji kumiliki Zahanati yake.

Kwa sasa wananchi wa shenda wanapata matibabu kwenye kituo cha afya Masumbwe ambacho kipo umbali wa zaidi ya kilometa mbili kitu ambacho kimekuwa kikileta changamoto kwa wakazi wa shenda zaidi wakinamama wajawazito na watoto.

Vilevile Kaimu Muhandisi wa Ujenzi bi Filomena Bango amesema Zahanati hiyo inajengwa kwa nguvu za Wananchi ambao mpaka sasa wameshafyatua matofali 300 wameshaleta mawe ya kutosha na wanaendelea kushirikia na fundi . Bi Filomena amesema wananchi watakapoishia serikali itachukua jukumu la kumalizia wananchi walipoishia. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe akimwaga maji kwenye nondo zilizoandaliwa kwa ajili ya msingi wa Zahanati
 Mkuu wa Wilaya y a Mbogwe Mh Martha Mkupasi akikagua matofali yaliyofyatuliwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Shenda
 Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi akihutubia wananchi wa kijiji cha Shenda wakati wa uzinduzi wa waujenzi wa Zahanati ya Shenda
Wananchi wa Kijiji cha Shenda wakishirikiana na kuchanganya Zege litakalotumika kujenga zahanati ya Shenda

MWENYEKTI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) WA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili kuongoza Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akifungua  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
 Waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzani wakiwasili ukumbuni kuomba ridhaa ya kurudi CCM wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
 Waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzani wakiwasili ukumbuni kuomba ridhaa ya kurudi CCM wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo aliyepata kuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha ACT akiomba na kukubaliwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo aliyepata kuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha ACT akiomba na kukubaliwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwanachama wa CHADEMA Bw. Lawrence Masha akiomba na kukubaliwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwanachama wa CHADEMA Bw. Lawrence Masha akipeana mkono na  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

 Aliyekuwa mwanachama mwandamizi wa ACT Bi. Edna sunga  akiomba kurudi na kukaribishwa  CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

 Aliyekuwa mwanachama mwandamizi wa ACT Bi. Edna sunga  akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Bw. Samson Mwigamba akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Bw. Samson Mwigamba akipeana mkono na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Bw. Samson Mwigamba akipeana mkono na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kiinana kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.
Aliyekuwa  Mshauri wa Chama cha ACT Wakili Albert Msando  akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017


Aliyekuwa  Mshauri wa Chama cha ACT Wakili Albert Msando  akipeana mkono na  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA)  Bw. Patrobas Katambi  akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

 Wanachama sita wa vyma vya upinzani wakionekana aada ya kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiendesha Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole akiwapatia mashati wanachama sita wa vyama vya baada ya kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole akiongea na wanachama sita wa vyama vya baada ya kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.PICHA NA IKULU
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole akipata picha ya kumbukumbu na wanachama sita wa vyama vya baada ya kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017



UMEME USIKATIKE BILA SABABU MAALUM- SUBIRA MGALU

$
0
0
Na Teresia Mhagama.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa hawakati Umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea wananchi adha ya kukosa nishati hiyo.

Naibu Waziri aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme ambapo vituo vya kupozea Umeme alivyovitembelea ni Mbagala, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre.

“Umeme ukatike pale inapostahili tu, na endapo tatizo linatokea mfano kwenye mifumo ya Umeme ni muhimu mkatoa taarifa mapema kwa wananchi,” alisema Subira Mgalu.

Aliongeza kuwa ukatikaji wa Umeme unasababisha malalamiko kutoka kwa Wananchi kwani kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli nyingi hasa za kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato.

Aidha Naibu Waziri aliwaagiza watendaji wa TANESCO wanaosimamia mradi huo wa TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika tarehe 15 Desemba, 2017.

Vilevile alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake kutaboresha hali ya upatikanaji wa Umeme katika jiji la Dar es Salaam.

"Nawaomba watanzania wawe na matumaini na Serikali ya Awamu ya Tano kwani inajitahidi katika Ujenzi wa miundombinu ya Umeme, nia ikiwa ni nishati ya Umeme kupatikana muda wote," alisema Naibu Waziri.
kwa upande wake, Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel  Manirabona alisema kuwa Shirika hilo linafanya juhudi mbalimbali ili utekelezaji wa mradi huo ukamilike ndani ya muda ulioelekezwa.

Mradi wa TEDAP unahusisha upanuzi na ujenzi wa Vituo Vipya  19  vya  kupoza  Umeme  wa  Msongo wa kV 132/33 na kV 33/11 pamoja na ujenzi wa njia za Umeme wenye Msongo wa kV 132, kV 33 na kV 11 katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Kilimanjaro.

Gharama za utekelezaji wa mradi husika ni  Dola za Marekani milioni 43, ambazo zimetolewa na Benki ya Dunia (WB) kupitia Mradi huo.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa kwanza kushoto) akiwa katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel  Manirabona.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili  kushoto) akikagua mitambo ya Umeme katika kituo cha City Centre jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha ni watendaji kutoka TANESCO.
 Baadhi ya mitambo ya Umeme katika kituo cha Mbagala  jijini Dar es Salaam iliyojengwa chini ya mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.
 Miundombinu ya kusafirisha Umeme  wenye Msongo wa kV 132 iliyojengwa katika eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili  kushoto) akikagua mitambo ya Umeme katika kituo Kipawa jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha ni watendaji kutoka TANESCO na Wizara ya Nishati.

VYAKULA VITANO MUHIMU KWA UKUAJI WA AKILI YA MTOTO

$
0
0

Na Jumia Food Tanzania

Miongoni mwa changamoto zinazowakumba wazazi wengi wa kitanzania ni kushindwa kufahamu na kupangilia vyakula sahihi kwa ukuaji wa afya za watoto wao. Afya ya akili ya mtoto ni kitu muhimu na cha kuzingatia kwani humfanya mtoto aweze kufanya shughuli tofauti kwa ukamilifu ikiwemo uwezo wake wa kujifunza shuleni pamoja na kushiriki michezo mbalimbali na wenzake.
Baadhi ya wazazi kwa kutokufahamu huwapatia watoto wao vyakula ambavyo huwa haviwasaidii watoto kwenye hatua ya ukuaji. Inawezekana watoto huwa hawapendelei vyakula hivyo muhimu kwa afya zao, lakini inashauriwa kuanza taratibu na hatimaye wanazoea. Jumia Food imekukusanyia aina tano za vyakula ambavyo ukianza kumpatia mtoto wako utashangazwa na ukuaji wa afya ya akili yake.

Mayai. Virutubisho vinavyopatikana kwenye mayai ni muhimu kwenye utengezaji wa seli zinazotunza kumbukumbu kwenye ubongo. Kadiri tunavyokuwa na seli nyingi ndivyo tunakuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu. Hivyo ni vizuri kuzingatia kujumuisha aina hii ya chakula unapomtayarishia mtoto wako chakula, kwa mfano asubuhi kabla mtoto hajakwenda shuleni.  

Maziwa. Maziwa yasiyo na mafuta yanajulikana kuwa chanzo kikubwa cha protini, Vitamini D na fosforasi. Lakini pia kalsiamu inayopatikana ndani yake inasaidia namna miili yetu inavyodhiti nishati. Kalsiamu pia ina mchango mkubwa kwa uzalishaji wa insulini kwenye miili yetu. Mbali na kunywa maziwa kama yalivyo unaweza kunogesha kwa kuongeza chokoleti. Wataalamu wanasema kwamba kuna kiasi kidogo cha ‘kafeini’ kwenye maziwa ya chokoleti, na yanakuwa karibu na kiasi sawa cha sukari iliyopo kwenye juisi za matunda.  

Matunda. Ukuaji wa afya ya akili ya mtoto huhitaji matunda kwani humsaidia kwenye mchakato mzima wa kujifunza. Lakini pia matunda husaidia katika mchakato mzima wa kulainisha choo hivyo kusaidia kwa kiasi kikubwa watoto wengi wanaokumbwa na changamoto hiyo. Ukiachana na maji na mazoezi, matunda ni mbinu bora ya kuwafanya watoto kuwa na afya bora na hivyo akili kuwa tayari kwa kujifunza. Ili kutomtia mtoto uvivu katika kula matunda, unaweza kumuandalia kwa kuyakata kwa mtindo wa vipande vidogovidogo.   
Maji. Jambo ambalo wazazi wengi hawalifahamu ni ambavyo watoto wao hunywa kiasi kidogo sana cha maji kutwa nzima. Wataalamu wengi wamekuwa wakionya namna maji ambavyo huwa yanapuuzwa kama chakula muhimu kwenye mwili wa binadamu, si kwa watoto tu bali hata watu wazima. Watoto muda mwingi huwa wanakuwa kwenye pilikapilika zao bila ya kuwa na maji ya kutosha mwilini. Kutokunywa maji au kutumia kwa kiasi kidogo huwafanya watoto kuhisi njaa isiyo ya lazima. Hakikisha kuwa unajumuisha maji kwenye kila mlo unaomuandalia mtoto wako.
Nyama. Ukosefu wa madini ya chuma ni miongoni mwa tatizo sugu linalotokana na upungufu wa lishe, na huongoza kwa magonjwa yanayotokana na upungufu wa lishe duniani. Na kutokufanya vizuri kwa watoto shuleni huweza kuwa dalili mojawapo. Kiasi cha nyama unachokitumia kwenye mlo kila siku kina faida kubwa ambayo huwezi kuifikiria. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, hata kiasi kidogo unachokula kwa kimeonyesha utofauti mkubwa kwenye uwezo wa mwili kufyonza madini ya chuma kutoka vyanzo mbalimbali.

Inafahamika kwamba wazazi wengi huwapatia watoto wao vyakula ambavyo ni muhimu kwenye ukuaji wao. Kama mzazi au mlezi jaribu aina mbalimbali ya vyakula mbali na vilivyoorodheshwa humu, fuata ushauri wa wataalamu mbalimbali wa afya au kusoma zaidi majarida tofauti ya afya na lishe.  

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATASHASTA NDITIYE ATEMBELEA TUME YA TAIIFA YA TEHAMA NA TCRA-CCC

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela (katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, alipowasili ofisini hapo katika ziara yake ya kutembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Tumeya Taifa ya TEHAMA, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani), alipowasili katika tume hiyo, jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto),  wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akatoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia),  katika wa ziara hiyo. 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini wakati wa ziara hiyo. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, akimkaribisha Naibu Waziri, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), kuzungumza na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya TEHAMA.
Naibu Waziri, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya TEHAMA katika ziara hiyo.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prisca Ulomi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) katika ziara yake ya kutembelea Tume ya Taifa ya TEHAMA, jijini Dar es Salaam.  
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akitoa maelezo kwa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia niNaibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye. 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prisca Ulomi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) katika ziara yake ya kutembelea Tume ya Taifa ya TEHAMA, jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Tumeya Taifa ya TEHAMA, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani), alipowasili katika tume hiyo, jijini Dar es Salaam.   
Katibu Mtendaji wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC), Mary Shao Msuya, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani),  wakati wa ziara hiyo. 
Naibu Waziri, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC), katika ziara hiyo.  
Naibu Waziri, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akifafanua jambo, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC), katika ziara hiyo. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akiwasilisha majukumu na Taarifa ya Utekelezaji ya tume hiyo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani), alipotembelea tume hiyo, jijini Dar es Salaam.  
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akiwa pamoja na wafanyakazi wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela (hayupo pichani), wakati akiwasilisha majukumu na Taarifa ya Utekelezaji ya tume hiyo, jijini Dar es Salaam.

UKARABATI WA DARAJA LA MBEZI KIBANDA CHA MKAA MOROGORO ROAD WAFIKIA HATUA NZURI

$
0
0
 Wakandarasi kutoka Wakala wa Barabara nchini Tanroads wakiendelea na ukarabati wa Daraja la Mto Mbezi ,eneo la Kibanda cha Mkaa  ambapo liliharibika kutokana na Mvua zilizonyesha Mwanzoni mwa mwezi huu na kusababisha uharibifu mkubwa na kutishia kufungwa kwa barabara ya Morogoro ambayo ndio sehemu kubwa ya kusukuma uchumi wa Dar es Salaam
 Sehemu ya Daraja hilo inavyonekana kwa upande jinsi Daraja Hilo lilivyo haribika na Mvua zinazoendelea hivi sasa nchini.
 Wakndarasi wanaojenga Daraja hilo wakijadiliana juu ya ujenzi katika eneo hilo

--

UKARABATI WA DARAJA LA MBEZI KIBANDA CHA MKAA MOROGORO ROAD WAFIKIA HATUA NZURI

$
0
0
Kuku wakiendelea kuandaliwa ndani ya Soko la Kisutu. Picha zote na MaendeleoVijijini.

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini.

SAUTI za kuku zinasikika hata ukiwa nje ya jengo dogo ndani ya Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, lakini ghafla zinakoma na zinasikika nyingine.
Siyo kwamba kuku hao wanahitaji chakula ama wanacheza, bali hapa ni machinjio, na sauti zinapokoma ujue tayari zimekwishapigwa kisu na zinaandaliwa kwa ajili ya kitoweo.

Nje ya jengo hilo unaweza kuwa umekuta akinamama wengi wakiwa wamelundikana huku wakiwa wamekalia ndoo zao.Hawa nao wanasubiri huduma, wanataka kununua utumbo, miguu pamoja na vipapatio vya kuku hao wanaochinjwa ili wakafanye biashara.

Akinamama hawa wanatoka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na hapa Kisutu ndiko mahali pekee ambako wanaweza kupata bidhaa hiyo wanayokwenda kuuza mitaani.Bila shaka baadhi yetu tumekutana ama tumewakuta akinamama wakiuza firigisi na utumbo mitaani, basi amini kwamba asilimia kubwa wanapata bidhaa hiyo katika eneo hili la Kisutu.

Ukiingia ndani ya jengo hilo usishangae ukasalimia usiitikiwe na watu wengi, japokuwa waliomo ni wengi.Kabla hujajua usimame wapi, utasikia sauti ya mtu akikutaka radhi kwamba anaomba kupita ama anataka kuweka mzigo.Naam. Kila mtu hapa yuko ‘busy’ na kazi inakwenda mtindo mmoja, na hata kutokukuitikia si kwamba wanafanya kiburi ama hawajakuona, la hasha. Kwa sababu wanataka kuhakikisha kazi wanayoifanya inakuwa katika hali bora hasa ikizingatiwa kwamba hicho ni chakula kwa afya ya binadamu.

Mazingira ya ndani yanaridhisha kutokana na usafi ambao unazingatiwa sana na wahusika licha ya changamoto za hapa na pale.
Hawa ni wanaushirika wa Kisutu Poultry Farm Cooperative Society (KIPOCOSO), ambao wamekuwepo katika soko hilo kwa zaidi ya miaka 28 na ndio waanzilishi wa kuchinja kuku jijini Dar es Salaam.

Japokuwa hivi sasa baadhi ya masoko yana machinjio ya kuku, lakini wengi wanaohusika na uchinjaji wamejifunza ama wamewahi kufanya shughuli hizo katika Soko la Kisutu.Kuku walionyonyolewa, kuchunwa ngozi au kukatwakatwa wanaweza kukutoa udenda wangali wabichi na wamewekwa mafungu mafungu.

“Kila fungu unaloliona hapo lina mwenyewe, hawachanganyani kabisa,” ndivyo anavyoeleza Bw. Hamisi Malamla, Mwenyekiti wa KIPOCOSO.
Anaongeza: “Kazi yetu hapa ni kuchinja, kuku wote wana wenyewe na kila mmoja hapa ndani anakwenda hapo nje kwenye mabanda wanakonunua kuku na kutafuta oda, akiipata anakuja kuchinja na kuwatengeneza.”

Bw. Malamla anasema kwamba, asilimia kubwa ya kuku wanaoliwa jijini Dar es Salaam wanachinjwa na kuandaliwa katika soko hilo, sehemu ambayo pia ni maarufu kwa wauzaji wa kuku – wa nyama wa kisasa pamoja na wa kienyeji.Kuku 3,000 kwa siku
Ndani ya jengo hilo lililowekwa terazo, kujengwa masinki bora pamoja na majiko matatu makubwa yanayotumia gesi, takriban kuku 3,000 huchinjwa kila siku.

Licha ya kufanya shughuli zao kwa ufanisi, lakini unapozungumza na wanaushirika hawa utagundua kwamba wana mawazo makubwa ya maendeleo tofauti na unavyoweza kuwadhania.

“Malengo yetu ni kujikita katika uwekezaji wa kilimo na mifugo, tunataka tuanze kufuga wenyewe kuku (wa kisasa na kienyeji), kuuza kuku wenyewe, kutotolesha vifaranga, kutengeneza vyakula vya kuku pamoja na kusambaza madawa,” anasema Bw. Malamla.

Anasema kwamba, ikiwa wataanza uwekezaji wa kufuga kuku itakuwa ni hatua kubwa kwao kwani watakuwa na uhakika wa kuchinja na kuuza, na kwamba oda wanazozipata kwa sasa zitakuwa ni nyongeza tu na ziada.
Malamla anasema, kwa uzoefu walionao, ikiwa watajikita pia katika ufugaji wanaweza kulisha wananchi wengi jijini Dar es Salaam na kwamba hata kuku watakaowafuga wanaweza kuongezeka ubora tofauti na baadhi ya wanaouzwa sokoni hapo ambao mara nyingi huwa hawana uzito mkubwa.

“Tukianza ufugaji ni dhahiri tutaongeza ubora kulingana na mahitaji ya soko na hatuwezi kubahatisha, kwa sababu hapa wakati mwingine kuku wanaadimika na inapotokea hivyo maana yake tunakosa kazi ya kufanya,” anasema.

Anaongeza kwamba, tangu uongozi wake ulipoingia madarakani mwezi Machi 2017 (miezi nane iliyopita) wamefanikiwa kujiwekea akiba ya kutosha ambayo inawapa msukumo wa kuangalia fursa za uwekezaji ili kuongeza kipato pamoja na kupanua wigo wa ajira.

Usajili

Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachinja Kuku Soko la Kisutu (KIPOCOSO), Bw. Hamisi Malamla (kushoto) akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Uongozi, Mzee Shaaban Hassan Bogoma leo hii walipotembelewa na MaendeleoVijijini.

KIPOCOSO, ambacho ni miongoni mwa vikundi nane vinavyounda Umoja wa Wafanyabiashara Soko la Kisutu (UWASOKI), kilisajiliwa Juni 28, 1989 kama chama cha ushirika na kupewa hatia namba DSR-382.

Kikundi hicho cha ushirika kina jumla ya wanachama 57 na kinaongozwa na Bw. Malamla kama mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti ni Zuberi Luwono, Hassan Ally Sozigwa (Katibu), na wajumbe ni Shaaban Hassan Bogoma, Ally Omari Vullu, Suleiman Kitalambo na Juma Said Mwinyi.

Malamla anasema kwamba, kwa utaratibu waliojiwekea, kila mwanachama kati ya hao 57 lazima kila siku achangie Shs. 4,000 ambapo Shs. 2,000 ni kwa ajili ya gesi na Shs. 2,000 kama ada.“Utaratibu huu ni kila siku, hivyo kwa kukusanya Shs. 2,000 za ada kila siku tuna uwezo wa kuingiza Shs. 114,000 kila siku na kwa maana hiyo kwa mwezi tunaweza kuingiza wastani wa Shs. 3 milioni.

“Tunao wasaidizi 30 wanaofanya shughuli za kuchinja pia humu ndani, lakini hawa hawahesabiwi kama ilivyo kwa wanachama wenyewe, na mara nyingi wasaidizi hawa huwa ni wale wanaowasaidia wanachama husika,” anaongeza.

Kwa mujibu wa Malamla, hivi sasa wanayo akiba ya kuridhisha ingawa inaweza isitoshe kuanzisha shughuli za ufugaji mkubwa ambazo zinahitaji fedha nyingi zaidi.“Hatujapiga hesabu, lakini najua shughuli hizi zinahitaji fedha nyingi zaidi, tunaamini kwa dhamira ya dhati tuliyonayo, ipo siku tutafanikiwa tu katika mipango yetu,” anasema.

Mbali ya akiba ya fedha benki, lakini ushirika huo unamiliki viwanja takriban 21 vyenye ‘Offer’ katika eneo la ekari 10 huko Mbutu, Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo miongoni mwa viwanja hivyo ni eneo la ekari moja ambalo wanataka waanzie ufugaji wa kuku na samaki.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Bw. Henry Mwatwinza Mwimbe, anasema kwamba, KIPOCOSO ni miongoni mwa vyama vya ushirika vya msingi vilivyoonyesha mafanikio makubwa katika kipindi kifupi.

“Kimeanzishwa muda mrefu, lakini kimepitia katika uongozi mbovu ambao pengine haukuwa na malengo, uongozi wa sasa tangu ulipoingia madarakani mwezi Machi 19, 2017 umeweza kufanya mambo makubwa sana kwa usimamizi wetu na bado tunaendelea kuwasaidia maoni na mambo mbalimbali kuhakikisha kwamba wanapiga hatua,” anasema Mwimbe.
Mwimbe anasema kwamba, kwa hatua waliyofikia, KIPOCOSO wanaweza kabisa kukopesheka kwani licha ya akiba waliyonayo, bado wanayo rasilimali ardhi na wana malengo ya kuwekeza katika kilimo na ufugaji.

Changamoto
Pamoja na mafanikio waliyonayo, lakini wajasiriamali hao wanasema kwamba, wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, hususan masuala ya usafi wa mazingira.
Mzee Shaaban Bogoma anasema kwamba, mifumo ya majitaka iliyowekwa na Halmashauri ya Jiji (mifumo ya DSSD) haikidhi mahitaji na wakati mwingine mitaro hufurika na kuchafua mazingira.

“Majengo ya jirani hapa yameweka mifumo ya nje ya kumwaga maji, sasa mvua ikinyesha maji yote yanaingia kwenye mfumo wetu na kwa vile wakati mwingine unakuwa umeziba, basi maji hufurika na kuleta kero kubwa ndani ya soko,” anasema Mzee Bogoma.

Kwa upande wake, Malamla anasema kwamba, bila DSSD kurekebisha mifumo ya majitaka, hali itaendelea kuwa tete na kuhatarisha afya za wafanyabiashara na walaji.

“Majengo mengine mara nyingi hutiririsha maji machafu kwa muda mrefu bila watendaji wa halmashauri kufuatilia, lakini ikitokea kwamba mfumo wetu, ambao ni mdogo na unazidiwa, ukatiririsha maji yenye damu kutokana na mitaro kuziba, hapa huwa ni mshike mshike,” anasema.

Amezitaka mamlaka husika kuhakikisha zinawajibika kwa nafasi zao ili kuweka mazingira bora katika soko hilo kwa kulinda afya za walaji na wafanyabiashara kwa ujumla, kwani huduma yao ni muhimu kwa afya ya binadamu na usafi ndiyo kipaumbele cha kwanza.

Kuhusu masuala ya utawala, Malamla ameupongeza uongozi wa TFC kwa kutambua shida zao pamoja na kuwapa miongozo ya mara kwa mara ambayo imezidi kuwaimarisha na kupata fikra mpya za uwekezaji.

 Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com. Simu: +255 656 331974.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AMJULIA HALI MZEE SIMAI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo alimtembelea na kumjulia hali Mzee Abdulrazack Mussa Simai 'Kwacha' ambaye amelazwa MOI.

Mzee Abdulrazack Mussa Simai 'Kwacha' ni Mzee wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia alishawahi shika nafasi mbali mbali za Uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wapigwa msasa jinsi ya kumpima mgonjwa umeme wa moyo (ECG)

$
0
0
 Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pal Bhadreshwara akionyesha namna  ya kumpima mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram - ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
 Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijadili namna  ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram - ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaonyesha wauguzi jinsi   ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram-ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
 Afisa Uuguzi kutoka  Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia Deconne Jones akiwaeleza jinsi ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram - ECG) Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Danieli Yohana (katikati) na Mali Sabuni (kulia) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayofanyika JKCI.
 Afisa Uuguzi kutoka  Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia Kiasha Munnis akifundisha jinsia   ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) kwa wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na wauguzi hao.
 Maafisa Uuguzi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia kwa makini maelekezo  ya  jinsi ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
 Maafisa Uuguzi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia kwa makini maelekezo  ya  jinsi ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
Mfunzo ya jinsi ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) yakiendelea.  
Picha na JKCI

Menejimenti ya TAA yakutana na Wajumbe wa TUGHE

$
0
0

  1. Kaimu Mwanasheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Joachim Maambo akijitambulisha kwenye mkutano wa Menejimenti na Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wa kuihusha mkataba wa zamani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango (wa kwanza kushoto) akiandika masuala mbalimbali kwenye mkutano wa wajumbe wa TUGHE na Menejimenti ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wa kuihusha mkataba wa zamani.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa mkutano wa Menejimenti na Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), akiandika masuala mbalimbali wakati wa kuihusha mkataba wa zamani.Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) na Menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuihusha mkataba wa zamani.
  

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATANO LEO NOVEMBA 22,2017

SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WAFANYABIASHARA WA MBOLEA WANAOKWEPA BEI ELEKEZI

$
0
0

Na EmanuelMadafa,Mbeya

SERIKALI imewataka wafanyabiashara wa mbolea nchini kuhakikisha wanafuata bei elekezi ya uuzaji wa mbolea iliyowekwa na serikali ili kumsaidia mfanyabiashara mdogo aweze kuuza kwa rejareja.

Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Naibu waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa wakati akifungua mkutano wamakatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini .

Amesema kuwa endapo itagundulika kwamba kuna mfanyabiashara wa jumla anamuuzia mfanyabiashara wa rejareja kwa bei itakayomfanya ashindwe kuuza kwa bei elekezi wizara itamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungia biashara yake

Mwanjelwa amesema ofisi yake inaushahidi kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wa jumla wamekuwa wakiwauzia mawakala wanaouza kwa bei elekezi ya serikali hivyo kuleta mkanganyiko na kuwafanya wauze mbolea hiyo kwa bei zaidi ya elekezi .

Amesema katika Mikoa ya Ruvuma,Lindi ,Mtwara ,Mwanza na Geita wapo wafanyabiashara ambao sio waaminifu wamekuwa wakifungua mifuko na kuuza mbolea ya kupandia (DAP) kwa Shilingi 2,000 kwa kilo kwa lengo la kujipatia kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kwa mfuko wa kilo 50 badala ya bei elekezi ya shilingi elfu hamisini na moja.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora wake kwa kufunguliwa kwa kuachwa wazi wafanyabiashara hao wanawaingizia hasara kubwa wakulima hasa katika kipindi cha mavuno.

Kutokana hali hiyo Naibu waziri huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kuacha tabia hiyo mara moja ili kumpa fursa Wakala aweze kuuza kwa bei ya rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao .

Mkutano huo unalenga kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system-BPS )na usimamizi wa mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata mbolea bora kwa bei nafuu sanjali na kuongeza usalishaji wenye tija.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza katika Mkutano wa Makatibu Tawala na Washauri wa kilimo wa Mkoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Katika KUKUMBI WA kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya Nov 21 ,2017. 
Washiriki wa Mkutano wa Makatibu Tawala Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini unaolenga kuongeza uwezo uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System -BPS) na Usimamizi wa bei ya mbolea ,katika ukumbu wa mikutano Mkapa jijini Mbeya Nov 21 mwaka huu. 
Mshiriki akichangia katika Mkutano huo.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa katika Piha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo.

Naibu Waziri Ulega akutana na wananchi wa kijiji cha Sunguvuni

$
0
0

 Naibu wa Waziri na Uvuvi,Abdallah Ulega akipokea taarifa ya ujenzi wa Zahanati ya Sunguvuni mkoani Pwani.


Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  amesema miundombinu ya barabara za vijiji zikijengwa zitafanya vijiji kuinuka kiuchumi.

Ulega aliyasema hayo wakati alipokutana na wananchi wa kijiji cha Singuvuni kata Mkuranga  wilayani Mkuranga, amesema kuwa taasisi ya barabara za vijijini na Mijini Tarura ni suluhisho kwa barabara za vijijini.

Amesema kuwa wananchi wa sunguvuni wanachangamoto ya barabara ambapo changamoto hiyo itatuliwa na Tarura.

Amesema kuwa Tarura itashighulika na  barabara katika wilaya ya Mkuranga na hatimaye wananchi wataweza kuinuka kiuchumi kutokana na miundombinu hiyo.

Katika ziara hiyo ametoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Sunguvuni pamoja na kuahidi mifuko 20 ya Saruji ili ujenzi huo uende kwa kasi

Aidha amesema kuwa wanachi Sunguvuni wafanye kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo kutokana na kuwa na ardhi yenye Rutuba.

Meneja wa Tarura wilaya ya Mkuranga,Peter Shirima amesema wameshatenga milioni 18 kwa ajili ya kushughulikia sehemu korofi na amesema barabara zote wameshazipitia na kilichobaki ni utekelezaji.
 Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo ,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Sunguvuni mkoani Pwani.
 .Meneja wa Tarura,Peter Shirima akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa barabara.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga, Ally Msikamo akizungumza juu ilani ya CCM na wananchi wa Sunguvuni mkoani Pwani.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
 Wananchi wa Sunguvuni mkoani Pwani  wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
Muonekano wa jengo la  Zahanati ya Sunguvuni mkoani Pwani.


KONGAMANO LA WASOMI WANATAALUMA KUFANYIKA JUMAMOSI HOTELI YA LANDMARK UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WANAFUNZI waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini Jumamosi ya Wiki hii wanatarajia kufanya kongamono kubwa la kihistoria kujadili namna watakavyoweza kutumia taaluma zao kusaidia jamii, kanisa na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

Alisema licha ya muungano huo kuundwa na vijana wa kikristo lakini vijana wote wasomi kutoka katika vyuo na shule za sekondari na madhehebu mbalimbali wanaalikwa ili kuchangia mada zitakazo jadiliwa na mgeni rasmi atakuwa ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

Mwambapa alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali na kuona ni jinsi gani kila mmoja na taaluma yake ataweza kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kuifanyia kazi.

"Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizurio kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mwambapa alisema kongamano hilo litafanyika Hoteli ya Landmark Ubungo jijini Dar es Salaam na litahudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali,sekondari baadhi wa viongozi.

 Mratibu wa Kongamamo la Wasomi Wanataaluma wa Kikristo liitwalo Tanzania for Jesus Prayer Movement ambalo mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus,  Ephrahim Mwambapa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Kanisa la Abundant Bressing Center (ABC), Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Hoteli ya Landmark siku ya Jumamosi. Kulia ni Mjumbe wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli.
Mratibu wa Kongamano hilo, Ephrahim Mwambapa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

NCC Yatakiwa Kuzingatia Ubora wa Miundombinu Nchini

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limetakiwa kuzingatia ubora katika kutekeleza kazi zake ili kuokoa fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa alipokuwa akijitambulisha na kuongea kwa mara ya kwanza na Wafanyakazi wa Baraza hilo jana jijini Dar es Salaam.Kwandikwa amesema kuwa Taasisi hiyo ni muhimu na ina manufaa kwa nchi ingawa kuna maeneo ambayo yanahitaji kusukumwa zaidi ili kazi zinazofanywa zizidi kuleta tija zaidi kwa Taifa.

“Baraza hili ni kama jicho katika Wizara kwa sababu majukumu yake yamejikita katika kusimamia Sera, hivyo Wafanyakazi tunatakiwa tujikite zaidi katika kufanya kazi zinazoonyesha ubora wa hali ya juu”, alisema Kwandika. 

Akizungumzia juu ya upunguzaji wa gharama za ujenzi, Naibu Waziri amesema kuwa gharama za ujenzi zinabadilika mara kwa mara, hivyo ni lazima zichunguzwe ili ujenzi ufanyike kwa bei ndogo lakini uwe katika kiwango bora zaidi na fedha zinazobaki zitumike kwa shughuli nyingine.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa NCC, Matiko Mturi amesema ili kutekeleza majukumu yake kikamilifu, kwa mwaka huu wa fedha Baraza limejiwekea malengo mbalimbali yakiwemo kukusanya maoni ya Wadau na kuandaa kuhusu utendaji wake ili kufanya maboresho ya utoaji wa huduma na shughuli zinazotekelezwa na Baraza.

Malengo mengine ni kuandaa na kukamilisha Kanuni za utekelezaji washeria, kuratibu na kutoa mafunzo kwa Wadau, kutoa ushauri wa kiufundi na kutatua migogoro, kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi inayotumia fedha za Umma pamoja na jitihada za kutunisha Mfuko wa Maendeleo ya Ujenzi.

“Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Oktoba mwaka huu, tumetoa ushauri mbalimbali ikiwa ni jukumu letu la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za kuishi za magomeni, tulitathmini usahihi wa idadi ya nondo katika ujenzi wa jengo la maabara iliyopo katika eneo la Mabibo, pia tulifanya tathmini ya thamani ya pesa katika jengo la dharura lililopo Makumbusho pamoja na tathmini ya kiufundi ya miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara”, alisema Mturi

Baraza la Taifa la Ujenzi lilianza kazi rasmi mwaka 1981 likiwa na lengo kuu la kuboresha shughuli zinazofanywa na Sekta ya ujenzi ambapo jukumu lake kubwa ni kutoa uongozi wa kimkakati wa kuendeleza Sekta ya ujenzi kwa nia ya kuboresha uwezo wa Wataalam na Taasisi za ndani zinazotoa huduma katika Sekta ya ujenzi.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Matiko Mturi (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa mara baada ya kuripoti ofisini hapo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi wa Baraza hilo.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Matiko Mturi (kulia) akitoa taarifa fupi mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa pamoja na wafanyakazi wa baraza hilo alipofika kwa mara ya kwanza ofisini hapo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi wa Baraza hilo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa akiongea na wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) jana Jijini Dar es Salaam katika kikao kilichofanyika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi hao.

AWESO AWATAKA WAKANDARASI KUWA WAZALENDO

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bubutelo wilayani Chemba.


Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza na wananchi wa Bubutelo katika ziara ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimia viongozi wa kijiji cha Bubutelo

Wananchi wa Bubutelo wilayani Chemba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.

WAZIRI JENISTA ATEMBELEA VITUO VYA HALI YA HEWA ARUMERU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mwikolojia Bi.Clara Manase alipokuwa akieleza faida ya kituo cha Utoaji wa Taarifa za Hali ya Hewa kilichojengwa katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha mkoani Arusha.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano na baadhi ya Watendaji wa Serikali alipofanya ziara Wilayani Arumeru kujionea Vituo vya Hali ya Hewa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Novemba 21, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano na baadhi ya Watendaji wa Serikali alipofanya ziara Wilayani Arumeru kujionea Vituo vya Hali ya Hewa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Novemba 21, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika ziara na Baadhi ya Watendaji wa Serikali walioongozana naye kutembelea Vituo vya Hali ya Hewa vilivyofungwa na Mradi waKuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Arumeru.

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images