Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO NOVEMBA 11,2017


DC IGUNGA HAITIMISHA ZOEZI LA KUPOKEA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH-OFAB

$
0
0
 Wakulima wa Kijiji cha Igogo wanaunda Kikundi cha Imala Makoye katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakiwa wameshika mbegu ya mahindi ya Wema 2109 baada ya kukabidhiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika jana wilayani huo. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa mkuu wa wilaya hiyo, John Mwaipopo.
 Kaimu Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Athumani Mgunya akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Igogo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi. Kulia ni Ofisa Ugani wa Kata ya Nanga, Ambele Mwangomo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akimkabidhi mbegu ya mahindi mkuu huyo wa wilaya ya Igunga.
 Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo akionesha mbegu hiyo kwa wakulima.


 Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo, akizindua upandaji wa mbegu hizo katika mashamba darasa ya wilaya yake katika Kijiji cha Igogo kwa  kupanda mbegu ya mahindi ya Wema.
 Wanakikundi wa Imala Makoye ambao ndio wasimamizi wa shamba darasa hilo wakiangalia mbegu hiyo ya mahindi.
 Mkulima wa Kijiji cha Igogo, Ibrahim  Salum akizungumzia changamoto za kilimo walizokuwa wakikabiliana nazo kwa matumizi ya mbegu za kienyeji walizokuwa wakizitumia.
 Mtafiti Dk. Betrice Lyimo, akishiriki kuandaa shamba darasa la Viazi Lishe katika Kijiji cha Mwanzugi kilichopo Kata ya Igunga. Kulia ni mkulima Solo Sai wa kijiji hicho na Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA mkoani Morogoro.
 Mtafiti Dk. Betrice Lyimo akizungumza na wakulima wa kijiji cha Mwanzugi.
 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru mkoani Mwanza, Mariana Ernest (katikati), akimuelekeza jambo mkulima wa Kijiji cha Mwanzugi Solo Sai (kulia), namna ya kupanda mbegu ya viazi lishe.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa mbegu bora hizo katika mkoa huo.

Na Dotto Mwaibale, Igunga Tabora

MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, John Mwaipopo amehitimisha zoezi la ugawaji wa mbegu bora katika mikoa ya Kagera, Geita na Tabora kwa kuipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwapelekea mbegu bora za mihogo, mahindi na Viazi lishe wilayani humo kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

Pongezi hizo alizitoa jana wakati akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Igogo kilichopo Kata ya Nanga katika uzinduzi na kukabidhiwa mbegu hizo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji vinne vya Igogo, Mwanzugi, Sungwizi na Busomeke.

Alisema changamoto kubwa waliyokuwa nayo wakulima katika Halmshauri hiyo ni kukosekana kwa mbegu bora za mihogo na mahindi jambo liliofanya uzalishaji wa mazao kuwa mdogo.

Mwaipopo alisema kuletewa kwa mbegu hizo kutaongeza mori wa kilimo kwa wakulima wa wilaya hiyo na kuondokana na ukosefu wa chakula badala ya kutegemea zaidi zao moja la mpunga.

Alisema kazi kubwa ya serikali ni kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa mradi huo kwa nguvu zote ili kazi kubwa iliyofanywa na watafiti kutoka Vituo vya Ukiliguru Mwanza, Maruku mkoani Tabora na Ilonga mkoani Morogoro isipotee bure.

Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hizo ya mihogo aina ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana ina uwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa kama ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima na ya mahindi ikistahimili hali ya ukame na kutoa mazao mengi.

Mutagwa aliwaomba wakulima hao kuyatunza mashamba hayo ambayo yamegharimu fedha nyingi hadi kukamilika kwake hivyo wayaendeleze kwa ajili ya kuja kutoa matunda kwa wakulima wa wilaya hiyo na kupata chakula cha kutosha na ziada kuuza.

Akieleza lengo la COSTECH na OFAB kuendesha program hiyo ya kugawa mbegu katika mikoa ya Kagera, Geita na Tabora, Mtafiti kutoka OFAB, Dk. Beatrice Lyimo alisema kuwa kazi ya COSTECH ni kuhakikisha matunda ya kazi nzuri za tafiti yanawafikia wakulima na wananchi wengine kwenye Nyanja mbalimbali hivyo hii ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

Alisema kwa miaka mingi tafiti mbalimbali nzuri zimekuwa zikifanywa na watafiti hapa nchini lakini haziwafikii walengwa akitolea mfano wakulima,lakini COSTECH ikatafuta fedha na kuitoa tafiti hiyo kwenye vituo vya utafiti na kuwapelekea wakulima ili kusaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabili kwenye kilimo chao.

Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa mbegu bora za mazao hayo kwenye wilaya tano za mkoa huo ambazo ni Urambo, Sikonge, Uyui, Nzega na Igunga alisema mbegu hizo zitatoa faraja na uzalishaji mkubwa wa mazao kwa wakulima.

Alisema kuwa wakazi wa mkoa huo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupata chakula kidogo kutokana na kutegemea mazao ya chakula mihogo na viazi vitamu lakini kwa kupata mbegu hizo watapata mazao mengi.

Alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora hizo kutawasaidia wananchi kupata chakula cha kutosha na lishe bora kutoka kwenye viazi lishe na akachukua fursa hiyo kuishukuru  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo OFAB kwa kuwapelekea mbegu hizo.

Alitaja mbegu walizopata kutoka COSTECH na OFAB kuwa ni pingiri za mihogo 38,000, mbegu za viazi lishe 75,000 na mahindi kilogramu 50.

Alisema jumla ya vikundi 26 na wakulima 557 wa mkoa huo wamenufaika na mradi huo na kuwa mkoa umeamua kuanzisha kilimo cha mazao mengine ya biashara ya korosho na alizeti ili yawe mbadala wa zao la tumbaku ambalo limekuwa likiharibu mazingira.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushiriana na  Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), waligawa mbegu za migomba, viazi lishe, mihogo, na mahindi katika Mikoa ya Kagera, Geita na Tabora ili kuinua kilimo na uzalishaji wa mazao ya chakula ambapo zoezi hilo lilifikia tamani jana wilayani Igunga mkoani Tabora.

MHANDISI MTIGUMWE ATANGAZA KIAMA KWA MAAFISA UGANI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akiwasili katika Ofisi za Taasisi ya Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru). Mwingine ni
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Taasisi ya Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Afisa Mfawidhi -Horti-Tengeru akisoma Risala kwa niaba ya watumishi wenzanke wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Bi Alice M. Kavishe akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.

Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Dkt Stephen Sebastian Kuoko akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.

Na Mathias Canal, Arusha

Serikali imekuwa ikiongeza idadi ya wanafunzi katika Vyuo vya Kilimo na kwa sababu hiyo Maafisa Ugani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka ambapo hali hiyo imewezesha Karibu kila Kata hapa nchini kuwa na Afisa Ugani.

Lakini pamoja na kuwepo kwa wataalamu hao wa kilimo bado uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini yakiwemo mazao ya chakula na biashara si wa kuridhisha ambapo wakulima wanalima na kupanda pasina hata kufuata hatua za kitaalamu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi akizungumza na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI TENGERU) kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Alisema lengo la Serikali kusambaza  Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ilikuwa  kuwasaidia  wakulima  waweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi na kuongeza mavuno.

Hata hivyo jambo hilo limekuwa kinyume kwani asilimia kubwa ya maafisa ugani ama hawafanyi kazi zao ipasavyo ama wameshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Wizara ya kilimo inaandaa utaratibu wa kuwarudisha shule maafisa ugani wasiofaa kutokana na uchache wa ellimu zao na uwajibikaji huku wale ambao watashindwa kabisa kuwa msaada kwa wakulima baada ya masomo wizara itapendekeza waondolewe kazini.
Alisema Maafisa ugani hao Watafanyiwa usaili upya ili kubaini uwezo wao kwani wengi wao wameajiriwa na serikali lakini wakulima hawanufaiki na kilimo tafsiri yake Wataalamu hao ama hawatekelezi wajibu wao au hawana uwezo wa kutekeleza ipasavyo.

Aidha, alisema Maafisa ugani kote nchini wanatakiwa kuwekeza kwenye utoaji wa Huduma ya  Ugani kwa Wakulima  ili iwe rahisi kwa Mkulima kusaidika katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ya biashara na kilimo.

Sambamba na hayo pia aliwasihi Wakufunzi katika chuo hicho kujiendeleza kielimu huku akisema kuwa Wizara ya kilimo lazima itengeneze mpango wa kuwaendeleza wakufunzi ili kuzalisha wataalamu wenye ufanisi zaidi.

Alisema anatambua kuwa Mahitaji ni makubwa katika vyuo vya kilimo hivyo Wizara inatazama namna ya kuongeza chuo kingine kama hicho huku akiwasisitiza wataalamu hao kubadili mfumo badala ya kusoma kwa jumla masomo mengi na kufikia hatua ya kuchagua eneo maalumu la kusoma (Kozi) kwani Kilimo ni somo pana.

“Nategemea muandae mpango maalumu ambao utapelekea Kuwa na kozi za muda mchache sio lazima kuwa na kozi za muda mrefu pekee kama ilivyo hivi sasa” Alisema Mhandisi Mtigumwe

Katika hatua nyingine amewataka Watumishi wote kuongeza spidi katika utendaji wa kazi ili kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali ya awamu ya tano yenye kauli mbiu ya HapaKaziTu.

Sambamba na kutembelea na kuzungumza na watumishi na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mbogamatunda na Maua (HORTI TENGERU) Akiwa ziarani Mkoani Arusha Katibu Mkuu Mhandisi Methew Mtigumwe alitembelea pia Taasisi ya Utafiti Horti Tengeru, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kaskazini (NZARDI) na Taasisi ya Utafiti ya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki.

YALIYOSEMWA NA DK. HASSAN ABBAS KATIKA KIPINDI CHA VIJANA TZ JUU YA MAFANIKIO /UTENDAJI WA SERIKALI NA CHANGAMOTO KATIKA TASNIA YA HABARI

$
0
0
“Ofisi yangu ina jukumu la kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ya Serikali; Kusajili na kufungua Magazeti; Kusaidia Watu wa mifumo mingine ya Serikali kusema” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Uhuru wa vyombo vya habari upo wa kutosha. Serikali imeruhusu uhuru wa Vyombo vya habari. Kuna Redio zaidi ya 150, tuna redio zaidi ya 30, kuna Magazeti zaidi ya 110 yanayotoka nchini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Serikali ina simamia Wananchi wapate habari sahihi na si kulishwa habari mbovu. Serikali tunalisimamia hili” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu.“Changamoto iliyopo ni kuhakikisha habari zsahihi zinawafikia Watu wote kwa wakati” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Rais @MagufuliJP amefanikiwa sana kuleta mageuzi ya kifikra. Kujenga hari ya Uzalendo, nidhamu, uwajibikaji kwa Watu wake wakiwemo Watumishi wa Umma na Wananchi” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu.“Rais @MagufuliJP ameleta nidhamu kubwa ya matumizi ya fedha za umma. Mathalani amefanikiwa kudhibiti safari za nje zisizo na tija” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Hapo nyuma zilitumika bilioni zaidi ya 200 kwa safari tu wakati hivi sasa zimetumika bilioni 25 tu kwa safari tumeokoa pesa nyingi”@TZ_MsemajiMkuu

“Rais @MagufuliJP ameleta mageuzi ya kudhibiti Wafanyakazi hewa zaidi ya 20,000 na kuokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 238. Ni mageuzi makubwa” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Tumeondoa wafanyakazi hewa takribani elfu 20 kwa zoezi hilo tumeokoa bilioni 238” @TZ_MsemajiMkuu.“Hawa wanaopiga kelele juu ya mageuzi ya rasilimali za madini. Ipo siku watanyamaza wakiona manufaa ya wazi. Serikali ya @MagufuliJP imeonyesha uzalendo kwenye madini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu.“Zipo nchi kubwa duniani awapati 50/50 kwenye Madini sisi tumeweza @TZ_MsemajiMkuu

“Serikali itaendelea kuhakikisha kila kilicho chetu tunakipata”@TZ_MsemajiMkuu

“Kwenye vyeti feki Serikali ya Rais @MagufuliJP imeokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 148 ambazo zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo.” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Sekta ya habari ni sekta nyeti na Sheria hii ya habari tuliyo nayo sasa imeleta maboresho na ubora kwenye sekta ya habari nchini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Huwezi kutoa habari kwa kuingilia faragha ya mtu” @TZ_MsemajiMkuu

“Huwezi ukakiacha kituo cha radio kinawachochea wakulima wakawaue wafugaji arafu ukasema wana haki ya habari “@TZ_MsemajiMkuu

“Sheria mpya ya huduma ya habari vimeweka ustawi wa vyombo vya habari na si kweli ipo kwa ajili ya kufungia habari.” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Popote duniani hakuna nchi yenye sheria inayosema andika chochote” @TZ_MsemajiMkuu

“Hakuna nchi yeyote Duniani inayotoa Uhuru kwa vyombo vyao vya habari kuwa na uhuru wa kuandika chochote kile wanachojisikia” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Uandishi wa habari ni taaluma sasa ukikiuka sisi kama serikali hatuwezi kukuacha”@TZ_MsemajiMkuu

“Sisi tunailea sekta yote ya habari”@TZ_MsemajiMkuu
“Wananchi wapuuze habari kuwa Serikali inafungia vyombo vya habari inapojisikia bali ina zingatia sheria” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Chombo cha habari kinatakiwa kifuate miiko”@TZ_MsemajiMkuu

“Vijana waamue kufanya kazi, wawe Wazalendo, wamwogope Mungu. Safari ya Mabadiliko ni ngumu lakini inahitaji uvumilivu” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Watanzania wamuunge mkono Rais @MagufuliJP atimize utekelezaji wa ilani ya uchaguzi” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Mwakani 2018 mwezi Julai Serikali italeta ndege kubwa ya kisasa itakayokuwa inakwenda popote pale Duniani” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

Mheshimiwa Rais @MagufuliJP alikuta mikopo inatolewa kiasi cha bilioni 48 kwa mwaka Lakini sasa hivi tumefikia bilioni 472 @TZ_MsemajiMkuu

“Fedha zipo na watapata kila mwanafunzi mwenye haki ya kupata”@TZ_MsemajiMkuu

“Serikali ya Rais @MagufuliJP inatoa Tsh. Bilioni zaidi ya 400 kwa Wanafunzi. Kwa mara ya kwanza fedha imetangulia vyuoni kabla ya Wanafunzi kuanza masomo” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Serikali imeboresha makusanyo kutoka Tsh. Trilioni 9.9 mpaka Tsh. Trilioni 14 kwa mwaka” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

Mheshimiwa @MagufuliJP alipoingia madarakani tulikuwa tunakusanya kodi kwa kiasi cha “Trilioni 9.9.Leo hii tunakusanya trilioni 14 kwa mwaka haya ni mafanikio makubwa”@TZ_MsemajiMkuu

“Serikali imeleta miradi ya kihistoria nchini ya kuzalisha umeme kupitia miradi ya Kinyerezi 1 & 2” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Hivi tunapozungumza kuna watu hawalali kuna watu wanajenga reli Usiku na mchana”@TZ_MsemajiMkuu

Dk. Hassan Abbas ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari na Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali aliyasema hayo katika kipindi cha VijanaTz kilichorushwa Mubashara siku ya Ijumaa Novemba 10, 2017 kupitia mitandao ya kijamii ya UVCCM ya Twitter, Facebook na Instagram

IMEANDALIWA NA;

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi 
UVCCM Taifa

Rais Magufuli amaliza ziara ya siku 3 Uganda, Rais Museveni atoa tamko dhidi ya ICC

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye gwaride la Kimya lililoandaliwa kwa heshma na Jeshi la Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uganda na kurejea nchini.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifurahia ngoma ya asili iliyokuwa ikipigwa na watoto wa nchini Uganda katika eneo la mpakani la Mutukula kabla ya kurejea nchini.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mpakani Mutukula upande wa Tanzania mara baada ya kuwasili akitokea Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mpakani mwa Tanzania na Uganda (Mutukula) kuhusu  ujenzi wa barabara ya Kutoka Miziro hadi Mutukula bila kupitia wilayani Misenyi. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mpakani Mutukula upande wa Tanzania mara baada ya kuwasili akitokea Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mpakani Mutukula upande wa Tanzania mara baada ya kuwasili akitokea Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wakuu wa Majeshi ya Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake nchini Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa mpakani  Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tau nchini Uganda. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa mpakani  Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tau nchini Uganda. PICHA NA IKULU

WADAU WA MADINI WATAKIWA KUHAKIKISHA MADINI YANANUFAISHA JAMII

$
0
0
Wadau wa madini wametakiwa kuhakikisha sekta hiyo inaakisi maendeleo ya jamii inayozunguka eneo hilo ili waone faida ya kuwepo kwa rasilimali hiyo muhimu. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Luhumbi aliyasema hayo mjini Geita kwenye ufunguzi wa majadiliano ya wachimbaji wadogo Tanzania yaliyowashirikisha wadau wa madini wa nchi mbalimbali duniani. 

Akizungumza kabla ya washiriki hao hawajaanza safari ya kutembelea migodi ya madini ya dhahabu, Luhumbi alisema faida ya uwepo wa madini hayo inapaswa kuonekana dhahiri kwa jamii. Alisema uwepo wa rasilimali ya madini ya dhahabu mkoani Geita bado haujaonekana ipasavyo kwa jamii ya eneo hilo kwani zinapaswa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara, maji, elimu, afya na mengineyo. 

"Hatutaki kuona rasilimali ya madini inaoneka kuwa ni laana kwa jamii badala ya baraka, kwani kupitia tunu hiyo wananchi wanapaswa kunufaika kwa kuona maendeleo yanafanywa kwenye maeneo hayo," alisema Luhumbi. Alisema sekta ya wachimbaji wadogo wa madini inafanywa na idadi ya watu milioni moja hadi milioni moja na nusu nchini hivyo wanapaswa kuwekewa mazingira rafiki yatakayoboeesha maisha yao. 

Mkurugenzi wa asasi ya Haki Madini, Amani Mhinda alisema wameandaa mdahalo huo kwa uwezeshwaji wa taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo  (IIED) kituo cha kimataifa cha utafiti wa misitu (CIFOR) na kampuni ya ushauri ya MTL. Mhinda alisema lengo ni kutoa suluhu juu ya changamoto zinazomkumba mchimbaji mdogo nchini na kupendekeza majawabu. Alisema sekta ya uchimbaji madini nchini ni kati ya sekta zinazokua kwa kasi kubwa na yenye mchango mkubwa wa uchumi wa Taifa. 

Alisema ingawa mipango mahususi ya kisera juu ya uchimbaji mdogo imeanzishwa, bado kuna changamoto nyingi hasa katika uelewa, ujasiri, mipango, fedha na taratibu zinazokwamisha utekelezaji wa sera na maboresho. Mchimbaji wa madini wa kampuni ya Nsangano Gold mine, Renatus Nsangano alisema bado wachimbaji wadogo wana changamoto ya kufanya kazi bila kufanya utafiti. Nsangano alisema endapo wangekuwa wanafanya utafiti na kubaini madini yalipo ingekuwa na tija kubwa kwa wachimbaji wengi. 

Hata hivyo, alisema wamesaidia jamii zinazowazunguka kwenye maendeleo mbalimbali ikiwemo ya sekta ya elimu, afya na maji. 
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Luhumbi akizungumza na wadau wa madini juu ya rasilimali hiyo kunufaisha jamii inayozunguka eneo hilo. 
 Mkurugenzi wa kampuni ya Nsangano Gold mine ya Nyarugusu Mkoani Geita Renatus Nsangano (kulia) na Mkurugenzi wa kampuni ya Kadeo, Christopher Kadeo (wa pili kulia) wakiwa na wadau wa madini waliotembelea migodi yao ya dhahabu. 
 Mdau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Joseph Lyimo akivuta udongo kwa kutumia nyenzo katika mgodi wa dhahabu kwenye machimbo ya wachimbaji wadogo wa Nyarugusu Mkoani Geita. 
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wa mgodi wa Nsangano Gold mine ya Nyarugusu Mkoani Geita, wakiendelea na shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kwenye moja kati ya migodi yao.

Alpha Abdul ashinda kinyang'anyiro cha Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 Mtwara

$
0
0

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Mtwara, Alpha Abdul akionesha umahiri wake wa kufokafoka kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mshindi wa shindano hilo la kusaka vipaji leo.
Tano bora walioingia kwenye mchujo wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 mkoani Mtwara.

Majaji wakiongozwa na Nickson George (katikati) wakijadili jambo.
 Tatu bora walioingia kwenye mchujo wa Tigo Fiesta Supa Nyota Mtwara.


WANAFUNZI 250 WAPATA MAFUNZO YA GIRL GUIDES TEMEKE

$
0
0
 Baadhi ya  Girl Guides ambao ni wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za Manispaa ya Temeke wakionesha moja ya alama muhimu za Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), baada ya kupata mafunzo ya awali  katika Shule ya Msingi Mbagala, Dar es Salaam leo. Wanafunzi wa kike 250 walishiriki mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke,  Leonida Komba ( wa tatu kushoto waliosimama)

Girl Guides hao walipata mafunzo kuhusu historia ya Girl Guides duniani, kanuni, malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwake.

Pia hufundishwa ujasiri, ukakamavu, mambo ya uongozi, maadili, kujitolea pamoja na uzalendo.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke, Leonida Komba (kushoto) akiwahamasisha Girl Guides wakati wa mafunzo hayo




 Girl Guides wakiwa na furaha baada ya kupata mafunzo ya chama hicho kuhusu kanuni, historia ya Girl Guides Duniani, malengo na madhumuni yake.
Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke, Leonida Komba (wa pili kulia waliosimama) akiwa na walimu ambao ni walezi wa Girl Guides wa shule walikotoka wanafunzi hao.

Kamati Kuu ya AFCON yazinduliwa

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON under 17 mikakati mbalimbali itakayosaidia kufaikisha mashindano ya 2019 yatakayofanyika nchini (kulia) Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw Leodgar Tenga
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON Bw Leodgar Tenga (kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya mashindano yatakayofanyika 2019 nchini katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe na (kushoto ) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wallace Karia.



Na Anitha Jonas – WHUSM-Dar es Salaam

Serikali yazindua Kamati Kuu ya maandalizi ya Africa Cup of Nation Under 17 (AFCON) yenye wajumbe ishirini na tano kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika nchini mwaka 2019.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa uteuzi wa wajumbe hao wa kamati ulizingatia sekta muhimu zitakazo husika moja kwa moja katika kufanikisha mashindano hayo.

“Nawapongeza wajumbe wote kwa kukubali uteuzi huu maana kazi ya kamati hii si ya kulipwa bali ni kujitolea kwa manufaa ya nchi yetu na ninaimani kubwa kuwa tutafanya kazi nzuri na kwa kufanikisha mashindano haya tutakuwa tumelipa taifa heshima kubwa katika ulimwengu wa soka”,alisema Mhe.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo Mhe. Mwakyembe alisema kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo atakuwa yeye mwenyewe, Makamu Mwenyekiti atakuwa Mjumbe wa CAF na Rais wa heshima wa TFF Bw. Leodgar Tenga pamoja na Bw.Hendry Tandau kutoka Kamati ya Olimpiki nchini ambaye atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Leodgar Tenga alitoa angalizo kwa TFF kuzingatia kigezo cha umri kwa watoto hao wanaowaanda kwa ajili ya mashindano hayo ili kuepuka kuvunja sheria kwani mashindao hayo yanalega vijana waliyochini ya umri wa miaka kumi na saba na si zaidi ya hapo.

Pamoja na hayo Kamati hiyo inawajumbe mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Paul Makonda,Mkurugenzi wa ATCL Bw.Ladislaus Matindi,Mohamed Dewji na wengine.

Mamlaka za Maji Nnchi Zatakiwa Kuanzisha Vituo Maalum vya Kupokelea Malalamiko ya Wateja

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Meja Jenerali Kitundu, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Hapi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Shirika hilo mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Wafanyakazi wa Dawasco Bw. Abdallah Jongo akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi wa Shirika hilo mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele (mwenye tai) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele (kulia) akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco) Mhandisi Cyprian Luhemeja zawadi ya saa yenye picha za wajumbe wa Bodi ya Dawasco iliyomaliza muda wake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo pamoja na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Dawasco Prof. Toli Mbwete (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi mpya ya Tano ya Wakurugenzi wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco) mara baada ya kumaliza hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele akiwasili katika viunga Mako Makuu ya Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco)kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo, Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasco Prof. Tolly Mbwete na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.

SPIKA NDUGAI AZINDUA HOTELI YA FANTASY MSALATO, MJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Hoteli ya Fantasy iliyojegwa katika Kata ya Msalato, Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Mhe. Mussa Hassan Mussa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Amani, Zanzibar na ayefuatia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula . Wengine katika picha kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony Mavunde na Mbunge wa Kijitoupele, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiweka Jiwe la msingi la Ujenzi wa Awamu ya pili ya Hoteli ya Fantasy iliyopo Msalato, Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Mhe. Mussa Hassan Mussa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Amani, Zanzibar na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony Mavunde
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akipanda Mti mara baada ya kuzindua Hoteli ya Fantasy iliyojegwa katika Kata ya Msalato, Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza wakati alipokwenda kuzindua Hoteli ya Fantasy iliyojegwa katika Kata ya Msalato, Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Mhe. Mussa Hassan Mussa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Amani, Zanzibar. Wengine katika picha kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde na anayefuatia ni Mbunge wa Kijitoupele, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha.


PICHA NA BUNGE

RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akikagua kitalu cha miche ya Mikorosho ambayo itaanza kugaiwa bure kwa wananchi kwa lengo la kuipanda na kukuza kilimo cha zao la korosho wilayani Mpwapwa
Sehemu ya Kitalu cha Miche ya Mikorosho kilichopo eneo la Magereza Mpwapwa, jumla ya tani sita (6) za mbegu bora za mikorosho zimeoteshwa kwa lengo la kugawa bure miche ya mikorosho kwa wananchi kuipanda na kukuza kilimo cha zao hilo Wilayani Mpwapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge namna miti ya mikorosho ilivyozaa korosho kwenye shamba darasa la Magereza Mpwapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha kukamua mbegu za alizeti na usindikaji mafuta ya alizeti cha mjasiriamali Ndg. Sangito Akyoo. 



Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge amewataka watumishi wa Umma na Taasisi mbalimbali kwenye Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuwahudumia Wananchi kikamilifu na kwa uadilifu wakitambua kuwa sasa Mkoa wa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.

Aidha amesema yapo baadhi ya maeneo Mkoa bado haufanyi vizuri hususani katika sekta ya elimu ambapo hali ya ufaulu hairidhishi.

Akiwa wilayani Mpwapwa katika ziara yake ya kutembelea wilaya za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kujitambulisha Dkt. Mahenge amesema eneo la Elimu ya Msingi na Sekondari hali ya ufaulu hairidhishi ambapo Mkoa umeshika nafasi ya 24 kati ya Mikoa 26 kwenye matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017, Wakati kwa upande wa Matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne mwaka 2016 Mkoa ulikuwa wa 19 kati ya Mikoa 26.

Amesema viongozi hao wanayodhamana kubwa kwa Wanadodoma kwenye masuala yote ya maendeleo kama vile Elimu, Afya, Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kutumia fursa ya kuwa jirani na Serikali katika kusukuma mbele masuala ya Maendeleo kwenye Mkoa.

Amewataka Viongozi na Watendaji wote kwenye Wilaya za Mkoa wa Dodoma kutambua wana jukumu kubwa la kusimamia elimu kwenye Wilaya zao na ameagiza kila Wilaya ikae na kufanya tathimini ya sababu ya kufanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani ya msingi na sekondari na kutafuta majibu ya changamoto hizo na pia kubuni mikakati itakayo ukwamua Mkoa kielimu na baadae mipango hiyo ya Wilaya ijadiliwe pamoja ili kutoka na mkakati mmoja wa Mkoa wa kupandisha hali ya Elimu na Ufaulu kwenye Mkoa wa Dodoma.

Dkt. Mahenge amezitaka Wilaya za Mkoa wa Dodoma kujipanga vizuri kwenye Sekta ya kilimo akiainisha kuwa Viongozi na Watendaji kwenye Mkoa wana jukumu la kuhakikisha tatizo la upungufu wa chakula linakuwa historia kwenye Mkoa wa Dodoma kwa kuhimiza Wananchi wetu kulima mazao yenye kustawi hata katika mazingira ya maji kidogo na hali ya hewa ya Mkoa wa Dodoma kama Mtama, Uwele, Muhogo na Alizeti.

Aidha, Katika kukuza mapato na uchumi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, Dkt. Mahenge amezitaka Halmashauri hizo kwa sasa kuanza uwekezaji kwenye kilimo cha Korosho ambacho kimewasaidia wakulima wengi kuinua hali ya uchumi kwenye maeneo wanayolima zao hilo.

Amesema tayari wataalamu wa kilimo wamebainisha kuwa zao hilo linauwezo wa kustawi vizuri na kuwa na mavuno ya kuridhisha kwenye Mkoa wa Dodoma na kiuchumi soko la Korosho lipo na bei ya zao hilo kwenye soko ni nzuri. Ameipongeza Wilaya ya mpwapwa kwa jitihada walizoanza za kuwekeza kwenye kilimo cha Korosho na amezitaka Wilaya nyingine Mkoani Dodoma kuona namna nazo zinavyoweza kuanza utekelezaji wa mpango huo wa kilimo cha Korosho.

Dkt. Mahenge amezitaka Wilaya za Mkoa wa Dodoma kuweka mkakati wa utekelezaji wa Kampeni ya Serikali ya Uanzishaji wa Viwanda kwa kila Mkoa uliozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Seleman Jafo kwa kuzishirikisha hadi ngazi za chini kwenye wilaya zetu na kutaka mkakati huo ulenge kuanzisha viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotokana na malighafi ya mazao yanayolimwa kwenye Mkoa wa Dodoma.

Aidha, ametaka Mkakati huo wa uanzishaji Viwanda kwa kila Wilaya uwajumuishe Vijana na Wanawake, kwa kuwaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Dodoma kuhakikisha wanatenga asilimia kumi (10%) kwenye bajeti zao za Halmashauri kwa ajili ya miradi ya uzalishaji mali na uchumi kwa vijana na wanawake, na fedha hizo zipelekwe kwenye kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa ajili ya makundi hayo.

Dkt. Mahenge amebainisha kuwa tayari amekutana na kuzungumza na makundi mbalimbali kwenye Mkoa yakiwemo ya Wazee, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Wafanyabiashara na Wakuu wa Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu ambapo amekutana na Malalamiko ya baadhi ya watumishi kutokuwa waadilifu na kutotekeleza wajibu wao ipasavyo wa kuwahudumia wananchi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri amemwelezea Dkt. Mahenge kuwa bado Makusanyo ya Wilaya hiyo hayaridhishi kwani kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Wilaya ya Mpwapwa ililenga kukusanya zaidi ya shilingi 2,800,000,000 lakini mapato halisi yalikuwa Shilingi takribani Bilioni moja, akibainisha kuwa hali hiyo inatokana na uchache wa vyanzo vya mapato hivyo ili kukuza mapato na hali ya uchumi tayari Wilaya ya Mpwapwa imeanza utekelezaji wa Mkakati wa kukuza kilimo cha Korosho.

“Kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho tayari Wilaya ya Mpwapwa tumepokea jumla ya tani sita (6) za mbegu bora na za muda mfupi za Korosho na pia tumefikia makubaliano na Bodi ya Korosho ya kujenga kiwanda cha kubangua Korosho hapa Mpwapwa jambo ambalo litakuza sana kilimo cha korosho na kuingizia Wananchi na Wilaya kwa ujumla pato kubwa na kukuza uchumi” amebainisha Mheshimiwa Shekimweri.

Mheshimiwa Shekimweri amesema tayari Wilaya ya Mpwapwa imeanza kuitikia Maelekezo ya Serikali ya kuanzisha Viwanda na tayari Wilaya imetenga eneo la hekta 3.7 kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda ambapo baada ya upimaji wa eneo hilo jumla ya viwanja 40 vilipatikana kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Pamoja na kuzungumza na watumishi wa Serikali Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge alitembelea kitalu cha miche ya Korosho kwenye Gereza la Mpwapwa,alitembelea kituo cha utafiti wa Mifugo Mpwapwa, Mradi wa kiwanda cha kukamua alizeti na kujibu kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Chitemo.

MAHAFALI YA TISA YA KIDATO CHA NNE KOM SEKONDARI 2017 YAFANA

$
0
0
Shule ya Sekondari Kom iliyopo mjini Shinyanga leo Jumamosi Novemba 11,2017 imefanya mahafali ya 9 ya kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2006. 

Mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne mwaka 2017 yaliyohudhuriwa na wazazi na wageni mbalimbali alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.

Akizungumza katika mahafali hayo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema mabadiliko yoyote yanaletwa na ushirikiano hivyo kupitia ushirikiano.lisema shule hiyo imekuwa maarufu nchini kutokana na elimu bora inayotoa na kutokana na hali hiyo imeupatia sifa mkoa wa Shinyanga.

“Sisi kama serikali tunajivunia uwepo wa shule hii katika mazingira yetu kwani inatutangaza, tupo tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto zinazojitokeza ili kusukuma gurudumu la maendeleo”,alieleza Matiro.“Tupo tayari kuhakikisha kuwa tunashirikiana na sekta binafsi na milango yetu ipo wazi na panapotokea changamoto msisite kutufikia”,alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi kuwekeza kwenye elimu kwa watoto kwani huo ndiyo urithi wenye thamani katika maisha yao.Katika hatua nyingine aliipongeza shule hiyo kuajiri watu 63 katika shule kwani wanaunga mkono lengo la serikali la kuzalisha ajira kwa wananchi.
Aidha aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha shule ya awali na msingi kitendo ambacho kinatokana na ushirikiano uliopo kati ya shule na wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kusukuma maendeleo ya shule.

Matiro aliwataka wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kuwa mfano katika maeneo wanakokwenda na kuhakikisha matendo yao yanaendana na mambo waliyofundishwa shuleni.Naye Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi aliishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapa katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inafikia malengo yake.

Alisema Kom sekondari shule hiyo imetimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake na imekuwa daraja la elimu kwa wanafunzi ambao wengi wamekuwa wakiingia kidato cha tano na kujiunga katika vyuo mbalimbali.“Shule yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani,mfano kati ya wanafunzi 160 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2015,145 walijiunga na masomo ya kidato cha tano,na mwaka 2016 kati ya wanafunzi 144 waliofanya mtihani wa kidato cha nne,133 walijiunga kidato cha tano”,aliongeza Koyi.

“Naomba wazazi muendelee kutuamini na kuleta wanafunzi katika shule hii ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali”,alieleza Koyi.Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo,Mwita Warioba alisema shule hiyo hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 542,walimu 32 huku akisisitiza kuwa lengo la shule hiyo ni kutoa elimu bora na tayari shule hiyo pia imeanzisha shule ya awali na msingi.“Shule yetu ina miundo mbinu ya kutosha,madarasa yapo ya kutosha,tuna umeme wa Tanesco,maji kutoka ziwa Victoria,mabweni 8,viwanja vya michezo,maktaba moja,maabara mbili ikiwemo ya Computer”,aliongeza Waryoba.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne,Jackline Benson alisema walianza kidato cha kwanza wakiwa 104,ambapo wavulana walikuwa 52 na wasichana 52 lakini idadi iliongezeka na hivyo idadi ya waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 154,kati yao wasichana ni 73 na wavulana 81. 
Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2017 katika shule ya sekondari Kom wakimpokea mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya shule hiyo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom,Jackton Koyi akimpokea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa ajili ya kushiriki mahafali ya kidato cha nne katika shule hiyo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwapungia mkono wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom .
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom .
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Zena Ali akimweleza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro historia ya shule ya sekondari Kom wakati wa maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika shule hiyo 
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kom wakionesha ramani ya dunia kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa maonesho ya taaluma wakati wa mahafali hayo 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Rajuu Masudi ambaye ni mtaalamu wa kuchora akieleza kuhusu sanaa ya uchoraji inayofanywa na wanafunzi wa shule ya sekondari Kom 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kom,Safia Ali akitoa maelezo kuhusu maonesho ya sayansi kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Wahitimu wa kidato cha nne 2017 katika shule ya sekondari Kom wakiandamana 
Wahitimu wakiandamana kuelekea ukumbini
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom.Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule Peter Kugulu,kushoto ni mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi 
Wahitimu wakiingia ukumbini 
Mkuu wa shule ya sekondari Kom,Mwita Waryoba akielezea historia ya shule hiyo
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi akizungumza wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom 
Wahitimu wa kidato cha nne wakipunga mkono 
Wahitimu wa kidato cha nne,Scholastica Simon na Dickson Nyansika wakikata keki wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka 2017 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimlisha keki mhitimu wa kidato cha nne Dickson Nyansika 
Mahafali yanaendelea 
Wanafunzi wakiwa wamevaa mavazi mbalimbali ya ubunifu 
Wanafunzi wakiimba shairi 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ANGALIA PICHA NYINGI ZAIDI ZA MAHAFALI <>

WATU WATANO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA AJALI YA LORI NA NOAH MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Habari kutoka Wilayani Hai,mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa watu watano wanadaiwa kupoteza na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia ajali ya Lori kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Noah maeneo ya kikavu kwa Sadala.

Aidha ,taarifa za awali kutoka kwa Daktari wa zamu hospitali ya wilaya ya Hai,Agness Temba alieleza kuwa,katika ajali hiyo wamepokea miili ya watu wa tano.Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Hai, na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.





Wasanii watembelea Duka la Tigo mjini Mtwara

$
0
0
Wasanii Stamina na Chege wakiwa na mtoa huduma ya mauzo wa duka la Tigo Mtwara, Farida Salum wakiangalia simu zinazouzwa, mara baada ya wasanii wa Tigo Fiesta walipotembelea duka hilo leo.
Wafanyakazi wa duka la Tigo mjini Mtwara wakipiga picha ya pamoja na msanii Janjaroo.
Wateja wakipata huduma leo.
Mashabiki wa muziki wa bongo fleva wakishuhudia wasanii waliotembelea duka la Tigo mtaa wa stand kuu mjini Mtwara.
Wasanii Genevieve na Lulu Diva wakimkabidhi Fulana na Tiketi ya kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta mjini Mtwara, Ramadhani Kimango
Wasanii Madee na Mr. Blue wakimkabidhi zawadi fulana na tiketi mteja wa Tigo, Hassan Mussa ya kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta mjini Mtwara leo.
Msanii Aslay akijiselfisha na wafanyakazi wa duka la Tigo Mtwara.
Mashabiki wa muziki wa bongo fleva wakishuhudia wasanii waliotembelea duka la Tigo mtaa wa stand kuu mjini Mtwara.


KILIMO AJIRA YANGU-BODI YA KOROSHO

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI LEO NOVEMBA 12,2017

TAARIFA KWA UMMA

Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto) mabati yaliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya Meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, nondo zilizochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, mifuko ya saruji iliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani mara baada ya meli hiyo kuwasili na mizigo hiyo kutoka jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Pemba pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi wa nyumba za polisi katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni alisema wadau wamemchangia shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 12 za Jeshi la Polisi ili kukabiliana na ukosefu wa nyumba za polisi katika mikoa hiyo. Awamu ya ujenzi wa nyumba hizo ni ya kwanza, na awamu ya pili itakua mikoa ya mipya nchini ambayo ni Geita, Simiyu, Katavi na Songwe. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Mwajuma Majid Abdalla, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (wapili kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman (kulia), wakitoka ndani ya meli ya Azam Sealink katika bandari ya Mkoani, mara baada ya Naibu Waziri Masauni kuwakabidhi mifuko ya saruji, mabati, ndoo za rangi pamoja na nondo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba za polisi katika mikoa hiyo ya Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Othman akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), katika kikao cha ndani kilichofanyika katika ukumbi wa Bandari ya Mkoani, kabla ya Naibu Waziri Masauni hajawakabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika mikoa ya Pemba. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi, Ustawi wa Jamii, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Zanzibar, Shadia Mohamedi Suleiman, wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla, na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea tunda aina ya fenesi kutoka kwa Mkazi wa Chakechake Pemba, Kauthar Issihaka mara baada ya Naibu Waziri huyo kukabidhi vifaa vya ujenzi wa nyumba 12 za polisi katika Mikoa ya Pemba. Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika katika Bandari ya Mkoani mara baada ya Meli ya Azam ya Sealink kufikisha vifaa hivyo kutoka jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla, Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Shahani Mohamed Shahani.


NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewahamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini na kufanikisha kupata vifaa vya ujenzi wa mradi wa awamu ya kwanza wa nyumba za Polisi Mikoa ya Pemba, Zanzibar.


Mradi huo umeanza katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo nyumba kumi na mbili zinatarajiwa kujengwa ili kufanikisha askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi ndani ya mikoa hiyo waweze kuishi katika nyumba za jeshi pamoja na kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za makazi ya polisi hao, pia mradi huo utajenga nyumba katika mikoa mipya nchini pamoja na makao ya nchi Dodoma.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, katika Bandari ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba, jana, Mhandisi Masauni alisema, ujenzi wa nyumba hizo utakua ni wa hatua ya awali, lakini mipango mbalimbali itaendelea kuwezesha nyumba nyingi zaidi kujengwa katika eneo hilo ili kuhakikisha baadhi ya askari wanaoishi nje ya kambi za polisi waweze kuishi kambini ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi.


“Leo nimewakabidhi wakuu wa mikoa hawa vifaa vya ujenzi ambavyo ni mifuko ya saruji, nondo, ndoo za rangi na mabati ili waweze kusimamia zoezi hili la ujenzi wa nyumba za askari wetu kwa umakini mkubwa,” alisema Masauni na kuongeza;


“Tunajenga nyumba hapa Pemba ni mradi wa awamu ya kwanza, kwa awamu ya pili tutaenda katika maeneo mengine ya nchi, hususani mikoa mipya yaSimiyu, Geita, Katavi na Songwe na pamoja na Makao ya nchi Dodoma, kwa kuwa askari wetu hawa wanafanya kazi kubwa sana kwa kuwalinda raia wa nchi hii kuendelea kuwa salama kwa wao wenyewe pamoja na mali zao.”


Alisema anawashukuru wadau mbalimbali kwa kujitolea kutoa vifaa hivyo ili kufanikisha suala hilo na aliwataka watanzania wawe na moyo kama wadau hao kwa kuipenda nchi yao, kupenda maendeleo kwa kutoa misaada mbalimbali.


Masauni alifafanua kuwa, suala la maendeleo halina siasa, tuijenga nchi, katika mazingira mengi ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa maana ya Unguja katika suala la kujitolea wamekua wanafanya hivyo, ila kuna changamoto kidogo kwa upande waPemba pana tatizo la masuala ya kisiasa, watu wamekua wakiingiza siasa mbele katika masuala ya nchi katika mikoa hiyo ya Pemba, ambapo alisema jambo hilo sio jema katika maeneleo ya nchi.


“Serikali zote mbili ya Bara na Visiwani zipo kuwahudumia wananchi wote, wakati wa siasa umepita, sasa hivi tunataka kila mmoja ashiriki katika masuala yote ya kimaendeleo, askari hawa wanaangalia usalama wa watu wote, bila kujali hitikadi, dini ya mtu, wapi anatoka, bila kujali rangi yake bila kujali kabila lake,” alisema Masauni.


Alisema viongozi wa Serikali katika mikoa ya pemba wamekua wakipata tabu kuhamasisha katika masuala mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao, hivyo wao kama serikali kuu wameamua kupeleka maendeleo katika maeneo ambayo yanakua yana tabu katika kuhamasisha masuala ya maendeleo, hivyo wakaamua waje mikoa hiyo ya Pemba katika awamu hiyo ya kwanza ya mradi.


Akizungumzia ujio huo wa Naibu Waziri pamoja na ujenzi wa nyumba hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla, alisema anamshukuru kiongozi huyo kwa kuwaletea maendeleo hayo makubwa ya ujenzi wa nyumba za polisina kumuhkikishia vifaa walivyopokea watasimamia ujenzi wa nyumba hizo kwa nguvu zao zote.


“Sisi wakuu wa mikoa tunakushuru naibu waziri kwa hili ulilolifanya, tunakuhakikishia tutasimamia ujenzi huu kwa juhudi zote mpaka nyumba zitakapokamilika, tunasema asante sana kwa kuhamasisha wadau na hatimaye kufanikiwa kupata vifaa hivi,” alisema Mwajuma.

MHANDISI MTIGUMWE ATEMBELEA KITUO CHA UKAGUZI WA MAZAO MPAKA WA HOLILI NA TARAKEA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisikiliza maelezo ya utendaji kazi katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akifungua bomba ili kuona kama maji yanatoka wakati akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA.



Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe Leo Novemba 11, 2017 ametembelea Vituo vya ukaguzi wa mazao vilivyopo Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ili kujionea ufanisi wa utendaji kazi sambamba na kubaini Changamoto zinazowakabili ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa ushuru.

Katika ziara hiyo ya kikazi Mhandisi Mtigumwe ametembelea Kituo cha HOLILI na TARAKEA ambavyo vipo upande wa Tanzania ikiwa ni mpakani mwa Tanzania na Kenya.HOLILI ni moja ya mpaka kati ya Tanzania na Kenya ambalo upo umbali wa takribani Kilomita 25 Kutokea Himo Njiapanda huku Mpaka wa TARAKEA ukiwa umbali wa Takribani Kilomita 58 kutokea Himo Njiapanda.

Miongoni mwa Changamoto alizozibaini katika ziara hiyo kwenye Vituo vya ukaguzi wa Kilimo kwenye hivyo mipaka miwili ni pamoja na uduni wa vifaa vya kufanya kazi za Kiofisi, Kutokuwa na vifaa vya kufanya kazi ya kupimia Sampuli ya mazao katika Maabara ya Holili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mtigumwe amewataka watumishi wanaosimamia ukaguzi wa mazao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji Rushwa kwani kwa mtumishi atakayebainika kufanya hivyo sheria zitachukuliwa haraka dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mpaka huo wa TARAKEA una jumla ya Njia za panya 250 kutokea Mpaka wa Hororiri mpaka kufikia mpaka wa Namanga.Aidha, Alisema serikali inaendelea na juhudi mbalimbali za kuzikabili Njia za panya zote ili kubaini kila aina ya uhalifu unaofanywa ikiwemo magendo yanayopitishwa kinyemela.


Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images