Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO NOVEMBA 10,2017


ETIHAD AIRWAYS SPONSORS SWALHA MSABAHA'S STYLE AND BEAUTY WORKSHOP IN DAR

$
0
0



Ailende Okorumu, Country Manager, Etihad Airways Tanzania congratulates Mr. Juma Wilson, a return ticket winner to Abu Dhabi-UAE, during Swalha Msabaha’s beauty & style workshop held at Serena Hotel in Dar es Salaam recently.The Airline was a co-sponsor of the event.
Ailende Okorumu, Country Manager, Etihad Airways Tanzania (centre) congratulates Mr. Juma Wilson, a return ticket winner to Abu Dhabi-UAE, during Swalha Msabaha’s beauty & style workshop held at Serena Hotel in Dar es Salaam recently.

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI LA BOMBA LA MAFUTA GHAFI, WAFUNGUA KITUO CHA PAMOJA CHA HUDUMA ZA MPAKANI MJINI MUTUKULA

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiwa wamesimama wakati nyimbo za Taifa za nchi zao pamoja na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikipigwa kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Mke wa Rais wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni wakati nyimbo za taifa zikipigwa  kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitambulisha ujumbe alioongozana nao kwa mwenyeji wake  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni huku wake zao wakifurahia baada ya  viongozi hao kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiongozana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere baada ya kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakisalimiana na viongozi wa kampuni ya Total ya Ufaransa wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta wakiweka  jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017. Picha na IKULU

JUKWAA LA UTU WA MTOTO LAWAJENGEA UWEZO MABINTI KUPAMBANA NA VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YAO

Watu 6 Mbaroni Kwa Kukutwa na Nyaya za Umeme Mali ya TANESCO

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 07/11/2017 huko maeneo ya Tegeta IPTL lilifanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T. 897 ARF aina ya FUSSO likiwa limebeba nyaya za umeme Roller/Drum 05 zikiwa ndani ya gari hilo.

Aidha dereva wa gari hilo aliwaelekeza askari watuhumiwa wenzake na baada ya upekuzi zilikamatwa Roller/drum 02, mashine ya kupaka, rangi na makopo Mmatatu (3)matupu ya rangi yaliyotumika kubadilisha uhalisia wa Roller/drum, zote zilikutwa kwa mtu aitwaye ZAWAKO KASIBA na mke wake, mkazi wa IPTL Tegeta na watuhumiwa wengine wanne.

Watuhumiwa wote wamekamatwa na mawasiliano yalifanyika na Shirika la umeme (TANESCO) na walifika kuzitambua nyaya hizo na kugundua kuwa ni mali za Shirika ambazo ni DRUM 07 zikiwa na mita 21,000 zenye thamani ya Tsh Milioni 70.7

Jumla ya watuhumiwa sita wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo akiwemo mwanamke mmoja.

Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaotuhumiwa kuhujumu miundo mbinu ya TANESCO.

PROMOSHENI YA NUNUA NA USHINDE YAFIKIA TAMATI KWA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI WA TIGO-MASASI MTWARA

$
0
0
Meneja Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo Akikabidhi Kofia Ngumu na Funguo ya pikipiki kwa mshindi wa shindano la Nunua Ushinde Saudi Chimatilo Mkazi wa Chiungutwa,Masasi Mkaoni Mtwara Shindano hilo ni kwa wanunuzi wa Sim aina ya Tecno R6 na Tecno S1 ambapo washindi walikabidhiwa Seti za Television pamja na Pikipiki.
 Mshindi wa Shindano la NUNUA USHINDE Saudi Chimatilo akiwa katika Pikipiki yake mara baada ya kushinda promosheni hiyo inayojumuisha Simu aina ya Tecno R6 na Tecno S1 8.
Meneja Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo akitoa maelezo kwa mteja wa Simu aina ya Tecno R6 kwa Faraji Said Lembe Mkazi wa Masasi katika Duka la Huduma kwa Wateja lililopo Masasi Mkoani Mtwara Simu ya Tecno R6 inauzwa shilingi laki moja na tisini na Tano kama Promotion.

 Meneja Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo akikabidhi simu aina ya Tecno S1 kwa mteja Faraji said Lembe mara baada ya kupata maelezo katika Duka la Huduma kwa wateja lililopo Masasi Mkoani Mtwara.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVENI KATIKA IKULU YA MASAKA NCHINI UGANDA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la mkutano baina ya wajumbe wa nchi mbili za Tanzania na Uganda katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja aliombatana nao katika Mazungumzo na ujumbe wa Uganda uliokuwa ukiongozwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa pamoja na ujumbe wa Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za Asili cha Cranes Performance mara baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
Kikundi Cranes performance kikitumbuiza katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Masaka Uganda. PICHA NA IKULU

MHISPANIA AWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA BAISKELI.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

MPANDA milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.

Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.

Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa ,za Mlima Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,

Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anaeleza hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .

Shelutete anaeleza namna ambavyo Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limekuwa mstari wa mbele katika kubuni aina mpya ya bidhaa za utalii ili kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.

Kwa upande wake Juanito Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na barafu katika Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto aliyokutana nayowakati wa kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa yam lima ambayo imekuwa ikibadilika kila mara.

Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.

Shirika la Hifdhi za Taifa (TANAPA) limejipanga kuhakikisha usalama wa hali ya juu kwa wageni watakaofanya aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi zake kwa kuwa na taahadhari sambamba na waongoza wageni waliobobea katika kazi ya Utalii. Mwisho.

Prof. Elisante Aagiza Kiwanda cha Viuadudu Kujitangaza

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akiongoza kikao alipokutana na uongozi wa kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) katika ziara yake ya kikazi jana Wilayani Kibaha. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Ramson Mwilangali.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kuzazilisha Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) Bw. Samwel Mziray akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya kiwanda hicho wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto) jana Wilayani Kibaha. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Joseph Rwegasira Bushweishaija
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel Profesa Elisante Ole Gabriel akisikiliza maelezo kuhusu dawa za kuulia mazalia ya mbu toka kwa Meneja wa Uzalishaji katika kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) Mhandisi Aggrey Ndunguru alipotembelea katika kiwanda hicho jana Wilayani Kibaha. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji Prof. Joseph Rwegasira Bushweishaija .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akisoma maelezo katika chupa ndogo ya dawa za kuulia mazalia ya mbu alipotembelea kiwanda cha kuzalisha dawa hizo cha Tanzania Biotech Production Limited kilichopo Kibaha Mkoani Pwani jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Ramson Mwilangali na Mhandisi Aggrey Ndunguru.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Joseph Rwegasira Bushweishaija na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Ramson Mwilangali wakati wa ziara yao katika kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) jana Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akikagua mitambo ya kuzalishia bacteria ambayo hutumika katika kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) wakati wa ziara yake jana Wilayani Kibaha mkoani Pwani. Kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho Mhandisi Aggrey Ndunguru.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) mara baada ya kumaliza ziara yake jana Wilayani Kibaha mkoani Pwani. Prof. Elisante amefanya ziara hiyo ikiwa ni kujitambulisha na kutembelelea baadhi ya taasisi na miradi iliyo chini ya Wizara yake.

Picha na: Frank Shija – MAELEZO

DC NYASA AITUPIA LAWAMA TBA KWA KUKWAMISHA UJENZI WA OFISI YA MKURUGENZI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya NYASA ISABELA CHILUMBA amemwomba mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME kuhakikisha anaingilia kati ujenzi wa nyumba yake ,ofisi ya mkurungenzi baada ya kuonekana TBA kushindwa kuifanya kazi kwa wakati huku TBA wakida kuwa maji ndiyo tatizo licha ya kuzungukwa na ziwa naysa habari kamili hii hapa video yake.

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) SASA LAFIKILIA KUJA NA UTALII KWA BODA BODA NA BAJAJI

$
0
0
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru mara baada ya kufanikiwa kufika huku akiendesha baiskeli . 
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto)  na Ramon Abecia (Kulia) katika kilele cha Uhuru walipoanda kwa kutumia baiskeli .
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal aakiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia walipoianza safari ya kuelekea kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto)  na Ramon Abecia (Kulia) walipofika katika kituo cha kupumziki cha Horombo.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akiendesha baiskeli katika eneo la Saddle wakati wa kuekelea kituo cha Kibo .
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akikokota baiskeli yake  katika eneo lenye mawe wakati akiekelea kituo cha Kibo 
Muongoza Watalii,Ally Chuwa akitoa msaada wa kufunga viatu kwa Ramon Abecia wakati akielekea kituo cha Kibo.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litafikiria matumizi ya Boda boda na Bajaji kwa wageni watakao hitaji kutembelea Hifadhi zake endapo yatajitokeza maombi ya kutosha kuhusu matumizi ya vyombo hivyo.

Hatua hiyo inatokana na bidhaa mpya ya Utalii wa kutumia Baiskeli iliyoanzishwa hivi karibuni katika Hifadhi za Taifa za Mlima Kilimanjaro na Arusha kuanza kuwa kivutio kwa watalii kutoka nchi mbalimbali walioanza kufanya utalii wa Baiskeli.

Miongoni mwa watali hao ni pamoja na mpanda  milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal aliyeweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.

Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.
Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa ,za Mlima Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete amesema hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
Shelutete amesema namna ambavyo Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limekuwa mstari wa mbele katika kubuni aina mpya ya bidhaa za utalii ili  kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.
Kwa upande wake Juanito Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na barafu katika Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto aliyokutana nayowakati wa kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa yam lima ambayo imekuwa ikibadilika kila mara.
Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.
Shirika la Hifdhi za Taifa (TANAPA) limejipanga kuhakikisha usalama wa hali ya juu kwa wageni watakaofanya aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi zake kwa kuwa na taahadhari sambamba na waongoza wageni waliobobea katika kazi ya Utalii.

Mahakama yatupilia mbali maombi ya matunzo ya mtoto dhidi ya Mwanamuziki Diamond Platnum

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Diamond Platnum.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 10/2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa mahakama hiyo.

Hakimu Devotha alitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika kutokana na msanii Diamond kuwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto.

Katika pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakamani hapo anadai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.

Awali Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine alikuwa anaomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond. Mwanamitindo huyo alifungua kesi hiyo mahakamani hapo akiiomba mambo mbalimbali likiwemo la matunzo ya mtoto waliozaa na msanii huyo.

Katika kesi hiyo, Hamisa anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi. Hamisa alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Kupitia hati hiyo ya madai, mwanamitindo huyo anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Hata hivyo, Diamond aliwasilisha hati ya majibu kinzani akipinga maombi hayo ya Diamond akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi sh. milioni tano kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

SPIKA JOB NDUGAI AZUNGUMZA NA WABUNGE WALIOSHIRIKI MAFUNZO NCHINI CHINA

$
0
0

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea zawadi aliyopewa na Chuo Kikuu cha Guangdong kilichopo Jijini Guangzhou China, wakati wa ziara ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, zawadi hiyo ilikabidhiwa na kiongozi wa Msafara , Mheshimiwa. Augustino Masele (kushoto) na wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Msafara, Mheshimiwa Augustino Masele (kushoto) iliyotoka Chuo Kikuu cha Guangdong kilichopo Jijini Guangzhou China, wakati wa ziara ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (watatu kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) wakati wa kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.

PICHA NA OFISI YA BUNGE

WAGONJWA 15 WAFANYIWA UPASUAJI WA KUPANDIKIZA MISHIPA YA DAMU KATIKA MOYO NA KUREKEBISHA MSHIPA MKUBWA WA DAMU KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU.

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India wamefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa wagonjwa 15 katika kambi maalum ya upasuaji ya siku sita inayomalizika kesho.

Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hii ambayo imeanza Jumatatu tarehe 8/11/2017 hadi Jumamosi tarehe 11/11/2017 ni ya upasuaji wa kufungua kifua kwa watu wazima. Upasuaji uliofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), na kubadili milango miwili hadi mitatu ya moyo (Valve Replacement).

Kwa mara ya kwanza hapa nchini tumefanya upasuaji wa kurekebisa mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair).

Tulifanya upasuaji kwa wagonjwa watatu kwa siku, wote hawa wanaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika. Baadhi yao ambao tumewafanyia upasuaji jana na juzi wako katika chumba cha uangalizi maalum na wengine wako wodini wameshaanza kufanya mazoezi.

Kama wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nje ya nchi Serikali ingelipia zaidi ya milioni 405 kwani gharama za mgonjwa mmoja kwenda kutibiwa nje ya nchi ni zaidi ya milioni 27. Gharama za matibabu haya hapa nchini kwa wagonjwa 15 ni milioni 225 (milioni 15 kwa mgonjwa mmoja).

Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri. Tunawashauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati.

Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.

Kwa namna ya kipekee Taasisi inaishukuru Hospitali ya Seifee kutokana na ushirikianao mzuri tuliokuwa nao, licha ya kutoa matibabu kwa wagonjwa tumekuwa tukibadilishana ujuzi wa kazi wakati wa kufanya upasuaji. Kwa mwaka huu hii ni mara ya pili kwa wataalamu hawa kuja katika Taasisi yetu. Mwezi wa tatu mwishoni tulifanya nao kambi ya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa nane (8).

Aidha tunatarajia kuwa na kambi maalum ya matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo maalum wa Cathlab kwa watu wazima  itakayoanza tarehe 14/11/2017 hadi tarehe 19/11/2017. Katika kambi hii ambayo tutashirikiana na wenzetu kutoka Taasisi ya Sharjah Charity kutoka Falme za Kiarabu tunatarajia kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 50.

Tunawaomba wananchi waendeleee kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanahitaji kuongezewa damu wakati wanapatiwa matibabu. Mgonjwa mmoja anahitaji damu kati ya chupa 5 hadi 6.

Kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ambao wanapenda kuchangia damu tunawaomba wafike Taasisi ya Moyo iliyopo Muhimbili mkabala na Maabara kuu. Kwa maelezo zaidi wawasiliane kwa simu namba 022-2151379 au 0713304149.

 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Roberth Mallya na kushoto ni Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi Anjela Muhozya akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee Ali Ascar Beliranwalwa. 
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Roberth Mallya na kushoto ni Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi Anjela Muhozya akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee Ali Ascar Beliranwalwa. 
Mkutano wa waandishi wa Habari ukiendelea  kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Upasuaji uliofanyika  ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement) na kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair).

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi wakati alipomtembelea Waziri mkuu ofisini kwake mjini Dodoma leo Novemba 10/2017 kwa mazungumzo ya kikazi.Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera Bunge,Kazi Ajira,Vijana na Walemavu Jenista Mhagama.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfafanulia jambo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara Joyce Sokombi.(chadema) wakati wa Majadiliano ya Mapendekezo ya Mpango  wa Taifa wa Fedha kwa Mwaka 2018/2019 bungeni Dodoma leo Novemba 10/2017.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Martha Mlata (CCM) wakati wa Majadiliano ya Mapendekezo ya Mpango  wa Taifa wa Fedha kwa Mwaka 2018/2019 bungeni Dodoma leo Novemba 10/2017.


WARSHA YA WANACHAMA WA UMOJA WA POSTA AFRIKA KWA NCHI ZINAZOZUNGUMZA KIINGEREZA YAFANYIKA JIJINI ARUSHA NOVEMBA 6 HADI 8, 2017

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete, akizungumza wakati akiifungua warsha ya kimataifa ya wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, ilioanza jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Mount Meru, Novemba 6 na kumalizika Novemba 8, 2017.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta duniani (UPU), Bi. Loilinda Dieme, akizungumza katika warsha hiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Younous Djibrine, akizungumza katika warsha hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa akizungumza katika warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dkt. Haruni Kondo (kulia), akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa katika warsha hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa (kulia), akiteta jambo na mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Haruni Lemanya kwenye warsha hiyo.
Baadhi ya sehemu ya washiriki wa warsha hiyo, kutoka Tanzania, wakiongozwa na Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, Bw. Macrice Mbodo (kushoto), wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa.
Baadhi ya sehemu ya washiriki wa warsha hiyo, kutoka nchi mbalimbali, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa.
Baadhi ya sehemu ya washiriki wa warsha hiyo, kutoka nchi mbalimbali, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa.
Baadhi ya sehemu ya washiriki kutoka Tanzania, wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dkt. Haruni Kondo, akizungumza kwenye warsha hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa PAPU, Bw. Younous Djibrine.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete (wa nne kulia, waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo, mara baada ya kuufungua, jijini Arusha.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kufunguliwa warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dkt. Haruni Kondo (katikati), akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa (kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Younous Djibrine, baada ya ufunguzi  wa warsha hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa (kushoto), akigongeshana glasi na baadhi ya washiriki wa warsha katika hafla ya kuwakaribisha jijini Arusha kwa ajili ya warsha hiyo. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Younous Djibrine.

WARSHA  ya Kimataifa ya wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, imefanyika jijini Arusha, Tanzania ikizishirikisha nchi mbalimbali barani Afrika.

Katika warsha hiyo, ijulikanayo kama ‘operational readness for e-commerce,’  ilianza Novemba 6 na kumalizika Novemba 8, 2017,  Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete, aliwataka kuwa na utayari wa kibishara ili waweze kuendana na mabadiliko ya tekinolojia.

"Tukiongeza ubunifu wa kufanyakazi kwa mbinu za kisasa kwa kutumia huduma za intaneti, wateja wengi watavutiwa na kuendelea kuwepo kwenye soko na kuweza kukabiliana na ushindani wa kibishara." Alisema.

Naye Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa, akizungumza katika warsha hiyo, alisema kwamba hivi karibuni shirika lake limeanzisha Kampuni tanzu za uchukuzi na fedha kwa njia ya posta, ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya sasa na baadaye.

Warsha hiyo, imewashirikisha zaidi ya washiriki 50 kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zinazozungumza lugha ya kiingereza, na imefadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Umoja wa Posta Duniani (UPU).

Lengo la warsha hiyo ni kuziimarisha nchi wanachama  kibiashara pamoja na kukamilisha mpango maalum wa taifa na kuweka malengo na kuanzisha mfuko maalum wa mradi wa huduma bora ‘quality of service fund (QSF) project’.

Pia kuweka mikakati maalum ya ushirikiano katika biashara ya mtandao e-commerce, kuweka viwango, kurahisisha na kuimarisha mifumo ya kiutendaji.

Warsha hii ni mwendelezo wa warsha nyingine iliyofanyika jijini Nairobi mwezi mei 2017.

BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU

$
0
0
Tarehe 20 Mei, 2017 Ofisi ya Makamu wa Rais iliutaarifu umma kuhusu utaratibu wa kufanya shughuli zote zinazohusu ukusanyaji, usafirishaji, biashara na urejeleshaji wa taka hatarishi kama vile vyuma chakavu, "Oil" chafu, matairi yaliyotumika, taka za kieletroniki na za umeme na taka zitokanazo na kemikali. 

Ofisi iliwataka wale wote wanaofanya shughuli hizi hapa nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo. Aidha, kuzingatia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira ambayo Tanzania ni mwanachama ikiwa ni pamoja na kuwa na vibali vya biashara husika.

Ofisi inapenda kuukumbusha umma kuwa bado baadhi ya wanaokusanya, kusafirisha na kurejeleza taka hatarishi hawana vibali kama inavyohitajika. Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, kanuni ya 39 hadi 46 zinatoa muongozo wa hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa ili shughuli husika zifanyike.

Hivyo, Ofisi inawakumbusha tena wale wote wanaofanya shughuli za uuzaji na ununuzi wa taka hizi kuhakikisha wanafanya biashara na wale wenye vibali tu. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009. 

Aidha, Kanuni ya 47 (3) ya Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009 inatoa adhabu kwa mtu ambaye anashindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa, ambapo baada ya kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia anaweza kutozwa faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000.00) au kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja. 

Mhandisi Joseph Kizito Malongo

KATIBU MKUU
OFISI YA MAKAMU WA RAIS

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO UGANDA, PIA AZUNGUMZA NA WANAHABARI MBALIMBALI MASAKA NCHINI UGANDA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watanzania waishio nchini Uganda katika eneo la Masaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakizungumza na wanahabari mara baada kumaliza ya kufanya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha umahiri wa kupiga ngoma pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika eneo la Kyotera nchini Uganda.


PICHA NA IKULU

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Leo Novemba 10, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Mhe Jenista Joakim Mhagama ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu


Na Mathias Canal, Dodoma

Serikali imesema kuwa Mpango wa Serikali wa kuwapelekea wakulima wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma mbegu mpya za Kahawa ni mahususi kwa ajili ya kuinua uzalishaji kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Kuendeleza Zao la Kahawa katika kipindi cha miaka 10 yaani mwaka (2011 – 2021).

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) amebainisha hayo leo Novemba 10, 2017 Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mhe Martin Mtonda Msuha (Mb) Aliyetaka kufahamu kuhusu kushuka Kwa takwimu katika miaka ya hivi karibuni ya uzalishaji wa Kahawa Wilayani Mbinga kwa mkulima mmoja mmoja (out growers) ambapo alitaja sababu za mojawapo zilizopelekea kushuka kwa uzalishaji huo kuwa ni pamoja na kuzeeka kwa miti ya kahawa.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa Katika mpango huo, utafiti na usambazaji wa miche bora itatolewa ili kuondokana na miche yenye tija duni na iliyozeeka. Ambapo Utekelezaji wake unafanyika kwa kushirikiana na wadau hususani Tanzania Coffee Research Institute (TaCRI).

Alisema, Kituo cha Utafiti na uzalishaji miche cha Ugano kilichopo Wilayani Mbinga, katika mwaka 2016/2017 kilizalisha na kusambaza miche bora ya kahawa 270,869 na kazi mpaka hivi sasa inaendelea.

Aidha, Mfuko wa Maendeleo ya Kahawa (Tanzania Coffee Developemnt Fund (TCDF) umefadhili na kupunguza bei kutoka shilingi 300 kwa mche mmoja hadi shilingi 150 kwa vituo vyote nchini vilivyoko chini ya TaCRI ili miche hiyo isambae kwa kasi.

Mhe Mwanjelwa alisema mnada wa kahawa huendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Kahawa Na. 23 ya Mwaka 2001 hivyo Serikali haina mpango wa kuanzisha soko la mnada wa kahawa Wilayani Mbinga au mahali pengine nchini kwa sababu uwepo wa miundombinu ya mashine ya kielektroniki ya kuendeshea mnada iliyopo Moshi, maabara ya kuonjea kahawa, wataalamu wa kuendesha mnada huo, gharama za mnunuzi ambapo atalazimika kwenda katika kila mnada kama utawekwa kila mahali ambapo kahawa inazalishwa.

Alisema uzoefu unaonyesha kuwa nchi nyingi duniani huweka mnada sehemu moja tu ili kurahisisha uendeshaji. Aidha, tangu kuanzishwa kwake kabla uhuru, mnada uliwekwa Moshi kwa kuwa ndiko kulikuwa na wanunuzi na biashara ukilinganisha na maeneo kama Kagera ingawa uzalishaji unafikia hadi asilimia 40 ya nchi nzima.

“Mnada unauza kahawa ikiwa kwenye maeneo ya uzalishaji (Ex-Mbinga, Ex-Mbeya n.k.) kinachopelekwa Moshi ni sampuli tu kwa ajili ya uonjaji. Aidha, Serikali imeanzisha Soko la Bidhaa (Commodity Exchange) ili kupunguza gharama za uendeshaji wa masoko ya mazao ikiwemo kahawa” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa kifungu Na. 29 (ii) cha Kanuni za kahawa 2013, ni kosa kwa mtu yeyote kununua matunda ya kahawa (ripe cherry) hivyo Serikali inakataza biashara ya kahawa mbichi. 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mbinga na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma sambamba na wahusika wengineo wote kwamba hairuhusiwi kabisa uuzaji wa kahawa mbichi.

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LATOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI SHINYANGA

$
0
0

Shirika la kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa pikipiki kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto la jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 10,2017 wakati wa kukabidhi pikipiki moja kwa jeshi la polisi,Meneja wa shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga Benety Malima alisema pikipiki hiyo itasaidia katika ufuatiliaji wa makosa mbalimbali yakiwemo ya jinai. 

“Shirika letu limekuwa likiendesha mafunzo kuhusu ukusanyaji wa vielelezo kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi kwa ushahidi mahakamani,tumebaini kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo ni usafiri,kutokana na hali hiyo tumeona tuangalie namna ya kuwezesha usafiri ili kukabiliana na vitendo vya ukatili katika jamii”,alieleza Malima. 

Akipokea pikipiki hiyo SSP Lutusyo Mwakyusa aliyemwakilisha kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi. 

“Tunalishukuru shirika la Save the Children, huu ni msaada mkubwa sana kwetu kwani utasaidia kuokoa maisha ya watu,na hiki ni kielelezo tosha cha ushirikiano kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,naomba wadau wengine waige mfano wa shirika hili ili kujenga jeshi letu la polisi”,alieleza Mwakyusa. 

Aliwataka wadau kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa matukio ya ukatili yanatokomezwa.
Pikipiki iliyotolewa na shirika la Save The Children kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ili itumiwea na dawati la jinsia na watoto kufuatilia matukio ya ukatili wa kijinsia  mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto.
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Mwakyusa
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akikabidhi funguo ya pikipiki kwa SSP Lutusyo Mwakyusa
Mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Mwakyusa akijaribu kuendesha pikipiki iliyotolewa na shirika la Save The Children.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images