Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1426 | 1427 | (Page 1428) | 1429 | 1430 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya TPB wakichangia damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe jijini Mbeya Nov 11 mwaka huu .
  Zoezi la kuchangia damu likiendelea ..........

  Afisa Oparesheni Benki ya TPB Ndugu Mustafa Mmanga akichania Damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe tamasha hilo la uchangiaji Damu limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la WE CARE  TANZANIA lenye makao makuu yake jijini Mbeya na kudhaminiwa na Benki ya TPB Mkoa wa Mbeya Nov 11 mwaka huu ambapo kauli mbiu ya tamasha hilo ''NIOKOE NIISHI ''.

  Meneja benki ya TPB Mkoa wa Mbeya Ndugu Humphrey Julius akipokea cheti shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la WE CARE Bi,Elizabeth Maginga kwa katambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha zoezi la uchangiaji Damu jijini Mbeya .

  Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika tamasha hilo la uchangiaji damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe jijini Mbeya Nov 11 ,2017.

  Mkurugenzi shirika la WE CARE  Bi, Elizaberth Maginga akizungumza katika Tamasha hilo la uchangiaji damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe jijini Mbeya .
  Zoezi la Uchangiaji likiendelea

  Tpb benki wakisakata rumba
  Benki ya TPB katika picha ya pamoja na Meza kuu..
  Vijana wa Boda boda katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TPB .Picha  Mr pengo na JMblog


  0 0  0 0


  Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema Mkoa wa Dodoma hauna sababu zozote za kukumbwa na tatizo la upungufu wa Chakula wala Njaa kwa wananchi wake kwa kuwa unazo fursa za kutosha za kuzalisha mazao ya chakula yanayotosheleza mahitaji ya Mkoa.

  Aidha amesema mkoa huo una fursa za kuzalisha mazao ya biashara yatakayoweza kuwainua kiuchumi wa mwananchi na Mkoa kwa ujumla.

  Dk. Mahenge ameyasema hayo mwishoni mwa wiki akiwa katika ziara Wilayani Kongwa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Wilaya za Mkoa wa Dodoma.

  Kufuatia hali hiyo, Mkuu huyo amewataka Viongozi na wataalamu kuwasimamia wananchi kupanda mazao yanayotumia maji kidogo na kustawi kwa ufanisi Mkoani Dodoma kama Mtama, Uwele, Muhogo, Alizeti na Sasa zao la Korosho lililothibitika kustawi vizuri kwenye Ardhi ya Dodoma.

  Aidha amewataka viongozi na Wataalamu wa kilimo wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanawaelimisha na kuwasimamia wananchi kutekeleza mkakati wa kilimo wa Mkoa unaolenga kuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji ya Mkoa, kwa kuachana na kilimo cha mazoea badala yake unasisitiza kilimo cha maarifa, na cha kisasa.

  Amewatoa hofu wananchi kuwa zao la mtama mbali na kutumika kama chakula lakini lina soko la uhakika kwa ajili ya viwanda vya kutengeneza vinywaji hivyo hata kama mwananchi hataki kula mtama anaweza kuuza na akanunua chakula anachokitaka mwenyewe lengo likiwa kuwa na uhakika wa chakula.

  Amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi kwa kuanzisha kampeni ya kuondoa njaa wilayani Kongwa (ONJAKO) na kuzitaka Wilaya nyingine kuiga mfano huo.

  Awali, akielezea Kampeni ya ONJAKO Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwenye wilaya hiyo kila kaya, pamoja na mazao mengine ni lazima kulima heka mbili (2) za mtama kwa ajili ya chakula na endapo kaya yoyote itakayokaidi muhusika atalazimika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (50) na endapo atashindwa basi adhabu ya kifungo cha miezi mitatu (3) itamkabili, Lengo likiwa kuhakikisha kila kaya inazalisha chakula cha kutosheleza mahitaji yake.

  Kadhalika, Dk.Mahenge amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Rehema Madenge kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Dodoma kuhakikisha kila Wilaya ina ainisha mahitaji ya vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya elimu ili vifaa hivyo vinunuliwe kwa mfumo wa pamoja moja kwa moja kutoka Viwandani baada ya kupata idhini ya Wizara ya Kisekta lengo likiwa kupunguza gharama za vifaa.
   
  Amepiga marufuku tabia za viongozi na Wakuu wa Idara kwenye Wilaya kukaa tu ofisini na kuwataka waweke ratiba ya mara kwa mara ya kutembelea shule kufanya ukaguzi ili kubaini changamoto halisi zinazo kabili hali ya utoaji elimu na kuzitafutia majibu ya kudumu, pia ametaka Wilaya ziwape walimu ushirikiano unaohitajika ili waweze kutekeleza jukumu la kuwafundisha watoto kwa ufanisi zaidi.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua mradi wa maji ya chemichemi kwenye kijiji cha Kongwa Maji
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua mashine ya kusukumia maji kwenye mradi wa maji ya chemichemi kijijini Kongwa Maji
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Suguta Wilayani Kongwa.
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akiwasalimia Watoto wenye Ulemavu wa Viungo na matatizo ya akili wanaotibiwa kwenye kituo cha Watoto cha Mlali Kongwa.


  0 0

  Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde  mwishoni mwa wiki amekabidhi matofali 3000 na mifuko ya saruji 100 katika Kata ya Makutupora kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Shule za Msingi Mpya za Mbande na Muungano Wilaya ya Dodoma mjini mkoani Dodoma.

  Msaada huo alioukabidhi umetoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka  ambayo ilikabidhi zawadi kwa washindi katika droo ya michezo hiyo,Mavunde aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza zaidi ili kusaidia kuboresha Elimu nchini.
   
  Waziri Mavunde alisema kuwa ujenzi wa shule hizo utasaidia kupunguza adha inayowapata wanafunzi kutembea umbali mrefu  wa zaidi ya kilomita 7 kufuata shule katika eneo la Veyula.
   "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakikabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa mmoja wa viongozi katika kata ya Makutupora  kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande. Kwa ajili  ya ujenzi wa madarasa mawili  kila moja.
    "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakiwashukuru baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa kata ya Makutopora mara baada ya kukabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
  Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoka kijiji cha Makutopora na Mbande kushuhudia tukio la makabidhiano ya matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande,iliyotolewa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka ikishirikiana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde.  0 0

  Msanii Jux akitoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.

  Janjaro akitumbuiza katika tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.

  Genevieve Mpangala akitumbuiza katika jukwaa la TIgo fiesta mapema usiku wa uamkia jumapili katika viwanja vya 

  Aslay akiimba na mashabiki zake katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jumapili.

  Chege akitumbuiza katika jukwaa la tigo mkoani Mtwara 

  Msanii Snura akitumbuiza katika jukwaa la  Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jumapili.

  Lulu diva akiwa katika jukwaa la Tigo fiesta amasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.
  Madee akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.


  0 0

  Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (katikati) katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa Utalii Domina Moshi (kushoto)
  Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (kulia) akiwa na Afisa Utalii Mwandamizi, Martin Mrema (katikati) wakiwa wanatabasamu huku wameshika kwa pamoja moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu. 
  Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (Kulia) akiwa na Afisa Utalii Domina Moshi (katikati) wakiwa wanatabasamu huku Bi. Kiangi akiwa ameshika kwa moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha yake aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akionesha moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi kabla ya kumkabidhi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akilishwa keki na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Wakishuhudiwa na Afisa Utalii, Marygoreth Mushi (kwanza kulia) na Mary Msekela (wa pili kulia)
  Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake.
  Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii wakimsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akimpongezana na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa hafla fupi ya kustaafu kwake mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) wakiwa wenye furaha na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa hafla fupi ya kustaafu kwake mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma.Picha na Lusungu Helela- MNRT


  Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Utalii wameombwa kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deograsius Mdamu, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi

  Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Wizara hiyo , Bi. Uzeeli Kiangi katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu mwanzoni mwa mwezi Julai kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma akiwa ameitumikia Wizara kwa kushika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33.

  Akizungumza katika hafla hiyo alisema ‘’ Watumishi ni kiungo muhimu katika kumsaidia Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutekeleza majukumu yake, ni matumaini yangu kuwa mtampa ushirikiano katika hili’’

  Amesema kupitia ushirikiano huo utasaidia kupelekea Wizara kutimiza azma ya kufikia watalii milioni 8 na fedha za kigeni dola bilioni 20 kila mwaka kufikia mwaka 2025.Aidha, Bi.Kiangi aliwataka watumishi kuzingatia miiko ya kazi zao kwa kutojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa wanapotimiza majukumu yao, la sivyo serikali hii ya awamu ya tano haitawaacha salama.

  ‘’Wakati wa utumishi wangu nilijitahidi kukwepa kupokea rushwa kwa kuwa sikujua huyu anayetaka kunihonga katumwa na nani na kwanini anipe rushwa wakati natimiza majukumu yangu jihadharini na watoa rushwa’’ alisisitiza

  Katika hatua nyingine, Bi. Kiangi aliwataka watumishi wenye tabia ya kujituma kufanya kazi pale tu wanapohisi kazi hiyo ina malipo wajirekebishe mara moja kwa kuanza kufanya kazi zote zenye malipo na zisizo na malipo kwani zina umuhimu katika kuwajenga kitaaluma.

  Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu alisema Idara yake imejipanga kufanya kazi kwa kasi zaidi na kuendeleza yale ambayo Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Kiangi aliyokuwa akiyapigania kwa ajili ya maendeleo ya utalii.

  ‘’Wizara inatambua mchango wako tangu ulipoajiriwa mwaka 1984, tunakuahidi tutakutumia pale tunapohitaji utaalamu wako ili kuhakikisha Wizara inafikia malengo iliyojiwekea’’ alisisitiza

  Kwa upande wake, Afisa Utalii Mwandamizi, Josephat Msimbano wakati amesema Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa utumishi wake alikuwa ni kiongozi aliyeichukia rushwa na yeyote aliyethubutu kutaka kumhonga ili ahudumiwe kwa minajili ya kupindishwa kwa sheria aligonga mwamba.

  Naye Afisa Utalii, Domina Moshi amesema kwa upande wake, Bi Uzeeli Kiangi alikuwa ni mshauri mzuri, alikua zaidi ya mama na alipenda watumishi wajiendeleze kielimu na ndiye aliyemfanya aende masomoni nchini kujiendeleza kielimu.

  Bi. Uzeeli Kiangi kastaafu kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma akiwa ameihudumia Idara ya Utalii katika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33 ambapo aliajiriwa mwaka 1984 kama Afisa Utalii Daraja la tatu ambapo alipandishwa madaraja hadi kufikia Afisa Utalii Mwandamizi daraja la kwanza mwaka 2007.

  Mwaka huo huo alipandishwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Leseni na Uthibiti kwa kipindi cha miaka mitano. Pia, mwaka 2013 hadi julai 2017 alikuwa Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii


  0 0

  KAMPUNI ya bia nchini ya TBL imepewa tuzo ya kwanza ya matumizi bora ya magari makubwa ya mizigo ya Mercedes Benz Actros ambayo yametimiza zaidi ya kilomita milioni moja huku yakiwa bado katika hali bora.TBL ina magari kumi ya aina hiyo ambayo yamefanya kazi kwa miaka 17.Tuzo hiyo imetolewa na DAIMLER kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya CFAO nchini Tanzania ambayo ndiyo mawakala pekee wa magari ya Mercedes Benz nchini Tanzania. 

  Tuzo hiyo Mercedes-Benz Actros yenye kubeba jina la ‘Mileage Millionaire’ kutokana na kupita kilomita milioni moja, imetolewa kuonesha kuridhishwa kwa watengenezaji wa magari hayo juu ya uimara wake. TBL ina magari zaidi ya 80 ya Mercedes Benz.Magari yote hayo yamefikisha kilomita milioni 11 katika miaka 17 ya kuwa barabarani. Kilomita hizo ni sawa na kuzunguka dunia mara 275.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo akisalimiana na kuwakaribisha baadhi ya wageni waalikwa waliowasili kwenye hafla ya tuzo ya Mileage Millionaire kwa kampuni ya bia ya TBL. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.[/caption] Gari linaloongoza katika ‘Mileage Millionaire’ ni Actros modeli ya 3340, ambalo limefikisha kilomita 1,519,459 tangu lilipoingizwa TBL mwaka 2000. Magari mengine ni Actros za mwaka 2002,2003 na 2004 zikiwa na wastani wa kilomita kati ya kilomita milioni 1.02 na 1.5.Magari hayo yamekuwa yakitumika katika njia zote za Tanzania kupeleka vinywaji kutoka Dar es salaam, Arusha na Mwanza kwenda maeneo mbalimbali ya Tanzania.Kwa mujibu wa taarifa magari yote hayo yalinunuliwa moja kwa moja kutoka CFAO Motors Tanzania.Bosi wa magari ya kibiashara ya Daimler upande wa Afrika, Naeem Hassim alisema katika kukabidhi tuzo hizo kwa TBL kwamba kuwa na magari ya aina hiyo katika kampuni yake kufikisha zaidi ya kilomita milioni 1 na bado yakiwa ‘vijana’ si jambo la kushtusha kwa Mercedes-Benz Actros. [caption id="attachment_3142" align="aligncenter" width="1404"]Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa CFAO Motors Tanzania Bi. Tharaia Ahmed (katikati) akifurahi jambo na mmoja wa wageni waalikwa kabla ya kuanza kwa hafla ya utoaji tuzo ya Mileage Millionaire. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo na kulia ni Mwakilishi wa CFAO, Simon Faraldo.[/caption] Alisema Actros yamejitanabaisha kwa ubora wake na kuaminika kwake:” ni dhahiri kuwa na magari kama haya ni uwekezaji wenye maana kubwa, ni vyema wateja wakayambua kwamba Actros ni gari la kuaminika.”Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo alisema katika utoaji tuzo huo kwamba wanafurahi sana kusherehekea kilomita zaidi ya milioni moja ya magari ya ACTROS.Alisema ni mafanikio makubwa kuwa na magari hayo na hiyo inamaananisha kwamba ni imara na yanayoaminika yakiwa yametengenezwa kuhimili hali mbaya zaidi na kwamba wateja wanaweza wakawategemea kwa huduma bora za mauzo na pia uhudumiaji wa gari lenyewe ili liweze kudumu zaidi.Akipokea tuzo hiyo mwakilishi wa Tanzania Breweries Limited, ambaye ni meneja wa lojistiki wa Afrika Mashariki James Nyoike alisema kwamba amefurahi sana kuwa sehemu ya simulizi lenye mafanikio katika uendeshaji wa kampuni kwa kuwa na magari yenye sifa kubwa wa uimara. [caption id="attachment_3143" align="aligncenter" width="1404"]Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (kushoto) akifafanua jambo kwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya kuitunuku kampuni ya TBL tuzo ya Mileage Millionaires baada ya magari yake 10 aina ya Mercedes Benz Actros kupitisha kilometa zaidi ya milioni moja na yakiwa bado ni imara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro.[/caption] Alisema anafurahia huduma ya matengenezo inayopata magari yake kila yanapotakiwa kutengenezwa, pamoja na mafunzo kwa madereva hali iliyowezesha kuwapo kwa udumu zaidi kwa magari.“Tuna zaidi ya magari 80 ya Mercedes Benz kuanzia modeli za 2000 hadi 2016. Magari haya yamethibitisha ubora wake kazini na kuwa sehemu muhimu sana ya kazi zetu hasa za usambazaji wa bidhaa” alisema Nyoike.Katika mahojiano alisema kwamba gari lililopitisha kilomita milioni 1.5 T 418 AAT limeendeshwa na dereva mmoja Moses Ulenga kwa miaka 10.“Nasikitika kwamba hakuhudhuria sherehe hizi, yuko safari” alisema Nyoike ambaye alisema pamoja na kufuata utaratibu wa service wa gari pia wamekuwa wakifanyia matengenezo ya kuzuia uharibifu na kwamba madereva wake wamefunzwa na zipo taratibu za kufuata zenye kuonesha nidhamu ya barabara. [caption id="attachment_3152" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaires, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.[/caption] Naye Tharaia Ahmed Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko amesema kwamba wamemua kutoa tuzo hiyo kwa TBL kama sehemu ya kuonesha namna gani ushirikiano kuanzia mauzo hadi matunzo unavyoweza kumnufaisha mtu ambaye ananunua magari hayo kutoka CFAO.Alisema TBL imeonesha ubora wa magari hayo na kuaminika kwake katika safari ambazo wakati mwingine ni ngumu sana kwa kuzingatia mazingira vyetu.CFAO Motors Tanzania ambayo zamani ilijulikana kama DT Dobie ni kampuni tanzu ya kundi la makampuni ya CFAO ya Ufaransa. CFAO Motors iliundwa 1952na ni wakala wa magari mbalimbali Mercedes-Benz ya kibiashara, ya abiria na ya binafsi. [caption id="attachment_3132" align="aligncenter" width="1404"]Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo akizungumza katika hafla ya kuitunuku kampuni ya TBL tuzo ya Mileage Millionaire baada ya magari yake 10 aina ya Mercedes Benz kupitisha kilometa zaidi ya milioni moja na yakiwa bado ni imara. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro.[/caption] [caption id="attachment_3131" align="aligncenter" width="1404"]Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim akizungumzia ubora wa magari ambayo yanauzwa na CFAO Motors na mipango ya kampuni hiyo kuendelea kuuza magari imara kwa mazingira ya Afrika.[/caption] [caption id="attachment_3133" align="aligncenter" width="1404"]Picha ya pamoja kabla ya kukabidhi tuzo ya Mileage Millionaire.[/caption] [caption id="attachment_3134" align="aligncenter" width="1404"]Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mileage Millionaire mwakilishi wa kampuni ya bia TBL, Denis Dismas (katikati). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo.[/caption] [caption id="attachment_3135" align="aligncenter" width="1404"]Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wateja wa CFAO Motors Tanzania waliohudhuria hafla hiyo ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire.[/caption] [caption id="attachment_3153" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaires, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (kushoto) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya bia ya TBL mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3144" align="aligncenter" width="1404"]Picha ya pamoja ya Uongozi wa CFAO Motors Tanzania na ugeni kutoka makao makuu ya kampuni hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3145" align="aligncenter" width="1404"]Uongozi wa Kampuni ya CFAO Motors Tanzania na mgeni kutoka DAIMLER katika picha ya pamoja mbele ya gari moja kati ya 10 aina ya Mercedes Benz Actros ya kampuni ya bia ya TBL iliyopitisha kilometa 1,519,459 na kupelekea kukabidhiwa tuzo ya Mileage Millionaire. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.[/caption] [caption id="attachment_3138" align="aligncenter" width="1404"]Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa CFAO Motors Tanzania Bi. Tharaia Ahmed akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuzo ya Mileage Millionaire iliyotolewa na CFAO Motors Tanzania kwa kampuni ya bia TBL.[/caption] [caption id="attachment_3139" align="aligncenter" width="1404"]Mkuu wa (Logistics Services) wa kampuni ya bia TBL, James Nyoike akizungumza na waandishi wa habari namna TBL imefanikiwa kutunza magari yake aina Mercedes Benz Actros na kuweza kufikisha kilometa 1,519,459.[/caption] [caption id="attachment_3140" align="aligncenter" width="1404"]Wawakilishi wa kampuni ya bia TBL, James Nyoike (wa pili kushoto) na Denis Dismas (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (wa kwanza kulia).[/caption]

  0 0

  Wafanyakazi wa Tigo walioshiriki katika mbio ndefu za  Tigo Dodoma Half Marathon wakiwa na bango linalosema 'Tumekusoma' kabla ya kuanza kwa mbio hizo ndefu jijini Dodoma leo. Tumekusoma ni  kampeni mpya ya Tigo inayolenga kuwapa wateja wake urahisi wa kutumia huduma za simu pamoja na faida zaidi za bonasi kila watakapotumia namba mpya ya *147*00# kununua muda wa maongezi, bando, data na kufanya miamala ya fedha.
  Mshindi wa mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon, Dickson Marwa  akimaliza mbio hizo zilizofanyika mjini Dodoma hapo jana. 
  Baadhi ya waheshimiwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na medali na vyeti walivyotunukiwa kwa kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana.  Naongoza kwa mfano na vitendo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dr Hamisi Kigwangala akimalizamio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana. Mhe Dr. Kigwangala alishiriki katika mbio za kilometa 21.


  Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon (wanaume), Dickson Allan wa Mara akipokea zawadi zake za ushindi kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana SHoza baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijino Dodoma jana.


  Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon, Dickson Allan wa Mara akipngezwa na Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.

  Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon kwa wanawake, Noela Remi Khaday akipokea medali kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo  baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.

  Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon kwa wanawake, Noela Remi Khaday akipokea zawadi zake kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shoza baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.


  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe Vumilia Nyamoga akimtunuku Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shoza zawadi ya medali baada ya kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half-Marathon zilizofanyika katika mji wa Dodoma jana.
  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akitoa wito kwa watanazania  kujitokeza kwa wingi uwanja wa uhuru tarehe 25/11/2017 kushangilia pambano la bondia Ibrahim Class (kushoto)  wanchini akitetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini leo jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo  kambini  Joe Gym  Kawe. yake ya mazoezi .
   Bondia Ibrahim Class (kulia) akifanya mazoezi na Mwalimu Msaidizi Bw.Kelvin Magembe (kushoto) kuonyesha uwezo wake mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia)alipomtembelea kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano litakalofanyika kati yake na Bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017 Uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
   Bondia Ibrahim Class (kulia) akimkabidhi  zawadi ya tisheti yenye jina lake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipomtembelea bondia huyo  kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano la tarehe 25/11/2017 katika uwanja wa uhuru na bodia wa Afrika ya Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati leo jijini Dar es Salaam.


  Na Anitha Jonas WHUSM.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kumshangilia bondia Ibrahim Class katika pambano lake la kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia kutoka Afrika ya Kusini  Koos  Sibiya.

  Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo jana  jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake bondia  kwa pambano litakalofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017.

  “Bondia huyo anauwezo mkubwa na amekwisha kushinda mara mbili kwa Afrika na kwa mkanda huu wa kugombea ubingwa wa dunia nimeona ni vyema akapigania hapa nchini ili watanzania waweze kuona uwezo wake na pamoja na kumongezea ari ya kupambana kwa ajili ya watanzania walikuja kumuunga mkono,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

  Akiendelea  kuzungumza katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alisema  atasimamia mchezo wa ngumi na kuhakikisha unarudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani kwa kuhakikisha anadhibiti wapiganaji wanaokwenda kwenye mapambano na kununuliwa huku wakililetea sifa mbaya taifa ya kutumika kupandisha watu madaraja.

  Kwa upande wa Bondia Ibrahim Class wa nchini aliwahakikishia watanzania kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha anauchukua ubingwa huo na mkanda huo kubaki nchini huku akiwataka watanzania kuja kujionea wenyewe namna atakavyopambana na kuonyesha uwezo wake.

  “ Nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa  waje kujionea wenyewe jinsi gani nitakavyo mpiga huyo mwafrika kusini na kuchukua mkanda nimejiandaa vizuri na mazoezi ninayofanya niyakiwango cha juu,”alisema bondia Class.
  Pamoja na hayo nae Rais wa TPBC Bw.Chaurembo Palasea aliongeza kuwa mchezo wa ngumi umekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ulingo kwa ajili ya kufanyia mazoezi kwani hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa sekta ya mchezo wa ngumi. 

  Halikadhalika Waziri Mwakyembe  amesema kuwa serikali itaanzisha bodi itakayosimamia sekta ya ngumi kwa lengo la kuondoa kukosekana kwa dira ya usimamizi wa sekta ya ngumi nchini.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungungumza na Mbunge wa Urambo Tabora, Magreth Sitta, nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Joseph Ngonyani(Maji Marefu) nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena, nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe. William Ngeleja akitoa maelezo ya awali kuhusu utendaji kazi wa kamati hiyo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 bungeni Mjini Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uratibu wa Maafa na namna Serikali inavyojenga uwezo wa Idara hiyo ili kuongeza tija wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa .
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu Maafa Novemba 12, 2017 bungeni Dodoma.
   Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu  (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 Mjini Dodoma.
   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Idara yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe hao iliyoandaliwa na Ofisi hiyo mjini Dodoma.
   Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe.  Aida Kenani akichangia hoja wakati wa wakati  wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa bungeni mjini Dodoma.
   Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa mhe. Abdallah Mtolea (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati na Watendaji wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi hiyo kwa lengo la kutoa uelewa wa masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
  Mmoja wa wawezeshaji kutoka Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ili kutoa uelewa wa masuala  ya Menejimenti ya maafa nchini Novemba 12, 2017. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)

  Na. MWANDISHI WETU
  Ofisi ya Waziri Mkuu imeendesha warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo inayohusu Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini.
  Akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Novemba 12, 2017 Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.William Ngeleja alieleza kuwa warsha hiyo itawajengea uwezo wajumbe wa Kamati hususani katika utekelezaji wa majukumu yao.

  "Warsha hii ni muhimu kwa wajumbe wa kamati kwani itaongeza uelewa kuhusu sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 pamoja na dhana nzima ya Menejimenti ya Maafa"

  Akifanua mhe.Ngeleja amesema warsha hiyo itasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kamati hasa katika kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya maafa.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwaeleza wajumbe kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini ili kujenga uwezo wa Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali pindi maafa yanapotokea hivyo warsha hii inatija kwa wajumbe wote.

  "Warsha hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wajumbe kuhusu namna bora ya kupambana na majanga yanapoytokea nchini na madhara yake, vyanzo na sababu za kutokea, hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia, kupunguza  madhara, kujiandaaa , kukabili na kurejesha hali katika ubora zaidi" Alisisitiza Mhe. Mhagama.

  Sambamba na hilo Mhe. Mhagama alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini kwa kuanzisha Idara ya uratibu wa maafa inayotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

  Pamoja na hatua hizo Serikali ina sera ya Taifa ya Usimamizi wa maafa ya mwaka 2004 ambayo inaeleza hatua na majukumu ya wadau mbalimbali katika shughuli za Manejimenti ya maafa na kutoa muongozo wa utekelezaji wake.

  Aidha mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mhe.Elibariki Kingu alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendesha warsha hiyo na kushauri serikali kuwekeza zaidi katika kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza hapo nchini.

  AWALI
  Mada zilizowasilishwa katika warsha hiyo zilijikita katika Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa hapa nchini ikiwa ni moja ya jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuwajengea uwezo wadau na wananchi kwa ujumla ili kuweza kuyakabili maafa pindi yanapotokea. Warsha ilikuwa ya siku moja iliyojumuisha wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu masuala ya Menejimenti ya Maafa iliyofanyika Bungeni Dodoma.


  0 0

                      Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Vijijini ADLG iliyopo Jijini Mwanza, Jimmy Luhende akichangia mada kwenye Mkutano wa Sekta ya Uziduaji 2017 uliofanyika Mjini Dodoma.

  Novemba 02-03, 2017 ulifanyika Mkutano wa Sekta ya Uziduaji (Madini, Mafuta na Gesi) Mjini Dodoma ambapo miongoni mwa maazimio kwenye mkutano huo ni Asasi za Kiraia kushiriki ipasavyo katika kuhakikisha Taifa linanufaika na Rasilimali zake.

  Ungana na BMG kujua yaliyojiri kwenye mkutano huo ulioandaliwa na muungano wa Asasi za Kiraia zinazoangazia masuala ya Utawala Bora kwenye sekta ya Uziduaji nchini HakiRasilimali. Tazama HAPA ufunguzi wa mkutano huo. Tazama HAPA hafla ya usiku baada ya mkutano huo. Mwanasheria Veronica Zano (kushoto) kutoka Zimbabwe akichangia mada kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Vijijini ADLG iliyopo Jijini Mwanza.[/caption]  


  0 0

  Na.Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Chama cha Wamiliki wa Mabasi Yaendayo Mikoani (TABOA) na Umoja wa Wasafirishaji Abiria Jijini Dar es Salaam (UWADAR) wamekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao kuwa Novemba 14 mwaka huu watakuwa na mgomo wa kusitisha huduma za usafirishaji.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa UWADAR, Kismat Dhalla wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwa ajili ya kukanusha suala hilo.

  Dhalla amesema kuwa taarifa hiyo iliandaliwa na vyama hivyo lakini ilishatolewa katika vyombo vya habari siku nyingi zilizopita hivyo kuna baadhi ya watu wameamua kuisambaza upya bila ridhaa ya wahusika.

  “Ni kweli ile taarifa ni ya kwetu lakini tulishaitoa siku nyingi na mgomo huo haukufanyika kwa kuwa tuliahidiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kuwa itayafanyia kazi madai yetu”, alisema Dhalla.

  Dhalla ameongeza kuwa tayari SUMATRA imeandaa mkutano na wadau ambao utafanyika mnamo Novemba 15 mwaka huu kwa ajili ya kujadili kuhusiana na baadhi ya Kanuni zilizotungwa katika Sheria hiyo ya SUMATRA.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa SUMATRA, Tumaini Silaa amesema kuwa lengo la SUMATRA ni kuhakikisha kuwa usafiri unapatikana muda wote na unamfaidisha msafiri na msafirishaji ndio maana mamlaka hiyo inajitahidi kuyamaliza malalamiko ya TABOA na UWADAR pindi yanapojitokeza.

  “Sisi kama SUMATRA tunaona kuwa hakuna mgogoro kati yetu na wadau wa usafiri isipokuwa ni kutoelewa Kanuni ambazo zimepitishwa na Mhe. Waziri mwenye dhamana hivyo tutakapokutana katika mkutano huo tutaeleweshana kwani tunaamini kuwa kanuni zilizoandaliwa ziko vizuri”, alisema Bw.Silaa.

  Amefafanua kuwa baadhi ya watu bado wanachanganya Kanuni za mwaka 2007 ambazo zimefutwa na kanuni hizi mpya lakini wanatakiwa kufahamu kuwa kanuni mpya zimeweka usawa kwa upande wa msafirishaji, abiria, dereva na kondakta.

  Pia, kanuni hizo mpya bado hazijaanza kutumika mpaka pale SUMATRA itakapotoa elimu ili kila mmoja awe na uelewa na Sheria na Kanuni zake.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Mkurugenzi wa taasisi ya AL Hikma Nurdeen Kishki amesema kuwa kwa sasa waumini wake pamoja na jamii inayozungumza  wanaweza kupata mawaida yake, hadhara, hotuba  na hadithi mbalimbali kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

  Shekh Kishk ameweka wazi akaunti zake za mitandao ya kijamii facebook, twitter , instagram sambamba na kufungua TV ya Online itakayokwenda kwa jina la Kishki Online Tv.

   Akizungumza wakati wa utambulisho wa akaunti hizo, Shekh Kishk amesema kuwa jamii iliyokuwa inamfuatilia kwa kipindi kirefu walikuwa wanalalamika kwa  kukosa mawaidha yake ambapo kwa kiasi kikubwa kinazidi kuwasogeza karibu nae.

  “ Jamii inayonifuatilia ilikuwa inalalamika kila wakati wakisema kwanin Shekh haufungui mitandao ya kijamii na wengine walitaka kunifungulia ila sikuwa tayati, ila kuna baadhi ya watu walikuwa wanatumia mgongo wangu kufungua akaunti za facebook kwa kutumia jina langu na wakifanikiwa kwani walipata watu wengi kwa kipindi kifupi,”amesema Shekh Kishk.

  Shekh Kishk amesema kuwa,  katika akaunti hizo watu wataweza kupata darasa mbalimbali za hadithi, mawaidha, hotuba, hadithi na kutakuwa na usomaji wa Quran katika sauti saba, mbali na hilo kutakuwa na video za mawaidha na hotuba ambazo anazitoa wakati  akiwa katika ziara za mikoani na hata nje ya nchi kwani amekuwa anatembea na watu wa habari kila mahala.

  Amewatoa hofu watu kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii ndiyo inaweza kusababisha kufanya maovu ila ukiamua kuitumia vizuri inaweza kukuletea faida.

  Kwa upande wa katibu wake anayejulikana kwa jina la Masawe, alisema kuwa kwa kipindi kirefu alikuwa anasumbuliwa na watu mbalimbali kwa nini Shekh Kishk hafungui akaunti za kijamii  ila baad aya kukaa naye na kushauriana tukaamua kufungua na katika muda wa saa 24 ameweza kupata marafiki 5000 na kuamua kuwa na page ya facebook.
   Shekhe Nurdeen Kishk akiwaonyesha waandishi wa habari jina analotumia katika mtandao wa kijamiiya facebook, twitter na instagram sambamba na Kishk Online Tv leo Jijini Dar es salaam.
   Shekh Nurdeen Kishk akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kufungua akaunti za mitandao ya kijamii facebook, twitter na instagram sambamba na Kishk Online Tv zilizotambulishwa rasmi leo.
  Katibu wa Shekh Nurdeen Kishk akizungumza na waandishi kuhusu namna jamii ilivyokuwa inatamani kuona Shekh anakuwa na akaunti katika mitandao ya kijamii.


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akiongea na menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). Keshoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Prof. Sylvia Temu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru. (Picha na HESLB) 
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). Keshoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Prof. Sylvia Temu. (Picha na HESLB) 
  Baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Bodi ya Mikopo katika mkutano na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ambaye amefanya ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). (Picha na HESLB) 

  Na Mwandishi Wetu
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amewataka wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuongeza ubunifu ili kuondokana na changamoto wanazokutana nazo.

  Prof. Mdoe amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 13, 2017) alipokua akiongea na Menejimenti ya HESLB katika ziara aliyoifanya katika makao makuu ya HESLB jijini Dar es Salaam.

  “Pamoja na mafanikio mnayoyapata hasa katika ukusanyaji wa mikopo lakini bado kuna changamoto…zikiwemo za malalamiko ya vigezo vya utoaji mikopo ambavyo mnahitaji kuwa wabunifu kwa kuwashirikisha wadau,” amesema kiongozi huyo katika ziara yake ya kikazi.

  Kwa mujibu wa Prof. Mdoe, nia ya Serikali ni kuona malalamiko yote ya wadau yanatafutiwa ufumbuzi kwa haraka, na ili hilo litimizwe ni muhimu kwa wafayakazi wa taasisi za umma kuwa wabunifu zaidi.

  Awali akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu huyo katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul- Razaq Badru alisema taasisi yake imejipanga kuhakikisha huduma inazotoa zinaakisi matarajio ya Serikali na kwamba mkazo umewekwa kwenye kuongeza kasi ya ukusanyaji mikopo na kushirikisha wadau katika kuboresha vigezo vya utoaji mikopo kwa miaka ijayo.

  “Katika mwaka 2016/2017 pekee, tulikusanya zaidi ya Tshs 116 bilioni na wastani wa makusanyo yetu kwa mwezi kwa sasa ni Tsh 12 bilioni. Tunataka kufikisha Tsh 15 bilioni kwa mwezi ifikapo mwakani,” amesema Bw. Badru katika mkutano huo uliohidhuriwa pia na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Sylvia Temu.

  Wakati huohuo, HESLB imewakumbusha wanafunzi wote ambao hawajaridhika na mikopo waliyopangiwa au kukosa, kuhakikisha kuwa watatemebelea mtandao wa Bodi (olas.heslb.go.tz) wanakata rufaa na kuwasilisha kwa maafisa mikopo waliopo kwenye vyuo vyao kabla ya tarehe 19 Novemba mwaka huu.

  Ufafanuzi huo unafuatia baadhi ya wanafunzi walikosa mikopo au kutoridhika na mikopo waliyopangiwa kufika katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam na zile za kanda zilizopo Dodoma, Arusha, Mwanza na Zanzibar.

  Mwishoni mwa wiki, HESLB ilitangaza kufungua dirisha la rufaa ambalo litafungwa Novemba 19, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili. Kwa muibu wa HESLB, lengo ni kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo Novemba 30, 2017.

  Maelezo ya kina kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufaa yatatolewa kupitia tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kwenye mkutano wa Tume na vyama hivyo ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Novemba 26, 2017. Mkutano huo umeliofanyika leo jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Jaji  Mst. Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhani akitoa mada kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati Tume ilipokutana na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam leo. 
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (wa tatu kulia) akiwa meza kuu na Makamu Mwenyekiti Jaji Mst. Hamid Mahmoud Hamid( wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani )wa pili kulia), Makamishna wa NEC Jaji Mst. Marry Longway na Asina Omari na kulia ni Mwakilishi wa Mkuuu wa Jeshi la Polisi (IGP), kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasa uliofanyika Dar es Salaam jijini leo.
  Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Yeremia Maganja akichangia mada kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari baada ya ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage   (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Pwani Casimir mabina.Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Saumu Rashid. 
  Picha na Hussein Makame-NEC

  Hussein Makame-NEC
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistolces Kaijage amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili ya Uchaguzi.

  Jaji Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa NEC na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kuelekea Uchaguzi mdogo wa madiniwa.

  Alisema iwapo ukiukwaji au uvunjaji wa Maadili  hayo utatokea, Chama au Mgombea awasilishe malalamiko hayo mbele ya Kamati husika ili ishughulikiwe kisheria.

  Aliwakumbusha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Tume inayo mamlaka ya kuruhusu kuwepo kwa Kampeni za Uchaguzi katika maeneo ya Uchaguzi na siyo Mikutano ya Vyama vya Siasa. 

  Hivyo, kampeni hizo zifanyike kwenye Kata husika na inategemewa kuwa Mikutano ya Kampeni italenga kuwashawishi, kwa namna ya kistaarabu, wananchi wa Kata husika ili wamchague Mgombea anayefanyiwa kampeni. 

  ” Kwa mujibu wa kipengele cha 2.1. (c) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 tunategemea kila Chama cha Siasa kiendelee kufanya Kampeni kwa mujibu wa ratiba. Kampeni zote zinatakiwa kuanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni” alisema Jaji Kaijage. 

  Aliongez kuwa kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Tume imekwisha kutoa ushauri kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya ili katika kipindi hiki cha Uchaguzi wahakikishe wanazingatia wajibu wao na ukomo wa madaraka yao katika shughuli za Uchaguzi kuanzia kipindi cha Kampeni hadi kutangazwa kwa Matokeo. 

   Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kailima Ramadhani aliaviomba Vyama vya Siasa kuwahimiza wanachama na wapenzi wao walioandikishwa kuwa Wapiga Kura wajitokeze  Siku ya Uchaguzi kwenda Kupiga Kura zao bila hofu yoyote  kuhusu usalama wao.

  “Ni imani ya Tume kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa mtakuwa chachu ya kuwaongoza na kuwaelekeza wanachama, wafuasi na mashabiki wenu katika kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu’ alisema Kailima.

  Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba, 2017 ambapo wapiga kura 333,309 wanategemewa kupiga kura siku ya uchaguzi huo.

  0 0

  Meza kuu kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Mhe. Wilson Masilingi, Naibu Waziri wa afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman,Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Anisa  Mbega, Bi.Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) !, Bwn. Assenga kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. wakifuatilia jukwaa la afya lililoandaliwa na DICOTA katika kuwakutanisha wadau wote nje na ndani ya Marekani sekta ya afya kuwatambua na kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika sekta hiyo nchini Tanzania. Jukwaa la afya lilifanyika siku ya Jumamosi Novemba 11, 2017 Martins Crosswind Greenbelt, Maryland nchini Marekani. Picha naVijimambo Blog na Kwanza Production
  Bwn. Lunda Asmani akiwakaribisha wadau wote na kufungua jukwaa la afya.
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akisoma hotuba yake kwenye kongamano la Afya lililofanyika siku ya Jumamosi Nov 11, 2017 Greenbelt, Maryaland nchini Marekani. Katika hotuba hiyo aliwashukuru DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo la wadau wa afya kwa kuthamini kazi kubwa inayofanywa na wadau hao na jitihada binafsi zinazofanywa kwa kusaidia ndungu zao nyumbani Tanzania pia alisema Rais Dkt John Pombe Magufuli anatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora kwa nchi yao.
  Balozi wa African Union nchini Marekani, Mhe.Arikana Chihombori Quao akichangia kwenye jukwaa hilo na kueleza changamoto nyingi nchi za Afrika inazopata katika sekta hiyo kutokana na miundo mbinu kuwa duni na sababu kubwa inachangiwa na wakoloni walivyoligawa bara la Afrika na kuwa nchi mbalimbali kwa kuogopa nguvu ya Afrika na utajiri wake usije ukaongoza Dunia.
  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman akiwashukuru Diaspora kwa mchango mkubwa kwa sekta ya afya Zanzibar na baadae kutoa salamu za Rais wa Zanzibar Mhe. Dr Ali Mohamed Shein kwa kutoa shukurani zake na kuthamini mchango mkubwa wa Diaspora hasa katika sekta ya Afya.
  Balozi Anisa Mbega mkuu wa idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishiriki jukwaa la Afya kwa kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo na kuwakutanisha wadau wa afya na Serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora.
  Balozi Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa DICOTA kwa kuandaa jukwaa la afya na baadae kutoa mfano wa mtu akiwekewa fedha na afya bora yeye atakimbilia kwenye fedha kwa sababu hatambui umuhimu wa afya njema ni zaidi ya fedha kwa maana kwamba binadamu wengi hawaelewi umuhimu wa afya lazima tutambue hilo huku akitolea mfano mwingine wa nyani unapo mwekea fedha na ndizi yeye atachangau ndizi kwa sababu anajua bila ndizi maisha yake yapo hatarini. 
  Dr. Mary Banda kutoka Jambo Tanzania akielezea jinsi alivyotumia elimu yake kwa kuelekeza nguvu yake kusaidia sekta ya afya mkoa wa Kagera.
  Bi. Christine Lasway kutoka MyAfyaPal akielezea umuhimu wa afya na jinsi anavyoelekeza nguvu zake katika kusaidia sekta ya afya nchini Tanzania.
  Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

  Bi.Tausi Suedi kutoka Childbirth Survival Tanzania akielezea jinsi alivyojikita katika kusaidia kuokoa maisha ya mtoto hasa wakati wa uzazi Tanzania kwa kutoa elimu kwa wakunga na wazazi kabla na baada ya kujifungua ikiwemo kwapelekea mahitaji muhimu kabla ya kujifungua.
  Dr. Secelela Malecela kutoka Janet Weir Children's Hospital akieleza anavyoguswa katika kuelekeza nguvu zake katika sekta hiyo Dodoma.
  Bi. Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) akitoa shukurani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa jitihada za Diaspora katika sekta ya afya Zanzibar na kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa la Afya na kuwaasa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuendeleza na kuthamini utamaduni wetu.
  Dr. Frank Mimja akielezea umuhimu wa kusaidia sekta ya afya Tanzania na jitihada anazofanya kwa kupeleka madaktari Tanzania na kuwaelekeza wadau waliohudhuria jukwaa la Afya njia iliyosahihi kupitia katika kutimiza ndoto na azma yako ya kusaidia ndugu zetu Tanzania.
  Kutoka kushoto ni Bwn. Lunda Asmani DICOTA, Bi. Adila Hilal Vuai kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

  Juu na chini ni wadau wa jukwaa la afya wakifuatilia jukwaa hilo wakati likiendelea.
  Picha juu na chini ni wadau wa afya wakizungumzia na kubadilishana mawazo katika kuweka nguvu ya pamoja katika kusaidia sekta ya afya Tanzania.
  Juu na chini ni picha za pamoja na wageni waheshimiwa,
  Juu na chini ni mazungumuzo na wageni waheshimiwa.
  Mahojiano yaliyofanywa na kwanza Production.

  0 0

  Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma

  Serikali imerejesha hati ya  Kiwanja Namba 9331 kilichopo kitalu namba 91 Msalato Dodoma kwa mmiliki wake halisi Bw. Sagaf Omari na Bi Madina Hassan ambao ni wamiliki halali wa kiwanja hicho kilichouzwa kwa Bw. Lucas Mlay  wa Jijini Dar es Salaam kwa shilingi milioni 35  kwa njia zisizo halali.

  Akizungumza wakati akimkabidhi hati hiyo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa kiwanja hicho  chenye ukubwa wa takribani hekta mbili na nusu kiliuzwa bila mmiliki halali wa kiwanja hicho kuwa na taarifa kupitia kwa wanasheria wasio waaminifu waliosaidia kutaka kufanikisha wizi wa kiwanja hicho.

  “Niwatahadharishe Mawakili wote na wanasheria ambao wanashirikiana na watu wasio waaminifu kutaka kudhulumu viwanja vya wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawachukuliwa hatua kali za kisheria na kwa kuanza tutaanza na hawa mawakili waliofanikisha mchezo huu wakumdhulumu mama huyu na mume wake kiwanja chao wanachomiliki kihalali” Alisisitiza Lukuvi

  Akifafanua Waziri Lukuvi amesema kuwa Wizara yake imejiridhisha kuwa nyaraka zilizowasilishwa ili kubadilisha umiliki wa kiwanja hicho ni za kughushi na  wamiliki halali wa kiwanja hawakuwa na taarifa kuhusu kuuzwa kwa kiwanja chao hadi walipopata taarifa kwa majirani na kuamua kuchukua hatua kwa kuwasilisha malalamiko yao katika Ofisi yake.

  “Nimechukua hatua na tayari yule mwanasheria aliyehusika katika kughushi nyaraka za kiwanja hiki na kukiuza ameshakabidhiwa kwa vyombo vya dola kwa hatua zaidi hivyo ni vyema watu wote wenye nia yakudhulumu viwanja vya wananchi masikini wakaacha tabia hiyo mara moja kwani Serikali ya Awamu ya Tano itawachukulia hatua kali mara moja ili kukomesha tabia hii ”Alisisitiza Mhe. Lukuvi

  Kwa upande wake  Bi. Madina Hassan akipokea hati ya Kiwanja hicho amemshukuru  Waziri Lukuvi kwa hatua anazochukua katika kuhakikisha wanyonge wanapata haki hasa pale panapojitokeza watu wanaojaribu kudhulumu viwanja vya wananchi masikini .

  “Kwa kweli naishukuru Serikali ya Awamu ya Tano jinsi inavyotusaidia wanyonge ili tupate haki zetu hasa katika sekta hii ya ardhi nawaombea kwa Mungu ili awalinde Viongozi hawa” alisisitiza bi Madina.

  Kwa upande wake mnunuzi wa Kiwanja hicho Bw. Lucas  Mlay amesema kuwa hakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya sheria na hakutambua kuwa hati za kiwanja hicho zilikuwa zimeghushiwa na kuongeza kuwa angetambua hilo asingelipa zaidi milioni 35 ili kununua kiwanja hicho.

  Naye Msajili wa  Hati wa Wizara hiyo Bw. Geofrey William amesema kuwa ni vyema wananchi hasa katika Mkoa wa Dodoma wakachukua hatua kujiepusha na utapeli wa viwanja unaoendeshwa na baadhi ya watu hasa kwa viwanja ambavyo havijaendelezwa kwa muda mrefu.

  Aliongeza kuwa kumekuwa na wimbi la watu kuwasilisha maombi ya kupotelewa na hati ili kufanya mchakato wa kubadili umiliki wa viwanja ikiwa ni sehemu ya mbinu zinazotumiwa na matapeli.

  Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha vitendo vya kuwazulumu wananchi masikini viwanja, mashamba  na maeneo ya umma ikiwa ni moja ya mikakati yake kuhakikisha kuwa wanachi wote wanapata haki sawa bila kujali hali ya kipato au wadhifa.

  0 0

  NA ESTOM SANGA- DODOMA

  Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Huruma Mkuchika amesema serikali itaendelea kuunga mkono mchango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kutatua kero zinazowakabili wananchi katika kupambana na umasikini ili vita hiyo iwe endelevu .

  Mheshimiwa Mkuchika amesema jambo muhimu kwa TASAF ni kuhakikisha kuwa walengwa wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wanafikiwa na kunufaika na huduma za mfuko huo huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili mema katika utendaji kazi wa wadau wote wanaohusika na utekelezaji wa Mpango huo .

  Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF zilizowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga mjini Dodoma, Waziri Mkuchika ameuagiza uongozi wa TASAF kuhakikisha kuwa unawatumia kikamilifu Maafisa maendeleo ya Jamii walioko katika maeneo mbalimbali nchini kuhamasisha shughuli za maendeleo na kupambana na umasikini.

  “tunao maafisa maaendeleo ya Jamii nchini kote,lakini nina wasiwasi na namna wanavyotumiwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,naagiza TASAF mtumie vizuri hazina hiyo ya wataalamu katika utendaji kazi wenu” ameagiza Waziri Mkuchika.

  Aidha Waziri huyo ameitaka menejimenti ya TASAF kuhakikisha kuwa inaandaa mipango thabiti katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kipindi kirefu huku akisisitiza kuwa walengwa wa Mpango huo wanapaswa kuwekewa mazingira yatakayowawezesha kujitegemea hata baada ya kuondolewa kwenye shughuli za Mpango.

  Akitoa taarifa ya utekelezaji,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mfuko huo umeendelea kuwajengea msingi wa kujitegemea walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini nchini kote,kazi ambayo amesema imefanyika kwa mafanikio makubwa.

  Walengwa wengi hivi sasa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwenye maeneo yao huku akitaja mafanikio makubwa katika utekelezaji wa masharti ya elimu na afya kwa walengwa jambo ambalo amesema linaendelea kusaidia juhudi za serikali za kupambana na adua ujinga na maradhi.

  “Kumekuwa na mwitikio mkubwa katika kuwapeleka watoto kutoka kaya masikini kupata elimu na huduma za afya, kwani hayo ni miongoni mwa masharti ya Mpango, na hyo kwetu ni mafanikio makubwa” amesisitiza Bwana Mwamanga.

  Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mfuko huo kwa sasa unakabiliwa na changamoto ya kufikia takribani asilimia 30 ya vijiji ambavyo havikufikiwa katika awamu inayokaribia kukamilika, hivyo jitihada zaidi zinafanywa ili kupata fedha za kukamilisha vijiji hivyo katika awamu itakayofuata.
   Mheshimiwa Mckuchika akitazama nakala za vipeperushi,taarifa na majarida yenye taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF,Ofisi kwake mjini Dodoma. 
   Waziri Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na Utumishi wa Umma ,baada ya kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF ofisini kwake mjini Dodoma, aliyevaa Kaunda suti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga.
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Mhe. George Mkuchika (aliyevaa tai nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislau Mwamanga,ofisi kwa Waziri mjini Dodoma.

  0 0

  NA ESTOM SANGA- DODOMA

  Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Huruma Mkuchika amesema serikali itaendelea kuunga mkono mchango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kutatua kero zinazowakabili wananchi katika kupambana na umasikini ili vita hiyo iwe endelevu .

  Mheshimiwa Mkuchika amesema jambo muhimu kwa TASAF ni kuhakikisha kuwa walengwa wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wanafikiwa na kunufaika na huduma za mfuko huo huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili mema katika utendaji kazi wa wadau wote wanaohusika na utekelezaji wa Mpango huo .

  Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF zilizowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga mjini Dodoma, Waziri Mkuchika ameuagiza uongozi wa TASAF kuhakikisha kuwa unawatumia kikamilifu Maafisa maendeleo ya Jamii walioko katika maeneo mbalimbali nchini kuhamasisha shughuli za maendeleo na kupambana na umasikini.

  “tunao maafisa maaendeleo ya Jamii nchini kote,lakini nina wasiwasi na namna wanavyotumiwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,naagiza TASAF mtumie vizuri hazina hiyo ya wataalamu katika utendaji kazi wenu” ameagiza Waziri Mkuchika.

  Aidha Waziri huyo ameitaka menejimenti ya TASAF kuhakikisha kuwa inaandaa mipango thabiti katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kipindi kirefu huku akisisitiza kuwa walengwa wa Mpango huo wanapaswa kuwekewa mazingira yatakayowawezesha kujitegemea hata baada ya kuondolewa kwenye shughuli za Mpango.

  Akitoa taarifa ya utekelezaji,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mfuko huo umeendelea kuwajengea msingi wa kujitegemea walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini nchini kote,kazi ambayo amesema imefanyika kwa mafanikio makubwa.

  Walengwa wengi hivi sasa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwenye maeneo yao huku akitaja mafanikio makubwa katika utekelezaji wa masharti ya elimu na afya kwa walengwa jambo ambalo amesema linaendelea kusaidia juhudi za serikali za kupambana na adua ujinga na maradhi.

  “Kumekuwa na mwitikio mkubwa katika kuwapeleka watoto kutoka kaya masikini kupata elimu na huduma za afya, kwani hayo ni miongoni mwa masharti ya Mpango, na hyo kwetu ni mafanikio makubwa” amesisitiza Bwana Mwamanga.

  Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mfuko huo kwa sasa unakabiliwa na changamoto ya kufikia takribani asilimia 30 ya vijiji ambavyo havikufikiwa katika awamu inayokaribia kukamilika, hivyo jitihada zaidi zinafanywa ili kupata fedha za kukamilisha vijiji hivyo katika awamu itakayofuata.
   Mheshimiwa Mckuchika akitazama nakala za vipeperushi,taarifa na majarida yenye taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF,Ofisi kwake mjini Dodoma. 
   Waziri Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na Utumishi wa Umma ,baada ya kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF ofisini kwake mjini Dodoma, aliyevaa Kaunda suti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga.
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Mhe. George Mkuchika (aliyevaa tai nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislau Mwamanga,ofisi kwa Waziri mjini Dodoma.

older | 1 | .... | 1426 | 1427 | (Page 1428) | 1429 | 1430 | .... | 1898 | newer