Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1421 | 1422 | (Page 1423) | 1424 | 1425 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Uongozi wa klabu ya Azam FC imeamua kuvunja mkataba na mshambulizi wake, Yahaya Mohammed raia wa Ghana baada ya kuona ameshindwa kuwapatia kile ambacho wanakihitaji kwa muda wote aliokuwa ametumikia kwenye klabu hiyo.

  Mwishoni mwa wiki baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting , Kocha Mkuu wa Azam  Aristica Cioba aliweka wazi mkakati wake wa kutaka kupata washambuliaji  wengine wawili ili kuongeza nguvu ya kikosi chake.

  Akitoa ufafauzi wa maamuzi hayo, Msemaji wa Azam Jaffary Idd Maganga alisema kuwa wamefikia uamuzi wa kuvunja mkataba na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 baada ya kuonesha kiwango duni tofauti na matarajio yao walipomchukua mwaka jana wakati wa dirisha Dogo la usajili.

  "Nichukue nafasi hii kuwafahamisha kwamba hatutaendelea kuwa naye, uongozi umekutana naye, wamezungumza kuhusiana na suala lake na wamemalizana. Hivi sasa Mohamed sio mchezaji tena wa Azam  baada ya makubaliano kati yake na uongozi," alisema ..

  Maganga amesema tayari wameshampatia release letter na pamoja na hayo tayari wameshampatia kila kitu ikiwemo tiketi ya ndege ambapo wanatarajia ataondoka kurudi kwao Ghana Jumanne hii.

  "Tutamkumbuka Yahaya, kwa Maana kwamba yale ambayo ameyafanya kwenye timu yetu, ametusaidia kupata ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na pia msimu ndiye aliyefunga bao la kwanza," alisema.

  Mbadala wa Yahaya Mohamed kwa mujibu wa Afisa Habari Jaffary Maganga, ni kwamba atatangazwa baada ya benchi la ufundi kufanya tathmini na kuchambua wale wanaowahitaji.

  Mshambuliaji huyo alijiunga na Azam akitokea Aduana Stars ya Ghana, ambayo aliisaidia kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ghana msimu 2015/16, Mohammed pia aliiibuka mfungaji bora namba mbili wa ligi hiyo kwa mabao 15 aliyofunga nyuma ya Latif Blessing wa Liberty Proffesional aliyetupia 17.

  Mohammed alikuwa moja ya wachezaji  kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika mwaka juzi nchini Afrika Kusini na timu hiyo kuwa washindi wa pili.  0 0

   Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru katika uchaguzi mdogo wa kumpata diwani atakayekuwa kiongozi wa kata hiyo huku CCM wakimuombea kura mgombea wao Baraka Kimata  
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Kitwiru

  Na Fredy Mgunda,Iringa

  Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kufanya siasa safi kwa kutoa hoja za msingi wakati wanaomba kura kwa wananchi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru unaoendelea hivi sasa.

  Akizungumza na blog hii Bashir alisema kuwa wapinzani wamekuwa wakitoa lugha za matusi kwa wananchi wakati wakiomba kura majukwaani.

  “Kila wakisimama jukwaani ni matusi tu utafikiri ndio kura zenye mimi naomba watumie lugha za kistaarabu kuomba kura kwa wapiga kura kwa wananchi wa kata ya Kitwiru na kuwafanya wananchi kumchagua kiongozi wanaemtaka” alisema Bashir

  Bashir alisema kukitukana chama chama mpinduzi ni kukikosea heshima kwa kuwa chama hicho kimekuwa kikifanya kampeni za kistaarabu bila kutoa maneno ya machafu kwa wapinzani na kuendelea kuwaaminisha wananchi kuwa CCM inafanya kampeni za kistaarab.

  “Yaani saizi wakisimama kwenye majukwa kazi yao ni kutoa lugha chafu dhidi ya chama chetu hivyo mimi nawaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa watulivu na kuhakikisha mgombea wa chama cha mapinduzi anashinda kwa kishindo” alisema Bashir

  Aidha Bashir aliwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpigia kura mgombea wa chama cha mpinduzi (CCM) ambae atawaletea maendeleo kwa kufuata na kutekeleza vilivyo ilani ya chama hicho kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayofanya.

  “Huku CCM kuna mfumo ambao unawaongoza viongozi wetu na mambo mengi yanafanywa kwa kufuata utaratibu hivyo wananchi wanatakiwa kumwamini Baraka Kimata kwa maendeleo ya kata ya Kitwiru” alisema Bashir

  Bashir amewataka viongozi wa CCM kutumia lugha nzuri wakati wa kuomba kura na matusi kuwaachia wapinzani na kutengeneza utofauti baina ya CCM na vyama vingine.

  “Niwaombe wanakitwiru kuhakikisha tarehe ishirini na sita mwezi huu Baraka Kimata anaibuka mshindi katika uchazi huu mdogo wa kata hiyo” alisema Bashir

  Lakini Bashir amewahakikishia wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) na wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa watashinda kwa kishindo kutokana na mikakati ya chama hicho ambayo ipo imara na dhabiti kwa ajili ya kushinda kata hiyo.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi barabara ya Kyaka-Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakipeana mikono baada ya Rais kufungua rasmi barabara ya Kyaka-Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na viongozi wengine wakimsaidia kushika utepe anaoukata kama ishara ya kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua rasmi barabara ya Kyaka-Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mzee Nekemia Kazimoto (80) na mkewe Florence Kazimoto baada ya sherehe za kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijumuika katika sala na Mzee Nekemia Kazimoto (80) na mkewe Florence Kazimoto na binti yao  Lucy Kazimoto alipomtembelea kumjulia hali baada ya sherehe za kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa mjini Bukoba waliomsimamisha ili awasalimie wakati akirejea kutoka Karagwe kwenye  sherehe za kufungua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa Km 59.1 eneo la Kayanga wilayani Karagwe mkoa wa Kagera leo Novemba 7, 2017. Picha na Ikulu

  0 0


  0 0


  0 0

  Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tz Prison Novemba 19.

  Mazoezi hayo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru, Yanga  wamefanya mazoezi bila nyota wao nane walioitwa katika timu za taifa pamoja na mjeruhi watatu ambao ni kiungo Thabani Kamusoko, Washambuliaji Donald Ngoma  na Amissi Tambwe.

  Lakini imewakosa wachezaji wake watano walioitwa katika timu za taifa kubwa na ile ya vijana.Walioitwa katika timu ya taifa, Taifa Stars ni Ramadhani Kabwili, Kelvin Yondani, Gadiel Michael, Raphael Daud na Ibrahim Ajibu Migomba.

  Kwa mujibu w daktari wa timu Dr Edward Bavu  ameweka wazi kuwa majerehui hao wanaweza kurejea dimabni Novemba 10 kwa ajili ya kuanza mazoezi mepesi na kisha kujiunga na wenzao kwa mazoezi ya pamoja.

  Kwa sasa hawajafika asilimia 100 ila sio Ngoma pekee, bali hata kiungo  Kamusoko na Tambwe pia wanaweza kuanza mazoezi wiki. Matarajio yetu hadi wiki ijayo watakuwa wameungana na wenzao kikamilifu."

  Ngoma ambaye kwa sasa yupo nchini kwao akiendelea na matibabu atarejea siku yoyote kwa ajii kujiunga na wenzake akianza mazoezi ya taratibu.

  Yanga wanaoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 17 wataumana na Tz Prisons wakiwa wametoka kupata sare tasa dhidi ya Singida United mwishoni mwa wiki hii.

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

  Serikali imesema itahakikisha vijiji vyote visivyo na umeme vinapata umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme vijijini awamu ya Tatu (REA-III) unaotegemewa kukamilika mwaka 2020/21.

  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea Hassan Masala juu ya mpango wa Serikali katika kusambaza umeme katika kata zilizobaki wilayani Nachingwea kupitia REA III.

  “Mradi wa REA III utajumuisha vipengele vitatu vya Densification, Grid Extension na Off gridrenewable ambapo Mkoa wa Lindi chini ya miradi ya uendelezaji wa grid (Grid extension) katika Mzunguko wa kwanza unatekelezwa kwa muda wa miezi 24 na Kampuni ya Stategrig & Technical Works Ltd,” alifafanua Naibu Waziri huyo.

  Aliendelea kwa kusema, katika wilaya ya Nachingwea mpango wa Awamu ya Tatu utavipatia umeme vijiji 30 ambapo kazi za utekelezaji wa mradi zilianza Julai mwaka huu na zinatarajiwa kukamilika Juni 30, 2019.

  Mgalu amesema, vijiji vilivyobakia vitapatiwa umeme katika mzunguko wa pili wa REA III utakaoanza Aprili, 2019 hadi Desemba 2021.

  Vile vile amesema, kazi ya kupeleka umeme mzunguko wa kwanza itahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 380, ufungaji wa transfoma 18, ujenzi wa njia za msongo wa kilovoti 0.4 zenye urefu wa kilomita 360 na uunganishaji wa wateja 5,710 katika Mkoa mzima wa Lindi.

  Aidha amesema, kwa upande wa Wilaya ya Nachingwea jumla ya wateja 1,200 wataunganishwa, ambapo kwa sasa Mkandarasi anaendelea na upimaji wa njia za umeme na tayari amefikia asilimia 30 na kazi za upimaji zitakamilika mwishoni mwa Novemba 2017.

  0 0

  Benny Mwaipaja, Dodoma
  SERIKALI imewalipa pensheni wafanyakazi 245 wa iliyokuwa Kampuni ya Simu ya TTCL, chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kiasi cha shilingi bilioni 12.7.
  Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratias Ngalawa, aliyetaka kufahamu, lini Serikali ingewalipa wafanyakazi wa TTCL wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki madai ya pensheni yao.
  Dkt. Kijaji alisema kuwa malipo hayo yamefanyika kwa wafanyakazi 245 ambao wamelipwa fedha zao kwa mkupuo ambapo kati yao wastaafu 54 walifariki dunia na malipo yao kulipwa warithi wao.
  “Wastaafu 198 wanaendelea kulipwa malipo ya nyongeza ya pensheni ya kila mwezi” alisema Dkt. Kijaji.Alisema kuwa malipo hayo yanafuatia uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi namba 69/2005 ambapo wafanyakazi hao 254 waliishitaki Serikali kupinga uamuzi wa kusitisha mfuko uliojulikana kama East Africa Non Contributory Pension Scheme.
   “Katika Shauri hilo, Mahakama Kuu iliamua kuwa, uamuzi wa Serikali kusitisha mfuko huo haukuwa sahihi kisheria na hivyo kuamua wafanyakazi 254 waliokuwa katika shauri hilo walipwe madai yao ambayo yalijumuisha malipo ya mkupuo, riba pamoja na pensheni yao ya kila mwezi” aliongeza Dkt. Kijaji.
  Alisema kuwa baada ya uamuzi huo wafanyakazi wengine 324 nao walifungua kesi Makahama Kuu wakitaka walipwe pensheni kama wenzao walivyolipwa wakati hawakuwa sehemu ya wafanyakazi waliofungua na kushinda kesi hapo awali.“Mahakama Kuu iliamua kuwa, wafanyakazi waliofungua kesi ya awali ndio walipwe madai yao, na kwamba deed of settlement iliyosajiliwa Mahakamani ilihusisha wafanyakazi hao pekee” alifafanua Dkt. Kijaji.
  Alisema wafanyakazi wengine ambao hawakuwa sehemu ya kesi hiyo hawawezi kulipwa kwa kutumia hukumu na tuzo ya kesi ambayo hawakuwa sehemu yake na kusisitiza kuwa, Serikali haiwezi kulipa madai mengine ambayo hayakuthibitika kisheria.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisistiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma Novemba 7, 2017.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akisisitiza jambo kuhusu mkakati wa Serikali kuboresha mazingira ya Ajira hapa nchini walipokutana leo Mjini Dodoma katika kikao cha Wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw .Geodfrey Simbeye akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akichangia mada kuhusu ushiriki wa watu wenye ulemavu katika programu zinazotekelezwa na Serikali katika masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi ili kujikwamua kiuchumi.
  Wajumbe wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Kujadili Masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma.

  PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA

  0 0

  NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini leo amefungua semina ya wajasiriamali wapatao 2000 wa Jimbo hilo.

  Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Cavilam wilayani Dodoma ambapo wajasiriamali hao watapata nafasi ya kujifunza juu ya elimu ya Ujasiramali na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

  Aidha amesema kupitia semina hiyo watatoa walimu 205 ambao watazunguka katika kata zote 41 za Dodoma Mjini kwenda kufundisha vikundi vya wakinamama,Vijana na Wazee katika masuala ya utengenezaji bidhaa na kuongeza thamani,Ufugaji wa Kuku, Samaki na Mafunzo ya kilimo Bora.

  Mavunde amesema baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo litaandaliwa kongamano lingine kubwa litakalohusisha Taasisi za fedha na Mifuko ya Uwezeshwaji ili wajasiriamali wapate fursa ya kufahamu namna ya kuifikia mikopo na ruzuku zitakazosaidia upatikanaji wa mitaji ya kufanyia shughuli za uzalishaji mali.
   Mbunge wa Dodoma mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akifungua semina ya wajasiriamali Dodoma.
   Mbunge wa Dodoma mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akizungumza na wajasiriamali.
  Washiriki wa semina ya ujasiriamali


  0 0

   Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi aina ya Wema, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Peres Boniface Magiri wakati wa uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazi lishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga wilayani humo jana.
   Wanakikundi cha Aliselema wakishusha mbegu ya mihogo tayari uzinduzi wa shamba darasa.
   Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza kabla ya kuanza uzinduzi huo katika Kijiji cha Isunda kilichopo Kata ya Nkolye.
   Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Pares Magiri akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Isunda.
   Wanakikundi cha Aliselema wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akielekeza namna ya kupanda mihogo.


    Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akimuelekeza namna ya kupanda mbegu ya mihogo mkuu wa wilaya hiyo.
   Mwenyekiti wa Kikundi cha Aliselema, Amir Hassan akipanda mbegu ya mihogo.
   Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa akipanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa.
   Mwenyekiti wa Kikundi cha Aliselema, Amir Hassan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto waliyokuwa nayo ya kupata mazao kiduchu kwa kutumia mbegu zisiso bora.

   Wakulima wakisubiri kuelekezwa namna ya upandaji wa mbegu hizo za mihogo.
   Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Pares Magiri akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Kisanga kabla ya uzinduzi wa shamba darasa la viazilishe.
   Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akimuelekeza namna ya kupanda mbegu ya viazilishe katika kijiji cha Kisanga.
   Wanawake wa Kijiji cha Kisanga wakiwa kwenye uzinduzi huo wa shamba darasa la mbegu ya viazilishe.
   Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru mkoani Mwanza, Mariana akielekeza namna ya upandaji wa viazilishe.
   Mkuu wa Wilaya, Peres Magiri akipanda mbegu ya viazilishe wakati wa uzinduzi wa shamba hilo.
   Mwalimu wa Baraka Kita wa Shule ya Msingi Sogea B, akipanda mbegu hiyo ya viazilishe.
   Mkulima, Mariam Said akipanda mbegu ya viazilishe 
  Mwalimu George Adamu Mwalwizi, akizungumzia mbegu mpya ya viazi lishe walioletewa kuwa itakuwa ni mkombozi kwao na wanafunzi.

  Na Dotto Mwaibale, Sikonge Tabora

  WANAFUNZI wilayani Sikonge mkoani Tabora wataanza kunufaika na viazi lishe baada ya kupokea mbegu bora ya viazi hivyo, mihogo na mahindi ya Wema kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

  Hayo yameelezwa katika Kijiji cha Kisanga na Mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface Magiri wakati akizungumza na wakulima kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazilishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga.

  Magiri alisema baada ya kuotesha mbegu hiyo ya viazilishe kwa wingi kitakachofuata ni kuanzisha utaratibu wa wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kupata chakula cha mchana badala ya kwenda nyumbani.

  Alisema wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa hayo yanatunzwa na kutoa mrejesho.

  Aliongeza kuwa shule mbalimbali zitaanzisha mashamba ya viazilishe hivyo ili kumaliza tatizo la kukosa chakula kama sio kulipunguza.

  "Tunahitaji matokeo chanya ya mashamba darasa hayo yawasaidie wakulima wengine katika wilaya hiyo na kuwa atahakikisha anatembelea mara kwa mara yalipo mashamba hayo" alisema Magiri.

  Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura aliwaambia wakulima kuwa hekta moja ya muhogo kwa kutumia mbegu hiyo bora inaweza kutoa tani 25 hadi 32 wakati viazi itatoa tani 7 hadi 9 kwa Hekta moja.

  Alisema kuwa endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya muhogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye viazi wanapata tani moja hadi 3.

  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hiyo ya mahindi imefanyiwa utafiti na inavumilia ukame wakati ile ya mihogo ikivumilia magonjwa kama batobato na michirizi kahawia huku zikitoa mavuno mengi.

  0 0

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa maelekezo mbalimbali ya masuala ya kiutumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri ya Wilaya ya Madaba Bw. Shafi Mpenda na kushoto kwakwe ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw. Bwai Biseko.
  Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilaya ya Madaba wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) aliyoyatoa katika halmashauri hiyo, wakati ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.
  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bw. Biseko Bwai akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijiji Bw. Simon Bulenganija akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Ruvuma, yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
  Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini kuhusu taratibu zinazohusu menejimenti ya Rasilimaliwatu serikalini, wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ya kuhimiza uwajibikaji.
  Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilay ya Songea Vijiji wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya katibu mkuu huyo ya kuhimiza uwajibikaji katika Hamashauri hiyo.

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma nchini kuzingatia uadilifu katika utendaji kazi, kujituma, kuwajibika kwa wananchi na kwa Serikali ili kujenga Utumishi wa Umma uliotukuka.

  Dkt. Ndumbaro amesema hayo, katika ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Ruvuma yenye lengo mahususi la kubaini changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma katika maeneo yao ya kazi na kuzitafutia ufumbuzi ili kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza Watumishi wa Umma juu ya mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

  Dkt. Ndumbaro akiwa katika Halmashauri za Wilaya ya Madaba na Songea Vijijini amewaeleza watumishi wa halmashauri hizo kuwa, misingi ya uadilifu na uwajibikaji itajengwa na watumishi hao kwa kubadili utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea (business as usual).

  Dkt. Ndumbaro amesema kwamba, Wakurugenzi pamoja na Wakuu wa Idara nchini wana jukumu kubwa la kusimamia utendaji kazi katika maeneo yao ya kazi ili kubadilisha tabia za baadhi ya watumishi wasiowajibika ipasavyo, na kuwafanya watekeleze wajibu wao kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa.

  “ Ninyi Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mhakikishe mnahimiza nidhamu kwa Watumishi wa Umma katika maeneo yenu, mtumishi akikosea achukuliwe hatua mara moja kwa mujibu wa Sheria , Kanuni na Taratibu za Utumishi wa umma zilizopo” Dkt. Ndumbaro amefafanua.

  Dkt. Ndumbaro amebainisha kuwa, kama kuna watumishi wasiotimiza wajibu wao na hawachukuliwi hatua zozote za kinidhamu au za kisheria dhidi yao, kitendo hicho huwakatisha tamaa watumishi wanaojituma katika utendaji kazi wao.

  Aidha, Dkt. Ndumbaro amekemea tabia iliyojengeka kwa baadhi ya watumishi ya kuwakatisha tamaa watumishi wanaojituma na wanaozingatia maadili. “Viongozi tusipokemea na kuwachulia hatua watumishi wenye tabia ya kuwabeza na kuwakatisha tamaa watumishi wanaojituma kazini, ni dhahiri kuwa itashusha morali ya utendaji kazi wa watumishi wanaochapakazi” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.

  Dkt. Ndumbaro amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kuwatambua watumishi wanaofanya kazi kwa bidii kwa kuwapa moyo na motisha, ikiwa ni pamoja na kuwaandikia barua za kuwapongeza ama kuwapa vyeti ikiwa ni mkakati wa kukuza utamaduni wa watumishi kupenda kufanya kazi.

  Pia, Dkt. Ndumbaro hakusita kuwasisitiza Maafisa Utumishi, Watumishi wa Masijala na Makatibu Mahususi kuwa na lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wateja wa ndani na wa nje pindi wanapofika kwao kupata huduma.

  Dkt. Ndumbaro anaendelea na ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma katika Halmashauri za Wilaya ya Songea Mjini, Tunduru, Mbinga, Nyasa, na Namtumbo.

  0 0

  Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Singida umezidi kushika kasi wananchi wakifika kwa wingi kupata huduma ya Usajili unaohusisha uchukuaji wa alama za Kibiolojia, picha na Saini ya Kielektroniki.

  Kwa kushirikiana kwa karibu na Maafisa Usajili, Watendaji wa Kata na Serikali za Mtaa, watumishi wa Mamlaka wamekuwa wafakifanya jitihada kubwa za kuhakikisha Wananchi wanatambua umuhimu wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa pamoja na Matumizi yake Msingi na kushiriki kikamilifu kujisajili. 

  Pamoja na misururu mirefu wananchi hao wameonyesha kutokata tamaa kwa foleni ndefu badala yake wamekuwa wakihamasishana kushiriki ili kila mmoja kupata haki yake msingi kusajiliwa.

  Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa 12 ya Tanzania ambayo zoezi hilo linaendelea kwa sasa ukiwemo mkoa wa Mbeya, Njombe, Songwe, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Iringa.
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA Ndugu Thomas William pamoja na Ndugu Innecent Baraza Meneja Usimamizi wa Majengo (Kushoto) wakifuatilia kwa karibu Uingizwaji wa taarifa za waombaji wa Vitambulisho vya Taifa wakati wa Zoezi la Usajili na Utambuzi linaloendelea Mkoa wa Singida. 
  Wanachi katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, wakifanyiwa usajili wa Maombi ya Vitambulisho vya Taifa katika zoezi la Usajili wa Mkupuo (Mass Registration) linaloendela hivi sasa Mkoani humo.
  Baadhi ya Wananchi katika kata ya Kindai Halmashauri ya Manispaa Singida wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye chumba cha uchukuaji alama za kibaiolojia, picha na saini ya kielektroniki. 
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara Mamlaka ya Vitambulisho Ndugu Thomas William akisimamia zoezi la ugawaji wa fomu za Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.

  0 0


  0 0


  Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeendelea na zoezi la ukamataji wa Wadurufu wa kazi za sanaa na wakwepa kodi kupitia kazi hizo.

  Zoezi hilo limeendelea katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ambapo pia imesisitizwa kuendelea nchi nzima.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart amewaasa Wafanyabiashara wote kufuata taratibu kuhakikisha wanauza bidhaa zenye Stika ya TRA.

  "Uzeni bidhaa zenye Stika ya TRA, acheni kuwaibia Wasanii, wakati huu ni wakati wa Serikali kupata haki yake na Wasanii pia wapate haki zao,wafaidi jasho la kazi yao", amesema Msama

  Pia amewaasa Watanzania wanaonunua kazi hizo za sanaa kuacha kununua kazi ambazo hazina Stika ya TRA, amesema Watanzania wanapaswa kujifunza kulipa Kodi kupitia kazi hizo zenye Stika halali ya TRA.

  "Wale wanaoburn CD, Wanaoingiza nyimbo kutumia Kompyuta muache, zoezi hili sio Dar es Salaam pekee zoezi ni la nchi nzima na tutahakikisha kila anayenunua bidhaa hizo ananunua bidhaa zenye Stika", amesisitiza Msama.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart wakiwa wamevamia moja ya duka linalofanya biashara ya kuuza kazi za Wasanii kwa kuziingiza kwenye flash disk ama CD kwa kutumia Kompyuta,maeneo ya Vingunguti mapema jana jijini Dar.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart,wakienelea na ukaguzi wao wa kubaini Wakwepaji kodi na wanao durufu kazi za Sanaa,maeneo mbalimbali kati ya jiji la Dar na kwingineko
  Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart,wakiwa wamemkamata mtu mmoja (jina lake halikutambulika mara moja),aliyekuwa akiuza CD za filamu mbalimbali (ndani na nje ya nchi),maeneo ya Kariakoo jana jioni,jijini Dar zikidaiwa kutokuwa na Stika ya TRA ,kufuatia msako mkali unaofanywa na kampuni hiyo kila kona ya jiji la Dar
  Mmoja wa Askari akiweka alama ya maandishi kwenye moja ya furushi lenye CD zinazodaiwa kutokuwa na Stika ya TRA (inayoonesha ulipaji kodi),mara baada ya kukamatwa mapema jana maeneo ya Kariakoo,jijini Dar,Zoezi hilo linaendeshwa na Kampuni ya Msama Auction Mart ikishirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na jeshi la polisi.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikalini.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Novemba 7, 2017) wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

  Waziri Mkuu amesema ni vema  viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.

  Pia amewataka viongozi hao wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii kuwa Rais Dkt. John Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao kiutendaji.

  “Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla.”

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiwekee utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za Wabunge na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.

  Pia amewataka wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

  Waziri Mkuu amesema Mawaziri na Naibu Mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

  Pia wasimamie utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.
  Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa aongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina jana Novemba 7/2017 Mjini Dodoma. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

  0 0

  Mazungumzo yakiendelea. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanne Marie Kaarstad. 
  Prof. Mkenda na Balozi Oyen wakimsikiliza Balozi Kaarstad mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao .
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya Norway kwa Serikali ya Tanzania, Balozi Arild Oyen ambaye alifika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe maalum. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Norway hususan katika sekta za Nishati, Elimu na Utamaduni. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 08 Novemba, 2017. 
  Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Balozi Oyen (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Jestas Nyamanga, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Salvatory Mbilinyi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika na Bi. Ramla Hamis, Afisa Mambo ya  Nje.
   
  Prof. Mkenda akiagana na Balozi Oyen

  0 0

  Na. Prisca Libaga-MAELEZO, Arusha.

  Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imezifutia usajili dawa mbalimbali za kutibu magonjwa ya binadamu na kuziondoa kwenye soko pamoja na kusitisha matumizi yake kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa wagonjwa.

  Hayo yameelezwa jana Jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya wakufunzi wa ufuatiliaji juu ya ufundishaji na uhamasishaji wa masuala ya udhibiti wa madhara yatonayo na matumizi ya dawa zisizosalama kwa watendaji wa afya kutoka Wilaya zote za mkoa wa Arusha.

  Bw. Sillo mesema katika kudhibiti matumizi ya dawa zisizofaa TFDA imeondoa dawa ya sindano aina ya Chloramphenical kwenye soko baada ya shirika la afya Duniani WHO, kubaini dawa hiyo ina madhara kwa watumiaji, Pia mamlaka hiyo imefuta usajili wa dawa zingine kama vile Ketoconazole, (vidonge) Phenylpropanalamine,Dextropropoxyphene,Nimesulide,stavudine 40, Gatifloxacin,Rofecoxib, pamoja na Celecoxib baada ya kuthibitika zina madhara kwa watumiaji. 

  Aidha matumizi ya dawa kama vile Kanamycin,Amikacin na Levofloxacin zimebadilishwa ili ziweze kutumika kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa kifua kikuu pekee.

  Mkurugenzi huyo wa TFDA amesema mafunzo hayo yanashirikisha wakufunzi 60 nchini kote na yanafanyika katika mikoa mbalimbali yakiwashirikisha Madaktari, Manesi, na wafamasia walioko kwenye hospitali, vituo vya afya na Zahanati.

  Bw.Sillo alieleza kwamba, lengo la mafunzo hayo ni kuongeza idadi ya wakufunzi wa masuala ya usalama wa dawa kutoka 73 hadi 133 na tayari katika kipindi cha miaka mitatu 2014/ 15 hadi 2017/18, Mamlaka ya chakula na dawa imehamasisha watendaji wa afya wapatao 2000 nchini kote na sasa uhamasishaji unaendelea katika mkoa wa Katavi.

  Alisema mara baada ya mafunzo hayo wakufunzi hao watafundisha wenzao kwenye maeneo yao ya kazi ili kuongeza uelewa kwa wataalam wengi zaidi kufahamu taratibu zilizoko za udhibiti wa madhara yanayotokana na matumizi ya dawa zisizofaa.

  Aliwakumbusha wakufunzi hao kwamba kila mtendaji wa afya ana wajibu wa kulinda afya za wagonjwa anao watibu au kuwahudumia na wajibu huo ni pamoja na kuhakikisha wagonjwa wanabaki salama na ikiwa watapata madhara hatua za kuwatibu zinachukuliwa na kutoa taarifa ili kuzuia kusambazwa zaidi kwa dawa zinazoleta madhara. 

  Bw. Sillo alifafanua kuwa, kumekuwa na baadhi ya wataalam wa afya kudhani kuwa kwa kutoa taarifa kuwa dawa ina madhara inaonekana kuwa wao ndio wanaosababisha madhara hayo na kusisitiza kuwa dhana hiyo sio ya kweli, hivyo akawasisitiza watoe taarifa sahihi ili wananchi wafahamu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa pamoja na hatua za kuchukua. 

  Mamlaka ya chakula na dawa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma wametengeneza mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za usalama na madhara ya dawa ambao ulizinduliwa Oktoba 2016 na Waziri wa afya Mh.Ummy Mwalimu. 

  Kabla ya kuzinduliwa mfumo huo taarifa za usalama na madhara ya dawa zilikuwa zikitolewa kwa kutumia fomu maalumu za njano ,kijani na blue ambapo watoa huduma za afya walikuwa wakitumia fomu za njano huku wagonjwa wakitoa taarifa kwa kutumia fomu za za kijani, na fomu za bluu zilitumika kutoa taarifa za ubora wa dawa na kama kuna dawa duni au bandia kwenye soko.

  0 0


  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisiitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu Kikuu cha Dar es salaam leo Novemba 8, 2017.
  Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Novemba 8, 2017.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Novemba 8, 2017.
  Washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Novemba 8, 2017.

  Na Mathias Canal, Dar es salaam


  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Novemba 8, 2017 amefungua Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lenye dhima ya kujadili masuala muhimu yanayohusiana na PHM na mchango wake katika uhakika wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda nchini Tanzania kwa ajili ya kupunguza upotevu, kuimarisha usalama wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda.


  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa alisema kuwa anataraji kongamano hilo litakuwa na mjadala muhimu kujadili masuala muhimu yanayohusiana na Kuzuia Upotevu wa Mazao kabla na baada ya kuvunwa (PHM).

  Alisema Serikali imeweka msisitizo wa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi na kwa Wabia wa Maendeleo kuwekeza katika eneo hilo la PHM.

  “Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa sekta binafsi itahakikisha mchakato wa kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza upotevu unakuwa shirikishi na unatekelezwa na wadau kwa ufanisi”
  “Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa hili ni tukio kubwa sana kwa Wadau wa Mpango wa kupunguza Upotevu wa Mazao baada ya Kuvunwa (PHM) nchini tangu jitihada za kushughulikia suala hili zianze na kwa sasa suala hili linaanza kueleweka kwa wadau wengi tofauti na uko nyuma ambako msisitizo ulikuwa juu ya uzalishaji na tija” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
  Alisema, Kulingana na takwimu zilizopo bado kuna upotevu mkubwa wa mazao ya chakula ambao unafikia wastani wa asilimia 30 mpaka 40 kwa mazao ya nafaka na mikunde na kwa wastani wa asilimia 50 kwa mazao ya mboga na matunda.

  Alisema ili kupunguza upotevu wa mazao ni muhimu sana na ni mkakati mzuri wa kuihakikishia nchi usalama wa chakula na lishe. Kuwepo kwa chakula cha kutosha katika Taifa na katika ngazi ya kaya ni msingi wa Taifa lenye uchumi imara, watu wenye afya nzuri na amani. Alisema kuwa jitihada za kushughulikia UPOTEVU WA MAZAO BAADA YA KUVUNWA zilianza miaka ya 1980 baada ya kujitokeza kwa wadudu waharibifu wa mazao wajulikanao kama Dumuzi ambao walisababisha upotevu mkubwa wa mazao na kuhatarisha uhakika wa chakula nchini Tanzania.

  Aliongeza kuwa Kuanzia wakati huo mabadiliko ya kisera katika sekta ya kilimo yalianza kujitokeza kupitia Serikali ya Tanzania hasa madiliko yanayolenga kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa. Sambamba na hayo pia alisema kuwa jitihada nyingi nchini Tanzania za kupunguza upotevu wa mazao zimefanyika zikiwemo Kujenga maghala kupitia Miradi mbalimbali, Kuanzishwa Kitengo cha Hifadhi na Usindikaji wa Mazao, chini ya Idara ya Usalama wa Chakula na jukwaa la wadau (TPMP), Kuanzishwa kwa mashirika ya kubuni teknolojia mbali mbali zinazohusiana na PHM kama vile SIDO, CAMARTEC, Kuigizwa kwa masuala ya PHM kwenye Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), na Kuanzishwa kwa miradi na juhudi mbalimbali zinazohusu PHM kama vile MIVARF, GPLP, COWABAMA.

  Mhe Mwanjelwa alibainisha kuwa jitihada zote hizo hazikufanikiwa vizuri kwa sababu ya kukosa mfumo mzuri wa kuratibu kazi zote PHM zilizotekelezwa na wadau mbalimbali matokeo yake kukajitokeza wadau kutekeleza kazi zinazofanana bila kujuana na maeneo mengine hayakushughulikiwa kikamilifu. Hali hii ili sababisha matumizi mabaya ya rasilima na kushindwa kuwa na mipango madhubuti ya kutekeleza shughuli za maendeleo. 

  Aidha, aliwataarifa kuwa maandalizi ya Mkakati wa Kuzuia Upotevu wa Taifa yako hatua za mwisho ambapo Mkakati huo utaunganisha wadau wote wanaojishughulisha na kazi za kupunguza au kuzuia upotevu wa mazao ya chakula.

  “Ni Imani yangu kama mkakati huo utatekelezwa kikamilifu upotevu wa mazao utapungua kufikia wastani wa asilimia 5 nchini Tanzania” Alisisitiza Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa.Ksatika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa alilipongeza jukwaa la wadau (TPMP) kwa kushirikiana vizuri na Wizara ya Kilimo, HELVETAS, Swiss Inter-cooperation-Tanzania, ANSAF na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa maandalizi ya kongamano hilo.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Zungu akisoma dua ya kuiombea nchi na Bunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye ulemavu akiwasilisha Taarifa ya Mwaka ya Chuo kikuu cha Dodoma kwa mwaka 2015/2016 kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Dk.Christine Ishengoma akiuliza swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe.Joseph Kakunda akitolea ufafanuzi maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Nchemba Mhe. Juma Nkamia wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugora akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mhe.Subira Mgalu akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Juma Aweso akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalah Ulega akiotolea ufafanuzi maswali ya wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.

older | 1 | .... | 1421 | 1422 | (Page 1423) | 1424 | 1425 | .... | 1903 | newer