Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi  Mtendaji wa FERUSCO Sustainable Development,Bw. Felisi Ngonyani mbele mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.2 wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo katika mikoa ya kanda ya ziwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng’i Issa  wapili kulia, Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa tatu kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na Mbunge, Bw. Joseph Musukuma kulia na Meneja Tawi  TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama  wa tatu kulia akimkabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi wa Mtandao wa ViVOBA Endelevu (Visudent) Kamara Mohamed kulia, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa wa pili kulia, Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa watu kushoto, Meneja Tawi  TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto. 
Wanachama wa Vikundi vya VICOBA wakiwa katika uzinduz wa utoaji wa mikopo ya uwezeshaji ambapo vikundi 272 vilipata mikopo toka Benki Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance Chini ya Udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), 

Vikundi vya VICOBA 272 vya mikoa ya Kanda ya Ziwa vimenufaika na uwezeshaji wa mikopo ya Tsh. bilioni 2. 8 toka Benki ya Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance PLC ili wanachama wake waweze kuitumia katika shughuli za ujasiriamali na kushiriki katika uchumi wa taifa lao.

Vikundi vya VICOBA vilivyo nufaika na mikopo hii vinatoka katika Wilaya au halmashauri za Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara kwa lengo la kuviwezesha viweze kushiriki katika kuondoa umasikini miongoni mwa wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo hiyo mkoani Geita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama alisema mkopo huo ni sehemu ya Uwezeshaji wananchi kupitia vikundi vya ViCOBA ili waanzishe au waimarishe miradi yao ya ujasiriamali.

 ‘’Huu ni uwezeshaji Mkubwa na tunataka mkatumie fedha hizi kuendeleza miradi yenu ya ujasiriamali ili ikazalishe na muweze kuondokana na hali duni ya vipato,” na hiyo pia itawasaidia kushiriki katika uchumi wa nchi,aliongeza kusema,Bi Mhagama.

Mikopo hiyo imetolewa na TPB na UTT Microfinance PLC chini ya udhamini wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Akifafanua zaidi alisema TPB ilitoa Tsh.bilioni 2.7 kwa vikundi 228 na UTT Microfinance imetoa Tsh.milioni  100, 300,00 kwa vikundi viwili vyenye wanachama 30.

Pia alizitaka taasisi zote za kifedha hapa nchi kuanza kwenda katika wilaya au halmashauri kutoa huduma za kifedha kama mikopo ilia wananchi waweze kuzitumia katika mirdi yaujasiriamali.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Bi. Beng’i Issa alisema mikopo hiyo imedhaminiwa na baraza kupitia mfuko wa taifa wa uwezeshajii wananchi kiuchumi imetolewa kwa masharti nafuu na ni mwendelezo wa udhamini inaoufanywa ili mikopo itolewe kwa wajasiriamali kupitia SACCOS na VICOBA.

“Vikundi hivi ni matunda ya taasisi mwanvuli  zilizokubali kushirikiana na serikali kuvianzisha na kufundisha elimu ya VICOBA,” serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hizi katika kazi ya kuzidi kuwawezesha wananchi aliongeza kusema

Alizitaja taasisi hizo mwamvuliza za VICOBA ni pamoja na Peoples Long Life Initiative (PLI), Ferusco Organisation VICOBA Sustainable Development Agency (FOVSDA), Upepo Wetu na VICOBA Sustainable Development Nertwork VISUDENT.

Kwa Mujibu wa Bi. Issa ni kwamba taasisi hizo mwanvuli pia zitahusika katika kusimamia maresjesho ya mikopo ya vikundi ili kuhakikisha zinarudi kwa wakati na vikundi vingine viweze kupata.

Alisema serikali kwa sasa imejielekeza katika kufikia uchumi wa viwanda na viwanda na  uwezeshaji huo unalenga wananchi wananzishe au kukuza viwanda vidogo vidogo ili mazao ya hapa nchini yaweze kuongezewa tham ani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi alisema mikopo niyo ni ya kujivunia na yenye manufaa makubwa katika kukuza vipato vya wananchi kuondokana na umasikini katika kanda hiyo.

Serikali inafanya kazi kubwa ya kuweka mazingira wezeshi na kuibua fursa na serikali za mikoa ya kanda yetu tutahakikisha mikopo hii inaleta tija,” Wanachama wa vikundi hivyo wanafanya shughuli mbalimbali za kijasiriamali, aliongeza Kusema,Bw. Lughumbi.

Baraza hilo la Taifa linafanya kazi chini ya sheria uwezeshaji namba 16 ya mwaka 2004 na limedhamiria kuhakikisha uwezeshaji huo unawakomboa wananchi kiuchumi.

Tamasha kubwa la Tigo Fiesta lakutanisha maelfu ya wakazi wa Morogoro

$
0
0

Wasanii Ben Pol na Jux wakishirikiana kuimba wimbo wao NAKUCHANA kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi.

Country Boy akiimba na maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha la Tigo Fiesta 

Rich Mavoko akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta mkoani Morogoro mapema usiku wa kuamkia jumatatu.

MimiMars akiimba katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jumatatu mkoani Morogoro.


Barnaba akitumbuiza kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta mkoani Morogoro.

NedyMusic aktumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta mapema juzi katika viwanja vya Jamhuri mkoani Dodoma.

Nandy akiburudisha wakazi wa Morogoro katika Tamasha la Tigo fiesta mapema juzi katika viwanja vya Jamhuri

Madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani hawavumiliki kuendelea kumiliki leseni-Muslim

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim amesema kuwa madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani, hatawavumilia kuendelea kumiliki leseni walizozipata.

Muslimu aliyasema hayo wakati alipokutana na vyama vya madereva jijini Dar es Salaam, amesema madereva lazima wafuate sheria za usalama bila kufanya hivyo leseni zao zitafutwa.

Amesema udereva ni kazi zilivyo kazi zingine hivyo lazima kazi hiyo iheshimike kwa kufuata sheria za usalama barabarani barabarani kutokana na asilimia 80 ya uchumi inabebwa na madereva hao.

Kamanda Muslim amesema ameomba majina ya madereva kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambao wanachezea vidhibiti mwendo ili aweze kufunga leseni za madereva wanaofanya mchezo huo.

Nae Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, SACP Johansen Kahatano amesema kuwa kazi ya madereva kupandisha nauli sio kazi yao kwani wanaotakiwa ni wamiliki kupeleka maombi Sumatra juu ya gharama za uendeshaji,Kahatano amesema suala la madereva kulalamikia mikataba ya ajira haliko kwao na badala yake kazi hiyo itafanywa na idara ya ajira ambao ndio wanaweza kujua juu mikataba ya maderva jinsi itavyokuwa.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim akizungumza katika mkutano wa vyama vya madereva juu kufuata sheria za usalama barabarani, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, SACP Johansen Kahatano akizungumza na madereva jinsi Sumatra inavyofanya kazi katika kuhakikisha huduma za usafiri zinatolewa bila mwananchi kupata kikwazo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi ya Mikoani, Ibrahim Samwix akionyesha jinsi ya ajali katika picha hazipo pichani katika mkutano wa madereva jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya madereva waliofika katika Mkutano na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
.Picha ya Basi iliyoacha barabara na kutokana na spidi.
Basi likiwa na spidi 106 ambapo ni makosa ya usalama barabarani

Pan African Energy yatoa Sh 85 milioni kama ufadhili wa Chuo vikuu kwa wanafunzi kutoka kisiwa cha Songo Songo

$
0
0
Kampuni ya uchimbaji, uchakatuaji na uuzaji wa gesi asilia, Pan African Energy Tanzania Ltd, imetoa kiasi cha sh 85.1 milioni kwa ajili ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi watano wanojiunga na vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.


Fedha hizo ni mwendelezo wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi hao kutoka katika Kisiwa cha Songo Songo,iliyoanza nao tangu kidato cha kwanza hadi cha sita na hatimaye chuo kikuu.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, Meneja Uwajibikaji wa Kijamii, Andrew Kashangaki amesema ufadhili huo una lengo la kuwawezesha vijana kielimu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali.


“Miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ni elimu na sisi katika kuunga mkono juhudi hizo tumeona tuanze na wanafunzi katika ngazi ya chini na kwenda nao hadi chuo kikuu,” amesema Kashangaki.


Kashangaki amefafanua kuwa kigezo cha wanfunzi hao ilikuwa ni kufaulu mtihani wa darasa la saba, ambapo katika wengi waliofauu waliwachukua 10 aliopata alama za juu na kuwalipia kusoma katika Shule ya Sekondari Makongo  jijina Dar es Salaam, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.


Amesema kadri walivyokuwa wanaendelea na masomo walikuwa wanapungua hivyo waliofanikiwa kuingia kidato cha sita walikuwa nane


-->

WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Mwaka wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb), akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Mwaka wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitambulisha washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2017 unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma na kujumuisha Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Taifa, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Mitaa na wawakilishi kutoka Sekta na Mashirika mbalimbali nchini.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Elimu Bw. Tikson Nzunda akifafanua neno wakati wa Mkutano MKuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2017 unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma kuhusu umuhimu wa kuwatumia wataalamu wa Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yao.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akitambulisha malengo ya Mkutano Mkuu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii 2017 na kumkaribisha Mgeni rasmi Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb) akisisitiza maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kuelekea uchumi wa Viwanda wakati akifungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Mandeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
 Baadhi ya Maaafisa Maendeleo ya Jamii wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb)(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.  
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI mara baada ya kufungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Mjini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb) (katikati) akijadiliana jambo na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Elimu Bw. Tikson Nzunda (kulia) mara baada ya kufungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Mjini Dodoma kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali imewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kurejesha ari na hamasa ya jamii kushiriki katika kazi za maendeleo ili kutoa mchango katika kufikia Tanzania ya Viwanda na yenye uchumi wa kati.

Kauli hii imetolewa MJini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 12 wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unafoanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Mhe. Ummy Mwalimu  amesema kuwa kupitia Mkutano huo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa  kutoa  mapendekezo kuhusu mbinu bora zitakazosaidia kurudisha ari na hamasa ya jamii kushiriki katika maendeleo na hivyo kusaidia kufikia uchumi  wa kati na wa viwanda.

Mhe. Ummy Mwalimu amefafanua kuwa wataalam wa maendeleo ya jamii ndiyo wenye jukumu la kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya kisekta hususan kilimo, afya, elimu, na miundo mbinu na kadhalika.

“Wataalam wa  Maendeleo ya Jamii watumie fursa hii kujitathmini ili kupata majibu ya namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki kwenye uzalishaji na kutokomeza ukatili wa jinsia ambao unapunguza kasi ya kufikia uchumi wa kati na maendeleo jumuishi” alisema Mhe. Ummy.

Waziri Ummy ameeleza kuwa Kaulimbiu ya Mkutano wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa Mwaka 2017  ambayo ni  “Amsha Ari ya Ushiriki wa Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda” inatafsiri azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa na Tanzania ya Viwanda ili kufikia uchumi wa kati. 
     
Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa katika awamu ya sasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wana wajibu wa kuelimisha na kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za uzalishaji kwa bidii kwa kuzalisha mali ghafi zinazohitajika na viwanda na kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Bibi Sihaba Nkinga amefafanua kuwa malengo ya Mkutano huo umezingatia  tathmini ya mchango wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii katika kuamsha  ari na hamasa ya wananchi kushiriki na kuchangia maendeleo kwa kushirikiana na viongozi wa Sekta na Idara nyingine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amewaasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na wadau  kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujitoa katika kufanya kazi za kujiletea maendeleo katika maeneo yao.

Lengo la Mkutano huu wenye kauli mbiu isemayo “Amsha Ari ya Ushiriki wa Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda” ni kuhakikisha Wizara na wadau wanashirikiana katika kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za maendeleo na kusimamia Mpango ya kutokomeza ukatili wa jinsia ambao kwa kikasi kikubwa unapunguza kasi ya Taifa kufikia uchumi wa viwanda.

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA UJENZI,MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongozaa kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017,   cha Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji  kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
 Wakurugenzi wa Idara zilizokatika Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji  wakiwa kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017, kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
 Waziri wa  Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Balozi Ali Abeid Karume (katikati) alipowasilisha Muhtasari wa  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017, wakati wa kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wengine ni  Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa BLM Nd,Salum Maulid Salum(kulia) na Naibu wa Wizara hiyo Mhe.Mohamed Ahmed Salum
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar Bi.Riziki Jecha Salim (kulia) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu Idara yake wakati wa kikao cha siku moja  Uongozi wa Wizara hiyo cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017,kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Katibu Mkuu wa  Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa BLM,pia Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi  Nd,Salum Maulid Salum (wa pili kulia) alipokuwa akichangia wakati wa  kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017,   cha Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji  kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia),akiwepo na Waziri Balozi Ali Abeid Karume na Naibu wake Mohamed Ahmed Salum (kushoto).(Picha na Ikulu).

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ulioanza leo tarehe 6 na unatarajiwa kumalizika tarehe 8 november, katika ukumbi wa APC Bunju, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya mashine ya kuchora kadi za mifumo ya umeme inavyofanya kazi na Mhandisi Vedastus Sichilima kutoka D.I.T (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo amefungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi. Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya APC Bunju wilayani Kinondoni, umeandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikianana Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ya nchini Finland. 

Akihutubia washiriki katika Mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “wekeza katika elimu ya ufundi na mafunzo kwa Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda” Makamu wa Rais alisema kaulimbiu hiyo inaenda sambamba na agenda ya serikali ya kutekeleza dira ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025. “Ni dhahiri kuwa elimu ya ufundi ni nguzo muhimu ya kufikia agenda ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025” alisisitiza Makamu wa Rais

Makamu wa Rais alisema amefarijika kuona kuwa Mkutano huo umepambwa na magwiji wote kutoka taasisi na vyuo vya elimu ya ufundi pamoja na wadau wote wa utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo. Aidha, alisisitiza kuwa anatambua kuwa kutoa elimu ya ufundi ni mkakati muhimu sana utakaosaidia kubadili fikra na mitazamo ya raia walioelimika na kuwa mahiri katika stadi na maarifa ya kutosha kusaidia kukabiliana na changamoto za maendeleo ya nchi yetu.

Sambamba na hilo, Makamu wa Rais aliwapongeza waajiri waliojitokeza katika mkutano huo na kuwaasa kwamba wao ni kiungo muhimu sana katika kuleta maana halisi ya mkutano huo. Makamu wa Rais alisema ili kuzalisha na kuendeleza rasilimali watu bora katika kada ya kati ni lazima kuwepo mahusiano mazuri baina ya taasisi zinazotoa mafunzo ya ufundi na waajiri. Mahusiano hayo ndiyo yatakayozalisha wataalam bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Akizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini, Makamu wa Rais alisema ni pamoja na kutokuwepo kwa muunganiko wa kutosha kati ya taasisi zinazotoa elimu na mafunzo ya ufundi na waajiri kama vile viwanda, mabenki, taasisi za afya na vyombo vya habari. Aidha, upo uelewa mdogo miongoni mwa wadau na jamii kwamba elimu ya ufundi inahusu masuala ya useremala, uashi, ufundi makenika, kushona nguo na mambo yanayofanana na hayo. Pamoja na hayo upungufu wa miundombinu stahiki katika vyuo vya ufundi ili kutoa mafunzo yenye viwango vya ubora wa hali ya juu nayo ni changamoto.

Makamu wa Rais alisema wakati nchi inaelekea kwenye uchumi wa Viwanda, hatuna budi kujipana kuandaa wataalamu wa kutosha hivyo Serikali imeelekeza Baraza kuanda, kupitia upya na kuboresha Mitaala kwenye maeneo muhimu ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa utoaji wa Elimu ya Ufundi inayojibu matatizo ya jamii, inayoandaa vijana wenye umahiri wa kuweza kupambana na changamoto za maendeleo katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia.

Mwisho Makamu wa Rais alisema kuwa ni matarajio yake Mkutano huu utatoa maazimio na ufumbuzi wa namna ya kukabiliana na changamoto za utoaji wa Elimu ya ufundi na kuishauri Serikali ipasavyo juu ya hatua za kuchukua ili elimu itolewayo iendane na mahitaji ya Soko la ajira.

Makamu wa Rais aliwashukuru na kuwapongeza Taasisi ya Elimu ya watu Wazima ya Finland kwa kushirikiana na NACTE katika kuandaa mkutano huo .

Aidha aliwapongeza Jamhuri ya Watu wa Finland kwa kuadhimisha miaka 100 ya uhuru.

AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI

$
0
0
mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za kupandisha ngazi ya rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo (habari picha na woindeshizza blog )
Mbunge akiwa na wananchi waliouthuria katika sherehe hizo
Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rrika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo.


Wazazi hususa ni jamii ya kimasai wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike na wale ambao ni walemavu badala yake wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae.

Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi katika sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha

Alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni walemavu jambo ambalo linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu kutokana na kufichwa huko

“kwakweli wazazi wanavyoficha watoto wao hususa ni walemavu wanawanyima haki yao mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa kiongozi hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapo maliza shule wanakuja kuwasaidia “alisema Amina

Aidha pia aliwataka wazazi hawa wa jamii ya kimasai na hata wale wa makabila mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto hao wakike nao wanahaki ya kupata elimu kwani elimu ni bure ,kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo ni vyema kama wazazi wakawasimamia watoto hususa ni wakike wakaenda shule

Aliongeza kwa kuwasihihi watoto wa kike kuweka kipaumbele swala la elimu kwani elimu ndio kila kitu katika maisha yao na iwapo watasoma kwa bidii wanaweza kuwa viongozi wakubwa wa serikalini hapo baadae

Alisema kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha kusoma kisa wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza kukimbilia maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza alafu maisha watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri

TAARIFA KUTOKA BODI YA MIKOPO(HESLB) KUHUSU UFAFANUZI KUHUSU SIFA NA TAKWIMU ZA UTOAJI MIKOPO KWA 2017-2018

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu sifa na taratibu za utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018. Taarifa hii inalenga kutoa ufafanuzi kufuatia maoni ya baadhi ya wadau kuwa baadhi ya waombaji mikopo wenye sifa wanakosa mikopo ya elimu ya juu.
i.Uyatima: Waombaji ambao wamefiwa na wazazi na hivyo kushindwa kumudu gharama za elimu ya juu. Kwa mwaka huu, waombaji yatima wanapaswa kuthibitisha uyatima wao kwa kuwasilisha vyeti vya vifo vya wazazi wao vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);

ii.Wenye ulemavu: Waombaji wa mikopo wenye ulemavu wanapaswa kuambatisha barua kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa inayothibitisha ulemavu huo;

iii.Uduni wa kipato: Waombaji ambao wanatoka kwenye familia zenye vipato duni, miongoni mwao wakiwamo wale wenye barua za uthibitisho kuwa waliosomeshwa kwenye masomo yao kabla ya kujiunga na elimu ya juu;

Pamoja na sifa/vigezo hivi, kila mwombaji ni lazima awe amepata udahili au kuthibitisha udahili katika taasisi moja ya elimu ya juu ambayo atajiunga kwa ajili ya masomo na asiwe na umri wa zaidi ya miaka 30.Aidha, tunapenda kufafanua kuhusu takwimu za utoaji mikopo kwa mwaka 2017/2018 kama ifuatavyo:

i.Bajeti ya jumla ya mikopo kwa mwaka 2017/2018 ni TZS 427.54 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 122,623. Fedha hizi zinajumuisha malipo ya ada za wanafunzi wenye mikopo pamoja na fedha za chakula na malazi, vitabu n.k;
ii.Fedha zinazohitajika kwa malipo kwa ajili ya Robo ya Kwanza ya mwaka 2017/2018 ni TZS 147.06 bilioni ambazo tayari Bodi imeshapokea kutoka Serikalini;
iii.Hadi leo, Novemba 6, 2017, jumla ya wanafunzi 29,578 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 96.5 bilioni na fedha zao tayari zimeshatumwa vyuoni ili kuwawezesha kuanza masomo;
iv.Aidha, fedha za mikopo ya wanafunzi wote wanaoendelea na masomo zimetumwa vyuoni ili kuwawezesha kuendelea na masomo.
Kufunguliwa kwa dirisha la rufaa.

Tunapenda pia kuwajulisha waombaji wa mikopo wote kuwa dirisha la rufaa litafunguliwa Jumatatu, Novemba 13, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili. Maelezo ya kina yatatolewa kupitia tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).

Tunatoa wito kwa uongozi wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafuzi na kuwasilisha kwa Bodi ya Mikopo. Lengo ni kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa rufaa zao ifikapo Novemba 30, 2017.

Imetolewa na:

Abdul-Razaq Badru
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Novemba 6, 2017

RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA WAKURUGENZI WAWILI BUKOBA MKOANI KAGERA JIONI YA LEO

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHATOA SOMO KWA LABOUR PARTY UINGEREZA

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewakilishwa nchini Uingereza na Ndg. Ngemela Lubinga Katibu wa NEC Mwenye dhamana ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Ndugu Lubinga ameongoza ujumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano Mkuu wa Chama rafiki cha Labour. Katika Mkutano huo Chama cha Labour kimeweka mikakati ya kurejesha Chama hicho katika kushika hatamu ya uongozi nchini Uingereza.

Akiwakilisha salamu za Comrade John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM katika Mkutano huo Ndg. Lubinga amesisitiza, …ni lazima vyama rafiki na hasa vyenye mrengo wa kijamaa kusimama pamoja katika kuhakikisha usawa na haki inapokuja katika uvunaji wa rasilimali madini hasa katika nchi za Afrika.

Katika mazungumzo yake na Viongozi waandamizi wa labour Ndg. Lubinga amewahakikishia mahusiano ya kidugu ambayo yamejengwa kwa muda mrefu kati ya vyama hivi viwili, CCM itaendelea kuyaenzi.

Aidha Ndg. Ngemela Lubinga alijulisha viongozi hao kuwa CCM inaendelea kufanya Mageuzi Makubwa ambayo lengo lake ni kurejesha Chama chetu katika misingi yake, kuuimarisha kwa vitendo uhalisia kwamba CCM ni Chama Cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu. Kama sehemu ya Mageuzi haya ndani ya Chama na katika Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeielekeza Serikali kutoa elimu bure kutoka darasa la kwanza mpaka kidato cha nne na kuongeza maradufu mikopo kwa wanafunzi wote wenye uhitaji wanaosoma katika Vyuo Vikuu nchini alisema Ndg. Lubinga.

Akihitimisha salamu za CCM katika Mkutano huo Mkuu wa Chama Cha Labour, Ndg. Lubinga Amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha labour kuweka maslahi ya umma mbele na kushughulika na changamoto zao ikiwemo mahusiano ya Nchi ya Uingereza na Jumuiya ya Ulaya.

Nao viongozi wa Chama Cha Labour wamepongeza jitihada za Serikali ya CCM awamu ya Tano Chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwa madhubuti katika vita dhidi ya rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na kutetea haki ya watanzania katika rasilimali madini.

Ziara hii ya Ndg. Lubinga Nchini Uingereza ni muendelezo wa diplomasia ya Siasa na ujenzi wa mahusiano mema na vyama rafiki.

Imeandaliwa na Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Imetolewa na,

*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*
Novemba 6, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AKIFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wa pili kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi hao mara baada ya ufunguzi wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuashiria ufunguzi wa wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kukagua chumba cha abiria uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Dini mara baada ya ufunguzi wa uwanja huo wa Ndege.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na kumshukuru Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya shughuli za ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.
Wananchi wakishangilia wakati wa Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi huo wa uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

HOTUBA YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOKUWA AKIFUNGUA UWANJA WA NDEGE MJINI BUKOBA

UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUAGIZA CHAKULA UKIWA HAPO ULIPO?

$
0
0
Na Jumia Food Tanzania

Katika maisha ya sasa yenye pilikapilika takribani siku nzima, muda umekuwa ni bidhaa adimu na kitu ambacho kinazingatiwa sana. Si jambo la kushangaza kujikuta unapitiwa mpaka kufika saa kumi za jioni haujatia kitu chochote tumboni huku muda ukiwa hauko upande wako tena.

Lazima tukubaliane na uhalisia kwamba kuna wakati muda unakuwa sio rafiki ili kuendana na majukumu tuliyonayo, ukizingatia wengi wetu tukifanya kazi kwa waajiriwa ambao hutulipa kulingana na muda tunaotumia kazini. Ili kukabiliana na changamoto kama hii unahitaji mbadala wa kukufanya uendelee na shughuli zako za siku bila ya kuhofia kupoteza muda na kuhatarisha kazi yako.

Kutokana na maendeleo ya tekinolojia duniani hususani mtandao wa intaneti, hivi sasa kuna mfumo unaokuwezesha ukaagiza chakula na kukufikia papo hapo ulipo. Hii inamaanisha kwamba kama vile unavyokwenda kwenye mgahawa unaoupenda au kuuzoea, ukatazama orodha ya vyakula vilivyopo, bei zake na kuagiza chakula ukipendacho ndivyo Jumia Food inavyofanya.

Ikiwa na orodha ya takribani migahawa 70 tofauti yenye aina ya vyakula mbalimbali jijini Dar es Salaam, Jumia Food inawakutanisha wateja na watoa huduma kwa kuwarahisishia kuagiza chakula kwa urahisi na kuwafikia ndani ya muda mfupi popote pale walipo. Mtu anaweza kuwa anajiuliza kwamba atakuwa na uhakika gani kuwa chakula atachokiagiza kitakuja kama vile alivyotarajia?
Jibu ni rahisi. Tunafahamu kwamba kwa watanzania walio wengi bado ni wageni na huduma za mitandaoni kwa sababu huwa tunapenda kufanya maamuzi ya kufanya manunuzi juu ya bidhaa fulani mpaka tuione, kuigusa pengine kuijaribu. Lakini linapokuja suala la chakula watu wengi huwa wanafahamu mahali wanapopendelea kula, chakula wanachokipendelea, ladha pamoja na bei yake.

Hivyo basi kama mtu unakuwa unafahamu chakula ukipendacho kinapatikana mgahawa fulani kwanini usiagize na ukaletewa pale ulipo?
Sio kila siku utakuwa na muda wa kutosha wa kukufanya ukatoka kazini na kwenda nje kula. Na haimaanishi kwamba ukikosa muda wa kutoka nje basi ndio usipate fursa ya kula. Jumia Food imeliona hilo na kwa muda mrefu sasa na kuamua kuja na mfumo ambao utakuwa ni msaada kwako huku wewe ukiendelea na shughuli zako.

Kwa hiyo kama upo kazini na unafahamu kwamba umetingwa na kazi ambazo zinaweza kukupelekea ukakosa muda wa kwenda kupata chakula usiwaze. Kwa sababu unaweza ukatenga muda mfupi, nusu saa au saa moja kabla, kwa kuingia kwenye mtandao wao aidha kwa njia ya kompyuta, tabiti au simu yako ya mkononi na kuagiza chakula ukipendacho kutoka kwa mgahawa uupendao kisha ukaendelea na shughuli zako.

Kwa mfano, unaweza kuwa upo ofisini maeneo ya Posta, umetingwa na kazi au mvua imenyesha na muda wa kupata chakula cha mchana unakaribia na haufahamu utatoka vipi. Cha kufanya ni rahisi, ingia kwenye tovuti yao na kisha weka eneo ulilopo na kisha utaona migahawa yote iliyokaribu nawe inajitokeza kama vile Marrybrown au Rhapsody’s.

Lakini pia mfumo huu unakupatia fursa ya kujaribu vyakula vingine tofauti kutoka kwenye migahawa tofuati iliyo karibu nawe. Kwani unao uwezo wa kuperuzi kwenye tovuti na kujionea vyakula vilivyopo na gharama zao badala ya kutembelea mmoja baada ya mwingine au kwenda kula bila ya kujua gharama zao.
Mbali na mfumo huu kuwa na faida kubwa kwa wateja lakini pia una manufaa kwa wamiliki wa migahawa pia. Kupitia mfumo huu wamiliki wa migahawa hujipatia idadi kubwa ya wateja kutoka kila mahali ambao sio lazima wafike pale moja kwa moja. Hivyo basi kama mgahawa unatoa huduma ya vyakula vitamu na hauna sehemu ya kutosha kuwahudumia wote basi inaweza kuwafikishia chakula popote walipo. Ni rahisi kujiunga na haigharimu gharama yoyote.

Katika zama tulizopo sasa ambapo wengi wetu tunalipwa kulingana na muda tunaotumia kufanya kazi hatuna budi kuwa makini sana. Makampuni na taasisi nyingi hutoa muda wa saa moja kwa wafanyakazi wao kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Muda huo kama ukiugawa kwa makini kwenda kutafuta chakula, kula chakula, kupumzika kidogo na kisha kurudi kazini, utakugundua kwamba watu wengi hutumia takribani dakika 20 mpaka 30 kula huku zingine zikipotea njiani kwenda na kurudi kufuata chakula.

DK. KIGWANGALLA, "SIWEZI KUJARIBIWA NA SIWEZI KUCHEZEWA, SIKO HAPA KWA BAHATI MBAYA"

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hamdun Mansur (katikati) na Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Ndugu Bajuta wakisoma ramani ya Pori Tengefu Loliondo na mpaka wake na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuaza ziara ya kukagua maeneo hayo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana, pamoja na mambo mengine alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa kwa tuhuma za rushwa na kuhujumu jitihada halali za Serikali za kumaliza mgogoro huo. Aliagiza Mkurugenzi huyo afikishwe TAKUKURU kwa uchunguzi wa tuhuma hizo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana.
Dk. Kigwangalla (kulia) akimuhoji mmoja ya wananchi jamii ya wafugaji alipotembelea Pori Tengefu Loliondo jana.
Waziri Kigwangalla (kushoto) akioneshwa  mpaka wa Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tegefu Loliondo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hamdun Mansuri wakati wa ziara yake ya kukagua iwapo mifugo inaingizwa katika hifadhi ya Serengeti kama ilivyoripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari. 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 7,2017

TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA

$
0
0
 Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Angelina Kwinga mbegu ya mihogo inayostahimili ukame katika uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu hiyo ya mihogo, mahindi aina ya Wema 2109  pamoja na viazi lishe yalioanzishwa kwa ajili ya wakulima wa vijiji nane katika wilaya hiyo leo kwa ufadhili wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana  OFAB.



 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ugalla, Geofrey Magambo akizungumza katika uzinduzi huo wakati akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa Kata hiyo na Kijiji cha Isongwa.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza kwenye uzinduzi darasa wa shamba la mahindi katika Kijiji cha Isongwa kilichopo Kata ya Ugalla Ussoke wilayani Urambo mkoani Tabora.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akikabidhiwa mbegu ya mahindi ya Wema na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa.
 Wananchi wa Kijiji cha Isongwa wakisubiri kupata mafunzo ya upandaji wa mbegu ya mahindi katika shamba darasa.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro akitoa maelezo kwa wakulima wa Kijiji cha Isongwa jinsi ya kupanda mahindi aina ya Wema.
 Mkulima wa Kijiji cha Isongwa, Malando Malando akiuliza swali.
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni akiuliza swali.
 Wanawake wakulima wa Kijiji cha Isongwa wakijumuika kwenye uzinduzi huo wakiwa na watoto wao.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha uchimbaji wa mashimo kabla ya kupanda mbegu hiyo ya mahindi.
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni , akichimba mashimo.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha, akionesha namna ya kuweka mbolea kwenye mashimo yaliyochimbwa.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akipanda mahindi.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akipanda mahindi.



 Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi, akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi huo.
 Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Usisya namna ya kupanda mbegu ya viazi lishe.
 Wakulima wa Kijiji cha Kapiluka wakijiandaa kupanda mbegu ya viazi lishe.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Motomoto namna ya kupanda mbegu ya viazi lishe.

Na Dotto Mwaibale, Urambo Tabora

TAFITI za kilimo zinazofanywa hapa nchini na wataalamu zimewafikia wakulima wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109 na mihogo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji nane vya Isongwa, Ussoke, Usisya, Kapiluka, Vumilia, Kamalendi, Muungano na Songambele.

Alisema mara nyingi tafiti zilizokuwa zikifanyika zilikuwa zikibaki kwenye makabati bila ya kuwafikia walengwa na jambo lililofanywa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kuwafikishia wakulima matokeo ya tafiti hizo ni jambo zuri na limefurahiwa na kwa hapa kwetu ni mara ya kwanza kutokea.

"Tuna amini kuwa hivi sasa uchumi utastawi kuanzia ngazi ya familia, wilaya na hadi taifa na tutakuwa na chakula cha kutosha" alisema Malunkwi.

Malunkwi alisema katika wilaya hiyo walikuwa na changamoto kubwa ya kupata mbegu bora kwani wakulima wengi walikuwa wakitumia mbegu za zamani walizozizoea na kujikuta wakipata mazao kiduchu lakini kwa ujio wa mbegu hizo ni ukombozi mkubwa kwao.

Alitaja changamoto nyingine ambayo inapaswa kuangaliwa kwa karibu kuwa ni bei kubwa ya mbegu hiyo ya mahindi ambayo inauzwa shilingi 12,000 kwa kilo mbili huku kukiwa na debe moja la mahindi linalouzwa shilingi 10,000 ambalo wakulima wamekuwa wakilikimbilia kutokana na bei yake kuwa ya chini ingawa mazao yake hayana tija.

Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hiyo ya mahindi imefanyiwa utafiti na inavumilia ukame wakati ile ya mihogo ikivumilia magonjwa kama batobato na michirizi kahawia huku zikitoa mavuno mengi.

Alisema COSTECH katika mkoa huo imetoa kilo 60 za mbegu ya Wema, mihogo 40,000 na viazi lishe 75 ambapo katika wilaya hiyo vijiji nane vimenufaika kwa ajili ya kutengeneza mashamba darasa ambayo yatatoa mbegu zitakazosambazwa kwa wakulima katika maeneo mengine. 

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba alisema hivi sasa mwajiriwa ni mkulima ambaye analima kilimo chenye tija na si vinginevyo na kuwa serikali siku zote imekuwa ikihimiza kilimo bora ambapo aliwataka maofisa ugani kupanga ratiba za kuwafikia wakulima.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Angelina Kwinga aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kutekeleza ahadi ya kuwapelekea mbegu kama walivyo ahidi walipokuwa wakitoa mafunzo kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mapema mwaka huu.

JAFO: TAARIFA ZA WATUMISHI WALIOAJIRIWA 2058 IMEKAMILIKA.

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) amesema jumla ya watumishi wa Sekta ya Afya wapatao 2058 wamekwisha pangiwa vituo vya kazi kuanzia leo 06/11/2017 na taarifa zote zinapatikana kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Taarifa ya watumishi 2058 imekamilika na itarushwa kwenye mtandao wa OR TAMISEMI leo tarehe 6/11/2017 jioni, hivyo Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wanatakiwa kujiandaa kuwapokea watumishi hao ikiwemo kuwapatia stahiki zao”

Amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waajiri kuhakikisha wanachukua taarifa za watumishi walioripoti na kuwaingiza kwenye Mfumo wa Mishahara na kuwapangia katika maeneo ambayo ya uhitaji mkubwa ili kuboresha huduma za afya nchini.

Pia ameekeza watumishi wanaopangiwa vituo, kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu tangazo hili kutolewa.

Aidha, Waajiri wote watoe taarifa juu ya kuripoti kwa watumishio haa wapya na vituo walivyopangiwa siku 14 baada ya kuripoti kwao. Taarifa za Watumishi hao na Vituo vyao vya kazi, inapatikana katika Mtandao wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) wa www.tamisemi.go.tz

SERIKALI IMETOA BURE MBEGU NA VIUATILIFU KWA AJILI YA KILIMO CHA PAMBA KWA MKOA WA SINGIDA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi mmoja kati ya wa wakulima wa Pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama kilo kumi za mbegu za zao la pamba zilizotolewa bure na Serikali kwa wakulima hao. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga.
 Mkulima wa Pamba Bi Johari kutoka kijiji cha Kinyagiri Wilayani Mkalama akibeba mbegu za Pamba kilo kumi alizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi, mbegu hizo zimetolewa bure kwa wakulima wa Pamba Mkoa wa Singida.
 Mama Devid Mkulima wa Pamba wa Kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama akijifunza kwa vitendo namna ya kuandaa kamba inayotumika kuonyesha vipimo vya upana na urefu katika kupanda pamba badala ya kilimo cha mazoea cha kumwaga mbegu bila kufuata kipimo chochote.
 Wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Lyelembo Wilayani Mkalama wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini Marco Mtunga (hawapo pichani) kabla ya kupewa mbegu za pamba zilizotolewz bure.
 Wakulima wa pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama wakimfuatilia kwa makini mtaalam kutoka Bodi ya Pamba Nchini akiwaelekeza namna ya kupuliza dawa ya kuuwa wadudu waharibifu wa pamba, viuatilifu hivyo vitatolewa bure na serikali kwa wakulima wote wa pamba Mkoani Singida.

Serikali imeahidi kutoa bure pembejeo za kilimo kwa wakulima mbali mbali wa zao la pamba mkoani Singida kuanzia msimu huu wa kilimo ikiwa ni moja ya juhudi za kuhamasisha na kufufua kilimo hicho mkoani hapa.  

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga ameeleza hayo juzi katika vijiji vya Kinyangiri na Lyelembo wilayani Mkalama katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili kuhimiza Kilimo cha pamba mkoani Singida. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Biosustain iliyopo mjini hapa imepewa jukumu la kuleta na kusambaza mbegu na madawa yote yahusuyo kilimo cha pamba bure na kwamba gharama ya pembejeo hizo italipwa na Serikali. 

Kutokana na hilo, Mkurugenzi huyo amewataka Wakulima kutumia vyema fursa hiyo kwa kulima mashamba makubwa zaidi lakini pia kwa kuzingatia tija na ubora wa pamba. Amesema kuwa Wakulima wataweza kufanya hivyo tu iwapo pia watawatumia kikamilifu wataalamu wao wa kilimo na kufuata Kanuni na Taratibu za kilimo bora. 

“Mmepewa upendeleo maalum, kazi yenu sasa ni kulima tu, malipo ya mbegu na viuatilifu vyote italipwa na Serikali. Hapa hakuna kisingizio cha kushindwa kulima”, amesema Mtunga na kuongeza;
“Pandeni vizuri ili wakati mnatumia dawa, kiwango kikubwa cha dawa kisipotee bure maana kama hukupanda kwa mstari lazima kutakuwa na ugumu wa kupulizia mimea yako. Jengeni utamaduni wa kuwatumia wataalamu wa kilimo kama ilivyo kwa wafugaji mifugo yao inapopatwa na maradhi”.  

Aidha, amewataka wakulima wa zao hilo kuhakikisha wanang'oa masalia yote ya misitu ya pamba na kuichoma moto kwa kuwa, kwa kuacha kufanya hivyo wanaruhusu wadudu waliomo kwenye masalia kuendelea kunenepeana na hivyo kuhatarisha mazao mapya yanayopandwa.  

Mkurugenzi huyo amewasihi wakulima kuacha kuchanganya kilimo cha pamba na mazao mengine akisema kuwa tafiti zinaonesha pamba iliyochanganywa na mazao mengine hutoa vitumba vitatu tu ikilinganishwa na vitumba 10 kwa kilimo cha pamba iliyolimwa peke yake. 

Wakulima wa zao hilo wamemueleza Mkurugenzi huyo kuwa, moja ya sababu za kushuka kwa uzalishaji pamba kwenye maeneo yao ni pamoja na bei kuwa ndogo kwa kisingizio cha Soko la Kimatafa kushuka na kuchezewa mizani wanazotumia kupima mazao yao, hali inayowapunja kimapato.  
Hata hivyo, wamejibiwa kuwa suluhisho la kuchezewa mizani lipo mikononi mwao ili mradi tu wajenge tabia ya kuhoji mara moja wanapoona mambo yanaenda isivyo badala ya kusubiri hadi siku ya vikao.

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewataka watendaji wote wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Singida kulima ekari moja ya pamba kila mmoja ili kuamsha hamasa kwa wananchi wengine.

Dkt Nchimbi ameongeza kwa kuwataka watendaji hao kuliweka zao la pamba kama ajenga katika vikao vyao, huku akiwataka viongozi wa dini na vikundi vya kwaya kuonyesha mfano kwa kulima vizuri pamba.
Ameongeza kuwa vijana wanaocheza vijiweni ‘pooltable’ waache mara moja na kujikita katika kilimo cha pamba kwa kuwa ni chanzo kikubwa na cha uhakika cha kujipatia fedha na hivyo kuchangia kukuza uchumi.

Aidha amewataka wakulima wa pamba kuwasikiliza wataalamu na sio kupanda kwa mazoea huku akishauri kuwa mikutano yote inayohusu kilimo cha pamba ifanyike katika mashamba ya wakulima.Dkt Nchimbi ameeleza kuwa kauli mbiu mpya ya kilimo cha pamba kwa Mkoa wa Singida ni, ‘Singida Mpya, kwa Pamba yenye Tija’.

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
  Waziri wa  Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamad Rashid Mohamed (katikati) alipowasilisha Muhtasari wa  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017, wakati wa kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)wengine ni  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa BLM pia Kaimu Katibu Mkuu  Kiongozi Nd,Salum Maulid Salum (kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Nd. Lulu Msham Abdalla.
Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi alipokuwa akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika kikao cha siku moja  cha  Wizara hiyo  kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo p ichani),akiwepo na Naibu Katibu Mkuu Maryam Juma Abdulla Saadalla (kulia)
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),alipozungumza na Uongozi wa Wizara  hiyo  katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja (Picha na Ikulu)
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images