Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AHIMIZA LINDI WAJIPANGE MAANDALIZI YA BARAZA LA MAULID KITAIFA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wana-Lindi na wana-Ruangwa watumie fursa zilizopo ili kufanikisha maandalizi ya sherehe za Maulid na Baraza la Maulid Kitaifa mwaka huu.

Ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 5, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Lindi na wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja.

Waziri Mkuu amesema sherehe hizo zitafanyika Desemba mosi kwa mkesha wa Maulid na kufuatiwa na Baraza la Maulid litakalofanyika Desemba 2, saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Likangale.

Aliwataka wana-Ruangwa waharakishe kujenga nyumba za kulala wageni na sehemu za kula ili waweze kupokea ugeni huo mkubwa wa kitaifa. “Kila mmoja anayeona hapo kuna fursa, ni lazima aitumie vizuri,” alisisitiza.

“Kwa niaba ya wana-Ruangwa, tunamshukuru Mheshimiwa Mufti na Baraza la Maulamaa kwa kuridhia sherehe hizi zifanyike kitaifa hapa wilayani kwetu. Nitumie fursa hii kuwaomba Waislamu wote tuungane katika sherehe hizi licha ya tofauti za madhehebu yetu tuliyonayo,” alisema.

Alisema uamuzi huo wa BAKWATA ulitangazwa kwenye Baraza la Maulid lililofanyika Singida, mwaka jana ya kwamba wameamua kuadhimisha sherehe hizo kwenye ngazi ya wilaya badala ya kuwa inafanyika makao makuu kila mwaka.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaarifu viongozi hao kwamba maandalizi yanaendelea na kwamba vifaa mbalimbali kama mchele, vitoweo, unga wa ngano, sukari, maji, juisi, mahema, mikeka na mazulia vimekwishapatikana.

“Ninaomba Kamati ya Uhamasishaji iifanye kazi hii kwa kutambua kuwa jambo hili si la kwenu peke yenu, bali linaungwa mkono na Serikali, na hii ni kwa sababu Serikali yenu inafanya kazi kwa karibu sana na viongozi wa dini,” alisema.

Alisema misingi ya amani katika nchi hii imejengwa na mahubiri ya viongozi wa dini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji, Sheikh Ali Mohammed Mtopa alisema Ruagwa iko tayari na imepokea wito huo wa kitaifa. “Tunakuhakikishia wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na wawakilishi wa Mufti waliopo hapa kwamba tumepokea hiyo heshima,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Itifaki kutoka BAKWATA Makao Makuu na Msimamizi wa Malidi za Kitaifa, Sheikh Mohammad Nassir ambaye alisema wana Ruangwa an wana Lindi wanalo jukumu la kuhamasisha watu washiriki sherehe hizo.

“Hamasa haitatoka Morogoro au Dar es Salaam bali hapahapa Lindi. Tunataraji watu wasiopungua 10,000 watahudhuria sherehe hizi za Maulid kutoka wilaya zote za mkoa wa Lindi na hii ni mbali wawakilishi kutoka kila mkoa wapatao 100 -150,” alisema.

Waziri Mkuu anatembelea vijiji vya jimboni mwake ambako atahutubia wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, NOVEMBA 5, 2017.

LUSINDE "KIBAJAJI" ATIKISA KITWIRU KAMPENI ZA UDIWANI MKOANI IRINGA

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ISAYA MWITA LEO ALIPOKUWA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA KANISA L.A. KKKT

$
0
0
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo,walipokutana leo katika tamasha la maadhimisho ya miaka 500 ya kanisa la KKKT lililofanyika katika Uwanja wa Taifa.Wakwanza kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye .
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimsisitizia jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo walipokutana kwenye Tamasha la  maadhimisho ya miaka 500 ya Kanisa la KKKT  lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini hapa.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa na Waziri Mkuu Mstafu Frederick Sumaye wa kwanza kushoto ,kwenye tamasha la Maadhimisho ya miaka 500 ya kanisa la KKKT lililofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini hapa.

Wateja wa Tigo mjini Morogoro wajishindia Tiketi za kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta.

$
0
0

Wasanii Roma(kulia) na Zaiid wakimkabidhi mteja wa Tigo, Francis Wamonje(katikati)zawadi ya tiketi ya kwenda kishuhudia Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika leo mjini Morogoro.
Mteja wa Tigo mjini Morogoro, Idrissa Bakari (katikati) aliyejishindia tiketi ya kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta uwanja wa Jamhuri leo, akipokea tiketi yake toka kwa Wasanii, toka kushoto Barnaba,Mimi Mars, Maua Sama na Country Boy.
Msanii Barnaba akipiga picha 'selfie' na mfanyakazi wa duka la Tigo lililopo mtaa wa Stand Morogoro leo.

Msanii Mimi Mars akiteta jambo na mfanyakazi wa duka la Tigo mtaa wa Stand Morogoro mara baada ya Wasanii kutembelea duka hilo.

 Mteja wa Tigo mkoani Morogoro, Violent Mongi (wa pili kushoto) akikabidhiwa zawadi na Wasanii Vee Money, Genevieve na GNako mara  baada ya mteja kupata huduma ndani ya duka hilo.

Mtoa huduma wa duka la Tigo Morogoro mjini, Dorcas James akitoa huduma kwa wateja.

Mtoa huduma wa duka la Tigo Morogoro mjini, Theodore John akitoa huduma kwa wateja waliofurika kwenye duka hilo leo kupata huduma mbalimbali za bidhaa zitolewazo ndani ya msimu huu wa Tigo Fiesta kwa bei nafuu.

Tigo Yatangaza Mbinu za Usajili kwa Washiriki wa Dodoma Marathon

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana namna ya kujisajili mbio za Dodoma Marathon zitakazotimua vumbi jumapili ya tarehe 12 mwezi huu, ambapo utaweza kujisajili kwa Tigopesa kwa namba 0674 444 444 kwa punguzo la asilimia 10%. Pembeni ni Meneja wa Maendeleo wa Vision Sports, Raymond Mchani.
Watakaojisajili kupitia Tigo Pesa kupata asilimia 10% punguzo la bei. 
 Dodoma.  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania wakiungana na Vision Sports wametangaza kuanza kwa usajili wa washiriki katika mbio za Dodoma Marathon. Mji wa Dodoma utageuzwa kuwa kitivo cha mazoezi na furaha kwa familia nzima tarehe 12 Novemba wakati shindano hilo litakapohitimishwa. 
Usajili kwa Dar es Salaam unafanyika katika vituo maalum vya Duka la Tigo Shop lililopo Mlimani City, Duka la Simply Elegant lililopo Dar Free Market, Ghorofa ya Chini ya Kibo Complex eneo la Tegeta na Duka la Imalaseko SuperMarket lilipo eneo la Posta katikati ya jiji. Kwa Dodoma, usajili unafanyika katika eneo la Dodoma Hotel, Carnival, Cape Town Complex iliyopo Kisasa na Duka la Tigo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 
‘Wale watakaojisajili kwa njia ya Tigo Pesa watapata punguzo la bei la asilimia 10%. Wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha shilingi 13,500/- kutoka kwenye simu zao za mkononi kwenda namba ya Tigo Pesa 0674 444 444. Hapo hapo watapokea ujumbe utakaowataarifu kujisajili na eneo ambalo wanafaa kwenda kuchukua vielelezo vyao vya usajili,’ Meneja wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema. 
Kwa upande wake,Meneja wa maendeleo wa Vision Sports, Raymond Mchani kwa niaba ya  Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Sports aliwashauri washiriki kusoma vigezo na masharti ya ushiriki pamoja na taarifa nyingine muhimu kutoka kwenye tovuti ya Dodoma Marathon na katika vituo vya usajili. ‘Pia ni muhimu kwa washiriki kuhudhuria kikao cha maelezo kuhusu ushiriki na usalama wa washiriki kitakachofanyika kabla ya mbio kuanza saa kumi na mbili asubuhi, pale katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma. 
Tigo inathamini mbio za kilometa 21 za Tigo Dodoma Half Marathon. Dodoma Marathon pia itahusisha mbio ndefu za kilometa 42, mashindano ya kilometa 10 pamoja na yale ya kilometa 5 yatakayohusu wanafamilia na jamii yote kwa ujumla. Zawadi murwa zitatolewa kwa washiriki ikiwemo vyeti vya ushiriki, medali na zawadi za fedha kwa washindi wa mbio zote. Wanariadha mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizo. 
“Tuna furaha kubwa kudhamini shindano hili ambalo linahamasisha watu kuzingatia afya bora kwa kushiriki katika michezo, na pia kuinua vipaji katika michezo,” Henry Kinabo, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema. 
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya kidigitali nchini Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995.
Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali kwa kuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na huduma ya kwanza inayowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki.     
Tigo ni kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini na ni kampuni ya simu inayokuwa kwa kasi zaidi nchini kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini
Tigo inajivunia jumla ya watumiaji milioni 10 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.   
Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani. 
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WAANZA KUTANGAZA UTALII WA NDANI KUSINI MWA TANZANIA KWA NJIA YA RELI YA TAZARA

$
0
0
Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. Halfa hiyo ilifanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (kulia) na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG.
Baadhi ya wageni ambao ni wanaumoja wa CAAT wakifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania - CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam. Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi zaidi. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto) akitolea ufafanuzi wa masuala mbali mbali jinsi umoja wao ulivyo na lengo kuu la kuweza kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika.  Halfa hiyo iliyofanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam.
Burudani ya ngoma ikiendelea. Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akiingia ukumbini. Vijana wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (mwenye tai nyekundu) akiwa na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri wakiwa katika picha ya pamoja na wanaumoja wa CAAT. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATATU LEO NOVEMBA 6,2017

MKUTANO MKUU WA MWAKA 2017 WA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA WILAYA YA KISHAPU VINAVYOSIMAMIWA NA TGNP MTANDAO

$
0
0
Rahel Madundo akifurahia ushindi baada ya kutangazwa kuwa amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Wanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka katika vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao wamefanya Mkutano Mkuu mwaka 2017 wa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na baraza la kituo cha taarifa na maarifa la wilaya hiyo.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza Novemba 4,2017 hadi leo Jumapili Novemba 5,2017 umefanyika katika ukumbi wa Sheli ya BM kata ya Maganzo wilayani Kishapu.Mbali na mkutano huo kuhudhuriwa na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka kata saba,pia umehudhuriwa na maafisa watendaji wa kata pamoja na baadhi ya madiwani kutoka wilayani Kishapu. 

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kupanga mikakati na kuendeleza vituo vya taarifa na maarifa na kuunda baraza la kituo la wilaya ambapo wajumbe wa mkutano huo walichagua viongozi wa mtandao wa wilaya ambao kazi yao ni kusimamia shughuli zote za vituo vya taarifa na maarifa kwa wilaya hiyo ya Kishapu. 

Mkurugenzi wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu uliofanyika katika mkutano huo,John Myola alimtangaza bi Rahel Madundo (aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo kipindi kilichopita) kuwa mwenyekiti wa baraza hilo kwa muda wa miaka miwili. 

Pia alimtangaza Bi Kayaya Rashid kuwa makamu mwenyekiti,Peter Nestory kuwa katibu mkuu,Renatus Mahona katibu msaidizi,Hellen Samson mhasibu na Gayunga James,Pendo Michael,Scolastica Joseph na Agnes Lutamula kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji. 

Viongozi wengine ni Catherine Revocatus aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa vijana wilaya ya Kishapu,Suzana Yohana kuwa Katibu,Paul Masamaki kuwa mwakilishi wa kanda ya Mondo,Kulwa Jandikile kanda ya Negezi na Edward Charles kanda ya Kishapu. 

Akizungumza katika mkutano huo,Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba alisema vituo vya taarifa na maarifa vimesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa matukio ya ukatili wa kijinsia. 

“Tulianza harakati za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wilayani Kishapu mwaka 2012,katika maeneo ambapo kuna vituo vya taarifa na maarifa,jamii imejitambua ambapo wananchi wamejitambua na wamekuwa na ujasiri wa kupinga vitendo hivi lakini pia wanawake wamekuwa na ujasiri wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi”,alieleza Temba. 

Temba alibainisha kuwa wanaharakati wa masuala ya kijinsia kwa kushirikiana na madiwani wamechangia kwa kiasi kikubwa kuihamasisha halmashauri ya wilaya ya Kishapu kuwa na bajeti yenye jicho la kijinsia. 

“TGNP Mtandao inawapongeza sana viongozi wa vituo pamoja na madiwani kwa jitihada wanazofanya katika kuifanya halmashauri ya wilaya ya Kishapu kuwa mfano wa kuigwa katika kusimamia na kutetea masuala ya kijinsia”,aliongeza Temba. 

Naye Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Rahel Madundo,alisema tangu kuanzishwa kwa vituo hivyo mwaka 2012 wilayani humo,wanaharakati wameisadia jamii kujitambua na kuanza kudai haki zote za binadamu pamoja na kuingia katika vikao vya kata (WDC). 

“Akina mama wamejengewa uwezo wa kuongea kwenye mikutano ya hadhara na kuhudhuria mikutano mbalimbali kuomba nafasi za uongozi”,alisema Madundo. Aidha alilishukuru shirika la TGNP Mtandao kwa kuwapatia elimu ya uraghabishi ambayo imewasaidia kujitambua huku akiliomba shirika hilo kuongeza vituo vingine katika wilaya hiyo kwani sasa vipo saba pekee. 

Katika hatua nyingine aliiomba halmashauri ya wilaya ya Kishapu kuvipatia mikopo vituo vya taarifa na maarifa kwa ajili ya kujiendesha na kuanzisha miradi. Nao wajumbe wa mkutano huo walikubaliana kuwa kila shule ya msingi wilayani humo iwe na chumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi ambapo waliahidi kushiriki katika ujenzi wa vyumba hivyo. 

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa shirika linajihusisha na masuala ya haki za watoto na wanawake la Agape Aids Control Programme,John Myola aliyealikwa kushiriki mkutano huo,aliwataka viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa na madiwani kuendeleza ushirikiano walionao katika kuwatetea watoto na wanawake na kuepuka kutumiwa na wanasiasa wenye nia mbaya. 

“Bado matukio ya ukatili wa kijinsia yapo,watoto wanabakwa,wanapewa mimba,tafadhali fanyeni kazi kwa kuzingatia maslahi ya wananchi katika kutetea wanyonge,kuweni na ushirikiano,tunzeni siri ili kutowapa mwanya wahalifu,lakini pia jitahidini kutoa taarifa mahali panapohusika kwa wakati”,alieleza Myola. 

Naye Diwani wa kata ya Mwaweja,Makanasa Kishiwa alilishukuru shirika la TGNP mtandao kwa kuichagua halmashauri ya Kishapu kuwa miongoni mwa halmashauri 28 ambako vituo vya taarifa na maarifa vimeanzishwa na kuahidi kuwa madiwani wataendelea kuungana na shirika hilo katika jitihada za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia. 

Harakati za TGNP Mtandao wilayani Kishapu zilianza mwaka 2012 katika kata ya Songwa na baadae kuzaa vituo vya ishapu,Mondo,Ukenyenge,Mwaweja,Mwadui Lohumbo na kata ya Maganzo na mpaka sasa kuna jumla ya vituo 7 katika wilaya hiyo. 


Lengo kuu la kituo cha taarifa na maarifa ni kutoa elimu kwa jamii nzima,zikiwemo elimu ya kudai rasilimali za umma,ukatili wa kijinsia,mimba za utotoni na haki za binadamu. 

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI 




Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba akizungumza katika Mkutano mkuu mwaka 2017 wa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu leo Jumapili Novemba 5,2017 katika ukumbi wa sheli ya BM uliopo katika kata ya Maganzo wilayani Kishapu.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba akiwasisitiza wanaharakati wa masauala ya kijinsia kuongeza nguvu kukabilina na vitendo vinavyokiuka haki za binadamu 
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini 
Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba 
Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Rahel Madundo akizungumza katika mkutano mkuu mwaka 2017 wa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu. 
Wajumbe wa mkutano wakimsikiliza Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Rahel Madundo
Aliyekuwa katibu wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Samwel Kalima akizungu
Diwani wa kata ya Mwaweja,Makanasa Kishiwa akizungumza katika mkutano ambapo alilishukuru shirika la TGNP mtandao kwa jitihada mbalimbali linalozifanya katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wilayani Kishapu
Diwani wa viti maalumu kata ya Bunambiyu Helena Paul akizungumza ukumbini ambapo alisema vituo vya taarifa na maarifa vimewasaidia wanawake kujitambua na sasa kuna viongozi wanawake katika ngazi mbalimbali wilayani humo wakiwemo madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita waliowagaragaza wanaume katika uchaguzi huo mkuu wa mwaka 2015
Afisa Mtendaji wa kata ya Ukenyenge,Chief Ng'ombe akizungumza kwa niaba ya maafisa watendaji wilayani humo ambapo aliwataka wanaharakati wa haki za binadamu kuendelea kushirikiana na serikali katika kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia 
Mwenyekiti wa Mkutano huo,Abdul Mohammed Ngolomole ambaye ni diwani wa kata ya Songwa akimkaribisha Mkurugenzi wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu uliofanyika katika mkutano huo,John Myola ili kutoa utaratibu wa namna ya kuchagua viongozi wapya wa baraza la kituo la wilaya ya Kishapu. 
Kulia ni Mwenyekiti wa Mkutano huo,Abdul Mohammed Ngolomole ambaye ni diwani wa kata ya Songwa akimkabidhi vifaa vya uchaguzi Mkurugenzi wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu,John Myola 
Mkurugenzi wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu ,John Myola akizungumza wakati wa kutangaza majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali katika baraza hilo 
Mkurugenzi wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu ,John Myola akielezea utaratibu wa kupiga kura 
Wasimamizi wa uchaguzi wakigawa karatasi za kupigia kura baada ya wagombea wa nafasi mbalimbali ( hawapo pichani) kuomba kupigiwa kura 
Wajumbe wa mkutano wakiweka kura zao kwenye ndoo 
Rahel Madundo akifurahia ushindi baada ya kutangazwa kuwa amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu kwa kipindi kingine cha miaka miwili 
Rahel Madundo akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kumchagua tena kuwa Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu 
Bi Kayaya Rashid akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua kuwa makamu Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu.Kushoto ni Hellen Samson aliyechaguliwa kuwa mhasibu,kulia ni Rahel Madundo aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilayani humo.
Peter Nestory akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua kuwa katibu mkuu wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu. 
Picha ya pamoja: Viongozi waliochaguliwa kuongoza baraza la vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu 
Viongozi wa baraza la vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu 
Picha ya pamoja: Viongozi waliochaguliwa kuongoza baraza la vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu,madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba na Mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola 
Picha ya pamoja : Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba na Mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola. 


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

RC.MNDEME AMEWATAKA WAKUU WA IDARA KUWA NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA, CHRISTINE MNDEME amewataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya SONGEA kujituma kufanyakazi kwa kutatua kero za wananchi badala ya kukaa ofisini.

LAPF YACHANGIA SHILINGI MILIONI TANO UJENZI WA OFISI ZA WALIMU MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akipokea Msaada wa Fedha Taslimu Shilingi Milioni tano 5.000.000/= kutoka kwa Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa ajili ya Kununulia mifuko 500 ya Saruji katika kuchangia kampeni ya ujenzi wa Ofisi za Kisasa za walimu katika shule za Msingi na Sekondari Mko wa Dar es salaam.

Kampeni hiyo imeanzishwa na Mkuu wa mkoa wa Mh.Paul Makonda katika jijini la Dar es salaam, ambapo Ofisi zaidi ya 400 zitajengwa katika shule za jiji la Dar es salaam hivyo kuboresha utendaji kazi wa waalimu hao, Kalia anayeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Kanali Charles Mbuge, Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki ofisini kwa Mkuu wa mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akimsikiliza Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakati akizungumza kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na LAPF kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu katika shule za sekondari na Msingi katika mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwake katikati ni Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF na kulia ni Kanali Charles Mbuge Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisisitiza jambo wakati akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwake lulia ni Bw. James Mlowe Meneja Mawasiliano na Masoko Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

ASKOFU MALASUSA AONGOZA MAELFU YA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KATIKA IBADA YA MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA

$
0
0
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa  akiongoza  Maelfu ya Waumini wa KKKT wa Dayosisi hiyo katika Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa,iliyofanyika jana Uwanja wa Taifa,jijini Dar.


Naibu Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mission na Uinjilisti Mchungaji, Boniface Kombo akiongoza Lutrijia wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.
 Mchungaji Lewis Hiza akisoma somo la pili wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengezo ya Kanisa la KKKT iliyoadhimishwa na Dayosisi ya Mashariki  na Pwani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Mchungaji Muke Najua  kutoka nchini Afrika kusini akitoa mahubiri wakati  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa hilo iliyofanyika  Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Kundi la watoto zaidi ya 4000 waliopata Ubarikio wa Kipaimara wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa la KKKT Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Wachungaji mbalimbali wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani wakito ubarikio kwa Vijana wa kanisa hilo amabo wamepata kipaimara leo  katika Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.
 Wachungaji mbalimbali wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani wakito ubarikio kwa Vijana wa kanisa hilo amabo wamepata kipaimara leo  katika Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.
Waumini wa Kanisa la KKKT wakiwa katika  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Watoto wa Shule ya Jumapili wakiwa katika alaiki   wa Kanisa la KKKT wakiwa katika  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa akiwa katika Maandamano ya kuingia Uwanjani wakati wa Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa wakati wa Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa
 Waziri Mkuu wa Zamani Fredrick Sumaye akiwa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ibada ya miaka 500 ya  Matengenezo ya Kanisa

Waumini wa Kanisa la KKKT wakiwa katika  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

UVCCM: UTENDAJI MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA JPM KIELELEZO CHA UZALENDO

$
0
0
Kaimu katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCM) Shaka Hamdu Shaka (wa tatu kulia)akishiriki kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa kongamano la tathmini ya uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili wa serikali ya Rais John Magufuli kwenye Ukumbi wa BKM Mkoani Tanga jana.Kulia ni Mweyekiti wa ccm wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Khamis Mkoba(picha na Fahdi Siraji)
Chipukizi wa CCM Mkoa wa Tanga wakiimbisha Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa kongamano la tathmini ya uchambuzi wa miaka miwili ya serikali ya Rais John Magufuli kwenye Ukumbi wa BKM Mkoani humo.
Sehemu ya washiriki kwenye kongamano lililoandaliwa na uvccm kuhusu tathmini na uchambuzi wa miaka miwili ya utendaji wa serikali ya Rais Dk John Magufuli lilifanyika Mkoani humo (picha na fahd Siraji)
Katibu wa ccm mkoa wa Tanga Allan Kingazi akihutubia katika kongamano lililoandaliwa na uvccm kuhusu tathmini na uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili ya serikali ya Rais Dk John Magufuli 
Katibu wa uvccm wilaya ya Tanga mjini Abdurahman Killo akisoma tamko la uvccm kuunga mkono utendaji wa miaka miwili wa serikali ya Rais John Magufuli lilifanyika ukumbi wa BMK Mkoani Tanga.
Sehemu ya uwakikisjinwa Jumuiya ya Wanawake Mkoa Tanga walioshiriki kwenye kongamano la tathmini ya Uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili ya serikali ya Rais dk John Magufuli likifanyika mkoani Tanga.
Mwenyekiti wa uvccm Mkoa Tanga Abdiely Makange akizungumza kabla ya kumkaribisha Kaimu katibu mkuu wa uvccm Shaka Hamdu Shaka azungumze na makundi ya vijana wa vyuo na vyuo vikuu.mama lishe na boda boda kwnye Ukumbi bwa BMK Mkoani Tanga.
Kaimu katibu mkuu Shaka Hamdu Shaka akizumgumza kwenye kongamano lilioandaliwa na uvccm kuhusu tathmini ya uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili wa serikali ya Rais dk John Magufuli kwenye ukumbi wa bmk Mkoani Tanga jana.(picha na Fahdi Siraji)

DC SHINYANGA ASHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA NA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA,ASHINDANA NAO KUCHEZA MUZIKI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishindana kucheza muziki na watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija wakati wa hafla ya kula chakula cha pamoja kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited-Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameshiriki katika hafla fupi kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija mjini Shinyanga kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited inayomilikiwa na Crissant Mssipi.

Kabla ya kula cha pamoja na watoto hao,mkuu huyo wa wilaya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ulinzi walifanya usafi wa mazingira ikiwemo kupulizia dawa ya kuua wadudu kama vile kunguni katika mabweni yanayotumiwa na watoto hao.

Hafla fupi ya chakula cha pamoja iliyohudhuriwa pia na Afisa Mthibiti ubora wa Shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga,imenogeshwa kwa burudani ya muziki ambapo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro aliamua kucheza muziki na watoto hao hali iliyoongeza furaha zaidi kwa watoto hao.Akizungumza katika kituo hicho,Matiro ameitaka jamii kuondokana na dhana ya kuwabagua na kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kukata viungo na kuwaua akibainisha kuwa watoto wenye ualbino binadamu kama wengine na kinacho watofautisha ni rangi tu ya ngozi yao.

Amesema jamii ikibadilika watoto hao wataishi kwa amani na furaha kwa kujiona hawana tofauti na binadamu wengine ."Naomba jamii iondokane na matukio ya kuwanyanyasa watoto hawa ili nao waishi kwa amani na upendo ," amesema Matiro.Aidha alisema hivi karibuni serikali iliamua kuwarudisha majumbani baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi katika kituo hicho wakiwemo waliohitimu elimu yao ya msingi katika Shule ya Buhaghija hivyo akaitaka jamii kuhakikisha inawalinda na wanaishi kwa amani bila ya kubughudhiwa.

Naye msemaji wa Kampuni hiyo ya Ulinzi Twaha Makani, amesema mara baada ya siku chache kukitembelea kituo hicho waliguswa na vitu vingi vinavyohusu maisha ya watoto hao na hivyo kuamua kufanya shughuli za usafi wa mazingira, kupulizia dawa ya kuua kunguni pamoja na kula nao chakula cha pamoja.

Kwa upande wake mmoja wa walezi wa kituo hicho Bright Mduma mbali na kuishukuru kampuni hiyo ya ulinzi kwa kufanya usafi,kuua wadudu na kuandaa chakula,amesema kituo hicho kina jumla ya watoto 228, watoto wenye ualbino 144, wasiosikia 60 na wasioona 24.Mwandishi wa Malunde1 blog,Marco Maduhu alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha za matukio yaliyojiri.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza katika hafla fupi ya kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga ambapo aliwahakikishia ulinzi pamoja na kuboreshewa makazi yao.-Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Msemaji wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza na watoto hao ambapo alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana nao kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaendelea kuwakabili.
Msemaji wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza katika kituo cha Buhangija
Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga, akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija ambapo aliwataka wadau wajitokeze kuwasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili pamoja na kushiriki kula nao chakula cha pamoja na siyo kusubiri hadi siku za sikukuu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD wakipulizia dawa ya kuua kunguni katika mabweni ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Zoezi la kupulizia dawa ya kuua wadudu likiendelea
Sehemu ya Mashuka yakiwa yameanikwa baada ya kufuliwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akipika chakula kwa ajili ya watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
Watoto wenye ualbino wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD 
Watoto wakiendelea kula chakula
Baadhi ya walinzi wa kampuni hiyo nao wakishiriki kula chakula cha pamoja na watoto hao
Zoezi la kula chakula likiendelea
Watoto wakila chakula
Mtoto akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) uwezo wake wa kucheza muziki


Mkuu wa wilaya Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) akicheza muziki wimbo wa Diamond Platnumz zilipendwa na watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija


Mimi ni nomaaaa!! subiri nikuoneshe kazi mkuu.......


Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akifurahia show ya mtoto.....
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza na watoto hao
Kushoto ni Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga akicheza muziki
Watoto wakicheza mziki wa Kamatia chini 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza Kwaito na watoto hao
Watoto wakicheza muziki na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Watoto wakisakata rhumba
Watoto wakiendelea kucheza

Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mshindi wa Tigo Supa Nyota Morogoro aahidi makubwa

$
0
0

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Morogoro, Salum Munga akiimba kwenye kinyang'anyiro cha kumpata mwakilishi wa mkoa Morogoro

Majaji wakiendelea na majukumu yao

Mchujo wa washiriki

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Morogoro, Salum Munga akipongezwa na washiriki wenzake.



MSHINDI wa shindano la kuibua vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota, mkoa wa Morogoro, Salum Munga, ametamba kuibuka na ushindi katika fainali za mwaka huu. Kinda huyo jana aliibuka kidedea baada ya kuwapiku washiriki 106 chipukuzi waliojitojeza kuwania nafasi hiyo.

Washindi wa mashindano ya Tigo Supa Nyota kutoka mikoa 15 ya Tanzania watashindana kwenye fainali itakayofanyika Dar es Salaam mwezi huu ili kupata mshindi wa jumla. Mshindi wa Tigo Supa Nyota, atapata nafasi ya kuendelezwa kimuziki ikiwa ni pamoja na kuingia studio.

Mara baada ya kushinda, Munga. alisema, amepata nafasi, atahakikisha anaifanyia kazi vyema na kuwapa furaha mashabiki wake wa mkoa wa Morogoro. Alisema anejipanga vyema kuhakikisha analeta taji la Tigo Fiesta Supa Nyota kwa mara ya kwanza na kuweka historia.

Alisema anatambua kuwa ataenda kupambana na wasanii kutoka mikoa mbalimbali lakini atahakikisha anafanya vizuri na kutengeneza historia mpya. Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Kanda ya kati, John Tungaraza, alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanaibua vipaji na kuwapatia daraja wasanii chipukizi kupata nafasi ya kufikia malengo.

"Tutahakikisha vijana wanafikia malengo kwani Tigo kwa udhamini wetu tunaibua wasanii chipukizi ili kuwaendeleza na kufikia malengo, kwani hatutawapa nafasi wasanii wa nje", alisema.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WANANCHI WA MULEBA NA KEMONDO WAKATI AKIELEKEA BUKOBA MJINI MKOANI KAGERA

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Muleba wakati akiwa njiani kuelekea Bukoba mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba wakati walipokuwa wakiwasilisha kero zao mbalimbali.
 Baadhi ya wananchi wa Kemondo mkoani Kagera wakiwa juu ya miti kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akihutubia wananchi wa eneo hilo.
 Wananchi wa Kemondo wakifurahia wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
 Wananchi wa Muleba wakifurahia wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kemondo wakati akielekea Bukoba mjini. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwananchi Maarufu wa Muleba Hassan Milanga mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Muleba.
 Baadhi ya mabango wa Wananchi wa Kemondo mkoani Kagera wakiyanyanyua wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akipita katika eneo hilo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum  Kijuu mara baada ya kuwasili mkoani Kagera. PICHA NA IKULU


TAZAMA ZIARA YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI MKOANI KAGERA HIVI SASA

WAZIRI MKUU AWAPOKEA WANACHAMA 37 WA UPINZANI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 37 kutoka vyama vya CUF na CHADEMA ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw. Barnabas Essau wanachama 35 kati ya hao wametoka CUF na wawili wametoka CHADEMA.Wanachama hao walipokelewa jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Bw. Essau alisema wanachama hao wote wametoka kata za Mbekenyela na Matambalale. Walikabidhiwa kadi mpya za CCM, na kula kiapo cha uaminifu.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake wapya, Bw. Mohammed Issa Ndogoro ambaye amehamia kutoka CHADEMA, alisema wamejiunga na CCM baada ya kuridhishwa na mwelekeo wake. Alisema wameguswa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli inavyofanya kazi ya kutatua kero za wananchi. 

Alisema amekaa upinzani kwa miaka 23 lakini anaikubali CCM sababu ya uwazi wake na ameshangaa kuona akipewa kadi na stakabadhi ya walipo yenye jina lake, jambo ambalo hajawahi kuliona katika vyama vingine vya upinzani.

“Sote sisi tumehamia CCM, uhai wa chama ni michango. Nani aseme hapa kama aliwahi kupewa stakabadhi katika chama chake, na kama yupo nampa sh. 5,000/- sasa hivi,” alisema Bw. Ndogoro na kuamsha kicheko kwenye mkutano huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATATU, NOVEMBA 6, 2017.

WATAKAOKWAMISHA MALIPO YA KOROSHO KUKIONA-MAJALIWA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote watakaokwamisha malipo ya wakulima wa zao la korosho.

“Hatutamuacha mtu yeyote atakayesababisha wakulima kuchelewa kulipwa fedha zao. Tutawakamata wote na kuwachukulia hatua stahiki.”Ametoa kauli hiyo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbekenyera wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu alisema wakulima hao ni lazima walipwe fedha zao kwa wakati na asitokee mtu wa kuzitamani fedha hizo.“Mkulima amelima mikorosho mwenyewe, ameokotoa na kukodoa mwenyewe wao wamepewa dhamana ya kuziuza, hivyo wahakikishe wanawapelekea fedha zao na wala wasizitamani.”

Pia Waziri Mkuu amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika vya Msingi wahakikishe mkulima hakosi sh. 3,500 katika kilo moja ya korosho atakayoiuza baada ya kukatwa michango.Alisema bei ya juu ya korosho katika minada ya mkoa wa Lindi sh. ni 3,970 na ya chini sh. 3,800. “Vyovyote itakavyokuwa mkulima hawezi kukosa sh. 3,500, viongozi wa AMCOS mnisikie.”

Waziri Mkuu alisema hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa bei ya zao la korosho pamoja na kupungua kwa makato ya mkulima ambapo kwa sasa hayazidi sh. 300 katika kilo moja ya korosho.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATATU, NOVEMBA 06, 2017.

‘RUANGWA INAHITAJI SEKONDARI YA WASICHANA’-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa shule ya msingi Ng’au, katika kata ya Mnacho, Wilayani Ruangwa, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya msingi Ng’au, iliyopo kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya msingi Ng’au iliypo Wilayani Ruangwa, Daniel Chilemba kwa kusimamia ujenzi kikamilifu, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa shule, Novemba 5, 2017.
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wilaya ya Ruangwa inahitaji kuwa na shule ya sekondari ya wasichana ambayo ni ya bweni ili kupunguza tatizo la wasichana kukosa elimu.

Ametoa wito huo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ng’au, kata ya Mnacho wilayani Ruangwa mkoani Lindi ambako alienda kukagua ujenzi wa shule mpya ya msingi ambayo ujenzi wake ulianza wiki mbili zilizopita.

“Mpango wetu ni kujenga shule ya msingi mpya hapa kijijini Ng’au ili watoto wanaotoka ng’ambo hii wasome hapa hapa. Wakati wa masika nyote mnajua taabu wanayopata watoto wetu kukatisha kwenda ng’ambo ile,” alisema.

“Nimefurahi kukuta msingi wa vyumba tisa uko tayari na hii idadi inaweza kuongezeka. Wanakijiji tushirikiane kujaza kifusi ili kazi ya ujenzi iende haraka,” alisema.Waziri Mkuu alisema ng’ambo ya pili kuna shule ya msingi Mnacho ambayo ina madarasa 11 na wanafunzi waliopo ni karibu 500, na ndoto yake ilikuwa ni kuona ile shule inabadilika na kuwa ya sekondari.

“Ile shule ina historia na wakazi wengi kutoka Nandagala, Namahema, Chimbila ‘A’ na Chiemeka wamesoma pale. Mimi mwenyewe nimesoma pale kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule ilishazeeka, ndipo tukatafuta fedha ili ifanyiwe ukarabati na sasa ina miundombinu mizuri ndiyo sababu inaonekana inafaa kuwa ya sekondari,” alisema.

“Kwa vile shule ina miundombinu ya kutosha, ni vema ikawa ya bweni ambayo ni mahsusi kwa wasichana wa wilaya hii kwani tunalo tatizo la watoto wa kike kupata elimu, na wanahangaika sana,” alisema.

“Ujenzi wa hii shule ukikamilika, watoto wale 500 watahamia hapa na walimu wao na ile pale itapokea wanafunzi sekondari za wilaya hii ili tuwe na kidato cha kwanza hadi cha nne na ianze mara moja,” alisema.

Alisema shule hiyo itaitwa Lucas Malia kwa heshima ya mwalimu mkuu wa zamani wa shule hiyo ambaye alisomesha watu wengi katika wilaya hiyo na wengine sasa hivi ni viongozi Serikalini na jeshini. Mwalimu Malia hivi sasa ni marehemu.

Waziri Mkuu amerejea Dodoma leo asubuhi kuendelea na vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza kesho (Jumanne, Novemba 7, 2017).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATATU, NOVEMBA 6, 2017.
 

POLISI KIKOSI CHA RELI ,WANAWAKE DAWATI LA JINSIA WASHEREHEKEA KUANZISHWA KWA MTANDAO NA KUTEMBELEA WATOTO WALIOLAZWA KATIKA TAASISI YA MOYO (JKCI)

$
0
0
 Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akimpa zawadi ya dawa ya meno, maji ya kunywa na juisi  Hadija Selemani ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
  Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Rhoda Israel  akimpa zawadi ya juisi  Sada Issah ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Koplo Grace Ndyamukama akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia. Kulia ni Mama wa mtoto Nasra Khalfan.

 Maafisa wa  Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakigawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za mENO,  juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea na kufulia kwa watoto waliolazwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Jane John akimpa zawadi za maji ya kunywa, dawa ya meno,  juisi, mafuta ya kupakaa na  sabuni Maimuna Daud  ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akiongea jambo na wagonjwa walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Maafisa wa  Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea Taasisii ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kugawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za meno,  juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea  na kufulia kwa watoto waliolazwa  katika taasisi hiyo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
Picha na JKCI
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images