Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1422 | 1423 | (Page 1424) | 1425 | 1426 | .... | 1903 | newer

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Irenius Ruyobya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Oktoba, 2017 ambao umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2017. Kulia Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei Bi. Ruth Minja.

  Na: Veronica Kazimoto,

  Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2017. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Irenius Ruyobya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) amesema kupungua kwa Mfumuko wa Bei kunamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba, 2017 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Septemba, 2017.

  Ruyobya ameongeza kuwa, kupungua kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2017 kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba, 2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba, 2016.

  "Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa Mfumuko wa Bei ni pamoja na unga wa mtama kwa asilimia 2.6, samaki kwa asilimia 7.1, matunda kwa asilimia 2.7, mbogamboga kwa asilimia 7.4, maharage kwa asilimia 2.9, viazi kwa asilimia 14.4 na karanga kwa asilimia 7.8", amesema Ruyobya.

  Akizungumzia Mfumuko wa Bei kwa upande wa Afrika Mashariki, Irenius Ruyobya amesema Mfumuko wa Bei wa Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi asilimia 5.72 kutoka asilimia 7.06 mwezi Septemba, 2017 na nchini Uganda umepungua hadi asilimia 4.8 mwezi Oktoba, 2017 kutoka asilimia 5.3 mwezi Septemba, 2017. Mfumuko wa Bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

  0 0

  Naibu Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Mamlaka hiyo, Bw. Ulimbakisya Masomelu akiwaeleza Waajiriwa wapya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) juu ya kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu yao kikamilifu wakati wa Semina Elekezi ya Siku Kumi iliyoanza leo 08 Novemba, 2017 katika Chuo cha Kodi (ITA) Kilichopo Jijini Dar es Salaam.
  Waajiriwa wapya 400 walioajiriwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakipokea elimu ya Semina Elekezi toka kwa Maafisa Utumishi wa TRA kuhusu namna ya kutekeleza majukumu yao kwa weledi wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo ya Siku Kumi iliyoanza leo katika Chuo cha Kodi (ITA) kilichopo Jijini Dar es Salaam, 08 Novemba, 2017. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA,TRA).

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kutoa Semina elekezi ya siku 10 kwa Waajiriwa wapya 400 waliopata fursa ya kupata ajira katika Mamlaka hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo watendaji hao wakati wanapoenda kuanza majukumu ya kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

  Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Chuo cha Kodi cha TRA (ITA), Profesa Isaya Jairo na yanatarajiwa kukamilika baada ya siku kumi na kuwawezesha waajiriwa hao kumudu majukumu ya kukusanya mapato nchini kwa uadilifu.

  Akiongea wakati wa Semina hiyo, Naibu Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Mamlaka hiyo, Bw. Ulimbakisya Masomelu alisema kwamba, lengo la kubwa la kuwapatia mafunzo waajiriwa hao ni kuhakikisha kwamba TRA inakuwa na nguvu kazi kubwa ya rasilimali watu katika kutekeleza majukumu yake.

  Bwana Masomelu ameeleza kwamba, TRA ina majukumu makubwa ya kukusanya mapato nchi nzima na huo ni utaratibu wake wa kuwapatia mafunzo waajiriwa wake kwani mafunzo hayo yanawawezesha waajiriwa hao kuijua mamlaka hiyo jinsi inavyofanya kazi, ikiwemo mgawanyo wa majukumu (Organization Structure) pamoja na maadili ya utumishi.

  “Lengo la kuwapatia semina hii elekezi waajiriwa wetu wapya ni kuwawezesha waweze kutambua dhima kubwa ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo ni kukusanya mapato, waweze kutambua pia maadili ya utumishi ili wanapoenda kutekeleza majukumu yao waweze kutekeleza kulingana na maadili ya kiutumishi, lakini pia waweze kujua mgawanyo wa majukumu ya TRA katika vitengo vyao”, alisema, Masomelu.

  Kwa upande wake, Kaimu Meneja Mafunzo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bi. Pendo Mandia amesema kwamba, waajiriwa hao katika muda wao wote wa mafunzo ya siku kumi watapitishwa katika maeneo mbalimbali ili waweze kuyajua vizuri majukumu yao, ambapo baadhi ya mambo watayofanya ni pamoja na kufahamishwa juu ya muundo wa vitengo vyao, Sheria za Mamlaka ya Mapato, kufahamu Mkataba wa Huduma kwa Mlipakodi, kufahamu maadili na mwenendo wa utumishi wa umma.

  Ameongeza kuwa, pamoja na hayo yote, waajiriwa hao wapya mara baada ya kukamilisha taratibu zote za ajira katika mamlaka hiyo watakula kiapo cha uadilifu kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao. Kwa upande wao baadhi ya waajiriwa hao wapya wameonyesha nyuso za furaha ya kupata ajira TRA na kuahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi.

  0 0
 • 11/08/17--07:17: BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’


 • Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Ebenezer Massawe (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipa nauli kielektroniki kupitia huduma mpya iliyozinduliwa na Kampuni hiyo ya 'Uhuru Pay' wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika leo jijiji Dar es salaam. Toka kushoto ni Afisa wa BCX Justin Lawena, Mkurugenzi Mtendaji wa wa BCX Seronga Wangwe, Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi.

  Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Ebenezer Massawe (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipa nauli kielektroniki kupitia huduma mpya iliyozinduliwa na Kampuni hiyo ya 'Uhuru Pay' wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika leo jijiji Dar es salaam. Toka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BCX Tanzania, Seronga Wangwe, Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Seronga Wangwe (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake kati ya Tegeta Nyuki na Kivukoni hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi kwa kukubali kutumia huduma mpya ya ‘Uhuru Pay’ kwa ajili ya malipo ya nauli kielektroniki wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia toka kushoto ni Afisa wa BCX, Justin Lawena, Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX), Ebenezer Massawe na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda


  Mkurugenzi Mtendaji wa Business Connexion (BCX) Tanzania , Seronga Wange akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja Mauzo na Masoko wa BCX, Ebenezer Massawe na kulia ni Afisa wa Kampuni hiyo, Justin Lawena.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Seronga Wange (kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi.
  Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda (kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Business Connexion (BCX) leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi na kulia ni Meneja Masoko na Mauzo BCX, Ebenezer Massawe.  Abiria wanaotumia usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam sasa hawatosumbuka tena kuhusu kutembea na fedha taslim mfukoni au usumbufu wa makondakta wa kutokua na chenchi, lakini pia wamiliki wa daladala wataanza kuona faida katika uwekezaji wao, kutoana na kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kukusanya nauli kielektroniki uliozinduliwa na Kampuni ya BCX chini ya bidhaa yake ya ‘Uhuru Pay’.

  Tanzania inakuwa nchi ya nne Afrika kuzindua huduma hii baada ya Malawi, Zambia na Msumbiji ambako tayari imekwisha anza kutumika.

  Mfumo huu wa ulipaji wa nauli kielektroniki una lengo la kurahisisha usafiri kwa watumiaji wa usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam kwa kuwapa fursa ya kulipia nauli kwa kutumia kadi. Kama mradi wa majaribio mfumo huu utaanzishwa kwanza kwenye ruti ya Tegeta Nyuki na Kivukoni kabla ya kuhamia kwenye maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam.

  Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa BCX-Tanzania, Seronga Wangwe alisema ‘Uhuru Pay’ inalenga kurahisisha ulipaji wa nauli kwa wasafiri wa daladala na kuhakikisha kuwa abiria wanasafiri kwa utulivu na amani.

  Tofauti na hilo ni kuwa wamiliki wa daladala wataweza kupata faida katika uwekezaji wanaofanya kwenye mabasi hayo kutokana na udhibiti na uwazi wa mapato yanayokusanywa”.

  Aliongeza kuwa Abiria wa Daladala jijini Dar es salaam hawatakua na hofu tena ya kutembea na fedha taslim au usumbufu kutoka kwa Makondakta wa kutokuwa na chenchi, kwani kwa kupitia kadi ya Uhuru Pay watakuwa na Uhuru wa kupata huduma hiyo bila bugudha.

  Urahisi huu utaambatana na ofa mbalimbali zitakazopatikana kwa abiria wote kama punguzo kubwa la bei za kusafiri na wakati mwingine kusafiri bure kabisa.

  Seronga anaamini kuwa mfumo huu wa malipo kielektroniki utakubaliwa na Watanzania kwani tabia zao zinabadilika mara kwa mara na kukubali njia nyingine za malipo tofauti na fedha taslim. Hili ni jambo ambalo mataifa yaliyoendelea yamefanya kwa miaka mingi sasa, lakini mwenendo wa hivi karibuni wa malipo kupitia simu na matumizi ya kadi yanaonyesha kwamba kadi ya Uhuru Pay ni kitu ambacho Watanzania wanahitaji kwa sasa ili kuendana na mfumo wa maisha ya kisasa.

  Kwa upande wake, Meneja Mauzo na Masoko wa BCX, Ebenezer Massawe alisema, mradi huo umekuwa katika matengenezo kwa muda mrefu sasa, na umepitia hatua mbalimbali za majaribio ili kuhakikisha kuwa vipengele vyote vinafanya kazi kama inavyohitajika.

  “Mfumo huu tayari umeshafanyiwa majaribio ya kutosha na unazingatia kikamilifu sheria na kanuni zote, pamoja na mahitaji ya wahusika wanaohusika. Sasa tupo tayari kuingia kazini,” alisema Bw. Massawe.

  Akielezea jinsi mfumo huu unavyofanya kazi, Massawe alisema kuwa mfumo huo wa kielektroniki utaunganishwa na wamiliki wa mabasi ili waweze kufuatilia moja kwa moja mauzo ya tiketi ya kila siku na kuongeza kuwa ndio ni kitu pekee ambacho wamiliki huwa wanakosa katika mfumo wa biashara ya leo.

  Alisema abiria watakua na fursa ya kulipa kwa kutumia kadi ya Uhuru Pay ambayo itakuwa inapatikana katika vituo mbalimbali vya daladala, jijini Dar es Salaam.

  Alielezea zaidi kuwa, Uhuru Pay ni bidhaa ya BCX, ambayo inatoa suluhisho kwa matatizo mbalimbali ya kifedha iliyoanzishwa na Kampuni ya BCX kwa wateja wake ili kupunguza mzigo wa usimamizi wa ukusanyaji wa fedha pamoja na uhamishaji wa fedha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

  "Kwa sasa kadi ya Uhuru Pay itatumika kwa huduma za usafiri Daladala lakini baadae huduma zingine zaidi zitapatikana kwa kutumia kadi hiyo ikiwa ni pamoja na Malipo ya maduka makubwa katika, uwekaji gari mafuta, kutuma fedha kwa mitandao yote na akaunti za benki, malipo ya huduma kama LUKU, DAWASCO, NHC, AzamTV, ZUKU, Startimes, DSTV, nk "alisema.

  Kwa Upande wake, Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda alisema mfumo huo utaongeza makusanyo ya mapato kwa wamiliki wa daladala lakini pia mapato ya Serikali kwani wamiliki wa mabasi hayo watalazimika kulipa kodi kulingana na mauzo yao ya tiketi kwa siku.

  "Serikali bado haikukusanyi mapato ya kutosha yanayotokana na huduma za usafiri, hivyo tumeamua kuunga mkono teknolojia hii mpya ili kuhakikisha kwamba Serikali inakusanya kodi ya kutosha," Kahetano, aliongeza kuwa mara baada ya mfumo huu kuwa rasmi basi madereva na makondakta watapata ajira rasmi”.

  Aliongeza kuwa kupitia mfumo huu mpya, itakuwa rahisi kudhibiti suala la foleni kwenye ruti zinazotumia huduma hii kwa kuwa ni rahisi kujua njia ipi ina foleni na ipi haina.

  Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa madaladala, Emmanuel Mlaponi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania alitoa wito kwa wamiliki kuiunga mkono huduma mpya ya 'Uhuru Pay' ikiwa kama watataka kudhibiti na kuongeza mapato ya biashara yai

  0 0


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Misenyi(hawaonekani pichani) wakati akielekea katika kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Wilayani hapo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika wakati wananchi wa Misenyi walipokuwa wakiwasilisha Kero zao mara baada ya kusimama wakati akiwa njiani kuelekea katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo wialayani humo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa kwa shangwe na Mamia ya wananchi wa Misenyi mara baada ya kuwasili Wialayani hapo akitokea Bukoba mjini.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Misenyi wakati wakitoa kero zao mbalimbali mara baada ya kuwasili.
   Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akizungumza katika eneo hilo la Misenyi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wa pili kutoka kushoto , Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba wa kwanza (kulia) wakisikiliza mtaalamu wa Kilimo (haonekani pichani) aliyekuwa akielezea mambo mbalimbali katika mashamba ya miwa katika Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Shamba la miwa la Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Mitambo ya kuchujia na kuvutia maji kwa ajili ya Mashamba ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar, mitambo hiyo ipo pembezoni mwa Mto Kagera katika Wilaya ya Misenyi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mbegu na mbolea inayotumika katika mashamba hayo ya miwa ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja katika Mashamba hayo ya miwa na viongozi wa Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wa kwanza kulia akifatiwa na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda Charles Mwijage wa kwanza kulia.
   . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi (Vibarua) wanaofanyakazi katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar wakati akielekea kiwandani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya mashamba hayo ya miwa ya Kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo Wilayani Misenyi mkoani Kagera. PICHA NA IKULU


  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi. Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, huku Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (wa pili kulia waliosimama-tai nyekundu) akishuhudia, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili kulia waliosimama akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakionesha Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, baada ya kusainiwa katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)​

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird, wakielekea kusaini Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam
   Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Katibu Mkuu Wizara ya maliaasili na Utalii( wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa makini tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya Ujumbe wa Benki ya Dunia walioshiriki tukio la Tanzania na Benki hiyo kutiliana saini mkataba wa mkopo  nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi, akitoa neon la shukurani wakati wa kusainiwa kwa Mkataba wa Mkopo Nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia wenye thamani ya Dola  za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird.

  Benny Mwaipaja, Dar es Salaam.
  BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 150, sawa na takriban Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kufungua fursa za utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania.

  Mkataba wa mkopo huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi, Bi. Bella Bird.

  Bw. James alisema kuwa mkopo huo umelenga kuimarisha miundombinu ya utalii katika ukanda huo wa kusini ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, madaraja pamoja na kuibua fursa nyingi za utalii ili kuvutia watalii wengi zaidi.

  Alisema pia kwamba mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wananchi wanaozunguka maeneo ya utalii kwa kuanzisha miradi itakayo chochea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuendeleza uhifadhi katika maeneo yao.

  Aidha, mkopo huo utatumika katika kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko katika ukanda huo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea maeneo hayo badala ya hali ilivyo sasa ambapo watalii wengi wanatembelea vivutio vilivyoko ukanda wa Kaskazini.

  Mradi huo utakaotekelezwa kwa kiasi kikubwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania-TANAPA, utainufaisha zaidi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba na Selous.

  Alisema kuwa manufaa hayo yatalenga kujengwa viwanja vya ndege, barabara hifadhini, utunzaji wa mazingira utakao uwezesha mto Ruaha Mkuu kutiririsha maji muda wote katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kupitia uwanda wa Usangu.

  “Mpango wa kuibua fursa za utalii katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, umelenga kuimarisha usafiri wa anga na nchi kavu ambapo uwanja mkubwa na wa kisasa utajengwa mkoani Iringa pamoja na kuboresha barabara inayotoka Iringa hadi Msembe yenye urefu wa kilometa 105” alisema Bw. James

  Aisema kuwa hatua hiyo inatarajia kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi na kupunguza gharama za usafiri kutoka katika maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Kilimanjaro hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

  Bw. Doto James aliishukuru Benki ya Dunia kwa mkopo huo utakao changia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi wake kupitia sekta ya utalii.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali, Gaudence Milanzi alisema kuwa mradi huo, utahusisha ujenzi wa viwanja 15 vya ndege, ujenzi wa kilometa 982 za barabara kwenye hifadhi, kununua mitambo ya kukarabati barabara, kuimarisha reli ya TAZARA ili kuwawezesha watalii kufika kwenye Pori la Akiba la Selous.

  Aidha, alisema kuwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi watapatiwa mafunzo ya namna ya kuongoza watalii, kutoa huduma kwenye hoteli na kuwajengea uwezo wa kutengeneza bidhaa zinazohusiana na utalii ili wajiongezee kipato.

  Meja Jenerali Milanzi alisema kuwa wanategemea mradi huo utaongeza idadi ya watalii kutoka milioni moja hivi sasa hadi kufikia zaidi ya watalii milioni 2 ifikapo mwaka 2020.

  Akizunguza wakati wa tukio hilo, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, hapa nchini Bi. Bella Bird alisema kuwa mkopo huo ulioridhiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Jijini Washington DC Septemba 28, 2017, umelenga kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta hiyo ya utalii na kupunguzia umasikini wananchi wake.

  “Utalii na uhifadhi vinakwenda pamoja na kwamba vitu hivyo viwili vitaisaidia nchi kukua kiuchumi na kukuza ajira ya watu wake kwa kiwango kikubwa hivyo kuondokana na umasikini ikichagizwa pia na kilimo” alisisitiza Bi. Bella Bird.

  Alisema sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya watu na wanyama, ujangili, na ndiyo maana Benki ya Dunia imeamua kuisaidia Serikali na taasisi zinazojihusha na kudhibiti changamoto hiyo kwa kuzijengea uwezo wa kukabiliana nazo.

  Bi. Bird alisema kuwa mradi huo utakuja na suluhisho la changamoto ya wananchi kuwa sehemu ya uhifadhi kwa kuwapa miradi ya maendeleo itakayokuwa mbadala wa shughuli walizokuwa wakifanya kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuanzisha utalii wa kiutamaduni, kilimo ili waendeleze maisha yao.

  0 0

  Jokate na Khadija Kopa wakati wa mazoezi ya TOT
  NA BASHIR NKOROMO
  Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo amesema amefurahi na kufarijika sana kuona kundi la Tanzania One Theatre (TOT) likiwa bado lipo imara na kuendelea kutoa nyimbo mpya zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi na ala za muziki.

  Amesema, uimara wa TOT unafanya kundi hilo kuendelea kutoa mchango mkubwa  kwa kutoa nyimbo
  zenye hamasa kwa wananchi na hasa viongozi katika kuenzi amani, umoja, mashikamano wa kitaifa, uzalendo na uchapakazi na pia kuburudisha.

  Jokate amesema hayo, alipotembelea mazoezi ya yimbo za Mkutano Mkuu wa CCM taifa, na za Mikutano Mikuu ya Taifa ya Uchaguzi wa Jumua zote za Chama, yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

  "Kwa muda mrefu nyimbo zimekuwa ni sehemu muhimu ya kupeleka ujumbe kwa jamii. Nina furahi kuona kwaya ya TOT inaendelea kuenzi hili kwa kutoa nyimbo zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi.

  Hizi nyimbo walizotunga TOT kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na mikutano ya Uchaguzi Mkuu wa Jumuia za Chama ni nzuri, zinatoa hamasa hasa kwa viongozi wetu wakizisikia nina imani watapata morali ya kuwa bora zaidi katika kazi zao", amesema Jokate.

  Nyimbo hizo ambazo ambazo ni kwaya kundi la TOT juzi lilianza kuzirekodi katika Studio maarufu na ya kisasa  ya Highland Studio iliyopo Kigogo jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini alisema TOT imezitunga nyimbo hizo kwa ustadi mkubwa ili kuzifanya kuwa za kiwango bora kulingana na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuia zake na pia kuzingatia umuhimu wa mkutano huo mkuu wa CCM taifa na mikutano mikuu ya Uchaguzi Mkuu ya Jumuia hizo za chama.

  Amesema wimbo wa CCM umebeba maudhui ya kuwakaribisha Dodoma wajumbe wa Mkutano Mkuu 
  wa CCM, ukiwahimiza wajumbe hao kukamilisha kwa kushiriki kwa busara na umakini mkubwa kwenye mkutano huo ili kuhakikisha CCM inapata viongozi bora wenye uwezo wa kuendana na matakwa ya CCM Mpya na Tanzania Mpya na kasi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.

  Tumaini amesema nyimbo za Jumuia za Chama pia zina maudhui ya kuwakaribisha wajumbe Dodoma, lakini wao tofauti na CCM wajumbe wahawafanyi shughuli ya kukamilisha bali wanafanya uchaguzi, hivyo wimbo unawahimiza kuwa kidete kuhakikisha wanachagua viongozi bora ambao watakisaidia Chama kutimiza malengo na ilani yake kwa mafanikio makubwa.

  "Kwa upande wa umoja wa Umoja wa Vijana wa CCM tumeenda mbali zaidi, mbali na kuwahimiza kufanya uchaguzi kwa busara zaidi, lakini wimbo umehimiza vijana kujitambua na kuelewa kuwa UVCCM ndiyo chachu ya viongozi bora wa baadae wa CCM na pia watambue kuwa Vijana wa UVCCM ndiyo walinzi wa mstari wa mbele wa CCM hivyo lazima wawe wa kwanza kila mara kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM lakini pia wawe wa kwa kwanza na kwa haraka kuwajibu wapinzani wanapojaribu kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya CCM", alisema Tumaini.

  Alisema, katika nyimbo hizo ambazo Jokate ameshiriki kutoa mchango mkubwa kuziboresha kwa namna mbalimbali wakati wa utungwaji, wakati wa mkutano mkuu zitauzwa kwa wajumbe zikiwa kwenye CD na DVD hivyo wajumbe wajiandae kuzipata.
  Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo akiwa na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Abdul Aziz Salehe (kushoto) na Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini wakati wakishuhudia mazoezi ya nyimbo mpya za Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mikutano Mikuu ya Uchaguzi ya Jumuia za Chama, kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, juzi
  TOT WAKIREKODI STUDIO
   Mwimbaji wa TOT akiingiza sauti yake kwenye moja ya nyimbo nne zilizotungwa na TOT kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mikutano Mikuu ya Uchaguzi ya Jumuia za Chama, katika Studio ya Highland, Kigogo, Dar es Salaam, jana.
   Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini akisikiliza kwa makini wakati mwimbaji huyo akiingiza sauti yake kwenye wimbo
   Tumaini akiwa na fundi mitambo wa Studio ya Highland wakati wa kurekodi nyumba hizo
   Waimbaji Nusra Minja na margareth Mwiru wakiimba wakati wa kurekodi kwenye Studio hiyo
   Waimbaji Mroka Emmanuel na Issa Sabby wakiimba wakati wa kurekodi wakiimba wakati wa kurekodi kwenye studio hiyo
   Jerry na waimbaji wenzake wakiimba wakati wa kurekodi
  Neca Twalib ambaye ni mrithi wa aliyekuwa mwimbaji nguli na Mkurugenzi TOT John Komba, akiimba wakati wa kurekodi Studio. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

   Wanakikundi cha Upendo kilichopo Kijiji cha Magiri Kata ya Magiri katika Halmshauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wakiwa pamoja na watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera na Mwanahabari Coleta Makulwa wa RFA (wa pili kushoto), baada ya kukabidhiwa mbegu bora za Viazi lishe aina ya Kabode kwa ajili ya kuzipanda kwenye shamba darasa katika kata hiyo wilayani humo leo.
   Mbegu hizo zikiinuliwa juu baada ya kukabidhiwa.
   Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akimkabidhi mbegu za mihogo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Uyui, Hadija Makuwani kwa ajili ya kupanda katika shamba darasa katika Kijiji cha Isikizya wilayani humo. Wengine ni wakulima wa kijiji hicho.
   Wanakikundi cha Mapambano katika Kijiji cha Iberamilundi wakifurahi mbegu bora ya mihogo baada ya kukabidhiwa.
   Wakulima wa Kijiji cha Isikizya wakiwa kwenye uzinduzi wa shamba darasa.
   Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza na wakulima na wakulima wa Kijiji cha Isikizya (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel.   Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Uyui, Hadija Makuwani akizungumza na wakulima kabla ya kuzindua shamba darasa la mbegu ya mihogo katika Kijiji cha Isikizya.
   Wakulima wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Mkulima, Gervas Fungameza akiuliza swali.
   Mkulima Said Mirambo wa Kijiji cha Isikizya akiuliza swali.
   Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielekeza ubora wa mbegu ya mihogo aina ya mkombozi jinsi ya kuipanda
   Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Hadija Makuwani akizindua shamba darasa hilo kwa kupanda mbegu ya mihogo.
   Diwani wa Kata ya Isikizya akipanda mbegu hiyo.
   Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Uyui, Hamphrey Kilua akizungumza na wanakikundi cha Mapambano kabla ya kuzindua shamba la Viazi lishe katika Kijiji cha Iberamilundi.
   Wanakikundi cha Iberamilundi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wanakikundi cha Mapambano cha Kijiji cha Iberamilundi namna ya kupanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa.
   Mwenyekiti wa kikundi hicho, Jumanne Said Mnubi 
  akipanda mbegu hiyo.
   Katibu wa Kikundi hicho, Clementina Nyamizi akipanda 
  mbegu katika shamba darasa.
  Wanakikundi cha Upendo cha Kata ya Magiri wakiwa na mbegu zao mkononi za Viazi lishe

  Na Dotto Mwaibale, Uyui Tabora

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora imezipokea kwa mikono miwili mbegu bora za mahindi aina ya Wema, Viazi lishe na mihogo zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

  Mbegu hizo zimetolewa katika vijiji vitano vya wilaya hiyo kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa ambavyo vimetajwa kuwa ni kijiji cha Isikizya kilichopo Kata ya Isikizya ambacho kitakuwa na shamba darasa la zao la mihogo, Ibelamilundi ambacho pia zao lake ni mihogo, Kijiji cha Kigwa ambacho zao lake ni Viazi lishe, Igalula ambacho kitapandwa mahindi na Magiri ambacho kitakuwa na shamba darasa la zao la Viazi lishe.

  Akizungumza wakati wa kupokea mbegu hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Hadija Makuwani alisema wao kama wilaya wamezipokea mbegu hizo kwa mikono miwili na watazifanyia kazi ili waweze kupata mazao yenye tija.

  "Kwa kweli tunawashukuru sana COSTECH na OFAB kwa kutuletea mbegu hizi kwani tuna imani zitatuondelea changamoto ya kupata mazao machache kutokana na kutumia mbegu za kienyeji zilizozoeleka kwa wakulima wetu" alisema Makuwani.

  Makuwani alisema hata yeye kwa kuwa ni mkulima anaomba apatiwe mbegu hizo ili akazipande kwenye shamba lake ili hapo baadaye nawe aweze kusambaza mbegu hiyo.


  Diwani wa Kata ya Isikizya, Ally Mtelela alisema mbegu hizo zitazidisha ari kwa wakulima hao na wataondokana na kilimo kisicho na tija ambacho walikuwa wakitumia mbegu ambazo zilikuwa zikishambuliwa na magonjwa.

  Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura aliwaambia wakulima hao kuwa hekta moja ya mihogo iwapo watalipa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wataweza kupata tani 25 hadi 32 na kwa zao la viazilishe watapata tani 7 hadi 9 kwa hekta moja.

  Alisema matokeo hayo watayapata endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea hivyo wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya mihogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye Viazi lishe wanapata tani moja hadi tatu.

  Kibura alisema Viazi lishe hivyo aina ya kabode vina vitamini A ambavyo ni muhimu kwa watoto kwa lishe na rangi yake ni vya njano na vinaisaidia serikali kuacha kutumia matone ya vitamini A badala yake mtu akivila anapata vitamini hiyo moja kwa moja.

  Akizungumzia kuhusu mbegu Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hizo ya mihogo aina ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana ina uwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa kama ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima na ya mahindi ikistahimili hali ya ukame na kutoa mazao mengi.

  Mutagwa aliwaomba wakulima hao kuyatunza mashamba hayo ambayo yamegharimu fedha nyingi hadi kukamilika kwake hivyo wayaendeleze kwa ajili ya kuja kutoa matunda kwa wakulima wa wilaya hiyo na kupata chakula cha kutosha na ziada kuuza.

  Mkulima Clementina Nyamizi wa Kijiji cha Iberamilundi ambaye ni Katibu wa Kikundi cha Mapambano alisema wanaamini mbegu hizo zitawatoa katika umasikini na kuwa watazitunza na kuzilinda na wataachana kabisa na mbegu za kienyeji walizokuwa wakizitumia zamani.

  0 0

   Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga ukuta katika kituo cha afya Mganza Halmashauri ya Wilaya Chato.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akichanganya mchanga na simenti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mganza (Chato) alipofanya ziara ya kikazi ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.
  Akina mama wa kijiji cha Ilyamchele Wilayani Chato wakishiriki katika ujenzi wa vyumba viwili na Ofisi shule ya Msingi Ilyamchele  kwa kusogeza matofali kwa mafundi wa ujenzi.
  Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kuchimba msingi wa kujenga vyumba viwili na ofisi na wananchi wa kijiji cha Ilyamchele (awapo kwenye picha)katika uzinduzi wa kampeni ya kujenga vyumba vya madarasa na zahanati Wilayani Chato.

  NA JOEL MADUKA
  Mkuu wa Mkoa wa Geita amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa Zahanati Wilayani Chato ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Wilayani humo.


  Mhandisi Robert Gabriel amezidua kampeni hiyo kwa kushirikiana na wananchi kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa viwili pamoja na Ofisi katika shule ya msingi Ilyamchele ambayo inaongezeko la wanafunzi 2,212 kutoka 1,700. Darasa la pili linawanafunzi 407 ambao wanasoma kwa awamu mbili hivyo, kufanya shule hiyo kuwa na mahitaji ya vyumba vya madarasa 28.


  Akizungumza na wananchi baada ya kuchimba msingi Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Serikali inataka watoto wa Ilyamchele wafanane na watoto wa maeneo mengine kwa kukaa katika vyumba vizuri vya kisasa vyenye miundombinu ya kutosha na walimu wa kutosha. Hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote kushirikiana na viongozi wote katika utekelezaji wa miradi hii ili kumaliza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati.


  Aidha, Mkuu wa Mkoa amendelea na ziara hadi kijiji cha Mganza ambapo ameshiriki katika ujenzi wa kituo cha afya Mganza ili kuona hali ya wananchi kupata huduma katika vijiji inaimalika kwa kujenga Zahanati na vituo vipya vya afya.


  Miradi hii inatekelezwa na vikundi vya mafundi walioungana kwa kujitolea kufanya kazi hiyo pasipo kuwa na malipo isipokuwa kupatiwa chakula wanapokuwa katika eneo la kazi. Wananchi na wadau wanashiriki kwa kuleta maji, mchanga, sementi, kokoto na kushiriki katika ujenzi.   Mafanikio haya yanatokana na juhudi za Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa baada ya kuwasili mkoani Geita baada ya uteuzi wake aliamua kutoa semina kuhusu mikakati na njia za kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Tarafa, Maafisa elimu wa Wilaya na Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya zote.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  Bungeni Mjini Dodoma Novemba 8, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahi jambo na Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 8, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Geita, Upendo Peneza, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza katika mahojiano maalum ikiwa nisehemu ya maandalizi ya Kipindi cha Amka Badilika kitakacho kuwa kinarusha hewani na Chaneli mpya ya Filamu za Kiswahili za Tanzania ya JTV hivi karibuni. Kushoto ni Mtangazaji wa kipindi hicho Saitus Mtimbe.
  Mtangazaji wa Kipindi cha Amka Badilika kitakachokuwa kikirushwa hewani kupitia chaneli mpya ya TV ya JTV Bw. Saitus Mtimbe akimuuliza swali Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza katika mahojiano maalum ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kipindi hicho jana jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiagana na Mtangazaji wa Kipindi cha Amka Badilika kitakachokuwa kikirushwa hewani kupitia chaneli mpya ya TV ya JTV Bw. Saitus Mtimbe mara baada ya kumaliza mahojiano maalum ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Kipindi hicho jana Jijini Dar es Salaam.Picha na: MAELEZO

  0 0

  Kwa kutambua umuhimu wa afya kwa Wananchi ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM, imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha KALEMBO kilichopo katika kata ya kihungu wilayani mbinga mkoani ruvuma.

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

  Serikali imewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuwachukulia hatua wakandarasi wa maji wanaokiuka mikataba walioingia kwa kuchelewa kutekeleza miradi hiyo.


  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mufindi Kusini Mendrad Lutengano Kigola juu ya lini Serikali itamaliza kujenga mradi wa Kata ya Mtwango katika Vijiji vya Sawala, Mtwango, Rufana na Kibao. 

   “Viijiji vya Sawala, Mtwango, Rufana na Kibao katika kata ya Mtwango ni miongoni mwa vijiji 12 vilivyopendekezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kupatiwa huduma ya maji kupitia programu ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijjini,” alisema Awezo.

  Aliendelea kwa kusema, utekelezaji wa mradi huo ulianza Juni 01, 2015 na ulitakiwa kukamilika Juni 01, 2016 kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.36 ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni ujenzi wa miundombinu ya maji katika kijiji cha Sawala pekee ambapo hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 50.

  “Hadi mwezi Novemba, 2016 mkandarasi alikuwa hajakamilisha kazi na hivyo Halmashauri kuamua kuvunja mkataba na halmashauri ilitangaza upya zabuni kwa ajili ya ukamilishaji wa kazi zilizobaki,” alifafanua Aweso.

  Amesema kuwa, mkandarasi mwingine amepatikana na utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza Desemba, 2017 kwa muda wa miezi 12 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.81.

  Kutokana na ucheleweshaji wa mradi huo, Aweso amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwachukulia hatua wakandarasi wa maji ambao hawatekelezi miradi yao kwa muda uliopangwa ambao kwa kiasi kikubwa unawaathiri wananchi wanaohitaji huduma ya maji kutokana na mradi kutekelezwa kwa muda mrefu.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo – MAELEZO - DODOMA

  Serikali imesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 Jeshi la Polisi limetenga jumla ya shilingi  Bilion 2.2 kwa ajili ya kupunguza madeni ya Wakandarasi waliotekeleza miradi mbalimbali ya Jeshi hilo.

   Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni leo Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi  Jaku Ayoub kuhusu madai ya Mkandarasi aliyejenga vituo vya Polisi Mkokotoni Unguja na Madungu.

  Mhandisi Masauni ameeleza kuwa fedha hizo zilizotengwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Mkokotoni ambao umetengewa jumla ya shilingi  Milioni 200 ikiwa ni sehemu anayodai mkandarasi huyo.

  “Serikali inatambua madeni ya Wakandarasi wote ikiwemo Albatna Builing Contractor na ina nia ya dhati ya kuyalipa madeni yote ya Wakandarasi na washauri elekezi waliohusika katika miradi mbalimbali ikiwemo miradi iliyohusisha Jeshi la Polisi,” amefafanua Mhandisi Masauni.

  Wakati huohuo Mhandisi Masauni amesema kuwa, Serikali imekuwa na mpango wa kupeleka fedha za Maendeleo kwa ajili ya ukarabati na ununuzi wa samani katika Magereza nchini ikiwemo Gereza la Karanga.

  “Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inatekeleza mpango wa muda mrefu wa kuyaboresha majengo hayo kwa kuyafanyia ukarabati mkubwa unaolenga kuyaimarisha, kuyaboresha na kuyafanyia upanuzi,” amengeza Mhandisi Masauni.

  Aidha amesema kuwa, kutokana na ufinyu wa bajeti fedha hizo zimekuwa zikitolewa kwa awamu katika Magereza mbalimbali nchini ili kufanikisha uboreshaji wa majengo hayo.

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Waziri wa Madini , Angela Kairuki amesema kuwa serikali inataraji kupata mrabaha Zaidi katika madini ya Almasi yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K Nyerere kutoka kwa Kampuni ya Williamson Diamond iliyokuwa ikitaka kutoroshwa nchini kwenda nchini Ubelgiji.

  Waziri kairuki amesema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wakati akitoa ripoti ya Wizara ya Madini juu ya mzigo huo wa Almasi kutoka kampuni ya Williamson Diamonds.

  “tarehe 20/10/2017 almasi hizo zilisafirishwa kwenda ubelgiji na serikali ilituma maafisa wake kusimamia uuzwaji wa alamasi hizo ambapo tarehe 7/11/2017 almasi hizo ziliuzwa kwa dola za Marekani 10,261,227.76 hivyo thamani hii ni ongezeko la Dola za Marekani 2,069,582.77 sawa na asilimia 20.16%”amesema.

  Amesema kutokana na ongezeko hilo baada ya almas kuuzwa serikali itapata mrabaha Zaidi ambao ni mwisho kiasi cha Dola za Marekani 124,174,.97 na ada ya ukaguzi Dola za marekani 20,695.83 ambayo jumla yake ni dola za Marekani 144,870.80 sawa na shilingi Milioni 325.525 hivyo jumla ya mapato yote ya serikali kutokana na mauzo ya almasi hizi ni Dola za Marekani 718,288.95

  Aidha waziri kairuki amesema katika mzigo huo walikuta Almasi moja yenye rangi ya pinki ambayo ni adimu kupatikana na yenye uzito wa karatani 5.92 na kuuzwa kwa dola za marekani 2,005,555.00 sawa na shilingi Bilioni 4.51 .

  Alimaliza kwa kusema kuwa anawahakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea kuismamia kwa umakini rasilimali zetu za madini ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inanufaika ipasavyo.
  Waziri wa Madini Angela Kairuki akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ripoti ya faida iliyopata serikali katika Madini ya Almas kutoka mgodi wa Wiliamson Diamonds Ltd iliyokamatwa uwanja wa ndege wa Jk Nyerere.
  Waziri wa Madini Angela Kairuki akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ripoti ya faida iliyopata serikali katika Madini ya Almas kutoka mgodi wa Wiliamson Diamonds Ltd iliyokamatwa uwanja wa ndege wa Jk Nyerere.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini . Prof.Simon Msanjila akitoa ufafanuzi wa kitaalmu juu ya madini hayo yaliyouzwa huko ubelgiji.
  Kamishana wa Madini Mhandisi Benjamini Mchwampaka akizungumzia juu ya madini hayo yanavyoweza kuliongezea pato taifa.
  Wahariri wa gazeti la Jamhuri Mkinga Mkinga na Deodatusi Balile wakiteta jambo katika mkutano huo

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa George Kyando kuwaweka pembeni Mkuu wa Usalama barabarani wa Wilaya Inspector Suleiman Africanus pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa Inspector Michael Mwakasungula ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma kadhaa zilizoelekezwa dhidi yao.

  Agizo hilo amelitoa wakati akijibu kero za madereva wa bajaji na bodaboda wapatao 4352 kwa mkoa mzima waliowakilishwa na wenzao wa mjini Sumbawanga baada ya kukutana nao na kusikiliza vilio vyao katika Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

  Madereva 13 walipata nafasi ya kumuelezea Mh. Wangabo kero wanazopata wakiwa barabarani huku miongoni mwa kero hizo ambazo ni pamoja na kupokea rushwa, uonevu usio wa lazima barabarani na kuwaweka mahabusu kwa visingizio mbalimbali zilielekezwa kwa maafisa hao wa usalama barabarani.

  “Hawa wawili hawa na tuhuma mlizozitoa huenda zina ukweli, RPC nakuagiza nenda kazichunguze hizi tuhuma zote zilizotolewa hapa kwa kina na nyinyi muwe mashahidi kwenda polisi kutoa shuhuda zenu, halafu uchukue hatua stahiki, lakini wakati huo huo unapozichunguza hizi tuhuma wao uwaweke pembeni, uwape kazi nyingine,”

  Amesema kuwa hakuna mtendaji wa serikali ambaye amepangiwa sehemu akae milele na milele na kuwa mtumishi asijidanyanye kwamba bila ya yeye kazi za serikali haziwezi kwenda huku akijitolea mfano kuwa yeye ni Mkuu wa Mkoa wa 15 tangu kuanzishwa kwa Mkoa huu mwaka 1974, wote walionitangulia wamepiga kazi wameondoka nae ataondoka.

  Aidha, Mh. Wangabo amewasisitiza madereva hao kusomea sheria za barabarani na kupata leseni ilikupunguza ajali za barabarani katika Mkoa wa Rukwa huku akiwapongeza kwa takwimu zinzoonyesha kupungua kwa ajali hizi ukilinganisha na mwaka 2016.

  Katika kulisisitiza hilo Mh. Wangabo alimualika mwalimu wa mafunzo ya usalama barabarani ili kutoa mafunzo hayo ya siku 3 bure kwa madereva hao kwa lengo la kutokuwa na ajali katika Mkoa wa Rukwa.huku akimpa miezi 7 kamanda wa polisi mkoa kuhakikisha bodaboda wote 4352 wanakuwa na leseni na vitambulisho.

  Kwa upande wake kamanda wa polisi Mkoa ACP George Kyando ameeleza kuwa kwa ajali za bajaji na bodaboda mwaka 2016 kulikuwa na ajali 18 huku 11 zikisababisha vifo vya watu 20 wakati mwaka 2017 kuemtokea ajali 9 huku 5 zikisababisha vifo vya watu 7.

  Yona Mwangoka ni mmoja wa madereva wa bodaboda aliyedai kuwa na ushahidi wa video unaoonyesha ukusanyaji wa shilingi 40,000 kuwapa polisi ili kuachiwa kwa makosa mbalimbali huku risiti zao zikionesha shilingi 30,000, fedha ambazo zilikusanywa na kiongozi wa boda boda baada ya boda boda hao kukamatwa kwa kosa la kumpiga askari wa usalama barabarani tukio lililotokea siku mbili kabla ya Mkutano huo. 
   Baadhi ya Bajaji zikiwa zimepaki katika uwanja ulipofanyikia Mkutano wa madereva wa Bajaji na Bodaboda na Mkuu wa Mkoa. 

   Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa ACP George Kyando akitoa elimu ya usalama barabarani na kujibu baadhi ya kero zilizotolewa na madereva wa Bodaboda na bajaji wa Manispaa ya Sumbawanga. 
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na madereva wa Bodaboda na Bajaji wa Manispaa ya Sumbawanga katika uwanja wa Nelson Mandela.
  baadhi ya bodaboda zikiwa zimepaki uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.

  0 0


  0 0

  Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amewatoa hofu watanzania kuhusu ongezeko la Deni la Taifa akisisitiza kuwa Deni hilo ni himilivu.

  Bw. James amesema hayo Jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari wakati wa hafla fupi ya kutia saini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Shilingi bilioni 340 uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya Mradi wa kuendeleza utalii kwa vivutio vilivyoko katika ukanda wa kusini mwa Tanzania ujulikao kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW)

  Alikuwa akitolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya watu na vyombo vya habari vinavyozungumzia Deni la Taifa kwa kutumia neno Deni la Taifa “linapaa”

  Katibu Mkuu huyo ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali alisema kuwa Deni la Taifa ni himilivu kwa kutumia viwango vya kitaifa na kimataifa kwamba ili nchi iwe katika hatari ya kukua kwa Deni lake la Taifa inabidi lifikie asilimia zaidi ya 50 lakini kwa Tanzania kiwango cha deni hilo ni asilimia 32.

  “Deni letu lingekuwa linapaa, hata Benki ya Dunia wasingekubali kutukopesha kwa maana hiyo tukitaka kukopa tutafanya hivyo kwa kuwa tuko chini katika viwango vya ukopaji kwa asilimia zaidi ya 18” alisema Bw. Doto James.

  Kwa hiyo nawaomba hili mlichukue muuelimishe umma wa watanzania kwamba deni la Taifa ni stahimilivu, nchi inakopesheka vizuri.Novemba 7, 2017, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bungeni mjini Dodoma Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maanndalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 alisema kuwa Deni la Taifa limefikia dola za Marekani milioni 26,115.2 mwezi Juni mwaka 2017.

  Dkt. Mpango alieleza kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 17 ikilinganishwa na dola milioni 22,320.76 katika kipindi kama hicho mwaka 2016.Alisema ongezeko hilo lilichangiwa na mikopo mipya iliyochukuliwa ili kugharamia miradi ya maendeleo kama vile: Standard Gauge Railway; Strategic Cities; mradi wa usafirishaji Dar es Salaam (DART) na kupanua upatikanaji wa maji safi Dar es Salaam. 

  Deni hilo la Taifa linajumuisha deni la Serikali lililofikia dola za Marekani milioni 22,443.70 na deni la sekta binafsi la dola za Marekani milioni 3,671.50. Pamoja na ongezeko hili, viashiria vyote bado vinaonesha kuwa deni la Taifa ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu huku uwiano kati ya deni na Pato la Taifa umefikia asilimia 31.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.

  0 0


  Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira (kushoto) Mh. Antony Mavunde (Mbunge), akimkabidhi mshindi wa 14 wa mchezo wa tatu Mzuka Bw. Robert A. Changadiko(45), hundi ya shilingi milioni sitini , Mjini  Dodoma.
  Mshindi wa droo ya 14 ya Tatu Mzuka Bw.Robert A. Changadiko (kulia)aliyejishindia donge nono la shilingi milioni sitini wiki hii, akiwa na rafiki yake bwana Bw. Daudi Mwangoto (katikati), ambaye alizawadiwa shilingi milioni moja kutoka katika promosheni ya cheza na washkaji shinda na washkaji ya Tatu Mzuka, kushoto ni Bw.Edwin Kawito ni mshindi wa Tatu Mzuka droo ya kumi (10) aliyejishindia shilingi milioni sitini.
  Mshindi wa shilingi milioni sitini kutoka kijiji cha Msembata (Dodoma)Bw.Robert A. Changadiko mwenye umri wa maika 45, ambaye ni fundi minara,akifurahia ushindi wake.
   
  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mheshimiwa Anthony Mavunde leo amemkabidhi kitita cha shilingi Milioni 60 mshindi wa droo ya Tatumzuka Bwana Robert Changadiko ambaye alijishindia kiasi hicho katika ‘Jackpot’ ya wiki hii katika droo ya kusisimua iliyoonyeshwa siku ya jumapili kupitia vituo vya runinga kote nchini.

  Bwana Changadiko ambaye anafanya kazi kama fundi minara mjini Dodoma alielezea furaha yake juu ya ushindi huo ambao hakuutegemea na akaishukuru Tatumzuka kwa kutimiza hitaji lake la pesa wakati alipokuwa akizihitaji zaidi.

  "Niliamua kucheza Tatu Mzuka kutokana na matatizo niliyokuwa nayo ya kifedha ambapo nilihitaji fedha za haraka ili kukidhi mahitaji hayo. Kwakweli nina furaha kubwa sana na nashukuru kwamba nilijaribu bahati na ikatimia” alisema.Mavunde alimpongeza mshindi kwa kushinda kiasi hicho na Tatu Mzuka kwa ajili ya kuendelea kutengeneza mamilionea na kubadilisha maisha ya watu.

  "Ninakushauri kwamba kabla ya kuanza kutumia pesa yako,tenga muda kufikiri namna utakavyotumia fedha yako ili utimize malengo yako na ili pesa uliyojishindia ilete mabadiliko ya kweli katika maisha yako." Mheshimiwa Mavunde alishauri.Mheshimiwa. Mavunde alihitimisha kwa kusisitiza kwamba hizi pesa ambazo watu wanajishindia kupitia Tatumzuka ni fursa hasa kwa vijana kujitengenezea ajira na kubadilisha maisha ya wale walio karibu yao. 

  Afisa wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bi Patty Mtatiro alielezea kwamba Tatu Mzuka hadi sasa imetengeneza mamilionea 120 na kutoa zaidi ya shilingi bilioni 5.3. Akasema kwamba sio hivyo tu, tarehe 19 Novemba ambapo ni wiki mbili kutoka sasa Tatumzuka kupitia SUPA Mzuka Jackpot itatoa milioni 150 za uhakika kwa mshindi atakayejishindia.

  " Kwa sasa unaweza kushinda kwa njia 3 kwa kucheza mara moja tu kwa shilingi 500. Tatu Mzuka inakupa nafasi ya kushinda hadi Tz 6, 000,000 masaa 24 kwa siku. Kila Tzs500 unayoitumia inakupa nafasi ya moja kwa moja kuingia kwenye Mzuka Jackpot ya kila wiki ambapo unaweza kushinda zaidi ya shilingi Milioni 60. Namna ya tatu ni kupitia droo ya Supa Mzuka Jackpot ambapo dau la uhakika la Milioni 150 litatolewa kwa mshindi. Hakuna dili kali zaidi ya hili "alisema Bibi Mtatiro.

  0 0

   
  Kampuni za utengenezaji filamu za Mashauri Studios na Novitech kwa kushirikiana na Clouds Plus pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania imezindua rasmi mfumo wa kutengeneza, kutangaza, kuonyesha na kusambaza filamu za kitanzania ujulikanao kama Bongohoodz. 

  Akizungumza na waandishi wa habari, mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu na Mkurugenzi wa Mashauri Studios, Paul Mashauri, mfanyabiashara ambaye katika miaka ya hivi karibuni alimua kuwekeza katika filamu alisema Bongohoodz inakuja kuwasaidia waandaaji wa filamu nchini kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa hasa DVDs kutokana na usambazaji wa sinema feki unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu. “Baada ya kutoa sinema kazaa sokoni ikiwa ni pamoja na One Month Date mwaka 2014, Maisha ni Siasa na Bongo na Fleva mwaka 2015 tumegundua kuwa wizi wa kazi za sanaa ‘piracy’ ni mkubwa sana.

   Lakini kupitia Bongohoodz, watayarishaji wa sinema nchini hawatahitaji tena kusubiri mapato yao au uwekezaji wao urudi kwa kuuza DVDs, "Kimsingi hata katika nchi zilizopiga hatua katika sinema unazungumzia Hollywood (Marekani), Bollywood (India), China Film Industry (China) na Nollywood (Nigeria), mapato makubwa yanatokana na uonyeshaji wa sinema katika majumba ya sinema au ‘theaters’ wao wanaita ‘Box Office’. 

  Kwa sababu wizi wa kazi za sanaa upo dunia nzima," alisema Mashauri na kuongeza. "Lakini mapato ya kwanza wanayopata waandaaji wa sinema au ‘production houses’ yanatoka ‘Box office’ au katika nyumba za kuonyesha sinema. Ndio maana sisi tutasema, kwanini tusionyeshe sinema hizi nchi nzima katika matamasha makubwa ambapo watanzania watapata kuona sinema zinazoburudisha na kufundisha kwa bei nafuu kabisa huku wakifurahia vyakula mbalimbali, muziki, kisha filamu?” 

  Mashauri alisema kuwa wameanza jitihada za makusudi za kutangaza sinema hizi ikiwa ni pamoja na kuwatangaza wasanii na wazalishaji wa sinema,“Dunia nzima waigizaji wenye majina makubwa ndio wanaovutia walaji au wanunuzi wa filamu, hata kwetu imezoeleka hivyo. 

  Lakini ili muigizaji awe mkubwa lazima kazi yake ionekana, "Kwa msingi huo na kwa ushirikiano wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na wadau wetu Clouds Plus, tumeanzisha ‘reality show’ ijulikanayo kama ‘The Producers’ inayoruka Clouds Plus kupitia king’amuzi cha Azam Tv kila siku jumatatu hadi ijumaa saa moja mpaka saa moja na nusu usiku na marudio siku ya jumapili kuanzia saa nne asubuhi ambapo watanzania wataweza kuona namna sinema zinavyotengenezwa na wasanii wanavyofanya kazi zao," alisema Mashauri. 

  Mashauri alisema kupitia kipiendi hicho watu mbalimbali ambao wanandoto za kuwa waigizaji watajua nini wa natakiwa kufanya kwani wataona fursa ziliziopo katika tasnia ya uigizaji na changamoto zinazowapata waandaji na waigizaji. "Tunategemea kufanya kazi na waandaaji kumi kwa mzunguko wa miezi sita sita na kila Producer atatakiwa kuzalisha sinema ndani ya miezi sita na mchakato wa sinema yake utaonyeshwa katika reality show, sinema yake itatangazwa na kupelekwa sokoni," alisema Mashauri. 

  Naye Meneja wa Clouds Plus, Ramadhani Bukini, alisema Clouds Plus imeungana na Bongohoodz katika kufanikisha ukuaji wa soko la filamu nchini kwa kutoa fursa kwa wazalishaji wa sinema kuonyesha kazi zao na kuzipeleka sokoni kupitia matamasha. “Tumeungana na Bongohoodz tukiamini kuwa lazima kuwe na mbinu mbadala za kuuza sinema. Dunia imebadilika sana na huwezi kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Mfano, katika dunia ya leo, aina ya kompyuta zinazoongoza kwa kuuza duniani ni za Apple. 

  Watumiaji wa ‘computer’ hizi hawahamasiki kutumia DVDs. Inamaana tunakoelekea hata wenye deki za kuangalia DVDs ni wachache, "Watu wako kwenye simu za mikononi, ndio maana Clouds Plus ikaamua kuungana na Bongohoodz kuja na vyanzo vipya vya mapato kwa tasnia ya filamu Tanzania ikiwa ni pamoja na matamasha makubwa ya kuonyesha filamu. Kama imewezekana katika muziki tunaamini kabisa inawezekana katika filamu," alisema Bukini. 

  Naye mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Novitech ambayo inashirikiana na Mashauri Studios katika kutayarisha sinema, Mary Mgurusi alisema watanzania wasubirie kwa hamu kazi nzuri za filamu.

   “Tumeandaa sinema nzuri za kitanzania zenye maudhui tofauti tofauti ambazo tunaamini zinaburudisha na kufundisha. Tayari sinema ya Tatu Chafu imekamilika na tunatarajia kuizindua tarehe 16/12/2017 Mlimani City pamoja na Dar Live Mbagala. Baada ya uzinduzi huo, tunatarajia kuonyesha sinema hii nchi nzima katika mikoa mbalimbali. Zaidi ya Tatu Chafu zipo sinema nyingi katika maandalizi, mfano Tajiri kutoka India, What is Marriage, Rashid Snake Boy Matumla na School Bus," alisema Mgurusi.

older | 1 | .... | 1422 | 1423 | (Page 1424) | 1425 | 1426 | .... | 1903 | newer