Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

BOT YAWAJENGEA UWEZO WA KUTAMBUA NOTI BANDIA WATU WENYE ULEMAVU WA KUTOSIKIA WILAYANI CHATO

$
0
0
Bw,Patrick Fata ambaye ni Mhelimishaji kutoka BOT akielekeza na kutoa elimu namna ambavyo unaweza kutambua Noti bandia. 
Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarembe. 
Maafisa wa BOT wakifuatilia maelezo ya Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa BOT, Vicky Msina wakati alipokuwa akielezea juu ya elimu ambayo wanaitoa kwa viziwi. 
Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa BOT, Vicky Msina akielezea malengo ya kutoa elimu ya kuwawezesha viziwi kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti ili kuzitofautisha na noti bandia pindi wanapokuwa katika shughuli zao za utafutaji. 
Mwenyekiti wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (Kisuvita), Habibu Mrope akizungumza changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo watu ambao ni walemavu hususani wakati wanapokuwa wanakwenda kwenye huduma za kibenki. 
Bw,Patrick Fata ambaye ni Mhelimishaji kutoka BOT,akisisitiza swala la alama za fedha ambazo zinakuwepo kwenye noti. 
Kifaa ambacho kinatumika kuangalizia noti bandia na ile ambayo ni ya harari. 
Noti ambazo zinakuwa zimeharibiwa zikiwa kwenye mafungu fungu lenye rangi nyekundi ni elfu kumi na yenye rangi ya blue ni elfu tano. 


NA JOEL MADUKA,CHATO.

Benki kuu ya Tanzania (BOT)imekutana na kundi la watu wenye ulemavu wa kutokusikia na wale ambao hawaoni Wilayani Chato lengo likiwa ni kuwapatia na elimu ya utambuzi wa Noti bandia Wilayani humo.

Akizungumza kwenye semina ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa KKKT Wilayani Humo,Meneja msaidizi wa idara ya uhusiano wa BOT, Vicky Msina alisema elimu wanayoitoa imelenga kuwawezesha viziwi kutambua alama za usalama zilizopo katika noti ili kuzitofautisha na noti bandia wanapokuwa katika shughuli zao kwani mtu yeyote akikutwa na noti bandia ni kosa la jinai, hivyo wanawapa mafunzo ili wasikumbwe na kadhia hiyo.

“Ni muda sasa walituomba kuwapa mafunzo na hii ni kutokana na wengi wao kutokujua noti bandia wamekuwa wakijikuta wanabambikiwa na pia wanapo kwenda benki kupeleka fedha zao wahudumu huwadharau na wakati mwingine kwa wale wanao kwenda kuchukua fedha hupatiwa noti chafu jambo ambalo lilitusukuma kuwaelimisha juu ya hatua za kufuata ilikupatiwa haki zao za msingi kwenye huduma hizo,”alisema Msima.

Mwenyekiti wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (Kisuvita), Habibu Mrope alisema kuna tatizo kubwa la kutotambua noti bandia kwa Walemavu hali ambayo imechangia kuwarudisha nyuma kwani wanapokutwa na noti hizo huchukuliwa hatua za kisheria.

Hata hivyo kutokana na tatizo hilo Mkuu wa wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe aliwaahidi watu ambao wanamatatizo ya kutokusikia kufunguliwa kwa shule ambayo itawasaidia kujifunza lugha za alama kwania ya kuboresha mawasiliano kwenye jamii.

“Idadi ya wilaya yetu kuna Viziwi 347 ambapo ni sawa na asilimia 90 ya watu wenye ulemavu wa kusikia hawajui lugha za nyakati upekee idadi hii ni kubwa sana ni lazima Serikali ifanye jitihada za kuwa kwamua watu hawa ambapo kwa kushirikisha wadau mbali mbali, nitahakikisha ujenzi wa shule hiyo unaanza mara moja,”alisisitiza Tarambe

Kwa upande wake mmoja wa washirki wa semina hiyo, Issa Pastori, mkazi wa Buziku wilayani humo alishukuru kupatiwa mafunzo hayo na kwa upande wa suala la uanzishwaji wa shule maalum ya lugha za alama ameomba mchakato huo uanze haraka kwani ni mkombozi kwao.

DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro jana Ijumaa Novemba 3,2017 amewatembelea wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha Sayu kata ya Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kuwahamasisha kulima zao hilo kwa njia za kitaalamu/kisasa ili kilimo hicho kiwe na tija kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi.

Akizungumza katika kikao na wananchi wa kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo cha pamba,Matiro aliyekuwa ameambatana na wataalamu wa zao la pamba,aliwataka wakulima wa zao hilo wilayani humo kulima kisasa kwa kufuata kanuni 10 za kilimo ikiwemo kulima kwa kutumia kamba.

Alisema wananchi katika wilaya hiyo wamekuwa mstari wa mbele katika kulima zao la pamba lakini wamekuwa hawapati faida kutokana na kulima njia zisizo za kitaalamu.

“Tunataka kufanya kilimo biashara ili kiwe na tija,hatupati mazao ya kutosha kutokana na kutolima kitaalamu,naomba mwaka huu tuwasikilize wataalamu wetu wanatuambia nini,nataka tubadilishe maisha yetu kupitia pamba”,alisema Matiro.

Aliwashauri wananchi ambao hawana uwezo wa kunua mbegu za pamba wajiorodheshe majina yao,ijulikane wapo wangapi na wanahitaji mbegu kiasi gani ili serikali ya wilaya hiyo ione namna ya kuwasaidia ili waweze kulima kisasa.

“Tutaongea na wadau wa pamba ili tujue tunafanya nini,sasa hivi tunaingia katika msimu wa pamba,hatutaki pamba yetu kufanyiwa mambo yaliyokuwa yanafanyika huko nyuma,tunataka tuwe na chama cha ushirika ili hata tukiamua kuwapa mbegu wale walioshindwa waweze kupata kupitia chama chao cha ushirika”,alieleza Matiro.

“Kijiji hiki kinasifika kwa kilimo cha pamba na mazao mengine kama choroko na dengu,naomba mujitahidi kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo lakini msisahau kulima mazao ya chakula na muepuke kuuza chakula chote”,alieleza.

“Serikali haina shamba,jitahidini mnapolima mazao ya biashara limeni pia mazao ya chakula na mhakikishe mazao yale mnahifadhi kwa ajili ya chakula cha baadae”,aliongeza.

Aidha aliwahamasisha wananchi hao kupanda miti ili kukabiliana na tishio la jangwa mkoani Shinyanga ambapo kupitia kampeni ya Shinyanga Mpya,Mti Kwanza kila kaya inatakiwa kupanda miti kuanzia mitatu.

Katika hatua nyingine aliwataka wataalamu wa kilimo kukaa na wakulima na kuwashauri njia nzuri za kufuata katika kilimo.Mmoja wa wakulima katika kijiji hicho,Samwel Nkilijiwa alieleza kuwa tatizo kubwa wanalokabiliana nalo kuwa ni pembejeo ambao dawa za maji zinazotumika kuua wadudu hazijafanyi kazi kama ilivyokuwa kwa dawa za mafuta ambazo sasa hazitumiki.

“Hii dawa ya maji wanayotupa haiui wadudu wanaoshambulia pamba yetu,kwanza inawasha sana huwezi hata kumsogelea mke wako,tunaomba ile dawa ya mafuta tuliyokuwa tunaitumia zamani,hii haifai”,aliongeza Nkilijiwa.

Hata hivyo Mkaguzi wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama alisema tatizo la wakulima kulalamikia dawa ya maji inatokana na kipindi cha nyuma wafanyabiashara wa dawa hiyo walikuwa wanachakachua dawa hiyo na kuonekana feki na sasa serikali imechukua hatua hivyo hakuna dawa feki kinachotakiwa wakulima wafutae ushauri wa wataalamu wa pamba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sayu kata ya Pandagichiza leo akiwahamasisha kufuata njia za kisasa kulima zao la pamba-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Sayu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza wananchi kulima mazao ya biashara pamoja na yale ya chakula
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Mkulima wa Pamba Nicholaus Selena akieleza kero yake kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkulima wa Pamba Samwel Nkilijiwa akieleza changamoto wanayopata pale wanapotumia dawa ya maji ya kuua wadudu ambapo alisema dawa hiyo haiui wadudu hivyo kuomba dawa ya mafuta waliyokuwa wanatumia zamani 
Afisa Kilimo wa wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu akitoa ufafanuzi kuhusu kilimo cha pamba
Diwani wa kata ya Pandagichiza Charles Masele Kabogo akizungumza katika kikao hicho
Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Charles Maugira akizungumza katika kikao hicho
Mkulima wa pamba katika kijiji cha Sayu Ezekiel Nchange akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada ya kumpatia shamba mkuu huyo wa wilaya ili alime zao la pamba katika kijiji hicho
Mkaguzi wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama akitoa elimu kwa wakulima wa pamba juu ya njia ya kisasa ya kulima zao hilo
Mkaguzi wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama akionesha kamba zinazotakiwa kutumika katika kilimo cha pamba
Kaimu mwenyekiti wa kijiji cha Sayu Paul Selena akizungumza katika kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipokelewa katika shule ya msingi Sayu kwa ajili ya kupanda mti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya msingi Sayu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Shinyanga Mpya Mti Kwanza ambapo wananchi wamekuwa wakihamasishwa kupanda miti ili kukabiliana na hali ya jangwa mkoani Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea na zoezi la kupanda mti katika shule ya msingi Sayu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Sayu ambapo aliwasisitiza kuwa mabalozi wa upandaji miti katika jamii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na baadhi ya viongozi na wananchi wa kijiji cha Bulambila kata ya Mwalukwa ambapo pia ni maarufu kwa kilimo cha zao la pamba ambapo pia aliwahamasisha kulima zao hilo kwa njia za kisasa ili lilete tija
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiteta jambo na Diwani wa kata ya Mwalukwa,Ngassa Mboje ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WANAWAKE BARANI AFRIKA WAKUTANA TANZANIA KUJADILI AMANI YA BARA LA AFRIKA

$
0
0
Aliyekuwa katibu Mkuu wa Mkutano wa Beijing , Getrude Mongela akizungumza wakati wa mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Muasisi wa Mkutano wa Wanawake juu ya Amani na kutatua matatizo Barani Afrika, Dkt. Basirat Nahibi akizungumza juu ya suala la wanawake wa bara la Afrika kukutana kujadili na kuandaa upatanishi juu ya mgogoro wa kisiasa unaondelea nchini Kenya.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Muuandaaji wa mkutano huo kwa hapa Tanzania , Khadija akimkabidhi kitabu Aliyekuwa katibu Mkuu wa Mkutano wa Beijing , Getrude Mongela
Mwanahabari Mwanamke mkongwe nchini Radhia Mwawanga akichangia hoja katika mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mjumbe wa mkutano huo Madam Fanta Dissa Berthe akichangia jambo mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam jana
Mhariri wa jarida la mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika, Fatma Othman Moma akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Viongozi Wanawake walioshiriki Baadhi ya Viongozi Wanawake walioshiriki mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, wakifuatilia kwa makini,mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
Baadhi ya Viongozi Wanawake walioshiriki mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam jana wakisikiliza mada zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano huo.
Picha ya Pamoja ya Baadhi ya Viongozi Wanawake walioshiriki mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani Afrika.

MPANDA MILIMA MASHUHURI DUNIANI ,JUANITO OIZARZABAL APANDA MLIMA KILIMANJARO.

$
0
0
Mmoja wa wageni wanaofanya utalii kwa njia ya Baiskeli ,Ramon Abecia akiandaa baiskeli yake kabla ya kuanza safari ya kuelekea kilele cha Uhuru.
Mpanda milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal(katikati) raia wa Ureno na wenzake ,Ramon Abecia (kulia) na Eduardo Pascuaz wakijiandaa kuanza safari ya siku tano kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mpanda milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal(katikati) raia wa Ureno na wenzake ,Ramon Abecia (kulia) na Eduardo Pascuaz wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa safari hiyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa ,Mario Martos pamoja na waongoza watalii ,Ally Chuwa na Elvas Mlengwa kabla ya kuanza safari ya siku tano kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro
Eduardo Pascuaz akifunga kofia ngumu kabla ya safari ya kuelekea Kilele cha Uhuru kuanza.
Mpanda milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal(katikati) raia wa Ureno na wenzake ,Ramon Abecia (kulia) na Eduardo Pascuaz wakijiandaa kuanza safari ya siku tano kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Juanito Oiarzabal na wenzake ,Ramon Abecia  na Eduardo Pascuaz wakiianza changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Muongoza Watalii,Elvas Mlengwa wa kampuni ya Karibu Adventure akishusha Baiskeli maalumu kwa ajili ya zoezi la kupanda Mlma Kilimanjaro.
Baiskeli Maalumu zinazotumika kwa ajili ya kupanda Milima .
Muongoza Watalii ,Ally Chuwa wa Kampuni ya Karibu Adventure akiweka kumbukumbu za vipimo vya mratibu wa Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,Mario Martos  wa Safari Bike Africa kabla ya kuanza kupanda Mlima.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MPANDA milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal raia wa Ureno na wenzake wawili wameanza safari ya siku tano ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia lango la Kilema ikiwa ni aina mpya ya utalii iliyoanza kushika kasi katika hifadhi hiyo.

Hatua hiyo inatokana na jitihada za shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kueendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,kwa kuanzisha aina mpya ya bidhaa za utalii ili kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.

Miongoni mwa bidhaa hizo ni pamoja na zile zilizoanzishwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimajaro (KINAPA) ya kuzunguka mlima kwa kutumia Parachuti pamoja na kupanda Mlima kwa kutumia Baiskeli, utalii ambao umeanza kushika kasi.

Juanito Oiarzabal ambaye tayari ameweka rekodi nyingi duniani na kuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu kijulikanacho kama World Guinness Book amepanda mlima Kilimanjaro na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia kwa kutumia Baiskeli .

Mkurugenzi wa Utali wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA ) Ibrahim Musa amesema Oiarzabal atakuwa Mreno wa kwanza kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli na kwamba aina hi ya utalii na rafiki kwa mazingira ya Hifadhi.

Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa inayoratibu wa changamoto hii a kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli,Mario Martos amesema hatua hii ni mwanzo wa kufungua aina hii ya utali katika Hifadhi za Taifa za Arusha na Saadan.

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro limeweka utaratibu wa kufanya vipimo kwa wapandaji wa Mlima kwa wanao tumia Baiskeli pia kabla ya kuanza safari ya kuelekea kileleni.

Juanito na wenzake wawili wameianza safari ya siku tano ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli wakipita lango la Kilema ambapo wanatarajia kupita katika Kilele cha Mawenzi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea kilele cha Uhuru.

DK. HAMISI KIGWANGALLA AAGIZA RASIMU YA SERA MPYA YA MISITU IKAMILIKE NDANI YA MWEZI HUU WA NOVEMBA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA SHERIA NA KUNUNI MPYA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA SEKTA HIYO

$
0
0
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma jana kwa ajili ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.

Na Hamza Temba - WMU
............................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza kukamilishwa haraka kwa rasimu mpya ya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 2016 ili kuwezesha upatikanaji wa Sera, Sheria na Kanuni mpya za usimamizi wa rasilimali za misitu nchini kwa ufanisi zaidi.


Ameagiza wataalamu wa Wizara hiyo kukamilisha rasimu hiyo mwezi huu wa Novemba na iwasilishwe kwake mapema mwezi ujao (Desemba) ili aweze kupata ushauri zaidi wa wataalamu wengine huru kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na baadaye kutungiwa Sheria na Kanuni za utekelezaji.


Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana mjini Dodoma wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa misitu iliyolenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.

“Natoa agizo mchakato huu ukamilike ndani ya mwezi huu wa 11, tarehe moja mwezi wa 12 mlete rasimu ambayo nyie wataalamu mmeridhika nayo, muiwasilishe kwangu mimi na Mhe. Naibu Waziri, na siku hiyo mtakayoiwasilisha kwetu mniletee timu ya wataalamu watakaonishauri kwenye maeneo mbalimbali.


“Pamoja na hao wataalamu washauri nataka watu wengine huru wahusike kwenye kunishauri, ili nipate picha ya watu wengine huru kabla hatujatengeneza andiko ambalo tutalipeleka kwenye kikao cha baraza la Mawaziri, waje wanishauri maeneo yanayotaji maboresho, kuongeza ubunifufu au kukazia zaidi”. Aliagiza Dk. Kigwangalla.


Alisema amelazimika kuharakisha zoezi hilo ili Sera hiyo ikamilike haraka iweze kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo ongezeko la watu linalosababisha misitu mingi kuteketezwa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kupitia shughuli za kilimo na uanzishwaji wa makazi mapya.


Alisema pamoja na misitu kuonekana inachangia kidogo kwa asilimia 3.5 kwenye pato la taifa, bado mchango wake ni mkubwa kuliko inavyochukuliwa hivi sasa. Alisema tafiti zilizofanywa awali hazikuzingatia mambo muhimu ikiwemo mchango halisi wa misitu kwenye upatikanaji wa maji ambayo huzalisha umeme, hunywesha mifugo na wanyamapori, matumizi ya majumbani na kilimo cha umwagiliaji.


Alisema ili kupata mchango halisi wa misitu kwenye uchumi mpana wa taifa letu, Wizara yake imeshaandaa andiko maalum kwa ajili ya kuendesha utafiti mkubwa wa kubaini mchango huo na kazi inayofanyika hivi sasa ni ya utafutaji wa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali kufanikisha utafiti huo.


Akizungumzia Uhifadhi Shirikishi Jamii, Dk. Kigwangalla alisema kwa zaidi ya asilimia 32 ya maeneo yote nchini yamehifadhiwa kisheria, hivyo njia rahisi ya kuyalinda ni kupitia ushirikishwaji wa wananchi. “Bila kufanya hivyo hatuwezi kusema tuna askari wa kutosha kulinda misitu yote, mbuga zote za wanyama au mapori yote tengefu nchini.


“Lakini nje ya maeneo hayo kuna maeneo ya vijiji ambayo pia yamehifadhiwa, yote haya huwezi kusema utayalinda kirahisi sana bila ushiriki wa wananchi, kuwaleta wananchi kwenye uelewa wa pamoja, kwamba tunahifadhi kwa faida yao.


“Tuwaelimishe, kwa mfano usipohifadhi misitu kiwango cha mvua kitashuka, usalama wa chakula utaathirika, upatikanaji wa maji safi na salama utaathirika, upatikanaji wa umeme nao pia utaathirika, hivyo tunahifadhi kwa faida ya jamii kwa ujumla”. alisema Dk. Kigwangalla.


Awali akiwasilisha mada kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini, Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha Sokoine - SUA alisema changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni ukataji holela wa miti ambapo takwimu za NAFORMA zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza hekta 372,000 za misitu kwa mwaka.


Alisema changamoto nyingine ni uchomaji moto misitu, uvunaji wa mkaa, uingizaji mifugo kwenye maeneo ya hifadhi, kukosekana kwa mpango bora wa matumizi ya ardhi, utegemezi uliokithiri kwenye mazao ya misitu, uanzishwaji wa makazi mapya na utegemezi wa nishati ya kuni. Alisema changamoto hizo zinahitaji Sera madhubuti za kukabiliana nazo.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa alisema, Rasimu hiyo ya Sera mpya ya Misitu itakamilika kwa wakati kama alivyoelekeza Waziri Kigwangalla na kwamba maoni yote ya wadau yatazingatiwa katika Rasimu hiyo.


Warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini Dodoma iliandaliwa kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Uendelezaji wa Nishati Endelevu za Kisasa Tanzania (TATEDO), Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFCG), Wizara ya Maliasili na Utalii na Ubalozi wa Switzerland nchini. 
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa  warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo. 
Baadhi ya wajumbe walioshiriki warsha hiyo wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi kuhusu nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya na mazingira muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi kuhusu majiko banifu ya mkaa muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika warsha hiyo.
Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli akizungumza katika warsha hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) akipokea zawadi ya nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya na mazingira kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi (wa tatu kushoto) muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa. 
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo. 
 Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha Sokoine - SUA akiwasilisha mada kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini katika warsha hiyo.
Picha ya pamoja.
Meza kuu, Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania, Charles Meshak (wa pili kushoto), Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Doto Biteko (kulia).
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandhishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo. 

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUSOMESHA WAUGUZI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Ssuluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Afya Mh.Ummy Mwalimu, huku wakitembea mapema leo wakati akiongoza a matembezi ya hisani kwa ajili ya kusomesha Wauguzi Wakunga , matembezi hayo ya kilometa 4.5 yalianzia kwenye viwanja  vya Green Grounds, Oysterbay jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).




Picha ya pamoja na Washiriki wa Matembezi hayo ya Hisani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo ameshiriki katika Matembezi ya Hisani ya Kilomita Nne na Nusu yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Green Ground- Oysterbay mara baada ya matembezi hayo, Makamu wa Rais alisema takwimu za vifo vya kina mama zimeongezeka, hivyo wazo la kusaida kuongeza idadi ya wakunga ambao watasaidia kupunguza vifo hivyo ni zuri sana.

Makamu wa Rais alisema “nimefarijika kusikia kuwa mwaka 2016 matembezi haya ya hisani yalikusanya wastani wa shilingi milioni 290 pesa ambayo iliwekwa katika fungu la kusomesha wauguzi wakunga wapya 75 katika mafunzo ya ngazi ya cheti” . Makamu wa Rais alionesha kufurahishwa na malengo yaliyowekwa kwa miaka miwili ijayo ya kukusanya kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kusomesha wakunga wauguzi 400 katika ngazi ya cheti na diploma kwas njia ya masafa.

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa moja ya chanzo cha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua ni ukosefu wa wataalam wa kuwahudumia. Takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya akina mama hawaendi kujifungua katika vituo vyetu vya kutolea huduma kutokana na kukosekana kwa wataalam wa kuwahudumia akina mama hao.

Makamu wa Rais aliwahakikishia wadau wote wa sekta ya afya kwamba serikali ipo nao bega kwa bega katika kuhakikisha wanaotaka kuwekeza katika sekta hii wanafanikisha malengo yao. Aidha, alisema serikali inaendeleza juhudi za kuinua uchumi kwa kuongeza idadi ya viwanda ikiwa ni pamoja na viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba ili kuongeza upatikanaji na uboreshaji wa huduma muhimu za afya kwa binadamu.

Makamu wa Rais aliiagiza Wizara ya afya iusimamie kikamilifu mwongozo unaotaka kila kifo cha mama na mtoto kinachotokana na matatizo ya uzazi kijadiliwe ndani ya saa 24 katika kituo au hospitali husika kwa lengo la kubaini chimbuko la kifo hicho na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi huduma zinazotolewa katika kituo husika. 
Mwisho,Makamu wa Rais aliwashukuru wadau ,wahisani na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye matembezi hayo na kuwaomba kuendelea kushiriki na kuchangia fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga wauguzi.

ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA

$
0
0
 Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, (kushoto), akiwa na balozi wa EU nchini, Mhe.Roeland van der Geer, wakati amkizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Novemba 3, 2017.(PICHA NA HABARI/K-VIS BLOG;Khalfan Said)
 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

ULE msemo wa kiswahili wa "mgeni njoo mwenyeji apone", unaweza kutumika kufatsiri neema ambayo taifa limepata kufuatia ziara ya siku mbili nchini ya Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, pichani juu.
Mhe. Mimica alianza ziara yake Novemba 2, kwa kutiliana saini makubaliano na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mjpango, ambapo EU imeahidi kutoa kiasi cha Euro milioni 50 ambazo zitatumika kupeleka umeme vijijini.
Serikali inapambana kuhakikisha vijiji elfu 12 (12,000) ambavyo bado havina umeme nchini vinapata huduma ya umeme ifikapo 2020.Kwa mujibub wa Afisa Habari wa EU hapa nchini Bi.Susanne Mbise, msaada huo wa Euro milioni 50 utasaidia kupeleka umeme kwenye vijiji 3,000.
Ziara ya Kamishna Mimica, ililenga kutembelea shughuli mbalimbali ambazo EU imekuwa ikifadhili,
Miongoni mwa maeneo ambayo Kamishna Mimica alitembelea ni pamoja na bandari ya Dar es Salaam, ambapo akiongea na uongozi wa bandari hiyo, Kamishna Mimica a,lieleza utayari wa EU katika kusaidia kub oresha bandari hiyo kwani ina msada mkubwa sio tu kwa Tanzania bali pia kwa nchi majirani.
Kamishna Mimica pia ametembelea kituo kinachosaidia vijana cha Nafasi Art Space kilichoko  Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo aliweza kusikiliza maoni yao na kujadiliana nao masuala mbalimbali yahusuyo changamoto za ajira na pia ukatili dhidi ya mtoto wa kike. "Kamishna Mimica amesema EU itatoa Euro  milioni 500 ili kusaidia kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto". amesema Bi. Mbise.
Kamishna huyo wa EU, alikutana na kujadiliana na makampuni makubwa ya kibinafsi ili kuona jinsi sekta binafsi inavyofanya shughuli zake hapa nchini na ziara hiyo ilimuwezesha pia kukutana na viongozi wa asasi za kiraia hapa nchini.
 Mhe. Mimica, akipokewa na Kaimu Mkurugezni Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA), Bw. Lazaro twange, alipotembelea bandari ya Dar es Salaam, Novemba 3, 2017. EU ni mdau mkubwa katika kjuisaidia TPA kuimarisha miundombinu yake.
 Mhe. Mimica akizun gumza na uongozi wa juu wa TPA.
 Mhe. Mimica akipeana mikono na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dotto James, baada ya kusaini makubaliano ambapo EU itatoa Euro milioni 50 kusaidia usambazaji umeme vijijini. Takriban vijiji 3,000 kote nchini vitafaidika na msaada huo. Serikali inapambana kuwafikishia umeme wana vijiji wa vijiji 12,000 a,mbavyo bado havijapata umeme na mpango huu umepangwa kukamilika 2020.
 Mhe. Mimica akiwa na mazungumzo na mabalozi wanaotoka nchi za EU.
 Mhe. Mimica akisalimiana na Afisa Habari wa EU hapa nchini, Bi. Susanne Mbise. wakati a,lipofika Wizara ya Fedha na Mipango kusaini msaada huo wa fedha Euro milioni 50.
 Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, (kushoto), akiwa na balozi wa EU nchini, Mhe.Roeland van der Geer, wakiwadsili Nafasi Art Space, Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo alifanya maxungumzo na vijana mbalimbali kuhusu changamoto za ajira, ukatili dhidi ya wanawake na namna gani wanavyokabiliana nazo.
 Bi. Nasra akielezea kuhusu kazi ya sanaa ya mikono inayofanywa na vijana wa Nafasi Art Space.
 Msanii Nancy, wa Nafasi Art Space, (kulia), akishirikiana na Nasra pia wa Nafasi Art Space, wakimpatia maelezo Mhe. Mimica kuhusu sanaa za mikono wanazofanya.
 Mhe. Mimica na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na vijana wanaojishughulisha na masuala ya sanaa na kuzuia ukatili dhidi ya wasichana na akina mama.
 Oscar Kimaro, (kulia), kutoka Restless Development, akizungumza kwenye mkutano na Mhe. Mimica uliofanyika Nafasi Art Space, Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Jasmina Milovanovic kutoka Save the Children na Rebeca Corey wa Nafasi Art Space.
 Mhe. Mimica, akizungumza jambo wakati akipatiwa maelezo na Rebeca Corey wa Nafasi Art Space.
 Mgunga Mwanyenyelwa ,kutoka kituo cha Baba Watoto, akizunhgumza kwenye mkutano huo na Kamishna Mimica.
 Kamishna alipata fursa ya kukutana na kuzunguzma na viongozi wa asasi za kiraia.
 Wasanii wa Nafasi Art Space wakifanya vitu vyao.
 Msafara wa Kamishna Mimica ukipita barabara ya Bagamoyo Novembe 3, 2017 kuelekea Mikocheni kituo cha Nafasi Art Space.
 Msafara ukiwasili  Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Msafara wa Mhe. Mimica ukiwa bandari ya Dar es Salaam.
 Msafara wa Mhe. Mimica ukiwa bandari ya Dar es Salaam.

TADB YATINGA HONG KONG KUTAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI KWENYE MITAJI NA MIRADI MIKUBWA YA KILIMO NCHINI KUPITIA "ONE BELT ONE ROAD"

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania hivi karibuni ilipiga hodi mjini Hong Kong kujadiliana na Taasisi mbali mbali za Hong Kong na China kuhusiana na fursa za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mitaji na uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwana Francis  Assenga walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa makampuni na taasisi kadhaa zikiwamo  Benki ya China; China Capital Fund Management (Hong Kong);  First Shanghai Capital Ltd; Mwakilishi wa China Africa Industrial Forum Ndugu Wenbao Tan ambaye ni Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha China.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation Bwana Takashi Kawasaki na Mkurugenzi wa China Biodiversity Conservation and Green Development Foundation Prof. Frederick Charles Dubee.

Miongoni mwa yaliyojiri katika mazungumzo hayo ni jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na fursa zilizopo kwenye Mikakati ya 'Silk Road Economic Belt and the 21st-century Maritime Silk Road', ujulikanao kama 'One Belt and One Road Initiative' (OBOR) ambapo kwa mujibu wa Mkakati huo, Tanzania ndio lango kuu la kuingilia Afrika kwa fursa hizo za kiuchumi na kibiashara toka Asia ambapo Tanzania inakuwa kama kiungo muhimu hivyo kuweza kunufaika zaidi ya nchi nyingine.

Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na kukuza uwekezaji kwenye miundombinu ya aina zote, viwanda vikubwa na vya kati, biashara kati ya Afrika na Asia, na Huduma mbalimbali.

Aidha, Bwana Assenga alikutana pia na akina mama wa shirika lisilo la kiserikali la kukuza uchumi kwa akina mama wa Hong Kong wanamiliki pia Shule ya Sekondari kama mchango wao kwenye huduma za jamii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bwana Francis Assenga nara baada ya kupitia Mchoro wa Ramani ya Mkakati wa Kiuchumi wa 'One Belt One Road' mjini Hong Kong hivi karibuni kwenye tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo kupitia Mkakati huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzainia (TADB) Bwana Francis Assenga (Katikati) akiwa na viongozi mbali mbali mara baada ya kumalizika kwa Kikao chake na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa China Capital Fund Management (Hong Kong) Bwana James Wang (kushoto kwake). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa First Shanghai Capital Ltd Bwana Allen Wang; Mkurugenzi wa Landmark Investments Hong Kong na Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Bunge la China Dr. Annie Wu Chung; Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama; na Mkurugenzi Mtendaji wa First Shanghai Capital Ltd Bi. Fanny Lee.
Kikao kati ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya kutafuta mitaji na uwekezaji ya Hong Kong iitwayo China Alpha Fund Management (HK) kilichofanyika katika Jengo la Two Exchange Square mjini Hong Kong hivi karibuni ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utafutaji Mitaji na Uwekezaji ya Hong Kong Bwana James Wang (Katikati). TADB iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bwana Francis Assenga (Mwenye Shati la Bluu na Tai) na kushoto kwake ni Bwana Joseph Kahama ambaye ni Katibu Mkuu wa China-Tanzania Friendship Promotion Association. Kushoto wa Kwanza ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wawekezaji wa China Alpha Fund Management (HK) Ltd Bi. Kandice Au.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bwana Francis Assenga mwenye tai nyekundu kulia kabisa akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Benki ya China Hong Kong baada ya kumalizika kwa Kikao chao mnamo tarehe 20 Oktoba 2017. Kulia kwa Bwana Assenga ni Meneja Mkuu wa BOC Hong Kong Bwana Chan Man Stephen; Katibu Mkuu wa Taasisi ya Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama; na Watendaji wa Benki hiyo Bi. Yiu Oi Yin Doris, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Biashara inayoshughulikia Taasisi za Fedha; na Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji wa Mahusiano na Mabenki, Bwana Wong Chee Him Steve, wakiwa Makao Makuu ya Benki ya China mjini Hong Kong.
Bwana Francis Assenga katikati mwenye suti ya khaki ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB akipanda miti katika Shule ya Sekondari ya China Foundation mjini Hong Kong kuashiria kuunga mkono Mapinduzi ya Mkanda wa Kijani (Green Belt Revolution) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 35 ya shule hiyo ambapo Bwana Assenga alialikwa kama Mgeni Maalum wa Shule hiyo. Wageni wengine Maalum waliotoka nchi mbali mbali ni pamoja na Bwana Joseph Kahama ambaye aliyealikwa kama sehemu ya Jopo la Washauri wa Shule hiyo kwa miaka takriban 8 sasa na Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation Bwana Takashi Kawasaki (Mwenye Suti bila Tai Kulia kabisa) toka Tokyo, Japan na Mkurugenzi wa China Mfuko wa Uhifadhi Mazingira na Maendeleo ya Mkanda wa Kijani Profesa Frederick Charles Dubee (Mwenye Mvi na Tai katikati) toka Hienola, Finland.
Kaimu Mkurigenzi Mtendaji wa TADB Bwana Francis Assenga (Kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya China Foundation Secondary School (CFSS) Bwana Au Kwong Wing, zawadi toka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati Bwana Assenga alipokaribishwa kama Mgeni Maalum wa Shule kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Sekondari hiyo Mjini Hong Kong hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliwahimiza wanafunzi wa shule hiyo kuhifafhi mazingira na kujikita kwenye teknolojia mbali mbali za kilimo cha kisasa.
Baadhi ya Wageni Maalum toka nchi mbali mbali duniani walioalikwa kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya China Foundation Secondary School (CFSS) yaliyofanyika shuleni hapo njini Hong Kong hivi karibuni. Wa Nne toka kushoto mwenye tai nyekundu ni Bwana Francis Assenga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Wawakilishi wa Tanzania Bwana Francis Assenga (Kaimu Mkuruvenzi Mtendaji wa TADB) wa pili toka kushoto na Bwana Joseph Kahama (Katibu Mkuu wa Taasisi ya China-Tanzania Friendship Association) wakikabidhiwa Zawadi ya Utambuzi wa mchango wao kwenye shughuli za kiuchumi, kilimo na huduma za jamii kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya Jiji Hong Kong. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bwana Au Kwong Wing na Kukia kabisa ni Mratibu wa Maadhimisho hayo (Mwene shati jeupe).

Usajili Vitambulisho vya Taifa watinga Manyara, Singida

$
0
0
Wakazi wa Sinai na Magugu, Babati, Manyara wakishiriki kwenye zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa.


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la usajili wa watu katika wilaya zote za mikoa ya Manyara na Singida ambalo linalenga kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.

Kuwapatia Vitambulisho wananchi kutasaidia kutambulika pale wanapotaka kugawiwa pembejeo za Kilimo, kupata leseni za udereva na biashara, kusajili namba za Simu, kumiliki Ardhi, kupata mikopo, kufungua akaunti benki na matumizi mengineyo yanayohitaji utambulisho.

Mratibu wa Usajili wa mikoa ya Manyara na Singida, Thomas William ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema watu wengi wanajitokeza kusajiliwa baada ya kuelimishwa kuhusu umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa

WATANZANIA WASOGEZEWA MBELE FURSA ZA UWEKEZAJI NA MAENDELEO BANK

$
0
0
Wito umetolewa kwa wananchi kote nchini kuweza kujijengea utamaduni wa kuwekeza katika mfumo wa hisa na hasa katika hisa za Benki ya Maendeleo 

Wito huo kwa umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo, Ibrahim Mwangalaba jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kusogezwa mbele kwa zoezi lao la kuuza hisa za benki hiyo.Mwangalaba alisema njia kubwa ya kuwasaidia wananchi katika kujikwamua kimaisha ni kuchangamkiakia fursa zinazojitokeza ikiwemo ya kununua hisa za benki hiyo.Zoezi la uuzwaji wa hisa za benki hiyo ambalo lilianza Septemba 21, mwaka huu na lilikuwa limalizike leo sasa litandelea hadi Desemba 4, mwaka huu ili Watanzania wengi waweze kunufaika nalo.

Aliongeza kuwa lengo lao ni kuuza hisa zaidi ya mil.17 kwa Watanzania wapatao 170,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania.Benki ya Maendeleo ni ya Watanzania wote, hivyo tumeona ni vema zoezi hilo lifanyike nchi nzima kwani awali tulikuwa tayari tumewafikia Watanzania kutoka mikoa 13 pekee na sasa tutatumia muda ulioongezwa kufika mikoa yote," alisema Mwangalaba.

Hisa moja inauzwa kuanzia sh.600 na kima cha chini cha kumiliki hisa ni 100.

LIONS CLUB OF DAR ES SALAAM TANZANITES PROMOTES PEACE VIA ART

$
0
0
 The winner from  International School of  Tanganyika (IST) Sreelakashmi Jayasankaran (11).

The Lions club of Dar es Salaam Tanzanites organized a Peace Poster competition on saturday 4.11.2017. The Lions Club International focuses on this activity to promote peace in the world for the past 30years. The event organized by Lions Club of  Dar es Salaam Tanzanites, 2 schools participated - The Aga Khan Mzizima Secondary School and The International School of Tanganyika.
They had 20 participants present their master pieces, which were judged by Mr. Paul Ufford (UNICEF member), Mr. Muzu Suleimanji (a renowned artist from Tanzania) and Mr. Pranay Shah a Professional from the Digital Media World- DTP).

It was a breathtaking moment to see the beautiful art works on display, which clearly portrayed the talent of our future generation – tomorrow’s leaders.

Each art work uniquely spoke about how important it is to them to have a peaceful world to live in, where everyone, every religion, caste, color and creed lived with love, peace and harmony.

The Peace Posters chosen here will go for further competition to the Lions District and Lions Club International that is in Chicago USA. The Grand Prize winner chosen in the International has a chance of winning up to 5000USD- This finale winner will be announced in February 2018.

The winners of the local level competition, from International School of Tanganyika was Sreelakashmi Jayasankaran and the winner from Aga Khan Mzizima Secondary School was Magenta Jumwa . We wish them all the best for further competition.

RAIS DKT. MAGUFULI AKIWA MAPUMZIKONI CHATO MKOANI GEITA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha kwenye simu pamoja na Mama yake mzazi Suzana Magufuli (katikati) pamoja na mdogo wake Monica wa kwanza (kushoto). Rais Dkt. Magufuli yupo mapumzikoni katika Kijiji cha Lubambangwe Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha kwenye simu aliyokuwa akioneshwa na Mama yake mzazi Mama Suzana Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Lubambangwe Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza radio pamoja na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wa pili kutoka (kushoto) mdogo wake Monica wa kwanza (kushoto), na Dada yake Asteria wa kwanza (kulia). Rais Dkt. Magufuli yupo mapumzikoni katika Kijiji cha Lubambangwe Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza radio pamoja na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wa pili kutoka (kushoto) mdogo wake Monica wa kwanza kushoto. Rais Dkt. Magufuli yupo mapumzikoni katika Kijiji cha Lubambangwe Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU

RC WA MTWARA AMUAGIZA MKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO NA MENEJA WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KUANDIKA BARUA YA KUJIELEZA KWANINI WALIIDANGANYA OFISI YAKE.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho CBT Hassan Jarufu pamoja na Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika MAMCU Kuhakikisha wanaandika Barua ya Kutoa Maelezo kwa nini Waliidanganya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhusiana na Mkataba, Idadi ya Ununuzi wa Magunia ya Kubebea Korosho katika Kikao Kilichoketi Novemba,mosi  Mwaka huu.


Katika Kikao hicho Bodi ya Korosho Kupitia MAMCU walisema, wameagiza magunia Million1 kupitia Kampuni ya DIRMAN HOLDING LTD na Ndipo mkuu wa Mkoa akaagiza Kuletewa mkataba Huo na kubaini kuwa Baadhi ya wajumbe wa Mamcu Hawaujui Mkataba na Haujulikani Thamani yake laki pia Mkataba ni magunia Laki6.5 na sio Million1 walizozisema katika kikao Hicho.Hata hivyo magunia hayo mpaka sasa hayajulikani idadi kamili iliyoletwa

Katika Mkutano na waandishi wa Habari Ofini kwake, Mkuu wa mkoa Byakanwa amesema kutokana na Udanganyifu huo Ofisi yake imeamua Bodi ya Korosho isilipe Pesa yeyote kwa kampuni ya DIRMA HOLDING LTD kwa kushindwa kuleta magunia kwa wakati,kwani ilitakiwa kuleta Septemba 30/2017lakini mpaka sasa bado hajakamilisha na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya Mzabuni huyo.

Aidha Ameiagiza Bodi kuhakikisha inasambaza magunia ndani ya Kipindi cha Wiki Mbili zijazo ili malalamiko ya wakulima yaweze kuondoka.

Kutokana na Udanganyifu Huo Mkuu wa Mkoa anatarajia Kuunda kamati ili kuweza kuchunguza taratibu zinazotumika kuingia mikataba na wote waliohusika na kamati hiyo itaishauri nini cha kufanya kwa wahusika.

UZINDUZI WA UPIMAJI WA AFYA WATOTO WA KITUO CHA MAZIZINI UNGUJA.

$
0
0
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto iliyofanyika leo katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi (kulia) Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe.Moudline Cyrus Castico na Mke wa Balozi Mdogo wa China Mhe.Mama Liu Jie (kushoto) , [Picha na Ikulu.] 04/11/2017.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimpakata Mtoto Yussuf Abdalla Abdilah akifanyiwa uchunguzi wa Dr.Qin Qin (kulia) kutoka china akiwa ni miongoni mwa Madakatri wa kujitolea akati wa hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto iliyofanyika leo katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 04/11/2017.
Mke wa Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Mama Liu Jie (katikati) akimpakata mtoto wakati wa hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto iliyofanyika leo katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi,(kulia) Dr.Guo Yulan akiendelea na zoezi hilo,wakiwepo na Viongozi wengine Dr.Wang Hao,Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe.Moudline Cyrus Castico,Katibu Mkuu Bi.Fatma Gharib Bilali na Naibu Wazuiri wa Afya Mhe,Harusi Said Suleiman, [Picha na Ikulu.] 04/11/2017.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Mama Liu Jie (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa picha ya pamoja na Madaktari wa Kichina wakati wa hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto iliyofanyika leo katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi
Baadhi ya Madaktari wa kujitolea kutoka Jamhuri ya Watu wa China wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto wanaolelewa katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi iliyofanyika leo mgeni rasmi akiwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 04/11/2017. 
Baadhi ya Madaktari wa kujitolea kutoka Jamhuri ya Watu wa China,Wananchi na Watoto wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto wanaolelewa katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi iliyofanyika leo mgeni rasmi akiwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani)
Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea Watoto kiliopo Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto hao iliyofanyika leo mgeni rasmi akiwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 04/11/2017. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Mama Liu Jie(katikati kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiangalia Ngoma ya Utamaduni kutoka China iliyochezwa na vijana wa Zanzibar na China katika hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto iliyofanyika leo katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi, [Picha na Ikulu.] 04/11/2017. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Mama Liu Jie (kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakiwaangalia Watoto wa Kituo cha mazizini wakiimba Wimbo maalum wa kuwakaribisha wageni katika hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto iliyofanyika leo katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe.Moudline Cyrus Castico (kulia) akimkabidhi zawadi na Vifaa mbakli mbali Mtoto Ruwaida Abdalla Aly kwa niaba ya Watoto katika Kituo cha Mazizini,zilizotolewa na Mke wa Balozi Mdogo wa China Mhe.Mama Liu Jie (katikati) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa huduma maalum ya Upimaji wa Afya za Watoto iliyofanyika leo katika Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi,

TUME YA UCHAGUZI YATEUA MADIWANI 2 WA VITI MAALUM


MBEGU YA MAHINDI YA WEMA 2109 NA MIHOGO ILIYOTOLEWA NA COSTECH WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA KUONGEZA CHACHU YA KILIMO

$
0
0

Wakulima wa Kijiji cha Iponya katika Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wakifurahia kupata mbegu bora ya mihogo aina ya Mkombozi waliokabidhiwa na  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), kwa ajili ya kuanzisha shamba darasa la mbegu hiyo wilayani humo jana.
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akimkabidhi mbegu ya mihogo , Mwakilishi wa Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Furaha Chiwile wakati wa uzinduzi wa shamba hilo katika Kijiji cha Iponya. Katikati mwenye shati la kitenge ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Nsika Sizya.


 Watafiti wakiandaa shamba darasa la mahindi katika Kijiji cha Mponda.
 Wananchi wa Kijiji cha Mponda wakisubiri uzinduzi wa shamba darasa la mahindi.
 Ofisa Kilimo wa Wilaya Mbogwe, Stephen Shilemba akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Mponda kabla ya ufunguzi wa shamba darasa.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila, akitoa maelezo kwa wakulima wa Kijiji cha Mponda wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mahindi ya WEMA.
 Mtafiti kutoka COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo (kulia), akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Mponda.
  Mtafiti kutoka COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo, akimkabidhi mbegu ya mahindi ya Wema, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mbogwe, Stephen Shilemba. Kulia ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
 Mtafiti kutoka COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo, akimkabidhi mbolea ya kupandia mahindi aina ya DAP, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mbogwe, Stephen Shilemba.
 Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mbogwe, Stephen Shilemba, akimkabidhi mbegu ya mahindi aina ya WEMA, Ofisa Ugani wa Kata ya Lugunga, Dickson Namlanda.

 Wanawake wa Kijiji cha Lwazeze wakishuhudia uzinduzi huo.
 Mkulima wa Kijiji cha Lwazeze, Charles Kangai akichimba mashimo kwa ajili ya upandaji mbegu ya mahindi ya WEMA.




 Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, akielekeza jinsi ya upandaji wa mbegu hiyo ya mihogo aina ya Mkombozi.
 Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Nsika Sizya, akipanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa katika Kijiji cha Iponya.
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange, akipanda mbegu ya mihogo aina ya Mkombozi kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Iponya.

Na Dotto Mwaibale, Mbogwe, Geita.

MAKAMU Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Nsika Sizya amesema mbegu bora ya mahindi ya WEMA 2109 na mihogo aina ya Mkombozi waliyokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) itaongeza chachu ya kilimo wilayani humo.

Sizya aliyasema hayo wilayani humo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema yanayostahimili ukame na mihogo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji vinne vya Mponda kilichopo Kata ya  Luganga, Kijiji cha Ushetu kilichopo Kata ya Ushirika, Kijiji cha Lwazeze kilichopo Kata ya Ngemo na Kijiji cha Iponya kilichopo Kata ya Iponya.


Alisema changamoto kubwa waliyokuwa nayo wakulima katika Halmshauri hiyo ni kukosekana kwa mbegu bora za mihogo na mahindi ambapo alisema kwa kupata mbegu hizo kutaongeza ari na chachu ya kilimo kwa wananchi.

Aliishukuru CSTECH na OFAB kwa kuwapelekea mradi huo katika wilaya hiyo na kuupokea kwa shangwe kwa kuzingatia kuwa mihogo ni zao la biashara na chakula ambapo aliwataka wananchi kubadilika na kufanya kilimo chenye tija kama wataalamu wanavyowaelekeza.


Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula aliwaambia wakulima hao kuwa hekta moja ya mihogo iwapo watalima kwa kufuata ushauri wa wataalamu wataweza kupata tani 25 hadi 32 kwa zao la mhogo na viazi watapata tani 7 hadi 9 kwa hekta moja.

Alisema matokeo hayo watayapata endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea hivyo wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya mihogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye viazi wanapata tani moja hadi 3.

Mtafiti huyo alisisitiza kuwa mbegu hiyo ya Mihogo ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana kustahimili magonjwa hatari ya mihogo ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima wengi na kupoteza hadi asilimia 90 za mazao.

Mtafiti kutoka COSTECH, Dk. Beatrice Lyimo aliwataka wakulima wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na maofisa ugani kuyatunza mashamba hayo na wao kuwa walimu kwa wakulima wenzao.

"Nawaomba nyinyi mliobahatika kupata mashamba darasa haya muwe walimu wa kutoa mbegu bora ambayo mtaisambaza katika vijiji vingine ili kila mkulima aweze kufaidika" alisema Dk.Lyimo.

Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila alisema asilimia 75 ya wakulima katika mkoa huo wanategemea kilimo hivyo mafunzo yaliyotolewa kwa maofisa ugani kupitia COSTECH na OFAB yataongeza kasi ya uzalishaji hasa baada ya kupata mbegu hizo bora.

Alisema changamoto kubwa waliyonayo ni wakulima kushindwa kufuata kanuni bora za kilimo ingawa wameanza  kubadilika pole pole baada ya kupata mafunzo.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa maofisa ugani kwani waliopo kwa mkoa mzima ni 189 wakati wanaohitajika ni 512 na kuwa katika maeneo mengine ofisa ugani mmoja anahudumia vijiji tisa tena bila ya kuwa na usafiri wa uhakika.

Hadi jana Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), imeweza kuwafikia wakulima katika vijiji 22 vya wilaya za Mikoa ya Kagera na Geita na kutoa elimu kwa vitendo kwenye matumizi ya Sayansi na Teknolojia za kilimo kwa uzalishaji wenye tija ambapo kuanzia kesho kutwa Jumatatu Novemba 6,2017 watafanya kazi hiyo katika wilaya zote za Mkoa wa Tabora kwa kuanzisha mashamba darasa ya mbegu za mahindi ya WEMA na Mihogo.

WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA

$
0
0
Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITA) jijini Dar es Salaam, wametakiwa kutumia vyema teknolojia ya mawasiliano hususan mitandao ya kijamii kujifunza ili kupata maarifa badala ya kuitumia kwa mambo ambayo hayatawasaidia katika masomo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo wakati akiwakaribisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2017/18.Amesema vijana wengi wanatumia mitandao ya kijamii kwa masuala ya kijamii kwa kiwango kikubwa kuliko kuitumia kujifunza na kupata maarifa kwa mambo ambayo yatawasaidia kukuza kiwango cha elimu.

“Elimu ipo kila mahali siku hizi: katika vitabu, mitandao na tuna mambo mengi ambayo yanasaidia sana kujifunza tofauti na ilvyokuwa miaka 30 iliyopita. Ni wajibu wa wanafunzi kuitumia vyema mitandao hususan simu kujifunza na kupata maarifa”, alisema Prof. Jairo.

Mkuu huyo wa chuo amesema kwamba chuo cha kodi kinatumia mfumo wa kujenga umahiri kwa mwanafunzi ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu na ambao umelenga kumuwezesha mwanafunzi kujifunza badala ya kufundishwa. Ameongeza kwamba mfumo huo ndio utaratibu unaotumika ulimwenguni ili mwanafunzi anapohitimu awe na uwezo wa kujua nini cha kufanya katika fani yake na kwa Chuo cha Kodi ajue jinsi ya kukusanya kodi.

“Msije mkakaa mkategemea mtafundishwa tu na mtakaa na kumsikiliza mwalimu, hapana, tunawatarajia mjifunze kwa kutumia nyenzo mbalimbali zilizopo”, amesema Prof. Jairo na kuongeza kwamba huo ndio utaratibu unaotumika katika mfumo wa kujenga umahiri kwa mwanafunzi.

Katika hatua nyingine amewataka wanafunzi hao wa Astashahada ya Uwakala wa Forodha ya Afrika Mashariki, Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi na Stashada ya Uzamili ya Kodi, kuzingatia masomo kwani ndio lengo lao kuu la kuomba kujiunga na chuo cha kodi na kwa upande wake chuo cha Kodi kitatimiza wajibu wake kuhakikisha wanapata elimu wanayostahili na katika mazingira bora.

Aidha amewahakikishia wanafunzi hao kwamba wale watakaofaulu vizuri watapata ajira kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania kwani TRA huchukua wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha juu.Kuhusu maisha katika Chuo cha Kodi, Prof. Jairo amewataka wanafunzi hao kuishi kwa mujibu wa sheria za nchi pamoja na kufuata sheria ndogo ndogo na taratibu za chuo.

Pamoja na Mkuu wa Chuo cha Kodi, katika kuwakaribisha wanafunzi hao, pia walikuwepo Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma Justin Musa, Kaimu Mkuu wa Chuo, Utawala Emmanuel Masalu, Mkuu wa Huduma za Fedha Emmanuel Foya, Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO) Darafu Abdalah, Wakuu wa vitengo mbalimbali pamoja na walimu.
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo (aliyesimama) akizungumza na wanafunzi wapya waliojiunga na Chuo hicho kwa muhula wa masomo wa kuanzia 2017/18. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Huduma za Fedha Emmanuel Foya na Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Fedha na Mipango Emmanuel Masalu. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) .
Wanafunzi wapya katika Chuo cha Kodi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo
 
Wanafunzi wapya katika Chuo cha Kodi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo 
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo akisisitiza jambo kwa wanafunzi wapya waliojiunga na Chuo hicho kwa muhula wa masomo unaoanza 2017/18. Kushoto kwake ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Fedha na Mipango Emmanuel Masalu na Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Justin Musa. 
Mmoja wa wananfunzi akiuliza swali wakati wa tujio la kuwakaribisha wanafunzi wapya katika Chuo cha Kodi (ITA) 
Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Fedha na Mipango Emmanuel Masalu (Aliyesimama) akiwaeleza wanafunzi wapya katika Chuo cha Kodi masuala ya Utawala katika chuo hicho. Pamoja naye kutoka kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Justin Musa, Mkuu wa masuala ya Fedha Emmanuel Foya na Makamu Mwenyekiti wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO) Darafu Abdalal .

TASWA FC YAIADHIBU POLISI FC MABAO 5-0 UWANJA WA UHURU

$
0
0
  MSHAMBULIAJI wa Taswa Fc, Said Seif (kushoto) akiruka kumkwepa beki wa Polisi Fc, Andew Thomas, wakati wa mchezo wa kirafiki katika Maadhimisho ya 10 ya Mtandao wa Polisi yaliyoanza jana Nov 4 katika Uwanja wa Uhuru Dar esSalaam, yakitarajia kumalizika Nov 9 mwaka huu. Katika mchezo huo Taswa Fc ilishinda mabao 5-0. Picha na Muhidin Sufiani.
 DCP Mary Nzuki wa Jeshi la Polisi, akimkabidhi Ngao ya ushindi Nahodha wa Taswa Fc, Willbert Moland, baada ya Taswa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Polisi katika mchezo wa kirafiki wa Maadhimisho ya 10 ya Mtandao wa Polisi yaliyoanza jana Nov 4 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, yakitarajia kumalizika Nov 9 mwaka huu. Picha na Muhidin Sufiani.

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUSOMESHA WAUGUZI

PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA MKOA WA GEITA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato wakifunua kitambaa kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato wakifunua kitambaa kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipeana mikono na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato baada ya kufunua kitambaa kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipanda mti wakati wa sherehe za   uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigalla King akipanda mti wakati wa sherehe za   uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato akipanda mti wakati wa sherehe za   uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi) wakipanda mti wakati wa sherehe za   uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Wabunge wa Mkoa wa Geita wakipanda mti wakati wa sherehe za   uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara na mkoa wakikata utepe kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani Chato. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Sehemu ya watendaji wa Wizara, Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato wakiwa kwenye  sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.
Sehemu ya watendaji wa Wizara, Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato wakiwa kwenye  sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.


Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images