Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1416 | 1417 | (Page 1418) | 1419 | 1420 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameendelea na zoezi la kupita Duka kwa Duka, Mlango kwa Mlango Lusaka wezi wa kazi za Sanaa na wakwepaji wa Kodi hapa nchini.

  Zoezi hilo linaloendelea kwa nchi nzima, hapo jana liliendeshwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kamishna wa Kodi za Ndani - TRA, Elijah Mwandumbya amesema wameamua kufanya zoezi hilo ili kujiridhisha katika maduka ambayo yanafanya biashara za kazi za Wasanii.

  Mwandumbya amesema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuhakiksha wanaofanya biashara hizo wanalipa Kodi shahiki, na kuhakikisha Stempu za Kodi zimatumika katika kila CD; "Kwa maana Stempu mbili kwa CD moja yaani Stempu moja kwenye Kasha la CD hiyo na nyingine kwenye CD yenyewe", amesema.

  Pia kuhakikisha wale wanaofanya biashara za kazi za Wasanii wanavibali vya kufanya biashara hizo, ikiwa sambamba na kuwachukulia hatua stahiki ili kuhakikisha Wasanii hao wanapata haki zao katika kila kazi ambayo inauzwa sokoni.Amesema huo ni muendelezo wa Kampeni ambao unafanywa nchi nzima kutokana na kazi hiyo iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda miezi kadhaa iliyopita.

  "Kwa kazi za Wasanii wa kigeni upo utaratibu wakufuata katika Taasisi pamoja na Kampuni mbalimbali ili kuuza kazi za Wasanii hao", amesema Mwandumbya.  Mkurugenzi wa Msama Auction Mart Alex Msama akiwa sambamba na wafanyakazi wake kwa kushirikia na Jeshi la Polisi wakikamata vifaa vinavyotumika kurudufu kazi za wasanii (muziki),jana katika moja ya Mtaa Kariakoo jijini Dar
  Kamishna wa Kodi za Ndani - TRA, Elijah Mwandumbya akikagua moja ya CD ya filamu za hapa nchini,kubaini kuwa kama ina stika za TRA ama la,akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Msama Auction Mart Alex Msama ambao wamepewa dhamana ya kushirikiana na TRA kupapambana na maharamia wa kazi za wasanii wakiwemo na wale wanaokwepa kodi
  Ukaguzi ukiendelea kufanyika katika maduka yanayouza CD za Filamu,kubaini kuwa zinalipiwa ushuru na zina stika kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
  Baadhi ya Watuhumiwa na mafurushi yao ya CD zinazodaiwa kutolipiwa kodi na kukosa STIKa za TRA wakiwa nchini ya Ulinzi mara baada ya kufikiwa kituo cha polisi kati,jana jioni jijin Dar.

  0 0

  Mitambo ya kuzalisha umeme (System Turbine, no 2) kwa ajili ya mradi wa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi II iliingia nchini kupitia Bandarini Oktoba 16, 2017 na leo hii Novemba 03, 2017 imetolewa Bandarini na hivi sasa inaelekea kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi Kinyerezi II (MW 240) Jijini Dare es Salaam.

  Mradi huu wa Kinyerezi II uliwekwa jiwe la msingi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli achi 16, 2016. Mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 2018.
  Moja ya Gari iliyobeba Mitambo ya kuzalisha umeme (System Turbine, no 2) kwa ajili ya mradi wa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi II ikielekea eneo Kutakapojengwa Mradi huo.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akikagua  ujenzi wa Makao Makuu ya ofisi hiyo unaoendelea mkoani Dodoma. Ujenzi wa ofisi hiyo unatarajia kukamilika mwezi Februari, 2018.  
   Muonekano wa mbele wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
   Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
  Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma. Picha na Veronica Kazimoto.

  0 0


  0 0

  Mjumbe wa kamati kuu taifa kutoka chama cha walimu Mkoa wa Ruvuma Mwalimu Sabina Lupukila ametoa wito kwa walimu wote nchini kuacha tabia za kutembea na wanafunzi kwani kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi na kulete taswira mbaya kwa jamii kwani mwalimu ni kioo cha jamii,habari kamili hii hapa video yake.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akifafanua namna mtumishi anavyotakiwa kuwajibika pindi anapowahudumia wananchi  (aliyekaa) kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo. 
   Viongozi wa mashirika ya ya umma na mamlaka mbalimbali za seikali Mkoani Rukwa Waliohudhuria kwenye kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa mamlaka na mashirika ya umma. 

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo amewaasa watumishi wa mashirika ya umma na wakala wa serikali mkoani Rukwa kutotumia vyeo vyao kuwanyanyasa wananchi wanaowahudumia na badala yake wawasaidie kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa bila ya kujali, rangi kabila, dini na hali zao kiuchumi.

  Amesema kuwa watumishi wa serikali ni watumishi wa wananchi hivyo wanapaswa kujituma bila ya kujali vyeo vyao kwani vyeo hivyo havitakuwa na maana ikiwa wananchi hawapati huduma wanayoitarajia kutoka katika serikali waliyoiweka madarakani.

  “Sisi viongozi wa Serikali lazima tufanye kazi kwa kujituma na kujitoa na tukumbuke kuwa sisi ni watumishi tu, sio watu wa kujivuna ama wabinafsi na kujinadi kwa vyeo vyetu kwamba mimi meneja, daktari sijui nani, vyeo vyetu vitakuwa na maana pale tu tunapokwenda kwa wananchi na kuwapa huduma” Alieleza.

  Na kuongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha kuwa kila kiongozi anayehudumia wananchi anakuwa mtumishi wa wananchi na kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kuonya vikali watumishi wanaowahudumia wananchi kwa kutumia lugha chafu.   

  Ameyasema hayo kwenye kikao cha muda mfupi kilichowajumuisha viongozi kutoka katika mashirika ya umma, wakala na mamlaka mbalimbali za serikali zilizomo Mkoani humo ili kufahamu matatizo wanayokumbana nayo pindi wanapotimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi.

  Sambamba na hayo Mh. Wangabo amewataka watumishi wote Mkoani humo kuzingatia muda na kutekeleza kwa wakati mipango waliyojiwekea ili kazi zizae matunda na kutoa taarifa sehemu husika bila ya kusubiri kusukumwa.


  0 0

   Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.
   Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem aliyesimama akiongea na baadhi ya  wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam , katikati waliokaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Lwezimula.
   Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem kulia akimkabidhi zawadi ya mchango mkubwa katika Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu kushoto wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.
   Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem akichangia damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa MOI  Dkt. Respicious Lwezimula aliyesimama akiongea na baadhi ya  wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam, kulia aliyekaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakimsikiliza kwa makini ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam.
  Mwanachama wa Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa  Wanawake (WOW) Afrika Mashariki Bi. Rehema Mwangolombe akiwa katika maandalizi ya kuchangia damu  damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA ALLY DAUD- WAMJW.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akimtambulisha meneja mwajiri wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki kwa vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani wakati akifanya mkutano nao. Mkuu huyo wa wilaya alifanya ziara hiyo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA - KAJUNASON/MMG - KIBAHA.
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akijadiliana machache na meneja mwajiri wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki wakati alipofanya mkutano wake na vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akitolea ufafanuzi wa mambo machache kwa vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.
  Vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Asumpter Mshama.
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akaribishwa na uongozi wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki ili aweze kuongea na vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.
  Mkutano ukiendelea.
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama aliyeambatana na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wakifanya mkutano wa ndani na vingozi wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki  katika mambi yao waliyoiweka kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.
  Kamati ya ulinzi na usalama ikifuatilia kwa karibu.
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama (kushoto) na katibu tawala wilaya ya Kibaha Sozi Ng'ate (kulia) wakipata maelezo machache kwa kiongozi wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki wakati walipotembelea kambi yao iliyopo kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.

  0 0


  Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza,alipokuwa akizunguma nao mapema leo jijini Dar,
  ,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja  na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini.
  Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchin walipokuwa wakifuatilia mkutano huo mapema leo jijini Dar.

  pichani kati ni Mwenyekiti wa kikundi cha Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja  na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini,kulia ni Mkurugenzi wa
  Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi mapema leo,namna wanavyoshiriki zoezi la kukamata kazi feki za Wasanii,sambamba na wakwepa kodi kupitia kazi wasanii.

  Uzalendo Kwanza ikishirikiana na Kampuni ya Msama Auction Mart wameamua kuungana kwa pamoja katika kutokomeza kazi Feki za Wasanii hapa nchini.

  Uzalendo Kwanza kupitia kwa Mwenyekiti wake, Steve Nyerere wameungana na Msama Auction Mart pamoja na kushukuru juhudi zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya yakukamata Walanguzi wa kazi hizo.

  Steve Nyerere amesema wafanyabiashara katika Maduka Makubwa ya Filamu vifaa vya Soka wanafanya biashara hizo lakini hawalipi Kodi, hivyo wanawapongeza Msama Auction na TRA kuunga mkono  jitihada zakutokomeza wizi huo.

  "Wamejiajiri katika Taifa la Watanzania, wakipata faida kubwa, Kodi na Mapato makubwa yangepatikana", amesema Steve.Ameongeza kusema kuwa "Msama hatoshi, TRA peke yake hatoshi; Mhe. Rais hatoshi kama Wasanii wenyewe hatutounga mkono jitihada hizi".

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa anawashukuru Wasanii wa Tanzania kwa kuunga mkono juhudi hizo za kukomboa kazi zao.

  Pia amesema kuwa Zoezi hilo haliko jijini Dar es Salaam tu, zoezi hilo ni la nchi nzima."Popote ulipo kila mahali tutafika kuhakikisha unauza kazi halali zenye Stika za TRA", amesema Msama.

  Hata hivyo amewataka Wafanyabishara hao wanaofanya biashara ya kazi za Wasanii wa Tanzania kufuata taratibu ili kufanya biashara salama.

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji akizungumza katika mkutano wa Global Business Forum 2017 kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika, mkutano huo wa siku mbili umefanyika Dubai, UAE na kuhudhuriwa na watu 5860 wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na wafanyabiashara. (Picha na Clouds Media)

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amepongeza uamuzi wa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kufufua viwanda ambavyo vilikuwa havifanyi kazi.

  Dewji ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa Global Business Forum 2017 (GBF) kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

  Mfanyabiashara huyo ambaye anamiliki viwanda 41 alisema uamuzi aliochukua Rais Magufuli ni mzuri hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati.

  Dewji alisema kampuni yake ya MeTL Group itaendelea kushirikiana na serikali na katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo amejipanga kuhakikisha anatoa ajira kwa Watanzania 100,000 jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa nchi na kwa wananchi..

   “Nianze kwa kumpongeza Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa shabaha yake ya viwanda, ni nzuri sababu kuna ongezeko la thamani lakini pia watu wanaweza kupata ajira na pia hizi biashara zitalipa kodi ambazo zitaisaidia serikali kuwekeza kwenye mambo ya afya na maji na huduma za jamii. Mimi shabaha yangu kwenye miaka saba au nane ijayo MeTL Group tunataka tuajiri watu 100,000,” alisema Dewji.

  Dewji ambaye kwa mujibu wa jarida la Forbes ni tajiri namba moja nchini aliongeza kuwa utendaji wa Rais Magufuli ni wa kasi hivyo anategemea kuwa katika kipindi cha miaka michache ijayo uchumi wa Tanzania utakuwa umekuwa  sana.

  “Mimi naona kwa kasi ya Mhe. Rais kwenye miaka miwili au mitatu ijayo tutakuwa tumefika mbali sana, uchumi wetu kwasasa ni asilimia sita au saba lakini kama tukitaka kuondoa umaskini lazima nchi yetu ukuaji wa uchumi uanze kukua kwa zaidi ya asimilia 10, mimi nina muamini sana Mhe. Rais na shabaha yake kwahiyo Mungu atutangulie na sisi tupo nyuma yake tutafika hivi karibuni,” alisema Dewji.

  Pia Dewji alizungumzia umuhimu wa mkutano wa GBF ambao umekutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na wawekezaji alisema ni nafasi ya kipekee kwani pamoja na kujadili viwanda pia amepata nafasi ya kuwaelezea washiriki wa mkutano fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini.

  “Umuhimu ni mkubwa sana nakuja hapa kama MO lakini pia nawakilisha nchi yangu Tanzania, nimeitangaza nchi yangu ili watu waje na wawekeze, nimewaeleza mazingira yetu ya uwekezaji ni mazuri, tuna malighafi na tunahitaji viwanda angalau watu wetu wa Tanzania wapate ajira na serikali ipate kodi,” aliongeza Dewji.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imepata cheti cha mfumo wa uhakiki wa Ubora wa Huduma cha Kiwango cha kimataifa cha ISO  9001.2015  na kufanya mamlaka hiyo kuwa ya pili katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema kuwa mafanikio ya TFDA ni kutokana na kazi  wanayofanya katika udhibiti dawa na chakula kwa ajili ya kutumia bidhaa zenye ubora.

  Amesema kuwa TFDA ni mamlaka ambayo inagusa masilahi ya kila mtu na hakuna asiyetumia bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni kulinda afya za wananchi ambao wanaweza kufanya kazi na kuiletea taifa maendeleo hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

  Dk. Ndugulile amesema kuwa TFDA kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa chakula, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ni utekelezaji wa vitendo wa azma ya serikali ya awamu ya tano chini uongozi mahiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha upatikanaji wa wa huduma bora za afya hususani  upatikakanaji wa dawa , vifaa tiba na vitandanishi.

  Aidha amesema nyenzo zilizofanya mafanikio katika udhibiti ni maamuzi ya menejimenti zaidi ya miaka 10 wa kudhamiria kutekeleza mfumo wa uhakiki ubora wa huduma .

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema kuwa katika kuongeza huduma za udhibiti kwa wananchi wameanzisha ofisi saba za kanda ambazo zitahudumia katika mikoa iliyopo katika kanda hizo.

  Sillo amesema kuwa mamlaka imekuwa ikitekeleza mfumo wa uhakiki ubora kuanzia mwaka 2005 baada ya kufanya tathimini ya namna bora ya kufanya shughuli za udhibiti kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wateja.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo wakiwa wameshishika cheti cha mfumo wa Uhakiki Bora katika Kiwango cha Kimataifa Cha Iso 9001-2015.
  Meneja Uchunguzi wa Dawa na Vipodozi Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo mbele ya Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitembelea maabara katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo (wakatikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya TFDA Dkt Ben Moses.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa kwenye piha ya pamoja wakati akizindua CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 tukio lililofanyika katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea nchini Canada, Novemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea nchini Canada, Novemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  NA BASHIR NKOROMO.

  Kundi la Tanzania One Theatre (TOT Plus), limo kambini Wanamuziki wake wakijifua vikali katika mazoezi ya nyimbo tatu ambazo kundi hilo litaziipua hivi karibuni.

  Akizungumza wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo, Mkurugezi wa TOT Plus inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gasper Tumaini amezitaja nyimbo hizo kuwa ni 'Tumuunge mkono JPM',  'Amani ya Tanzania' na Hongera awamu ya tano'.

  Tumaini amsema, wimbo wa 'Tumuunge mkono JPM' ni wa kuwahamasisha Watanzania popote walipo kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika vita ya uchumi anayoongoza kwa kuhakikisha inaziba mianya inayotishia upotevu au matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

  "Kama unavyoona Rais tayari ameshaamua kwa dhati kupigana katika vita ya kubana mianya inayotishia upotevu au matumizi mabaya yanayofanya na baadhi ya watu kutumia rasilimali za nchi vibaya kwa kujinufaisha wao huku taifa likiendelea kuwa masikini

  Hii siyo vita ndogo, ni kubwa sana inayohitaji ujasiri na ari kubwa ya kujituma, hivyo ni lazima Watanzania wote tumuunge mkono ili asiyumbishwe na waliokuwa wanajinufaisha na rasilimali hizi", alisema Tumaini wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala, Dar es Salaam.

  Amesema, wimbo wa 'Amani ya Tanzania' kunahimiza Watanzania ndani na nje ya Nchi kuhakikisha pia wanaienzi amani ya nchi kwa kuunga mkono juhudi za kuiimanrisha zinazofanywa na viongozi wakiongozwa na misingi imara iliyowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na pia Rais wa Kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

  Akizungumzia wimbo wa tatu wa 'Hongera awamu ya Tano', Tumaini amesema, wimbo huo ni wa pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa kutimiza kwa vitendo ahadi zilizotolewa na CCM wakati wa kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi katika uchaguzi mkuu uliopita.

  "Tumeona ni vizuri kutunga wimbo huu wa kumpongeza kwa sababu utekelezaji wa ilani na ahadi alizokuwa akizitoa kwenye kampeni unaonekana wazi japokuwa sasa ni miaka miwili tu tangu tumchague, kwa kweli Rais Dk. Magufuli amechapa kazi hivyo inastahili kumpongeza", alisema tumaini.

  Amesema, nyimbo hizo ambazo ni kwaya tayari zimeshakamilika na sasa wanamuziki wanazifanyia mazoezi ya mwisho mwisho  kabla ya kuzirekodi ili zianze kusikika katika maeneo mbalimbali na hasa pale kundi hilo litakapokuwa likitumbuiza.

  Mmiliki wa theNkoromoBlog aliyefika kwenye mazoezi ya kundi hilo, alishuhudia wanamuziki wote wakiwajibika kila mmoja katika eneo lake, huku baadhi yao wakitokwa jasho kuliko hata wanapokuwa wakitumbuiza jukwaani katika maonyesho maalum.
   Mwanamuziki nguli Juma Abdallah 'Jerry' akikipapasa kinanda kwa mkoni mmoja kuonyesha umahiri wake, Kundi la TOT Plus lilipokuwa katika mazoezi ya nyimbo tatu, leo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala Dar es Salaam
   Waimbaji Neca Twalib aliyechukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mwimbaji nguli na Mkurugenzi wa TOT Plus Marehemu Kampteni John Komba, akiimba na mwenzake Corobian Mkinga wakati wa mazoezi hayo
   Patrick Thomas akizicharaza tumba wakati wa mazoezi hayo
   Mkurugenzi wa TOT Plus Gasper Tumaini (mwenye suti) akizungumza na baadhi ya wadau waliofika kushuhudia mazoezi hayo
   Jerry akikicharaza kinanda kwa madaha wakati wa mazoezi hayo
   Waimbaji Rosemary William, Sharifa Mohammed na Mwasiti Suleimani wakiimba wakati wa mazoezi hayo
   Mwimbaji nguli Hadija Kopa na wenzake wakiimba wakati wa mazoezi hayo
   Tumaini akiwa na wadau wakati wakifuatilia mazoezi hayo. Kulia ni Jerry
   Waimbaji wa TOT Plus wakiwa kwenye mazoezi hayo
   Waimbaji wa TOT Plus wakiwa kwenye mazoezi ya wimbo wa 'Amani ya Tanzania'
   Jerry na Tumaini wakifuatilia kwa makini mazoezi hayo. Kushoto ni mdau wa TOT Plus
   Alen Elias aka Mchungaji akikicharaza kinanda kwa makini
   Evans Peter na said Mpiluka wakiyacharaza magita wakati wa mazoezi hayo
   Godfrey Kanuti akilicharaza gita wakati wa mazoezi hayo
   Neka twalib na Mkinga wakishauriana jambo wakati wa mazoezi hayo
   Fundi mitambo akiwajibika wakati wa mazoezi hayo
   Tumaini akijadiliana jambo na viongozi wa bendi ya Vijana Jazz ambao walihudhuria mazoezi hayo
  Wanamuziki wa TOT Plus wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wakati wa mazoezi hayo.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Daktari bingwa wa upasuaji wa Hospitali ya Agakhan, Dkt Aidan Njau (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari juu ya huduma ya Upandikizaji wa Matiti kwa wanawake waliokatwa matiti kutokana na majanga mbalimbali ikiwemo karatani ya matiti kulia ni daktari bingwa wa upasuaji kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt Edwin Mrema. 
  Dkt Edwin akiwa na baadhi ya wataalam wa magonjwa mbalimbali ya upasuaji.

  Hospitali ya Aga Khan imeanza kutoa bure huduma ya kupandikiza matiti kwa akina mama waliopatwa na magonjwa mbalimbali yaliyowapelekea kukatwa kwa kiungo hicho muhimu, ikiwemo wale waliokatwa kutokana na magonjwa ya Kansa, ukatili na kuungua moto.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Aga Khan, Dr. Aidan Njau amesema huduma iliyoanza leo ni kuhudumia mgonjwa mmoja mmoja ili kusaidia wanawake wengi wenye matatizo hayo ambao wamekuwa wakiishi na maumivu makali hata kujisikia vibaya katika jamii .

  “Kwa kuanzia tunaanza na wale wanawake waliokatwa matiti yao, tutatoa nyama kwenye sehemu yake ya mwili na kuipandikiza kwenye sehemu iliyokatwa na kuufanya muonekano wake urudi kama ulivyokuwa" amesema Dk. Njau.

  Amesema huduma hiyo, itawafanya watanzania kushuhudia wanawake wakipandikizwa matiti jambo ambalo halijawahi kutokea hapa nchini na kuwaasa wanawake wenye matatizo hayo wajitokeze hospitalini hapo kwa wingi kwa ajili ya kupatiwa huduma hii ya bure.

  Amesema, upasuaji huo utafanywa na madaktari wawili ambao ni Daktari bingwa wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Aga Khan, Dr. Aidan Njau na Daktari bingwa Edwin Mrema kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wote wakiwa na lengo la kurudisha furaha kwa wanawake wenye matatizo haya waliyokwisha ipoteza.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
  Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohamed Aboud Mohamed (katikati) alipowasilisha Muhtasari wa  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017, wakati wa kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)wengine ni  Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya  Mzee (kulia) na Naibu Waziri Mhe.Mihayo Juma N'hunga.
   Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbali mbali za  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),alipozungumza na Uongozi wa Ofisi hiyo katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
   Viongozi mbali mbali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),alipozungumza na Uongozi wa Ofisi hiyo katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ikulu)

  0 0


  Mtoa mada na Mchambuzi wa Sera na Utafiti wa Kujitegemea Prof Marjorie Mbilinyi akiongea na washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam Novemba 3 2017 kwa udhamini wa Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung (FES). (Picha na Robert Okanda Blogs)
  Washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam Novemba 3 2017 kwa udhamini wa Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung (FES)
  (Juu na chini) Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa wakifauatilia mada
  Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa wakifauatilia mada
  Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa wakifauatilia mada
  Waratibu Miradi wa Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung (FES) Anna Mbise na Amon Petro, wakiandaa mada za kuwasilishwa na watoa mada wakati wa kuanza kwa mkutano huo.
  Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa wakifauatilia mada.
  Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), Dkt. Stefan Chrobot akiongea na washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa.
  Washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam Novemba 3 2017 kwa udhamini wa Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung (FES)
  Washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam Novemba 3 2017 kwa udhamini wa Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung (FES)
  Washiriki wa Mkutano wa Vijana uliojadili maswala ya Ukosefu wa ajira, Ushiriki katika Demokrasia na Maendeleo, uliokuwa na kauli mbiu, ‘Vijana ni wadau katika upatikanaji wa suluhisho katika Jamii, Uchumi na Changamoto za kisiasa, wakijisali kabla ya kuanza kwa mkutano huo jijini Dar es Salaam Novemba 3 2017.

  0 0


  0 0


  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa Yakobo Lucas ambaye alikuwa mojawapo wa washindi wa zawadi za pikipiki na televisheni za LED katika promosheni iliyokwisha ya 'Tigo Nunua Simu na Ushinde'. Jumla ya pikipiki 20 na TV 20 zilitolewa katika promosheni hiyo.


  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya televisheni ya LED kwa Farida Rajab  ambaye alikuwa mojawapo wa washindi wa zawadi za pikipiki na televisheni za LED katika promosheni iliyokwisha ya 'Tigo Nunua Simu na Ushinde'. Jumla ya pikipiki 20 na TV 20 zilitolewa katika promosheni hiyo.

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya televisheni ya LED kwa Salum Yahawa  ambaye alikuwa mojawapo wa washindi wa zawadi za pikipiki na televisheni za LED katika promosheni iliyokwisha ya 'Tigo Nunua Simu na Ushinde'. Jumla ya pikipiki 20 na TV 20 zilitolewa katika promosheni hiyo.


  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa Yakobo Lucas ambaye alikuwa mojawapo wa washindi wa zawadi za pikipiki na televisheni za LED katika promosheni iliyokwisha ya 'Tigo Nunua Simu na Ushinde'. Jumla ya pikipiki 20 na TV 20 zilitolewa katika promosheni hiyo.


  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 1416 | 1417 | (Page 1418) | 1419 | 1420 | .... | 1903 | newer