Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1415 | 1416 | (Page 1417) | 1418 | 1419 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiashiria kuzinduliwa kwa zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ,amezindua zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo na kuongeza kuwa ujenzi wa Ofisi utafanka kwa haraka, chini ya Vijana wenye morali ya kazi kutoka JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.

  Ramani ya ofisi hizo inaonyesha kuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani, Taa za kisasa na Umeme.

  Akizungumza Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti RC Makonda amesema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika Mazingira mazuri yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.

  Sanjali na hayo Makonda amewapongeza Walimu wa shule za msingi kwakuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa Darasa la saba ukilinganisha na nafasi ya nne waliyo pata mwaka jana na amewaomba kutoichia nafasi hiyo , pia walimu wa shule za sekondari nao wajitahidi ili waongoze katika matokeo ya mtihani kitafa.

  "Rais ,ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi"alisema.

  Amewataka Viongozi kuacha Siasa kwenye mambo ya Msingi yanayolenga kuleta maendeleo kwakuwa Maendeleo hayana chama wala ubaguzi wa Dini."walimu hawa wanapowafundisha watoto wetu hawawaulizi vyama vyao wala dinizao tena watoto wenyewe hawa hawana vyama naombambeni ndugu zangu tuwe wamoja katika mambo ya maendeleo ,nashangaa kuna Wilayamoja wao hawatamani jambo jema nikupinga tu ,madai yao eti watanipa kiki,mmi sitafuti kiki nafanya kazi".

  Awali mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza wakati wa ukaribisho amemshukuru Rc Makonda kwa moyo wake wa kuwajali walimu kwa kuona shida yayao na kuahidi kufanya naye kazi begakwabega i kuendelea kutatua kero za wali na wananchi kwa ujumla ,Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar es Salaam Lazalo Mambosasa, Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule ,Diwani, Pamoja na wanachikutoka maeneo mbalimbali ya wilaya Ilala.

  Naye Diwani wa kataya Majohe Mwenyevyake Waziri amepongeza hatua ya mkuu wa koa wa Dar es salaam kwa juhudi anazozifanya katika shuguli za maendeleo na kusema kuwa anamuuga mkono aendelee mbele zaidi."kwakweli hatamimi ilikuwa ni shauku yangu kuona walimu wakifanya kazi katika mazingira mazuri wanakuwa naofisi nzuri na anachokifanya Makonda kitukizuri napia kama kiongozi wa serila anatimiza wajibu wake mimi nimtakie kilalakheri" Alisema Waziri.

  Nao baadhi ya wananchi walihudhuria uzinduzi huo wamesema weshukuru hatua hiyo na kusema kuwa walimu walikuwa wanadharirika ,walidharaulika walikuwa kamawametengwa ukienda ofisi za wizara zingne wanaofisi lakini wao walisahaulika sasa watafanya kazi kwa moyo kwakuwa watakuwa huru na maboyao .

  Kwa upande wake Mwenyekti wa kamati ya ujenzi Canal Mbuge amewataka watanzani kuendelea kuchagia ujenzi huo ilikujenga mshikamano na utaifa kwa kujitolea katika mambo ya maendeleo na kuahidi kuwa wao kama wasimamizi wa ujenzi huo watahakikisha ujenzi huo unafanyika kwa ubora na viwango na kukamilika kwa wakati.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akilakiwa na baadhi ya viongozi wa majeshi pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar alipokwenda kuzindua zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo.
  Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhiwa riasala iliyosomwa na mkuu wa shule ya msingiMajohe Grace Ndaro wakati wa uzinduzi wa zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo
  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza na wananchi wa kata ya Majohe wakati wa uzinduzi wa zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo
  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akipanda mti.
  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa kazini kuashiria uzinduzi wa ujenzi za ofisi hizo ukiwa tayari umepamba moto.
  Wananchi waliojitokeza.

  0 0

   Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akihutubia katika mkutano wa Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika  Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni. 
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Watanzania wanaosoma nchini China (TASAFIC) Bw. Remidius Emmanuel akizungumza katika mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
   Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China (Mwambata wa Elimu) Bw. Lusekelo Gwassa Akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa TASAFIC kwa Mwaka 2017.
   Baadhi ya Watanzania wanaosoma nchini China waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika  Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni. 
  Baadhi ya Watanzania waliohudhuria  Mkutano Mkuu wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi Mbelwa Kairuki

  Na Happiness Shayo- China.

  Balozi wa Tanzania  nchini China  Mhe Mbelwa Kairuki amewataka Watanzania wanaosoma katika Taifa hilo  kutumia fursa hiyo kuunga mkono juhudi za Tanzania kuelekea Uchumi wa kati ifikapo  mwaka 2025.
  Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma katika  Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Wuhan, Jimbo la Hubei.

  Balozi Kairuki alisema kuwa yapo maeneo kadhaa ambayo Watanzania hao wanaweza  kutoa michango yao katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwenye ujenzi wa Viwanda  ili sekta hiyo isaidie na kuleta tija katika ukuaji wa Uchumi. 

  Akizungumzia kuhusu sekta ya Utalii, Balozi Kairuki  aliitaja China kama soko jipya wanalopatikana watalii na kwamba kwa mwaka 2016 ni Wachina Millioni 120 waliokwenda nje ya nchi kutalii sawa na idadi ya watu wote wa  nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Burundi  na Rwanda,  idadi inayoonekana ni kubwa sana,ambapo kwa mwaka huo huo ni watalii 30,000 walipokelewa Tanzania kutoka China.

  “Zipo hatua kadhaa ambazo sasa zimechukuliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China, hivi sasa tunazungumza  na kampuni kubwa inayomiliki mitandao ya kijamii hapa ya  China ya TENCENT ili tuweze kutumia mtandao wao wa QQ kurusha vivutio vyetu vya utalii hapa China mubashara, lakini pia mwezi huu tulikuwa na Mazungumzo na Serikali ya China kuwajulisha nia ya shirika letu la ndege la Air Tanzania kuanza safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou. 

  Matarajio yetu ni kuona kwamba ifikapo Mwezi Septemba mwakani lengo hilo linatimia. Vilevile tumeanza kuzungumza na Mamlaka za China kuangalia uwezekano wa mashirika ya ndege ya China kuifanya Tanzania kuwa kitovu (HUB) ya safari zao Barani Afrika. Maana yake nini? Ndege kadhaa za China zinazokwenda Afrika zitakuwa zitasimamna (stopover) pale Dar es salaam au KIA au Mbeya (Songwe) kwa ajili ya kujaza mafuta na kupata huduma nyinginezo. Alisema Balozi Kairuki.

  Kwa upande wa Sekta ya Elimu Balozi Kairuki  amewataka Watanzania wanaosoma katika taifa hili kuendelea kutafuta fursa za masomo hapa China kwa faida ya watanzania wengine na kwamba China ina vyuo takribani 2000 hivyo jambo hili sio jukumu la Ubalozi pekee, hususani maeneo yenye upungufu katika taifa letu, huku akitoa kipaumbele kwenye  kozi za Kilimo na Uhandisi ambazo alizitaja kama nguzo muhimu katika Uchumi wa viwanda.

  “Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu. Kilimo kimeajiri zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wote ambao wengi wao wapo vijijiji. tunahitaji kilimo kuzalisha malighafi za viwandani na hatuwezi kutimiza malengo ya kujenga uchumi wa viwanda bila kufanya maboresho makubwa ya sekta ya kilimo.Lakini pia tunaamini kabisa Mtanzania anayekuja kusoma uhandisi hapa China mbali na elimu ya darasani, atapata pia exposure kubwa ya kazi za uhandisi zinazofanyika hapa China na tayari tumeanza kuzungumza na makampuni ya ujenzi ya hapa China kuyaomba yatoe fursa kwa wanafunzi watanzania kufanya elective programs ili mshiriki kwenye miradi mikubwa ya ujenzi.

  Aidha , Balozi Kairuki aliwataka Watanzania hao kutumia fursahizo kuvutia wawekezaji . “Tunahitaji uwekezaji wa mitaji, teknolojia na ujuzi katika kuanzisha na kuendesha viwanda nchini na  kazi yetu kubwa ni kuendelea kuvutia uwekezaji wa viwanda kutoka China sambamba na kutafuta teknolojia rahisi na nafuu zinazoweza kupelekwa nyumbani kuwezesha watanzania kufanya shughuli za uzalishaji. 

  Hivi sasa uwekezaji nchini kutoka China unakadiriwa kufikia dola za kimarekani Bilioni 3.7. Lengo letu ni kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 5 ifikapo mwaka 2020. Wanafunzi wanaosoma China ni muhimu kuwatumia pia Wahadhiri katika vyuo vyao, ambao wengi wao wanayo mahusiano na wa kichina ambao wana mitaji na wangependa kuwekeza barani Afrika. Alisema Kairuki.

  Akihitimisha hotuba yake Balozi kairuki  aliwataka Watanzania hao  kuheshimu tamaduni na sheria za taifa la China,Kila mmoja kutambua kusudi la uwepo wake hapa nchini kuepuka maisha ya kifahari, Kuchukua tahadhari  juu ya Madawa ya Kulevya, kuepuka migomo  kwa kuzingatia taratibu na sheria za vyuo vyao,kutunza na kulinda Afya zao na kwa wanafunzi wa shahada za uzamili na Uzamivu aliwataka  kufanya Tafiti zenye tija kwa Taifa la Tanzania.Ingawa pia alitumia nafasi hiyo kuwatambua Watanzania kadhaa wanaosoma katika Taifa hilo kutambua michango wao mkubwa walioutoa kwa manufaa ya Tanzania kupitia sekta ya Kilimo na Uhandisi. 

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Bw. Remidius Emmanuel alisema Mkutano huo  ulilenga kuwakutanisha Watanzania wote wanaosoma katika taifa la China  kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali juu ya Elimu na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo lakini pia kutengeneza sauti ya pamoja na kuona namna bora zaidi ya kutumia fursa hiyo ya uwepo wao katika taifa hilo kwa manufaa ya  Tanzania.

  “Tunamshukuru sana Balozi wetu Mhe. Mbelwa Kairuki wakati wote amekuwa karibu na sisi lakini kutumia muda mwingi kuzifanya taaluma zetu katika matumizi mapana yanayolenga kuendana na sera za nchi yetu hususani kipindi hiki ambacho taifa letu liko kwenye kasi ya kuelekea uchumi wa kati.Kwa hiyo Madaktari,Wataalam kilimo ,Wahandisi,Wachumi  na wataalam wengine wote  sasa wanaelekeza taaluma zao  kwa manufaa ya taifa letu” Alisema Remidius.

  Mapema akisoma Taarifa ya Mkutano huo Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw,Hussein Mtoro alisema  mbali na kuwaunganisha Watanzania kwa Umoja wao , Shirikisho hilo linalo jukumu la kuhakikisha Watanzania wote wanaosoma katika taifa la China  wanatoa mawazo,fikra zao ,kwa kutumia taaluma na uzoefu wao  kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.

  "Shirikisho limeweza kuweka mazingira mazuri kwa Watanzania wanaowasili China kwa mara ya kwanza kila mwaka, tunaendelea kutatua changamoto kwa baadhi ya mawakala wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiwatelekeza na kuwalaghai wanafunzi wapowaleta katika taifa hili,  lakini tunajivunia kuwa na  wataalamu mbalimbali ambao kutoa michango wa moja kwa moja kwa taifa letu, Mfano  wataalam kutoka fani za  Kilimo na uhandisi".Alisema Bw. Hussein

  Mkutano huo Ulihudhuriwa na Watanzania wanaosoma katika  Taifa la China  na baadhi ya watumishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China.

  0 0

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya meza kuu na wageni wa alikwa, tukio lililojiri katika viunga vya Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA).
   Watumishi wa umma na wageni waalikwa wakiwa wakifuatilia kwa ukaribu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu(MB) hayupo kwenye picha, mapema katika uzinduzi wa Maabara hamishika uliofanyika katika ofisi za TFDA.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara hamishika hizo, wakwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa, watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya TFDA Bi. Zainabu na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Hiiti B. Sillo.
  Mh. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kuhusu Maabara hamishika hiyo wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa.
   Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa ni Taasisi bora kwa Bara la Afrikakatika kudhibiti dawa na chakula ili watanzania wapate huduma bora.Ummy ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Maabara Hamishika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa katika kulinda afya za  wananchi ni kupata dawa zinazostahili ambazo zimedhibitiwa na TFDA.Amesema kuwa matumizi ya dawa zisizo sahihi zinarudisha kasi ya uchumi ambayo inatokana na watu kuingia  gharama za kununua dawa hizo mara kwa mara na tatizo kubaki pale pale.

  Ummy amesema kuwa licha ya kudhibiti dawa lakini TFDA isiwe kikwazo cha uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo wawekezaji wanatakiwa kufuata taratibu za nchi zilizowekwa.

  Aidha amesema kuwa kazi ya TFDA ni kuhakikisha afya za wananchi zinalindwa kwa kuwa na wananchi wenye afya njema na wanaweza kuwfanya kazi na kuliletea Taifa maendeleo.

  Amesema TFDA inatakiwa kuzingatia tathimini ya kina ya kisanyasi pamoja na matokeo ya uchunguzi wa maabara hivyo maabara  ya TFDA ni kiungo muhimu katika kutekeleza jukumu la kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa hizo.

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema jukumu la TFDA ni kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa wa bidhaa ya chakula na dawa, vipodozi na vifaa tiba na vitandanishi ili kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na matumizi ya bidhaa duni na bandia.

  0 0

  HALMASHAURI zote nane za Mkoa wa Dodoma zimekubaliana kuwa na utaratibu wa ziara za kubadilishana uzoefu hususan katika uendeshaji wa vikao na mikutano ikiwemo Baraza la Madiwani.

  Hayo yalisemwa jana na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe wakati akiwatambulisha baadhi ya Wenyeviti na Wataalam wa Halmashauri za Wilaya za Mkoani humo waliohudhuria mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Dodoma ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa ushirikiano huo.

  Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma, ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa White Zuberi Mwanzalila ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mheshimiwa Danford Chisomi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Samweli Kaweya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Rachel Chuwa. 

  Halmashauri zinazounda Mkoa wa Dodoma ni Manispaa ya Dodoma, Bahi, Chamwino, Kongwa, Mpwapwa, Kondoa Mji, Kondoa Vijijini, na Chemba.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa White Zuberi Mwanzalilaakijitambulisha kwa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma jana. Picha Zote-Ramadhai Juma-Ofisi Ya Mkurugenzi Manispaa Ya Dodoma
  Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia mkutano wa Baraza jana katika ukumbi wa Manispaa.
  Baadhi ya Wageni Waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Robert Mwinje, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma White Zuberi (wa pili kushoto), na Mwneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Danford Chisomi (wa pili kulia). Kushoto ni Meya wa Jiji la Mbeya Mstahiki David Mwasilindi.

  0 0


  Afisa Magereza Bwana Neuro Mbwilo amejishindia dau kubwa kuwahi kutolewa na Tatu Mzuka la shilingi milioni 110 kupitia Mzuka jackpot iliyoonyeshwa kupitia vituo mbalimbali vya runinga nchi nzima siku ya Jumapili ya Tarehe 29 Nov 2017.

  Kama ma milioni ya wachezaji wengine nchini Tanzania, Mbwilo alidhani ilikuwa ni fursa nzuri kutumia Shilingi 500 kubadilisha maisha yake pamoja na familia milele.

  Bwana Mbwilo, ambaye ni Askari gereza wilayani Temeke alielezea mshtuko wake juu ya bahati iyo iliyomtembelea. "Ni hisia ambayo haielezeki kabisa. Nina furaha kubwa sana, nimejawa na shukrani nyingi,na kwangu hii ni ajabu kabisa ", alielezea mbele ya vyombo vya habari.

  Katika kutoa hundi ya ushindi huo wa milioni 110 Bwana Sebastian Maganga, Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka alielezea zaidi juu ya ushindi huo mkubwa lakini aliwakumbusha Watanzania kwamba kuna njia nyingi za kushinda kupitia Tatu Mzuka. Alifafanua kuwa katika wiki 13 tu Tatu Mzuka imetengeneza zaidi ya washindi milioni 2 na kutoa billion 4 kwa washindi.

  Watanzania wanachokipenda kuhusu Tatu Mzuka sio mzuka jackpot tu ya kila wiki lakini pia ukweli kwamba kila ukicheza inakupa nafasi ya kushinda hadi milioni sita kila saa" alisema Maganga

  "Mambo yanavutia zaidi mwezi huu ambapo unaweza kushinda kila saa, kuingia kwenye droo ya ‘Jackpot’ ya Jumapili ambayo dau lake ni Milioni 60 wiki hii , na zaidi ya hapo ukicheza unapata nafasi ya bure ya kuingia kwenye droo kubwa yenye dau la kuvunja rekodi la Tshs 150million ya Supa Mzuka Jackpot itakayofanyika Novemba 19 mwaka huu ".

  Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bwana Felix Lyaniva ambaye alihudhuria mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi yake leo alizungumzia kuhusu matokeo chaya ya ushindi huo kwenye wilaya yake.

  "Afisa Mbwilo, sasa umekuwa balozi wa Tatu Mzuka katika Wilaya yangu. Natumaini utatumia fursa hii kubadili maisha ya watu wengine kama ambavyo Tatu Mzuka imebadilisha yako kwa kutumia vizuri mamilioni uliyojishindia. " alisema Mheshimiwa Lyaniya.

  Ingawa maisha yake yamebadilishwa milele, Afisa Mbwilo anapanga kuendelea kufanya kazi yake, akisisitiza kwamba ni mshahara wake ndio uliompa nafasi ya kucheza na kushinda.
   Mshindi wa millioni 110 Bwn. Mbwilo akiwa na washkaji zake wawili Juma Athuman na Joseph Haule Walio zawadia  milioni moja moja na Tatu Mzuka kwenye promotion ya "Cheza na Washkaji na Shinda na Washkaji".
    Bwana Mbwilo akisherekea ushindi wake na Mke wake Nyumbani kwao Keko.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva ( Kushoto)  akimkabidhi Mfano wa hundi ya sh Milioni 110 Ofisa ya Jeshi la Magereza Neuro Mbwilo, ambaye ni mshindi wa bahati nasibu ya Mzuka jackpot, Dar es Salaam.


  0 0

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), akizungumza na wajumbe katika mkutano wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), lililofanyika mkoani Kigoma.
   Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa baraza la tisa la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (hayupo pichani) katika ufunguzi wa baraza hilo, mkoani Kigoma.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi akitoa taarifa ya utendaji kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (kulia), mkoani Kigoma.
   Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Samson Hanga akizungumza na wajumbe katika mkutano wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), lililofanyika mkoani humo.
   Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa baraza la tisa la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakiimba wimbo wa mshikamano katika ufunguzi wa baraza hilo, mkoani Kigoma.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa katika Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala huo, lililofanyika mkoani Kigoma.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani Kigoma.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), amewapongeza Wakala wa barabara nchini (TANROADS), kwa mikakati wanayotumia kudhibiti vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini.

  Akifungua Mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi la TANROADS mjini Kigoma, Naibu Waziri Kwandikwa, amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watendaji wake wote wanakuwa waadilifu ili rasilimali chache zitumike kwa manufaa ya wote.

  “Hakikisheni kila mtakaye mkamata kwa vitedo vya rushwa hatua za kisheria anachukuliwa ikiwemo na kufukuzwa kazi ili kuonyesha kuwa jambo la rushwa tunalichukia na hatulipendi katika Serikali”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

  Naye Mtendaji Mkuu Wa Wakala huo Eng. Patrick Mfugale, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja watumishi 71  wamefukuzwa kazi katika vituo mbalimbali vya mizani hapa nchini kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.Ameongeza kuwa TANROADS wamejipanga kuhakikisha miradi yote ya ujenzi na vituo vya mizani vinafanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kujenga imani kwa wananchi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS Hawa Mmanga, amemuhakikishia Naibu Waziri wa Ujenzi kuwa wakala wake umejipanga kutekeleza kikamilifu ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja hapa nchini kwa wakati, ubora na kuzingatia thamani ya fedha.

  Wajumbe wa baraza la TANROADS kutoka mikoa yote  nchini wamekutana katika mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi ili kutathimini utendaji kazi wao na kuibua mikakati mipya itakayowezesha wakala huo kufanya kazi zake kwa weledi na kwa kukidhi mahitaji ya nchi.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda amewatahadharisha Viongozi wa dini nchini kujihadhari na kuwaozesha wasichana ambao hawajamaliza elimu ya kidato cha nne ili kuwakamata wazazi wote wanaoshiriki kuwaozesha watoto wao kwasababu ya kupewa mimba wakiwa masomoni.

  Amesema kuwa watoto wa kike wanashindwa kumaliza masomo kwasababu ya mimba ama kuozeshwa jambo ambalo limeendelea kuisumbua serikali katika juhudi zake za kuokoa maisha ya watoto wa kike ili waendelee na masomo na kuongeza kuwa Wilaya ya Nkasi kuna tatizo sugu la mimba kwa kuwa na mimba 152 kati ya 325 kwa Mkoa mzima.

  Amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini sana maisha ya watoto wa kike na inaendelea kuweka mikakati ya kila namna ili kuhakikisha kuwa wasichana hao wanapata elimu stahiki, kwa kuanza na elimu bure na kuendelea na mikakati ya marekebisho ya sheria kadhaa ili watoto wa kike waendelee na masomo.

  “Haiwezekani mtu anatakatisha fedha hapati dhamana, halafu mtu anampa mimba mwanafunzi na kisha anapata dhamana, tunakoelekea ili uolewe lazima uwe na “leaving Certificate” ama tujue kuwa hukusoma kabisa ili tuwahoji wazazi, mwananfunzi ambae ataolewa kwa kukatishwa masomo kamata wote na funga miaka 30, wazazi wa pande mbili, aliyeoa, aliyeolewa, wanaoshangilia, aliyefungisha ndoa wote miaka 30 jela,” alifafanua.

  Aidha, amewashauri wanaharakati kuungana pamoja katika kuwaelimisha watoto wa kike na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha mimba zinapungua na kuwa vitendo hivyo haviendelei, ili kuwainua watoto wa kike kielimu.

  Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya katika majumuisho ya ziara yake ya siku moja katika Mkoa wa Rukwa kwa kutembeleavituo vya afya, Shule zinazoendelea kujengwa pamoja na miradi ya maji.

  Sambamba na hilo Mh. Kakunda pia ameagiza kutosajili vijiji, vitongoji wala kupeleka umeme kwenye hifadhi na kuwaondoa wale wote waliopo kwenye hifadhi na kusisitiza kuwa wananchi wasidanganyike na viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwambia kuwa watawalindwa ili kuendelea kuharibu hifadhi, jambo hilo halipo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Milundikwa Pius Msongoli wakati alipotembelea shule hiyo inayoendelea kujengwa huku serikali ikichangia shilingi milioni 250 za ujenzi wa shule hiyo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (Kaunda suti Nyeusi) akitoa maagizo ya kuwaondoa wale wote waliopo ndani ya hifadhi ya msitu wa mfili, kwa kuwa wanachangia kuharibu chanzo cha maji na bwawa la Mfili.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya ujenzi wa maabara inayoendelea kujengwa katika shule ya sekondari Milundikwa mbele ya Mkuu wa Shule hiyo Pius Msongole, Katibu tawala wa Wilaya ya Nkasi Festo Chonya pamoja na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Emanuel Mtika.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (aliyeshika chepe) akisaidia ujenzi wa wodi za kituo cha afya Nkomolo, Wilayani Nkasi.

  0 0


  Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky) mara baada ya kuzuru katika kiwanda hicho kilichopo katika eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara. (Picha Zote Na Mathias Canal).
  Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
  Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).


  0 0

  Balozi wa Norway nchini Tanzania kupitia kwa Balozi wake Balozi Bi. Hanne-Marie Kaarstad leo wameweza kutiliana saini mkataba wa udhamini wa donge nono la kiasi cha Dola 128200(USD) ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Milioni 300, ambazo zitaenda kusaidia Shirika lisilo la Kiserikali la Busara Promotion kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara 2018. Halfa hiyo ya kutiliana saini imefanyika mapema leo Novemba 2,2017 katika Ubalozi wa Taifa hilo la Norway, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari. 

  Awali Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud alishukuru Ubalozi wa Norway nchini Tanzania kwa kutoa udhamini huo ambao utasaidia uhai wa tamasha hilo ambalo limejizolea sifa kwa muda mrefu. “Sauti za Busara imepata msaada, shukrani kwa ubalozi wa Norway nchini Tanzania. Norway inaonyesha mfano mzuri wa kuigwa Duniani kwa kuchangia katika maendeleio ya kudumu na mazingira rafiki. Kama ilivyo katika malengo yake nchini Tanzania. 
  Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kutiliana saini. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na kulia ni Ofisa wa Busara Promotions.

  Ubalozi wa Norway tangu mwaka 2009 unatoa mchango mkubwa wa kifedha kwa shirika la Busara Promotions, ili kuliwezesha kutimiza mpango mkakati wake hii ni pamoja na kusaidia shughuli za kiutendaaji wa tamasha kwa kila mwaka na tunafurahia kwani tunaamini utaendelea pia kwa mwakani” alieleza Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud. Pia akifafanua umuhimu wa tamasha la Sauti za Busara, Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud alibainisha kuwa, tamasha hilo limekuwa likiunganisha watu wa rika na asili tofauti huku pia likiheshimu uhuru wa kujieleza sambamba na kuleta umoja, Amani na kuimalisha jamii. 

  “Tamasha la Sauti za Busara linatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sekta ya muziki kukutana na kujifunza. Linaimarisha utaalamu katika sekta ya Sanaa nchini hivyo yote haya lengo kuu la tamasha ili ni kuhakikisha kutangaza amani, mshikamano na kuheshimu tamaduni tofauti” alimalizia Yusuf Mahmoud. 

  Kwa upand wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad ameahidi kuendeleza ushirikiano na Busara Promotions katika kusaidia Sanaa na Utamaduni ambapo lengo kuu ni kukuza mashirikiano na maingiliano ya kitamaduni kupitia sanaa hasa muziki katika jamii kwa njia ya tamasha hilo la kila mwaka la Sauti za Busara. “Najisikia furaha sana katika siku ya leo katiliana saini udhamini huu mnono. 

  Tumekuwa na Busara Promotion kwa muda mrefu kuanzia 2008 mpaka sasa tukiendelea kukuwa zaidi na kuleta mageuzi kwa jamii hasa kuleta mageuzi makunwa sana kwa jamii ya Wazanzibar, Tanzania Bara na Ukanda wa Afrika kwa ujumla. Tunaamini Sauti za Busara wamejijengea mizizi imara Visiwani Zanzibar na Tanzania Bara kwa ujumla kupitia tamasha lao ambalo linainua na kulinda utamaduni wa Mzanzibar huku pia likilinda hutu na utamaduni wake ndani ya visiwa hivyo vya Zanzibar.” Alieleza Balozi Bi. Anne-Marie Kaarstad. 

  Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakitiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. Wengine wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa Norway na Busara Promotions.

  Balozi huyo aliongeza kuwa, tamasha hilo pia limekuwa na nguvu kubwa ikiwemo kukusanya watu wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Dunia na kukutana mahala pamoja kufurahia. Aidha, Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud amebainisha kuwa, msimu wa Sauti za Busara kwa 2018, tayari wametangaza listi ya wasanii na vikundi ambapo jumla ya vikundi 20 kutoka Tanzania Bara, pia vipo kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, DRC, Nigeria, Morocco, Algeria, Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Misri Sudan, Gambia. 

  Pia vipo vikundi kutoka nchi za Reunion, Norway, Denmark na Switzerland. Katika vikundi hivyo vinatarajia kuwa na Wasanii 400, ambapo wataonyesha uwezo wao kwenye majukwaa matatu tofauti, shoo 46 zote zikiwa asilimia 100 ‘live’ kwa siku nne mfululizo. Pia kutakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo warsha na semina kwa wanamuziki wa ndani na nje ambao watapata kubadirishana ujuzi na mbinu za kukuza sanaa na masoko ya muziki wao. 
  Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakibadilishana hati walizotiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Amina Shaban (kushoto) akiupokea ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya, ukiongozwa na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo Bw. Neven Mimica (katikati) na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw. Roeland van de Geer, walipokuwa wanawasili Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa msaada wa Euro milioni 50 kwa Tanzania.


  Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akitoa maelezo ya ujio wa ugeni huo kuwa ni neema kwa nchi ya Tanzania kwani Umoja wa Ulaya wametoa msaada wa Euro Milioni 50 utasaidia vijijini 3600 nchini kupata umeme.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) na akimweleza jambo Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Mr. Neven Mimica wakati wa hafla fupi ya Umoja wa Ulaya (EU) kutiliana saini makubaliano ya msaada wa Euro milioni 50 kwa ajili ya kusaidia usambazi wa umeme vijijini kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza umeme Vijijini (REA).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiwa pamoja na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Bw. Neven Mimica wakisaini Mkataba wa msaada wa fedha za kusaidia usambazaji wa umeme Vijijini (EURO milioni 50) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Mr. Neven Mimica, wakibadilishana hati za makubaliano ya msaada wa ruzuku ya kiasi cha EURO Milioni 50 katika ukumbi wa wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiwa na Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa msaada wa utekelezaji wa nishati ya umeme vijijini katika ukumbi wa Wizara ya fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiagana na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Bw. Neven Mimica, baada ya kusaini mkataba wa msaada wa Euro milioni 50 ambazo Umoja huo umeipatia Tanzania kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini REA.


  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango


  ………………


  Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

  TANZANIA imezidi kupata neema kutoka Jumuiya ya Kimataifa ambapo Novemba 2, 2017, Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 50, takriban Shilingi bilioni 130 kwa ajili ya kufadhili Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Mkataba wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Neven Mimica.

  Msaada huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya nishati ya umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao wa usambazaji umeme.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu wake.“Umoja wa ulaya ni wadau wetu muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu na mikubwa wanayotupatia, na kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema Bw. James

  Alisema kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo bila masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya viwanda itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Bw. Doto James alisema kuwa tangu Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini REA uanze miaka 9 iliyopita, idadi ya vijiji vilivyounganishiwa umeme imeongezeka kutoka vijiji 400 mwaka 2008 hadi kufikia vijiji 4395 hivi sasa.

  Alisema kuwa ni matarajio ya Serikali kwamba ifikapo mwaka 2020, vijiji vyote 12,000 hapa nchini vitakuwa vimeunganishwa na nishati hiyo hivyo kuchochea shughuli za uzalishaji viwandani na kiuchumi kwa wananchi, vitaimarika.

  Kwa upande wake, Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Neven Mimica, amesema kuwa msaada huo wa Euro milioni 50 wanaoutoa ni sehemu ya msaada wa Euro milioni 207 ambazo wanachama wengine wa Umoja huo, ikiwemo Sweden, Uingereza, Norway na Benki ya Dunia, watatoa kufanikisha mradi huo wa usambazaji umeme vijijini kupitia REA.

  “Nguvu hizi za pamoja zitaviwezesha takriban vijiji 3,600 vilivyoko maeneo mbalimbali ya nchi ambapo watu zaidi ya milioni 1 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo” Alisema Bw. Mimica.Alisema hatua hiyo itachangia kuimarika kwa ubora wa maisha ya wananchi wa Tanzania, kuimarika kwa sekta za afya, elimu na kuleta faida za kijamii na kiuchumi zinazoonekana kwao moja kwa moja hususan wanawake na watoto.

  Misaada ya Umoja wa Ulaya kwa Tanzania imejikita katika Nyanja tatu za Utawala bora, Umeme na Kilimo endelevu ambapo Umoja huo kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (EDF) umetenga kiasi cha Euro milioni 626 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014-2020

  0 0

   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua nyaraka mbalimbali alipotembelea Kiwanda cha China Paper Corporation.

    Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua kiwanda cha China Paper Corporation.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akizungumza katika kiwanda cha China Paper Corporation..


  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya ukaguzi wa masuala ya kazi na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.

  Mavunde alianza ziara hiyo katika shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM) ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kutoa maagizo kwa Menejimenti ya Uongozi wa Shule hiyo kutoa mikataba kwa wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini kinavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kuagiza Taasisi za Serikali kuchunguza malalamiko juu ya unyanyasaji kwa wafanyakazi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa menejimenti.

  Mavunde pia alitembelea Kiwanda cha China Paper Corporation ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kuiagiza Menejimenti ya Kiwanda hicho kuhakikisha sheria za Kazi zinafuatwa kwa kutoa Mikataba kwa wafanyakazi wote na kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa ikiwemo usalama wa mazingira ya kufanyia kazi.Pamoja na maagizo hayo kwa kiwanda,Naibu Waziri Mavunde aliwataka wafanyakazi nao kutimiza wajibu wao na kutumia njia sahihi za malalamiko yao bila kuvunja sheria za nchi.

  Wakati huo huo,Naibu Waziri Mavunde amewaaguza Afisa Kazi Mfawidhi na Afisa wa Uhamiaji wa mkoa wa Kilimanjaro kuzishikilia hati za kusafiria za raia wa kichina 9 mpaka watakapowasilisha Vibali vya kufanya kazi nchini na Vibali vya makazi.

  0 0

  Mgeni rasmi, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifungua semina kuhusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa kwa Wanachama wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC) iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.


  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akifuatilia semina kuhusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa kwa Wanachama wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC) iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma. wa pili kulia ni katibu wa Bunge, Mheshimiwa Stephen kagaigai, wa pili kushoto ni katibu wa Chama hicho, Mheshimiwa Daniel Mtuka na kushoto ni kaimu Mwenyekiti wa Chama hicho, Mheshimiwa Cecilia Pareso.
  Spika wa Bunge Mheshimiwa, Job Ndugai (kulia) akipokelewa na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC), Mheshimiwa Cecilia Pareso (kushoto) kwenda kufungua semina kuhusu maadili na Mapambano dhidi ya rushwa iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
  Wanachama wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC) wakifuatilia semina kuhusu maadili na Mapambano dhidi ya rushwa iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0

   Trade and Development Bank (TDB), ‎Director Syndications & Strategic Initiatives, Samuel Mugoya delivers his key note address to the audience from financial institutions, private sectors, government institutions and other invited dignitaries  at the function  to official launch the brand name from PTA Bank to TDB in Dar es Salaam recently.
   Trade and Development Bank (TDB), Director Corporate Affairs & Investor Relations, Mary Kamari talking to the audience from financial institutions, government and other invited dignitaries at the function to official launch the brand name from PTA Bank to TDB.
   Rand Merchant Bank Head, East Africa Loan Solutions, Misheck Chingaya (left) chats to some invitees attended the function organised by Trade and Development Bank (TDB)  to official launch the brand name from PTA Bank to TDB. From second left are, National Housing Corporations Director of Treasury and Business Development, David Shambwe, TDB Principal Project and Infrastructure Finance, Neema Siwingwa, FNB Head of Business Development, Mussa Mhando and NHC Business Planning Manager, Arden Kitomari. 
   TDB Bank Principal Project and Infrastructure Finance, Neema Siwingwa (second left), National Housing Corporation Business Planning Manager, Arden Kitomari (left) together with other invited dignitaries admires a performance from Tanzanian local band.
   TDB Bank senior officials poses for a memento photograph with some invited guests. 
  Traditional ngoma artists entertain the audience during the official launching ceremony of the brand name from PTA Bank to TDB.

  0 0


  0 0

  Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi ya Wema 2109, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya kwa ajili ya kupanda katika shamba darasa katika Kijiji cha Msasa kilichopo Kata ya Runzewe wilayani humo leo. Wengine kutoka kulia ni Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula na Mtafiti, Dk. Beatrice Lyimo  kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
  Maofisa Ugani wakiandaa shamba darasa la mahindi ya Wema  katika Kijiji cha Kabagole kilichopo Kata ya Busonzo litakalosimamiwa na Kikundi cha Igembensabho.
  Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya, akizungumza na wakulima wa Kikundi cha Igembensabho.
  Wanakikundi cha Igembensabho wakiwa wameshosha mikono ikiwa ni ishara ya mshikamano.
  Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akimkabidhi mbegu ya mhogo aina ya Mkombozi, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya kwa ajili ya kupanda katika shamba darasa katika Kijiji cha Msasa kilichopo Kata ya Runzewe wilayani humo leo. Wengine kutoka kulia ni Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula na Mtafiti, Dk. Beatrice Lyimo  kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
  Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya akikmabishi mbegu ya Wema Ofisa Ugani wa Kijiji cha Kabagole, Ponsian Pancras.
  Mtafiti wa Kilimo kutoka Kituo cha Utafiti wa Ilonga mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akiwafundisha wakulima wa Kijiji cha Kabagole namna ya kupanda mahindi ya Wema. Kulia ni Ofisa Ugani, David Makabila kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  Katibu wa Kikundi cha Igembensabho, Jacob Nsunzu akizungumza na waandishi wa habari.
  Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya akikmabishi mbegu ya Wema Ofisa Ugani wa Kijiji cha Msasa, Mohamed Mwangeni. Katikati ni Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
  Mtafiti wa Kilimo kutoka Kituo cha Utafiti  Ilonga mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akiwafundisha wakulima wa Kijiji cha Msasa, namna ya kupanda mahindi ya Wema.

  Na Dotto Mwaibale, Bukombe Geita

  WAKULIMA wilayani Bukombe Mkoani Geita wameiomba Serikali na wasambazaji wa mbegu bora za mahindi ya WEMA 2109 yanayostahimli ukame kufikisha mbegu hizo wilayani humo ili kuweza kutatua changamoto ya  mavuno kidogo wanayoyapata kila mwaka kutokana na mabadiriko ya tabia nchi na wadudu.

  Ombi hilo limetolewa na wana Kikundi cha Igembensabho kwenye Kijiji cha Kabagole Kata ya Busonzo wilayani Bukombe mkoani Geita wakati wakipokea mbegu bora za mahindi  yaliyozalishwa na Mradi wa WEMA kwa ajili ya kupanda kwenye shamba darasa la kikundi hicho ili waweze kuyalinganisha na aina za mahindi wanayolima kila mwaka na mahindi hayo yenye sifa ya kustahimili ukame yaliyotolewa na  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

  Akizungumza  kwa niaba ya wanakikundi hicho, Adam Kasalamsigwa alisema kuwa kutokana na sifa walizoambiwa na wataalamu kwenye mahindi hayo yatakuwa mkombozi kwa wakulima wengi kutokana na aina zingine za mahindi waliyozoea kupanda kushindwa kutoa matokeo waliyokuwa wakiyatarajia baada ya mvua kukata mapema kabla mahindi hayajazaa.

  “Tunashukuru mmetuletea mbegu hizi ili tufanye majaribio na kuona jinsi mahindi haya yanavyostahimili ukame lakini mmetuambia tayari mmeshayafanyia majaribio kwenye maeneo mengine ya Tanzania na kuonyesha mafanikio makubwa hivyo hatuna sababu ya kusubiri hadi msimu ujao tuleteeni mbegu hizo tununue na kupanda” alisisitiza Kasalamsigwa.

  Aidha wakulima hao wameiomba Serikali kuona sababu ya kuziingiza mbegu hizo kwenye ruzuku ya pembejeo ili ziweze kuwafikia hadi vijijini kwa bei nafuu ili ziweze kukinzana na mabadiliko ya taba nchi ambayo yamekithiri sana kwenye wilaya hiyo na maeneo mengine.

  Akitoa maelekezo ya namna ya kupanda mahindi hayo Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda aliwaambia mahindi hayo baada ya kufanyiwa utafiti kupitia mradi wa mahindi yanayotumia maji kwa ufanisi (WEMA) waliyajaribu kwenye maeneo mbalimbali kwenye mikoa ya Morogoro na Tanga na kuonyesha kufanya vizuri kuliko aina nyingine za mahindi wanayolima wakulima.

  Ngolinda aliwasisitiza kuwa pamoja na wao kupata mbegu hizo zinazostahimili ukame lakini ni lazima wazingatie kanuni bora za kilimo cha mahindi ikiwemo matumizi ya mbolea za kupandia na kukuzia ,kupanda kwa mistari na nafasi  na kufanya Palizi lakini wasipofanya hivyo hawawezi kupata mavuno yanayostahili badala yake watapata hasara kama mahindi mengine.

  Aliwataka kuzingatia suwala la kupanda kwa mistari na nafasi ili kuweza kumshakikishia mkulima anatumia shamba lake vizuri badala ya kupanda holela na kujikuta amepanda miche michache kwenye shamba akidhani ni ekari moja kumbe ni miche inayoenea kwenye nusu ekari iliyopandwa vizuri.

  Ngolinda aliwashauri wakulima kulima ekari moja kitaalamu na kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ili apate mavuno makubwa badala ya kulima ekari tano ambazo anatumia nguvu nyingi na gharama kubwa lakini mwishoni anapata mavuno sawa na mtu mwenye ekari moja.

  “ Unalima ekari tano bila kufuata kanuni bora za kilimo alafu unapta magunia 25 ya mahindi wakati mwenzako analima ekari moja tuu kwa kufuata kanuni bora za kilimo na anapata hadi gunia 30 hii ni tofauti kubwa sana kwa hiyo wakulima naomba mbadilike” alisistiza Ngolinda.

  Aidha Mtafiti huyo wa zao la mahindi aliwaambia kuwa kufanya majaribio hayo kupitia mashamba darasa kwenye mkoa mzima wa Geita ni kutaka kuwaonyesha wakulima hao mbinu za kisasa za kilimo na matumizi ya mbegu bora yanavyoweza kumsaidia mkulima kuzalisha kwa tija ili aachane na kilimo cha mazoea ambacho hamkimsaidii mkulima kuondokana na umasikini lakini kupata chakula cha kutosha.

  Awali akizungumza na watafiti hao kutoka COSTECH, Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiriguru Mwanza na Maruku mkoani Kagera kabla ya kwenda kutembelea mashamba darasa na kufanya uzinduzi huo kwenye wilaya hiyo ,Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo,  Dionis Myinga ameishukuru COSTECH na OFAB kwa kusaidia kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wakulima kwa kuwapelekea mbegu hizo bora ambazo zinajibu changamoto mbalimbali sugu za wakulima.

  Myinga alisema sio wataalamu hao wametembea umbali mrefu kutoka Dar es salaamu hadi Geita ili kufikisha matunda ya utafiti kwa wakulima hivyo wilaya yake itafanya kazi bega kwa bega katika kuhakikisha malengo ya mpango huo yanafikiwa ili kuchochea uzalishaji wa mazao hayo kupiti mashamba darasa hayo.

  “Tafiti zipo nyingi sana kwenye vituo vya utafiti na vyuo vikuu lakini zinabaki kwenye makabati tuu na hazitumiwi kwenye kutatua tatizo lililokusudiwa lakini kila utafiti ungefika kwa mlengwa naamini Tanzania tungekuwa mbali sana kwenye mambo mbalimbali hususani kilimo” alisema Myinga.

  Katika kuonyesha kuridhika kwake na maelezo ya mbegu za mahindi na mihogo iliyoletwa kwenye wilaya yake akaomba  mbegu za kununua za mihogo hiyo aina ya Mkombozi za kutosha kupanda shamba la ekari kumi ili iwe mfano kwa wakulima wilayani humo pamoja na kuwa chanzo cha kusambaza mbegu nyingi kwa wakulima wengi zaidi.

  Vijiji vilivyonufaika na uanzishwaji wa mashamba darasa katika wilaya hiyo ni Kijiji cha Msasa na Kabagole ambapo mashamba hayo yatasimamiwa na vikundi.

  Watafiti hao kesho siku ya Ijumaa wanatarajia kwenda Halmshauri ya Mji wa Buchosa Sengerema kwa ajili ya kazi ya kuanzisha mashamba darasa na kisha wiki ijayo kwenda kumalizia  kazi ya kusambaza mbegu hizo Mkoa wa Tabora.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akimkabidhi Cheti cha Shukrani Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, kutoka kwa Shirikisho la Vyama vya wenye ulimavu Tanzania, SHIVYAWATA, wakati wa Tamasha la Sita la Watu wenye Ulemavu, lililofanyika kwenye ukumbi wa LAFP, Makumbusho jijini Dar es Salaam, leo Nov 2, 2017. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akizungumza wakati wa Tamasha hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Taifa, Ummy Nderiango.
  Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, akizungumza wakati wa Tamasha hilo.
  Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, akionyesha Cheti alichokabidhiwa katika Tamasha hilo.
  Mgeni rasmi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tamasha hilo.
  Mgeni rasmi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tamasha hilo.
  Wakipasha misuli baada ya mazungumzo ya muda mrefu
  Salamu.......
  Paleeee, umeona eeeh....

  0 0

  Waziri Mpina na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bukoba wakielekea katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katika kata ya katerero kijijini Kyerwa leo.
  Katika picha ikionekana sehemu ya ng’ombe aliyepigwa chapa katika kata ya Katerero kijijini Kyerwa leo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi. Saada Malunde baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro, wengine katika picha ni askari wanyamapori wa pori hilo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi Saada Malunde wakizungumza baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro.  NA MWANDISHI MAALUM – KATERERO

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhanga Mpina amewataka wafugaji nchini kutembea kifua mbele kwa kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo, Mpina ameyasema hayo leo aliposhiriki katika zoezi la kupiga chapa Mifugo katika Kijiji cha Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero halimashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera, na kuwataka viongozi kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.

  Waziri Mpina alipofika katika kata ya Katerero aliwakuta wafugaji wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la uwekaji alama katika mifugo yao na kushiriki zoezi hilo kwa kuonyesha msisitizo.

  Mara Baada ya kushiriki zoezi hilo, Waziri Mpina aliwataka wafugaji hao kuendelea kujitokeza kwa wingi na kuleta mifugo yao kupigwa chapa na kusema kuwa zoezi hilo ni la manufaa na faida kwa wafugaji kwani litaweza kuwasiadia kuhepuka maambukizi ya magonjwa ya wanyama kwa mifugo yao kuto kuchanganyikana na mifugo mingine sambamba na kusaidia upotevu wa mifugo.

  Akiongea katika zoezi hilo diwani wa kata ya Katerero Bw. Nuru Abdul Kabendera alisema kuwa, amefurahishwa na ziara ya Waziri Mpina katika kata ya katerero kwani ni mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka katika ngazi ya juu ya serikali na kumuomba Mpina kupitia Wizara yake kutatua changamoto inayoikabili kata hiyo la josho la kuoshea ng’ombe ambapo Waziri Mpina amehaidi kuitatua.

  Katika hatua nyingine Waziri Mpina ametembelea mapori ya Burigi yaliyopo wilayani Biharamulo ambapo ameupongeza uongozi wa mkoa kwa uporasheni iliyofanyika ya kuondoa mifugo katika mapori tengefu na hifadhi za misitu ambapo amewashuhudia wanyama pori ambao tayari wamerejea katika mapori hayo huku mkuu wa wilaya hiyo Bi SAADA MALUNDE Akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano katika zoezi la kuondoa mifugo.

  Aidha, Mpina amewataka wakuu wa Mikoa ya mipakani kuwasilisha kwake taarifa ya uondoshwaji wa mifugo katika mikoa yao mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la oparesheni ondoa mifugo.

  Waziri MPINA amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani kagera kubwa akiwa ameagiza mifugo yote iliyokamatwa kutoka nje ya nchi itaifishwe na kupigwa mnada haraka sana kwa mujibu wa sheria.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Mhandisi Victor Seif akieleza majukumu ya TARURA kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Bw.Abdul Digaga akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

  ……………

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema hatavumulia kuwa na watumishi mizigo ambao hawatimizi majukumu yao kikamilifu na kuleta mabadiliko katika sekta ya barabara ambayo ni nguzo ya uchumi nchini.

  Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wabunge wa Kamati ya kudumu Serikali za mitaa(TAMISEMI) sambamba na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kuhusu majukumu ya Wakala wa barabaraza vijijini na mijini(TARURA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma

  Mhe. Jaffo amesema Serikali ilishatoa muongozo wa malengo ya utendaji kazi katika utumishi wa umma na kuwapima kulingana na malengo yao hivyo watumishi ambao watashindwa kutekeleza na kufikia malengo waliyopangiwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kiutumishi.

  Amesema kuwa Serikali haitavumilia suala zima la ubadhilifu kwa watumishi wa umma, kwa kuwa Serikali haiwezi kumbeba mtu ambaye ni mbadhilifu kwa kuwa Serikali inahitaji kuleta mabadiliko katika utendaji kazi na kuleta maendeleo kwa jamii.

  Amesema kuwa Taruara ni chombo kipya hivyo haitaji kuajiri watumishi ambao ni mzigo ambao waleta sura mbaya kwa jamii kabla chombo hiki hakijafanya kazi ya kuwahudumia wananchi katika kutatua kero ya miundombinu ya barabara vijijini na mijini.

  Amewataka Wabunge wa kamati zote mbili (LAAC&TAMISEMI) kusimamia utekelezaji wa miradi iliyoko chini ya TARURA na kuhakiki ubora wa miradi hiyo na kukosoa pale wanapoona miradi haitekelezwi kwa viwango vinavyotakiwa ili wahusika waweze kurekebisha makosa kabla ya kukabidhi miradi hiyo kwa wahusika.

  Aidha aliwahisi Wabunge kuendelea kuishauri TARURA kwa kuwa chombo hiki kimeundwa kwa ajili ya kutoa majibu ya changamoto za Wananchi hivyo ni wajibu wetu kuwasilisha yale yote ambayo tunaona yanawakwaza wananchi katika majimbo yetu.

  Mhe Jafo amemuuagiza Mkurugenzi wa TARURA Mhandishi Victor Seif kuhakikisha Mameneja katika ngazi ya Wilaya wanasaini Mkataba wa Makubaliano ya kazi “Performance contract”na kuwafuatilia utendaji wao kwa mujibu wa Mkataba na atakeyeshindwa kufikia malengo yaliyowekwa atolewe bila kigugumizi ili kupisha watendaji wengine watakaofanya kazi kulingana na matakwa ya Serikali.

  Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif amesema kulingana na muundo na majukumu ya Wakala wa Barabara mahitaji halisi ya watumishi ni 3,222 lakani mpaka sasa ni watumishi 1,147 wameshapatikana ambapo 47 wako Makao Makuu, 103 Mikoa na 997 katika halmashauri, na pia kuna upungufu wa watumishi 2,075 katika kada mbalimbali.

  TARURA ina majukumu ya Msingi ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara zenye urefu wa Km 108,946.2 za vijini, mijini pamoja na madaraja, na kati ya hizo barabara 56,000 zinafanyiwa uhakiki ili ziweze kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali ili zitambulike kisheria na Km 52,946.2 tayari zimeshatambulika na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera amevitaka vyama vya ushirika wilayani hapo kuhakikisha wanatumia mizani yenye lengo la kumsaidia mkulima wa zao la korosho awezekupata matunda mema bala ya kulalamika kila siku hayo ameyasema wakati wa kuzindua mnada wa korosho katika kata ya nakapanya mkoani RUVUMA habari kamili hii hapa VIDEO YAKE.

  0 0

   Mwenyekiti wa Halmashauri MH. Ramadhani Diliwa wa tatu kushoto akizungumza na vikundi juu ya usimamizi bora wa matrekta hayo kwa lengo la kuchochea matumizi ya zana bora zakilimo
   Mwenyekiti wa Halmashauri MH. Ramadhani diliwa akijaribu kuwasha trekta mojawapo Kama ishara ya majaribio baada ya matengenezo.
   Muendeshaji wa trekta aliyeshika usukani wa trekta akitoa ufafanuzi wa vitendo kwa Mkurugenzi Mtendaji William Makufwe mwenye shati jeupe juu ya namna ya uendeshaji wa trekta hilo
   Mkurugenzi Mtendaji William Makufwe wa pili kushoto akizungumza na wanavikundi juu ya kujali muda wa kutumia na kupumzisha matrekta ili yaweze kudumu. Pembeni ni Mwenyekiti wa Halmashauri
   Baadhi ya Matrekta yaliyokabidhiwa kwa vikundi vya wakulima Leo.
   Picha ya pamoja Kati ya Viongozi wa Halmashauri na wanavikundi Mara baada ya makabidhiano.
  Mwenyekiti wa Halmashauri MH Ramadhani Diliwa akimkabidhi Kiongozi wa kikundi cha umoja wa marafiki Mkata  nakala za mkataba .


  Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni umekabidhi matrekta manne (4) kwa vikundi vya uzalishaji na kuvitaka vikundi hivyo kutumia matrekta hayo kwa lengo la kuchochea kasi ya maendeleo ya kilimo kwenye maeneo yao. 

  Akikabidhi matrekta hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa amewaeleza vikundi kuwa Halmashauri imeamua kuwapa matrekta hayo kama mtaji kutokana na utayari wa vikundi vyenyewe kwani vikundi vipo vingi ambavyo vingeweza kupewa na hivyo watambue wanao wajibu wa kuyatunza na yasiwe chanzo cha migogoro. 

  Amesema kuwa Halmashauri inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya kuhudumia wananchi, matrekta yaliyotolewa wangeweza kutoa hata kwa mtu mmoja mmoja lakini yametolewa kwa vikundi ili kuchochea maendeleo na kurahisisha utunzaji wa mradi huo. 

  “kasaidianeni matrekta haya yakachochee na kuboresha kilimo, kuongeza uzalishaji na tija asitokee mtu mmoja kati yenu akawa ni chanzo cha mafarakano, Halmashauri haitavumilia tutawapokonya na kuwapa wahitaji wengine” alisema 

  Ameongeza kuwa matrekta yote matengenezo yake yapo chini ya Suma JKT hivyo iwapo kutatokea hitilafu yoyote wasitumie mafundi wa mitaani kuyatengeneza badala yake yafikishwe kwa walengwa wa matengenezo, na kuwataka wasitumie mradi huo kwa lengo la kujinufaisha mtu binafsi. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe amesema kuwa matrekta yamekabidhiwa kwa vikundi kwa kuamini vitarahisisha katika utunzaji na kuvitaka vikundi hivyo kutumia matrekta hayo kama iivyokusudiwa kwa kuzingatia muda wa kufanya kazi na kuyapumzisha ili yaweze kudumu. 

  Aidha ameongeza kuwa matrekta yote mbali ya kuwa mali ya vikundi lakini yapo kwenye Vijiji hivyo ni wajibu wao kutoa taarifa ya usimamizi wa matrekta hayo kwenye uongozi wa Vijiji ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mapato ghafi (10%ya mapato) kwenye miradi ya maendeleo ya Vijiji vyao na mwisho wa siku kuongeza uzalishaji utakaopelekea wananchi kuishi kwa amani na utulivu. 

  “Matrekta haya ni mradi kama ilivyo miradi mingine , naomba yasiwe chanzo cha migogoro,kuwepo na uaminifu na uwazi katika kuendesha mradi, hii ni mali ya kikundi sio ya mtu binafsi na taarifa zote ziwekwe kwenye maandishi ikiwa ni pamoja na kuziwasilisha kila baada ya miezi mitatu.” Alisema Mkurugenzi. 

  Halmashauri iliingia makubaliano na vikundi vya wakulima kuchangia 20% kwa aajili ya matengenezo ya matrekta ambapo Halmashauri imetumia zaidi ya Tsh.36,218,000/= kwa ajili ya kununua vipuri mbalimbali katika kuyakarabati matrekta kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo. 

  Vikundi vilivyokabidhiwa leo matrekta ni pamoja na Kikundi cha Amani Vicoba Misima, umoja wa marafiki Mkata, kikundi cha wakulima Mandera na kikundi cha maziwa Kwamsisi Saccos. Vikundi vyote vimeshukuru kupokea Matrekta hayo na kuahidi kuyatunza vizuri. 

  Imetolewa na : 
  Kitengo cha Teknolojia, Habarai na Mawasiliano. 
  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. older | 1 | .... | 1415 | 1416 | (Page 1417) | 1418 | 1419 | .... | 1903 | newer