Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAWA KINARA KATIKA MAPAMBANO YA UKATILI WATOTO BARANI AFRIKA

$
0
0
Na Humphrey Shao Globu ya Jamii

TANZANIA imetajwa kuwa ni nchi ya kwanza barani afrika katika mapambano dhidi ya ukatili watoto kulinganisha na mataifa mengine.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa shirika la Kimataifa linaloshughulikia haki za watoto, Elimu na Ushauri, Michael Gibbons alipokuwa akitoa mada katika mkutano wa kujadili masuala ya ukatili kwa watoto na Wanawake uliofanyika jijini Dar es Salaam Leo.

Gibbons amesema Tanzania ndio nchi pekee Afrika iliyoweka nguvu kubwa katika mapambano ya ukatili wa mtoto pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya elimu kutokana na sera yake ya Elimu Bure.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa afya jinsia Wanawake na Watoto, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Magreth Mussai amesema Serikali inatumia takribani Bilioni 6.7 kutibu naa kushughulikia matokeo ya ukatili.

“katika kulinda watoto baada ya matukio ukatili kutokea Taifa linatumia Bilioni 6.7 kwa ajili ya kushughulikia Mahakamani, Matibabu na hatua zote anazostaili mtoto na Wanawake baada ya ukatili kutokea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki Elimu nchini John Kalaghe amesema asilimia 52.6% ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto hutokea mashuleni jambo ambali limekuwa likipigiwa kelele na wazazi wengi.

Kalaghe amesema ukatili wa watoto ni moja ya jambo ambalo linasumbua katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na kutaja watoto wa kike na wakiume hapa nchini upitia ukatili wa kupigwa mashuleni kwa asilimia 52.6 %.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki Elimu,John Kalaghe akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia haki za Watoto, Elimu na Ushauri, Michael Gibbons akizungumza katika Mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto na Wanawake , Magreth Mussai akizungumza katika mkutano huo kwa Niaba ya Waziri wa Afya Wanawake jinsia na watoto.
Meneja Maendeleo na utawala wa shirika la kutetea Watoto nchini Uganda , Deogratias Yiga. akizungumza kwenye mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki.
baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki.
baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki.
baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki
wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki wakiwa katika Picha ya pamoja

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA YA UZINDUZI WA MRADI WA KUJENGA UWEZO KWA TAASISI KATIKA UDHIBITI WA KEMIKALI NA TAKA SUMU

$
0
0
 Mgeni Rasmi katika warsha ya uzinduzi wa Mradi wa kujenga uwezo kwa Tasisi katika udhibiti wa kemikali na taka sumu , Bwana Richard Muyungi ambaye ni Mkurugenzi idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akiongeakatika uzinduzi wa warsha hiyo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Magdalena Mtenga akiongea wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira.
 Sehemu ya Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Mwakilishi wa UNEP  Bibi Nalimi Sharma akiongea katika warsha hiyo, pembeni yake Mkurugenzi wa Mazingira Ofsis Ya Makamu wa Raisambaye  ni Mgeni Rasmi Bwana Richard Muyungi
 Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali.

Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto katika suala zima la usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu. Taka sumu nyingi zimekua tishio kwa Wananchi hasa Wanawake na Watoto. 

Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi  ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,  Bwana Richard Muyungi alipokua akifungua warsha ya uzinduzi wa mradi wa kujenga uelewa kwa Taasisi za Serikali katika udhibiti na usimamizi wa kemikali na taka sumu jijini Dar Es Salaam.

Pia ametoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) kwa msaada wa kifedha katika kuanzishwa kwa mradi huo, ameongeza pia  Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo wakaitumie vema elimu watakayoipata katika sehemu zao za kazi ili kuongeza weledi na maarifa.

Akiongea katika warsha hiyo Mwakilishi kutoka UNEP Bi.Nalimi Sharma amesema amefurahi sana kuhushuria uzinduzi wa warsha ya mradi huo na kuona jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika suala zima la usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu. Ameongeza kuwa UNEP itaendelea kutoa msaada wa kifedha kwa kwa Ofisi ili kuendelea kuimarisha shughuli za usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu.

MAKANDARASI KUKUTANA JIJINI DAR, KUJADILI MAENDELEO YA UKUAJI WA VIWANDA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Mhandisi Lawrence Mwakyambiki (katikati) akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) katika utambulisho wa mkutano wa chama hicho utakaofanyika Novemba 17, 2017 Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mauzo wa benki ya cba Bi.Kunenguda Dedede na kushoto ni Mkuu wa Masoko kutoka NMB Bi.Linda Teggisa.
Meneja Mauzo wa benki ya cba Bi.Kunenguda Dedede akieleza jambo kwa waandishi wa habari( hawapo pichani)  kuhusu mkutano wa makandarasi hapo novemba 17, 2017 katika ukumbi wa diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa masoko  kutoka NMB Bi.Linda Teggisa na Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Mhandisi Lawrence Mwakyambiki.(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)

Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Chama cha Makandarasi (CATA) kinachounganisha wakandarasi wote nchini kinatarajia kukutana Novemba 17, 2017 kujadili kuhusu ukuaji wa viwanda nchini mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Akizungumuza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhandisi Lawrence Mwakyambiki alisema kuwa  Serikali ya Aawamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli iko kwenye njia ya ujenzi wa viwanda kwa hiyo sekta ya ujenzi inahitajika kwa kiasi kikubwa kwenye sera hii ya viwanda.

“Lengo la mkutano huu kwa wakandarasi hawa ni kutaka kuleta mchango wao katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania na wameona kwamba kama wazawa wanaowajibu wa kutoa mchango katika katika ujenzi wa viwanda nchini”, alisema Mhandisi Mwakyambiki.

Aidha Mhandisi Mwakyambiki aliseka kuwa katika maendeleo ya taifa tasnia ya ujenzi ni muhimu kwani inabeba vitu vingi na kuwawezesha wananchi kupata huduma stahiki kama elimu na afya na kuwataka makandarasi kufanya kazi zo kwa ufanisi mkubwa.

Katika mkutano huu ambapo CATA watakuwa waratibu vyama vingine vya wakandaarasi vikiwemo Tanzania Civil Engineering Contractors Association(TACECA) pamoja na Association of Citizen Contractors(ACCT) na  mabenki  ya cba na NMB ambayo yatatoa ufadhili wa mkutano huo.

Akibainisha miradi itakayochukua nafasi katika majadiliano hayo Mwakyambiki alisema kuwa katika serikali hii ya awanu ya tano miradi inayohitaji  wakandarasi ni Ujenzi wa miundombinu ya reli(SGR), sekta ya maji, bomba la kusafirisha mafuta ghafi(uganda –tanzania) pamoja na ujenzi wa makao makuu ya nchi Dodoma.

Aidha aliongeza kuwa katika mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuliwa na wakandarasi zaidi ya 200 ambao watatoa mawazo yao kuelekea ujenzi wauchumi wa viwanda kama sera ya awamu ya tano inavyoelekeza  ni muhimu kwa ujenzi wa taifa.

Mhandisi Mwakyambiki alisema kuwa katika kutambua mchango wa wakandarasi ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kutokea Tanzania katika tasnia hiyo na mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa katibu mkuu wa sekta ya ujenzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Injinia Joseph Nyamuhanga.

WAKAZI WA BAGAMOYO WAKUNWA NA TAMASHA LA EFM MZIKI MNENE

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Hip Pop Nchini, Izo Busines akitoa Burudani kwa wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo katika Tamasha Maarufu la Mziki Mnene lililofanyika katika Bar ya Dunda Dunda linaloandaliwa na Efm Radio kwa kushirikiana na Tv E
 Mkali wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Prince Dully Sykes akiimba na Mashabiki wakati wa Tamasha la Muziki Mnene linaloandaliwa na Radio ya Efm na Tv E ambalo lilifanyika katika Bar ya Dunda Dunda Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
 RDJ Mamy kutoka Efm Radio akitoa burudani kwa wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo kwenye Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika katika Bar ya Dunda Dunda
  Mkali wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Prince Dully Sykes akiimba na Mashabiki wakati wa Tamasha la Muziki Mnene linaloandaliwa na Raido ya Efm na Tv E ambalo lilifanyika katika Bar ya Dunda Dunda Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
 Msanii Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Dudubaya akitoa Burudani kwa Mashabiki wake wa Bagamoyo katika Tamasha la Mziki Mnene lililoandaliwa na Efm Radio.
 Mkali wa Muziki wa Singeli nchini Msaga Sumuakitoa burudani kwa wakazi wa Bagamoyo wakati wa Tamasha la Muziki Mnene lililoandaliwa na Kituo cha Radio cha Efm na Tv E katika Bar ya Dunda Dunda.
  Mkali wa Muziki wa Singeli nchini Msaga Sumuakitoa burudani kwa wakazi wa Bagamoyo wakati wa Tamasha la Muziki Mnene lililoandaliwa na Kituo cha Radio cha Efm na Tv E katika Bar ya Dunda Dunda.
 RDJ Timber Mtu Mbaya akitoa Burudani kwa wakazi wa Bagamoyo wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililoandaliwa na Efm Radio na  Tv E.
 RDJ Black kitoa Burudani kwa wakazi wa Bagamoyo wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililoandaliwa na Efm Radio na  Tv E.
Mashabiki wakishangilia Tamasha la Efm MZIKI MNENE Katika Bar ya Dunda Dunda Bagamoyo.

CLINIC YA METHANONE ZANZIBAR YAPATIWA VIFAA VYA KUCHUNGUZA WATEJA WAO

$
0
0
 Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la dawa za Kulevya na Uhalifu  (UNODC) Bi. Immaculate Nyoni  akimkabidhi boksi lenye vifaa vya kupimia mkojo watumiaji dawa ya Methadon ambao wanatumia  aina nyengine ya dawa kinyume na taratibu katika hafla iliyofanyika Kliniki Methadone Kidongochekundu.
 Rais wa watumiaji dawa ya Methadon Zanzibar Hilal Nassor akizungumza na wandishi wa habari baada ya kukabidhiwa vifaa vya kuwatambua watumiaji wa tiba ya Methadone na baadae kutumia dawa aina nyengine.
Baadhi ya watumiaji dawa za Methadone wakisubiri kupatiwa huduma katika Kliniki yao iliyopo Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo- Chekundu Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

Na Ramadhani Ali – Maelezo .
          
Wagonjwa wanaotumia dawa aina ya Methadone kama tiba baada ya kuathirika kutokana na dawa za kulevya na wanaoutumia aina nyengine ya dawa  kwa njia za siri wamepatiwa muarubaini baada ya kupatikana vifaa maalumu vya kumgundua mtumiaji kwa kumpima mkojo.

Vifaa hivyo vinavyojulikana kwa jina la DOAKIT vimetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu (UNODC).Mratibu wa Mradi wa Taifa wa kupambana na HIV/AIDS kwa wafungwa, Immaculate Nyoni ambae ni afisa wa UNODC Tanzania amemkabidhi vifaa hivyo Mratibu wa huduma za ukimwi kwa watu wa makundi maalum Zanzibar Dkt. Shaaban Hassan katika hafla iliyofanyika Kliniki ya Methadone iliopo ndani ya hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo- chekundu.

Immaculate alisema UNODC itaendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapatia tiba sahihi wagonjwa walioathirika na dawa za kulevya.Alisema kwa kuanzia wameleta DOAKIT 1500 ambazo zinaweza kutumika kwa kipindi cha miezi mitatu kwa mujibu wa idadi ya wagonjwa wanaotumia Methadone waliosajiliwa katika kliniki hiyo.

Daktari dhamana wa hospitali ya Kidogochekundu Dkt. Khamis Othman alilishukuru shirika la UNODC kwa kuwapatia msaada huo ambao kwa kipindi cha mwaka mmoja walikuwa na upungufu mkubwa na kupelekea baadhi ya wagonjwa kutumia aina nyengine ya dawa bila kujulikana.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za kutumia tiba ya Methadone mgonjwa hatakiwi kutumia aina nyengine ya dawa za kulevya na akifanya hivyo hupata madhara makubwa kwa kuongeza kiwango cha dawa mwilini.

Alisema DOAKIT ni viifaa vyenye uwezo wa kugundua aina sita ya dawa za kulevya kwa kuchunguza mkojo wa mtumiaji na vinaweza kutumika katika maeneo mbali mbali kuwachunguza watumiaji wa dawa hizo.Dkt. Khamis alieleza kuwa Kliniki ya Methadone ya Kidongochekundu ilianzishwa mwaka 2015 na imesajili wagonjwa 434 ambao wanapatiwa  tiba kamili na imekuwa mkombozi wa vijana wengi waliokubali kujiunga.

Alisema kazi ya Methadone ni kusaidia kuondosha hamu ya kutumia Heroine na dawa nyengine za kulevya hatimae mtumiaji huacha kidogo kidogo kutumia dawa hizo.Hata hivyo amekiri kuwa bado wanakabiliwa na changamoto kubwa kwani baadhi ya wagonjwa wanaotumia Methadone hukosekana baadhi ya siku na wanatumia dawa nyengine za kulevya kwa siri.

Wagonjwa wanaotumia Methadone wamekiri kuwa inawasaidia  kujitambua na imewarejesha katika mfumo bora wa maisha na wanaaminika ndani ya jamii zao.
Amina Omar mkaazi wa Jangombe, alietumia dawa za kulevya kwa miaka 25, alisema wakati anatumia dawa hizo alikuwa hajitambui na alidhoofu kufikia uzito wa chini ya kilo 40 na baada ya kutumia Methadone hivi sasa uzito wake umefikia kilo 80.

IGP SIRRO ATAKA JESHI LA POLISI KUDUMISHA MICHEZO

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Maofisa na Askari Polisi kote nchini kushiriki michezo ili kujenga Afya,ukakamavu na urafiki baina ya wenyewe kwa wenyewe na raia.

IGP Sirro ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji wa TAEKWONDO waliofanya vizuri katika michezo ya Taekwondo Pumsae (kucheza Kata), Taekwondo Gyeokpa ( kuvunja kibao kwa kuruka Juu) na Taekwondo Gyeorugi (Mapigano) iliyomalizika hivi karibuni ambapo timu ya Polisi iliibuka na ushindi wa kwanza  katika timu 17 zilizoshiriki.

Sirro alisema Jeshi la Polisi litaendelea kutilia mkazo michezo ya aina mbalimbali na atahakikisha Askari na Maofisa wanapata fursa ya kushiriki michezo kwakuwa kwakufanya hivyo kutasaidia pia kulitangaza Jeshi la Polisi na kujenga mahusiano na jamii."Hakikisheni hamrudi nyuma,tutawapa sapoti ya kila namna ili tusiwe wasindikizaji bali tuweze kutoa ushindani na kufanya vyema na ni jambo linalowezekana kwa kuwa ari na morali ipo"Alisema Sirro.

Kwa Upande wake Mkuu wa Michezo wa Jeshi la Polisi,Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philip Kalangi alisema ushindi wa timu hiyo ni chachu katika kujiandaa na michezo ya majeshi ya EAPCCO itakayofanyika hapa nchini mwakani ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.

mashindano hayo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Jamhuri ya korea ukishirikiana na Chama cha Walimu wa Taekwondo kutoka korea (Korean Taekwondo Masters Association) ambayo ni mashindano ya Taekwondo ya kitaifa yaliyofanyika tarehe 21/10/2017 ambayo yalishilikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka  nchi nzima ambavyo ni Makongo Juu, Kariakoo,Shark TKD,Twiga Triple A,HTC DSM, KILI, Vingunguti,Arusha Morden,TCC,AICC,UAUT pamoja na vilabu vya Polisi ambavyo ni DPA, MPA na ZPA.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na viongozi wa Jeshi la Polisi  Sambamba na Askari Polisi walioshiriki na kujinyakulia medali mbalimbali katika mashindano ya mchezo wa Taekwondo iliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association)
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na askari wa jeshi hilo wanaounda timu ya Taekwondo ambao walishiriki na kujinyakulia medali mbalimbali katika mashindano ya Taekwondo yaliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association) yaliyoshirikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka nchi nzima.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simoni Sirro akimvisha medali askari Polisi ambaye ni miongoni mwa askari waliojinyakulia medali katika mashindano taekwondo iliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association). Picha zote na Jeshi la Polisi

RC Rukwa aahidi kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Rukwa katika Sekta zote

$
0
0
​Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo amewatahadharisha watumishi kutobweteka baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen kustaafu na kumkabidhi yeye kijiti cha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya mkoa.

Amesema kuwa hatomwangusha Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumkabidhi madaraka hayo na kuahidi kuwa ataimarisha elimu inayoonekana bado ipo chini kwa ufaulu lakini pia kuendeleza kasi ya uzalishaji katika kilimo.

“Baada ya kusoma kabrasha hili la kukabidhiana ofisi kuna mambo mengi ya kuyazingatia ikiwemo, elimu, kilimo, ulinzi na usalama, utunzaji wa mazingira, uvuvi na uwekezaji katika viwanda. Hasa katika elimu maana mimba ni nyingi, kuna upungufu wa madawati, upungufu wa vyumba vya madarasa lakini pia kiwango cha ufaulu hakijafikia kile kilichopo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo ni asilimia 80 kwa darasa la saba,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo katika makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mapema leo hii tarehe 31/10/2017 katika ukumbi wa ofisi hiyo, jambo lililoshuhudiwa na watumishi wa sekretariet ya Mkoa pamoja na baadha ya Halamashauri.

Katika kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufanisi Mh. Wangabo amesema kuwa hupemda kusikiliza mipango ya watendaji inayotekelezeka ili waweze kuitekeleza kama walivyoipanga nay eye ataisimamia na kutoa ushauri wa kuongeza kasi ya utekelezaji pale inapobidi ili kuyafikia malengo waliyojiwekea kwa wakati.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewashukuru watumishi wote wa serikali katika Mkoa wa Rukwa pamoja na wananchi wa mkoa kwa kumpa ushirikiano katika kipindi chote alichokuwepo na kuwaomba waendeleze kumpa ushirikiano huo huo Mkuu wa Mkoa mpya ili naye aweze kufanya majukumu yake kwa ufanisi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Leonard Wangabo (kushoto) na Mh. Zelote Stephen (Waliokaa) katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
 Mkuu nwa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Leonard Wangabo akisalimiana na Meneja wa PS3 Mkoa wa Rukwa Bi. Rose wakati wa kumkaribisha Mh. Wangabo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tayari kwaajili ya Kuanza kazi.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) akimkabidhi nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo. katika makabidhiano ya ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 
 Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) akisaini nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa kwaajili ya Kumkabidhi ofisi hiyo Rukwa Mh. Joackim Wangabo.

TAARIFA KWA UMMA: VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YA TANZANIA.


RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa. 

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali. 

Makonda amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 hadi 120 ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Coach kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali. Aidha Makonda amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa. 

Amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari wajivunie kufanyakazi chini ya Mkuu wa Mkoa mwenye kuwapenda na kuwajali. 

Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi. 

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James ambapo wote kwa pamoja wamempongeza mkuu wa mkoa kwa hatua kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikaribishwa na viongozi wa jeshi wakati alipokwenda kukabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akimkabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa wakishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva,Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James. 
Mabasi 10 chakavu yakiwa yanatoka katika Chuo cha Polisi Kilwa Road kuelekea Mkuranga kwenye ofisi za Kampuni ya Dar Coach kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho na kuwa ya kisasa zaidi. 
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa ndani ya basi la Magereza. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva,Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James wakati wa kukagua mabasi 10 chakavu kabla ya kupelekewa kwenye gereji ya Dar Coach kwa ajili ya matengenezo.Picha zote na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

PTA BANK BECOMES TDB - WITH INCREASED COMMITMENT FOR FUNDING IN EASTERN AND SOUTHERN AFRICA

$
0
0
Trade and Development Bank (TDB), Principal Project and Infrastructure Finance Officer, Neema Siwingwa (right), addresses a press conference in Dar es Salaam yesterday to announce the changes of its trade name which were former known as Eastern and Southern Africa Trade and Development Bank (PTA Bank) to TDB. Looking on is Trade and Development Bank (TDB), Director Corporate Affairs & Investor Relations, Mary Kamari. 
 
 The Eastern and Southern African Trade and Development Bank, commonly known as PTA Bank, has changed its official brand name to TDB (Trade and Development Bank).

Since its establishment over three decades ago, the Bank has operated under its legal name ‘’Eastern and Southern African Trade & Development Bank” as well as two trading names in English and in French: PTA Bank / Banque de la ZEP. Through the revitalization of its corporate branding, the Bank will be trading under one trade name (Trade and Development Bank – TDB) and a new logo while its legal name ’Eastern and Southern African Trade & Development Bank” will remain unchanged.

The leading regional multilateral Development Finance Institution (DFI) has also announced that it will continue to increase financing for priority sectors such as infrastructure, manufacturing, industry and agribusiness across the 21 member states it operates in, over the next five years.

“Our rebranding represents our rejuvenation and recommitment to innovate and play a more active role in promoting trade, economic development and regional integration, at a crucial time when the region is looking to more vigorously advance economic transformation and ratchet up the tapering growth ,” said Admassu Tadesse, President and Chief Executive of the Trade and Development Bank.

Mr. Tadesse further stated, “In recent years, we have been giving a big boost to our financing of trade, enterprise and infrastructure, which is evidenced in the tripling of our loan assets in the past five years. We have made substantial contributions to the rising economic growth and infrastructure development in the region, in line with regional and international development strategies, notably those aimed at achieving the Sustainable Development Goals and Africa’s Vision 2063. We have funded several landmark projects such as Kilwa Power in Tanzania, the Fibre Optic Backbone Project in Burundi and renewable energy projects such as Turkana Wind Power in Kenya, Hydromax Minihydro in Uganda, and industrial projects such as cement and steel plants in DR Congo, Djibouti, Zambia, Rwanda, Ethiopia and Zimbabwe. We will continue scaling up, with continued attention to sustainability and good corporate governance.”

The rebranding follows several years of improved asset quality, healthy profitability and innovation, on the back of a series of institutional reforms aimed at strengthening and modernizing the Bank. “We have dramatically increased our capacity to meet the rising demand for the Bank’s products and services, thanks to the strong funding partnerships we have built up with long term funders and investors. Our shareholder base has increased by more than 50% in recent years, with several new institutional investors and Member States. Indeed our equity capital has tripled since we embarked on the current corporate plan in 2012” added Mary Kamari, Director of Corporate Affairs and Investor Relations.

The Trade and Development Bank will continue to support independent power and transport projects, as well as agribusiness, and industry, alongside trade financing of essential commodities such as fertilizer, equipment, agricultural commodities and petroleum. Trade finance is typically provided on a structured basis, with emphasis on self-liquidation mechanisms, term lending is done mostly on a balance sheet, and at times on a project basis, with tenors ranging up to three years for trade related financing, and up to 15 years for infrastructure projects. The Bank has also financed numerous agribusiness projects throughout eastern and southern Africa, notably Malawi and Sudan, and provided important asset finance facilities to the air-transport sector in the region, with Rwanda Air, Kenya Airways and Ethiopian Airlines benefitting.

SPIKA NDUGAI MGENI RASMI KATIKA UFUNGUZI WA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 90 YA KANISA KUU LA ROHO MTAKATIFU, DAYOSISI YA CENTRAL TANGANYIKA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katika) akikata utepe wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 90 ya Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya kanisa kuu la Roho Mtakatifu Mjini Dodoma. wa tatu kulia ni Askofu wa Dayosisi hiyo, Dkt. Dickson Chilongani. Spika wa Bunge, alikuwa mgeni rasmi katika Maonesho hayo.


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na waumini wa kanisa kuu la Roho Mtakatifu, Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 90 ya Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya kanisa hilo Mjini Dodoma. Spika wa Bunge, alikuwa mgeni rasmi katika Maonyesho hayo.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mheshimiwa Albert Obama akiongoza kikao cha pamoja kati ya kamati hiyo na watendaji kutoka kituo cha zana za kilimo na Teknolojia Vijijini (KAMATEC) wakati wakipokea, kujadili na kuchambua taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa KAMATEC kilichofanyika leo Mjini Dodoma.




Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wajumbe wa kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, katika kikao cha kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kushoto ni kiongozi wa msafara na Mwenyekiti wa Kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, Mheshimiwa Dkt. Mark Yeboah na wanne kulia ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai




Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza kiongozi wa msafara na Mwenyekiti wa Kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, Mheshimiwa Dkt. Mark Yeboah (wa pili kushoto) wakati wa kikao na wajumbe wa kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, kikilenga kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. kulia ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipatiwa maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa kanisa kuu la Roho Mtakatifu, Dayosisi ya Central Tanganyika, Ndg. Grace Lisasi (katikati) alipotembelea Banda la Umoja wa Wanawake wa Kikristo (UWAKI) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 90 ya Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya kanisa hilo Mjini Dodoma. Spika wa Bunge, alikuwa mgeni rasmi katika Maonesho hayo.

PICHA NA OFISI YA BUNGE

VIJUSO VYA MAGAZETI YAB LEO JUMATANO NOVEMBA MOSI,2017

WAKULIMA WILAYA YA CHATO WAFURAHIA KUPATA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi (kushoto), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akimkabidhi mbegu ya viazi lishe kwa ajili ya shamba darasa la Kijiji cha Kibehe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani Chato leo. 
 Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiandaa shamba lao la mbegu.
 Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiwa kwenye uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe na mihogo.
 Mtafiti wa Mazao ya Mizizi wa Wilaya ya Chato, Monica Mulongo akizungumzia vitamini A inayopatikana kwenye viazi lishe ambayo ni muhimu kwa watoto.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya viazi lishe. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari.
 Mtafiti Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro akizungumzia ubora wa mbegu ya Wema pamoja na upandaji wake.


 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari , akionesha mbegu ya mahindi ya Wema baada ya kukabidhiwa.

 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, akiwaonesha wakulima wa Kibehe jinsi ya kupanda mbegu ya mhogo.
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho.
  Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula akitoa maelezo kwa wakulima wa vijiji vya Ipandikilo na Kitongoji cha Kaseni jinsi ya kupanda mbegu ya mhogo.
 Watafiti Bestina Daniel na Ismail kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mahindi katika Kijiji cha Bukiliguru.
 Mshauri wa Jukwaa la ioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange akipanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa la Kijiji cha Itale.
 Wakulima wa Kijiji cha Bukiliguru wakishiriki kuapanda mbegu za mahindi katika shamba darasa.
 Mtafiti Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro akiwaelekeza wakulima jinsi ya kupanda mbegu bora ya mahindi ya Wema inayovumilia ukame.
Wakulima wa Kijiji cha Bukiliguru wakifuatilia uzinduzi wa shamba la mihogo.

Na Dotto Mwaibale, Chato

WAKULIMA Wilaya Chato mkoani Geita wamefurahia mbegu bora ya mihogo, mahindi na viazi lishe waliopewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kuanzisha mashamba darasa ya mbegu hizo na kuzisambaza kwa wakulima wengine katika maeneo mengine.

Wakizungumza wilayani hapa leo kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu hizo katika vijiji vya Kibehe, Ipandikilo, Kitongoji cha Kaseni, Kijiji cha Itale na Bukiliguru kilichopo Kata ya Bwanga walisema mbegu hizo walizokabidhiwa na COSTECH kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo ni mkombozi kwao.

Ofisa Kilimo wa Kata ya Kachwamba,  Hamisi  Matesi alisema Costech kuwapelekea wakulima mbegu hizo itawasaidia sana kupata chakula wananchi wa kata hiyo ziada watauza.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho alisema wakulima walikuwa wakipata mavuno machache ya mahindi na mihogo kwa kuwa hawakuwa na mbegu bora hivyo baada ya kufunguliwa kwa shamba darasa la mbegu hizo katika maeneo yao wanategemea kupata mazao mengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari aliwataka wananchi hao kutambua kuwa mpango huo wa serikali ya awamu ya tano unawategemea sana wakulima katika kilimo hivyo fursa hiyo walioipata ya kupelekewa mbegu hizo wasiipoteze.

“Hakikisheni  mbegu hizi bora za mihogo mnazopewa mnazitunza  ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo hiki kupitia shamba darasa hili ili kila mkazi wa Chato aweze kulima na kuzalisha kwa tija” alisema Mhandisi Hari.

Hari ameishukuru COSTECH kwa kuamua kuipatia wilaya hiyo mashamba darasa katika vijiji hivyo kwani anaamini mbegu hizo zitasimamiwa vizuri na kisha kuwafikia wakulima wengi zaidi ili waweze kuachana na mbegu zao za zamani ambazo zinashambuliwa na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu  Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha matunda ya tafiti hizo yanawafikia walengwa.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi ikiwamo ya mahindi yanayostahimili ukame ya Wema 2109 zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato katika mihogo.

Dk. Bakari aliwataka wakulima hao kuyatunza mashamba darasa hayo na kubwa baada ya muda mfupi watarudi kuangalia maendeleo yake.

JUMIA KUWAWEZESHA WATEJA KUFANYA MANUNUZI KWA PUNGUZO LA MPAKA 70%

$
0
0

  Meneja  Mauzo wa Jumia Tanzania, Bw. Idd Mkumba, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa kampeni hiyo jijini Dar es salaam jana. Kulia ni   Masoko wa Jumia Tanzania, Bw. Albany James na Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko,  Jumia Travel Tanzania, Geofrey Kijanga .
 Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko,  Jumia Travel Tanzania, Geofrey Kijanga akizungumza katika mkutano huo.

Mkutano na wanahabari ukiendelea

Na Jumia Travel

Ikiwa imebaki takribani miezi miwili mwaka 2017 kuisha, Jumia Tanzania imejizatiti kuja na kampeni iliyopewa jina la ‘BLACK FRIDAY’ ambayo itawawezesha wateja wake kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali mtandaoni kwa punguzo la mpaka alisimia 70 kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa kampeni hiyo Meneja Mauzo wa Jumia Tanzania, Bw. Idd Mkumba amebainisha kuwa kutokana na mafanikio makubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika mwaka jana na kushuhudia watanzania wakifanya huduma za mtandaoni ambapo takribani oda 600 kwa siku wameona ni vema kuirejesha tena kwa kishindo mwaka huu.

“Mwaka 2016 ulikuwa ni wenye mafanikio kwa upande wa kampeni yetu ya BLACK FRIDAY kwani ndani ya muda wa siku tano tuliyoifanya wateja wengi waliweza kufanya manunuzi mtandaoni. Hivyo basi kwa mwaka huu tena tumeiboresha Zaidi kwa kuongeza siku kutoka tano mpaka 11 ambapo kampeni itaanza rasmi kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4. Na kwa kuongezea hapo ni kwamba safari hii wateja wa Dar es Salaam hawatofaidika pekee yao kwani tumejitanua Zaidi mpaka mikoa mingine kwa mara ya kwanza na kuzifikia sehemu za Visiwani Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Musoma,” alisema Bw. Mkumba.

Meneja Mauzo huyo wa Jumia Tanzania aliendelea kwa kufafanua kuwa, “Lengo kubwa la kampeni hii ni kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo na kuwarahisishia watanzania kufanya huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao mahali popote walipo huku wakiendelea na shughuli zao. Tanzania ni mojawapo ya taifa linaloendelea Afrika na duniani likiwa na watumiaji wa simu za kisasa na mtandao wa intaneti wanaoongezeka kila kukicha. Hivyo basi nasi tunaitumia fursa hiyo kwa kuwahamisisha watanzania kuitumia teknolojia hiyo kwa manufaa Zaidi, ambapo badala ya kutumia muda mwingi kwenda madukani wanaweza kufanya hivyo wakiwa palepale walipo.”

“Katika kuwaondoa hofu wateja ambao wanahofia kwamba pengine bidhaa zinaweza kuwa hazina ubora kutokana na ukubwa wa ofa tunazotoa, ni kwamba Jumia Tanzania tunafanya huduma zetu kwa sera ya kulipia pale unapopokea bidhaa yako. Hii humpatia mteja kujiridhisha kwamba bidhaa aliyoiagiza ni sahihi ndipo alipie. Na kwa kuongezea, ada ya malipo ya kufikishiwa mzigo kwa wateja wetu popote walipo itashuka ili kuhamasisha manunuzi Zaidi. 

Kwa kumalizia kuhusiana na kampeni ya BLACK FRIDAY ambayo itawapatia fursa wateja kupata punguzo la bei mpaka la asilimia 70, tumeingia ubia na makampuni kadhaa makubwa ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa kama vile Samsung, Startimes, Tronic,… Lakini pia kutokana na kuanza kwa huduma kwenye mikoa mipya niliyoiorodhesga hapo juu, tumetoa ofa kwa wateja watakaofanya manunuzi ya kuzidi shilingi 100,000 watajipatia punguzo la 50% ambapo itawabidi watumie neonsiri J695D,” alihitimisha Bw. Mkumba.

Akifafanua Zaidi juu ya dhana nzima ya kampeni hiyo, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Bw. Albany James amesema kuwa utamaduni wa BLACK FRIDAY umeanzia nchini Marekani ambapo makampuni wafanyabiashara hutoa punguzo la bei za bidhaa na huduma mbalimbali ili kuukaribisha msimu wa mapumziko na Krisimasi.

“Utamaduni huu wa kufanya punguzo kubwa la bei mbalimbali za bidhaa na huduma ulianzia nchini Marekani na kushika kasi sehemu zingine duniani kutokana na faida kubwa kwa wafanyabiashara na wateja kwa ujumla. Ni kipindi ambacho watu wengi hufanya maandilizi ya msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya. Na nadhani utamaduni huo hata kwa sisi watanzania pia tunautumia hivyo basi kupitia Jumia Tanzania wateja wataweza kununua bidhaa mbalimbali muhimu kwa msimu huo kama vile za nyumbani, umeme, mavazi, vyombo vya kupikia nakadhalika. Kwa hiyo ningependa kuwatoa hofu wateja wetu kwamba ni bei za bidhaa ndizo zitakazopungua na sio ubora kama wengi wanavyodhahania,” alisema na kumalizia Bw. James.

Katika kunogesha kampeni hii Jumia Tanzania pia imeshirikiana na makampuni tanzu ya Jumia hapa nchini kama vile Jumia Travel na Jumia Food ambayo nayo yanajihusisha na huduma kwa njia ya mtandao. Ushirikiano huo utawapatia faida wateja watakaokuwa wakifanya manunuzi mtandaoni kupata ofa kama vile za malazi ya bure pamoja na punguzo kubwa kwa hoteli mbalimbali za kifahari nchini.

Akizungumza kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania, Bw. Geofrey Kijanga ameelezea kuwa wao kama watoaji wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao mbali na kutoa ofa ya kulala bure kwenye hoteli kwa wateja lakini pia watatoa punguzo kubwa la bei za huduma za malazi ambalo litadumu mpaka mwezi Desemba.

“Tunafahamu kwamba tunaelekea kuumaliza mwaka ambao hugubikwa na msimu wa mapumziko na sikukuu za Krisimasi na Mwisho wa Mwaka, suala la watu kwenda kutembelea na kupumzika sehemu mbalimbali ni muhimu. Katika kulirahisisha hilo Jumia Travel itatoa punguzo kubwa la huduma za malazi kwa hoteli inazofanya nazo kazi nchini. Kwa hiyo mteja hatowaza kuhusu gharama za malazi popote atakaposafiri yeye au pamoja na familia yake. Hivyo basi ni muda muafaka kwa watanzania kuzitumia ofa hizi kwani huwa ni za kweli na hurahisisha gharama kubwa ambazo wanaweza kuziingia kuzipata kwa njia nyinginezo za kawaida,” alisema na kuhitimisha Bw. Kijanga.

Hii ni fursa kwa watanzania wote kwa ujumla kujiaandaa vema na msimu wa mapumziko na sikukuu unaokuja kwa kufanya manunuzi ya gharama nafuu Zaidi mahali popote walipo kuanzia Novemba 24 na kuendelea kwa siku 11 mwaka huu. Ili kufahamu Zaidi na kujua mengi juu ya ofa zitakazotolewa watanzania wanatakiwa kuwa kutembelea mitandao ya Jumia Tanzania pamoja na kurasa zao za mitandao ya kijamii. Lakini pia kutakuwepo na zawadi mbalimbali kupitia njia za vocha na kuponi kwa wale watakaokuwa wakifuatilia kurasa hizo kwa karibu na kujibu maswali mbalimbali.

MAVUNDE ASISITIZA KUWA NA NGUVU KAZI YA VIJANA WENYE UJUZI KATIKA UJENZI WA UCHUMI WA TAIFA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akizungumza na vijana katika Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akikagua maendeleo ya Vijana ambao wanasomeshwa na Serikali kupitia mpango wa Ukuzaji Ujuzi Nchini katika Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro. 

…………….


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde leo ametembelea Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro na kukagua maendeleo ya Vijana ambao wanasomeshwa hapo na Serikali kupitia mpango wa Ukuzaji Ujuzi Nchini.

Akizungumza na Vijana hao ambao wanasomea masomo ya Komputa,Mavunde amewataka Vijana hao kuutumia ujuzi watakaoupata hapo chuoni kujiajiri kwa kuunda vikundi na Makampuni ili wapate nafasi ya kuwezeshwa kupitia mifuko ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi nchini na hivyo kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa Ajira kwa Vijana.

Mavunde pia amewaeleza Vijana hao kwamba watambue siku zote wao ndio moyo wa Taifa na hivyo ndio nguvu kazi inayotegemewa kwa kiasi kikubwa ndio maana Serikali inaona umuhimu wa kuwekeza katika Mpango huu wa ukuzaji Ujuzi ili kuhakikisha Taifa linakuwa na nguvu kazi yenye ujuzi stahiki katika kuelekea nchi Uchumi wa Viwanda na ya kipato cha kati.

Kwa upande wao Vijana hao wanufaika na Mpango huu wameishukuru serikali kwa kutekeleza mpango huu wa ukuzaji ujuzi ambao utawasaidia kupata ujuzi na baadaye kuweza kujiajiri na Kuajiri Vijana wengine.

Mpango huu wa ukuzaji ujuzi unatarajia kuwanufaisha Vijana 3445 ambao serikali itagharamia mafunzo yao katika kozi za Tehama,Umeme,Ushonaji,Useremala,Uchomeleaji,Kuweka vigae,Ufundi bomba,Upigaji chapa na Ufundi Magari.

SERIKALI YATUMIA BILIONI 514 KUMALIZA TATIZO LA MAJI JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA), Mhandisi Ruth Koya wakipeana mikono na Mkandarasi-Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering ya China, Chen Xianghua mara baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la Arusha.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA), Mhandisi Ruth Koya akisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la Arusha, kushoto ni Mkandarasi kutoka Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering ya China, Chen Xianghua wanaotekeleza mradi huo.
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la Arusha.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA), Mhandisi Ruth Koya (kushoto), Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro (katikati) na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe katika hafla ya kusaini wa mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la Arusha.Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza katika hafla ya kusaini wa mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la Arusha.

……………………………………………………………………………….

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha (AUWSA), leo imeingia mikataba ya Dola za Marekani 233,915,581 ambazo ni takribani Shilingi 514,614,278,200 za Tanzania kumaliza kabisa tatizo la maji katika Jiji la Arusha na Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

Fedha hizo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao wamechangia Dola za Marekani 210,962,581 na Serikali ya Tanzania ikichangia Dola 22,953,000 ili kukamilisha mradi huo.

Kazi zitakazotekelezwa ni uchimbaji wa visima virefu, ujenzi wa matenki, ulazaji wa mabomba ya majisafi na majitaka, ujenzi wa mtambo wa kutibu maji, ujenzi wa mabwawa mapya ya kutibu majitaka, ujenzi wa Makao Makuu ya Mamlaka na Ofisi za Kanda pamoja na ununuzi wa vitendea kazi.

Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa Jiji la Arusha kwa asilimia 100 hadi mwaka 2030 na kutapunguza kiasi cha maji yanayopotea kutoka asilimia 45 ya sasa mpaka kufikia asilimia 20. Aidha, mradi utaongeza mtandao wa kuondoa majitaka kwa asilimia 30. Mradi huu unategemea kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na kuboresha huduma nyingine za kijamii zikiwemo Afya na Elimu.

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Jijij la Arusha kwa sasa ni asilimia 44, sawa na wastani wa lita milioni 40 kwa siku na mradi huu unategemea kuongeza kiwango na kufikia lita milioni 200 kwa siku.

BASHE AUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT MAGUFULI KATIKA KUSIMAMIA RASIMALI,KUFUNGA MIANYA YA RUSHWA NA KURUDISHA NIDHAMU YA KAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe amekua na mkutano wa wazi na wananchi uliojikita katika kuelezea mafanikio na changamoto za miaka miwili ya kipindi cha ubunge wake.

Aidha Malengo makubwa ya mkutano huo yalikuwa ni:
1. Kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa uwazi ili kuongeza nafasi ya ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika mijadala ya maendeleo.

2. Kueleza juhudi za kuleta maendeleo zilizokwishafanywa na Ofisi ya Mbunge katika kipindi cha miaka miwili (2)

3. Kutambulisha miradi mikubwa ya Elimu, Afya na Maji inayoendelea ndani ya Jimbo la Nzega Mjini;
Elimu
- Ujenzi wa Shule ya kwanza ya wanawake
- Utoaji wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wote wanaofaulu Jimboni kupitia Bashe Scholarship Awards 
- Ugawaji wa Vifaa vya shule na madaftari 37,000 
- Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Kidato cha Tano na Sita 
- Ujenzi wa zaidi ya vyumba vya madarasa 32 ya Shule za Msingi  kwenye kata 10 jimboni

Afya
- Ujenzi wa Nyumba za waganga 
- Ujenzi wa Zahanati kwenye kila Kata
- Ugawaji wa Vitambulisho vya Matibabu kwa wazee 
- Upanuzi wa kituo cha Afya cha Zogolo kuwa na hadhi ya Hospitali

4. Kuelezea miradi ya uwezeshaji kwa akina mama na vikundi vya wajasiriamali ambayo imefanywa na Ofisi ya Mbunge ikiwemo;
 - Utoaji wa mikopo kwa vijana
- Utoaji wa mikopo kwa wanawake
- Utoaji wa pikipiki kwa vijana

5. Kuelezea mradi mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria ambao tayari umeshaanza utekelezaji wake hivyo kuwahamasisha wananchi kulinda mali na kuwa tayari kupisha maeneo ambayo mradi utapita ili kuweza kutatua kanisa shida ya Maji Nzega.

6. Upatikanaji wa fedha za Maendeleo zaidi ya Bilioni Moja na Milioni Mia Tank nje ya Bajeti.
(a)  259,000,000 - Ujenzi Shule ya Bweni ya Kwanza Nzega ya Kidato cha Tano na Sita
(b) 384,000,000 - Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya wasichana Nzega Kidato cha Kwanza hadi Sita 
(c) 400,000,000 - Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji. Fedha hizi amezitoa Mhe. Dr. John Pombe Magufuli baada ya kumuomba alipotembelea kwa nyakati tofauti Nzega na Tabora.
(d) 500,000,000 - Ujenzi na Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Zogolo kuwa na hadhi ya hospitali.

7. Kuelezea mafanikio na maendeleo makubwa ya ukuaji wa sekta ya elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini kwa kipindi cha miaka miwili tangu amekua Mbunge kama ifuatavyo;
Ufaulu Elimu ya Msingi Nzega
2014 - 48%
2015 - 54%
2016 - 74%
2017 - 90.66%

Ufaulu Elimu Sekondari IV
2014 - 59%
2015 - 72%
2016 - 77%
2017 - 82%

Ufaulu Elimu Sekondari II
2015 - 79%
2016 - 81%
2017 - 87%

Mwisho; Mhe Hussein Bashe ameunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika kusimamia rasilimali; kufunga mianya ya rushwa na kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.

Kwa upande mwingine Mhe. Bashe amemshukuru Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa Namna ambavyo amekua bega kwa bega katika kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Nzega Mjini kutatua changamoto mbalimbali.

Mheshimiwa Bashe amesema ya kuwa  ...."Mwaka 2015 katika viwanja hivi vya parking nikiwa na Mgombea urais wakati huo Mhe. John Pombe Magufuli nilimuahidi kuwa Mimi sitakua mbunge wa ndio Mzee ila nitamsaidia sana katika kuishauri serikali, kuitetea na pia kuikosoa pale inapobidi ili kuboresha ufanisi wa serikali na Chama cha Mapinduzi."
 Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe akiwahutubia wananchi jimboni kwake katika mkutano wa wazi na wananchi,Mh Bashe alijikita katika kuelezea mafanikio na changamoto za miaka miwili ya kipindi cha ubunge wake.
 Baadhi ya Wananchi wa Nzega wakimsikiliza Mbunge wao,Mh bashe alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa wazi.

WILAYA YA CHATO YATAKIWA KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita amewataka Viongozi wa Serikali Wilayani Chato kusimamia na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo ili thamani ya fedha zinazotolewa ionekane. 

Akizungumza baada ya kuwasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa, amesema kuwa umefika wakati watendaji kuacha tabia ya kukaa Ofisini bali waende maeneo mbalimbali ya Wilaya ambapo kunatekelezwa miradi ili kusimamia kwa karibu miradi inayoendelea. 

" Wananchi wanatakiwa kusimamiwa ata kama fedha ni za kwao ili kuweka miradi katika ubora unaotakiwa"Alisisitiza Lughumbi. Aidha, alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato kuhakikisha wananchi wanakuwa katika vikundi ili vishiriki katika ujenzi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika vijiji kwa kuchangia michango midogo midogo kama vile kutafuta mawe, kokoto, mchanga. Kazi kubwa ya Halmashauri ni kuhakikisha wahandisi wanasaidia kupeleka michoro na kusimamia ujenzi wa miradi ya Zahanati na madarasa katika vijiji husika. 

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatilia ujenzi wa Bweni la wanafunzi shule ya Sekondari Jikomboe ambalo limegharimu kiasi cha Shilingi milioni 75 ili kujiridhisha kama fedha hizo zimetumika kama ilivyokusudiwa na kuona kama thamani yake inaonekana. 

Akiwa Wilayani Chato Mheshimiwa Robert Gabriel ametembelea shule ya Msingi Chato na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita na vyoo, ujenzi wa Zahanati ya kijiji Mganza, ujenzi wa Bweni shule ya Sekondari Zakia Meghj pamoja na Ujenzi wa Soko la dagaa Kasenda na kuagiza takukuru kufika katika miradi hiyo ili kufuatilia matumizi ya fedha katika miradi ya Zahanati, Bweni na madarasa. 

Vilevile Mkuu wa Mkoa ametembelea ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na kupongeza jitihada za utekelezaji wa mradi huo zinazoendelea kwa kufikia asilimia 63. Awali Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita Mhandisi Haruna Senkuku alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa uwanja huo una Run way ya Kilometa 3 ambapo hadi kukamilika mradi utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 39. 
Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa uwanja wa ndege Chato ukiendelea.
Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya ya Chato baada ya kuwasili Wilayani Chato.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Chato pia ni waziri wa Nishati Mheshimi Dkt Medard Kalemani. 
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita Mhandisi Haruna Senkuku akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Uwanja wa ndege Chato alipotembelea na kujionea ujenzi katika moja kati ya ziara yake ya kikazi Wilayani Humo.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongoza viongozi katika ukaguzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.(PICHA NA MAGESA JUMAPILI AFISA HABARI MKOA WA GEITA)

Taasisi ya kijamii ya The Desk and Chair Foundation yatoa msaada wa kisima cha maji jijini Mwanza

$
0
0
Na David John Mwanza .

TAASISI ya kijamii ya The Desk and Chair Foundation ya jijini Mwanza imetoa rai kwa Serikali kuwa na mawasiliano ya karibu ili kujuwa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo watanzania hususani wenye uhitaji maalum.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Ofisini kwake jijini hapa Mwakilishi mkazi wa Taasisi hiyo hapa nchini yenye Makao yake Makuu nchini Uingereza Sibtain P.L Maghjee amesema kuwa taasisi yake inashughulika na matatizo ya watu hususani walemavu na hata jamii kwa ujumla.

Amesema kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo ni kukosekana kwa mawasiliano ya karibu kutoka Serikali ili kupata takwimu za watu au jamii yenye uhitaji. " Taasisi yetu imekuwa ikifanya kazi nyingi katika jamii ikiwamo kuchimba Visima pamoja na kusaidia Ambulence kwa ajili ya wagonjwa katika vituo vya afya. mbalimbali hapa nchini na zaidi vijijini "amesema Meghjee

Akizungumzia zaidi taasisi hiyo amesema mbali na huduma hizo lakini pia wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali ya ufundi, wa aina mbalimbali kwa vijana ambapo mwisho wa siku wanajiajiri wenyewe. Amesema kuwa wao kama taasisi pia wanatengeneza Ambulence kwa kutumia mafundi hao ambao wanafundishwa kupitia Kalakana yao iliyopo Greenview eneo la Ghana jijini hapa.

Pia akizungumzia misaada wanayoitoa amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo hususani visima ambavyo wanakabidhiwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuvithamini. " Unajuwa Ndugu mwandishi lazima watu wajenge nidhamu ya kutunza na kuthamini vitu ambavyo wanapewa kwani kufanya hivyo kunawapa moyo hata watu wanaotoa. "amesema.

Amesema licha ya uchimbaji wa visima hivyo lakini pia taasisi imekuwa ikifanya mambo mbalimbali tangu kuazishwa kwaks mwaka 1979 hapa nchini na wametengeneza basikeli 30 kwa ajili ya walemavu ambazo zitakabidhiwa hivi karibuni.
Mwakilishi mkazi wa Shirika la The Desk and  Chair Foundation  Sbtain P.L Meghjee  (shati la drafti) akikabidhi kisima katika moja ya maeneo ambayo wametoa huduma hiyo hapa nchini .

SERIKALI,WADAU WA MAENDELEO NA TASAF WAENDELEA NA VIKAO KAZI VYA KUTATHIMINI UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI MJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

NA ESTOM SANGA-TASAF

Vikao Kazi vya Serikali na Wadau wa Maendeleo vinaendelea kufanyika mjini Dar es salaam kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Mapitio hayo ni utaratibu wa kawaida wa kupima mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaohudumia kaya za walengwa zipatazo MILIONI MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

Washiriki wa vikao kazi hivyo vinavyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za makao makuu ya TASAF mjini Dar es salaam, ni pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali kutoka Wizara ya Fedha, serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Ofisi ya Rais,Benki ya Dunia,UNICEF,Shirika la Misaada la Ireland,na Shirika la Misaada la Uingereza DFID.

Wengine ni kutoka UNDP,USAID ,ILO,Fundacion Capital,Brac Tanzania, SVPO Zanzibar,PO- RALG Dodoma, VPO-DOE,MOHCDGEC ,Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Ujenzi,na Wizara ya Kilimo. TASAF imekuwa ikishirikiana na Wizara na wadau hao wa Maendeleo katika kutekelezaji jitihada za serikali za kupunguza adha ya umaskini kwa wananchi wanaoishi katika umasikini uliokithiri.

Vikao kazi hivyo ambavyo vinafanyika baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa Mpango pia vinajadili muundo wa Awamu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya masikini na vitahitimishwa hapo kesho na kisha siku inayofuata andiko la pamoja la mapendekezo ya kuboresha utekelezaji wa Mpango litafikiwa na kisha kuwasilishwa serikalini kupata idhini.
Moja ya kundi la watendaji wa serikali, wadau wa maendeleo na TASAF wakiendelea na mjadala.
Pichani, baadhi ya maafisa wa TASAF na wadau wa maendeleo wakiendelea na majadiliano juu ya masuala ya uboireshaji wa shughuli za mpango.
Pichani ya juu na chini ni wajumbe wa kikao kazi cha maafisa wa TASAF na wadauy wa maendeleo wakiwa kwenye moja ya kumbi kujadili mafanikio na changamoto wa Mpango wa kunusuru kaya masikini.
Pichani baadhi ya washiriki wa vikao kazi kati ya wadau wa maendeleo, TASAF na serikali wakiendelea na mjadala.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images