Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1412 | 1413 | (Page 1414) | 1415 | 1416 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizundua rasmi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania –TPB Bw. Sabasaba Moshingi baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimpongeza Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende, Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, kumkabidhi Mwenyekiti huyo, Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na masuala ya fedha (Financial Sector Deepening Trust-FSDT), Bw. Sosthenes Kewe, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb), akichangia mada kuhusu umuhimu wa huduma za fedha hususan vijijini, kabla Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, hajazindua rasmi 
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (Sera), akizungumza maneno ya utangulizi wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akizungumzia mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali kwa kuja na Sera ya kuhudumia Sekta Ndogo ya Fedha nchini ijulikanayo kama Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo (Mb), akielezea utayari wa Wizara yake katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea umuhimu wa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028 katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini katika jamii, wakati wa uzinduzi wa sera hiyo mjini Dodoma.

  Picha na Kitengo cha Mawasiliano serikalini-Wizara ya Fedha nan Mipango  Na Benny Mwaipaja, Dodoma


  MAKAMU wa Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN, amezinduzi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, tukio litakalofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

  Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoa huduma ndogo za fedha kupunguza riba za mikopo na tozo mbalimbali ili kufanikisha lengo la Sera hiyo ambalo ni kuimarisha huduma jumuishi za fedha kwa kujenga mazingira wezeshi yatakayoleta ufanisi wa utoaji wa huduma ndogo za fedha nchini kwa wananchi wenye kipato cha chini.

  “Ninawaomba pia muongeze ubunifu katika kutoa huduma zinazohitajika na wananchi wa kipato cha chini pamoja na kupeleka huduma hizo katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao au biashara zao” aliongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan

  Alizitaka taasisi za huduma za fedha kuwaelimisha wananchi kabla ya kutoa huduma hizo ili kupunguza athari wanazozipata wananchi.

  “Ni matarajio yangu kuwa, Wizara ya Fedha na Mipango itashirikiana na wadau katika kutekeleza Sera hii na kuhakikisha malengo ya Sera ambayo ni kukuza uchumi na kupunguza umaskini yanafikiwa” alisisitiza

  Alisema Ripoti ya Finscope ya mwaka 2017 ambayo iilionesha kuwa Tanzania imepiga hatua kwenye suala zima la huduma jumuishi za fedha (financial inclusion) na kufikia asilimia 72 kwa 2017, huku changamoto kuu iliyoainisha ni elimu/uelewa mdogo wa huduma za fedha kwa wananchi.

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alisema kuwa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake itaweka mazingira yatakayowezesha kuchochea maendeleo stahiki na ubunifu wa Huduma Ndogo za Fedha ili kukidhi mahitaji halisi ya wananchi wa kipato cha chini na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

  Alisema kuwa Sera hiyo itaongeza utoaji wa huduma bora na jumuishi ya Kifedha Vijijini na kutungwa kwa sheria ambazo zitawalinda wananchi dhidi ya baadhi ya taasisi za kifedha zinazoibuka na kuwa kero kwao kwa kuweka riba kubwa pamoja na kupatiwa huduma zisizoridhisha.

  “Sera ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake vitaendelea kutoa miongozo kwa wadau wote na kuchochea uanzishwaji wa washiriki wapya na ukuaji wa waliopo ili kutoa ushindani zaidi ili kuleta matokeo yatakayoongeza huduma rasmi, kukuza utamaduni wa kuweka akiba, kuimarisha sekta ndogo ya fedha, ambayo yatachangia ukuaji wa uchumi, ajira na kupunguza umaskini” Aliongeza Dkt. Mpango

  Sekta ya huduma ndogo ya fedha nchini inajumuisha aina ya watoa huduma za fedha wafuatao: benki na taasisi za fedha zinazotoa huduma ndogo za fedha; vyama vya ushirika wa kuweka akiba na kukopa; kampuni za huduma ndogo za fedha kama vile BRAC, Blue Finance, Tujijenge, Platinum n.k,

  Nyingine ni asasi za fedha zisizo za Serikali, Mifuko na Programu za Serikali; na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii kama vile asasi za kijamii, benki za kijamii za vijiji (VICOBA), Ushirik a wa akiba na mikopo vijijini (VSLAs), Ushirika wa akiba na mikopo kwa zamu (ROSCAs), wakopeshaji binafsi na wengine wanaotoa huduma zinazohusiana na fedha.

  Serikali kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa Huduma Ndogo za Fedha kwa wananchi wa kipato cha chini iliamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2000 kwa kutunga Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wa Sera hiyo kwa kipindi cha miaka kumi ili kutatua changamoto zilizojitokeza katika sekta ndogo ya fedha

  Changamoto hizo ni pamoja na ongezeko la idadi ya watoa Huduma Ndogo za Fedha; Ukosefu wa mfumo wa Sheria na Kanuni za kusimamia Taasisi Zisizochukua Amana na Vikundi vya Fedha vya Kijamii; Ukosefu wa mfumo wa kumlinda Mtumiaji na mtoa Huduma Ndogo za Fedha na uelewa mdogo wa masuala ya fedha; Kutokuwepo na uwazi katika vigezo na masharti ya utoaji mikopo; Viwango vya juu vya riba; na Kuibuka kwa taasisi zisizo kuwa na uaminifu.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nyakato nje kidogo ya jiji la Mwanza mara baada ya kufungua kiwandaa cha Sayona Drinks ltd kilichopo Nyakato.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Katikati ya jiji la Mwanza wakati akitokea Nyakato.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati mmiliki wa Kiwanda cha Sayona Drinks Subhas Patel alipokuwa akionesha bidhaa mojawapo ya kiwanda hicho.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja mbunge wa Ilemela Angelina Mabula wakati Kwaya ya Makongoro ilipokuwa ikitumbuza katika viwanja vya Mwatex Nyakato jijini Mwanza
  Kwaya ya Makongoro ikitumbuiza
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini wimbo wa kwaya ya Makongoro kabla ya kuhutubia mamia ya wananchi Nyakato mkoani Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wananchi wa Nyakato mara baada ya kuwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato mara baada ya kumaliza kuwahutubia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha Sayona Drinks kilichopo Nyakato jijini Mwanza.  PICHA NA IKULU

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde leo amezindua programu ya Urasimishaji Ujuzi kwa Vijana ambao wana ujuzi lakini hawakupitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya Ufundi(Recognition of Prior Learning).

  Ufunguzi huo wa Program hii ya Urasimishaji Ujuzi ambao unagharamikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu umefanyika leo katika Chuo cha VETA Jijijni Tanga na kujumisha jumla ya Vijana 701 kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara wanatarajiwa kunufaika na mpango huo.

  Akizungumza na Vijana hao, Mh.Mavunde amesema serikali inatekeleza mpango mkubwa wa ukuzaji ujuzi kwa Vijana unaolenga kuwafikia takribani Vijana Milioni 4 nchi nzima kwa lengo la kuwajengea ujuzi stahiki utakaowasaidia kupata Ajira na kujiajiri wenyewe.

  Aidha Naibu Waziri Mavunde amewataka Vijana wote kuchangamkia fursa mbalimbali zitokanazo na ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima,Uganda-Tanga ambapo serikali kuu na serikali ya Mkoa wameendelea kujenga mazingira rafiki ya kuhakikisha Vijana wanafikia malengo yao.

  Wakizungumza baada ya kuzinduliwa program hiyo, Vijana hao wameishukuru Serikali kwa Mpango huu wa urasimishaji ujuzi ambao unawapa fursa ya kupewa cheti cha Ufundi kutoka VETA bila kupitia utaratibu wa kawaida wa masomo ambapo takribani Vijana 3900 watanufaika na Mpango huu nchi nzima.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa programu ya Urasimishaji Ujuzi.
  Mbunge wa Handeni Vijijini Mboni Mhita akizungumza katika uzinduzi wa programu ya urasimishaji ujuzi.

  washiriki wa uzinduzi wa programu ya Urasimishaji Ujuzi.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma wakati akikagua mashine ya kucharangia mawe kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
  Mkandarasi wa Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation Zhu Wan Li akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto), kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa akisikiliza maelezo ya Mhandisi Mkazi anayesimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami kutoka Kampuni ya DOCH Limited, Eng Mekbib Tesfaye, wakati akikagua ujenzi wake, mkoani Kigoma.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kidahwe-Kasulu yenye urefu wa KM 63 inayojengwa kwa kiwango cha lami, ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 52, mkoani Kigoma.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa, akisikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Raphael Ndimbo (kushoto), katika chumba cha maabara ya mkandarasi wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (Mb), amewataka wananchi wanaopata nafasi za kazi katika miradi ya ujenzi wa barabara kuwa wazalendo katika kulinda vifaa na kuepuka vitendo vya hujuma vinavyoweza kujitokeza ili kuhakikisha miradi hiyo inaenda kwa kasi na kumalizika kwa muda uliopangwa.

  Mhe. Kwandikwa ametoa kauli hiyo wilayani Kasulu mkoani Kigoma, alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 inayojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation na kuelezwa kuwa kuna wizi wa mafuta kiasi cha lita elfu 23 zilizoibiwa hivi karibun ambapo amewataka wananchi kuwa na uzalendo kwanza katika miradi yote ya ujenzi katika maeneo yote.

  “Wizi wa namna hii haukubaliki na mtandao ni mkubwa hivyo naagiza vyombo vya usalama vichukue hatua kali mapema ili kuweza kuondoa madhara makubwa zaidi”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

  Amewataka makandarasi na wasimamizi wa miradi kutoa elimu kwa waajiriwa kila siku kabla ya kuanza kazi kukemea tabia za wizi na ubadhilifu wowote utakaowezea kutokea kwani ni moja ya sababu za miradi pia kuchelewa na gharama kuongezeka.

  Kuhusu suala la ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami Mhe. Kwandikwa, ameridhishwa na kasi ya ujenzi ya mkandarasi huyo ambapo mpaka sasa maendeleo ya mradi umefikia asilimia 52.

  Ameongeza kuwa mkandarasi aendelee kushirikiana na wananchi wa maeneo hayo kwa kuwatengenezea barabara nzuri ya mbadala hasa kipindi hiki cha mvua ili iweze kutumika kwa urahisi na kufanya wananchi kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo.

  Aidha, Mhe. Kwandikwa, amesisitiza kuwa nia ya Serikali ni kufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami kwakuwa ni kiungo kikuu kwa nchi za Congo DRC, Burundi na Rwanda na mkoa wenye uzalishaji mkubwa katika sekta ya uvuvi, kilimo, madini na utalii.

  Naibu Waziri Mhe. Kwandikwa ametoa wito kwa madereva wote nchini kuzingatia upakiaji wa mizigo kulingana na sheria na utaratibu waliopewa ili kuweza kuzilinda barabara zetu nchini zinazojenga kwa fedha nyingi.

  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma, amesema mradi wa ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 60 ambazo zote ni fedha za ndani na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwakani.

  Ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami ukikamilika utafungua fursa za ajira na uchumi na hivyo kuunganisha vizuri mkoa huo na mikoa mingine ya nchi.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Kigwangalla “Sasa tutakamata majangili kuliko kukamata nyara” Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake hiyo ni kuhakikisha wanachukua hatua za haraka katika kulinda rasilimali za Taifa kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili nchini. 
   
  Dkt. Kigwangalla amesema hayoi mapema leo mjini Dodoma wakati wa akielezea namna walivyojipanga kukamata majangili kabla hawajhafanya ujangili. “Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini.
   
   Ameeleza Dkt.Kigwangalla Aidha, ameendelea kutuma salamu kwa majingili wote kuachana na baishara hiyo kwa kujisalimisha ama kukimbia kwani kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa mtandao mpana wa majingili. “Jana tumefanikiwa kumkamata Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. 
   
  Amekutwa na risasi 356, magazines 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha. Wizara yangu imejipanga na tutaendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili huu” alimalizia Dkt.Kigwangalla. Dkt.Kigwangalla amebainisha kuwa, tayari vikosi maalum kwa kushirikiana na Wizara yake wakiwemo wale wa Wanyama pori wanaendelea na uchunguzi wa ndani hasa katika mitandao ya Majangili wakubwa wa ndani na nje ya Nchi. 
   
  Mwisho. CODES: Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake hiyo ni kuhakikisha wanachukua hatua za haraka katika kulinda rasilimali za Taifa kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili nchini. Dkt. Kigwangalla amesema hayoi mapema leo mjini Dodoma wakati wa akielezea namna walivyojipanga kukamata majangili kabla hawajhafanya ujangili. 
   
  “Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini. Ameeleza Dkt.Kigwangalla Aidha, ameendelea kutuma salamu kwa majingili wote kuachana na baishara hiyo kwa kujisalimisha ama kukimbia kwani kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa mtandao mpana wa majingili.
   
  “Jana tumefanikiwa kumkamata Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. Amekutwa na risasi 356, magazines 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha. Wizara yangu imejipanga na tutaendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili huu” alimalizia Dkt.Kigwangalla.
   
  Dkt.Kigwangalla amebainisha kuwa, tayari vikosi maalum kwa kushirikiana na Wizara yake wakiwemo wale wa Wanyama pori wanaendelea na uchunguzi wa ndani hasa katika mitandao ya Majangili wakubwa wa ndani na nje ya Nchi.
  Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu aliyekamatwa akijipanga kuingia Hifadhi ya Serengeti
  Baadhi ya risasi zilizokamatwa na jangili huyo
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla akiwa pamoja na Mhifadhi wa Mkuu wa Serengeti William Mwakilema pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro wakiangalia mpaka unahishia pori tengefu la Loliondo-Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti mwishoni mwa wiki wakati wa kukagua maeneo hayo yenye mgogoro na wafugaji.

  0 0

  Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mkuu wa idara ya Kilimo ya halmashauri ya Meru,Grace Solomon kwenye kilele cha siku tatu za maonesho ya Jukwaa la Wakulima Meru(Juwame) eneo la Leganga. 
  Meneja kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa Kilimanjaro,Ebenezer Shao . 
  Mkulima ambaye ameandaa mashamba darasa mengi kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima wilayani Arumeru,Letayo Nnko akiwa na baskeli aliyokabidhiwa. 
  Meneja kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa Arusha,Kaanael Kitomary . 
  Wananchi wakijifunza mbinu bora za kilimo kutoka kwenye mabanda yaliyoandaliwakuwahudumia wakulima. 
  Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.


  Arusha.Kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini imewatambua kwa kuwapa zawadi wakulima bora watatu waliotangazwa washindi kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji ya Nanenane kanda ya Kaskazini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Themi jijini hapa mwezi Agosti mwaka huu na mkulima mmoja aliyeongoza kwa kuandaa mashamba darasa. 

  Meneja Kiongozi wa kampuni hiyo nchini,Frank Wenga alisema wameamua kutoa zawadi za baiskeli zenye boksi maalumu la kubebea pembejeo wakati wa kilele cha Jukwaa la Wakulima Meru (Juwame) baada ya kutambua uwezo wao katika kilimo cha kisasa kinachozingatia kanuni za matumizi ya mbegu bora.

  "Kampuni yetu inawapongeza kwa kuonesha mfano wa kuigwa katika mikoa yenu,naamini wakulima wengine wataiga mbinu sahihi za kilimo mnazotumia kufikia malengo hadi kutambuliwa kwenye maonesho ya kanda ya kaskazini kama wakulima bora nasi tukiwa wadau tunawapongeza,"alisema Wenga

  Walionufaika na baiskeli hizo zenye thamani ya Sh 1.2 milioni ni mkulima bora kutoka mkoa wa Kilimanjaro ni Ebenezeri Shao,Kaanael Kitomari kutoka mkoa wa Arusha, Boay Tlem mkoa wa Manyara na Letayo Nnko mkulima kutoka halmashauri ya Meru ambaye ameandaa mashamba darasa mengi zaidi kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima wenzake.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo,Nnko alisema itamsaidia katika shughuli za kilimo na kuishukuru kampuni ya Monsanto kwa kutambua juhudi zake za kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usalama wa chakula.Awali Mkuu wa idara ya kilimo katika halmashauri ya Meru,Grace Solomoni alisema wakulima wamekua wakipata changamoto ya kupata mbegu bora kwa wakati na wakati mwingine wamejikuta wakinunua mbegu bandia na kupata hasara.

  Aliwataka wafanyabiashara wa makampuni ya mbegu kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa wakati ili kuwawezesha kuwa na kilimo chenye tija na sio kulima kwa mazoea kwaajili ya kujikimu tu.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akisalimiana na watumishi  pamoja na wakuu wa idara mbali mbali Mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akisalimiana na mwenyeji wake ambaye kwasasa amestaafu kwenye kiti cha ukuu wa Mkoa ,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za Mkoa huo kwaajili ya makabidhiano ya kuanza shughuli na majukumu ya kazi.
   Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akimkabidhi hati ya pongezi Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga.
  Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga  akionesha Hati ya pongezi ambayo amepatiwa na Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akiagana na watumishi.
  Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akimkabidhi Mkuu wa Mkoa mambo muhimu ambayo ameyaandika wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi.
  Wakuu wa Wilaya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa huo pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM).
   Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa kwenye ofisi yake kwaajili ya kuanza shughuli rasmi.(PICHA NA MADUKA ONLINE)
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi amewataka watumishi na wakuu wa wilaya Mkoani humo kuwatumikia kikamilifu wananchi wenye matarajio makubwa kwa serikali yao.

  Mhandisi  Lughumbi aliyasema  hayo alipozungumza na watumishi na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo katika hafla ya kukabidhiwa ofisi na Mtangulizi wake Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga aliyestaafu nafasi hiyo.

  Alisema amefika kwenye Mkoa wa Geita kufanya kazi hivyo watumishi wote wawajibike kuchochea maendeleo kwa kasi ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu.

  “Nimeingia katika Mkoa huu kama mlivyonikaribisha mmenikaribisha nimekuja kufanya kazi  nimekuja kutumika nimetumwa kuwa mtumishi kwa mwendo tulionao hatuna muda wa kupumzika ni kipindi cha mageuzi lazima tugeuze kitu kigeuzike watu wajue tumegeuza  hata wanaofuatilie waone mambo yapo sawa sawa  ukione maendeleo yanakimbia ujue uku kulipokuwa  kunachelewa vilikuwa vipindi vigumu vya matengenezo”Alisema Lughumbi.

  Pia amezungumzia tatizo la uduni wa miundombinu ya elimu na shida ya maji inayoendelea kuwasumbua wananchi wa Geita.

  “Wakina mama bado wanandoo kichwani   katika Mkoa tupo asilimia hamsini upatikanaji wa maji safi na salama  kuna watu wamecheza na  fedha ya umma maji hayajaja tangu miaka ya sabini meja jenerali wewe ulikuwa mpole mimi naenda kwenye  sait nitakuwa mkali kidogo hasa ambao wanacheza na mali ya umma”Alisisitiza Lughumbi.

  Mkuu wa Mkoa mstaafu, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alisema kwa sasa anakwenda kupumzika na kuwataka wanaobaki kulitumikia taifa wafanye kazi kwa weledi na kasi inayoendana na ile ya Rais Dr John Magufuli.

  Mkoa wa Geita ni Kati ya Mikoa ambayo ilianzishwa mwaka 2012,na wakuu wa Miako ambao wamepita hadi sasa ni watatu ,Magalula Said Magalula,Fatuma Mwasa na Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu hivi karibuni na kumpisha ,Mhandisi Robert Lughumbi.


  0 0


  Na.Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni.

  Taarifa hizo za Mh. Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017.

  Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Bw. Daniel Masolwa Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa za Takwimu (NBS),kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS,pamoja na  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Johnson Nyella wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari.

  Masolwa amesema kuwa upotoshaji huo uliofanywa na Mh. Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonesha kuwa juhudi znazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano hazina manufaa kwa Wananchi.

  “Napenda kukanusha kauli ya Mh. Zitto kuhusu taarifa zake zinazodai kuwa takwimu za Pato la Taifa zimepikwa, Mh. Zitto anatakiwa kujua kwamba kazi ya kukokotoa takwimu za Pato la Taifa ni ya kitaalam na inafuata miongozo inayotolewa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Takwimu na Shirika la Fedha Duniani (IMF)”,alisema Masolwa.

  Ameongeza kuwa miongozo hiyo ni pamoja na mifumo ya pato la Taifa ya mwaka 2003 na 2008 na mwongozo wa kuainisha shughuli za kiuchumi Toleo la Nne ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka  2016 Tanzania imekuwa nchi ya pili kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kwa utoaji, uchambuzi, usimamizi na usambazaji wa takwimu  kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

  Aidha Bw.Masolwa ametoa wito kwa taasisi yoyote ile au mtu binafsi anayetaka kutayarisha takwimu rasmi  kwa ajili ya kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo kupata maelezo ya kina kuhusu ukokotoaji na miongozo mbalimbali.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyella amesema kuwa Mh. Zitto amekokotoa ukuaji wa Pato la Taifa anaodai kuwa ni sahihi kwa kuangalia tofauti kati ya ongezeko la ujazi wa fedha na mfumuko wa bei jambo ambalo sio sahihi kulitumia kama kipimo.

  “Ukokotoaji wa aina hiyo umejengwa juu ya nadharia inayoitwa ‘quantity theory of money’ ambayo inasema mfumuko wa bei hutokea pale fedha zinapoongezeka kwa kasi zaidi kuliko uzalishaji wa vitu halisi ambayo si sahihi kutumia nadharia hiyo kuelezea mfumuko wa bei na ukuaji wa uchumi katika kipindi cha muda mfupi kama Mh. Zitto alivyofanya,” alifafanua Bw.Nyella.

  Wawakilishi hao wa Benki Kuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wamelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya taarifa za Ukuaji wa Pato la taifa kutolewa na Mh.Zito, na wakawaasa Wananchi na wanasiasa kuacha kupotosha takwimu za serikali na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kupotosha umma kwa makusudi.
  Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo ichani) wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato la taifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu Johnson Nyella
  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu Johnson Nyella (kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo ichani) wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato lataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa.

  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo


  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, David Umoh, pamoja na Mtaalam wa Huduma kwa Wateja, Kitengo cha Biashara, Sarah Cyprian wakizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya Tumekusoma inayoendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma *147*00#.  Namba *147*00#  itawawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi, pamoja na kupata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hiyo mpya.
  Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandhishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa salaam.
  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania, leo imezindua rasmi kampeni mpya ya Tumekusoma, ambayo ni mkakati mkubwa wa kufikia wateja wake na bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao kwa muda muafaka. Kampeni hii ya Tumekusoma pia inaendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma ya *147*00# itakayowawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi. Wateja wa Tigo watakaotumia namba hiyo mpya pia watapata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hii mpya.

  Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya Tumekusoma jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alisema, ‘Tumesoma hitaji la watumiaji wa mitandao ya simu la menu au namba ya huduma ambayo itarahihisha hatua za kununua vifurushi au kufanya miamala ya fedha. Menu hii mpya inajibu mahitaji hayo yote. Ni rahisi sana kutumia. Pamoja na haya, namba mpya ya *147*00# inawapa wateja ofa kabambe ya nyongeza ya muda wa maongezi, SMS na data kila mara watakaponunua vifurushi kupitia namba hii,’ Umoh alisema.
  Alibainisha faida nyingine kubwa ya menu hiyo mpya ni ofa za Chapchap, zinazowawezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vinavyoendana na mahitaji na tabia zao za kipekee za matumizi ya simu, jambo ambalo linaendana na lengo la Tigo la kuwaongezea thamani wateja wake. ‘Tumesoma mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho muafaka linaloendana na mahitaji yao ya kipekee kupitia menu hii inayorahisisha matumizi yao ya simu kupitia mtandao wetu ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini,’ alisema.

  Tigo inaendelea kuwa mtandao unaoongoza kwa kuzindua bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja. Tigo ndio mtandao ulioleta mageuzi makubwa zaidi katika mifumo ya bei ya mitandao ya simu za mkononi nchini. 

  Tigo pia ndio iliyokuwa mtandao wa kwanza kuzindua huduma za vifurushi vya sauti na data, ndio mtandao wa kwanza kuzindua simu za kisasa zenye mfumo wa lugha ya Kiswahili na pia ndio mtandao wa kwanza nchini kuzindua huduma ya Tigo Pesa iliyowezesha wateja wake kufanya miamala ya fedha nje ya nchi iliyokuwa na uwezo wa kubadili thamani ya fedha kulingana na thamani ya fedha ya nchi husika.

  ‘Kupitia Tumekusoma, tunawakaribisha wateja wote wa Tigo wajiunge nasi katika safari hii ya kumbukumbu ya hatua tulizopiga na mafanikio makubwa tuliyopata katika kipindi hiki cha kuwahudumia Watanzania. Tunawakaribisha nyote kuungana nasi katika mageuzi ya kidigitali nchini na kufurahia mtandao wetu wa Tigo ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini Tanzania,’ Umoh alisema. 

  Menu mpya iliyoboreshwa ya *147*00# inaanza kufanya kazi leo na wateja wa Tigo wanaweza kuanza kupata bonasi murwa kwa manunuzi yote wanayoyafanya. Tunawakaribisha wateja wetu wakae mkao wa kupokea ofa zaidi kabambe huku tukiendelea katika safari hii ya kuwahudumia wateja wetu kwa urahisi zaidi na kwa ubora wa hali ya juu.


  0 0

  Afisa mtendaji wa kata ya  Ng’ang’ange bwana Aron Mwenzegule akiwa mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela wakibadilisha mawazo wakati wa ziara ya kutembelea shule ya msingi Mdeke
   Mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce akizungumza mbele ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wakati wa ziara ya kubaini changamoto za shule hiyo
  Mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela akiwa makini kusikiliza anachoambiwa na mwalimu wa shule ya msingi Mdeke wakati wa ziara yake katika shule hiyo.

  Na Fredy Mgunda,Kilolo.

  Shule ya msingi ya Mdeke iliyopo kata ya Ng’ang’ange wilayani kilolo ina walimu 6 wanaowafundisha zaidi ya wanafunzi 440 na kusababisha kutotolewa kwa elimu bora kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

  Hayo yamebaini wakati wa ziara iliyofanywa na wajumbe wa  kati za siasa wa  chama cha mapinduzi (CCM) wilayani kilolo walipokuwa wameenda kwa lengo la kufanya usafi katika kata ya Ng’ang’ange

  Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usafi mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce alisema kuwa shule inajumla ya walimu 9 lakini walimu walimu watatu wameenda kusoma hivyo walimu waliopo shuleni ni walimu sita na kusababisha ugumu wa kuwafundisha wanafunzi wa shule hivyo.

  “Tuna jumla ya wanafunzi 448 na walimu tupo 6 sasa utaona kiasi gani tunapata ugumu wakufunzisha wanafunzi na kuwapa elimu bora kwa kuwa walimu tumezidiwa na idadi ya wanafunzi huku walimu wengine wakifundisha masomo ambayo hawayawezi vizuri” alisema Aloyce

  Aloyce alisema kuwa licha ya kuwa kuna walimu sita lakini walimu wawili wanafundisha elimu ya awali na walimu wanne ndio wanafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba hapo ndio utakundua kiasi gani kazi ya ualimu katika shule hii inakuwa ngumu.

  “Ukiangalia tuna madarasa saba hivyo walimu wanne tu ndio tunafundisha hapo utaona kwa kiasi gani tunapata ugumu wa kufundisha na kuwapa elimu bora wanafunzi wetu hivyo tunawaomba mtufikishie kilio chetu huko juu ili kuweza kutatua tatizo hili” alisema Aloyce

  Aidha Aloyce alisema kuwa walimu wa shule hiyo wamekuwa wakijitoa kufundisha kwa jitihada zao zote na kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo licha ya kuwa na changamoto lukuki.

  “Ukingalia mwaka huu tulikuwa na wanafunzi 53 na waliofaulu ni wanafunzi 40 hivyo utagundua kwa kiasi gani sisi walimu wa shule hii tunahitaji pongezi kwa kazi tunayoifanya licha ya changamoto zinazotukabili walimu wa shule hii ya Mdeke” alisema Aloyce

  Lakini Aloyce alisema kuwa walimu wanakumbana na changamoto ya nyumba za walimu hivyo inawalazimu walimu kuishi umbali wa zaidi ya kilimeta mbili hadi ufike shule hivyo utaona kuwa walimu mara kwa mara wanafika shule wakiwa wameshachoka na kuathiri swala la ufundishaji wanafunzi.

  “Mwalimu anatoka mbali sana sasa unafikiri mwalimu huyo akifika shule inakuaje hivyo na hii changamoto tunaomba mtupelekee huko kwa viongozi wa ngazi za juu mfano tunawalimu anayenyonyesha hebu angalia mwalimu hadi anyonyeshe unafikiri atafika shule saa ngapi tatizo la nyumba ni kubwa sana” alisema Aloyce

  Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo Saidi Kiponza alisema kuwa wameziona changamoto zilizopo katika shule hiyo na kwenda kuzifikisha kwa viongozi wa ngazi za juu ili kuweza kuzitafutia ufunzi na kwafanya wafanyakazi wa serikali kuitekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kikamilifu.

  “Sisi hatujaja kwa maonyesho tumekuja kufanya kazi na kuhakikisha viongozi wa serikali wanaitekeleza vilivyo ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020 ili chama hiki kiendelee kuwa madarakani miaka yote” alisema Kiponza

  Naye mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela alisema kuwa lengo la ziara hiyo katika kata ya Ng’ang’ange ni kufanya usafi na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi  na kuzipeleka kwa viongozi wa serikali kuzitafutia ufumbuzi wa changamoto ambazo tunakuwa tumezibaini na kuzitatua.

  “Unajua ukujua eneo gani kunachangamoto gani inakuwa kazi rahisi sana kuzitafutia ufumbuzi mapema na kuwafanya wananchi waendelee kukiamini chama cha mapinduzi kwa kazi yake inayofanywa chini ya Rais wetu Dr John Pombe magufuri kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo” alisema Gervas Kahemela.


  Usikose kutembelea blog hii kwani bado kuna habari ya kuhudhunisha kutoka katika shule hii ya Mdeke ilyopo wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.

  0 0

  Meneja Mauzo wa Jumia Tanzania, Iddy Mkumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Black Friday utakaoweza kutoa punguzo la asilimia 70 kwa bidhaa atakayoinunua mteje kupitia tovuti ya Jumia Tanzania  itakayoanza mwezi wa Novemba 24 hadi Desemba 04 mwaka huu kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mwanza,Morogoro, Mara na Zanzibar.
  Afisa Masoko na Mahusiano ya Jamii wa Jumia Travel, Geofrey Kijanga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Jumia Travel inavyotoa huduma za malazi na namna walivyopunguza bei kwa msimu huu wa sikukuu leo kwenye ofisi za Jumia Tanzania jijini Dar Es Salaam
  Maneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi Kampuni ya Jumia Tanzania akizungumzia kuhusu siku ya Black Friday itakayofanyika kwa takribani siku kumi na moja (11) kuanzia mwezi wa Novemba 24 hadi Desemba 04 mwaka huu.
  Mkutano ukiendelea kwenye ukumbi wa ofisi ya Jumia Tanzania jijini Dar es Salaam leo

  Ikiwa imebaki takribani miezi miwili mwaka 2017 kuisha, Jumia Tanzania imejizatiti kuja na kampeni iliyopewa jina la ‘BLACK FRIDAY’ ambayo itawawezesha wateja wake kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali mtandaoni kwa punguzo la mpaka alisimia 70 kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa kampeni hiyo Meneja Mauzo wa Jumia Tanzania, Bw. Idd Mkumba amebainisha kuwa kutokana na mafanikio makubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika mwaka jana na kushuhudia watanzania wakifanya huduma za mtandaoni ambapo takribani oda 600 kwa siku wameona ni vema kuirejesha tena kwa kishindo mwaka huu.

  “Mwaka 2016 ulikuwa ni wenye mafanikio kwa upande wa kampeni yetu ya BLACK FRIDAY kwani ndani ya muda wa siku tano tuliyoifanya wateja wengi waliweza kufanya manunuzi mtandaoni. Hivyo basi kwa mwaka huu tena tumeiboresha Zaidi kwa kuongeza siku kutoka tano mpaka 11 ambapo kampeni itaanza rasmi kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4. 

  Na kwa kuongezea hapo ni kwamba safari hii wateja wa Dar es Salaam hawatofaidika pekee yao kwani tumejitanua Zaidi mpaka mikoa mingine kwa mara ya kwanza na kuzifikia sehemu za Visiwani Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Musoma,” alisema Bw. Mkumba.

  Meneja Mauzo huyo wa Jumia Tanzania aliendelea kwa kufafanua kuwa, “Lengo kubwa la kampeni hii ni kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo na kuwarahisishia watanzania kufanya huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao mahali popote walipo huku wakiendelea na shughuli zao. 

  Tanzania ni mojawapo ya taifa linaloendelea Afrika na duniani likiwa na watumiaji wa simu za kisasa na mtandao wa intaneti wanaoongezeka kila kukicha. Hivyo basi nasi tunaitumia fursa hiyo kwa kuwahamisisha watanzania kuitumia teknolojia hiyo kwa manufaa Zaidi, ambapo badala ya kutumia muda mwingi kwenda madukani wanaweza kufanya hivyo wakiwa palepale walipo.”

  “Katika kuwaondoa hofu wateja ambao wanahofia kwamba pengine bidhaa zinaweza kuwa hazina ubora kutokana na ukubwa wa ofa tunazotoa, ni kwamba Jumia Tanzania tunafanya huduma zetu kwa sera ya kulipia pale unapopokea bidhaa yako. Hii humpatia mteja kujiridhisha kwamba bidhaa aliyoiagiza ni sahihi ndipo alipie. Na kwa kuongezea, ada ya malipo ya kufikishiwa mzigo kwa wateja wetu popote walipo itashuka ili kuhamasisha manunuzi Zaidi. 

  Kwa kumalizia kuhusiana na kampeni ya BLACK FRIDAY ambayo itawapatia fursa wateja kupata punguzo la bei mpaka la asilimia 70, tumeingia ubia na makampuni kadhaa makubwa ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa kama vile Samsung, Startimes, Tronic,… Lakini pia kutokana na kuanza kwa huduma kwenye mikoa mipya niliyoiorodhesga hapo juu, tumetoa ofa kwa wateja watakaofanya manunuzi ya kuzidi shilingi 100,000 watajipatia punguzo la 50% ambapo itawabidi watumie neonsiri J695D,” alihitimisha Bw. Mkumba.

  Akifafanua Zaidi juu ya dhana nzima ya kampeni hiyo, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Bw. Albany James amesema kuwa utamaduni wa BLACK FRIDAY umeanzia nchini Marekani ambapo makampuni wafanyabiashara hutoa punguzo la bei za bidhaa na huduma mbalimbali ili kuukaribisha msimu wa mapumziko na Krisimasi.

  “Utamaduni huu wa kufanya punguzo kubwa la bei mbalimbali za bidhaa na huduma ulianzia nchini Marekani na kushika kasi sehemu zingine duniani kutokana na faida kubwa kwa wafanyabiashara na wateja kwa ujumla. Ni kipindi ambacho watu wengi hufanya maandilizi ya msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya. Na nadhani utamaduni huo hata kwa sisi watanzania pia tunautumia hivyo basi kupitia Jumia Tanzania wateja wataweza kununua bidhaa mbalimbali muhimu kwa msimu huo kama vile za nyumbani, umeme, mavazi, vyombo vya kupikia nakadhalika. Kwa hiyo ningependa kuwatoa hofu wateja wetu kwamba ni bei za bidhaa ndizo zitakazopungua na sio ubora kama wengi wanavyodhahania,” alisema na kumalizia Bw. James.

  Katika kunogesha kampeni hii Jumia Tanzania pia imeshirikiana na makampuni tanzu ya Jumia hapa nchini kama vile Jumia Travel na Jumia Food ambayo nayo yanajihusisha na huduma kwa njia ya mtandao. Ushirikiano huo utawapatia faida wateja watakaokuwa wakifanya manunuzi mtandaoni kupata ofa kama vile za malazi ya bure pamoja na punguzo kubwa kwa hoteli mbalimbali za kifahari nchini.

  Akizungumza kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania, Bw. Geofrey Kijanga ameelezea kuwa wao kama watoaji wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao mbali na kutoa ofa ya kulala bure kwenye hoteli kwa wateja lakini pia watatoa punguzo kubwa la bei za huduma za malazi ambalo litadumu mpaka mwezi Desemba.

  “Tunafahamu kwamba tunaelekea kuumaliza mwaka ambao hugubikwa na msimu wa mapumziko na sikukuu za Krisimasi na Mwisho wa Mwaka, suala la watu kwenda kutembelea na kupumzika sehemu mbalimbali ni muhimu. Katika kulirahisisha hilo Jumia Travel itatoa punguzo kubwa la huduma za malazi kwa hoteli inazofanya nazo kazi nchini. Kwa hiyo mteja hatowaza kuhusu gharama za malazi popote atakaposafiri yeye au pamoja na familia yake. Hivyo basi ni muda muafaka kwa watanzania kuzitumia ofa hizi kwani huwa ni za kweli na hurahisisha gharama kubwa ambazo wanaweza kuziingia kuzipata kwa njia nyinginezo za kawaida,” alisema na kuhitimisha Bw. Kijanga.

  Hii ni fursa kwa watanzania wote kwa ujumla kujiaandaa vema na msimu wa mapumziko na sikukuu unaokuja kwa kufanya manunuzi ya gharama nafuu Zaidi mahali popote walipo kuanzia Novemba 24 na kuendelea kwa siku 11 mwaka huu. Ili kufahamu Zaidi na kujua mengi juu ya ofa zitakazotolewa watanzania wanatakiwa kuwa kutembelea mitandao ya Jumia Tanzania pamoja na kurasa zao za mitandao ya kijamii. Lakini pia kutakuwepo na zawadi mbalimbali kupitia njia za vocha na kuponi kwa wale watakaokuwa wakifuatilia kurasa hizo kwa karibu na kujibu maswali mbalimbali.

  0 0

  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa Wataalamu wetu wanafanya matengenezo ya dharura katika Mfumo wa kupokea gesi kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia cha Kinyerezi I.

  Hivyo Kituo kitazimwa Saa 6:00 mchana hadi Saa 7:00 Mchana ili kupisha matengenezo. 

  Baadhi ya maeneo mbalimbali ya nchi katika kipindi hicho yatakosa umeme.
  Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. 
  Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

  Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo
  Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

  Tovuti: www.tanesco.co.tz
  Mitandao ya Kijamii
  www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu


  Imetolewa na:- 
  Ofisi ya Uhusiano

  TANESCO Makao Makuu

  31/10/2017

  0 0

   Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel,Arusha)

   Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii


  Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakijiandaa kwenda kupaka rangi madarasa katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii

    Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana

  Mmoja wa wazazi shuleni hapo akishiriki zoezi la umwagiliaji wa maua katka maadhimisho ya huduma kwa jamii iliyoratibiwa na Shirika na Haki Elimu


  Wafanyakazi wa Haki Elimu wakiwa wananendelea na zoezi la upakaji rangi shule hapo jana

  Aliyeshika ndoo nyekundu ni Abraham Lazaro kutoka  Idara ya Habari na uchechemuzi akiwa na mfanyakazi mwenzake wakiendelea na zoezi la umwagiliaji  katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii
  Mwanafunzi shuleni hapo akiwa amebeba ndoo kwaajili ya kubebea maji kwaajili ya shughuli ya umwagiliaji shuleni hapo jana


  Meneja Idara ya Huduma, fedha na Utawala Daniel Luhamo akichimba shimo la kuhifadhia taka ngumu shuleni hapo


  Mfanyakazi wa Haki Elimu Raphael akiendelee na shughuli ya upakaji rangi


  Rose Mwenda Mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu kutoka Idara ya Ushiriki na Uwajibikaji wa jamii akipaka rangi bati katika shule yaMukulat iliyopo Mkoani Arusha
  Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari  Mukulat Stella Massawe akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa HakiElimu John Kalage, zawadi  iliyotengeneza katika klabu yao ya wanafunzi ya Njoo Tuzungumze

  Mkuu wa Miradi HakiElimu - Boniventura Godfrey akibeba ndoo za kuchotea maji kwaajili ya umwagiliaji


  Baadhi ya wazazi wakisalimia katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na tunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu


  Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri   akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini John Kalage kwa kutambua umuhimu wa elimu Nchini

   Picha ya pamoja

  Na Pamela Mollel,Arusha


  Shirika lisilo la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mwingi  kwakutafuta maji.


  Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.


  Shirika hilo la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat  watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya kifugaji.


  Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii  ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora


  Ameiomba jamii kushirikiana na mashirika yasyoyakiserikali kupungumza changamoto  yanaozikabili shule za msingi na sekondari na kuitaka jamii kuhakikisha wanatunza miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi walikuwa wanapata shida kwa usafuri umbali mrefu kutafuta maji.


  Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha miradi shirika la haki elimu Boniventura Godfrey amesema kwa kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchni tayari wameanzisha mpango maalumu wa kuzisaidia shule za msingi na sekondari 127  katika wilaya ishirini na mbili kwa kuwasaidia miradi ya maji,uwekaji wa umeme wa jua ,ukarabati wa madarsa,na upelekaji wa vifaa vya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kuapata elimu katika mzngira bora.  Awali wakizungumzi miradi hiyo wanafunzi wa shule ya sekondari Mukulat  Stella Massawe wamelishukuru shirika la haki elimu kwa uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo kwa kuwa mradi huo wa maji utawapungumzia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa kusafuri umbali mrefu kwa kutafuta maji pamoj na kutumia muda wa masomo hivyo ,kupungua kwa changamoto hizo kutapunguza suala la utoro kwa wanafunzi. 


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi waliokuwa wamepanga foleni kulipa ushuru katika mnada wa Malendi Wilayani Iramba.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi akikagua mnada wa Malendi Wilayani Iramba ambapo amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha anajenga vyoo na kufikisha huduma za maji ndani ya mwezi mmoja.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Malendi na maeneo ya jirani waliokuwa katika mnada huo wakinyoosha mikono kumsalimia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowatembelea mnadani hapo.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amempa mwezi mmoja Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba, kujenga vyoo bora katika Mnada uliopo Kijiji cha Malendi, kata ya Mgongo Wilayani humo.

  Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea mnada huo ambapo wananchi wamelalamika kukosa huduma za vyoo na maji kwa kipindi kirefu huku halmashauri ikikusanya ushuru bila kuwaboreshea miundombinu ya mnada huo.

  “Mkurugenzi nakupa mwezi mmoja hapa kuwe na vyoo bora vikiwa na matundu sita kwa ajili ya wananchi hawa pamoja na huduma za maji, kipindi cha mvua kinaanza, lazma muwajali wananchi hawa kwakuwa kipindupindu kinaweza kulipuka hapa”, ameeleza Dkt Nchimbi.

  Ameongeza kuwa kwakuwa hakuna vyoo wananchi watajisaidia maeneo ya jirani na mnada na mvua zikianza zitatiririsha uchafu huo katika eneo la mnada na makazi ya wanakijiji cha Malendi na hivyo kusababisha mlipuko wamagonjwa hasa Kipindupindu.

  Dkt Nchimbi amesema Mkurugenzi huyo ajenge vyoo vyenye matundu sita pamoja na kuvuta huduma za maji kwakuwa maji husaidia usafi wa eneo hilo na kupunguza uwezekano wa magonjwa hayo.

  “Halmashauri mna jukumu la kuhakikisha mnada huu una miundombinu yote hasa ya maji na vyoo kwakuwa mnakusanya ushuru pia kumbukeni kuhakikisha huduma zinapatikana vizuri mnadani hapa”, ameelekeza Dkt Nchimbi.

  Aidha amewataka Wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na idara za usafi wa mazingira na Wakala wa barabara vijijini (TARURA) wanahakiki njia na mitaro ya kupitisha maji ili mvua zisilete maafa pamoja na kuhakiki mabwawa ili baada ya mvua kuisha waweze kuvuna maji ya kutosha.

  Dkt Nchimbi ameeleza kuwa mvua za msimu uliopita zilileta maafa ya kipindupindu hivyo hatarajii kwa mvua za msimu huu kuleta tena magonjwa kwakuwa wakurugenzi wametahadharishwa mapema uwepo wa mvua za wastani na juu ya wastani.

  Ameongeza kwa kuwashauri wananchi kuimarisha makazi yao ili yaweze kuhimili mvua hizo pamoja na kujenga vyoo bora ili wasipate magonjwa hasa kipindupindu.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba Marietha Kasongo amesema amelipokea agizo hilo na kuongeza kuwa mwezi mmoja unatosha kujenga vyoo hivyo na kufikisha huduma za maji mnadani hapo.

  Amesema halmashauri ilikuwa na mpango wa kujenga vyoo na kuvuta maji mnadani hapo hivyo agizo la Mkuu wa Mkoa limewaamsha ili waweze kutekeleza mipango yao kwa haraka zaidi.

  Awali Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imetangaza kuwa Mkoa wa Singida unatarajiwa kupata mvua za wastani na juu ya wastani, aidha wastani wa mvua kwa Mkoa wa Singida ulikuwa ni Milimita 500 mpaka 850.

  0 0

   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.
   Wananchi wa Butimba na Mkuyuni wakifurahi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria molders and polybags kilichopo Igogo jijini Mwanza.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mafundi wa Kiwanda cha Victoria molders and polybags mara baada ya kutengeneza Tanki la kuhifadhia maji.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia utengenezaji wa viti vya plastiki katika kiwanda cha Victoria molders and polybags katika eneo la Igogo jijini Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfuniko uliotengenezwa katika kiwanda hicho cha Victoria molders and polybags Igogo jijini Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya ya jiji la Mwanza James Bwire mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria molders and polybags Igogo jijini Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha madawa cha  Prince Pharmaceuticals kilichopo Buhongwa nje kidogo jijini Mwanza. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Yeremias  Ngerangera, Namtumbo

  Athmani  Amani  mkazi wa kijiji  cha Naikesi  kata ya kitanda  wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma  anawaomba  watanzania  kumsaidia  fedha  za kugharimia  matibabu  ya mtoto  wake  Shaziri  Athmani (12) anayesumbuliwa  na tatizo  la moyo kuwa  mkubwa.

  Mtoto  Shaziri  Athamani  ni mwanafunzi  wa darasa  la nne  shule  ya msingi Naikesi  iliyopo  kata ya Kitanda  wilayani Namtumbo  awali  alikuwa anasumbuliwa  na kuvimba  miguu  hali iliyokuwa  inamkosesha  masomo  yake  darasani  mara kwa  mara kuanzia  mwaka  2016.
  Mwaka  huo  huo  mwezi  Septemba  baba yake  alilazimika kumpeleka  Hospitali  ya Mkoa  Songea  kuangalia tatizo  la kuvimba  kwa  miguu  ya mtoto huyo  na  baada ya kupata  vipimo  wakashauriwa  kuenda  Hospitali  ya  Peramiho  .

  Bwana  Athamani  alidai  kuwa  hakuwa  na fedha  za kumpeleka  mtoto  peramiho  kwa  kipindi  hicho  na badala yake  alirudi  naye  nyumbani  Naikesi  kwenda  kuuza  mifugo  lakini fedha hizo  hazikumwezesha  kukidhi  mahitaji  ya  kumtibu  mwanoa katika  Hospitali  ya  Peramiho  baada  ya  kufika  katika  Hospitali  hiyo  na kumaliza  fedha  yake  yote  aliyokuwa  nayo  katika  vipimo  pekee .

  Baada  ya kupatiwa  vipimo  na  kubaini  Tatizo la  mwanae  alirudi  na mwanae  mpaka  kijijini  kwake  kujipanga  upya  kwa  ajili  ya  matibabu ya  mwanae  na  kujitahidi  kwa kile  anachokipata  anunue  dawa  kwa  ajili  ya  mwanae  huyo.

  Pamoja  na  jitihada  hizo  hali ikaendelea kuwa  sio  nzuri  na ndipo  alipolazimika kufanya  kazi  za  kulima  mashamba  ya watu  ili apate  fedha  za kumtibu  kijana wake  na  mwaka  huu  mwezi  oktoba  alimpeleka  kijana wake  huyo  peramiho  na  baada  ya  kufika  peramiho  na kupatiwa  vipimo  alishauriwa  na  madaktari  kumpeleka  mtoto  huyo  Hospitali  ya  Muhimbili Dar es Salaam.

  Hata  hivyo  mzazi  huyo  alifika  katika  ofisi  ya  Katibu  tawala  wa wilaya  ya  Namtuimbo  na kufanya  mazungumzo  na  Kaimu  katibu  tawala  wa wilaya  ya Namtumbo   Alkwin  Ndimbo  kwa  lengo  la  kupatiwa  msaada  wa matibabu  wa  kijana  wake  huyo.

  Alkwin  alidai kuwa  kuna  sababu  ya  watanzania  wenye  moyo  kumsaidia  mtoto  huyo  kwa  michango  yao  ili  mzazi  wa kijana  huyo  aweze kumpeleka  kijana  wake  huyo  Hospitali ya Taifa  Muhimbili  na  bila  michango  kutoka  kwa  watanzania wenye  moyo  mzazi huyo  hana uwezo  wa  kumpeleka  kijana wake huyo  Hospitali  ya Taifa Muhimbili.

  Kwa  watanzania  wenye  moyo  wa  kumsaidia  mtoto  huyo  wanaweza  kumpigia  mzazi wake  kupitia  namba  0629629872  au  unaweza  kumtumia  fedha  kupitia  namba  hiyo  ambapo  kwa  sasa  mzazi huyo  amerudi  kijijini  kwake  Naikesi  akiwa  na  mgonjwa  wake  akihangaika  kupata fedha  za  kumpeleka  mtoto wake huyo  Hospitali  ya Taifa  Muhimbili.

  0 0

    Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi. Sihaba Nkinga akiwashukuru wadau wa masuala ya watoto wakati wa kikao na wadau hao kutoka Shirika la JSI kujadili Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa Kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Mwongozo wa Kitaifa wa Utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma.
   Afisa Ustawi wa Jamii, Dkt. Philibert Kawemame akiwasilisha  kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(wanne kushoto) Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa Kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Mwongozo wa Kitaifa waUtambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma.
   Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kulia) kuhusu Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Mwongozo wa Kitaifa wa Utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma.
   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akichangia jambo kuhusu Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Mwongozo wa Kitaifa wa Utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma.
   Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodatha Makani akichangia jambo kuhusu Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Muongozo wa Kitaifa wa Utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma.
   Mkaguzi wa Ndani  kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Elightness Mchome akichangia jambo kuhusu Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Mwongozo wa Kitaifa wa Utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma.
   Mwakilishi wa Shirika la JSI Bw. John Stephen akimshukuru Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kushoto) mara baada ya majadiliano kuhusu Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Mwongozo wa Kitaifa wa Utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma.
   Baadhi ya watendaji wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia kikao cha majadiliano kuhusu Rasimu ya Mfumo Jumuishi wa kitaifa wa Usimamizi wa Mashauri ya Watoto na Mwongozo wa Kitaifa wa Utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Wizara ulipo UDOM Dodoma. 

  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. WAMJW

  0 0

  Prof. Idris Rai (standing), the Vice Chancellor gives welcome remarks to new students

   Prof. Idris Rai, the SUZA Vice Chancellor informed the new students that SUZA tends to put students at the centre of everything it does so their experience at SUZA and their success is important to each and every SUZA community member. “Your arrival here marks a new chapter in the history of your life so do utilize to the maximum the opportunities built in your programmes at the University”, he added.

  He informed the new candidates that Zanzibar in the past was the fulcrum of various disciplines of education for Eastern Africa region and now the State University of Zanzibar intends to reclaim this seemingly lost status through the candidates it admits by imparting to them the appropriate skills and knowledge.

  Prof. Rai advised students to be more self-reliant as they will be responsible for what they do and that they will have to ensure that they do the work required for them to do. “There will be no one to check up on you, you are matured enough and accountable to yourself., make sure you attend your lectures, labs and tutorials, do the assignments and read the material advised by your lecturers and tutors also ensure that you make enough time for private study; develop a study plan; go to the library and use the on-line learning resources which are fortunately accessible at SUZA”, he insisted.
  A cross-section of the newly admitted students for 2017/2018 academic year pay attention listening to instructions from the SUZA Management Team.

  He then enlightened the new students that some of them who will manage to come out with flying colours in their studies may have the opportunities to pursue collaborative education abroad through partnerships which SUZA has engaged in with other higher learning institutions which enable SUZA students to spend at least one semester abroad.

  The Vice Chancellor updated students to realize that they are not alone and therefore if they find things difficult they do not have to run away, instead they have to seek help from the university management through the Dean of Students who is a good advisor  and is here for this purpose. He wished all the admitted students every success at the State University of Zanzibar and declared his confidence on them that they will find it an enormously rewarding experience.

  Meanwhile, Dr. Haji Mwevura Haji, the Deputy Vice Chancellor – Academics, Research and Consultancy congratulated the new students for having secured their university place and for having the good sense to choose to study in the State University of Zanzibar. He told them that there were so many applicants in all over fifty academic programmes of different levels existing at SUZA and the majority of them have met entry qualifications but due to limited chances only a few have been selected so the selected ones should not squander the chances they acquired.

  Dr. Mwevura drew the candidates’ attention that by being here they will have the opportunity to learn new things, acquire new knowledge, develop new skills and enhance their personal attributes in profound ways that will equip them for life after university. “The great thing is that you are doing something that you have chosen to do, not something that was chosen for you by others so you have to work hard to achieve your goal”, the DVC Academics continued to remind them.

  Earlier when welcoming the new students and giving her words of advice Ms. Salha Khalfan Khamis, the Dean of Students requested them to continue preserving the university environments of all campuses which are currently in nice-looking situation, she also urged them to comply with all  SUZA Students’ By-laws for the betterment of their existence in the university. 

  Over 2,000 new students have been enrolled in various programmes for 2017/2018 academic year at the State University of Zanzibar; these will be allocated in Tunguu, Chwaka, Maruhubi, Mbweni, Nkrumah and Vuga Campuses depending on their areas of studies. Classes for them and the continuing students will commence on Monday 6th November, 2017.

  0 0

  Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta kuu za matumizi ya Ardhi na Asasi za Kiraia wamekutana kwa ajili kuendelea kurejea Mwongozo wa ushirikishaji katika kupanga mipango ya matumizi ya Ardhi pamoja na kukamilisha kazi ya rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto zinazoikabili mipango ya matumizi ya ardhi ikiwemo kuutafsiri kwa lugha ya kiswahili.
   Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi, pamoja na kupongeza kazi nzuri ambayo inafanywa na kikosi kazi, lakini pia lizungumzia swala la mipango miji,upangaji wa mipango bora ya matumizi ya ardhi utakaozingatia mtazamo wa kuipeleka nchi katika Dira ya viwanda na pamoja na swala la mabadiliko ya Tabianchi, ili wananchi wawe tayari kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabianchi kunatakiwa kuwe na mipango mizuri ya matumizi ya ardhi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu, Sera na Mawasiliano wa TumeBi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi kazi ya kikosi kazi ya kukamilisha andiko la Mkakati wa changamoto za mato za matumizi ya Ardhi ikiwa ni pamoja na kuandaa mwongozo na kubadili andiko kwa lugha ya kingeleza ili lipate kusomwa na wafadhiri pia wadau wengine.
  Afisa Mipango kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald Mwakipesile (wa kwanza kulia) akiwapitisha kikozi kazi katika maeneo mbalimbali ya kukamilisha mkakati wa kutatua changamoto za matumizi ya Ardhi nchini.
  Afisa Tawala wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bi. Nakivona Rajabu akitoa mrejesho wa kikao kilichofanyika na Mh. William Lukuvi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokuwa anakabidhiwa Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi cha tarehe 14.08.2017 mjini Morogoro.
  Wanakikosi kazi wakiwa wanafuatilia mrejesho huo
  Wanakikosi kazi wakiwa katika makundi kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja kulibadili andiko la mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi kwa lugha ya kingeleza ili uweze kuja kusomwa na wafadhiri pamoja na wadau wengine mbalimbali.

  Bw. Paulo Tarimo  kutoka Wizara ya Kilimo akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
  Bw. Emmanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, akitoa maoni yake wakati wa mkutano huo.
  Bwana Daniel Ouma(kushoto) Afisa Miradi kutoka TNRF akichangia jambo wakati kikosi kazi kikiendelea na kazi.
  Bw. Mbaraka Stambuli kiongozi wa Kipengele cha maendeleo ya kisera na kitaasisi katika programu ya kuwezesha umilikishwaji wa Ardhi, akichangia jambo la maboresho wakati wa kubadilisha andiko katika lugha ya kingeleza.
  Bwana Herman Nyanda Afisa wanyama pori (TAWA) mwandamizi katika dawati la ushirikishwaji jamii katika uhifadhi wa wanyama pori akichangia hoja wakati shughuli ya kubadilisha andiko katika lugha ya kingeleza inaendela
  Kikosi kazi wakiendelea na kazi


  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mbele), akitoka kuangalia ukarabati wa meli ya Mv.  Clarius, katika Bandari ya Mwanza, leo. Meli hiyo inatoa huduma katika visiwa vilivyo kwenye ziwa Victoria.
   Muonekano wa Meli ya Mv. Umoja yenye uwezo wa kubeba behewa 22. Meli hiyo inasafirisha mizigo kutoka Bandari ya Mwanza kuelekea Bandari ya “Port Bell” Uganda.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa nne kulia), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, alipofika Bandari ya Mwanza leo kujionea maendeleo ya ukarabati wa meli ya MV. Clarias katika Bandari hiyo.
   Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kushoto mbele) wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa meli katika Bandari ya Mwanza, leo.
   Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia), hatua zilizofikiwa za ukarabati wa meli ya Mv. Clarius na Mv. Umoja katika Bandari ya Mwanza.
  Mafundi wakiendelea na ukarabati wa meli ya Mv. Clarius leo katika Bandari ya Mwanza. Kukamilika kwa ukarabati wa Meli hiyo inayotoa huduma katika visiwa vilivyo katika ziwa Victoria kutarudisha huduma za usafirishaji na abiria katika visiwa hivyo.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na yakisasa itakayotoa huduma za usafirishaji katika  Ziwa Victoria.

  Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Profesa Mbarawa, amewataka wafanyakazi wa Kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili kazi hiyo ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.

  “Mkandarasi ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki wa kimahesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na muda mfupi”, amesema Profesa Mbarawa.Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa, amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya Mv. Clarias na Mv. Umoja ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa, na hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Bandari  ya “Port Bell”, nchini Uganda.

  “Kukamilika kwa meli kuwiane na kasi ya kutafuta mzigo mwingi ili meli hizi zifanye biashara wakati wote na kuhakikisha Kampuni yenu inapata mapato mengi yatakayowawezesha kujiendesha kwa faida”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

  Naye, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi, amemhakikishia Profesa Mbarawa, kuwa wamejipanga kufanya ukarabati mkubwa wa meli za Mv. Victoria, Butiama na Liemba ili kuziwezesha meli hizo kufanya kazi katika ubora wake wa awali na kupunguza tatizo la usafiri katika ziwa Victoria na Tanganyika.

  “Tumeweka mkakati wa kuhakikisha tunazikarabati meli zetu zote ili ziwe katika ubora unaostahili wakati wote”, amefafanua Bw. Hamissi.
  Katika kuhakikisha maendeleo ya kibiashara na kuichumi  yanafikiwa katika Ukanda wa maziwa makuu  nchini, Serikali imejipanga kuhakikisha inafufua usafiri wa meli za abiri na mizigo katika ukanda huo.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

older | 1 | .... | 1412 | 1413 | (Page 1414) | 1415 | 1416 | .... | 1903 | newer