Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

WANAHABARI WA TANZANIA WATEMBELEA KAMPUNI YA HUWAWEI NCHINI CHINA

$
0
0
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, wakiwa ndani ya Kiwanda cha Kampuni ya  Huwawei walipotembelea Kiwanda hicho kuijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
 Wanahabari wakiwa katika kiwanda hicho.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja  Shenzhen nchini China, walipokwenda kutembelea kampuni ya Huwawei na kuijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikwemo utekelezaji wa mradi wa elimu wa Smart Education na e-Education unaotekelezwa katika shule ya msingi Baogang iliyopo nchini humona hivyo kukabiliana na tatizo la uhaba walimu.mpango huo pia wanatarajia kuuleta hapa nchini ili kuweza kuboresha sekta ya elimu.

SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na Viongozi na watumishi wengine wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera (hawapo pichani) alipotembelea ofisi hizo kuhusu kuhakikisha Taasisi zote za Serikali zinapata huduma kutoka Wakala huo, alipofanya ziara katika Mkoa huo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maagizo kwa Kaimu Meneja  wa Wakala Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi, kuhusu kuwahudumia Taasisi zote za Serikali kwa kuwa ndio wajibu wa Wakala huo, alipofanya Ziara katika Ofisi hizo za Mkoani Kagera.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akielezea namna atakavyoshirikiana na Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini katika Mkoa huo ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi adili ya fedha za Serikali, Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea Ofisi za Wakala huo Mkoani Kagera.
 Kaimu Meneja wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) namna tetemeko la ardhi lilivyo haribu miundombinu ya Ofisi hizo, alipotembelewa na Naibu Waziri huyo katika Ofisi za GPSA Mkoani humo.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba  Bw. Deodatus Kinawiro (kulia) akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) alipotembelea Ghala la Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoani Kagera.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akitembelea maeneo ya Ofisi za Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) ambapo aliweza kupata maelezo namna  Wakala huo unavyofanya kazi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa nne kushoto), Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro (wa tano kulia), Kaimu Meneja wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi  Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi (wa tatu kushoto) na watumishi wengine wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa ziara ya Naibu Waziri huyo katika Ofisi hizo Mkoani Kagera.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Benny Mwaipaja, Kagera.

NAIBU waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameziagiza Mamlaka na Taasisi zote za Umma kufanya ununuzi wa vifaa na mafuta kupitia Wakala wa Serikali wa ununuzi na ugavi (GPSA) kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge na kuwaonya wahusika wote watakaoendelea kukaidi maagizo hayo kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo mkoani Kagera baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoani humo na kubaini kuwa taasii na idara nyingi za umma zinafanya manunuzi nje ya mfumo wa GPSA jambo ambalo amesema ni ukiukwaji mkubwa wa sheria.

Alisema kuwa lengo la Serikali la kuanzishwa kwa wakala huo pamoja na mambo mengine ilikuwa kudhibiti matumizi ya Serikali na kuonya kuwa Serikali haitakubali kuona sheria zinakiukwa kwa makusudi na kwa malengo yanayoonesha kuna nia isiyo njema katika matumizi ya fedha za umma.

“Hili si ombi ni maelekezo na ni agizo, taasisi zote zipate huduma kutoka kwa wakala wetu (GPSA) kwani Serikali ilikuwa na dhamira ya uwepo wa matumizi sahihi ya fedha za matumizi wanazopelekewa na ndiyo maana ukaanzishwa Wakala huu” Alisema Dkt. Kijaji

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro, akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, aliiagiza Wakala wa Ununuzi na Ugavi (GPSA) mkoani humo kumpelekea orodha ya taasisi ambazo hazitumii huduma za wakala huo ili aweze kuchukua hatua.

Alisema kuwa ni jambo lisilofaa kwa Taasisi za Umma kukiuka sheria na kwamba watatekeleza maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango haraka ili kuokoa fedha za Serikali na kuweka uwajibikaji.

Awali, Kaimu Mkuu wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoa wa Kagera Bi. Dorothea Bugenyi alieleza kuwa katika kipindi cha miaka 3 iliyopita Wakala huo umeongeza makusanyo yatokanayo na mauzo ya vifaa na mafuta kutoka Shilingi bilioni 1.9 hadi kufikia Shilingi bilioni 2.34.

Alisema kuwa mapato hayo yangekuwa makubwa zaidi endapo taasisi zote za umma zingetii sheria na kufanya manunuzi yao ya vifaa na mafuta kutoka kwa Wakala huo na kuiomba Serikali kuusaidia Wakala huo kuziagiza taasisi zake za umma kutekeleza sheria hiyo kwa vitendo.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA IRELAND

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajli ya Diaspora na Maendeleo ya Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon aliyeambatana na Balozi wa Ireland nchini Tanzania.

Katika mazungumzo yao walitilia mkazo katika masuala ya Biashara na uwekezaji hasa ikizingatiwa kwamba nchi zote mbili mazingira yake yanaruhusu .

Makamu wa Rais alimuambia Waziri huyo Tanzania ni nchi nzuri na rafiki kwa kuwekeza hivyo wanakaribishwa kuwekeza hasa katika viwanda na teknolojia, Waziri huyo alieleza kuridhishwa kwake  na jitihada za Tanzania katika kusimamia uchumi wake kwa ujumla.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alielezea vifo vya wakina mama kabla na wakati wa kujifungua na watoto wachanga na kuiomba Serikali ya Ireland kupitia Waziri huyo kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo hilo, ambapo waziri huyo alioneshwa kuguswa sana hasa pale Makamu wa Rais alipoelezea uzoefu wake mwenyewe aliowahi kukutana nao wakati anajifungua mtoto wake wa tatu.

Makamu wa Rais na Waziri huyo kutoka Ireland kwa pamoja walikubaliana katika suala zima la kuboresha elimu, mafunzo  na kubadilishana ujuzi hasa katika masuala ya Afya, Teknolojia na Anga.Mwisho Makamu wa Rais alisema Ushirikiano wa nchi mbili hizi ni wakudumu na kuiomba Serikali ya Ireland kuendelea kushirikiana na kusaidia Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajili ya Diaspora na Maendeleo Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam akiongozana na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada la Irish Ndugu Ruairi De Burca's. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajili ya Diaspora na Maendeleo Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

DKT. KALEMANI NA WAZIRI WA MAFUTA NA GESI OMAN WAJADILI VIPAUMBELE VYA USHIRIKIANO NISHATI.

$
0
0
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tano kulia),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa pili kushoto), Balozi Mteule wa Oman hapa nchini, Ali Al Mahruqi (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa Tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa pili kulia).
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa nne kushoto),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Nne kulia) wakiwa katika Ofisi ya  Waziri wa Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa tatu kulia), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa pili kulia), Balozi Mteule wa Oman hapa nchini, Ali Al Mahruqi (wa kwanza kulia). Wengine ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kushoto), na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa kwanza kushoto).
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tano kulia),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Tatu kushoto)  wakiagana mara baada ya kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa kwanza kushoto),  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa Tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa pili kulia).

Na Teresia Mhagama, DSM.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi wamekutana  jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano lengo likiwa ni kuendeleza Sekta ya Nishati nchini.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo Waziri huyo kutoka Oman aliambatana na Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Naibu Waziri wa Utalii na Balozi wa Oman nchini Tanzania.
Kwa upande wa Tanzania, viongozi mbalimbali walishiriki katika majadiliano hayo akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo na watendaji wengine kutoka Idara ya Nishati na Sheria.

Kwa upande wake Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Rumhi, alisema kuwa lengo la Ujumbe huo kufika wizarani ni kujadiliana na watendaji wa Wizara ya Nishati kuhusu maeneo ambayo ingependa ishirikiane na nchi hiyo ya Oman na kwamba nchi hiyo ipo tayari kushirikiana  na Tanzania.

“ Hapo zamani, Sisi Oman hatukutumia Gesi yetu vizuri kwa kuwa tulifanya haraka kuiuza nje ya nchi lakini ninyi mnayo fursa sasa ya kuitumia gesi yenu ndani ya nchi ili kutengeneza ajira pamoja na kuiendeleza kwa matumizi mbalimbali, na ikiwa ziko fursa za ushirikiano ili kuendeleza nishati hii, sisi tupo tayari,” alisema Dkt. Rumhi.

Akizungumzia uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Oman, Dkt. Rumhi  alisema kuwa, nchi hiyo inauthamini undugu uliopo na kwamba watalizingatia hilo katika kutekeleza miradi ya ushirikiano  ambayo itahusisha wasomi watanzania ambao wameonyesha kuwa na  uwezo wa kuendeleza Sekta  ya Nishati.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt Kalemani,  alisema kuwa Tanzania imegundua Gesi Asilia kiasi cha futi za ujazo trilioni 57.25 huku matumizi yakiwa ni chini ya asilimia 30 hivyo bado kuna Gesi ya kutosha kwa ajili ya miradi mipya ya  uzalishaji Umeme na katika kuanzisha viwanda kama vya kemikali na mbolea.

Alisema kuwa kwa sasa Umeme unaotumika nchini, unazalishwa kwa kutumia Gesi Asilia kwa zaidi ya asilimia 50 na kueleza kuwa, Serikali inahitaji kuzalisha Umeme mwingi zaidi kwa kutumia Gesi hiyo.

“ Pamoja na hayo kwa leo napenda kuomba mambo manne ya ushirikiano ambayo yatawafaidisha watanzania. Jambo la kwanza ni kuendeleza ushirikiano katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na Bonde la Eyasi Wembere ambayo katika tafiti za awali yameonesha kuwa na viashiria vya mafuta, hivyo ni muhimu kushirikiana katika tafiti zinazofuta na hatimaye kuthibitisha endapo maeneo hayo yana mafuta kama viashiria vinavyoonesha,”  alisema Dkt Kalemani.

Alitaja eneo la Pili ambalo Tanzania inahitaji ushirikiano ni  kujenga uwezo wa Wataalam ikiwemo utoaji wa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa kuwa Tanzania bado inakua katika Sekta ya mafuta na Gesi hivyo ni muhimu kwa Tanzania kuwa na wataalam wengi zaidi.

 Alitaja jambo la Tatu la ushirikiano kuwa ni uzalishaji Umeme kwa kutumia Gesi asilia jambo litakalopelekea gharama za nishati hiyo kupungua kwa wateja  na vilevile kuongeza kiasi cha Umeme nchini tofauti na megawati 1451 zilizopo sasa kwani lengo ni kufikia megawati 5000 ifikapo mwaka 2020 na megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

“Jambo la Nne, ni nchi ya Oman kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania katika mradi wa usambazaji Gesi majumbani, viwandani na kwenye magari jambo litakalopelekea ajira kwa wananchi wetu, kutunza mazingira na kuongeza idadi ya viwanda nchini ikiwemo kiwanda mnachotarajia kujenga hapa nchini,” alisema Dkt Kalemani.

Alisema kuwa kwa sasa mradi wa majaribio ya usambazaji Gesi majumbani umeshaanza, ambapo nyumba 70 zimesambaziwa Gesi hiyo jijini Dar es Salaam huku lengo likiwa ni kuendelea  kusambaza Gesi hiyo jijini Dar es Salaam,  Lindi,  Mtwara na kisha katika mikoa mingine nchini.

Naye Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alishukuru Ujumbe wa Oman kwa kuitembelea Wizara ya Nishati na Ujumbe huo kutoa matumaini katika kuyafanyia kazi maombi ya Waziri wa Nishati na kwamba ana imani undugu baina ya pande hizo mbili utaendelezwa hasa katika kuendeleza miradi ya Nishati nchini.

WAZIRI MKUCHIKA: TOFAUTI KUBWA YA MISHAHARA SERIKALINI KUKOMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Watumishi wa TaGLA mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipata maelezo kuhusu mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi wakati wa mikutano ya kieletroniki (Video Conference) katika ofisi za TaGLA wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea taarifa (nakala ngumu na laini) zenye shughuli zinazofanywa na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw. Charles Senkondo baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokewa na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipofanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi katika ofisi za Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald Ndagula akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya Waziri kumaliza kuzungumza na watumishi wa bodi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijionea utunzaji wa kumbukumbu alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Idara ya Kumbumbuku na Nyaraka za Taifa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea nyaraka mbalimbali zinazohusu utunzaji wa kumbukumbu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Charles Magaya katika ofisi za Idara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

 Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo akieleza kuhusu utendaji wa taasisi anayoiongoza wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa kutoka Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) akiwasilisha mada kuhusu kazi na mafanikio ya wakala wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika wakala hiyo mapema leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifuatilia mada iliyowasilishwa kuhusu kazi na mafanikio ya TaGLA alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan P. Mlawi, na Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TaGLA, Bw. Charles Senkondo.





Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeagizwa kufanya utafiti wa kina utakaowezesha kuwa na uwiano sawa wa malipo ya mishahara na masilahi ya watumishi wote serikalini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mkuchika amesema kuna baadhi ya taasisi/Idara za Serikali zinalipa watumishi wake mishahara mikubwa tofauti na taasisi nyingine jambo ambalo limekuwa likisababisha watumishi kutotulia sehemu moja na kutafuta masilahi bora zaidi sehemu nyingine.

“Hii haiwezekani, mmesoma darasa moja, fani moja na mko cheo kimoja, lakini mnalipwa mishahara tofauti wakati serikali ni moja, ni lazima mlifanyie utafiti wa kina suala hili. Masilahi ya watumishi wa umma lazima yawe sawa” Waziri

Mkuchika amesisitiza na kuongeza kuwa kumekuwa na malalamiko mengi serikalini kuhusu tofauti kubwa ya mishahara miongoni mwa watumishi wa Serikali Kuu na baadhi ya taasisi za serikali.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka watumishi wa Bodi hiyo kuwa wabunifu na kupendekeza mambo ambayo yatawavutia Watumishi wa Umma kufanya kazi Serikalini kwa dhati kwa kuzingatia taaluma zao na mgawanyo wa majukumu. “ Kila mtumishi ana taaluma yake na mgawanyo wa majukumu aliyopewa wakati anaanza kazi, hivyo ni vema kila mtu akazingatia hayo ili kuwa na utendaji bora serikalini,” Mhe. Mkuchika amesema.

Mhe. Mkuchika, ameendelea na ziara ya kikazi ya kujitambulisha na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake, ambapo leo ametembelea Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ni matokeo ya Tume ya Rais ya Malipo ya Mishahara ya mwaka 2006 iliyopewa jukumu la kuishauri Serikali namna ya kuboresha malipo ya mishahara na motisha nyingine katika Utumishi wa Umma.

TRUMARK WAPATA MAFUNZO YA KUBORESHA UFANISI TOKA SHIRIKA LA PUM KUTOKA NCHI YA NETHERLANDS

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akimshukuru Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka  nchi ya Netherlands,  Paulus Joseph Maria Jaspers wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 Washiriki wa mafunzo hayo kutoka Trumark wakiwa katika majadiliano. Kutoka kulia ni Meneja wa Idara ya Biashara na Masoko wa Kampuni hiyo, Grace Sikazwe, Mratibu wa Miradi, Gwamaka Mwakijengele na  Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini, Ismail Omcoi.
 Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka  nchi ya Netherlands,  Paulus Joseph Maria Jaspers akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo wakati wa mafunzo hayo. Wengine ni maofisa wa kampuni ya Trumark.
Maofisa wa Kampuni ya Trumark wakiwa kwenye mafunzo hayo. Kutoka kulia ni MaryRose Mphuru, Adam Musoni na Msusa Geuzye.


Picha ya pamoja.

 Mkufunzi akipongezwa.
 Mtaalamu wa Idara ya picha wa kampuni hiyo, Juma Diwani akiwa kwenye mafunzo hayo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Trumark imepata mafunzo ya kuboresha ufanisi wa kazi kutoka Shirika la PUM-Netherlands Senior Exparts.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwakilishi wa Shirika hilo, Deogratias Mbona alisema mafunzo hayo yanatoa fursa kwa walengwa kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo biashara.

"Mafunzo haya yanatolewa katika nchi 31 duniani na yameweza kuyanufaisha makundi mbalimbali ya jamii hasa vijana" alisema Mbona.

Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa kujitolea na yamelenga kuwawezesha vijana katika biashara, kilimo, uzalishaji viwandani na utoaji wa maarifa kutoka kwa wakufunzi wa shirika hilo waliobobea katika masuala hayo.

Kwa Kampuni ya Trumark ambayo imetoa maofisa wake 10 kushirika mafunzo hayo wao watanufaika na uboreshaji wa miradi na kupanua masoko pamoja na kukutanishwa na wadau wengine wa mataifa mbalimbali na kubadilishana nao uzoefu.

MKURUGENZI WA ILEJE ATEMBELEA KILWA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai kulia akisalimiana na mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Haji Mnasi ,mara baada ya Mkurugenzi huyo kufika ofisini kwake jana kwaajili ya kumsalimu kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Zabron Bugingo(Picha na Pamela Mollel Kilwa)
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai kulia akisalimiana na mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Zablon Bugingo katikatimkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe

TAARIFA YA KUONGEZA MUDA WA UTOAJI WA LESENI ZA MACHAPISHO MBALIMBALI NCHINI


ZIMAMOTO WAKONGA NYOYO ZA WANANCHI MAONESHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Sajini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji toka Makao Makuu, Damian Muheya (Kulia), akiwaelimisha wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jinsi vizimia moto vya awali (Fire Extinguisher) vinavyotumika pindi moto unapotokea, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
 Wananchi wa Mjini Kilimanjaro wakiwa katika banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakipata elimu juu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwenye vyombo vya Usafiri na Usafirishaji, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”.
 Wananchi wa Mjini Kilimanjaro wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kitengo cha Maokozi Saidi Seng’endo (Kushoto) walipotembelea banda hilo, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. 
 Picha ni sehemu ya mabanda ya washiriki mbalimbali wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”.
 Picha watoto wakimsikiliza Konstebo Saidi Seng’endo juu ya matumizi ya kifaa kinachohifadhi hewa safi (Breathing Apparatus) kwa ajili ya kumsaidizi Askari wa Zimamoto kwenye matukio mbalimbali.
Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi toka Makao Makuu, Saidi Seng’endo (Kushoto), akiwa na Konstebo wa Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Simba Mikidadi (Kulia), wakiwaonesha wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jinsi baadhi ya vifaa vya gari maalum la maokozi  (Fire Rescue Tender) vinavyotumika pindi ajali inapotokea barabarani, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu, tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

RC APIGA MARUFUKU UTOAJI WA LESENI ZA UCHIMBAJI WA MADINI AMANI MUHEZA

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jumuiya Tatu za Zigi Juu,Zigi Chini na Kuhuhwi zilizopo kwenye Bonde la Mto Pangani katika eneo Amani wilayani Muheza na mradi wa maji mserereko kwa ajili ya vijiji vya Mashewa,Kimbo na Shembekeza

MKUU wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel


MKUU wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza katika uzinduzi huo
Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP ambao wamefadhili mradi huo akizuungumza katika uzinduzi huo
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza akizungumza katika uzinduzi huo Jumanne Omari
Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi kushoto akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi kushoto akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na uchimbaji haramu wa madini katika eneo la Hifadhi ya Amani wilayani Muheza
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akitembelea maeneo hayo kujionea athari ambazo zimetokana na uchimbaji haramu wa madini kwenye eneo la vyanzo vya Maji Amani na Hifadhi ya Msitu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jumuiya ya watumiaji wa Maji na Mradi wa Maji Mserereko kwa vijiji vya Masheww,Kimbo na Shembekeza wilayani Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akizundua mradi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo anayeshuhudia mwenye kilembe cheusi kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Mhandisi Zena Saidi




Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akimtwisha ndoo mkazi wa eneo hilo kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa kwanza kulia ni Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga,Mhandisi Laurian Rwebembeza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said

Sehemu za wananchi wakishuhudia uzinduzi huo


MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ameitaka wizara ya Madini kuacha kuendelea kutoa leseni za uchimbaji wa madini eneo hifadhi ya Amani wilayani Muheza huku wakitaka zilizotolewa kufutwa kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea kwenye eneo hilo.

Kwani uchimbaji huo umekuwa na madhara makubwa kuharibu mazingira kutokana na kutumia kemikali ambazo huingia kwenye maji na hivyo kuleta adhari kubwa kwa binadamu ambayo huyatumia kwa matumizi mbalimbali.

Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Jumuiya za watumiaji maji Bonde Dogo la Mto Zigi katika Uzinduzi wa Jumuiya tatu za Zigi Juu,Zigi Chini na Kihuhwi zilizopo Bonde la Pangani.Mradi huo wa Maji wa Mserereko ulihusisha vijiji vya Mashewa,Kimbo na Shembekeza wilayani Muheza Mkoani Tanga.

Alisema pia licha ya kupiga marufuku hiyo lakini watahakikisha wanawachukulia hatua watumishi watakaoshirikiana na wachimbaji kwa kuwakamata na kuwapeleka kwenye vyombo vya dola ili kuweza kukomesha tatizo hilo.

“Labda nisema tu sisi kama mkoa tumepiga marufuku uchimbaji wa madini katika eneo hili la Amani lakini pia tunaitaka Wizara ya Nishati wasiendelea kutoa leseni za madinina mtu atakayekwenda kuchukua leseni hela yake itakuwa imeibiwa”Alisema

“Lakini pia niseme pia kwa wale ambao leseni wamepewa zifutwe kwani kuendeleza uchimbaji huo kunaweza kusababisha madhara makubwa sana kwa uharibifu wa mazingira “Alisema.Alisema iwapo uharibifu huo utaendelea utasababisha hata upatikanaji wa maji kutokuwa mzuri hasa ukizingatia uwepo wa mahitaji muhimu ya maji kuongezeka kutokana na mradi wa bomba la mafuta watu watashindwa kupata maji.

“Natambua kuwepo kwa wawakilishi kutoka shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa la (UNDP) na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) ambao wanafadhili mradi wa usimamizi wa pamoja na rasilimali za maji kupitia usimamizi endelevu wa matumizi bora ya ardhi katika mabonde madogo ya mito Ruvu na Zigi”Alisema.

Alisema changamoto za kupungua kwa maji unazidi kuongezeka na kuathiri shughuli za kiuchumi ikiwemo za kijamii hususani za uzalishaji wa chakula,viwanda,umeme na kulinda bayoanuai.

“Upungufu huu huchangia na sababu mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi na shughuli za kibinadamu zinazoongezeka siku hadi siku hasa za uchimbaji wa madini,ukataji ovyo wa misitu “Alisema.Naye Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi alisema utalii ikolojia umekuwa ukikua kila ambapo kwa mwaka 2007 /2008 watalii walishuka na kufikia 320 na kupanda mpaka mwaka jana 685 ambo ni watalii ambao wana mchango mkubwa kuileta mapato nchi.

Alisema pia kuanzishwa kwa miradi inayo saidia kuzua kasi ya uharibu wa mazingira kwa wananchi kuboresha kipato chao imesaidia kupunguza kwa asilimia kubwa uharibifu wa mazingira.

“Miradi ya ufungaji vipepeo, kilimo cha uyoga ambacho wanashirikiana na Unesco muhoga,karafuu,iliki ufugaji swa samaki,nyuki kwa wadau hao umesaidia kwa asilimia kubwa wananchi waweze kupata kipato “Alisema.
Kwa upande wake,Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga,Mhandisi Laurian Rwebembeza amesema hakuna leseni yoyote itakayotolewa kwa wachimbaji wa madini eneo la Amani wilayani Muheza kutokana na maeneo yao kutengwa kwa
ajili ya uhifadhi.

Licha ya hivyo lakini pia wamefuta leseni 14 za wachimbaji wa madini ikiwemo kutoa tahadhari kwa watakaoendelea na zoezi hili kuacha mara moja kabla hawajakumbana na
mkono wa kisheria.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

HAKUNA MATATA’ YA TUMAINI MSOWOYA KUACHIWA ALBAMU YAKE OCTOBER 29

$
0
0




Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera anatarajia kuwa mgeni rasmi katikauzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tumaini Msowoya, katika ukumbi wa Highland Hall mjini Iringa.

Wageni wengine wa heshima kwenye uzinduzi huo ni Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha Baby Baraka Chuma, wachungaji kutoka makanisa mbalimbali.

Akizungumza na Mwanaspoti, Msowoya alisema tayari albamu hiyo yenye nyimbo nane imeshakamilika.“Naenda Iringa kurudisha shukrani zangu kwao, nataka wajue nipo huku sio tu kwa sababu ya kazi bali huduma ya kuimba niliyoanza ”

Alizitaja nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo kuwa ni Hakuna Matata, Mwamba, Amenitengeneza, Furaha, Mungu Mkuu, Wanawake Jeshi Kubwa, Samehe na Mungu wa Rehema.

“Kazi hii nimeifanya chini ya usimamizi wa JB Production ikisimamiwa na Producer Smart Bilionea Baraka. Ndiye meneja anayesimamia kazi zangu kwa sasa,’ alisema Msowoya.


Wasanii watakaomsindikiza

Meneja wa Msowoya, Smart Bilionea Producer Baraka alisema tayari waimbaji na kwaya mbalimbali kutoka Iringa na Dar es Salaam watamsindikiza kwenye uzinduzihuo.Alizitaja kwaya zizothibitisha kumsindikiza kuwa ni Wakorinto wa Pili kutoka Mufindi, Muhimidini na kwaya ya Vijana kutoka Iringa mjini.

Baadhi ya waimbaji ni Christopher Mwahangila anayetamba na wimbo wa ‘Mungu ni Mungu tu’, Mchekeshaji na mwanamuziki mpya wa Injili Tumaini Martine maarufu kwa jina la Matumaini wa Kiwewe, Christine Mbilinyi, Moses Simkoko, Ritha Komba na Witness Mbise kutoka Dar es Salaam.

Wengine ni Rebecca Baraka, Jesca Msigwa, Ester Mgunda, Rebecca Mwalingo, Dennis Lukosi, Wadi Mbelwa, Peter Mgaya, Rehema Chawe, Twaibu Mgogo, Emma Sanga na Victoria Mwenda kutoka Iringa.

“Waimbaji watakaomsindikiza ni wengi na bado tunaendelea kuwasajili wengine. Bado tupo kwenye mazungumzo na Bahati Bukiku ambaye anaangalia ratiba yake, ikiwa sawa tutakuwa pamoja,”alisema.

Aliwatanzania kupokea kazi ya Msowoya kutokana na ubora wake wa nyimbo zilizobeba ujumbe unaoweza kuisaidia jamii.


Historia


Hakuna Matata ni albamu ya pili ya Msowoya baada ya ile ya kwanza ya Natembea kwa Imani kutofanya vizuri sokoni.

“Bahati mbaya niliitengeneza kutokana na kiwango kidogo hivyo iliishia kabatini, namshukuru Mungu kwa sababu kazi hii ni nzuri na wakazi wa Iringa wameipokea. Naamini itapokelewa kote,”alisema.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OCTOBER 19,2017

Multi Choice Tanzania kuadhimisha miaka 20 ya kuwapo nchini kwa maonesho ya bidhaa zake

$
0
0

Meneja Uhusiano wa Multi Choice Tanzania Johnson Mshana akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na shamra shamra mbalimbali katika siku hiyo ya Kampuni ya Multichoice Tanzania kutimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania.
Meneja Uendeshaji Baraka Shelukindo akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Kampuni ya Multichoice Tanzania kutimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania. Baraka amesema kuwa katika Kusheherekea maadhimisho ya miaka 20, Multichoice imeandaa maonesho ya siku 2 yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia siku ya leo Alhamis tarehe 19/10/2017 na kesho Ijumaa tarehe 20/10/2017 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. "Katika maonesho haya utapata kushuhudia maendeleo ya Teknolojia yetu ya tangu 1997 mpaka sasa na huduma mbali mbali zitolewazo na Multichoice",amesema Baraka.
Mkuu wa Channel ya Africa Bongo Magic Barbara Kambogi akifafanua zaidi kuhusiana na hafla hiyo,alisema kuwa Kutakuwa na mabanda kadhaa likiwemo la Supersport, MNET, Maisha Magic Bongo, Fashion, Banda la watoto na mengine mengi,na kwamba kutakuwepo na Ofa kabambe ndani ya siku 2 za Maonesho, ambapo Mteja atajipatia full set ya DStv kwa sh. 59,000 tu hii ikijumlisha kifurushi cha mwezi mmoja BURE kwa king’amuzi cha HD cha Zappa. Kwa King’amuzi cha Explora Mteja atapata Kwa sh. 240,000 pamoja na kifurushi cha Compact cha mwezi mmoja BURE.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini

Wasanii wa Tigo Fiesta watembelea Duka la Tigo mjini Songea

$
0
0

Wafanyakazi wa Tigo, Laurian Gideme , Jacob Sisala na Andrea wakiwa wapozi kwenye picha ya pamoja na msanii Jux mara baada ya wasanii kutembelea duka la Tigo Songea mapema wiki iliyopita.
Wafanyakazi wa Duka la Tigo Mjini Songea wakipiga picha ya pamoja na Dogo Janja.
Wafanyakazi wa Duka la Tigo Mjini Songea wakipiga picha ya pamoja na GNako na Dogo Janja mapema wiki iliyopita.

Kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili Lulu yaanza kuunguruma leo.

$
0
0
 Elizabeth Michael "Lulu" akiwa katika Mahakama kuu Dar es salaam akisubiri akitafakari jambo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili ya mauaji ya bila kukusudia
 Muigizaji wa Filamu nchini, Elizabeth Michael "Lulu" akiwa katika Mahakama kuu Dar es salaam akisubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili ya mauaji ya bila kukusudia. Lulu anakabiliwa na kesi ya kifo cha aliyekuwa muigizaji mwenzake wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012 jijini Dar es salaam. Kulia ni Mama wa Muigizaji huyo.
Shahidi wa Kwanza wa upande wa upande Jamuhuri katika kesi ya mauaji ya bila kukusudia dhidi ya marehemu Steven Kanumba, inayomkabili msanii maarufu nchini, Elizabeth Michael ameieleza mahakama kuu kuwa licha ya kumwambia Lulu abaki na Kanumba yeye alipomfuata daktari lakini aliondoka na kumuacha peke yake

Shahidi huyo, Bosco Seth (30) ambaye pia ni kaka Wa Marehemu Kanumba ameyasema hayo leo mapema mbele ya Jaji Sam Rumanyika wakati akitoa ushahidi wake. Kabla ya kuanza kutolewa kwa ushahidi, Lulu alikumbushiwa mashtaka yake ambapo ilidaiwa April mwak 2012 huko Sinza Vatcan wilaya ya Kinondobi alimuua bila kukusidia Kanumba, Lulu alikana shtaka hilo.

Akiongozwa na Wakili wa serikali Faraja George, Bosco amesema baada baada ya kupata taarifa za kudondoka kwa Kanumba kutoka kwa Lulu alimpigia simu daktari wao aliyemtaja kwa jina la Paplas ambaye alimtaka kwenda kumchukua Hospitalini kwake na kwa kuwa hakukuwa na usafiri aliwasha Gari na kimfuata na kumuomba Lulu abaki na Kanumba.
Wakati narudi na Dk, Lulu alinipigia simu akasema Kanumba nimemuwekea mpaka maji kifuani lakini haamki ninaindoka, nikamwambia nisubiri lakibi mpaka nafika pale sikumkuta*.

Alidai baada ya Dr kufika na kumpima alimshauri wampeleke Muhimbili, ambapo kwa msaada wa jirani yao aliyemtaja kwa jina la Baraka walimbeba Kanumba na kumuingiza kwenye gari hadi Muhimbili.

Amedai wakati wanaangaika kumuingiza Kanumba kwenye gari, mama mwenye nyumba alisikia akafungua mlango aliposikia tatizo nae aliwasha gari lake na kutusindikiza, ambapo walienda moja kwa moja Emergency na baada kumfanyia Kanumba uchunguzi Dr aliwaambia kuwa ameishafariki na kituambia tufuate taratibu za polisi.

Amedai walienda polisi Urafiki ambako wakiwa huko Lulu alikuwa akimpigia Dr Paplas Simu ndipo polisi wakamuomb Dr aweze kuwasaidia kumpata Lulu ambapo asubuhi ya Aprili 7, baada ya wao kumaliza kuhojiwa Lulu alakamatwa.

Akielezea jinsi tukio Lilia to lies alidai, Aprili 4 mwaka 2012 alishinda nyumbani na kaka Kanumba toka asubuhi na ilipofika mida ya saa kumi jioni, Kanumba alimuomba asitoke na wangetoka pamoja usiku wa saa sita.

Akadai ilipofika SAA sits kasoro za usiku Kanumba alimwambia wajiandae watoke, ambapo yeye alikuwa Wa Kwanza kumaliza kujiandaa lakini alipotoka chumbani kwake akielekea sebuleni, alikutana na Kanumba akipita kwenye koridoni huku akiwa amevalia taulo kuelekea sebuleni, akipaka Mafuta kichwabi, sebuleni kwa nje kulikuwa na Gari la Lulu, nikamuuliza mbona tunachelewa akanijibu sasa hivi tunaondoka.

Akadai kuwa, Kanumba ndiye alimfungulia mlango lulu, waliingia wote ndani akiwa chumbani kwake ambako alirudi kumsubiria Kanumba huku mlango wake ukiwa wazi kidogo, wakati wakitembea Koridoni kuelekea chumbani kwa Kanumba alisikia wakigombana huku Kanumba akimuuliza lulu kwa nini anaongea na boyfriend wake mbele yake,.

Aliendelea kudai kuwa muda wote huo walikuwa wakivutana, Lulu akitaka kutoka nje na Kanumba akimvutia ndani mara waliingia chumbani na mlango ukafungwa. Nilisikia sauti za kupigana na muda mfupi kidogo Lulu alifungua mlango na kuja chumbani kwangu akasema, Kanumba amedondoka sijui amekuwaje


Alidai aliondoka hadi chumbani kwake, alimkuta Kanumba amedondoka kwa kuegemea ukuta huku akiwa hawezi kupumua, (amesafocate), alimchukua na kumlaza chini kisha akampigia simu Dr Paplas kulikuwa na alama mbili za nywele zilizokuwa zinaonyesha kuwa alipoburuzika,
Alidai, Mazingira ya chumba hicho cha kaka yake yalikuwa ya kawaida kama Siku zote.

alidai baada ya hapo aliwasha gari na kwenda kumchukua Dr ndipo Lulu akanipogia simu na kusema Kanumba haamki. Aisha Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alimuuliza Shahidi kama ushahidi aliotoa mahakamani unafanana na maelezo a logo to a by polisi alisema ndio,Kibatala alimuuliza shahidi huyo ni wapi aliwaeleza polisi kuwa alimuacha mshtakiwa Lulu peke yake Marehemu Kanumba wakati anaenda kumtafuta Dr, Paplas alisem hakuwaeleza.

Akaongeza kuwa yeye alikuwepo kwenye postmotam ya kawaida na wala hakuwepo wakati wakichukua sampuli za mwili kupeleka maabara.
Kesi itaendelea kesho.


NEWZ ALERT:MWENYEKITI MTENDAJI WA KAMPUNI YA BARRICK GOLD AWASILI JIJINI DAR KWA NDEGE MAALUM

$
0
0
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Profesa John L. Thornton akiwasili Dar kwa ndege maalum Jumanne jioni kuhudhuria mazungumzo ya biashara ya madini ya dhahabu, maarufu kama MAKINIKIA baada ya majadiliano ya kina, baina ya wataalamu wa Tanzania na wa Kampuni hiyo ambayo yamekuwa yakiendelea kwa karibu miezi mitatu sasa. Hii ni mara ya pili Prof Thornton kuja Tanzania kwa shughuli hiyo.

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Profesa John L. Thornton akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa JNIA,jiji Dar kwa ndege maalum Jumanne jioni kuhudhuria mazungumzo ya biashara ya madini ya dhahabu, maarufu kama MAKINIKIA baada ya majadiliano ya kina, baina ya wataalamu wa Tanzania na wa Kampuni hiyo ambayo yamekuwa yakiendelea kwa karibu miezi mitatu sasa. Hii ni mara ya pili Prof Thornton kuja Tanzania kwa shughuli hiyo.

KANGI LUGOLA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Faustine Kamuzora  (kulia) mara baada ya mazungumzo ambapo  Mhe. Kangi Lugola alijitambulisha  kwa mara ya kwanza kama Naibu wa Wizara hiyo kwa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (katikati)akitembea kwa miguu akielekea ofisini kwake barabara ya Luthuli mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Faustine Kamuzora. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Barclays launches 'TwendeKazi & BaloziMwanafunzi' scholarships programs

$
0
0
 Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), is convoyed by Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left), University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo (right), some Barclays senior officials and invited dignitaries before the launching ceremony of  Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
 Barclays Bank Head of Marketing and Corporate Relations Aron Luhanga (third left), and University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo, sign contract documents to officiate the launching  of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday. Looking on from left are Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji, Barclays Head of Human Resources, Patrick Foya, UDSM  Deputy Corporate Counsel, Dr. Saudin Mwakaje and Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako.
 Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), addresses participants during the official launching of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
 A cross section of partakers during the launching ceremony of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
 Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left) and University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo (right) in a souvenir photo pose with some Barclays senior officials and other invited dignitaries after the official launching of   Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
 Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left) and University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo (right) pose for a memento picture with  some senior Barclays officials and some invited dignitaries after the official launching of   Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left) Junior Achievement Tanzania Director,  Hamis Kasongo (right), pose for a reminder photo with  some Barclays senior officials, representatives from university colleges and other  dignitaries after the official launching of   Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.


KITUO CHA CHILD IN THE SUN WAPOKEA MSAADA WA KOPYUTA 10 TOKA VODACOM TANZANIA FOUNDATION.

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Wakiwa wamebeba kompyuta 10 zilizotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo kwa watoto hao kituoni hapo.

 Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Wakiwa wameshikilia kompyuta 10 walizokabidhiwa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo yao kituoni hapo.

  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Jacquiline Materu(wapili kulia)na Meneja biashara kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Grace Lyon(kulia)wakiwapigia makofi ya kuwapongeza baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam baada ya kuwakabidhi msaada wa kompyuta 10 uliotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo yao kituoni hapo.


Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Khalid Ismail akipokea moja ya kompyuta kati ya 10 kwa niaba ya wenzake toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Jacquiline Materu(kulia)Msaada huo uliotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo ya watoto hao kituoni hapo.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakicheza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Walipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kukabidhi msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa na Vodacom Tanzania Foundation  kwa ajili ya mafunzo kwa watoto hao kituoni hapo.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUKAMILIKA MAJADILIANO KATI YA TANZANIA NA BARRICK GOLD CORP

Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images