Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MBIO ZA TIGO DODOMA HALF MARATHON ZAZINDULIWA RASMI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma -  Jordan Rugimbana akizungumza na waandishi wa habari anayefuatia ni Kaimu Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini - Henry Kinabo na mwisho ni Mkurungenzi Mtendaji wa Vision Investment, Ally Nchahaga wakizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika uzinduzi rasmi wa mbio ndefu za Dodoma almaarufu Dodoma Marathon. Mbio hizo zimethaminiwa na Tigo Tanzania na zinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma mwezi  Novemba mwaka huu.
(Kutoka kushoto)  Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dodoma - Robert Mabonye , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma -  Jordan Rugimbana ,Kaimu Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini - Henry Kinabo na Mkurungenzi Mtendaji wa Vision Investment, Ally Nchahaga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa mbio ndefu za Dodoma almaarufu Dodoma Marathon. Mbio hizo zimethaminiwa na Tigo Tanzania na zinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma  mwezi Novemba mwaka huu.  
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika atika uzinduzi rasmi wa mbio ndefu za Dodoma almaarufu Dodoma Marathon. Mbio hizo zimethaminiwa na Tigo Tanzania na zinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma  mwezi Novemba mwaka huu.   .


Ziara ya Waziri Makamba visiwani Zanzibar yaingia siku ya pili

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (kushoto) akimsikiliza Kapteni Abdallah Juma Abdallah Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Zanzibar alipokuwa akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za bandari mara baada ya Waziri Makamba kupata fursa ya kuwatembelea.2
Viongozi waandamizi wa Bandari – Zanzibar wakifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba alipotembelea bandari hiyo hii leo kujionea utendaji kazi wao na kuwapa fursa ya kuianisha changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo.
3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar  wa (pili kulia). Waziri Makamba amefanya ziara ya kutembelea ofisi zao na kupata fursa ya kufanya majadiliano kwa manufaa na ustawi wa Muungano wetu.
4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akiwa katika kikao na Menejimenti ya Bodi ya Mapato Zanzibar. Wa pili kushoto ni Kamishna wa Bodi Bw. Amour Hamil Bakari na Bi. Khadija Shamte  Naibu Kamishna. Waziri Makamba yuko ziarani Zanzibar kutembelea Taasisi za Muungano na zile zisizo za Muungano.
…………………………………………………………………….
Imebainika kuwa Bandari ya Zanzibar ni miongoni mwa Vyanzo vya Mapato vinavyopelekea ukuaji wa uchumi baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na fursa zilizopo katika nyanza za biashara.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Captain Abdallah Juma Abdallah katika siku ya pili ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ambapo amepata fursa ya kutembelea Bandari ya Zanzibar.
Katika siku ya pili ya ziara yake ya siku saba Visiwani Zanzibar Waziri Makamba amebainisha kuwa lengo la ziara yake ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa masuala waliyokubaliana katika vikao baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar katika vikao vya mashirikiano.
“Niko Zanzibar kwa ziara ya kikazi na nimejikita zaidi katika kushughukikia masuala ya uchumi ikiwa ni pamoja na masuala ya Bandari, Forodha, Kodi na kubaini changamoto zilipo, utekezaji wa maazimio yaliyokubaliwa katika vikao vya majadiliano na kuangalia maeneo mapya yanayohitaji kuingizwa katika mfumo wa utatuzi,” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amesema kuwa kuwepo kwa bandari ni ufanisi kwa uchumi na ni namna bora ya kuimarisha  Muungano  na ustawi wa Zanzibar na pande zote mbili za Muungano hazina budi kuondoa changamoto zilizopo kwa manufaa ya wote.
Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Mapato Zanzibar na kuwafahamisha kuwa lengo la Serikali zote mbili ni kuhakikisha kuwa pande zote mbili za Muungano zinanufaika na fursa za uchumi zilizopo, na kila upande unufaike na fursa zilizopo katika mambo ya Muungano na yale yasiyo ya Muungano.
Katika ziara hiyo Waziri Makamba amewataka  watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania upande wa Zanzibar kuzifanyia kazi changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza kwa haraka, kupunguza urasimu na kuongeza elimu kwa umma ili kujenga uelewa kwa wananchi  juu ya mambo yanayopaswa kuzingatiwa na yale yasiyopasa ili kuondoa vikwazo vinavyojitokeza katika bandari ili kuondoa malalamiko ya wananchi.
Nae Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  kwa upande wa Zanzibar Bw. Mcha Hassan Mcha amesema kuwa ni vema wananchi wazingitae kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ikiwa pamoja na kupata risiti halali kwa kila bidhaa wanazonunua ili kuepuka usumbufu pindi wasafirishapo bidhaa baina ya Tanzania bara na Zanzibar.
Ziara ya Waziri Makamba visiwani Zanzibar itaendelea kesho kwa kutembelea miradi mbalimbali ya Mazingira.

Naibu Waziri Lugola Afanya Ziara Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC)

$
0
0


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Dkt Vedast Makota wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo katika baraza hilo mapeme hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (kushoto) akipata maelekezo toka kwa mtaalamu wa maabara wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo katika baraza hilo mapeme hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na watumishi wa Baraza la Taifa la Mazingira (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo katika baraza hilo mapeme hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na watumishi wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo katika baraza hilo mapeme hii leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Dkt Vedast Makota (kulia) akizungumza na watumishi baraza hilo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (kushoto) mapeme hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo katika baraza hilo mapeme hii leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira(NEMC) Dkt Vedast Makota (kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (kushoto) wakati alipokutana na Menejimenti ya baraza hilo akiwa katika ziara ya kikazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola (kushoto) akifafanua jambo kwa Menejimenti ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) wakati wa ziara yake ya kikazi katika baraza hilo mapema hii leo, kulia aliyesimama ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira Dkt Vedast Makota.

Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI TORONTO CANADA.

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada,Jack Zoka baada ya liwasili Toronto Oktoba 19, 2017 kwa ziara ya kikazi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).PMO_5550
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada,Jack Zoka baada ya liwasili Toronto Oktoba 19, 2017 kwa ziara ya kikazi. Kulia ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DKT. KIGWANGALLA:TANZANIA NA OMAN KUANZISHA UTALII WA PAMOJA WA KIHISTORIA NA UTAMADUNI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7650
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, Kulia ni Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7652
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7659
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akiteta jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
1J8A7663
Bendi ya Jeshi la Taifa la Oman wakipiga nyimbo za Taifa hilo zinazofanyika wakati wa vita na ukombozi
1J8A7672
Baadhi ya wananchi wakiwa na bendera za Taifa la Oman na Tanzania wakishuhudia tukio hilo
1J8A7679
Baadhi ya Askari Maji wa kikosi cha Oman wakiwa katika tukio hilo.
1J8A7753
Dkt. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani)
1J8A7786
Wachezaji wa Oman wakionesha ngoma za Utamaduni wa Taifa hilo.
…………….
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema  Tanzania na Nchi ya Oman zimefanya mazungumzo katika kuimalisha sekta ya Utalii hasa kwenye Utalii wa kukuza Utamaduni na ule wa Kihistoria uliokuwepo miaka mingi kwa Mataifa hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla amebainisha hayo jioni ya jana Oktoba 18,2017, wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya nyimbo na ngoma za Taifa la Oman yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo pia tukio lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na viongozi wa Taifa hilo la Oman ambao wapo Nchini kwa ziara ya kusambaza Ujumbe wa Amani na Upendo kupitia meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia maonyesho ya ngoma na nyimbo hizo za Taifa la Oman, Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa, Watanzania wameweza kujifunza na kufurahia utamaduni wa Oman hasa kupitia nyimbo, ngoma na mashahiri ambapo amebainisha kuwa Serikali itaendeleza ushirikiano mwema hususani wa Kiutaduni na kukuza Utamaduni.
“Watanzania na watu wa Taifa la Oman ni ndugu. Hivyo kupitia ngoma  na nyimbo hizi walizoonesha hapa zinafanana sana za zile za Visiwa vya Zanzibar na ukanda wetu huu wa Pwani wa Tanzania.
Pia hata baadhi ya viongozi waliokuja na msafara huu wanazungumza vizuri lugha ya Kiswahili bila kuchanganya na lugha nyingine huku wengine kama mulivyowaona wana asili ya Tanzania ikiwemo Visiwa hivyo vya Zanzibar ambapo walizaliwa huko.” Ameeleza Dkt. Kigwangalla.
Aidha, ameeleza kuwa, kwa sasa wanakusudia kutengeneza chanzo kipya cha Utalii ambacho kitakuwa ni cha Kihistoria na Kiutamaduni baina ya Mataifa hayo mawili  na kufafanua kuwa, Histoia ya Tanzania hasa Lugha ya Kiswahili huwezi kukitenganisha Bara la Arab hususani watu wa Oman.
“Kuna wengine wasomi wa Historia na utamaduni wa Uislamu wamebainisha kwenye taarifa za kisayansi, kuwa pengine hata dini ya kiisilamu ilianza kufika ukanda wa Pwani wa Afrika Mashariki kabla ya hata haijafika baadhi ya Nchi ya Mashariki ya Kati.
Hii ni pamoja na makaburi ya kale kule Bagamoyo, Pemba na sehemu nyingine za Tanzania ambapo kwa pamoja yanaonesha uwepo wa Waislamu na mashekhe wa kiisilamu waliofika kuanzia mwaka 1200 mpaka hadi 2000, miaka mingi iliyopita.” Alibainisha Dkt. Kigwangalla.
Ameongeza kuwa: “Wao wakitangaza vivutio vyao, watavitangaza na vivutio vyetu vya Tanzania. Lakini pia sisi tutatumia fursa vivutio tulivyonavyo ambavyo wao hawana kama Mbuga za Wanyama kuwaalika watu wa Omani kuja kutalii Tanzania, kipindi cha Mwezi Juni, Julai hata Agosti wao ni kipindi cha joto kali kwani wakati mwingine  msimu huo kule wao wanakuwa na utaratibu wa kutoa rikizo ama mapumziko ya muda wa zaidi ya siku 30 hadi 40 hivyo tutatumia  fursa ya kipindi hicho na hata wale wanaowapokea Oman waweze kuja Tanzania kutalii” alieleza.
Pia alimalizia kwamba,  ushirikiano huo, utaongeza soko kubwa la kiutalii.
Msafara huo wa viongozi wa Oman wakiwemo Mawaziri na wafanyakazi wa Meli hiyo ya Mfalme wa Taifa hilo unajumuisha watu zaidi ya 300 ambapo leo Oktoba 19,2017, umetembelea Wilaya ya Bagamoyo kujinea fursa za kiuwekezaji na uchumi katika ukanda huo wa Pwani huku Meli hiyo kesho Oktoba 20,2017 ikitarajiwa kuondoka kuelekea Mombasa Nchini Kenya.

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MAKUBALIANO YA KAMATI ZA TANZANIA NA KAMPUNI YA BARRICK GOLD KUHUSU MAKINIKIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp.Profesa John L. Thornton alipokutana nae wakati wa kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton akiwa na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold Richardc William huku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Florens Luoga nao pia wakiweka saini ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton wakimsikiliza Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba akitoa muhtasari wa ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold Richardc William na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo baada ya kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017.

DKT. KIGWANGALLA ATOA SIKU SABA KWA MIFUGO, MATREKTA NA VIFAA VINGINE KUTOKA NJE YA NCHI KUONDOLEWA NDANI YA PORI TENGEFU LOLIONDO

TAMASHA LA KIJANA PAZA SAUTI, WAJIBIKA LAFANA JIJINI MWANZA

$
0
0
Afisa Mradi kutoka UNA Tanzania, Saddam Khalfan akielezea kuhusu mradi wa Kuwajengea uwezo vijana kushiriki katika michakato ya maamuzi na utekelezaji wa sera ya maendeleo ya vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika lililofanyika katika Viwanja vya Furahisha, Jijini Mwanza. Mradi huo unatekelezwa na asasi za vijana kumi na saba Tanzania bara na Visiwani chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society. Kushoto ni Kaimu Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, William Mnyippembe.
Mgeni rasmi Kaimu Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, William Mnyippembe akifungua Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika kwa kutoa ujumbe kwa vijana kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kujiendeleza kielimu na kukuza kipato.
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Mwanza, Gilbert Otieno akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika lililowakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya za Nyamagana na Ilemela lililolenga kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo, michakato ya maamuzi na kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za chini hadi juu pamoja na kuongeza uelewa wao juu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngaza wakiimba shairi la kuhamasisha vijana kushiriki katika michakato ya maamuzi na kutobaki nyuma katika kujitafutia taarifa za maendeleo.  
Mkurugenzi wa YEV Mwanza, Jonathan Kassibu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika na kazi za taasisi yake ya kuunda majukwaa ya vijana na kuwajengea uwezo vijana katika kata nne za Manispaa ya Nyamagana, jijini Mwanza chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwanza wakiimba wimbo wa AMKA KIJANA ambao ulilenga kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa na kutokubweteka.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika shindano la uchoraji wa picha za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakionyesha picha hizo kwa washiriki na majaji wakati wa Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika lililofanyika jijini Mwanza.
Wanafunzi wakiwashangilia washiriki wa shindano la uchoraji wa Picha ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.
Wanafunzi wakiigiza kuhusu Tabia za Vijana na mienendo yao wakati wa Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika liliondaliwa na UNA Tanzania, YEV Mwanza kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika liliondaliwa na UNA Tanzania, YEV Mwanza kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society.
Msanii wa miondoko ya 'HipHop' nchini Tanzania, Kala Jeremiah akitumbuiza wimbo wake mpya wa KIJANA ambao unalenga kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo na kushiriki katika michakato ya maamuzi na kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya chini hadi juu katika Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika liliondaliwa na UNA Tanzania, YEV Mwanza kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society. Tamasha hili limefanyika katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza. 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akutana na Wafanyabiashara Jijini Mwanza

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akutana na Wafanyabiashara Jijini Mwanza Inbox x BMG HABARI 5:04 PM (6 hours ago) to Habarileo, Full, MJENGWA, Zanzibar, KASSIM, MUHIDIN, Michuzi, Kisiwa, Raia, Majira2006, Uhuru, Leo, GAZETI, Tanzania, Uhuru, Habarileo, Zanzibar, Nipashe, MO-BLOG, Mtanzania, Mwananchi, Dira, Gazeti, HABARI, Picha
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji jana amekutana na wafanyabiashara Jijini Mwanza kwa ajili ya kusikiliza na kutatua baadhi ya kero za kibiashara kutoka kwa wafanyabiashara hao chini ya chama chao cha TCCIA.

Dkt.Kijaji aliwahakikishia wafanyabiashara hao kwamba serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara huku akibainisha kwamba mashine za kutolea stakabadhi EFD's sasa zinatolewa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA na hivyo wafanyabiashara hao wataondokana na baadhi ya kero walizokuwa wakikumbana nazo kutoka kwa mawakala wa mashine hizo ikiwemo kuzinunua kwa bei kubwa.

Awali wafanyabiashara hao walilalamikia suala la machinga kupanga bidhaa zao kando ya milango ya maduka yao ambapo Naibu Waziri Kijaji aliwasihi kuwa na subira wakati serikali utaratibu wa kuwasajili na kuwapatia machinga vitambulisho kama ilivyoelezwa kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 na hatimaye kuwaboreshea maeneo yao ya kufanyia biashara.
Na Binagi Media Group
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (kushoto), akizungumza na wafanyabiashara Jijini Mwanza jana. Wengine ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari (katikati) pamoja na Naibu Kamishina wa Kodi za Ndani TRA Makao Makuu, Beatus Nchota.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (aliyesimama), akizungumza na wafanyabiashara Jijini Mwanza jana. Wengine ni Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee (wa kwanza kushoto), Injinia Boniphace Nyambele aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari (kulia).
Naibu Kamishina wa Kodi za Ndani TRA Makao Makuu, Beatus Nchota, akizungumza kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari, akizungumza kwenye kikao hicho
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicho akiwemo Makamu wa Rais wa TCCIA, Joseph Kahungwa (kushoto)
Baadhi ya wafanyabiashara Jijini Mwanza ambao walihudhuria kikao cha majadiliano baina ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji
Baadhi ya wafanyabiashara Jijini Mwanza ambao walihudhuria kikao cha majadiliano baina ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji.

Mawakala wa benki ya CRDB watakiwa kuendeleza uadilifu

$
0
0
Mawakala wa benki ya CRDB kupitia huduma ya Fahari Huduma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza, wakiwa kwenye semina iliyoyandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kuwajengea weledi na uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja.

Mawakala kutoka wila ya za Nyamagana, Ilemela, Magu, Misungwi, Kwimba, Sengerema pamoja na Ukerewe walihudhuria kwenye semina hiyo iliyofanyika alhamisi iliyopita Oktoba 12,2017 Jijini Mwanza.

Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura Calystus aliwasihi mawakala hao kuwa waaminifu katika kuwahudumia wateja ikiwemo kutunza siri za mihamara ya pesa za wateja wao huku wakitoa huduma bora kama ilivyo ada ya benki ya CRDB wanayoiwakilisha katika maeneo yao.

Mawakala hao walieleza kwamba semina hiyo itawasaidia kuboresha huduma zao kwa wateja na hivyo kuwahimiza wateja wa benki ya CRDB kuendelea kutumia huduma za benki hiyo kwani zinapatikana kwa urahisi katika maeneo yote nchini.
Na Binagi Media Group

Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura Calystus, akifungua semina hiyo
Meneja wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Mafwimbo Mulungu akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa wa CRDB, Danford Muyango akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa BIMA kutoka benki ya CRDB tawi la Nyanza, Jackline Jubilate akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Meneja biashara wa CRDB tawi la Nyanda, Eugenius Mashishanga (kushoto), akizungumza kwenye semina hiyo
Baadhi ya wakala wa CRDB wakichangia mada kwenye semina hiyo
Baadhi ya mawakala wa benki ya CRDB wakiwa kwenye semina hiyo
Bonyeza HAPA CRDB ilivyoadhimisha Wiku ya Huduma kwa Wateja Geita

Serikali Kujenga Mabwawa 10 Ya Kuogelea, Tanzania Yaanza kwa Vishindo

$
0
0
Muogeaji wa Tanzania kwa upande wa wanawake, Maia Tumiotto akishindana na wenzake katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini. Sonia alishinda katika mashindano hayo.2
Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania  wakijaindaa kuchupa katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.
3
Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania  wakijiandaa ku-dive  katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.
4
Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania  waki-dive  katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.
5Kocha wa timu ya Tanzania, Michael Livingstone akisimamia mazoezi ya timu ya Tanzania katika mashindano ya Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.
…………..
Na Mwandishi wetu
Serikali imeahidi kujenga mabwawa 10 ya kisasa ya kuogelea kwa ajili ya kuendeleza mchezo  huo hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa nchini, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kanda ya tatu ya Afrika yanayoandelea kwenye bwawa la shule ya Kimataifa ya Heaven of Peace (Hopac).
Waziri Mwakyembe alisema kuwa wamefarijika sana na vipaji vya waogeleaji wa Tanzania katika mashindano  hayo ambayo yameshirikisha jumla ya nchi sita ikiwemo ya Tanzania. Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Sudani, Afrika Kusini na Zambia.
“Nimesikitika sana kusikia kuwa kuna wawekezaji walikuja hapa kutaka kujenga bwawa la kuogelea kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huu na kukatishwa tamaa na baadhi ya watendaji wa wizara yangu,”
“Nawaahidi kulishughulikia suala hili kabla ya mwisho wa mwezi huu, nitakutana na Waziri wa Tamisemi na kuona ugumu upo wapi hasa kwa shule maarufu ya msingi ya Oysterbay ambayo ilikuwa iwe ya kwanza kujengewa  bwawa la kisasa la kuogelea,” alisema Waziri Mwakyembe.
Alisema kuwa malengo yake ni kuona mchezo wa kuogelea unafikia kiwango cha juu kabisa kwani amegundua nchi ina vipaji vingi, lakini wanashindwa kufikia kiwango cha juu kutokana na kukosa miundombinu ya kisasa.
Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka aliipongeza  serikali kwa ahadi hiyo ambacho ni kilio chao cha siku nyingi.
“Tumefarijika sana na ahadi za serikali, kama mnavyojua, tumekuwa tukiangaikia suala la kupata bwawa la kisasa la kuogelea miaka mingi, naamini mafanikio ya ahadi hiyo yataleta msisimko mpya kwa waogeleaji na wadau wake,” alisema Namkoveka.
Namkoveka pia aliwapongeza wachezaji wa Tanzania kwa kuanza kwa vishindi mashindano hayo na kutwaa medali 21 ambapo, nane ni za dhahabu. Waogeleaji, Sonia Tumiotto na Natalie Sanford kila mmoja alitwaa medali mbili za dhahabu katika mashindano hayo.
Waogeleaji wengine waliotwaa medali za dhahabu I Elia Imhoff, Emma Imhoff, Behnson Tara, Marin De Villard na timu ya relay kupitia kwa Collins Saliboko, Hilal Hilal, Sonia Tumiotto na Emma Imhoff.

Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Kuanza Hivi Karibuni: Waziri wa Oman

$
0
0
Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maeneo ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA) Kapteni George Simbakalia alipokuwa katika ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi akitazama jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo wakati wa ziara yake wilayani Bagamoyo leo. Waziri huyo ametembelea maeneo ya uwekezaji ya Mamlaka ya Maeneo ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA), maeneo ya Kihistoria la Kaole na eneo itakapojengwa bandari.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya akielezea jambo mbele ya Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi alipotembelea eneo la bandari ya Bagamoyo wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya uwekezaji wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Naibu Waziri wa Utalii wa Oman Bi. Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi (mwenye ushungi).
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya akipokea zawadi toka kwa Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majjid Hemed.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwaonyesha eneo la bahari ujumbe kutoka Serikali ya Oman unaoopngozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi (mwenye miwani mwenyeusi) walipotembelea eneo la Bandari ya Bagamoyo iliyopo Mbegani katika ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji na historia wilayani Bagamoyo leo. Mwenye vazi la kitenge ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majjid Hemed, Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya wakitoka katika Bandari ya Bagamoyo wakati wa ziara ya Waziri huyo katika maeneo ya uwekezaji kiuchumi (EPZA), maeneo ya kihistoria la Kaole na eneo itakapojengwa bandari mpya.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Utalii wa Oman Bi. Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi, Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. Al Mahruqi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majjid Hemed wakimsikiliza mhifadhi ya makumbusho ya mali kale ya Kaole walipotembelea eneo hilo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi wakiangalia kisima cha maji ya baraka kilichopo katika eneo la ulipojengwa msikiti wa kwanza pwani ya mashariki katika eneo la Kaole wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yakutembelea eneo la Bandari ya Bagamoyo iliyopo Mbegani, maeneo ya uwekezaji na historia wilayani Bagamoyo leo.
Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi akinywa maji toka katika kisima cha maji ya baraka kilichopo katika eneo la ulipojengwa msikiti wa kwanza pwani ya mashariki katika eneo la Kaole wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yakutembelea eneo la Bandari ya Bagamoyo iliyopo Mbegani, maeneo ya uwekezaji na historia wilayani Bagamoyo leo.
Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania mara baada ya kutembelea eneo itakapojengwa bandari mpya wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. Al Mahruqi, Balozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima, Naibu Waziri wa Utalii wa Oman Bi. Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya, Waziri wa Uwekezaji wa Oman Salem Bin Nasser Al Ismaily. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 20,2017

MBUNGE RITTA KABATI AMEKERWA NA MIMBA ZA UTOTONI KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KWAKILOSA

$
0
0
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea na wanafunzi,wazazi na walimu wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka huu 2017 katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo katika manispaa ya Iringa 
Baadhi ya wanafunzi na wazazi walihudhuria sherehe za kuhitimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo kata ya Mwangata.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi cheti mmoja ya wanafunzi wa kike aliyehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekerwa na uwepo wa mimba za utotoni katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo kata ya Mwangata manispaa ya Iringa kwa kuwa kitendo hicho kinachosababisha kushuka kwa elimu katika shule hii.

Akizungumza wakati wa shererhe za kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka huu Kabati alisema kuwa amesikitishwa kusikia kila mwaka kuna wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili ya kupata ujauzito.

“Jamani tumekuwa tukitoa elimu kila mara juu ya madhara yanayotoka na upatikanaji wa mimba za utoto za hiii shule imekuaje kila mwaka wanafunzi wanapata mimba hii haikubariki katika jamii kabisa maana hawa wanafunzi ndio tegemeo la taifa kwa sasa” alisema Kabati


Kabati aliwataka wazazi na walimu kuwalinda wanafunzi wa kike ili wasikumbane na ardha ya kupata mimba wakiwa watoto wadogo kwani kunapoteza muelekeo wa maisha yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.


“Haiwezekani kila mara wazazi mnakuwa wa kwanza kuwa chanzo cha kuwaharibu watoto na kwanini wazazi mnafanya hivyo maana watoto hawa ndio watakao wasaidia hapo baadae ndio maana mkiwa mmezeeka kwa hiyo ndio watakuwa msaada katika maisha yenu naombeni muwatunze watoto wenu” alisema Kabati


Aidha Kabati aliwataka wanafunzi wote mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla kuacha kufanya mapenzi wakiwa na umri kama wao hivyo wanapaswa kujilinda ili kufikia malengo yao waliojiwekea na walidhike na kipato walicho nacho wazazi wao.


“Hivi kaka mimi ningeanza mapenzi nikiwa na umri kama wenu unafikiri ningefikia malengo haya niliyonayo hivyo nawaomba msifanye mapenzi mkiwa na umri mdogo ili baadae mje kufikia malengo yenu” alisema Kabati


Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Hudson Luhwago aliwatupia lawama wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo kwa kutowalea katika malezi mazuri wanafunzi hao.


“Yaani kabisa mzazi anakuja na wanafunzi anamuombea ruhusa kuwa walikuwa fiesta wote hivyo mtoto amechoka hawezi kuja shule hii ni aibu na ukweli unaoendelea kwa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule hii” alisema Luhwago


 Luhwago alisema kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanawanaume zaidi ya watano na wazazi wanayajua hayo lakini wanashindwa kuwakemea watoto wao na ndio maana wanakuja shule wakiwa na kiburi hata kwa walimu.


“Wanafunzi hawa wanaomaliza hitimu shule leo walikuwa wanakiburi kwa sisi walimu hadi ikabidi tukae kama wanalimu tuwajadili lakini chanzo chote ni malenzi mabaya wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya wazazi au walezi wao” alisema Luhwago


Akisoma risala kwa mgeni rasmi makamu mkuu wa shule Praygod Makongwa alisema kuwa hadi sasa kuna mwanafunzi ameachishwa shule akiwa kidato cha kwanza kwa sasbabu ya kuwa mujamzito na hata hawa wanaohitimu hii leo mwenzao mmoja alikatisha masomo akiwa kidato cha pili kwa kuwa na ujauzito.


“Sisi kama walimu wa shule hii tushazoe kuona wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili ya kupata mimba na ukiangalia kwa umakini walimu tunawalea wanafunzi kwa maadili yanayotakiwa tatizo lipo kwa wazazi hao unakuta mtoto na mzazi wapo disco pamoja wanakunywa pombe pamoja sasa hapo utapata matokeo gani?” alisema Makongwa



Lakini Makongwa alisema kuwa shule imejiwekea mikakati ya kuhakikisha inajenga majengo ya mabweni kwa wanafunzi ili kumaliza tatizo la mimba za utoto na kuboresha elimu ya shule ya sekondari ya Kwakilosa.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA WAFANYAKAZI MIZANI KUACHA RUSHWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mwenyesuti), akiangalia namna shughuli za upimaji wa magari zinavyoendeshwa katika mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mkoa huo, Mhandisi Mibala Ndilindi.

Msimamizi wa shughuli za mzani wa Tinde kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS),mkoani Shinyanga, Bw. Lugembe Vicent (kushoto), akitoa taarifa ya kiutendaji ya mzani huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa. Mzani huo unapima magari 300 kwa siku.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa, akiangalia namna watumishi wa mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga wanavyopima na kurekodi taarifa za magari yanaoingia kupima uzito kwenye mzani huo.

Magari yakiwa katika foleni kusubiri huduma za upimaji uzito ili kuendelea na safari kwenye mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga.

Muonekano wa barabara ya Uyovu- Bwanga (KM 45) kwa kiwango cha lamii iliyopo mkoani Geita, ikiwa imekamilika kwa asilimia 98.

RC GAMBO AFUNGUA KIKAO MKAKATI CHA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza na wanachama wa baraza la wafanyakazi wa shirika la Bima la taifa leo jijini Arusha mara alipoalikwa kama mgeni ramsi kufungua kikao cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa veta jijini Arusha jana 
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe na viongozi wa baraza la wafanyakazi wa shirika la Bima la Taifa leo katika ukumbi wa Veta jijini hapa mara bada ya kufungua mkutano wa baraza hilo. 
Baadhi ya wanachama wa baraza la wafanyazi wa shirika la Bima la Taifa wakiwa katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika leo ndani ya chuo cha Veta jijini Arusha, 
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akinyanyua mikono na viongozi wa baraza la wafanyakazi wa Bima la Taifa leo katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika chuo cha Veta jijini Arusha,kushoto kwake ni mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Bima la Taifa,Laston Msongole. 
Mwenyekiti wa bodi ya shirika la Bima la Taifa,Laston Msongole aliyeshika kipaza sauti akizungumza katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo jana katika ukumbi wa veta jijini hapa,pembeni yake ni mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo 

DAKTARI WA KANUMBA AMEIEEZA MAHAKAMA KUWA KANUMBA ALIFIA NYUMBANI

$
0
0
 Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiongea jambo na wakili wake, Peter Kibatala wakizungumza jambo kabla ya kuanza kusomwa kesi yake ya kuua bila kukusudia jijini Dar es Salaam leo.
 Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiwa na wazazi wake katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akisubiri kusomewa mastahaka yanaymkabili jijini Dar es Salaam leo.
Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akitoka katika mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam mara baada ya kesi yake kumaliza kusomewa na kuhairishwa mpaka Jumatatu Oktoba, 23, 2017.
Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiwa nje ya mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa kesi ya kuua bila kukusudia ya msanii mwenzake Steven Kanumba.

 
DAKTARI wa familia ya msanii maarufu wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, Dkt, Paplas Kagaia, ameileza mahakama Kuu ya Tanzania kanda Dar es Salaam Kanumba alifariki toka nyumbani baada ya kumpima na kukuta mapigo yake ya moyo hayakuwepo.

Dk, Paplas amedai hayo leo Oktoba 20, 2017 huu wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

Amedai kuwa, baada ya mdogo wa marehemu kumfuata hospitali kwake na kumwambia kuwa Kanumba amefariki, alichukua kipino cha sukari na shindikizo la Damu(pressure) na kwenda moja moja nyumbani kwake Sinza ambako baada ya kufika nyumbani kwake alimpima sukari na kukuta io kawaida lakini alipompima pressure haikuwepo kabisa. 

Daktari Huyo mwenye elimu ya stashada ya juu (Advance diploma) aliyejipatia Elimu yake chuo cha uuguzi cha jeshi cha Lugalo amedai kuwa, alikuwa daktari wa familia ya Kanumba kwa zaidi ya miaka mitano na anamiliki Hospitali yake binafsi ya St. Anna iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam alikuwa akimtibu Kanumba magonjwa ya kawaida na hakuwahi kugundua tatizo lake lolote. 

Mahojiano kati ya Dr Paplas na Wakili wa serikali Batlida Mushi yalikuwa kama ifuatavyo;

Wakili: Ulipata wapi taarifa kama ya kuugua kwa Kanumba?
Shahidi: Nikiwa naudumia wagonjwa kama kawaida nilipigiwa simu na Seth akiniomba niende kumuona Kanumba amedondoka, nikamwambia muda ule ulikuwa ni usiku sana aende kumchukua.

Wakili: kwani nini Seth akupigie wewe simu?
Shahidi: Nilikiwa daktari wa familia yao kwa miaka kama mitano hadi sita.

Wakili: Baada ya kukupigia simu, ulifanya nini?
Shahidi: Nilichukua vifaa vya mashine ya sukari na BP, niliingia chumbani kwake nikifuatana na Seth nilipofika nilikuta Kanumba amelala chini chali, nikampima sukari ilikuwa normal nikampima pressure mapigo ya moyo hayakuwepo kabisa.

Wakili:Baada ya kujua mapigo ya moyo hayapo ulifanya ulichukua hatua gani?
Shahidi: Nilimwambia Sethi Fanya umvalishe nguo wafanye utaratibu wa kumpeleka hospitali kubwa ya Muhimbili akafanyiwe Vipimo.
 
Wakili: Baada ya hapo ulifanya nini?
Shahidi: Baada ya kumvalisha nguo kwa kisaidiana na kijana mmoja wa jirani na mama mwenye nyumba tulimpeleka Muhimbili kitengo cha emergency.

Wakili: Mlipofika Muhimbili kitengo cha Emergency ulifanya nini?
Shahidi: Nilimuomba Dk tuliyemkuta pale ampime Kanumba na alipompima alisema kuwa ameshafariki.

Wakili: Wakati huo anapimwa mlikuwa mahali gani?
Shahidi: Alimpima pale pale nje hata ndani hatukuingia, alitushauri tufuate taratibu za polisi, alituambia twende Kituo cha polisi cha Slender Bridge tukachukue PF3.

Wakili: Mlipokuwa Polisi nini kiliendelea?
Shahidi: Tulipewa askari ili watusaidie kupeleka maiti Mochuari kisha tukaambiwa twende Kituo Osterbay Polisi tukatoe Maelezo. 

Wakili: Unamfahamu Lulu?
Shahidi: Ndiyo

Wakili: Unamfahamuje?
Shahidi: Nimemfahamu kwa kupitia Kanumba.

Wakili: Unamfahamu kama nani?
Shahidi: Alikuwa mpenzi wake Marehemu Kanumba.

Wakili: Je Aprili 7 mwaka 2012 baada ya wewe kwenda Polisi Osterbay ulimuona?
Shahidi: Hapana sikumuona.

Wakili: ulimuonea wapi?
Shahidi: Nilimuona usiku kwenye saa 11 alikuwa Sinza sehemu moja inaitwa Bamaga, baada ya yeye kunipigia simu.

Baada ya kumaliz kutoa ushahidi wake kwa upande wa mashtaka wakili wa utetezi, Peter Kibatala naye alipata nafasi ya kumuhoji shahidi huyo ambapo mahojiano yao yalikuwa hivi;

Wakili Kibatara: Kwa nini ulipofika eneo la tukio ulimpima Sukari?
Shahidi: mtu akianguka ghafla Mara nyingi sukari inaweza kuwa imeshuka
Wakili Kibatala, kabla ya Octoba 7 uliwahi kumfanyia uchunguzi marehemu kuhusu sukari.

Shahidi: Hapana
Wakili: Uliwahi kumfanyia vipimo kama anauvimbe kichwani
Shahidi: hapana.

Wakili: je ulimkuta na jeraha lolote?
Shahidi hapana.

Wakili Kibatara: Ni sahihi kuwa mshtakiwa alikuwa anakupigia simu Mara kwa Mara?
Shahidi: Ni sahihi kweli alikuwa akinipigia hata kabla hajaenda hospitali.

Wakili Kibatara:Ni sahihi kwamba mshtakiwa alikuwa anakupigia simu Mara kwa Mara akifikiria kuwa marehemu alikuwa amezimia tu?
Shahidi; Ndiyo ila alikuwa na hofu kama marehemu amekufa.


Wakili Kibatara: Ni sahihi kuwa mshtakiwa alikuwa anaogopa kuonana na wewe kwa sababu alidhani uko na marehemu na ulikuwa na mtego tu wa kumkamata ili andeleze tabia yake ya wivu uliopindukia?
Shahidi: hapana.

Wakili Kibatala: umesema, mlikutana na mshtakiwa Bamaga, kwa nini mshtakiwa alikubali kuonanana wewe Bamaga?, Ni ushawishi gani ulimwambia hadi akakubali kuja?
Shahidi: alikubali tukutane Bamaga alikuwa hajui kwamba Kanumba ameshafariki, yeye ndio alinipigia simu akasema si umesema Kanumba hajafa nikamwambia ndio akasema tukutane Sinza nikasema tukutane Bamaga.

Naye shahidi wa tatu, mrakibu msaidizi wa Polisi PF 16519 ASP Ester Zefania akitoa ushahidi wake huku akiongozwa na wakili wa Serikali,  Ayoub Abood amedai, Oktoba 7, 2012 akiwa kituoni Osterbay alipewa maelekezo na Mkuu wa upelelezi Wa mkoa Wa Kinondoni Camilius wambura kwenda Sinza kwa Kanumba kufuatilia taarifa alizopata za kifo cha Kanumba.

Amedai aliondoka na askari watatu pamoja na msanii Ray ambaye aliwaongoza hadi kwa Sinza kwa marehemu ambako alikuta watu wengi wengine wakilia kuashiria hali ya msiba mahojiani yake na Wakili Abood yalikuwa hivi;

Wakili: Baada ya kufika hapo nyumbani ulifanya nini?
Shahidi : Nilijitambulisha wa watu waliokuwepo pale kuwa Mimi ni askari kutoka kituo cha polisi cha Osterbay, nikaitiwa mdogo wake Kanumba Seth, ambapo nilipomuuliza nini kilitokea alinielezea kwa kifupi.
Baada ya hapo mimi pamoja na askari 2 pamoja na Ray tulioingia chumbani kwa marehemu kwa ajali ya uchunguzi.

Wakili : Baada ya kuingia humo chumbani ulikuta hali gani? na  mliweza kuona kitu gani katika chumba hicho?
Shahidi:Kitanda kilikuwa kimevurugwa, pembeni yake kulikuwa na stuli juu yake ilikuwa na chupa ya soda aina ya Sprite, glass iliyokuwa na kinywaji nusu na chupa ya whisky ya Jackie Daniel, pia pembeni chini ya tendegu za kitanda kulikuwa na panga na pembeni yake kulionekana michirizi ya mburuzo wenye rangi kama nyeusi isiyokolea.

Wakili: Baada ya hapo nini kilitokea?
Shahidi: Nilimpigia simu kamanda Wambura na kumpatia taarifa ambaye aliniambia angetuma timu ya wapelelezi wa matukio kutoka mkoani na eneo la tukio libaki vilevile.

Wakili: Baada ya kufika wakuu wa upelelezi ulifanya nini?
Shahidi: Nilindoka nikarudi kituoni.

Wakili: Baada ya kufika kituoni ulimkuta nani?
Shahidi; Nilimkuta kamanda Wambura ambaye alinipa (task) jukumu la kumtafuta Lulu apelekwe kituoni hapo kwani kwa taarifa alizokuwa nazo atakuwa anafahamu nini kilimpata Kanumba.

Wakili: Alikupa Huyo Daktari kwa ajili gani?
Shahidi; Alinipa Daktari Paplas ili tusaidiane nae kumpata Lulu kwani ndio alikuwa akiongea naye  Mara nyingi ambapo alimpigia simu na kukubaliana kukutana nae bamaga ndipo waliweza kumkamata.

Wakili Kibatala nae alimhoji
mrakibu msaidizi wa Polisi PF 16519 ASP Ester Zefania mahojiano yao yalikuwa hivi;
 
Wakili Kibatala: Mlipomkamata Lulu mlimpeleka hospitali?
Shahidi; Ndio
Wakili Kibatala: Mlimpeleka Lulu hospitali kutibiwa nini?
Shahidi: sifahamu, sikuingi kwa kwenye chumba cha daktari.
Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba sababu ya kupelekwa Lulu kwa daktari kuwa alipigwa na ubapa wa panga mapajani na alikuwa na maumivu
Shahidi; Sifahamu.

Kesi hiyo itaendelea Oktoba 23, 2017( Jumatatu) na shahidi wa nne atatoa ushahidi wake.

DC KIGAMBONI AZINDUA MPANGO WA DARMAERT NA VIFAA VYA MAWASILIANO WAKATI WA DHARULA NA MAAFA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa utendaji kazi wa Uokoaji na Majanga
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa Mpango wa DarMaert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akikata utepe  kuashiria uzinduzi wa chumba cha Mawasiliano DarMaert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa.
 Muwakilishi wa Benki ya Dunia, Erick Dikson akizungumza mara baada ya kukabidhi  vifaa kwa tasisi ya Dar Meart kwa ajilya Majanga na uokoaji
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akizungumza na kuahidi Kiwanja kwa ajili ya Kikosi cha Zima moto mkoa wa Dar es Salaam na mpango wa DarMaert na ghala kwa ajili ya kuwasaidia katika huduma za majanga.
Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi amabye ni mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Zima Moto waliohudhuria uzinduzi wa mpango wa Dar Maert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa.

MONDULI AMKENI MAENDELEO YATALETWA MA SISI WENYEWE- GAMBO

$
0
0
 MKUU wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo yuko katika ziara ya siku mbili wilayani Monduli mkoani Arusha.Katika ziara ziara hiyo iliyoanza tarehe 20/10 /2017  Gambo ametembelea Kata ya Moita vijiji vya Kilimatinde, Moita Bwawani na Moita Kiloriti, pamoja na kutembelea miradi mbalimbali, kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo Mhe Gambo amefanya mikutano ya hadhara katika kila kijiji alichotembelea.
Mhe Gambo amehamasisha wananchi wa Kata hiyo kujiletea maendeleo yao wenyewe na akawapongeza kwa kujenga ofisi ya kata kwa nguvu zao wenyewe na akamwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kumalizia ujenzi huo na akaelekeza jengo hilo liwe limekamilika kabla ya mwezi wa kumi na mbili 2017.
"Kata hii yetu wana Moita na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe na sio kumsubiri mzungu atuletee, katika risala yenu mmesema hapo shule ya msingi Kilimatinde  kuna upungufu wa darasa moja, tutakwenda kuchanga hapahapa tujenge darasa hilo" alisema Gambo.
Katika harambee hiyo Mhe Gambo amewachangia wananchi hao bati 60, wanachi wawili wamechanga tofali 2000 kwa kutoa shilingi milioni 4 na chama cha mapinduzi wilaya kimetoa mifuko thelathini kuchangia ujenzi wa darasa hilo.
Ziara hii imezindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani, darasa lililojengwa kwa mpango wa 'Lipa kwa matokeo (P4R)'.
Mkuu wa mkoa Gambo ameambatana na wataalam kutoka sekta mbalimbali ikiwemo maji,barabara na umeme ambapo kero mbalimbali za wananchi hususan maji ndio iliyoonekana kuwa changamoto katika eneo hilo lakini wataalam wakawakikishia wananchi  kwamba serikali inafanyia kazi kilio chao na ndani ya muda mfupi tatizo hilo litakwisha katika sehemu kubwa.
Ziara hii inaendelea leo tarehe 21/10/2017 na Mhe Gambo anatembelea kijiji cha Kipok kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Kipok ambapo atafanya mikutano miwili ya hadhara na kuzungumza na wanachi wa vijiji vya Kipok na Loolera.
 Mhandisi Amboka meneja wa TARURA mkoani Arusha akitoa maelezo kwa wananchi namna wakala huo wa barabara za vijijini utakavyotoa huduma katika kata hiyo kwa mwaka huu wa fedha 2017/18.
 

 RC Gambo amezindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani,mradi huu umetekelezwa na fedha za 'Lipa kwa matokeo' P4R.
 RC Gambo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Moita Kiloriti alipokwenda kutembelea mradi wa maji unaohudumia kata hiyo.

KAMPUNI YA KILUA INDUSTRIAL GROUP YAANDAA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING,NCHINI CHINA

$
0
0
Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies imeandaa kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa  kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Mohamed Said Kilua amesema kuwa kongamano hilo linatarajia kufanyika Oktoba 25,2017 katika hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano jijini Beijing,litakalojumuisha wafanyashabiashara wamiliki wa viwanda na makampuni  wapatao 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.

“Sisi Kilua Industrial Group of Companies tumeamua  kuibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda, na kwa njia moja ama nyingine iweze kuzigeuza rasimali maliasili  kuwa bidhaa”alisema Kilua.

Tanzania iliyojaaliwa ardhi yenye rutuba kwa kilimo cha mazao ya Chakula na Biashara,haiwezi kutafsiri maendeleo hayo ya Kilimo bila kuzigeuza bidhaa zilizoandaliwa kwa soko la ndani na lile la Kimataifa bila kuwepo na viwanda vidogo/vya kati na vikubwa vitakavyozalisha bidhaa zenye viwango vyenye ubora katika ushindani wa soko”alisisitiza Kilua.
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua (pichani shoto) pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali ya mkoa wa Pwani wakipatiwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huateng Metalluargical Co.Ltd, Chunsheng Jiang (wa nne kulia) kuhusiana na michoro waliyopewa kama zawadi, ikionesha mandhari ya maeneo mbalimbali ya jiji la Beijing pamoja na shughuli zao nchini China.

Viongozi hao ni Mkurugenzi wa halmashauri Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani (kofia nyekundu), Mansouly Ally ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha, Afisa Biashara (M) Pwani Suleiman Sirindwa, Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Mhina. 

Viongozi hao wamekuja jijini Beijing nchini China kwa ziara iliyoratibiwa na Kampuni ya Kiluwa Group of Companies,chini ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wake Mohamed Said Kiluwa (mwenye koti la njano). 
Aidha baada ya kukutana leo viongozi hao pamoja na wadau wakuu wa mambo ya viwanda nchini China, ambapo Oktoba 25 kutakuwepo na Kongamano utakaohusu masuala ya viwanda,utakaojumuisha wadau wapatao 200 kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhina akikata kipande cha nyama ya Mbuzi,ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha wageni na wenyeji kwenye chakula cha jioni kiliochoandaliwa na wenyeji wa Beijing,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua,kulia ni Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja na Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga wakishuhudia tukio hilo usiku huu.  
 Baadhi ya wenyeji ambao nao wanatarajiwa kushiriki kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika Octoba 25,2017 chini ya Uratibu mkubwa wa kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies,jijini Beijing nchini China chin
 Wageni wakiandaliwa chakula jioni


Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images