Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1400 | 1401 | (Page 1402) | 1403 | 1404 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Na: Fatma Salum (MAELEZO)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa hana mpango wa kufuta mbio za mwenge wa uhuru kutokana na madai ya baadhi ya watu wanaosema kwamba hauna faida.

  Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Zanzibar alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

  “Mwenge wa Uhuru hatutaufuta kwa sababu unachochea maendeleo, katika kipindi cha uongozi wangu na Dkt. Shein Mwenge utaendelea kukimbizwa nchini kote,” alisisitiza Rais Magufuli.Alisema kuwa baadhi ya watu wanaodai kwamba mwenge huo unaleta hasara kutokana na gharama zinazotumika, wazingatie kuwa bajeti ya kukimbiza mwenge ni ndogo ukilinganisha na faida kubwa inayopatikana kupitia miradi inayotekelezwa kutokana na hamasa ya mbio za mwenge kwenye maeneo mbalimbali kote nchini.

  Aidha alibainisha kuwa mwenge wa uhuru ni moja ya tunu za nchi ya Tanzania na alama ya uhuru na utaifa wetu hivyo kuufuta ni sawa na kufuta alama kubwa inayotambulisha nchi yetu.“Mwenge huu unatuunganisha watanzania na kuimarisha muungano wetu na yeyote atakayejaribu kuharibu amani au kuvuruga muungano tutapambana naye,” alisema Rais Magufuli.

  Akizungumzia kuhusu kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Nyerere, Rais Magufuli alisema kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuyaenzi kwa vitendo mambo yote mazuri yaliyoachwa na muasisi huyo wa taifa letu ili tuweze kuwa na Tanzania yenye maendeleo.Alisema kuwa Mwl. Nyerere ameacha mengi mazuri hivyo ni mfano wa kuigwa katika nchi yetu kwa sababu alikuwa ni mzalendo, mpigania uhuru, mpenda amani, haki na usawa kwa wote.

  “Serikali zote mbili zimejipanga kuyasimamia na kuyatekeleza mambo yote mazuri yaliyoachwa na waasisi wa nchi hii Mwl. Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuwa uzalendo wao na mapenzi mema kwa taifa letu vimeweza kutufikisha hapa tulipo,” alisema Rais Magufuli.Akizungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika Serikali ya Awamu ya Tano Rais Magufuli alisema kuwa baada ya Serikali kuchukua hatua za kudhibiti sekta ya madini uzalishaji umeongezeka ikiwemo almasi na tanzanite.

  Aidha alibainisha kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), mwaka 2017 miradi 271 ya uwekezaji imeanzishwa yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.4. Alisema kuwa ana uhakika Tanzania itafanikiwa kufikia uchumi wa kati kwa kuwa viwanda vingi vinaendelea kujengwa na Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili tuweze kufika tunapokusudia.

  Akitoa taarifa kwa Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama alisema kuwa miradi 151 yenye thamani ya shilingi bilioni 569.8 imezinduliwa na mbio za mwenge kwenye Halmashauri na Mikoa mbalimbali nchini.

  Aidha alieleza kuwa miradi 21 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 ilibainika kuwana kasoro ikiwemo ubadhirifu wa fedha za umma hivyo haikuzinduliwa. Mbio za Mwenge wa uhuru zilizinduliwa mapema mwaka huu mkoani Katavi na kilele chake kimefanyika Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

  0 0

  Na TIGANYA VINCENT-RS-TABORA

  SERIKALI mkoani Tabora imesitisha likizo kwa muda kwa Maafisa Ugani na Watumishi wote wanaowatakiwa kuwasaidia wakulima ili waweze kulima kilimo kinachozingatia utalaamu kwa ajili ya kuwawezesha kuzalisha mazao mengi na kwa tija.

  Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo na Seketarieti ya Mkoa huo.

  Alisema kuwa wakati msimu wa mvua unakaribia kuanza sio vema watumishi wa kada hiyo wakaanza likizo kwani wanapaswa kutumia kipindi hicho kuwafanya kazi ya kuwasaidia na kuwaelimisha wakulima ili wafanye vizuri katika shughuli zao na kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kupitia mavuno mazuri watakayopata.

  Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa likizo ni haki ya mtumishi inabidi wazingatie kuwa likizo zao haziathiri wakulima katika kipindi hiki muhimu kwa ajili ya kilimo.Alisema kuwa baada ya shughuli za kilimo kukaa vizuri Maafisa hao wanaweza kuendelea na likizo zao ikiwa watakuwa wamehakikisha kuwa kwenda kwao likizo hakutakuwa na athari kwa wakulima.

  Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewaagiza Maafisa Ugani wote kuondoka maofisini na kwenda kwa wakulima katika kipindi hiki ili kuhakikisha kila mkulima anazingatia kanuni bora za kilimo kulingana na mazao anayolima.Alisema kuwa lengo ni kutaka Mkoa wa Tabora uwe mfano wa kuigwa katika ulimaji wa kilimo cha kisasa na chenye tija.

  Mwanri alisema kuwa katika msimu ujao wa kilimo Mkoa wa Tabora umepanga kulima mazao ya Pamba, Tumbaku na Korosho kama mazao ya biashara na alizeti kwa ajili ya kuvutia wawekezaji katika viwanda vya mafuta.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo aliunga mkono hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ya kusisitisha likizo za Maafisa ugani na kusema kuwa Maafisa hao kazi zinapendeza wakati wa msimu wa kilimo na sio wakati mwingine.Alisema kuwa anatumaini Maafisa hao watalipokea agizo hilo kwa mtazamo chanya kwa kuwa ni sehemu nzuri ya kuonyesha kuwa wao wapo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima na hasa wanapoanza shughuli zao.

  Aidha Mkuu wa Wilaya huyo alisema kuwa mwaka huu wanataka kufanya mapinduzi ya kilimo kwa kuwaondoa Wataalamu hao kutoka Ofisi kwenda vijijini kuwasaidia wakulima ili adhima hiyo ifanikiwe.Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema kuwa hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kusimamisha likizo hadi katika kipindi cha Krismas (X-Mas) kinalenga kuongeza tija kwa wakulima kwa Maafisa Ugani kuelekeza nguvu zaidi katika kuwa karibu na wakulima zaidi katika kipindi hiki.

  Alisema kuwa lengo la agizo hilo linakusudia kuhakikisha kuwa Mkoa wa Tabora unazalishaji mazao ambaye yamepewa kipaumbe kwa wingi na tija ili kuhakikisha wakulima wananufaika na shughuli zao na kuondokana na umaskini.

  Kikao hicho cha siku tatu kilienga kujengeana uwezo na kukumbusha majukumu ya kila mtumishi wa mkoa wa Tabora wakiwemo Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi, Wakuu wa Idara , Wakuu wa Vitengo na Seketarieti ya Mkoa.

  0 0

   Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, leo Oktoba 14, 2017
   Wahandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, leo Oktoba 14, 2017

  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, Mtwara
  WAHANDISI na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wanapambana usiku na mchana kuzifanyia matengenezo mashine za kufua umeme, ili kuondoa tatizo la kukosekana kwa umeme kwa vipindi virefu kila siku kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.

   Akizungumza mjini hapa leo Oktoba 14, 2017, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia Uzalishaji, Mhandisi Kaitwa Bashaija, (pichani juu), amesema kwa sasa Wahandisi na mafundi wa shirika hilo wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kutengeneza mitambo hiyo na hivyo kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

  K-VIS BLOG ilishuhudia mafundi hao wakifanyakazi ya kurekebisha mitambo hiyo katika kituo cha kuzalisha umeme wa kutumia gesi asilia mkoani Mtwara leo Oktoba 14, 2017.

  “Mitambo hii ina kiasi cha mika 10 tangu ifungwe, na kadiri miaka inavyokweda ndivyo ongezeko la uhitaji wa umeme hususan mkoani Mtwara linazidi kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi,” Alisema Mhandisi Bashaija.

  Alisema, miaka michache iliyopita baadhi ya mitambo iliweza kuzimwa na bado hali ya umeme ilikuwa imara.Wiki iliyopita Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani aliagiza TANESCO kufanya juhudi za ziada kuhakikisha tatizo la umeme mkoani Mtwara na Lindi linapatiwa ufumbuzi wa haraka.

  Kutokana na hali hiyo Naibu Mkurugenzi huyo wa TANESCO, alisema kuwa kwa sasa wana mipango ya muda mfupi na mrefu katika kuhakikisha wanaimarisha miundombinu ya umeme katika mikoa ya kusini.

  Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, alisema kuwa licha ya changamoto hiyo kwa sasa bado mitambo iliyopo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme katika mikoa hiyo.

  “Pamoja na hali hii lakini kwa sasa tunakwenda vizuri kiasi ila si sana maana umeme kuna wakati unarudi na kukatika. Na tunaamini tutafanikiwa kurudi katika hali ya kawaida na kikubwa tunawaomba wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kutuvumilia kwani nasi tunajua umuhimu wa umeme katika shughuli za uzalishaji.” Alitoa rai Mhandisi Chinumba.


   Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, akizungumzia hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi wa haraka.
   Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia mkoani Mtwara Oktoba 14, 2017.


   Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia zualishaji umeme, Mhandisi Costa
   Msanifu gazeti wa gazeti la Mwananchi, Bi. Lilian Timbuka akiuliza swali.
   Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, akizungumzia hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi wa haraka. Kulia ni Mhandisi Bashaija.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Shirika la Ugavi la Umeme (TANESCO), TANESCO Saccos Ltd, Somoe Nguhwe akiwasilisha ripoti ya mwaka ya saccos hiyo, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka, uliofanyika katika Ukumbi wa LAPF Kisenga jijini Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE/JOHN BADI/DAILY MITIKASI BLOG 
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James akifungua mkutano huo. 
  Sehemu ya Wanachama wa Saccos hiyo, kutoka mikoa yote ya Tanzania wakiwa katika mkutano huo. 
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James akikabidhi Tuzo ya Mwanachama Bora wa Mwaka 2017 kwa Mwanachama Sabina Daati. 
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James akikabidhi Tuzo ya Mwanachama Bora wa Mwaka 2017kwa Mwanachama Renatus Mfilinge. 
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James na Viongozi wa Saccos hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo ya Mwanachama Bora 2017.

  0 0


  0 0

  Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kushoto) wakiwa katika mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo Bw. Amadou Hott, (wa tatu kulia), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati, Bw. Amadou Hott (kushoto) akisikiliza kwa makini wakati wa mkutano na Waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) mkoani Dodoma, kulia ni Mkurugenzi wa benki hiyo anayeshughulika masuala ya maendeleo ya mifumo ya umeme, Bw. Henry Baldeh.
  Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakiwa katika mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) mjini Dodoma.


  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) akichukua kumbukumbu wakati wa mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) (hawapo pichani) kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga, mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dorothy Mwanyika (kulia), akichukua kumbukumbu wakati wa mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) (hawapo pichani) kushoto ni Kamishna wa Bajeti wa Wizara hiyo Bi. Marry Maganga akisikiliza kwa makini wakati mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.


  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati, Bw. Amadou Hott (kushoto), akifurahia jambo wakati wa mkutano uliowahusisha viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Mipango (hawapo pichani) wenginie ni sehemu ya ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) walioshiriki mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.


  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia), akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati Bw. Amadou Hott baada ya kumaliza mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (wa nne kulia) na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati Bw. Amadou Hott (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo na ujumbe wa benki hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia), akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.


  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati, Bw. Amadou Hott wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango


  …………….

  Benny Mwaipaja, Dodoma

  MAKAMU wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, anayeshughulikia masuala ya nishati Bw. Amadou Hott amesema kuwa Tanzania iko katika njia sahihi kutaka iwe na asilimia 16 ya hisa kwenye miradi inayowekezwa katika sekta ya madini na mafuta ili rasilimali hizo ziweze kuwanufaisha wananchi na wawekezaji.

  Makamu huyo wa Rais ametoa kauli hiyo mjini Dodoma alipofanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kuhusu namna benki hiyo inavyoweza kusaidia kulikwamua Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kutoka katika mzigo wa madeni unaolikabili ili liweze kujiendesha kibiashara bila kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.

  Alisema kuwa nchi kadhaa duniani, zenyewe ama kwa kutumia kampuni ilizoziteua zina hisa ya kati ya asilimia 14 hadi 16 za hisa za bure katika miradi ya rasilimali za madini ili pande zote zinazohusika katika mikataba hiyo ziweze kunufaika na rasilimali za nchi.  Alitolea mfano wa baadhi ya nchi ikiwemo Senegal ambazo zinatekeleza sera kama hizo na hakuna matatizo yoyote kati ya nchi hizo na wawekezaji na kwamba anaona nia njema ya Tanzania katika kulinda rasilimali zake.

  “Jambo la msingi linalotakiwa ni kuhakikisha kuwa makubaliano ya suala hili kati ya Serikali na Sekta binafsi yawe ya wazi, usawa na haki na ni muhimu wawekezaji wakakubaliana na utaratibu huo” aliongeza Bw. Hott.

  Hivi karibuni kumekuwa na mjadala baada ya mwekezaji mkubwa, Bilionea Aliko Dangote kunukuliwa na vyombo vya habari nchini uingereza akiitahadharisha Serikali kuhusu uamuzi wake wa kuchukua hisa 16 za bure katika sekta ya madini na mafuta kwamba utawatisha wawekezaji.

  Akizungumzia deni la TANESCO, Hott alisema kuwa Benki yake inakusudia kuipatia Tanzania kiasi cha dola milioni 200 za Marekani ili iweze kupunguza deni la dola zaidi ya milioni 370 ambazo Shirika hilo linadaiwa na taasisi mbalimbali ili liweze kujiendesha kibiashara.

  Akizungumza yaliyojiri kwenye kikao na mgeni wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango ameishukuru Benki hiyo kwa misaada mbalimbali na mikopo yenye mashari nafuu inayoipatia Serikali, ambapo katika sekta ya nishati peke yake, kufikia mwaka 2019, itakuwa imetoa zaidi ya Dola bilioni 1.1.

  “Tunaendelea kujadiliana namna bora zaidi ya kutekeleza masharti yaliyomo kwenye fedha hizo dola milioni 200 ambazo benki hiyo imeonesha nia ya kuipatia Serikali ili iweze kupunguza madeni ya TANESCO yanayofikia Dola milioni 370” alisema Dkt. Mpango

  Dkt. Mpango alisema kuwa Benki hiyo pia imeionesha nia ya kusaidia utekelezi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Stieglers Gorge utakaozalisha megawati 2,100 ambao utakuwa mkombozi mkubwa wa mapinduzi ya viwanda.

  “Lakini pia AfDB wamekubali kutupatia fedha za kujenga awamu ya kwanza ya miundombinu ya kusafirisha umeme wa ukanda wa Kaskazini Magharibi, unaoanzia Mbeya, Sumbawanga hadi Nyakanazi, kiasi cha Dola za Marekani milioni 123 na benki hiyo inajadiliana na Shirika la Maendeleo la Korea ili itupatie kiasi kingine cha Dola milioni 60 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo” Alisema Dkt. Mpango

  Aidha, Benki hiyo itafadhili mradi wa umeme unaotumia joto ardhi (geothemo) kwenye ukanda wa Bonde la Ufa wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 91 lakini wao watatoa Dola milioni 65.

  “Miradi mingine ya nishati itakayofadhiliwa na Benki hiyo ni ule ulioko Kakono, Mto Maragarasi wenye uwezo wa kuzalisha megawati 44.5, mkopo ambao unatarajiwa kupatikana ifikapo Novemba, 2018 na tumekubaliana mradi huu uweze kutekelezwa haraka iwezekanavyo” Alifafanua zaidi Dkt. Mpango

  Alisema kuwa mradi mwingine utaotekelezwa na Benki hiyo ni mradi mkubwa wa kupeleka na kusambaza umeme kwenye miji mikuu yote hapa nchini unaogharimu Dola milioni 274, unaotarajiwa kukamilika ifikapo Julai, 2019 ili miji hiyo iweze kuchochea uwekezaji wa viwanda kwakuwa na nishati imara na ya bei nafuu.

  Dkt. Mpango aliisifu Benki hiyo kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania na kwamba uhusiano huo utaendelea kuimarishwa kwa faida ya pande hizo mbili.

  0 0

  Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka wa Meneja Uzalishaji wa Mbegu,Pheneas Chikaura(kulia) katika Kiwanda cha Kuzalisha mbegu za pamba cha Quton wakati wa ziara yake kiwandani hapo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.


  Waziri wa Kilimo, Mhe.Charles Tizeba akikaribishwa na Mkurugenzi wa Quton Tanzania Limited Ndg.Pradyumansinh Chauhan, alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Mbegu za Pamba cha Quton kilichopo kata ya kasoli Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
  Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, Ndg. Boazi Ogola(wa pili kushoto) akimuongoza Waziri wa Kilimo, Dkt.Charles Tizeba (aliyeweka mkono kifuani) na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu kuelekea kuona kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri huyo Mkoani Simiyu.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited, Ndg.Pradyumansinh Chauhan akitoa taarifa ya uzalishaji wa mbegu za pamba zilizotolewa manyoya katika kiwanda cha kampuni hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.


  …………..


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt. Charles Tizeba amewataka wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba mbegu kwenye kiwanda cha kuchakata(kutoa manyoya) mbegu za pamba cha Quton na akasema watakaogoma kupeleka hawatanunua pamba msimu ujao.

  Waziri Tizeba ameyasema hayo jana alipotembelea kiwanda hicho katika Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa lengo la kujionea hali ya uzalishaji wa mbegu ya pamba inavyoendelea.

  Amesema suala la wenye viwanda vya kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba mbegu katika kiwanda cha kuchakata mbegu za pamba(kuondoa manyoya) siyo la hiari na walishapewa maelekezo, hivyo wanapaswa kupeleka pamba mbegu katika kiwanda cha Quton ili zitolewe manyoya na baadaye zipelekwe kwa wananchi.

  “ Nimeambiwa watu wa Quton wanashindwa kufanya kazi kwa shift tatu kwa siku kwa sababu walio na mbegu kwenye viwanda vyao vya kuchambua pamba hawataki kuleta pamba hapa, wakati wanayo maelekezo na hii siyo hiari mbegu ikishatengwa na Bodi ya Pamba si yao” alisema Tizeba.

  “Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nakuagiza wapelekee ujumbe huu kwamba ginner atakayegoma kuleta pamba mbegu hapa Quton hanunui pamba mwaka kesho, wanapaswa walete mbegu zitolewe manyoya ziende kwa wananchi ili wapate mbegu bora, katika hili sitabembelezana na mtu” alisisitiza Tizeba.

  Aidha, Mhe.Waziri amesema mahitaji ya mbegu ya pamba iliyotolewa manyoya kwa nchi nzima ni takribani tani 8000, hivyo ili kufikia kiwango hicho katika siku zilizobaki kuelekea msimu wa kilimo cha pamba, kiwanda cha Quton kinapaswa kufanya kazi saa 24 kwa kuwa uzalishaji wa sasa wa tani 60 hadi 65 kwa saa 16 kwa siku hautaweza kufikia lengo hilo.

  Wakati huo huo Waziri Tizeba ametoa wito kwa wananchi Mkoani Simiyu kutopanda pamba sasa kwa kuhofia mvua kukatika mapema, badala yake wasubiri taarifa rasmi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa juu ya hali ya mvua katika ukanda huo itakayotolewa muda mfupi ujao,ambayo baadaye itatumika kuwashauri wakati muafaka wa kupanda, japo alieleza kuwa taarifa ya jumla ya utabiri wa hali ya hewa inaonesha mvua itanyesha juu ya wastani.

  Pia Mhe.Waziri amewahakikishia wananchi kuwa bei ya mbolea imeshuka, hivyo akawataka wataalam wa Kilimo kuwaelimisha wananchi juu ya bei elekezi ya mbolea kwa kila wilaya, ili wasiuziwe kwa bei kubwa na akasisitiza kuwa bei ya mbolea na mbegu mwaka 2018 itapungua zaidi kwa kuwa Serikali imefuta takribani kodi 80 katika kilimo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amesema Mkoa wa Simiyu unazalisha pamba kwa wingi, ambapo katika msimu wa mwaka 2016/2017 umezalisha takribani asilimia 65 ya pamba ya nchi nzima, hivyo akaomba wananchi wa mkoa huo wasaidiwe kupewa mikopo ya zana bora za kilimo na pembejeo nyingine kupitia mfuko wa pembejeo ili kuongeza uzalishaji zaidi.

  Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited Ndg. Pradyumansinh Chauhan amemuomba Waziri wa Kilimo kuhamasisha wananchi kutumia mbegu za pamba zilizotolewa manyoya ili kuongeza uzalishaji kwa kuwa hazishambuliwi kwa urahisi na magonjwa na zinapunguza kiasi cha mbegu kinachotumika shambani ambapo kilogramu sita tu hutumika kwa hekali wakati zenye manyoya hutumika hadi kilogramu 15.

  0 0

  3RD ANNUAL TEF ENTREPRENEURSHIP FORUM WAS HELD ON OCTOBER 13-14 IN LAGOS
  1,300 AFRICAN SMEs, POLICYMAKERS, INCUBATORS FROM 54 COUNTRIES IN ATTENDANCE
  Lagos, Nigeria, October 16, 2017 – The Tony Elumelu Foundation (TEF), Africa’s leading philanthropy dedicated to supporting entrepreneurship, concluded its 3rd annual TEF Entrepreneurship Forum on 14th of October 2017 in Lagos.

   
  The Forum hosted more than 1,300 participants from 54 African countries. The most diverse and inclusive gathering of African entrepreneurs on the continent, the Forum continued its strong tradition of showcasing innovation across sectors, including Agriculture, Technology, Healthcare, Fashion and Energy/Power Generation.

  Launched in 2015, the Forum was born out of the Foundation’s $100 million commitment to identify, train, mentor and fund 10,000 African entrepreneurs, over a decade, through the TEF Entrepreneurship Programme.

  During a powerful keynote address, Tony O. Elumelu, CON, the philanthropist and Founder who is also the Chairman of the United Bank for Africa, spoke of his belief, that a vibrant African-led private sector is the key to unlocking Africa’s economic and social potential.

  “Africa’s development, which must be private-sector led and entrepreneurially driven, will have at its heart, young African innovators and their transformative ideas.  Only they will create the millions of jobs Africa needs. The Forum has brought together Africa’s most important developmental force, her young entrepreneurs who will become catalysts for Africa’s economic liberation.

  We have united the African entrepreneurship ecosystem, putting the entrepreneurs at centre stage. I want to thank those heads of government and other key policymakers, who have supported our firm belief that the private sector is the engine for growth and the private sector players, who are models of our philosophy of Africapitalism – the idea that business will drive change and that change must deliver economic and social wealth” he explained.

  The two-day event, which involved plenary panels and masterclasses, provided theTony Elumelu Entrepreneurs with a platform to network and connect with business leaders, policymakers and investors.

  Focusing on the Forum’s theme of training and mentoring, speakers discussed topics that educated, empowered and inspired the entrepreneurs, addressing the key stages needed to successfully launch a business.

  The speaking programme emphasised the Foundation’s role of uniting entrepreneurs and policymakers, as a means of ensuring that private and public sectors work together to create the best possible operating environment for entrepreneurship to thrive. Political and private sector leaders from across Africa, including HE Aminu Bello Masari, Governor, Katsina state; HE Abdul’aziz Abubakar Yari, Governor, Zamfara state; Mr. Lionel Zinsou, Former Prime Minister, Republic of Benin; Oba Otudeko, Chairman, Honeywell Group; Alhaji Aliko Dangote, Chairman, Dangote group, directly addressed the conditions needed for stimulating entrepreneurial growth, whilst senior members of global development institutions, including Wale Ayeni, Senior Investment Office, International Finance Corporation; Stephen Tio Kauma, Director Human Resources, Afrexim Bank and Andre Hue, Deputy Country Director, Agence Française de Développement, spoke of a new paradigm, driven by the need for a private sector-led change.

  “The private sector working with the public sector can achieve so much by way of development. African governments should move beyond rhetorics and implement their ideas,” Oba Otudeko enthused.

  Addressing the 3rd cohort of TEF entrepreneurs the Vice President of Nigeria, Professor Yemi Osinbajo said: “This generation of young people will do the exceptional. You are the reason Africa will work. The length and breadth of display of talent have shown that there is indeed hope”.

  The Forum also witnessed multiple partnerships between United Nations Development Programme (UNDP) and the Foundation, and between French bilateral development bank, Agence Française De Développement (AFD) and TEF. 

  Commending both agencies for their commitment to promoting youth entrepreneurship in Africa, Elumelu called on other individuals and developmental institutions to partner with the Foundation and expand the scale of its impact. “We call on friends of Africa to partner with the Foundation, to scale our impact beyond the 1,000 entrepreneurs a year. Real opportunity exists to tap into Africa’s potential and our entrepreneurs offer a gateway to participating in both economic success and creating social wealth”.

  TEF partners including Microsoft, Sage One and Greentec also held training workshops and side events aimed at approaches to strategically scale up business. The United Bank for Africa (UBA) has proudly supported the forum.

  ####

  About TEF

  Founded in 2010 by philanthropist Tony O. Elumelu CON, The Tony Elumelu Foundation is one of the foremost African philanthropic organisations. The Foundation believes that the private sector holds the key to unlocking Africa’s economic potential.

  On Twitter: @TonyElumeluFDN 

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitembea kwenye mitaa ya Stone Town mjini Zanzibar wakielekea katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa ajili ya ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakipokewa na Askofu Augustine Shayo walipowasili  katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa ajili ya ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa wakishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na mtoto Goodluck Cosmas Ndulu wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili wakishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na mtoto Goodluck Cosmas Ndulu wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili wakishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa wakishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Augustine Shayo katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Augustine Shayo katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli akiombewa na Askofu Augustine Shayo katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na Askofu Augustine Shayo na watawa vkatika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na Askofu Augustine Shayo na watawa vkatika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitembea kwenye mitaa ya Stone Town mjini Zanzibar wakielekea katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa ajili ya ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.PICHA NA IKULU

  0 0

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wakulima na wafugaji wa vijiji vinne alivyotembelea vya wilaya ya Mkuranga kuondokana na tofauti zao na badala yake wapendane.

  Hayo aliyasema katika ziara yake kwa wananchi wa jimbo lake la Mkuranga-Pwani ambapo aliweza kuelezwa kero mbalimbali na kuahidi kuzishughulikia.

  Katika ziara hiyo pia aliweza kuchangia jumla ya fedha kiasi cha shilingi Mil.6 pamoja na mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati zilizomo katika vijiji hivyo.

  Aidha pia amewaomba wananchi kuunda vikundi mbalimbali vya ujasiriamali hususani ufugaji wa kuku samaki na mifungo mbalimbali ili kuwawezesha kuondokana na umaskini.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega ambaye ni Mbunge wa Mkuranga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyanduturu akiwa ni ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji cha Nyanduturu kata ya Nyamato ambayo pia amechangia Millioni moja na nusu pamoja na saruji 50 ili kufanikisha ujenzi huo unaoendelea.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wakazi Wa kijiji cha Mvuleni kata ya Nyamato wakati wa ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake katika wizara hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ambapo aliwachangia Shilingi milioni moja na nusu pamoja na mifuko 50 ya saruji kufanikisha zahanati inayojengwa kijijini hapo.
  Mwenyekiti wa kijiji cha Mvuleni,Mohammed Mpunjika akimkabidhi risala yao Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipofanya ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa kijiji cha Mvuleni jana alipofanya ziara yake ya kwanza kijijini hapo.
  Mmoja wa akina mama kutoka katika kijiji cha Tipo kata ya Nyamato akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati alipofanya ziara yake .
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga,Ally Mohammed akizungumza jambo.
  Naibu Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiteta jambo na baadhi ya wamasai ambao ni wafugaji katika kijiji cha Kifumangao kabla ya mkutano wake kuanza hapo jana.
  Naibu Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika jengo linalojengwa la zahanati ya Kifumangao ambapo ametoa zawadi ya fedha miliono moja na nusu pamoja na saruji mifuko 50. Jana katika ziara yake hiyo kwa vijiji vinne amechangia jumla ya mifjko 200 ya saruji pamoja na jumla ya fedha milioni sita.


  Muonekano wa jengo hilo.

  0 0

  Na Jumia Travel 

  TAKRIBANI wadau 150 wa sekta ya utalii wa ndani na nje ya Tanzania wameshiriki kwenye Maonyesho ya tatu ya Kimataifa ya Utalii (SITE – Swahili International Tourism Expo) yaliyofanyika kuanzia Oktoba 13 mpaka 15 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) yamefanyika kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake kwa mara ya kwanza mwaka 2014 ambapo idadi ya washiriki imeonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa na kuvutia mataifa zaidi ya 13 kama vile Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda, Rwanda, Malawi, Mauritius na Shelisheli.

  Maonyesho hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo waziri mpya kwenye sekta ya utalii na maliasili nchini, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangala.
  Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo Makamu wa Rais alibainisha kwamba sekta ya utalii nchini imekuwa na mchango mkubwa kwenye pato la taifa kwani inachangia jumla ya asilimia 17 na hivyo kuifanya mojawapo ya sekta muhimu katika kukuza uchumi wa nchi. Mbali na hapo sekta hiyo inatarajia kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka milioni 1.2 mpaka kufikia milioni 2 kufikia mwaka 2020.

  Akitoa ushuhuda wake baada ya kutembelea Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro siku chache zilizopita, ambapo kihistoria sehemu hiyo ndimo yanapatikana mabaki ya binadamu wa kwanza kuwahi kuishi duniani, alisema kuwa Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vya kitalii vya kila aina ambavyo ni nadra kupatikana sehemu zingine duniani. Kuwepo kwa vivutio vingi kumepelekea kutajwa na taasisi, mitandao na majarida mbalimbali duniani ikiwemo mtandao wa SafariBookings ambao umeitaja Tanzania kuwa ni kinara kwa kutembelewa zaidi na watalii barani Afrika.
  Kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala alibainisha kuwa ili sekta hiyo iendelee kukuwa na kufikia malengo iliyojiwekea ni lazima kufanyiwa marekebisho, yakiwemo kufungiwa mfumo wa kieletroniki utakaofanikisha uongezaji kasi ya mapato huku akiwatoa hofu watalii juu ya upatikanaji wa vibali vya viza ambapo amesema vitakuwa vikitolewa kwa muda wa nusu saa.

  “Kuna changamoto kidogo ya upatikanaji wa viza kwa watalii wanaowasili hususani muda wanaochukua pale wanapofika uwanja wa ndege kusubiria mpaka kuipata. Na hili ni eneo ambalo tunakusudia kuwekeza zaidi na kupitia huu mfumo jumuishi wa mtandao wa mawasiliano wa serikali tutaweza kupunguza muda wa kusubiria kupata viza mara watalii wanapowasili uwanja wa ndege,” alisema na kuhitimisha Waziri huyo mpya wa Maliasili na Utalii, “Na ni eneo ambalo kwa kweli ili kufanikiwa tunakusudia kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kufanya maboresho.”
  Jumia Travel ni miongoni mwa wadau wa sekta ya utalii walioshiriki kwenye maonyesho hayo ya kimataifa ya utalii kwa mara ya kwanza ambayo kwa kiasi kikubwa huwakutanisha washiriki wa ndani na kimataifa pamoja.

  Akizungumzia juu umuhimu wa maonyesho kama hayo nchini, Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo inayojihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika na duniani, Bw. Kijanga Geofrey amesema kuwa ni fursa kubwa kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kukutanishwa kwa pamoja na kushirikishana shughuli wanazozifanya na namna ya kusonga mbele zaidi.
  “Ni mara ya kwanza sisi kushiriki kwenye maonyesho haya ya kimataifa ya utalii na yametupatia fursa kubwa ya kukutana na wadau wengine ambao kwa namna moja ama nyingine shughuli zetu zinahusiana kwa kiasi kikubwa. Sekta ya utalii ina mlolongo wa shughuli nyingi na mojawapo wa shughuli hizo ni malazi, na hapo ndipo Jumia Travel tunapoingia na kurahisisha huduma hiyo kupatikana wakati na muda wowote ili mradi kuwepo na mtandao wa intaneti, aidha kwa kutumia kompyuta, tabiti au simu ya mkononi,” alisema Bw. Geofrey.
  “Uwepo wetu hapa umetupatia fursa ya kukutana na wadau ambao tunafanya nao kazi, tunaotamani kufanya nao kazi na wengine ambao wanatusikia lakini hawakuwa wanafahamu namna ya kutufikia. Hivyo basi tumepata fursa ya kukutana nao na kubadilishana mawazo ya namna ya kukuza ushirikiano zaidi ili kuifanya sekta ya utalii ni ya kuvutia zaidi nchini Tanzania hususani huduma za malazi. 

  Kwa sababu miongoni mwa jambo ambalo huwakwamisha watanzania wengi kusafiri na kutalii sehemu mbalimbali nchini ni gharama za juu za malazi. Lakini sisi tunataka kuwaaminisha kwamba suala hilo siyo la kweli kwani malazi yapo ya kila aina kukidhi kipato cha kila mtu na siyo kama wao wanavyodhani,” alihitimisha Meneja huyo wa Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Tanzania.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwakaribisha vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwakaribisha vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwakaribisha vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipakua chakula na mmoja wa vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru aliowaalika kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017.
   Picha ya pamoja


  0 0


  Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
  Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
  Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
  Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
  Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
  Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwa jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
  Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwapandisha mori mashabiki wake walioamua kupanda  jukwaani na kuonyesha uhodari wao wa kucheza muziki huo, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
  Dansa wa Dula Makabila akionyesha umahiri wake wa kucheza Singeli
  Vijana wa kundi la Mkubwa na Wanawe wakishambulia jukwani
  Msanii wa muziki wa Singeli akionyesha umahiri wake wa kuteka mashabiki
  Wachezaji wa timu zilizoshiriki kunogesha tamasha hilo wakichuana vikali kuwania mpira. 
  Wachezaji wa timu zilizoshiriki kunogesha tamasha hilo wakichuana vikali kuwania mpira.
  Mchuano mkali wa soka kwenye tamasha hilo
  Wanamuziki wa bendi ya TOT Plus wakishiriki kunogesha tamasha hilo. Kulia ni kiongozi wao Abdul Misambano
  Mcheza shoo wa TOT Plus Gabriel Romao maarufu kwa jina la Matukutuku akionyesha uwezo wake jukwaani
  Matukutuku wa TOT akicheza hadi kwa kichwa chini kukata kiu ya machabiki kwenye tamasha hilo
  KatamuTamu wa TOT Plus akionyesha uwezo wake wa kucheza shoo jukwaani
  Mtangazaji wa Uhuru FM Kigwa akichangasha jukwaa
  "Mashabiki piga keleeeee" Kigwa akihamasisha uchangamfu kabla ya Vijana Jazz kupanda jukwaani
  Waimbaji wa Vijana Jazz wakiimba kwa hisia kali kudhihirisha kuwa muziki wa dansi bado una nafasi na mashabiki wake wapo.
  Kijana Saamata Hussein wa Vijana Jazz akionyesha umahiri wa 'kukaanga chips' jukwani
  Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Dansi, Anna Mwaole akionyesha bado wamo, wakati akiimba na bdndi hiyo ya Vijana jazz. Anasema yeye ni Kongoro la supu lisiloisha utamu na pia ni kisu cha mgema
  Cosmas Adilian na Mohammed kandera wakionyesha umahili wa kupuliza tarumpeta katika bendi hiyo ya Vijana Jazz
  Shabiki akionesha 'kuguswa maisha yake' na burudani zilizokuwa zikimimika kutoka makundi mbalimbali kwenye tamasha hilo
  Mwimbaji wa Mwenge Jazz Shukuru Majaliwa akionyesha hisia zake wakati akiimba kibao cha siku nyingi cha Zena.
  Mwenge Jazz wakishambulia jukwaa
  Mwimbaji wa Mwenge Jazz akikoleza kwa kusakata muziki jukwaani
  Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akifurahia jambo na mwenzake wakati wa tamasha hilo, kabla ya kuanza utambulisho wa baadhi ya watangazaji wa kituo hicho cha radio
  Mtangazaji waa Kipindi cha Uhuru Fleva ambacho ndicho kilikuwa mwenyeji wa tamasha hilo, Saidi Ambua, akimtambulisha Mtangazaji Steven Mhina Dungumalo
  Akiendela kumtambulisha Mhina
  Mhina akisalimia
  Mhina akazungumza kisha utambulisho ukaendelea kwa wengine
  Mwajuma Yamka wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba akiwa na Meneja rasiliamali watu wa Uhuru FM Paul Mg'ong'o kwenye tamasha hilo
  Sabrina Kado akitoka kupoza koo na Wanamuziki wenzake
  Ambua akiteta jambo na mwanamuziki nguli Hussein Jumbe kwenye tamasha hilo
  Angel Akilimali akiwa na Mwanamuziki Isha Mashauzi kwenye tamasha hilo
  Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa na Hussein Jumbea na Isha Mashauzi
  Paul Mng'ong'o akisalimiana na Kiongozi wa FM Academia Nyoshi El Saadat
  Ma DJ John Dilinga na Fast Edie wakiwa kwenye tamasha hilo
  Msondo Ngoma wakiwa jukwaani kwenye Tamasha hilo
  Romanus Mng'ande aka Romario akifanya vitu vyake na Bendi ya Msondo
  Pince Muumini Mwinjuma akiwa na Wanamuziki wake kwenye tamasha hilo
  Mwanamama akitafuta wateja wa Ming'oko kwenye tamasha hilo la Gusa Maisha yao
  Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM kwenye tamasha hilo
  Wananchi waliohudhuria tamasha hilo la 'Gusa maisha yao' wakifurahi kuonyesha kuguswa na tamasha hilo ambalo lilikuwa mahsusi kumueenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere. PICHA ZAIDI ZINAENDELEA TAFADHALI/>BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Kilimanjaro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.

  Makamu wa Rais anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Kilimanjaro kesho Oktoba 16, 2017.

  Kauli mbiu ya mwaka huu ni ” Zuia Ajali-Tii Sheria Okoa Maisha”

  Ufunguzi huo utafanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo katika Manispaa ya mji wa Moshi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

  0 0


   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia), akimsikiliza Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa NBC, Dorothea Mabonye (wa pili kushoto), huku wenzake wakiangalia wakati akitembelea banda la NBC katika maadhimisho hayo.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia), akisalimiana na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Witness Leverian alipokwenda kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana. NBC ilikuwa ni kati ya wadhamini wa maadhimisho hayo ambapo imezindua akaunti maalumu ya kikundi iitwayo ‘NBC Kikundi Account’ ili kuwawezesha watanzania kiuchumi katika kikundi cha watu kuanzia watano na kuendelea.  
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Bidhaa na Wateja Rejareja wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo alipokwenda kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini ambapo ilizindua akaunti maalumu ya kikundi iitwayo ‘NBC Kikundi Account’ ili kuwawezesha watanzania kiuchumi. Akaunti inafunguliwa na  watu kuanzia watano na kuendelea. Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Beng`i Mazana Issa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Japhet Justine, Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Edwin Christant na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Anna Dominick.

   Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Witness Leverian (kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
   Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Rosina Simbila (kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
  Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Stephen Ngereza (kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Zanzibar Oktoba 15, 2017 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi.Sophia Mjema mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitotokea Zanzibar Oktoba 15, 2017 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina Lazaro Mambosasa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Zanzibar Oktoba 15, 2017 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Bi.Sophia Mjema mkuu wa Wilaya ya Ilala mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Zanzibar Oktoba 15, 2017
  PICHA NA IKULU

  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi mapema leo kabla ya kurejea jijini Dar

  0 0


  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R) Semistocles Kaijage amewataka wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa madiwani kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ili kuepuka kuisababishia serikali hasara.

  Jaji Kaijage ameyasema hayo leo (Tarehe 15.10.2017) mjini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.“…Tusipozingatia na kufuata taratibu za uchaguzi tunaweza kusababisha kesi nyingi za uchaguzi na kuitumbukiza nchi katika gharama ambazo zingeweza kutumika katika huduma za jamii,” ameonya Jaji Kaijage.

  Mhe. Kaijage amesema kuwa hamasa katika siasa za Tanzania imeongezeka sana na kwamba kumekua na ongezeko la hali ya kutokuaminiana haswa katika mchakato wa uchaguzi na kwamba endapo wasimamizi hawatafanya kazi yao kwa ufasaha wataitumbukiza nchi kwenye matatizo makubwa.

  “Mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mna uwezo wa kufanya kazi hii, kitu cha muhimu ni kujiamini na kujitambua. Pia kuhakikisha mnayajua vyema maeneo yenu mnayofanyia kazi, kuhakikisha mnawatumia vizuri wasaidizi mlio nao kwa matokeo bora,” alisema.

  Jaji Kaijage amewakumbusha washiriki wa mafunzo hayo juu ya jukumu lao la kuimarisha imani ya wananchi kwa NEC, na kwamba Imani hiyo itadumishwa endapo watafanya kazi kwa uwazi, uhuru na kwa ufanisi wa hali ya juu bila kuegemea upande wowote.Ameogeza kusema kwamba uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kisheria na kikanuni zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa.

  “Hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na usio na malalamiko au vurugu wakati wa mchakato wa uchaguzi kuanzia utoaji wa fomu, uteuzi wa wagombea, uratibu wa kampeni, upigaji kura, kuhesabu kura, kujumlisha hesabu za kura na kutangaza matokeo,” alisema.

  Aidha, Jaji Kaijage, amewaasa wasimamizi wenye uzoefu kujiepusha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wazingatie mafunzo ambayo watapewa na tume pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zinazosimamia uchaguzi.

  Mkutano huo wa ufunguzi ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Bw. Ramadhan Kailima na maafisa wa kada mbalimbali wa NEC pamoja na wasimamizi, wasimaizi wasaidizi na maafisa wa uchaguzi 230 ambao walikula kiapo cha kuheshimu maadili ya uchaguzi.

  Awali Bw. Kailima amesema kwamba uchaguzi mdogo umepangwa kufanyika kwenye Kata 43 tarehe 26 mwenzi Novemba, mwaka huu. “Uchaguzi mdogo unafanyika kwenye Kata 43 ambazo zipo kwenye mikoa 19 kwenye Halmashauri 36 na Majimbo 37 kwa hiyo uchaguzi huu mdogo unafanyika karibia maeneo ya nchi nzima,” alisema Kailima.

  Uchaguzi huo unatarajiwa kuhusisha wapiga kura waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wapatao 336,182 katika jumla ya vituo vya kupigia kura 893 ambapo Kata yenye wapiga kura wengi wanafikia 58,622 na Kata yenye wapiga kura wachache wanafikia 1,402. 

  0 0


  0 0

  Binagi Media Group

  Maelfu ya wapenzi wa burudani Jijini Mwanza jana wamefurahia tamasha la Mziki Mnene linaloandaliwa na EFM radio na ETV za Jijini Dar es salaa ambapo wasanii mbalimbali akiwemo Kala Jeremiah walipata shangwe kubwa kwenye tamasha hilo lililofanyika uwanja wa CCM Krumba.


  Wasanii wengine waliokonga nyoyo za mashabiki zao ni TID, Snura, Young Killer, Baraka Da Prince, Shoro Mwamba pamoja na Msaga Sumu huku Stone Fire akiibuka mkali wa Singeli Michano Mwanza baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 20.


  Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika anasema tamasha hilo mbali ya kuwa ni sehemu ya shukurani kwa wasikilizaji wa redio hiyo pamoja na watazamaji wa TVE, pia limelenga kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii hususani wa Singeli.  Tayari limekwisha fanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Mtwara na Mwanza na kwamba litaendelea katika mikoa mingine hivyo mashabiki wa burudani waendelee kufuatilia EFM Radio na TVE kwa taarifa mbalimbali ikiwemo tamasha la Mziki Mnene linalopewa nguvu na Biko pamoja na Cocacola.

  Mkali wa Singeli, Msaga Sumu akidondosha burudani kwenye jukwaa la Mziki Mnene CCM Kirumba Jijini Mwanza. Shoro Mwamba akishambulia jukwaa la Mziki Mnene na ngoma za moto moto za Singeli. Young Killer alikonga nyoyo za mashabiki zake Jijini Mwanza. Kala Jeremiah alidondosha burudani kali kiasi cha mashabiki kugoma asishuke jukwaani. Mnyama TID akitumbuiza kwenye jukwaa la Mziki Mnene Jijini Mwanza. Watangazaji wa EFM Radio wakisherehesha tamasha hilo.
  Dj Ommy Craizy akifanya yake kwenye jukwaa la Mziki Mnene Jijini Mwanza. Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika akizungmzia tamasha la Mziki Mnene. Shangwe za wapenzi wa burudani Jijini Mwanza kwenye tamasha la Mziki Mnene.

  0 0

  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi leo Jumapili Oktoba 15,2017 amezindua na kufungua Pastoreti mpya ya Kanisa la AICT Mto Yodani lililopo Shunu mjini Kahama mkoani Shinyanga.
  Ibada ya uzinduzi na ufunguzi wa kanisa hilo imehudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga,ambapo askofu Kezakubi pia alihubiri katika Ibada ya Jumapili katika kanisa hilo.
  Akizungumza kanisani hapo,Askofu Kezakubi aliwataka viongozi na waumini wa kanisa hilo kutumia jengo hilo kwa ajili a ibada na siyo vinginevyo.“Nimefungua kanisa hili mlitumie kwa ajili ibada,pia kuwaita watu wengine waje kusikia neno la mungu ,sitaki kusikia mnatumia nyumba hii ya ibada kutukanana na kufanya mambo yasiyompendeza Mungu”,alieleza Askofu Kezakubi.
  “Ni aibu kusikia kelele kwenye kanisa,watu kutukanana kwene nyumba ya Mungu,kama kuna mabaraza yanafanyika kanisani basi yafanyike kama ibada,vivyo hivyo upande wa kwaya,sitaki kusikia mtu anatukuzwa kanisani,mwenye kutukuzwa ni Mungu pekee”,aliongeza Askofu Kezakubi.
  Katika hatua nyingine alisema mchungaji ndiye mwalimu na msimamizi mkuu wa masuala ya kiroho hivyo kuwataka wachungaji kufanya kazi yao vyema kwa kuepuka kuwa wavivu na kutolegea kuwaombea na kuwatembelea waumini.Askofu Kezakubi alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha baadhi ya watu wanaopinga viongozi wa dini  kwenye makanisa kuacha tabia hiyo kwani wanakwamisha kazi ya Mungu huku akiwataka viongozi na waumini kushikamana katika kumtumikia Mungu. 

   "Kuna watu wapo kwenye makanisa yetu kwa bahati mbaya,wakiingia kanisani wanaanza vita badala ya kuwaunga mkono viongozi wao ili wafanye kazi yao vizuri,wakristo mnatakiwa pia kuwatunza watumishi wa mungu,tuwatunze watu waliolitumikia kanisa kwani tusipowatunza tunakosa baraka",alieleza Askofu Kezakubi.

   Aidha aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuiombea serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo viovu."Wakristo mnapaswa kumtii mungu,tuenende katika maisha anayotaka bwana,tusimame imara na kukataa mambo mabaya,kama mtu ataliharibu hekalu la Mungu,Mungu atamharibu mtu huyo",alisema.
  Akisoma risala Mwalimu Lucas Matanya alisema Kanisa la AICT Mto Jordani lilianzishwa Novemba 13,2013 chini ya Mwinjilisti Nicodemus Lufega likiwa na wakristo 7 wakisali chini ya mti na baadae idadi iliongezeka kidogo wakajenga banda ambapo waliendelea na ibada katika eneo la Lugela mtaa wa Shunu mjini Kahama.
  “Kanisa hili limekuwa tawi la AICT Kahama Mjini na kwa ushirikiano uliopo,walinunua eneo na kuanza kujenga jengo hili la kuabudia na nyumba ya kichungaji,choo na kuweka uzio,lengo likiwa ni kuhakikisha wanapata huduma za kiroho karibu na makazi yao”,alieleza.
  Aidha alisema Baraza la Utumaji la Dayosisi ya Shinyanga limemtuma Mchungaji Daudi Kazimoto kuwa mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.
  Alizitaja changamoto zinazolikabili kanisa hilo kuwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kununulia eneo ili kupanua eneo la kanisa kwani lililopo ni dogo lakini pia ukosefu wa jengo la utawala.
  ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINIAskofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akizungumza kabla ya kuzindua kanisa la AICT Mto Jordan leo Jumapili Oktoba 15,2016 mjini Kahama-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Waumini wa kanisa la AICT Mto Jordan wakishuhudia zoezi la ufunguzi wa kanisa hiloMchungaji Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akisoma neno la Mungu wakati wa zoezi la kuzindua kanisa la AICT Mto JordanMwalimu Lucas Matanya akisoma risala kuhusu kanisa hilo jipya
  Waumini wa kanisa hilo wakishuhudia zoezi la uzinduzi wa kanisa hilo
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi  akikata utepe
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akisoma maandishi baada ya kukata utepe
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akifungua kufuli ili aingie kwenye kanisa jipya la AICT Mto Jordan
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiingia kanisani
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiingia kanisaniAskofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiwapungia mkono waumini wa kanisa la AICT walioingia katika kanisa la AICT Mto Jordan
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza ibada fupi ya ufunguzi wa kanisa la AICT Mto Jordan
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza ibada katika kanisa la AICT Mto Jordan
  Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kanisani
  Mchungaji Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akizungumza wakati wa ibada hiyo
  Viongozi mbalimbali wakiwa kanisani
  Muonekano wa kanisa la AICT Mto Jordan 
  Muonekano wa kanisa la AICT Mto Jordan
  Kiongozi wa Ibada ya Jumapili leo Oktoba 15,2017,Mchungaji Adam Nzoka akizungumza baada ya uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan
  Mchungaji Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akizungumza wakati wa ibada katika kanisa la AICT Mto Jordan baada ya uzinduzi wa kanisa la AICT Mto JordanWaumini wa kanisa hilo wakifuatilia ibada
  Viongozi wa kanisa la AICT wakisali wakati wa ibada ya Jumapili. Kulia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan,mchungaji Daudi Kazimoto,katikati ni Makamu wa Askofu kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Aron Malyuta na kushoto ni Mchungaji Adam Nzoka
  Kaimu Katibu Mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga ,Mchungaji Timoth Shadrack akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria zoezi la uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan

  Mchungaji Simon Temu kutoka kanisa la AICT Ngudu mkoani Mwanza akijitambulisha

  Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aron Malyuta akitoa neno wakati ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan


  Viongozi wa kanisa la AICT wakiwa wamesimama kabla ya Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi hajaaza kuhubiri neno la Mungu katika kanisa la AICT Mto Jordan
  Kikundi cha sifa wakiimba wimbo wa kuabudu
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi ambaye ndiye Mlezi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga akitoa mahubiri wakati wa Ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan baada kuzindua kanisa hilo
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiendelea na mahubiri
  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akimtambulisha 
  Mchungaji Daudi Kazimoto kuwa ndiye mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.

  Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akieleza sifa za Mchungaji Daudi Kazimoto ambaye amebobea katika neno la Mungu hivyo ana uweza mkubwa wa kuongoza hilo na kuwataka waumini wa kanisa hilo kumpa ushirikianoAskofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza zoezi la mchango kwa ajili kupanua eneo la kanisa la AICT Mto YordanAskofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza zoezi la changizo hilo
  Kwaya kutoka AICT Kahama Mjini wakimwimbia MunguViongozi wa Kanisa la AICT wakiwa katika Ibada ya JumapiliViongozi wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya JumapiliWaimbaji kutoka kwaya ya AICT Kahama Mjini wakiimba na kuchezaWaumini wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya Jumapili
  Emmaus  Gospel Band wakiimba na kuchezaEmmaus  Gospel Band wakiendelea kucheza na kuimbaViongozi mbalimbali wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya Jumapili

  Kwaya ya Akina Mama wakiimba wakati wa ibada hiyo

  Ibada inaendelea

  Kwaya ya AICT Bethelehemu mjini Kahama wakiimba na kucheza

  Kwaya ya AICT Majengo wakiimba na kucheza

  Kwaya ya AICT Galilaya Mhongolo ikiimba

  Kwaya ya AICT Nyakato ikiimba
  Kwaya ya Waberoya wakiimbaPicha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

older | 1 | .... | 1400 | 1401 | (Page 1402) | 1403 | 1404 | .... | 1896 | newer