Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

OPERESHENI YA KUWAPIMA MACHO WAKAZI WOTE WA SINGIDA KUANZISHWA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kuanzisha operesheni maalumu ya kuwapima macho wakazi wote Mkoani hapa hususani watumishi wa serikali.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mapema jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Duniani ambapo asilimia 94 ya watu wenye upofu Mkoani Singida wanasumbuliwa na matatizo ya macho ambayo yanazuilika.

Amesema ili watumishi wa umma waweze kutoa huduma iliyo bora wanatakiwa kuwa na uoni mzuri hivyo kuwapima ni hatua kubwa itakayosaidia kutibu na kuzuia upofu mapema.

“Mganga Mkuu wa Mkoa sasa tunataka uanzishe operesheni tupimwe wote macho, inasikitisha kusikia hao wote waliopata upofu takribani watu elfu 25 wangeweza kupona endapo wangegundulika mapema kwakuwa matatizo yaliyowasababishia upofu yanazuilika”, amesema Dkt Nchimbi na kusisitiza kuwa,“Halmashauri zote tengeni bajeti za kununua dawa za macho pamoja na kuhakikisha wananchi wenu wote wanapimwa macho ili magonjwa yanayozuilika yapewe matibabu mapema, watendaji msione fahari kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa macho wakati mngeweza kuwasiadia”, ameeleza Dkt Nchimbi.

Awali, Dkt Nchimbi amepokea kifaa cha kisasa aina ya Auto Perimeter Glautefield Lite kutoka kwa Shirika la Sight Saver, chenye uwezo wa kuona taswira na matatizo ya macho vizuri, ambacho kwa nchi nzima kinapatikana mkoani Singida peke yake.Amesema kifaa hicho kitawasaidi madaktari bingwa wa macho Mkoani hapa kutoa huduma bora huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapatiwe huduma kwani uwepo wa kifaa hicho bila kutumika kitakuwa hakina manufaa.

Dkt Nchimbi ameongeza kuwa, kutokunywa maji ya kutosha husababisha uoni hafifu ambao hupelekea upofu unaozuilika, hivyo amelishauri shirika la Sight Savers kuweka mpango wa kuboresha upatikanaji wa maji na kufanya utafiti hasa maofisini endapo watumishi wanakunywa maji ya kutosha kwakuwa yanasaidia kuzuia upofu.

Kwa upande wake Meneja Mipango na Uendeshaji wa Shirika la Sight Savers Nchini Mhandisi Koronel Kema amesema shirika hilo limeanzisha mradi wa kuboresha huduma za macho mkoani Singida utakaogharimu shilingi bilioni 2.8, mradi utakaodumu kwa muda wa miaka minne.

Kema amesema mradi huo utafadhili ujenzi wa kliniki za macho katika halmashauri za Iramba, Manyoni na Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ili waweze kutumia vifaa vyenye thamani ya milioni 300 ambavyo vimetolewa na shirika hilo.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Singida umeongezewa mradi mwingine utakao anza mapema mwakani na kuhusisha upimaji wa wananfunzi wote na walimu wao mashuleni ili kuweza kutibu na kuzuia upofu katika hatua za awali.

Mmoja wa wagonjwa Said Mwiru aliyefanyiwa upasuaji katika jicho lake kwenye maadhimisho hayo amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa kabla ya upasuaji huo hakuweza kuona chochote ila siku moja baada ya matibabu hayo anaweza kuona vizuri.Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Salum Manyatta amesema ataongeza kasi katika kutekeleza agizo la mkuu wa Mkoa kwakuwa walikua tayari wameshaanza kuwapima watumishi katika baadhi ya halmashauri.

Manyatta amesema zoezi lililofanyika la upimaji watumishi katika halmashauri ya Wilaya ya Manyoni limebainisha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watumishi hao walikuwa na matatizo ya macho ambayo yangepelekea upofu.

Katika kuadhimisha siku ya afya ya macho duniani, shirika la Sight Savers limeendesha zoezi la upimaji wa macho kwa watu 200 Mkoani hapa ambapo 84 kati yao wamegundulika kuwa na tatizo la macho linalosababisha wapoteze uwezo wa kuona, huku Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni ‘Afya ya Macho kwa wote’.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea kifaa cha kisasa cha vipimo vya macho aina ya Auto Perimeter Glautefield Lite kutoka kwa Shirika la Sight Saver, aliyeshika kipaza sauti ni Meneja Mipango na Uendeshaji wa Shirika la Sight Savers Nchini Mhandisi Koronel Kema.
Daktari wa macho akimfanyia uchunguzi wa macho mmoja kati ya wagonjwa waliojitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Mkoani Singida.
Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho Said Mwiru akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Singida (hayupo pichani) kuwa anaweza kuona na kuwatambua watu kwa kutumia jicho alilofanyiwa upasuaji. Kabla ya upasuaji huo Mwiru amesema jicho hilo lililkuwa halioni.
Baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa macho wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida (hayupo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Duniani, akina mama hao wamefanyiwa upasuaji kwa hisani ya shirika la Sight savers.

PRINCE AGHA KHAN AZINDUA STEMPU ZA POSTA ZENYE KUMBUKUMBU ZA TAASISI YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiangalia picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake wakati alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, kabla ya kuzizindua jijini Dar es Salaam jana. Walioshika bango lenye picha za stempu hizo kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akikabidhiwa bango lenye  picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake na kaimu postamasta  Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, wakati wa uzinduzi wa stempu hizo jijini jana. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, mara baada ya kuzindua stempu hizo.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan, akielezwa jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati akiangalia moja ya vikundi vya burudani vilivyotumbuiza katika uzinduzi huo. 
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (wa pili kulia), akimueleza jambo  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi (kulia), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, baada  ya uzinduzi wa stempu hizo. 
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mara baada ya uzinduzi huo jijini jana.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mara baada ya uzinduzi huo. 
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, wakati wakizungumza jambo, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, baada ya uzinduzi wa stempu hizo.  
Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), na kaimu Postamasta Mkuu Bw.Macrice Mbodo (kulia), akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa Shirika hilo, kwenye ofisi ya Posta uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere mara baada ya kumalizika uzinduzi huo.
Hizi ni baadhi ya stempu zenye kumbukumbu za taasisi ya Agha Khan zilizozinduliwa na kiongozi huyo jijini jana. 
Hii ni moja ya stempu yenye kumbukumbu ya taasisi ya Agha Khan zilizozinduliwa na kiongozi huyo jijini jana.

Hizi pia ni baadhi ya stempu zenye kumbukumbu za huduma mbalimbali za kijamii zinazofadhiliwa na taasisi ya Agha Khan nchini, zilizozinduliwa na kiongozi huyo jijini jana.

TAREHE 12 Oktoba, Mkuu wa Taasisi ya Agha Khan Foundation, Mtukufu Karim al-Hussayni  Agha Khan ambaye pia ni kiongozi Mkuu wa Jumuia ya Ismailia duniani na mtu anayeheshimika sana hasa kwa jamii ya Kihindi, alizuru nchini Tanzania na kufanya shughuli mbali mbali za Kitaifa na kibinafsi nchini.

Pamoja na kuwa na manufaa makubwa kwa nchi pia ziara hiyo ilikuwa muhimu sana kwa Shirika la Posta Tanzania.

Mbali na kutembelea miradi mbali mbali inayofadhiliwa na taasisi yake, alipata fursa ya kuzindua stampu zilizochapishwa na Shirika la Posta zinazoelezea au kuonyesha kumbukumbu muhimu za taasisi ya Agha Khan.

Uzinduzi wa stampu hizo ulifanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa ndege wa mwl.nyerere akiwa njiani kurudi ,baada ya ziara yake hapa nchini kukamilika.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi kwa niaba ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Joseph Pombe Magufuli ndiye aliyemkabidhi stampu hizo kutoka kwa Kaimu Postamasta Mkuu bw.Macrice Mbodo.

Stampu hizo, zenye kumbukumbu maalum za Agha Khan ni pamoja na jengo la dispensary ya zamani iliyojengwa na taasisi ya Agha Khan mjini Unguja pamoja na za picha za shughuli mbalimbali za kijamii zilizofadhiliwa na taasisi hiyo.

Uchapishaji wa stampu hizo, ulidhaminiwa na taasisi hiyo, kwa gharama ya shilingi milion 52, zikiwa ni stempu maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya Diamond Jubilee- miaka 60 ya tangu kusimikwa kwake kuwa Imamu Mkuu wa dhehebu la Shia Ismailia.

Mwaka 2007, taasisi ya Agha Khan waliweza pia kufadhili uchapishaji wa stampu maalum za kuadhimisha Golden Jubilee (1957-2007), kwa kiasi cha dola 10,573.24 .Stampu hizo zilikuwa na dhamani ya shilingi 267,059,000/=

Stampu hizo zitaweza kutumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida (postage) na zaidi kwa wakusanya stampu (stamps collectors), ambao mbali na kuweza kuzipata kupita kaunta za Posta na mawakala wa stampu, pia kwa sasa wanaweza kuzipata kupitia duka maalum (online) ambalo limeanzishwa na shirika la Posta.


Mteja yeyote akiwa popote Duniani anaweza kununua kupitia Web site ya Posta, ambapo ataingia kwenye kipengele cha e-busness na bonyeza e-service, kisha e-shop na atapata aina mbalimbali za stampu na maelekezo ya namna ya kununua.

Dc Sofia Mjema awaongoza mamia ya vijana wa UVCCM wilaya ya ilala katika zoezi la kufanya usafi hospitali ya Mnazi mmoja

$
0
0
Mkuuwa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema  aliye vaaqkilemba ,aliye upande waq  kushoto ni Diwani wa kata ya Ilala  Mhe. Saad Kimji akifagia na vijana wa  Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Ilala  katika Hospital ya Mnazi mmoja  jijini Dar es salaam leo katika kuelekea madhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Mwalimu JK nyerere.
Mmoja wa viongozi wa umoja wa vijana CCM ilala akimpati zawadi ya Sabuni mama mzazi Ruth Eliya  aliye jifungua jana katika Hospital ya mnazimoja ,aliye upande wamisho kulia ni Mkuuwa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema .
Diwani wa kata ya Ilala Mhe.Saad Kimji akizungumzaz na waandishi wa  habari baada ya zoezi la kufanya usafi  na kutoa misaada katika hospital ya mnazi mmoja 
 Katibu wa umoja wa vijana UVCCM  Wilaya ya Ilala Irene Moleli akizungumza na wana habari  baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi na kutoa misaada katika hospital ya  Mnazi mmoja , moja ya misaada ilitolewa hapo ni sabuni ya unga na sabuni za mche.
 Mganga mfawidhi wa Hospital ya mnazi mmoja Helman Ngonyani, akitoa neno la shukrani kwa  UVCCM na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema baada ya kuhitika kwa ziara hiyo.
 Baadhi ya vijana  wa UVCCM  wakizoa taka  katika Hospital ya Mnazi mmoja , 
 Baadhi ya vijana  wa UVCCM  wakizoa taka  katika Hospital ya Mnazi mmoja .

Na Mwandishi wetu Dar

Katika  kuazimisha siku ya kumbukumbu ya  kifo cha mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema leo ameongoza  umomoja wa Vijana CCM, Wilaya ya Ilala kufanya usafi na kugawa  misaada ya kijamii katika Hospital ya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.

Akizungumza baada ya zoezi hilo Mhe. Mjema amesema , Wameamua kufanya usafi  na kugawa zawadi hizo ili kumuenzi Babawa Taifa na amewapongeza vjiana wote walijitokeza katika shuguli hiyo kwani nitendo la uzalendo amabalo linawafanya watu wengi kumkumbuka mwalimu Nyerere kwa uadilifu wake alivyo litumika Taifa enzi ya uhai wake.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospital hiyo Helmani Gonyani, amewashukuru vija wa umoja huo kwa kutembelea hospitali hiyo na kufanya usafi na kuwataka tena iwapo wata pata nafasi siku nyingine wafanye hivo kwani wamefariji wagonjwa na kuhamasisha umoja wa kitaifa.

Naye diwani wa kata ya Ilala Saad Kimji akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa kata hiyo  ameushukuru uongozi wa hospital hiyo kwa mapokezi  na ushirikiano wa walioupata  katika hospital hiyo na kupongeza watumishi wote wa hospital kwa uzalendo wao na kutoa huduma kwa  , na kutoa wito kwa vijana wa Illala kuwa wazalendo kwa kufanya kazi za kijaamii bila kujali itikadizao  za kisiasa.

Irene Godfrey Moleli  ni katibu wa umoja wa vijina  wa wilaya ya Ilala , amesema , UVCC Wilaya hiyo  umeandaa bonanza  na ligi ya mpira kwaajili ya kumuenzi hayati Mwalimu Julias Nyerere ambapo itaanza  tarehe 21 hadi 28 mwezi kakatika jimbo la Segerea na amewakaribisha vijana wote kuhudhuri uzinduzi wa ligi hiyo na kushiriki michezo kwa muda wote wa ligi hiyo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO OCTOBER 14,2017

Injinia Manyanya afanya ziara yake ya kwanza ya kikazi akiwa Wizara ya Viwanda

$
0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya afanya ziara yake ya kwanza ya kikazi akiwa Wizara ya Viwanda kwa kutembelea kongano la ngozi na bidhaa za ngozi katika eneo la zuzu Mkoani Dodoma.

Aidha Mhe. Waziri amewaagiza watendaji wa wizara kufanya juhudi za haraka za uendelezwaji wa eneo hilo kwa hakuna sababu ya kuchelewa ambapo mhe. Naibu waziri ametoa muda wa miaka miwili hilo eneo liwe limeanza kuwekewa miundombinu na huduma nyingine.

Pia mhe. Waziri ametembelea eneo la SIDO lililotengwa kwa ajili ya kongano la alizeti ambapo pia amewaagiza watendaji kufanya juhudi za haraka kuharakisha mchakato wa uendelezwaji wa eneo hilo, Mhe. Naibu waziri alihitimisha ziara yake kwa kutembelea ofisi za SIDO na kutembelea ajasiliamali walioko chini ya SIDO na kujionea shughuli za ujasiriamali zinazofanywa katika eneo hilo.

Mhe. Naibu waziri ataendelea na ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara kuanzia wiki ijayo na kujionea utendaji wa kila taasisi.
 Darasa maalumu la mafunzo ya uzalishaji na utengezaji wa bidhaa za ngozi lililopo Kizota, mkoani Dodoma.
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akishuhudia bidhaa mbalimbali zinazotengezwa na wanafunzi wanaojifunza utengezaji wa bidhaa za ngozi pembeni ni ndugu. Stephano Ndunguru, meneja wa mafunzo SIDO, Dodoma.
 baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengezwa na wanafunji wanaojifunza utengezaji wa bidhaa za ngozi.
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akizungumza na watendaji wa SIDO, Dodoma.

 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akiangalia bidhaa zinazotengezwa na wajasiriamali wa SIDO.
 baadhi ya bidhaa za wajasiriamali wa SIDO, Dodoma.
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akichomelea alipowatembelea wajasiriamali wa vyuma SIDO, Dodoma.
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akikagua eneo maalumu kwa ajili ya kongano la ngozi, Zuzu mkoani Dodoma.

DKT ANGELINA MABULA AAHIDI WATAALAMU WA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI SINGIDA.

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeahidi kutoa timu ya wataalamu watakao suluhisha mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida na Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara.

Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula ametoa ahadi hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Singida katika kijiji cha Singa tarafa ya Kinampundu Wilayani Mkalama ambapo amesema Wizara yake itatoa wataalamu watakaoweza kutatua mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 30.

“Kwakuwa pande zote mbili za Mkalama na Hanang’ zimekutana mara kadhaa bila mafanikio, nitaleta wataalamu wafike eneo la mpaka ili wataalam hao wawasomee alama moja baada ya nyingine, kila mmoja wenu afahamu eneo lake mwisho ni wapi, nadhani hapo tutakuwa tumewasaidia wananchi wetu”, amesema Dkt Mabula.

Amesema wananchi wa Kijiji hicho cha Singa wasiwe na wasiwasi endapo baada ya kuonyesha mpaka wao mashamba yao yakionekana yapo wilaya ya Hanang’ wataruhusiwa kuendelea kuyamiliki ila watatakiwa kwenda kujitambulisha katika Uongozi wa Wilaya hiyo.

Aidha Dkt Mabula amesema timu hiyo ya wataalamu itahakikisha inasuluhisha migogoro yote ya mipaka ya wilaya hiyo ambayo ngazi ya wilaya imeshindikana kutatuliwa.

Amewashauri wananchi hao kutouza au kugawa ardhi yao ovyo ovyo kwakuwa ardhi ni mali na mtaji popote pale hata kama ni vijijini hivyo watunze ardhi yao na kuiongezea thamani kwa kuipima na kuwa na hati ya umiliki.

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walitoa malalamiko kwa Naibu Waziri huyo huku wakimueleza kuwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu umesababisha baadhi yao kupelekwa mahakamani kwa madai ya kuvamia mashamba.

Mzee Anaftali Amosi Majii amemueleza Naibu waziri kuwa taarifa za mgogoro huo zilitolewa muda mrefu na kuongeza kuwa wananchi wamechoka kushitakiwa kwa makosa ya uvamizi wa mashamba wakati wao wanaamini wanayamiliki kwa uhalali jambo ambalo linawachelewesha kimaendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama Mhandisi Geofrey Sanga amesema Wilaya ya Mkalama ina migogoro ya mipaka kwa wilaya tano zinazowazunguka.

Mhandisi Sanga ameeleza kuwa Mkalama ina migogoro ya mipaka kati yake na Wilaya za Mbulu, Iramba, Hanang’ na Wilaya ya Singida jambo ambalo linawafanya baadhi ya wananchi kukwepa kuchangia shughuli za maendeleo wakidai wao sio wa Wilaya hiyo.

Wakati huo huo Naibu Waziri Dkt Angelina Mabula amefanya ziara Wilaya ya Iramba na kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika masijala ya Ardhi ya Wilaya hiyo ambapo hakuridhishwa na utunzaji wa nyaraka pamoja na utendaji usioridhisha unaosababisha wananchi kuchelewa kupata hati za viwanja.

Dkt Mabula pia hakuridhishwa na kasi ndogo ya upimaji viwanja na utoaji wa hati wilayani humo huku akiwataka kuacha kukusanya kodi mbalimbali za ardhi kwa utendaji wa kimazoea bali wafanye kazi bidii.
Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akizungumza na wataalamu wa ardhi, viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya na Manispaa ya Singida [hawapo pichani], Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi. 
Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singa tarafa ya Kinampundu Wilayani Mkalama, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jaksoni Massaka.
Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Ardhi wa Wilaya ya Iramba Lugano Sanga kuhusu utuzanji wa nyaraka za idara hiyo.
Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi hati ya kumiliki kiwanja chake kilichopo Mjini Dodoma.

TANZANIA YANG’ARA KATIKA TUZO ZA SAFARI ZA KITALII AFRIKA.

$
0
0
Sekta ya Utalii nchini imezidi kujiimarisha katika masoko ya kitalii ulimwenguni hivyo kuendelea kushinda tuzo mbalimbali katika biashara ya Utalii.

Katika hafla ya 24 ya Utoaji Tuzo ya kila mwaka ya Safari za Kitalii Afrika kwa mwaka 2017 iliyofanyika Kigali nchini Rwanda wiki hii, Tanzania imejinyakulia tuzo mbali mbali ambazo zimedhihirisha kuimarika kwa sekta ya Utalii nchini.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Kitalii ya Radisson Blu mjini Kigali, kwa mwaka wa pili mfululizo, Mlima Kilimanjaro umeshika nafasi ya kwanza kuwa kivutio kikuu cha utalii barani Afrika.

Kwa upande wa huduma za hoteli, Tanzania ‘imekomba’ tuzo za juu tano za ubora ambapo hoteli ya kifahari ya Diamonds La Gemma Dell’Est iliyoko ncha ya Kaskazini Magharibi ya Kisiwa cha Zanzibar imenyakua nafasi mbili za juu.

Katika tuzo hizo, Hoteli ya Thanda iliyoko katika kisiwa cha Shungimbili wilaya ya Mafia imetununikiwa Tuzo ya Hoteli Bora za Visiwa cha Maraha mwaka 2017 ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo kunyakua tuzo hiyo.

Hoteli ya Kisiwa cha Mnemba kilichoko Kaskazini Mashariki ya Pwani ya Zanzibar imepata Tuzo za Hoteli bora za Visiwa vyenye Faragha huku hoteli ya Four Seasons Safari Lodge ya Serengeti imejinyakulia Tuzo ya Hoteli Bora za Mbugani.

Tuzo za Safari za Kitalii zilianzishwa mwaka 1993 kwa lengo la kutambua, kuwazawadia na kusherehekea mafanikio ya wadau katika sekta ya utalii.

Hivi sasa Tuzo hizo zinatambuliwa ulimwenguni kuwa kiwango cha ubora katika sekta hiyo ambapo washindi wanafikia viwango ambavyo wengine wanashindana kuvifikia.

Kila mwaka hafla za Tuzo za Safari za Kitalii hufanyika ulimwenguni kote kwa kuwatukutanisha watu mashuhuri katika matukio ya kikanda kutambua na kusherehekea mafanikio ya mtu moja moja na makundi.

Article 2


LAPF YAFUNGUA OFISI YA KANDA YA MAGHARIBI MKOANI GEITA

$
0
0
Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba Akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Kushoto Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,Kulia Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud na wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Geita Mji Constatine Kanyasu wakikata utepe kwaajili ya kuzindua ofisi za LAPF kanda magharibi 
Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba akiingia kwenye viwanja vya sherehe vya uzinduzi wa ofisi za kanda ya magharibi. 
Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba ,akiwa pamoja na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Hermani Kapufi na Meneja wa Kanda ya magharibi Vonnes Koka akimkaribisha Naibu waziri wa TAMISEMI. 
Wageni waalikwa wakifuatilia tukio 
Burudani zikiendelea kikundi cha Ngoma kutoka Mkoani Geita. 
Wageni waalikwa wakiwa wakifuatilia kwa makini burudani ya Ngoma. 

Jamaaa akionesha makeke yake kwa kula mchanga mwingi zaidi mdomoni. 
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu waziri wa TAMISEMI. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akiwatambulisha baadhi ya watumishi na viongozi ambao walikuwa meza kuu. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akitoa salaam za halmashauri ambayo anaiongoza. 
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisalimiana na wananchi wakati wa zoezi la uzinduzi wa ofisi za kanda. 
Meneja wa Kanda ya magharibi Vonnes Koka akiwakaribisha wastaafu pamoja na wale ambao wanatakiwa kupewa fao la uzazi kwaajili ya kupatiwa hundi. 
Philip Ngika ni Mstaafu aliyestaafu hivi karibuni na kupatiwa mafao yake kiasi cha zaidi ya Milioni 72 na Naibu waziri wa TAMISEMI. 
Mwanachama wa LAPF ambaye amenufaika na fao la uzazi na kupatiwa kiasi cha zaidi ya Shilingi Laki sita 
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud Sanga,Akimkabidhi Mgeni rasmi Naibu waziri wa TAMISEMI madawati miaka moja ambayo yametolewa kwenye halmashauri ya mji wa Geita. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akizungumza na Wanafunzi na kuwataka kusoma kwa bidii ili waje kufaulu masomo yao pindi watakapofika Darasa la Saba 
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu akiomba halamshauri ya mji kupanishwa adhi ya kuwa Manispaa. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akiwa mbele ya jengo la LAPF
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akitembelea ofisi za LAPF 
Mgeni Rasmi naibu waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa LAPF. PICHA NA JOEL MADUKA



Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba ameziagiza halmashauri zinazodaiwa kwa kutokupeleka michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kutathmini kiasi wanachodaiwa na wakati wa maandalizi ya bajeti wahakikishe wanakwenda na mikakati ya kiasi walicholipa wanachodaiwa na namna ya kulipa madai kwenye mifuko hiyo.

Agizo hilo limetolewa leo wakati Bw Sinkamba akizindua ofisi za mfuko wa penisheni wa LAPF kanda ya magharibi ambayo itahudumia Mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita na Wilaya ya Sengerema na Halmashauri ya Buchosa.

Amesema miongoni mwa maeneo yanayodaiwa na mifuko ya hifadhi ni pamoja na watumishi wa Halmashauri hususani watendaji wa kata na vijiji na kwamba ni vema Halmashauri zikajua kiasi wanachodaiwa na kuandaa mikakati ya kulipa na kupeleka taarifa ya malipo kwa TAMISEMI.

Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud Sanga, ameeleza katika kuendelea kuboresha huduma ya mfuko huo wamekuwa wakilipa mafao mapema zaidi kwa mwanachama anayekaribia kustaafu na kwamba wamejidhatiti kutoa huduma bila usumbufu kwa wastaafu wanapohitaji mafao yao.Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema wanaamini kwa mashirika kuendelea kuweka ofisi za kanda ni njia mojawapo ya kukuza mji wa Geita na kufikia azma ya kuufanya mji huo kuwa Manispaa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Bw Constantine Kanyasu amemuomba Naibu waziri wa TAMISEMI, Kuipandisha hadhi Halmashauri hiyo ili kuwa Manispaa kutokana na shughuli zilizopo kwenye Halmashauri hiyo kwa sasa.Mmoja wa wastaafu Bw Philip Ngika ameushukuru mfuko huo kwa namna unavyoendelea kuwajali wastaafu kwa kuwa yeye ni miongoni mwa watu wakaopatiwa mafao yao mapema zaidi.

Ziara ya Naibu Waziri Ujenzi barabara ya juu (Fly Over) Tazara

$
0
0
 Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu (Fly Over) jana jijini Dar es Salaam.
Meneja mradi (TANROADS) Anold Maeda (kulia) akitoa maelezo kwa  Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly Over) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi huo jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhandisi Mkazi kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Kiyokazu Tsuji.  
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja mradi (TANROADS) Anold Maeda (wa tatu kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara ya TAZARA jana jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (Katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja mradi (TANROADS) Anold Maeda (wa tatu kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya juu unaondelea katika makutano ya barabara ya TAZARA jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhandisi Mkazi kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Kiyokazu Tsuji.

 Picha Na Eliphace Marwa - Maelezo

WAZIRI KAMWELWE AKAGUA MIRADI YA MAJI KISARAWE

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani kufuatilia maendeleo ya Sekta ya Maji katika wilaya hiyo.

Dhumuni la ziara hiyo ilikua ni kukagua utekelezaji ya miradi ya maji inayotekelezwa na serikali katika wilaya hiyo, yenye changamoto kubwa ya huduma ya maji licha ya kuwa ni moja ya miji ya muda mrefu na historia kubwa nchini.

“Nimetembelea wilaya kadhaa za mkoa Pwani zikiwemo Rufiji, Mkuranga na Kibiti, lakini hapa Kisarawe kuna changamoto kubwa. Inabidi tufanye kazi ya ziada ili kuinua kiwango cha huduma ya maji ambacho ni asilimia 46, naagiza viongozi wa wilaya mje ofisini kwangu Dodoma tuweke mikakati ya kuinua hali ya maji Kisarawe”, alisema Inj. Kamwelwe.

Inj. Kamwelwe alisema kuwa anamshukuru Mhe. Rais kwa kuagiza DAWASA waje Kisarawe, kwa kuwa watasaidia kuinua kiwango cha huduma ya maji kwa wakazi wa Kisarawe. DAWASA watatoa maji Ruvu Juu na baada ya miezi 15 maji yatakuwa yamefika Kisarawe. 

Aidha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji alitembelea miradi ya maji ya Mengwa, Kikwete na bwawa la maji la Chole Semvula lilioanza utekelezaji wake mwaka 2013 ambalo utekelezaji wake ulikuwa umesimama kwa changamoto mbalimbali, na kusema kuwa ni bwawa zuri, lililo katika mazingira mazuri na lina maji na kuagiza kuanza utekelezaji wake mara moja. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Inj. Romanus Mwag’ingo akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji inayotegemewa kutekelezwa na DAWASA katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akitoa maagizo kwa viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji. 
1. Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akiwa mbele ya Bwawa la Maji la Chole Semvula alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akiwa kwenye mradi wa maji wa Mengwa pamoja na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji.

WAZIRI WA AFYA AFANYA MAZUNGUMZO NA MADAKTARI BINGWA

$
0
0
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Jumuiya ya Kiislamu Duniani(WAMY)kuhusiana na matibabu watakayoyaendeshaKisiwani Pemba mazungumzo yaliofanyika katika Hoteli ya Mizingani Forodhani mjini Unguja.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akipokea Zawadi ya Sahani baada ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Jumuiya ya Kiislamu Duniani(WAMY) kuhusiana na matibabu watakayoyaendesha Kisiwani Pemba mazungumzo yaliofanyika katika Hoteli ya Mizingani Forodhani mjini Unguja.

Kiongozi wa Ujumbe wa Madaktari bingwa kutoka Jumuiya ya Kiislamu Duniani (WAMY) Dk,Sultan akizungumza machache kuhusiana na matibabu watakayoyaendesha wakati walipokutana nakufanya mazungumzo katika Hoteli ya Mizingani Forodhani mjini Unguja.madaktari hao watakuwepo kisiwani Pemba kutoa matibabu mbalimbali ikiwemo matatizo ya akina mama na mifupa kwa siku 10.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANIZBAR.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS SHINYANGA 2017 WAUNGA MKONO KAMPENI YA UPANDAJI MITI SHINYANGA

$
0
0
Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017”,wameunga mkono kampeni ya upandaji miti iliyoanzishwa katika wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro hivi karibuni ili kupambana na hali ya ukame/jangwa mkoani humo. 


Mapema leo Ijumaa Oktoba 13,washiriki hao wa shindano hilo la mrembo wa mkoa wa Shinyanga linalotarajiwa kufanyika Oktoba 15 mwaka huu,walimwagilia maji miti mbalimbali iliyopandwa mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga mwaka 2017,Grace Shija alisema pamoja na kufanya maandalizi ya shindano hilo pia wanashiriki katika shughuli za kijamii. 

“Sisi kama sehemu ya jamii tumeamua kushiriki katika kampeni ya upandaji miti kwa kumwagilia maji miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kwa kujaza maji kwenye chupa zilizowekwa kutiririsha matone ya maji kwenye miti hiyo”,alieleza Shija. 

Akizungumzia kuhusu shindano la Miss Shinyanga mwaka huu alisema jumla ya warembo 12 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga watachuana siku ya Jumapili Oktoba 15,2017 katika ukumbi wa NSSF ya Zamani mjini Shinyanga kuanzia saa mbili usiku ili kupata mrembo wa mkoa mwaka huu. 

Aliwataja wadhamini katika shindano hilo kuwa ni TBL,Shujaa Gin & Vodka,Butiama Club,Diamond Fields Hotel na Lulekia Sound and Decoration. Nimekuwekea picha hapa chini wakati washiriki wa shindano la Miss Shinyanga wakishiriki zoezi la kumwagilia maji katika miti iliyopandwa hivi karibuni mjini Shinyanga. 

Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 wakitoka Diamond Fields Hotel walipoweka kambi mjini Shinyanga wakielekea kwenye maeneo ambayo yamepandwa kwa ajili ya kuweka maji kwenye miti hiyo.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 
Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017” wakiwa wamebeba madumu ya maji kwa ajili ya kuweka kwenye miti ambayo inamwagiliwa maji kwa njia ya makopo ya maji yaliyotobolewa kwa ajili ya kutoa matone kidogo kidogo 
Mshiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 akimwaga maji kwenye kopo jingine 
Mrembo akimwagia maji mti kwa kuweka maji kwenye kopo lililowekwa kwenye mti 
Zoezi la kumwagilia maji miti likiendelea 


Warembo wakielekea katika eneo jingine kwa ajili ya kumwagili maji miti iliyopandwa hivi karibuni 
Mrembo akimwagilia mti 

Zoezi la kumwagilia miti likiendelea 
Mrembo anamwagilia maji mti 
Zoezi la kumwagilia maji likiendelea 
Mrembo akimwagilia maji mti 


Warembo wakimwagilia maji mti 


Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga wakimwagilia maji mti 
Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2017 wakijaza maji kwenye makopo ili waendelee kuweka kwenye makopo yaliyowekwa kwenye miti 
Zoezi la kujaza maji kwenye makopo likiendelea 
Zoezi la kumwagilia maji likiendelea 
Warembo wakimwagili maji kwenye miti 
Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 wakirudi kambini baada ya kumaliza kumwagilia maji kwenye miti iliyopandwa mjini Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA KUZIMA MWENYE, NYERERE DAY NA WIKI YA VIJANA ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikvishwa skafu baada ya kuwasili kuongoza sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mwakilishi wa familia ya Mwalimu, Mhe. Makongoro Nyerere wakati akiwasili kwenye sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein wakiteta jambo wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Vijana wa Halaiki wakitumbuiza kwenye sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Mwenge wa uhuru wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Vijana shupavu sita waliokimbiza mwenye wa Uhuru mwaka 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya kuhitimishwa kwa sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na wakimbiza mwenge wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga wananchi baada ya kuongoza sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.PICHA NA IKULU.



DKT.NDUGULILE AANZA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA KASI.

$
0
0
 Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile aliyesimama akiongea na watumishi wa Taasisi ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) hawapo pichani wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC)  Dkt. Joyceline Kaganda kulia wakati alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es salaam.
 Watumishi wa Taasisi  ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) waliokaa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile aliyesimama mbele wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya watendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani wakati alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Taasisi  ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam,  , wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIMR Dkt. Yunus Mgaya.
 Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile katikati akiingia katika ofisi za  Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea ofisi hizo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC Dkt. Joyceline Kaganda.


TUMUENZI BABA WA TAIFA KWA KUIGA MAISHA YAKE-MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye ibada maalum ya kumuombea Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili Zanzibar (katikati) ni Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) ni Mke wa Waziri Mkuu mama Marry Majaliwa. Oktoba 14, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini waliyo hudhuria kwenye ibada maalum ya kumuombea Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili Zanzibar, Oktoba 14, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania waendelee kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuiga maisha yake na utendaji wake.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) aliposhiriki ibada maalumu ya kumuombea Mwl. Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili Zanzibar.

Ibada hiyo ya kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo cha Mwl. Nyerere ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru uliozimwa leo katika mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.

Katika Idaba hiyo Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanamuenzi Mwl. Nyerere kwa kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.Awali, Katibu wa Jimbo Katoliki Zanzibar Padri Cosmas Shayo ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaomba waamini wamuenzi Mwl. Nyerere kwa kudumisha umoja na mshikamano wa Taifa.

“Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliwapenda watu wote bila kujali Imani zao wala itikadi zao. Alikuwa mzalendo na alitaka Watanzania waishi maisha bora.”

Padri Shayo aliongeza kuwa tunu za amani na umoja zilikuwa miongoni mwa falsafa kuu ya Mwl. Nyerere, ambapo matokeo yake ni umoja na mshikamano wa Taifa uliopo.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Idd, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi Jenista Mhagama, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa.

Wengine ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Bi. Mauldine Castico, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira Bw. Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Bi. Stella Alex Ikupa na mwakilishi wa familia ya Mwl. Bw. Makongoro Nyerere.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAMOSI, OKTOBA 14, 2017.             

TAMASHA LA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA ARUSHA KURINDIMA KESHO

$
0
0

Na Woinde Shizza,Arusha

Tamasha la waandishi wa habari, kanda ya kaskazini, linatarajiwa kufanyika jumapili, octobar 15 katika uwanja wa General Tyre ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Katika tamasha hilo, ambalo litashirikisha wanahabari zaidi ya 500, kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro,limedhaminiwa na shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kampuni ya vinywaji baridi ya Coca cola na kampuni ya ya vinywaji baridi ya SBC (T) Limited na Palace Hoteli.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma, alisema tamasha hilo, limeandaliwa na TASWA kwa kushirikiana na kampuni ya Arusha media na maandalizi yote yamekamilika.

Juma alisema katika tamasha hilo, bingwa atazawadiwa kikombe na fedha taslimu jumla ya shilingi 500,000, mshindi wa pili fedha taslimu 100,000 na kwa upande wea mpira wa pete mshindi ni kikombe na fedha taslimu jumlaya sh 300,000 na mshindi wa pili sh 50,000.

Alisema pia kutakuwa na michezo ya mbio za magunia, kuvuta kamba, mbio za vijiko, riadha na masumbwi ambapo tayari waambuzi wanaotambuliwa na mashirika mbali mbali ya michezo watakuwepo.

Hata hivyo, alisema wadhamini wengine wa tamasha hilo wanatarajiwa kutangazwa, ili kuhakikisha wanahabari wanaburudika ambapo pia kuwa kuwa na benki maalum ambayo itatumnbuiza siku za tamasha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Jamila Omar alitoa wito kwa wanahabari wote na familia zao kujitokeza katika tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka mkoani Arusha.

Alisema kauli mbio ya tamasha hilo, ambalo linaendama na maadhimisho ya kumbukumbu ya mwalimu nyerere ni michezo ni ajira, michezo ni kazi tufanye kazi kwa bidii kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda.

Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alizitaja timu ambazo zitashiriki kuwa ni TASWA Dar es Salaam, Triple A,RadioSunrise , chuo cha uandishi habari cha Arusha(AJTC)timu ya Arusha One Fm, TASWA Arusha,Radio ORS ya Manyara ,NSSF na timu ya Wazee Klabu.
wakwanza kulia ni Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma katikati ni Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Jamila Omar akiongea na waandishi wa habari

DK. MAGUFULI NI KAMA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Naungana na Mamilioni ya Watanzania katika kumbukizi ya maadhimisho ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kilichotokea Oktoba 14, 1999.

Mwalimu Nyerere aliyezaliwa April 13, 1922 kijijini Butiama aliamua kuiacha kazi yake ya Ualimu na kuingia kwenye mapambano makali ya kusaka Uhuru wa Tanganyika ambapo jitihada zake za dhati zilizaa matunda Disemba 9, 1961 kwa kupata Uhuru toka kwa Mwingereza.

Mwalimu Nyerere aliamini katika nguvu ya umoja na mshikamano baina ya nchi na nchi. Kutokana na ujasiri, ushupavu na nia ya dhati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964 na hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliohusisha Muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar.

Mwalimu Nyerere alijenga nchi kwa misingi ya ujamaa na kujitegemea, alijenga mashirika ya umma, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akipinga vikali masuala ya ukabila, udini, ubaguzi na rushwa. Hakika alijenga misingi imara ya amani na mshikamano.

Hakuishia kusaka Uhuru wa Tanganyika tu bali aliendeleza harakati za kusaka Uhuru na ukombozi wa nchi za kusini mwa jangwa la sahara na Afrika nzima.

Licha ya kazi Kubwa aliyoifanya na Watu wengi kuendelea kuhitaji utumishi wa Mwalimu Nyerere lakini aliamua kung'atuka rasmi Urais mwaka 1985.

Hakika Watanzania, Afrika na Dunia nzima ilipigwa ganzi Kubwa ilipopata habari ya kifo cha Mwalimu Nyerere na daima dumu ataendelea kukumbukwa. Hakika Dunia haitokaa imsahau kamwe Mwalimu Nyerere.

Leo hii tunaadhimisha kumbukizi miaka 18 bila Mwalimu Nyerere tukiwa na faraja Kubwa ya kumpata kiongozi mwenye matendo, mawazo, hulka, misimamo inayofanana nae.

Naam! Namzungumzia Rais wa awamu ya tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye Serikali yake inaongozwa kwa misingi ile ile kama aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere.

Rais Magufuli anafufua mashirika ya umma (mfano Reli, ndege na Simu); Anajenga uchumi wa viwanda; Analinda Rasilimali za Taifa (Mfano Madini); Anatoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha nne; Anapiga vita rushwa na ufisadi; Serikali yake hataki iburuzwe na Mataifa tajiri; Anaijenga CCM isiyokumbatia matajiri; Anaendeleza mapambano dhidi ya Wahujumu uchumi; Kuhakikisha Serikali inahamia Dodoma; Kupigania haki, usawa, amani na mshikamano baina ya Watanzania. Hakika haya yote yalikuwa ni mawazo, fikra na matendo ya Mwalimu Nyerere.

Tukiwa tunaadhimisha kumbukizi ya miaka 18 bila ya Mwalimu Nyerere, ni jukumu letu Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo kwa kuzingatia Yale mema na kukemea Yale maovu ambayo yalikuwa chukizo kwake. Tuendelee kuunga mkono Serikali ya Rais Magufuli ambayo imeonyesha matendo yasiyo na shaka ya kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere.

Hakika Dunia inakumbuka Wema, Busara, Upendo, amani, hekima na ucheshi wako Mwalimu Julius Nyerere.

Pumzika kwa Amani Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Mungu Ibariki Tanzania.

IMETOLEWA NA;

Emmanuel J. Shilatu
14/10/2017
0767488622

KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA LAFANA MKOANI GEITA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa kongamano katika maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zikiwasilishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa kongamano katika maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Mchambuzi na mshauri wa sera katika Wizara ya kilimo Ndg Revelian Ngaiza Akiwasilisha mada kuhusu mchango wa sera za kilimo katika mageuzi ya uchumi wa viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Meneja wa Muendelezo wa wakulima wadogo TADB Ndg Joseph MabulaAkiwasilisha mada kuhusu Mikopo nafuu kwa mapinduzi ya kilimo na viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa uendeshaji Mwandamizi Utoaji Mikopo na kudai madeni Kutoka Mfuko wa Pembejeo Ndg Joshua Kalab akiwasilisha mada kuhusu Mchango wa mfuko wa pembejeo katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kupambana na njaa na kupunguza umasikini hususani vijijini wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini kutoka Wizara ya Kilimo Ndg Issa Sabuni akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Katibu wa Chama cha Biashara Tanzania Mkoa wa Kagera (TWCC) Bi Paskazia Sebastian akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa Mfawidhi kutoka Taasisi ya udhibiti wa mbegu TOSCI Mkoa wa Mwanza Ndg Ngura JosephAkiwasilisha mada kuhusu Mchango wa mbegu bora katika usalama wa chakula wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.

Afisa Kilimo Mkuu kutoka Wizara ya kilimo Bi Mwanaid KiyaAkiwasilisha mada kuhusu Sumu kuvu kwenye mahindi: Madhara katika sekta ya kilimo, Biashara na afya ya binadamu wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.

Na Mathias Canal, Geita

Zikiwa zimesalia siku mbili kufikia kilele cha maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambapo maadhimisho hayo huanza Octoba 10 kila mwaka na kufikia ukomo Octoba 16, wadau mbalimbali kutoka sekta ya kilimo na nyinginezo wameshiriki Kongamano la Maadhimisho ya chakula lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Katika kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga aliwasisitiza wataalamu wa kilimo kuwasaidia wakulima nchini ili kuongeza ufanisi katika kilimo kutoka katika kilimo kwa ajili ya chakula pekee badala yake na kuwa na kilimo tija kwa ajili ya chakula na biashara. 

Alisema kuwa ili kuongeza ufanisi na kukuza soko la mazao ya chakula na biashara nchini watanzania wanatakiwa Kuwa wazalendo na kupenda vyakula vitokanavyo na mazao mbalimbali yanayozalishwa nchini. 

Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita aliwapongeza wadau mbalimbali walioshiriki katika Kongamano hilo ambao ni Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Vikundi vya wajasiriamali, Makampuni ya simu, na Shirika la umeme Tanzania TANESCO ambapo alisema kuwa imani yake kuwa kongamano hilo litaibua chachu katika uzalishaji wa kilimo na uhifadhi bora wa chakula.

Alisema kuwa umuhimu wa kongamano hilo unaakisi Kaulimbiu ya maadhimisho ya Chakula duniani kwa mwaka 2017 isemayo Badili mwelekeo wa uhamaji; Wekeza katika usalama wa chakula na maendeleo Vijijiniikiwa ni sehemu ya ubashiri wa kutokea mzozo mkubwa wa chakula.

Alisema jukumu muhimu la kilimo cha familia katika kuangamiza njaa na umaskini ni kuhakikisha kuna usalama wa upatikanaji wa chakula na lishe bora, kuboresha kipato, kusimamia vyema rasilimali, kuyalinda mazingira na kufanikisha maendeleo endelevu, hususani katika maeneo ya mikoani.

Katika Kongamano hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo Mada ya Mchango wa sera ya kilimo katika magaezi ya uchumi wa viwanda, Mikopo nafuu kwa mapinduzi ya kilimo na viwanda, Mchango wa mfuko wa pembejeo katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kupambana na njaa na kupunguza umasikini hususani vijijini.

Mada zingine rafiki katika kongamano hilo ni pamoja na Mchango wa mbegu bora katika usalama wa chakula, Umuhimu wa kilimo cha mazao ya mizizi kwa kuboresha lishe na kipato cha jamii, sumu Kuvu kwenye mahindi (Madhara katika sekta ya kilimo, Biashara na afya ya binadamu), Msingi wa uhuru wa kiuchumi na Tanzania ya Viwanda sambamba na Ufugaji nyuki unaoongeza mavunoya asali na kipato katika kaya.

Akiwasilisha mada kuhusu mchango wa sera za kilimo katika mageuzi ya uchumi wa viwanda Mchambuzi na mshauri wa sera kutoka Wizara ya kilimo Ndg Revelian Ngaiza Alisema kuwa Sera ya Taifa ya kushajiisha uwekezaji ya mwaka 1996 na Sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 imeiweka sekta ya kilimo kama sekta kiongozi katika uchumi hivyo Sekta hiyo imeendelea kuwa uti wa mgongo katika kukuza uchumi kwa kipindi cha kati na cha muda mrefu.

Alisema kuwa Será ya Taifa ya kilimo ya mwaka 2013 ilidhamiria Kuwezesha kuwepo mabadiliko ya sekta ya kilimo kuwa kilimo cha kisasa, kibiashara na sekta yenye ushindani ili kuhakikisha usalama wa chakula na upunguzaji wa umaskini kutokana na ongezeko la uzalishaji wa mazao yenye ubora.

Aliendelea kusema  kuwa katika Serikali ya Awamu ya tano kumekuwa na mikakati na programu mbalimbali ambazo zimetekelezwa na kuchangia kikamilifu katika kukuza kilimo na hifadhi ya jamii.  Alitaja programu na mikakati ambayo ni Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDS) wa mwaka 2002; na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II) ya mwaka 2006.

Ngaiza alisema Mabadiliko ya ukuaji wa sekta ya kilimo hadi kufikia kuchangia kwa kiasi kinacho ridhisha katika ukuaji wa uchumi wa Viwanda na upunguzaji wa umaskini bado kunahitajika juhudi za kila mdau miongoni mwao ni Serikali, wakulima, sekta binafsi, wanataalum n.k ili kutimiza azma hiyo.

Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Chakula Duniani hapa nchini Tanzania Kitaifa yatafikia ukomo tarehe 16 Oktoba 2017 katika Viwanja vya CCM Kalangalala, ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Dkt Charles Tizeba. 

Maadhimisho ya kwanza ya siku hii yalianza mwaka 1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na maadhimisho ya  miaka 72 ya kuanzishwa kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.

NEC YASISITIZA AMANI NA UTULIVU UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATIKA KATA 43

$
0
0
NEC –DODOMA

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan amewaasa wadau wa uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika katika Kata 43, Novemba 26 unafanyika kwa amani na utulivu.

Bw. Kailima ameyasema hayo leo (Jumamosi) mjini Dodoma wakati wa maandalizi ya mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi yanayotarajiwa kuanza kesho (Jumapili) mjini hapa.

“Mlango wa kuchukua fomu kwa ajili ya uteuzi utafunguliwa kuanzia tarehe 20 saa moja na nusu asuhuhi mpaka 25 mwenzi huu, na fomu zinatakiwa kurejeshwa na uteuzi utafanyika tarehe 26 mwenzi Oktoba saa kumi kamili jioni. Nawasihi wadau wote wa uchaguzi tufanye uchaguzi wetu uwe wa amani na utulivu, natumaini kama ambavyo nchi yetu ni kisiwa cha amani na kwa jinsi tulivyojipanga (Tume) uchaguzi utakua wa amani na utulivu,” amesema.

Bw. Kailima amesema kuwa katika mchakato wa kuendea siku hiyo ya uchaguzi NEC hairuhusu mikutano ya vyama vya siasa bali inaruhusu mikutano ya kampeni.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi hairuhusu mikutano ya vyama vya siasa, Tume inaruhusu mikutano ya kampeni kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe 27 Oktoba mpaka tarehe 25 Novemba 2017, siku moja kabla ya uchaguzi. Kampeni lazima ziendeshwe kwa utaratibu uliopangwa,” amesema Bw. Kailima.

Akizungumzia kuhusu maadili ya Uchaguzi, amesema kwa mujibu wa Kifungu Namba 124A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume, Serikali na vyama vya siasa vyote vinapaswa kukubaliana na maadili ya uchaguzi ambayo yalisainiwa na wadau wote tarehe Julai 27, 2015.

“Nitoe wito kwa wadau wa uchaguzi kwamba pale ambapo patakua na ukiukwaji wa maadili, malalamiko yapelekwe kwenye kamati husika saa 72 baada ya tukio husika, kwa ngazi hii ya udiwani malalamiko yanatakiwa yapelekwe kwenye kamati ya maadili ngazi ya Kata ambayo wajumbe wake ni vyama vyote vya siasa vyenye wawakilishi walioteuliwa. Msimamizi msaidizi ngazi ya Kata ndiyo mwenyekiti wa kamati,” amesema.

Bw. Kailima ameongeza kusema kwamba endapo maamuzi hayataridhiwa wahusika wanaruhusiwa kukata rufaa ngazi ya Jimbo ambapo msimamizi wa uchaguzi atatoa maamuzi na endapo hayakuridhiwa jambo hilo litakua ni lalamiko la uchaguzi baada ya uchaguzi kukamilika.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba mafunzo hayo yatahusisha washiriki 144 ambao ni Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimizi wasaidizi na maafisa uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata na yatafanyika kwa siku tatu kuanzia kesho Oktoba 15 hadi 17, 2017.

“Uchaguzi huu mdogo utafanyika kwenye Kata 43 ambazo zipo kwenye mikoa 19, Hamashauri 36 na Majimbo 37 kwa hiyo uchaguzi huu mdogo unafanyika karibia maeneo ya nchi nzima,” alisema Kailima.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images