Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1401 | 1402 | (Page 1403) | 1404 | 1405 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza katika hafla ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki ( wa nane kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa tano kushoto) akiwa Wakurugenzi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii katika hafla ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Mtendaji Bodi ya Utalii, Devota Mdachi akiwa na mshindi wa kwanza Peter Philemon aliyeibuka katika kipengele cha Wapagazi bora kwa mwaka 2017 mara baada ya kumkabidhi tuzo. Kushoto ni Katibu wa tuzo hiyo, Ally Mtemvu. Lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na kuhamasisha utoaji wa huduma bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya juu kwa watalii nchini.
  Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deogratius Mdamu akimkabidhi cheti na mshindi wa kwanza, Yohana Tumaini aliyeibuka katika kipengele cha Wapishi bora kwa mwaka 2017 ikiwa lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na kuhamasisha utoaji wa huduma bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya juu kwa watalii nchini
  Baadhi ya Waongoza watalii bora wakifuatilia kwa makini utoaji wa tuzo kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Lusungu Helela- Maliasili
  Mkurugenzi wa Masoko wa Hifadhi ya Taifa ya Tanzania,Ibrahim Musa akikamkabidhi cheti mmoja wa washindi katika katika hafla ya utoaji tuzo kwa waongoza watalii iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga Iringa Damas Mgimwa akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi wakati wa kukata utepe wa kufngua choo hicho
  Mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakikagua ubora wa vyumba vya vyoo hivyo
  Hili ndio jengo jipya la choo kipya kilichojengwa na Tosamaganga Alumni Association kwa gharama ya shilingi millioni 30
  Hawa ni baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha  fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo.

  Na Fredy Mgunda.

  Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha  fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo kwa kuwa ndio umekuwa msingi bora wa mafanikio ya wanafunzi wengi waliosoma katika shule hiyo.

  akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi choo hiyo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa lengo ni kukikisha kila wakati wanatafuta pesa za kusaidia kukarabati shule hiyo kutokana na miundombinu ya sasa si rafiki kwa wanafunzi.

  "Maendeleo niliyopata mimi ni kutokana na kupata elimu katika shule ya Tosamaganga hivyo lazima tuikumbuke kwa kuendelea kuipatia msaada kadili tunavyoweza maana ukituangalia hapa unatuona wote tunavipato vizuri hivyo ni budi kukumbuka wapi tumetoka na tulikotoka kupoje tujia hivyo tutaithimini hii shule kila wakati kama tulivyofanya hivi sasa" alisema Mbilinyi

  Mbilinyi aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.

  “Leo nimerudi katika shule hii ya Tosamaganga kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi  tumeanza kwa kujenga choo lakini changamoto bado zipo nyingi" alisema Mbilinyi

  kwa upande wake mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa aliwataka wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya hiyo wawe vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali kurudisha fadhila katika shule hiyo.

  "Nimekuwa nikipiga kelele muda mrefu kwenye vyombo vya habari muda mrefu juu ya kuzijali hizi shule zilizotuletea mafanikio ila saizi naanza kuona matumaini ya wanafunzi wengi wanazikumbuka shule walizosoma hapo awali ni jambo kubwa na la faraja sana" alisema Masunya 

  Masunya  alisema kuwa shule nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbli zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule walizosoma.

  “Wafanyakazi na viongozi mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania” Alisema Masunya

  Naye Wakili msomi Protas Ishengoma aliwaomba wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.

  “Hebu angalia sisi tuliosoma hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado ipo pale pale na inazidi kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili kurudisha fadhila kwa kuwa wengi wetu tumepata mafanikio makubwa kutoka shule hii,tunaviongozi wengi,matajili wengi ,wakulima wakubwa sana hapa nchini wote wamesoma katika shule hii”.alisema Ishengoma

  Shule ya Tosamaganga ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali,taasisiza Umma na sekta walijengewa msingi wa kwanza wa maisha sasa kwanini leo hii hawazi kumbuki.

  katika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake. 

  0 0  0 0


  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Zabron Bugingo,akielezea mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa waandishi wa habari waliohitimu mafunzo ya uwandishi wa habari vijijini Mkoani Morogoro pindi walifanya ziara katika halmashauri hiyo jana.(Picha na Pamela Mollel).

  Picha ikionesha miche ya korosho ikiwa katika hatua ya awali ya uoteshwaji.
  Picha ikionesha jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohitimu mafunzo ya uwandishi wa habari za vijijini wakiwa katika boti kuelekea katika ziara ya kuona na kujifunza magofu ya kale kisiwani kilwa.
  Mkazi wa Kilwa Masoko akiwa amebeba beseni la Samaki tayari kwa kufanyashughuli za ujasiliamali.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilwa Zabron Bugingo akiwa ameambatana na timu ya waandishi wa habari waliohitimu mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini katika ziara kisiwa cha kilwa Masoko.
  Baadhi ya waandishi wa habari walihitimu mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini wakiwa wameshuka katika boti tayari kwa kuanza ziara katika mji wa kihistoria Kilwa Masoko.
  Mkuu wa kitengo cha uhifadhi katika mji wa kihistoria kilwa Revocatus Wejja,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walihitimu mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini pindi walipofanya ziara katika eneo hilo.
  Moja ya eneo katika mji wa kihistoria kilwa Masoko ambapo panadaiwa kuwa nyumba za kale zilifunikwa.
  Moja ya waandishi wa habari waliokuwa katika ziara hiyo Felician Shija akiangalia eneo linalodaiwa kufukiwa nyumba za wakoloni katika kisiwa cha kilwa Masoko.
  Picha ikionesha shule ya Msingi Kisiwani iliyopo jirani na Mji wa kihistoria wa kilwa masoko.
  Baadhi ya waandishi wa Habari Adam juam na Agustino Kihombo wakiwa katika jiwe la shule ya Msingi Kisiwani iliyopo jirani na Mji wa Kihistoria Kilwa Masoko.
  Baadhi ya Makabuli ya wakoloni yaliypo katika kisiwa cha kilwa masoko.

  Mkuu wa kitengo cha uhifadhi katika mji wa kihistoria kilwa Revocatus Wejja,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari namna watakavyoboresha mlango wa msikiti ambao ulikuwa ukitumika na wakoloni katika kisiwa cha kilwa msoko kushoto Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Zabron Bugingo,
  Mkuu wa kitengo cha uhifadhi katika mji wa kihistoria kilwa Revocatus Wejja,akiwaonyesha waandishi wa habari sehemu ya kuchanganyia chokaa kwaajili ya kuboresha majengo hayo
  Mkuu wa kitengo cha uhifadhi katika mji wa kihistoria kilwa Revocatus Wejja,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusiana na gereza ambalo lilikuwa likitumika na wakoloni
  Jengo la msikiti ambao ulikuwa ukitumika na wakoloni katika kisiwa cha kilwa masako

  0 0

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kuhusu namna ya kuikabili Sumu Kuvu kutoka kwa Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya Boga kutoka kwa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mara baada ya kutembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  Afisa habari na Uelimishaji Jamii kutoka Mamkaka ya Chakula na Dawa Bi Robert Feruzi (Kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa jinsi Mamlaka hiyo inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo kutoka Benki ya wakulima (TADB) Ndg Joseph Mabula (Kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (KUshoto) jinsi inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akionyesha Mvinyo uliotengenezwa na wajasiriamali wadogo wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akikagua mashine mbalimbali katika Banda la kampuni ya POLY MACHINERY CO.LTD kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akikagua baadhi ya vyakula vilivyohifadhiwa kwenye vifungashio kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.

  Na Mathias Canal, Geita

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.

  Alisema kuwa elimu hiyo inatakiwa kutolewa katika maeneo mbalimbali nchini ili wananchi waweze kutambua namna bora katika uandaaji wa mashamba wakati wa msimu wa kilimo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mashamba hayashambuliwi na magugu wala wadudu waharibifu.

  Naibu Waziri ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam mara baada ya kutembelea Banda hilo wakati wa Maonesho ya 36 ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita kuanzi Octoba 10 mpaka Octoba 16.

  Dkt Mwanjelwa alisema kuwa wakulima wengi nchini wanalima pasina kufahamu taratibu za kilimo cha kisasa jambo ambalo linapelekea mazao yao kuathiriwa na wadudu husani Sumu Kuvu na kupelekea uduni wa mavuno.

  Alisema kuwa endapo Taasisi hiyo ya (IITA) itaongeza nguvu ya utoaji elimu kwa wakulima kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya kilimo, wananchi watanufaika na kilimo chao ikiwa ni pamoja na kuwa na mavuno mengi.

  Alisema Sumu Kuvu inahatarisha afya za watumiaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara, kwani chakula na malisho ya mifugo iliyo athiriwa na sumu kuvu hupunguza uzalishaji huku mazao yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa kutekelezwa au yanauzwa kwa bei ya chini.

  Aidha, zipo athari za moja kwa moja kwani endapo binadamu au mnyama atakula chakula chenye malisho yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu anaweza kupoteza maisha.

  Kwa upande wake Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam alisema kuwa Sumu Kuvu huzalishwa wakati fangasi aina ya Aspergillus anaposhambulia mbegu shambani/ghalani.

  Aliongeza kuwa Ukuaji wa fangasi na athari za sumu kuvu husababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Ukame wa ongezeko la joto), Mbinu duni za kilimo kabla na baada ya kuvuna mazao kwa mfano; ukaushaji hafifu wa mazao punde yanapovunwa, na uhifadhi duni wa mazao ghalani na wadudu waharibifu.

  Sumu Kuvu ni aina za kemikali za sumu zinazozalishwa na aina ya Ukungu au Fangasi wanaoota kwenye mbegu za nafaka kama vile mahindi, mbegu za mafuta kama karanga, jamii ya kunde na pia mazao ya mizizi. Pia sumu Kuvu hupatikana katika bidhaa za mifugo kama vile maziwa, mayai na nyama pale ambapo chakula kinacholiwa na mifugo kitakuwa kimechafuliwa na sumu hizo.

  Sambamba na hayo pia Naibu waziri wa Kilimo  Mhe Dkt Mary Mwanjelwa alitembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya kilimo, Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Banda la Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA).


  Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani hufanyika kila mwaka kuanzia Octoba 10 mpaka Octoba 16 ambapo kwa mara kwanza  yalianza mwaka 1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na maadhimisho ya  miaka 72 ya kuanzishwa kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.

  0 0

  Washindi wa zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
  Meneja usambazaji wa Coca-Cola Mwanza, Samwel Makenge akikabidhi pikipiki kwa baadhi ya washindi wa promosheni ya mchongo chini ya Kizibo inayoendelea katika mikoa ya kanda ya ziwa. --- Promosheni ya ‘Mchongo chini ya kizibo’iliyozinduliwa na Coca-Cola mkoani Mwanza hivi karibuni inazidi kuibua washindi ambapo wakazi watatu wa jijini Mwanza wamejishindia Pikipiki na wengine wanaendelea kujishindia televisheni na zawadi mbalimbali. 
   
  Promosheni hii inahusisha vinywaji vya Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida na inafanyika mkoani Mwanza na mikoa mingine ya kanda ya ziwa ikiwemo mikoa jirani yake ya Shinyanga na Kigoma na itawawezesha wateja kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure.
   
   Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi,alisema lengo la promosheni hii kubwa ni kuwazawadia na kuwashukuru wateja wanaotumia bidhaa za kampuni. 
   
  “Tumewaletea promosheni hii kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu wote wanaotumia bidhaa zetu kama mnavyoona leo washindi wa promosheni hii wamekabidhiwa zawadi zao,natoa wito kwa wananchi kuzidi kuichangamkia ili kujishindia zawadi kwa kuwa bado kuna zawadi nyingi za kushinda”alisema Kisusi. 
   
  Mmoja wa washindi wa Pikipiki,TV, Almes Issa, mkazi wa kitongoji cha Mkuyuni akiongea kwa furaha alisema kuwa hakuamini macho yake baada ya kunywa soda ya Coca-Cola na kufanikiwa kukusanya vizibo vinavyowezesha kupata zawadi ya Pikipiki “Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi ambavyo nimeweza kukabidhiwa zawadi yangu kwa haraka,natoa wito kwa wakazi wa Mwanza tuchangamkie promosheni hii tuweze kujishindia zawadi kama nilivyoshinda mimi”alisema. 
   
  Naye mkazi wa Misungwi, Augustino Juma,ambaye ameshinda Pikipiki alisema kuwa kwa ushindi aliopata maisha yake yamebadilika kwa kuwa ataitumia katika shughuli za biashara ya ‘bodaboda’kwa ajili ya kuogeza kipato cha familia. 
   
  Washindi wengine waliokabidhiwa zawadi mwishoni mwa wiki ni Lucas Gwanjingi aliyejishidia pikipiki,Maria Simon aliyejishindia TV na Enock Matusera aliyejishindia T shirt ya Coca-Cola. Kisusi, alisisitiza kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. 
   
  Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’.
   
   Alisema zawadi zote kubwa zitatolewa kwa washindi kiwandani na zawadi ndogondogo zitatolewa kwa mawakala wanaouza bidhaa za kampuni na magari ya usambazaji vinywaji vya Coca-Cola.

  0 0

  Serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.

  Hayo yamebainishwa wilayani Mwanga na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipozindua rasmi oparesheni maalum ya uvamizi na utambuzi wa mifugo hiyo tokea angani.

  Mpina alisema kuwa uvamizi wa mifugo hiyo tokea nchi jirani ya Kenya unaleta changamoto kubwa ya malisho ya mifugo ya ndani ya nchi unaopelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji na husababisha mmomonyoko wa udongo na uharibifu wa mazingira.

  Baada ya kupokea taarifa ya timu ya wataalam iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Mifugo na Uvuvi Dkt Maria Mashingo, iliyofanya oparesheni hiyo maalum kwa kutumia ndege ya shirika la taifa la hifadhi ya wanyamapori, (TANAPA) taarifa iliyobaini kuwepo kwa makundi makubwa ya ng’ombe waliokuwa wakihama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuwepo kwa idadi kubwa ya Maboma, Waziri Mpina alisema ,

  “ Haiwezekani ng’ombe wanaingia kwa makundi makubwa hivi nchini na watendaji wa serikali wapo, lazima kutakuwa na shida katika utendaji, Oparesheni hii itakuwa ni ya mwisho, kwa ng’ombe watakaoingia tena watendaji watatolewa sadaka.” Alibainisha Mpina.

  “Yawezekana ng’ombe wote 4000 ambao inasemekana walitoroshwa hapo awali wapo, hivyo Oparesheni ianze rasmi tuwakamate ng’ombe wote, tuheshimu sana sheria, na nchi jirani tushirikiane katika mambo tuliyokubaliana kisheria na lolote litakalotokea katika suala hili la uvamizi wa mifugo sheria itachukua mkondo wake na tusilaumiane” Alisisitiza Mpina.

  Awali wataalam waliyokuwepo katika oparesheni hiyo maalum waliezeza kuwa mifugo mingi iliyoonekana kutokea angani ilikuwa zaidi katika maeneo ya malisho na maji ya vijiji vya kiti cha Mungu,njiapanda,kirya na kitongoi cha Mangulai.

  Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilya ya Mwanga imeingia kazini tayari kwa kuanza oparesheni hiyo maalum. 

   Katika picha kikosi kazi maalum cha oparesheni ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga inayotokea katika nchi jirani ya Kenya , mbele ni rubani wa ndege hiyo maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani akiongoza ujumbe huo kupanda ndege katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na kikosi kazi maalum kikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Maria Mashingo na Rubani wa ndege hiyo  maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani walipokuwa wakijiandaa kwenda kwenye oparesheni maalum ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika wilaya ya Mwanga wanaotokea katika Nchi jirani ya Kenya.
  Waziri Mpina akimpungia mkono Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvivi Dkt Maria Mashingo akiwa na baadhi ya wajumbe wakiingia  kupanda ndege maalum kuanza oparesheni ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga wakitokea Kenya.

  0 0

  Wasanii Jux na Mimi wakimkabidhi mteja wa Tigo, Tumaini Mwikanalo zawadi kwenye duka la Tigo jijini Mbeya.
  Mtoa huduma akipiga picha 'selfie' na wasanii Dogo Janja na Ben Pol.
  Ben Pol akiangalia simu dukani halo.

  Msanii wa bongo fleva STAMINA akipokea simu smartphone aliyonunua kwenye duka la Tigo jijini Mbeya toka kwa mtoa huduma wa Tigo Mohammed Musa jana. Hii ni sehemu ya punguzo litolewalo ndani ya msimu huu wa Tigo Fiesta.


  0 0

   Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Upendo Njogolo  (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo katika soko la Zakhem  Dar es Salaam, kuhusu kampeni inayoendelea ya akaunti za Malengo ya benki hiyo. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
   Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Evansia Kassuma (katikati), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo katika soko la Zakhem, Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana, kuhusu kampeni inayoendelea ya akaunti za Malengo ya benki hiyo. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
   Waendesha bodaboda wa eneo la Kimara, Dar es Salaam wakimsikiliza Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Upendo Njogolo  (kushoto), wakati akizungumza nao kuhusu kampeni inayoendelea ya akaunti za Malengo ya benki hiyo. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
   Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiangalia wacheza shoo wakati wa kampeni inayoendelea ya akaunti ya Malengo ya Benki ya NBC. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
   Kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC pia ilifikishwa hadi katika kijiwe cha muuza kahawa huyu ambako walijulishwa fursa wanazoweza kuzipata kiuchumi wakifungua akaunti ya Malengo ya NBC ambayo licha ya kujishindia zawadi mbalimbali lakini pia hakuna gharama za kila mwezi za kuendeshea akaunti hiyo hivyo kuwezesha akiba zao kukua.

  Wachuuzi wa mboga mboga nao wakisikiliza kwa makini jinsi wanavyoweza kubadisha maisha yao kiuchumi mara watakapojiunga na akaunti aya Malengo ya NBC. Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC inafanyika nchini kote ambapo washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.


  0 0

  Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Eng. Nyamhanga Wanda, akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, mkoani Mbeya.
  Mkandarasi anayejenga jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Kannan Thiyagamoorthy, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, mkoani Mbeya.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, (kushoto) , akikagua ujenzi wa jengo la abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Waziri huyo alifanya ziara ya ukaguzi na kuangalia maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi huo hadi sasa. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa.
  Muonekano wa Jengo la abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA). Jengo hilo limetakiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi Januari, 2018
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza na wananchi wa Tunduma wakati akikagua upanuzi wa njia nne ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45, mkoani Mbeya.
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Songwe Eng. Yohane Kasaini (katikati), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), wakati wa ukaguzi wa upanuzi wa njia nne ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45, mkoani Mbeya.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45 inayojengwa kwa njia nne, mkoani Mbeya ili kupunguza msongamano wa magari jijini hapo.

  ………………………………………………………………………


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa mkandarasi GM Construction anayejenga jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), kukamilisha ujenzi huo.

  Amesema Serikali hairidhishwi na kasi ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limetumia miaka minne badala ya miwili iliyokubalika katika mkataba wa awali hivyo kumtaka mkandarasi huyo kuhakikisha analikabidhi jengo hilo ifikapo Januari 30 mwakani.

  “Kushindwa kukamilisha jengo hili ifikapo mwezi Januari mwakani itakuwa ndio tiketi yako ya mwisho ya kutopewa kazi kwasababu Serikali hii inafanya kazi kwa kuzingatia ubora na muda”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa kusimamia kikamilifu ujenzi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa

  “Ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege kwa sasa unasimamiwa na TANROADS na uendeshaji wake unasimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuongeza kasi ya ujenzi wa viwanja vya ndege na ubora wa huduma zinazotolewa katika viwanja hivyo”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa, amekagua upanuzi wa barabara katika mji wa Tunduma unaolenga kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo na kuwahakikishia wananchi kuwa ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi ujao.Amewataka wakazi wa Tunduma kuilinda miundominu ya barabara hizo kwa kuzingatia matumizi sahihi ili kuleta usalama kwa wananchi.

  Naye Meneja wa TANROADS, mkoa wa Songwe Eng. Yohane Kasaini, amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kwamba barabara za michepuko zitaongezwa katika eneo la Tunduma ili kurahisisha shughuli za kibiashara na uzalishaji katika mji huo.

  Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua miundombinu katika mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.

  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb.) akizungumza na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya kuhusu kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya biashara, viwanda na uwekezaji kati ya Tanzania na India. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Oktoba, 2017. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.), Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Magabilo Murobi (hawapo pichani). 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima (wa pili kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Magabilo Murobi (wa kwanza kulia) wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mwijage na Balozi wa India nchini (hawapo pichani). 
  Mhe. Dkt. Kolimba akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Waziri Mwijage na Balozi Arya. 
  Mazungumzo yakiendelea

  0 0

  Mwanafunzi wa kidato cha nne, Doroth Samson akizungumza na waandishi wa habari

  WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist iliyopo Boko Basihaya katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameonyesha kufurahishwa na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya '3D' yenye maana ya !Nidhamu, Nidhamu, Nidhamu! kuwa imewaongezea morali wa kufanya vizuri darasani. 

  Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wanafunzi hao walisema kampeni hiyo imewasaidia sana katika kufanya vizuri katika masomo yao darasani kwa kile walichodai kuwa kuwa bila ya nidhamu katika jambo lolote hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana. Doroth Samson mmoja wa wanafunzi hao wa kidato cha nne shuleni hapo alisema hawana budi kuupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuzindua kampeni hiyo kwani imewasaidia kuwaongezea nidhamu ya hali ya juu ambayo ni chachu ya kufanya vizuri katika masomo yao. 
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya John Baptist, Aspiter Kibona akizungumza na waandishi wa habari. 


  Akaongezea pia, kutokana na nidhamu "Kwa kweli naweza kuthubutu kusema shule hii ni ya pekee ya wasichana ambayo inaongoza kwa nidhamu ya hali ya juu sana na kizuri zaidi nidhamu iliyopo shuleni hapa si kwa wanafunzi pekee bali ni kuanzia kwa Mkurugenzi, Mkuu wa shule, walimu na wafanyakazi wengine, " alisema Samsoni. 

  Mwanafunzi mwingine wa kidato cha tatu shuleni hapo, Vanessa Kyamasi yeye kwa upande wake alisema anajivunia kusoma katika shule hiyo kwani ina kila sifa inayotakiwa kwa mwanafunzi anayependa kusoma. Kyamasi alisema shule hiyo ni moja ya shule za kuigwa nchini kutokana na nidhamu kubwa iliyopo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo chache inayochangia wafanye vizuri katika masomo yao darasani.. 

  Naye Mkuu wa shule hiyo, Aspiter Kibona lengo la kampeni hiyo ni kumkomboa mtoto wa kike katika kuhakikisha anafanya vizuri katika masomo yake darasani. Kibona alisema waliamua kuzindua kampeni hiyo ikiwa ni kauli mbiu yao kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walimu na wafanyakazi wengine kuzingatia nidhamu muda wote ambayo itaendelea kuchochea maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
  Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiwa wanajisomea darasani.

  ‘Maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi hutokana na mambo mengi ila moja kubwa ni nidhamu ya hali ya juu ambapo shule yetu ndio msingi wake mkuu wa matokeo mazuri kwa wanafunzi wetu, Mwaka jana kati ya wanafunzi 33 ambao walimaliza kidado cha nne wanafunzi 30 walifanikiwa kwenda kidato cha tano’ 

  Akiendelea kufafanua kuhusiana na maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi Mr. Kibona aliwakaribisha wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na kidato cha kwanza na kwamba usaili kwa mhula unaokuja umeshaanza. Ambapo utamalizika tarehe 4/ 11/2017. Fomu za kujiunga zinapatikana katika maeneo yafuatayo Shuleni-Boko Basihaya, Msimbazi Center Duka No 19, Tanzania Schools Directory-Sinza, Michele Saloon –Mbezi Beach Africana Kwa maelezo Zaidi ya jinsi ya kujiunga na shule ya John Baptist unaweza kuyapata kupitia tovuti www.johnbaptistsec.co.tz, simu no 0754002900/0754002700

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mwanjelwa akipokea zawadi ya boga lenye uzito wa kilogramu 11 kutoka kwa Afisa Kilimo (Kitengo cha Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo) kutoka Halmashauri ya Bukombe katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofikia kilele leo tarehe 16 Oktoba, 2017 Mkoani Geita

  0 0

  *Asisitiza Uwaziri si fursa ya kujitajirisha          
                             
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri watumie madaraka yao kwa manufaa ya Taifa na kamwe wasiyatumie kama fursa ya kujitajirisha wao binafsi.

  Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 16, 2017) alipozungumza na baadhi ya Mawaziri, Manaibu na Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

  Amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza kwamba amewateua ili wafanye kazi na kamwe wasitumie madaraka waliyopewa kwa maslahi yao binafsi.

  “Madaraka haya ya Uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za wananchi kwa wakati.”

  Amesema Mawaaziri na Manaibu Waziri wazingatie Katiba ya nchi, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Serikali katika utekelezaji wa majikumu yao ya kila siku.Waziri Mkuu amesema Mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

  Pia utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri wahakikishe wanakwenda kufanya ufuatiliaji wa tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao.

  Pia amewataka Mawaziri hao wakasimamie kikamilifu ukusanyaji wa mapato na kuanzisha vyanzo vipya vya ukusanyaji pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu.Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri hao wakapunguze urasimu katika utekelezaji wa malengo ya Serikali kwa sababu wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa wakati.

  Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bw. Suileiman Jaffo pamoja na Manaibu wake Bw. Joseph Kandege na Bw. George Kakunda, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile.

  Wengine ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu wake Bw. Jumaa Aweso, Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijabe na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.

  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Bw. Josephat Hasunga, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Naibu wake Bw. William Ole Nasha, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Abdallah Ulega pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.


  0 0

   Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56) akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka aliyonayo.

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
  MHASIBU wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56), leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka tisa matatu ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo  wizi akiwa mtumishi wa umma, kujipatia fedha kwa njia ya uongo na utakatishaji wa fedha USD 150,000.

  Mwendesha mashtaka wakili wa serikali, Wankyo Simon amedai Octoba 25 mwaka jana, katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania katika jiji la Maputa nchini msumbiji mshtakiwa Joyce kwa lengo la kufanya udanganyifu alighushi barua ya tarehe 25 October 2016 kwa madhumuni ya kuonesha kuwa ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.

  Imedaiwa kuwa, akaunti zote hizo zipo katika benki ya Millennium Bim-Julius Nyerere Maputo, huku akijua kuwa siyo kweli.

  Aidha mshtakiwa Joyce anayeishi Temeke anadaiwa Februari 10 mwaka huu huko huko Ubalozini nchini msumbiji, alighushi USD 100,000 na pia Aprili 12 mwaka huu alighushi tena USD 40,000.
  Katika shtaka linguine Wankyo alidai kuwa, Oktoba 25, mwaka jana katika benki ya Millenium Bim-tawi la Julius Nyerere lililopo Maputo nchini Msumbiji. 

  Imedaiwa, mshtakiwa akifahamu na kwa njia ya udanganyifu aliwasilisha nyaraka ambayo ni barua ya tarehe Oktoba 25 mwaka jana kwa dhumuni la kuonyesha kuwa,  ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.

   Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56) akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka aliyonayo.

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
  MHASIBU wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56), leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka tisa matatu ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo  wizi akiwa mtumishi wa umma, kujipatia fedha kwa njia ya uongo na utakatishaji wa fedha USD 150,000.

  Mwendesha mashtaka wakili wa serikali, Wankyo Simon amedai Octoba 25 mwaka jana, katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania katika jiji la Maputa nchini msumbiji mshtakiwa Joyce kwa lengo la kufanya udanganyifu alighushi barua ya tarehe 25 October 2016 kwa madhumuni ya kuonesha kuwa ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.

  Imedaiwa kuwa, akaunti zote hizo zipo katika benki ya Millennium Bim-Julius Nyerere Maputo, huku akijua kuwa siyo kweli.
  Aidha mshtakiwa Joyce anayeishi Temeke anadaiwa Februari 10 mwaka huu huko huko Ubalozini nchini msumbiji, alighushi USD 100,000 na pia Aprili 12 mwaka huu alighushi tena USD 40,000.
  Katika shtaka linguine Wankyo alidai kuwa, Oktoba 25, mwaka jana katika benki ya Millenium Bim-tawi la Julius Nyerere lililopo Maputo nchini Msumbiji. 

  Imedaiwa, mshtakiwa akifahamu na kwa njia ya udanganyifu aliwasilisha nyaraka ambayo ni barua ya tarehe Oktoba 25 mwaka jana kwa dhumuni la kuonyesha kuwa,  ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.

  Pia aligushi barua ya Februari 10 mwaka huu ili kuhamisha USD 100,000 na barua ya Aprili 12 mwaka huuu ili kuhamisha USD 40,000.
  Mshtakiwa Joyce anadaiwa pia kuwa, katika siku tofauti tofauti kati ya Oktoba 25 mwaka jana na Aprili mwaka huu, katika ofisi hizo za Ubalozi, akiwa muajiriwa wa utumishi wa umma wa kitengo cha fedha ubalozini hapo, aliiba USD 150,000 mali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

  Pia Joyce anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha pesa kwa njia ya udanganyifu kwa kujifanya kuwa ameelekezwa kutoa fedha hizo kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inaymilikiwa na Joyce Moshi huku akaunti zote hizo zimehifadhiwa kwenye benki hiyo ya Millenium.

  katika shtaka la mwisho imedaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Octoba 25 mwaka jana na Aprili 12 mwaka huu alijipatia USD 150,000 huku akijua kuwa fedha hizo ni matokeo ya kosa la kughushi.

  Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerudishwa rumande kwa kuwa kosa la utakaishaji halina dhamana na kesi hiyo imeairishwa hadi Octoba 30 mwaka huu.
  Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

  Pia aligushi barua ya Februari 10 mwaka huu ili kuhamisha USD 100,000 na barua ya Aprili 12 mwaka huuu ili kuhamisha USD 40,000.
  Mshtakiwa Joyce anadaiwa pia kuwa, katika siku tofauti tofauti kati ya Oktoba 25 mwaka jana na Aprili mwaka huu, katika ofisi hizo za Ubalozi, akiwa muajiriwa wa utumishi wa umma wa kitengo cha fedha ubalozini hapo, aliiba USD 150,000 mali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

  Pia Joyce anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha pesa kwa njia ya udanganyifu kwa kujifanya kuwa ameelekezwa kutoa fedha hizo kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inaymilikiwa na Joyce Moshi huku akaunti zote hizo zimehifadhiwa kwenye benki hiyo ya Millenium.

  katika shtaka la mwisho imedaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Octoba 25 mwaka jana na Aprili 12 mwaka huu alijipatia USD 150,000 huku akijua kuwa fedha hizo ni matokeo ya kosa la kughushi.

  Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerudishwa rumande kwa kuwa kosa la utakaishaji halina dhamana na kesi hiyo imeairishwa hadi Octoba 30 mwaka huu.
  Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Leo siku ya Oktoba 16 dunia inaadhimisha Siku ya Chakula Duniani ambapo Shirika la Chakula Duniani (FAO) kila mwaka huadhimisha kwa shughuli na kauli mbiu mbalimbali. Kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Badili Hali ya Uhamiaji ya Baadaye: Wekeza Katika Usalama wa Chakula na Maendeleo ya Vijijini.’ Kwa mujibu wa FAO, dunia inapitia mabadiliko kadha wa kadha kila kukicha. 
   
  Watu wengi wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na sababu tofauti kama vile kuongezeka kwa migogoro na kutokuwepo usalama wa kisiasa. Lakini njaa, umasikini, na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa yanayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa ni sababu zingine za muhimu zinazochangia katika kupelekea watu kuhama.
  Miongoni mwa changamoto kubwa inayowakumba watu siku za hivi karibuni ni katika upatikanaji wa chakula, matumizi yake na namna ya kudhibiti ili kutoleta athari katika mwili. Kwa kuwa leo ni maadhimisho ya ‘Siku ya Chakula Duniani,’ Jumia Travel ingependa kukushirikisha aina za vyakula vya kupunguza au kuacha kula kabisa kama unataka kupunguza uzito wa mwili wako.
  Chipsi. Kwa wakazi wengi wa sehemu za mijini kama vile jiji la Dar es Salaam, chipsi ni mojawapo ya chakula kinachotumiwa na idadi kubwa ya watu. Na hii ni kutokana na upatikanaji wake kwa urahisi karibu kwenye kila maeneo wanapoishi. Kwa mujibu wa tafiti, chakula hiki kinaongeza uzito mwilini kutokana na kuwa na kalori nyingi ndani yake na ni rahisi kuzila nyingi zaidi kwa mpigo. Tafiti pia zinaendelea kwa kuelezea kuwa chipsi pengine ndiyo chakula kinachochangia kuongeza uzito kuliko chakula chochote. Hivyo basi, kwa afya yako unashauriwa kuvichemsha kwa maji na kula badala ya kukaanga.
  Vinywaji vyenye sukari nyingi. Vinywaji vinavyotengenezwa na kuongezewa sukari ili kuwa vitamu vinatajwa kuwa ni mojawawapo vyakula hatari zaidi kiafya duniani. Vinahusishwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa uzito na vinaweza kuwa na madhara zaidi mwilini endapo vitatumiwa kwa kiasi kikubwa. Ingawa vyakula hivi huwa na kalori nyingi lakini ubongo wako hauvitambui kama ni vyakula vigumu. Kwa hiyo, kama una nia ya dhati kabisa ya kupungua uzito ni vema ukaachana na vinywaji vya aina hii.

  Chokoleti. Inafahamika watu wengi hupendela chokoleti kutokana na utamu wake lakini ni hatari sana kiafya. Hutengenezwa kwa kuongezewa sukari nyingi zaidi, mafuta na unga uliosafishwa zaidi kiwandani kwa kiasi fulani. Chokoleti zina kalori nyingi huku virutubisho vikiwa ni vichache. Kipande cha kawaida cha chokoleti kina kadiriwa kuwa kalori takribani 200-300, huku vipande vikubwa zaidi vinaweza kuwa nazo nyingi zaidi. Lakini kwa bahati mbaya unaweza kukutana na chokoleti karibu kila mahala tena zikiwa zimewekwa kwa kutamanisha zaidi ili kukushawishi kununua. Inashauriwa kama unataka kula chakula kidogo cha kawaida badala yake kula kipande cha tunda au karanga angalau.
  Juisi za viwandani. Juisi nyingi za matunda unazoziona madukani zinakuwa na virutubisho vidogo sana ukilinganisha na tunda halisi. Nyingi huwa zinatengenezwa viwandani na kuongezewa sukari. Kiukweli, huwa na sukari nyingi na kalori sawa na soda, tena inawezekana vikazidi. Kwa kuongezea juisi za viwandani hazina nyuzinyuzi ambazo unaweza kuzipata kwenye matunda halisi. Hivyo basi unashauriwa ni vema ukala tunda kamili badala ya juisi kwani faida zake haziwezi katu kulingana kama wengi tunavyoamini.

  Mikate, biskuti na keki. Vyakula hivi huongezewa na virutubisho vingi ambavyo havina faida kwa mwili. Tena wakati mwingine huongezewa mafuta hatarishi ambayo yanahusishwa kuwa chanzo cha magonjwa tofauti. Kwa kawaida vyakula hivi havishibishi hivyo utatamani kuvitumia zaidi na hivyo kupelekea kula sumu zaidi.
  Baadhi ya vileo (hususani bia). Kwa kiasi kikubwa pombe hutuongezea kalori nyingi kuliko wanga na protini mwilini mwetu. Hata hivyo, suala la kunywa pombe na kuongezeka uzito bado halijadhibitishwa moja kwa moja. Unywaji wa pombe wa kawaida unaweza kuwa hauna matatizo na wakati mwingine huhusishwa na kupunguza uzito. 
   
  Lakini kwa upande mwingine, unywaji wa kupindukia hupelekea kuongezeka kwa uzito wa mwili. Aina ya kileo unachokunywa pia ni kitu cha kuzingatiwa. Kwa mfano, unywaji wa bia unawdza kupelekea kuongezeka uzito, huku unywaji wa divai (wine) unaweza kuwa na faida kwa afya ya mwili.

  Aiskrimu. Chakula hiki ni kitamu sana lakini ni hatari kwa afya ya mwili wako. Kwani kina kalori nyingi na huongezewa sukari nyingi kwenye utengenezaji wake. Matumizi kwa kiasi kidogo hayana madhara lakini ni vigumu sana kujizuia kutokutumia kiasi kikubwa kwa wakati mmoja. Unaweza kutengeneza wewe mwenyewe nyumbani ili kuweka virutubisho vingi zaidi lakini pia kujizuia kutumia nyingi zaidi, tenga kiasi kidogo na kingine kifiche ili kujizuia zaidi.

  Pizza. Chakula hiki ni maarufu sana maeneo ya mijini kutokana na upatikanaji wake wa haraka lakini sio vizuri kiafya kabisa. Huwa na kalori nyingi na kutengenezwa kwa kuongezewa virutubisho hatari kwa afya kama vile unga na nyama zinazochakatwa viwandani.
  Kutokana na makala haya unaweza kuwa umegundua kwamba vyakula vingi huwa vinatengenezwa viwandani na kuwekewa kemikali nyingi ili kuongezewa ladha na kutumika kwa muda mrefu zaidi. Jumia Travel ingepependa kukushauri kula vyakula vya asili zaidi au kupika mwenyewe kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unajitengenezea fursa ya kuepuka magonjwa mengi zaidi sasa na siku za usoni.

  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma.

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Khamis Mgalu, ameripoti rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma asubuhi hii, Oktoba 16, 2017.
  Naibu Waziri Mgalu amepokelewa na watumishi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini waliopo Dodoma, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda.

  Baada ya kuwasili, Naibu Waziri ametumia muda mfupi kuzungumza na wafanyakazi ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma.

  Akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya wafanyakazi, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Miriam Mbaga, amemwahidi Naibu Waziri kuwa, wafanyakazi wako tayari kumpa ushirikiano yeye na viongozi wengine wa Wizara ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwatumikia wananchi kikamlifu.

  Naibu Waziri Mgalu, ni miongoni mwa Mawaziri wapya walioteuliwa na Rais John Magufuli na kuapishwa Oktoba 9, 2017, wakati alipofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
   Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Subira Mgalu, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani), aliporipoti rasmi Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Miriam Mbaga, akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, wakati wakimpokea Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).
   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akizungumza na wafanyakazi aliporipoti rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
   Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Amon Marco (wa pili kutoka kulia), akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), wakati Naibu Waziri alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akisalimiana na watumishi, alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

  0 0

  Na Mwandishi wetu wa Globu ya Jamii
  KATIKA kuazimisha kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo  cha hayati Baba  wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Chama Cha Mapinduzi(CCM)  katibu wa chama wilaya ya ubungo ,  Salum  kali  ameweka jiwe la Msingi kwa ajili ya   ujenzi wa ofisi za chama katika tawi la sinza "A"  


  Akiutubia wanachama walio  jitokeza  katika shughuli  hiyO  kali amesema, Baba wa taifa  alitengeneza  heshima kwa  Mtanzania  aheshimu  kwanza  maadili ya taifa lake ndio aweze  kuheshimiwa na watu wengine.

  aidha kali amesema kuwa ,  Mwalimu Nyerere  aliamini ndani ya  chama  cha mapinduzi  CCM ndiko  kunapo patikana  viongozi bora  ambao wana uwezo  wa kufanya  kazi  kwa umakini pasipo  malumbano wala fujo  kama tunavyo  ona kwa wenzetu  wa pembeni.

  "Mwalimu Nyerere  aliamini  viongozi wa ccm  pekee ndio wanao weza  kusimamia  amani ya nchi hii na ndio kitu ambacho  mpaka sasa chama cha mapinduzi  kinaendelea kufanya  kupitia Rais   wa  Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli" amesema Kali.  katibu kali amesema  Baba wa Taifa   alitengeneza  upendo  huku akidumisha  amani  kubwa  ambapo  mataifa  mengi  walikuwa  wakimtumia Mwalimu  Nyerere  kwa kutafuta  Amani  katika nchi zao  na wengi  kuja  kusoma na kujifunza Tanzania  ili  waweze   kwenda kusaidia  nchi zao,  alitolea mfano moja ya nchi ya Msumbiji  na nyingine  nyingi  ambazo  zilikuja  kujifunza nchini  kwetu.

  Aidha ameongeza kuwa  sisi leo tunashindwa  kukumbuka  maadili na misingi ya Baba  wa taifa  aliyo  iweka  akiwa na nia ya  kutuunganisha  watanzania  wawe kitu kimoja,  pia waipende nchi  yao ,  wapende  maendeleo ya taifa  lao ili tusonge mbele.

  Pamoja na hayo katibu  kali  alizidi  kusema Baba  wa Taifa  aliamini mno kwenye  uaminifu,  uadilifu na uwajibikaji  huku  akiwatilia  mashaka  wale wote  walio kuwa  wanataka  kwenda  ikulu  kwani alichokua anaamini Baba wa Taifa  kuwa  URAIS  ni utumwa  ila  alishangaa kuona watu  wanagombania  kwenda ikulu. 

  Adha katibu kali  alisema  walio  zaliwa  mwaka 1974  watakumbuka  ilikuaje , lakini  watu  wanasahau  sana , sasa ivi  vijana  wa Kitanzania  wanabeza  Taifa  la TANZANIA   linalo  ongozwa na ccm, kwa kusema maisha magumu , huku  vijana hao wakiwa wamekaa na kazi  hawataki kufanya  badala yake wamekuwa wakilala mika kwenye mitandao  kuwa maisha magumu  aliwaomba vijana na kuwasihi kufanya kazi kwani akuna kitu kinacho kuja bule na wasipende  kudanganywa .

  Alimalizia kwa kusema  kwa mwendo wa  wa mwenyekiti wake wa chama cha mapinduzi CCM  ambae pia ni Rais   wa Tanzania  ana uhakika  kabisa  mpaka  kufikia  mwaka  2020  upinzani Tanzania  utabaki  kuwa ni  mavumbi  kwani  haoni  kazi zozote ambazo  wabunge wa upinzani  wakifanya  zaidi ya vurugu  na kwamba hata wakifanya   bado wanatekeleza  irani ya chama cha  mapinduzi ccm  alitoa  rai kwa wana ccm wote  kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi Baba wa taifa kwa vitendo
   Katibu wa jumuia ya wazazi mkoa wa rukwa ndg chollaje nae alishiriki ujenzi huo
   Katibu wa chama akizindua jiwe la msingi la  ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Sinza "A"  Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam
   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM)  Salum  Kali akishiriki ujenzi wa ofisi za chama kata ya Sinza A.
   Katibu wa wilaya akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  kata ya sinza Shafii Diwani
   Katibu wa wilaya akiwa kabidhi kadi wanachama wapya walio jiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kutoka vyama mbalimbali
   Mmoja wa wazee wa Chama Cha  Mapinduzi  Wilaya ya Ubungo Bi siwema  akitoa nasaha kwa wanachama wenzake
  Viongozi wa jumuia ya umoja wa wanawake (UWT)  kata ya Sinza   wakishangilia.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Mradi  wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqqaro akisalimia na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa ili kuzindua mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.


   Ugawaji wa Vyeti kwa wadau wa Utalii katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Mdau wa Utalii akipokea Cheti cha Ushiriki katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Mdau wa Utalii akipokea Cheti cha Ushiriki katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Ndugu Hanspaul ,akipokea Cheti cha Ushiriki katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.

   Mdau wa Utalii akipokea Cheti cha Ushiriki katika uzinduzi wa Mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Dk. Simon Mduma akitoa neno la Shukrani kwa wadau wa utalii katika Uzinduzi wa Mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Ndugu Chambulo, akitoa neno la Hitimisho mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.

   Mwenyekiti wa Wakala wa Utalii nchini, TATO (Tanzania Associations of Tour Operators) Ndugu Wilbard Chambulo akigonga glasi na wageni waalikwa kabla ya kuanza kwa Uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Wageni Waalikwa wakipata vinywaji kabla ya Uzinduzi wa Mradi (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project)
   Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Utalii Nchini (TATO), Ndugu Sirili Akko  akiwakaribisha na kutoa ratiba fupi kwa wageni waalikwa kabla ya kuanza kwa Uzinduzi wa Mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Wadau wa Habari wakiwa katika Uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Meza Kuu, Watatu kutoka Kulia ni Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqqaro , Ndugu Chambulo, Mzee Nunes , Ndugu Gerald Bigurube (FZS-TZ) na Dk. Simon Mduma (TAWIRI) katika Uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.

   Mzee Nunes akitoa Mada fupi katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Wadau wa Utalii nchini wakisikiliza kwa Umakini katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Wadau wa Mradi , Kutoka Kushoto ni Ndugu William Mwakitelima (TANAPA), Ndugu Abraham Saidea (DE-SNARING TEAM), Ndugu Erik Winberg (FZS Project Manager)
   Wageni waalikwa
   Kamati ya Maandalizi
   Ukumbi
   Meneja wa Mradi, Ndugu Erik Winberg akitoa Maelezo na Picha ya Mradi wa utoaji mitego kwa Wanyama pori

   Ndugu Abraham Saidea, akionyesha Nyaya zitumikazo kutega wanyamapori katika mbuga ya Wanyama ya Serengeti katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.

   Msaidizi wa Mradi, Ndugu Abraham Saidea akitoa maelezo ya jinsi Majangili wanavyowatega kwa waya Wanyamapori katika Mbuga ya Serengeti katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.

   Mdau wa Utalii akiuliza Swali kwa waendesha Mada katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Mdau wa Utalii akiuliza Swali kwa waendesha Mada katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Ndugu Salehe akiuliza Swali kwa waendesha Mada katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.


  0 0

  Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, na kulia ni Kamu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.

   NA K-VIS BLOG/Mtwara.

  Serikali imewaomba wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuwa na subira, katika kipind hiki ambapo upatikanaji wa umeme kwenye mikoa hiyo umeathirika baada ya mashine 5 kati ya 9 za kufua umeme (turbines) kuharibika.

  Hata hivyo Mafundui wa TANESCO wamekuwa katika juhudi kubwa za kuzifanyia matengenezo mashine hizo, zilizofungwa miaka 10 iliyopita.

  "tayari tumeagiza vipuri kwa ajili ya kutengeneza mashine hizo ambazo kwa ujumla wake huzalisha Megawati 18 za umeme, ambazo zitawasili ndani ya siku 7 ili kuweza kuondoa tatizo la kuzimika umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara." Alisema Dkt. Kalemani.

  Alisema, baada ya kwasili kwa vipuri hivyo, kazi ya kuzifanyia matengenezo itaendelea na amememuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, kuleta wataalamu wote wa TANESCO popote walipo nchini, wafika Mtwara na kuungana na wataalamu waliopo ili kazi ya kuzitengeneza mashine hizo iende kwa kasi.

  Kati ya mshine 9 ni mashine nne tu zinazotoa Megawati 8 ndio zinafanya kazi, hali inayosababisha kuwepo kwa mgao wa umeme unaofikia hadi masaa 8 kwa siku.

   Dkt. Kalemani ambaye amewasili mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea juhudi za Mafundi wa TANESCO  za kurejesha upatikanaji wa umeme katika hali yake ya kawaida amesema vipuri hivyo vifungwe kwa muda wa siku tatu badala ya wiki 3na kwamba ndani ya siku 10 umeme utakuwa katika hali yake ya kawaida.

  Mkoa wa Mtawara na Lindi unategemea mashine hizo zinazozalisha umeme unaotumia gesi asilia.
  Ukiachilia mbali kuharibika kwa mashine hizo, miundombinu mingine ya umeme kwenye mikoa hiyo iko salama na katika ubora wa hali ya juu ambapo vituo vipya vya kupoza na kusambaza umeme wa 132kV hapo hapo mkoani Mtwara na kingine huko Mahumbika mkoani Lindi vinafanya kazi pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme (transmission lines), nao uko katika hali bora.


   Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Evod Mmanda, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt,. Tito Mwinuka, wakitembelea kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017.
   Waziri wa Nishati Dkt. Medardi Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika
   Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
    Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
   Fundi wa TANESCO, akichukua spana ili kuendelea na kazi.
   Hii ni moja kati ya mashine zizlizoharibika.


older | 1 | .... | 1401 | 1402 | (Page 1403) | 1404 | 1405 | .... | 1897 | newer