Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

ARUSHA WAANZA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAANZA KWA KISHINDO

$
0
0
Wananchi wa Kata za Themi, Sekei na Sombetini Wilaya ya Arusha mjini leo wameanza zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa kishindo; huku baadhi wakihangaika huku na huko kutoa nakala ya viambatisho vyao ili kujisajili kwa wakati.

Akizungumza katika Usajili huo Afisa Usajili wa Wilaya hiyo Bi. Juliet amesema wamepanga kukamilisha usajili wa Kata hizo ndani ya siku 9; na kwamba wananchi wote wanaoishi katika Kata hizo kujitokeza kwa wingi ili wasajiliwe.

Misururu ya wananchi imeonekana katika Kata za Themi na Sekei; huku baadhi wakihangaika kujaza fomu za maombi ya Usajili. Katika hali iliyoonyesha ushirikiano na kujizatiti kwa viongozi katika kuhakikisha wananchi hao wanahudumiwa, ofisi za Mitaa leo zilifungwa kwa muda na huduma zote kuhamia katika makao makuu ya Kata ili kuwaidhinishia wananchi fomu zao pamoja na kuwagongea mihuri kuthibitisha makazi yao.

Zoezi la Usajili kwa Wilaya ya Arusha Mjini linatazamiwa kukamilika ndani ya miezi miwili; ambapo wananchi wataweza kupata namba za Utambulisho (NIN) wakati hatua za uzalishaji Vitambulisho zikiendelea. Wilaya nyingine mkoani humo ambazo usajili unaendelea ni Karatu, Longido, Arumeru na Monduli.
Mmoja wa Wageni Wakaazi mkoani Arusha na mkazi wa Kata ya Sekei akikamilisha Usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Zoezi la Usajili kwa mkoa wa Arusha linahusisha wananchi wenye umri wa miaka 18 na kuendelea na Wageni Wakaazi wenye kuishi halali nchini.
Watumishi wa NIDA wakiingiza taarifa za wananchi kwenye mfumo kutumia mashine maalumu ya Usajili ambayo pia inauwezo wa kuhifadhi si tu taarifa za kawaida pia alama za kibaiolojia na picha za waombaji wa Vitambulisho wakati wa Usajili.
Ofisi ya Kata ya Themi ambako zoezi la Usajili limeanza rasmi, na kukutanisha mamia ya wananchi kupata huduma.
Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji makao makuu Arusha akihakiki uraia wa mmoja wa wananchi katika Kata ya Themi aliyefika kujiandikisha.

Wateja wa Tigo mkoani Njombe wafurahia huduma zitolewazo na Tigo msimu huu wa Fiesta

$
0
0

Mtoa huduma wa duka la Tigo mkoani Njombe, Vaileth Burton akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani leo hapo kupata huduma mbalimbali msimu huu wa Tigo fiesta 2017 ambapo bidhaa za Tigo zinapatikana kwa bei nafuu.
Mtoa huduma wa duka la Tigo mkoani Njombe, Israel Joseph akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani leo hapo kupata huduma mbalimbali msimu huu wa Tigo fiesta 2017 ambapo bidhaa za Tigo zinapatikana kwa bei nafuu.
Baadhi ya wateja wakipata huduma mbalimbali ikiwemo kujipatia tiketi za Tigo Fiesta mkoani Njombe.

PSPF YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE KWENYE KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

$
0
0
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akimkabidhi kijarida cha Mfuko huo chenye maelezo ya shunguli mbalimbali zinazotekelezwa na PSPF, kwa Mwanachama wa Mfuko amabye ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mstaafu, Mzee Thomas Martin Kiama, (73), nyumabni kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja leo Oktoba 6, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto, ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, na Afisa wa Unedeshaji Bw. Ernest Massay.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambao ni wastaafu, wameupongeza Mfuko huo kwa kupata pensheni za kila mwezi kwa wakati.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa PSPF kutembelea Wanachama wake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, walisema kimsingi malipo ya pensheni ya kila mwezi yamekuwa yakiingia kwenye akaunti zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.

“Mimi nashukuru penshni yangu napata bila shida, na inaingia kwenye akaunti yangu kwa wakati, hili napenda kuwapongeza sana.” Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu). Bw. Thomas Martin Kiama wakati alipotembelewa na ujumbe wa PSPF nyumbani kwake Oysterbay jana (Oktoba 6, 2017).

Najua zipo changamoto za hapa na pale, mimi ningependa muwe huru kabisa, ili muweze kutuhudumia vema sisi wanachama, vinginevyo huduma zenu nazifurahia, aliongeza Bw.Kiama, ambaye alistaafu mwaka 2005.

Kwa upende wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, nchini, Bibi. Mary Hariet Longway, naye aliipongeza PSPF kwa utoaji wa huduma na kwamba yeye anaridhishwa na utedaji kazi wake na kuwapongeza kwa kufika nyumbani kwake ili kupata maoni yake.

“Ninashukuru sana kwa kunitembelea kwani hii ni ishara ya jinsi mnavyotujali sisi wastaafu, lakini mimi kama Jaji mstaafu kwa utaratibu ulivyokuwa, sisi hatukuwa na bima za afya sasa kama mngetoa elimu ya jinsi ya kupata bima ya afya kupitia kwenu lingekuwa jambo jema.” Alishauri Bibi Longway amabye naye alistaafu mwaka 2005.

Alsiema, malipo ya kila mwezi ya Pensheni yake yamekuwa yakiingia kwenye akaunti yake bila shida yoyote.Naye askari wa Jeshi la Magereza (mstaafu), Bw.Kasim Salehe Mafanya, yeye naye aliipongeza PSPF, kwa huduma bora lakini akaomba utaratibu ufanyike ili pensheni hiyo iweze kuboreshwa na hivyo kuelndelea kuwa na manufaa zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya PSPF, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Bi. Mwanjaa Sembe, alisema, katika kuadhimisha Wiki ya Wateja Duniani, ofisi za PSPF kote nchini, zimefanya utaratibu wa kuwatembelea wanachama wake kwa lengo la kuwahakiki na kupokea maoni yao ili kuboresha utoaji wa huduma .Aidha katika Ofisi za Makao Makuu, Wakurugenzi an Mameneja waliungana na maafusa na wafanyakazi wa Mfuko huo, katka kuwahudumia wateja waliofika makao makuu.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Bibi Mary Logway, ambaye ni mwanachama wa PSPF, akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017, wakati alipotembelewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, kushoto.


Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wakwanza kushoto), akimsikilzia mteja (mwanachama) wa Mfuko, huku afisa aliye kwenye mafunzo kutoka Chuo Cha Usimamzi wa Fedha, (IFM), Bw. Paschal W. Divaz, (katikati), akifuatilia.
Bw. Silayo akisalimiana na wateja (wanachama) waliofika makao makuu ya Mfuko kuhudumiwa.



Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro, (kulia), akimuhudumia mteja (mwanachama) aliyekifa makao Makuu kuhudumiwa.
Meneja wa Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na mteja wake, (mwanachama) wakifurahia jambo wakati mwanachama huyo akipatiwa huduma. 
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, wapili kulia), akizungumza na afisa aliye mafunzoni, kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha, 9IFM), Bw.Paschal W. Diaz
Afisa Uchangiaji wa Hiari PSS, Bi.Mwajuma A.Mohammed, (kushoto), akimuhudumia mteja.
Afsia Mtekelezo, (CO), wa PSPF, Bi. Mwanaisha S. Waziri akiwa kazini.
Afisa wa PSPF aliye mafunzoni, Bw. Alpha Mkopi, (katikati), akiwahudumia wateja, waliofika ofisi za Makao Makuu kupata huduma.
Maafisa wa PSPF wakitoa huduma Oktoba 6, 2017. 
Mzee Kiama, (kushoto), akipitia maelezo ya uhakiki kabla ya kuweka saini yake. aliye nae ni Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe. 
Mzee Kiama akiweka saini kwenye fomu ya uhakiki.



Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimpa maelezo, Jaji Mstaafu, Bi. Mary Longway, kuhusu uhakiki wa uanachama wake PSPF. 
Bi. Longway akiweka saini wkenye fomu hiyo ya uhakiki. 
Mkuu wa kitengo cha Mikopo kwa Wanachama wa PSPF, Bi. Linda Bahati, akizungumza na simu ya kikazi ili kupata maeelzo ya ziada wakati akimuhudumia mteja Oktoba 6, 2017.

Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akizungumza na Mzee Kiama.
Jaji (mstaafu) Longway na mukuu wake, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyaakzi wa PSPF waliomtembelea ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017.

MASAUNI ATEMBELEA MRADI WA UMWAGILIAJI GEREZA LA KILIMO IDETE, ATAKA MKANDARASI ACHUKULIWE HATUA KALI KWA KUUTELEKEZA UJENZI WA MRADI HUO WA MABILIONI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia),


Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mzee Nyamka (kushoto), pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi hilo, wakitoka katika Gereza la Kilimo Idete lililopo Ifakara, mara bada ya Naibu Waziri huyo kupokeataarifa ya Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji uliosimama baada ya Mkandarasi kuutelekeza mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.5. Hata hivyo, Masauni alilitaka Jeshi hilo kufanya uchunguzi dhidi ya Mkandarasi huyo na ikithibitika anamakosa akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria.


Karani wa Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete, Ifakara, Mkaguzi wa Jeshi la Magereza, Juma Mtega, akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),chanzo cha ujenzi wa mradi huo. Masauni alifanya ukaguzi wa mradi huo wa mabilioni ya fedha ambao Mkandarasi aliutelekeza mwaka 2016. Hata hivyo, Masauni alilitaka Jeshi la Magereza kufanya uchunguzi dhidi ya Mkandarasi huyo na ikithibitika anamakosa akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria.
Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mzee Nyamka, akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), sehemu mbalimbali za Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete, Ifakara, wakati Masauni alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo wa zaidi ya shilingi Bilioni 2.5 uliosimama baada ya Mkandarasi wa mradi huo, kuutelekeza mwaka 2016. Hata hivyo, Masauni alilitaka Jeshi hilo kufanya uchunguzi dhidi ya Mkandarasi huyo na ikithibitika anamakosa akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akitoa maelekezo kwa viongozi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Morogoro ya kumchunguza na kumchukulia hatua za kisheria endapo itathibitika Mkandarasi aliyesimamisha Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete, Ifakara, alifanya makosa kwa kusimamisha ujenzi wa mradi huo wa mabilioni ya fedha, tangu mwaka jana 2016. Wapili kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mzee Nyamka.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitoa maelekezo kwa viongozi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Morogoro ya kumchunguza na kumchukulia hatua za kisheria endapo itathibitika Mkandarasi aliyesimamisha Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete, Ifakara, alifanya makosa kwa kusimamisha ujenzi wa mradi huo wa mabilioni ya fedha, tangu mwaka jana 2016. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mzee Nyamka.

Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mzee Nyamka, akimfafanuliaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), kuhusu Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete, Ifakara, wakati Masauni alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo wa zaidi ya shilingi Bilioni 2.5 uliosimama baada ya Mkandarasi wa mradi huo, kuutelekeza mwaka 2016. Hata hivyo, Masauni alilitaka Jeshi hilo kufanya uchunguzi dhidi ya Mkandarasi huyo na ikithibitika anamakosa akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiwasalimia Maafisa wa Gereza la Kilimo Idete lililopo Ifakara, mkoani Morogoro, wakati kiongozi huyo alipokuwa anawasili katika Gereza hilo kwa ajili ya kuutembelea Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji uliosimama baada ya Mkandarasi wa Mradi huo kuutelekeza mwaka jana 2016, mradi ambao unathamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 2.5. Gereza hilo linafanya kilimo cha zao la Mpunga na Mahindi.


Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NHIF YATOA HUDUMA ZA UPIMAJI KWENYE BONANZA LA MICHEZO JIJINI TANGA LEO

$
0
0


 Afisa Mdhibiti wa Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Dkt Lwi Kupaza akiangalia taarifa za moja ya wakazi wa Jiji la Tanga ambao walijitokeza kupima uzito,sukari na presha wakati wa bonanza la michezo ambalo limefanyika leo kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
 Daktari wa NHIF kushoto akimpima presha Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati wa bonanza la michezo
Afisa Mdhibiti Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dkt Lawi Kupaza akichukua maelezo ya Ofisa wa Polisi kutoka Ofisi ya RCO,Saidi Mwagara wakati wa bonanza hilo
Afisa Madai wa NHIF mkoani Tanga,Marry Daniel katikati aliyevaa tisheti ya njano akifuatilia taarifa wakati wa wananchi walipojitokeza kwenye banda lao kwenye bonanza la michezo ambalo lilifanyika viwanja wa shule ya Sekondari Popatlaly kupima afya 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akiwa kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kuangalia zoezi la upimaji wa afya kwa wanamichezo 150 waliweza kupima afya ambapo kati yao
waliokuwa na uzito mkubwa 65,waliokutwa na sukari juu wanne,waliokuwa na Presse sita na wasiokuwa na matatizo 75
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akiwaongoza askari wa Jeshi hilo kuwavuta kamba Bandari Tanga wakati wa Bonanza hilo leo
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akiwaongoza askari wa Jeshi hilo kuwavuta kamba Bandari Tanga wakati wa Bonanza hilo leo
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba kulia akifurahia jambo wakati wa bonanza hilo
 Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga,Crispinngonyani akiwaongoza idara hiyo kuvuta kamba kwenye bonanza hilo.
 wa Pili kutoka kushoto ni Afisa wa NHIF Mkoa wa Tanga akiteta jambo na wanamichezo walioshiriki bonanza hilo leo.
 Afisa Madai wa NHIF mkoani Tanga,Marry Daniel kulia kushoto ni Afisa Madai wa Mfuko huo pia Petro Aloyce wakigawa vipeperushi vinavyohamasisha huduma wanazozitoa kwa wanamichezo.
 Afisa Madai wa NHIF mkoani Tanga,Marry Daniel kulia akiendelea kuwahamaisha wanamichezo namna ya kuweza kujiunga na mfuko huo
 Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoani Tanga,Sadick Nombo kushoto akibalishana mawazo na Afisa Utumishi Mkoa wa Tanga,Jakobo Kingazi wakati wa bonanza hilo

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akisalimiana na moja kati ya timu zilizokuwa zinashiriki bonanza hilo ambapo alisema michezo ina imarisha mahusiano mazuri kazini na ni muhimu kuimarisha miili yao na kuongeza ufanisi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja .Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

PSPF YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE KWENYE KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

$
0
0
 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwatumikia wateja, (wanachama) wa Mfuko.
Bw. Mayingu ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku tuzo na zawadi wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyoanza Oktoba 2 na kumalizika Oktoba 6, 2017.
Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwanzo wa wiki ya mwezi Oktoba kila mwaka, hulenga kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao wa kuwahudumia wateja kwa kuzingatia weledi wa utoaji huduma bora kwa mteja.
"Wakati nikiwa Iringa nimepokea pongezi nyingi za Wanachama wetu, wakiwapongeza nyinyi wafanyakazi kwa kuwahudumia vizuri, hongereni sana na niwaombe muendele kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwani huo ndio wajibu wetu." Alisema Bw. Mayingu katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 6, 2017 kwenye ukumbi wa makao makuu ya PSPF, Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. 
Bw. Mayingu aliwapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo kote nchini, kwa kazi nzuri na kuwaeleza kuwa kitendo cha wafanyakazi na maafisa wa Mfuko huo kutoka maofisini na kuwafata wateja, (wanachama) majumbani kwao ili kuzungumza nao na kuwahudumia kimesifiwa sana.
"Kaimu Mkurugenzi Mkuu, alifuatana na baadhi yenu kwenda kule Kipunguni B. na kukutana na mwanachama wetu, Bw. Kassim Mafanya, ambaye alikipongeza kitedo kile na kusema hakutegemea maishani mwake yeye kama mstaafu angetembelewa nyumbani kwake na PSPF, hili ni jambo jema." Alibainisha Bw. Mayingu.
Wafanyakazi waliopata tuzo ni Elizabeth Shayo, kutoka kitengo cha Huduma Kwa Wateja, Makao Makuu, ambaye kupitia teknolojia, (mifumo), ni wateja wenyewe ndio waliompendekeza kutokana na maoni yaliyopokelewa lakini idadi ya watu aliowahudumia.
Mwingine ni Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), ambaye naye alitunukiwa tuzo na kupewa zawadi kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wateja bila kuchoka.
Tuzo hizo pia zimekwenda kwa walezi wa mikoa wa PSPF, kampuni mshirika ya Ardhi Plan Limited na pia makampuni washirika yaliyoshirikiana na PSPF kwenye wiki ya huduma kwa wateja, ambayo ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mabenki ya CRDB, NMB, TPB na Mwalimu Commercial Bank (MCB).
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.
 Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Elizabeth Shayo.
  Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Bi.Valley Malinga
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akiwa na maafisa waandamizi wa Mfuko huo.
 Baadhi ya wafanyakzi wa PSPF
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017


Meneja wa Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na AfIsa Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. January Buretta, wakihakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwenye hafla hiyo

Baadhi ya wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo

Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.


Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.


Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo
 Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, (kushoto)
 Bw. Mayingu akimpatia zawadi Afisa Mipango Miji wa kampuni mshirika na PSPF, Ardhi Plan Limited, Bi. Anna Lukindo.
 Mkurugenzi Mkuu na viongozi wengine wa Mfuko wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa tuzo
Picha ya pamoja na wadau

RC NCHIMBI AAGIZA KUVUNJWA KWA BODI YA USHIRIKA MSAI WILAYANI IRAMBA, NDANI YA WIKI MBILI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwaelekeza wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, wakishiriki kwa vitendo mafunzo yya kupima urefu kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Katibu Tawala Wilaya ya Iramba Pius Songoma akishiriki kuwaelekea wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.


Konyo Mjika ambaye ni mkulima hodari wa pamba wilaya ya Iramba kutoka kijiji cha Msai akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa zawadi ya kilo tano za mbegu ya pamba aliyopewa.
Zakaria Marko Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain itakayosambaza mbegu za pamba tani 300 mkoani Singida akizungumza na wakulima wa zao hilo Katika kijiji cha Msai Wilayani Iramba.


……………


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula, asimamie kuvunjwa kwa bodi ya Ushirika wa Kijiji cha Msai Wilayani Iramba ndani ya wiki mbili, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 50.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika mkutano na wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Msai, ambao wamemueleza kutokuwa na imani na viongozi wa bodi hiyo kutokana na upotevu wa fedha hizo na wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote.

Wakulima hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zaidi ya milioni 50 zilitolewa na seikali kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghala la ushirika wa kijijini hapo lakini hakukuwa na ujenzi wowote uliofanyika huku wakifuatilia hawapewi majibu sahihi.

Wamesema wana ushirika walijitahidi kutuma mwenyekiti wa Kijiji hicho kufuatilia upotevu huo bila mafanikio jambo lililowakatisha tamaa ya kuendelea na ushirika.

Dkt Nchimbi amesema “moja ya Muhimili wa mafanikio ya kilimo cha pamba ni ushirika ulio imara, tunakoelekea kwenye kilimo cha pamba chenye tija hawa wasiowaaminifu kwenye bodi watatukwaza na kutukwamishwa, kama bodi haifanyi kazi vizuri kwanini iendelee?, Mkuu wa Wilaya naimani kwa utendaji wako mzuri hili halitachukua zaidi ya wiki mbili”.

Aidha amemtaka Afisa Ushirika Mkoa wa Singida kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu wakati wa kuvunjwa kwa bodi hiyo kwakuwa kazi ya mkoa ni kusuluhisha sio kutafuta maelezo marefu huku wananchi wanapotezewa muda.

“Afisa Ushirika hakikisha tarehe ishirini mwezi huu bodi hiyo iwe imeivunjwe na kuundwa bodi mpya ambayo itasimamia ushirika kwa umakini ili kuinua kilimo cha pamba Iramba”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Aidha Dkt Nchimbi amewatoa hofu wakulima kwakuwa mbegu aina ya UKM 08 za manyoya pamoja na viuatilifu zitafika na kusambazwa kwa wakati huku akiwataka kupanda kitaalamu ili kwa ekari moja iwe na miche elfu 22 na mkulima avune zaidi ya kilo elfu moja za pamba.

Pia amewaagiza maafisa ugani wote kulima pamba ili mashamba yao yawe mashamba darasa, huku wakitakiwa kuhakikisha hakuna makosa katika hatua yoyote kuanzia kwenye kuandaa mashamba, kupanda na kwenye upuliziaji dawa, bila kusahau kutoa taarifa kwa wananchi katika kila hatua.

Dkt Nchimbi amewapa wakulima wawili hodari wa zao la pamba zawadi ya kilo tano kwa kila mmoja kama kianzio huku akiwaahidi kuwa mbegu za kutosha na viuatilifu kwa ajili ya maeneo yao watapatiwa.

Akisistiza kaulimbiu ya Singida mpya kwa pamba yenye tija amewataka Wanasiasa, watendaji wa serikali na viongozi wa dini washirikiane na serikali kwa pamoja katika kutoa hamasa na elimu ya kilimo cha pamba.

Dkt Nchimbi ametoa onyo kwa wauza pembejeo na wasambaaji wasio waaminifu ambao husambaza dawa zisizo halisi kuwa serikali itawabaini na kuwapa adhabu kali huku akiwataka wakulima wasinunue dawa bila ushauri wa maafisa ugani.

“Kuna dawa nyingine ukipuliza kwenye wadudu waharibifu wa pamba badala ya kufa wananenepeana, sasa ole wako serikali ikukamate wewe unayemuuzia mwananchi dawa feki hakika tuakushughulikia ipasavyo”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Kwa upande wake Konyo Mjika ambaye ni mkulima hodari wa pamba wilaya ya Iramba kutoka kijiji cha Msai amesema msimu wa mwaka jana amelima ekari nane na kupata kilo elfu sita ambapo ameweza kujenga nyumba nne za bati, kununua ng’ombe kadhaa na kuhudumia familia yake.

Mjika ameongeza kuwa ameweza kuvuna pamba nyingi kutokana na kusikiliza ushauri wa wataalamu wa kupanda kwa kufuata mistari, kuweka mbolea na viuatilifu mapema.Kutokana na mafanikio hayo Mkulima Mjika amesema kwa msimu huu anatarajia kulima ekarini shirini pamoja na kuwashauri wanakijiji wenzake walime pamba kwa wingi huku wakifuata ushauri wa wataalamu ili waweze kuvuna kwa wingi.

Naye Zakaria Marko Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain inayojihusiha na kilimo cha zao la pamba kwa mkataba amesema kwa msimu huu kampuni hiyo itasambaza mbegu za pamba tani 300 mkoani Singida.

Marko ameongeza kuwa uzalishaji wa pamba mkoani Singida umekuwa mdogo ukilinganisha na mahitaji ya kiwanda chao ambapo mwaka jana zilipatitana kilo milioni 1 na mwaka huu zikaongezeka hadi kilo milioni 1.5 kutokana na jitihada za wakuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa na viongozi mbalimbai.

Ameongeza kuwa Kijiji cha msai chenye wakulima wa pamba zaidi ya mia tano wameweza kuzalisha kilo laki tano huku wilaya ya Iramba yote ikizalisha kilo laki nane na nusu kwa msimu wa mwaka jana na mategemeo yakiwa makubwa zaidi kwa mwaka huu.

Marko amesema kutokana na msukumo wa serikali na Viongozi wa Mkoa wa Singia ni matarajio yake kiwanda cha Bio Sustain sasa kitazalisha kwa faida kutokana na kupata pamba ya kutosha hapa Singida na sio kuifuata mikoa ya jirani kama ilivyokuwa hapo awali.

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO OCTOBER 8,2017


Msimamo wa Askofu Niwemugizi Katiba Mpya Siyo wa Kanisa - Kadinali Pengo

BENKI YA CRDB YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA WILAYANI CHATO

$
0
0

Na Binagi Media Group.

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu 2017, benki ya CRDB jana simetoa semina kwa wateja wake katika wilaya ya Chato mkoani Geita na pia kupokea maoni yao ili kuboresha zaidi huduma zake.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini aliwahakikishia wateja wa benki hiyo huduma ya mikopo kwa muda wa siku saba na hivyo kuwahimiza wafanyabiashara kuitumia benki fursa hiyo kukuza mitaji yao ya biashara.


Aidha alisisitiza kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake ikiwa ni benki inayoongoza kwa kutoa mikopo hapa nchini huku pia jamii ikiendelea kunufaika na benki hiyo kupitia gawio la faida ambalo hutolewa kila mwaka ili kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.


“Tunaomba tuendelee kushirikiana pamoja ambapo CRDB ni benki ya muda mrefu iliyo salama na imara kufanya nayo kazi ikiongoza kwa zaidi ya miaka 10 sasa kwa kutoa huduma bora na zenye riba nafuu nchini”. Alisisitiza Nkini kwenye semina hiyo iliyojumuisha pia wateja wa CRDB kutoka Geita, Muleba, Ngara na Bihalamulo.
Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga alisema benki hiyo imeendelea kuwafikia wateja wake kote nchini kupitia huduma mbalimbali ikiwemo Fahari Huduma, Simu Banking pamoja na Internet Banking na hivyo kuwa benki yenye mtandao mkubwa unaowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki popote walipo.


“Huduma zetu ni bora kuliko benki nyingine yoyote nchini hivyo natoa rai wateja wetu kutumia huduma zetu ikiwemo mikopo kwa ajili ya mitaji ya biashara zao kwani tunao uwezo mkubwa wa kuwahudumia”. Alidokeza Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus.


Baadhi ya wateja wa CRDB, Mellia Alloyce pamoja na Ristides Ramadhan walikiri kunufaika na benki hiyo kupitia huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya mikopo na hivyo kukuza biashara zao huku hivi sasa wakifurahia uharaka wa huduma hiyo tofauti na hapo awali.


Katika hatua nyingine benki ya CRDB ilisaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A katika halmashauri ya wilaya ya Chato ambapo msaada huo ulijumuisha mifuko 150 ya saruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo.  Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji CRDB. Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye semina hiyo. Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga akizungumza kwenye semina hiyo. 
        Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas , akichangia mada kwenye semina hiyo.        

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KIGOMA YAKUTANA NA WADAU WAKE WA HAKI JINAI KUJADILI NAMNA YA KUSUKUMA MASHAURI

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama-Kigoma 

KAIMU Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi/Mkoa-Kigoma, Mhe. Flora A. Mtarania amewasihi Wadau wa Haki Jinai wa mkoa huo kushirikiana na Mahakama ili kumaliza mashauri yote yaliyofunguliwa mwaka huu ifikapo Desemba mwaka huu. 

Mhe. Mtarania aliyasema hayo mapema mwishoni mwa wiki iliyopita Oktoba 06 katika kikao maalum cha Kusukuma Mashauri ‘Case Flow Management Meeting’ kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mahakama hiyo ya Mkoa. 

“Mpaka sasa Mahakama ya Mkoa-Kigoma kuna jumla ya mashauri 24 ambayo bado hayajatolewa maamuzi ‘pending cases’ huku 16 yakiwa mashauri ya Madai na nane (8) ya Jinai, na kwa upande wa Mahakama za Wilaya kuna jumla ya mashauri 103 ambayo bado hayajakamilika huku mashauri 79 yakiwa ya Jinai na 24 mashauri ya Madai,” alisema Mhe. Mtarania. 

Alisema kuwa kesi hizo ambazo zina wastani wa kati ya miezi mitatu (3) hadi miezi sita (6) tangu kufunguliwa kwake Mahakamani zimekuwa zikikwama kwa sababu mbalimbali ambazo ni pamoja na kutopatikana kwa Mashahidi hali inayopelekea haki kutopatikana kwa wakati, upelelezi kutokamilika kwa wakati, fedha za Mashahidi kutotosheleza uhitaji na kadhalika. 

Aliongeza kuwa ni vyema Suala ya mchakato wa usikilizwaji wa kesi hadi ukamilikaji wake lifanyike kwa ushirikiano kati ya Mahakama na Wadau wa Haki Jinai ili haki ipatikane kwa wakati stahiki. 

Aidha; Mhe.Mtarani alisema kuwa lengo la vikao vya pamoja na Wadau wa Mahakama ni kujadili namna ya kusukuma mashauri ili yaweze kumalizika kwa wakati, kupeana mikakati ya kushughulikia mashauri na kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu wake katika mchakato mzima wa usikilizaji wa mashauri. 

Mhe. Mtarania aliendelea kusema kuwa vikao hivi hufanyika kila baada ya miezi mitatu na hiki ni kikao cha tatu (3) kufanyika kwa mwaka huu, huku akieleza kuwa kabla ya kikao hiki cha ngazi ya Mkoa kufanyika huwa kuna vikao vya kusukuma Mashauri ambavyo hufanyika kwa ngazi za Mahakama za Wilaya ili kuwasilisha mipango yao katika kikao cha Wadau cha Mkoa. 

“Kimsingi kwa hatua tuliyofikia sasa vikao hivi vimesaidia kumaliza mashauri yaliyokuwa yalikaa muda mrefu Mahakamani kutokana na sababu mbalimbali zilizosababishwa na Wadau,” alieleza Mhe. Mtarania. 

Kikao kilihudhuriwa na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi ambaye ndiye Mwenyekiti, Mwanasheria wa Serikali Mfawidhi, Mahakimu Wafawidhi wa Wilaya za Kasulu na Kibondo, Mkuu wa Takukuru-Mkoa, Afisa Uhamiaji wa Mkoa, Mkuu wa Upelelezi (RCO), Afisa Ustawi wa Jamii, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea na Mtendaji wa Mahakama-Kigoma. 

Hata hivyo, Wajumbe wa Kikao hicho waliazimia kufanya kazi kwa kushirikiana ili ifikapo Desemba 30, kesi ambazo hazijakamilika ziwe zimekamilika. 
Mtendaji-Mahakama ya Mkoa Kigoma, Bw. Humphrey Paya (kulia) akichangia jambo katika kikao hicho.
Wajumbe wakiwa katika kikao hicho (katikati) ni Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Wilaya-Kasulu, wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Mahakama-Kigoma, Bw. Humphrey Paya na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Ustawi wa Jamii, Manispaa ya Kigoma.
Wajumbe wakiwa katika kikao.
Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mhe. Flora Mtarania akiongoza kikao cha Kusukuma Mashauri ‘Case Flow Management Meeting’kilichofanyika katika Ukumbi wa Mahakama ya Mkoa Kigoma.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao cha Kusukuma mashauri ya Mahakama-Mkoani Kigoma.
Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kigoma,hata hivyo jengo hilo ni chakavu hivyo linahitaji ukarabati ili liendelee kukidhi mazingira ya bora ya kutolea haki kwa wananchi.

RAIS MAGUFULI AMEKATA KIU

$
0
0

Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kufanya mabadiliko madogo mapya kwenye Baraza jipya la Mawaziri alilolitanga Jumamosi Oktoba 7, 2017 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika Baraza hilo jipya limeongezeka Wizara mbili mpya ambazo ni Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetenganishwa na kuwa Wizara ya Kilimo na  Wizara ya Mifugo na Uvuvi; na Wizara ya Nishati na Madini imetenganishwa na kuwa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini kufanya Wizara kuwa 21 toka 19 za awali.

Pia kuna ongezeko la Mawaziri 2 na Manaibu Waziri 5. Baadhi ya wapya walioongezeka ni Mhe. Abdallah Ulega, Mhe. Kangi Lugola, Mhe. Faustine Ndugulile, Mhe. Mary Mwanjelwa, Mhe. Juliana Shonza, Mhe. Kakunda n.k

Mabadiliko haya mapya madogo yamekuja wakati ambao Wizara mbalimbali zikiwa hazina Mawaziri na Manaibu Waziri na hivyo kuja kuzipa mapengo yaliyokuwa yakisababisha kusua sua kiutendaji. Baadhi ya Wizara hizo ni Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Nishati na Madini.

Ukamilifu huu uliotokana na mabadiliko haya madogo umepeleka injini ya kuongoza nchi kukamilika na kuwa mpya na Watanzania tunatarajia maboresho makubwa ya utendaji kazi ya utekelezaji ilani ya uchaguzi kwa kasi ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo nchini.

Naendelea kumpongeza Rais Magufuli kwa kuteua Baraza lililokata kiu ya uteuzi kwa kuhakikisha kila kanda inapata uwakilishi, kuchanganya wakongwe na wapya, kuchanganya dini zote lakini Kubwa nina imani Baraza limejaa Watu weledi, wasomi wanaoendana na  nafasi walizopewa.

Katika mabadiliko haya Rais Magufuli ameendelea kuonyesha yeye ni kipenzi na Vijana kwa kuteua vijana wengi kwenye Baraza hili jipya la Mawaziri. Baadhi ya vijana waliopata fursa ya kuaminiwa ni Juliana Shonza, Abdallah Ulega, Dk. Faustine Ndugulile, Anthony Mavunde, Dk. Hamis Kigwangallah, Hamad Masauni, Mwigulu Nchemba, Mhe. Jafo, January Makamba na wengineo.

Vijana hawa wote walioteuliwa ni Watu weredi, makini na sahihi kabisa waliokuja kwa wakati sahihi. Kiukweli wametosha kabisa katika nafasi zao na watunze heshima ya asilimia 60 ya Vijana Watanzania na heshima ya Rais Magufuli aliyewaamini na kuwateua.

Rai yangu kwa Wateuliwa wote kwenda kufanya kazi kweli kweli ya kumsaidia Rais Magufuli kutekeleza ilani ya uchaguzi, kumsaidia kutimiza lengo la kuifanya nchi yetu kuwa Tanzania ya Viwanda yenye kufikia malengo ya uchumi wa kati na kwenda kutatua kero na shida za Watanzania.

Kama ambavyo Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli alivyowaamini, hata nami nikiwa sehemu ya Watanzania nina imani Kubwa na Baraza hili jipya la Mawaziri. Wakafanye Kazi kweli kweli.

Hakika kimya kingi kina mshindo mkuu. Hongera sana Rais Dk. Magufuli kwa kusuka Baraza la Mawaziri linaloendelea kuleta imani na amani kwa Watanzania la Hapa kazi Tu!

Mungu Mbariki Rais Dk. Magufuli
Mungu Ibariki Tanzania.

IMETOLEWA NA:

Emmanuel J. Shilatu
0767488622

UJENZI MAEGESHO YA KIVUKO LINDI KITUNDA WAKARIBIA KUKAMILIKA

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwanza kushoto) akitazama moja ya malighafi inayotumika katika ujenzi wa maegesho mapya ya Lindi Kitunda unaondelea Mkoani Lindi. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga maegesho ya Lindi Kitunda wakati alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi huo Mkoani Lindi. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwanza kushoto) akitoa maagizo kwa mkandarasi anayejenga maegesho ya Lindi Kitunda wakati alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo Mkoani Lindi. Kulia ni Mtaalamu wa Uchumi kutoka wakala huo Edgar Ruta, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Mhandisi Japhet Y. Maselle na mkandarasi anayesimamia ujenzi huo Ndugu Evans Martin. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.




Mafundi wa kampuni inayosimamia ujenzi wa maegesho ya kivuko Lindi Kitunda wakiendelea na ujenzi wa maegesho hayo upande wa Kitunda mkoani Lindi. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.




Mafundi wa kampuni inayosimamia ujenzi wa maegesho ya kivuko Lindi Kitunda wakiendelea na ujenzi wa maegesho hayo upande wa Kitunda mkoani Lindi. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.




Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Issack Mwanawima (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko Lindi Kitunda mkoani Lindi, wanaomsikiliza (wa pili kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt Mussa Mgwatu, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko wa wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle, pamoja na wawakilishi mbali mbali wa wakala huo. Ujenzi wa Maegesho hayo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na utasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo


Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa maegesho ya Lindi Kitunda Ndugu Evans Martin (wa kwanza kulia) akimuonyesha kitu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt Mussa Mgwatu (wa kwanza kushoto) wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho hayo mkoani Lindi ambao unaendelea. Ujenzi wa Maegesho hayo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na utasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko wa wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kulia) akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayesimamia ujenzi wa maegesho ya Lindi Kitunda wakati alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi huo mkoani Lindi, wa pili kulia anayetazama ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt Mussa Mgwatu. Ujenzi wa Maegesho hayo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na utasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.

MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA KUUTANGAZA UTALII WA TZ ZIARA YA THAILAND

$
0
0
 Mtaribu wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Resorce Afrika Limited, Idrissa Songoro akizungumza kuhusu maandalizi ya ziara ya mafunzo ya Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA),nchi Thailand inayotarajia kuanza katilati ya mwezi ujao Novemba mwaka huu. 

Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Adam Ngamange na Mwenyeikiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kisui . Kisui.UJUMBE wa Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) unaokwenda ziara ya mafunzo nchini Thailand, umejiandaa pia  kwenda kuutangaza utalii wa Tanzania.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Richard Mwaikenda

Akizungumza mjini Dar es Salaam wakati wa kikao cha maandalizi na baadhi ya Wana Mkikita watakaokwenda Thailand, Mtaribu wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Resorce Afrika Limited, Idrissa Songoro amesema kuwa maandalizi ya ziara hiyo kwa upande wa Thailand kwa asilimia kubwa yako tayari.

Amesema kuwa ziara hiyo ya wiki moja Wanamkikita watanufaika kwa mambo mengi, ambapo licha ya kutangaza vivutia mbalimbali vya utalii pia wataonesha utamaduni wa mapishi ya kila aina ya vyakula vya asili vya kitanzania.

Amesema Wanamkikita ambao miongoni mwao ni Wakulima, Wafanyabiashara na Wajasiriamali watapata wasaa wa kubadilishana mawazo na wenzao wa Thailand kwa lengo la kukuza ushirikiano katika masuala ya kibiashara,kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa.

Songoro amewaasa Wanamkikita kufanya maandalizi  ya uhakika ili wakienda Thailand wanufaike na ziara hiyo na kuwa na mrejesho mzuri watakaporejea nyumbani.

"Kitabia Wathailand wanafanana na Watanzania, kwani ni wakalimu, wapole, waungwana lakini pia ni wachapakazi na wako makini sana katika kila jambo wanalolifanya,"amesema Songoro.

Amesema kuwa Ujumbe huo utapata pia fursa ya kutembelea eneo la viwanda, mashamba ya wakulima pamoja na eneo la utafiti wa kilimo la Chiang Mai na Mji Mkuu wa Bangkok.

"Wathailand wana elimu mkubwa katika nyanja ya uhifadhi wa vyakula na kuviongezea thamani pamoja na kutangaza logo za kibiashara,. Pia wana mbegu za mazao mbalimbali zinazotoa mazao mengi kwa hekali, kwa mfano unaweza kuzalisha kabeji tani 25 kwa heka moja,"amesema Songoro.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kisui S. Kisui  aliwaasa Wanamkikita kuichangamkia ziara hiyo kwani watakaokwenda watanufaika kwa kupata fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo masuala ya kilimo cha kisasa na biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Adam Ngamange alielezea jinsi Mkikita ilivyopanga kuwaandaa wanajachama watakao kwenda huko kwa kuwapiga msasa kwa kutumia vikao na semina mbalimbali ili wawe na uelewa kwa kujua mambo mbalimbali watakayokwenda kufanya katika ziara hiyo muhimu.

Aliimpongeza Songoro kwa jitihada zake kwa kujitolea kwa moyo mkunjufu kuratibu ziara hiyo itakayokuwa na makubwa kwa Mkikita, Wanachama na Tanzania kwa ujumla.




 Songoro na viongozi wa Mkikita wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanamkikita wanaotarajia kwenda Thailand kwa ziara ya wiki moja.
 Dk. Kisui akielezea jinsi Mkikita ulivyojipanga kwa ziara hiyo, itakayowanufaisha wanachama kwa kukutana ana kwa anakwa mazungmzo  na wafanyabiashara na wakulima wa Thailand pamoja na kuingia nao mikataba mbalimbali. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Ngamange akifafanua jambo kwa wajumbe
 Ngamange akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mkikita wakati wa kikao hicho 
 Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao wakimsikiliza Songoro


 Songoro akifafanua jambo katika kikao hicho
 Ngamange akitoa shukrani kwa Songoro kwa uratibu wa ziara hiyo pamoja na kukubali kushiriki kwenye kikao hicho

 Elizabeth Ndangoba Mkurugenzi wa Fedha na Utawalawa Mkikita
 Catherine Edward Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mkikita
 Adam Ngamange
 Dk. Kisui akisisitiza jambo alipokuwa akifunga kikao hicho
 Songoro akijadiliana mambo na wajumbe wa Mkikita
 Mjasiriamali Mwambapa akiwa na Ngamange
 Songoro akihojiwa na African Swahili Televisheni
 Ngamange, Rose na Dk Kisui
Songoro akiwa na Mwambapa pamoja na Ngamange

Dk.Hamisi Kigwangalla: “Tuzidi kuombeana dua tu, sintowaangusha Watanzania”

$
0
0
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka watanzania kuendelea kumuombea dua pamoja na ushirikiano katika majukumu yake mpya.“Nimepokea salamu nyingi za pongezi na shukrani kwa Mungu aliye juu. Sintoweza kumjibu kila mtu, uungwana ni kutambua pongezi zenu na dua tele mlizotuombea, nawashukuru sana ndugu zangu. 

Tuzidi kuombeana dua tu.Tuna kazi ngumu ya kukimbia kukidhi matarajio ya kiongozi wetu Mkuu aliyetuamini na matarajio ya wananchi wenzetu. Binafsi nawaahidi nyote kuwa sintowaangusha! Ahsanteni sana ndugu zangu, natarajia ushirikiano wenu wa kila hali.” Alieleza Dk. Hamisi Kigwangalla. 

Awali taarifa za kuteuliwa kwake katika wizara nyingine, alizipata kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kwa njia ya simu wakati akiwa kwenye majukumu ya ziara ya kuboresha mfumo wa afya, akiwa Wilayani Nachingwea, Kata ya Kilimalondo umbali wa zaidi ya kilometa 100, kutoka Makao makuu ya Wilaya hiyo ya Nachingwea, aliweza kusitisha ziara yake hiyo ambayo alitakiwa kuendelea katika Vijiji na Wilaya nyingine ya Liwale.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.
Dk.Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa kituo cha Afya Kilimalondo wakati wa ziara hiyo
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vipya vya chumba cha upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi. Kituo hicho kilifungiwa kisifanye upasuaje mpaka kitakapokidhi vigezo, hata hivyo Dk.Kigwangalla alitoa miezi mitatu kiwe kimefanyiwa marekebisho na kianze kazi mara moja
Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi akimpatia taarifa Dk. Kigwangalla juu ya uteuzi wake mpya hivyo kusitisha shughuli zote zilizokuwa zimepangwa kuendelea katika wilaya hiyo.
Dk.Kigwangalla akiagana na viongozi wa Wilaya ya Nachingwea baada ya kusimamisha ziara yake kufuatia uteuzi mpya. Baada ya kupata taarifa hiyo kila kitu ilibidi kisimame hapo hapo. Namba za NW AMJW ilibidi ziondolewe na safari ya kutoka huko ianze.
Dk. Kigwangalla akiwa Mhe. Hassan Elias Masala (Mb.), Mbunge wa Jimbo la Nachingwea wakiagana mapema jana Oktoba 7,2017, majira ya saa nane za mchana baada ya kupata ujumbe wa kuteuliwa nafasi mpya. Hiyo ni baada ya kumaliza kazi kituoni hapo Kilimalondo na kuanza kuelekea Liwale, Kituo cha Afya Kibutuka, Ndipo alipopata taarifa kuna mabadiliko ya Baraza la mawaziri.
Awali kabla ya kupata taarifa za majukumu mapya, Dk. Kigwangalla alikuwa aendelee na ziara hiyo katikaWilaya ya Liwale, Kituo cha Afya Kibutuka.Dk. Kigwangalla alikuwa katika ziara yake hiyo ya kikazi ya siku tano ndani ya Mkoa wa Lindi ambapo alitoa maagizo mbalimbali ya kuhakikisha viongozi wa Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali wanatekeleza maagizo yote aliyotoa kwani ni maagizo halali ya kiserikali na watakaoshindwa watachukuliwa hatua. 

Miongoni mwa maagizo hayo ni pamoja na kila kituo cha Afya kuhakikisha kina chumba cha upasuaji kufuatia agizo/tamko la Mwandoya alilolitoa Novemba 2016, Mwandoya Meatu Mkoani Simiyu.

MWILI WA MWANAMUZIKI SHABANI YOHANA WANTED WAAGWA BOTSWANA

$
0
0
VIDEO YA WANAMUZIKI NA WAPENZI WA MPIGA GITAA SHABAN YOHANA WANTED WAKIAGA HUKO GABORONE BOTSWANA  KABLA YA SANDUKU LENYE MWILI WA SHABANI KUPELEKWA UWANJA WA NDEGE TAYARI KWA SAFARI YA KUJA TANZANIA. MWILI WA SHABANI UTAWASIRI DAR JUMATATU 9 OKTOBA ALFAJIRI.

MICHANGO INAHITAJIKA KWA AJILI YA KUWEZESHA KUSAFIRISHA MWILI KUTOKA DAR KWENDA  MICHUNGWANI MUHEZA KWA MAZISHI SIKU YA JUMANNE. KAMA UMEGUSWA UNAWEZA KUTUMA  CHOCHOTE NAMBA ZIFUATAZO
0713274747 NA 0763722557, ILI KUFANIKISHA MAZISHI YA MWANAMUZIKI HUYU.
SIKILIZA UMAHIRI ALIYOKUWA NAO KWENYE GITAA LA SOLO KATIKA WIMBO HUU

RC RUVUMA LAZIMA VIONGOZI WA WILAYA MTATUE MATATIZO YA MAENEO YENU.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dokta Bilinith Mahenge amefanaya ziara ya kukutana wananchi wa wilaya ya namtumbo kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili katika wilaya hiyo,na hapa mkuu wa mkoa Dokt Mahenge anakutana na maswali magumu kutoka kwa wananchi hao huku idara ya maji na kilimo yakipamba moto.

MSANII SHETTA KUNOGESHA USIKU WA KILIMANJARONIGHT ÖREBRO SWEDEN

$
0
0
Kwa wale wakazi wote wa nchi ya Sweden na nchi jirani za skandinavia mtakuwa na usiku wa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa kimataifa kutokea Sweden Tanzania  Uganda na nchi nyingine kadhaa  kwenye usiku wa kuitangaza nchi ya Tanzania kwa vivutio vyake vya utalii ikiwemo mlima mrefu barani Afrika Kilimanjaro.

Tunayofuraha kwamba msanii nyota wa mziki wa Bongoflaver Shetta atakuwepo kukuletea burudani kabambe ya mziki .
Usikose kuhudhuria ! 

Ni tarehe 14 Oktoba
Ukumbi ni kulturhuset Örebro
Järnvägsgatan 8 Örebro Sweden .
Ukipata ujumbe huu mtaarifu na mwezako.

SABA WANUSURIKA KIFO WAWILI WAJERUHIWA BAADA YA CARRY WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA

$
0
0
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba akikagua gari hiyo jioni hii
Watu saba wamenusurika kifo huku wawili  wakijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo baada ya gari ndogo waliokuwa wamepanda aina ya Carry kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ya Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda walieleza kuwa gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya reli wakati lijaribu kusimama ndipo lilipofeli breki na kuiparamia treni hiyo.

Ajali hiyo ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini  Tanga iliacha mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa ikitokea eneo la kwaminchi.

Akithibitisha kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati ikipita katika eneo hilo.

Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo kuwa ni T.343 DCQ  iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuingia  kwenye stesheni ya Tanga.

Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo walifikishwa  kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa gari hilo alitokomea kusikojulikana.

Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo,Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha reli wanakaa mita 50.

Awali akizungumza mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo,Said Kiruwasha alisema wakati wakiwa kwenye eneo hilo wakailiona gari hilo moshi likitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ndipo gari hilo lilipokuwa likipita ndipo ilipofeli breki baada ya kusikia honi ya treni hiyo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OCTOBER 9,2017

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>