Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1393 | 1394 | (Page 1395) | 1396 | 1397 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mshindi wa Tigo Fiesta Supanyota 2017 Njombe,  Diana Matimbwa  wa Njombe  akiimba kwa hisia wakati wa mashindano hayo mwishoni wa juma lililopita.
  Mashabiki wakimnyanyua Mshindi wa Tigo Fiesta Supanyota 2017 Njombe, Tigama Chanika kutoka Makambako  .
  Mshindi wa Tigo Fiesta Supanyota 2017 Njombe, Tigama Chanika kutoka Makambako  na Diana Matimbwa  wa Njombe  wamaeibuka washindi namba moja kati ya wasanii watano walio ingia kwenye mchuano wa kutafuta mshindi na wamefungana kwa viwango vilivyo pelekea wote waingie namba 1 bora Supanyota fiesta 2017 Njombe.


  0 0

  Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma, akiashiria uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania  (TBS), Prof. Egid Mubofu na kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa IFC-Banki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Uganda na Sudan Kusini, Dan Kasirye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga(K) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi.
  Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma (Kushoto), akipata maelezo kuhusu bidhaa za sola kutoka kwa Meneja Mkazi wa Kampuni ya Solar Sister, Fatma  Muzo,(katikati), pembeni yake ni ANSILA MAKUPA- BUSINESS DEVELOPMENT ASSOCIATE wakati wa uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam mapema iliyopita
  Waandishi wa habari wakichukua matukio katika hafla ya uzinduzi huo mapema wiki iliyopita jijini Dar es salaam.
  wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mapema wiki iliyopita

  Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 5 2017 – Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC, leo wametangaza uzinduzi wa kampeni ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa.
  Nishati inayotumia nguvu ya jua (Sola) na bidhaa za taa zimekuwa zikihitajika zaidi nchini Tanzania, Nchi ambayo familia nyingi za vijijini zinategemea taa za sola zilizo katika viwango duni na bidhaa zingine za umeme kwaajili ya mwanga. Taa ambazo zinaharibika kwa haraka sana na kuwasababishia wateja na watumiaji kupoteza gharama kubwa, jambo ambalo linapunguza uaminifu wao katika uhalali wa bidhaa za sola.
  Kampeni hiyo, iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” ina lengo la kuongeza ufahamu wa watumiaji kuhusu manufaa ya taa za kisasa za sola zenye ubora, ambazo zinasaidia wanajamii kufanya maamuzi yenye uhakika wakati wa manunuzi. Itakuwa inaonyesha aina mbalimbali za taa za sola ambazo zina waranti ambazo zinakidhi viwango vya mwanga ulimwenguni (Lighting Global Quality Standard) kampeni hii vile vile inatoa mbinu za kibunifu za biashara katika nishati ya sola kama vile huduma ya Pay-As-You-Go (PAYGO), huduma ya malipo kwa njia ya simu ambayo inamuwezesha mnunuzi kulipa kidogo kidogo, ambayo inafanya makundi mbalimbali yenye uwezo mdogo kifedha kumudu gharama za bidhaa hizo.
  Kampeni ya LightingAfrica inataka kuongeza kasi ya matumizi ya bidhaa zenye kiwango bora na zenye gharama nafuu, na inaweza kuboresha kiwango cha maisha ya wanajamii wa vijijini, ambao mara nyingi hutumia bidhaa za mafuta ya taa ambazo sio za uhakika na zina gharama kubwa kama vyanzo vyao vya mwanga.

  Kampeni ya IFC na Banki ya Dunia itatoa elimu katika soko la Tanzania kuhusu ubora wa bidhaa, na kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata thamani bora zaidi ya fedha zao,”  Alisema Mhandisi Edward Ishengoma Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala katika Wizara Wizara ya Nishati na Madini wakati wa ufunguzi rasmi wa kampeni hiyo.
  Kampeni ya Lighting Africa’s Tanzania itawafikia watumiaji na wanunuzi kupitia njia mbalimbali za matangazo na shughuli za kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari, maonyesho na kampeni ya nyumba kwa nyumba, kulingana na mahitaji ya kaya na kipato nchini kote.
  Kampeni ya Lighting Africa inafanyika katika nchi kumi zilizoko kando kando ya mwa jangwa la Sahara. Mpaka sasa programu hii imesha saidia takribani watu milioni 20.5 kufikia mahitaji yao ya msingi ya umeme. (Mwanga na kuchaji simu zao za mkononi) kwa kuuza zaidi ya bidhaa milioni 13 za sola. Lighting Africa/Tanzania ilianzishwa rasmi Septemba 2016 kwaajili ya kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha masoko ya kibiashara kwaajili ya bidhaa za sola zenye ubora nchini Tanzania, na kuwezesha upatikanaji wa taa nzuri zaidi na za kisasa zinazotumia nishati ya sola na upatikanaji wa suluhisho la nishati nchini.

  0 0


  Wasanii wa kizazi kipya wa kundi la Rostam wakiwa kwenye staili ya aina yake kwenye jukwaa la tamasha la  Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa sabasaba mjini Njombe usiku wa kuamkia jumamosi.

  Msanii Ommy Dimpoz akitoa burudani kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika  uwanja wa sabasaba mjini Njombe usiku wa kuamkia jumamosi.
  Aslay akiimba kwa hisia mapema wiki iliyopita katika jukwaa la Tigo Fiesta Mkoani Njombe
  Wasanii Jux, Nandy, Ben Pol na Maua Sama walipanda pamoja na kuimba  nyimbo zao mbalimbali kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa sabasaba mjini Njombe usiku wa kuamkia jumamosi.
  Mr blue akiwapagawisha wakaziwa mkoa wa Njombe mapema wiki iliyopita.
  Chege Chigunda akitumbuiza na madansa wake
  Darasa akiburudisha wakazi wa Mkoa wa Njombe mapema wiki iliyopita.
  Squeezer akiburudisha umati wa wakazi wa Njombe waliojitokeza katika Tamasha la Tigo Fiesta wiki iliyopita
  Vanesa Mdee akiwa katika jukwaaa la Tigo Fiesta Mkoani Njombe usiku wa kuamkia jumamosi.


  0 0

  Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo katika halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita.

  Walioketi ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodluck Nkini, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji CRDB.

  Na Binagi Media Group.
  Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, benki ya CRDB imechangia vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita ili kusaidia utatuzi upungufu wa vyoo katika shule za halmashauri hiyo.

  Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus alisema vifaa hivyo vitasaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A na kwamba vifaa hivyo vimejumuisha mifuko 150 ya theruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri ya Chato.

  Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo.

  Zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lilifanya ijumaa Oktoba 06,2017 katika halmashauri ya wilaya ya Chato ikiwa ni muda mfupi baada ya benki ya CRDB kutoa semina kwa wateja wake wilayani humo na pia kutoka maeneo jirani ikiwemo Muleba, Katoro na Biharamulo.
  Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.
  Zoezi la kukabidhi vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya Chato.
  Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea vifaa hivyo.

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Mamaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Agnes Lubuva (kushoto), akiwapatia maelezo wananchi pamoja na wajasiriamali kuhusu kazi na majukumu ya taasisi hiyo kwa jamii, walipotembelea banda hilo, wakati wa maonesho ya Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika, akitoa somo juu ya umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya baadaye ya familia, wakati alipokuwa akitoa elimu kwa wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali katika Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
  Wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Saaam, wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika, alipokuwa akitoa elimu kuhusu, Umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, wakati wa Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akitoa somo kwa wajasiriamali juu ya umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya sasa na baadaye ya familia, wakati wa Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
  Wajasiriamali wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (hayupo pichani) katika Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Wajasiriamali wakiwa makini wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, alipokuwa akitoa elimu kuhusu, Umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya baadaye na wakati matatizo,katika maadhimisho ya Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akitoa somo kwa wajasiriamali.
  Wajasiriamali wakiwa katika kongamano la Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, ambapo walielezwa kuhusu umuhimu wa kujiunga na kuweka akiba zao katika mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa manufaa ya sasa na baadaye na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (hayupo pichani), viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Wajasiriamali wakiwa na watoto wao, wakiwa kwenye kongamano hilo.
  Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akitoa elimu kwa wajasiriamali katika kongamano hilo.
  Wajasiriamali wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, alipokuwa akitoa elimu kuhusu, umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya sasa baadaye ya familia.
  Afisa Uhusiano wa Mamaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Agnes Lubuva (kulia), akigawa vipeperushi vya taasisi hiyo, kwa wajasiriamali waliohudhuria kongamano hilo la Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akijibu maswali ya wajasiriamali katika kongamano hilo.
  Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (kulia), akimsikiliza mmoja wa wajasiriamali, Benedicter Mng'etu kutoka Mburahati alipokuwa akiuliza swali kuhusu majukumu ya Taasisi ya SSRA katika kusimamia mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
  Maria Mwasimba, mjasiriamali, kutoka Mjimwema, akiuliza swali kwa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (hayupo pichani), katika kongamano hilo.
  Consolatha Komba, mjasiriamali, kutoka Keko Mwanga, akiuliza swali kwa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, katika kongamano hilo.
  Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akijibu maswali ya wajasiriamali katika kongamano hilo.
  Mjasiriamali Iddy Hassan, kutoka Tabata, akiuliza swali kwa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (hayupo pichani), wakati wa kongamano hilo.

  0 0


  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis, akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei kufungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. (Picha na Francis Dande).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa semina ya iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika mkoani Dodoma, mwishoni mwa wiki.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza katika semina hiyo.

  Dk. Charles Kimei akipongezwa baada ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali mkoani Dodoma.

  Dk. Charles Kimei, akipongezwa na mfanyabiashara wa mkoani Dodoma, Suzana Kweka, baada ya kutoa hotuba yake.
  Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali cha Benki ya CRDB, Elibariki Masuke akitoa mada katika semina hiyo.

  Baadhi ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

  Wafanyabiashara wakiwa katika semina hiyo.

  Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Benki ya CRDB, Elibariki Masuke (kushoto), akiwa katika semina hiyo.

  Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika semina hiyo.
  Meneja wa Amana wa Wateja Wadogo wa Benki ya CRDB, Abel Lasway, akitoa mada katika semina ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa mkoani Dodoma.
  Meneja wa Huduma Maalum Benki ya CRDB, Joyce Ishemoi akitoa mada kwenye semina ya Wafanyabiashara wa Dodoma.
  Meneja wa Benki ya CRDB Huduma za Kieletroniki, Mangire Kibanda, akitoa mada katika semina iliyowakutanisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Dodoma.
  Mfanyabiashara wa Dodoma akiuluza swali katika semina hiyo.
  Meneja Mahusiano Trade Finance wa Benki ya CRDB, Baraka Eusebio akitoa mada kwa Wajasiriamali.
  Mfanyabiashara wa Dodoma akiuliza swali.
  Mfanyabiashara wa mkoani Dodoma, Suzana Kweka, akitoa ushuhuda wake jinsi alivyopata msaada wa kukuza biashara yake kutoka Benki ya CRDB.
  Mmoja wa Wafanyabiashara akiuliza swali.
  Mkurugenzi wa Mikopo Benki ya CRDB, James Mabula,akijibu baadhi ya maswali ya Wafanyabiashara wa Dodoma wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo.
  Wafanyabiashara wa Dodoma wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis, akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei.

  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo Benki ya CRDB, James Mabula, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali, Elibariki Masuke, Elibariki Masuke na Mkurugenzi Benki ya CRDB Tawi la Dodoma, Rehema Hamis.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mabadiliko mbalimbali ya kampuni,katika utendaji kazi na kuwajibika kwa wafanyakazi na kuwasisitiza kuchapa kazi zaidi.
  Wafanyakazi wa Resolution Insurance wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Bw. Peter Nduati wakati akiongea nao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo akieleza kwa ufupi kuhusu IRAP na changamoto zake.
  Meneja wa Rasilimali Watu na Rasilimali Bi. Jennifer Mburu (kushoto) wa Kampuni ya Bima ya Resolution  akielezea Maana kamili ya IRAP na jinsi wafanyakazi wa Resolution watakavyotakiwa kuishi na Filosofia hiyo ili Kuboresha utendaji pamoja na Kumhudumia mteja kwa weredi. Kulia ni Bw. Melchizedek Muro Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja kutoka Resolution.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Dharura kwa Wateja kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution Bi. Batuli Karya akitoa mrejesho baada ya Chemsha Bongo kwa wafanyakazi kumalizika.
  Bi. Petronella Mwasanduba ambaye ni Mwenyekiti wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Bima ya Resolution-Tanzania akitoa majumuisho baada ya wakurugenzi kueleza jinsi ya utendaji mpya wa kazi wenye tija.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Resolution wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Dharura kwa Wateja Bi. Batuli Karya(hayupo Pichani) wakati wa mrejesho wa Chemsha Bongo
  Bw. Alphonse Michael (wa kwanza kulia) ambaye ni Mshauri Mkuu wa Biashara kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution Tanzania akitoa mwongozo wakati wa uzinduzi wa IRAP kwa ajili ya kuwajengea uwezo wafanyakazi.
   Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Resolution wakiwa katika  Chemsha Bongo 
  Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Bima la Resolution Bw. Melchizedek Nyau akisoma swali wakati wa zoezi la chemsha bongo ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Resolution wakirusha  Njiwa juu ishara ya uzinduzi rasmi wa IRAP
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akizindua Michezo kwa ajili ya kujengea uwezo wakafanyakazi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution Tanzania Bi. Maryjanne Mugo akizindua Michezo kwa ajili ya kujengea uwezo wakafanyakazi.
   Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Resolution wakiwa wanaendelea na michezo mbalimbali
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati (kushoto) akitoa zawadi kwa wafanyakazi.
  Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania


  0 0

   Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wanaendelea kupata burudani ya muziki kutoka wasanii nguli kutoka nchi za afrika kupitia onyesho la Coke Studio kupitia luninga ya clouds ambapo mwishoni mwa wiki Kolabo ya mwanamuziki nguli kutoka nchini Ali Kiba na mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Patoraking, imeacha gumzo kubwa. Kolabo hiyo ambayo imesukwa na msanii nguli wa kutengeneza muziki wa studio kutoka Nigeria,MasterCraft, ina mvuto mkubwa kwa watazamaji hususani vipao vya wanamuziki hawa vya ‘Chekecha Cheketua’ na ‘My Woman My everything’ ambavyo wameviimba kwa kushirikiana sambamba na kucheza pamoja kwenye jukwaa.
  Wanamuziki wengine waliopagawisha washabiki wa muziki katika onyesho hilo la tano ambao muziki wao umetengenezwa studio na msanii wa muziki wa studio kutoka Afrika ya Kusini ni SupaMega kutoka nchini Afrika ya Kusini,Olamide King Baddo kutoka nchini Nigeria na bendi ya Beca inayoundwa na wasanii wawili machachari wa muziki,Becky Sangolo na Carol Kamweru kutoka nchini Kenya. 

  Wakitoa maoni yao kuhusiana na onyesho hili,baadhi ya wapenzi wa muziki kutoka mikoa mbalimbali wanaolifuatilia walisema kuwa burudani za Coke Studio msimu huu ni moto wa kuotea mbali kwa kuwa kolabo za wanamuziki zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba zikionyeshwa zinaleta furaha na kumfanya mtazamaji kujiona anaangalia onyesho la wanamuziki hao mubashara (Live) Mbali na wasanii wa Tanzania,wasanii msimu huu wa tano wa Coke Studio unawajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon.
  Baadhi ya wasanii hao ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda ( Uganda).Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana. 

  Tangia onyesho hili lianze kuonyeshwa mwezi uliopita limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.

  0 0

  Chama cha Wataalam wa Urembo na Vipodozi Tanzania (CWUVT) wakutana Jijini Dar es salam kwa lengo la kuwakutanisha  pamoja wataalamu wa ngozi, wataalamu wa urembo, wataalam wa saluni,  wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi. Wanachama waasisi wa chama hicho walikutana chini ya Mwenyekiti Mama Shekha Nasser. Dhira ya Asasi hiyo ni kuinua, kuunganisha na kutumikia sekta ya Urembo na Vipodozi, watabibu wa ngozi na wataalamu wa Saluni ambao huboresha maisha ya watu kila siku. Pia kujenga na kudumisha wanachama ambao uwepo wao ni kukuza na kuunga mkono utaalam katika tasnia ya Urembo na Vipodozi kwa ujumla wake. 

  Wajumbe waasisi walioudhuria mkutano huo wameipitisha Katiba ya Chama hicho na kuazimia kujitoa na kushirikiana kwa pamoja katika kuelimisha, kuhudumia na kutetea haki za wataalam wa saluni, wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi katika tasnia ya Urembo na Vipodozi. 

  Chama hicho kimeona jinsi tasnia hii inakua kwa kasi, na mabadiliko ya kitechnologia hivyo wameona ni muda muafaka kwa Watanzania kuwa na uelewa zaidi kuhusu tasnia hiyo kubwa yenye Fursa kubwa ya Ajira hapa Nchini na kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi na hata kuingiza mapato ya kigeni.

  0 0


  MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikata utepe wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola (alieshika kipaza sauti) na Mkurugenzi wa Taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu Bi Semeni Gama (kulia kwa DC Hapi).

  MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikagua baadhi ya bidhaa zinazoandaliwa na wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu baada ya kizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

  MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akiongoza maandamano ya wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu kuelekea kwenye ofisi za taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam ambapo alizindua ofisi hizo mwishoni mwa wiki.


  MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi ameuomba uongozi wa Vicoba Endelevu hapa nchini kuhakikisha wanatanua mtandao wao uweze kuwafikia wananchi wengi zaidi wakiwemo walimu, wafanyakazi wengine wa serikali pamoja na wafanyabiashara ndogo ndogo ili kuisaidia serikali kufanikisha adhma yake ya kuyakomboa makundi hayo kiuchumi.

  Hapi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu iliyopo Bunju wilayani humo.

  “Niwaombe sana viongozi wa Vicoba mtanue zaidi mtandao wenu ili muwafikie maelfu zaidi ya wafanyabiashara ndogo ndogo, wafanyakazi mbalimbali wa serikali wakiwemo walimu na mshirikiane nao katika kuangalia namna bora zaidi ya wao kupata huduma za kifedha ikiwemo mikopo ili waongeze thamani ya mitaji yao,’’ alisisitiza.

  Zaidi, alitoa wito kwa wakina baba wahakikishe wanahamasisha wake zao pamoja na mabinti zao waweze kushiriki katika Vicoba ili kuinua vipato vya familia zao.

  “Mbali na wakina mama pia hebu tuwahamasishe zaidi wasichana ambao wamekuwa wakitumia muda na pesa zao katika urembo na kujipodoa na badala yake sasa wajenge utamaduni kujijenga kiuchumi zaidi kwa kushiriki katika vikundi hivi vya kijasiliamali pamoja na Vicoba,’’ alisema.

  Awali akitoa taarifa ya hali Vicoba endelevu hapa nchini, Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola alisema mtandao huo tayari unahusisha vikundi zaidi ya laki moja vikiwa na wanachama zaidi ya milioni mbili na laki mbili huku wakiwa na akiba ya zaidi ya Tsh Trilioni moja na milioni mia mbili.

  “Nitoe wito tu kwa wanajamii wazidi kushiriki katika Vicoba endelevu kwa kuwa ni mfumo ambao tayari umeonyesha kuwa unaweza kuwaonda katika umaskini,’’ aliomba.

  Akiizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu Bi Semeni Gama alisema taasisi hiyo inahusisha vikundi 128 kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya, Kigoma, Lindi, Tanga na Njombe ikiwa ina jumla ya wanachama hai 2,186 huku ikiwa na mtaji wa zaidi ya sh milioni 560.

  Pamoja na mafanikio hayo, Bi Semeni alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili taasisi hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa eneo ambalo lingetumiwa na taasisi hiyo kuanzisha mradi mkubwa wa kufuga kuku na kuanzisha shule ya chekechea.

  Hata hivyo, katika hotuba yake DC Hapi aliahidi kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaaa hiyo kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo kwa kuipatia ardhi taasisi hiyo kupitia mradi wa upimaji ardhi unaoendelea katika maeneo ya Mapwepande na Wazo.

  Mbali na wanachama kutoka vikundi mbalimbali vya Vicoba, shughuli hiyo pia ilihusisha uwepo wa taasisi mbambali za kifedha zikiwemo benki za ACB, CRDB, Benki ya Posta pamoja na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF

  0 0


  Tony Sugden, Mkurugenzi Mkuu na Mmoja wa Waanzilishi wa Kampuni ya Insight (Zamani Warrior Security) akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Insight ambayo ni Kampuni inayoaminika zaidi kwenye masuala ya ulinzi na Usalama Afrika Mashariki na Kati, katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam.
  Tony Sugden, Mkurugenzi Mkuu na Mmoja wa Waanzilishi wa Kampuni ya Insight (Zamani Warrior Security) akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Insight ambayo ni Kampuni inayoaminika zaidi kwenye masuala ya ulinzi na Usalama Afrika Mashariki na Kati, katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam.
  Allen Komba, Mfanyakazi wa Kampuni ya masuala ya Ulinzi ya Insight (Zamani Warrior Security) akipokea zawadi kutoka kwa Jacqui Sugden akiwa kama mmoja wa wafanyakazi aliyeitumikia kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007. Zawadi hiyo ilitolewa wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Insight ambayo ni Kampuni inayoaminika zaidi kwenye masuala ya ulinzi na Usalama Afrika Mashariki na Kati, katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam.

  Allen Komba, Mfanyakazi wa Kampuni ya masuala ya Ulinzi ya Insight (Zamani Warrior Security) akipokea zawadi kutoka kwa Jacqui Sugden akiwa kama mmoja wa wafanyakazi aliyeitumikia kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007. Zawadi hiyo ilitolewa wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Insight ambayo ni Kampuni inayoaminika zaidi kwenye masuala ya ulinzi na Usalama Afrika Mashariki na Kati, katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam.

  Kampuni ya WS Insight ambayo hapo awali ilijulikana kama Warrior Security jana usiku iliandaa chakula cha jioni katika hafla ya kuadhimisha muongo mmoja (miaka10) wa mafanikio, ikiwa ni miongoni mwa kampuni inayoaminika katika utoaji wa huduma bora za ulinzi na usalama ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

  Tukio hilo la chakula cha jioni lilifanyika jana usiku katika Hoteli ya Sea Cliff na liliwakutanisha zaidi ya wageni 100 kutoka katika sekta mbalimbali ambao waliburudishwa vilivyo na mchekeshaji mahiri kutoka Kenya, Eric Omondi. Pia kulikuwapo na zawadi kwa wafanyakazi ambao wameitumikia Kampuni hiyo kwa takribani miaka 10 sasa.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji na mmoja wa waanzilishi wa WS Insight, Tony Sugden alisema, “Baada ya kutimiza miaka 10, ninajivunia kusema kwamba hii ni kampuni yetu. Kampuni ilianza kufanya shughuli zake mkoani Arusha mwaka 2006 ambapo kwa sasa imeajiri watu 1,500 kwa Tanzania pekee na ina jumla ya wafanyakazi 7,000 kwa nchi tano ambazo tunatoa huduma.”

  “Ws Insight ilianzishwa kwa lengo la kutengeneza Mazingira salama ya kuwawezesha watu na biashara kuwa salama. Hilo ndilo jambo ambalo linatufanya kila wakati kufikiria majibu wanayohitaji wateja wetu na tunatimiza hayo yote kwa kufanya kazi zetu kwa kuzingatia uzoefu na ujuzi jambo ambalo linaongeza ufanisi katika upatikanaji wa taarifa kila wakati. Hakuna yeyote anayeweza kujilinganisha nasi kwa ufuatiliaji.”

  Kampuni yetu iliyoanzishwa Tanzania, imefanikiwa kujitanua hadi Sudan Kusini mwaka 2008, pia nchini DRC mwaka 2011. Zambia ilifika mwaka 2013 na Kenya mwaka 2014 huku tukibadili jina kutoka Warrior Security hadi kuwa WS Insight mwezi Machi mwaka huu. Kampuni ya Insight Group kwa sasa ina mapato ya Dola za Marekani milioni 35 kwa mwaka.

  Wateja wetu ni pamoja na Tier One Mining, Oil & Gas, UN, Mashirikia yasiyo ya kiserikali (NGOs), Serikali na taasisi za kibiashara ambazo zipo katika mazingira magumu duniani.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa pili kulia) akiongozwa na  Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi (kushoto) pamoja na Meneja mradi huo kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk mara baada ya kufika eneo la Soga - Kibaha jumamosi usiku kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
   Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi.
   Watanzania waliopata nafasi ya kufanyakazi katika mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wametakiwa kufanya kazi kwa uweledi na kuacha ubabaishaji. Ujumbe huo aliutoa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza usiku wa jumamosi katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali. 

  Kadogosa alisema mradi huo unatakiwa kwenda kwa kasi na kukamilika haraka hata kabla ya muda husika hivyo kila mtu atakayefanya kazi katika mradi huo anakikishe anafanya kazi na sio ubabaishaji utakaopelekea mradi huo kuchelewa. Aidha Kadogosa alisema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi usiku na mchana ili kuharakisha mradii huo na wakandarasi wanafanya haraka na kwa ukubwa wa mradi huu ni lazima tufanye kazi usiku na mchana.

   “Kama mnakumbuka wakati Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa alipokuja hapa alisema ni lazima twende kasi na wakandarasi wetu wameamua kwenda na kasi na sasa mnaona tuta linaendelea vizuri ni lazima mradi huu ufanywe usiku na mchana kutokana na ukubwa wake,”alisema.
   Msafara huo ulipofika eneo la mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga - Pwani.
   Shughuli ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga - Pwani ikiendelea.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa kwanza kulia) akiongea machache na makandarasi wa mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga -Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
   Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi. Kwa upande wake Meneja Mradi huo kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi alisema kazi inayoendelea kwa sasa ni kuendelea kusawazisha tuta ikiwa ni pamoja na kukata na kujaza, kujenga mifereji na madaraja ya reli pamoja na kuweka miundombinu ya umeme pamoja na vifaa vya kuongozea reli. “Kazi imeanzia kilometa sifuri kutoka Dar es Salaam kwa sasa hivi wakandarasi wanaendelea kazi ya tuta kukata na kujaza wana mitambo zaidi ya 106 na kazi kubwa ni kujenga tuta wanaendelea vizuri ili kuhakikisha wanakwenda kwa kasi inayotakiwa,”alisema Magedzi.
  Kwa upande wake Meneja mradi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk alisema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha mradi huo unatekelezwa usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

  0 0

  KUELEKEA siku ya uoni Duniani Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital) inatoa punguzo la bei za matibabu kwa asilimia 25 kwa watu ambao wataenda kutibiwa katika hospitali iliyop jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital),Adam Mwatima amesema kuwa hospitali ya Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital) inatoa huduma za upasuaji wa macho kwa gharama nafuu sana.

  Amesema kuwa kwawatu wenye bima za afya wanaweza kwenda kutibiwa katika hospitali hiyo kwa wale wenye bima za afya waliojiunga na hospitali hiyo hasa wenye bima za Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) pamoja na mifuko mingine.
   Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital),Adam Mwatima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa hospitali hiyo ya Kimataifa ya macho inapunguzo la bei kwa watakaoenda kutibiwa watapata punguzo la bei kwa pia kwa wale wenye bima ya afya watatibiwa kuitia bima zao. Kulia ni Meneja Masoko wa Hospitali ya Kimataifa ya Macho(The International Eye Hospital),Ilakoze Bidyanguze. 
   Daktari Bingwa wa upasuaji wa Macho wa hospitali ya kimataifa ya macho(The International Eye Hospital), Adyn Buren, Muuguzi wa (The International Eye Hospital), Denis Malanga, na Muuguzi wa hospitali ya Kimataifa ya macho (The International Eye Hospital), Ana Athanas wakimfanyia upasuaji mgonjwa wa macho aliyeenda kutibiwa katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam leo.

  Sehemu ya miwani ambayo hutolewa na Hospitali ya Kimataifa ya Macho (The Intarnationa Eye Hospital)iliyopo jijini Dar es Salaaam wa wale ambao wataenda kutibiwa katika hospitali hiyo.

  0 0

   Waziri wa Madini Angellah Jasmine Kairuki akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi. Jumla ya Mawaziri nane na Manaibu 16 wameapishwa pamoja na Katibu wa Bunge. 
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza akitia saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Justus Nditiye akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Kangi Lugola akipokea hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo hicho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Said Jafo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo mara baada kumalizika kwa hafla ya kiap oleo Ikulu Jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija - MAELEZO


  0 0

   Waziri wa Madini Angellah Jasmine Kairuki akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi. Jumla ya Mawaziri nane na Manaibu 16 wameapishwa pamoja na Katibu wa Bunge. 
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza akitia saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Justus Nditiye akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Kangi Lugola akipokea hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo hicho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Said Jafo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo mara baada kumalizika kwa hafla ya kiap oleo Ikulu Jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija - MAELEZO


  0 0

   Wauguzi wakiwa pamoja na Wananchi wakiungana pamoja na vituo mbalimbali vya afya katika maandamano ya  maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   aadhi ya Watoto wenye maradhi ya akili waliohudhuria katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Watoto wenye maradhi ya Akili wakionesha mchezo wa kuokota mbatata mbatata katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
  Watoto wenye maradhi ya Akili wakionesha mchezo wa magunia katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
  Mshindi wa mbio za magunia Salma Khamis Ame kutoka Skuli ya Mwanakwerekwe akipeleka mkono kusalimiana na mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Watoto wenye maradhi ya Akili wakishindana katika mashindano ya kula maandazi  katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Mshindi wa mashindano ya kula maandazi Mahad Said Ali akisalimiana na Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim akicheza muziki pamoja na watoto wenye maradhi ya akili katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk,Fadhil Muhammed Abdalla akitoa hotuba ya makaribisho katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Asha Abdulla Juma akielezea machache kuhusiana na maradhi ya Akili katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
  Mgeni Rasmi ambae ni Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali akitoa hotuba katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

  PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


  Na Pamela Mollel,Morogoro

  Waandishi hapa nchini wameshauriwa kuongeza muamko katika kuandika na kutangaza habari za vijijini kwa kuwa asilimia 75 ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini, ambako wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali

  Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Morogoro na mwenzeshaji Joe Nakajumo katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini iliyowakutanisha wanahabari kutoka mikoa mbalimbali iliyoratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania (UTPC).

  Nakajumo alisema kuwa waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuwa karibu na jamii ya vijijini kwa kutambua shughuli zao wanazozifanya na kuzifatilia kwa kuona mafanikio yao pamoja na kuibua kero zinazowakabili

  “Asilimia 75 ya wananchi wanaishi vijijini wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za kilimo,ufugaji ,uvuvi,ujasiriamali hivyo ni muhimu sana  kuwapa kipaumbela wananchi hawa”alisema Nakajumo.Aidha alisema kuwa moja ya majukumu ya msingi ya mwandishi wa habari ni kusaidia na kushiriki katika ujenzi wa taifa hivyo anapaswa kuudhihirishia umma kwa watu wote nchini wanapaswa kupata habari

  Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Adam Juma alisema kuwa mafunzo haya yatasaidia kuibua changamoto vijijini ambako panaoneka kusaulika kwa huduma mbalimbali za kijamii.Pia aliwaomba waandaji wa semina hii UTPC kuendeleza mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma hiyo

  Umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari lengo ikiwa kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi zao kwa kufata misingi ya taaluma .
  Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini mkoani Morogoro ,Semina hiyo imeratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC).
  Mwezeshaji wa semina Joe Nakajumo akifundisha katika mafunzo hayo leo Mkoani Morogoro.
  Kushoto ni Noria Damian ,katikati Editha Carlo pamoja Happines Mtweve wakifatilia mafunzo hayo.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini wakifatilia mafunzo hayo kwa ukaribu
  Amon Mtega kutoka Ruvuma Press club akiachangia mada katika mafunzo hayo ,kulia ni Queen Isack kutoka Kilimanjaro Press Club
  Kushoto ni mwakilishi kutoka Arusha Press club Pamela Mollel,katikati ni Adam Juma kutoka Mtwara Press Club wakifuatilia mafunzo hayo.
  Mwandishi wa habari Laudence Simkonda kutoka Mbeya kulia Oscar Simon kutoka Rukwa wakifuatilia mafunzo hayo..

  0 0

   Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega alieapishwa leo kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, akizungumza katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa Wilaya ya Mkuranga.
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga kimepata viongozi wapya wataongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano katika uchaguzi uliofanyika jana.

  Katika nafasi ya Mwenyekiti Wilaya imechukuliwa na Ally Msikamo kwa kura 749 baada ya kuwashinda wagombea wawili , Abdallah Kihato kura 189 na Mbaraka Mahanaka kura 44.

  Nafasi ya katibu Mwenezi Wilaya imechuliwa na Ben Mkulia kwa kura 89 na kuwabwaga wagombea wawili , Mchowi aliyepata kula 22 na Ali Ngalema kula Saba (7).

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya Mkuranga , Ali Msikamo amesema kuwa uchaguzi umeisha na kilechobaki ni kufanya kazi katika ya kuendesha chama katika kumsaidia Rais Dk. John Pombe Magufuli.

  Amesema kazi ya chama kazi ya chama wilaya kuishauri serikali katika kusaidia chama kuendelea kushika dola ikiwemo na maandalizi ya uchaguzi mkuu.

  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa uteuzi wa Naibu Waziri umetokana na wananchi wa Mkuranga na sio ujanja wake mwenyewe ndio uliomfanya aonekane.

  Amesema kuwa maendeleo ya Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuandaliwa mkutano utaohusisha wajumbe wote kuangalia walikotoka na wanako elekea.
   Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Wilaya  kwa kumpa ridhaa ya kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka miatano.
   Sehemu ya viongozi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi.

  Picha mbalimbali za uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
  Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0


  0 0

   Spika Mstaafu na Mwenyekiti  wa Bodi wa Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda, akizungumzia umhimu wa kutumia NHIF wakati wa uzinduzi wa huduma ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.
   Spika Mstaafu na Mwenyekiti  wa Bodi wa Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda , akizungumza na baadhi ya waumini baada ya kumaliza uzinduzi wa huduma ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.
   Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki  akiendelea kutoa maelezo ya umhimu ya mfuko huo kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.

  Bbaadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.

  SPIKA Mstaafu na  Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda  azindua huduma ya “TOTO AFYA KADI” kwenye nyumba za ibada.

  Akizungumza na waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge amesema  huduma hiyo itatolewa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwa  Sh. 50,400 kwa mtoto mmoja kwa mwaka.

  Makinda amesema kampeni hizo ambazo zitaendelea kwenye Madhehebu ya Dini lengo ni kuwa rafiki na huduma hiyo ili kufikia mwaka kesho watanzania asilimia zaidi ya  80 wawe wamejiunga na huduma hiyo.

  Makinda amesema kiasi hicho  cha Sh. 50,400 kitakachochangiwa kwa mwaka kitamuwezesha mwanachama huyo kupata matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

  Naye Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki amesema fao hilo pia hutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu kwa Sh. 50,400.

  Pia amesema NHIF hutoa huduma kwa vikundi vya  wajasiriamali walio kwenye vikundi vya watu kuanzia 10 kwa Sh. 76,800  kwa kila mwanachama mmoja ambaye atachangia fedha hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

older | 1 | .... | 1393 | 1394 | (Page 1395) | 1396 | 1397 | .... | 1897 | newer