Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1391 | 1392 | (Page 1393) | 1394 | 1395 | .... | 1896 | newer

  0 0

  BENKI ya CRDB tawi la Mlimani City kutoa mikopo kwa siku saba kwa wateja ambao ni wafanyabiashara wa kati (Small Medium Interpreses) ambao wataenda kukopa katika benki hiyo.


  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba.

  Amesema kuwa wiki hii ya huduma kwa wateja ni ya kukata keki na kufungua shampeini kwa wateja wa benki ya CRDB karibu kila tawi nchini kote kwaajili ya kuwashukuru wateja wake.

  Pia amewashukuru wafanyakazi wa Tawi lake kwa kufanya kazi kwa juhudi kama kuwajali pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vyeti vya shukrani.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akizungumza na wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam leo wakati alipotembelea katika tawi hilo kwaajili ya kudhimisha wiki ya Huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya Kwanza ya Oktaba kila mwaka. kushoto ni Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango.
   Mteja wa Muda mrefu, FaustaAssenga akikata keki kwaajili ya kushaherekea wiki ya huduma kwa wateja akishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay pamoja na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango na wateja wa benki hiyo Tawi la CRDB. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay jijini Dar es Salaam leo akimlisha keki Mteja wa Muda mrefu wa Tawila CRDB tawi la Mlimani City, Fausta Assenga ikiwa ni kwaajili ya kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wki ya kwanza ya mwezi Oktaba kila mwaka.


   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akiwalisha wateja keki wateja ambao ni wakuduma na wamuda mrefu wa Benki ya CRDB tawi la Mlimanicty jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay  akimlisha keki  Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka.
    Wateja wakifungua Shampeini kwaajili ya kushherekea wiki ya huduma kwa wateja leo katika benki ya CRDB tawi la Mlimani City.      Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akiwakabidh vyeti vya shukrani wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilangowakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa muda mrefu wa Benki ya CRDB tawi la Mlima city.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijni Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.


   Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


   Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akimkabidhi kijarida cha Mfuko huo chenye maelezo ya shunguli mbalimbali zinazotekelezwa na PSPF, kwa Mwanachama wa Mfuko amabye ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mstaafu, Mzee Thomas Martin  Kiama, (73), nyumabni kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja leo Oktoba 6, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto, ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, na Afisa wa Unedeshaji Bw. Ernest Massay.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambao ni wastaafu, wameupongeza Mfuko huo kwa kupata pensheni za kila mwezi kwa wakati.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa PSPF kutembelea Wanachama wake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, walisema kimsingi malipo ya pensheni ya kila mwezi yamekuwa yakiingia kwenye akaunti zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.
  “Mimi nashukuru penshni yangu napata bila shida, na inaingia kwenye akaunti yangu kwa wakati, hili napenda kuwapongeza sana.” Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu). Bw. Thomas Martin Kiama wakati alipotembelewa na ujumbe wa PSPF nyumbani kwake Oysterbay jana (Oktoba 6, 2017).
  Najua zipo changamoto za hapa na pale, mimi ningependa muwe huru kabisa, ili muweze kutuhudumia vema sisi wanachama, vinginevyo huduma zenu nazifurahia, aliongeza Bw.Kiama, ambaye alistaafu mwaka 2005.
  Kwa upende wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, nchini, Bibi. Mary Hariet Longway, naye aliipongeza PSPF kwa utoaji wa huduma na kwamba yeye anaridhishwa na utedaji kazi wake na kuwapongeza kwa kufika nyumbani kwake ili kupata maoni yake.
  “Ninashukuru sana kwa kunitembelea kwani hii ni ishara ya jinsi mnavyotujali sisi wastaafu, lakini mimi kama Jaji mstaafu kwa utaratibu ulivyokuwa, sisi hatukuwa na bima za afya sasa kama mngetoa elimu ya jinsi ya kupata bima ya afya kupitia kwenu lingekuwa jambo jema.” Alishauri Bibi Longway amabye naye alistaafu mwaka 2005.
  Alsiema, malipo ya kila mwezi ya Pensheni yake yamekuwa yakiingia kwenye akaunti yake bila shida yoyote.
  Naye askari wa Jeshi la Magereza (mstaafu), Bw.Kasim Salehe Mafanya, yeye naye aliipongeza PSPF, kwa huduma bora lakini akaomba utaratibu ufanyike ili pensheni hiyo iweze kuboreshwa na hivyo kuelndelea kuwa na manufaa zaidi.
  Akizungumza kwa niaba ya PSPF, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Bi. Mwanjaa Sembe, alisema, katika kuadhimisha Wiki ya Wateja Duniani, ofisi za PSPF kote nchini, zimefanya utaratibu wa kuwatembelea wanachama wake kwa lengo la kuwahakiki na kupokea maoni yao ili kuboresha utoaji wa huduma.Aidha katika Ofisi za Makao Makuu, Wakurugenzi an Mameneja waliungana na maafusa na wafanyakazi wa Mfuko huo, katka kuwahudumia wateja waliofika makao makuu.
   Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Bibi Mary Logway, ambaye  ni mwanachama wa PSPF, akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017, wakati alipotembelewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, kushoto.
   Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wakwanza kushoto), akimsikilzia mteja (mwanachama) wa Mfuko, huku afisa aliye kwenye mafunzo kutoka Chuo Cha Usimamzi wa Fedha, (IFM), Bw. Paschal W. Divaz, (katikati), akifuatilia.
   Bw. Silayo akisalimiana na wateja (wanachama) waliofika makao makuu ya Mfuko kuhudumiwa.
   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro, (kulia), akimuhudumia mteja (mwanachama) aliyekifa makao Makuu kuhudumiwa.
  Meneja wa Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na mteja wake, (mwanachama) wakifurahia jambo wakati mwanachama huyo akipatiwa huduma.
    Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, wapili kulia), akizungumza na afisa aliye mafunzoni, kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha, 9IFM), Bw.Paschal W. Diaz
   Afisa Uchangiaji wa Hiari PSS, Bi.Mwajuma A.Mohammed, (kushoto), akimuhudumia mteja.
  Afsia Mtekelezo, (CO), wa PSPF, Bi. Mwanaisha S. Waziri akiwa kazini.
   Afisa wa PSPF aliye mafunzoni, Bw. Alpha Mkopi, (katikati), akiwahudumia wateja, waliofika ofisi za Makao Makuu kupata huduma.
  Maafisa wa PSPF wakitoa huduma Oktoba 6, 2017.
  Mzee Kiama, (kushoto), akipitia maelezo ya uhakiki kabla ya kuweka saini yake. aliye nae ni Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe.
   Mzee Kiama akiweka saini kwenye fomu ya uhakiki.
  Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimpa maelezo, Jaji Mstaafu, Bi. Mary Longway, kuhusu uhakiki wa uanachama wake PSPF.
  Bi. Longway akiweka saini wkenye fomu hiyo ya uhakiki.
   Mkuu wa kitengo cha Mikopo kwa Wanachama wa PSPF, Bi. Linda Bahati, akizungumza na simu ya kikazi ili kupata maeelzo ya ziada wakati akimuhudumia mteja Oktoba 6, 2017.
   Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akizungumza na Mzee Kiama.
  Jaji (mstaafu) Longway na mukuu wake, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyaakzi wa PSPF waliomtembelea ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasili uwanja wandege wa Njombe, kwa ziara ya kikazi ya siku moja akitokea mkoani Ruvuma, ambapo atazungumza na maafisa na askari wa Jeshi hilo kuona changamoto wanazokutananazo wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoa Njombe, kwa ziara ya kiazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maafisa na askari wa Jeshi hilo kuona changamoto wanazokutananazo wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia.
  Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maafisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto wanazokutananazo wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia.Picha na Jeshi la Polisi

  0 0


  0 0

  Jengo la Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa kaskazini Unguja,kwa ufadhili ya Sheikh Saaed Al Buwardy chini ua Usimamizi wa Sheikh Yakob Osmna na mtoto wake Adil Yakob Osman,[Picha na Ikulu.] 06/10/2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika Viwanja vya Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini"A" Mkoa wa Kaskazini Unguja kabla ya kuuzindua msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa Sheikh Saeed Al Bwardy kwa usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake Adil Yakob
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Sheikh Abdulkadir Imamu wa Masjid Maamur kutoka Dar es Salaam pamoja na Viongozi wengine na mashekhe alipofika katika viwanja vya Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy na uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa Sheikh Saeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake AdilYakob
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bw.Samir Ayoub mmoja wa wanafamilia ya Bw.Yakoub Othman, msimamizi wa ujenzi wa msikiti masjid Saeed Al Buwardy katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini"A" Mkoa wa Kaskazini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa SheikhSaeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake AdilYakob
  Baadhi ya wananchi na Waislamu waliohudhuria katika uzinduzi wa Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa kaskazini Unguja,kwa ufadhili ya Sheikh Saaed Al Buwardy chini ua Usimamizi wa Sheikh Yakob Osmna na mtoto wake Adil Yakob Osman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi na Mashekhe mbali mbali mara baada ya kuuzindua Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa kaskazini Unguja,kwa ufadhili ya Sheikh Saaed Al Buwardy chini ua Usimamizi wa Sheikh Yakob Osmna na mtoto wake Adil Yakob Osman,
  Baadhi ya wananchi na Waislamu waliohudhuria katika uzinduzi wa Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa kaskazini Unguja,kwa ufadhili ya Sheikh Saaed Al Buwardy chini ua Usimamizi wa Sheikh Yakob Osmna na mtoto wake Adil Yakob Osman.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Mashekhe na Viongozi mbali mbali na Waislamu wakiwa katika Swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Abdulkadir Imamu wa Masjid Maamur kutoka Dar es Salaam (mbele) baada ya uzinduzi rasmi wa Msikiti Saeed Al Bwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa Sheikh Saeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake Adil Yakob Osman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa khutba ya uzinduzi wa Msikiti Masjid Saeed Al Bwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa Sheikh Saeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake Adil Yakob
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa khutba ya uzinduzi wa Msikiti Masjid Saeed Al Bwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa Sheikh Saeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake Adil Yakob,[Picha na Ikulu.] 06/10/2017.

  0 0

  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi wakimsikiliza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga( hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akifafanua jambo katika mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Mwezeshaji kutoka Shirika la Care Tanzania Bi Zenais Matemu akitoa mada katika Mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Baadhi ya washirki wa mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa katika mafunzo hayo yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi(kulia) akijadiliana jambo na Mwezeshaji kutoka Shirika la Care Tanzania Bi Zenais Matemu mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW  Na Kitengo cha Mawasiliano serikalini WAMJW


  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amewahimiza wanawake nchini kujiunga na vikundi vya kiuchumi katika kujiletea maendeleo.Ameyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya majaribio ya kuhamisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika katika wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

  Bibi Sihaba amesema kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi ni moja ya jitihada za utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000; Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/2022); Mpango wa Taifa wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/2021); na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.

  Ameongeza kuwa mwongozo wa uanzishaji wa vikoba utasaidia pia kuwa na takwimu za taarifa sahihi za vikundi kwa ajili ya uchambuzi na kujenga hoja kuhusu maamuzi ya ushiriki na uzingatiaji wa nafasi ya wanawake katika fursa mbalimbali.

  “Nijukumu la kila Mtaalamu wa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha mwongozo huu unatekelezwa ipasavyo na kuleta matokeo yaliyotarajiwa ya kuwawezesha wanawake kiuchumi ikiwemo kuboresha hali ya maisha yao” alisema Bibi Sihaba. Akiongea katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi amefafanua kuwa vikundi vingi vimekuwa vikiendeshwa bila kuwa na mwongozo na pia ukosefu wa elimu ya uendeshaji.

  Ameongeza kuwa hatua ya kuwepo mwongozo na elimu inayotolewa imetoa mbinu na kujenga uelewa ambao utatumika kuhamasisha wanawake kuunda vikundi na kuboresha vikundi mbalimbali vya kiuchumi kutegemea mazingira ya wanachama.Naye Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mvomero Bi. Sia Ngao amesema kuwa mafunzo ya mwongozo wa uundaji na uimarishaji wa vikundi vya kiuchumi ambayo yametolewa na Wizara mama yataimarisha usimamizi na uratibu wa vikundi kwa kuvifanya kuwa endelevu na kuwanufaisha wanawake wengi kutokana na waratibu kujengewa uwezo na upatikanaji wa elimu stahiki kwa walengwa mahususi.

  Kwa upande wake Mtaalamu wa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Mvomero Janeth Shishila amebainisha kuwa awali walikuwa wakiunda vikundi kiholela bila kuwa na mwongozo wa Kitaifa ila baada ya mafunzo haya yatawawezesha Idara kufanya kazi zake kwa umahiri zaidi katika kujenga ubia wa wanawake wajasiriamali ili kukuza faida ya kiuchumi, kijamii na kielimu kwa manufaa ya wanawake, familia na Taifa.

  Mwezeshaji kutoka Shirika la CARE Tanzania Bi Zenais Matemu ameeleza kuridhishwa na ushirikiano wanaopata kutoa Serikalini katika kuboresha hali za makundi yenye mahitaji maalum hapa nchini wakiwemo wanawake masikini. Dhumuni la mafunzo haya ya siku tatu yalikuwa yakifanyika kwa majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi, uzalishaji mali, viwanda vidogo vidogo, ili kukuza kipato na kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotokana na umasiki wa kipato katika kaya.

  Mbali na Halmashauri ya Mvomero, majaribio ya Mwongozo huu yatafanyika pia katika Halmashauri ya Rombo mkoani Kilimanjaro na kuzingatia uzoefu na maoni yatakayopatika kutoka kwa wadau kabla ya kuanza kutumika rasimi katika mikoa yote nchini.

  0 0

  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na waandishi wa habari Mjini Morogoro wakati akihitimisha zoezi la uhakiki wa NGOs nchini ulioanza Mwezi Agosti Mwaka 2017 kulia ni Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba.
  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akiwashukuru wadau wa mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini kwa ushirikiano wao katika zoezi zima la uhakiki wa NGOs nchini kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga.
  Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la NGOs Bw. Ismail Suleiman akitoa salamu za Baraza kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati wa kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki wa Mashiriki Yasiso ya Kiserikali Mjini Morogoro.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu wa Mashirikia Yasiyo ya kiserikali Bi. Tausi Mwilima (kulia) akitoa taarifa ya zoezi la uhakiki kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati wa kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki wa Mashiriki Yasiso ya Kiserikali Mjini Morogoro.
  Mwakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Abraham Salim akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati wa kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki wa Mashirika hayo. 
  Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wadau wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga( hayupo pichani) wakati wa zoezi la kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali nchini.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (kulia) akijadiliana jambo na mmoja wa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiseriakali nchini mara baada ya kuhitimisha zoezi la uhakiki kwa Mashirika hayo.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee wadau Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mara baada ya kuhitimisha zoezi la uhakiki kwa Mashirika hayo.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imehitimisha zoezi la uhakiki kwa Mashirika Masiyo ya Kiserikali nchini ulioanza Mwezi Agosti mwaka 2017.

  Akizungumza wakati wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu kukamilisha zoezi hilo Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa jukumu la Wizara ni kusajili na kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mujibu wa Sera ya kitaifa ya Mashirikka Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001.

  Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kwa kuimarisha mifumo ya uratibu kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini.Bibi Sihaba Nkinga ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni zilizopo katika kuendesha kazi zao katika kuhudumia jamii.

  “Tumekamilisha zoezi hili kwa kipindi tulichokiweka na ninawaomba wadau wetu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo katika utendaji wa shughuli zao la kila siku” alisema Bibi Sihaba.bibi Sihaba mefafanua kuwa Mashirika ambayo hayakuweza kuhakikiwa kwa sababu za msingi katika kipindi chote cha uhakiki, yanatakiwa kufika Ofisi ya Msajili wa NGOs ili kukamilisha zoezi hilo na mara baada ya tarehe hiyo muda wa uhakiki utasitishwa na mashirika hayo hayataruhusiwa kufanya kazi yoyote nchini kwa kushindwa kuzingatia taratibu.

  Kwa upande wake Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Marcel Katemba amewashukuru wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa kujitokeza kuhakiki Mashirika yao na kuwaomba kuendeleza ushirikiano uliopo kati yao na Serikali.“ Niwashukuru wadau wetu kwa kujitoa kwao na kuona umuhimu wa kushiriki na kuwa waangali wa zoezi hili la uhakiki wa Mashirika yao” alisema Bw. Katemba.

  Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Ismail Suleiman ameishukuru Serikali kwa kuendesha zoezi la uhakiki wa mashirikka hayo nchini kwa lengo la kusaidia kukuza ufanisi wa kazi zao.“Tunaishukuru Serikali kwa zoezi hili ambalo litatusaidia kuendesha shughuli zetu kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo”alisema Bw. Suleiman.

  Zoezi hili limefanikisha kuhakiki wa jumla ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 3,186 kati ya Mashirika 8,500 yaliyotarajiwa kuhakikiwa. Aidha, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2,655 yamesajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 na Mashirika 518 yamesajiliwa chini ya Sheria nyingine.

  0 0


  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na wachezaji wa timu ya African Sports kabla ya kuwakabidhi hundi milioni 2.1 leo
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi nahodha wa timu ya African Sports hundi ya milioni 2.1 leo wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hyo na wachezajiWAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya African Sports mapema leo mara baada ya makabidhiano hayo
  Mmoja kati ya viongozi wa timu ya African Sports wakimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo leo


  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewakabidhi timu ya African Sports “Wana kimanu manu”fedha milioni 2.1 kwa ajili ya posho za wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la pili Tanzania.Licha ya kukabidhi fedha hizo lakini pia aliwalipia kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF)Laki tano (500,000) kwa ajili ya leseni za wachezaji na ada ya ushiriki wa timu hizo.

  Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Waziri Ummy alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuiwezesha tmu hiyo kuweza kutimiza malengo yake ikiwemo kupanda daraja na kufikia hatua ya kucheza Ligi kuu soka Tanzania Bara.“Kwani iwapo timu hiyo itarejea Ligi kuu soka Tanzania Bara itasaidia kukua kwa fursa mbalimbali za kiuchumi katika Jiji la Tanga.

  “Sambamba na hilo lakini pia tumepokea mchango wa milioni 3 kutoka Kampuni ya GBP Oil ya Tanga ambao umeweza kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano wanayowakabili “Alisema.

  Aidha pia Waziri Ummy aliitaka timu hiyo wahakikishe wanafanya vizuri katika michuano hiyo ili kuweza kurejesha hadhi yake ya miaka ya nyuma ilipoweza kuwika katika medani ya soka hapa nchini.“Ndugu zangu wana African Sports msituangushe hakikisheni mnatumia misaada hii mnayoipata iweza kuwa chachu ya kufikia malengo yenu ya kufanya vizuri “Alisema.

  Hata hivyo pia Waziri Ummy aliwafungulia akaunti ya fedha wachezaji wote wa timu hiyo katika benki ya NMB ili iwe rahisi posho zao kulipwa moja kwa moja kupitia benki ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

   Ssehemu ya wananchi wakitoka kwenye semina ya ufugaji bora wa samaki wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na Taasisi ya NUEBRAND EC kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Joachim Komba wa Taasisi ya Eden Agri, akitoa elimu ya ufugaji bora wa samaki na faida zake wakati wa semina iliyofanyika  wakati wa wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji
   Wajasiriamali wakiata maelezo kuhusu ufugaji bora wa samaki aina ya kambare  waliokuwa wakioneshwa katika banda hilo la Eden Agri
   Wananci wakiwa banda la NSSF
   Wajasiriamali wakipata maelezo ya jinsi ya kunufaia na Benki ya NMB kuhusu mikopo mbalimbali
   Ofisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar,Aisha Ali Mohammed akimpatia maelezo mkazi wa Jiji kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo
   Maofisa wa Taasisi ya Nuru wakitoa maelezo  kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo
   Wajasiriamali wakisikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), Neema Fredrick (kushoto) na Godfrey Mshomari kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wajasiriamali wanachama wa mtandao huo. Aliyekaa ni Happiness Mshana.
   Ofisa Mkuu wa Elimu kwa Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, James Mtalika (Kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo wakati wa maonesho hayo
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akifafanua jambo kwa wajasiriamali kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo
   Meneja Uhusiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), Neema aktoa mafunzo kuhusu ulimaji bora wa kilimo cha mchaichai kinachoendeshwa na mtandao huo
   Mabanda ya taasisi zilizoshiriki kwenye maonesho hayo

  Maofisa wa Vicoba ambao ni sehemu ya wawezeshaji wa maonesho hayo

  0 0

  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
  Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Vijijini ikijihuzuru mbele ya wajumbe muda mchache kabla ya mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
  Msimamizi wa uchaguzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
  Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.
  Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.

  Na Mathias canal, Singida

  Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida  Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.

  Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya Ilongelo na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.

  Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni William Mwang'ima Nyalandu aliyepata kura 440, akifatiwa na FATUMA Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Alex Mdidi Lissu aliyepata kura 159.

  Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.

  Alisema kuwa pamoja na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa CCM Wilaya lakini pia nafasi zingine zilizowaniwa ilikuwa ni pamoja na Nafasi Ya Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya  ambapo Richard Niangusha Kwimba aliibuka mshindi kwa kupata kura  6, nafasi ya pili ni Khamisi Swalehe Kimu kura 35, Iddi Athumani Monko kura 8 na Swalehe Munkumbu Sungi aliyepata kura 3.

  Nyingini ni nafasi ya mkutano Mkuu wa CCM Taifa waliomba ridhaa katika nafasi hiyo ni watu 14 ambapo kati yao washindi ni Sabasaba Manase, Zainabu Abdaleah na Khadija Kisuda Lesso.

  Nafasi ya Halmashauri Kuu ya Wilaya waliogombea ni 27 ambapo kati yao walioshinda ni Sabasaba Manase, Edward Jared Ihondo, Japhet Ntandu Gham, Justin Joseph Monko, Mohamed Abdallah Ghamayu, Nkumbi Mohamed Kemi, Zuena Dunya, Simon Mumbai, Shabani Ally Mang'ola, na Wiliamu Mwang'imba Nyaland.

  Nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliomba  walikuwa watano lakini washindi kati yao ni Mchungaji Wilson Mtatuu Ihucha, na  Sada Njiku. Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoa ni Sabasaba Manase, Shaban Mang'old na Edward Jared Ihonde.

  Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Singida Bi Grace Shindika alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya wananchama na viongozi wote waliochaguliwa ili kuongeza ufanisi na nguvu ya chama katika Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(kushoto) akimsiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe alipokuwa anazungunza kuhusu namna benki ya Azania inavyowajali wateja wao wadogo wadogo, wa kati na wakubwa na kwenda nao bega kwa bega ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea pamoja nakueleza bidhaa walizonazo katika benki hiyo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema akizungumza kuhusu changamoto na faida anazozipata kupitia benki ya Azania pamoja na kushauri namna nzuri kuwajali wateja wao mara alipotembelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) ofisini kwake.
    Meneja wa benki ya Azania tawi la Tegeta, Geofrey S. Mahona(kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati wakifuatilia mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema alipokuwa akisisitiza jambo kuhusu benki ya Azania.
  Mkutano ukiendelea wakati wakati wa maofisa wa benki ya Azania pamoja na Mkurugenzi wao walipomtembelea mteja wao ofisini kwake kwa ajili ya kutaka kujua ni changamoto zipi anazipata kwenye biashiara yake. Kushoto ni uongozi wa Hospitali hiyo na kulia ni viongozi wa benki ya Azania.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) akimkabidhi hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(wa pili kutoka kushoto).
  Picha ya Pamoja

  0 0

  Afisa Masoko wa UTT AMIS akitoa elimu na kutoa huduma kwa wawekezaji wa zamani na wapya wa UTT AMIS katika maonyesho ya Tasisi za Fedha Mnazi Mmoja jijini DSM.
  Afisa Masoko wa UTT AMIS akitoa elimu na kutoa huduma kwa wawekezaji wa zamani na wapya wa UTT AMIS katika maonyesho ya Tasisi za Fedha Mnazi Mmoja jijini DSM.

  Afisa Masoko wa UTT AMIS akitoa elimu na kutoa huduma kwa wawekezaji wa zamani na wapya wa UTT AMIS katika maonyesho ya Tasisi za Fedha Mnazi Mmoja jijini DSM.

  0 0      
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2017. Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na maafisa waandamizi wa Ofisi ya Rais walikuwapo. Picha na Ikulu
  0 0


  0 0

  Mmoja wa wateja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo akikata keki kwa niaba ya wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe na kulia ni Meneja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akizungumza na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Azania Tawi la Kariakoo alipotembelea benki hiyo ili kuwa bega kwa bega na wateja katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuzungumzia baadhi ya bidhaa walizonazo katika benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akimlisha keki Meneja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni kwa niaba ya wafanyakazi wa tawi hilo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akiwalisha keki baadhi wateja wa benki ya Azania tawi la Kariakoo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo benki ya Azania iko bega kwa bega na wateja wao.
  Mmoja wa wateja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo akitoa maoni yake kuhusu benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
   Baadhi ya wateja wa benki ya Azania tawi la Tegeta wakitoa maoni yao kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe pamoja na kuishukuru benki hiyo kuwa na mfumo wa Simu uliorahisisha huduma nyingi.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akiwalisha keki wateja wa benki ya Azania tawi la Tegeta wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza  jumatatu Oktoba 02 mwaka huu.
  Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Tegeta, Geofrey Mahona akizungumza na wateja waliofika kupata huduma kwenye benki hiyo pamoja na kuwashukuru wateja hao kwa kuwa karibu na benki hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Azania tawi la Kariakoo.

  0 0


  Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael (kulia) akimkabidhi zawadi ya seti ya televisheni Amina Nachunga, mojawapo ya washindi wa promosheni ya nunua simu na ushinde jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya washindi sita wamejinyakulia zawadi za luninga na pikipiki katika promosheni hiyo inayoendelea, ambapo Tigo inawazawadia wateja wake wanaonunua simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote.

  Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael (kulia) akimkabidhi zawadi ya pikipiki Amina Khalfan, mojawapo ya washindi wa promosheni ya nunua simu na ushinde jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya washindi sita wamejinyakulia zawadi za luninga na pikipiki katika promosheni hiyo inayoendelea, ambapo Tigo inawazawadia wateja wake wanaonunua simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaban akizungumza wakati wa mahafali ya 8 ya  Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi katika Sherehe ya Mahafali ya nane ya bodi  yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
   Wahitimu wa Shahada ya Ununuzi na Ugavi  wakiwa katika Maandamano  wa Mahafali ya nane ya bodi ya watalaamu wa ununuzi na Ugavi.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaban akiongoza Maandamano wakati wa mahafali ya 8 ya  bodi ya Watalaamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika  Moshi(MOCU), Neema Kumburu  akipokea cheti cha chuo hicho kuongoza katika utoaji wa masomo hayo mwaka wa pili Mfululizo
   Hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi akitoa nasaha kabla ya kumkaribisha mgeni Ramsi katika Mahafali ya 8 ya chuo hicho
   Wahitimu wa Shahada ya Utaalamu wa Ununuzi na  Ugavi (PSPTB) wakisoma Kiapo Mbele ya Mgeni Rasmiwakati wa mahafali ya 8 ya  bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi,Ahmed Kilima akitoa hotuba ya Shukrani wakati wa kufunga  mahafali ya 8 ya  bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Wahitimu wa Shahada ya Utaalamu wa Ununuzi na  Ugavi (PSPTB),  katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 8 ya bodi

  Wafanyakazi wa bodi ya Ununuzi na ugavi wakiwa katika picha ya pamoja na  mgeni rasmi na meza kuu wakati wa kuhitimisha Mahafali ya 8 ya bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

  Brass Bendi kutoka Jeshi la Magereza nchini wakitoa Burudani wakati wa Mahafali ya Nane ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

  0 0

  JUMUIYA ya raia wa Comoro waishio Tanzania wameiomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini kusaidia kupatikana kwa ndugu yao Ammar Abdousoi Madou (26) aliyepotea na kutoweka kusikojulikana tangu tarehe 29 Juni mwaka huu.

  Akizungumza na Waandishi wa habari leo (jana) Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Jumuiya hiyo, Larifou Said alisema taarifa za kupotea kwa Madou ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala nchini Uganda ziliifikia familia yake tarehe 29 Juni, mwaka huu.

  Said anasema familia ya Madou ilipokea taarifa za kushikiliwa kwa Madou na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha tarehe 27 Juni, mwaka huu kutoka kwa rafiki wa karibu wa Madou anaeishi Mkoani Arusha na baadae kuelezwa kuwa aliachiwa huru tarehe 29 Juni mwaka huu, ingawa tangu kipindi hawajaweza kuonana nae hadi sasa.

  Anasema pamoja na familia hiyo kufanya jitihada mbalimbali za kufanikisha upatikanaji wa ndugu yao ikiwemo kufanya Mawasiliano ya mara kwa mara na vyombo vya usalama ikiwemo kuwasiliana na Idara ya upelelezi ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufahamu undani na sababu ya kukamatwa kwa Madou.

  Akifafanua zaidi Said anasema Jumuiya hiyo tayari imefanya mawasiliano na Ubalozi wa Komoro nchini, ambao nao uliandika barua katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuelezea malalamiko yao ya kupotea kwa ndugu yao ambapo pamoja na kuomba uchunguzi wa kina uendelee kufanywa na vyombo vya dola vya Tanzania.

  “Wiki iliyopita tulielezwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kuwa Madou aliachiwa huru, lakini tulipofunga safari kuelekea Arusha hatukumkuta bado tunaendelea kujenga imani na vyombo vya dola vya Tanzania lakini tunaomba jitihada ziendelee kuongezwa ili Madou aweze kupatikana” alisema Madou.

  Akielezea tukio la kukamatwa kwa Madou alisema, ndugu yao alirudi Tanzania mwezi juni mwaka huu kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Idd el fitri ambapo tarehe 27 juni mwaka akiwa njiani kurudi Uganda alikamatwa Moshi Mkoani Kilimanjaro akiwa katika basi yenye namba za Usajili T 502 DHF na baadae kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Arusha.

  Said anasema pamoja sheria kulitaka Jeshi hilo kumfikisha mtuhuhiwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili, Ofisi ya Polisi ilishindwa kumfikisha mtuhumiwa huyo katika mhimili wa dola na baadae kudai kuwa lilimwachia huru pasipo na kupatikana kwa vielelezo vinavyoonyeshwa kuachiwa kwake.

  Mwanasheria wa Jumuiya ya Raia wa Comoro waishio Tanzania, Larifou Said akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu tukio la kupotea kwa Mwanafunzi Raia wa nchi hiyo Ammar Abdousoi Madou (pichani) ambapo waliliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji wa ndugu yao huyo.

  0 0

  KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga 
  KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga 
  KAIMU Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt.Tito E. Mwinuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo kulia akiwa na Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale wakisikiliza kwa umakini hoja za wafanyakazi 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi akizungumza katika mkutano huo 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi kushoto akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka wakati wa kikao hicho 
  Mwenyekiti wa Tuico Tanzania,Paul Sangeze akizungumza katika mkutano huo 
  Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya Afya kwa wajumbe wa baraza hilo 
  Mmmoja wa wafanyakazi na mjumbe wa baraza hilo akichangia kwenye mkutano huo 
  mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Janet Vesso akichangia mada 
  Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi wa pili kutoka kushoto,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka kulia na Mwenyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze wa kwanza kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale


  BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeazimia kuunga mkono jitihada za Rais Dkt John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya watu wenye kipato cha kati kwa kufanya kazi kwa umahiri,uzalendo na ufanisi.

  Akizungumza katika ufungaji wa baraza hilo mwishoni mwa wiki mjini Tanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi alisema bodi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha shirika linafikia malengo yake muhimu.

  Alisema malengo hayo ambayo yanahitajika katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwa kasi kubwa kutakapotokana na kuwa na umeme wa uhakika ambao unaweza kusukuma gurudumu la maendeleo.Aidha alisisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya shirika hilo ili iweze kusaidia kutoa huduma zake wakati wote bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile.

  Hata hivyo aliwaasa wafanyakazi wa shirika hilo kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili isiweze kuibiwa ikiwemo kuhakikisha haihujumiwi na watu wanaoweza kufanya hivyo.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

older | 1 | .... | 1391 | 1392 | (Page 1393) | 1394 | 1395 | .... | 1896 | newer