Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

REACHING SUSTAINABLE DEVELOPMENT GOALS WITH NUCLEAR ENERGY

$
0
0
With globalized economics and a new era of global interconnectedness all counties and stakeholders share the same responsibilities, to ensure a safe and sustainable future for generations to come. 
In this regard the United Nation has traced 17 Sustainable Development Goals (SDG) to be followed by all nations for all nations. These goals provide clear guidelines to tackle the root causes of poverty, hunger, climate change and unite all necessary efforts to make a positive change for mankind and the planet. 

It is generally accepted that science and technological innovations need to play a fundamental role in assisting global leaders to find the answers to pending issues.It is therefore no surprise that nuclear science and innovative nuclear technologies are playing a major role in providing viable solutions to help achieve these ambitious SDG targets. It is well known globally that nuclear technologies have much to offer in the fight against poverty, hunger, dread diseases, and water shortages, not to mention its ability to provide sustainable and environmentally friendly electricity.

Let’s take a closer look these various applications.

Nuclear medicine helps millions of people across the globe to successfully fight cancer and has reducedthe mortality rate of non-communicable diseases by one third. Moreover, nuclear science centers and research facilities are indispensable in the production of radioisotopes which are used in complex medical treatments. 

The International Atomic Energy Agency (IAEA) provides training and seminars to improve cancer management across the globe.With the help of nuclear technologies Tanzanian doctors can now deliver more precise radiation treatment to patients with oncological diseases using modern scanning methods previously not available in the region. 

These new methods make it possible to treat more patients than before with more accuracy.As the population continues to grow rapidly in emerging countries, the availability of potable water remains one of the most pressing issues for the mankind. Innovativenuclear technologies can be used to desalinate ocean wateror to reducecontaminants in contaminated water, making it safe to use.A number ofcountries such as Kenya have already used nuclear technologies to manage water consumption more effectively. 

Nuclear and isotopic based techniques have helped Kenyan farmers to use water in a more cost-effective manner,the technique reduces costs by more than 50% when compared to standard irrigation. Isotopic techniques were used to determine the most efficient way to use saline groundwater and treated sewage water through drip irrigation.Drip irrigation reduced the amount of water needed by up to 30%, compared to sprinkler irrigation.

Water purification and desalination can be of huge benefit toTanzania, where it is difficult for many people in arid regionsto access clean water. Implementation of these technologies is of high importance for the East African country where nearly 23 million people don’t have full access to safe potable water. 

Sometimes water scarcity can be explained by climate change and environmental degradation, generated by carbon dioxide emissions, caused by burning coal or oil.Even in this respect nuclear science and nuclear power plants are playing an important role in both climate change mitigation and adaptation. Electricity generated by nuclear power plants is reliable, while the process of generation does not emit any hazardous substancesand pollutants into the air. 

To meet global targetsin thecombat against global warming, manyemerging countries are turning tonuclear power, as it is able to kill two birds with one stone – generate clean environmentally friendly electricity, at a very affordable price.

In addition to this, nuclear techniques render significant assistance to farmers in combating desertification and soil degradation. Isotopes make it possible to identify erosion spots and help to restore these affected zones.This leads to higher incomes, a diverse ecosystem and biodiversity.

MANGULA AKUTANA NA KIONGOZI WA PALESTINA

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula akizungumza na Naibu Namishina wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (FATAH) Dk. Uri Davis, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 3, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).

WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa  Dkt. Kissui Stephen  Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama wa mtandao huo walipowasili katika  eneo la shamba  hilo lililopo Ruaha- Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara la Papai. Kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji na  Mwanzilishi wa mtandao huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.  

Dk. Kissui amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaonesha Wakulima wanachama wa Mkikita  mashamba wanayotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia kuutangaza mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi kwenye kilimo.


Alisema kama mtu hawezi kulima mwenyewe kuna wataalamu mbao watawekwa shambani kwa gharama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo.


Pia,  Dk. Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazozalisha mara tatu zaidi na mbolea za Organic  ambazo hazina madawa na haziharibu ardhi ili kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahia.


Alisema pia Mkikita husaidia kutafuta  masuala ya masoko duniani kabla ya kuanza kulima zao husika.



"Sisi tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima kwenye masoko" Alisema Kissui.


Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) wakiwasili Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya kujionea shamba lenye ekari 3000 kwa ajili ya kuwekeza Kilimo cha PAPAI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea miradi ya kuhamasisha kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania, Adam Ngamange alisema katika mtandao wanafanya miradi ya uhamasishaji kilimo na ufugaji kibiashara.


Alisema waligundua Watanzania wengi wanalima lakini si kibishara ambapo wameanza na miradi mitano katika maeneo maalum kama Ruaha  ambako waendesha kilimo cha Papai kwa kufuata taratibu zote za msingi  za kilimo hai.


Aliongeza kuwa mradi huo utakaoanza na ekari 384 zitakazogawanywa katika mafungu ya ekari 32 na kupandwa katika utaratibu wa kili mwezi mara moja ili waweze kusambaza papai kwenye masoko makubwa.

 Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakitembelea na kukagua shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui (katikati) amueleza jambo Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.  
 Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha (alienyosha mkono), Amani Matinya akiwaonesha wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzaniaukumbwa shamba hilo na mbinu zinazotumika kumwagilia.
 Muonekano wa shamba hilo.
 Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzaniawakielekea kujionea maji yanayotoka Mto Lukosi unaotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
 Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzaniawakiangalia mashine zinazovuta maji kutoka Mto Lukosi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
 Muonekano wa Mto Lukosi.
 Mmoja wa wakulima wa eneo la  Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa (kulia) akifafanua jinsi maji yanavyo sambazwa kwa wakulima.
 Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzaniawakipanda kwenye basi tayari kuanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam.

HABARI/ PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

MSANII IZZO BIZNESS WA TANZANIA NA AVRIL WA KENYA WAPAMBA ONYESHO LA COKE STUDIO

$
0
0
Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wanaendelea kupata burudani ya muziki kutoka wasanii nguli kutoka nchi za Afrika kupitia onyesho la Coke Studio kupitia luninga ya clouds ambapo mwishoni mwa wiki Kolabo ya mwanamuziki kutoka nchini Izzo Business na Avril kutoka Kenya imeacha gumzo kubwa. Wanamuziki wengine waliopagawisha washabiki wa muziki katika onyesho hilo ni Mafizikolo kutoka Afrika ya Kusini kwa kushirikiana na msanii Nyashinski kutoka nchini Kenya na wasanii waalikwa Bill Nas (Tanzania),Sheebab (Uganda) na Asgeg Ashko (Ethiopia). Akiongea juu ya kolabo hili,Izzo Business alisema amefurahi kushirikiana na Avril kimuziki hususani wimbo walioimba pamoja unaojulikana kama 'Kanyonyi Kanja' na 'mabata mabata yanaogelea' ambao umeimbwa kwa lugha ya Kiswahili ukiwa na vionjo vya muziki wa bongofleva. Kupitia onyesho hili la Coke Studio linaloandaliwa na kampuni ya Coca Cola muziki wa Tanzania unazidi kutangazwa ikiwemo vipaji vya wanamuziki kutoka hapa nchini ambao wanashirikiana na wenzao kutoka Afrika na linarushwa kwenye luninga kwenye nchi zaidi ya 50. Wasanii wa Tanzania waliopo katika onyesho la Coke Studio msimu huu ni Ali Kiba, Rayvanny, Izzo Bizness, Nandy na mtengenezaji wa muziki wa studio nguli Nahreel. Wakitoa maoni yao kuhusiana na onyesho hili,baadhi ya wapenzi wa muziki kutoka mikoa mbalimbali wanaolifuatilia walisema kuwa burudani za Coke Studio msimu huu ni moto wa kuotea mbali kwa kuwa kolabo za wanamuziki zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba zikionyeshwa zinaleta furaha na kumfanya mtazamaji kujiona anaangalia onyesho la wanamuziki hao mubashara (Live).
Mbali na wasanii wa Tanzania,wasanii msimu huu wa tano wa Coke Studio unawajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon Baadhi ya wasanii hao ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya), Sami Dan (Ethiopia), Bebe Cool, Eddy Kenzo, Sheebah, Ykee Benda ( Uganda). Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius, Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana. Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AKUTANA NA WAGENI KUTOKA MAREKANI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani ikiongozwa na Mwinjilisti Rojas Matias, walipomtembelea ofisini kwake jana. 

Watumishi hao walikuwa na mkutano mkubwa wa injili tangu Septemba 27 hadi Oktoba Mosi, 2017 katika uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ulioandaliwa na kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola.

Mhe.Mongella aliwahakikishia ushirikiano mwema pindi watakapokuwa tayari kuwekeza katika shughuli mbalimbali ikiwemo za kielimu katika mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani
Wageni kutoka Marekani pamoja na mwenyeji wao Mchungaji Kulola, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani. Katikati ni Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani na kushoto ni Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati), Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani (kushoto) pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia)
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiwa pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia).
Katibu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Levi Matia (kushoto), akiwakaribisha wageni kutoka Marekani walipotembelea ofisini hapo jana.
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani ikiwa kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani ikiondoka katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza na mwenyeji wao Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (wa kwanza kushoto).
Salamu na wenyeji katika mitaa ya Jiji la Mwanza
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani pamoja na wenyeji wao fukwe za Ziwa Victoria ili kujionea mawe ya "Bismarck Rock" katika eneo la Kamanga
Walifurahia uzuri wa eneo hili na hakika hii ni nenmbo ya Jiji la Mwanza
Walifurahia ukaaji wa mawe haya
Pia ilikuwa furaha kugusa maji ya Ziwa Victoria mubashara
Eneo hili lina mijusi wakubwa hivyo walifurahia kuitazama mubashara
Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) kutoka kanisa la kimataifa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, katika fukwe za Kishimba Beach.

TIRA -YATOA MAFUNZO KWA ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOA WA PWANI KUKABILIANA NA WAMILIKI NA MADEREVA WANAOTUMI STIKA ZA BIMA FEKI

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, PWANI

KATIKA kukabiliana na kupambana na wimbi la wizi linalofanywa na baadhi ya wamiliki wa magari na pikipiki kuamua kutumia stika za bima bandia hatimaye Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za bima nchini (TIRA) imeamua kutoa mafunzo kwa askari wa kikosi cha usalamaa barabarani Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwapa uelewa.


Akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yamewashilikisha maafisa wa polisi pamoja na askari wa kikosi cha usalama barabarani Kamishina mkuu wa (TIRA) nchini Baghayo Sakwele amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwafundisha askari wa usalama barabarani mfumo mpya ambao utaweza kuwasaidia kutambua na kuhakiki stika za bima ambazo ni bandia na zinatumika kinyume kabisa na sheria na taratibu.

Kamishina huyo alibainisha kuwa kwa sasa wameamua kushirikiana na jeshi la Polisi ili kufanya msako wa kuwabaini wamiliki wa vyombo vya moto kutumia bima feki kitu ambacho kinachangia kwa kiasi kikubwa kupotea kwa pato la Taifa kutokana na vitendo vya wizi ambavyo vinafanyika, Ameongeza kuwa changamoto iliyopo ni wamiliki wengine wanafanya ujanja wa kutumia bima moja zaidi ya magari matano.

“Sisi kama TIRA ambao ndio wenye mamlaka ya utoaji wa stika za bima katika vyombo vya magari, tumeamua kushirikiana bega kwa bega na jeshi la polisi Mkoa wa Pwani ili kuhakikisha kuwa baaadhi ya wamiliki waliokuwa na tabia ya kutumia magari yao au pikipiki kwa kutumia bima bandia tunawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria na katika hili hatuwezi kuwavulimilia hata kidogo,”alisema Kamishina Sakwele.

Kwa upande wake Kaimu kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Blasilusi Chatanda alisema kuwa atalivalia njuga suala hilo la kufanya msako mkali ili kubaini mtandao unaojihusiha na kutengeneza bima feki ili kuwadhibiti wale wote ambao walikuwa wanatumia bima bandia kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

“Kama jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wenzetu wa Tira kwa kweli tutashirikiana nao kwa hali na mali na kwa kuwa wameshatupatia mafunzo kuhusiana na mambo mbali mbali ikiwemo kuwepo kwa wimbi la madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuwa na tabia ya kutumia stika za bima feki tunawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa hivyo askari wetu nina imani walilifanikisha suala hilo,”alisema Kamanda.

Nao baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Pwani ambao wameshiriki katika mafunzo hayo akiwemo George Peter, Laitiness Kimaro pamoja na Khalid Mohamed wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika masuala mbali mbali ya kuwaelimisha madereva wa magari na pikipiki kuhusiana na bima bandia na iliyo halali.

Walisema kuwa wana imani kuwa baada ya kujifunza mafunzo hayo wataweza kufanya kazi zao za barabarani kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa madereva wote wa vyombo vya moto ikiwemo magari pamoja na pikipiki kuhusiana na matumizi halali ya ukataji wa bima zao pamoja na madhara ya kukata bima amabazo ni feki.

“Kwa kweli sisi kama askari wa kikosi cha usalama barabarani katika Mkoa wa Pwani tumefarijika sana kuaptiwa mafunzo haya na wenzetu wa mamlaka ya husika, hivyo na sisi tutahakikisha elimu hii inakuwa ni chachu na mkombozi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku pindi tunapokuwa barabarani hivyo ni jambo ambalo kwa kweli ni faida kwetu,”walisema askari hao.

ASKARI hao wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Pwani mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo walikwenda kufanya ukaguzi wa magari barabarani kwa njia ya vitendo zaidi ambapo katika zoezi hilo wamefanikiwa kukamata baadhi ya magari na kuyapiga faini ambayo yamekuwa bado yakiendelea kutumia bima feki kinyume na sheria za nchi.

Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma

$
0
0
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuzungumza na wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma pamoja na Sekretarieti ya bodi hiyo wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula (aliyesimama) akitoa neno la shukrani mara baada ya kuzinduliwa kwa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula vitendea kazi mara baada ya kuzindua bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe na sekretarieti ya Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo



Eliphace Marwa-MAELEZO.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amezindua bodi mpya ya mishahara na masilahi katika utumishi wa umma mapema jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo waziri Kairuki ameitaka bodi hiyo kuzingatia misingi iliyopo kwenye hati maalum ya Rais ambayo inawataka kuzingatia vigezo ambavyo ni pamoja na malipo ya mishahara na masilahi kwa watumishi wa Umma yanapatikana na kuwa endelevu.

“Ni vema kuhakikisha utumishi wa Umma unavutia na kubakiza taaluma zinazohitajika katika kuendesha shughuli zake ili kuweza kuleta tija kwa kuzingatia uwazi, usawa na haki mahala pa kazi”, alisema Waziri Kairuki.Aliongeza kuwa endapo bodi itazingatia vigezo hivyo, ushauri watakaoutoa utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na hivyo kujenga imani kwa watumishi wa Umma na wadau wengine.

Waziri Kairuki aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa bodi hiyo na kusema kuwa Serikali iko pamoja nayo katika kuhakikisha masiilahi ya watumishi wa Umma yanaboreshwa ili kuongeza tija kwa kuwabakiza wataalam katika Utumishi wa Umma.Naye Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula ameahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza kwa kwa kufanya tafiti.

“Napenda kusema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika bodi tutashirikiana na Serikali katika kuboresha hali ya utendaji katika utumishi wa Umma kwa kufanya tafiti kwa lengo la kuishauri Serikali ili iweze kuwapatia maisha ya staha Watumishi wa Umma”, alisema Ndagula.

Waziri Kairuki aliwataja wajumbe wa bodi hiyo kuwa ni Mwenyekiti, Donald Ndagula,Makamu Mwenyekiti, Balozi Charles Mutalemwa ,Wajumbe George Mlawa na Bi Gaudentia Kabaka.Wengine ni Jaji Mstaafu Regina Rweyemamu, Meja Jenerali Mstaafu Zawadi Madawili na Kamishna Mwandamizi wa Polisi Mstaafu Jamal Rwambow.

Waziri Kairuki iliitaka bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanatekeleza jukumu lao la kuboresha masilahi ya watumishi ili wahamasike na waongeze tija katika utendaji kazi kwani,Serikali haiwezi kufanya maamuzi sahihi bila ya ushauri wa kitaalamu unaotokana na tafiti kuhusu maboresho ya masilahi ya watumishi wa Umma.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA DUKA LA BIMA YA AFYA LA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

$
0
0

 Sehemu ya muonekana kwa ndani duka la Bima ya Afya la Halmashauri ya Jiji la Tanga
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akiwa nje ya duka hilo akisubiri mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye duka hilo
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na watumishi wa mfuko huo mara baada uzinduzi wa duka hilo katikati ni Macrina Clemence ambaye ni Afisda Matekelezo wa Mfuko huo na kulia ni DaktariLuiza Mtafi 
 Sehemu ya watumishi wa NHIF Mkoani Tanga katikati ni daktari Luiza Mtafi kushoto ni Afisa Madai NHIF Mary Daniel na kulia ni Afisa Matekelezo,Macrina Clemence
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu wakifuatilia uzinduzi huo.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

WAZIRI MBARAWA: WAKANDARASI JENGENI BARABARA KWA VIWANGO

$
0
0

Serikali imesema itahakikisha inaendelea kuwasimamia wakandarasi wa Ujenzi wa Barabara kuhakikisha wanajenga barabara zote nchini kwa viwango vilivyokusudiwa na kumaliza kwa wakati ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa leo jijini Dar es salaam mara baada ya kukagua Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano jijini humo ambapo ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wake na kusisitiza kwa Wakala wa Baraba (TANROADS), mkoa wa Dar es salaam kuwa wakali katika usimamizi ili kuhakikisha barabara hizo zinajengwa kwa viwango vilivyokubaliwa kwenye mkataba.

“ Serikali imekuwa ikitumia Fedha nyingi katika kutekeleza miradi hii, hivyo TANROADS hakikisheni mnasimamia wakandarasi hawa kujenga barabara hizi kwa viwango na kwa wakati”, amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa utekelezaji wa awamu hiyo unaendelea vizuri ambapo unahusisha barabara ya Kifuru – Msigani (km 4.5) ambayo kwa sasa imefika asilimia 87, Goba – Makongo (km 4.5), nayo imefikia asilimia 52 na Goba – Madale (km 5) yenye asilimia 5.

Profesa Mbarawa ametoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi naTANROADS mkoa wa Dar es salaam wakati mradi huo ukiendeleaa kutekelezwa ili kusaidia kumaliza kwa wakati.

Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kushughulikia suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi wa maeneo hayo ambao wamepitiwa na mradi huo. Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Julius Ndyamkama, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa watasimamia mradi huo usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyo bora.

Mhandisi Ndyamkama amebainisha changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo suala la ulipaji wa fidia kwa baadhi ya maeneo hasa katika kipande cha barabara chenye urefu wa kilometa 1 kuanzia Mto Mbezi kuelekea Makongo.

Naye, Mratibu wa Mradi wa barabara ya Goba – Madale (km 5), kutoka kampuni ya Ujenzi ya Mwananchi Engineering and Contracting Co. Ltd (MECCO), Mhandisi Crispin Mwombeki, amesema kuwa tayari wameshakamilisha usanifu wa mradi na wanategemea kuanza kazi za Ujenzi hivi karibuni.

Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya mradi wa Ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam umeanza mwezi Desemba, mwaka 2016 ambapo umehusisha barabara tatu za Kifuru – Msigani (km 4.5), Goba – Makongo (km 4.5), na Goba – Madale (km 5) na kugharimu Jumla ya Shilingi Bilioni 24.2.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio akikabidhi moja ya Vifaa vya maabara kwa mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa Mhandisi Magayane Machibya wakati wa mahafali ya tisa ya ka kidato cha nne Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Kulia) akimkabidhi cheti Joyce Msumari (Kushoto) mhitimu wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa iliyopo jijini Dar es Salaam.  Joyce Msumari ni mmoja wa wanufaika wa Fao la Elimu linalotolewa na PPF kwa watoto wa wananchama wanaofariki wakiwa katika Ajira.  
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa, Mhandisi Magayane Machibya (Kushoto) na Mkuu wa Shule hiyo Sista Irene Natumanya wakifurahia kupokea vifaa vya maabara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio (hayupo pichani) 
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa Sista Irene Natumanya (Kulia) akimpa mkono wa shukrani Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio (Katikati) baada ya kukabidhiwa vifaa vya maabara na Mfuko wa PPF mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Shule hiyo Mhandisi Machibya Magayane.
 Wahitimu wa Kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Canossa wakitumbuiza katika mahafali ya 9 yaliofanyika Shuleni hapo mwishoni mwa wiki.
Vifaa vya maabara vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati wa mahafali ya 9 ya shule ya Sekondari ya Wasichana Canossa mwishoni mwa wiki.

MFUKO wa Pensheni wa PPF umetoa msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 6.7 kwa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi vifaa hivyo katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne shuleni mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio amesema Mfuko umeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kutengeneza uchumi wa viwanda.

Bw.Erio ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, amebainisha kuwa Mfuko wa Pensheni wa PPF utaendelea kushirikiana na taasisi za elimu nchini katika jitihada za kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia Bw.Erio amesema ushirikiano mzuri uliopo kati ya shule ya Canossa na PPF pia ni moja ya sababu kupeleka vifaa hivyo shuleni hapo..

“Shule ya Canossa imekuwa miongoni mwa waajiri wanaowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati bila kuchelewesha,na idadi kubwa ya wafanyakazi wake ni wanachama wa Mfuko wetu,” amefafanua Mkurugenzi Mkuu.

Sanjari na hilo, Mkurugenzi huyo wa PPF amesema katika shule hiyo Mfuko umeshasomesha wanafunzi 6 ambao wamenufaika na fao la elimu baada ya wazazi wao ambao walikuwa wanachama wa PPF kufariki wakiwa katika ajira.

“Mfuko pia unabeba jukumu la mzazi, kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2017, tumesomesha wanafunzi 1403 nchi nzima na zaidi ya shilingi 1.4 bilioni zimetumika katika kugharamia masomo yao’’. 

Mmoja wa wahitimu ambaye pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaosomeshwa na Mfuko wa PPF, Joyce Msumari ameshukuru PPF kwa kumlipia masomo yake tangu mzazi wake alipofariki  akiwa darasa la tano, miaka 7 iliyopita.

“Naishukuru PPF kwa kunifikisha hapa,na wazazi wengine wanaweza kujifunza kupitia kwangu maana hakuna anayeijua kesho yake hivyo unapojiunga na Mfuko huu utakuwa na uhakika wa masomo kwa mwanao pale ambapo Mungu ataamua kukuchukua na kuwaacha watoto wako wakiwa wanahitaji,” alisema mwanafunzi huyo.

DIAMOND AGAWA VIFAA TIBA NA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA AMANA

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akimsalimia mtoto wa Mama Nadia Iddi ambaye amejifungua katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam ambapo msanii huyo alifika kuwatembelea watoto waliozaliwa hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa
 Meneja wa Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond), Said Fellaakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufika katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kutoa msaada wa Vifaa tiba.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa ameongozana na Mtangazaji wa kipindi cha leo Tena Dahuu kwenda kutoa msaada katika hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam
 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond), akisalimiana na Mmoja ya wamama aliyopo na mtoto wake katika wodi ya watoto ya Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa katika maeneo ya Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam
 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa na Mtangazaji wa kipindi cha leo tena cha Clouds Fm Dahuu wakati alipowasili katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 33 WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ya kumbukumbu na wadau wa maendeleo na wafadhili wakuu wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiongea machache wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Bw. Gulma Hafeez Muccadam akisoma risala yao mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mhe Kassim majaliwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita Baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia ngoma ya Kigogo wakati akiwasili kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea banda la benki ya NMB na mabanda mengine kabla ya kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UZINDUZI WA MAKUMBUSHO MPYA YA OLDUVAI - NGORONGORO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, wengine pichani  ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia). ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia) mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo mbali mbali kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale kutoka Makumbusho ya Taifa Dkt. Agness Gidna mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia historia kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale iliyopo kwenye Makumbusho ya Olduvai mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia uzinduzi wa tovuti na mtanzao wa bure wa Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kufungua kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MATAPELI WA ARDHI WILAYANI KINONDONI KUKIONA-DC HAPI.

STARTIMES WAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUZINDUA CHANELI MPYA KWA WATEJA WAKE

$
0
0



KATIKA kusherekea wiki ya huduma kwa wateja kampuni inayotoa huduma za ving'amuzi Tanzania Wamezindua chaneli mpya kwa wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es aSalaam leo, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Startimes, Carter Luoh amesema kuwa kampuni hiyo wameongeza chaneli mpya katika king'amuzi ambapo wanajisogeza karibu na wateja wake.

Pia amesema kuwa Startimes inafuraha kubwa kutoa huduma za kidijitali kwa mikoa 17 kwa kutoa huduma za ving'amuzi ambayo imewafikia wateja wa mikoa zaidi ya 17 hapa nchini kwa kuwafikia wateja kwa kufungua zaidi ya mawakala 300.

Kwaupande wake Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa katika wiki hii muhimu ya huduma kwa wateja wamezindua chaneli nyingine mpya kwenye king'amuzi cha startimes pamoja na pamoja na chaneli zitakazokuwa kimetafsiliwa kwa kiswahili pamoja na movi za kihindi.



















 Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya king'amuzi cha Satrtimes katika kusherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ikiwa ni kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Amesema kuwa sherehe hizi zinaambatana na uongezwaji wa chaneli mpya kama vile ST Bollywood Afrika, ST Bollywood na FOX life. katikati ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) na Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo.
 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Kampuni ya Startimes kuzindua chaneli mpya katika king'amuzi cha Startimes wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja na kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo na Kushoto ni Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi.
 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya kwenye king'amuzi cha Startimes katika wiki ya huduma kwa wateja.
 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akikata keki kwa pamoja na wateja wa king'amuzi cha Startimes kwaajili ya kusherekea wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akiwalisha keki wateja jijiji Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua chaneli mpya katika king'amuzi cha startimes katika wiki ya huduma kwa wateja.

 Meneja wa mitambo wa Startimes, Yusuph Baracha akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwatembeza katika chumba cha kurushia matangazo na vipindi mbalimbali vya king'amuzi cha startimes.
 Meneja wa mitambo wa Startimes, Yusuph Baracha akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwatembeza katika chumba cha kurushia matangazo na vipindi mbalimbali vya king'amuzi cha startimes.
  Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

PICHA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO ZATAKIWA KUTOLEWA TAARIFA ZIWEZE KUONDOLEWA -TCRA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Taasisi ya kutetea watoto ya C-SEMA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini wamefungua dirisha 'portal' kwa ajili ya picha zinazohusu matukio ya watoto,  zenye maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto,  kuondolewa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika ufunguzi wa dirisha, Meneja Huduma wa Simu ya Mtoto , Thelma Dhase amesema kuwa picha za matukio za ukatili wa watoto hazitakiwi kuendelea kusambaa katika mitandao.

Amesema kuwa mfumo huo umeanza nchini lakini mradi huo unafanywa duniani nchi 18, ambapo kwa Afrika Tanzania ni ya Nne kuwa na mpango huo katika kutoa taarifa za picha za unyanyasaji wa kingono katika mitandao.

Dhase amesema kuwa mradi huo utasaidia kuongeza usalama wa watutmiaji wa mitandao kuhakikisha watoto waliothirika na picha za unyanyasaji wa kingono hawapitii unyanyasaji zaidi katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande wa Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Semu Mwakyanjala amesema picha za watoto zinaonesha ukatili au udhalilishaji wa watoto, hazitakiwi kusambazwa katika mitandao ya kijamii na mtu akipata picha hizo anatakiwa kutoa taarifa ziweze kutolewa katika mitandao.

Mwakyanjala amesema picha zinazodhalilisha watoto hazitakiwi kutokana na picha hizo zitaawathiri kisaikolojia wakishakuwa watu wazima.

Mradi wa kutolea taarifa za unyanyasaji wa kingono kwa watoto unaendeshwa na Internet Watch Foundation ambao unatekelezwa nchi 18 duniani.

.Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA),  Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa watumiaji wa mitandao kutoa taarifa juu ya picha za unyanyasaji wa kingono kwa watoto iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa huduma wa simu ya mtoto wa C-SEMA, Thelma Dhase akizungumza juu utoaji wa taarifa zinazohusiana na picha za unyanyasaji wa kingono kwa watoto kuweza kuondolewa katika kulinda watoto wengine leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandushi wa wakiwa wadau katika ulinzi wa watoto katika kutoa taarifa za picha za unaynyasaji wa kingono kwa watoto leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Semu Mwakyanjala akiwa katika picha ya pamoja na Taasisi ya C-CEMA.
.

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
IMGL7358
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
IMGL7421
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mheshimiwa Abdullah Makame (katikati) ambae ni kiongozi wa msafara wa Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
IMGL7447
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. ujumbe huo uliongozwa na Mheshimiwa Abdullah Makame (wa tatu kulia) ambae ni kiongozi wa msafara huo.
PICHA NA OFISI YA BU

Britam Insurance waanza kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi kwa Kampuni ya Britam Insurance wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja, katika makao makuu, Jengo la PPF Tower, jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi kwa Kampuni ya Britam Insurance wakionekana wenye furaha tele katika wiki ya huduma kwa wateja na wanawakaribisha sana.

WAZIRI Mwakyembe Awataka Wasanii wa Nyimbo za Dini Kuliombea Taifa Kudumisha Amani

$
0
0


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea wa ujumbe wa Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo amewapongeza kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.
02
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kwaya wa Furahini Benjamini Ng’imba (wa pili kushoto) kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma.
03
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mlezi wa wa Kwaya wa Furahini Zakayo Munyawi (wa kwanza kushoto) kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma.
04
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo amewapongeza kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

CRDB TAWI LA QUALITY CENTER WAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na wateja wa benki hiyo tawi la Quality Center jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa  Wateja  Duniani. (Na Mpiga Picha Wetu).
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akizungumza na Wateja wa Benki hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi hilo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NN General Supplies, Selina Letara, akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei,wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi Quality Center.
  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, baada ya kukutana na wateja wa tawi la Quality Center.
 Meneja wa Wateja wa Mikopo Midogo na ya Kati wa Benki ya CRDB, Mussa Mwinyidaho, akitoa mada.
 Meneja Mahusiano Huduma za Biashara, Baraka Eusebio, akitoa mada kuhusu huduma za Biashara.
Ofisa wa Benki ya CRDB Anayehusika na Ubadilishaji Fedha na Masoko ya Mtaji, Olais Tira, akitoa mada kwa wateja wa Benki ya CRDB (hawapo pichani), wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Quality Center.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PMM Estates  (2001), Dk. Judith Mhina, akichangia mada katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na Benki ya CRDB tawi la Quality Center.
 Ofisa Mikopo wa Benki ya CRDB, Eric Mgonja, akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa wameshika keki maalumu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Quality Center Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kushoto), akimkabidhi tuzo maalumu, Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Master Mind Tobacco, Joseph Dominic, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyofanyika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PMM, Dk. Judith Mhina, akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kushoto), wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
 Keki.
Wateja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center wakikata keki wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi hilo Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NN General Supplies, Selina Letara.
 Wateja wakipata keki.
 Kufungua Champagne.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (katikati), akigonganisha glasi na wateja.
Kunywa kwa afya.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center wakiwa katika picha ya pamoja.
 Picha ya pamoja.
 Zawadi kwa wateja.
Baadhi ya  wateja wakiwa na zawadi zao.
 Picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Easy Connection, Justus Bashara, akiishukuru Benki ya CRDB kwa niaba ya wateja wenzake.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images