Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1385 | 1386 | (Page 1387) | 1388 | 1389 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Washindi wa michuano ya Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika  Octoba 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wanatarajiwa kuondoka na zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 40 pamoja na medali, imefahamika. 


  Akizungumzia zawadi hizo jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe  alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/-  kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi na tano nao pia wakiibuka na zawadi  za medali na pesa taslimu.


  Kwa upande wa mbio za  Kilomita 21, Bidan alisema pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  Mil 2/- kila mmoja, sh. Mil 1/-  kwa washindi wa pili na sh. Laki 5/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na  zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.


   “Mbio za kilomita tano tunatarajia kwamba zitaongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, baadhi ya wakuu wa mikoa kutoka kanda ya Ziwa huku pia zikihusisha wadhamini wa mbio hizi kutoka mashirika mbalimabli yaani(Corporates).’’ Alisema.


  Aidha wadhamini ambao pia watashiriki katika mbio hizo ni pamoja na kampuni za Tiper, Puma Energy, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, New Mwanza Hotel, Real PR Solutions, Efm Radio, EF Out Door, CF Hospital na Afrimax Strategic Partnerships Limited.  Alibainisha kuwa mbio hizo za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.


  Alisema washindi wa mbio za Kilomita tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee watapatiwa sh 100,000/- kwa washindi wa kwanza huku washindi wa pili wakipata sh 70,000/ na watatu  wakipatiwa sh 50,000/-pesa taslimu.


   “Kwa washindi wa mbio za kilomita mbili na nusu zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 watapatiwa sh 50,000/-kila mmoja huku wa pili na watatu pia wakipatiwa pesa taslimu.’’ Aliongeza


  Zaidi aliongeza kwamba washindi kwanza kwenye  mbio fupi za uwanjani  za mita 100,200,  400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi watapatiwa zawadi ya sh 50,000/ kila mmoja (wanaume na wanawake), sh 30,000 kwa washindi wa pili huku washindi watatu wakiambulia kiasi cha sh 20,000 kwa kila mmoja.


  Akizungumzia usajili wa mbio hizo Bw. Bidan alisema kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani wanaweza kujisajili kwa kuchukua fomu katika vituo kadhaa vikiwemo Ofisi za michezo wilaya zote za mkoa wa Mwanza, Ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga,   Uwanja wa Nyamagana,  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino  Mwanza, Kituo cha michezo  Malya, Shule ya Kimataifa ya Isamilo, New Mwanza  Hotel na Ofisi za EF Out door zilizopo jingo la Rock City Mall.


  “Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya sita jengo la SHAMO Tower, Mbezi Beach , jijini Dar es, Salaam na EFM Jogging Club iliyopo Coco Beach  Dar es Salaam” alitaja.


  Zaidi kuhusu usajili wa mbio hizo zinazoandaliwa kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Bidan alisema unaweza kufanyika kupitia tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni www.capitalplus.co.tz


  Alitoa wito kwa washiriki zaidi kujisajili ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo mbali na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha hapa nchini pia zinalenga  kupambana na ujangili pamoja na kutangaza utalii katika mikoa iliyopo Ziwa ya Ziwa.  0 0

  Na Ismail Ngayonga.

  SERIKALI ya Awamu ya Tano inaingia katika mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/17-2020/21 unaojikita katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda na hivyo kufikia nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

  Uamuzi wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda umelenga katika kuleta maendeleo jumuishi na endelevu kwa kutumia rasilimali zilizopo na hivyo kuchangia katika pato la taifa pamoja na kutoa nafasi nyingi na endelevu za ajira.

  Ili kufikia malengo hayo juhudi mbalimbali zimefanywa na Serikali na mojawapo ya juhudi hizo ni kuandaa  Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NMSFEE) unaotekelezwa na Wizara na Taasisi zake; Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Sekta Binafsi pamoja na Wadau wa Maendeleo.

  Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi unasimamiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ambalo ni chombo cha juu kitaifa cha kusimamia, kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa shughuli zilizoainishwa katika ya Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004.

  NMSFEE unatekelezwa kupitia Mwongozo ulioandaliwa ili kutoa maelekezo ya namna ya kutekeleza ikiwemo uratibu, usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sera katika ngazi na sekta zote za kiuchumi.

  Kupitia NMSFEE mfumo wa uratibu wa uwezeshaji umepangwa kwa kuwa na kamati kuanzia ngazi ya Taifa hadi kijiji/mtaa na kila kamati ikiwa na majukumu yake kwa mtiririko endelevu. 

  Mkakati wa NMSFEE imeanisha sekta mbalimbali ikiwemo mifuko ya uwezeshaji, skimu za umwagiliaji, miundombinu ya barabara, miundombinu ya masoko, huduma ya nishati vijijini, huduma za maendeleo ya biashara, hali ya biashara, urasimishaji wa ardhi, mafunzo ya ujasiriamali, na maendeleo ya vikundi vya kifedha vya kijamii. 

  Katika kusimamia utekelezaji wa Mkakati huo, mwezi Julai mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizindua Mwongozo wa utekelezaji wa NMSFEE katika kupanga, kutekeleza na kutathmini mipango na miradi mbalimbali ya uwezeshaji wananchi kiuchumi hapa nchini

  Taarifa ya Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) inasema kuwa hadi kufikia Aprili 2017, Baraza limeweza kuendesha mafunzo kwa waratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika halmashauri na  mikoa, maafisa mipango na Wakurugenzi wa Halmashauri.  

  Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo watendaji hao kufahamu wajibu na majukumu yao katika kusimamia na kuratibu utekelezaji wa mipango ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

  Aidha mafunzo hayo yaliyowahusisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya yaliweza pia  yalitoa elimu kukuhusu miongozo ya kuanzisha, kuandikisha na kuendesha vikundi vya kifedha vya kijamii pamoja na Mwongozo wa ukusanyaji na utoaji wa taarifa za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

  Pia, waratibu wa uwezeshaji katika wizara na taasisi za Serikali wamepatiwa mafunzo hayo ili kusimamia kwa karibu utekelezaji, kuratibu, kukusanya na kutoa taarifa za utekelezaji wa mipango na miradi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika maeneo yao.

  Ushiriki wa wananchi katika shughuli za uchumi wa kisasa ni duni, hivyo kupitia Mkakati wa NMSFEE ni wajibu wa sekta binafsi, Serikali na wadau wa maendeleo kutoa nafasi kwa makundi yote kujiendeleza kikamilifu ili kuwajengea mazingira mazuri ya ujenzi wa uchumi imara unaoweza kuhimili ushindani katika soko la dunia.  
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Beng’ Issa.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Abdallah Ngodu akitoa neno la utangulizi kwa wajumbe wa jumuiya hiyo (hawapo pichani) wakati wa jukwaa la mafunzo kwa wajumbe hao katika mkutano wa 33 wa jumuiya hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
   Mwanyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Gulamhafeez Mukadam akizungumza na wajumbe wa jumuiya hiyo (hawapo pichani) wakati akifungua jukwaa la mafunzo kwa wajumbe wa jumuiya hiyo katika mkutano wa 33 wa jumuiya hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
   Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mh. Isaya Mwita akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) wakati wa jukwaa la mafunzo kwa wajumbe hao katika mkutano mkutano wa 33 wa jumuiya hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) wakimsikiliza Mwanyekiti wa Jumuiya hiyo Gulamhafeez Mukadam (hayupo pichani) wakati akifungua jukwaa la mafunzo kwa wajumbe hao katika mkutano wa 33 wa jumuiya hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) wakimsikiliza Mwanyekiti wa Jumuiya hiyo Gulamhafeez Mukadam wakati akifungua jukwaa la mafunzo kwa wajumbe hao katika mkutano wa 33 wa jumuiya hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

  0 0

  Airtel leo wamezindua shamra shamra za wiki ya huduma kwa mteja kwa kuwakaribisha wateja wake wote waliongia madukani kwao kwa kukata keki na kuzindua kifurushi maalum cha sh 1000 cha  OFA KABAMBE kinachodumu kwa siku tatu ikiwa ni  ishara yakuwashukuru wateja wote nchini.

  Akiongea katika makao makuu ya Airtel Meneja wa Duka la Airtel Bi Celine Njunju alisema “tunawashukuru wateja na wananchi wote kwa ujumla katika wiki hii ya huduma kwa wateja inayoanza tarehe 2 hadi tarehe 6 mwezi Oktoba duniani kote, kwa upendo kabisa Airtel inakupa kifurushi cha OFA KABAMBE kupitia  Airtel Money kitakachokupa uhuru wa kujichagulia kile unachokipenda kutoka Airtel”.

  Ukijiunga na Ofa kabambe ya Airtel Money, kwa Tshs 1000 tu! utapata GB 2, Dakika 110 za kupiga mitandao yote na SMS bila ya kikomo, huku ukiwa na uhuru wa kutumia kifurushi hiki ndani ya siku tatu toka pale ulipo nunua. 
  Alieleza kuwa “ili kujiunga  Piga *150*60# chagua 6 kufurahia vifurushi vinavyokupa MB na Dakika kibao pamoja na SMS bila ya kikomo”

   “uhuru ni wako tumia utakavyo ndani ya siku tatu. alisisitiza Bi Celine
  kwa upande wake Mkurugenzi  wa kitengo huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba alieleza kuwa “ wiki hii huadhimisha kila wiki ya kwanza ya mwezi oktoba kila mwaka, lakini kwetu  Airtel kila siku tunazingatia swala muhimu la kutoa huduma kwa wateja wetu wote kwa viwango vinavyotakiwa “Mwaka huu Airtel tumeipa wiki hii kauli mbiu Building Trust tukimaanisha kuendelea kuwajengea wateja wote Imani katika huduma tunazotoa” alieleza Bi Lyamba .

  Bi Lyamba aliendelea kusema “wiki hii pia Airtel tutakuwa na matukio mengi maalumu kwa wateja wetu lakini muhimu zaidi tunawakaribisha wote mtembelee katika ofisi zetu za huduma kwa wateja ili muendelee kujipatia huduma bora kama vile kusajili laini mpya, kujipatia simu na vifaaa vya mawasiliano original kwa bei nafuu na vitakuwa na ofa kabambe maalum kwa ajili yako, pia utaelekezwa jinsi yakutumia huduma zetu kama Airtel Money, Airtel Yatosha, huduma ya kukopa kwa Airtel Money yaani Timiza na nyingine nyingi
  Meneja wa duka la Airtel Makao Makuu Bi Celine Njuju akiongea na wateja leo wakati Airtel ilipozindua wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuzindua kifurushi cha OFA kabambe kinachopatikana kupitia Airtel Money kwa shilingi 1000 tu na kudumu kwa siku 3. kifurushi hiki pia kinampatia mteja GB 2, dakika za maongezi 110 kwenda mitandao yote pamoja na sms bila kikomo uzinduzi wa wiki.
  Katikati ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba akikata keki kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja inayoazimishwa duniani kote kuanzia octoba 2 hadi oktoba 6 huku akiwa amezungukwa na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel pamoja na  wateja wa Airtel waliotembelea duka la Airtel Moroco kujipatia huduma.
   Mmoja kati ya wateja wa Airtel Bw, Kassim Nguya akimlisha keki Mkurugenzi wa huduma kwa mteja Bi Adriana Lyamba maalum kwa kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huanzimishwa kila mwaka mwezi oktoba tarehe 2 hadi 6. airtel pia imezindua kifurushi cha OFA kabambe ambapo kwa  shilingi 1000 mteja anapata  GB 2, dakika za maongezi 110 kwenda mitandao yote pamoja na sms bila kikomo.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel huduma kwa mteja  wakiwa tayari kuwakaribisha wateja na kuwahudumia.
   Baadhi ya wateja wa Airtel waliotembelea duka ya Airtel Makao makuu leo wakilishwa keki na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba leo ikiwa ni kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja inayoazimishwa duniani kote kuanzia octoba 2 hadi 6. Airtel mwaka huu wamesherehekea wiki hio wakiwa na kauli mbiu yao ya BUILDING TRUST yaani kuwajengea wateja Imani kwa kuwapatia huduma zenye viwango. 

  0 0

   Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar walioapishwa leo na Viongozi wengine kazi iliyofanya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw. Khamis Ramadhan Abdala kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Aziza Iddi Suwedi kuwa  Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw. Kubingwa Mashaka Simba  kuwa  Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha  Bw. George Joseph Kazi kuwa  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, kabla alikuwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
   Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar wakipitia hati zao za viapo kabla ya kuapishwa Rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kushika wadhifa walioteuliwa hafla ya kiapo ilifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
   Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar  leo, (kutoka kulia) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar  Sheikh Khamis Haji na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Maalim.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya kuwaapisha rasmi leo katika hafla iliyofanyika  ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar (Picha na Ikulu).

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia  tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017. 
   Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia  tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017. 
   Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia  tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017. 
   Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa NBS, Chuo cha Mipango na baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17.  Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia  tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017. 
  Mwanasheria waOfisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Oscar Mangula akiwaapisha wadadisi waUtafiti waTakwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia  tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.

  Na: Veronica Kazimoto
  Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inatarajia kufanya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016/17 nchi nzima kuanzia kesho tarehe 3 Oktoba hadi tarehe 3 Novemba, 2017. 

  Akizungumza leo wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi watakaokusanya Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo amesema lengo la utafiti huo ni kutoa makadirio ya kiasi cha uzalishaji wa mazao makuu, idadi ya mifugo, mazao yatokanayo na mifugo na maeneo ya kilimo katika mikoa yote ya Tanzania.

  "Ningependa kuwasisitizia washiriki kuwa, dhumuni kubwa la utafiti huu wa  kilimo ni kutoa makadirio ya uzalishaji wa mazao makuu ya kilimo na maeneo yake yaliyolimwa pamoja na taarifa za mifugo katika mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", amesema Dkt. Mashingo.

  Aidha, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wakuu wote wa kaya watakaochaguliwa kushiriki kwenye utafiti huu, kutoa ushirikiano wa kutosha na hususan kutoa taarifa sahihi kuhusu hali ya uzalishaji wa mazao, huduma zinazotolewa na Maafisa Ugani na aina ya mbegu wanazotumia na kubainisha changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema jumla ya wadadisi 600 wamepatiwa mafunzo ya siku 5 kwa ajili ya kufanya utafiti huo nchi nzima.

  Dkt. Chuwa amefafanua kuwa madhumuni ya mafunzo kwa wadadisi hao ni kuwajengea uwezo wa kuhoji na kujaza madodoso ya wamiliki wa mashamba (wakulima) na namna ya kutambua mahali shamba lilipo kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho GPS.

  Utafiti huu wa Kilimo wa mwaka 2016/17 unafanyika chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar (OCGS) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. 


  0 0


  Mbunge wa Ilala Mussa Zungu (kushoto)  NA BASHIR NKOROMO.

  MBUNGE wa Ilala, Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu, amesema ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Barabara ya Olympio, katika kata Upanga Mashariki, huku akilalamikia ujenzi wa Barabara ya Mtaa wa Mfaume ambayo ujenzi wake umekwama. 

  Zungu amesema hayo leo alipokagua maendeleo ya ujuenzi wa barabara hizo ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami chini ya usimamizi na gharama za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

  "Kama mnavyoiona, barabara hii ya Olympio inayojengwa na kampuni ya kigeni ya China Railway Seventh Group (CRSG), imejengwa kwa kiwango kizuri kabisa, lakini hii ya Mtaa wa Mfaume yenye urefu wa mita 900, ambayo mkandarasi wake ni kampuni ya CASCO abayo ni ya mzawa mwenzetu 

  imekwama kumalizika, Sasa tunamtafuta Mwenyekiti wa Halmashauri tujue nini hasa kimesababisha ujenzi wa barabara huu kukwama", amesema Zungu.

  Amesema, wakati barabara ya Olympio yenye urefu wa mita 740  ujenzi wake umekamilika kwa kiwango kikubwa tangu Septemba 30, mwaka huu, ujenzi wa barabara ya  Mfaume umekwama hadi sasa kutokana na Mkandarasi kusimamishwa kuendelea kutokana na kuonekana anaijenga kwa viwango vya chini.

  Wakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG Zhou Cunfei, alisema licha ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 95, kampuni hiyo inamalizia sehemu chache zilizobaki na inainatarajia kuikabidhi rasmi Januari 2, mwakani.
   Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumza alipokagua ujenzi wa Barabara ya Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kulia ni Wakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou CunfeiWakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG ya China Zhou Cunfei akizungumzia wakati Zungu alipokagua ujenzi wa Barabara hiyo, leo. 
    Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akikagua ujenzi wa Barabara ya Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Wakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou Cunfei
    Mwenyekiti wa CCM Kata ya Upanga Mashariki, akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo ya Olympio
   Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akihitimisha kwa kuzungumza na ujumbe wake baada ya kukagua ujenzi wa Barabara ya Olympio na ya Mtaa wa Mfaume, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

  0 0

  SHIRIKA la ndege la Precision Air (PW) jana lilizindua safari zake za Serengeti mkoani Mara, kupitia Uwanja wa Ndege wa Arusha.

  Uwepo wa safari hizo za ndege utasaidia usafirishaji wa watalii kutoka nchi mbalimbali duniani na ndani ya Tanzania kutembelea hifadhi ya Serengeti kirahisi jambo ambalo litachangia ukuaji wa uchumi nchini.

  Pichani juu ni Wafanyakazi wa Ndege ya PrecisionAir na abiria  wakishuka katika Ndege kwenye Uwanja wa Seronera jana walipozindua safari za Viwanja vya  Dar es Salaam-Arusha - Serengeti.
    Wafanyakazi wa Ndege ya PrecisionAir wakishuka katika Ndege kwenye Uwanja wa Seronera jana.
   Wafanyakazi wa Ndege ya PrecisionAir wakivinjari katika Uwanja wa Seronera jana.
   Wafanyakazi wa Ndege ya Precision Air wakiwa katika Uwanja wa Seronera.
   Wafanyakazi wa Ndege ya PrecisionAir wakiwa katika picha ya pamoja katika uwanja wa Seronera.
   Wafanyakazi wa Ndege ya PrecisionAir wakiwa katika picha ya pamoja katika uwanja wa Seronera.
   Ndege ya PrecisionAir ikiwa katika Ofisi za Uwanja wa ndege wa Seronera. 

  0 0

  Chaneli ya Sinema Zetu inayopatikana katika Televisheni ya Azam, leo imetangaza rasmi uzinduzi wa Tamasha lake lakutoa Tuzo na mchango wa tasnia ya Bongo Movies maarufu 'Sinema Zetu International Film Festival' litakalofanyika kuanzia January Mosi, 2018 hadi February 28, 2018.

  Katika Tamasha hilo pia kutakuwa na Shindano litalokusanya Filamu zaidi ya 150 kutoka Mikoa mbalimbali kama Morogoro, Mwanza, Dodoma ambapo jumla ya Mikoa nane.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kiongozi Mkuu wa Tamasha hilo, Jacob Joseph amesema kuwa watazunguka Mikoa Sita kwa ajili ya kuzungumza na Wadau wa tasnia hiyo ikiwa sambamba na kutoa elimu yakutosha na kuweka uelewa juu ya Tamasha hilo.

  Mshauri wa Tamasha hilo, Prof. Martin Mhando amesema kuwa Shindano hilo la Filamu katika Televisheni litakuwa na vipengele vitatu ambapo litahusisha Bongo Movies 'Filamu Kubwa', Filamu Fupi za dakika 45, pia Makala za Filamu nazo zitahusika.

  Balozi wa Tamasha hilo, Elizabeth Michael 'Lulu' ameshukuru kupewa ubalozi katika Tamasha hilo ikizingatiwa kwamba yeye ni Msanii atakayebeba Nembo ya Taifa la Tanzania katika nchi jirani zitakazoshiriki Tamasha hilo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.
   Mshauri wa Tamasha hilo, Prof. Martin Mhando akifafanua jambo kwa Wanahabari kuhisiana na Tamasha hilo linavyoleta mapinduzi katika Lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.
   Balozi wa Tamasha hilo la SZIFF, Elizabeth Michael maarufu kama LULU akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Tamasha hilo la Kimataifa la Sinema Zetu na jinsi atakavyoshiriki kama Msanii wa Bongo Movie.
   Kiongozi Mkuu wa Tamasha la Filamu Kimataifa, Jacob Joseph akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar katika uzinduzi wa Tamasha hilo litakaloanza kufanyika January Mosi hadi February 28, 2018.


  0 0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

  Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

  “Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”

  Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.

  Aliwataja washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu, (MCB).

  Alisema, PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.Miongoni mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na maafisa wa PSPF.

  “Kwa kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema.
  Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
  Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
  Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa na Bi.Elizabeth Shayo, (kulia), makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
  Elizabeth Shayo, (katikati), Afisa Huduma kwa wateja wa PSPF, akitoa maelezo kwa Mwanachama aliyefika kupatiwa huduma.
  Afisa wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. January Iman Buretta, (kushoto), akizungumza na wanachama wa Mfuko huo waliofika makao makuu kupatiwa huduma Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza jana, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
  Ntimi Mwakajila, Afisa wa Huduma kwa njia ya simu, (Call Centre), Mfuko wa PSPF, akiwa kazini
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Fatma
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, (mbele), Meneja Masoko, Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Fatma Elhady, (wapili kulia), na maafisa wa kitengo cha huduma kwa njia ya simu wakiwahudumia wateja wa Mfuko kwenye kituo hicho.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, akizungumza na mmoja wa wateja waliofika kupatiwa huduma
  Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kulia), akipokea nyaraka kutoka kwa Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi.
  Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laima Maghimbi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani  Singida.
  Picha Na 2
  Wataalam kutoka ,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani).
  Picha Na 3
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi  uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani)
  Picha Na 4
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.
  Picha Na 5
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
  Picha Na 6
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande akifafanua jambo katika kikao hicho.
  Picha Na 7
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, Salum Mnuna katika kikao hicho
  …………………

  Asteria Muhozya na Greyson Mwase.
  Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani  Singida.

  Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017  wamefanya  kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

  Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema  maandalizi hayo ni  juhudi za Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa  Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta  Ghafi la  Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na  Eyasi nchini Tanzania.

  Dkt. Kalemani amesema baada ya Rais wa Uganda kukubali ombi hilo yalianza maandalizi kupitia vikao mbalimbali ambapo hatua iliyofikiwa kwa sasa ni wataalam kukutana na kubadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti katika maziwa husika.

  Amesema wataalam wataanza kwa kufanya ziara ya siku mbili katika Ziwa Eyasi Wembere mkoani Singida ili kupata picha halisi kabla ya kuanza kwa majadiliano ya kubadilishana mawazo ya namna bora ya utafiti katika maziwa husika.

  “ Sisi kama  Tanzania  tupo  tayari kubadilishana uzoefu na wataalam wa Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja;  hata hivyo pia tupo  tayari kubadilishana nao uzoefu  kwenye masuala ya  gesi kwa kuwa tuna utaalam huo, lengo likiwa ni kuimarisha sekta hizi za mafuta na gesi kwa nchi zote mbili,” amesema  Dkt. Kalemani.

  Ameongeza kuwa kwa kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia, wapo tayari kutuma wataalam nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti wa gesi nchini Uganda.

  Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda na kiongozi  wa ujumbe huo, Robert Kasande amesema kuwa wapo tayari kubalishana uzoefu ambapo watalenga katika kuangalia tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka mikakati ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na  Tanzania.

  0 0


  Wasanii Ben Pol na Jux wakiimba pamoja wimbo wao walioshirikiana ‘Nakuchana’ kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma usiku wa kuamkia jumatatu.
  Aslay akiburudisha wakazi wa Kigoma
  Msanii Chege na Nandy wakiimba pamoja wimbo wao walioshirikiana ‘kelele za chura’kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma usiku wa kuamkia jumatatu.
  Darasa akiburudisha wakazi wa Kigoma
  Wasanii Stamina na Maua sama wakiimba kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
  Mr blue akipagawisha umati wa wakazi wa kigoma

  Msanii wa Bongo flea Ommy Dimpoz akiimba kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
  Roma Mkatoliki akiimba kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
  Roma mkatoliki akiburudisha umati wa wanakigoma waliojitokeza katika viwanja vya Lake Tanganyika.
  Young D akiimba kwa hisia katika jukwaa la Tigo fiesta

  0 0


  Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula akihutubia katika hafla ya maadhimisho ya 32 ya makazi duniani kutoka kulia ni mkurugenzi wa nyumba Bw.Pius Tesha na wa pili kulia ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala maadhimisho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
  PICHA 1
  Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba kulia akitoa salam kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula wa kushoto  katika maadhimisho ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala.
  PICHA 2
  mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala kushoto akitoa maelezo kwa wadau wa nyumba na makazi katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula na wa pili kushoto ni Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba.

  PICHA 4
  Mkurugenzi msaidizi wa urasimishaji makazi Bi.Beritha Mlonda akiwasilisha makala ya urasimishaji makazi katika maeneo yaliyoko kwenye mkakati wa mpango wa makazi bora kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam hivi leo.
  PICHA 5
  Wadau wa nyumba na makazi wakifuatilia mkutano wa maadhimisho ya 32 ya makazi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo ambapo kauli mbiu ya mwaka  huu ni “sera za nyumba ,nyumba za gharama nafuu”.
  PICHA 6
  Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula, kulia ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala na kushoto ni Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa nyumba na makazi wa bodi ya mwenge Jijini Dar es Salaam katika madhimisho ya 32 ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo.(picha na paschal dotto- MAELEZO).
  ………………
  Na.Paschal Dotto-MAELEZO  .

  Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka wananchi kuzingatia Sheria wakati wa ujenzi wa makazi yao ili kuepuka kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa jambo linalosababisha bomoa bomoa isiyo ya lazima.

  Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Angelina Mabula aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi duniani ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Karimjee.

  Mhe.Mabula alisema kuwa ni vyema wananchi wazingatie sheria kabla hawajaanza kujenga makazi yao husika kwa kutoa taarifa kwenye ofisi husika ili kuepuka ukiukwaji wa Sheria za nchi katika ujenzi wa makazi.
  “Watanzania tunakumbushwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi kwa sababu ubomoaji unaofanyika siyo kwa makusudi bali ni kwasababu tu watu wamekiuka Sheria zilizopo na pengine watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali ambao wanawapa watu maeneo pasiporuhusiwa”, alisisitiza Mhe. Mabula

  Akizungumuzia mpango mkakati wa Wizara hiyo Mhe. Mabula alisema kuwa zaidi ya Miji 26 nchini ikiwemo Mtwara, Singida Mwanza na Dar es Salaam iko kwenye mchakato wa kupangilia makazi yake na kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya msongamano wa makazi.

  Aidha Mhe. Mabula alisema kuwa katika maadhimisho hayo ya 32 yenye kauli mbiu isemayo ‘Sera za Nyumba :Nyumba za Gharama Nafuu’ ambayo inalenga zaidi kuimarisha sera za nyumba na makazi kwa kufuata sheria na taratibu kwa ujenzi wa makazi ya jamii             yenye ubora zaidi.

  Mhe.Mabula aliongeza kuwa kwa Sera hii ina madhumuni makubwa katika kuhakikisha nyumba na makazi bora yenye huduma za msingi kwa jamii toshelezi ,kuwa na mazingira salama ya kuishi kwa wananchi wote hususani wenye mahitaji maalum wakiwemo watoto, vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu pamoja na upatikanaji wa usafiri na nishati endelevu zenye gharama nafuu ,ili kuwezesha yote haya ni lazima kujua Sheria inasemaje katika kupangilia miji iliyosalama kwa manufaa ya wote.

  Alibainisha kuwa huduma nyingine ambazo zinapatikana kwenye makazi yaliyo katika mpangilio mzuri ni upatikanaji wa maji safi na salama na mfumo mzuri wa uondoshaji maji taka kwa ajili ya afya ya binadamu pamoja na uwepo wa hewa safi na ya kutosha.

  “Ukienda kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kujengwa lazima wakati ukifika kwa wenyewe kulitumia watakuondoa tu kwa sababu si eneo sahihi la makazi kwa hiyo mimi niseme ili kuepuka hii bomoabomoa tusijenge bila kuwa na kibali maalumu kutoka kwenye taasisi inayohusika ili kuweza kukidhi matakwa ya sheria na taratibu za makazi salama”,alisema Mhe. Mabula.

  Chimbuko rasmi la maadhimosho ya siku ya makazi duniani lilitokana na Azamio namba 40/202 la baraza kuu la umoja wa mataifa lililopitishwa Desemba,1985 na kuanza rasmi mwaka 1986.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mabinti wa Kimasai waliojitokeza wakati wa mapokezi kwenye lango la kuingia kwenye hifadhi ya Ngorongoro ambapo anategemewa kuzindua Makumbusho Mpya ya Olduvai kesho tarehe 3, Oktoba 2017. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoka kwa Msaidizi Mkuu wa Lango Bw. Mansuet Valentine mara baada ya kuwasili kwenye hifadhi ya Ngorongoro ,Makamu wa Rais anategemewa kuzindua Makumbusho Mpya ya Olduvai kesho tarehe 3, Oktoba 2017. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  0 0

  •   Itashutiwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Cape Town na Acapulco, Mexico

  Ø  Mastaa wakubwa duniani kama Eric Dane wa Lastship ,Gerard Depardieu wa Life of Pie,  Thomas Kretschmann wa Avengers Pearl Thusi  wa  Quantico…kushiriki


  NYOTA ya aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Mtanzania Idris Sultan, inaendelea kung’ara  baada ya ‘kupata shavu’ la kushiriki filamu yenye bajeti ya dola za Kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 38.


  Idris pamoja na Mtanzania mwingine Ernest Napoleon, wataungana na mastaa wakubwa  duniani kama Eric Dame, mwigizaji Mmarekani, Gerard Depardieu wa Ufaransa, Thomas Kretschmann wa Ujerumani na wengine wengi kucheza filamu hiyo ya ujambazi wa kimataifa.


  Filamu hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘The Blue Mauritius’, inahusu majambazi watano wa kimataifa ambao wanasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya kuiba vitu mbali mbali vyenye thamani kubwa duniani.


  Idris na mwenzake Ernest Napoleon, watasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika kusini mapema mwakani kwa ajili ya filamu hii  kubwa kuwahi kuwahusisha Watanzania.
  “D Street inayo furaha kubwa kugeukia vipaji vya waigizaji wa Kiafrika kwa kuwaunganisha na waigizaji wa kimataifa kama itakavyokuwa kwa ‘The Blue Mauritius’,” anasema Dexter Davis, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya D Street Media Group ya Marekani, inayoanda filamu hiyo


  Kwa mujibu wa Davis, filamu hiyo itasambazwa siyo tu Marekani, bali pia katika majumba makubwa ya sinema dunia nzima.


  “Ernest na Idris watang’ara, tunasubiri kwa hamu kuwaona tena kwenye skrini kubwa wakifanya makubwa,” anasema Davis

  Mapema mwaka huu, wawili hao walicheza filamu iliyojulikana kama ‘Kiumeni’ ambayo pia Ernest alikuwa ni mzalishaji na kushirikiana na Daniel Manege kuiandika. Filamu hiyo ilishinda katika Tamasha la Timataifa la Filamu la Zanzibar ambalo Idris na washiriki wenzake walihudhuria

   “Ninayo furaha kubwa kufanya kazi na Idris katika filamu kubwa kama hii ya The Blue Mauritius. Ni mwaka wa pekee kwa mimi kufanikiwa kufanya kazi na D Street. D Street inabadilisha upepo kwa Afrika inapokuja kwenye suala la kutengeneza filamu,” anasema Ernest

  Kwa upande wake Idris anasema, “Nilikutana Dexter Davis kwenye Maonyesho ya Filamu ya Kimataifa ya Zanzibar mwezi Julai na nilifurahishwa na namna ambavyo amevutiwa na vipaji kutoka Afrika. Alivutiwa kufanya kazi na mimi baada ya kuona ushiriki wangu katika filamu ya ‘Ballin; On the Other side of the World’ na miezi miwili baadaye nilishiriki Katina filamu moja ya Kimarekani. Filamu hizi mbili zimenifanya niweze kufanya kazi nchini Marekani jambo ambalo nilitamani sana,”

  Filamu hiyo inatarajia kuanza kuzalishwa mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka ujao (2018).

  0 0

  Na.Vero Ignatus ,Mlandizi

  Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumtha mshana amewaasa wanawake kutokudharau kazi hata kama ni ndogo kwani kwenye hiyo ndogo ndipo nyingine kubwa itafuata.

  Ameyasema hayo Katika Kanisa la RGC lililopo Mlandizi ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la wanawake lililoambatana na Changizo kwa ajili ya kununua eneo la kiwanja cha kujenga kanisa

  Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mchungaji alipata nafasi ya kuhubiri katika kongamano hilo, ambapo amewataka wanawake kujiamini na kuaajibika kwani hata neno la Mungu linasema asiyefanya kazi na asili.

  "Nyumba ambayo mwanamke ni legelege nyumba hiyo haitaendelea kamwe,wanawake changamkeni wajibikeni nyie ndiyo nguzo ya familia hutamchosha mume wako" alisema

  Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi Kambi ya Waebrania Mlandizi Mercy Adam Mwakimomyile amesema kuwa Kongamano hilo limebeba kaulibiu isemayo Nguvu ndani ya Mwanamke(Power in Woman)ambapo imewafanya wanawake wajisikie wanaweza

  "Kutokana na uwezo uliopo ndani ya mwanamke basi leo tumeamua kuwa tunaweza kumjengea Mungu madhabahu kupitia kongamano hili" alisema

  Amesema katika kanisa hilo wato watoto zaidi ya elfu moja ambao wanafundishwa maadili kupitia neno la Mungu kuibua vipawa  mbalimbali vilivyopo ndani yao na kuviibua
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumta Mshama .Picha na Vero Ignatus Blog.
  Mkuu wa wilaya akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kanisa la GRC kambi ya Waebrania Mlandizi àliyepo kulia kwake ni mchungaji kiongozi wa kanisa hilo la Mlandizi.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumtha Mshama akiwa anaonyeshwa mipaka ya eneo la kiwanja cha Kanisa la GRC Kambi ya Warbrania Mlandizi aliyepo nae ni Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo  Mercy Adam Mwakimomyile.Picha na Vero Igbatus Blog.
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe.Assumta Mshama akiwa anaongoza maombi mara baada kuona eneo ambalo linatarajiwa kujengwa kanisa .Picha na Vero Ignatus Blog.Kuna Mama Mtume Deo Rwetaka 

  Mhe.Assumtha Mshama akihubiri neno la Mungu katika kanisa hilo la GRC lililopo Mlandizi.Picha na Vero Ignatus Blog
   Wa kwanza kulia ni Mchungaji Kiongozi wa RGC Kambi ya Waebrania Mercy Adam Mwakimomyile Mama Mtume Deo Rwetaka wa Kwanza kushoto,Mama Askofu Amon Lukama wa RGC Tanzania na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumtha mshana
  Baadhi ya waumini walioshiriki katika ibada hiyo ya Kongamano la Wanawake RGC Mlandizi.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Baadhi ya watoto wanaolelewa kanisani hapo wakiimba wimbo maalumu wa kuliombea Taifa la Tanzania pamoja na Rais wa nchi.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Ibada ya ikiendelra katika kanisa hilo la GRC Kibaha Mlandizi .Picha na Vero Ignatus Blog.

  0 0


  0 0

  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

  MFUKO wa Pensheni wa PSPF,  umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

  Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza leo Oktoba 2, 2017.

  “Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka,  huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”

  Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”
  Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,
  hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.
  Aliwataja washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu, (MCB).

  Alisema, PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.

  Miongoni mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na maafisa wa PSPF.

  “Kwa kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema Dkt. Msengi.

  0 0

  Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) akisaidiana na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti kutoa huduma kwa Happiness Muthali wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana.
  1. Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti wakifurahi jambo na mteja wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana
  Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) akitoa huduma kwa Happiness Muthali wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yamefanyika jana katika duka la Tigo Mlimani City jijini Dar.
   Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Chisel  akijadiliana jambo na Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti (katikati mapema jana katika duka la Mlimani city.
  wateja wakiendelea kupata huduma.


older | 1 | .... | 1385 | 1386 | (Page 1387) | 1388 | 1389 | .... | 1897 | newer