Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 4,2017


ARUMERU WASHIRIKI KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA STAILI YA AINA YAKE

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami akikagua fomu ya Bwana Kitomari baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya usajili Vitambulisho vya Taifa kabla ya kwenda kwenye hatua ya upigaji picha. Hapa ni Kata ya Makiba kituo cha CCM Arumeru Arusha ambako zoezi hilo linafanyika.


Hawa ni Watendaji katika vitongoji viwili vya Kijiji cha Valeska wakiendelea na zoezi la kuwahakiki wananchi wao na kuwathibitisha kuwa ni wakazi halali wa eneo lao kabla ya kuwaidhinisha kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea Wilayani Arumeru.
Huu ni muonekano wa nje ya jengo ambako usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaendelea Kata yaMakiba kijiji cha Valeska. Baadhi ya wananchi wakiwa wanabadilishana mawazo huku wakisubiri kupatiwa huduma.


Afisa Usajili Wilaya ya Arumeru ndugu Edward Bujune akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu umuhimu na faida za Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi la kuwasajili wananchi wa Wilaya ya Arumeru likiendelea.
Meneja Mifumo ya Komputa ndugu Mohamed Mashaka akirekebisha moja ya Kamera ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa zoezi la Usajili Wilayani Arumeru.
Meneja Uthibiti na Usambazaji ndugu George Mwandezi aliyeshika Kitambulisho akitoa elimu kwa wananchi kuhusu ubora wa Vitambulisho vya Taifa wakati wakiendelea na zoezi la Usajili Kata ya Makiba wakati viongozi hao walipofanya ziara kukagua maendeleo ya zoezi linaloendelea sasa katika Kata hiyo.
Mtendaji katika Kijiji cha Valeska Kata ya Makiba akihakiki fomu za wananchi kabla ya kuingia kwenye chumba cha uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki. Fomu hizo zimekuwa zikusanywa na kupitiwa iwapo zimekamilika kujazwa vipengele vyote 72 vinavyohitajika
Hawa ni baadhi tu ya wananchi katika kijiji cha Valeska wakiwa kwenye foleni ya picha na uchukuaji alama za kibaiolojia wakati zoezi la Usajili likiendelea kijini hapo.

……………………………………………………………………….

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wananchi katika Wilaya ya Arumeru Kata ya Makiba kijiji cha Valeska mkoani Arusha; wameonyesha kuelewa umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa kiasi cha kujiwekea mkakati wa kuhakikisha nishati ya umeme muda wote inakuwepo ili zoezi la Usajili linaloendelea kutosimama.

Pengine hii ni tofauti na mazoea ya siku zote katika uendeshaji wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa maeneo ambayo zoezi kama hilo limewahi kufanyika kiasi cha kuamsha morali zaidi kwa watumishi kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi kushiriki zoezi hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kata hiyo; mtendaji wa Kata hiyo amesema wao kama Kata wamehamasisha wananchi kujitokeza kusajiliwa na kutokana na ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wananchi wana imani Kata yao watakamilisha zoezi la Usajili ndani ya muda uliopangwa.

“Kama unavyoona hapa wananchi ndo wamekwenda wenyewe kutafuta genereta baada ya umeme kukatika na hawajashurutishwa na mtu… wamekusanyana na ghafla tunashtukia wanafunga genereta wakati tukiwa bado tunatafakari namna ya kufanya na wapi pa kupata huduma hiyo. Hii kwangu siyo kawaida kuona wananchi wakijituma hivi kwenye zoezi la kitaifa. Wananchi wana mwamko na shauku kubwa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa” alisema

Zoezi la kuwasajili wananchi katika Mkoa wa Arusha limeanza kwa kasi kubwa na katika Wilaya ya Arumeru zoezi hilo linaendelea katika Kata za Makiba, Maroroni na Kikwe. Usajili huu unahusisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea na unafanyikia kwenye vituo vya Usajili vilivyoanishwa na NIDA kwa kushirikiana na Uongozi wa Wilaya ya Arumeru.

Bonde la Eyasi Wembere laonyesha dalili ya uwepo wa Mafuta

$
0
0
Sehemu ya Bonde la Manonga mkoani Tabora ambalo miamba yake inaonesha uwezekano wa kuwa na viashiria vya Mafuta kutokana na sifa zake za Kijiolojia na Kijiofizikia. 
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika miamba inayoonekana katika kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga ikiwa ni ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika. 
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika Bonde la Manonga lililopo katika kijiji cha Kining’inila mkoani Tabora ambapo pia walichukua sampuli za miamba katika Bonde hilo ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika eneo la Sekenke mkoani Singida ambapo miamba ya Bonde la Wembere inaonekana ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere. Wa Tano kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini (Uganda), Robert Kasande, wa Pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo na wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga.


Na Teresia Mhagama, Tabora

Imeelezwa kuwa miamba iliyo katika Bonde la Eyasi Wembere hususan mabonde madogo (sub basin) ya Wembere na Manonga yaliyopo katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Singida na Simiyu inawezekana kuwa na mafuta kutokana na sifa zake za Kijiolojia na Kijiofizikia.

Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini (Uganda), Robert Kasande na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo katika Mkutano na Wananchi uliofanyika katika kijiji cha Mwashiku wilayani Igunga mkoani Tabora. Mkutano huo uliandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry.

Viongozi hao walitoa kauli hiyo baada ya timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania kufanya ziara katika Bonde hilo hususan mabonde madogo ya Wembere na Manonga na kutembelea miamba inayoonekana katika maeneo ya Sekenke mkoani Singida, na vijiji vya Mwanzugi na Kining'inila mkoani Tabora.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda alieleza kuwa baada ya kuona dalili hizo Timu hiyo itatoa mapendekezo mbalimbali kwa Wataalam wa Tanzania ili kuweza kufikia lengo la Serikali la kuchimba Mafuta katika Bonde la Eyasi na Ziwa Tanganyika .

Alisema kuwa endapo Mafuta yatapatikana katika Bonde hilo yataweza kusafirishwa katika Bomba la Mafuta linalotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na kuweza kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kugundua mafuta katika Bonde hilo kwani nchini nyingine ambazo Bonde hilo linapita kama Kenya na Uganda tayari wamegundua Mafuta.

Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo alisema kuwa kupatikana kwa mafuta katika eneo hilo kutaimarisha hali ya uchumi nchini na kuwaasa wananchi kujiandaa na fursa za kiuchumi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali wakati wataalam wakiwa wanafanya shughuli mbalimbali za kitafiti katika eneo husika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry aliwataka wananchi wanaozunguka Bonde hilo na Viongozi wa Serikali katika Mkoa huo kutoa ushirikiano kwa wataalam watakaofanya kazi za kitafiti ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa ufanisi.

Naye, Mjiofizikia kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli, (TPDC), Sindi Maduhu alisema kuwa bonde hilo la Eyasi Wembere lina ukubwa wa Kilomita za mraba 19,197 likiwa na takwimu za awali za kijiofizikia (Airborne gravity gradiometry) zilizokusanywa na kutafsiriwa mwaka 2015/2016.

WATANZANIA WAISHIO BOTSWANA WASIFU JUHUDI ZA RAIS DKT.MAGUFULI

$
0
0
Watanzania waishio nchini Botswana wamesifu juhudi zinazochukuliwa na Rais Magufuli za kupambana na mafisadi, wizi wa mali za umma, wafanyakazi hewa, mikataba mibovu na uporaji wa mali za nchi hasa madini. Hayo yalisemwa kwenye mkutano mkuu wa 24 wa chama cha watanzania waishio nchini Botswana uliofanyika mjini Gaborone kwenye kumbi za mikutano za Maharaja jumamosi iliyopita. 

Mgeni rasmi kwenye mkutano huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ambaye pia anaiwakilisha Botswana, Balozi Silvester Ambokile. Wageni wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wawaikilishi kutoka NSSF, CRDB, NHC (T) LTD na Solomon Stocker Brokers.

Akimkaribisha Mh. Balozi Ambokile ili afungue rasmi mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Watanzania Botswana, Bw. Nieman Kissasi, alisema kuwa Watanzania waishio nje kwa ujumla wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano za kuinua uchumi wan chi na kuleta nidhamu mahali pa kazi.

 Aidha Bw. Kissasi aliendelea kusema kuwa maendeleo yaliyoko kwenye nchi za kusini mwa Afrika yanaletwa na tabia ya viongozi na wananchi wa nchi hizo kuwa na nidhamu ya kutumia kwa uaminifu kile kidogo wanachokipata. Bw. Kissasi alisisitiza umuhimu wa Watanzania kutoa ushirikiano kwa serikali ili maendeleo ya kweli yaweze kupatikana kwa haraka.

Kwa upande wake Mh. Balozi aliwahakikishia watanzania wa Botswana kuwa serikali ya awamu ya tano itatumia uwezo wake wote ili kuwaletea watanzania maendeleo. Aidha aliwasihi watanzania waishio nje kufuata sheria na taratibu za nchi wanazoishi. Pia aliwasihi kuwekeza nyumbani na kudumisha utamaduni wa kitanzania hasa kueneza lugha ya Kiswahili.

 Mh. Balozi pia alikuwa na mkutano na watanzania wote siku iliyofuata. Mkutano huu ulifanyika kwenye hoteli ya Crystal Palace na ulifuatiwa na maonyesho ya huduma zitolewazo na mashirika ya NSSF, NHC, CRDB na Solomon Stock Brockers. 

Mh. Balozi alifunga mikutano hii kwa kuwapongeza watanzania waishio Botswana kwa kuwa na umoja miongoni nao na kuwasihi wale ambao hawajajiunga na umoja huo kufanya hivyo kwani ni umoja imara na uthabiti unaostahili kuigwa na watanzania waishio nchi zingine.
 PICHANI: Mh. Balozi akiongea na watanzania kwenye Hoteli ya Crystal Palace. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Watanzania Botswana, Bw. Nieman Kissasi.
 Meneja wa huduma za Diaspora wa CRDB, Bi Lucy Naivasha, akielezea huduma zitolewazo  kwa watanzania waishio nje nchi.
 Meneja wa NHC (T) LTD, Bi Sophia Mwema, akielezea huduma zitolewazo na NHC baada ya mkutano mkuu kwenye kumbi za mikutano za Maharaja mjini Gaborone
Mh. Balozi Ambokile, wa nne kulia akiwa na baadhi ya wageni na wanachama baada ya mkutano. Pamoja naye ni mwenyekiti wa Watanzania, Bw. Kissasi, wa tatu kushoto, Meneja wa CRDB, Lucy Naivasha, wa kwanza kushoto, Meneja wa NSSF, Bi. Halima Mjala, wa pili kushoto na mwakilishi wa Solomon Stock Brockers, wa tatu kulia.

FILAMU YA BEI KALI KUZINDULIWA RASMI KESHO MLIMANI CITY

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

FILAMU ya Bei Kali inatarajiwa kuzinduliwa kesho katika ukumbi wa Mlimani City Golden Premier huku wasanii wakijinasibu kuwa ni moja kati ya filamu bora ndani ya soko la filamu.

Filamu hiyo inayojulikana kwa jina la 'Bei Kali' itazunduliwa rasmi kesho kuanzia saa moja usiku ikiwa mbashara kupitia kituo cha televisheni cha Azam Tv kwenye chaneli ya Sinema zetu na kuanza kuingia mtaani.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Daud Michael 'Duma' amesema kuwa filamu hiyo iliyofanywa chini ya Kwetu Studio imeweza kuchukua waigizaji wakubwa akiwemo Irene Uwoya, Hemed Suleiman, Patcho Mwamba na Kaptu Rado.
Duma amesema kuwa filamu hiyo inayoelezea maisha ya kawaida yenye mahusiano ndani yake yakimuhisha mwanadada aliyetoroshwa na mwanaume mwingine na kuletwa mjini lakini alipofika akajiingiza katika mahusiano mengine tofauti na baadae mumewe akaja kumtafuta mjini.

Ameeleza kuwa, filamu hiyo imejaa uhalisia zaidi na ana imani wapenzi wa filamu za kitanzania wataoendezewa nayo kwani imeweza kugusa maisha hali ya kitanzania hasa katika mahusiano na ndoa.

Filamu hiyo, imesimamiwa na Kaptu Rado sambamba na Rashidi Mrutu ambapo Duma amesema itakuja kuwakamata mtaani kwa ubora mzuri na hata waigizaji wake wameweza kutendea haki sehemu walizopatiwa.

WANAFUNZI WAJENGEWA UWEZO WA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI.

$
0
0
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni kwao.
Ofisa elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto)  ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.

ILI kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda. 

Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule hiyo. 

Mhandisi Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini wapende masomo hayo. 

Alisema hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya viwanda. 

"Sisi kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema mhandisi Narya. 

Mgeni rasmi wa mahafali hayo, ofisa elimu ya msingi wa halmashauri ya mji wa Babati, Doroth Mwandila alimpongeza mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Edson Elias kwa kuongoza kwenye mtihani wa moku katika shule 37 za sekondari za halmashauri ya mji huo. 

Mwandila alisema ili kumuandaa kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza mwakani, anampa mwanafunzi huyo zawadi ya sh20,000 na atamnunulia vitabu, madaftari na kalamu pindi akianza masomo yake kwa lengo la kumpa motisha ya kusoma kwa bidii zaidi. 

Aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kwa mwaka huu, kuwafuatilia watoto wao ipasavyo kwenye mienendo yao ya kila siku wakiwa majumbani ili kuhakikisha wanawaanda vizuri kwa ajili ya kuanza elimu ya sekondari mwakani. 

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Daniel Gaitu alisema shule hiyo ilianzishwa rasmi Januari 2010 ikiwa na watoto watano, wavulana wawili na wasichana watatu na hivi sasa ina wanafunzi 253 kati yao wavulana 119 na wasichana 134. 

Gaitu alisema kwa upande wa taaluma, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani kwani wanafunzi wa darasa la nne walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye halmashauri ya mji huo katika mtihani wa Taifa wa mwaka 2013, 2014 na nafasi ya pili mwaka 2016. 

Alisema wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka jana walishika nafasi ya kwanza kwa mtihani wa Taifa kwenye halmashauri ya mji huo na darasa la saba wa mwaka huu wameshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa moku mkoa wa Manyara kwenye shule 37 za halmashauri ya mji wa Babati. 

kampuni ya Compass Communications Tanzania yapongezwa kwa kufanya mashindan ya miss universe

$
0
0
 Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Univerese mwaka jana, Jihan Dimachk (Kulia) na Miss Earth Tanzania, Lilian Loth.
Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na warembo, waandaaji na maofisa wa Basata mara baada ya kumalizika kikao cha pamoja cha kujadili mashindano hayo.
 Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).Anayesikiliza Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua na Afisa Sanaa, Bona Leon Masenge.

Na Mwandishi wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua wakati wa kufanya tathimini ya mashindano hayo na mashindano ya urembo kwa ujumla.

Mrembo Jihan Dimachk alishinda taji la Miss Universe mwaka jana  huku Lilian Loth akishinda nafasi ya pili katika mashindano hayo.

Shalua alisema Basata wamefarijika sana na jinsi mashindano hayo yanavyoendeshwa na hakuna malalamiko yoyote kuhusiana na zawadi na upendeleo.

Alisema kuwa kutokana na utaratibu mzuri wa mashindano yao, Basata imeridhia waandaaji wa mashindano hayo, kufanya mashindano ya mwaka huu na vile vile kuandaa mashindano ya kutimiza miaka 10 tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2007.

“Pamoja na kuwa na shindano moja kwa kushirikisha warembo wa mikoa tofauti, bado Basata imefarijika na jinsi mnavyoendesha na utaratibu unaotumia kuwapata warembo, uendeshaji wa mashindano mpaka kumpata mshindi,” 

“Tunajua kuwa kuna changamoto za wadhamini na kusababisha kufanya mashindano yenye kalenda fupi na kuondoa mlolongo wa matukio, hatua hii ni bora zaidi ili kuondoa malalamiko ya zawadi na mambo mengine, huu ni mfano wa kuigwa,” alisema Shalua.

Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajihidi kuongeza wigo ili kuona warembo wengi zaidi kutoka mikoa tofauti wanashiriki katika mashindano yao.

Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini na kufikia malengo yao katika kuendeleza Sanaa hapa nchini.

“Kwa sasa kuna changamoto kubwa ya wadhamini wa mashindano, kuna haja ya kupata msaada kutoka Basata ambao ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa,” alisema Maria.

TAWI LA BENKI YA NMB LA NELSON MANDELA MJINI MOSHI YASHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

$
0
0
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akimlisha keki mkuu wa Mko wa Kilimanjaro ,Ana Mghwira wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiwaongoza wageni wengine wakati wa kupata Chai iliyoandaliwa na Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja .
Baadhi ya Wateja wa Benki ya NMB wakipata Chai katika tawi la Nelson Mandela mjini Moshi.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela,Emmanuel Kishosha akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira wakati akimkaribisha kuzungumza na Wateja a Benki hiyo waliojumuika katika Chai ya asubuhi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza na Wateja wa Benki ya NMB wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba Mosi.
Baadhi ya Wateja wa Benki ya NMB pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliotoa wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja katika Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi ,Emanuel Kishosha akielezea Historia ya Benki hiyo ilipotoka na wapi ilipo sasa kwa Wateja wa Benki hiyo .
Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakifurahia wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba mosi.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira cheti cha kutambua mchango wake wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akionesha cheti chake alichokabidhiwa na Benki ya NMB.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akikabidhi Vyeti kwa Wadu mbalimbali kwa niaba ya Benki ya NMB kwa kutambua mchango wao katika kufanikisha utendaji kazi wa Benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akikata Keki kwa ajili ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja katika Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akimlisha keki Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na Wateja wa Benki hiyo na viongozi mbalmbal waliohudhuria kuanza kwa wiki ya Huduma kwa Wateja.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

PROMOSHENI YA ‘MCHONGO CHINI YA KIZIBO’YALETWA NA COCA-COLA

$
0
0
 Kikosi kazi cha timu ya mauzo ya Nyanza Bottlers katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mchongo chini ya kizibo.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi (katikati),akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo
Msafara wa magari ya kampuni ya Nyanza Bottlers yakipita mitaani katika mji wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.

Kampuni ya Coca-Cola, imezindua kampeni kubwa ya wiki 10 kwa wateja wake inayojulikana kama ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ ambayo itawawezesha wateja wake wa mikoa ya kanda ya ziwa na jirani kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure. 

 Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi, alisema lengo la promosheni hii ni kuleta msisimko zaidi kwa wateja wanywaji wa soda zote zinazozalishwa na kampuni ya Coca-Cola waliopo mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, na mikoa mingine jirani ya kanda ya ziwa.

 “Kampuni yetu ya Coca-Cola katika kutoa shukrani kwa wateja wetu wanaotuunga mkono tumekuwa tukifanya promosheni mbalimbali zenye lengo la kuleta furaha na kubadilisha maisha yao kupitia Coca-Cola na promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ tunayoizindua leo. Kwa kunywa soda aina yoyote inayozalishwa na kampuni ya Coca-Cola wataweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, bodabado, televisheni aina ya SONY LED zenye inchi 32, T-shirts , kofia na soda za bure.” Alisema Kisusi. Alisema ili mteja kujishindia zawadi atabandua.

Iambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 na zaidi ya shilingi milioni 400/- zimetengwa kwa ajili ya kushindaniwa na wateja, ambapo kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele.

 Kisusi aliongeza kuwa pia zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilizvyo zawadi kubwa. “Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia promosheni hii ili waendelee kuburudika na soda zinazotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola sambamba na kunufaika kwa zawadi za kuleta furaha na kuboresha maisha yao, familia zao na wapendwa wao.”

 Kuhusu jinsi ya kupata zawadi alisema kuwa zawadi zote kwa washindi zitatolewa bila urasimu wa aina yoyote kuanzia kwenye maduka ya rejareja, mawakala maalumu wa kusambaza vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola na kwenye kiwanda cha Nyanza Bottlers. Soda za kampuni ya Coca-Cola ambazo zitakuwa na zawadi kwenye ganda la vizibo ni Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida.

HAB MKWIZU ATEULIWA NA KUWA MWENYEKITI WA BODI MPYA YA TSN

MKURUGENZI WA MASHTAKA AFUNGUA MAFUNZO YA UELIMISHAJI KUHUSU MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

$
0
0

 Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga (wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
 Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga kwenye Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
 Mkurugenzi wa Bw. Mashtaka Biswalo Mganga akifungua Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
 Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka katika Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo). (Picha zote na Mpiga picha wetu)

Na Sebera Fugence – Afisa Uhusiano Mwandamizi (WCF)Morogoro.
IMEELEZWA kuwa waajiri ambao hawajisajii na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Biswalo Mganga katika mafunzo ya uelemishaji wa Mawakili wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofanyika Mkoani Morogoro jana. (leo).

Mheshimiwa Mganga alisema   hatua za kisheria zitachukuliwa kwa waajiri watakaobainika kutenda makosa mengine yakiwemo ya kutowasilisha michango katika Mfuko kwa wakati.

Alisema lengo la Serikali ni kuona kila mfanyakazi anayeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi anapata mafao yake kama ambavyo imeeekezwa katika Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi  Sura 263 ikisomwa pamoja na kanuni zake za mwaka 2016.

“Mafunzo haya yatatoa fursa kwa Ofisi yangu na Maafisa wengine kueleza uzoefu wao kuhusu  namna ya kuendesha Mashauri ya Jinai zikiwemo changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto hizo hasa pale wanaposhughulikia kesi dhidi ya waajiri wanaokiuka sheria.
Alisema Ofisi yake ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha kuwa matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yanatekelezwa kikamilifu na wale wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.

Nae Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) nchini  Bw. Masha Mshomba alisema  Ofisi  ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali  ipo kwa mujibu wa Sheria ya Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na moja kati majukumu yake ya msingi ni kufungua, kusimamia  na kuendesha mashauri ya jinai katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

Alisema Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha malengo ya Mfuko huo yanafikiwa kwani ndio wasimamizi wakuu katika uendeshaji mashauri ya jinai yakiwemo makosa ya jinai yaliyoainishwa kwenye Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. 

Aliitaja changomoto inayoikabii Mfuko huo kuwa ni  idadi kubwa ya waajiri ambao hawajajisajili na hawachangii kwenye Mfuko na kuongeza kuwa changamoto hiyo isipopatiwa suluhisho la haraka itaathiri uwezo wa  Mfuko kulipa fidia kwa wafanyakazi.

Alisema hadi kufikia juni 30, 2017 Mfuko umelipa fidia ya kiasi cha Shilingi 613,843,555.64 ikiwa ni gharama za matibabu fidia ya ulemavu wa muda mfupi na ulemavu wa kudumu.
Kwa upande wa usajili Bw. Mshomba amesema hadi kufikia juni 30, 2017 mfuko tayari ulikuwa umesajii waajiri 7,857 ambapo hadi kufikia juni 31, 2017 inakadiriwa kuwa  zaidi ya waajiri 13,918 waliopo Tanzania Bara hawajasajiiwa kwenye Mfuko.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iiyoanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya mwaka 2015 kwa lengo la kushughuikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia ama kuugua ama kufariki wakati wakitekeeza majukumu ya mwajiri kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

TRA YATOA MAFUNZO KWA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA TAASISI ZA SERIKALI

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Jairo akiongea machache kabla kumkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa tatu kushoto) kufungua semina ya siku mbili ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. Kutoka (kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Rasilimali watu, Dkt. Amos Ibrahim, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Maswala ya Ufundi, Michael Muhoja na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akiongea na wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. Kutoka (kulia) ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Taalum, Utafiti na Ushauri, Dkt. Lewis Isemwi, Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Isaya Jairo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Maswala ya Ufundi, Michael Muhoja. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Baadhi ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za serikali wakijisajili tayari kushiriki katika semina ya siku mbili ya mafunzo ya kuongenzwa uelewa wa maswala ya kodi jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 4 2017. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja watendaji waandamizi wa TRA, Chuo cha Kodi, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na washiriki wa semina hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa washiriki wa semina hiyo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Jairo katika viwanja vya Chuo cha Kodi Mikocheni jijini Dar es Salaam alifanya ufunguzi semina ya siku mbili kwa wahasibu wa wakaguzi wa Taasisi za ummaa Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Maswala ya Kodi wa TRA, Michael Muhoja. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akiongea na wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. Kutoka (kulia) ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Taalum, Utafiti na Ushauri, Dkt. Lewis Isemwi, Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Jairo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Maswala ya Ufundi, Michael Muhoja. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 
Meneja ukaguzi wa mahesabu ya kodi wa TRA, Beatus Mchota akitoa mada kwa wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017.


Mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akilakiwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Taalum, Utafiti na Ushauri, Dkt. Lewis Isemwi alipowasili kwa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

MKURUGENZI WA MASHTAKA AFUNGUA MAFUNZO YA UELIMISHAJI KUHUSU MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

$
0
0
NA SEBERA FUGENCE – AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI (WCF), MOROGORO

IMEELEZWA kuwa waajiri ambao hawajisajii na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Biswalo Mganga katika mafunzo ya uelemishaji wa Mawakili wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofanyika Mkoani Morogoro jana. (leo)

Mheshimiwa Mganga alisema   hatua za kisheria zitachukuliwa kwa waajiri watakaobainika kutenda makosa mengine yakiwemo ya kutowasilisha michango katika Mfuko kwa wakati.

Alisema lengo la Serikali ni kuona kila mfanyakazi anayeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi anapata mafao yake kama ambavyo imeeekezwa katika Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi  Sura 263 ikisomwa pamoja na kanuni zake za mwaka 2016.

“Mafunzo haya yatatoa fursa kwa Ofisi yangu na Maafisa wengine kueleza uzoefu wao kuhusu  namna ya kuendesha Mashauri ya Jinai zikiwemo changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto hizo hasa pale wanaposhughulikia kesi dhidi ya waajiri wanaokiuka sheria.
Alisema Ofisi yake ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha kuwa matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yanatekelezwa kikamilifu na wale wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.

Nae Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) nchini  Bw. Masha Mshomba alisema  Ofisi  ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali  ipo kwa mujibu wa Sheria ya Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na moja kati majukumu yake ya msingi ni kufungua, kusimamia  na kuendesha mashauri ya jinai katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Alisema Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha malengo ya Mfuko huo yanafikiwa kwani ndio wasimamizi wakuu katika uendeshaji mashauri ya jinai yakiwemo makosa ya jinai yaliyoainishwa kwenye Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Aliitaja changomoto inayoikabii Mfuko huo kuwa ni  idadi kubwa ya waajiri ambao hawajajisajili na hawachangii kwenye Mfuko na kuongeza kuwa changamoto hiyo isipopatiwa suluhisho la haraka itaathiri uwezo wa  Mfuko kulipa fidia kwa wafanyakazi.

Alisema hadi kufikia juni 30, 2017 Mfuko umelipa fidia ya kiasi cha Shilingi 613,843,555.64 ikiwa ni gharama za matibabu fidia ya ulemavu wa muda mfupi na ulemavu wa kudumu.Kwa upande wa usajili Bw. Mshomba amesema hadi kufikia juni 30, 2017 mfuko tayari ulikuwa umesajii waajiri 7,857 ambapo hadi kufikia juni 31, 2017 inakadiriwa kuwa  zaidi ya waajiri 13,918 waliopo Tanzania Bara hawajasajiiwa kwenye Mfuko.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iiyoanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya mwaka 2015 kwa lengo la kushughuikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia ama kuugua ama kufariki wakati wakitekeeza majukumu ya mwajiri kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Biswalo Mganga kwenye Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro leo Oktoba 4, 2017.

Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka katika Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro
Mkurugenzi wa Bw. Mashtaka Biswalo Mganga akifungua Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro
Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga (wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 15 katika ajali ya lori Mkoani Rukwa

MARUFUKU KUWAKAMATA WAUGUZI BILA YA KUFUATA TARATIBU-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku tabia ya baadhi ya viongozi katika maeneo mbalimbali nchini kuwakamata na kuwaweka ndani watumishi wakiwemo wauguzi bila ya kufuata taratibu.

Pia amewataka wauguzi nchini kufanya kazi kwa weledi, uaminifu pamoja na kufuata maadili ya taaluma yao kwa kuwa maisha ya wagonjwa yako chini yao.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 04, 2017) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 45 wa Chama cha Wauguzi Tanzania, mkoani Lindi.

“Naagiza viongozi wote kufuata na kuzingatia sheria. Kama kuna makosa ya kitaaluma, Mabaraza husika yashughulikie jambo hilo na ni marufuku kuwaweka ndani watumishi kwa tuhuma za kitaaluma.”Amesema kwamba katika sekta ya afya bila wauguzi ambao ni kundi kubwa kati ya Wanataaluma wa Afya, Serikali haitaweza kutekeleza ipasavyo mikakati mbalimbali iliyopangwa kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo.

Katia hatua nyingine Waziri Mkuu amewaasa wauguzi wote nchini kuhakikisha wanazingatia kiapo cha maadili ya kazi yao na kwamba Serikali haitamvumilia yeyote atakae bainika kwenda kinyume.“Nanyi Wauguzi mnao wajibu wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia kiapo na miiko ya taaluma yenu. Tunazo taarifa kuhusu baadhi ya Wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa, kuomba rushwa na wengine kujihusisha na vitendo vya wizi wa dawa.”

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha afya za Watanzania wote zinaimarika ili kuendana na kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya kuinua uchumi na kufikia wa kiwango cha kati, hivyo ni lazima watoe huduma bora kwa wananchi.Pia amewaomba waunge mkono kwa nguvu zote jitihada za Serikali katika kuhakikisha miundombinu na vifaa vyote havihujumiwi na watu wachache ili viwe msaada mkubwa hususani kwa akina mama wajawazito ili wajifungue salama.

Akizungumzia kuhusu upungufu wa wauguzi nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo Wauguzi na Wakunga na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu zaidi.
Awali, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamis Kigwangalla alisema baadhi ya viongozi katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakiwakamata na kuwachukulia hatua watumishi wa Sekta ya Afya bila ya kufuata taratibu, jambo ambalo si sahihi.

Mkutano huo umehudhuriwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Kigwangalla, Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania Bw. Paul Magesa, Mbunge wa Lindi Mjini Bw. Hassan Kaunje, Mbunge wa Kuteuliwa Mama Salma Kikwete(MB) Viti maalum.Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Gustav Moyo, Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bw. Stewart Mbelwa.

Wengine ni Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Abdallah, Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Uuguzi Bw. Ndementria Vermund, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania Dkt. Obadia Nyongolena wawakilishi wa wauguzi kutoka mikoa yote nchini.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATANO, OKTOBA 04, 2017.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisoma Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) ambao umeanza leo Oktoba 4,2017 Mkoani Lindi. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mwenezi msaidizi wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Johari Yusuf, baada ya ufunguzi wa Mkutano wa chama cha wauguzi leo Oktoba 4,2017 Mkoani Lindi.katikati  ni mweye beji shigoni ni Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania Bwana Poul Magesa .kulia kwa katibu mwenezi ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania Sebastian Luziga.

WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI MAZAO YA NYUKI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)(kulia)akitundika Mzinga katika Banda la Nyuki la Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima(hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb)(kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ofisini kwake kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki yaliyofanyika Mkoani humo katika kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akizungumza na wananchi wa wilayani hiyo (hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) akizindua Manzuki (Shamba la Miti lenye Mizinga ya Nyuki) ya Kikundi cha Wafugaji nyuki cha Malela Wilayani Itilima wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) (kulia) kabla ya kuanza safari kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani humo.


Na Stella Kalinga, Simiyu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani amesema Wafugaji Nyuki wanayo fursa kubwa ya kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuchakata, kufungasha na kuongeza thamani mazao ya nyuki na kutengeneza vipodozi kutokana na mazao ya nyuki.

Mhandisi Makani ameyasema hayo jana wakati alipozungumza na wafugaji wa nyuki na wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, chini ya Kauli Mbiu “UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA UNACHANGIA KATIKA UKUAJI WA VIWANDA”

Amesema Mazao ya Nyuki ni malighafi ya Viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya vyakula vinavyotumia asali, viwanda vya dawa na vipodozi na viwanda vya utengenezaji vinavyotumia nta katika kuzalisha maturubai, dawa za kung’arisha viatu na bidhaa nyingine, hivyo wafugaji wanao wajibu wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki na ujuzi wa kuyaweka katika ubora na kuyaongezea thamani.

Aidha, ametoa wito kwa wafugaji wa nyuki kuungana katika vikundi vyenye usajili ili waweze kuzalisha asali kwa wingi na yenye kufanana, kwa kuwa ikiwa watazalisha kila mmoja kwa utaratibu wake, asali hiyo haiwezi kuchanganywa na itakuwa na ubora na sifa tofauti, lakini ikiwa wataungana na kuzalisha asali nyingi kwa pamoja wakaipima kwa viwango vya ubora unaotakiwa wataweza kupata soko.

Sanjali na hilo amesema Serikali itahakikisha inawaunganisha wafugaji nyuki na walaji wa ndani na nje na akabainisha kuwa kwa miaka zaidi ya 11 imekuwa na ushirikiano na soko la Ulaya ambapo sampuli za asali kutoka maeneo mbalimbali zimepelekwa Ulaya na taarifa za maabara zinathibitisha kuwa asali ya Tanzania ni salama kwa afya ya mlaji.

Aidha, amesema katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki Serikali pia inaendelea kutoa elimu kwa wafugaji wa nyuki kuachana na matumizi ya mizinga ya asili ambayo ni duni na inachukua nafasi kubwa wakati uzalishaji wake ni mdogo na kuwahamasisha kuanza kutumia mizinga ya kisasa.

“ Nawaagiza Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki nchini na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia jukwaa hili, kwamba mbuni njia rafiki ya kuweka msisitizo katika utoaji wa elimu, uhamasishaji na kupima mafanikio kila mwaka; taarifa ya utekelezaji wa maagizo haya itolewe mara kwa mara, taarifa ya kwanza baada ya agizo hili itolewe katika siku ya maadhimisho kama haya mwaka kesho 2018” aliagiza Naibu Waziri

Katika hatua nyingine Mhe. Makani amepongeza juhudi zinazofanywa na Mradi wa LVEMP II katika kuboresha mazingira na kubainisha kuwa pamoja na kuhifadhi rasilimali za asili za Bonde la Ziwa Victoria ambayo husaidia kutunza vyanzo vya maji na mazingira hayo yanafanywa kuwa mazingira bora kwa ufugaji nyuki, ambapo katika wilaya ya Itilima kuna vikundi 22 vyenye mizinga 2080 ya nyuki vinavyofadhiliwa na LVEMP.

Akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki amesema idadi ya wafugaji na mizinga ya nyuki imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo kwa sasa kuna jumla ya vikundi 91 vyenye jumla ya mizinga 5824 na akaahidi kuwa mkoa utaendelea kusimamia uboreshaji wa mazingira ya ufugaji nyuki na kusimamia vikundi vinavyoanzishwa katika Halmashauri., ili wafugaji wanufaike na kujiimarisha kiuchumi

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Ndg.Herberth Haule amesema shughuli ya ufugaji wa nyuki inasaidia katika uhifadhi wa mazingira na kujenga uchumi kwa wananchi hususani vikundi vinavyojishughulisha na kazi hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Ezekiel Mwakalukwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za Afrika zinazoruhusiwa kuuza asali yake katika soko la Ulaya na nchi ya China

Nao wafugaji wa nyuki na wajasiriamali wa mazao ya nyuki wameiomba Serikali pamoja na wadau wengine kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza vifungashio kwa kuwa suala hilo ni changamoto kwao ambayo inawalazimu kuagiza vifungashio nje ya nchi kwa kutumia gharama kubwa.

Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa kwa mwaka 2017 yameadhimishwa kwa mara kwanza Mkoani Simiyu yakiwa ni maadhimisho ya tano kufanyika hapa nchini, ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2013 Mkoani Singida.

WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI

$
0
0
Ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda. 

Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule hiyo. Mhandisi Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini wapende masomo hayo. 

Alisema hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya viwanda. 

"Sisi kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema mhandisi Narya. 

Mgeni rasmi wa mahafali hayo, ofisa elimu ya msingi wa halmashauri ya mji wa Babati, Doroth Mwandila alimpongeza mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Edson Elias kwa kuongoza kwenye mtihani wa moku katika shule 37 za sekondari za halmashauri ya mji huo. 

Mwandila alisema ili kumuandaa kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza mwakani, anampa mwanafunzi huyo zawadi ya sh20,000 na atamnunulia vitabu, madaftari na kalamu pindi akianza masomo yake kwa lengo la kumpa motisha ya kusoma kwa bidii zaidi. 

Aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kwa mwaka huu, kuwafuatilia watoto wao ipasavyo kwenye mienendo yao ya kila siku wakiwa majumbani ili kuhakikisha wanawaanda vizuri kwa ajili ya kuanza elimu ya sekondari mwakani. 

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Daniel Gaitu alisema shule hiyo ilianzishwa rasmi Januari 2010 ikiwa na watoto watano, wavulana wawili na wasichana watatu na hivi sasa ina wanafunzi 253 kati yao wavulana 119 na wasichana 134. 

Gaitu alisema kwa upande wa taaluma, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani kwani wanafunzi wa darasa la nne walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye halmashauri ya mji huo katika mtihani wa Taifa wa mwaka 2013, 2014 na nafasi ya pili mwaka 2016. 

Alisema wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka jana walishika nafasi ya kwanza kwa mtihani wa Taifa kwenye halmashauri ya mji huo na darasa la saba wa mwaka huu wameshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa moku mkoa wa Manyara kwenye shule 37 za halmashauri ya mji wa Babati. 
 Ofisa elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto)  ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni kwao.

WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB

$
0
0
Wafanyabiashara wadogo na wakati wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiinua kiuchumi kwa kuchukua mkopo inayotolewa na benki ya CRDB ndani ya siku saba. 

Akizungumza kwenye sherehe za ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja duniani, meneja wa CRDB tawi la Babati Ronald Paul alisema mkopo huo wa miezi mitatu utawanyanyua kiuchumi wajasiriamali hao. Paul alisema wajasiriamali hao wachangakie fursa hiyo ambayo imeanzishwa wiki hii ya huduma kwa wateja dunia, ambapo pia itaendelea kutolewa na benki hiyo kwa siku zote zinazoendelea kuwepo. 

Alisema wamejipanga kuboresha zaidi huduma kwa wateja wa benki yao, hivyo wajasiriamali wa mjini Babati, wilaya za Kiteto, Mbulu, Simanjiro, Hanang' na miji midogo ya Mirerani, Magugu, Galapo, Haydom na Dareda, wachangakie fursa hiyo.

Alisema wiki ya huduma kwa wateja dunia, itafikia kileleni jumamosi ijayo mjini Babati, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera ambaye atazungumza na wadau wa benki ya CRDB."Siku hiyo kutakuwa na shamrashamra za kutosha kwani wadau wenye ushawishi kwa jamii watakuwepo kwenye tawi hili la CRDB Babati, ambapo watatueleza mambo mawili matatu yatakayowanufaisha wajasiriamali wetu," alisema Paul. 

Aliwaahidi wateja wa benki hiyo kuwa huduma zimeboreshwa zaidi hivyo wafike na kujionea wenyewe kwa kuweka fedha, kufungua akaunti au kuchukua mikopo, kwani hata riba zao ni nafuu tofauti na taasisi nyingine za fedha. Mmoja kati ya wajasiriamali wa mji mdogo wa Magugu wilayani Babati, Elizabeth Seluhinga alisema huu ndiyo wakati wa kuchangamkia fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kiuchumi kupitia mikopo inayotolewa na benki hiyo. 

Seluhinga alisema yeye ni mjasiriamali wa nyanya kwenye mji mdogo wa Magugu na anatarajia kuchukua mkopo kwenye benki ya CRDB ambapo ameambiwa ndani ya siku saba atakuwa ameshapatiwa fedha za mkopo. 

Alisema wajasiriamali wasiogope kuchukua mikopo ili kuboresha biashara zao kwani hata wafanyabiashara maarufu nchini, wengi wao wamenyanyuka kimaisha kwa kuchukua mikopo na siyo vinginevyo. 
 Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, wakiwa kwenye viwanja vya benki yao tayari kabisa kwa kutoa huduma kwa wateja wao kwenye wiki ya huduma kwa wateja dunia ambayo itafikia kilele jumamosi ijayo.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Ronald Paul, akizungumza jana na waandishi wa habari juu ya wiki ya huduma kwa wateja dunia ambayo itafikia kilele jumamosi Ijayo. 

MATOKEO YA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI

$
0
0
Jumla ya wananchi 600 wameshiriki katika zoezi la upimaji wa magonjwa ya Moyo ambao ulienda sambamba na utoaji wa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani iliyofanyika tarehe 29/09/2017 katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Wananchi walioshiriki katika zoezi hilo walipimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na kupewa ushauri. Asilimia 80 ya wananchi waliopimwa siku hiyo walikutwa na matatizo ya shinikizo la juu la damu na wengine walikutwa na matatizo mengine ya Moyo.

Aidha wagonjwa 400 waliokutwa na matatizo ya moyo walipewa dawa na baadhi yao walianzishiwa kliniki ili wataalamu wetu waweze kufuatilia maendeleo ya afya zao kwa ukaribu na kuweza kupata huduma ya matibabu kwa ukaribu zaidi.

Kwa namna ya kipekee tunazishukuru sana kampuni zinazotengeneza dawa za binadamu za Tata Africa Holdings (T) LTD, Reddy’s, na Phillips ambazo ziligawa dawa bure kwa wananchi waliokutwa na matatizo ya Moyo.

Tunawaomba wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na hivyo kuanza matibabu mapema. Asilimia kubwa ya wagonjwa tunaowapokea katika kliniki zetu baada ya kuwafanyiwa vipimo tunawakuta mioyo yao haiko katika hali nzuri. Hii inaonyesha kuwa wana matatizo ya Moyo pasipo kujifahamu.


Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

04/10/2017

TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

JIJI la Dar es Salaama ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi kubwa duniani, huku ukuaji huo ukiathiri sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo sekta ya usafirishaji.

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 inakadiria kuwa jiji la Dar es Salaam lina wakazi milioni 2.4 na kuwa na kiwango cha ongezeko la idadi ya watu cha asilimia 4.4 kwa mwaka huku ongezeko hilo likisababisha kujitokeza kwa mapungufu katika utoaji wa huduma mbalimbali.

Tangu miaka ya 1990 kumekuwa na mipango mbalimbali ya kuboresha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo kuanzisha barabara za njia moja, kuanzisha maegesho ya magari ya kulipia, na kuhamasisha kujengwa kwa majengo yenye maegesho ya magari.

Pamoja na jitihada za serikali ya jiji la Dar es Salaam na serikali kuu kuboresha usafiri Jijini humo, bado kuna kero kubwa ya usafiri wa abiria, hasa wakati wa saa za asubuhi na jioni ambapo ambapo ilimlazimu mwananchi kuchukua takribani masaa matatu, kwa mfano, kutoka Mbezi Juu hadi katikati ya jiji.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, tangu mwaka 2008 Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam imekuwa ikitekeleza miradi maalum ya ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu za Jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Miradi wa Ofisi ya TANROAD Mkoa wa Dar Es Salaam, Julius Ngusa anasema mradi wa ujenzi wa barabara za pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam wa awamu ya tatu ni moja ya mikakati ya Serikali ya kushughulikia tatizo sugu la msongamano wa magari katika Jiji hilo ambapo utekelezaji wake ulianza tangu wa mwaka wa fedha 2008/2009.

Anasema kupitia mradi huo, Serikali ilichagua barabara tisa kwa ajili ya kujengwa katika kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Ubungo Bus Terminal-Kigogo-Kawawa (6.4 km), barabara ya Jet Corner-Vituka-Davis Corner (km 12), barabara ya Kinyerezi-Kifuru-Msigani-Mbezi mwisho (10 km), Tanki bovu-Goba (9.0 km), Kimara baruti-Msewe-Changanyikeni (2.6 km).

Anazitaja barabara nyingine kuwa ni pamoja na Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi/Morogoro (km 20) , Kigogo Round about-Jangwani-Twiga katika bonde la msimbazi (km 2.72), Tabata Dampo-Kigogo na Ubungo Maziwa- Mabibo External (Mandela) (2.25 km).

Mhandisi Ngusa anasema miradi hiyo inajengwa katika awamu tatu za utekelezaji, ambapo hadi sasa awamu ya kwanza ya miradi hiyo iliyohusisha ujenzi wa barabara zenye jumla ya kilometa 19.42 tayari imekwishatekelezwa na kukamilika tangu mwaka 2008.
Anaitaja miradi iliyokamilika ni pamoja na barabara ya Ubungo-Kigogo-Kawawa iliyokamilika mwaka 2010 kwa gharama ya Tsh. Bilioni 11.44, barabara ya Kigogo-Msimbazi-Jangwani iligharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 7.64 ambayo ilikamilika mwaka 2017 pamoja na barabara ya Jet Corner-Vituka-Devis Corner iliyokamilika mwaka 2011.

“Kuhusu Awamu ya pili yenye urefu wa kilometa 27.5 na ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40, ujenzi wake ulianza mwaka 2014 ambapo hadi sasa kazi za ujenzi zilizokamilika kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Tangi Bovu (Samaki Wabichi)-Goba km 9 ilikamilika mwaka 2016 kugharimu kiasi Tsh. Bilioni 8.6 ” anasema Ngusa.

Kwa mujibu wa Ngusa anasema pia katika awamu hiyo mwaka 2016 Serikali pia ilikamilisha ujenzi wa Barabara ya Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi Mwisho (km 20), kwa gharama ya Tsh. Bilioni 6.7.

Akifafanua zaidi Ngusa anasema miradi mingine iliyokamilika ni pamoja na Barabara ya kilungule (Maji Chumvi)- External/Mandela km 3.3, ambapo mradi huo ulikamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Tsh. Bilioni 4.4.

Aidha Ngusa anasema mradi wa barabara ya kimara baruti-msewe (km 2.6) uliopaswa kukamilika mwak 2016, umeshindishwa kukamilika kwa wakati kutokana na kutokuwepo kwa nafasi ya kujenga barabara, ambapo hata hivyo hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2017 mradi huo umefikiaa asilimia 80 ya utekelezaji wake.

Mhandisi Ngusa anasema awamu ya tatu ya utekelezaji wa miradi hiyo ulioanza kutekelezwa mwaka 2016 na 2017 unahusika ujenzi wa barabara za Kifuru-Msigani, Goba-Makongo na Goba-Madale zenye urefu wa kilometa 14.1 na unatarajia kukamilika mwanzoni na mwishoni mwa mwaka 2018.

“Miradi ya barabara ya Goba-Madale na Goba-Makongo hadi kufikia Septemba 30, mwaka huu imekamilika kwa asilimia 50-52 wakati ule wa Kifuru-Msigani umekamilika kwa asilimia 87, malengo ni kuhakikisha kuwa miradi hii inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora na viwango tulivyojiwekea” anasema Mhandisi Ngusa.

Anasema baadhi ya changamoto inayokabili miradi hiyo ni pamoja na baadhi ya nyumba zinazohitaji fidia, ambapo hata hivyo TANROAD kwa kushikiana na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) zimeanza zoezi la uthamini na malipo yatalipwa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI.

Anasema Serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara za Msongola-Mbande (km 1), ununio-mbweni (km 1), kitunde-kivule (km 3.2), Dege-Gomvu (km 1) na inatarajia kuanza awamu ya nne ujenzi wa barabara za Msigani-Mbezi mwisho (km 2) na Makongo-Ardhi (km 5) wakati wowote kutoka sasa kutegemeana na upatikanaji wa fedha.

Kukamilika kwa miradi hii kutasaidia kuongeza tija na ufanisi katika kuchochea kasi ya maendeleo katika Jiji la Dar es salaam na taifa zima kwa ujumla hasa tukizingatia zaidi ya 80% ya pato la ndani la Taifa linachangiwa na Jiji la Dar es salaam.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images