Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1384 | 1385 | (Page 1386) | 1387 | 1388 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha Kleruu wakifuatilia maada inayowasilishwa kuhusiana na Mradi wa SPANEST jinsi inavyoshirikisha wananchi katika masuala ya uhifadhi mara baada ya kufunguliwa kwa kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. (Picha na Lusungu Helela- MNRT)
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa kwenye picha ya pamoja na Sekretarieti ya Waandaji wa kongamano mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa (Picha na Lusungu Helela- MNRT).
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, amefungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa.

  Kongamano hilo limefanyika kwa muda wa siku moja katika Ukumbi wa Chuo cha Walimu wa Kleruu likiwakutanisha wasomi na wahadhiri kutoka vyuo vikuu nchini, wanafunzi pamoja na wadau wa utalii wanaofanya shughuli za kiutalii likiwa na lengo la kutathmini na kuangalia namna mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inavyoweza kunufaika kutokana na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo.

  Sambamba na kongamano hilo, maonesho hayo yanaendelea kufanyika hadi Oktoba 2 katika viwanja katika viwanja vya Kichangani yakiwa yamewakutanisha Wajasiriamali wadogo 350 kutoka kona zote za mikoa hiyo.Akizindua Kongamano hilo Naibu Waziri Makani amewataka wananchi kuanza kuutupia macho utalii wa nje ya hifadhi kwa kuwa watalii wengi kwa sasa hawaji kuangalii wanyamapori pekee.

  Amesema watalii wa siku hizi wamechoka kuangalia wanyamapori wanataka kujifunza kuhusu utamaduni wetu pamoja na vyakula vyetu vya kiasili.Mbali na kuwa na utajiri wa makabila tofauti tofauti, Makani alisema Nyanda za juu Kusini imejaliwa kuwa na vivutio vya Malikale ambayo bado havijatangazwa vya kutosha.

  Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga alisema Iringa inasifika kwa kuzalisha wataalamu wa tasnia ya utalii kutokana na uwepo wa chuo Kikuu cha Tumaini kuwa ndo chuo cha kwanza kutoa shahada ya Utalii lakini imekuwa nyuma kiutalii akitolea mfano wa hoteli zinazojengwa ni za chini ya kiwango licha ya watalaam kuwepo.

  Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, David Jamhuri alisema mkoa umejipanga kuhakikisha kuwa fursa za utalii kwa mikoa ya Nyanda za juu Kusini zinafunguka kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa wa kwanza kunufaika kutokana namipango waliyojiwekea

  Pia aliwataka viongozi wa Kiserikali kila wanapopata nafasi ya kuzungumza na wananchi watumie fursa hiyo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

  Muongoza watalii wa Kampuni ya Chabo Tours, Serafino Liduino aliitaka Serikali kuanza kuona umuhimu wa kutoa mafunzo mashukeni ili kutengeneza kizazi kinachojua thamani ya kuhifadhi mazingira ili vivutio asilia viendelee kuwepo kutokana na tishio la mabadiliko ya tabia ya nchi yanajitokeza kwa sasa.

  0 0  0 0

  Wakati dunia ikisherehekea siku ya Utalii Duniani, Jumia Travel imebainisha kwamba matumizi ya tekinolojia za kisasa hususani mtandao wa intaneti una manufaa makubwa katika kuvitangaza vivutio vya kitalii kimataifa.
  Akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea nchini Tanzania, Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Kimataifa, Bw. Abdesslam Benzitouni ameweka wazi kwamba Tanzania haina budi kutumia ipasavyo njia zote za kidigitali ikiwemo mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Youtube na Instagram kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watumiaji. 

  “Intaneti imekuwa na mchango mkubwa kwenye sekta ya utalii na ukarimu hususani kwenye kutoa taarifa. Tofauti na kipindi cha nyuma hivi sasa watu wanaweza kupata taarifa muda wowote na mahali popote walipo bila ya kutembelea moja kwa moja eneo husika.

   Jumia Travel inazitumia njia zote za mtandaoni kuzionyesha na kuzitangaza hoteli pamoja na vivutio vya kitalii nchini. Tovuti na kurasa za mitandao yetu ya kijamii tuzipatia hoteli tunazoshirikiana nazo fursa kubwa ya kujitangaza na kuonekana mtandaoni ambapo kwa kiasi kikubwa huongeza idadi ya wateja,” alisema Benzitouni. 
  “Wakati dunia ikisherehekea siku ya Utalii Duniani, bara la Afrika limeshuhudia idadi ya watalii kufikia milioni 58 mwaka 2016. Na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka maradufu ndani ya miaka 15 ijayo na kufikia milioni 130. Mafanikio hayo yamechangiwa na ukuaji wa kasi wa sekta ya usafiri wa anga, ambapo mashirika ya ndani na kimataifa yana mchango mkubwa kwenye kuwasafirisha watalii ndani na nje ya nchi, ” aliongezea Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Kimataifa.
  Aliendelea na kufafanua zaidi kwamba kwa Tanzania kutajwa kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zinatembelewa zaidi barani Afrika, sawa na nchi zingine kama vile Morocco, South Africa, Rwanda na Namibia, ni dalili nzuri kwamba utalii unaleta tija kubwa na inaweza kunufaika nao kwa kutumia mbinu tofauti ili kuvutia wageni wa kimataifa zaidi.

  “Kupitia ripoti ya Utalii na Ukarimu ambayo Jumia Travel tuliiwasilisha mapema mwaka huu, tuligundua kwamba idadi ya watalii kwa mwaka 2016 iliongezeka kwa 16%. Pia kuongezeka kwa idadi ya watanzania wanaotumia mtandao wa intaneti kunaashiria matumizi ya mifumo mipya ya kidigitali. 
  Tunaweza kuitumia katika kuvitangaza vivutio vyetu, kutoa taarifa za kutosha zaidi, pamoja na bei nzuri na zenye ushindani kwenye soko ili kurahisisha shughuli za kitalii. Tafiti zinaonyesha idadi kubwa ya watalii wanaotembelea Afrika wanatokea nchi za bara la Asia zaidi. Kwa mfano, 10% ya Wachina wanaosafiri duniani hutembelea zaidi nchi za Afrika,” alihitimisha Benzitouni.

  Kati ya mambo ya msingi ambayo Jumia Travel inajitahidi kuyaangazia kwenye sekta ya utalii na ukarimu nchini Tanzania pamoja na kwingineko ilipo Afrika ni gharama za juu za malazi. Kwa waafrika wengi, malazi yamekuwa ni kati ya changamoto kuu inayokwamisha shughuli za kitalii kwa miaka kadhaa sasa. 
  Kulipatia ufumbuzi hilo kampuni hiyo imejizatiti kuhakikisha kwamba inaweka aina zote za malazi kwenye mtandao wao ili yafikiwa kwa urahisi na wateja. Lengo kuu ni kumuwezesha kila mtu aweze kupata huduma ya malazi kwa gharama nafuu licha ya uwezo alionao.

  0 0

  Harbinder Sethi
  Na Dotto Mwaibale

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine mshtakiwa Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ndani ya siku 14.

  Korti imesema iwapo hilo halitatekelezwa, mkuu wa gereza afike mahakamani kujieleza. Sethi yupo mahabusu katika Gereza la Segerea.

  Amri hiyo ya mahakama imetolewa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kudai kesi ilipangwa leo Ijumaa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba shauri lipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

  Baada ya maelezo hayo, wakili Joseph Makandege anayemwakilisha Sethi alieleza kuwa kumekuwepo mfululizo wa amri za Mahakama zikiagiza mteja wake akapatiwe matibabu na kufanyiwa uchunguzi Muhimbili.

  “Hadi leo asubuhi tuliwasiliana na mteja wetu na kubaini hajapelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama amri za Mahakama zilivyoagiza, hivyo ni rai yetu kwamba kitendo hicho cha kutotekelezwa amri za Mahakama ni ukaidi wa amri halali za Mahakama yako tukufu,” amesema Makandege.

  Alisema kwa kuwa upande wa mashtaka umekaidi amri za Mahakama, anaomba itoe adhabu inayostahili.Makandege alisema kitendo cha upande wa mashtaka cha kutotekeleza amri za Mahakama kinasigana na kukiuka mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka .

  “Mkurugenzi wa Mashtaka katika kutekeleza majukumu yake anapaswa kuongozwa na kutenda haki, lengo ni kutogeuza mashtaka ya jinai na mahakama kuwa ni vyombo vya utesaji,” amesema.Ameomba Mahakama itoe adhabu stahiki kwa kuwa hilo linaonyesha dhahiri kuwa mashtaka yaliyopo ni ya hila yenye lengo la kuwaadhibu washtakiwa na hasa mshtakiwa wa kwanza Sethi kabla hawajahukumiwa.

  Wakili Makandege ameiomba Mahakama iitupilie mbali hati ya mashtaka na kuwaachia huru washtakiwa ili Sethi apate wataalamu wa matibabu yake katika hospitali ikiwemo Muhimbili.Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai tatizo limeshajitokeza katika utekelezaji wa amri za Mahakama.

  Swai amedai Magereza wamekuwa wakiwatibu wafungwa na mahabusu hata pasipokuwa na amri ya Mahakama.Alisema kilichojitokeza ni utaratibu wa kumpeleka Sethi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.“Tumejitahidi kuwasiliana na Magereza wapo katika hatua za mwisho, tunaomba muda wa ziada ili tuiwezeshe Magereza kukamilisha utaratibu wa kumpeleka Sethi Muhimbili, hatujakataa tunaomba muda,” amesema Swai.

  Hakimu Huruma Shaidi amesema ni lazima amri za Mahakama zifuatwe. Ameahirisha kesi hadi Oktoba 13.Alisema hadi siku hiyo, Sethi awe ameshapata matibabu na iwapo atakuwa hajapatiwa, mkuu wa gereza alipo afike mahakamani kujieleza.

  Katika kesi hiyo, Sethi na James Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi wakidaiwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kighushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola 22,198,544.60 za Marekani na Sh309,461,300,158.27.

  Wanadaiwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  0 0

  Meneja Abdallah Mrisho na mkewe, Catherine Mdamu wakiwa katika pozi la furaha, muda mfupi baada ya kufungwa kwa ndoa yao.Meneja Mrisho na mkewe, wakiwa na wanafamilia (walioshika magazeti), wakifurahi kwa pamoja baada ya kufungwa kwa ndoa yao.Bibi Harusi, Catherine (katikati) akiwa na wanafamilia (wenye nguo nyeupe) na wafanyakazi wenzake, Women With Voices (WWV) wenye nguo za bluu.Daaab! Maharusi na wanafamilia wakiwa katika pozi maarufu kwa jina la dab!Maharusi wakiwa na wapambe wao, Said Mdoe na mkeweWakifurahia jambo baada ya kufungwa kwa ndoa yao.

  Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, jana (Jumamosi, Sept. 30,2017) alifunga ndoa ya kifahari na Catherine Mdamu, iliyolifanya Jiji la Dar es Salaam lisimame kwa muda, ikifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.Katika sherehe hiyo, wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na mkurugenzi wao, Eric Shigongo, jamaa na marafiki, walijumuika kula, kunywa mpaka kusaza na kucheza muziki mzuri, mpaka usiku sana huku kukiwa na 'special appearance' ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

  Harusi ya Abdallah na Catherine, Mlimani City - Part 1

  Harusi ya Meneja Abdallah na Catherine, Mlimani City - Part 2


  0 0


   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai akielezea jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali, Save the Children Tanzania Bi. Jasminka Milovanic
  MK1aMK2
  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali, Save the Children Tanzania Bi. Jasminka Milovanic akifafanua jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kukulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto toka WizaraMaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai.
  MK3
  Afisa Habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Anthony Ishengoma akisisitiza jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara.
  MK4.
  Mwakilishi kutoka asasi ya kiraia ya CAMFED Bi. Theresia Moyo akielezea jambo mbele ya Wahariri wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kutoka kulia ni Mwezeshaji wa Kitaifa toka Taasisi ya Tanzania Girl Guides Bi. Emiliana Stanslaus na Mwakilishi wa Room to Read Bi. Rachel Mbushi.
  MK5
  Mtaalam wa Haki za Watoto toka Shirika lisilo la Kiserikali, Save the Children Tanzania Bi. Neema Bwaira akisisitiza jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Familia toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Rose Minja.
  MK6
  Mhariri wa Habari kutoka kituo cha televisheni cha Channel Ten Bibi. Esther Zelamula akichangia mada wakati wa wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara.
  Na: Mpiga Picha Wetu.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na kiongozi na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kitabu kutoka kwa Katibu wa Malezi Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, Mahmood Hamsin, baada ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (kulia) ni. kiongozi na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  ……………………………………………………………………………….

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za kidini nchini wahakikishe wanawapiga vita watu wote wanaopanga na kutaka kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa sababu watakwamisha maenendeleo.

  Amesema Serikali inaelewa kwamba dini ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya maendeleo ya ustaarabu wa mwanadamu kwani inatoa elimu ya maadili mema yenye kuwafanya waumini waepukane na maovu mbalimbali.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Oktoka 01, 2017) wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa 48 wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya uliofanyika katika eneo la Kitonga kata ya Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam. Amesema kila Mtanzania anatakiwa ahakikishe anadhibiti matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.”Tanzania ni nchi salama na yenye utulivu, hivyo ni lazima wote tushirikiane kuitunza.”

  “Napenda niwahakikishieni kuwa Serikali inaunga mkono juhudi za Jumuiya za kidini katika kupiga vita maovu ya kila aina; mathalan utumiaji wa dawa za kulevya, wizi, rushwa, uzinzi ambao husababisha madhara mengi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.” Amesema iwapo dini zetu zitatumika vizuri tutaweza kwa haraka sana kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la ‘Hapa kazi tu’ kwani kila mtu ataepuka uzembe na kuwajibika ipasavyo.

  Waziri Mkuu amesema ana imani kwamba jumuiya hiyo kama zilivyo taasisi zingine za kidini itaendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii yetu kwa kuwapatia waumini wao na wananchi kwa ujumla elimu na maarifa ya kuboresha tabia zao na maadili yao kiroho.Amesema amani na utulivu uliopo nchini unatokana na mambo mengi ikiwemo na wananchi kupata ustawi, kuweza kufanya shughuli zao vizuri na kuwa na imani na Serikali yao, ambayo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi hususan wanyonge wanapata faraja ndani ya nchi yao.

  Waziri Mkuu amesema mambo yameweza kupatikana baada ya Serikali kupambana na rushwa na ufisadi pamoja na kuimarisha maadili ya watumishi wa umma, ambayo vimekuwa ni vyanzo vya kupotea kwa amani na utulivu katika baadhi ya nchi. “Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na ufisadi, kupitia mikataba mibovu na kuimarisha maadili ili kujenga imani kwa wananchi, kuondoa migongano na tofauti ya kipato, kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za umma, kuleta tija kwa kuongeza thamani ya huduma na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.”

  Awali, Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema Jumuiya hiyo imekuwa ikifanya mikutano kila mwaka kwa lengo la kukumbushana misingi sahihi ya dini tukufu ya kiislam pamoja na kukuza undugu wao.

  Sheikh Chaudhry amesema mkutano wa mwaka huu umejumisha watu zaidi ya 4,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wageni kutoka nchi za Uingereza, Canada, Rwanda, Uganda, Ujerumani, Kenya, Burundi, Malawi na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

  Amesema Jumuiya hiyo mbali na masuala ya kidini pia inatoa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu, maji na afya kwenye mikoa tofauti tofauti nchini.

  0 0

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akitoa zawadi kwa mmoja wa wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na wazee katika moja ya banda la Maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwapungia mkono wazee wakati wakiingia kwa maandamano kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.


  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu za Mkoa kwa Mgeni Rasmi wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 kwa Mgeni wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini Mzee Sebastian Bulegi akisoma hotuba kwa niaba ya Wazee nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017 .

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akizungumza na wazee wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017 .
  Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi (hayupo Pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

  ……………………………………………………………….

  Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

  Vijana nchini wameshauriwa kujitolea na kuwatunza wazee katika maeneo yao ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa maendeleo yao na taifa.

  Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wazee katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kila Oktoba Mosi ya kila mwaka. Mhe. Mwinyi amesema kuwa jukumu la kuwatunza na kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii pia ina nafasi yake katika kuwatunza wazee hasa Vijana.

  Mhe. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali imejitaidi sana kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za Afya na kuwatunza wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali ya wazee nchini. “Niwaombe vijana mtutunze sisi wazee kwani na sisi tulikuwa vijana kama ninyi na mkiweka utamaduni huu utawasaidia na ninyi mkiwa wazee hapo baadae” alisema Mhe. Mwinyi.

  Kwa upande wake Waziri wa Afya, MAendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Mstaafu Mhe. Mwinyi kuwa Serikali itaendelea kuwatunza wazee nchini na kuhakikisha wanapata hudumu zote muhimu. “Nikuhakikishie Mhe. Mwinyi kuwa tutaendelea kuwatunza wazee kwa kuwapatia huduma muhimu hasa huduma za Afya” alisema Mhe. Ummy.

  Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini Mzee Sebastian Bulegi amemuomba Mhe. Mwinyi kufikisha shukurani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa moyo wake wa kuwajali wazee nchini.

  “Mhe. Mwinyi naomba utufikishie shukurani zetu kwa Mhe.Rais Magufuli kwa kutujali wazee hasa kwa kutatua changamoto zetu zinazotukabili” alisema Mzee Sebastian.

  Siku ya Wazee Duniani huadhimishwa Oktoba Mosi kila mwaka kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa linalozitaka nchi wanachama kutenga siku maalumu ya kutafakari mchango wa Wazee katika maendeleo ya jamii na kuwaenzi ili wawe na maisha bora na yenye matumaini na Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “ Kuelekea uchumi wa Viwanda:Tuthamini Mchango, Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa maendeleo ya Taifa”.

  0 0

  Rais mstaafu wa awamu ya nne dk.Jakaya Kikwete ,akitoka kutembelea bweni alikuwa analala wakati akisoma shule ya sekondari Kibaha mwaka 1966-1969, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo,huku akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa pili kushoto,na viongozi wa shule ya sekondari Kibaha na shirika la elimu Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)


  Baadhi ya wahitimu wakiimba wimbo maalum katika mahafali hayo.
  Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha aliyochorwa na mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, Mkoani Pwani, wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo .

  Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akizungumza wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne ya shule ya sekondari Kibaha mkoani Pwani ,shule ambayo aliwahi kusoma mwaka 1966-1969 .

  Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi)


  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

  Rais mstaafu wa awamu ya nne ,dk.Jakaya Kikwete ,ametoa rai kwa wadau na viongozi ambao wametokea katika chimbuko la shule ya sekondari ya Kibaha;” ,Kuangalia namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa ambayo inasababisha mlundikano wa wanafunzi madarasani.

  Aidha amesema mbegu ya kuwa yeye mwanasiasa ilipandwa shuleni hapo, baada ya kuchaguliwa kiongozi wa baraza la shule kutokana na harakati zake za kutetea haki za wanafunzi .

  Dk.Kikwete aliyasema hayo shirika la elimu Kibaha ,wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha ambako alipata elimu yake ya sekondari mwaka 1966 hadi 1969.

  Alisema ,atashirikiana na wadau mbalimbali kuona namna bora ya kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa madarasa .

  Dk.Kikwete alisema , haipendezi na hajafurahishwa na hali ya miundombinu ilivyokuwa chakavu hali inayoathiri mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji .

  Rais huyo mstaafu wa awamu ya nne ,alieleza changamoto hizo si sababu ya kushindwa bali uwepo wa changamoto huongeza umakini ,bidii na ubunifu ili kukabiliana nazo .

  Alifurahishwa kusikia serikali imejizatiti kukarabati shule kongwe nchini na shule ya sekondari Kibaha ikiwemo ,;”Hivyo aliwaomba wavute subira maana kulingana na kasi ya awamu ya tano anaamini ukarabati huo hautachelea .

  Alielezea ,shirika la elimu Kibaha ni chemchem ya elimu bora ,iliyozaa viongozi bora na wataalamu wanaoliletea sifa nzuri taifa .

  Dk.Kikwete alieleza kuwa ,pia shirika hilo ni tunu muhimu iliyoachwa na muasisi na baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na nchi za Nordic .

  “Jamii ya watanzania inaendelea kushuhudia matokeo mazuri ya shule ya sekondari Kibaha katika mitihani ya kitaifa kwa kidato cha nne na cha sita “

  “Pia ushindi na tuzo katika nyanja zingine na mafanikio kwa wanajumuia ya shule hii ni ushahidi tosha kwamba ,shirika hili ni chemchemya elimu bora na iliyozalisha wanasiasa,madaktari,maprofesa ,wataalamu na viongozi wa juu” alifafanua dk.Kikwete .

  Kuhusu miradi ya uzalishaji kwenye shirika hilo ,alisema ni wazo la kulifanyia kazi ,itawasaidia kuwajengea vijana moyo wa kupenda kazi za mikono na utakuwa mtaji .

  Dk.Kikwete, aliwatakia wahitimu mafanikio mema katika mtihani wa kidato cha nne kitaifa unaotarajiwa kuanza kufanyika octoba 30 mwaka huu .

  Kabla ya shughuli ya mahafali hayo, alipata fursa ya kwenda kutembelea bweni alilokuwa akilala ,maktaba ,maabara na maeneo mengine shuleni humo .

  Awali mwenyekiti wa bodi ya shirika la elimu Kibaha, prof.Patrick Makungu ,alisema shirika linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia fani za ufundi .

  Alieleza ,shirika hilo ni taasisi ya kihuduma iliyoanzishwa miaka 54 iliyopita ,na jukumu lake kubwa ni kupigana na kushindwa maadui ujinga ,maradhi na umasikini .

  Prof .Makungu alisema mkakati wao ni kuhakikisha wanatoa wanafunzi na wanavyuo wenye maarifa ,ujuzi na nidhamu katika elimu ya msingi ,sekondari ,ufundi stadi ,mafunzo maafisa tabibu na uuguzi .

  Nae mwalimu Mkuu shule ya sekondari Kibaha,Chrisdom Ambilikile alisema shule hiyo ipo vizuri kitaaluma ambapo imekuwa ikifanya vizuri miaka 13 mfululizo sasa .

  Alisema mwaka jana walipanda ufalu kitaifa kufikia nafasi ya 16 kutoka ya 69 hivyo wanatarajia kupanda zaidi .

  Ambilikile alisema, wanatatizo la upungufu wa madarasa matano ,ambao unasababisha mlundikano wa wanafunzi katika vyumba vichache vilivyopo .

  Shule hiyo, ilianzishwa mwaka 1965 kwa msaada wa kifedha wa nchi za Nordic ikiwa na wanafunzi 110 kwa sasa ina wanafunzi 728 wote wakiume ,walimu 57 ,Na wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 116 .

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la benki ya TPB Mto wa Mbu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Profesa Lettice Rutashobya. Uzinduzi wa tawi hilo la Mto wa Mbu ulifanyika jana huko Mto wa Mbu, Arusha.

  Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa benki ya TPB Ignas Mkawe, mara baada ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo hulo Mto wa Mbu, Mkoani Arusha. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.

  Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Simbamwene kikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya TPB huko Mto wa Mbu, Mkoani Arusha.
  Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi huo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja, Ester Mfuru, wa tawi la Benki ya TPB huko Mto wa Mbu, wakati wa uzinduzi wa tawi hili. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Prof. Lettice Rutashobya.
  Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Bank Profesa Lettice Rutashobya, akikabidhi zawadi ya ngao kwa Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo lililopo Mto wa Mbu Arusha. Akitazama ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
  Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya TPB Mhe. Dkt. Philip Mpango (c) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo. Kutoka kulia waliokaa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshigi na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Profesa Lettice Rutashaobya. Kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Waliosimama nyuma ni baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo.  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Benki ya TPB mara baada ya kuwasili kwenye tawi la Benki hiyo , tayari kwa kulizindua. Kulia na Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya TPB, Sabasaba Moshingi
   
  Benki ya TPB imeendelea kusogeza huduma zao karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha.

  Lengo la kufungua tawi hilo ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na wao kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa huo waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.

  Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki yao.Alisema pia wananchi wa Arusha, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.

  ‘Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’ alisema Profesa Rutashobya.

  Alisema kwa sasa lengo lao kubwa ni kuendelea kutoa huduma bora zaidi ili kuwanufaisha wananchi wa kipato cha chini.‘TPB inaendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi kwani mbali na kufungua tawi hili, mwazoni mwa mwaka jana tulifungua matawi katika Mkoa wa Ruvuma, Kilimanjaro na Babati mkoani Manyara,’ alisema.

  Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango alisema serikali itakuwa bega kwa bega na TPB kutokana na jitihada zake za kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na hata mawakala.

  ‘Mimi binafsi na serikali tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha taasisi za kifedha nchini zinatoa msukumo unaotakiwa katika shughuli za kiuchumi nchini, ikiwemo kuwawezesha wazalishaji kuboresha ufanisi na tija kwa mambo ya msingi katika ukuaji wa uchumi,’ alisema.

  Alisema pia serikali itaendelea kutoa msukumo kwa sekta za kibenki pamoja na zingine juu ya umuhimu wa kutumia teknolojia ya kisasa katika uzalishaji na utoaji wa huduma kwa kuamini kwamba teknolojia bora huwezesha kuboresha ufanisi, kupunguza gharama na kupanua wigo wa soko.Naye Meneja wa TPB tawi la Mto wa Mbu, Selestine Mteta alizitaka taasisi mbalimbali vikiwemo vyuo, mashirika na hata shule kufungua akaunti za taasisi na TPB ili kupata huduma za kisasa na zenye gharama nafuu.

  0 0  0 0


  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

  Kampuni ya Msama Auction Mart imempongeza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kauli yake kuhusu wizi wa kazi za sanaa nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama amesema kuwa Kampuni yao imeona kuwa Waziri huyo ameonesha nia yakupoteza kabisa kazi feki za Sanaa.

  Hatua hiyo ya Waziri pia itawagusa wenye kazi zao ambao ni Wasanii wa kazi hizo ikiwemo Wasanii wa Bongo Fleva, Nyimbo za Injili, Maigizo na Filamu.

  Msama amesema kuwa doria za kumaliza wizi huo wa kazi za Wasanii inaendelea kwa nchi nzima, ambapo Mkoa mmoja tu ndiyo wenye ahueni yakupunguza wizi huo ambao ni Mwanza.

  "Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inategemea kuanza zoezi lakumaliza kazi feki za sanaa nchini, zoezi ambalo lisilokuwa na mwisho", amesema Msama.

  Pia Msama ameonya wale wote wanaofanya biashara za kuuza kazi feki, ambapo amesema kuwa watakapokamata Kompyuta za kufanyia kazi hizo basi hazitarudi tena kwa wahusika.

  Wafanyabiashara wa Filamu za Nje nao wametakiwa kuacha kufanya biashara hizo bila kibali cha mwenye kazi husika, kwani hatua hiyo inaikosesha Serikali mapato

  0 0  0 0

  Na Hamza Temba - WMU
  ....................................................................
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amepokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuagiza rasimu hiyo ifanyiwe marekebisho ya mwisho kabla ya kuwasilishwa kwa wananchi kwa ajili ya mijadala na hatua zaidi za kukamilisha rasimu hiyo.

  Alipokea taarifa hiyo juzi (Ijumaa, Septemba 29, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mjini Iringa. Aliagiza kuundwa upya katiba hiyo alipofanya ziara ya kikazi kwenye eneo la Jumuiya hiyo katika kijiji cha Tungamalenga wilayani Iringa mapema mwezi Agosti mwaka huu.

  Kufuatia ziara hiyo pamoja na taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza suala hilo alibaini mapungufu mbalimbali ya kikatiba na kuamua kutoa agizo la kuundwa upya kwa katiba hiyo  na kuvunja kabisa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo. Miongoni mwa mapungufu hayo ni katiba iliyokuwepo awali kukinzana na Sheria mama pamoja na kanuni zake.

  Katiba kutoeleza namna ya upatikanaji wa viongozi na namna ya kuwawajibisha, kutoeleza majukumu ya bodi ya wadhamini kwa usahihi na namna ya upatikanaji wa bodi hiyo pamoja na kutoleza wajibu wa wawekezaji katika jumuiya kwa jumuiya yenyewe na kwa Serikali kwa ujumla wake.

  Kubwa zaidi ambalo lilisababisha kuvunjwa kwa bodi hiyo ni jumuiya hiyo kujiendesha kwa hasara huku ikiomba fedha kwa wahisani kwa ajili ya kujiendesha wakati kimsingi asasi hiyo ilipaswa kuwa msaada mkubwa kwa wanachama wao ambao ni vijiji vinavyounda Jumuiya hiyo.

  Taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo iliwasilishwa kwenye kikao hicho na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Kissah Mbilla kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo. Taarifa hiyo ilijadiliwa na kutolewa mapendekezo mbalimbali ya kuiboresha.

  “Baada ya michango yote hii mizuri tuliyotoa hapa leo, nendeni sasa mkairekebishe vizuri izingatie maeneo yote ya msingi ikiwemo mgawanyo sawa wa mapato, kuzingatiwa kwa maeneo ya mapito ya wanyamapori na idadi ya wanachama ijumuishe vijiji vyote vilivyoanzisha Jumuiya hiyo ili kuepusha migogoro ya baadaye inayoweza kujitokeza” aliagiza Prof. Maghembe.

  Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ambaye ni alikuwa Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na Waziri Maghembe kuchunguza mgogoro huo wa MBOMIPA, baadhi ya wajumbe wa tume hiyo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Iringa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Amina Masenza.

  Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA iliundwa mwaka 2007 ikiwa wanachama ambao ni vijiji 21 vilivyopo katika tarafa ya Idodi na Pagawa kwenye halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijini mkoani Iringa. Eneo la jumuiya lina ukubwa wa kilomita za mraba 777 na linapakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

  Eneo hilo limekuwa likitumika kwa ajili ya shughuli za utalii wa picha, utalii wa uwindaji, utalii wa kiutamaduni na utalii wa kutembea kuangaliwa wanyama. Miongoni mwanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni ndege wa aina mbalimbali, mamba, tembo, nyati, swala na wengineo wengi ambao huingia na kutoka kutokea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo.  Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakati wakiagana baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo mkoani Iringa jana.  Nyuma yake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela. 
  Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo baada ya Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo. 
   Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akichangia hoja ya kuboresha rasimu ya katika mpya ya MBOMIPA katika kikao hicho.
  Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Kissah Mbilla akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya Waziri Maghembe na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Iringa.

  0 0   Mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva Khalid Mohammed 'TID Mnyama' Akiwa amebebwa juu na Mashabiki waliofia Kilimani bara wakati wa Tamasha la Mziki Mnene linaloendeshwa na Rdio ya EFM kupitia programu ya nje ndani

   Mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva Khalid Mohammed 'TID Mnyama' akiimba na Mashabiki wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
   RdJ Mamy akifanya vitu vyake katika Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
   RDJ Majey Majizo akicheza na Tantable wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
   Msanii wa Muziki wa Singeli Manfongo akiimba wakati wa  Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
   Msanii wa Bongo Fleva Shetah akiimba na Mashabiki wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
   RDJ SPUR akionesha ufundi wa kucheza na mashine wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
   Mkali wa Muziki wa Singeli nchini , Virus Mdudu akifanya mashambulizi katika jukwa la Mziki Mnene  lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
   Mtangazaji wa Kipindi cha Genge , Pido akifanya yake kwenye Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
  Mashabiki walifika katika Tamasha la Mziki Mnene  lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam

  0 0


  
           
   
  On Saturday September 30th, the Rotary Club of Bahari, Dar es Salaam will be breaking ground on anenvironmental conservation project along Barack Obama Road.
  Prof Faustine Kamuzora Permanent Secretary in the Vice-President's Office planting the tree during campaign to conserve environment along Barack Obama Road in Dar es Salaam over the weekend.  

  President Amyn Lalji plating a tree 
  Rotary Bahari Dar es Salaam President Amyn Lalji speaks to the audience during the planting trees companing
  Rotary Dar Marathon Chair Catherinerose Barretto planting a tree.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Sherif El Barbary akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kumtambulisha Mkurugenzi huyo mpya kwa vyombo vya habari uliofanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wateja wa Zantel kutarajia huduma bora zaidi na kuhaidi kuifikisha Kampuni hiyo mbali zaidi. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Joanitha Rwegasira Mrengo.
  Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Joanitha Rwegasira Mrengo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya kumtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Zantel kwa waandishi wa habari iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu mpya wa Zantel Sherif El Barbary.
  Mkurugenzi Mkuu mpya wa Zantel, Sherif El Barbary akisalimiana na Mwandishi wa gazeti la DailyNews, Abduel Elinaza wakati wa hafla ya mkutano na waandishi wa habari iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam.

  Dar es Salaam: Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu Zantel wataweza kuendana na mabadiliko ya kidunia katika sekta ya Mawasiliano kupitia mfumo ulioboreshwa wa data na sauti baada ya kumalizika kwa kazi ya uboreshaji wa mfumo mpya wa mtandao wa kisasa ili kuongeza ubora wa bidhaa na huduma kuelekea mwaka 2018.

  Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Sherif El Barbary alisema amedhamiria katika kuboresha ubora wa mtandao huo na kuwafikia wateja nchi nzima na kuenea sehemu kubwa zaidi Tanzania, kwa kutoa huduma bora na kuifanya Zantel kukua katika soko la ushindani kwenye sekta ya Mawasiliano.

  “Tunatarajia kuwafuata wateja wetu walipo na kuwapa kile wanachostahili ili kuhakikisha kwamba wanamudu gharama na kuongeza kipato kupitia malengo na dira yetu,” alisema.

  El Barbary aliongeza kuwa, Zantel ipo katika hatua za mwisho kumalizia uboreshaji wa mfumo wa mtandao na haina shaka kwamba, imekuwa kampuni ambayo inatoa huduma bora za mtandao wa data nchini katika mikoa zaidi ya 22 ambapo wanapata mfumo ulio na kasi ya 4G, huku malengo yake yakiifanya kuongoza katika soko na mfumo mpya wa kisasa na kidigitali.

  Alisisitiza kwamba Zantel itataendelea kushirikiana na Serikali ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa kila nyanja.

  “Tumetengeneza zaidi ya ajira 5,000 nchi nzima. Hizi ni zile rasmi na zisizo rasmi kupitia mfumo wa EzyPesa ambapo una takribani mawakala 2,500. Pia tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi wetu wa Zantel. Hii ni tofauti na wasambazaji wetu ambao wamekuwa wakifanya kazi na watu mbalimbali kusambaza bidhaa na huduma zetu, “aliongeza.

  Kwa upande wa huduma za kijamii, Zantel imekuwa ikishiriki kupitia M-Health ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali ambayo imekuwa ikisaidia kuimarisha sekta ya afya kwa kuboresha huduma bora za afya hususani za mama wajamzito na watoto. Kwa kuunganisha mifumo ya intaneti ya data imekuwa njia rahisi ya kutoa elimu kupitia kampeni mbalimbali.

  Zantel imekuwa ikiangazia eneo jingine ambalo ni pamoja na na kufanya biashara kwa jumla na makampuni, jambo ambalo limekuwa nyenzo muhimu kwenye biashara. Zantel inasimamia njia mbili ambazo ni EASSy & SEAS ambayo ni mifumo ya chini ya bahari ambayo imepita hadi Dar es Salaam. Mifumo hii imesaidia kuliunganisha taifa kwenye mfumo wa intaneti kwa njia ya saterite inayosaidia kusafirisha sauti na huduma za data.

  Kwa kuboresha ubora wa bidhaa na huduama pamoja na na bidhaa za Ezypesa ambayo ndiyo huduma ya kwanza kuzinduliwa ambayo iliambata na huduma ya simu ya kibenki inayofahamika Mobile Islamic Banking ambayo inashirikiana na People’s Bank of Zanzibar ambapo asilimia 85 ya wakazi wa Zanzibar wanaitegemea.

  “Hivyo tunaahidi mambo makubwa mazuri yanakuja kwa wateja wetu siku zijazo,” aliongeza El Barvary.
  BWANA SHERIF BARBARY ALITEULIWA KUWA OFISA MKUU MTENDAJI JULAI 1, 2017

  El Barbary ana uzoefu wa takriban miaka 20 kwenye sekta ya Mawasiliano, na ameshika nafasi mbalimbali za juu za utawala ambazo ni taasisi za kimataifa.

  Kabla ya kujiunga na Zantel, El Barbary alikuwa Ofisa Ufundi na Mawasiliano Tigo nchini Chad tangu mwezi Machi 2016, amefanya kazi kama msimamizi wa masuala ya mtandao na shughuli za IT na ufuatiliaji. Pia amekuwa kaimu Meneja Mkuu nchini Chad kwa miezi mitatu kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

  El Barbary amefanya kazi miaka 6 Huawei kabla ya kujiunga na Millcom akiwa kama meneja wa huduma ukanda wa Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika. Pia amekuwa kwa miaka 6 kama COO kampuni ya Glextel akihusika na usimamizi wa utoaji huduma za wireless na mtandao, ambapo alikuwa akisimamia takribani makampuni 10 yanayofanya shughuli zake Afrika na Mashariki ya Kati.

  Pia amefanya kazi na Lucent Technologies na amekuwapo kwa miaka kadhaa Amerika Kusini akifanya kazi na Kampuni ya Hewlett Packard and CML Telus ambako alipata uzoefu zaidi katika masula aya biashara akiwa kama Mkuu wa Kitengo cha Channel Operations.

  Sherif El Barbary anajaza nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Benoit Janin ambaye ameitumikia kampuni hii kwa mwaka moja na miezi 10. Zantel imekuwa ikifanya shughuli zake tangu mwaka 1999 ikiwa na hisa za asilimia 85 pamoja na asilimia 15 hisa za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  0 0

   Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala wakipunga mkono kwa wageni waalikwa wakati wa hafla yao ya kutimiza Miaka 71 ya ndoa iliyofanyika katika hoteli ya Srena Jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu maharufu na Viongozi wa kitaifa


   Naibu Waziri wa Afya nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula akimuweka Sawa mama yake wakati wa hafla ya kutimiza miaka 71 ya ndo yao mara baada ya vita kuu ya pili ya Dunia
   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi akiwa na Mkewe wakitoa pongezi kwa Mzee Sylvester Lubala mara baad ya kutimiza miaka 71 ya ndoa
    Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala wakiw akatika picha ya pamoja na watoto wao 18 wakati wa hafla ya miaka 71 ya ndoa
    Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala akiwa katika picha ya pamoja ya Mawaziri waliofika katika hafla yake ya miaka 71 ya ndoa
    Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
    Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala akigonga glass na wazee wenzie wa Tanzania Region wakati wa hafla ya kutimiza miaka 71 ya ndoa
    Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala wakijianda akula keki ya miaka 71 ya ndoa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam
    Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala akiwa katika pichaya pamoja ya Wajukuu na Vitukuu waliohudhulia hafla ya miaka 71 ya ndoa yake
   Mkurugenzi wa Dira Televisheni na Msama Promoton, Alex Msama akihojiwa na moja wa Watangazaji wa kipindi cha Chereko kinachorushwa na TBC
    Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Angelina Mabula akiwa na Wadogo zake wakati wa hfla ya kutimiza miaka 71 ya ndoa ya Baba yake
    Mkurugenzi wa Dira Televisheni na Msama Promoton, Alex Msama akiteta jambo na Mzee Gachuma wa Mwanza wakati wa hafla  hiyo
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Ally Api akigonga glasi na Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala wakati wa hafla ya kutimiza miaka 71 ya ndoa yao  0 0

  Although economic development in Zanzibar is often associated with tourism, agriculture contributes greatly to the Islands' economy and food security. In fact agriculture is the primary sources of income for roughly 70 percent of the islands’ population.

  According to KhatibJumaKhatib, the Rice Research Programme Coordinator at Zanzibar's Agricultural Research Institute (ZARI), rice is the preferred crop in Zanzibar.He also confirmed that the demand is there and that the region has the potential to grow more.

  In recent years the demand for the grain was so high that Zanzibar started to import nearly 80% of the rice it needed. Yet the farmers in the region exclaimed that they could close that gap if they had adequate agricultural extension services to guide them on the use of fertilizers and other modern technology.

  Zanzibar's Ministry of Agriculture and Natural Resources implemented aspecial strategy with a view of increasing rice production by developing irrigation systems, training farmers and introducing improved varieties of rice.

  By employing a mutation induction process, scientists are able to create a new variety of rice which is more resistant to diseases, water shortages or high level of salinity in the soil.Mutation is a natural process, but if left up to nature can take millions of years to occur. With the use of specialized equipment which emits a safe level of irradiation the process is sped up considerably.   

  With the support of the IAEA and Food and Agriculture Organization (FAO), Zanzibar has put this technique to good use and a new variety of rice known as "SUPA BC" has been introduced to the region. According to KhatibJuma, the new variety of rice is very popular because it has several advantages over other rice varieties and brings higher yields.

  In order to cultivate more and stronger varieties of rice, a special biotechnology laboratory has been set upin Zanzibar. The nuclear technology application is assisting local farmers to create modified seeds which are even moreresilient to diseases.

  By increasing the local production of rice through the introduction of improved and new varieties, Zanzibar can reduce its dependence on imports, save money and create more jobs.

  0 0

  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa masuala ya sekta ya ardhi nchini kuhusu mifumo mbalilmbali inavyotumika katika kutoa huduma kwa wananchi.

  Akifungua warsha hiyo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiluka alisema, hadi sasa wizara inatumia mfumo zaidi ya mmoja kutoa huduma za kila siku kwa mwananchi. Uwepo wa mifumo hiyo katika utoaji huduma za sekta ya ardhi ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha huduma. Ili kufikia malengo, ni lazima kuwepo na mfumo mmoja utakaounganisha mifumo yote hiyo kwa lengo la kuongeza ufanishi na kuboresha huduma.

  Uundaji wa mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (Intergrated Land Management Information System, ILMIS) unatekelezwa na Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishiriana na wataalamu kutoka kampuni ya IGN FI kwa udhamini wa Benki ya Dunia. Uundaji huu ulishaanza na kwa sasa mfumo uko katika hatua ya majaribio.

  Dhumuni kuu la uundaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi ni kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi kwa kuboresha usahihi katika taarifa za ununuzi ardhi, usajili, upimaji na pia katika kusimamia ardhi kwa ujumla wake.

  Utekelezaji wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS), utahusisha mambo mbalimbali kama vile njia rahisi na rafiki ya kusimamia uundaji na uendelezaji wa mfumo wenyewe, majaribio ya mfumo katika utekelezaji, ubadilishaji wa taarifa za ardhi zilizopo mfano taarifa za upimaji na ramani, hatimilki na kuziweka katika mfumo.

  Naye Msajili Msaidizi wa Hati, Appolo Laizer alisisitizia umuhimu wa utumiaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS) kwa wadau wa sekta ya ardhi alipokuwa akielezea jinsi hatimilki zitakavyotolewa na mfumo huo.

  Alisema, utoaji wa hati kupitia mfumo utaongeza usalama katika nyaraka za umiliki, huduma sahihi, salama na kwa unafuu zaidi. Mfumo utapunguza muda wa kuhakiki taarifa katika uhamisho wa milki kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kuongeza ulinzi kwenye maeneo yaliyotengwa kama hifadhi ya barabara, misitu au maeneo ya wazi.

  Utoaji wa hatimilki kwa kutumia mfumo utasaidia sana kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro ya ardhi kwa kulinda umiliki wa mwananchi. Pia mfumo utaondoa migogoro ya umilikishaji wa hati kwa mtu zaidi ya mmoja pamoja na kuongeza ulinzi wa hatimilki katika taasisi za kifedha.
   Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitoa ufanunuzi juu ya ujenzi wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi (ILMIS).
   Wadau wa Sekta ya Ardhi wakisiliza taarifa kuhusu mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi nchini kutoka kwa mtaalamu (hayuko pichani).
  Wadau wa masuala ya sekta ya aAdhi wakiwa katika picha ya pamoja

older | 1 | .... | 1384 | 1385 | (Page 1386) | 1387 | 1388 | .... | 1897 | newer