Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

QNET kuongeza mauzo ya moja kwa moja na kuunda fursa za ujasiriamali Tanzania

$
0
0
Kutoka kushoto, Mshauri wa bodi ya QNET David Sharma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Hamisi Kigwangalla, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk. Adelhem Meru na meneja mkuu wa QNET-Tanzania Benjamin Mariki wakikata utepe wakati wa ufunguzi wa ofisi ya shirika hilo niching mapema jana. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Hamisi Kigwangalla, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk. Adelhem Meru Mshauri wa bodi ya QNET David Sharma, meneja mkuu wa QNET-Tanzania Benjamin Mariki wakisoma gazeti lenye biddhaa za kampuni hiyo mara baada ya wa ofisi ya shirika hilo nchini. 
Mshauri wa bodi ya QNET David Sharma, akifafanua jambo mara baada ya ufunguzi wa ofisi za shirika hilo mapema jana 
Baadhi ya wafanyakazi wa Qnet wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa ofisi hiyo hapa nchini mapema jana.

IMARISHENI TAKWIMU ZA UJENZI NCHINI: PROF. MBARAWA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.


Wadau wa sekta ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mayunga Nkunya (kulia), akifafanua jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Samson Mturi akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Bw. Milton Lupa (aliyesimama), kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, jijini Dar es Salaam.
Mkadiriaji Majenzi na Msanifu Majengo Neema Kifua (wa pili kulia), akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, alipotembelea mradi huo leo, jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.

Akifungua warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba na miundombinu mingine.

“Sekta ya Ujenzi ina mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na imara.

Ameongeza kuwa mapendekezo yatakayotolewa na wadau hao yatarahisisha utekelezaji wa miundombiu mbalimbali ambayo italeta chachu kwa sekta nyingine zikiwemo za kilimo, nishati, utalii, viwanda, madini na uendelezaji wa biashara na nchi nyingine za kikanda.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ongezeko la miradi ya ujenzi imechangia Serikali kutafuta wataaalm waliofanya tafiti kwa ajili ya uboreshaji wa baraza hilo wataongeza tija na ufanisi wa sekta hii muhimu ya ujenzi kwa wadau, wananchi na Serikali.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la NCC  Prof. Mayunga Nkunya amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa baraza lake litasimamia michango yote itakayotolewa na wadau hao na kuahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili NCC ikiwemo za takwimu ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kwa kuwa ni sekta mtambuko.

Sekta ya Ujenzi ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi hapa nchini na ina mchango mkubwa kwa Pato la Taifa ambapo mwaka 2016 sekta hiyo ilichangia asilimia 14 ya Pato la Taifa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

DOKTA MPANGO AAGIZA WATUMISHI WA TRA BANDARINI DAR ES SALAAM WAFUMULIWE

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akiwa katika kikao na Maafisa Waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) alipofanya ziara ya kukagua utendaji ambapo aliwataka kuchukua hatua dhidi ya watumishi wasiowaaminifu wanaolikosesha Taifa mapato stahiki.
Meneja wa Idara ya Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bandari ya dar es Salaam, Bw. John Micah (kulia) na Meneja anaye husika na suala la Mafuta Bw. Stephen Malekano (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) alipofanya ziara Idara ya Forodha, Bandarini, Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Forodha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), bandaro ya dar es Salaam, Bw. John Micah, akifafanua jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), alipofanya ziara ya kushitukiza bandarini, Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Maafisa waandamizi wa Mamlaka ya mapato Tanzania-TRA, alipofanya ziara ya kushitukiza bandari ya Dar es Salaam na kuagiza kitengo cha ukaguzi na upimaji wa mizigo bandarini kifumuliwe baada ya watumishi wake kutofanyakazi ya kukusanya mapato ya Serikali ipasavyo
Afisa Kitengo cha Bandari Majahazi, Bw. Mahmood Makame, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) kuhusu changamoto ya elimu kuhusu masuala ya kodi kwa wateja wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kushitukiza katika ofisi hiyo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika Kituo cha Forodha Bandarini, kilichoko katika Bandari ya Dar es Salaam na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kufanya mabadiliko makubwa ya watumishi walioko katika idara ya upimaji na ukaguzi wa mizigo baada ya kubainika kuwa baadhi yao wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na upotevu wa mapato ya Serikali.

Dokta Mpango ametoa muda wa siku saba kwa TRA kumpa taarifa kamili ya utekelezaji wa maagizo hayo, ikiwemo kuwahamisha watumishi wote waliokaa muda mrefu kwenye eneo hilo la upimaji na ukaguzi wa mizigo ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali katika Bandari hiyo.

Ameshangazwa na kitendo cha Mapato katika Bandari ya Dar es Salaam kutoongezeka licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, kuboresha Bandari hiyo kutokana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kushirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi ya serikali.

“Pamoja na kuwepo kwa mitambo ya kukagua mizigo (Scanners), baadhi ya bidhaa zinakadiriwa kodi ndogo ikilinganishwa na thamani ya mizigo huku mizigo mingine ikiwa si ile iliyotajwa kuwemo kwenye makontena na hupitishwa na watumishi wasio waaminifu” alisisitiza Dokta Mpango.

Aidha, Waziri huyo wa Fedha na Mipango ameuagiza ungozi wa TRA kuhakikisha kuwa wanaongeza mapato katika bandari ya majahazi kutoka wastani wa mapato ya shilingi bilioni 3.5 kwa mwezi hadi shilingi bilioni 5, kulingana na malengo yaliyowekwa baada ya kubainika kuwa kuna ukwepaji mkubwa wa mapato ya Serikali katika eneo hilo.

Dokta Mpango ameuambia uongozi huo wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kuhakikisha kuwa Bandari ya Majahazi ianze mara moja kutumia mfumo wa kukusanya mapato ujulikanao kama TANSIS ili kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi.

Aidha, ameviagiza vyombo vya dola kuwachunguza watumishi wote wakiwemo wa ngazi za juu katika idara ya forodha bandarini na kuwachukulia hatua kali wale wote watakao bainika kujihusisha na vitendo vyovyote vinavyoikosesha Serikali mapato yake.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 23,2017

WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA TAWI LA KAMPUNI YA MABATI ALAF DODOMA

$
0
0
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage Septemba 9, 2017 alifungua tawi la Kiwanda cha mabati ALAF katika mkoa wa Dodoma eneo la Kizota kitalu namba 148.

Kufunguliwa kwa tawi hili katika mkoa wa Dodoma ni kutokana na maamuzi ya serikali  kuamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa vitendo  na  kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais John Magufuli katika “ USHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA TAIFA”.

Kufunguliwa kwa tawi hili  kutaimarisha maendeleo ya mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani.

Wateja kutoka Dodoma na Singida  sasa wataweza  kupata suluhisho la mahitaji ya bidhaa za uezekaji kutola ALAF.

Tunauza  bidhaa zilizo tayari kwa matumizi kulingana na mahitaji ya mteja hasa mabati ya rangi  pamoja na kutoa ushauri wa kiufundi na kiutaalamu.

Kwa sasa kiwanda chetu cha ALAF kina matawi manne Mbeya, Mwanza, Arusha na Dodoma.

Kuhusu kampuni ya ALAF
Kampuni ya ALAF ni sehemu ya kampuni ziliyoko chini ya Kampuni   ya SAFAL, kampuni inayoongoza bila mpinzani ktika utoaji wa bidhaa bora za uezekaji barani Afrika.Kampuni ya SAFAL inaendesha shughuli zake katika nchi 13 kuanzia mashariki,kati na kusini mwa bara la Afrika.

Tukiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika biashara, ALAF tunaongoza  katika uzalishaji  wa bidhaa za  uezekaji za chuma.Katika kuongezea bidhaa zake za upauaji, bidhaa za kitaalamu pia zinauzwa na ALAF kama misumari (fixtite fastener), steel pipes, na Hollow section pamoja na viambatanisho muhimu kwa uezekaji.

Baadhi ya bidhaa zinazotolewa na ALAF ni Lifestile, Romantile, Versatile, Tekdek (It5), Resincot na Simba Dumu.
Wasilana nasi kwa namba hizi  Dar es Salaam- O768 555 560, Arusha - 0763 707 071, Mbeya - 0765 555 560,  Dodoma - 0764 131442  na Mwanza 0682 808 080. 

Tunapatikana pia kuitia mitandao ya kijamii Facebook -Alaf Limited na Instagram - Alaf Limited.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage akifungua tawi la kampuni ya mabati ya ALAF  Dodoma. Kushoto ni meneja mkuu Upauaji  (roofing) wa Kampuni ya mabati  ALAF, Dipti Mohanty  akishuhudia ufunguzi huo.

ONYESHO LA COKE STUDIO LAZIDI KUMPAISHA MAFANIKIO YANGU - ALI KIBA

$
0
0
Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema moja ya mafanikio anayojivunia nayo katika kazi ya muziki kwa mwaka huu ni ushiriki wake tena katika onyesho la Coke Studio msimu wa mwaka huu. Ali Kiba ambaye amefanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki nguli kutoka Nigeria, Patoranking, amesema katika mahojiano hivi karibuni kuwa anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki kwenye msimu wa tano wa Coke Studio unaoendela ambapo kwa hapa nchini onyesho lake linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni. 

Anasema ushiriki wake kwa mara ya moja ya kwenye mafanikio kwani rekodi yake imezidi kuongezeka katika anga la kimataifa na ameweza kujiongezea washabiki ambao wanafuatilia shindano hili kupitia luninga,vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Mbali na kuongelea mafanikio ya kupata washabiki amesema kuwa amefurahi kufanya kolabo na msanii wa nje ya nchi kwa kuwa ameweza kujifunza mengi kupitia ushiriki wake kwenye Coke Studio.
“Jambo lingine ambalo naliona ni kubwa kama msanii ni kukubalika kufanya kazi na kampuni kubwa kama Coca Cola kazi hii imenifanya nizidi kujiongezea mashabiki na umaarufu wangu kuongezeka”Alisema. Alisema onyesho la Coke Studio linadhihirisha kuwa muziki wa Bongo Fleva unazidi kukua na kuwa maarufu sehemu mbalimbali barani Afrika kutokana na jinsi linavyofuatiliwa na idadi kubwa ya watu hususani vijana. 

Aliwataka wanamuziki wachanga wanaochipukia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanapata mafanikio na kuongeza kuwa mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi na makampuni makubwa ya biashara mojawapo ikiwa ni kushiriki kwenye maonyesho makubwa kama haya. “Fani ya muziki inazidi kukua kiasi kwamba wakati wa kufanya muziki wa ndani tu imekwisha na inabidi kuvuka mipaka na kolabo kama hizi za Coke Studio zinasaidia kupata uzoefu na kufungua milango ya mafanikio”.Alisema. Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao yuko nao katika msimu wa Coke Studio mwaka huu.Wanamuziki hao ni , Rayvanny, Izzo Bizness, na Nandy.

CRC yazinduwa mradi wa utoaji huduma za msaada wa kisheria

$
0
0
KITUO cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC kimezinduwa mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, yaani Kinondoni na Ubungo.

Akizungumza na wadau wa mradi huo yaani baadhi ya wasaidizi wa sheria, maofisa ustawi wa jamii, wanasheria, mahakimu, Askari Polisi Dawati la Jinsia, maofisa watendaji wa mitaa kutoka wilaya za Kinondoni na Ubungo, Mwenyekiti wa CRC, Saida Mukhi aliwataka wadau hao kushirikiana ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinakomeshwa na kupungua.

Alisema lengo la mradi huo unaofadhiliwa na shirika la Legal Service Facilities (LSF) ni kuhimarisha zaidi upatikanaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Aliongeza kuwa mradi huo utajikita zaidi katika utoaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa waathirika na kuhakikisha mfumo wa upatikanaji wa haki unafanya kazi vizuri.

“…wadau katika maeneo hayo mnatakiwa kuhakikisha tunapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na wahusika kunyimwa uhuru,” alisema Bi. Saida Mukhi akifungua warsha ya wadau hao.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo akifafanua zaidi kwa washiriki wa semina hiyo alisema mradi huo utaendeshwa katika Kata za Makumbusho na Kawe kwa Wilaya ya Kinondoni huku kwa Wilaya ya Ubungo utajikita kwenye Kata ya Saranga.

Alisema CRC itashirikiana na wadau katika maeneo hayo kuhakikisha inapiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vimekuwa na madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii na mara nyingine kuwanyima uhuru.
Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni na Ubungo. Kulia ni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo.Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Ofisa Mradi wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Suzan Charles akitoa ufafanua juu ya mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam.Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi akichangia mada.
Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya Saranga).Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya Saranga).Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa na mgeni rasmi Bi. Saida Mukhi.

WAZIRI MBARAWA ALITAKA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI KUAANISHA GHARAMA ZA UJENZI WA MIRADI YAO

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku moja ya wadau wa sekta ya ujenzi iliyohusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam jana.
  Mwenyekiti wa Baraza hilo Mayunga Nkunya (wa tatu kushoto) akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa baada ya kutoa hutuba yake.
 Mwenyekiti wa Baraza hilo Mayunga Nkunya, akitoa hutuba katika semina hiyo.

 Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo wakimsikiliza Wziri Mbarawa.
 Wadau wa sekta ya ujenzi.
 Taswira ya ukumbi wa semina.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameliagiza Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kuhakikisha linaanisha gharama za Ujenzi wa miradi mbalimbali badala ya kutegemea makadilio ya Wakandarasi wanaopetekeleza miradi. 

Alisema hayo Jijini Dar es salaam jana wakati akifungua Semina ya Wadau wa Ujenzi iliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi ambapo amesema kutokan na utaratibu mbovu uliopo hivi sasa Watanzania wanatumia hata vifaa visivyokuwa na ubora wowote. 

"Sekta ya ujenzi ina mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa na huwezesha utekelezaji wa miundombinu mbalimbali kuimarika na kuwa kichocheo  kikubwa kwa sekta nyingine za kiuchumi ikiwe kilimo,utalii nishati na viwanda" alisema Mbarawa. 

Mwenyekiti wa Baraza hilo Mayunga Nkunya amemhakikishia Waziri huyo kuwa changamoto zote zilizopo kwenye Sekta hiyo zitajadiliwa katika Semina hiyo na kupatiwa majibu ili kuepusha hasara na athari ambazo zinaweza kulikumba Taifa endapo hatua hazitachukuliwa. 

Alisema changamoto ambazo waziri amewapa amezitoa kwa baraza watazisimamia vizuri na kuhakikisha viwango vya ujenzi vinatekelezeka kwa lengo la kuimarisha  ubora wa majengo na miundombinu kwa ujumla. 

Aliongeza kuwa kutokana na kukosekana kwa Ushirikiano kutoka kwa wadau wa Ujenzi ndio sababu za changamoto hizo kujitokeza hivyo kupitia mkutano huo anaamini watafungua sura mpya ya maendeleo katika sekta hiyo na taifa kwa ujumla.



SALAMU ZA SHUKRANI NA MWALIKO WA HITMA YA MAREHEMU HAJAT MWL. BATOUL ABDALLAH MBAROUK

$
0
0
Familia ya Alhaj Sudi Suleiman Madega, Katibu Mkuu (Mst) Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).

Inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msaada wa hali, mali na faraja walioipatia familia katika kipindi kigumu cha kuuguza, msiba na hatimaye kumpuzisha kwenye nyumba yake ya milele mpendwa wao Hajat Mwalimu Batoul Abdallah Mbarouk aliyefariki tarehe 16 Agosti, 2017 na kuzikwa tarehe 17 Agosti, 2017. 

Hajat Batoul A. Mbarouk alikuwa Mke wa Sudi S. Madega; na Mama wa Suleiman, Amir, Dr. issa, Maryam, Zuhura na Asha Madega. Pia, Mkwe wa Maryam Hamza Chum, Nuru Kassim Kisesa, Daud Buswelo na Hawa Kadyanji.

Kwa kuwa ni ngumu kumshukuru kila mmoja, itoshe kusema ahsanteni sana nyote. Hata hivyo, kipekee familia inapenda kufikisha salamu maalum kwa wafuatao:-
             i.        Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ya Ocean Road ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwaka huu mwanzoni na hatimaye kuaga dunia tarehe 16 Agosti, 2017. Hususa, Dr. Steve, Dr. Kezia , Dr. Mathew, Dr. Chacha, Dr. Ruta  Dr. Abdi Sangali , Sister Sapine,  Sister Wema , Sister Ester , Sister Doris , Sister Kimath , Sister Eliza , Joel Makanyaga, Mkulia, Alawi, Solomon na wengine wote;
            ii.        Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwezi Agosti, 2016;
           iii.        Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais (Mst) wa Jamhuri Muungano wa Tanzania na mkewe Mh. Mwl. Salma Rashid Kikwete (Mb) na familia yao;
          iv.        Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU);
            v.        Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT). Hususan, Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa wa Pwani na Walimu wote;
          vi.        Mh. Jaji (Mst) Harold R. Nsekela (Kamishna wa Maadili), Uongozi na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
         vii.        Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg. Kailima Ramadhani na Mkurugenzi wa Utawala Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndg. Hamis A. Mkunga;
        viii.        Alhaji Masoud Msangi, Mkurugenzi Mtendaji Nduvini Auto Works;
          ix.        Majirani wa marehemu wa Mbagala, Mbezi na Chang’ombe;
            x.        Vile vile, tunapenda kutambua familia zifuatazo:-
Ukoo wa Kanyama na Mbarouk popote pale walipo, Familia ya Mh. Luteni (Mst) Abdallah Kihato, familia ya Mh. Mohamed S. Jegame, familia ya Marehemu Balozi Isaya Bakari Chialo, familia ya Dr. Hamza Juma Chum, familia ya Brigedia Jenerali (Mst) Ussi Khamis wa Zanzibar, familia ya Kassim Kisesa, familia ya Masoud Sultan, familia ya Bakari O. Sangali, familia ya Issa Sechonge, familia ya Kisarazo, familia ya Idris Mavura, familia ya Marehemu Mwl. Hemed Ally Kimeah, familia ya Mbaruku Nguzo, familia ya Mbegu na wengine wote.

Pamoja na salamu hizi, familia inawaarifu na kuwaalika rasmi katika Arobaini ya Marehemu Mwalimu Mbarouk itakayofanyika nyumbani kwake Mbagala siku ya jumapili tarehe 24 Septemba, 2017 kuanzia saa 5 asubuhi mpaka 8 mchana.

Kwa mawasiliano tafadhali wasiliana na Ndg. Amir Sudi Madega kupitia Namba 0716875737.

Innalilahi Wainailahi Rajioun,
Ahsanteni Sana

UJUMBE KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WATEMBELEA MIGODI YA WACHIMBAJI WADOGO MKOANI SINGIDA.

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi (katikati) akiongea na ujumbe wa Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais walipomtembelea Ofisini kwake kwenda kujitambulisha kabla ya kuanza ziara ya kutembelea Wachimbaji wadogo wadogo katik Mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga(wa mwisho kushoto) toka Ofisi ya Makamu wa Rais wakipata maelezo jinsi Wachimbaji wadogo wanavyoingia kwenye mashimo kwa kutumia kamba kutoka kwa Kiongozi wa Mgodi wa Wachimbaji wadogo wa Mpipiti katika Wilaya ya Singida Vijijini Bwana Geston Ali.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga akiangalia jinsi dhahabu inavyochujwa kutolewa katika udongo kwa kutumia maji katika mgodi mdogo wa Mpipiti uliopo wilaya ya Singida Vijijini.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji (katikati) , Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga pamoja na Afisa Afya Mazingira Bi Suzan Nchala wakionyeshwa na Bwana Athman Mrisho (Mkurugenzi wa mgodi) jiwe linakuwa kabla ya kuingizwa kwenye mashine kwa kuvunjwavunjwa katika mgodi mdogo wa Sekenke wilayani Iramba mkoani Singida.


…………………………………………………………………………………


Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bibi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wamefanya ziara katika migodi ya Mpipiti pamoja na Sekenke iliyopo katika Wilaya ya Singida vijijini na Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.

Dhumuni ni ziara hiyo ni kujifunza na kuangalia kwa ukaribu jinsi Wachimbaji hao wanavyofanya shughuli zao za kila siku hususan katika suala zima la mazingira. Wakiwa aktika ziara hiyo waliongea na Viongozi wa Wachimbaji hao wadogo na kujionea shughuli hizo za uchimbaji katika migodi hiyo zinavyokwenda. Viongozi hao wa Wachimbaji walitoa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika uchimbaji ikiwemo miundombinu mibovu , umeme na garama za ukodishaji wa mashine za kuvutia maji(pampu) na kompresa.

Kabla ya kuanza ziara hiyo ujumbe huo ulipata nafasi ya kumtembelea Katibu YTawala wa Moa wa Singida Dkt. Angela Mageni Lutandula Ofisini kwake na kujitambulisha na kumweleza dhumuni la safari yao mkoani humo. Akiongea Katibu Tawala aliwakaribisha Wajumbe hao mkoani Singida na kuwasititiza wakajionee wao wenyewe shughuli hizo za uChimbaji wa madini kwa Wachimbaji wadogowadogo mkoani kwake.

SERIKALI YADHAMIRIA KUFIKISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJI VYOTE NCHI NZIMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigalla King (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Kweinsewa kilichopo kata ya Nkolamo, wilaya ya Korogwe Vijijini mkoani Tanga wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa minara na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwenye vijiji.
Bibi Mwanafuraha Nyange, mkazi wa kijiji cha ziwa Jipe kilichopo Kata ya Jipe wilaya ya Mwanga kwenye mkoa wa Kilimanjaro akieleza umuhimu wa mawasiliano vijijini kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara yao ya kukagua ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu na wakazi wa kijiji cha ziwa Jipe kilichopo wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Norman Sigalla King.


…………………………………………………………………


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kufikisha huduma za mawasiliano kwenye vijijini vyote nchi nzima na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wote, kwa wakati, uhakika na muda wote.


Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga wakati wa ziara iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia UCSAF ya kuwapeleka wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kukagua maendeleo ya ujenzi wa minara ya simu za mkononi, hali ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi na changamoto zilizopo kwa wananchi wa maeneo husika. Wakiwa kwenye ziara hiyo kata ya Jipe iliyopo Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro Eng.

 Ulanga amesema kuwa mnara wa Vodacom uliojengwa kwenye eneo hilo unahudumia zaidi ya wananchi 1,200 kwenye vijiji zaidi ya nane. Hadi hivi sasa UCSAF imejenga minara ya simu za mkononi kwenye maeneo saba yaliyopo Wilaya ya Mwanga na Same mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na kampuni za simu za mkononi. Vile vile, Kamati imetembelea minara iliyopo kata ya Nkalamo iliyopo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Eng. Ulanga ameongeza kuwa Serikali kupitia UCSAF inaendelea kutoa ruzuku kwa kampuni za simu za mkononi ili ziweze kufikisha mawasiliano kwenye vijiji vyote nchi nzima ambapo hadi hivi sasa UCSAF imetoa jumla ya dola za marekani milioni 41.5 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 93.3 kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini kwenye kata 518 ambazo zitajengwa minara ya mawasiliano. Mpaka sasa jumla ya kata 391 kati ya kata 518 zimefikishiwa huduma ya mawasiliano katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwezi Machi 2013 mpaka mwezi Agosti 2017 mwaka huu.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara ya mawasiliano vijijini kwenye Wilaya ya Bahi, Chamwino mkoani Dodoma na Gairo kwenye mkoa wa Morogoro, ameziagiza kampuni za simu kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano vijijini zinapatikana masaa yote 24, siku saba za wiki na katika kipindi cha mwaka mzima bila kukatika, kwa uhakika na kwa wakati wote. 

Hali ya ukosefu wa mawasiliano kwa nyakati za usiku imekuwa ikijitokeza kwenye baadhi ya maeneo ya vijijini ambako hakuna nishati ya uhakika ya umeme ambapo kampuni za simu zinatumia umeme wa jua kuendesha minara ili iweze kutoa mawasiliano kwa wananchi.

 Hali hiyo imedhihirishwa na wananchi wa kijiji cha Kweinswa, waishio kata ya Nkalamo iliyopo Wilaya ya Korogwe Vijijini mkoani Tanga ambapo mzee Kajembe Kijarala ameiambia Kamati kuwa changamoto hiyo wanaipata wanakijiji kwa nyakati za usiku hasa wakati wa kipindi cha masika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King amesema kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia Kamati yake itaendelea kuhakikisha kuwa Serikali inafikisha huduma za mawasiiano vijijini kwa wananchi wote mikoa mbali mbali. Prof. King amesisitiza kuwa wananchi wa vijiji mbalimbali kulikojengwa minara ya simu za mkononi washirikiane na kampuni za simu kulinda miundombinu ya mawasiliano ili waendelee kunufaika na uwepo wa minara hiyo kwenye makazi yao.

Nao wananchi wanaoishi kwenye makazi hayo wamesema kuwa uwepo wa minara ya simu za mkononi imewawezesha kupata huduma mbali mbali za mawasiliano ikiwemo kurahisisha mawasiliano baina yao, kutuma na kupokea pesa, kupeana taarifa za ugonjwa na misiba na kutumia kama huduma za kibenki. 

“ Mawasiliano yanashika kila siku, hamna tatizo lolote, Serikali imefanya vizuri kuweka mnara badala ya wananchi wa Jipe kwenda mbali mpaka Moshi au kutumia mnara wa Ugweno, nikiwasiliana na simu mara moja naenda hapo SACCOSS natoa hela,” amesema Bibi Mwanafuraha Nyange, mkazi wa kijiji cha Ziwa Jipe, kata ya Jipe iliyopo Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha, ujenzi, usimikaji wa minara na ufiishaji wa huduma za mawasiliano vijijini zimekuwa zikifanywa kwa pamoja kati ya Serikali na kampuni za simu za mkononi ikiwemo Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Airtel, MIC TIGO, Vodacom, Zantel na Halotel. Kampuni hizi zinapatiwa ruzuku na Serikali kwa njia ya ushindani na wao kuongeza fedha zao kukamilisha ujenzi wa minara na ufikishaji wa huduma za mawasiliano vijijini na kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara. 

Changamoto zinazoyakabili maeneo ya vijijini ni idadi ndogo ya wakazi, uwezo mdogo wa kifedha wa wakazi wa eneo husika kwenye matumizi huduma za mawasiliano vijijini (ARPU-Average Revenue Per User), ukosefu wa nishati ya uhakika ya umeme na barabara. UCSAF imeanzishwa kwa sheria ya Bunge Na. 11 ya mwaka 2006 kwa lengo la kufikisha mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 apatikana jijini Mwanza

$
0
0

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza, Fatuma Msafiri akiimba wakati wa kumtafuta mkali wa kipaji cha kuimba jijini Mwanza
Msanii Chipukizi Lusinde Michael a.k.a Real Da Best akionesha umahiri wake wa kufoka foka kwenye mchuano wa kusaka kipaji cha Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 jijini Mwanza

Top 2 wakisubiri kutajwa kwa mshindi kati yao.
Majaji wakijadiliana jambo.
Wasanii walioingia Top 4 wakisubiri mchujo wa kuingia top 2.

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza akibubujikwa na machozi ya furaha mara baada ya kutangazwa kushinda shindano la kusaka vipaji vya kuimba Supa Nyota msimu huu wa Tigo Fiesta 2017, Pembeni mshindi wa pili Lusinde Michael a.k.a Real Da Best.
Sehemu ya umati uliojitokeza kushiriki Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 jijini Mwanza.

Majaji wakiongozwa na Nickson wakiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza Fatuma Msafiri.

MKUU WA MKOA WA TANGA APOKEA VIFAA TIBA KUTOKA KWA UZALENDO KWANZA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mapema jana mjini Tanga. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - TANGA. 

 Vifaa vilivyotolewa na wasanii na wachezaji hao katika uwanja wa Tangamano ikiwa ni Kampeni ya Uzalendo kwanza ni pamoja na Ultra Sound, mashine ya X- Ray, Wheel Chair, Magongo ya walemavu na craches. Shigella amepokea vifaa hivyo ikiwa ni moja ya Kampeni ya UZALENDO KWANZA ambayo inaongozwa na wasanii na wacheza mpira ikiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuchangia maendeleo ya nchi. Ambapo vifaa hivyo vinagawiwa katika hospitali za Ngamiani, Makorola, Pongwe na Mikanjuni. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akitokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Vijana wazalendo wa UZALENDO KWANZA wakibeba vifaa Tiba ambavyo walitoa kwa ajili ya hospitali za mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella aliwataka wasanii na wacheza mpira hao kuhakikisha wanatumia umaarufu walionao ili kuweza kuwavutia wawekazaji kutoka nje ya nchi ili kukuza uchumi wa nchi.

"Wasanii mnadhamana kubwa ya kuhakikisha mnatumia vema vipaji vyenu ili kuweza kusaidia juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda kwa wao kuvutia wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza katika nyanja mbalimbali." alisema "Ninatambua asilimia kubwa mlizunguka kwenye kampeni mkiwaomba watanzania wamchague Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na dhamira yake nzuri ya kuletea maendeleo lakini pia hivi sasa mnashirikiana naye kwenye sekta ya afya kwa kumuunga mkono kwa kutoa mchango wenu niwaambie huu ni uzalendo ambao ni msingi wa maendeleo ya Taifa""Kwa mfano Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na wazee wengine walipigania Taifa hii kwa sababu ya uzalendo na ndio maana mnaona Rais wetu namna anavyopambana kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa na kutunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadae kwa lengo la kila mtanzania kuweza kunufaika nazo "
Wananchi wakifuatilia wakati halfa ya ugawaji wa vifaa tiba. Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, akiwashukuru UZALENDO KWANZA kwa jinsi walivyoweza kujitoa kwa hali na mali vifaa tiba kwa hospitali za mkoa wa Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa akitoa msisitizo kwa wasanii wa Tanga kuwa na moyo kama wa UZANDO KWANZA wa kuweza kujitoa kwa moyo mmoja wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. 
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. 
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere akieleza machache wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.Akikabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Kampeni ya UZALENDO KWANZA, Steven Mengele 'Nyerere' alisema uzalendo kwanza imemaua kuchangia vifaa tiba kwa hospitali ya Tanga na kwamba kampeni hizo zitaelekea mikoa mingine mbali mbali ikiwemo Lindi na Mtwara, Dodoma, Arusha, na Mwanza.
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere akiwatambulisha baadhi ya wazanii ambao wanaunda UZALENDO KWANZA.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella akimtunza msanii wa UZALENDO KWANZA ambaye alikuwa akitoa burudani.
Meza kuu ikifuatilia tukio wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Mhe. Thobias Mwilapwa na mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. Kutoka kulia ni mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa na mwishoni kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi.
Wasanii wa UZALENDO KWANZA akitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akisalimiana na Msanii Ruby ambaye ni mmoja ya wana UZALENDO KWANZA wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere.
UZALENDO KWANZA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vifaa tiba.. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa (wa kwanza kushoto), Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi (mwenye tisheti ya mistari) pamoja na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere  wakati akipokea vifaa tiba kutoka kwa UZALENDO KWANZA ambao wametoa vifaa tiba.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizindua kampeni ya upandaji miti ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo Septemba 23,2017-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack amezindua kampeni ya upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ili kuboresha mazingira Shinyanga na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa. 

Kampeni hiyo inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, imezinduliwa leo Jumamosi Septemba 23,2017 katika manispaa ya Shinyanga ,kwa lengo la kuboresha mazingira ya mji wa Shinyanga,maeneo ya taasisi,maeneo ya wazi,maeneo yanayozunguka kaya,kandokando ya barabara na sehemu zingine ambazo hazina miti. 

Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hiyo,Telack alisema kutokana na mvua haba katika mkoa wa Shinyanga, kumekuwepo na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha kuwepo na hali ya jangwa. Telack aliwataka wananchi na wadau wote kuhakikisha wanatunza miti hiyo na kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani. 

“Tutakuwa wakali,kuanzia sasa ni marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=”,alieleza mkuu huyo wa mkoa. 

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro alisema uzinduzi wa kampeni hiyo umeanza na barabara 25 za mji wa Shinyanga ambapo jumla ya miti 3000 imepandwa na ofisi zote kata 17 za manispaa ya Shinyanga zitaendelea kutekeleza zoezi hilo. 

“Kampeni hii ni kwa wilaya ya Shinyanga,leo tumeanza katika manispaa ya Shinyanga,tunataka wilaya yetu iwe na mandhari nzuri ya kuvutia,ardhi iboreke,tuzuie upepo mkali katika majengo,tuhifadhi vyanzo vya maji,kuongeza vivuli katika maeneo ya kupumzikia,kujinasua na athari za mabadiliko ya tabia nchi lakini pia jamii itanufaika na miti ya matunda itakayopandwa”,alifafanua Matiro. Alibainisha kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,sasa wilaya hiyo imekuja na teknolojia rahisi ya kumwagilia miti kwa njia ya matone,teknolojia ambayo inatumia maji kidogo lakini inaweza kumwagilia miti mingi na kwa muda wote. 

“Tumekuwa tukipanda miti kila mwaka lakini miti hii ilikumbwa na changamoto nyingi wakati wa usimamizi na kusababisha miti mingi kufa,kwa sasa tumekuja na mpango huu mpya wa kupanda miti itayosimamiwa na wananchi na wadau wote”,alieleza Matiro. Alisema kauli mbiu hiyo ya Upandaji miti ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ina maana ya kuwaasa watu wote wa Shinyanga kuachana na tabia ya kuharibu miti na hivyo wahifadhi miti. 

“Tutatekeleza kampeni hii katika halmashauri zote,kila halmashauri itaanzisha kitalu na kuzalisha miche isiyopungua 25,000,kila kata ipande miti isiyopungua 1000 na iwe na kitalu cha kudumu,ofisi za mitaa na vijiji miti 100,vitongoji miti 50,kila mwananchi miti isiyopungua mitatu na taasisi zote zipande miti”,alifafanua Matiro.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha kampeni hiyo,taasisi mbalimbali zitachangia mbegu,miche na kupanda miti ili kufikia lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1,500,000 kwa mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya upandaji miti ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro wakati wa uzinduzi huo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya upandaji miti ambapo alisema miongoni mwa malengo yake ni kuhifadhi ardhi na kuiongezea thamani,kuzuia mmomonyoko wa adhi na kuboresha mazingira
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.Alieleza kuwa kila kiongozi akialikwa kwenye tukio lolote,kabla ya shughuli ni vyema kwanza apande mti.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akisisitiza kuwa kampeni hiyo inalenga kujinasua na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Wananchi wakiwa wameshikilia vijiti vinavyotumika katika zoezi la upandaji miti.
Uzinduzi unaendelea
Mdau wa Mazingira Ezra Manjerenga akieleza namna ya kupanda miti hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akipanda mti nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakishuhudia mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akipanda mti.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akichomeka vijiti kwenye mti aliopanda.
Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui akipanda mti nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 'Shinyanga mpya,mti kwanza'.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB na wananchi wakishuhudia Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui akipanda mti.
Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui akishindilia udongo kwenye mti alioupanda.
Wananchi wakitoka katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakielekea kwenye barabara mbalimbali mjini Shinyanga kwa ajili ya kupanda miti.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akiweka udongo kwenye mti alioupanda nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiwa katika ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akichimba shimo kwa ajili ya kupanda mti katika barabara ya Hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Mwananchi akifurahia baada ya kumaliza kupanda mti katika Barabara ya Shinyanga - Mwanza.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 24,2017


TAMASHA LA TULIA TRADITIONAL DANCES FESTIVAL 2017 TUKUYU MBEYA

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wakicheza pamoja na wasanii wa kikundi cha Ngoma cha Wasonjo kutoka Ngorongoro, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Masebe Rungwe, wakicheza jukwaani wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Keifo Kyela, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Kanengwa, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Lipango Mbozi Mkoa wa Songwe, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
Majaji wa shindano la ngoma Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, wakifuatilia burudani zilizokuwa zikiendelea jukwaani wakati wa Tamasha hilo kwenye Uwanja wa Tandale, Tukuyu. Picha na Muhidin Sufiani
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Lipango Mbozi Mkoa wa Songwe, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
Wasanii wa kundi la kughani mashahiri ya Asili, Mwandurusa kutoka Kyela, wakighani mashahiri yao jukwaani wakati wa Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia) akiwaongoza baadhi ya viongozi na wadau kucheza Kwaito jukwaani wakati wa Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani
Mwanadada maarufu wa kuchezea mpira,Hadhara Charles, akionyesha umahiri wake jukwaani wakati wa Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akimtunza fedha mwanadada, Hadhara Charles, maarufu wa kuchezea mpira,baada ya kuonyesha umahiri wake jukwaani katika Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Wasonjo kutoka Ngorongoro, wakicheza ngoma yao ya asili wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
Waratibu wakimsindikiza msanii wa filamu nchini Senga, wakati akiwasili uwanjani hapo na ‘kuchafua hali ya hewa’ baada ya kuanza kufuatwa na wananchi kila alikopita kiasi cha kumzuia njia asipite kuingia eneo maalumu waliloandaliwa wasanii wenzake. Picha na Muhidin Sufiani

UJUMBE KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA MIGODI MKOANI TABORA.

$
0
0
  Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga na Afisa Mazingira Bi Suzan Nchala wakiangalia sehemu ambapo mawe yaliyopondwa husafishwa ili kupata dhahabu walipotembelea mgodi wa Igulubi wilayani Tabora.
Mmiliki wa mgodi mdogo wa Igulubi Bwana Steven Siyame akiwaonyesha wajumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais waliofanya ziara katika mgodi huo uliopo Igunga Tabora jinsi mashine ya kuvunjia mawe inavyofanya kazi( haipo pichani).
 
 Mkurugenzi  wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wakiangalia mashine  ya kuingia shimoni inayotumiwa na Wachimbaji wadogo wa mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
 Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wakionyeshwa na Afisa madini kanda ya Taabora Injinia Kasweke aina za mawe  yenye dhahabu yanayopatikana katika Mgodi mdogo wa Igulubi wilayani Igunga mkoa wa Tabora.


Wachimbaji wadogo wa migodi wametakiwa kutunza mazingira katika maeneo yote yanayozunguka migodi pamoja na usalama kwa Wafanyakazi katika katika migodi hiyo. Rai hiyo imetolewa na ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ulipotembelea mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora katika ziara inayofanywa na Ujumbe huo wa kutembelea migodi ya Wachimbaji wadogo.

Wakiongea katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Bi Magadalena Mtenga walisema kuwa utunzaji wa mazingira ni kitu cha muhimu sana na pia usalama kwa Wafanayakazi katika migodi hiyo ni muhimu pia. Walimshauri Mkurugenzi wa mgodi huo Bwana Steven Siame kuwa karibu na Taasisi za Serikali ili kuweza kufahamu mambo yote yanayotakiwa katika suala zima la uchimbaji ikiwemo Baraza la Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya kujua kanuni za utunzaji wa mazingira.

Ujumbe huo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais upo katika ziara ya kutembelea migodi midogo inayomilikiwa na Wachimbaji wadogo kwa ajili ya kujifunza na kuona shughuli hizo za Uchimbaji zinavyofanyika katika migodi hiyo likiwemo na suala la utunzaji wa Mazingira kwa ujumla.

VIJANA WATAKIWA WASIPISHANE NA FURSA KWENDA NJE YA NCHI NA KUWAACHIA WAGENI

$
0
0

  Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa, akiwa amebeba mfano wa picha ya ndege wa kuashiria amani, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
 Maandamano ya kuadhimisha siku hiyo yakifanyika.
 Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wawakilishi mbalimbali na viongozi wa dini  wakiwa wamebeba mfano wa ndege huyo.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Sheikh Hemed Bin Jalala akizungumzia umuhimu wa amani nchini
 Afisa Habari Kitengo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa-UNIC, Stella Vuzo, akizungumzia ushiriki wa UNIC katika kudumisha amani.
 Wanahabari wakiwa kazini katika maadhimisho hayo.
 Wananchi wakishuhudia maadhimisho hayo.
 Wasanii wakionesha umahiri wa kucheza na nyoka katika maadhimisho hayo.
 Kiongozi wa Chama cha Scout Tanzania, Kamishna Mkuu Msaidizi Kazi Maalum, Mary Anyitike akiwa na vijana wake kwenye maadhimisho hayo.
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia wahamiaji la IOM,  Dk. Quasim Sufi, akihutubia. Kutoka kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Suzan Kaganda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP, Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), Emanuel Lukuya na  Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa.
  Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa, akihutubia.
 Maadhimisho yakifanyika

Scout wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi mbalimbali.

Na Dotto Mwaibale

VIJANA wametakiwa wasipishane na fursa kwa kwenda nchi ya nchi kuzitafuta wakati wenzao wa nchi hizo wakija kunufaika nazo hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

"Vijana acheni mipango ya kwenda kuzitafuta fursa nje ya nchi kwani wenzenu kutoka nchi hizo wamekuwa wakija kunufaika nazo hapa nchini" alisema Mussa.

 Alisema serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni vizuri hali hiyo ikatumika kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo hasa katika wakati huu nchi ikiingia katika uchumi wa viwanda.

Aliwataka wazazi na walezi kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuwaepusha kujiingiza katika makundi yasiofaa.

Katika hatua nyingine Kamishna Mussa alisema amani ya nchi itadumishwa na kila mtu na kuwa watu waondoe dhana ya kuwa amani hiyo italetwa na vyombo vya dola ikiwemo polisi.

Alisema suala la amani si la mtu mmoja bali ni la kila mtu jeshi la polisi kazi yake ni kuilinda na kumkamata mtu yeyote anayeonekana kusababisha viashiria vya kutoweka kwa amani hiyo.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia wahamiaji la IOM,  Dk. Quasim Sufi alisema amani ni jambo la muhimu kwa nchi na mustakari wa maendeleo.

Alisema bila ya amani hakuna kitu kitakacho weza kufanyika na ndio maana UN imekuwa ikisisitiza amani duniani kote.Sheikh Hemed Bin Jalala alisema amani ndiyo msingi wa dini zote ya kiislam na kikristo na kuwa amani haipaswi kuchezewa kwani ndio neema tuliyopewa na mwenyezi mungu.

Jalala alisema amani ni msingi wa dini uliojengwa kiimani na kutakiwa kuihubiri na kuwa wale wanaohubiri vita na machafuko wanatoka katika dini ya mashetani.Afisa Habari Kitemgo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa-UNIC, Stella Vuzo aliwataka vijana kuendelea kuidumisha amani iliyopo nchini kwani wao ndio rahisi kurubuniwa kutokana na kuwa wengi.

"Katika maadhimisho ya siku ya amani duniani tunapenda kuwashirikisha vijana kutokana na wingi na umuhimu wao katika kutunza amani" alisema Vuzo.Alisema vijana watumie fursa ya amani iliyopo nchini katika kufanya shughuli zao za  maendeleo badala ya kukaa bure.

Vuzo alisema Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni  " Pamoja Katika Kudumisha Amani: Heshima, Usalama na Utu kwa wote"

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na taasisi mbalimbali kama  Global Peace Tanzania, Global Network of Religions for Children- GNRC, Chama cha Scout Tanzania, Asasi ya Vijana wa Umoja wa mataifa YUNA Tanzania, wanafunzi na wananchi.

Makala Maalum ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki 2017 (JAMAFEST),Kampala-Uganda

DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kabla ya kuchagua uongozi wapya kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya.
Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Mwenye shati la Njano) akifurahia jambo wakati wajumbe wa mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya hiyo wakiimba pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Mzee Jumanne Ally Ngaa akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Mwenye shati la Njano), Mbunge wa Jimbo la Singida Mgharibi Mhe Elibariki Kingu (Wa Kwanza kushoto Pichani) na viongozi wengine wakifatilia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi.
Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu akifurahia jambo wakati akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi wakimlaki mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kabla ya kuchagua uongozi wapya kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya.

Na Mathias Canal, Singida

Vijana wametakiwa kusimamia misingi ya Nidhamu ndani na nje ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa kuhuisha mshikamano ili kulinda misingi ya Utaifa na uwajibikaji kwani wao ndio nguvukazi ya Taifa na ushindi wa Chama Cha Mapinduzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi kwenye mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi.

Mhe Mtaturu alisema kuwa Dhana ya Demokrasia ni jambo muhimu linalohitaji kuheshimiwa na kuenziwa ndani ya Chama na  Jumuiya zake hivyo kuimarisha nidhamu, mshikamano na upendo ndio silaha pekee itakayoleta heshima ndani ya jumuiya ya vijana wa CCM ili iweze kusonga mbele zaidi na kuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha kipato cha vijana.

Alisema kuwa Nia ya UVCCM ni kujenga na kudumisha haiba  njema ya kuendelea kuheshimu misingi ya demorasia ya kweli, yenye kuchunga  adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila mwanachama anayetaka kutumia haki ya kuchagua au kuchaguliwa.

Alisema kuwa mkutano huo unapaswa kuchagua viongozi waadilifu watakaohuisha misingi ya mshikamano na ujenzi wa CCM Mpya ili kuondoa  malumbano yenye kupandikiza chuki na kupalilia mifarakano isio na ulazima.

Alisema wapo baadhi ya vijana wanatumia vibaya nafasi zao katika Jumuiya hiyo kwa kuwachafua wenzao kwenye mitandao ya kijamii na wakati mwingine wapo wanaothubutu kuwatukana wenzao matusi ya nguoni kinyume na ustaarabu, ubinadamu na misingi na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi.

Wapo baadhi yao hujivika kofia ya Jumuiya wakitumia  njia hatari na batili, kwa kukebehi, kutuhumu wenzao kinyume na utaratibu huku baadhi yao hata kufikia kutoa madai  yanayovuka mipaka na  kubeba taswira ya  Jinai au  madai. 

“Ndugu zangu Kwa miaka yote wanajumuiya na viongozi wote wa CCM wamekuwa wakiishi kwa kuzingatia misingi ya Umoja, Upendo, mashauriano na kudumisha Maelewano hivyo nakushaurini nyote kuvienzi ili kuwa na CCM Mpya itakayowaletea wananchi maendeleo na kuendelea kuongoza dola” Alisema mHe Mtaturu

Mhe Mtaturu alisema Uchaguzi ni kipimo cha kupevuka na kielelezo cha ukomavu wa demokrasia ya kweli bila mizengwe au hila ndani ya chama na Jumuiya kwa lengo la kusimamia shabaha na misingi sahihi itokanayo na miongozo, maelekezo na kuheshimu utaratibu unaohimizwa na Chama Cha Mapinduzi .

Alisema Ili kuonyesha  kutii na kufuata maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli kila mwanachama anapaswa kujitambua, kujiheshimu, kufuata misingi ya katiba na kuepukana na rushwa ili kulinda heshima ya Chama Cha Mapinduzi.

Mhe Mtaturu pia alizitaja fursa zilizopo katika Wilaya ya Ikungi ambazo vijana wanaweza kuzitumia ili kuimarisha kipato chao kuwa ni pamoja na Kilimo cha Korosho, Mpunga, Pamba na Ufugaji wa kuku.

Pia aliwasihi vijana kuanzisha vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na kuvisajili ili waweze kupatiwa mikopo ya asilimia 5% kwa vijana inayotolewa na Halmashauri za Wilaya kote nchini.

“Nawakumbusha kuwa tumeanzisha Mfuko wa Elimu Wilaya ili kuboresha elimu katika Wilaya yetu kwa hiyo nawasihi vijana wote kujitokeza kwenye kata zenu ili kushiriki shughuli ya ufyatuaji matofali ambayo tumeelekeza kila Kata kufyatua matofali 10,000” Alisema Mtaturu

Mhe Mtaturu pia aliwasihi vijana kushiriki kufanya kazi za kijamii ikiwa  ni  pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020, kushiriki kuona shughuli mbali mbali za uzalishaji Mali kupitia makundi ya vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza  mtaji  wa miradi yao. 

Sambamba na hayo pia aliwatakia uchaguzi mwema wenye amani na utulivu, ambapo aliwasihi pindi watakapomaliza uchaguzi huo kuwa wamoja na kuvunja makundi ili kuendelea kuimarisha Jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images