Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1375 | 1376 | (Page 1377) | 1378 | 1379 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Kwa mujibu wa baadhi ya wamiliki wa hoteli za jijini Dar es Salaam wanadai kwamba hali ya biashara ni ngumu kidogo ukilinganisha na miaka miwili iliyopita. Na hiyo ni kutokana na sababu kwamba baadhi ya huduma ambazo walikuwa akizitegemea sana kupungua, ikiwemo kukodisha kumbi kwa ajili ya mikutano.
  Kupitia kampeni yake ya kuhamasisha maeneo mbalimbali ya vivutio nchini Tanzania, Jumia Travel imekuwa ikitembelea hoteli tofuati na kufanya mahojiano. Katika zoezi hilo wamiliki na mameneja wa hoteli huulizwa juu ya masuala mbalimbali kuhusu 
  mwenendo wa biashara na mazingira kwa ujumla.

  Baada ya kuangazia maeneo na hoteli tofauti za visiwani Zanzibar, jiji la Dar es Salaam nalo limepata fursa hiyo. Yafuatayo ni mahojiano na Bi. Lusinda ambaye ni Meneja Mkuu wa hoteli ya Slipway ya jijini Dar es Salaam:  

  JT: Unaizungumziaje hoteli yako?
  Lusinda: Ni hoteli ya kifahari yenye vyumba 72 tofauti kwa ajili ya wageni ikiwa inapatikana eneo la Peninsula ya Msasani. Mbali na kutoa mandhari nzuri ya bahari ya Hindi pia tumezungukwa na maduka kadhaa kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa mbalimbali za asili.  

  JT: Ni wageni wa aina gani hutembelea zaidi hotelini kwenu? Je hupendelea/kuulizia shughuli gani zaidi?

  Lusinda: Mara nyingi tunapokea wageni kutoka nje ya nchi ukilinganisha na wa hapa nyumbani. Tofauti na sehemu zingine, jiji la Dar es Salaam halina vivutio vingi ambavyo wageni wakifika hupenda kuvitembelea. Hivyo basi kutokana na uzoefu wetu 
  hapa wengi hupendelea kwenda kutembelea Visiwani Zanzibar, pia huulizia sehemu za kwenda kujionea shughuli za kisanaa na kitamaduni.      

  JT: Unauzungumziaje ukuaji wa utalii wa ndani?
  Lusinda: Kwa maoni yangu, ukuaji ni wa kusuasua ukilinganisha na idadi ya wageni wanaokuja nchini na kutembelea vivutio vya kitalii. Nadhani zinahitajika jitihada za kutosha katika kuvitangaza vivutio vyetu, kurahisisha gharama pamoja na kubadili dhana nzima juu ya utalii.  

  JT: Unalizingumziaje jiji la Dar es Salaam kwa upande wa kitalii?
  Lusinda: Kwa asilimia kubwa jiji la Dar es Salaam halina sehemu za kutosha kwa ajili ya shughuli za kiutalii bali kutingwa na sehemu za kibiashara. Kwa uzoefu wangu nilionao hapa hotelini, wageni wengi wanaokuja ni kwa ajili ya shughuli za kibiashara. Na baadhi yao hufanya kama ni kituo kwa ajili ya kwenda sehemu 
  nyingine zenye vivutio vya kitalii kama vile Visiwani Zanzibar, Arusha, Serengeti au Kilimanjaro.  

  JT: Unaionaje hali ya biashara kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha nyuma? Lusinda: Ni nzuri, kwa hoteli za Dar es Salaam ambapo ni jiji la kibiashara. 

  Biashara haina msimu kwamba itafika kipindi fulani watu wataacha au kupumzika. Muda wote, majira yote ya mwaka jiji hili limejawa na pilika nyingi za wafanyabiashara. Kwa mfano, sisi hapa tunapokea wageni wengi kuanzia katikati ya 

  mwanzo wa mwaka yaani Januari mpaka katikati ya mwisho wa mwaka, Disemba. Nimekuwa  nikisikia baadhi ya maoni ya wamiliki na mameneja wa hoteli juu ya kubadilika kwa 
  biashara hususani kupungua kwa huduma ya kumbi za mikutano tofauti na miaka miwili iliyopita kabla ya kuingia serikali mpya. Ninachoweza kusema ni kwamba suala hilo linategemea meneja au mmiliki wa hoteli alijijengea vipi misingi ya biashara yake. 
  Kama ulikuwa unategemea biashara kwa upande huo ni kweli unaweza kuathirika, lakini kama ulijipanga na kujiimarisha kwenye maeneo mengine natumaini mambo  yatakuwa yanakwenda vizuri.   

  JT: Unadhani mifumo ya mtandaoni ina mchango wowote kwenye sekta ya utalii nchini?
  Lusinda: Ndiyo, ina mchango mkubwa tu kwani inasaidia katika kuongeza idadi ya wageni kwenye hoteli. Kutokana na mabadiliko ya tekinolojia, hatuwezi kuwa  tunategemea wateja wanaokuja moja kwa moja hotelini. Kwa mfano, hoteli yetu inapokea wageni wengi kutoka nchi za Marekani, Uingereza pamoja na nchi za 
  Scandinavia (Denmark, Norway, Sweden na Finland).    

  JT: Unauonaje usharikiano baina ya hoteli yako na Jumia Travel? Je una manufaa yoyote?
  Lusinda: Ushirikiano ni mzuri na una manufaa kwetu kwani unatuongezea njia tofauti za kujitangaza zaidi. Jitihada zinahitajika zaidi katika kuhakikisha kwamba  wanawafikia wateja wengi zaidi. 

  Kwa mfano, Tanzania kwa sasa inashuhudia kukua kwa 
  kasi kwa watu wa daraja la kati ambao wana uwezo kwenye kufanya matumizi. Hivyo basi ni fursa kuwalenga watu wa kundi hili kwa njia tofauti kama vile kubuni huduma na vifurushi vya bei ambazo zitawavutia zaidi.  

  JT: Kwa kumalizia, una maoni gani juu ya ushindani uliopo kwenye soko kwa sasa ukizingatia hoteli kadhaa mpya zikizidi kuzinduliwa?  
  Lusinda: Mimi ninaamini kwamba kuna fursa za kutosha kwa kila mmoja wetu kufanya biashara. Kila hoteli ina namna ya kufanya biashara na wateja inaowalenga kutokana  na upekee na huduma ilizonazo. Hivyo, dhana ya kwamba kuzidi kufunguliwa kwa hoteli mpya kutafanya wateja kupungua sidhani kama ina ukweli ndani yake. Cha zaidi ninachokiona kufunguliwa kwa hoteli mpya ni chachu katika ukuaji wa sekta ya utalii nchini na kunatakiwa kuhamasishwa zaidi.  

  0 0

  Baadhi ya wananchi wakiwa katika chumba cha usajili tayari kusajiliwa.


  Hawa ni baadhi tu ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la Usajil Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa. Kwa sasa zoezi hili linafanyika kwa awamu ngazi ya Kata ili kutoa fursa kwa wananchi wote wenye sifa kusajiliwa.
  Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akiingiza taarifa za wananchi kwenye mfumo kabla ya kuchukua taarifa za kibaiolojia za wananchi wa Kilolo ambako zoezi kwa sasa linaendelea.
  Mmoja wa wananchi akichukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kukamilisha hatua za Usajili Vitambumnbulisho vya Taifa. Mkoa wa Iringa ni moja ya Wilaya zinazo endelea na Usajili kwa sasa kati ya mikoa 11 ya Tanzania.

  …………………………

  Wananchi wa Wilaya ya Kilolo wameendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa baada ya kukamilisha awamu ya kwanza ya usajili ambayo ni kujaza fomu za maombi ya Usajili na fomu zao kupitishwa na Serikali za Vijiji wanakoishi.

  Zoezi linaenda sambamba na uhakiki wa taarifa za wananchi wanaoomba kupewa vitambulisho vya Taifa chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya Mitaa na Vijiji kabla ya kutoa nafasi kwa wananchi kuweka Mapingamizi ya wazi kwa wale waombaji wanaotiliwa shaka uraia wao kabla ya kuendelea na mchakato wa Uzalishaji.

  Wilaya ya Kilolo ni Wilaya ya mwisho kukamilisha zoezi hili kwa mkoa wa Iringa na hivyo kutoa fursa ya kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho vya Taifa kielektroniki.

  Mbali na Iringa mikoa mingine inayoendelea na zoezi hilo ni ya Kanda ya Ziwa ikiwemo; Geita, Shinyanga, Mwanza, Manyara na Singida.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimfariji Mbunge Mstaafu wa Mpwapwa Mjini Mhe. Gregory George Teu (kushoto) kwa Msiba wa familia yake uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, kabla ya kuanza kwa mazishi yatafanyika leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.


  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akiwasili katika Msiba wa familia ya Mbunge Mstaafu wa Mpwapwa Mjini Mhe. Gregory George Teu uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, ambapo mazishi yatafanyika mapema leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza viongozi Mbali mbali wa serikali katika kuaga miili ya familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, katika msiba uliofanyika leo nyumbani kwake Mpwapwa Mkoani Dodoma.

  Wananchi Mbali mbali waliohudhuria katika Msiba wa familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, katika mazishi yaliyofanyika leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.


  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akiongoza viongozi Mbali mbali wa serikali katika misa ya kuaga miili ya familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, uliofanyika leo katika kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa)iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.


  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiweka Shada ya maua katika mazishi ya familia ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, yaliyofanyika leo katka makaburi ya kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa) iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.


  PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa mashuka ya Kimasai) akiongea na washiriki wa tamasha la Ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust leo wilayani Tukuyu mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akifungua tamasha la ngoma za jadi leo wilayani Tukuyu mkoani humo ambapo amesisitiza Watanzania kukuza na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania hatua inayoongeza fursa ya ajira kwa vijana mkoani humo.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi ya CD kutoka kwa Mchungaji Damian Matipa wa Kanisa la Uponyaji Mbeya Mjini yenye nyimbo za kumpongeza Naibu Spika kwa kazi anazofanya.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mara baada ya kuwasili Tukuyu mkoani Mbeya.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi Mtaafu Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa tamasha la Ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust leo wilayani Tukuyu mkoani Mbeya.
  Ngoma ya Bugobo gobo kutoka Bujara mkoani Mwanza
  Baadhi ya viongozi wakiwa wamebeba moja ya vifaa Bugoyangi (nyoka) vinavyotumiwa na kikundi cha kucheza ngoma cha Bujora mkoani Mwanza.
  Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu, Mbeya


  Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu Mbeya


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Watanzania kuenzi na kuimarisha utamaduni wao ili kuepukana na chamgamoto ya utamaduni kutoka nchi za magharibi unaoletwa ukuaji wa sayansi na teknolojia.


  Prof. Elisante ametoa kauli hiyo leo Tukuyu wakati wa ufunguzi wa tamasha la Ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson inayojishughulisha na masuala ya kukuza na kuendeleza utamaduni nchini.

  Prof. Elisante amewahakikishia vijana kuwa kuwekeza mahali salama, hivyo waendelee kukuza sanaa yao iweze kujijengea jina na kutambulika ndani na nje ya nchi.

  “Vijana muendelee kuthamini utamaduni wetu, tusiposimamia, kuwekeza na kuthamini utamaduni wetu, utamaduni wan chi za magharibi utawachukua vijana wetu na kuacha tunu yetu ya asili tangu enzi za babu zetu” alisema Prof. Elisante

  Prof. Elisante amewahakikishia waandaaji wa tamasha hilo kuwa Serikali ipo sambamba nao na kuwataka wapanue wigo wa tamasha hilo ili liweze kuwa na matawi na kuwafikia watu wengi zaidi nchi nzima.

  Akifungua tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema limekuwa kichocheo cha kukuza na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania hatua inayoongeza fursa ya ajira kwa vijana mkoani Mbeya. 

  “Utamaduni ukitumika vizuri una fursa nyingi kwa vijana katika maeneo mbalimbali ikiwemo tasnia ya sanaa ambayo itawasaidi kujipatia ajira hatua inayowasaidia kuinua kipato chao na uchumi wa taifa” alisema Mkuu huyo wa mkoa.

  Kwa upande wake Mwasisi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka huu limakuwa na wigo mpana kwa kushirikisha vikundi vya ngoma kutoka maeneo mbalimbali nchini.

  Kuhusu manufaa ya tamasha hilo, Dkt. Tulia amesema kuwa mwaka jana taasisi hiyo ilipeleka vijana 20 kupata mafunzo ya kitaalamu kwenye fani ya sanaa na utamaduni katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na mwaka huu wanatarajia kupeleka vijana 27 ili waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kufanya shughuli zao kwa tija.

  Tamasha hilo linahusisha mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Lindi, Katavi, Dodoma, Kagera, Tanga, Mtwara, Kigoma na wenyeji mkoa wa Mbeya.

  0 0
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa akimtolea ufafanuzi wa zawadi ya kinyango Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam uku katibu Mkuu wa (CCM) akishuhudia zoezi hilo,wakati wa hafla ya Chakula cha Jion ilioandaliwa na kinana.
   Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza kabla ya Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam kukabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa wakati wa hafla ya Chakula cha Jion.
   Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza na balozi wa Vietnam Nguyen kim Doanh.


   Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akifurahia jambo na wageni wake toka chama cha Kikomunisti cha Vietnam (VCP) jana wakati wa hafla ya chakula cha jion.
   Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jion.
   Wajumbe wa Chama cha kikomunisti cha Vietnam (VCP) pamoja na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazaza CCM wa (pili toka kushoto) wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
  Baadhi Wajumbe wa Sekretariet wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
   Katibu Mkuu wa CCM Comred Abdurahman Kinana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Juma Kimbisa pamoja na Katibu wa idara ya SUKI kanal mstaaf Ngemela Rubiga wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion  Katibu mkuu wa CCM alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar DKT.Abdallah Mabodi akiagana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika hafla ya chakula cha Usiku ilioandaliwa na Katibu mkuu wa CCM Comred Abdulrahman kinana Mjini dodoma.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Comred Abdulrahman Kinana akiagana na Mgeni wake Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha jion aliomwandalia mgeni wake   Mjini dodoma.   (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)  0 0

   Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),  Frederick Ntobi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha juu ya matumizi ya vyombo vya habari Mtandaoni (Online Media) iliyowashirikisha wanachama wa Tanzania Bloggers  Network (TBN), kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA; KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA  wakihudhuria warsha hiyo
   Sehemu ya wamiliki wa mitandao mbalimbali wakihudhuria warsha hiyo ya siku moja   Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi (kulia) akiwa meza kuu.  Anayefuata ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,  Mhandisi James Kilaba, Mwenyekiti wa Kamti ya Maudhui ya TCRA, Bibi Msoka na James Kilimba ambaye ni Mkurugebnzi wa Bodi ya TCRA.

   Mablogga wakiwa makinini kusikiliza wakati wa warsha hiyo. Kutoka kushoto ni Kranz Mwantebele,  Adam Mzee na Dotto Mwaibale  0 0

   Naibu Kamishna wa utawala polisi makao makuu DCP Leonard .l. Paulo alie katikati akiongozana na wenyeji wake mkuu wa chuo cha polisi kidatu baada ya kuwasili chuoni hapo ACP, Zarau .H Mpangule alie mkono wa wa kushoto na alieko kulia ni Kamanda wa polisi Msitafu DCP  Venance Tossi.  Picha na Jeremia.
   Kamanda wa polisi Msitafu DCP Venance Tossi  wakijadili jambo na Naibu Kamishna wa utawala polisi makao makuu DCP Leonard .l. Paul.
  Naibu Kamishna wa utawala polisi makao makuu DCP Leonard .l. Paul akilakiwa au kupokelewa kwa shangwe na  wakanguzi waliokuwa wanaitimu mafunzo yao katika chuo cha polisi Kidatu.

  0 0

   Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Davis Mwamunyange, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Ndanto Fc, Peter Mwakingwa, baada ya kushika nafasi ya nafasi ya kwanza na kutwaa kombe la fainali za 'Tulia Cup 2017' kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO MEDIA GROUP)
   Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Davis Mwamunyange, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Isange, Frank Asilih, baada ya kushika nafasi ya pili katika fainali za 'Tulia Cup'kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.
   Beki wa timu ya Isange Fc, Zawadi Andombwisye (kushoto) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Ndanto Fc, Erick Mwangoye, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5.
   Beki wa timu ya Ndanto Fc,Fidelis Yeo (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Isange Fc, Hussein Thom, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5.
    Wachezaji wa Isange Fc, Shadrack Kandrum (kushoto) na Hussein Thom (kulia) wakimdhibiti Mandela Chaile, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5. 
   Beki wa timu ya Isange Fc, Shadrack Kandrum (kulia) akimdhibiti mshambuliaji wa Ndanto Fc, Julius Mtawala, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5.
   Luteni General, James Mwakibolwa, akiongozana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tulia Ackson, kukagua timu ya Ndanto fc kabla ya mchezo wa fainali dhidi ya Isande Fc, katika mchezo wa fainali wa 'Tulia Cup' kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.
   Luteni General, James Mwakibolwa, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Netiboli ya Kimo,Salome Sanyondo, baada ya kushika nafasi ya pili katika fainali za 'Tulia Cup'kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya. 
  Luteni General, James Mwakibolwa, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Netiboli ya Wizara ya Mambo ya Ndani, baada ya kushika nafasi ya kwanza katika fainali za 'Tulia Cup'kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya. 

  0 0

  Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Boniface Mhabe kushoto akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kwa Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Sub Agro Trading anda Engineering,Neema Ng'unda kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza jana ilkiwa ni kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kilimo wa pili kutoka kushoto ni  
  Afisa  Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli 
  HOSPITALI ya Teule wilayani Muheza Mkoani Tanga imepata msaada wa mashuka 50 kwa ajili ya kukabiliana na uhaba uliopo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu kutoka maeneo mbalimbali hasa vijijini.

  Hatua ya uhaba huo unatokana na uchakavu wa wa mashuka unaotokana na
    kufubaa unaosababishwa na maji wanayotumia kufulia kutokana na uhaba wa maji hali iliyopelekea kuwepo uhitaji kila wakati ili kuweza kukithi mahitaji ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.

  Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,
    Boniphace Mhabe wakati akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kampuni ya Suba Agro Trading na Engineering ambao ni mzalishaji wa mbegu bora zamahindi kwa kushirikiana na Cimmity taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mahindi na Ngano.

  Shuka hilo zilitolewa kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito
    kwenye hosptali ya Teule Muheza,Hospitali ya wilaya ya korogwe na ile ya wilaya ya Handeni lengo kubwa likiwa kuwaondolea changamoto zinazowakabili.

  "Vitanda vipo vingi lakini tatizo kubwa ni mashuka na hili linatokana
    na asilimia kub wa kuchakaa kutokana na maji lakini pia wakati mwengine yanabadilika rangi jambo ambalo limekuwa changamoto kwao.

  Aidha alisema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia
    msaada huo ambao umefika wakati muafaka kwa kusadia baadhi ya vikwazo wanazokutana navyo wakati wa utoaji wa huduma  za afya.

  Awali akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Afisa Masoko na
    Mauzo wa Kampuni hiyo,Neema Ng'unda alisema alisema wamekuwawakishiriki katika kuhamasisha kilimo Tanzania hususani kwa wakina mama ambao ndio nguzo kubwa hapa nchini kufikia mafanikio.

  Alisema wamelenga wanawake kwa sababu ndio muhimili muhimu kwenye
    jamii wa kuwawezesha wakina baba kwenye kulima kilimo bora ambapo kinaweza kuwainua kiuchumi.

  "Lakini pia tunawashukuru wakulima wote Tanzania kwa kutumia mbegu zao
    kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho kinaweza kuwa mkombozi kijiinuakimaendeleo na kukuza mitaji yao "Alisema.

  Naye kwa upande wake,Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao
   makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli alisema zoezi hili limelenga kurudisha fadhila kwa wakina mama wa Tanzania maana ndio wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kilimo.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kushoto) katika kikao chake kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba, 2017. Kikao hicho kilishirikisha wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
  Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani).
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA), Chalers Sangweni (kulia) na mjiolojia kutoka mamlaka mamlaka hiyo, Simon Nkenyeli (kushoto) wakifuatilia majadiliano mbalimbali katika kikao hicho.
  Mtaalam wa Masuala ya Nishati kutoka Ubalozi wa Sweden Nchini, Jorgen Eriksson (kushoto) akieleza jambo katika kikao hicho. Kulia ni Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt ( wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao hicho. 

  0 0

   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma.Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ambapo aliwashauri wafanyakazi nchini kupima afya mara wanapostaafu ili kujihakikishia kama hawajaathirika na kazi walizokuwa wanafanya.Katikati ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule na Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda 
   Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule akiongea naViongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi, kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi na kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda
   Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule (KUSHOTO) na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Jones Majura(KULIA) wakiteta jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi baada ya ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi leo Mjini Dodoma
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma. PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO,DODOMA.


  Na: Lilian Lundo – MAELEZO Dodoma.

  Wafanyakazi nchini wameshauriwa kupima afya zao mara tu wanapostaafu ili kujihakikishia ikiwa hawajaathirika na kazi ambazo wamekuwa wakizifanya.

  Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Eric Shitindi alipokuwa akifungua semina ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi juu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, leo Mjini Dodoma.

  “Kumekuwa na mazoea kwa wafanyakazi kupima Afya pale tu wanapoajiriwa na kutotilia maanani upimaji afya zao mara wanapostaafu ili kujua ikiwa kazi wanazozifanya zimewaathiri kwa kiasi gani,” amesema Shitindi.

  Ameendelea kwa kusema kuwa, upimaji wa afya mara baada ya kustaafu utasaidia watumishi kujua afya zao na ikiwa watakuwa wameathirika upitia kazi walizokuwa wakizifanya basi mwajiri atawajibika mkulipa fidia mtumishi huyo.

  Aidha amesema kuwa licha ya juhudi za Serikali katika kusimamia Usalama na Afya maeneo mengi ya kazi sio ya kuridhisha kutokana na waajiri wengi kutokuzingatia sheria na kanuni mbalimbaliza Usalama na Afya.

  Hivyo basi kutokana na waajiri hao kutofuata sheria na kanuni hizo kumesababisha maeneo mengi ya kazi kulalamikiwa kutokana na ukiukwaji wa sheria hizo.

  Vile vile amesema kuwa baadhi ya waajiri na wafanyakazi wana uelewa mdogo  kuhusu kuzingatia maelekezo ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ikiwemo matumizi sahihi ya vifaa kinga.

  Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda amesema kuwa, wameamua kuandaa semina hiyo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi hapa nchini ili na wao wakatoe elimu hiyo kwa wafanyakazi wote nchini kutokana na wafanyakazi hao kutokuwa na uelewa mzuri juu ya masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi.


  0 0


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Alli Karume  akipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na SSRA kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mamlaka Bw. Sabato Kosuri alipotembelea banda hilo  wakati wa maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika mkoani Kigoma.

  Na. Zawadi Msalla. 

  Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Alli Karume ameitaka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kusimamia kwa ukaribu michango ya Wanachama kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii  ili itumike kwa malengo yaliyokusudiwa kwa mujibu wa Sheria zilizoanzisha mifuko hiyo. 

  Wito huo umetolewa jana mjini Kigoma na Waziri Karume alipotembelea banda la SSRA kwenye maonesho ya wiki ya Bahari duniani yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya msingi Mlole Mkoani humo.

  Waziri Karume alisema SSRA inawajibu mkubwa wa kumlinda mwanachama wake ili kuhakikisha hapati matatizo pale anapotakiwa kupata mafao yake.Pia alisisitiza kuwa Itakuwa ni jambo la kuumiza sana inapotokea mwanachama mwenye matumaini ya kupata mafao yake atakapoambiwa mfuko umefilisika na hivyo mafao anayoyatarajia hawezi kuyapata.

  Aidha Mhe. Karume aliipongeza SSRA kwa elimu wanayoendelea kuitoa kwa jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na  jinsi wanavyo simamia maboresho mbalimbali yanayoendelea katika sekta hiyo. 
  Hata hivyo alisema bado SSRA inawajibu mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii ili kushawishi wananchi kuona umuhimu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwani wapo wananchi wengi wasio fahamu umuhimu wa  mifuko hiyo na wengi wao hupata shida inapofikia kipindi cha uzeeni.

  Awali akitoa maelezo ya shughuli za SSRA Afisa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka hiyo  Bw. Sabato Kosuri alimhakikishia Mhe. Waziri usalama wa  michango ya wanachama kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

  Bw.Kosuri alisema  tayari SSRA imeweka miundombinu imara ya kusimamia eneo hilo ikiwa ni pamoja na miongozo ya uwekezaji pamoja na kaguzi za mara kwa mara ili kuhakikisha mifuko inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria kanuni na taratibu na hivyo kuwahakikishia usalama wachangiaji wote kwenye mifuko ya hifadhi ya  jamii.

  Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii iliundwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 (Toleo la 2015) kwa lengo la kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa manufaa ya Wanachama na Taifa kwa ujumla. Mamlaka ilianza kazi rasmi mwishoni mwa Mwaka 2010.

  Mamlaka ina jukumu la msingi la kuhakikisha kwamba Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inakuwa endelevu, inaendeshwa kwa kufuata kanuni, taratibu na kisheria, wanachama wanapata taarifa za Mifuko/michango yao, na mafao yaliyobora.

  0 0


  Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC. Pamoja nae kutoka kushoto ni Askofu Ambele Mwaipopo, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Askofu Dk. Alex Malasusa, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank Bw. Amulike Ngeliama. 

  Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akizungumza na wageni waalikwa jana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC uliofanyika jijini Dar esSalaam.
  Wakati Maendeleo Bank ikiwa ni taasisi ya nane ya fedha kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Serikali imesema asilimia 60 ya miamala ya fedha nchini haipiti kwenye mifumo rasmi.
  Hivyo, benki na taasisi za fedha zimetakiwa kuongeza ubunifu ili sekta hiyo iweze kuchochea maendeleo ya uchumi. Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa za Maendeleo Bank PLC na kwamba, kwa sasa ni asilimia 40 tu ya miamala ya fedha hupita katika mifumo rasmi.
  Maendeleo Bank inakuwa benki ya kwanza kuhitimu kutoka dirisha la ukuzaji mashirika machanga (Enterprise Growth Market) na mwaka 2016 ilipata tuzo ya kampuni bora katika makampuni yanayokua kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
  Dk. Mpango alisema sekta ya benki ni muhimu katika kukuza uchumi na kwamba, kupitia huduma za fedha kwa kutumia simu za mikononi, Tanzania ni kati ya nchi zinzoongoza Afrika kwa kusogeza karibu huduma za kibenki kwa wananchi.. “Kwa hili Benki ya Maendeleo lazima muongeze ubunifu ili kuvutia wateja zaidi kutumia huduma zenu,” Dk. Mpango alitaka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuongeza nguvu ya kuelimisha jamii umuhimu wa umiliki wa hisa.
  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba alisema, tangu benki ianzishwe mwaka 2013 imekuwa namafanikio makubwa ikiwamo kuongeza matawi kufikia matatu.
  Mwangalaba alisema mwaka 2015, benki ilipata faida ya Sh. 175 milioni na mwaka 2016 iliongezeka na kufikia Sh. 555 milioni. Pia, kwa miaka minne imelipa kodi ya Sh. 2.42 bilioni.
  Ailongeza kuwa mwaka 201/16, benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili na ilikusanya zaidi ya Sh. 2.8 bilioni, hivyo kufikisha jumla ya Sh. 7.30 bilioni.“Leo tunashuhudia uzinduzi wa uuzaji wa hisa ukiwa na lengo la kuongeza mtaji kwa Sh. 15 bilioni, ambazo zitatumika kuimarisha shughuli za uendeshaji,” alisema.Tangu benki ianzishwe imefanikiwa kukusanya amana zaidi ya Sh. 39 milioni na kutoa mikopo zaidi ya Sh. 28.0 milioni. Pia, mali za benki zina thamani ya Sh. 49 bilioni.Mwangalaba alisema iwapo watafanikiwa kuuza hisa na kupata ntji wa Sh. 15 bilioni, wanatarajia kuimarisha utendaji wa benki hiyo kwa kiwango kikubwa.


  0 0  0 0

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limemkamata mwanamke mwengine akiwa na jumla ya kete 969 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya DVD.

  Mwanamke huyo ambaye amekamatwa na wenziwe wawili wanaume katika maeneo ya PBZ Chake Chake anakuwa wa pili kukamatwa ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya Septemba 9 mwezi huu kukamatwa mwengine akiwa na jumla ya kete 3621.

  Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Madungu Chake Cheke Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed Shikhan amemtaja mwanamke huo ni Asha Mohamed Issa (30) mkaazi wa Wawi Chake Chake, huku wenzake wakiwa ni Ali Nyoro Tirima (32)wa Wawi na Salim Said Kombo 23 mkaazi wa Konde Wilaya ya Micheweni.

  Aidha Kamanda Shikhan amesema jeshi la polisi Mkoa wa Kusini Pemba tayari inayo majina ya mabaharia wanaofanya kazi katika meli zinazotoka Unguje kuelekea Pemba wanaotumiwa kusafirisha madawa ya kulevya na kuwataka kuacha vitendo hivyo kwani jeshi hilo linawafuatilia.

  “Ni kwamba wito wangu kwa mabaharia wa meli zinazotoka Unguja kuja Pemba, tayari tunayo majina ya mabaharia wa meli zote MV Mapinduzi, meli za Bakhresa zote hao ndio ambao wanatoa msaada mkubwa kwa waleta madawa ya kulevya yanapita katika mikono yao,tunawajua na tunawafuatilia kwa karibu”

  Aidha kamanda huyo amewawata amewataka wamilika wa makampuni kuwatahadharisha mabaharia wao, kuacha kutumiwa na wahalifu wa madawa ya kulevya wa bangi na unga wanaopeleka madawa ya kulevya kisiwani humo kwani watawakamata.

  Kwa upande mwengine Kamanda Shekhan amewaonya wanawake wanaojiingiza kufanya biashara za madawa ya kulevya kuacha kabisa biashara hizo na kutafuta nija halali za kujipatia kipato.

  “Kweli huyu ni mwanamke wa pili kumkamata kwa mkoa wetu, lakini natoa wito kwa wanawake hiyo sio biashara ya kusema wanaweza wakapata utajiri , warudi nyuma watafute biashara zinazokwenda na maadili ya biashara” Septemba 9 mwaka huu jeshi la Polisi Mkuu wa Kusini Pemba huko maeneo ya Mkoani Pemba ilifanikiwa kumkamata na kete 3621 Zuhura Ahmed Ali (29) wa Jadida na alifikiswa mahakamani kwa mara ya kwanza Septemba 14.
   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed Shikhan akizungumzia kukamatwa kwa madawa hayo.
  Mzigo wa madawa hayo

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofuatana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Msikiti Masjid Jaamiu Zinjibar baada ya kuufungua rasmi leo,ambao umejengwa Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami wakati alipotembelea sehemu mbali mbali mara alipofungua Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea Shahada na Ufunguo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Msikiti Masjid Jaamiu Zinjibar leo uliojengwa kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman katika maeneo ya Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi,Picha na Ikulu

  0 0

  Wasanii walio katika list ya watumbuizaji wa Fiesta jijini Mwanza wakishuka kwenye gari kuingia katika duka la Tigo Jijini Mwanza mapema leo mchana.  Mteja wa mtandao wa Tigo Edith Shekifu, akipokea zawadi kutoka kwa msanii wa hip hop Fareed Kubanda(Fid Q) ndani ya duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.


  Mteja wa mtandao wa Tigo Kilinga James, akipokea zawadi kutoka kwa msanii wa hip hop Fareed Kubanda(Fid Q) ndani ya duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.


  Wasanii wa bongo fleva Fareed Kubanda(Fid Q) na Rayvanny wakimpa zawadi mteja Lidya Mtamizi, kwenye duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.


  Msanii bongofleva Rayvanny akipiga selfie na mteja wa Tigo, kwenye duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jones Kilimbe akifungua rasmi warsha ya vyombo vya Habari Mtandaoni iliyo wahusisha Blogu na 'Online Tv' katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
   Bw. Thadeus Lingo kutoka TCRA akiendesha mada kuhusu Matumizi Salama ya Mitandao ya Kijamii
   Mwakilishi wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Maxence Melo akiwasilisha mada juu ya Maudhui ya Mtandaoni na Changamoto zake.
   Mratibu Msaidizi wa Polisi Joshua Mwangasa akitoa mada juu ya Hali ya Usalama Mtandaoni

   Mzee Abdul Ngarawa Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka TCRA akitoa neno la Busara wakati wa warsha hiyo ambapo alisisitiza kuzingatia uzalendo umuhimu wa kutazama utu na staha ya mtu
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba (Kushoto) akiongoza majadiliano kwa ujumla ambapo wadau walichangia mawazo na kuuliza maswali mbalimbali
  Bwana Daniel Mbega Mmiliki wa Blogu ya Maendeleo Vijijini akichangia mawazo yake wakati wa warsha hiyo
   Bw. William Malecela Maarufu kwa jina la Le Mutuz mmiliki  Blogu ya Wananchi na Le Mutuz Tv Onine akichangia mambo mbalimbali na kutoa maoni yake wakati wa Warsha hiyo
   Mwenyekiti wa  Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Joachim Mushi (kulia) akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya waendesha wote wa mitandao kwa TCRA kuendesha warsha hiyo
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba pamoja na wadau wengine wakizindua Rasmi Kampeni ya kusisitiza matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii awamu ya Pili ambapo Kauli mbiu inasema "Usinitumie Sitaki na Simtumii Mwengine Nitakuripoti"
   Baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Bi. ValerieNdeneingo-Sia Msoka akitoa neno la kufunga wakati wa Warsha hiyo.
   Wadau mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo  Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania

  Na. Paschal Dotto-MAELEZO.
  Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) imetia nia kuboresha mawasiliano kwa umma hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watanzania kupata elimu bora ya maendeleo na kujenga uchumi uliobora.

  Haya yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo Dkt. Jonas Kilimbe  alipokua akihutubia hadhara ya wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni (blogu na Online TV) katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya “kusisitiza matumizi bora ya mitandao ya kijamii”  iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

  Katika hafla hiyo, Dkt. Kilimbe alisema kuwa kwa sasa teknolojia ya mtandao inakua kwa kasi kwa hiyo huduma za habari zinapatikana kila sehemu kwa njia ya mtandao na kufanya matumizi ya mitandao kuwa makubwa.

  “Sekta ya mawasiliano kwa umma imepiga hatua kubwa sana duniani kwa sasa, kwa kiasi kikubwa mtandao unachangia kuwepo kwa habari nyingi. Tanzania inajumla ya televisheni za mitadaoni zipatazo 50 pamoja na blogu 150 ambazo zote zinatoa taarifa kwa wananchi, hii inaashiria kuwa mawasiliano kwa umma yamehamia zaidi kwenye mtandao”, alisema Dkt.Kilimbe.

  Aidha Dkt.Kilimbe alisema kuwa sekta hii inapaswa kuangaliwa zaidi kwani ni sekta muhimu kwa ujenzi wa Taifa na kuwaasa vijana kutumia vizuri teknolojia hiyo kwa kujielimisha kuhusiana na masuala ya maendeleo kuliko kutumia vibaya mitandao hiyo.

  “Tuna jukumu zito na ni kubwa kwa sababu sekta hii ya mawasiliano imeshikiria kila kitu na tasnia ya habari ina nguvu kubwa sana kwa kuleta elimu ya maendeleo kwa wananchi kwa hiyo waandishi mitandaoni tumieni weledi  mkubwa kwa habari za maendeleo.”, alisisitiza Dkt. Kilimbe.
  Dkt.Kilimbe alisema kuwa katika matumizi ya teknolojia hii mpya yanapaswa kuzingatiwa  kwa ajili ya ujenzi wa taifa hasa kwa wale wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii inawapa elimu kubwa ya maendeleo.

  Aidha Dkt. Kilimbe amekishukuru chama cha wamiliki wa blogu na televisheni mtandaoni(TBN) kwa kuleta umoja na kuzingatia maadili na weledi wa umilikajia wa vyombo hivyo kwa kuwahabarisha wananchi.

  Naye mtoa mada na mwakilishi kutoka TCRA Bw. Thadeus Lingo alisisitiza usalama wa matumizi ya mtandao akisema kuwa idadi ya watumiaji wa mitandao imeongezeka duniani kuanzia Julai 1, 2017 na kufikia bilioni 3.8 huku kati ya hao bilioni 3.4 ambayo ni sawa na asilimia 92 ni watumiajia wa mitandao ya kijamii hali iliyosababisha kuongezeka kwa vyombo vya habari kuhamia mtandaoni, kwa hiyo weledi unahitajika katika kuhabarisha umma kwa njia hii.
   

older | 1 | .... | 1375 | 1376 | (Page 1377) | 1378 | 1379 | .... | 1898 | newer