Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA BLK YA NCHINI INDIA YAFANYA UPASUAJI WA MOYO KWA WAGONJWA 64

$
0
0
 Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India Ajal Kajul akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji  wa kufungua na bila kufungua  kifua  wagonjwa 64. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge.
  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Hospitali ya B.L.K ya nchini India   ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji  wa kufungua na bila kufungua  kifua  wagonjwa 64. Kulia  ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India Ajal Kajul.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikilliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Taasisi hiyo ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji  wa kufungua na kufungua kifua  wagonjwa 64. (Picha na JKCI)


MADAKTARI kutoka  Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete kwa ushirikiana na wenzao wa Hospitali ya B.L.K ya nchini India wamewafanyia wagonjwa 64 upasuaji wa moyo  ambao ni wa kufungua na bila kufungua  kifua.

Kati ya hao wagonjwa nane walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na 52 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua (catheterization)  kwa kutumia mtambo wa Cathlab.

Pia madaktari hao wamepata mafunzo ya kufanya upasuaji wa milango miwili ya moyo  ambapo awali huduma hiyo ilikuwa haitolewi kwenye taasisi hiyo .

Mafunzo hayo ya siku tano yaliyo ongozwa na wataalamu kutoka Hosipitali ya BLK ya Nchini India itasaidia serikali kuokoa zaidi ya milioni 30 ambazo zingetumika kwaajili ya matibabu ya mgonjwa wa moyo wenye uhitaji wa upasuaji wa  milango miwili  ambapo asilimia 25 ya wagonjwa wana uhitaji huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana Dar es Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo  Peter kisenge alisema kupitia kambi ya siku tano ya  madaktari nane wanaotibu maradhi ya moyo ,Wataalamu wa usingizi ,Wataalamu wa kutoa damu kwenye mapafu ,kutoka Hosipitali ya BLK ya nchini India imesaidia kutoa mafunzo ya uwekaji na upasuaji wa milango miwili kwenye moyo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo ambapo huduma hiyo itakuwa ya kwanza kutolewa hapa nchini.

Mbali na huduma hiyo Dk Kisenge alisema tayari madaktari watatu wa taasisi hiyo wanaweza kutoa huduma ya uwekaji wa milango miwili ya damu kwenye moyo  huku Daktari mmoja akipata mafunzo ya miaka miwili  nchini india.

Kuanza kwa huduma hiyo alisema watasaidia watoto wadogo ambao milango yao imeziba ambapo awali walikuwa hawafanyiwi upasuaji kutokana kutokuwepo kwa ujuzi wa upasuaji wa milango hiyo.
Alisema kwa wagonjwa 64 waliofanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo wangesafirishwa nchini india serikali ingepoteza zaidi ya bilioni 6 .

Kwa upande wake Daktari Bingwa Upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Hosipitali ya BLK ya Nchini India Dk Ajal Kajul alisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa madaktari hapa nchini ambapo baadhi ya madaktari walioambatana nao watabaki katika taasisi hiyo kwaajili ya kuendelea kutoa mafunzo zaidi.

 Dk. Kaul alisema wataendelea kuonyesha ushirikiano wa kutoa ujuzi kwa madaktari wa hapa nchini ambapo octoba mwaka huu watatoa mafunzo ya upandikizaji wa figo,na wagonjwa wenye matatizo ya mgongo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili.

TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL LAFANA

$
0
0
 Kikundi cha ngoma ya asili ya Sindimba toka mkoa wa Mtwara,Wakicheza ngoma hiyo jana wakati wa mashindano ya ngoma za asili yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ya”Tulia Traditional dances festival 2017”yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya tandale mjini Tukuyu wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya.
 Wakazi wa Tukuyu wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya wakifatilia mashindano ya ngoma za asili yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ya”Tulia Traditional dances festival 2017” yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Tandale mjini humo.
 Majaji wa mashindano ya ngoma za asili yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ya”Tulia Traditional dances festival 2017” wakifatilia kwa karibu mashindano hayo yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya tandale mjini tukuyu wilaya Rungwe mkoani Mbeya.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimfanyia mahojiano Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia kuhusiana na mashindano hayo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Tulia Ackson akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia wakati wa ufunguzi wa mashindano ya ngoma za asili yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ya”Tulia Traditional dances festival 2017”.

TAMASHA la ngoma za kitamaduni lililopewa jina la Tulia Traditional Dance Festival, limeanza kwa mbwembwe mjini Tukuyu, mkoani Mbeya jana, likishirikisha vikundi zaidi ya 100 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo litafikia tamati kesho.  

Akizungumza tamasha hilo akiwa Tukuyu jana, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ambaye ndiye mwasisi wake, alisema kuwa anajisikia furaha kuona tukio hilo limepokewa vizuri mno na wakazi wa Tukuyu na mkoani Mbeya, lakini pia na Tanzania kwa ujumla.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na mwitikio umekuwa mkubwa mno kuonyesha jinsi Watanzania wanavyothamini tamaduni zao. Matamasha kama haya ni muhimu mno kwani hutoa fursa ya kutangaza utamaduni wetu wa kitanzania na kuwa moja ya kivutio badala ya kutegemea vivutio vya kiutalii vilivyozoeleka kama Mlima Kilimanjaro, mbuga na hifadhi za wanyama na vinginevyo.

“Nawaomba wabunge waandae matamasha kama haya katika maeneo yao ili baadaye washindi watakaopatikana, waweze kushiriki katika tamasha letu hili ili kulifanya kuwa la kitaifa zaidi, hii itasaidia kuwaonyesha vijana wetu wa kizazi cha sasa kufahamu tamaduni zao, kuona mababu zao walikuwa wakifanya nini.

“Kwa serikali, iandae na kuunga mkono matamasha ya utamaduni kama sehemu ya kuenzi utamaduni wetu kwani vijana wengi wamekuwa wakibobea katika tamaduni za kigeni kutokana na kutofahamu tamaduni zao,” alisema.

Aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kujitosa kudhamini tamasha hilo la aina yake ambalo anaamini litafana vilivyo mwaka huu.Alisema tamasha hilo limeshirikisha vikundi zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali, hali inayotoa picha kuwa kwa sasa ni tukio la kitaifa, akiwataka wanasiasa, hasa wabunge, mashirika, taasisi na kampuni mbalimbali kujitokeza kulidhamini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mwori, alisema kuwa huu ukiwa ni mwaka wao wa kwanza kudhamini tamasha hilo, wanajisikia fahari kubwa kuungana na Muheshimiwa Dk Tulia kusapoti tukio hilo, wakiwa kama miongoni mwa wadau wa masuala ya burudani, michezo na mambo ya kijamii.

“Vodacom Tanzania tunajisikia fahamu kuwa sehemu ya tamasha hili kupitia udhamini wetu, tumeona ni vema kudhamini tamasha hili kwani lina manufaa makubwa kwa jamii ya kitanzania, hasa katika suala zima la kuuenzi utamaduni wa Mtanzania,” alisema.

Aliongeza: “Kama kila mmoja wetu anavyofahamu, Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusapoti matukio mbalimbali ya kijamii kama sehemu ya kuionyesha jamii jinsi tunavyoijali kwani ndio wadau wetu wakubwa waliotuwezeshja leo hii kuwa mtandao bora kabisa wa mawasiliano hapa nchini.”

Alisema kama ambavyo wamekuwa wakisapoti matukio mbalimbali ya kimichezo na utamaduni kama vile udhamini wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mashindano ya Dance 100%  na mengineyo, wataendelea kudhamini tamasha hilo miaka ijayo kadri itakavyowezekana.

Aliwataka wadau wengineo wa sanaa na burudani kwa ujumla hapa nchini kujiotokeza kudhamini tamasha hilo ambalo anaamini linaweza kuwa dira ya utamaduni wa Mtanzania iwapo litapewa sapoti inayostahili.

Naye mkazi wa Iromba, Mbaye ambaye amehudhuria tamasha hilo, Kenneth Sanga, alilimwagia sifa tamasha hilo akisema kuwa linakumbusha tulikotoka likitoa fursa kwa vijana wa sasa kufahamu watu wa zamani walikuwa wakifanya nini.

“Kuna watu wa kutoka maeneo mbalimbali wamehudhuria tamasha hili, hili ni jambo kubwa sana hivyo ni vema serikali ikaunga mkono jitihada hizi zilizoonyeshwa na muheshimiwa Dk Tulia kwa kuendesha matamasha kama haya katika maeneo mbalimbali nchini,” alisema Sanga.

Ecobank yazindua njia salama ya malipo kwa mtandao

$
0
0

Ecobank yaja na suluhisho la kufanya malipo salama kwa njia mtandao kupitia MASTERPASS na MVISA . 

Ecobank katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa suluhisho kwenye sekta ya biashara ya huduma za kibenki hapa nchini leo imezindua applikesheni ya simu za mkononi itakayojulikana kama Ecobank Mobile App – MASTERPASS NA MVISA ili kusaidia wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kufanya Malipo kwa njia rahisi na kwa usalama zaidi mahali popote.

Mtanzania yeyote ataweza kutumia teknolojia hii ya mpya ya MASTERPASS QR na MVISA kulipia gharama mbali mbali kwa kutumia simu zao za mkononi kwa kupitisha Quick Response (QR) kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa au watoa huduma ndani na nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi, Mwanahiba Mzee alisema “applikesheni ya Ecobank Mobile App ilizinduliwa Februari mwaka huu lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi ili wateja wa Ecobank na wale wasio wateja wa bank hii waweze kutumia applikesheni hii duniani kote”.

‘Applikesheni ya Ecobank Mobile App ni njia rahisi ya kujipatia huduma za kibenki ndani ya nchi 33 ambazo Benki yetu inafanya biashara lakini pia unaweza kuitumia ukiwa kokote duniani. Wateja wanaweza kupakua applikesheni Ecobank Mobile App na papo hapo kujifungulia akaunti ya Ecobank kwa njia ya mtandao na kuanza kupata huduma za kibenki kama vile kufanya malipo au kuhamisha fedha bila kutembelea tawi lolote la Benki”, alisema Bi Mzee.

“Tunayo furaha kwamba applikesheni yetu ni sulushisho la huduma za haraka za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi na bado inaendea kuboreshwa zaidi na zaidi na sasa tunatumia teknolojia ya Masterpass QR na Mvisa kwa kufanya malipo mbali mbali, aliongeza.

Bi Mzee aliongeza kuwa Masterpass QR na Mvisa ni njia za mtandao (kidigitali) ambazo humfanya mteja kulipa kwa kadi ya Benki au akaunti zake za benki ambazo pia zimeunganishwa katika mtandao huu kwa kugusisha na kufanya malipo. ‘Hii ni njia ya kutumia simu za mkononi ambapo mnunuzi ataweza kumlipa muuzaji au mtoa huduma yeyote na hivyo inakuwa ni suluhisho kwa wajasiriamli wadogo, wa kati na wakubwa’, aliongeza Bi Mzee.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi Swere Ndabu alisema “Ili kutumia huduma hii wateja wa Ecobank na wasio wateja wa Ecobank wanatakiwa kupakua Applikesheni ya Ecobank Mobile App kwenye smartphone zao kisha wanajisajili kwa kutumia kadi ya Visa au Master , au kufungua akaunti ya Ecobank Xpress papo hapo na kuanza kufanya miamala ya malipo. Kwa wale ambao ni wateja wanatakiwa kupakua na kuanza kutumia applikesheni kwa kutumia debit card au Ecobank Retail internet banking.”

“Kwa kutumia applikesheni hii wakati wa kufanya Malipo, mteja atanufaika kwa kuokoa muda wake na kupunguza gharama za kutembelea tawi la Benki, ataweza pia kufanya Malipo kwa haraka na kwa usalama zaidi pamoja na kuongeza mauzo kwa vile njia hii itachochea matumizi au manunuzi salama. Vilevile itamsaidia muuzaji sana kwani ni njia rahisi ya kutunza kumbu kumbu za mauzo.” alisema Swere.

Swere aliongeza kuwa kwa kutumia applikesheni ya Ecobank Mobile App mteja anaweza akahamisha fedha kwenye akaunti yake ya Ecobank akiwa hapa nchini au nje ya Tanzania, pia ataweza kuhamisha fedha kwenda Benki nyingine hapa nchini au kwenda kwenye kadi za Visa duniani kote na pia kwenye mitandao ya simu za mkononi ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.
  Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ,Ecobank Tanzania, Mwanaiba Mzee, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA .Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati  na Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja reja, Ndabu Sware (kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja Reja wa Ecobank Ndabu Lilian Sware (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Kati kati Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki hiyo Mwanaiba Mzee na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakifuatilia kwa umakini wa Uzinduzi  wa huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Ecobank Tanzania inakuwa Benki ya kwanza hapa Tanzania kuzindua huduma ya Mobile App ambayo inakuwa ni suluhisho kwa huduma za kifedha.

MSANII WA MUZIKI WA ASILI,MPOTO AWASILI NCHINI CHINA KWAAJILI YA KUHAMASISHA UTALII.

$
0
0

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto akiwa na mwenyeji wake katika viwanja ambavyo Tamasha la Utalii linafanyika nchin China.
 Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewasili nchini China leo katika eneo ambalo litakuwa likionesha utalii ikiwa ameenda huko kwaajili ya kuwakilisha nchi katika tamasha la Utalii Duniani ambalo litafanyika kuanzia Leo Septemba 21,2017.
 Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto akiwa katika picha nchini China.

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewasili nchini China Jumatano hii kwaajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duaniani. 

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kitendawili’, aliondoka nchini Tanzania siku ya Jumatatu akiwa ameambatana na kikundi chache cha ngoma kikiwa na jumla ya watu sita pamoja na yeye mwenyewe.
Akiongea na mwandishi wetu akiwa nchini humo baada ya kuwasili katika eneo ambalo litafanyika tamasha hilo, Mpoto amesema Alhamisi hii wataanza kufanya maonyesha hayo katika tamasha hilo ambalo linayakutanisha mataifa mbalimbali duniani.

“Kama nilivyowaambia watanzania wakati naondoka Tanzania, tumekuja China kwaajili ya watanzania, tumekuja kuwawakilisha wao, tunatangaza utalii wa ndani, lugha zetu za makabila zaidi ya 120, lugha yetu hadhimu ya Kiswahili, mbuga zetu za wanyama kwahiyo sisi tutawaambia Tanzania ni nchi ambayo ina kila kitu kama ukiamua kuitembelea,” alisema Mpoto.

Aliongeza,“Tumejiandaa vizuri kufanya kile kitu tulichokipanga, watanzania wananijua mimi ni mtu gani kwenye hizo anga, Kiswahili ni lugha yangu kwahiyo naweza kusema tumejipanga kuuonyesha ulimwengu tuna kitu gani ambacho tumewaletea na bila shaka kila ambaye amekuja katika eneo hili atondoka na meseji ya Tanzania ni sehemu sahihi ya kuitembelea,”

Pia amewataka watanzania kuwaunga mkono wasanii ambao wanafanya jitihada mbalimbali za kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali za utalii kwa kuwa utalii ni moja kati vyanzo vizuri vya mapato nchini.

“Uwepo wangu mimi hapa sio kwaajili ya familia yangu, hiki ninachokifanya hapa ni kwaajili ya watanzania, yule mtalii ambaye atakuja Tanzania baada ya kusikia meseji yangu ile pesa anayolipa kwaajili ya kutalii ndio ile ambayo inajenga hospitali na kununua dawa. Kwahiyo mimi ningewataka watanzania kuwa wazalendo kwenye mambo ya msingi ambayo bila shaka yanaleta tija kwaajili ya watanzania wote," alisema Mpoto.
Muimbaji huyo amesema kila mtanzania anaweza kuitangaza nchini yake kwa mazuri hivyo wamewaka watanzania kuwa wazalendo na kudumisha amani iliyopo.

KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA WA KIFO CHA CASSIUS O. MDAMI

$
0
0
Tangu umetuacha tumetafakari mengi tukidhani umesafiri utarudi lakini kumbe haikuwa hivyo. Kuwa kwako mbali na familia kumetufanya kujifunza mengi kuhusu maisha na kutafakari muda ambao tulikuwa pamoja katika maisha ya hapa duniani wakati wa furaha na uchungu.

 Unakumbukwa na mke wako Rose na watoto wako Martina, Grace, Gideon, Gonsalver na Gibson. Umetimiza mwaka sasa tangu umetuacha; pengo lako ni kubwa katika kila kona ya maisha na hata katika Tasnia ya Habari uliyoitumikia katika muda mwingi wa maisha yako kwa kutuonyesha kwa vitendo maana ya kuipenda na kuithamini kazi katika maisha. 

Tumekosa simulizi za kusisimua za Utalii wa Ndani, ulichimba na kuchimbua mengi ambayo kama si kwa jitihada zako binafsi tusingeyajua kamwe… tumebaki na msemo wako maarufu “Falsafa ya Ufagio ni Unyenyekevu”. Faraja yetu ni Mungu aliye Baba wa Yatima na mume wa Wajane (Kutoka 22:22-24). Tunaamini katika Ufufuo na Uzima na siku moja tutafurahi nawe mbinguni (Yohana 11:25-26). 

Mungu akupe pumziko la Milele, upumzike kwa Amani - Amina

WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA PEACE CORPS WAPATAO 57 WAAPISHWA KUHUDUMU NCHINI KWA MIAKA MIWILI

$
0
0
 Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Inmi Patterson aliwaapisha wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps wapatao 57 kuhudumu nchini Tanzania katika kipindi cha miaka miwili katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Peace Corps jijini Dar es Salaam. 

Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa Kimarekani watakaofanya kazi katika sekta ya elimu watapangiwa kuhudumu katika wilaya za Iringa, Mufindi, Same, Kyela, Masasi, Maswa, Singida Vijijini, Lushoto, Chamwino, Hai, Rombo, Wete, Rungwe, Njombe, Iringa Vijijini, Sumbawanga, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Hanang, Mbeya, Nachingwea, Hanang, Iramba, Kiomboi, Mbeya Rural, Shinyanga na Singida Mjini.
Mgeni rasmi katika hafla hii alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Leonard D. Akwilapo. Hafla hii ilihudhuriwa pia na wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps wanaoendelea kuhudumu na wale waliohudumu hapo zamani pamoja na maafisa kutoka mashirika mengine yanayojihusisha na wafanyakazi wa kujitolea. 

Akizungumza na wafanyakazi hao wa kujitolea Kaimu Balozi Patterson alisema: "Wakati ambapo kuna uwezekano kwamba mnaweza kuwa Wamarekani wa kwanza kuishi na wafanyakazi wenzenu au majirani wa Kitanzania, ni wazi kwamba kwa Watanzania hao nyinyi mtaendelea kuwa wawakilishi wa Watu wa Marekani."

Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa zaidi ya miaka 50, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:

• Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao;
• Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;
• Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.

Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolewa wa Peace Corps 2,500 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1961.  Peace Corps hutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wenye utaalamu katika nyanja mbalimbali ambao hupangiwa kufanyakazi katika jamii wakifundisha katika shule za sekondari (hisabati, sayansi na Kiingereza), wakitoa elimu ya afya na utunzaji wa mazingira.

UMOJA WA MASOKO MKOA WA DAR ES SALAAM WACHANGIA VYAKULA KWA AJILI YA WAFYATUAJI TOFALI

$
0
0
 Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Mwajuma Magwiza akipokea msaada vya vyakula kutoka kwa Mwenyekiti wa MUMADA, Mohamed Mwekya ikiwa kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ujenzi wa ofisi za walimu.


MUUNGANO wa Umoja wa Masoko ya Mkoa wa Dar es Salaam (MUMADA) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mohamed Mwekya wamekabidhi kilo za mchele 2835, Kilo 600 za Maharage pamoja Chumvi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ujenzi wa ofisi za walimu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mwenyekiti wa MUMADA, Mwekya amesema kuwa wao kama wafanyabishara wameguswa na harakati za RC Makonda katika kuboresha elimu hususani mazingira ya walimu, hivyo wameamua kutoa mchango wao huo ambao wana imani utasaidia.

Mwekya amesema wataendelea kushirikiana na na serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwataka wadau wengine wa maendeleo waunge mkono jitihada hizo zenye lengo ya kuboresha elimu kwa walimu kukaa ofisi zenye hadhi na taaluma yao.

Nae Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Mwajuma Magwiza amesema kuwa mchango huo utakwenda kwa shughuli iliyokusudiwa na wana imani kila mmoja akijitolea watatimiza lengo la kujenga ofisi 19 za walimu katika wilaya ya Kinondoni.
 Sehemu ya msaada vyakula kwa ajili ya watu wataofyatua tofali kwa ajili ya ujenzi ofisi za walimu.
.Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Mwajuma Magwiza akiwa katika ya pamoja na Muungano wa Umoja wa Masoko ya Mkoa wa Dar es Salaam (MUMADA) leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)



ZAIDI YA MILIONI 400 KUTUMIKA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ENEO LA PONGWE HADI MUHEZA

$
0
0
Mhandisi wa Mradi wa Maji kutoka eneo la Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza kutoka kampuni ya Koberg Construction Co.Limited Mhandisi Stepheni Kingili kushoto akitoa maelekezo kwa Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu namna watakavyoanza kutekeleza mradi huo kuanzia kesho(leo) wakati wa halfa ya makabidhiano ya vifaa vya mradi huo yaliyofanyika ofisi ndogo za mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) eneo la Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ndogo za mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa,Mhandisi Joshua Mgeyekwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akiingia kwenye halfa hiyo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu 
Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa halfa hiyo 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Luiza Mlelwa akizungumza katika halfa hiyo 
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akizungumza katika halfa hiyo 
Sehemu ya wagen kutoka maeneo mbalimbali waliojitokeza kushuhudia makabidhiaano haayo 
Sehemu ya wadau waliohudhuria makabidhiano hayo eneo la Pongwe Jijini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajaabu wa pili kutoka kulia akiongozana na baadhi ya viongozi kukagua mabomba yatakayotumikaa kwenye mradi huo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Luiza Mlelwa na kushoto ni Mhandisi wa Mradi huo ambao utatoa maji Pongwe Jijini Tanga Hadi wilayani Muheza
Moja kati ya vifaa mbalimbali vitakayotumika kwenye mradi huo.
Sehemu ya Mabomba ambayo yatatumika kwenye mradi huo mkubwa utakaogharimu zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya kutoa maji eneo la Pongwe Jijini Tanga Hadi wilayani Muheza


WANANCHI wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga wataondokana na adha ya huduma ya maji baada ya Serikali kutenga fedha zaidi ya milioni 400 kwa ajili mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka eneo la Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza.

Hatua hiyo ina lenga kuondoa changamoto ya uhaba wa maji wilayani Muheza ambayo ilikuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi kutokana na kutumia muda mwingi kusaka
huduma hiyo badala ya kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

Akizungumza jwakati wa kukabidhi mabomba yatakayotumika kwa mkandarasi wa mradi huo katika eneo la Pongwe Jijini Tanga, Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema mradi huo utakuwa ndio mkombozi mkubwa kwa wananchi.

Alisema mradi huo ambao ni mkubwa ni moja kati ya ahadi za Rais John Magufuli alipofanya ziara mkoani Tanga ambapo alihaidi kuhakikisha wakazi wa mji huo wanaondokana na changamoto ya uhaba wa maji.

"Kwanza nimshukuru mh Rais kwa kutekeleza ahadi yake mapema jambo ambalo limetupa faraja kubwa sisi wakazi wa Muheza na vitongoji vyake lakini niwaambie katika mradi huu nitakuwa mkali sana na nitafuatilia kila mwezi kuhakikisha unajengwa kwa viwango kutokana na thamani ya fedha"Alisema.

Aidha alimsisitizia mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kuhakikisha ajira zitakazotolewa ziwalenge vijana waliopo katika maeneo hayo ili kuweza kupunguza ukali na ugumu wa maisha kwao na jamii zinawazunguka.

Awali akizungumza katika makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi ya maji inayotarajiwa kutekelezwa wilayani Muheza ili kumaliza tatizo la maji wilayani humo.

Alisema katika mradi huo mamlaka hiyo imetumia zaidi ya milioni 30 katika bajeti zake kufanya tathimini ya mradi huo huku serikali itokea fedha zote ambazo zitatumika katika mradi huo ambao utakwenda sanjari na ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji eneo la Kilapura litakalokuwa na ujazo wa lita laki saba.

"Lengo la mamlaka ya maji na serikali ya wilaya ya Muheza pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya huduma ya maji ambayo ndio kilio chao kikubwa kwa wilaya hiyo "Alisema.

Akizungumzia suala la utunzaji wa mradi huo,Mhandisi Mgeyekwa alisema mradi huo ni mali ya wananchi hivyo lazima wahakikishe wanakuwa mabalozi wazuri wa kulinda miundombinu ya maji ili iweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo.

Naye kwa upande wake,Mkandarasi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Koberg Construction Limited,Mhandisi Stephen Kingili alisema mradi huo utatekelezwa kwa wakati ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi wa wilaya ya Muheza kuweza
kunufuika na huduma hiyo.

Alisema utekelezaji wa mradi huo utaanza kutekelezwa kesho (Septemba 21) ambao utakamilika Mei 19 mwakani ukichukua miezi 8 ili kuweza kukamilika na hivyo wananchi kuweza kuutumia.

Aidha alisema mradi huo utakuwa na urefu wa km 16.9 kutoka eneo la Pongwe Jijini Tanga mpaka Muheza mjini ambao utakwenda sambamba na maungio ya kuchepusha maji katika vijiji vyote utakaopita ili kuwarahisishia wananchi kuweza kujiunganishia huduma hiyo pindi wanapokuwa wakihitaji.

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Tigo yatoa msaada wa mfumo wa kidigitali wa elimu Mkoani Mwanza

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella,akitata utepe wakati wa uzinduzi wa programu ya kompyuta yenye vitabu vya masomo ya shule za sekondari(Tigo eSchool) iliyounganishwa kwenye shule ya sekondari Pamba mkoani Mwanza jana na Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella,akimshukuru Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya(kushoto) baada ya kuzindua programu ya kompyuta yenye vitabu vya masomo ya shule za sekondari(Tigo eSchool) iliyounganishwa kwenye shule ya sekondari Pamba na Kampuni ya Tigo, Jumla ya shule tano za mkoa huo zimeunganishwa na huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akijaribu huduma ya Tigo eSchool kwenye shule ya Sekondari Pamba mkoani Mwanza. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa, Alli Maswanya (kushoto)na Mbunifu waTovuti toka Shule Direct, Rajabu Mgeni.


Sekondari tatu za Mwanza zapokea msaada kutoka mradi wa Tigo E-schools

Mwanza 21 Septemba, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania kupitia mradi wa Tigo E-schools imetoa msaada wa mfumo wa teknologia kwa masomo kumi na moja (11) ya shule kwa sekondari tatu (3) za Mkoani Mwanza.

Ikiwa ni sehemu ya shughuli za jamii zinazoendana na msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa, msaada huu unaonesha sifa kuu ya Tigo kama mtandao unaoelewa wateja wake na kuwapa huduma zinazoendana na mahitaji yao. Kupitia mradi wa Tigo e-schools, Tigo imeona na kuelewa hitaji la wanafunzi la maarifa ya Tehama, na inakutana na hitaji hili kupitia utoaji wa kompyuta zilizounganishwa na intaneti na mifumo mbali mbali ya elimu.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mfumo huo, Meneja Kanda wa Tigo, Ali Maswanya alisema kuwa mfumo huo utawaandaa wanafunzi kuibua fursa na kuwa sehemu ya mabadiliko ya Tehama ulimwenguni.

‘Dunia ya sasa inaendeshwa kidigitali. Mradi wa Tigo E-shools unawaandaa wanafunzi kuwa sehemu ya ulimwengu huu wa kidigitali. Kupitia mfumo huu, wanafunzi wataongeza busara, kupanua mitazamo na ubunifu wao, na hivyo kuibua fursa pamoja na kukabiliana na changamoto zinazoendana na ulimwengu wa sasa wa digitali,” Maswanya alisema.

Alitaja shule za sekondari zilizofaidi kutoka kwa msaada huo Mkoani Mwanza ni Shule ya Sekondari Pamba, Sekondari ya Mwanza na Sekondari ya Mirongo. Tigo E-schools pia itasambaza mfumo huo wa elimu kwa shule 52 za sekondari katika mikoa 12 kati ya mikoa 15 ambayo msimu wa Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa utazuru mwaka huu.

Mwaka 2016, Tigo ilifanya makubaliano na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwezesha kusambazwa kwa mtandao katika shule za sekondari nchini ili kuchangia mpango wa miaka miwili wa serikali kuleta mabadiliko ya elimu kwa njia ya mtandao.

Kama sehemu ya makubaliano hayo, Wizara ilitoa majina ya shule zisizokuwa na maabara ya kompyuta na pia kutoa mwongozo wa utekelazaji wa mradi huo. Tigo ilishiriki katika ujenzi na kuunganisha maabara mpya za kompyuta na mtandao, na hatua ya tatu ni ya kuunganisha shule husika na teknologia hii ya elimu kwa njia ya mtandao.

“Kupitia mpango wetu endelevu wa kuwekeza katika hudma za jamii, Tigo inachangia jitahada za serikali za kuigeuza Tanzania kuwa na uchumi wa maarifa ifikapo mwaka 2025.” Maswanya aliongeza.

Shule ambazo zitaunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama ni Arusha Day, Ilbouru na Arusha Sekondari mkoani Arusha; Mwanza, Pamba na Mirongo Sekondari mkoani Mwanza; Tabora Girls na Milambo Sekondari mkoani Tabora; na Mpwapwa Sekondari mkoani Dodoma.

Shule nyingine ni Iringa na Kleruu Sekondari mkoani Iringa; Matalawe na Songea Girls Sekondari mkoani Songea; Njombe na Mpechi Sekondari mkoani Njombe; Morogoro Municipal na Mzumbe Sekondari zilizopo Morogoro; pamoja na Handeni na Shemsanga Sekondari huko Tanga.

Shule nyingine zitakazofaidi mfumo huu wa elimu kutoka Tigo e-schools ni Lyamungo Sekondari na Machame Girls Sekondari huko Moshi; Newala Day na Masasi Day Sekondari zilizopo Mtwara na kwa mkoa wa Dar es Salaam, sekondari za Mbagala, Kibamba, Benjamin Mkapa na Makumbusho zitaunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama.

‘Kwa mara nyingine, natoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa kuiruhusu Tigo Tanzania kuwa sehemu ya mipango yake ya kuiingiza Tanzania katika mfumo wa uchumi wa maarifa,’ Meneja huyo wa Tigo alimaliza.

Tigo ni mdau muhimu wa elimu na imetoa michango mbali mbali kuinua viwango vya elimu nchini. Mwaka jana Tigo ilichangia madawati zaidi ya 7,100 katika shule za mzingi nchini kote. Vilevile Tigo imetoa kompyuta 77 zilizounganishwa na mtandao wa kasi zaidi wa Tigo kwa vituo vya elimu ya juu nchini.

ZITTO KABWE AHOJIWA NA KAMATI YA BUNGE LEO

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini Mheshimiwa Zitto Kabwe akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge leo mjini Dodoma mbunge huyo alipoitwa kuhojiwa juu ya Shutma za kudharau Mhimili wa Bunge. (Picha Ofisi ya Bunge)
Mweyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Mheshimiwa Kapteni Mstaafu George Mkuchika akiongoza Mahojiano ya Kamati hiyo leo Bungeni Mjini Dodoma ambapo Mheshimiwa Zitto kabwe aliitwa  kuhojiwa juu ya shutma za kudharau Mamlaka ya Bunge.

JWTZ LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LA UJENZI WA UKUTA MERERANI-SIMANJIRO MKOANI MANYARA

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ laanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano.
Helikopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuyo akitua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano. Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limenanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
 Helkopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuhyo ikitua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Simanjiro na wananchi mara baada ya kutua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Meja Jenerali Michael Isamuhyo akisalimiana na baadhi ya wakazi wa eneo la Mererani,mara baada ya kutua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipenya kwenye vichaka wakati wa kukagua eneo litakalojengwa ukuta.
  Meja Jenerali Michael Isamuhyo akitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A mpaka D katika eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 21, 2017, tayari kwa kuanza kazi ya kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kufuatia amri ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyotoa jana ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee. 
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akioneshwa ramani ya vitalu A hadi D katika eneo la madini ya Tanzanite huko Mererani.
Meja Jenerali Michael Isamuhyo akitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A mpaka D katika eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 21, 2017, tayari kwa kuanza kazi ya kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kufuatia amri ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyotoa jana ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee.

TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO

$
0
0
Kaimu Mkrugenzi Mkuu wa TACAIDS Bw.Jumanne Issango akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano kuhusu changamoto na mafanikio katika kupambana na virusi vya ukimwi nchini kulia ni Kaimu Mkurugenzi Muitiko wa kitaifa wa TACAIDS Bi.Audrey Njelekela mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za TACAIDS leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO) 

Na Fatma Salum – MAELEZO
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeendelea kuiasa jamii kuhusu kubadili tabia ili kuepuka maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani ugonjwa huo bado ni janga kwenye nchi yetu.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Bw.Jumanne Issango alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio na changamoto za tume tangu ilipoanza kutekeleza majukumu yake.
“UKIMWI bado ni changamoto katika maendeleo ya Taifa letu na umeendelea kuathiri kila sekta, kila imani, matajiri na masikini nchini kote hivyo ni wajibu wa kila mmoja kujitathmini mwenendo wake na kuacha tabia hatarishi ambazo zinachangia kuongeza maambukizi ikiwemo uasherati, ngono zembe, ulevi na kadhalika,” alisema Issango.
Alieleza kuwa kwa miaka ya karibuni hali ya maambukizi ya UKIMWI imeendelea kupungua ingawa kuna tofauti kwenye mikoa, wilaya na makundi ya kijamii.Issango alibainisha kuwa kiwango cha maambukizi Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na takwimu hizo ni kutokana na Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI mwaka 2012.
Kwa mujibu wa utafiti huo wanawake walioambukizwa ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.8 ambapo idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kuishi na VVU ni zaidi ya milioni 1.5.“Mikoa inayoongoza kuwa na maambukizi makubwa ni Njombe asilimia 14.8, Mbeya asilimia 9 na mikoa yenye maambukizi ya chini zaidi ni Manyara asilimia 1.5, Tanga asilimia 2.4 na Dodoma asilimia 2.9,” alifafanua Issango.
Aidha alisema kuwa licha ya maambukizi mapya kupungua kwenye jamii bado kiwango cha maambukizi kwenye makundi maalum kimeendelea kuongezeka.Akitaja makundi hayo Issango alisema kuwa ni pamoja na madereva wa magari ya masafa marefu, wachimba madini, wavuvi, wafungwa na wale wanaofanya biashara ya ngono.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muitikio wa Kitaifa kutoka Tume hiyo Bi. Audrey Njelekela alisema Serikali kupitia TACAIDS inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na janga hilo ikiwemo kuandaa na kutekeleza mikakati madhubuti itakayosaidia kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa.
“Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2013/14 – 2017/18 unalenga ifikapo 2018 kiwango cha maambukizi kishuke kufikia asilimia 0.16 ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo utafiti unaonesha maambukizi ni asilimia 0.32,” alisema Njelekela.
Alitaja hatua nyingine zinazochukuliwa na tume hiyo ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa umma hasa kwa vijana, wanawake wajawazito na makundi maalum ikiwemo kujenga Vituo vya Maarifa vinavyotoa huduma za VVU/UKIMWI kwa madereva wa magari ya masafa marefu. 
Aliongeza kuwa juhudu za Serikali kutoa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARVs) zimesaidia kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo ambapo kwa sasa wanaotumia dawa hizo ni zaidi ya watu laki 8.
Pia Serikali imeanzisha Mfuko wa Udhamini wa Shughuli za Kudhibiti UKIMWI kwa ajili ya kusaidia kununua dawa, kutoa elimu ya UKIMWI, kupima, kufanya tafiti na kutoa elimu ya uzazi kwa vijana.
TACAIDS ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 22 ya mwaka 2001 kwa lengo la kutoa uongozi wa kimkakati, uratibu na kuimarisha juhudi za wadau wote wanaojishughulisha na kudhibiti UKIMWI nchini.

SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu.





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye eneo la uwekaji jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha, Septemba 21, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo

Baadhi ya Wananchi wa Longido wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa wakati alipozungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha, Septemba 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Longido kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha Septemba 21, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea kirungu ikiwa ni zawadi ya asili ya Kabila la Wamasai kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya Longido, Thomas Olengulupa kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea usinga ikiwa ni zawadi ya asili ya Kabila la Wamasai kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya Longido, Thomas Olengulupa kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arsha Septemba 21, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mrisho Gambo.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


…………………….


CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama wilayani Longido mkoani Arusha kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 15.8.

Waziri Mkuu ameweka jiwe hilo la msingi leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Longido Mjini pamoja na kijiji cha Oltepesi ambao chanzo chake ni kutoka mto Simba wilaya ya Hai mkoani Kilimanajro.

Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kupeleta wataalamu wilayani Longido ambao watashirikiana na Halmashuri za wilaya ya Longido na tarafa ya Loliondo kutafuta vyanzo vingine vya maji ili wananchi waweze kupata maji ya kutosha.

Waziri Mkuu amesema asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya za Longido na Ngorongoro ni wafungaji hivyo wanahitaji maji mengi watakayoyatumia katika matumizi yao ya kawaida ya nyumbani pamoja na kunyweshea migugo.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo pamoja na miradi mingine midogo tisa katika wilaya ya Longido kutumia vifaa vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia viwanda.


Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.

Awali Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Lwenge aliwaagiza Wakandarasi wanaojenga mradi huo kuhakikisha wanajenga kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyohitajika pamoja na kumaliza kwa wakati. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2018.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, SEPTEMBA 21, 2017.

WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA

$
0
0

Na John Nditi, Ulanga.
KAMPUNI ya TanzGraphite imesema itawajengea nyumba zenye hadhi ya juu kaya za  kijiji cha Epanko, wilayani Ulanga , mkoani Morogoro  zinazohama kwa kupisha mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini ya Kinywe (Graphite) na itahakikisha kuwa,  maisha ya watu wanaohama yanabaki kama ilivyokuwa awali ikiwa na  kuboreshwa zaidi.

Meneja Mahusiano wa TanzGraphite, Bernard Mihayo , alisema hayo kwenye taarifa ya Kampuni hiyo  katika  kikao cha tisa cha kikosi kazi kilichokutana  Septemba 14, mwaka huu  mjini Mahenge , wilayani humo.

Kikao hicho kilichokuwa ni cha kujadili na kupokea mrejesho wa vikao vya wananchi kuhusu mpango wa uhamishaji makazi (RAP) kupisha mradi wa madini ya kinywe wa Epanko kilihudhuriwa na  wajumbe  wa vitongoji vya  Kazimoto, Epanko A, Itatira , Mbera, Epanko B na Luli .

 Wawakilishi wengine ni kutoka   ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Ofisi ya madini mkoa , Ofisi ya  wilaya ya Ulanga , halmashauri na wadau wengine wa mradi huo.

Madini ya Graphite ‘Kinywe’ kwa sasa yanahitajika kwa wingi duniani kutokana na matumizi ya  kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo betri za simu , kompyuta mpakato ‘laptop’  na penseli .

Kwa mujibu wa Meneja Mahusiano wa TanzGraphite , utafiti uliofanywa na  Kampuni  hiyo umebaini madini hayo yanapatikana kwa wingi  na kwa ubora zaidi eneo la Kijiji cha Epanko, wilayani Ulanga, mkoa wa Morogoro.

Alisema ,ndani ya eneo linalohitajika kuendesha mradi , lina kaya zipatazo 320 ambazo nyumba zake zimejengwa zaidi kwenye mabonde ambayo pia yanatumika kwa shughuli za kilimo.

Meneja Mahusiano wa TanzGraphite alisema , kaya nyingine zipatazo 80  zinaishi nje ya eneo la mradi , isipokuwa  zinamiliki ardhi na mashamba ndani ya eneo la mradi huo.

Pamoja na hayo alisema, ndani ya eneo la mradi kuna miundombinu ya kijamii kama shule ya msingi, ambayo ndiyo shule pekee iliyopo katika kijiji cha Epanko , Kanisa Katoliki,  na jengo la zahanati ya kijiji ambayo bado haijakamilika.

Naye Mwakilishi wa Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Morogoro, Athuman Kwariko alisema , serikali ipo tayari kusimamia sekta ya madini na inajipanga kuanzisha  Kamisheni ya Madini.

Alisema , madini ni mali ya wananchi na yanakasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa manufaa ya watu wote  na  kwa hiyo Serikali inasisitiza uwekezaji  na  kusimamia sekta ya madini na wananchi kuwa tayari kuwapokea wawekezaji kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Kamati ya kikao  kazi hicho , Valence Kidumu alisema, pamoja na mipango  mizuri iliyowasilishwa na Kampuni katika  kikao hicho  aliishauri Kampuni  iwasilishe  taarifa hiyo kwenye  kikao cha Baraza la Madiwani kinachotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

“ Taarifa hii tuliyoipokea leo hapa ni nzuri na unaungwa mkono na wajumbe wote , lakini ni vyema Kampuni ikatoe pia  kwa Madiwani kwenye  kikao cha baraza kinachotarajia kufanyika  Oktoba  mwaka huu kwa kupata baraka zao” alisema  Kidumu ambaye pia ni Ofisa Ardhi wa wilaya hiyo.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa mkoa  wa Morogoro, Lucas Mwaisaka , aliwataka viongozi wa serikali ya Kijiji Epanko kuitisha kikao  halali utakachoridhia kupitishwa kwa mpango wa uhamishaji wa makazi  ili utekelezaji  uweze  kuanza  na Kampuni hiyo.

Awali  mkuu wa wilaya ya Ulanga, Jacob Kassema alisema, juhudi  kubwa zimefanyika kutoa  elimu ya ushirikishwaji wananchi kuhusu miradi mbalimbali ukiwemo wa Epanko ambapo  asilimia 82 ya kaya za zimekubali kuthaminiwa kupisha mradi uchimbaji wa madini ya Kinywe.
 Kiongozi wa wa kimila wa kabila la Wapogoro wa kijiji cha Epanko , wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro  (Mbuyi ), Redemta Masura ( wapili kushoto) akiwa na viongozi  wa Kijiji hicho wakipitia  taarifa  ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko , wakati wa kikao cha tisa cha Kikosi Kazi iliyowashirikiasha wajumbe wa kutoka vitongozi sita wa kijiji hicho , viongozi kiserikali na kijamii kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
 Baadhi ya viongozi wa serikali wa wilaya ya Ulanga na mkoa wa Morogoro wakiungana na vitongoji vya kijiji cha Epanko wakiwemo na wakimila na kijamii  kupitia   taarifa  ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko katika kikao cha tisa cha Kikosi Kazi cha mpango wa uhamishaji makazi  kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
 Baadhi ya viongozi wa kamati ya Kikosi kazi  kutoka serikali  za vitongoji vya kijiji cha Epanko wakiwemo wa kimila na kijamii  wilayani  Ulanga  wakijumuika na wa ngazi ya wilaya hiyo na mkoa wa Morogoro kupitia   kwa pamoja taarifa  ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko  kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Lucas Mwaisaka (kulia) akimkabidhi  Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Epanko, Kata ya Nawenge, wilayani Uanga, Eliza Liwemba, ( kushoto) Mpango wa Uhamishaji Makazi (RAP) wa Mradi wa Madini wa Epanko  wakati wa kikao cha tisa cha Kikosi Kazi cha mpango huo kilichowashirikisha wajumbe wa kutoka vitongozi sita wa kijiji hicho , viongozi kiserikali  ya wilaya  na  mkoa ambacho kilifanyika hivi  karibuni mjini Mahenge. ( Picha na John Nditi).

TaSUBa KUFANYA TAMASHA LA 36 LA KIMATAIFA BAGAMOYO

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) (wa pili kushoto) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la 36 linalohusu Sanaa na Utamaduni Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) 21 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni toka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) (kushoto) akitolea ufafanuzi kwa Waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la 36 linalohusu Sanaa na Utamaduni Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) 21 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakichukua taarifa wakati wa Mkutano wa Waandishi wa habari uliohusu kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la 36 linalohusu Sanaa na Utamaduni Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) 21 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.


PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM


………………………………..


Na. Neema Mathias- MAELEZO


21,Septemba,2017.


Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeandaa tamasha la 36 la Kimataifa kuanzia tarehe, 23 hadi 30, Septemba litakalofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo mjini Bagamoyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Dkt.Hebert Makoye alisema kuwa tamasha hiyo litakuwa na kauli mbiu isemayo ‘sanaa na utamaduni katika kupiga vita madawa ya kulevya’.

“Kauli mbiu hii ni mahsusi katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kupiga vita matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya nchini” alisema Dkt. Makoye.

Aliongeza kuwa wakati wa tamasha elimu ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya itatolewa ikiwalenga hasa vijana ambao ndio waathirika wakuu wa dawa hizo ambapo kutakuwa na midahalo na makongamano kuhusu athari za matumizi ya dawa hizo.

Aidha alisema kuwa midahalo na makongamano hayo yatawahusisha vijana ambao watatoa ushuhuda juu ya matumizi ya dawa za kulevya,wamiliki wa vituo vya dawa za kulevya na wanasheria ambao watatoa mada mbalimbali kuhusu suala la dawa za kulevya kwa ujumla.

“Takwimu zinaonesha kuwa, idadi kubwa ya waathirika wa madawa ya kulevya ni vijana, kwa kuwa asilimia kubwa ya nguvu kazi katika tasnia yetu ni vijana tamasha letu mwaka huu limeamua kulenga kutoa elimu kuhusu ubaya wa matumizi ya dawa hizo kwani kupitia sanaa tutaweza kuwafikia vijana kwa kiwango kikubwa zaidi,” alieleza Dkt. Makoye.

Alifafanua kuwa, malengo ya tamasha hilo yamekuwa yakiboreshwa kwa kujikita katika mada mbalimbali ambapo lengo kubwa ni kutunza na kuenzi sanaa na utamaduni wa mtanzania, mwafrika na dunia nzima, pia tunalenga kutengeneza jukwaa ambalo wanafunzi wa TaSUBa watalitumia kupima kiwango chao cha umahiri katika sanaa kwa mwaka katika fani za sanaa za maonyesho na ufundi.

Malengo mengine ni kukutanisha watu wa tamaduni tofauti kutoka sehemu mbalimbali duniani ili kuonyesha utajiri wao wa sanaa na utamaduni pamoja na kutengeneza jukwaaa ambalo ni kiungo cha kujenga mahusiano ya wasanii wa ndani na nje ya nchi kupitia maonyesho ya sanaa kwa lengo la kubadilishana mawazo katika kuendeleza tasnia hiyo.

Vilevile amesema kuwa, mwaka huu wameamua kufanya maboresho katika tamasha hilo ambapo kutakuwa na maonyesho rasmi yatakayofanyika mchana kwa ajili ya watoto na vijana na kutoka katika shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa tamasha hilo, John Mponda amesema watakuwa wanaanza kwa warsha ambapo wadau mbalimbali watatoa elimu kuhusu masuala ya jamii kujitambua , kujenga uzalendo na kujitoa katika utumwa wa matumizi ya dawa za kulevya.


Aidha, Mponda ameeleza kuwa katika maonyesho hayo vijana wajasiriamali waliojiajiri watapata muda wa kutangaza biashara zao mbalimbali ikiwemo sanaa, vyakula lishe, vyakula dawa pamoja na kutambua mashirikisho mbalimbali ya sanaa.

Tamasha la mwaka huu litashirikisha vikundi zaidi ya 68 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo nje ya Tanzania tutakuwa na vikundi kutoka Kenya, Ufaransa, Uingereza, Zimbabwe, Mayyote pamoja na Korea na litafunguliwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe.

Dkt. Makoye aliwashukuru wadhamini wa tamasha hilo ambao ni pamoja na  Pepsi, CRDB Bank, Azam Group, Azam Tv,TBC, EFM, E TV, Mlimani Media, Habari Cooperation ltd, TSN, Millenium Hotel, Country Club, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ester decoration.

Taasisi ya Sanaa Bagamoyo TaSUBa ilianzishwa mwaka 2007 kwa malengo ya kutunza na kuenzi utamaduni wa Mtanzania, kuendesha tafiti na shughuli mbalimbali za sanaa na tamaduni na kukuza bidhaa za sanaa.

DOKTA MPANGO AIHIMIZA WAINGEREZA KUKUZA ZAIDI BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungungumzo na wabunge kutoka nchini Uingereza waliomtembelea Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba.
 Baadhi ya wabunge wa mabunge ya Uingereza wakiwa katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt, Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kushoto), akiongoza majadiliano na Ujumbe wa Wabunge watano pamoja na maafisa kadhaa kutoka nchini Uingereza, walipomtembela na kufanya naye mazungumzo Jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Ujumbe kutoka Tanzania walioshiriki mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na baadhi ya Wabunge kutoka nchini Uingereza, Jijini Dar es Salaam (kulia ni Mkurugenzi wa masuala ya Sheria Bi. Susana Mkapa akifuatiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Paul Sangawe.
 Kamisha wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Mgonya Benedicto (kushoto) na Msajili wa Hazina, Dkt. Oswald Mashindano, wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na wageni wake, Wabunge wa Mabunge ya Uingereza (Baraza la Mamwinyi na Bunge la Wawakilishi).
 Kiongozi wa Wabunge wa Bunge la Uingereza waliotembelea nchini na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mhe. David Linden, akizungumza namna nchi hiyo inavyosaidia masuala mbalimbali​ nchini ikiwemo Elimu na lishe.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akizungumza na Wabunge kutoka Nchini Uingereza waliomtembelea katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na kuipongeza nchi hiyo kwa kuisadia Tanzania katika masuala mbalimbali, amesisitiza ushirikiano wa nchi hizo mbili ujikite zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge kutoka Uingereza, Mhe. David Linden (katikati) na Wabunge wengine kutoka Uingereza, Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati)akijadili jambo na baadhi ya maafisa walioambatana na Wabunge wa Bunge la Uingereza baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao ulioangazia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Elimu, lishe, na Matumizi adili ya rasilimali fedha,  Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Tanzania imetoa rai kwa Serikali ya Uingereza kubadili mfumo wa uhusiano wake kwa kujikita zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji badala ya kutoa misaada ya kawaida ili nchi iweze kukuza uchumi wake kwa haraka zaidi.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wabunge kutoka mabunge ya uingereza (Baraza la Mamwinyi na Bunge la Wawakilishi).

Dokta Mpango amesema kuwa kiwango cha mtaji ambacho Serikali ya Uingereza imewekeza nchini hadi sasa ni Paundi bilioni 2.5 lakini kwa upande wa biashara kati ya nchi hizo mbili, hali si nzuri.

"Mwaka 2015 Tanzania iliuza nje bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 22.5 na kununua bidhaa kutoka Uingereza zenye thamani ya Dola milioni 150, kiwango ambacho ni kidogo sana na tunahitaji kufanya biashara zaidi" Alisisitiza Dkt. Mpango.

Alielezea hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua kuimarisha uchumi wa viwanda na kuelezea changamoto kubwa ikiwa na namna ya kuendeleza kilimo kwa ajili ya kupata malighafi za viwanda na kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuwa kilimo ndicho kinaajiri idadi kubwa ya Watanzania.

Dkt. Mpango alitoa wito kwa Serikali ya Uingereza kuwekeza zaidi katika viwanda vitakavyoongeza thamani ya bidhaa mbalimbali ikiwemo kujenga viwanda vya kutengeneza matrekta na zana nyingine za kilimo, kusindika bidhaa za mazao ya wakulima pamoja na kuwekeza katika sekta za kuongeza thamani ya madini na nishati ya umeme.

Dokta Mpango aliwaeleza Wabunge hao kwamba hivi sasa Serikali imepiga hatua kubwa kiuchumi na kuishukuru Uingereza kwa mchango mkubwa inaoutoa kusaidia Elimu, Lishe, Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma na afya kwa upande wa lishe, uwekezaji ambao kwa pamoja umefikia zaidi ya paundi milioni 180.

Kwa upande wake, kiongozi wa Wabunge watano waliomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa David Linden, amesema wamefurahishwa na namna Tanzania inavyopiga hatua kubwa kimaendeleo na kudhibiti vitendo vya rushwa.

Amesema kuwa wameridhishwa na kiwango cha miradi wanayoifadhili katika sekta ya elimu na afya hususan masuala ya lishe kwa watoto na kwamba nchi yao itaendelea kuisaidia Tanzania ili iweze kufikia malengo yake kiuchumi na kijamii

Wabunge hao wapo nchini tangu Jumapili iliyopita na wanatembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza.

SEKRETARIETI YA CCM CHINI YA KINANA YAFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM MJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM abdulrahman Kinana akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Chau Van Lam alipowasili kwa ajili ya mazungumzo na Sekretarieti ya CCM chini ya Kinana, jana katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-zanzibar Jumanne Mabodi. Katikati ni katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Kiongozi huyo akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Jumanne Mabodi
Kiongozi huyo akiendelea kusalimia viongzi wa CCM
Kiongozi huyo akiendelea kusalimia viongozi wa CCM
Kiongozi huyo akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
Kiongozi huyo akimsalimia Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi ya CCM
Kinana akimpeleka mgeni wake eneo la kufanyia mazungumzo
Mazungumzo yakianza
Mazungumzo yakiendelea
Mazungumzo yakiendelea
Kinana akitambulisha ujumbe wake kwa mgeni
Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma akizungumza na mwandishi wa Uhuru Fm aliyekuwa akifuatilia mazungumzo hayo

Ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo hayo
Chau akimpa zawadi Kinana baada ya mazungumzo hayo
Kinana akimshukuru kwa zawadi mgeni huyo
Chau akimpa zawadi nyinyine Kinana
Chau akimpa zawadi ya Kitabu cha misingi ya Kimunisti cha Veitnam, Kinana
Chau akizawadia Kinana tarumpeta la kisili ya Veitnam
Kabla ya kumkabidhi akaliungurumisha kidogo
Kinana akaipokea zawadi
Kisha Kinana akaonyeshwa kidogo namna ya kuliungurumisha
Kisha akalipuliza kwa uhodari
Kinana akapewa zawadi ya kofia ya asili ya Kivietnam
Akaipokea kwa furaha kofia hiyo
Kisha akaivaa kofia hiyo akiifurahia 
Akaendelea kuifurahia kofia hiyo 
Kinana akajibu mapigo na yeye kwa kumpa zawadi ya picha maridhawa ya kuchorwa
Chau akaipokea zawadi hiyo kwa furaha
Kinana akimweleza Chau undani wa picha hiyo
Kisha ikapigwa picha ya pamoja 
Kinana akaagana na mgeni wake
Kinana akimsindikiza mgeni wake baada ya mazungumzo hayo 
Ngemela akizungumza na waandishi kuwajulisha kilichojiri kwenye mazungumzo hayo

ZIFUATAZO NI PICHA ZA MAPOKEZI CHAU ALIPOWASILI DODOMA













Prof, Mbarawa Aitaka Bodi Mpya ya TTCL Kujipanga

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo mbele ya wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simu ya TTCL katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Maria Sasabo na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Omary Nundu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya TTCL Mhandisi, Omary Nundu akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Maria Sasabo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya mawasiliano) Dkt. Maria Sasabo akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Kampuni ya Simu ya Mkononi ya TTCL leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhandisi Omary Nundu na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya TTCL wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija – MAELEZO


Thobias Robert-Maelezo


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mkame Mbarawa ameitaka Bodi Mpya ya Wakurugenzi ya kampuni ya mawasiliano nchini (TTCL) kuhakikisha kuwa inasimamia vyema kazi na majukumu yake ili kuiwezesha kampuni hiyo kujiendesha kibiashara na kuimarisha huduma za mawasiliano hapa nchini.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo ambapo aliwasisistiza kuwa wachape kazi ili kurahisisha huduma mbalimbali za kimawasiliano hapa nchini na kuhakikisha kuwa wanaendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano yenye sera ya hapa kazi tu.

“Nataka bodi mjue tunakwenda wapi katika kampuni hii lakini pia tunahitaji kufanya kazi kwa juhudi, kushindana na makampuni mengine ya simu, mhakikishe mapato makubwa yanatoka kwenye data halikadhalika tujue mnapaswa mjue strenght (nguvu) yenu iko wapi maana tusipojibu maswali haya hatuwezi kufanya ushindani na makampuni mengine,” alifafanua Prof. Mbarawa.

Aidha Prof. Mbarawa alisema kuwa, Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji katika sekta ya mawasiliano kiasi ambacho kimeongeza mapato pamoja na ushindani wa huduma ya mawasiliano na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo hapa nchini.

Prof. Mbarawa aliongeza kuwa serikali imefanya mabadiliko yaliyofanywa na serikali ili kuipa nguvu Kampuni ya TTCL ikiwa ni pamoja na kuondoa ubia wa umiliki wa TTCL na wawekezaji asilimia 35 na kuzirejesha serikalini, kujenga mkongo wa taifa wa mawasilino, kujenga kituo cha taifa cha kuhifadhi kumbukumbu (Data center) pamoja na kulipa madeni ya kampuni hiyo.

Aidha Prof. Mbarawa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi kuhakiksha kuwa TTCL inaleta mabadliko na maendeleo katika kufikia sera ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda, kuongeza wateja na watumiaji wa huduma zitokanazo na TTCL, kuwafikia watumiaji wengi zaidi nchini kote na kuendelea kuwa kampuni bora ya mawasiliano.

Prof. Mbarawa aliongeza kuwa, TTCL ni lazima wabadilike katika utoaji wa huduma zake, ili kuendana na manadiliko ya teknolojia ambapo amewaeleza kuwa kwenye sekta ya mawasiliano mambo yanabadilika kila siku, sekta inakua haraka na hata uendeshaji wake unabadilika.

“Mathalani ukiangalia makampuni makubwa kwa sasa, mapato yao yamebadilika kutoka kwenye sauti hadi data pamoja na miamala ya pesa hivyo TTCL wanapaswa wajipime waangalie uwezo wao uko wapi na nguvu zao ziko wapi ili waweze kujipanga vizuri kuhakikisha wanashindana na makampuni mengine ya mawasiliano hapa nchini,” alifafanua Prof. Mbarawa. 

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mhandisi Omary Nundu, alisema kuwa tangu ateuliwe katika bodi hiyo mambo mengi wameyafanya hadi sasa ikiwemo kuifufua kampuni hiyo, kushirikiana na wadau wengine wa mawasiliano pamoja na kuanzisha TTCL Pesa.

“Kwa sasa tunahudumia watu laki tatu hapa nchini, lakini tumenuia mwisho wa mwaka huu wa fedha 2017/2018 tufikie wateja milioni moja na baada ya miaka mitano yaani ifikapo 2021/2022 tuwe na wateja milioni tano ambapo tutakuwa tumefikia asilimia 10 ya wateja wa soko la mawasiliano hapa nchini,” alifafanua Mhandisi Nundu.

Aidha, Mhandisi Nundu aliendelea kusema kuwa mwaka 2016, TTCL ilipata bilioni 0.21 katika soko lake na zaidi mwaka huu wanatarajia kupata bilioni 0.3 na kwamba wanatarajia kupata faida ya zaidi ya bilioni 40 ifikapo 2022 baada ya makato ya kodi.

“Katika kuyafanikisha matarajio yote haya, tunapaswa kupata jumla ya dola za kimarekani milioni 673, ambapo dola milioni 300 tunatarajia kuzipata kama mtaji wa uwekezaji kutoka serikalini, huku kampuni ikitafuta njia nyingine za kuapata fedha zilizobaki katika mpango na matarajio yetu,” alifafanua Mhandisi Nundu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo alisema sekta ya mawasiliano ni kiungo muhimu katika kukuza uchumi kwa kurahisisha mawasiliano ya kati ya mtu na mtu na taifa kwa ujumla kwa kurahisisha usambazaji na upatikanaji wa huduma na bidhaa kutoka sehemu moja na nyingine.

“Sera ya serikali ya kuelekea uchumi wa viwanda inatoa fursa kubwa kwa sekta ya mawasiliano kukua, pia ukuaji wa shughuli za uchumi unachochea mahitaji ya mawasiliano kuongezeka ikiwemo serikali mtandao, tiba mtandao, elimu mtandao, biashara mtandao, utangazaji mtandao kwa njia ya runinga na radi,” alifafanua Dkt.Sasabo.

Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL iliteuliwa rasmi mwezi Februari 2017,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni jitihada za kufufua na kurejesha kampuni hiyo katika ushindani, kusimamia mawasiliano yote ya serikali na kujiendesha kwa faida. Kwa sasa serikali inajiandaa kupeleka muswada bungeni ili kuirasimisha TCCL iwe na bajeti ya kujitegemea.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 22,2017

MWANAMUZIKI JOHN KITIME ANAKUALIKA WEWE KIJANA WA ZAMANI NA WASASA KATIKA BURUDANI YA MUZIKI WA ENZI HIZO PALE SALANDER BRIDGE KILA IJUMAA

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images